Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAONGOZA DUNIANI KWA KUWA NA UTAJILI WA URITHI WA ASILI BAADA YA BRAZIL

0
0





Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Kitaifa, Profesa Audax Mabula akizungumza katika ufunguzi huo ambapo amesema Tanzania inajivunia kuwa na Lugha kuu nne zilizopo Barani Afrika. Wakati wa ufunguzi huo leo Oktoba Mosi katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la Wanne Star wakicheza ngoma za utamaduni jukwaani wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo leo Oktoba mosi, Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wadau wa Utalii Tanzania, Bwana Abdukadir Luta Mohamed (Katikati) akiwa kwenye meza kuu wakati wa tamasha hilo.


Tanzania ni ya pili kwa Urithi wa Maliasili baada ya Taifa la Brazil la Bara la Amerika ya Kusini kwa kuwa na vivutio vingi vya Asili.

Hayo yameelezwa leo wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha la Urithi Wetu (Urithi Festival) linalofanyika katika viunga vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar-es –Salaam na Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wadau wa Utalii Tanzania, Bwana Abdukadir Luta Mohamed.

Amesema kuna vivutio vingi vya urithi wa utamaduni, ukiweka pamoja vivutio vya utalii wa asili na utamaduni, Tanzania inaweza kuongoza kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani. Bwana Mohamed amevitaja baadhi ya vivutio hivyo kuwa pamoja na tamaduni, makabila, mila, desturi, vyakula na Malikale.

Awali akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Kitaifa, Profesa Audax Mabula ameeleza kuwa Tanzania inajivunia kuwa na lugha kuu nne zilizopo Barani Afrika.

Amezitaja lugha hizo kuwa ni Wabantu ambao inawajumuisha makabila kama vile Wasukuma, Wajita na Wanyamwezi, Wanailotiki inawajumuisha Wamaasai, Wakushitiki-inayojumuisha Wairaq,Wambulu, Wakhoisan –inayowajumuisha Wahadzabe na Wasandawe.

Profesa Mabula ameeleza kuwa, Kabila la Wasandawe limeanza kupotea lakini ni imani kuwa kabila hilo litaendelezwa kupitia tamasha la Urithi Wetu. Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Kitaifa amesema “Utalii wa Utamaduni utainuliwa kupitia Urithi festival.

Amewaomba Watanzania kushiriki vema kwenye Tamasha hili na kuvaa mavazi ya Kitanzania kama vitenge, ngozi, batiki, shuka na mavazi mengine ya asili katika maadhimisho haya na ya kila Mwezi wa tamasha la Urithi. “Urithi festival inatoa fursa kwa watu wote. Tunapenda waje hapa waone ubunifu, vitu muhimu na mambo ya ubunifu wa kila aina” Amesema Profesa Mabula.

Ameongeza kuwa, Watu tuheshimu Urithi wetu wa Utamaduni ili kuchochea Utalii wa ndani na nje ya Nchi. Tamasha hilo limepambwa na vikundi mbalimbali vya ngoma za kiasili, sarakasi, nyimbo, Wajasiriamali, vyakula vya kiasili ikiwemo nyama choma za porini kama swala na nyati zilnazouzwa kwa shilingi elfu Nane kwa kilo.

Naye Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela katika kuunga mkono Tamasha la Urithi Wetu, imekabidhi fulana 100 katika hafla hiyo. Tamasha hilo ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka, linaandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, na lilizinduliwa rasmi Septemba 15 mwaka huu jijini Dodoma na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan likiwa na lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini.

Imeelezwa kuwa, baada ya Tamasha hilo kufungwa rasmi jijini Dar-es-Salaam litaendelea kufanyika Jijini Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeida Karatu, ambako ni njia kuu ya kuingilia katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na Serengeti kuanzia Oktoba 8 hadi 13.

NFRA YAENDELEA KUSISITIZA UBORA WA MAZAO KUTOKA KWA WAKULIMA

0
0
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akikagua mahindi wakati wa ununuzi katika kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma. 
Afisa ubora wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Masanja akikagua mahindi kwenye kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.



Na Mathias Canal, NFRA

Zoezi la kununua nafaka ya mahindi kwa ajili ya akiba ya Taifa ya Chakula unaendelea katika maeneo mbalimbali kote nchini ambapo wakulima kwa kiasi kikubwa wameitikia wito uliotolewa na Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) wa kutonunua mahindi yasiyokuwa na ubora.

Pamoja na Ubora wa mahindi kuwa changamoto katika maeneo mengi nchini kutokana na hali ya msimu wa mwaka Jana kuwa na jua Kali na mvua za msimu jambo lilolopelekea Mazao kuharibika yakiwa shambani.

Katika hatua nyingine Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba ameendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya ununuzi ambapo hivi tarehe 1 Octoba 2018 alitembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma kukagua mwenendo wa zoezi la ununuzi katika kituo hicho.

Katika ziara hiyo ya Mtendaji Mkuu wa NFRA mkoani Ruvuma, Meneja wa Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya alieleza kuwa Kanda ya Songea pekee imepangiwa kununua jumla ya tani 7, 000 kwa awamu ya kwanza ya ununuzi na hadi kufikia leo tarehe 1 Oktoba 2018 Kanda hiyo imeshanunua zaidi ya tani 6000. 

Ili kuimarisha dhana ya Ushirika, Wakala umenunua kwa kiasi kikubwa mahindi kupitia vyama ya Ushirika na vikundi vya wakulima yaani SACCOS na AMCOS ambazo jumla yake zinakuwa 23 ambazo ndizo zilizobainishwa na uongozi wa Mkoa wa Ruvuma. 

Vikundi hivyo vya wakulima ni kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Songea vijijini, Mbinga mji, Mbinga vijijini, Namtumbo na Wilaya ya Nyasa.Vumilia aonyesha kuridhishwa na hali ya ubora wa nafaka iliyonunuliwa na kuwahimiza watumishi wa NFRA kuendekea kusisitiza na kununua mahindi yenye vigezo vya ubora unaokubalika kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Chakula.

Katika hatua nyingine Bi Vumilia amewapongeza watumishi wa NFRA kwa kazi nzuri ya kiuweledi wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao na wakala kwa ujumla..

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 2,2018

0
0

 tanzanite-dondoshAmtanzania-DONDOSHA-frontmwananchi-dondosha-magazetiraia-mwema-dondosha-fronttanzania-daima-dondosha-magazetitanzanite-dondosha-magazetitanzania-daima-dondosha-magazeti-michezoraia-mwema-dondosha-michezojamvi-la-habari-dondosha-michezomwananchi-michezo-dondosha-magazetimtanzania-DONDOSHAbingwa-dondosha-magazetibingwa-michezo-dondosha-magazeti

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA

0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro kabla ya kuikabidhi taarifa hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (kulia). Wengine katika picha Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda (wa pili kushoto) na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Bi. Merry Mwanjelwa.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro pamoja na watendaji wa Wilaya ya Kilosa wakati wa kukabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. kulia ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Wengine katika picha wa pili kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Bi. Merry Mwanjelwa.

Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda.

aadhi ya viongozi wa halmashauri za vijiji saba wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa kuwapa taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.

Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa halmashauri za vijiji saba kuhusu taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.
 
 

Na Munir Shemweta, Morogoro 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji saba vya wilaya hiyo na mpango wa utekelezaji wake na kuagiza wote waliohusika kupotosha mipaka ya eneo hilo akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Lukuvi alitoa agizo hilo leo mkoani Morogoro wakati akikabidhi taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Jaji wa Mahakama Kuu ambaye sasa ni jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacob Mwambegele kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe kuhusiana na mgogoro wa mipaka ya kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani vya Mambegwa, Mbigiri, Dumila, Matongolo na Mfulu vilivyopo Wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. 

“Wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika process yote ambayo kwa kiasi fulani imeigharimu serikali fedha nyingi na kuipa maumivu serikali katika suala hilo ni lazima wachukuliwe hatua kali” alisema Lukuvi. 

Taarifa ya uchunguzi ilibaini chanzo cha mgogoro ni kukosekana ushirikishwaji wa vijiji jirani katika kuainisha na kuweka mipaka ya kijiji cha Mabwegere jambo lililosababisha kijiji kiwe na eneo la ukubwa wa hekta 10, 234 kuliko hata kijiji mama cha Mfulu chenye hekta 1,717 jambo lililothibitishwa na ukweli kwamba mipaka ya kijiji hicho imeingia ndani ya mipaka ya kata tatu za Mbigiri, Msowero, na Kitete ingawa kiutawala kijiji cha Mabwegere kinaratibiwa na kata ya Kitete. 

Hata hivyo, Waziri wa Ardhi alisema wizara haijakifuta kijiji cha Mabwegere bali itaanza kutekeleza mapendekezo ya uchunguzi ya kufuta mipaka ya kijiji hicho ambapo sasa TAMISEMI kwa kushirikiana na wilaya ya Kilosa itatakiwa kuanza mchakato wa kuandaa upya mipaka ya vijiji hivyo kwa njia shirikishi. 

Katika taarifa yake, Jaji Jacob Mwambegere alipendekeza kwa nia ya kuboresha utendaji kazi, weledi, maadili na umakini na uwezo wa kulinda na kutunza kumbukumbu katika idara ya Upimaji na Ramani na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi hatua za kinidhamu zichukuliwe ili kuzuia migogoro ya ardhi. Kwa mujibu wa Lukuvi, Wizara ya Ardhi ilikosea katika zoezi la upimaji wa kijiji cha Mabwegere lakini wilaya ya Kilosa itakuwa na jukumu la kuanza mchakato upya wa uanzishaji wa kijiji hicho. 

Alisema, kwa kuwa serikali inaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani ni jukumu la Tamisemi kwa kushirikiana na wilaya ya Kilosa kuhakikisha mipaka inaandaliwa upya kwa ajili ya kuanzishwa kijiji upya.
Waziri wa Ardhi alisisitiza kuwa shughuli za binadamu kama vile ufugaji na kilimo hazihusiani na masuala ya mipaka, hivyo wilaya ya Kilosa pamoja na kushughulikia suala la mipaka lazima iandae mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuanza kupendekeza maeneo ya ufugaji kwa vijiji vyote saba na kusisitiza kuwa ni lazima busara itumike katika kushughulikia jambo hilo. 

Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda alisema uanzishwaji kijiji cha Mabwegere haukufuata sheria na kuwataka wataalamu kuacha kuwa na nidhamu ya woga na kuzingatia kanuni na sheria katika kutekeleza majukumu yao. Aidha, amemuelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI kuunda timu itakayochunguza mchakato mzima wa kuanzisha kijiji hicho, na kila atakaebainika kuhusika na uanzishaji wa kijiji hicho kinyume na sheria achukuliwe hatua. 

Naye naibu Waziri wa Kilimo Merry Mwanjelwa alisisitiza hatua kuchukuliwa kwa wote waliohusika na kusema katika serikali hii ya awamu ya tano ni lazima kufufua makaburi kwa minajili ya kubaini wote waliohusika kuidanganya serikali. 

Taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa mipaka kati ya kijiji cha Mabwegere chenye jumla ya hekta 10,234 na mifugo takriban 24,146 na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa àmbao mara kadhaa ulisababisha vifo vya watu tangu mwaka 2008 lifanyika kwa muda wa siku sitini ambapo uchunguzi wake ulizingatia uanzishwaji, upimaji, utolewaji hati miliki kwa kijiji cha Mabwegere, maeneo yenye mgogoro na hatua zilizokwishachukuliwa juu ya mgogoro huo, uwiano wa ardhi, mifugo na mahitaji mengine ya ardhi pamoja na vyanzo vingine tofauti vya mgogoro. 

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiambatana na Manaibu waziri Tamisemi Joseph Kakunda na Kilimo Merry Mwanjelwa amekutana na viongozi wa Halmashauri za vijiji hivyo saba na kuwasomea taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani. 

Lukuvi amewaeleza wananchi hao kuwa ameikubali taarifa nzima ya uchunguzi kwa kuwa sheria inampa nafasi ya kuikubali au kuikataa taarifa hiyo, hivyo kuikubali kwake ni mwanzo wa utekelezaji wa mapendekezo ya uchunguzi na ndiyo maana aliamua kwenda kuwaeleza ukweli wa suala hilo. 

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi viongozi wa wizara nne za Ardhi, Tamisemi, Kilimo pamoja na wizara ya Uvuvi na Mifugo walikaa pamoja na na kupanga mpango wa utekelezaji uchunguzi huo na namna ya kushughulikia mgogoro baina ya kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani.

BENKI KUZITAMBUA HATI ZA HAKIMILIKI ZA KIMILA

0
0
Mratibu wa Mradi wa kuwezesha umilikishaji ardhi (LTSP) akitoa taarifa fupi ya mradi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na wafadhili wa mradi mjini Ifakara kabla ya kuanza ziara ya uwandani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias Kabundugulu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya (kulia) wakitia saini katika kitabu cha wageni kwenye ofisi ya kijiji cha mbuyuni ambapo pamoja na viongozi hawa, wafadhili wa mradi na wafanyakazi wa LTSP walishiriki katika ziara hii.
Afisa Ardhi mteule wa Wilaya ya Kilombero Syabumi Mwaipopo (alioyeshika karatasi) akiwaelezea Naibu katibu mkuu pamoja na wafadhili mchakato mzima wa kuipata hati ya hakimiliki ya kimila inavyopatikana.
Mmoja wa watumishi wa LTSP akiwaonesha wageni jinsi kazi ya kupima vipande vya ardhi inavyofanyika uwandani.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kukagua majina yao kama yapo sawasawa kabla ya hati kuchapishwa. Hili ni zoezi muhimu katika kuhakikisha hakuna makosa katika hati itakayochapishwa.

SERIKALI  imedhamilia kuunda mpango mkakati utakaoziwezesha benki nyingi nchini ziweze kutambua hati miliki za kimila ili kuwawezesha  wananchi kujikwamua kiuchumi wakitumia hati zao kama dhamana ya mikopo. Azma hiyo imekuja baada ya kuona mafanikio ya kupima na kurasimisha Ardhi katika Wilaya tatu za mfano za Kilombero,Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro kulikofanywa na wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LTSP).

Akizumgumza baada ya kutembelea Wilaya za Kilombero na Ulanga akiambatana na wafadhili Wa mradi Wa LTSP ili kuona hatua za utekelezaji Wa mradi,Naibu Katibu Mkuu Wa wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mathias Kabundugulu amesema Mradi huo umetekeleza kwa vitendo Sera ya wizara ya miaka mitano. Amesema kwa kipindi cha miaka miwili toka kuanzishwa kwa mradi Wa LTSP mwaka 2016 mafanikio makubwa yameonekana kwa zoezi kwenda kwa haraka zaidi na wananchi wengi kupata hatimiliki za kimila na za vijiji na hiyo ni kutokana na kwenda na teknolojia mpya ya upimaji ya kutumia simu tofauti na teknolojia waliyoanza nayo ikiwemo ya kutumia GPS.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa pia amebaini  wananchi katika Wilaya hizo wameupokea vizuri mradi na wameonyesha matumaini na imewapanua kiakili hasa baada ya kuelewa kuwa hati hizo wanaweza kuchukulia mkopo baada ya baadhi ya benki kuanza kuzipokea na kuwapatia mikopo. Hata hivyo Kabundugulu ameonyesha kufurahishwa baada ya kuona akinamama wengi kumiliki hati na kusema kuwa serikali wanajivunia kwani wanaweza kumiliki nguvu ya kiuchumi.

Akizungumzia Mpango Wa wizara kulitunza Bonde LA mto Kilombero,Kabundugulu amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya Maliasili na utalii wiki ijayo watatuma timu ya wapimaji na kuweka kambi katika vijiji vyote vyenye muingiliano Wa mipaka na eneo la hifadhi ili kuweka mipaka na kuwaondoa wavamizi wote ili kunusuru eneo hilo ambalo asilimia 65 ya Maji yake yanaingia katika mto Rufiji.

Naye Mkuu Wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya amesema mradi umekuwa na faida kwa wananchi Wa Wilaya yake kwani umemaliza migogoro ya wakulima na wafugaji sambamba na kupunguza migogoro ya mipaka baina ya kijiji na kijiji.

Kwa upande wake Mratibu Wa mradi Wa LTSP Godfrey Machabe amesema toka kuanza kwa mradi wamejaribu kutumia teknolojia tofauti ili kuendana na kasi ya kupima na kuwapatia hati wakazi Wa Wilaya hizo na teknolojia  ya kutumia simu ndio imekuwa na mafaniko makubwa na ana imani ikiendelea kutumika itasaidia kurahisisha upimaji katika maeneo mengi nchini. Machabe ametaja mafanikio ya mfumo Wa kutumia simu kuwa toka waanze kuutumia takribani kwa siku katika wilaya hizo wanazalisha vipande vya Ardhi 1800 tofauti na zamani walipotumia mifumo mingine walikuwa wakizalisha vipande vya Ardhi 400 tu kwa Siku.

Rais Magufuli akutana na Wajasiriamali wa Feri Jijini Dar es Salaam na awachangia shilingi Milioni 20

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 01 Oktoba, 2018 ameahidi kutoa shilingi Milioni 20 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya wajasiriamali wa eneo la Feri katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam na ameahidi kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao.

Mhe. Rais Magufuli amekutana na Wajasiriamali hao ambao wanajumuisha Wavuvi Wadogo na Mamalishe wakati akiwa katika mazoezi ya jioni pamoja na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli ambaye pia amewachangia wajasiriamali wanawake shilingi Milioni 5.

Pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli, wajasiriamali hao wameomba awasaidie wasifukuzwe na Manispaa ya Ilala katika eneo hilo, na badala yake wawekewe utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao.

Pia wameomba waondolewe ushuru unaotozwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kwa mitumbwi ya wavuvi wadogo wa samaki, kama ambavyo Serikali imewaondolea ushuru wakulima wanaopeleka sokoni mazao yasiyozidi tani moja.

Aidha, Wajasiriamali hao wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kuiongoza nchi na kushughulikia kero za Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwatembelea na kuwasikiliza kwa mara ya pili.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi maombi ya Wajasiriamali hao na amewapongeza kwa juhudi zao za kujitafutia kipato.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
01 Oktoba, 2018

NAIBU WAZIRI OLE NASHA AITAKA KAMPUNI YA UJENZI KUWASILISHA MICHORO NDANI YA WIKI MOJA

0
0

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipokea taarifa ya Elimu ya Mkoa wa Ruvuma kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Elimu Mkoi huko.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa mwalimu wa somo la uchomeleaji (welding) Onesmo Pela katika Chuo cha Ufundi Veta Songea .
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo Wilayani Ruvuma

………………………………

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ametoa wiki moja kwa mtaalamu Elekezi wa Kampuni ya Archquants Service Limited kuhakikisha inawasilisha michoro ya kazi za nje ya Chuo cha ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Namtumbo kilichopo Mkoani Ruvuma ili ujenzi wa chuo hicho uweze kukamilika.

Mheshimiwa Ole Nasha ametoa agizo hilo wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho ambapo amesema ucheleweshwaji wa michoro hiyo unapelekea kuchelewesha ukamilishaji wa mradi huo.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kuhakikisha wanaanzisha kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro mechanics) katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Songea ili kupata vijana wengi watakaosomea fani hiyo.

Naibu Waziri amesema ukanda wa Nyanda za Juu Kusini unategemea sana kilimo, hivyo kuanzishwa kwa kozi hiyo kutasaidia wananchi wengi kupata uelewa wa kina kile wanachokisoma na baadae kutekeleza kwa vitendo.

“Serikali inatilia mkazo Elimu ya ufundi na imejielekeza katika kuhakikisha inapanua fursa ya vijana wengi kupata Elimu ya ufundi na ndio maana Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuweka Vyuo vya VETA katika kila Wilaya na Mkoa,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha

Naibu Waziri Ole Nasha yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayasni na Teknolojia

OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA

0
0
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ametoa wiki moja kwa mtaalamu Elekezi wa Kampuni ya Archquants Service Limited  kuhakikisha inawasilisha michoro ya kazi za nje ya Chuo cha ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Namtumbo kilichopo Mkoani Ruvuma ili ujenzi wa chuo hicho uweze kukamilika. 

Mheshimiwa Ole Nasha ametoa agizo hilo wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho ambapo amesema ucheleweshwaji wa michoro hiyo unapelekea kuchelewesha ukamilishaji wa mradi huo. 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kuhakikisha wanaanzisha kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro mechanics) katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Songea ili kupata vijana wengi watakaosomea fani hiyo. 

Naibu Waziri amesema ukanda wa Nyanda za Juu Kusini unategemea sana kilimo, hivyo kuanzishwa kwa kozi hiyo kutasaidia wananchi wengi kupata uelewa wa kina kile wanachokisoma na baadae kutekeleza kwa vitendo. 

“Serikali inatilia mkazo Elimu ya ufundi na imejielekeza katika kuhakikisha inapanua fursa ya vijana wengi kupata Elimu ya ufundi na ndio maana Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuweka Vyuo vya VETA katika kila Wilaya na Mkoa,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha 

Naibu Waziri Ole Nasha yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayasni na Teknolojia.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (katikati) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,wakielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (katikati) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.pichani kusho ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipewa maelezo kuhusina na maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (wa tatu kulia) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

ORODHA YA PILI WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO YA SHAHADA YA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2018/19

0
0

ORODHA YA PILI WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO YA SHAHADA YA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2018/1

0
0


MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKAZI DUNIANI YAFANYIKA JIJINI DODOMA

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Dkt. Angeline Mabula akitoa Salaam za Siku ya Makazi Duniani katika ukumbi wa Treasury Square – Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala; Bwn. Tutubi Mangazeni, watendaji kutoka Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia kwa makini Salaam za Mhe. Mabula katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani. 
 Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Dkt. Angeline Mabula na baadhi ya Watumishi wa Wizara katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Dkt. Angeline Mabula na Katibu wa Wizara; Bi Dorothy Mwanyika wakisalimiana na baadhi ya wananchi wa eneo la Chang’ombe – sokoni waliojumuika nao katika kufanya usafi wa eneo hilo katika kuadhimisha Siku ya Makazi Duniani.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Dkt. Angeline Mabula na Katibu wa Wizara; Bi Dorothy Mwanyika wakishirikiana na  baadhi ya wananchi wa eneo la Chang’ombe – sokoni na viongozi wa eneo hilo katika kufanya usafi wa eneo hilo katika kuadhimisha Siku ya Makazi Duniani.
 Wadau mbalimbali wakishirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wananchi wa eneo la Chang’ombe katika kufanya usafi katika eneo hilo kuadhimisha Siku ya Makazi Duniani.

TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI

0
0

Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar akitoa hotuba wakati wa hafla ya uzunduzi wa miundo mbinu ya vyoo katika shule ya msingi ya Pugu Kajiungeni ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia mjema, Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, walimu, wanafunzi, Maofisa ma maofisa kutoka taasisi ya HMT

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema( katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Vyoo bora 12 na vyumba Viwili kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaa, Wengine kwenye picha ni mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust (TMT) Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wapili kulia) Mkuu wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni,Ropiana Alponce (Kushoto) pamoja na viongozi wengine, Msaada huo umejengwa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akihutubia wageni waalika katika hafla hiyo.

Wanafunzi wasichana wakipokea baadhi ya zawadi zilizotolewa na marafiki wa taasisi ya HMT wakati wa hafla hiyo.

Mgeni rasmi akikagua miundombinu ya choo cha kisasa kilichojengwa na HMT chini ya mpango wake wa Vyoo Bora kwa Kila shule


Taasisi ya Hassan Maajar Trust (HMT), imeendeleza dhamira yake ya kuboresha mazingira ya shule za msingi nchini, ambapo imekabidhi jengo la vyoo shule ya msingi Pugu Kajiungeni, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam. Jengo hilo lililogharimu jumla ya Shillingi milioni 65,000.00 lina vyumba 12 na sehemu maalumu kwa wavulana -urinals, ambapo vyumba 2 ni kwa ajili ya ya watoto wenye ulemavu na chumba cha staha kimoja (Dignity Room) kwa ajili ya wasichana wenye mahitaji ya staha. 
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar, alikabidhi vyoo hivyo kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi. Rophina Aloyce Kawishe, katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema, ambaye alikuwa mgeni rasmi, walimu, wanafunzi, na wawakilishi kutoka Shirika la Water Aid. 
 
Akiongea katika hafla hiyo, Balozi Maajar amesema “Hii ni mara ya kwanza kwa HMT kujenga vyoo vya shule, na tumefurahia kukamilisha mradi huu wa kwanza. Kwa kipindi kirefu nyuma, HMT ilikuwa inajulikana kwa kampeni yake kubwa ya ‘Dawati Kwa Kila Mtoto’ ambayo imefanikiwa kwa kutoa madawati 10,000, na kunufaisha zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 nchini. 
 
Tuliona vilevile vile kuna changamoto ya uhaba wa vyoo mashuleni. Imekuwa fursa nyingine ya Taasisi ya HMT na wafadhili wake kuunga nguvu kwa pamoja kwa kampeni mpya yenye kauli mbiu, Vyoo Bora Kila Shule. Aidha amesema, kila safari ni hatua ya kwanza na kwa mradi huu ndiyo hatua ya kwanza kwa HMT kutimiza lengo la kujenga vyoo shule za msingi zilizo na mahitaji na hasa shule zilizo na idadi kubwa ya wanafunzi wenye ulemavu. 
 
Alisema Kupitia hafla tofauti za ukusanyaji fedha kama vile ‘Fundraising Gala’ na ‘Matembezi ya Hiyari’, HMT kupitia kampeni ya Dawati kwa kila Mtoto ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha umma kuona kuwa wajibu wa kuboresha mazingira ya shule zetu si wa serikali pekee na kuweza kuchangia madawati hadi pale serikali ilipolivalia njuga tatizo lile. Kwa HMT ni faraja kubwa kuona idadi kubwa ya watoto wetu siku hizi wakiwa hawakai tena chini. 
 
Kwa kampeni mpya, Vyoo Bora Kila Shule HMT inakusudia kuwasha tena mshumaa kuangazia tatizo la vyoo kwa kuhamasisha umma kuchangia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi zilizo na wanafunzi wengi na vyoo vichache. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema, aliipongeza, HMT, kwa kuamua kuzikabili changamoto za kuboresha mazingira ya elimu kwa kutoa misaada ya madawati, huduma za maktaba na kujenga miundombinu ya vyoo. 
 
“Kwa niaba ya serikali nawapongeza kwa jitihada mnazofanya kuboresha mazingira ya kupata elimu mashuleni” alisema. Taasis ya WaterAid wameisaidia shule kwa kuipa vifaa vya kuvunia maji ya mvua, jambo ambalo limeongeza ubora wa vyoo vilivyojengwa na HMT kwa sababu mazingira ya vyoo yatakuwa masafi naya afya zaidi. 
 
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Pugu Kajiungeni, Bi. Rophina Aloyce Kawishe, ameishukuru taasisi ya HMT kwa kutoa msaada huo ambao alisema utawezesha wanafunzi wa shule hiyo kusomea katika mazingira rafiki kutokana na kuwa na miundombinu bora ya vyoo na madarasa “Ukosefu wa vyoo vya kutosha kwa muda mrefu imekuwa ni changamoto kubwa katika shule zetu, tunawashukru kwa msaada huu”, alisema. 
 
Taasisi ya Hassan Maajar inafanya maandalizi ya kujenga majengo mengine mawili ya vyoo shule za msingi Nia Njema na Majengo zilizoko Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi huu wa kumi na HMT imetenga kiasi cha Shillingi 140 Milioni kwa ajili ya ujenzi huo. 
 
Taasisi ya HMT inajulikana zaidi kwa kampeni yake ya Dawati kwa Kila Mtoto ikiwa ni makakti wa kutimiza ndoto yake ya kuboresha mazingira ya kusomea katika shule za msingi nchini. Tangu kuanzishwa kwake, imekuwa ikihamasisha umma na kuchangia madawati, kuboresha maktaba na kutoa vitabu, na hasa kwa watoto wa madarasa ya awali ili kujenga tabia ya kujisomea, vile vile kuongeza ufahamu juu ya changamoto zinazowakabili wanafunzi wakiwa shuleni. 
 
HMT inajivunia mafanikio kwa kuona hamasa kwa watu binafsi, mashirika ya umma na hadi serikali kuamua kulivalia njuga tatizo al upungufu wa madawati shuleni. Kwa kampeni hii mpya Vyoo Bora Kila Shule, HMT ina imani watu wengi wataendelea kuhamasika kushiriki kwa kutambua kuwa ni jukukumu letu sote kuondoa tatizo la vyoo mashuleni na siyo tu kazi ya serikali peke yake.

OKTOBA 1 YA KILA MWAKA NI MWEZI WA ROZARI TAKATIFU

0
0
Na Mwandishi Wetu Globu ya Jamii

WAUMINI wa Kanisa Katoliki Duniani kote leo wameanza kusali Rozali Takatifu ikiwa kila mara husali lakini kwa mwezi huu inawalazimu kusali zaidi na unajulikana ni Mwezi wa Rozali.

Katika Kalenda ya Kanisa katoliki leo waumini wote wameanza kusali Rozari Takatifu kwa mujibu wa imani ya kanisa katoriki.Hivyo waumini wa Kanisa katoliki wanaalikwa kusali Rozari takatifu kila mara.

Oktoba ni mwezi ambao umewekwa kwaajili ya Bikira Maria na mama wa Kanisa waumini wa kanisa hilo leo wanasali Sala mbalimbali kwa mwombezi Bikira Maria.

HISTORIA YA ROZARI

Ni kwamba sala ya Rozari inasemekana kuanzishwa na Mt. Dominico aliyezaliwa mnamo mwaka 1170 na kufariki mwaka 1221 na hiyo sala Mt. Dominico aliipata kwa njia ya ufunuo ambapo Bikira Maria alimtokea na kumwamuru awe anasali rozari.

 Bikira Maria alimwamuru mtakatifu Dominico kusali rozari kwa kipindi hicho iwe kama silaha yake ili kupambana na uzushi uliokuwa umeibuka ukipingana na mafundisho ya Kanisa, na huo uzushi uliitwa ‘ Albigensia’ hili ni kundi lilokuwa na imani kuwa Duniani kuna nguvu nguvu mbili zenye uwiano sawa lakini hupingana na kupigana moja baada ya nyingine, nazo nguvu hizo ni Mungu na Shetani.

 Hivyo waliamini kabisa kuwa Mungu na Shetani wana nguvu sawa ( Dualistic ).Pia  waliamini kuwa dunia hii imejaa uovu kwa kuwa iliumbwa na mwovu. Ni kwa msingi huu Kanisa liliamua kupambana na hawa wazushi ambao pia walionekana kupotosha mafundisho ya Kanisa.

 Ndipo tunaona Bikira Maria anamtokea Mtakatifu Dominico na kumwambia asali rozari ili kupambana na mafundisho hayo ya kizushi. Ni Papa Pio V ambaye mnamo mwaka 1569 alihidhinisha rasmi kusali rozari kwa kanisa nzima na kuhidhinisha rozari iwe jinsi tunavyoiona sasa. 

Katika zile zama za kati watawa wamonaki walizoea kusali zaburi 150, na kwa upande wa waumini Walei ambao kwa kipindi hicho hawakujua kusoma zaburi iliwabidi wasali sala ya Baba yetu mara 150 badala ya zaburi 150 na hizo baba yetu walizisali kwa kuhesabu punje 150 zilizokuwa zimefungwa kwenye kamba ndefu ambayo kwa lugha ya kitaalamu iliitwa “ Corona” au kwa Kiingereza “ Crown” kadiri ibada kwa Bikira Maria ilivyoendelea kushamiri mnamo Karne ya 12, sala kwa Bikira Maria ilianzishwa na hivyo kuanza kusali salamu maria 150 baadala ya baba yetu 150.

Salamu Maria 150 hapo baadaye zilikuja kugawanywa katika makundi/ mafungu na Mtawa mdominica aliyeitwa Henry Kalkar ( 1328-1408), ambapo kila tendo la rozari lilikuwa na mafungu 50 ya salamu Maria ambapo pia kila fungu liligusia maisha ya Bikira Maria na Yesu katika historia ya wokovu wetu. 

Zaidi ya hapo mtawa mwingine wa mdominican aliyeitwa Alanus de Rupe aliendelea kugawanya hiyo historia ya matendo ya wokovu wetu katika matendo ya furaha,uchungu, nautukufu kama tunavyoyaona sasa. (NB Matendo ya mwanga hayo ni ya majuzi siyo ya wakati ule). 

Na ni kuanzia hapo Bikira Maria amepewa nafasi kubwa katika shirika la watawa wa Dominican. 

Hivyo utamaduni wa kusali rozari umeendelea karne hata karne, mfano Papa Leo XIII (1878-1903) aliweka msisitizo mkubwa juu ya ibada ya rozari kwa Bikira Maria. 

Kuanzia Septemba 1 mwaka 1883 Baba Mtakatifu Leo XIII aliandika jumla ya barua za kichungaji 11 zote zikiwa zinaweka mkazo juu ya rozari.

 Hivyo Rozari ni sala inayotokana na maandiko matakatifu( Biblia).

 Mafumbo ya rozari yote yanapatikana katika agano jipya ambapo ndo tunaona matendo ya Bikira Maria na Yesu Kristo katika wokovu wetu.

Waumini wanakumbushwa uchungu aliopata Bikira Maria Katika maisha yake hasa ule utabiri wa Simeoni kwa Bikira Maria juu ya mateso na kifo cha mwanae Yesu, Matendo saba ya furaha kwa Maria ambapo yaananza na kupashwa habari kwa Bikira Maria na Malaika wa Bwana, kupalizwa mbinguni, na matendo ya huruma ya Bikira Maria kwa wale ambao wanaendelea kuteseka hapa duniani.

BODABODA ZINAZOINGIA KATIKATI YA JIJI LA DAR SASA KUKIONA-KAMANDA MAMBOSASA

0
0
*Ndani ya saa 24 zakamatwa 104, wahusika kufikishwa mahakamani


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limeanza operesheni maalumu ya kukamata bodaboda zote zinazoingia katikati ya Jiji ambapo ndani ya saa 24 wamekamata pikipiki 104.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu operesheni ambazo wanazifanya.

Amefafanua Polisi wameanza operesheni ya kukamata waendesha bodaboda ambao wanaingia katikati ya mji wakati wamezuiliwa kuingia mjini.Kamanda Mambosasa amesema baadhi ya bodaboda ambazo zimekamatwa zimetokana na makosa ya kutovaa kofia ngumu kwa wanaoendesha,kupitia njia tofauti na utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria na kupakia mishikaki.

"Ni marufuku bodaboda kuingia katikati ya Mji,hatuwezi kuacha hilo likaendelea kufanyika.Walishakatazwa kuingia katikati ya mji." Mbali ya kuwakamata wanaiongia mjini pia tunaendelea na operesheni ya kukamata bodaboda ambazo zinatumika kutenda matukio ya uhalifu.Pia tutakamata bodaboda ambazo wanaoziendesha wanashindwa kufuata sheria za usalama barabarani.

*Bodaboda zimekuwa kero kubwa kwa wananchi kwani wamekuwa wakichangia kusababisha ajali kwa kupitia barabara ambazo haziruhusi.Barabara ya kwenda wao wanaitumia kwa kurudi tena wakiwa wamebeba mishikaki."Wengine wanapita hapa hapa nje Ofisi za Jeshi la Polisi na hawana wasiwasi.Tunajua tunapozungumzia bodaboda kunakuwa na maneno mengi lakini lakini niseme watu wafuate maelekezo ambayo tunayatoa," amesema Mambosasa.

Ameongeza kutokana na operesheni hiyo wameshakamata bodaboda 104 kutokana na makosa mbalimbali likiwamo la kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.Pia amesema kwamba kuna baadhi ya waendesha bodaboda kabla ya kufanya makosa wanaandaa faini na kisha wanalipa.Hivyo amesema inaonekana faini zimezoeleka na hivyo wahusika watapelekwa mahakamani.

Wakati huo huo Mambosasa amesema Polisi kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) wamefanikiwa kukamata watu 60 ambao wanatuhumiwa kujihusisha na kuhujumu miundombinu ya umeme na kujiunganishia umeme bila itaratibu na kuchezea mita za Luku.Kamanda Mambosasa amesema wapo ambao wamefikishwa mahakamani na wengine wanaendelea kuhojiwa na kisha watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Amesema kuwa wanaojihusisha na kuhujumu miundombinu ya umeme wafahamu opereshenii hiyo ni endelevu na kwamba watakaoendelea wajue wao ni wafungwa watarajiwa kwani hatabaki salama.

KESI UTAKATISHAJI FEDHA DHIDI YA ALIYEKUWA MHASIBU TAKUKURU YAKWAMA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

KESI  ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake halali, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai na wenzake wanne, imeshindwa kuendelea kusikilizwa  sababu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina hela ya kuwaleta mashahidi.

Wakili wa Serikali, Pius Hila akisaidiana na wakili kutoka Takukuru, Vitalis Peter ameeleza hayo, leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba,  kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Wakili Hilla amedai walishaita mashihidi  kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam lakini wameshindwa kufika kwa kuwa Mtendaji wa Mahakama hakuwa na fungu la  fedha, kwa  ajili ya kuwalipa.Ameendela kueleza kwa sasa wamepata  kibali kutoka kwa  Mtendaji wa Mahakama ambacho kinawaelezea kuwa malipo yatasubiri fedha zitakapoingia lakini mashahidi wameshindwa kuja kwa  gharama zao wenyewe.

"Mheshimiwa hakimu kutokana na hali hiyo, tunaomba terehe fupi kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi hii," ameeleza Hilla.Kutokana na maelezo hayo, Wakili wa Utetezi Alex Mgongolwa aliwasilisha maombi mawili mahakamani hapo.

,"Mheshimwa, tunaomba jitihada za kuwapata mashahidi hao waliopo nje ya mkoa wa Dar rs Salaam ziendelee na pia  ni rai yetu kwa  mahakama upande wa mashtaka walete mashahidi ambao hawahitaji kuombewa kibali na hawatoki nje ya mkoa wa Dar es salaam ili Kesi hii iweze kuendelea," amedai Wakili Mgongolwa.

Kutokana na hayo, Hakimu Simba amesema, mahakama itazungumza na Mtendaji wa Mahakama ili kutafuta fedha sehemu yoyote ili mashahidi hao waweze kuja mahakamani na kutoa ushahidi kwa sababu kesi hiyo ni ya muda mrefu.Kesi imeahirishwa hadi  Oktoba 15 na 16, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Mpaka sasa ni shahidi  mmoja wa upande wa mashtaka, Ayoub Akida(52) ambaye ni Ofisa Utumishi Mkuu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ameshatoa ushahidi wake dhidi ya Gugai.Mbali na Gugai, washtakiwa wengine, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zisizoendana na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbali mbali.Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali zisozoendana na kipato chake, analodaiwa kutenda kati ya January 2005 na Decemba 2015.

 Akiwa ofisa wa umma ameajiriwa na TAKUKURU alikutwa akimiliki mali za zaidi ya Sh. bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa

SERIKALI YANUNUA MA SHINE ZA MIONZI ZENYE THAMANI YA BILIONI 1.74

0
0


Na.WAMJW, Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua mashine za Mionzi (digital X-ray) zipatazo kumi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea mashine hizo kwenye Bohari ya Dawa(MSD)  jijini hapa.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikaki inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwa ni lengo  la kuhakikisha huduma za afya zinawafikia watanzainia wote karibu na maeneo wanayoishi.

"Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali,hivyo tunaboresha na kuimarisha huduma za tiba na uchunguzi wa magonjwa katika hospitali zetu kuwa na vifaa vya kisasa zaidi na kuondokana na utaratibu wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi".Alisema,Waziri Ummy Mwalimu.

Alisema mashine hizo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa 10 ambazo X-ray za zamani zimekwisha muda wake na zimekua zikiharibika mara kwa mara.

Alizitaja hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi,Morogoro,Njombe,Ruvuma,Simiyu na Singida pamoja na hospitali  za Wilaya ya Magu na Nzega.

Aidha,Waziri Ummy alisema katika bajeti ya mwaka 2018/2019, Wizara yake imepanga kununua mashine za mionzi nyingine zipatazo ishirini na nne(24) zenye thamani ya shilingi bilioni 4.1 ambazo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za Mikoa na Wilaya ambazo hazina au zina X-ray za kizamani au chakavu.

Akizungumza kwa niaba ya Waganga Wakuu wa hospitali   zinazopelekwa mashine hizo,Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana Dkt.Mashack Shimwela alisema ujio wa mashine hizo za kisasa zitasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa uchunguzi  za mionzi pia utunzaji wa mazingira tofauti na aina zilizokuwa zikitumika mwanzo

Aidha,alisema mashine hizo zina ubora wa picha  pia ina mifumo ya Tehama ambayo ni rahisi kusomwa hata nje ya hospitali husika endapo hakuna msoma picha 

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akionesha baadhi ya mashine za mionzi  10 zilizonunuliwa na Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na kusambazwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa.
 Waziri Ummy akiongea na vyombo vya habari wakati wa kupokea mashine hizo za mionzi (digital X-ray) ambazo zitaboresha huduma za afya nchini hususani za uchunguzi wa mionzi
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt.Mashack Shimwela,akiongea na waandishi wa habari baada ya kupokea mashine hizo(picha zote na Wizara ya Afya)

MAHAKAMA YAGOMA KUFUTA KESI YA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI AVEVA,NYANGE

0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haiwezi kifuta kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange maarufu Kaburu sababu kesi hiyo imeishafikia hatua ya usikilizwaji wa awali.

Badala yake Mahakama kwa mara nyingine, imetoa amri na kuwapa siku 14 upande wa mashtaka kutekeleza amri iliyoitoa ya kuwataka aidha wafute mashtaka dhidi ya Zacharia Hanspoppe na mfanyabiashara, Franklin Lauwo au wabadilishe hati ya mashtaka kwa kuwaondoa washtakiwa hao ili kesi isikilizwe.

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kutokana na ombi la mawakili wa washtakiwa hao wakiongozwa na Nehemia Nkoko kuiomba mahakama ifute kesi hiyo kwa sababu upande wa mashtaka wameshindwa kuiendesha.

Akisoma uamuzi huo hakimu Simba amesema amepitia hoja za pande zote mbili na ameona kuwa, huu si muda muafaka wa kufuta kesi hiyo kwa sababu tayari ilikuwa katika hatua ya (PH) na pia ilishatoa amri ambayo bado haijatekelezwa.Hakimu Simba amesema upande wa mashtaka wanatakiwa watekeleze amri iliyotolewa Mei 12 mwaka ,2018, kwa hiyo haiwezi kufuta kesi hiyo, kwa sababu itafuta hadi amri ambayo tayari ilishaitoa na haijatekelezeka.

"Si muda mwafaka wa kufuta kesi hii, natoa siku 14 kuanzia kesho kwa upande wa mashtaka kufanya mabadiliko na kama hawatafanya hivyo, Mahakama inaweza kuamua vingine itakavyoona inafaa, " amesema Hakimu Simba.Aidha Hakimu Simba ametaka amri hiyo itekelezeke kwa sababu hawajulikani ni lini Hansoppe na Lauwo watakamatwa  wakati Aveva na Kaburu wapo mahabusu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 16 mwaka 2018 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa PH.Awali, Wakili wa utetezi, Nkoko aliomba Mahakama hiyo iwafutie mashtaka, washtakiwa hao kwa sababu wameshindwa kuiendesha kesi hiyo.Akijibu hoja hiyo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi akisaidia na Wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai,  aliiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa sababu bado wanaifanyia kazi amri waliyopewa na mahakama ya kumtafuta Hanspope na Lauwo.

Amedai Septemba 14 mwaka huu, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa wanawatafuta Hanspope na Lauwo jambo ambalo ni moja ya utekelezaji wa amri iliyotolewa na mahakama.

Katika kesi hiyo washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 10 likiwemo la kula njama, matumizi mabaya na kughushi nyaraka ikionyesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli.

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA WATENDAJI WA OFISI YAKE KUJADILI UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2015-2020 NA MAAGIZO YA MHE.RAIS JIJINI DODOMA.

0
0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi hiyo (hawapo pichani) alipokutana nao kujadili utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 na Maagizo ya Mhe. Rais Dkt.John Magufuli aliyoyatoa katika kikao cha kufungua Bunge la kumi na moja la tarehe 20 Novemba 2015 kilichofanyika Ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma Oktoba 1, 2018 Kulia kwake ni Naibu wake anayeshughulikia wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa na kushoto kwake Mhe.Anthony Mavunde anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana.
PC 2
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi hiyo wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Maagizo ya Mhe. Rais aliyoyatoa katika kikao cha kufungua Bunge, Jijini Dodoma.
PC 3
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akielezea jambo kwa Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vya Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa Kikao kazi hicho.
PC 4
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Peter Kalonga, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, akiwasilisha hoja kwa Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vya Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa kujadili utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 na Maagizo ya Mhe. Rais Dkt.John Magufuli aliyoyatoa katika kikao cha kufungua Bunge la Kumi na Moja Novemba 2015.
PC 5
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakisililiza maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokutana nao kujadili utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na Maagizo ya Mhe. Rais aliyoyatoa katika kikao cha kufungua Bunge la tarehe 20 Novemba,  2015.

PC 6
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakisililiza maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi hicho.

PC 7
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia uwasilishwaji wa hoja kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi hicho.
PC 8
Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Maagizo ya Mhe. Rais aliyoyatoa katika kikao cha kufungua Bunge la kumi na moja la tarehe 20 Novemba, 2015 walipokutana Oktoba 1, 2018 Dodoma.

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YASAINI MKATABA WA UTENDAJI KAZI NA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA

0
0

TANZANIA YAFANIKIWA KUPAMBANA NA RUSHWA NA KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI KWA ZAIDI YA BILIONI 500

0
0







Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Utumishi,George Mkuchika
Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa hapa nchini na kufanikiwa kuongeza Makusanyo ya serikali kwa mwezi kutoka sh,Bilioni 800,000 na kufikia sh, Trillion 1.3 katika kipindi cha miaka minne. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Utumishi,George Mkuchika wakati alipokuwa akifungua mkutano wa nchi wanachama wa Afrika ,ulioandaliwa na umoja wa Afrika kupitia bodi maalumu ya ushauri kuhusu Masuala ya Mapambano ya Rushwa (AUABC).Hayo yameelezwa mapema Leo jijini Arusha na w

Mkuchika amesama kuwa mafanikio dhidi ya vitendo vya Rushwa yameipaisha kimataifa Tanzania na kuwa nchi ya pili Katika nchi za Afrika mashariki ikiongozwa na nchi ya Rwanda katika kupambana na rushwa. Amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi binafsi za serikali katika kudhibiti Mianya ya rushwa,ikiwemo suala la utoaji wa risiti za elekroniki ,kuzuia utoroshwaji wa Mali Asili za Nchi na kudhibiti matumizi ya serikali. “Tanzania imeanza kuonja matunda ya kupambana dhidi ya rushwa baada ya jamii kuanza kuelewa umuhimu wa kuichukia rushwa na tumefanikiwa kuongeza mapato ya serikali kutoka kiasi cha sh, bilioni 800 hadi Trillion 1.3 kwa mwezi”Amesema Mkuchika. 

Aidha amezitaka nchi za Afrika kuiga mfano huo ili nchi hizo ziweze kuwa na kuwa na kauli moja katika mapambano ya kweli dhidi ya vitendo vya rushwa na kuyafanyiakazi kwa vitendo maadhimio Yale yote ya kwenye mikutano yao pale wanapokutana .Hata hivyo Amesema nchi nyingi za Afrika zimekuwa nyuma kuhusu suala la mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na kupelekea nchi zao kukosa maendeleo . 

Awali Mhadhili idara ya taaluma za Rushwa kutoka chuo kikuu cha St.John’s tawi Dodoma, dkt.Alfred Sebahene Amesema tatizo la vitendo vya rushwa bado ni kubwa kwa nchi nyingi za Afrika na baadhi ya nchi zimekwama kulitokomeza kutokana na mifumo iliyopo ikiwemo Migogoro ya ndani. 

Amesema mkutano huo utatoa dira na mwelekeo wa vitendo vya rushwa kwa nchi za Afrika ambapo pamoja na mambo mengine watatoa mkazo kwa nchi hizo ili kuhakikisha suala la rushwa linapigwa vita kika kona kwa nchi za Afrika.
Mkutano huo wa Umoja wa Afrika umeyakusanya mataifa takribani 25 kutoka.nchi mbalimbali za Afrika ukiwajumuisha wadau wa rushwa,watafi na wataalamu mbalimbali ukiwa na lengo la kupima mafanikio kwa nchi hizo dhidi ya vitendo vya rushwa
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images