Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT: Mkurugenzi Mtendaji mpya Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akaribishwa rasmi ofisini kwake

0
0
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB  Bw. Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles. Kimei (kulia) wakati alipowasili rasmi kazini kwa siku ya kwanza leo Oktoba 1, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Bw. Ally Laay.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akipokea vitendea kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles Kimei wakati alipowasili rasmi kazini kwa siku ya kwanza, Oktoba 1, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles Kimei (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, (wa pili kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji,

PROFESA NDALICHAKO AWATUMBUA WAWILI WIZARANI KWAKE

0
0
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

WAZIRI Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwaondoa kwenye vyeo vyao Mratibu wa Miradi na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu kwa kushindwa kusimamia majukumu yao na kupelekea baadhi ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati.

Aliwataja viongozi ambao wanatakiwa kuondolewa katika nafasi zao na kuondolewa katika Wizara hiyo ni Mratibu wa Miaradi kuwa ni Fredrick Shuma na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu Basiliana Mrimi.

Profesa Ndalichako alitoa kauli hiyo jana wilayani Nzega wakati akikagua mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu Ndala na kukutana miradi hiyo iko katika hali isiyoridhisha. Alisema utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu cha Ndala hauridhishi na kusababisha kushindikana wanachuo wengi kuanza katika mwaka huu wa masomo.

Profesa Ndalichako alisema watendaji hao ni miongoni mwa waliosababisha vifaa kwa ajili ya vyuo vya ualimu vya sayansi kupelekwa katika vyuo ambavyo havifundishi sayansi na kupelekea baadhi kupitwa na wakati na kusababisha hasara kwa Serikali. o Aidha Waziri huyo ametoa onyo kwa Mhandisi wa Wizara hiyo George Sambali kwa kushindwa kukagua miradi ya ujenzi inayoendelea hadi wasubiri Waziri na Naibu wake watembelea ndio nao waonekana jambo ambalo linasababisha kujengwa kwa miradi ambayo sio mizuri na inachukua muda mrefu.

Alisema suala la kuhakiki ubora wa miradi ni kazi ya wataalamu na sio kungoja viongozi waendele ndio marekebisho yafanyike jambo linalosababisha baadhi ya miradi kuchelewa. Profesa Ndalichako alimwonya Mkuu wa Chuo cha Ualimu Ndala Abinego Ndikumwe kutopokea majengo yaliyokarabatiwa na United Builders ambayo yameonyeshwa huku yakiwa na mapungufu mengi.

Alisema kabla ya kuyapokea wahakikishe wahusika wamefanyia kazi mapungufu yote na kufikia Mwezi Novemba wakabidhi kazi ikiwa imekamilika. Kuhusu Kampumi ya Unite Builders ambayo inakarabati na kujenga baadhi ya majengo ameitaka kuhakikisha inakabidhi kazi ifikapo Novemba ikiwa katika hali nzuri na kuongeza nje hapo hawatapa kazi yoyote ya Serikali.

Alisema majengo ambayo watajenga lazima yaonyeshe thamani ya bilioni 3.1

LUGOLA ASEMA POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA

0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza mwananchi wa Kijiji cha Basanza Wilayani Uvinza, mkoa wa Kigoma, alipokua aamuuliza maswali, baada ya Waziri huyo kuwataka wakazi wa kijiji hicho kutoa kero mbalimbali zinawakabili wilayani humo. Lugola pia alisema dhamana hizo zinapaswa kutolewa saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko alipokua anatoa taarifa yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Lugola aliwataka Polisi nchini watoe dhamana saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko (kushoto) alipokua anatoa taarifa yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Katika hotuba yake kwa maafisa wa Wilaya hiyo, Lugola aliwataka Polisi nchini watoe dhamana saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Felix Mwagara, MOHA-Kasulu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi kutoza fedha kwaajili ya huduma ya dhamana kwa watuhumiwa waliopo mahabusu katika vituo vya polisi nchini.

Lugola pia alisema dhamana hizo zinapaswa kutolewa saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Basanza wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, leo, Waziri Lugola alisema ni marufuku kwa askari yeyote atakayeshindwa kutoa dhamana kwa kosa ambalo lina dhamana.

“Hii tabia sijui imetoka wapi ambayo imejengeka kwa baadhi ya askari polisi, eti mtu akiingia mahabusu ya polisi siku ya Ijumaa ikifika siku ya Jumamosi na Jumapili hawatoi dhamana wakisema dhamana mpaka Jumatatu, hii tabia sio sahihi na ife haraka iwezekananavyo,” alisema Lugola.

Lugola aliwataka wananchi nchini kuhakikisha wanaripoti matukio ambayo yanavunjwa na baadhi ya polisi hao ambao wengi wao wanatengeneza mazingira ya rushwa. “Kuna tabia ambayo imezoelewa katika jamii, eti kuingia polisi ni bure ila kutoka ni fedha, hii kauli nataka ife, kwasababu nawajua polisi na hawanidanyi kwa lolote, hivyo ole wao ambao watawanyanyasa wananchi kuwaomba fedha,” alisema Lugola.

Lugola alisisitiza kuwa, dhamana ni haki ya mtu endapo hilo kosa linadhaminika hivyo mwanachi yeyote atakaeombwa fedha anapaswa kuripoti tukio hilo kwa viongozi wa polisi ili polisi achukuliwe hatua za kinidhamu. Aidha, Waziri Lugola aliwataka maaskari wa usalama barabarani kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi na si kuwaandikia makosa madereva kwa kuwakomoa endapo magari yao yanamakosa.

“Gari likiwa na kosa liandikiwe faini, hilo sina shida nalo, lakini utakuta baadhi ya askari wanaandika makosa mengi ili watengeneze mazingira ya rushwa, hii ssi sahihi ” alisema Lugola

BENKI YA FINCA MICROFINANCE YAZINDUA PROGRAMU YA SHINDANO LA ‘KUZA OFISI NA FINCA’ MSHINDI ATANYAKUA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI KUMI

0
0


Mku wa maswala ya kibiashara wa FINCA microfinance bank Emmanuel Mongella (kulia na mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa benki hiyo Nicholous John wakiongea na waadishi wa habari katika uzinduzi wa programu ya Kuza ofisi na FINCA ilioanza kuonyeshwa na TVE jijini Dares salaam.

…………………………..


Lengo la shindano la TV ni kutoa elimu ya fedha na biashara kwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo

Benki ya FINCA Microfinance inaendelea kuwa benki ambayo inahamasisha ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi ya uwepo wake nchini Tanzania.

 Benki inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania, Benki ya FINCA Microfinance leo imezindua shindano la runinga ambalo lina lengo la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, ufahamu na kisha kuwapatia zaidi ya TZS Millioni 10 kwa wazo bora la biashara litakalokuwa limewasilishwa.

Awali Shindano hilo linalojulikana kama ‘Kuza Ofisi na FINCA’ lilifanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zimeunganishwa kimkakati katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa program katika runinga jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John alisema kwamba lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao. Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo.

“Hii ni Hatua ya pili la shindano ambapo washindani 8 wamechaguliwa na jopo la majaji kushiriki katika kipindi cha TV, ‘Kuza Ofisi na FINCA’ kitakachokuwa kinarushwa kupitia TVE na kuendeshwa na mtangazaji wa Efm Emamnuel Kapanga. Mwishoni mwa shindano, mshindi mmoja mwenye bahati ataondoka na zawadi nono ya zaidi ya TZS milioni 10”, Alisema Nicholous, akiongeza kwamba washiriki wengine wenye vigezo pia watakuwa na nafasi ya kujipatia mikopo kutoka benki hiyo.

Kwa upande wake, mkuu wa maswala ya masoko wa benki ya FINCA Microfinance Benki, Emmanel Mongella amesema: “Kampeni ya Kuza Ofisi na FINCA ni sehemu ya FINCA kusherehekea miaka 20 ya uendeshaji wa shughuli zake nchini Tanzania ambapo benki ya FINCA imekuwa maarufu kwa utoaji wa masuluhisho bora na aina mbalimbali za akaunti, Mikopo na huduma zingine ambazo zinajumuisha mahitaji ya watu binafsi na taasisi.”

Emmanuel pia alisema, “Ushirikishwaji wa Kifedha na Uvumbuzi wa Kidigitali ni msingi wa biashara yetu, shindano hili ni ahadi nyingine ambayo Benki ya FINCA Microfinance inatoa kwa watanzania kwamba iko kwaajili ya kuwasaidia katika misaada ya kifedha kupitia elimu na kuwawezesha wateja wetu kuweza kupata maendeleo endelevu ya biashara zao”.

Akizungumzia maono ya uzinduzi wa programu hii John alisema, “nawasii watu wote waangalie programu hii katika stesheni ya TVE maana kuna mambo mengi ya kufurahisha pamoja na elimu ya biashara”

You Alone (God) - Regina Avit (Official Audio)

0
0

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUKUZA UELEWA WA SHUGHULI ZA JUMUIYA HIYO KWA WANANCHI WAKE

0
0
Zamaradi Kawawa, MAELEZO, Windhoek, Namibia 

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC zinatakiwa kukuza uelewa wa shughuli za SADC kwa wananchi wake kwa kufundisha mashuleni historia ya ukombozi wa nchi hizo pamoja na kutumia wimbo wa SADC na bendera yake kwenye shughuli za kitaifa na kimataifa.

Baraza la SADC la Mawaziri wa nchi wanachama wanaoshughulikia sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na Uchukuzi walikubaliana hayo katika kikao kilichofanyika Septemba 27,2018 Windhoek, Namibia baada ya kufunguliwa na Waziri wa Madini na Nishati wa Namibia Mheshimiwa Tom Alweendo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo.

Kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kilisema wananchi wa SADC wanatakiwa kuelimishwa kuhusu SADC kwa kufahamu historia yake na ukombozi wa nchi wanachama, alama za SADC zikiwemo bendera, nembo, wimbo na itifaki yake kwa kuhusisha elimu hiyo kwenye mtaala wa elimu kwa nchi wanachama.

Akifungua kikao hicho, Waziri wa Madini na Nishati wa Namibia Mheshimiwa Alweendo alisema kuna taarifa nyingi nzuri za kuwaeleza wananchi wa nchi wanachama kuhusu SADC hivyo ni jukumu la Serikali za nchi za SADC kuelimisha na kuwaeleza wananchi wake wakati chombo hicho kkiendelea kujiimarisha.

Kikao hicho cha siku moja kilichokutana kwa lengo la kupitia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya nchi wanachama kwenye maeneo ya sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na uchukuzi kilisimama kwa dakika moja kabla ya kuanza ili kuonyesha masikitiko yao kwa vifo vya watanzania zaidi ya 200 vilivyotokana na ajali ya MV Nyerere Ziwa Victoria, Mwanza.

Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bi. Susan Mlawi kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambaye kwa niaba ya Serikali alipokea salamu za pole kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo kufuatia vifo vya watanzania zaidi ya 200 vilivyotokana na ajali ya MV Nyerere kwenye Ziwa Victoria mkoani Mwanza hivi karibuni.

Aidha, Kikao hicho kiliipongeza Tanzania kwa kupata tuzo ya dunia ya usalama wa anga baada ya kufaulu kwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na Baraza la usafiri wa anga duniani vinavyohusu uhakika wa usalama wa anga.Wakati wa kikao hicho cha baraza la SADC la Mawaziri wa sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na Uchukuzi, Bi Mlawi alieleza nia ya Tanzania ya kupeleka mgombea kwenye nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na kuomba ushirikiano wa nchi wanachama wa SADC wakati wa uchaguzi ukifika.

Alimtaja mgombea huyo kuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr Agnes Kijazi, mwanamke msomi wa ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD) mwenye uzoefu wa miaka 30 kwenye masuala ya hali ya hewa kutoka nchi za SADC.Mheshimiwa Alweendo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho alisema nchi wanachama wa SADC zimepiga hatua kubwa kwenye masuala ya hali ya hewa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya satellite iliyoimarisha kwa kiasi kikubwa matokeo ya utabiri wa hali ya hewa hivyo kuwezesha nchi kukabiliana na majanga ya ukame, mafuriko na moto yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr. Agnes Kijazi ambaye pia alitambulishwa katika kiako hicho aliiambia Idara ya Habari-MAELEZO kuwa Tanzania inajipanga kutekeleza miradi miwili mikubwa ya SADC ikiwemo uboreshaji wa chuo cha yaifa cha hali ya hewa kilichopo Kigoma pamoja na uwekaji wa miundo mbinu ya kisasa ya utabiri wa hali ya hewa itakayoimarisha huduma za utabiri wa hali ya hewa kwa nchi ili kupunguza umaskini. 

Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC ina nchi wanachama 16 zikiwemo Namibia ambaye ni mwenyekiti na Tanzania ni Makamu mwenyekiti wa Jumuiya hiyo. Nchi nyingine ni Zimbabwe, Zambia, Malawi, Afrika Kusini, Botswana, Angola, Msumbiji, Eswati, Lesotho, DRC, Mauritius, Comoro, Seychelles na Moroco.

TIGO FIESTA 2018 – VIBE KAMA LOTE YAJA NA PROMOSHENI YA DATA KAMA LOTE

0
0







Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Tigo, David Umoh (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo katika uzinduzi wa promosheni ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya Tigo *147*00#, katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga.

Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo katika uzinduzi wa promosheni ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya Tigo *147*00#, katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote. Kushoto ni Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Tigo, David Umoh.



Kwa mara ya kwanza msimu wa Tigo Fiesta 2018 waja na promosheni murwa inayompa mteja bonasi la uhakika lenye thamani ya hadi mara mbili ya kifurushi cha intaneti papo kwa hapo.

 Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni murwa kwa wateja wote watakaonunua vifurushi vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#. Mteja atapokea bonasi la uhakika papo kwa hapo lenye thamani hadi mara mbili ya kifurushi cha intaneti atakachonunua katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018.

Akitangaza promosheni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema, “Kuendana na msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, promosheni hii ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa wateja wote wa Tigo wanafurahia maisha ya kipekee ya kidigitali huku wakisambaza matukio ya Tigo Fiesta 2018 mubashara kutoka sehemu yoyote ile ya nchi kupitia mtandao wenye kasi ya juu zaidi wa 4G+.”

Hali kadhalika, Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Katika mikoa yote ya Tigo Fiesta 2018, wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

Tigo ni mtandao unaojulikana kwa promosheni kabambe na ubunifu wa kipekee unaoendana na mahitaji halisi ya soko, hivyo kuifanya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa wateja wake zaidi. Kwa hiyo tumejizatiti kuwapa wateja wetu promosheni bora zaidi katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018. Tunawakaribisha wateja wetu kufurahia ofa hizi murwa.

MSTAHIKI MEYA WA JIJI ALIPOKUTANA NA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE

0
0
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam ,Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ofisini kwakwe Karimjeee jijini hapa.katika mazungumzo hayo Meya Mwita na Mbowe wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapa.Picha na Christina Mwagala ,Afisa habari Ofisi ya Meya qa jiji.




HAKIKISHENI WAFANYAKAZI WANAELEWA WAJIBU NA HAKI ZAO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI-SSRA

0
0
 Mkurugenzi wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter, (kushoto), akimpongeza mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Tathmini, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini (SSRA), Bw. Joseph Mutashubilwa, baada ya kufungua magfunzo ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyowaleta pamoja viongozi na watendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) na kufanyika mjini Morogoro Oktoba 1, 2018.
Bw.Mutashubilwa, (aliyesimama) akitoa hotuba hiyo. Kushoto ni Bw. Anselim Peter na kulia ni Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Bw.Henry Mkunda


NA K-VIS BLOG, MOROGORO

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini (SSRA) Dkt. Irene Isaka, amewataka viongozi na watendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) kuhakikisha wanachama wao wanafahamu wajibu na haki zao katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Dkt. Isaka ameyasema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kwa viongozi na watendaji wa TUGHE taifa na mikoani kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Utafiti na Tathmini SSRA, Joseph Mutashubilwa mjini Morogoro Jumatatu Oktoba 1, 2018.

“Kwa kufanya hivi tutakuwa tunaepusha migogoro na tunadumisha mahusiano sehemu za kazi hali itakayowavutia wawekezaji kuja nchini kwa wingi na hivyo kutimiza dhamira ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.” Alsiema Dkt. Isaka. Dkt. Isaka pia aemwataka washiriki hao wa mafunzo kusambaza elimu watakayoipata kwa kuwatembelea na kuwapa elimu wanachama wa chama hicho na kumtaka kila kiongozi/mtendaji aliyeshiriki awe na mpango kazi utakaoonesha idadi ya wanachama alionao katika eneo lake na namna atakavyowafikishia elimu hii ambayo ni muhimu kwao kuifahamu.

“Nina imani kwa kufanya hivi tutakuwa tumewasaidia kwa kiasi kikubwa wanachama wetu kuujua Mfuko, kazi zake na pia kufahamu nini wanapaswa kufanya baada ya kupata matatizo wakati wakiwa wanatekeleza majukumu ya mwajiri.” Alifafanua. Akinukuu kifungu cha 72 (4) cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, Mkurugenzi Mkuu huyo wa SSRA alisema kifungu hicho chan sheria kinatamka nafasi ya uwakilishi wa vyama katika kamati za afya na usalama mahali pa kazi ambapo mwajiri anatakiwa kutunza kumbukumbu hizo na kamati inatakiwa kukagua ili kuona kama hilo linafanyika.

Hayo yote ni katika kuhakikisha kwamba upo ushirikishwaji wa baina viongozi/watendaji na Serikali katika kulinda afya za wafanyakazi sehemu za kazi. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter alisema, semina hiyo ya mafunzo ni muendelezo wa hatua ya Mfuko kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ambayo ni wadau wa Mfuko na nia kubwa ni kuwajengea uelewa wa madhumuni ya kuanzishwa kwa Mfuko, Sheria na jinsi Mfuko unavyofanya kazi.

Alisema katika kipindi cha miaka miwili tangu Mfuko uanze kutekeleza majukumu yake, kumekuwepo na mafanikio makubwa ya kutimiza jukumu kuu la kuanzishwa kwa Mfuko la kupokea madai na kulipa fidia na hadi sasa Mfuko tayari umekwishalipa fidia zaidi ya shilingi bilioni 4.4. Naye Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Hery Mkunda, yeye alisema, mafunzo hayo yatawezesha kuongeza uelewa kuhusu wajibu wa mwajiri na haki kwa mfanyakazi katika kuelewa sheria hiyo ya Fidia. “Washiriki hawa ambao ni Makatibu wa Mikoa wa TUGHE ambao wao ndio husimamia haki na maslahi ya wafanyakazi sehemu zao za kazi kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria.” Alisema.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter alisema, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, akizunguzma kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter akitoa mada.

Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Hery Mkunda, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo hayo.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
 
 Bw. Peter (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada.
 Mshiriki kutoka TUGHE Kilimanjaro, Simon E Msuya, akizungumza
  Mshiriki kutoka mkoa wa Morogoro, …..akizungumza
 Katibu Mkuu wa TUGHE, Bw. Hery akiuliza swali kuhusu utaratibu wa kutoa mafao kwa mtu aliyepata ajali wakati akitekeleza majukumu ya kazi ya mwajiri
 Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE taifa (Afya) Mhandisi Amani Msuya akizunhgumza
 Mwakilishi toka Mkoa wa Tanga, Bi. Flora C Urassa akiuliza swali.
 Mwakilishi toka Mkoa wa Mbeya, Bi.Janeth Masawe, akiulzia swali.
 Bw. Rugemalira M. Rutatina, akiuuliza swali.
 Mwakilishi toka Mkoa wa Pwani, Bw. Shadrack C. Mkodo akiuliza swali.
 Mwakilishi wa TUGHE Mkoa wa Ruvuma Bw. Athanas B. Tarimo akiuliza swali.
Bw. Steven R. Wadi akiuliza swali, (kulia) ni Msimamizi na mjuongozaji wa semina Bi. Laura Kunenge.

Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Anselim Peter, (kushoto), akibadilishana mawazo na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma, Bw. Mchenya M. John
Meneja wa huduma za Sheria Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Kitandu Ugula (kushoto), akibadilishana mawazo na Afisa Uhusiano na Uhamasishaji Mamlaka hiyo, Bi. Zawadi Msalla
 Meza kuu katika picha ya pamoja kundi la kwanza
  Meza kuu katika picha ya pamoja kundi la pili.
  Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi.

SUKOS KUTOA ELIMU JINSI YA KUJIKINGA NA MAAFA, MAJANGA KWENYE JAMII

0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

TAASISI isiyo ya kiserikali SUKOS inayomilikiwa na Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova imezinduliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kova Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2014  ambayo inatoa , huduma ya uokoaji,usimamizi,uhamasishaji wa jamii kuhusiana na namna ya kukabiliana na maafa ya aina mbalimbali ikiwa ni harakati za kuunga mkono juhudi za Serikali kukabiliana na maafa na majanga .

Kova ameeleza mabadiliko ya nchi yetu kwa sasa   haiwezi kuepukana na majanga na kutokana na uzoefu na  utendaji wake wa kazi na Jeshi la Polisi lilitoa msaada wa hali na mali kuhakikisha wananchi wanarudi Kwenye maisha yao ya kila siku.

 Kova ameyataka  kwa mashirika yasiyo ya Serikali  kusaidia wananchi wanaofikwa na kadhia hiyo ili kupata hifadhi kwa muda pamoja na chakula.Hata hivyo  ametoa pole kwa  ajari iliyotokea Mkoa wa Mwanza kwa kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere mkoani Mwanza Katika Wilaya ya Ukerewe  na kusababisha athari kubwa ya kimaisha na mali katika jamii.

Aidha, amefafanua kazi ya taasisi hiyo ni  kutoa elimu kuhusu namna ya kujiokoa katika maafa ikishirikiana na kampuni ya CocaCola,Taasisi ya Mpango wa Taifa ya Damu salama,na Cops Security.Pia amesema tarehe sita kutakua na  mbio za mwendopole ambazo zitafanya katika Uwanja Taifa kuelekea viwanja vya Jakaya M. Kikwete saa moja asubuh pamoja na tukio la uchangiaji wa damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa hospitalini.

Kova ametoa rai kwa wananchi kujitokeza Oktoba  6 ili kujifunza vingi likiwemo suala la kujikinga na kujiokoa kwenye majanga na maafa yatakayotokea mahali popote .
 

TAIFA STARS YAANZA KAMBI KUJIANDAA DHIDI YA CAPE VERDE KUFUZU AFCON

0
0
Kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaanza rasmi leo kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Africa mwakani dhidi ya Cape Verde.

Kambi hiyo inayoanza leo itaanza na wachezaji wanaocheza ndani kabla ya kuungana na wale wanaocheza nje ya Tanzania.Mazoezi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lager yanatarajiwa kuanza kesho asubuhi kwenye Uwanja wa JKM Park,MNAZI Mmoja.Maandalizi yatakuwa chini ya Kocha Mkuu Emmanuel Amunike,Wasaidizi Hemed Morocco na Emeka Amadi.

Madaktari Dr Richard Yomba na Gilbert Kigadya

Mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 12,2018 kwenye mji wa Praia huko Cape Verde na mchezo wa marudiano utachezwa Oktoba 16,2018 Uwanja wa Taifa.

Kikosi kilichoitwa

Aishi Manula (Simba)
Salum Kimenya(Tz Prisons)
Frank Domayo(Azam FC)
Salum Kihimbwa(Mtibwa),
Kelvin Sabato(Mtibwa)
David Mwantika(Azam FC) 
Ally Abdulkarim Mtoni(Lipuli)
Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )
Beno Kakolanya (Young Africans)
Hassan Kessy (Nkana,Zambia)
Gadiel Michael (Young Africans)
Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini)
Aggrey Morris (Azam FC)
Andrew Vicent (Young Africans )
Himid Mao (Petrojet,Misri)
Mudathir Yahya (Azam FC)
Simon Msuva (Al Jadida,Morocco)
Rashid Mandawa (BDF,Botswana)
Farid Mussa (Tenerife,Hispania)
Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium)
Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan)
Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania)
Yahya zaydi(Azam FC)
Kelvin Yondan (Young Africans)
Paul Ngalema (Lipuli)
Jonas Mkude (Simba)
John Boko (Simba)
Shomari Kapombe (Simba)
Feisal Salum (Young Africans)
Abdallah Kheri (Azam FC)

MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JEKA MIAKA MITANO

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MFANYABIASHARA, Hafidhi Jonggradgorn amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kukiri kutenda makosa wawili likiwemo la kukutwa na madini ya Coloured Gemstones yenye usurp Wa kilogramu 67.76 na thamani ya USD 105.757.

Aidha Mahakama imeamuru madini hayo yataifishwe na wapewe Tume ya Madini. 

Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori kumsomea mashtaka mshtakiwa huyo na alikiri makosa yote.

Akisomewa hati ya mashtaka, imedaiwa Kati ya Januari Mosi 2017 na June 3 mwaka huu maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, nchi za Falme za Kiharabu na India mshtakiwa akiwa si mtumishi wa umma kwa makusudi alifadhili biashara ya mchongo wa jinai kwa lengo la kujipatia faida. 

Katika shtaka la pili, Wakili Nyantori amedai Juni 3 mwaka huu maeneo ya Mikocheni A mtaa wa Chwaku mshtakiwa huyo alikutwa na vito vya madini ya Coloured Gemstones Kilogramu 67.76 yenye thamani ya Dola za Marekani USD 105.757 bila ya kuwa na leseni na uhalali wa kuwa na madini hayo.

Kabla ya kusomewa hukumu hiyo Wakili Nyantori aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali itakayokuwa fundisho kwa wengine wanaofanya makosa kama hayo. Pia ameiomba Mahakama kutoa amri ya kutaifisha madini hayo kwa mujibu wa sheria na kuelekeza yawe chini ya Tume ya madini.

Katika utetezi wake, wakili wa Utetezi Habibu Mwenye anayemtetea mshtakiwa ameiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwani anafamilia inamtegemea na kuwa Mtejatu wake huyo tangu alipoingia nchini mwaka 1989 hakuwahi kufikishwa Polisi wala mahakamani mpaka siku ambapo aliletwa kwa mashtaka hayo, hana rekodi ya uharifu. 

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mashauri alisema mshtakiwa anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine hivyo katika shtaka la kwanza anamuhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni mbili au jela miaka miwili na katika shtaka la pili anamuhukumu faini ya Sh. Milioni tatu au kwenda jela miaka mitatu. 

Hakimu Mashauri amesema Mahakama pia imetoa amri ya kuyataifisha madini hayo na kuyapeleka Tume ya madini. Hata hivyo mshtakiwa huyo alilipa faini na kuachiwa huru.

MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MFANYABIASHARA, Hafidhi Jonggradgorn amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kukiri kutenda makosa wawili likiwemo la kukutwa na madini ya Coloured Gemstones yenye usurp Wa kilogramu 67.76 na thamani ya USD 105.757.

Aidha Mahakama imeamuru madini hayo yataifishwe na wapewe Tume ya Madini. 

Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori kumsomea mashtaka mshtakiwa huyo na alikiri makosa yote.

Akisomewa hati ya mashtaka, imedaiwa Kati ya Januari Mosi 2017 na June 3 mwaka huu maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, nchi za Falme za Kiharabu na India mshtakiwa akiwa si mtumishi wa umma kwa makusudi alifadhili biashara ya mchongo wa jinai kwa lengo la kujipatia faida. 

Katika shtaka la pili, Wakili Nyantori amedai Juni 3 mwaka huu maeneo ya Mikocheni A mtaa wa Chwaku mshtakiwa huyo alikutwa na vito vya madini ya Coloured Gemstones Kilogramu 67.76 yenye thamani ya Dola za Marekani USD 105.757 bila ya kuwa na leseni na uhalali wa kuwa na madini hayo.

Kabla ya kusomewa hukumu hiyo Wakili Nyantori aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali itakayokuwa fundisho kwa wengine wanaofanya makosa kama hayo. Pia ameiomba Mahakama kutoa amri ya kutaifisha madini hayo kwa mujibu wa sheria na kuelekeza yawe chini ya Tume ya madini.

Katika utetezi wake, wakili wa Utetezi Habibu Mwenye anayemtetea mshtakiwa ameiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwani anafamilia inamtegemea na kuwa Mtejatu wake huyo tangu alipoingia nchini mwaka 1989 hakuwahi kufikishwa Polisi wala mahakamani mpaka siku ambapo aliletwa kwa mashtaka hayo, hana rekodi ya uharifu. 

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mashauri alisema mshtakiwa anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine hivyo katika shtaka la kwanza anamuhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni mbili au jela miaka miwili na katika shtaka la pili anamuhukumu faini ya Sh. Milioni tatu au kwenda jela miaka mitatu. 

Hakimu Mashauri amesema Mahakama pia imetoa amri ya kuyataifisha madini hayo na kuyapeleka Tume ya madini. Hata hivyo mshtakiwa huyo alilipa faini na kuachiwa huru.

SPIKA AINDIKIA TUME YA UCHAGUZI KUHUSU KUJIUZULU KWA MBUNGE WA JIMBO LA SERENGETI.

0
0

MV MBEYA KUTATUA CHANGAMOTO ZA USAFIRI ZIWA NYASA

0
0

Meli ya MV Mbeya II ikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi wake kwenye Bandari ya Kyela ambapo inatarajia kukamilika Mwezi Desemba Mwaka huu na itakuwa ikihudumia Abiria 200 na mizigo tani 200 kwenye Ziwa Nyasa.
Baadhi ya mafundi wa ujenzi wa Meli ya MV Mbeya II wakiendelea na kazi hiyo kwenye Bandari ya Kyela Mkoani Mbeya,kukamilika kwa ujenzi wa Meli hiyo kutasaidia usafirishaji wa Mizigo tani 200 na Abiria 200 kwenye Ziwa Nyasa.

Na Leonard Magomba

Kukamilika kwa ujenzi wa meli mpya ya abiria ya MV Mbeya II kunatarajiwa kutatua changamoto za usafiri wa abiria na mizigo katika mwambao wa Ziwa Nyasa.

Meli hiyo ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 80, itakuwa meli ya kwanza ya kisasa ya abiria ambayo itaunganisha mikoa mitatu ya Mbeya, Njombe na Ruvuma pamoja na nchi jirani za Malawi na Zambia.

Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa, Bw. Abed Gallus amesema kwamba ujenzi wa meli hizo ambao unafanywa na kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine, ni moja ya juhudi zinazofanywa na TPA kuboresha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo majini. “Ujenzi wa meli hii ya abiria, ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa meli tatu za TPA katika Ziwa Nyasa zilizolenga kutatua changamoto za usafiri wa abiria na mizigo majini,” amesema Gallus.

Bw. Gallus amesema kwamba TPA, ilianzisha mradi wa meli tatu zikiwemo mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja na moja ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 200. Amesema kwamba miradi hiyo ilitekelezwa kwa awamu mbili tofauti ambapo awamu ya kwanza ilihusisha meli mbili za mizigo, MV Ruvuma na MV Njombe ambazo ujenzi wake ulikamilika mwezi Julai, 2017.

Ujenzi wa meli ya abiria ya MV Mbeya II ambao umefikia asilimia 80 unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Disemba, 2018 na umegharimu kiasi cha Tsh.9 bilioni za kitanzania. Asilimia 20 iliyobaki katika kukamilisha mradi huo wa meli inahusu ufungaji wa engine, generate, uwekaji wa vyumba na mambo mengine madogo madogo katika umaliziaji wa ndani na nje ya meli.

Meli hiyo ya abiria inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa watumiaji wa usafiri wa majini kutokana na ukweli kwamba itakuwa na uwezo wa kubeba mizigo na abiria kwa wakati mmoja. MV Mbeya II inatarajia kufanya safari zake katika bandari mbalimbali kongwe na nyingine mpya zitakazoanzishwa na TPA katika mwambao wa Ziwa Nyasa ili kuleta ufanisi katika usafirishaji wa abiria na mizigo ziwani.

MKUTANO MKUBWA WA UONGOZI KUFANYIKA OKTOBA 19 JIJINI DAR

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kinatarajia kufanya Mkutano Mkubwa wa Kwanza wa Uongozi utakaofanyika tarehe 19 Novemba 2018 katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye atawakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama . 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka amesema lengo kuu la mkutano huo ulioandaliwa na ATE kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (Confederation of Norwegian Enterprise, NHO) unalenga kuwaleta pamoja viongozi wa mashirika mbalimbali wakiwemo wanawake na wanaume ili kujadili namna ya kuongeza idadi ya viongozi wanawake katika nafasi za juu kabisa za uongozi.

Dkt Mlimuka amesema kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu ya ‘Uongozi wenye Ufanisi kwa Mazingira yanayobadilika Kibiashara’ na katika utafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa taasisi na makampuni yaliyofanikiwa kuwa na wanawake katika nafasi za juu za uongozi yamepata matokeo chanya kama vile ongezeko la uzalishaji jambo ambalo Chama cha Waajiri wangependa kulifanikisha kwa wanachama wao na wasio wanachama pia katika kuunga mkono jitihada za kitaifa za kujenga Tanzania ya Viwanda ili kufikia Uchumi wa Kati ifikapo Mwaka 2025. 

Aidha amesema kuwa, jitihada hizi zinaendana na juhudi ambazo zinafanywa na Chama cha Waajiri Tanzania na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) kwa kutoa mafunzo ya Mwanamke wa wakati Ujao (Female Future) yaliyozinduliwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshiwa Samia Hassan Suluhu mwaka 2016. Mpaka sasa jumla ya wanawake 66 wamepatiwa mafunzo haya ambapo awamu ya kwanza walikuwa 36 kwa mwaka 2016 na awamu ya pili walikuwa 30 kwa mwaka 2017. Sasa tupo kwenye awamu ya tatu ambapo wanawake 20 wanashiriki. 

Dkt Malimuka ameelezea kuwa, Programu hiyo imefanikiwa kuandaa wanawake kwa ajili ya nafasi za juu za uongozi na kuwapa uwezo wa kuingia kwenye Bodi za Wakurugenzi na kushiriki katika kutoa maamuzi ambapo wanawake kadhaa waliohitimu tayari wamefanikiwa kupata nafasi za juu za uongozi na pia kuwa wajumbe kwenye bodi mbalimbali huku mchango wao ukionekana dhahiri. 

Amewaomba wadau mbalimbali kushiriki katika Mkutano huu ili kujipambanua kama kampuni au taasisi zinazounga mkono jitihada za kuleta uongozi bora wenye kuleta maendeleo katika jamii nzima. Pia tumefungua milamgo kwa mashirika, makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo zitapenda kujitangaza kupitia mkutano huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mkutano Mkubwa wa Kwanza wa Uongozi utakaofanyika tarehe 19 Novemba 2018  jijini Dar es salaam .

ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI

0
0
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smitha Bhalia akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa kwa mkazi wa Kigamboni wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani ambapo Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) walifanya upimaji bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni. Katika upimaji huo makampuni mbalimbali ya dawa za binadamu yaligawa dawa bure kwa watu waliokutwa na matatizo yaliyohitaji kutumia dawa.


Na Genofeva Matemu – JKCI


1/10/2018 Zaidi ya watu 300 wamefanyiwa upimaji wa magonjwa ya moyo pamoja na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya ya moyo katika maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni.

Katika upimaji huo uliofanywa na madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) jumla ya watu 169 wakiwemo watoto walipimwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram ECHO) na 135 ambao ni watu wazima walipima kipimo cha kuangalia jinsi umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography-ECG).


Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Rweyemamu alisema kwa upande wa watoto waliwaona 34 sita kati yao walikutwa na matatizo ya moyo na watu wazima 10 walikutwa na matatizo wote hao wamepewa rufaa ya moja kwa moja ya kwenda kutibiwa JKCI.

“Wananchi wengi tuliowaona na kuwafanyia vipimo wamekutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu ambapo tumewapa dawa za kwenda kutumia pamoja na ushauri na wachache kati yao tumewapa dawa za ugonjwa wa kisukari”, alisema Dkt. Rweyemamu.

Wananchi hao walifanyiwa vipimo hivyo wakati Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Tanzania walipokuwa wakiadhimisha siku ya moyo duniani iliyofanyika hivi karibuni katika hospitali ya Vijibweni iliyopo Wilaya ya Kigamboni na kutoa dawa za moyo kwa asilimia 80 ya wananchi waliopimwa na wengine wachache kupewa dawa za kisukari

Akizungumza na wananchi wa Kigamboni waliohudhuria upimaji huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile aliwataka wananchi hao kutoishia kufanya upimaji kwenye siku za maadhimisho tu bali kujitokeza mara kwa mara kupima afya zao na kutunza mioyo yao kwa kula milo yenye lishe bora, kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ya mara kwa mara, pamoja na kupunguza matumizi ya pombe na sigara.

“Wataalamu wa magonjwa ya afya tunaamini kwamba tiba sahihi za magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kuyakinga; serikali imejipanga kuanzisha mpango wa taifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ili tuweze kuzishusha huduma za magonjwa hayo hadi katika ngazi za kata katika vituo vyetu vya afya” alisema Mhe. Dkt. Ndungulile.

“Naipongeza sana Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya kwani imekua ikitumika kama shamba darasa kwa kutoa elimu kwa madaktari wengine waliopo mikoani lakini pia kutoa madaktari bingwa wa taasisi kwenda kwenye jamii kutoa huduma ya afya”, alisema Mhe. Dkt. Ndungulile

Siku ya moyo duniani huazimishwa Duniani kote kila mwaka tarehe 29 Septemba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni , “kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”

INTERNATIONAL YOUNG FASHION DESIGNERS SHOWCASE TOUR IN TANZANIA

0
0

Group photo from left: Ms Angel Hon, Curator of International Young Fashion Designers Showcase Tour, Ambassador Ramadhani Mwinyi, Deputy Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs, MrsPinda, Dr Annie Wu, Honorary Consul of the United Republic of Tanzania to Hong Kong and Macau, Hon MizengoPinda, Former Prime Minister of Tanzania Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist BoardHon Angela Kairuki, Minister of Minerals, United Republic of Tanzania, Mr Joseph Kahama, Secretary General of Tanzania China Friendship Promotion Association and Mr Matindi, CEO of Air Tanzania.
Opening speech by Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist Board.
Speech by Dr. Annie Wu, initiator of the showcase tour, Honorary Consul of the United Republic of Tanzania to Hong Kong Administrative Region.
Speech by Honorable Mizengo Peter Pinda, Former Prime Minister and Member of International Panel of Advisors on Belt and Road Initiative


Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Kenny Li from Hong Kong
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Mountain Yam from Hong Kong
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Mary Yu from Hong Kong
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Veronica Angel from Panama
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Tony Vergara from Panama.
Group photo of all attended designers and models.


*Talented Young Fashion Designers Gathered in Enchanting Africa

After the shows in Iceland and Panama, “International Young Fashion Designers Showcase Tour” set off her journey to Dar es Salaam as its third stop. A gala fashion show held at Hyatt Regency of Dar es Salaam on Sept 28 featuring the collections of the participating international young fashion designers.

To support the Belt and Road Initiative (BRI) launched by the Chinese Government to promote trade, infrastructure and networking strategy among countries, the “International Young Fashion Designers Showcase Tour” is organized aims to provide a platform for the young fashion designers to showcase their works globally.

This project is initiated by Dr. Annie Wu, SBS, JP, initiator of the showcase tour and the Honorary Consul of the United Republic of Tanzania to Hong Kong and Macau, to boost her relationship between China and Africa.

It is honored that Hon. Mizengo Peter Pinda, Former Prime Minister of Tanzania was present as the Guest of Honour. He officiated the catwalk show together with Dr Annie Wu and Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist Board. They were joined by Mrs Pinda, Hon Angela Kairuki, Minister of Minerals, United Republic of Tanzania, Ambassador Ramadhani Mwinyi, Deputy Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs, Mr Joseph Kahama, Secretary General of Tanzania China Friendship Promotion Association, Ms Angel Hon, Curator of “Belt and Road International Young Fashion Designers Showcase Tour”, Mr Xu Chen, Minister Councellor of the Embassy of China in Tanzania and Mr Matindi, CEO of Air Tanzania.

“Dar es Salaam is an amazing and vibrant city filled with exotic and vivacious fashion, and I am incredibly thrilled to see the young fashion designers to be present here with positive energy and attitude, sharing their lively collections with the public. Getting inspired by this resourceful and ample city, the designers continue to express their enthusiasm of fashion with designers from various countries,” Dr. Annie Wu said.

The catwalk show presented the work of 11 designers from various countries including Tony Vergara and Veronica Angel from Panama, Hildur Yeoman from Iceland, Kemi Kalikawe from Tanzania, Junne Liu, Jarel Zhang from China, including the Trio-designer team, Lina, Yingzi, and Yuzhu from Kanoe, and Mary Yu, Kenny Li, Singchin Lo and Mountain Yam from Hong Kong.

Apart from their own outfits, the specially produced "Belt & Road" collection will be featured by selected African and Asian models.To enhance the blending of African and Chinese culture, special performances were arranged. The fashion show was opened by a local DJ and an African drummer, mixing African drums with the modern electro-acoustic. In addition, Anna Chau, the first female face-changing master from Hong Kong, gave a special Face Changing performance, blending the unique elements from the Chinese and African cultures and accompanied by brand new music arrangement and choreography. Prior to the show, Lee Wai Woo, a calligrapher from Hong Kong, offered the guests a fan with Chinese calligraphy, aiming to promote Chinese culture to the world.

“International Young Fashion Designers Showcase Tour” is initiated by Dr. Annie Wu, organized by “Belt and Road International Young Artist Development Centre”, curated by Ms. Angel Hon and coordinated by PR Network. After the inaugural show in Reykjavik in Iceland and second is Panama City, then Dar es Salaam in Tanzania and finally .

The event in Tanzania is co-sponsored by the Tanzania Tourist Board and Tanzania China Friendship Promotion Association.

AIRTEL YAZINDUA MNARA WA MASAFA YA 3G MIKUMI, WATU ZAIDI YA ELFU 30 KUNUFAIKA WAKIWEMO WATALII

0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua mnara wa mawaliano wenye uwezo wa kutoa huduma za Intanet kwa kiwango cha 3G kwa wakazi wa Kata ya Mikumi  ikiwa ni hatua ya Kampuni hiyo kurahisha huduma za masafa ya Mtandao kwa wateja wake na watalii wanaotembelea katika hifadhi ya taifa ya Mikumi.

Akizindua Mnara huo wenye uwezo wa kutoa huduma za mtandao kwa masafa ya 3G Diwani wa kata ya Mikumi Rivinus Mwawira amesema, Mbali na upatikanaji wa Masafa ya Mtandao lakini pia wakazi wake Zaidi ya elfu 30 watapata fursa mbalimbali za kimaendeleo kama kutuma na kupoke fedha kwa urahisi na pia huduma ya mawasiliano ya kawaida ya simu za mkononi.

“Mimi na wananchi wangu wa Mikumi tumekuwa na shauku kubwa ya kupata manara huu, lakini jambo kubwa zaidi ni upatikanaji wa Masafa ya 3G kwani utaturahisishia sana kazi zetu kwani ukiwa na Internet ya uhakika kila kitu kinakua rahisi”Amesema bw Mwawira

“Manufaa Mengine yanayopatikana kutokana na uwepo wa Mnara huu hapa kwetu ni pamoja na wanafunzi kujisomea kwa kutumia program mbalimbali zinazopatikana mtandaoni ikiwa ni pamoja na Masomo ya Ufundi ya VSOMO inayotolewa kwa ushirikiano baina ya Airtel na VETA” Amesisitiza Diwani huyo

Kwa upande wake Meneja mauzo wa Airtel Kanda ya Morogoro Gibson Renatus alielezea kuwa manufaa yanayopatikana baada ya kuzinduliwa kwa mnara huo katika eneo la mikumi ni pamoja na upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi, Huduma ya Airtel Money na huduma bora za mtandao za 3G.

Baadhi ya Wananchi wa eneo la Mikumi wameelezea furaha yao baada ya kuboreshwa kwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni ya Airtel katika eneo lao.

“Sasa hivi tunaweza kutuma na kupokea fedha kwa urahisi kupitia Airtel Money, tunapata internet yenye kasi ya 3G na pia hatupati tabu kupiga na kupokea simu tukiwa popote ndani nan je ya eneo letu la Mikumi” walieleza wananchi hao

Kuzinduliwa kwa mnara huo wenye uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano na mfumo wa Internet wa 3G utawawezesha wakazi Zaidi ya elfu 30 wa kata ya mikumi na maeneo ya jirani kutuma na kupokea fedha, kuwa na mawasiliano ya uhakika wakati wote, kutumia internet kupakua na kupakia taarifa mbalimbali na hivyo kurahisha shughuli zao za kila siku.

Diwani wa Kata ya Mikumi Rivanus Mwawira akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa kampuni ya simu ya Airtel  wenye uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano ya kawaida na masafa ya internet ya 3G katika eneo la Mikumi, Wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Wanaoshuhudia ni Meneja Mauzo wa Airtel Mkoa wa Morogoro Gibson Renatus mwenye Fulana Nyekundu na Maofisa wa serikali ya mtaa na kitongoji cha Mikumi Mjini
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Jackson Mmbando akitoa ufafanuzi kwa Diwani wa kata ya Mikumi Rivanus Mwawira mwenye Suti na Maofisa wengine wa serikali na watendaji wa kampuni ya  Airtel wakati wa hafla ya uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wenye uwezo wa wa kutoa huduma ya masafa ya 3G katika eneo la Mikumi, wilayni Kilombero mkoani Morogoro hivi karibu.

Waziri Mwakyembe avipa wiki mbili vilabu ya mchezo wa Kriketi kujisajili

0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM,Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wiki mbili kwa vilabu vyote vya mchezo wa Kriketi nchini ambavyo havijasajiliwa  kufika Baraza la Michezo La Taifa kwa ajili ya kujisajili .
Akizungumza na wadau hao wa mchezo huo jana katika Ukimbi wa mikutano  uliopo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa ni wajibu wa kila kilabu cha mchezo nchini kufuata sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya michezo.

“Kama kuna kilabu chochote cha mchezo wa kikreti kipo na hakijasajiliwa, natoa wiki mbili  kuweza kufuata taratibu na sheria za usajili ili viweze kutambulika kisheria ” alisema Dkt. Mwakyembe.Aidha aliongeza kwa kuutaka uongozi wa Chama cha Kriketi Tanzania kuhakikisha unatenga siku moja  kwa ajili ya mkutano na wanachama wake ili kupata nafasi ya kupitia vipengele vinavyounda katiba ya chama hicho kwa ajili ya maboresho mbalimbali.

Vilevile Waziri Dkt. Mwakyembe  alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali  zinazokikabili chama hicho cha mchezo wa Kriketi na kuhaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo.

Kwa Upande wake Kaimu Katibu  Mtendaji wa Baraza la Michezo  la Taifa Bw.Makoye  Nkenyenge amewataka wanachama hao kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Dkt. Mwakyembe kwa kuhakikisha wanasajili vilabu vyote ambavyo havijasajiliwa.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na wadau wa mchezo wa Kriketi  alipokutana nao hapo jana katikati ukumbi wa mkutano uliopo Uwanja wa Taifa, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kushoto) akieleza jambo kwa wadau wa chama cha kriketi Tanzania walipokutana nao jana uwanja wa Taifa wa Michezo, katikati ni  Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  na kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Makoye Nkenyenge. 
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Makoye Nkenyenge (kulia) akizungumza na  wadau wa chama cha kriketi Tanzania walipokutana nao jana uwanja wa Taifa wa Michezo, katikati ni  Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kushoto). 
  Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania Bw. Taher Kitisa akizungumza wakati wa kikao kilichowahusisha wadau wa chama cha Kikreti pamoja na Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha), kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Mchezaji wa Kriketi ambaye pia ni Kocha wa mchezo huo Bw. Hussein Mohamedi akichangia jambo katika kikao kilichowahusisha wadau hao pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Hayupo katika Picha),katika kikao  kilichofanyika jana uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images