Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1683 | 1684 | (Page 1685) | 1686 | 1687 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk akifungua mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo wa Ubunge na udiwani utakaofanyika katika jimbo la Liwale na kwenye kata 37 leo jijini Dodoma.
  PICHA NA 2
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo wa Ubunge na udiwani utakaofanyika katika jimbo la Liwale na kwenye kata 37.
  PICHA NA 3
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Emmanuel Kawishe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria wakati wa mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Oktoba 13 mwaka huu.
  PICHA NA 4
  Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo, jijini Dodoma.
  PICHA NA 5
  Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo, jijini Dodoma leo.

  Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Oktoba 13 mwaka huu katika jimbo la Liwale na kwenye Kata 37 za Tanzania Bara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni za uchaguzi.

  Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi.
  Jaji Mbarouk amewataka Wasimamizi hao kufanya kazi kwa ufanisi, uhuru, uwazi na bila kuegemea upande wowote ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani na utulivu.

  Amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.

  “ Tunakutana hapa ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi, natumaini mtatumia fursa hii kubadilishana uzoefu katika kutekeleza jukumu hili lililo mbele yenu”  Amesema Jaji Mbarouk.

  Jaji Mbarouk ametoa wito Wasimamizi hao waepuke madhara yanayotokana na ukiukaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi akisisitiza kwamba katika kipindi hiki chaguzi  zinafanyika katika mazingira ambayo yana hamasa kubwa ya Kisiasa, kutoaminiana na wakati mwingine kutawaliwa na mihemko ambayo imekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
  Aidha, amewaeleza Wasimamizi hao kuwa wameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo kwa kuwa wanao uwezo mkubwa wa kufanya kazi hivyo wajiamini na kujitambua.

  Ametoa wito kwa Wasimamizi hao kuhakikisha kwamba wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi na wanawatumia vyema wasaidizi walio nao katika maeneo yao ya kazi kwa matokeo bora.“Naomba mjue mna jukumu la kuimarisha imani ya wananchi pamoja na wadau wote wa uchaguzi kwa Tume. Hivyo mfanye kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, bila kuegemea upande wowote.Kufanya kazi kwa uhuru na kwa uwazi kutasaidia kudumisha amani katika maeneo yenu ya Uchaguzi” Amesema.

  Kuhusu kufanyika kwa Uchaguzi huo mdogo Oktoba 13 mwaka huu,  Jaji Mbarouk amesema kuwa kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura 292, ni jukumu la Tume kusimamia, kuendesha na kuratibu uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi.Amesema kwa nyakati tofauti Tume imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika jimbo la Liwale.

  Pia amefafanua kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa, Sura, 292 alitoa taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 37 kutoka katika Halmashauri 27 zilizopo katika Mikoa 13 ya Tanzania Bara.

  Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti wa NEC  Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ameeleza kuwa jumla ya wagombea 6 waliteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la liwale ambapo mgombea mmoja alijitoa baada ya uteuzi huo kukamilika.

  Ameongeza kuwa katika Kata 37 za Tanzania Bara jumla ya wagombea 56 waliteuliwa kugombea udiwani katika Kata hizo.

  0 0


  Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi. 

  Mageuzi makubwa katika sekta ya madini nchini yameifanya sekta hiyo kuendelea kuongeza mapato ya Serikali kutoka bilioni 194.6 ilizopanga kukusanya mwaka 2017/18 hadi kufikia shilingi bilioni 301.6 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 55.

  Hayo yameelezwa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mkoani Geita wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Serikali.

  Dkt. Abbasi ameeleza kuwa ongezeko hilo la mapato katika sekta ya madini limechagizwa na mabadilikomkatika sheria za madini, kujengwa kwa ukuta wa Mirerani na kuzuia kwa usafirishaji wa mabaki (kaboni) ya dhahabu nje ya mkoa yanapochimbwa madini.

  “Mheshimiwa Rais aliagiza kujengwa ukuta eneo la wachimbaji wadogo la Mirerani na April mwaka huu ukuta huo ulikamilika na kuwezesha kuongezeka kutoka kilo 164.6 za madini ya Tanzanite yenye thamani yas milioni 71.8 mwaka 2016 hadi kufikia kilo 449.6 zenye thamani ya shilingi milioni 893.8 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2018”, ameeleza Msemaji Mkuu wa Serikali.

  Ameeleza kuwa kutokana na usimamizi mzuri, makampuni ya uchimbaji madini yameendelea kutoa mchango wake kwa jamii ambapo Geita Gold Mine imetoa shilingi bilioni 9.2 kwa mkoa wa Geita kama mchango wa kampuni hiyo kwa maendeleo ya mkoa huo.

  Aidha, Msemaji Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa zuio la kaboni zenye dhahabu kusafirishwa na kuchakatwa nje ya mkoa zinakozalishwa limesaidia kuongeza pato kwa Serikali kufikia shilingi milioni 850 kwa mwezi Agosti mwaka huu kutoka shilingi milioni 400 kwa mwezi April.

  Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali, Wizara ya Nishati na Madini imeendelea kufanya mageuzi mbalimbali ikiwemo kujenga vituo saba vya umahiri vitakavyokamilika Disemba mwaka huu kwa thamani ya shikingi 11.9 kuwapatia wachimbaji wadogo mafunzo na utaalamu zaidi wa uchimbaji. Aidha, vituo vinne vya mfano pia vitajengwa kwa thamani ya shilingi tono kuwasaidia wachimbaji kupata teknolojia rahisi ya uchenjuaji wa madini na kuyaongezea thamani.

  Kwa upande wa sekta ya afya, Dkt. Abbasi ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa wa vifaa, wataalamu na majengo umefanyika katika hospitali za Muhimbili, Mloganzila, MOI, Bugando, Benjamin Mkapa na ambapo hivi sasa Tanzania inapokea wagonjwa kutoka Komoro, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia kwa ajili ya kupata matibabu ya kibingwa ya moyo, figo, mifupa na kuongeza uwezo wa kusikia.

  “Serikali imeendelea kusogeza huduma za afya karibu kwa wananchi kwa kujenga hospitali za rufaa katika mikoa saba, hospitali za Wilaya 67 zinajengwa mwaka huu kwa gharama ya shilingi bilioni 105 na tayari vituo vya afya 210 pamoja na nyumba za wahudumu wa afya vimejengwa” amesisitiza Dkt. Abbasi.

  Katika hatua nyingine, Dkt Abbasi ameeleza kuwa hali ya uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa imara ukikua kwa takribani asilimia 7.0 mpaka 7.1 kwa mwaka na kwamba kwa mujibu wa ripoti mbalimbali ikiwemo ya World Economic Forum, Tanzania ni ya tisa duniani kwa ukuaji wa uchumi na kwa Afrika inashika nafasi ya tano kwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi.

  Ameeleza kuwa hali nzuri ya ukuaji wa uchumi unaifanya Serikali kuendeleza mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, miundombinu, afya na nishati ili kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

  Miongoni mwa mageuzi makubwa yanayoendelea nchini ni pamoja na uchezi wa miundombunu kama reli ya kisasa ya Standard Gauge, ujenzi wa bwala kubwa la kuzalisha umeme wa megawati 2100 kutoka bonde la mto Rufiji na hivi karibuni ambapo Rais alizindua barabara ya Juu (Flyover) iliyopo TAZARA jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Wazee 576,370 wamenufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini nchini tangu februari mwaka 2018 chini ya TASAF na kati ya hao wanaume ni 217,947 na Wanawake 358,423 kwa pande zote za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema hayo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo mjini Arusha akitaja Siku hii kuwa inatukumbusha wajibu wetu katika kuwalinda, kuwatetea na upatikanaji wa huduma bora kwa wazee.

  Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa serikali inatekeleza Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 kwa kuanzisha Mpango wa Utambuzi wa Wazee katika Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo wazee wote wasiojiweza hapa Nchini.

  Aidha pamoja na utekelezaji Sera hiyo pia aserikali inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza mauaji ya wazee ambao utazinduliwa ifikapo Juni mwaka 2019 lakini pia serikali itapitia Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 ili iendane na hali halisi ya maisha ya Wazee.

  ‘’Kutokana na umuhimu wa uwepo wa wazee katika familia, jamii na Taifa letu hatuna budi kuitumia siku hii ya leo kuhamasishana, kuelimishina na kukumbushana wajibu wetu kwa wazee wetu ili kuwawezesha kuishi maisha bora yenye staha’’. Aliongeza Dkt. John Jingu.Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Fabian Daqaro ambaye amezindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee ya Mwaka 2018 amesema wazee wote watanufaika na msamaha wa kodi wa nyumba ambazo wanaishi lakini msamaha huo hautausika na nyumba zote za biashara kama vile vyumba vya maduka au nyumba za kupangisha.

  ‘’Naomba nieleweke vizuri kama nyumba yako ni kuishi na haitumiki kwa biashara itapata msamaha wa kodi lakini kama nyumba yako au nje ya nyumba yako yenye uzio ina sehemu za kufanyia biashara itatozwa kodi ya serikali nendeni ofisi za Mapato nakuweka takwimu zenu sahihi watawahudumia’’.Alisistiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Fabian Daqaro.Mkuu huyo wa Wilaya Arusha pia amewataka watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo kuweka kumbukumbu sahihi za Wazee mkoani humo ili wazee waendelee kutambuliwa ili kuwawezesha wazee hao kupata huduma muhimu ikiwemo Afya,malazi chakuala, ulinzi na hifadhi ya Jamii ya Uzeeni.

  Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani huadhimishwa hapa Nchini kila tarehe 1 mwezi wa kumi kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa linalozitaka Nchi Wanachama kutenga Siku maalumu ya kutafakari mchango wa wazee katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akiongea wakati wa uzinduzi wa Siku ya Kimataifa ya Wazee leo jijini Arusha.
   Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Bw. Fabian Daqaro akiongea wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa Siku ya Kimataifa ya Wazee leo jijini Arusha.
   Mkuu wa Wilaya ya Arusha wakwanza kushoto Bw. Fabian Daqaro, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu katikati na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftali Ng’ondi wakikagua baadhai ya kazi za ujasiliamali za kikundi cha wazee walipotembelea mabanda ya Wazee kujionea shughuli zao.
   Wazee wa Jiji la Arusha walijitokeza kwa wingi kupima Afya wakati wa madhimisho ya Siku ya kimataifa ya Wazee yanayoendelea Jijini Arusha.
  Wazee wa Jiji la Arusha walijitokeza kwa wingi kupima Afya wakati wa madhimisho ya Siku ya kimataifa ya Wazee yanayoendelea Jijini Arusha.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Zimbabwe anayekipiga sasa hivi katika Kikosi cha Azam Donald Ngoma, amerejea tena dimbani baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

  Ngoma aliyesajiliwa Azam msimu wa 2018/19 akitokea Yanga amekaa nje ya Uwanja toka ligi kuanza akiwa anauguza majeraha ya muda mrefu aliyoumia akiwa anaitumia klabu yake ya zamani.

  Azam jana ilikuwa katika Uwanja wake wa nyumbani Azam Complex wakiikaribisha Lipuli na kutoka suluhu, na kushuhudia mshambuliaji huyo akicheza kwa mara ya kwanza toka asajiliwe na timu hiyo kutokea Yanga. Ngoma alifanikiwa kuingia katika kipindi cha pili dakika ya 62 kuchukua nafasi ya kiungo mkabaji Mudathir Yahya na 

  Licha ya kutoka kwenye majeraha ya takribani mwaka mmoja, Ngoma alionekana kuanza vema jana mechi yake ya kwanza akicheza kwa kujituma na kupambana kwenye dakika zote.Kwa upande wake binafsi baada ya kumalizika kwa mchezo huo jana, Ngoma amefurahia sana kurejea tena uwanjani baada ya kutoka kwenye majeruhi licha ya timu yake kutopata ushindi dhidi ya Lipuli.

  “Azam imenifanyia vitu vikubwa sana na mimi nimefurahi sana kuwa hapa, kuvaa jezi ya Azam, ni kitu kizuri na nimefurahi sana kwa mechi yangu ya kwanza, nafikiri tunatakiwa kuchukua pointi zaidi,"“Tunakiwa kushinda mechi zaidi hususani mechi za nyumbani, tunatakiwa kupata pointi zinazohitajika, nafikiri tunatakiwa kujiboresha tunatakiwa kufanya vizuri zaidi, tunatakiwa kushinda haswa mechi za nyumbani,” alisema.

  Mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe, aliwapa tano mashabiki wa timu hiyo akidai kuwa wamekuwa wakiwapa sapoti mwanzo mwisho licha ya kutowafurahisha katika mchezo huo.“Mashabiki wamekuwa wakifanya kazi nzuri unajua wamekuwa wakijaribu kutusukuma kila mara kwa bidii hata pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri hususani mechi ya leo tulitakiwa kuwapa furaha lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kufanya hivyo lakini nawaahidi mambo mazuri yanakuja,” alisema.
  Mshabuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe anayekipiga Azam Donald Ngoma (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Lipuli Novat Lufunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliochezwa jana usiku na kumalizika kwa timu hizo kutoka Suluhu ya 0-0.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Limemtangaza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kuwa mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara (TPL) kati ya Simba na Yanga.

  Simba na Yanga zinakutana kesho katika mchezo wa Ligi kuu kuanzia majira ya saa 11 jioni ukiwa ni mchezo uliosubiriwa kwa muda mrefu.

  TFF wametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wao wakimtangaza Job Ndugai kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo ya watani wa jadi huku viongozi mbalimbali nao wakitarajia kuja kushuhudia mchezo huo.

  Simba na Yanga zinakutana kesho katika Ligi kuu Tanzania Bara ikiwa ni mara ya 93, Yanga akishinda mara 34 na Simba mara 26 huku wakitoka sare mara 30.Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini utakuwa wa kusisimua kwa kila upande kutaka kuibuka na ushindi.

  Mitaani kumekuwa na tambo mbalimbali kutoka kwa mashabiki, kila upande wakisifia kikosi chao kwa upande wa Simba wenye alama 10 baada ya kucheza mechi 5 watashuka dimbani bila mshambuliaji wao John Bocco anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu lakini wakiwa na washambuliaji wengine Kama Meddie Kagere, Emanuel Okwi, Marcelo Kaheza na Adam Salama. 

  Kwa upande wa viungo Simba wamekuwa na muunganiko mzuri kutoka Jonas Mkude, James Kotei, Mohamed Ibrahim, Clatous Chama na Shiza Kichuya huku mabeki wao Pascal Wawa, Mohamed Hussein, Shomar Kapombe na Erasto Nyoni wakitegemea kupewa nafasi kubwa ya kulinda lango lao linalindwa na Aishi Manula.

  Yanga wenye alama 12 baada ya kucheza michezo minne kwa upande wao wana kikosi chenye wachezaji wengi wachanga akiwemo beki wa kulia Paul Godfrey, Gadiel Michael akicheza kushoto kati wakiwa na Kelvin Yonda sambamba na Dante na kwa upande wa viungo Yanga wamekuwa na idadi nzuri ya wachezaji wa kati ila katika mechi nne zilizopita Papy Tshimbimbi na Feisal Salum "Fei Toto' wamekuwa wanaanza pamoja ikiwemo na Deus Kaseke na Mrisho Ngasa.

  Kwa upande wa washambuliaji Yanga wamekuwa wanatumia mipira mirefu kutoka kwa Ibrahim Ajib aliyeonesha uwezo mkubwa sa a akifunva goli moja na akitoa nafasi za goli nne akiwa na Heritier Makambo na Amis Tambwe aliyecheza mchezo wake wa Kwanza dhidi ya Singida na kufanikiwa kufunga goli 2 ila katika nafasi ya golikipa Yanga haijawa na uhakika wa nani anayeanza ila Beno Kakolanya anapewa nafasi kubwa baada ya kuonesha uwezo mkubwa kwenye mechi yao dhidi ya Singida 

  Kwenye mchezo wa msimu timu hizo zilicheza jumla ya mechi tatu, Mbili zikiwa za Ligi ambapo Simba alifanikiwa kushinda mchezo moja kwa goli 1-0 likifungwa na Erasto Nyoni, mchezo mmoja wakitoka sare 1-1 magoli yakifungwa na Shiza Kichuya kwa upande wa Simba na Obrey Chirwa akisawazisha. Mchezo mwingine ni Ngao ya Jamii Simba wakishinda kwa mikwaju ya penati baada ya kumalizika kwa dakika 90.

  Yanga waliokuwa wameweka kambi yao Mji kasoro bahari Morogoro na Simba hapahapa Jijini Dar es Salaam zitashuka dimbani kutafuta nani zaidi.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba (wa pili kulia) wakisaini mkataba wa kibiashara leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo Vodacom watatumia huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika huduza za data na sauti maeneo mbalimbali kuboresha mawasiliano. Nyuma ni wanasheria wa makampuni hayo wakishuhudia.


  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba (kulia) wakipongezana mara baada ya kubadilishana nakala za mkataba wa kibiashara leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo Vodacom watatumia huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika huduza za data na sauti maeneo mbalimbali kuboresha mawasiliano. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Jim James Yonazi akishuhudia tukio hilo pamoja na Ofisa Msimamizi wa Mkongo wa Taifa.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Jim James Yonazi (katikati) akizungumzia tukio hilo kwenye hafla hiyo ya kusaini mkataba wa kibiashara kati ya Vodacom na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Kushoto ni Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba (kulia) kabla ya tukio la kusaini mkataba wa biashara na Vodacom ya kutumia huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano leo jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba wakionesha mikataba hiyo mara baada ya kusainishana.
  Mh. Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Jim James Yonazi (wa pili kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba (wa pili kulia) mara baada ya kusaini mkataba wa biashara na Vodacom ya kutumia huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi.  Na Joachim Mushi, Dar es Salaam


  KAMPUNI ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania leo imesaini mkataba wa kibiashara na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) wa kutumia Huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) utakaowezesha mkongo kusambaza huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini.

  Hafla ya makubaliano hayo ya kibiashara imefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo TTCL Corporation imewakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Ndugu Waziri Kindamba na Vodacom ikiwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Hisham Hendi.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Kindamba alisema Vodacom amekuwa mteja wa Mkongo wa Taifa tangu Mei Mosi, 2013 na hadi sasa anatumia huduma za ukubwa wa STM-4 (Jumla 7) na STM-16 (Jumla 9), huku akiongeza kuwa Mkataba mpya uliosainiwa unaongeza viwango vya matumizi ya Mkongo kwa Vodacom kwa STM-16 (Jumla 2) na STM-64 (Jumla 1) wenye thamani ya Shilingi bilioni 25.6 bila VAT.

  “..Mkataba wa leo unatufanya sisi NICTBB na TTCL kutambua uzito wa majukumu tuliyokabidhiwa na Serikali ya kuhakikisha kuwa huduma za Mkongo zinaimarishwa ili watoa huduma za Mawasiliano hapa nchini waboreshe huduma zao na kuwafikia wananchi wengi zaidi,” alisema.

  “Mkataba wa leo unatufanya sisi NICTBB na TTCL kutambua uzito wa majukumu tuliyokabidhiwa na Serikali ya kuhakikisha kuwa huduma za Mkongo zinaimarishwa ili watoa huduma za Mawasiliano hapa nchini waboreshe huduma zao na kuwafikia wananchi wengi zaidi,” aliongeza Kindamba.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Ndugu Hisham Hendi akizungumza katika hafla hiyo alisema unalenga kuboresha huduma za mawasiliano za sauti na data kanda ya ziwa kati kaskazini na mikoa ya kusini ya Tanzania kwa kuwezesha kuleta maendeleo kupitia huduma teknolojia ya mawasiliano.

  Alisema Vodacom inatumia mkongo kwa takribani zaidi ya miaka 5 na kwa mwaka huu Vodacom inakodisha mkongo huo ambao miundombinu yake imesambaa kwa urefu wa kilomita zipatazo 7,560 nchini kote kwa kipindi cha miaka 10 kwa thamani ya dola za Kimarekani USD11.2 milioni bila VAT.

  “miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano imesambaa katika eneo kubwa kwa urefu na unao uwezo mkubwa wa kuwezesha kurusha mawasiliano ya data kwa ufanisi mkubwa, teknolojia hii itawezesha wateja wa Vodacom kupata mawasiliano mazuri zaidi nchini kote,” alisisitiza Ndugu Hisham Hendi.

  Hadi sasa wateja wanaohudumiwa na mkongo wa Taifa wa mawasiliano ni pamoja na kampuni ya TTCL, Vodacom, Tigo, Viettel, Airtel, Simbanet, Zantel, Raha, Smile, Sasakwa, eGA na ISP wengine yanatumia Mkongo wa Taifa kufikisha huduma zao kwa wateja. Mkongo wa Taifa hutumiwa pia na nchi za Afrika Mashariki na eneo la Maziwa makuu yaani Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na Zambia na hivyo kuufanya Mkongo huu kuwa na umuhimu wa kipekee kwa mawasiliano.

  0 0


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa mgombea Udiwani wa Kata ya Kibutuka katika Halmashauri ya Wilaya Liwale, Tume imefanya hivyo kwa kuzingatia Kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa kikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015.

  Rufaa hiyo iliwasilishwa na mgombea Udiwani kutoka Chama cha Wananchi CUF, Ndugu Mdohoma Bashiru Ismaili akitaka arejeshwe kuwa mgombea udiwani katika Kata ya Kibutuka kupitia chama hicho. Kuenguliwa kwake kulitokana na kuwekewa pingamizi na mgombea mwenzake kwa madai kuwa majina yake katika fomu ya uteuzi yalitofautiana na Msimamizi wa uchaguzi kukubaliana na pingamizi hilo na hivyo kumuengua.

  Tume katika kikao chake cha tarehe 30 Septemba 2018, imekubaliana na maelezo ya mrufani na kuelekeza arejeshwe kuendelea kuwa mgombea Udiwani katika Kata ya Kibutuka, Halmashauri ya wilaya ya Liwale kwa kuwa imejiridhisha kwamba mrufani wakati wa kujaza fomu yake ya uteuzi Na. 8C alianza na jina la mwisho likifuatiwa na majina mengine kwa kuwa ndilo alilotaka lianze kuandikwa kwenye karatasi ya kupigia kura.

  Kwa mujibu wa Maelekezo ya Tume kuhusu ujazaji wa fomu Na. 8 C ya Uteuzi katika kipengele namba (2) yanatoa uhuru kwa mgombea kuanza na jina ambalo angetaka liandikwe kwa herufi kubwa kwenye karatasi ya kupigia kura.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavikumbusha Vyama vya Siasa na Wagombea wanaoshiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Liwale na Udiwani katika Kata mbalimbali za Tanzania Bara, utakaofanyika tarehe 13 Oktoba 2018 kuzingatia Sheria na Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015, wakati wote wa kampeni na hata Siku ya Uchaguzi

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi. Semina hiyo imefanyika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

  Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu, Diana Masalla akiwaelimisha wafanyabiashara kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
  Afisa Kodi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Shaban Makumlo akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
  Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu, Adelaida Rweikiza akiwaelimisha wafanyabiashara kuhusu Mfumo wa Maadili kwa Watumishi wa TRA wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

  Baadhi ya wafanyabiashara wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakifurahia hotuba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Jerry Muro wakati wa ufunguzi wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya Mabadiliko ya Sheria za Kodi, Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi na Mfumo wa Maadili kwa watumishi wa TRA. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)


  ……………………….


  Na Veronica Kazimoto,Arumeru

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amewahimiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ili kufikia azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

  Akizungumza wakati akifungua semina ya wafanyabiashara hao iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa, maendeleo yanayopatikana kutokana na kodi, hayawanufaishi walipakodi pekee bali taifa zima kwa ujumla.

  “Ndugu zangu wafanyabiashara kodi mnazolipa ndio zinaiwezesha serikali kujenga nchi na kutoa huduma mbalimbali za jamii kama vile elimu, afya, miundombinu ya usafirishaji, maji, umeme na mengine mengi,” alisema Muro.

  Aliongeza kuwa, nchi nyingi zilizoendelea duniani, wananchi wake hulipa kodi kwa wakati na hiari, hivyo ili Tanzania ifikie uchumi wa kati na wa viwanda ni lazima wananchi wajenge tabia ya kulipa kodi kwa wakati.Aidha, Mkuu wa Wilaya huyo, amewasisitiza wafanyabiashara hao kutumia Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFD) na kuhakikisha wanatoa risiti kila wanapouza bidhaa au huduma mbalimbali kwani mashine hizo huwasaidia kutunza kumbukumbu na kujua mwenendo wa biashara zao.

  Kwa upande wake Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Diana Masalla alisema kuwa, lengo la semina hiyo ni kuongeza uelewa juu ya Mabadiliko ya Sheria za Kodi, Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi na Mfumo wa Maadili kwa watumishi wa TRA.

  Semina za wafanyabiashara na watumishi wa TRA katika Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara zimemalizika ambapo watumishi wamesisitizwa kuzingatia maadili wakati wafanyabiashara wametakiwa kuchangamkia msamaha wa riba na adhabu na kutoa taarifa pale ambapo mtumishi yeyote wa TRA atajiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa maadili ikiwa ni pamoja na kuomba au kupokea rushwa.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi akihutubia wananchi katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani humo inayokwenda kwa jina la "Iringa Mpya" ambapo watedaji kutoka wilaya zote na wataalam walijumuika pamoja katika mkutano huo.

  Ali Hapi amepokea kero mbalimbali za wananchi katika mkutano huo na baadhi kuzipatia ufumbuzi hapohapo kupitia watendaji wa idara mbalimbali  na zingine zikichukuliwa kwa ajili ya kuchukua hatua mbalimbali za utekelezaji ili kuzitatua.

  Mh. Ali Hapi amesema kampeni ya Iringa Mpya ndiyo kwaza imezinduliwa inaendelea mpaka Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli atakaposema inatosha sisi tulioaminiwa na Mh. Rais tunaendelea kutekeleza makujukumu aliyotukabidhi ili kutatua changamoto na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika mkoa wa Iringa.

  Hapi amesema ninaagiza watendaji wote kuhakikisha wanakwenda vijijini kwa wananchi ili kuwasikiliza na kutatua kero zao vinginevyo nitawapiga nyundo kabla mie sijapigwa nyundo na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli.
  4
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi kulia Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela katikati na MNEC wa mkoa wa Iringa CCM na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Salim Asas pamoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata wakipiga makofi katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara ya mkoani humo ya kampeni ya Iringa Mpya leo.
  6
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela kulia na MNEC wa mkoa wa Iringa CCM na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Salim Asas katikati pamoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata wakijadiliana jambo katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa.
  7
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela na msanii Bill Nas wakifanya vitu vyao katika mkutano wa Majumuisho ya Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa iliyomalizika leo iliyokuwa na kampeni ya kauli mbiu ya "Iringa Mpya".
  8 9
  Picha mbalimbali zikimuonyesha Msanii Bill Nass akifanya vitu vyake mbele ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa leo.
  10 11
  Zuwena Mohammed 'Shilole'akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah huku mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Willium akiangalia.
  12
  Zuwena Mohammed 'Shilole'akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela huku NEC wa Mkoa wa Iringa CCM na Kamimu Mwenyekiti Ndugu Salim Asas akiangalia.
  13
  Zuwena Mohammed 'Shilole'akicheza na baadhi ya wananchi walemavu waliohudhuria katika mkutano huo.
  14 15
  Baadhi ya watendaji na wananchi wa mkoa wa Iringa waliohudhuria katika mkutano huo.
  16
  Zuwena Mohammed 'Shilole'akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
  17 18 20
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi kulia Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela katikati na MNEC wa mkoa wa Iringa CCM na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Salim Asas wakiwa jukwaa kuu.
  21
  Zuwena Mohammed 'Shilole'akifanya vitu vyake mbele ya jukwaa kuu la viongozi.
  22
  Baadhi ya akina mamam wakitumbuiza katika mkutano huo.
  24
  MNEC wa mkoa wa Iringa na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Salim Asas akitoa salam zake katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa leo.
  25
  Mbunge wa Viti Maalum CCM kutoka Mkoa wa Iringa Mh. Ritha Kabati akitoa salamu zake katika mkutano huo.
  26
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi ili kuzungumza na wananchi katika mkutano huo.
  27
  Steve Nyerere na Mpoki wakifanya vitu vyao kabla ya Mkuu wa mkoa wa Iringa kuhutubia mkutano huo.
  28
  Mpoki akisalimia meza kuu.
  29
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ali Hapi na viongozi wenzake meza kuu wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
  30
  Picha mbalimbali zikionyesha baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
  31 32

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kushoto) akiongea na waandishi kuhusiana na viwanja vya ndege kuchagiza uingiaji wa watalii nchini. Kulia na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula.  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imejipanga kupitia kaulimbiu yake kuifungua Tanzania kwa ulimwengu kupitia sekta ya Utalii nchini, kwa kuimarisha usafiri wa anga ili kuhakikisha watalii wote wanafikia vivutio vyote vya utalii kwa haraka zaidi.

  Hayo yamebainishwa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela alipokuwa akizumgumza na waandishi wa habari siku ya ushiriki wa Mamlaka katika Tamasha la Urithi Wetu linaloanza leo Jumatatu (Oktoba Mosi, 2018) kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

  “Viwanja vyetu vya ndege ndio milango mikuu wa watalii kupita, hivyo tupo hapa kuwaambia wananchi, wadau pamoja na Jumuiya za Kimataifa kwamba sasa kuna fursa ya kutanganza vivutio vya kitalii kupitia viwanja vyetu vya ndege kwa kuwa vinatumika kwa usafiri wa anga lakini pia tunaweza kuvitumia kibiashara kwa kutangaza vivutio vyetu” alisema Bw. Mayongela.

  Bw Mayongela pia amewapa wito Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutangaza vivutio vilivyopo kupitia Viwanja vya ndege lakini pia kuwaeleza wadau kwa njia mbalimbali zilizopo Tanzania ili watalii wanapowasili waweze kupata picha halisi ya maeneo ya kutembelea akiwa nchini.

  Aidha Bw. Mayongela ameongeza kwamba Mamlaka ina mtandao mkubwa na inasimamia viwanja 58 vilivyopo chini ya serikali, ambavyo vipo kila sehemu penye vivutio vya utalii na wamejiimarisha kuhakikisha huduma bora ya usafiri wa anga.

  “Sehemu ya Kaskazini mwa nchi yetu ambapo ndio kuna vivutio vingi, vipo viwanja vya ndege vya kutosha, tuna Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), Kiwanja cha Lake Manyara ambacho kimejengwa kwa mkakati wa kutumika kwa watalii na kinafanya vizuri sana kwa kuingiza watalii wengi, vilevile tuna mpango wa kujenga kiwanja kipya katika Mkoa wa Manyara,” alibainisha Bw. Mayongela.

  Akizungumzia miundombinu ya Viwanja vya Ndege kwa Kanda ya Kusini ameeleza kwamba serikali imejitoa kufanya maboresho ya kiwanja cha Mtwara kwa lengo moja kuu la kuvutia watalii wengi zaidi ili waweze kushuhudia vivutio vya utalii vilivyopo maeneo hayo.

  “Serikali inaboresha kwa kufanya upanuzi na ukarabati mkubwa wa Kiwanja Cha Ndege cha Mtwara, pamoja na sababu za kiuchumi lakini pia lengo ni kuvutia watalii wengi zaidi ili waweze kushuhudia vivutio vilivyopo, sio hivyo tu lakini pia Kilwa masoko tuna kiwanja, Lindi tuna kiwanja, Nachingwea mpaka Masasi kote tuna viwanja” Alisema Bw. Mayongela.

  Akizungumzia upande wa nyanda za juu Kusini Bw. Mayongela amebainisha kwamba baada ya ukarabati mkubwa kukamilika kutakuwa na kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe, Njombe mpaka Iringa kutakuwa na viwanja vizuri vya ndege ili kuhakikisha kwamba vivutio vilivyopo Tanzania vinafikika kwa urahisi.

  Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof Audax Mabula ameeleza kwamba Tamasha la Urithi Wetu lililobuniwa na Wizara ya Maliasili na Utalii lina madhumuni makuu mawili ikiwemo ya kuwezesha kuonyesha fursa zote zinazoizunguka tasnia hii.

  “Madhumuni makuu ni kuendeleza, kutambua na kuhifadhi urithi wetu wa utamaduni kwa ajili ya kizazi kilichopo na kinacho kuja lakini pili ni kubadili urithi wetu wa utamaduni kuwa zao la utalii hayo ndio malengo makuu mawili” alisema Prof Mabula.

  TAA wametoa msaada wa fulana 100 kwa ajili ya washiriki wa tamasha la Urithi Wetu, ambalo litafikia tamati Oktoba 6, 2018 kwa kufungwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu Mji Mwema Kigamboni ambapo alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wastaafu,(kulia) na kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wakati wa mazishi ya IGP mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Askari Polisi wakishiriki kushusha mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu kaburini wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu baada ya mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Picha na Jeshi la Polisi)

  0 0

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akitoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro wakati wa ziara yake ya kukagua mashamba makubwa katika wilaya hiyo, kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly.
  ????????????????????????????????????
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akiwasili katika ofisi za wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kukagua mashamba makubwa katika wilaya hiyo, kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly.
  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro Mwl Mohamed Utaly akizungumza katika kikao baina ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara ya kukagua mashamba makubwa katika wilaya hiyo.
  ????????????????????????????????????
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua moja ya majalada ya hati za Ardhi katika ofisi za wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kukagua mashamba makubwa katika wilaya hiyo.
  ????????????????????????????????????
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akitoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro wakati wa ziara yake ya kukagua mashamba makubwa katika wilaya hiyo (Picha zote na Munir Shemweta-Wizara ya Ardhi
  ………………………….

  Na Munir Shemweta, WANMM Mvomero
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameshangazwa na ucheleweshaji utoaji hati miliki za ardhi kwa wananchi katika halmashauri ya wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro.

  Dkt. Mabula alibaini hali hiyo baada ya kuelezwa na Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Keneth Mwenda kuwa hati 53 bado hazijapelekwa ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kati kwa ajili ya kukamilishwa ili kugawiwa kwa wananchi.

  Hali hiyo ilimshtua Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo hakuridhishwa na sababu za ucheleweshaji utoaji hati hizo kwa wananchi kwa sababu tu wameshindwa kuzipeleka ofisi ya Kanda huku baadhi ya hati hizo zikiwa ni za tangu mwaka 2017 na kuagiza majalada ya hati hizo 53 kuwasilishwa kwake mara moja kabla ya hajaondoka ili kujiridhisha na maelezo hayo.
  Dkt. Mabula alikuwa wilayani Mvomero katika ziara yake ya siku moja mwishoni mwa wiki kukagua Mashamba makubwa kwa lengo la kubaini mashamba yasiyoendelezwa ili hatua za kisheria zichukuliwe ikiwemo kuyafuta mashamba yote ambayo hayajaendelezwa.

  Baada ya kuletewa na kukagua majalada, Dkt. Mabula aliagiza hati hizo kuwasilishwa haraka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Kati kabla ya tarehe 10 Oktoba, 2018 kwa ajili ya kusainiwa na kurejeshwa ili zitolewe kwa wamiliki.

  ‘’Hati inaweza kuandaliwa kwa siku tatu na kwa mfumo wa sasa hati inaweza kupatikana kwa siku moja lakini ninyi mnakaa nazo bila kuzifanyia kazi kwa haraka kitu ambacho kinawachelewesha wananchi kupata hati zao jambo linalowafanya walalamike.’’ alisema Dkt. Mabula.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amezitaka halmashauri zote nchini kuipa kipaumbele sekta ya ardhi kwa kuwa sekta hiyo ina mchango mkubwa katika kuingizia serikali mapato na kubainisha kuwa fedha nyingi zinazotumiwa na idara mbalimbali katika halmashauri nyingi zinatoka katika sekta ya ardhi.

  Alisema katika halmashauri nyingi alizotembelea amebaini idara ya ardhi kuwa idara pekee iliyotelekezwa kwa kutopatiwa mgao wa fedha wa kutosha pamoja na mahitaji muhimu kama magari kwa ajili ya kuiwezesha kufanya kazi zake kwa ufanisi. 

  Katika halmashauri ya wilaya ya Mvomero imeelezwa kuwa idara nyingine kama Afya na Elimu zimekuwa zikipatiwa fedha nyingi za matumizi hadi kufikia milioni mia mbili huku idara ya ardhi ikiambulia milioni moja jambo linaloifanya idara hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

  Aidha, Aliwataka watumishi wa idara ya ardhi katika wilaya ya Mvomero kuacha kufanya kazi maofisini pekee na badala yake watenge muda wa siku tatu ndani ya wiki moja kuenda kwa wananchi kwa ajili ya kutatua kero za ardhi.
  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwl. Mohamed Utaly amekiri idara ya ardhi kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata fedha kidogo kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za kushughulikia migogoro ya ardhi pamoja na kupima maeneo.

  Awali akisoma taarifa kuhusiana na sekta ya ardhi katika halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri hiyo Rugembe Maiga alieleza kuwa jumla ya mashamba 26 hayajaendelezwa katika wilaya hiyo na tayari wahusika washapelekewa wito wa kujieleza kuhusiana na kutoendeleza mashamba na kati ya hao waliopelekewa wito huo wamiliki 12 walitekeleza huku 14 wakiwa kimya jambo linaloifanya halmashauri kuanza mchakato wa kuyafuta.

  0 0


  Msanii wa Bongo Flava – Ben Pol akitumbuiza katika ufunguzi wa matamasha ya mwaka huu ya Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana usiku. Tamasha hilo linahamia katika mji wa Sumbawanga mwisho wa wiki hii. 
  DOGO JANJA JANJAROO
  Msanii wa Bongo Flava – Dogo Janja  akitumbuiza katika ufunguzi wa matamasha ya mwaka huu ya Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana usiku. Tamasha hilo linahamia katika mji wa Sumbawanga mwisho wa wiki hii. 
  NANDY
  Msanii wa Bongo Flava – Nandy akitumbuiza katika ufunguzi wa matamasha ya mwaka huu ya Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana usiku. Tamasha hilo linahamia katika mji wa Sumbawanga mwisho wa wiki hii. 
  ROSTAM ROMA NA STAMINA
  Wasanii wa Bongo Flava – Roma (kushoto) na Stamina (kulia) wanaounda kundi la Rostam wakitumbuiza katika ufunguzi wa matamasha ya mwaka huu ya Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana usiku. Tamasha hilo linahamia katika mji wa Sumbawanga mwisho wa wiki hii. 
  ………………………………
  Wasanii wa nyumbani wafanya makubwa kuwapagawisha mashabiki huku tamasha likihamia Sumbawanga.
  Morogoro,Msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote, umeanza kwa kishindo katika viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro huku wasanii wa nyumbani wakifanya onesho bab-kubwa lililoacha gumzo midomoni mwa maelfu ya mashabiki waliofurika kushuhudia tamasha hilo la kila mwaka.
  Milango ilifunguliwa saa kumi na mbili kamili na kushuhudia wasanii wanaochipuka walioshiriki katika shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota wakifungua jukwaa. Wasanii hao wachanga kutoka mjini Morogoro waliongozwa na washindi Supa Nyota kimkoa, Michael Yusufu (Belly 255) na Abdul Michael (V Dax).
  Shangwe kubwa zaidi zililipuka wakati kundi linalokuja kwa kasi la Mesen Selekta pamoja na msanii Whozu anayetambaa na wimbo wake wa Huendi Mbinguni walipopanda jukwaani na kusababisha vumbi kutifuka miongoni mwa mashabiki huku wengi wakisikika wakinongona kuwa vijana hao ni moto wa kuotea mbali katika tasnia ya sasa ya bongo flava.
  Wasanii wengine waliofanya kazi kubwa kukonga mioyo ya mashabiki ni pamoja na kundi la Rostam linaloundwa na wasanii Roma na Stamina, , Fid-Q aliyeambatana na msanii wa kike wa mziki wa kufokafoka Rosaree, Ben Pol, Mr Blue Kabayser, Dogo Janja, Maua Sama , Nandy, pamoja na Belle 9 ambaye ndiye aliyekuwa wa kwanza kupanda jukwaani kama msanii mwenyeji wa Morogoro. Wasanii wote walionesha uwezo mkubwa wa kuimba na kumiliki jukwaa, huku wote wakiwa wamejiandaa kikamilifu pamoja na wacheza dansi waliokuwa wamevalia sare za kuvutia.  
  Msanii mkongwe ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi – Professor Jay ambaye aliambatana na wasanii wengine wakongwe ikiwemo Black Rhino waliwashangaza mashabiki ambao hawakutegemea ujio wa wasanii hao wakongwe kwa kufanya onesho la kukata na shoka, na kuwafanya hata wale waliokuwa wameanza kutoka uwanjani kurudi ndani na kukesha hadi jogoo wanawika.
  Akizungumza katika onesho hilo lililoshirika 100% wasanii wa nyumbani, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe alisema kuwa mbali na shamrashamra za mwanzo wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, msimu huo ulikuwa umeibua fursa nyingi za biashara katika mji huo.
  ‘Tunatambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Bali na kutoa fursa ya kuutangaza mkoa wetu, pia imeongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama nitilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,’ alisema mkuu huyo wa mkoa. 
  Kuendana na msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo pia inaendesha promosheni za kusizimua kwa wateja wake ikiwemo ile ya kutoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha tiketi kilichotangazwa kwa kila mkoa husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
  Wateja wa Tigo pia wanapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi za thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH 10 milioni. Kushiriki wateja wanapaswa kujiunga kwa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.
  Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu litashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.

  0 0  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasisitiza wasanii wa filamu nchini kuthamini kazi zao za filamu na kutokubali kuziuza kwa bei ya chini wanapopata nafasi za kuziuza katika televisheni za nje, leo jijini Mwanza alipokuwa akizindua Filamu ya Brother K katika ukumbi wa Misterious Cinemax  uliyoko Rockcity Mall,ambapo filamu hiyo imetengenezwa na wasanii wa filamu wa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na msanii mkongwe wa filamu nchini Bi.Johary Changula.
  PIX 2
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania kutoka Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kusimamiwa kwa kazi za filamu mikoani wakati wa uzinduzi wa filamu ya BROTHER K leo jijini Mwanza kwa kusema kuwa katika kila halmashauri kuna bodi iliyochini ya Afisa Utamaduni kwa ajili ya kukagua kazi za filamu,katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe na wakwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mwanza Mjini Stanslaus Mbalula.
  PIX 3
  Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mwanza Mjini Mheshimiwa Stanslaus Mbalula (kushoto) akimpongeza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kwa jitihada zake za kusimamia vyema sekta ya filamu nchini pamoja na sekta zake zote za wizara yake wakati wa uzinduzi wa filamu ya BROTHER K leo jijini Mwanza.
  PIX 4
  Msanii wa Filamu kutoka Mkoa wa Mwanza maarufu kama Brother K (katikati) akimweleza  na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe changamoto ya upatikanaji wa stika za TRA mikoani kwa ajili ya kazi za Filamu mara baada ya uzinduzi wa filamu iitwayo BROTHER K leo jijini Mwanza.
  PIX 5
  Msanii Mkongwe wa filamu nchini Johary Changula akieleza ushiriki wake katika filamu ya BROTHER K iliyozinduliwa leo jijini Mwanza na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe.
  PIX 6
  Baadhi ya wasanii wa filamu yalishiriki katika filamu ya BROTHER K wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  (watatu kulia) mara baada ya uzinduzi wa filamu hiyo uliyofanyika katika ukumbi wa sinema wa Mestrious,wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania kutoka Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo,wakwanza kushoto ni  Msanii Mkongwe wa filamu nchini Johary Changula na wakwanza kulia ni Msanii wa Filamu kutoka Mkoa wa Mwanza maarufu kama Brother K.

  …………………….
  Na Anitha Jonas – WHUSM – MWANZA
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wasanii wa filamu nchini kutambua thamani ya kazi zao za filamu.

  Mheshimiwa Mwakyembe  ametoa agizo hilo leo jijini Mwanza alipokuwa akizindua filamu ya BROTHER  iliyotengenezwa na wasanii wa filamu wa mkoa huo kwa kushirikiana na msanii mkongwe wa filamu Bi.Johary Changula.
  “Kwanza niwapongeze kwa kazi nzuri mliyofanya nimeanza kuona mabadiliko katika tansia hii sasa, kuna mabadiliko makubwa katika upande wa sauti, mwanga na hata namna ya uigizaji ongezeni bidii mkiendelea hivi mtapata mafanikio makubwa na pia msipende kuuza kazi zenu nje kwa bei chini tofauti kazi za nchi jirani,”alisema Dkt.Mwakyembe.

  Akiendelea kuzungumza na Waziri Mwakyembe aliupongeza uongozi wa ukumbi wa Sinema wa Misterious wa jijini Mwanza kwa kutenga siku mbili ambazo ni Ijumaa na Jumamosi kwa ajili ya kuonyesha filamu za Kiswahili kutoka ndani ya nchi hii ni hatua kubwa ya uthubutu ningependa kuona na kumbi zote nchini zinaiga mfano huo.

  Aidha,Nae Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alifafanua kuhusu  changamoto ya upatikanaji wa stempu za TRA kwa kazi za filamu kwa kusema kuwa tayari serikali imeshaanza  kulishughulikia suala hilo kwa kuaandaa nakala laini ya stempu hizo zitakazo sambazwa katika ofisi za TRA mikoani ili kuondoa kero hiyo.

  “Kufuatia maombi yenu ya kuitaka ofisi yangu ije tena kwa ajili ya kutoa elimu ya uandaaji wa kazi za filamu basi tutajipanga na tutahitaji kuona wadau wengi wakifika ili tuweze kuhakikisha wadau wa filamu wanaanda  kazi bora mara baada ya kupata elimu ya uaandaji wa miswada ya filamu,”alisema Bibi.Fissoo.
  Pamoja na hayo Katibu Mtendaji huyo aliendelea kusisitiza kuwa ukaguzi wa kazi za filamu kwa mikoani upo kisheria chini ya bodi ya filamu katika Halmashauri ambapo inaongozwa na Afisa Utamaduni hivyo siyo lazima kazi ya filamu ipekwe katika ofisi za Bodi ya Filamu Dar es Salaam kwa ukaguzi.

  Halikadhalika nae Mwenyekiti wa Chama cha Waandaji wa Filamu Mkoa wa Mwanza Bw.Abdallah Mohamed  alimweleza Waziri Mwakyembe kuwa umoja huo unatarajia kujenga jego la uandaaji wa kazi za filamu kwa kushirikiana na wawekezaji.

  0 0  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akiwapongeza wakazi wa Jimbo la Bukombe kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia fainali za DOTO CUP 2018 zilizofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Uyovu leo Wilayani Bukombe,mashindano hayo yaliandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Madini Mheshimiwa Dkt.Dotto Biteko.
  PIX 2
  Mabingwa wa Mpira wa Miguu katika Mashindano ya DOTO CUP 2018 Ushirombo Rangers wakiwa wanashangilia ushindi wao mara baada ya kukabidhiwa kombe la ushindi leo katika fainali za mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Uyovu ,Wilayani Bukombe.
  PIX 3
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akimpongeza mshindi wa mbio za kukimbiza kuku kwa wanawake Bi. Elizabeth Boniphace  katika mashindano ya DOTO CUP 2018 yaliyofanyika leo katika uwanja wa Uyovu Wilayani Bukombe,wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Madini Mheshimiwa Dkt.Dotto Biteko.
  PIX 4
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akikagua timu ya watoto wadogo  wanaojiita Yanga kabla ya timu hiyo kuanza kupambana na wenzao wanaojiita timu ya Simba wote kutoka kituo cha Don Bosco katika fainali za  mashindano ya DOTO CUP 2018 yaliyofanyika leo katika uwanja wa Shule ya Msingi Uyovu na mashindano hayo yalikuwa yameandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Madini Dkt.Dotto Biteko.
  PIX 5
  Timu ya wanawake waliyojiita simba na wapinzani wao wakijiita yanga wakishindana kuvuta kamba katika mashindano ya DOTO CUP 2018 yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Uyovu Wilayani Bukombe  ambapo Timu ya Yanga iliibuka mshindi.
  PIX 6
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Madini Dkt.Dotto Biteko akiwashukuru wakazi wa Jimbo la Bukombe kwa kushiriki vyema katika mashindano ya DOTO CUP 2018 aliyoyaanda kwa katika jimbo lake ambapo fainali zimefanyika leo  katika Uwanja wa Shule ya Msingi Uyovu.
  PIX 7
  Kapteni wa Timu ya Mpira wa Pete wanawake kutoka Timu ya Ushirombo Bi.Alinda Deogratious  akimtambulisha wachezaji wa Timu mgeni rasmi wa fainali za mashindano ya DOTO CUP 2018 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe kabla ya kuanza mechi dhidi ya timu ya Runzewe  leo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Uyovu Wilayani Bukombe.
  Pix 8
  Timu ya watoto wadogo kutoka kituo cha Don Bosco ambao wanajiita Simba – Yanga wanaojiita ambao ni SIMB Wilayani Bukombe wakisakata kabumbu katika fainali za mashindano ya DOTO CUP 2018 jana katika uwanja wa Shule ya Msingi Uyovu, mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo Bukombe  ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko.
  ………………………
  Na Anitha Jonas – WHUSM, BUKOMBE
  GEITA

  Waziri wa Habari wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe ameahidi kusaidiana na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mheshimiwa Dkt. Dotto Biteko katika kuboresha viwanja vya michezo kwa jimbo hilo kutokana na hari ya Michezo aliyoiona Wilayani hapo.
  Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo katika Uwanja wa Michezo wa Shule ya Msingi Uyovu,Wilayani Bukombe Mkoani Geita alipokuwa akifunga fainali za mashindano ya DOTO CUP 2018 yaliyokuwa yameanza tangu Mwezi Julai Mwaka huu Wilayani hapo.

  “Nimefurahishwa sana kuona hari ya mwamko wa michezo mkubwa kwa Wilaya  hii kwanza ningependa Halmashauri ya Wilaya ianze kuonyesha jitihada za kuboresha viwanja vya michezo kwa kuandaa michoro ya viwanja na ofisi yangu ipo tayari kuwapa wataalamu  kwa kazi hiyo,kwa kufanya hivi itasidia kujua namna nitakavyoweza kuwasilisha maombi ya kuboresha viwanja hivi kwa wadau na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF),”alisema Dkt.Mwakyembe.

  Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Waziri huyo alisisitiza kuwa michezo ni ajira kwa vijana hivyo vijana wasikate tamaa kwani maendeleo  ya sekta ya michezo yanategemea zaidi vijana.Halikadhalika waziri huyo mwenye dhamana ya michezo  alitoa pongezi kwa wakazi wa Bukombe kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia fainali za michezo hiyo.

  Aidha,Naye Mbunge wa Jimbo la Bukombe  ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Dkt. DOtto Biteko ambaye ndiye aliyeandaa mashindano hayo ya DOTO CUP  alimshukuru Waziri Mwakyembe kwa kuweza kufika na kufunga mashindano hayo pamoja na wanamichezo wote waliyojitokeza kushiriki mashindano kwa pamoja na  waratibu wa mashindano na walimu wamichezo yote kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika vizuri na pia.

  Pamoja na hayo nae Afisa Michezo Wilaya ya Bukombe Bibi.Jenipha Kisusi alieleza kuwa mashindano hayo yalienda sambamba na zoezi la uchangia wa damu salama kwa ajili ya kuongeza benki ya damu katika hospitali ya Uyovu wilayani hapo.

  Halikadhalika Bibi.Kisusi alieleza kuwa mashindano hayo kwa ujumla yalihusisha michezo mbalimbali ikiwemo Mchezo wa Riadha kwa mita mia moja,Mbio za Baiskeli,Mpira wa Wavu,Mpira wa Pete,Mchezo wa Karate,Mpira wa Miguu pamoja na michezo kama kuvuta kamba pamoja na kukimbia na magunia.

  Hata hivyo katika msimu huu wa 2018 katika mashindano hayo Timu ya Mpira wa Miguu  Ushirombo Rangers ndiyo iliyochukua ubingwa kwa misimu huu kwa kuifunga 2 -0 Timu ya Small Tiger.

  0 0

  Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

  SIKU ya moyo duniani imeadhimishwa Septemba 29 ikiwa lengo mahususi kwa kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kujua na kupima magonjwa mbalimbali ya moyo, pamoja na kuelimisha jamii juu ya athari mbalimbali zinazotokana na magonjwa ya moyo.

  Akizungumza katika maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa afya, wazee, jinsia na watoto Faustine Ndugulile amesema kuwa  maadhimisho ya Siku ya Magonjwa ya Moyo Duniani mwaka yamekuja na kauli mbiu ya ‘MOYO WANGU, MOYO WAKO’ kwa lugha ya kiingereza  My heart, Your heart, ikiwa na lengo la kusisitiza juu ya kila mmoja wetu kufanya uchunguzi wa moyo ili kujua hali yake.

  Aidha amesema; "Magonjwa ya moyo yanaongoza kwa kusababisha vifo duniani. Inakadiriwa kuwa watu 17,500,000 hufa kila mwaka duniani kote kutokana na magonjwa ya moyo na kiharusi. Ugonjwa wa moyo ni ugonjwa ambao unaathiri watu wa rika na jinsia zote; watoto, watu wazima, wake kwa waume. Aidha, Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kwamba asilimia 40% ya vifo vyote vinavyotokea duniani vinasababishwa na magonjwa ya moyo. Pia nusu ya vifo ambavyo vinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza vinatokana na magonjwa ya moyo na vilevile asilimia 80% ya vifo hivi hutokea kwenye nchi zenye uchumi wa kati na wa kiwango cha chini" amesema Ndugulile.

  Aidha imeelezwa kuwa matumizi ya tumbaku na bidhaa zake yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu 6,000,000 duniani kila mwaka na pia huchangia kusababisha asilimia 10% ya wagonjwa wenye magonjwa ya moyo. Vilevile moshi wa sigara kwa watu wasiovuta sigara (second hand smoking) husababisha vifo vya watu laki sita (600,000) na kati ya hao 28% ni watoto. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani (WHO).

  Pia amesema kuwa kama hatua madhubuti za kinga, uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka, tatizo la Moyo ifikapo mwaka 2035 litaongezeka na kufikia makadirio ya wagonjwa wapya milioni 131,978,870 (sawa na ongezeko la 45% kutoka hali ilivyo kwa sasa), huku ongezeko kubwa likiwa katika ukanda wa nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa moja wapo.

  Pia ameeleza kuhusu tafiti wa viashiria vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliofanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) mwaka 2012, ulionyesha kuwa kuna ongezeko kubwa la viashiria vinavyosababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 15.9% ya wananchi wanavuta sigara, asilimia 29.3% wanakunywa pombe, asilimia 97.2% wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa wiki.

   Aidha utafiti ulionyesha asilimia 26% ya wananchi ni wanene kupita kiasi, asilimia 26% wana lehemu nyingi mwilini, asilimia 33.8% wana mafuta mengi mwilini, asilimia 9.1% wana kisukari na asilimia 25.9% wana shinikizo kubwa la damu. Utafiti pia ulionyesha 25% ya wananchi waliohojiwa hawajishughulishi na kazi zinazotumia nguvu na hawafanyi mazoezi yeyote. Viashiria hivi ndivyo vinavyochangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

  Moja wapo ya sababu kubwa za magonjwa ya shinikizo la damu ni kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye misuli ya moyo. Kuziba kunaweza kusababishwa na mafuta yaliyomo kwenye chakula ambayo huenda huganda katika kuta za mishipa hiyo, hali ambayo hutokea pole pole na huchukua muda mrefu hadi mishipa kuziba kabisa. Matumizi ya tumbaku, uzito uliozidi na kutofanya mazoezi huchangia sana uwezekano wa kupata ugonjwa wa shinikizo la damu na  hii hupelekea mtu kupata matatizo hayo. 

  Imeelezwa kuwa ugonjwa wa Moyo umekuwa na vyanzo mbalimbali vinavyosababisha tatizo hili kukua kwa kasi hapa nchini na Duniani kote. vyanzo hivyo vikubwa ni pamoja na: Mtindo wa kimaisha (Life Style), Ulaji usiofaa, Kutofanya Mazoezi, Matumizi ya pombe, Uvutaji wa Sigara na matumizi ya bidhaa zitokanazo na Tumbaku  

  Ili kuzuia ugonjwa wa Moyo na maradhi mengine yasiyo ya kuambukiza ni muhimu kufuata kanuni za afya ambazo ni ulaji bora, na mtindo bora wa maisha ambao ukifuatwa vyema huweza kwa kiasi kikubwa kuzuia mtu kupata maradhi ya Moyo . 

  Na ametoa rai kwa wananchi wote nchini watoe ahadi kwa ajili ya moyo wangu, moyo wako na mioyo ya watu wengine, na tuchukue hatua madhubuti za kujikinga dhidi ya magonjwa ya moyo na kuweka ahadi ya mtu binafsi ya kupika na kula chakula kinachokidhi viwango vya afya,

  Ahadi ya kujitahidi kufanya mazoezi na kuwafundisha na kuwahimiza watoto wetu kufanya mazoezi,ahadi ya kutovuta sigara na kutumia bidhaa za tumbaku, na kuwahimiza wapendwa wetu ambao wanavuta sigara na kutumia bidhaa za tumbaku kuacha kabisa, ahadi kwa watoa huduma za afya, kujitahidi kutoa huduma bora ya kuelimisha, kukinga na kuokoa maisha, 

  ahadi ya viongozi wa kitaifa kufanikisha mpango mkakati wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na amewakaribisha wananchi wote kwenye zoezi la uchunguzi linaloendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
  Kwa upande wake Rais wa Chama cha madaktari wa moyo nchini Dkt. Robert Mvungi amesema kuwa tatizo la moyo ni kubwa na gharama ni kubwa na kinga ni sisi wenyewe kubadili mifumo ya maisha. 

  Na amesema kuwa kuna tishio kwa ugonjwa wa moyo kwani watu wenye umri mdogo hupata ugonjwa wa moyo na amesema baadhi ya visababishi ni pamoja na presha ambapo zaidi ya asilimia 20 ya watu wa chini ya miaka 25 wana presha.Sigara, mfumo wa maisha na matumizi ya pombe.

  Amewaasa wananchi kubadili mifumo ya maisha,kufanya mazoezi  na kuepuka matumizi ya sigara na pombe.
   Matembezi ya Siku ya Moyo Duniani yakiendelea, ambayo kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya 'Moyo wangu, Moyo wako"
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  akiongoza mazowezi siku ya Moyo Duniani yaliyoanzia viwanja vya Leaders Club na kumalizikia viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es sala, matembezi hayo yamebeba kauli mbiu ya "Moyo wangu Moyo Wako". Wakwanza Julia ni Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Wizara ya Afya.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya mabanda yaliyokuwepo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani. Kushoto kwake ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania Dkt. Robert Mvungi, kulia kwake ni Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Wizara ya Afya Dkt. Amalberga Kasangala


  Madakitari wakitoa elimu na kipima afaya za wananchi walijitokeza katika maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani.(picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

  0 0
  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
  Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wameendelea kuboresha huduma ya maji sehemu mbalimbali ikiwemo kuongeza maji ya kutosha katika bandari ya Dar es Salaam.

  Mkakati huo umeanza kutekelezwa rasmi  na Mkoa wa Dawasa Ilala kwa kuanza zoezi maalum la kuunga Bomba kubwa la kipenyo nane ili  kupeleka Huduma ya maji ya kutosha Bandarini.

  Meneja wa mkoa Ilala Judith Singinika  amesema kuwa zoezi linatekelezwa kulingana na agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Makame Mbarawa  alilolitoa alipotembelea mamlaka hiyo ya Bandari.

  Amesema kuwa, kukamilika kwa zoezi la kuunga bomba hilo kutaongeza wingi wa maji katika bandari hiyo ya Dar es salaam na kuhakikisha kuwa mahitaji ya huduma ya maji kwenye eneo lote la Bandari yanafikiwa. 

  Aidha kazi hii itawezesha pia meli zote za abiria na mizigo zinazotia nanga katika bandari hii kibwa kuliko zote nchini zinapata maji safi na kukidhi mahitaji.

  Hapo awali, Bandari walikuwa wananunua maboza kutoka nje kwa ajili ya matumizi ya meli zinazotia nanga na Profesa Mbarawa alipiga marufuku na kuwataka watumie maji ya Dawasa kwa usalama zaidj.

  Kazi hii ni utekelezaji wa  agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profes Makame Mbarawa alilolitoa tarehe 30/7/2018 wakati wa ziara ya ya kutambua Wateja wakubwa wa maji Dar es salaam.
  Ujenzi wa kuunga bomba kubwa la maji lenye kipenyo nane ili  kupeleka Huduma ya maji ya kutosha Bandarini ukiendelea kufuatia agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profes Makame Mbarawa alilolitoa tarehe 30/7/2018 wakati wa ziara ya ya kutambua Wateja wakubwa wa maji Dar es salaam.

  0 0

  Anaandika Dixon Busagaga.

  IMANI haba na zile za kishirikina zimeendelea kushika kasi kwa nchi za Afrika huku  watu wenye ulemavu wa Ngozi “Albino” wakiwa waathirika wakubwa kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa kuuawa na kisha kunyofolewa viungo kwa imani za kishirikina.

  Matukio haya yanatajwa kuendelea kukithiri katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, ambapo nchini Zimbabwe ipo imani ya kwamba muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi akishiriki tendo la ndoa na mwenye ulemavu wa ngozi "Albino " atakuwa amepona .

  Lissa Marange ni miongoni mwa washiriki 25 kutoka nchi zaidi ya nane walioshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kupeleka ujumbe maalumu kwa viongozi wa Afrika kuongeza nguvu katika mapambano ya vita dhidi ya ukatili kwa watu wenye Ualbino.
   Pichani wa pilia kulia ni Lissa Marange ambaye ni miongoni mwa washiriki 25 kutoka nchi zaidi ya nane walioshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kupeleka ujumbe maalumu kwa viongozi wa Afrika kuongeza nguvu katika mapambano ya vita dhidi ya ukatili kwa watu wenye Ualbino.
   Baadhi ya washiriki 25 kutoka nchi zaidi ya nane walioshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kupeleka ujumbe maalumu kwa viongozi wa Afrika kuongeza nguvu katika mapambano ya vita dhidi ya ukatili kwa watu wenye Ualbino.  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wachimbaji wadogo wa madini waende Benki wakakope mitaji kwa sababu wana uhakika wa kudhaminiwa na Benki Kuu.

  “Msihofu kukopa, kukopa ni jambo la kawaida sana. Nenda mkakope ili mpate mitaji ya kununua mitambo ya kuchenjua dhahabu na madini mengine,” amesema.

  Ametoa wito leo (Jumapili, Septemba 30, 2018) wakati akifunga maonesho ya mkoa wa Geita ya dhahabu, madini, teknolojia ya madni na uwekezaji yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita. Maonesho hayo yalianza Septemba 24, mwaka huu.

  Waziri Mkuu amesema, wakati akikagua mabanda ya maonesho kwenye viwanja hivyo, ameelezwa kwamba gharama ya mtambo unaohitajika kwa wachimbaji wa kati inafikia sh. milioni 10. “Naomba niwaeleze wanaGeita kwamba mnakopesheka, nendeni mkaombe mikopo ili mnunue mitambo ya kuchenjua dhahabu,” amesisitiza.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amewaeleza wana-Geita kwamba siri kubwa ya kufanikiwa kupata mikopo ni kwa wao kuunganisha nguvu kwa kujiunga kwenye vikundi ili wawe na malighafi ya kutosha mitambo hiyo.

  “Wakuu wa wilaya za Mkoa huu simamieni zoezi hili kwa sababu wilaya zenu zote zinachimba madini. Simamieni uundaji wa vikundi na mwende mkawasemee benki pale wanapokwama.”

  Akielezea kuhusu makusanyo ya fedha kutokana na mauzo ya dhahabu kwenye mkoa huo, Waziri Mkuu amesema tangu Aprili mwaka huu, mapato yanayotokana na madini yameongezeka kutoka sh. milioni 400 na kufikia sh. milioni 850 Agosti, mwaka huu.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wazazi wawapeleke watoto wao kwenye vyuo vya ufundi vya VETA ili wakajifunze taaluma ya uchongaji wa madini na vito kama eneo jipya la ajira nchini.
   Mwanafunzi wa mwaka pili katika chuo cha VETA Moshi, Careen Vedasto akiendesha kifaa cha kuchimbia madini kilichobuniwa na wanafunzi na walimu wa chuo hicho mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimuuliza maswali mwanafunzi wa VETA Moshi, Jesca Jonathan (mwenye rasta), kuhusu utaalamu wa kuchonga vito na madini alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Wa pili kulia ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kifungashio cha kopo la kahawa aina ya AMIMZA alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Kulia ni Afisa mauzo wa TANICA PLC, Revina Peter akitoa maelezo. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea maelezo ya mtambo wa kuchenjua madini unaoweza kumilikiwa na wachimbaji wa kati alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Anayetoa maelezo ni Katibu Msaidizi wa UMUMAGE, John Ngenda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


older | 1 | .... | 1683 | 1684 | (Page 1685) | 1686 | 1687 | .... | 1897 | newer