Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1682 | 1683 | (Page 1684) | 1685 | 1686 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu akionyesha ishara ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani.


  Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani.


  NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE

  NAIBU Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu amelitaka shirika la umeme (Tanesco) lizingatie kufikisha umeme katika taasisi za umma ikiwemo shule na zahanati ili ziondokane na changamoto hiyo. Aliyasema hayo ,kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe ,mkoani Pwani wakati alipokwenda kuwasha umeme kijijini hapo .

  Subira alisema, kwanza shirika hilo lihakikishe linaipatia umma shule ya msingi Kisanga ili waondokane na adha hiyo.“Tanesco wakati wa kuunganisha umeme mhakikishe taasisi hizo ikiwemo zahanati,shule na ofisi za serikali zinapata umeme ili kurahisisha utoaji huduma kupitia miradi ya umeme vijijini (REA)” alisema.

  Aidha Subira alieleza ,wizara ina malengo ya kuhakikisha umeme unawaka kila kijiji ambapo kwa sasa miradi iko mingi lengo likiwa ni kufanikisha suala hilo.“Pia wananchi wanapaswa kutumia miradi hiyo kwani itakapokwisha bei haitakuwa hii ya 27,000 itaongezeka hivyo wachangamkie fursa hiyo,” alisisitiza Subira. 
   
  Diwani wa kata ya Kisanga, Pili Chambuhi alisema,kijiji hicho kupata umeme ni mkombozi kwao kwani utasaidia kufanya shughuli ndogondogo za ujasiriamali. Alielezea hadi sasa jumla ya nyumba 60 zimeunganishiwa umeme.Pili, alisema kuwa shirika hilo linapaswa kupeleka huduma hiyo kwenye maeneo ya ndani ndani na si maeneo ya barabarani peke yake.

  0 0


  Na Benny Mwaipaja, WFM, Tanga

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na wafanyabiashara mkoani Tanga na kuwaeleza kuwa Serikali imeanza kulipa  madai ya marejesho ya kodi ya Ongezeko la thamani (VAT Refund) kwa kampuni na wafanyabiashara mbalimbali nchini wakiwemo waagizaji wa sukari za viwandani ambao madai yao yamehakikiwa kuanzia mwezi huu wa Septemba, 2018.

  Kauli hiyo ya Serikali inafuatia maombi ya wafanyabiashara wa mkoa huo walioitaka Serikali kuwalipa wafanyabiashara wanaodai kurejeshewa fedha zao zinazotokana na kufanya biashara zao nje ya nchi pamoja na  wazabuni mbalimbali.

  Waziri Mpango amesema kuchelewa kulipwa kwa madai hayo kunatokana na kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu hivyo kutaka kuingizia Serikali hasara kwa kulipa madai hewa. ‘Kuna baadhi ya wafanyabiashara sio waaminifu, mfano tulipofanya uhakiki tuligundua madai hewa ya pembejeo ya zaidi ya Shilingi bilioni 87’, alisema Waziri Mpango.

  Dkt. Mpango aliwahakikishia wafanyabiashara wote nchini kuwa serikali itahakikisha inaweka mazingira mazuri ili kila mwananchi mwenye nia njema aweze kufanya biashara halali itakayomletea faida na serikali iweze kukusanya kodi bila ya kumuonea mtu. 

  Awali Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Bw. Deogratias Ruhinda, alisema kuwa wafanyabiashara hasa wakulima wa zao la Mkonge wanakutana na changamoto kubwa kutokana na serikali kuruhusu na kutoa msamaha wa baadhi ya kodi kwa wafanyabiashara wanaoingiza Kamba za manila hapa nchini, hivyo kulifanya zao la mkonge kutokuwa na soko hapa nchini kutokana na bei ya Kamba hizo za nje kuwa chini ukilinganisha na Kamba zinazotokana na mkonge.

  Aidha wafanyabiashara hao waliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza kina cha Bandari ya Tanga ili meli kubwa ziweze kuja katika bandari hiyo na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kwenda nje ya nchi tofauti na ilivyo sasa ambapo bidhaa nyingi kutoka Tanga zinasafirishwa kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam au Mombasa jambo linalowaongezea gharama kubwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga.

  Akijibu hoja mbalimbali za wafanyabiashara hao, Dkt. Philip Mpango, aliwahakikishia kuwa Serikali itazipitia na kuzitolea ufafanuzi kero zote zinazohusu kodi ili kurahisisha biashara na kuweka mahusiano mazuri kati ya wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania, hali ambayo itaongeza mapato kwa serikali. Pia amesema Serikali inalifanyia kazi suala la wingi wa kodi anazolipa mfanyabiashara kwa Taasisi mbalimbali za serikali ili kodi hizo ziweze kutozwa sehemu moja  na kupunguza adha wanazopata walipa kodi.

  Waziri Mpango aliwataka wafanyabiashara hao kutosita kuishauri serikali njia bora ya kukusanya kodi na kutoa maoni yao jinsi ya tozo mbalimbali zinazotozwa na serikali kwa kuiandikia Mamalaka ya Mapato Tanzania au Wizara ya Fedha na Mipngo ili serikali iweze kuboresha maeneo yenye mapungufu kwa faida ya Taifa. Pia Mh.Waziri amewataka wafanyabiashara kote nhini kushiriki katika mikutano ya sera za kodi inayondaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango ambayo huanza mwezi Disemba hadi Januari kila Mwaka.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb), akiongea na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga alipokutana na wafanyabiashara hao katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, kusikiliza maoni na changamoto zinazowakabili katika masuala ya kodi. 
   Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara hao Jijini Tanga kuhusu kuimarisha ushirikiano kati yao na Serikali ili kuliletea maendeleo Taifa.
   Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh.Thobias Mwilapwa akiwahutubia wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kabla ya Kumkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kuzungumza na wafanyabiashara hao  katika Mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
   Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), (waliokaa mbele) wakiwa katika mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga.
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0   Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akionesha Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania mara baada ya kuizindua, kushoto ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
  2 (7)
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akimkabidhi Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kati Ezekiel Kitilya mara baada ya kuizindua ripoti hiyo.
  5 (5)
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akimkabidhi Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania (Picha zote na Hassan Mabuye-WANMM).
  4 (6)
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akifuatilia uwasilishwaji Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania.
  3 (6)
  Baadhi ya washiriki waliohudhuria uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi.

  Na Munir Shemweta, Dodoma

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema kasi ya utoaji hati za umiliki wa ardhi na makazi imeongezeka kwa kasi ambapo hadi kufikia septemba mwaka huu 2018 jumla ya hati 25,463 zimeandaliwa.

  Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa uwasilishwaji matokeo ya utafiti kuhusu haki na usalama na umiliki wa rasilimali ardhi na makazi jijini Dar es salaam leo Mabula alisema jumla ya hati 17,680 zilikuwa zimewasilishwa ofisi za kanda kwa ajili ya usajili na hati 9,739 zimeshakamilika.

  Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na Wizara yake katika kutoa hati lakini takwimu zinaonesha kuwa hati nyingine zimeandaliwa katika halmashauri lakini zilizowasilishwa kwenye ofisi za kanda husika ni chache  kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuandalia hati

  Kwa mujibu wa Mabula, kuna hati nyingi zinaonekana kuwasilishwa ofisi za kanda lakini hati zilizokamilika ni chache kutokana na hati nyingi zilizowasilishwa katika ofisi za kanda kuwa na upungufu mbalimbali na hivyo kusababisha hati hizo kutokamilika kwa wakati.

  Akigeukia suala la haki na usalama na umiliki wa rasilimali ardhi na makazi kwa wananchi waishio vijijini, Mabula alisema hadi kufikia Mei 2018 jumla ya vipande vya ardhi 96,257 vimepimwa katika vijiji 91 na hati za kimila 20,583 zimeandaliwa na vijiji 20 vimeandaliwa na mipango ya makazi ambapo jumla ya viwanja 18,224 vimepimwa kwa ajili ya kuandaliwa hati ya haki miliki ya kimila.

  Kwa mwaka 2018/2019 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kuandaa hati za kimila 120,000, mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji 30 na mpango wa kina kupima viwanja 20,000 kwa lengo kumuwezesha mwananchi wa kawaida kuwa na uhakika na usalama ya miliki yake na kuepusha migogoro.

  0 0

   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali yanayuhusu Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini na ameziagiza NGOs kuleta taarifa za fedha za mwaka 2016 na 2017 na utekelzaji wa miradi yake kwa ofisi ya Msajili  ndani ya siku 30 . Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.


  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeyaagiza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuwasilisha kwa Msajili wa Mashirika hayo taarifa za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2016 na 2017 ndani ya siku thelathini kuanzia leo Septemba, 28, 2018.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali yanayuhusu Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.Dkt. Ndugulile  ameyataka pia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwasilisha taarifa inayoonesha miradi iliyotekelezwa kwa fedha iliyopatikana  kwa mwaka wa 2016 na 2017 na kutoa taarifa ya vyanzo vya mapato husika ikiambatana na hati za makubaliano za vyanzo husika kwa kipindi cha miaka hiyo.

  Naibu Waziri Dkt. Ndugulile ameeleza kuwa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 inasisitiza misingi ya uwazi na uwajibikaji kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.Amesisitiza  kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 29(a) na (b) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Na. 24 ya mwaka 2002, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yana wajibu wa kuwasilisha taarifa za kazi na fedha kila mwaka kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kwa Umma.

  Ameongeza kuwa Kanuni za utendaji za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali za mwaka 2008 zinasisitiza uzingatiaji wa misingi ya uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi, masuala ya fedha na utawala hivyo wanufaika wa miradi yao, Halmashauri wanapofanya miradi na vyombo vya habari wana haki ya kupata taarifa hizo.Dkt. Ndugulile ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa miongozo hiyo bado Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mengi yamekuwa yakikiuka matakwa husika hivyo kuleta mkanganyiko katika jamii.

  “Serikali itaendelea kufuatilia na haitosita kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo kuzifutia usajili NGOs ambazo zitashindwa kutekeleza agizo hili ndani ya muda uliopangwa” alisisitiza Dkt. Ndugulile.Pia Dkt.Ndugulile ameziagiza NGOs nchini zizingatie ushiriki wa wazawa wa ndani katika miradi wanayoitekeleza kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za NGOs hapa nchini.Aidha Dkt. Ndugulile ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutuma taarifa zao za fedha na za miradi kila mwaka kama ilivyoagizwa kupitia barua pepe ifuatayo dngo@communitydevelopment.go.tz .

  Maagizo haya kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanakuja siku chache mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) Dkt. John Jingu kufuatilia utendaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini wakati alipokuwa akimuapisha kuwa Katibu Mkuu huyo  katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.

  0 0

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, kuhakikisha wamewakamata wahusika wa mauaji ya watu wanane yaliotokea mwezi mmoja uliopita katika Kata ya Kitanga yaliosababishwa na mgogoro wa wakulima na wafugaji kijijini humo.

  Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kitanga wilayani humo, jana, Waziri Lugola alitoa siku mbili kwa Jeshi hilo kukamilisha kazi hiyo kwa kufanya operesheni maalum ili kuondoa taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.

  “Lazima tupendane, kwanini tunauana, wasukuma na waha wote ni ndugu, tushirikiane, tupendane ili tuweze kuishi kwa Amani, hizi chuki nataka ziishe, mkuu wa wilaya shirikiana na polisi ili hili tatizo liweze kuisha haraka iwezekananavyo.,” alisema Lugola.

  Waziri Lugola aliongeza kua, katika siku mbili alizotoa anataka watuhumiwa wote wawe wamekamatwa na kushtaki kwa mauaji ya watu wanane.
  Huku akiwa anashangiliwa na wananchi hao, Lugola alisema Serikali itaendelea kuwalinda wananchi wake kwasababu Tanzania ni nchi ya Amani na pia watu wake wana upendo.

  Lugola pia alimtaka Mkuu wa Wilaya wa Kasulu…..kupitia Kamati yake ya Ulinzi na usalama ihakikishe wanatoa maeneo ya wafugaji na pia marufuku kwa wafugaji hao kuingiza mifugo mashambani.

  “Mkulima haupaswi kwenda kulima sehermu ya malisho ya mifugo, halikadhalika wafugaji marufuku kuingiza mifugo yenu katika eneo la wakulima, huo ni utaratibu mzuri, tuufuate na tuzingatie ili kuimarisha Amani katika eneo hili,” alisema Lugola.

  Aidha,  katika hatua nyingine Waziri Lugola alizungumza na wananchi wa mji wa Kasulu na kusema Serikali inaangalia uwezekano wa kuandaa vibali maalum vitakavyoruhusu wakulima wa wilaya hiyo kuwatumia vibarua kutoka nchi za Burundi na Kongo ili kupunguza wahamiaji haramu wanaokuja mkoani Kigoma kufanya kazi za kilimo ambao baadhi yao si waamini.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kata ya Kitanga, Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara katika kata hiyo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi baada ya kutokea mauaji katika eneo hilo yaliyotokana na vurugu ya wakulima na wafugaji mwezi uliopita. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza mwananchi wa mjini Kasulu alipokua aamuuliza maswali, baada ya Waziri huyo kuwataka wakazi wa mji huo kutoa kero mbalimbali zinawakabili wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mkazi wa Kijiji cha Kitanga, Shabani Funyenge, alipokua anamfafanulia jinsi ugomvi wa wakulima na wafugaji ulivyoanza katika Kijiji hicho, Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma, uliosababisha watu wanane kuuawa. Lugola alitoa siku mbili kwa watuhumiwa wa mauaji hayo wawe wamekamatwa.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Geita Mjini Mhe. Constantine Kanyasu mara baada ya kuwasili Mkoani Geita, kujionea Maonesho ya Dhahabu yanayofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita, kuanzia Septemba 24 hadi Septemba 30, 2018.
  PICHA F
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony akiangalia bidhaa za Wajasiriamali katika Maonesho ya Dhahabu yanayofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita, kuanzia Septemba 24 hadi Septemba 30, 2018.
  PICHA H
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi. Robert  Gabriel  wakitoka katika Banda la Maonesho la Mamlaka ya Mapato Tazania (TRA), katika Maonesho ya Dhahabu yanayofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita, kuanzia Septemba 24 hadi Septemba 30, 2018.
  PICHA A
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi. Robert  Gabriel(kulia) wakati alipofika Mjini Geita kujionea Maonesho ya Dhahabu yanayofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita, kuanzia Septemba 24 hadi Septemba 30, 2018.
  PICHA B
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi. Robert  Gabriel(kulia) wakifuatilia masuala mbalimbali yalikuwa yakiwasilishwa na wadau wa sekta ya madini katika kikao kilichofanyika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita, kwenye Maonesho ya  Dhahabu kuanzia Septemba 24 hadi Septemba 30, 2018.
  PICHA C
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kampuni ya NGM Gold Mine inayomilikiwa na Bw. Gungu Silanga ambaye ni mkazi wa Simiyu wakati alipofika Mkoani  Geita Mjini Geita kujionea Maonesho ya Dhahabu yanayofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita, kuanzia Septemba 24 hadi Septemba 30, 2018.

  PICHA G
  Baadhi ya wananchi wa Mji wa Geita wakiangalia teknolojia mbalimbali zinazotumika katika uchimbaji wa dhahabu, katika Maonesho ya Dhahabu yanayofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita, kuanzia Septemba 24 hadi Septemba 30, 2018.
  PICHA E
   Baadhi ya Viongozi na wadau wa Madini wakifuatilia kikao kilichofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita, wakati wa  Maonesho ya  Dhahabu yanayofanyika kuanzia Septemba 24 hadi Septemba 30, 2018.
  Na Stella Kalinga, Simiyu.

  Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Geita wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi. Robert  Gabriel kwa ubunifu waliofanya wa kufanya Maonesho ya Kipekee ya dhahabu hapa nchini.

  Mtaka ameyasema hayo mara baada ya kuzungumza na viongozi wa Mkoa wa Geita na kutembelea mabanda ya maonesho katika Maonesho ya Dhahabu yanayofanyika  Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita kuanzia Septemba 24, 2018.

  Amesema Watanzania wengi wamekuwa wakienda kushiriki maonesho ya dhahabu katika mataifa mbalimbali barani Afrika na nje ya bara la Afrika lakini kupitia maonesho haya Watanzania wameanza kujionea teknolojia mbalimbali za uchimbaji wa madini hapa nchini.

  “ Ninawapongeza sana viongozi wa Geita kwa kuandaa maonesho haya ya kipekee hapa nchini, tumekuwa na shughuli nyingi sana za uchimbaji madini lakini sisi sote ni mashahidi shughuli hizi tumekuwa tukiziona wakati wa Mei Mosi kupitia kile chama kinachohusisha watu wanaofanya kazi za madini, hatujapata jambo linaloonesha shughuli za migodini na mazao yanayotokana na migodi kama dhahabu” alisema Mtaka.

  Ameongeza kuwa ubunifu huo uliofanywa na Viongozi wa Mkoa wa Geita hasa wa kuyapa maonesho haya jina la Kiswahili ya “Maonesho ya Dhahabu” ambalo linasadifu shughuli zinazofanyika katika mkoa huo ambao ni mzalishaji mkubwa wa dhahabu, utachangia kuongeza watalii na wageni wengi watakaokuja hapa nchini kupitia maonesho hayo.

  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi. Robert Gabriel ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushuhudia maonesho hayo ili kujionea teknolojia za uchimbaji madini, kupata huduma za kifedha katika taasisi za kifedha, kupata huduma na elimu juu ya utatuzi wa changamoto za kibiashara hususani upatikanaji wa mitaji na changamoto za uchimbaji katika kliniki ya biashara.

  Aidha, Mhandisi. Gabriel amesema maendeleo katika mkoa wa Geita hayaepukiki kutokana na sekta ya madini kuwa na  mchango mkubwa katika uchumi ambapo amebainisha kuwa kupitia uchimbaji dhahabu mkoa unapata ushuru, fedha za msaada kwa  jamii (Corporate  Social Responsibility) kutoka kwenye makampuni yanajihusisha na uchimbaji madini zilizosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Mhe. Leonald Bugomola amesema maonesho ya dhahabu mwaka 2019 yataanza mapema na Halmashauri yake kama mwenyeji wa maonyesho hayo imejipanga kutafuta eneo kubwa zaidi ekari 100 ,  kwa kuwa mpango wa mkoa ni kuwa na maonesho yenye hadhi ya Kimataifa yatakoshirikisha washiriki wengi ikilinganishwa na mwaka huu.

  Nao baadhi ya wachimbaji wadogo wameshukuru uanzishwaji wa maonesho hayo ambayo yatasaidia kupata utaalamu juu teknolojia mbalimbali zinazotumika kuchimba madini na kupata elimu ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya madini kutokana na wadau mbalimbali kukutanishwa pamoja na kujadiliana kuhusu maendeleo ya sekta ya madini.

  Maonesho ya Dhahabu mkoani Geita yameanza Septemba 24, 2018 na yanatarajiwa kuhitimishwa Septemba 30, 2018 yakiwa na Kauli Mbiu: TEKNOLIJIA BORA YA UZALISHAJI WA DHAHABU KWA MAENDELEO YA KIJAMII NA UCHUMI WA VIWANDA”
  MWISHO.

  0 0

  Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

  Waandishi wa habari jioni hii wagomewa kuingia ndani Kwenye hafla ya uzinduzi wa filamu ya D.A.D ya Msanii wa kibongo nchini  wema sepetu maarufu kamaambayo amemshirikisha msanii kutoka nchi ya Ghana Van Vicker.

  Akizungumza nje ya ukumbi Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema shughuli hiyo ilishanunuliwa na moja ya chombo cha habari hapa nchini ambao wana mamlaka yote ya kurusha kwa matangazo ya moja kwa moja na kupiga Picha zote.

  Mmoja wa wanahabari akiongea na Michuzi TV ameeleza kuwa ni vibaya kwani mpaka kuweza kuingia ndani ni lazima kulipa Dola elfu 20 .

  Hivyo basi kitendo hiko kilichofanywa na waandaji wa shughuli hiyo kimewanyima nafasi wanahabari ,na sio la haki kwani mpaka alipofikia nguvu nyingi zimetokana na kushirikiana na wanahabari.

  Kitendo hiko kinaweza kuibua matabaka,pamoja na chuki kutokana na ubaguzi huo uliofanyika katika hafla hiyo na watu kutafsiri vibaya kuwa imeonekana chombo hicho kuwa bora kuliko vingine.

  Van Vicker aliwasii nchini jana kwa ajili ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyofanywa miaka mitatu iliyopita.

  0 0

   *Ni leo Septemba 29 ,kufanyika katika ukumbi wao uliopo Mikocheni B kuanzia saa tisa alasiri
  *Wasanii maarufu ndani na nje ya nchi kutoa burudani

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
   NAFASI Art Space katika kusheherekea miaka 10 tangu kuanzisha kwake wanatarajia kufanya tamasha kubwa na la aina yake leo kuanzia saa tisa alasiri ambapo wasanii maarufu katika uchoraji, uimbaji na waimbaji wa muziki wa dansi wafanya show kwa mashabiki na wapenzi wa Sanaa ndani na nje ya nchi.
  Tamasha hilo linatafanyika katika Ukumbi wa Nafasi Art Space uliopo Michokeni B jijini Dar es Salaam na kwamba hakutakuwa na kiingilio chochote na lengo la kufanya hivyo ni kutoa nafasi kwa mashabiki na wapenzi wa sanaa kufika kwa wingi.
   Akizungumza na Michuzi Blog jana kuhusu Tamasha hilo ambalo limepewa jina la Sanaa Yetu Festival, Ofisa Maendeleo Biashara na Masoko wa Nafasi Art Space Agnes-Senga Tupper amesema katika kusheherekea miaka 10 ya Nafasi Art Space wanatarajia kufanya show hiyo matata ambayo itagusa sanaa za aina zote nchini Tanzania.
  Amesema zaidi ya wasanii 19 wa uchoraji, uimbaji , wanamuziki wa dansi ni miongoni mwa watakaotoa burudani kwa mashabiki wao ambao kwa kipindi cha miaka 10 wamekuwa wakiwaunga mkono.
  Tupper amefafanua kwamba “Mwaka 2008 kikundi kidogo cha wasanii wa Tanzania walijikusanya na kuanzisha Nafasi Art Space kwa ajili ya wasanii nchini kuwa na sehemu ya kufanya kazi zao, pamoja na msaada kutoka Denmark Embassy, Nafasi Art Space ilianzishwa.Tangu wakati huo, Nafasi imeweza kusaidia wasanii zaidi ya 100 nchini Tanzania kuendeleza na kukuza vipaji vyao .
   “Hii imewapatia wapenzi wa sanaa fursa ya kuona, kujifunza na kufahamu sanaa na utamaduni jijini Dar es Salaam pamoja na nje ya nchi. Hivyo kwa mwezi huu wa Septemba, Nafasi Art Space imekuwa ikisherehekea miaka 10 kwa kufanya matukio mbalimbali ya kisanaa kwa ajili ya umma,”amesema Senga.
   Ametaja baadhi ya matukio ambayo wameyafanya kama sehemu ya kusheherekea miaka 10 ambayo kesho ndio kilele chake ni pamoja na kufanya mkutano na waandishi wa vyombo vya habari, uzinduzi kwa kuchora live soko la Karume, kutembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wameshiriki kwenye kipindi cha Jukwaa la Sanaa pamoja na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA).
  Pia wameshiriki Siku ya Usafi Dunaini kwa kusafisha eneo la Coco Beach, kufanya warsha ya sanaa katika Shule ya Mgulani na Chang’ombe za jijini Dar es Salaam pamoja na uchoraji Graffiti Live Nafasi Art Space.
  Senga amesisitiza “Kwa kumalizia tunafanya bonge moja la Festival –Sanaa Yetu Festival .Hivyo Septemba 29 (Jumamosi)  wakati wa Festival hiyo ikiendelea kutakuwa na nafasi ya kuchora T-shirt kwa mashabiki watakao hitaji. Pia kutakuwa na maonesho, uuzaji wa sanaa za uchoraji kutoka kwa wasanii mashuhuri dunia nzima ambao ni wanachama wa Nafasi,”amesema Senga.
  Pia amesema baada ya hapo itafuata Show ya wasanii kama vile Muda Africa,  Wamwiduka Band, Wahapahapa Band, Bagamoyo Players, Fashion Show ya Makeke International.Kisha watamaliza na Mfalme wa Kisengeli Mfalme Ninja Na DJ Frank.
  “Septemba hii ni fursa kwa Nafasi kusherehekea mafanikio ya sanaa ya kisasa nchini Tanzania kwa kutoa shukrani kwa wafadhili na mashabiki wetu, na kuleta jamii pamoja katika ujenzi wa kizazi kijacho cha wasanii na wapenzi wa sanaa.  Nisisitize hakuna kiingilio na watu wa rika zote wanakaribishwa.Lakini Michango ya tunapokea,”amesema Senga.
  Kuhusu mgeni rasmi amesema wanatarjia kuwa na mgeni rasmi katika tamasha hilo ambaye atatoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania hasa kwa kuzingatia ndio wafadhili wakuu wa Nafas Art Space.
  Baadhi ya matukio ambayo wameyafanya kama sehemu ya kusheherekea miaka 10 ambayo leo ndio kilele chake ni pamoja na kufanya mkutano na waandishi wa vyombo vya habari, uzinduzi kwa kuchora live soko la Karume, kutembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wameshiriki kwenye kipindi cha Jukwaa la Sanaa pamoja na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA).
   Michoro mbalimbali ilichorwa na vijana wenye vipaji ikiwa ni sehemu ya maandalizi
   Vikundi mbalimbali vilishiriki kuelekea kilele cha  NAFASI Art Space ambapo leo inatimiza miaka 10 tangu kuanzisha kwake

  0 0

  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imekabidhi rasmi majukumu kwa Balozi wa Hiari wa Utalii Bi Bi Judith Raymond Mushi aliyepewa jukumu la kufanya kazi na TTB ya kuvitangaza vivutio vya Tanzania katika nchi ya Italia. Bi. Judith ambaye ni Mtanzania ambaye anafanya kazi ya kufundisha Lugha ya Kiswahili nchini Italia. 

  Wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Septemba 27, 2018 katika ofisi za TTB jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TTB Bi. Devota Mdachi amemkabidhi rasmi sharia na taratibu zinatakiwa kufuatwa wakati anatekeleza jukumu hilo kupitia matukio mbalimbali atakayokuwa anahudhuria akiwa italia. 
  Pamoja na msaafu huo Bi . Judy alikabidhiwa majarida yenye taarifa za utalii wa Tanzania yanayotumiwa kama nyenzo ya kutangazia utalii wa Tanzania katika masoko mbalimbali ya Utalii Duniani. 

  TTB imeweka utaratibu maalumu wa kuwapata mabalozi wa hiari wa Utalii.

  0 0


  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano ya uelimishaji wa tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma ya afya wapatao 111  kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma, yaliyokuwa yakiendeshwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi mjini Singida, wakionyesha stika za utambuzi wa mtoa huduma (Daktari) kwenye vituo vyao vya kazi, mwishoni mwa mafunzo hayo Septemba 28, 2018.

    NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida
  MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF umefanikiwa kutoa mafunzo kwa madaktari na watoa huduma ya afya wapatao 765 nchini nzima Tanzania Bara, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omary, amesema.

  Dkt. Omary ameyasema hayo leo Septemba 28, 2018 mwishoni mwa mafunzo ya siku tano ya uelimishaji wa tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma ya afya wapatao 111 kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma yaliyokuwa yakifanyika kwenye chuo cha Uhasibu Mkoani Singida.

   “Katika kipindi hiki cha miaka miwili ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko kupokea madai na kulipa mafao ya fidia, tayari tumetoa elimu kwa madaktari na watoa huduma ya afya 765 na haya ni mafanikio makubwa katika suala zima la kufanya tathmini iliyo sahihi ili hatimaye mfanyakazi mwenye madai aweze kulipwa fidia stahiki.” Alibainisha Dkt. Omary. 

   Alisema elimu waliyoipata washiriki hao itawaweka kwenye nafasi nzuri ya kutoa haki kwa pande zote mbili, mfanyakazi (mdai fidia) na Mfuko wenyewe kwani sasa wataweza kufanya tathmini ya ulemavu (impairment assessment) inayozingatia muongozo na misingi ya sharia.Kwa mujibu wa sheria, Mfuko ili uweze kulipa mafao ya fidia kwa mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, ni budi daktari amfanyie tathmini ya kiwango cha maumivu au jeraha lililopelekea ulemavu uwe ni wa muda au wa kudumu, lakini pia daktari atafanya tathmini kwa mfanyakazi aliyepata maradhi yatokanayo na kazi ili hatimaye matokeo ya tathmini hiyo ndiyo yatakayotumiwa na wataalamu wa Mfuko katika kufikia maamuzi ya kulipa fidia kwa muhusika.

  Aidha Mfuko pia unajukumu la kulipa fidia kwa wategemezi wa Mfanyakazi aliyefariki akiwa anatekeelza wajibu wake wa kazi.

  Akiahirisha mafunzo hayo, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Ernest Mugeta, alisema ni matarajio ya mafunzo kwa washiriki kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu na pasiwepo ushawishi wa mali au fedha ili haki itendeke."Nawaasa ndugu zangu madaktari, haya mafunzo mliyoyapata, mkatumie ujuzi huo kwa makini. Ninyi sasa ni wataalamu mliobobea ili kuusaidia Mfuko kufikia malengo yaliyokusudiwa.” Alisema Dkt. Mugeta.Aliwaomba madaktari kufanya kazi hiyo ya tathmini kwa umakini wa hali ya juu kwani matokeo ya tathmini hiyo yanahusu maisha ya mtu, kwa vile taarifa ya tathmini ndiyo itakayotumiwa na Mfuko kutoa fidia kwa muhusika.Alitahadharisha kuwa daktari au mtoa huduma ya afya, endapo atafanya kazi hiyo ya tathmini kinyume cha sheria, basi ajue kuwa amevunja sheria na anaweza kushtakiwa.Akitoa shukrani, kwa niaba ya washiriki wengine, Dkt.Yohana Masonda, alisema, mafunzo hayo yatakuwa nyenzo bora katika utendaji wao wa kazi kwani sasa wamepata uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.Alisema kabla ya mafunzo hayo walikuwa wakifanya akzi hizo sio kwa utaalamu sana ama umahiri na kwamba faida za mafunzo kwao ni kutoa tathmini nzuri kwa waathirika wa ajali au magonjwa yatokanayo na kazi.

  Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Ernest Mugeta, (katikati) akipeana mikono na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF) Dkt. Abdulsalaam Omary, baada ya kufunga mafunzo hayo Septemba 28, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa kundi la wataalam wa afya mahala pa kazi, Dkt. Robert Mhina.
   Meneja Madai na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi 9WCF), Dkt. Ali Mtulia akitoa mada.
   Dkt. Pascal Mages, kutoka WCF akiwasilisha mada ya namna kwa wajumbe
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bi. Laura Kunenge, (Kulia), akimkabidhi stika ya utambuzi wa mtoa huduma, mshiriki kutoka Mkoani Dodoima Dkt. Rehema Sovela, mwishoni mwa mafunzo hayo.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omary, akitoa hotuba ya ukaribisho.

   Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
   Mgeni rasmi, Dkt.Ernest Mugeta, (kushoto), akimkabidhi cheti cha ushiriki, Dkt.Mushi kutoka hospitali ya Rufaa ya Maweni Mkoani Kigoma.
   Mgeni rasmi, Dkt.Ernest Mugeta, (kushoto), akimkabidhi cheti cha ushiriki, Dkt.Upendo Mabongo, kutoka kituo cha afya Kibakwe Mkoani Dodoma

   Picha ya pamoja meza kuu na madaktari kutoka Mkoa wa Kigoma
    Picha ya pamoja meza kuu na madaktari kutoka Mkoa wa Tabora.
    Picha ya pamoja meza kuu na madaktari kutoka Mkoa wa Dodoma
  Picha ya pamoja meza kuu na  madaktari kutoka mkoa wa Singida.

  0 0

  Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani  Akikabidhi hundi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Singisi ,Safira Ndelwa.Benki hiyo imetoa msaada huo kwa ajili ya mabati na ukarabati wa madarasa.Picha na Pamela Mollel,Arusha
  Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani  Akikabidhi hundi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Singisi ,Safira Ndelwa.Benki hiyo imetoa msaada huo kwa ajili ya mabati na ukarabati wa madarasa
  Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya milioni 4 kwa ajili ya kusaidia shule ya msingi Singisi.
   Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani  akikabidhi hundi kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Singisi
   Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani  akipokea zawadi kutoka wanafunzi wa shule ya msingi Singisi.
   Picha ya pamoja

  CBA YATOA MSAADA WA MILIONI 4 SHULE YA SINGISI
  Na Pamela Mollel,Arusha.
  Benki ya  CBA  imetoa msaada wa shilingi milioni 4 kwa shule ya msingi Singisi kwa ajili ya mabati pamoja na ukarabati wa shule hiyo ili kusaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa na uchakavu wa majengo.
  Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano,Julius Konyani  alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kusaidia  watoto wa kitanzania waweze kupata elimu bora ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.Julius alisema kuwa benki hiyo imeamua kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi kwa kutoa fedha hizo licha ya msaada huo wamekua wakisaidia chumba cha watoto njiti kwa kutoa vifaa vya kitaalamu ili kuokoa maisha ya watoto.
  Mkuu wa Shule hiyo Safira Ndelwa    ameshukuru msaada huo ambapo amesema kuwa msaada huo utawasaidia kumalizia ujenzi wa uzio wa shule hiyo pamoja na kukarabati majengo ya shule hiyo ambayo ni chakavu.Hata hivyo ameiomba benki hiyo iweze kuwasaidia kuwajengea vyumba vya madarasa kwani shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa madarasa hali inayosababisha msongamano darasani inayowalazimu kuingia darasani kwa awamu huku walimu wakifundisha kwa zamu.
  “Tunaomba benki ya CBA isituache iendelee kutusaidia katika maeneo mengine ambayo kuna changamoto ili wanafunzi waweze kusoma katika hali bora” Alisema .Diwani wa Kata ya Seela Singisi Penzila Palangyo amesema kuwa ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya elimu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inasonga mbele na kusaidia maisha ya watu wengi

  0 0

  Na. VERO IGNATUS, ARUSHA

  Wakati tukielekea kusherehekea siku ya wazee septemba 30 imeelezwa kuwa zaidi ya asilimia 80% (takriban mil2)ya wazee hapa nchini wanaishi vijijini. 
  Akizungumza na vyombo vya habari kamishna wa ustawi wa jamii kutoka wizara ya Afya jinsia wazee na watoto Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa juhudi  za ziada zinashitajika ili kuwafikia na kuweza kuhakikisha wanapata huduma stahiki kama ilivyo katika sera ya Taifa 
  Ng'ondi amesema maadhimisho ya siku ya wazee duniani kitaifa yatafanyika jijini Arusha ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Alhaji Ally Hassan Mwinyi

  Aidha kwa mujibu wa shirika la Help Age International limeweka wazi kuwa hapa nchini asilimia 27%  ya wazee wote (677,043) wanaishi wenyewe bila msaada wa mtu yeyote.Amesema kuwa zaidi ya asilimia 83% ya wazee wote (2.1m) wanaishi katika familia na kupata angalau matunzo ya familia tofauti na wenzao ambao wanaisha wangali pekee yao
    Nchini Tanzania  kuna familia ambazo wazee wamekuwa wakibeba majukumu ya kuwalea watoto yatima kama takwimu zinavyoonyesha asilimia 40% ya watoto yatima wanalelewa na familia za wazee.Mara baada ya uzinduzi wake kesho wazee watapata fursa ya kupata huduma ya kupima afya kupata ushauri wa kitabibu pamoja na ufunguzi wa maonyesho ya kazi mbali mbali za mikono zinazofanywa na wazee.
  Kauli mbiu ya mwaka huu ni Wazee ni Hazina ya Taifa: Tuenzi Juhudi za Kutetea Haki na Ustawi Wao’’. Kaulimbiu hii inahimiza Serikali na Jamii kwa ujumla kutambua na kuenzi jitihada za Wazee katika ujenzi wa Taifa letu.“Tarehe moja mwezi ujao itakuwa siku ya wazee nawaombeni nyote kujitokeza kwa wingi wakiwemo wazee wetu kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid”alisema Dkt.Ng’ondi
  Mmoja ya wazee aliohojiwa mkazi wa jiji la Arusha Swalehe Allly amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inatakiwa kuonyesha juhudi zake kwa kuwaandalia wazee wetu angalau pensheni kama takwimu zinavyoonyesha kuwa Tanzania Bara 96% ya wazee wote hawana pension ya uzeeni
  Amesema kuwa tuige mfano na kuonyesha juhudi za serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa kuwapatia  Wazee 58,371 kati yao 27,000,(46 %) wanapata pesheni Wenye umri wa Miaka 70.“Hapa utaona jinsi maisha ya uzee yalivyo kuwa na mtihani kama juhudi za maksudi hazitachukuliwa na serikali zetu kote ulimwenguni kuhakikisha wazee wanapata matunzo stahiki kama tawimu hizi” alisema Ally
   Imeonyesha juhudi kama hazitachukuliwa na kufanyiwa kazi, asilimia Zaidi ya 50% ya familia za wazee wanaishi chini ya kiwango cha umaskini. kigezo- Benki ya Dunia.
   Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Alhaji Ally Hassan Mwinyi (picha kutoka Maktaba)

  0 0   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiongoza dua ya kuwaombea marehemu na waliopata manusura katika ajali ya Mv.Nyerere baada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti Masjid Tambaza Jijini Dar es Salaam jana
  DSC_8343
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Waumini wa dini ya kiislamu mara baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Masjid Tambaza Jijini Dar es Salaam jana
  DSC_8376
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Waumini wa dini ya kiislamu mara baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Masjid Tambaza Jijini Dar es Salaam jana,
  Picha na Ikulu

  0 0


  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na watumishi wa kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita ambapo aliwasisitiza umuhimu wa kufanya kazi ya uandishi wa Habari kwa kuzingatia weledi.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akishiriki Kipindi cha Moja kwa moja katika kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita ambapo aliongelea masuala mbalimbali ikiwamo miradi mikubwa inayotekelezwa na iliyotekelezwa na Serikali katika kipindi cha Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita
  Mwenyekiti Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete akishiriki Kipindi cha Moja kwa moja katika kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita ambapo alisistiza kuwa wataendelea kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano Serikalini na kuendelea kurahisisha uhusiano kati ya waandishi wa habari na Maafisa Habari wa Serikalini.
  Katibu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Abdul Njaidi akiongea na watumishi wa kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita ambapo ambapo aliwasisitiza kuhusu umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo katika mkoa wa Geita.

  Watumishi wa kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokutana nao.

  0 0  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpima shinikizo la damu mwandishi wa habari kutoka Gazeti la Mtanzania Veronica Romwald kuashiria uzinduzi wa upimaji afya ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Septemba. Uzinduzi huo ulienda  sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari ikiwemo kiharusi, madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo, lishe bora kwa afya ya moyo na tezi dume.
  upimaji 2
  Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nancy Mallya akimpima sukari kwenye damu Mwandishi wa Habari Mkongwe Allan Lawa wakati wa uzinduzi wa upimaji afya ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Septemba. Uzinduzi huo ulienda  sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari ikiwemo kiharusi, madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo, lishe bora kwa afya ya moyo na tezi dume.
  upimaji 3
  Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophylly Mushi akitoa ushauri wa afya ya moyo kwa  Mhariri wa gazeti la Habari Leo Mgaya Kingoba mara baada ya kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wa uzinduzi wa upimaji wa afya ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inayoadhimishwa kila mwaka  tarehe 29 Septemba. Uzinduzi huo ulienda  sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari ikiwemo kiharusi, madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo, lishe bora kwa afya ya moyo na tezi dume.
  upimaji 4
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakipata ushauri kabla ya kufanyiwa  vipimo vya magonjwa ya moyo wakati wa uzinduzi wa upimaji afya ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Septemba. Uzinduzi huo ulienda  sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari ikiwemo kiharusi, madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo, lishe bora kwa afya ya moyo na tezi dume.Picha na JKCI

  0 0

  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akipiga makofi na wajumbe wengine kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli pamoja na wajumbe wengine wakiwa wamesimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka na kuwaombea Majeruhi na waliopoteza maisha katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea Septemba 20,2018 katika ziwa Victoria kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halimashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akiongoza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018

  0 0


  0 0


   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018.
  a (2)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimkambidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018.
  a (3)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimkambidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018.
  a (4)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Jaji Mstaafu Harold Nsekela akimuongoza  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kula kiapo cha maadili ya viongozi baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018.
  a (5)
  a (6)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea baada ya kumuapisha  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018
  a (7)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea baada ya kumuapisha  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018
  a (8)
  a (9)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika  wa Bunge la Jamhuri Mhe. Job Ndugai na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja baada ya Dkt. Damas Daniel Ndumbaro  kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018.
  a (11)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akifurahia jambo na viongozi wa CCM Mkoa wa Ruvuma  baada ya kumuapisha  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018 

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kalinzi, Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati Waziri huyo alipofanya ziara wilayani humo kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wilayani humo. Waziri Lugola alitangaza operesheni kuanza kwa operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu mkoani Kigoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga. Kulia ni Mwanasheria wa Sekretaireti ya Mkoa wa huo, Said Kamugisha. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiyaangalia majina ya watuhumiwa waliopo mahabusu katika Kituo cha Polisi Manyovu, wilayani Buhigwe, Mkoa wa Kigoma, alipokua anaonyeshwa na Askari Polisi wa zamu kituoni hapo, Peter Charles. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiwahoji watuhumiwa (hawapo pichani) ndani ya mahabusu ya kituo cha Polisi Manyovu wilayani Buhigwe, Mkoa wa Kigoma, alipofanya ziara katika kituo hicho kujua utendaji kazi wa Polisi wa kituo hicho kilichopo mpakani na nchi ya Burundi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Luteni Kanali, Michael Ngayalina, na nyuma yake ni Mkuu wa Kituo hicho, Nickobay Mwakajinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Na Felix Mwagara, MOHA-Buhigwe

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameitaka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma ishirikiane na Jeshi la Polisi kufanya operesheni maalum ya kuwaondoa wahamiaji haramu mkoani humo.

  Akizungumza na mamia ya wananchi katika uwanja wa Mnanila mjini Manyovu wilayani Buhigwe, leo, Lugola alisema anataarifa za kutosha kuhusu wahamiaji haramu kutoka nchi za jirani wapo mkoani humo, hivyo lazima waondolewe kwa mujibu wa sheria.

  Lugola ambaye alikua akishangiliwa na wananchi baada ya kutoa agizo hilo, pia alikemea tabia ya baadhi ya watu wanaohifadhi raia hao wa kigeni ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.

  “Sasa natoa agizo hili na litekelezwe, Uhamiaji mkoa washirikiane na polisi kuwaondoa raia hawa wa kigeni ambao wameingia nchini kwa njia zisizo halali, nataka operesheni hii ianze mara moja,” alisema Lugola.

  Lugola pia aliirudia kauli hiyo ya kuondolewa kwa wahamiaji hao haramu alipokua anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Kalinzi, Wilaya ya Kigoma Vijijini, na kuongeza kuwa anashangaa wahamiaji hao wanaendelea kuwepo mitaani huku maafisa uhamiaji wakiwepo mkoani humo.

  “Hivi inakuaje, wananchi wanalalamika hapa kuhusu uwepo wa wahamiaji haramu, lakini Uhamiaji mpo, mnakaa kimya tu, mnataka mpaka mimi nije ndio nitoe maelekezo haya? Hii sitaki kusikia tena, nataka operesheni hii ianza mara moja na iwe endelevu,” alisema Lugola.

  Hata hivyo, Lugola alisema katika operesheni hiyo lazima maafisa wa uhamiaji wawe makini wakati wanawaondoa wahamiaji haramu pekee na sio kuwasumbua wananchi wa Kigoma ambao ni raia halali wa nchi hiyo.

  Lugola alifafanua kuwa operesheni hiyo itasaidia kupunguza matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambapo kwa kiasi kikubwa hutekelezwa na wahamiaji hao haramu.

  Aidha, Waziri Lugola akiwa wilayani Buhigwe, pia ametembelea kituo cha Polisi cha Manyovu kilichopo mpakani na nchi ya Burundi na kukagua utendaji kazi wa askari Polisi wa kituo hicho pamoja na kuiwahoji watuhumiwa waliopo mahabusu kujua makosa yaliyowafanya wawepo ndani ya kituo hicho.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), Selemani Jafo akifunga Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akitoa neno la Utangulizi wakati wa ufungaji wa Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.
  Baadhi ya wadau wa elimu walioshiriki katika Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.

  Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi walioshiriki kama Wadau wa Elimu katika Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.
  Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Lydia Wilberd akitoa salamu za asasi hiyo kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Wadau wa Elimu wametakiwa kuendelea kufanya tathmini ya elimu kwa kujadili mafanikio na changamoto za sekta hiyo ili kuboresha na kukuza elimu nchini.

  Hayo yamebainishwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Selemani Jafo alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Elimu.

  Waziri Jafo amesema kuwa nchi nyingi ambazo hazina rasilimali za madini wala vivutio vya utalii zinaendelea kuwekeza katika rasilimali elimu ambapo baadae nchi hizo huwa tajiri na kutoa misaada kwa nchi masikini.

  “Taifa linalowekeza vizuri katika sekta ya elimu ndilo Taifa lenye nafasi kubwa ya kukomboa wananchi wake na taifa kiujumla hivyo kutathmini juu ya elimu inayotolewa nchini kwetu ni jambo la muhimu sana”, alisema Jafo.

  Waziri Jafo amewasisitiza wadau wa elimu walioshiriki katika mafunzo hayo kutekeleza maazimio yote yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ili kuendelea kutoa matokeo chanya katika sekta hiyo.

  Vile vile ametoa rai kwa wadau wa elimu kuendelea kutoa michango yao ya hali na mali katika kuinyanyua sekta ya elimu nchini ili kwa pamoja taifa la Tanzania liweze kujinasua katika umasikini kupitia elimu.

  Aidha, amewataka wadau wa elimu kuwa huru katika kutoa mawazo yao bila kuogopa na kuwahakikishia kuwa milango ya ofisi hiyo iko wazi kukubali changamoto mbalimbali zinazopelekwa na inaendelea kuzitatua.

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu amesema kuwa kwa pamoja mkutano huo umejadili juu ya uboreshaji wa elimu nchini hasa juu ya suala la uwazi katika mipango na utekelezaji wa bajeti za elimu.

  “Ili kuboresha sekta ya elimu nchini uwazi ni jambo la msingi hivyo tunawaomba wenzetu wa mashirika na taasisi tunaosaidiana katika sekta hii wajitahidi kuweka bajeti zao wazi kama Serikali inavyofanya ili kuboresha zaidi sekta hii”, amesema Dkt. Ave Maria.

  Mkutano huo umeshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi, Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Taasisi zisizo za kiserikali.

older | 1 | .... | 1682 | 1683 | (Page 1684) | 1685 | 1686 | .... | 1898 | newer