Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 28, 2018

0
0





















Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018

0
0
 Kikosi cha timu ya Arusha United  wanautalii kama wanavyoonekana pichani. 
Msemaji wa timu ya Arusha United wana utalii Jamillah Omar

Na. VERO IGNATUS, ARUSHA

Ni septemba 29/2018 ni siku ua  kuanza rasmi ligi daraja la kwanza msimu wa kwanza  wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya Mkoa huo ya Arusha United Wanautalii siku ya tarehe 29 wakati timu hiyo itakapomenyana na Rhino Rangers Fc ya Tabora.

Msemaji wa timu ya Arusha United wana utalii Jamillah Omar akizungumza na waandishi wa habari  katika uwanja wa Shekh Amri Abeid  amesema anatarajia wana Arusha watajitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuishangilia timu hiyo ambayo kwa sasa inarudisha Mkoa huo  katika ramani ya soka nchini ambayo imepotea kwa muda mrefu.

Jamillah amesema kikosi cha timu ya Arusha United  wanautalii kimedhamiria  kuingia ligi kuu mwakani kutokana na kuwa na kikosi imara chini ya kocha mkuu Felix Minziro  ambae anahistoria safi katika soka nchini.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji  wa timu ya Arusha United wana utalii Fikiri Elias amesema timu yake imejiandaa vyema kukabiliana na timu ya Rhino Rangers Fc kutoka Tabora na wauhakika na ushindi wa point tatu.

Kwa mara ya kwanza tangu ipate usajili timu ya Arusha United wana utalii itajitupa uwanjani rasmi kuanza kushiriki ligi daraja la kwanza mwaka huu ikiwa katika safari yake ya kuelekea ligi kuu mwakani.

KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI WA Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amesema wamefanikiwa kukipindua kivuko cha MV.Nyerere na kukiweka sawa.

Kivuko hicho kilipinduka na kuzama katika ziwa Victoria  Septemba 20 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 226 huku watu 41 wakipatikana wakiwa hai.

Akizungumza jioni hii kuhusu kivuko hicho Waziri Kamwelwe amesema hatimaye leo wamefanikiwa kukiweka sawa na kazi ambayo imebakia ni kukovuta ili kiwe mwaloni kwa ajili ya kuendelea na hatua iliyobakia."Tunashukuru makundi yote kwa namna ambavyo wamefanikisha kukiweka sawa kivuko hiki ambacho kilipinduka na kusababisha maafa ya Watanzania wenzetu.

"Zaidi ya watu 570 wameshiriki katika kufanikisha kivuko hicho tunakipindua baada ya kupinduka.Tunawashukuru wananchi wa Ukara kwa namna ambavyo wameshiriki katika kuokoa maisha ya watu 40,"amesema Waziri Kamwelwe.

Ameongeza kuwa kivuko hicho ambacho kimewekwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa TanzaniaVenance Mabeyo ataelezea hatua ambayo inafuata baada ya kukamilisha hatua ya kwanza.Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi ya Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Venance Mabeyo amesema baada ya hatua ya kukisimamisha kivuko hicho kwa asilimia 85, kazi iliyobaki sasa ni kuondoa maji ambayo yamejaa ndani ya kivuko hicho.

" Kwa sasa tumefanikiwa kwa asilimia 85 kwani bado kuna hatua ambayo inafuata ya kuondoa maji,"amesema.Amefafanua baada ya kukipindua kivuko hicho na kisha kutoa maji watakivuta  Mwaloni kwa ajili ya kuanza kufanyiwa matengenezo.

Amesema pia watahakikisha wanasafisha eneo hilo ili kuangalia kama kuna chochote ambacho kimebakia na lengo ni kuacha eneo hilo likiwa salama."Tunataka wananchi Ukara wasiwe na hofu baada ya kukamilisha shughuli za kuondoa kivuko hicho kilipo na kukiweka Mwaloni," amesema Mabeyo.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella amesema msiba huo ulikuwa ni wa kitaifa licha ya kwamba limetokea mkoani Mwanza katika Wilaya ya Ukerewe katika eneo la Ukara.Amesema kuwa baada kikupindua kivuko hicho kwa sasa ni kuendelea kutoa maji yaliyomo.Amesema kuwa baada ya kutokea ajali hiyo Rais Dk.John Magufuli alikuwa akiwasiliana naye kwani alihakikisha anapata taarifa kwa kila kinachoendelea.

"Saa moja baada ya ajali hiyo kutokea Rais Magufuli alinipigia simu na kutoa maelekezo, pia nikapigiwa simu na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa." Tunashukuru kwa ushirikiano ambao umeoneshwa baada ya kutokea ajali hii kwani Watanzania wote wameonesha kuguswa na ajali hii mbaya.Tuendelee kishikamana na ukweli tukio hili limetufundisha jambo kubwa,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza.

Ametoa shukrani kwa makundi mbalimbali ambayo yameshiriki kikamilifu katika msiba huo ambapo pongezi hizo amezielekeza pia kwa vyombo vya habari kwa namna ambavyo wametoa taarifa sahihi kuhusu kinachoendelea.

RC HAPI ABAINI MADUDU MANISPAA YA IRINGA

0
0



Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akizungumza na wananchi wa mkoa huo jana tarehe 27 Septemba 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akihutubia mamia ya wananchi wa Kihesa waliojitokeza katika mkutano wa hadhara hapo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara katika Machinjio ya Ngelewala wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wake jana tarehe 27 Septemba 2018.


Udhaifu, upigaji kwenye miradi inayosimamiwa na manispaa vyabainika,
Migogoro ya ardhi Kihesa yateka mkutano.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amefichua madudu katika miradi ya machinjio mapya ya Ngelewala yaliyojengwa na fedha za serikali kwa milioni 900 takribani miaka 9 bila kukamilika huku manispaa wakihitaji shilingi bilioni 1.3 ili kukamilisha.

Tukio hilo limetokea jana wakati alipotembelea machinjio hayo ambapo kwenye taarifa iliyosomwa na afisa mifugo imetoa maombi kwa serikali kuwaongezea shilingi bilioni 1.3 kukamilisha machinjio hayo huku fedha za awali shilingi milioni 928 zimetumika machinjioni hapo bila kukamilika mpaka sasa.

Mkuu huyo wa mkoa akanusa harufu ya upigaji baada ya kuomba BOQ kutoka kwa mhandisi wa halmashauri manispaa ya Iringa Michael Sakala na kuikosa hivyo kuagiza uchunguzi kufanyika kwa mradi huo wa machinjio na endapo itabainika yeyote amehusika kwenye upugaji wa mradi huo basi achukuliwe hatua.

Aidha mkurugenzi Mpya wa manispaa Iringa ameeleza mbele ya RC kuwa naye alishtushwa na Fedha hizo zinazoombwa wakati kwa tathmini Mpya waliyofanya wamebaini kuwa ikipatikana shilingi milioni 300 hadi 400 tu machinjio hayo yataanza kufanya kazi na kuingiza mapato.

Katika hospitali ya Frelimo, mkuu wa mkoa amezindua jengo la kufulia nguo na kukausha pamoja na mashine mbili za kufulia kwenye hospitali ya Frelimo lililojengwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Iringa lenye thamani ya shilingi milioni 32 na kuwapongeza kwa hatua hiyo ya kuisaidia jamii yake hivyo kujenga mahusiano mazuri.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa hakuridhishwa Na taarifa ya ujenzi wa maabara na jengo la uchunguzi kwa shilingi milioni 560 unaotaka kufanywa katika hospitali hiyo. Mkuu wa Mkoa ametaka maelezo ya kina na nyaraka zote za ujenzi akidai pesa hizo ni nyingi sana.

”Tunajenga vituo vya afya vilivyo na majengo matano hadi sita ikiwemo wodi za kulaza kwa milioni 400 hadi 450 kwenye Mkoa wetu. Leo hii majengo mawili madogo inakuaje yagharimu milioni 560?Hapa kuna harufu ya upigaji.”
Alisema Mkuu wa Mkoa akikagua ramani za majengo hayo.

Mwisho,amehutubia mkutano wa hadhara kwa kusikiliza kero za wananchi huku kero kubwa zikiwa ni migogoro mingi ya ardhi, usimamizi mbovu wa miradi na kuwataka wahusika kutembelea kata hiyo kwa ajili ya kutatua migogoro.

”Manispaa hii imejaa ubabaishaji.Migogoro ya ardhi na dhuluma kwa wanyonge vimekithiri sana.Mradi wa machinjio umekwama miaka karibu minne,mnataka niwaombee bilioni 1.3. Mkurugenzi Mpya kaja kagundua akipata milioni 300 tu machinjio inaanza.

Nyinyi mliodai mnaongoza manispaa miaka yote mmeshindwa kwasababu mmetawaliwa na upigaji mtupu. Majengo mawili ya kawaida mmebariki milioni 560, kamati ya fedha inayoongozwa na Meya inafanya kazi gani??Nawahakikishia wananchi, nitatembea kila kona na nitasimamia kikamilifu fedha za serikali ambazo ni kodi zenu. Hakuna wa kunizuia wala kunikatisha tamaa…”Alisema RC Hapi huku akishangiliwa na wananchi wa Kisesa.

”Mkurugenzi wewe ni mpya hapa,saidiana na DC simamia vizuri miradi na watendaji wako ili kero hizi zishughulikiwe.”

ZIARA IRINGA MPYA

WABUNGE WAALIKWA NA BUNGE LA CHINA KUSHIRIKI SEMINA YAKUJENGEWA UWEZO

0
0
Kushoto katika picha ni Mheshimiwa Maida Abdallah, akifuatiwa na Mheshimiwa Munira Khatib, Mheshimiwa Kiza Mayeye, Mheshimiwa Joram Hongoli na mwisho kulia ni Mheshimiwa Fredy Mwakibete.
Mheshimiwa Kiza Mayeye akichangia mada katika semina hiyo. Semina hiyo iliwakilishwa na nchi saba za bara la Afrika na Asia.
Mheshimiwa Fredy Mwakibete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Msafara huo wa wabunge akitoa neon la shukrani baada ya kumalizika kwa semina hiyo. Semina ilikuwa inahusu kupeana mikakati mbalimbali ya kuweza kufanikisha malengo 17 ya millennia. Wabunge walipata kujifunza kutoka China ambao wamekuwa mara zote walitimiza malengo ya millennia kwa wakati.

MASHIRIKA YATAKIWA KUHUDUMIA JAMII KWA KURUDISHA FAIDA WANAYOPATA

0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Taasisi na mashirika mbali mbali hapa nchini yametakiwa kurudisha sehemu ya faida wanayo ipata ili kuhudumia Huduma za kijamii zikiwemo Mausala ya afya elimu na watoto wasiojiweza Sanjari na maafa mbali mbali

Akizungumza wakati akitoa msaada kwenye shule ya Msingi na ufundi Sing’isi wilayani Arumeru mkoani Arusha mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA bwana Julias Konyani amesema kwamba katika faida wanayo ipata watakikisha wanaendelea kusaidia sekta ya elimu nchini

Aidha ameyataka mashirika mbali mbali kuona namna ya kurudisha faida wanayopta katika kuhudumia masuala mbali mbali ya kijamii ikiwemo kusaidiana na serikali katika hatua mbali mbali za kuwaleta maendeleo wananchi hususani benki hiyo ilipokuwa ikikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 4 katika shule ya msingi na ufundi ya Sing’isi 

Amezitaka taasisi mbali mbali kujitokeza katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya ,kutoa elimu bure na kuwawezesha wanafunzi kupata elimu ya awali bila kuwepo na changamoto ya madarasa pamoja na uhaba wa vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya kusoma na kufundishia

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Singisi Safira Ndelwa ametaja changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hiyo kuwa ni uchakavu wa miundo mbinu ya majengo katika shule hiyo ikiwemo uhaba wa vyumba vya kusomea na uzio wa shule.

‘’Shule hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uzio uhaba wa vyumba vya madarasa mashine ya kuchapisha mitihani pamoja na nyumba za walimu ‘’alisema mwalimu Ndelwa

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Anjela Izack ameshukuru benki hiyo kwa msaada huo na kuomba kuongezewa madarasa mawili kwa lengo la kuondoa usumbufu wa wanafunzi wenzake kusoma kwa awamu mbili kwani wanachoka na masomo yao na kujikuta wakishindwa kushika masomo na maendeleo kushuka.
Sehemu ya Wanafunzi wa shule ya msingi na ufundi Sing'isi wakiwa na mfano wa hundi waliokabidhiwa na benki ya CBA jana wilayani Arumeru 
Pichani ni Mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA bwana Julias Konyani akiwa na mwalim mkuu wa shule ya ufundi na msingi Sing'isi Safira Ndelwa wakati wa makabidhiano ya Hundi kutoka Benki ya CBA picha zote na mahamoud ahamd Meru

DKT NDUGULILE ATOA MWEZI MMOJA KWA UONGOZI TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUTATUA CHANGAMOTO ZAKE

0
0
Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amefanya ziara katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikiwa ni miongoni mwa ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake katika kuboresha utendaji kazi. 

Dkt Ndugulile jana Septemba 27,2018, pamoja na kufanya ziara  katika taasisi hiyo na kujionea mazingira halisi,pia alifanya mkutano na menejimenti, wafanyakazi pamoja na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii,ambapo pamoja na mambo mengine Mh Naibu Waziri alisomewa taarifa ya maendeleo ya taasisi na mipango ya baadae. 

“Nimeskia taarifa nzuri ya maendeleo na mafanikio pamoja na changamoto za Taasisi, nawaagiza viongozi kutatua changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wenu na sisi kama serikali tutazifanyia kazi zile zinazotuhusu. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa huduma zinaendelea kutolewa kwa ubora na maslahi ya watumishi yanaboreshwa”. Alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Ndugulile ametoa maagizo kwa menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii kufanyia kazi kwa muda mwezi mmoja tu,baadhi ya mambo ambayo ameona yanahitaji ufumbuzi wa mapema ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii. 

Katika kuhitimisha mkutano wake na uongozi, wafanyakazi pamoja na serikali ya wanafunzi wa Taasisi, Mh. Naibu Waziri Dkt. Ndugulile amepongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi na ameahidi wao kama Wizara kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Ustawi wa jamii katika kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wananchi.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akisikiliza ripoti ya utendaji kazi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Taasisi Dkt. Zena Mabeyo.
 Wajumbe wa menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii wakimsikiliza Mh. Naibu waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana nao Jana.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akizungumza na Watumishi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile  akipokelewa na Kaimu Mkuu wa Taasisi Ya Ustawi wa Jamii  Dkt Zena Mabeyo alipofika kutembelea Taasisi hiyo jana,jijini Dar Es Salaam.

MICHUZI TV LIVE: SHEREHE ZA KUMUAGA KAMISHNA JENERALI MSTAAFU WA MAGEREZA TANZANIA

0
0

VIGOGO SITA WA KAMPUNI YA CHAI YA MPONDE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI

0
0

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Tanga jana imewafikisha mahakamani vigogo sita wa Kampuni ya Chai ya Mponde Tea Estate Limited kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya dola za kimarekani 15,050,254.00 sawa na shilingi za kitanzania Bilioni 30.

Kosa hilo linadaiwa lilitendeka kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2000 na 2013 ambapo watuhumiwa hao baada ya kukosa dhamana wamepelekwa kwenye Gerezani wakisubiri kesi yao itakapotajwa tena.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Takururu mkoani Tanga Christopher Mariba alisema kosa hilo ni kunyume na aya ya kumi ya Jedwali la kwanza la kifungu cha 57(1) na kifungu cha 60(2) cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 pitio la mwaka 2002,iliyofanyiwa marekebisho kwa sheria namba 3 ya mwaka 2016.

Aliwataja waliofikishwa mahakamani kuwa ni Nawab Abdulrahim Mulla, Shahdad Nawab Mulla,William Shelukindo,Richard Abraham Mbughuni, Richard Madadi Semroki na Rajabu Ali Msagati ambao ni wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Mponde Tea Estate Company na kusomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa mkoa wa Tanga Desdery Kamugisha.

Alisema baada ya kusomewa mashitaka hayo washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo huku pia mahakama hiyo ikizuia kusikiliza maombi ya dhamana ya washtakiwa kwa sababu zilezile kwamba haina mamlaka ya kisheria yakusikiliza shauri hilo.

Akitolea ufafanuzi wa mashtaka hayo Mkuu huyo wa Takukuru mkoani Tanga alisema vigogo hao ni wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya MPONDE TEA ESTATE LIMITED ambayo awali ilikuwa inajulikana kama MPONDE TEA FACTORY kampuni ambayo kabla ya ubinafsishaji ilikuwa ni mali ya serikali.

“Uchunguzi wa Takukuru umebaini kwamba vigogo hawa kwa nyakati tofauti walifanya udanganyifu kwa kuagiza mizigo na malighafi mbalimbali kwa niaba ya wakulima wadogo wadogo wa chai waliopo wilayani Lushoto mkoani Tanga wakati si kweli… Vigogo hao wamekuwa wakifanya vitendo hivi na kisha kufanikiwa kuingiza vifaa vya thamani ya zaidi ya sh.bilioni 135.

Alisema kwa udanganyifu huo,vigogo hao waliomba na kupata msamaha wa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wa zaidi ya sh. Bilioni 35 wakati wakijua kwamba mizigo na malighafi hizo hazikuwa ni kwa ajili ya walengwa ambao ni wakulima wadogo wadogo wa chai.

Alieleza kwamba kwa mantiki hiyo vigogo hao wameisababishia serikali hasara ya sh.Bilioni 30 ambazo zingelipwa na kuingia katika mfuko wa serikali.

“Lakini kwa hesabu za haraka haraka sh.bilioni 30 zingeweza kujenga kilometa 30 za barabara ya lami,Zahanati 60,Madarasa 1500,Visima vya maji 1000 au viwanda vidogo vidogo 60 kwa wakazi wa mkoa wa Tanga “Alisema.

Hata hivyo alisema Takukuru mkoani Tanga inatoa wito kwa watanzania wote hususani wakazi wa Jiji la Tanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo katika kufichua walarushwa wenye lengo la kuzorotesha maendeleo ya watanzania.

NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA

0
0





BENKI ya NMB Plc imesema itashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma.

Mpango huo ulielezwa jana na Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa mazungumzo mafupi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) unaoendelea jijini Dodoma.

Mponzi alisema kwa sasa NMB inawasaidia zaidi ya wakulima wadogo wadogo milioni moja nchi nzima, na kwamba benki itaendelea kutenga fedha za kutosha ili kusaidia wakulima wengi zaidi.

“Kwa sasa, NMB imetenga zaidi ya shilingi billioni 500 kwa ajili ya kusaidia wakulima hapa nchini lengo likiwa kusaidia jitihada za serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu alisema kwa sasa Serikali inapeleka nguvu zake katika kukuza kilimo cha zao la mchikichi mkoani Kigoma, na hivyo akaitaka benki ya NMB kuisaidia Serikali katika kufanikisha azma hiyo kwa kuwasaidia wakulima wa michikichi mkoani humo.

“Tumekuwa tukiwashawishi wakulima mkoani Kigoma kujikita katika kilimo cha michikichi lakini kwa bahati mbaya wakulima wengi hawana mitaji ya kulima michikichi kwa wingi. Nitafurahi kama benki yenu kupitia mikakati yake itawawezesha wakulima wa michikichi,” alisema.

Aidha, Waziri Mkuu ameomba kukutana na uongozi wa benki ya NMB mapema wiki ijayo mkoani Kigoma ili kwa pamoja waweze kupanga mkakati kazi wa kuwasaidia wakulima mkoani humo kulima michikichi kwa ufanisi na wingi zaidi.

“Kwa sasa tunapambana ili kuhakikisha mazao yote ya biashara yanayostawi hapa nchini yanalimwa kwa kiwango kikubwa ili kuchochea kasi ya uchumi wa viwanda kupitia rasilimali za ndani. Ningependa tukutane Kigoma ilituone namna ya kuwezesha zao la michikichi kulimwa kwa wingi,” Majaliwa alieleza.

Akielezea mikakati mingine ya benki, Mponzi alisema NMB itaendelea kutanua wigo wa huduma zake ili kuhakikisha watanzania wengi zaidi wananufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.

“Hivi karibuni tumezindua mfumo ambao unamwezesha mteja au mwananchi yeyote kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi, ambapo namba yake ya simu ndiyo inakuwa namba yake ya akaunti. Ni matarajio yetu kwamba kwa kupitia mfumo huu shirikishi watanzania wengi zaidi, hususani wakulima wa vijijini,” aliongeza.

Pamoja na hayo, alieleza kuwa NMB itaendelea kushirikiana na mamlaka za Serikali za mitaa hapa nchini katika kuleta maendeleo chanya.

NMB imekuwa mdhamini mkuu wa mikutano ya mwaka ya ALAT, na kwa mwaka huu, benki imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuwezesha mkutano huo muhimu uliyowakutanisha zaidi ya wajumbe 500 kutoka mikoa mbalimbali.


Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi (kulia) akitoa maelezo ya huduma za kifedha zinazotolewa na benki hiyo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) alipotembelea Banda la Benki hiyo jana Jijini Dodoma kwenye monyesho ya Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT). Benki ya NMB imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kufadhili mkutano huo, ikiwa ni kwa mwaka wa sita mfululizo sasa. Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi pamoja na Meneja Mwandamizi wa Biashara za Kilimo wa NMB -Isaac Masusu.
Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) wakati wa mkutano mkuu wa 34 wa jumuiya hiyo unaoendelea jijini Dodoma.

TANZANIA YAPEWA TUZO YA KIMATAIFA YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA (NCD) DUNIANI.

0
0
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akipokea tuzo ya Kimataifa ya kupambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Duniani toka kwa Makamu Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dkt.Soumya Swaminatha Mjini New York,Marekani

SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata Tuzo ya Kimataifa ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs) kama vile Kisukari, Shinikizo la Damu, Magonjwa ya Moyo na Saratani.

Tuzo hiyo ya Kimataifa, imekabidhiwa leo tarehe 27 Septemba, 2018 kwa Waziri ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu na Kikosi kazi maalumu cha Umoja wa Mataifa mahususi kwa kupambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (UN Interagency Task Force on the Prevention & Control of NCDs- UNIATF). Hii ni kutokana na juhudi za Wizara ya Afya za kupambana dhidi ya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD), hususan kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.

Tuzo hiyo ya kimataifa ya mwaka 2018, imekabidhiwa kwenye mkutano wa wa viongozi wa juu wa Umoja wa Mataifa (United Nations High Level Meeting on NCDs) unaofanyika Mjini New York, Marekani.

Tanzania ni miongoni mwa nchi tisa Duniani ambazo zimefanikiwa kupata tuzo hiyo ambayo imetolewa kwa mara ya kwanza katika ngazi ya Kiserikali Dunianii, na ilichaguliwa kupata tuzo hiyo baada ya mapendekezo yaliyoandikwa na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza vya Tanzania (TANCDA). Hii ni kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata habari ya namna ya kujikinga na magonjwa haya.

Timu ya UNIATF imeipongeza Tanzania kwa kuanzisha programu ya kuhamashisha jamii kufanya mazoezi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku.

“Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD) ndiyo yanayoongoza duniani kwa sasa kwa kusababisha ulemavu na vifo vingi. Nchini Tanzania asilimia 34 ya Vifo vilivyorekodiwa Hospitali mwaka 2017 zimesababishwa na magonjwa haya. Isitoshe kupambana na NCD ni miongoni mwa mikakakati ya Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu (SDG) ya kupunguza kwa theluthi moja vifo vya mapema vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ifikapo mwaka 2030. Amesema Waziri Ummy.

Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza ni magonjwa sugu au ya muda mrefu, ambayo hayawezi kuambukizwa kwa maana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Magonjwa haya yapo mengi nayo ni kama vile kisukari, saratani, shinikizo la damu na mishipa ya fahamu, magonjwa sugu ya mfumo wa hewa, magonjwa sugu ya figo, macho na meno, selimundu (siko seli) na mengineyo.

Waziri Ummy amelishukuru Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza la Tanzania (TANCDA) baada ya kuandika andiko la kuitambulisha Dunia kuhusu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, na dunia kuona umuhimu wa juhudi hizo.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na TANCDA na wadau wengine inaamini mikakati madhubuti, Sera mbalimbali za afya zikiwekwa, kutekelezwa na kuhakikisha Watanzania wanakuwa na elimu sahihi ya kujikinga na kuyadhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza, itaboresha afya ya wananchi.

Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Afya)

TTCL YATOA POLE YA MILIONI 25 MAAFA YA KIVUKO CHA MV NYERERE

0
0

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) limetoa mchango wa pole ya shilingi Milioni 25 kusaidia katika maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea wiki iliyopita Kisiwani Ukerewe, Mkoa wa Mwanza. Pichani kulia ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Bw. Jalili Bakari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Tanzania, Ndugu Waziri Kindamba akikabidhi nakala ya hundi ya malipo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akishuhudia.
Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Bw. Jalili Bakari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Tanzania, Ndugu Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya kukabidhi nakala ya hundi ya malipo ya mchango wa pole ya shilingi Milioni 25 iliyotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) ikiwa ni pole yao kwa maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea hivi karibuni kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akishuhudia.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela katikati akishukuru mara baada ya kupokea pole hiyo ya shilingi Milioni 25 kusaidia katika maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere.

SEHEMU YA VIVUTIO KATIKA ZIWA VICTORIA

0
0

Mwalo wa kijiji cha Igombe wilayani Ilemela mkoani Mwanza ukiwa umepambwa na mitumbwi ya wavuvi wa samaki katika ziwa Victoria hivi karibuni. Eneo hilo ni marufu kwa uvuvi na uuzaji samaki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kisiwa cha Makobe kilichopo kwenye ziwa Victoria kati ya wilaya ya Ilemela na Ukerewe mkoani Mwanza ni moja kati visiwa vingi vilivyopo katika ziawa hilo vyenye makazi ya wavuvi. Picha hii imepigwa hivi karibuni.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TIGO FIESTA 2018 – VIBE KAMA LOTE KURINDIMA MOROGORO

0
0


 Msanii wa  bongo flava Boniventure Kabogo – Stamina (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote mjini Morogoro leo. Tigo imetangaza punguzo la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR pamoja na kuzindua shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo. Pamoja naye ni (kuanzia kushoto), Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM Gardner Habash, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Morogoro, Stephen Kunambi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo – William Mpinga, Afisa Michezo wa Manispaa ya Morogoro – Asteria Mwang’ombe , msanii wa bongo flava Abednego Daniel – Belle 9, na mtangazi wa Clouds FM Kenneth Frank – Kennedy the Remedy.
 IMG_1534
Msanii wa  bongo flava Boniventure Kabogo – Stamina (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote mjini Morogoro leo. Tigo imetangaza punguzo la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR pamoja na kuzindua shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo. Pamoja naye ni (kuanzia kushoto), Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM Gardner Habash, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Morogoro, Stephen Kunambi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo – William Mpinga, Afisa Michezo wa Manispaa ya Morogoro – Asteria Mwang’ombe , msanii wa bongo flava Abednego Daniel – Belle 9, na mtangazi wa Clouds FM Kenneth Frank – Kennedy the Remedy.
IMG_1548
 Wasanii wa Bongo Flava (kuanzia kushoto) Z Anto, Mr Blue Kabayser na Ben Pol wakisalimiana wakati wa hafla ya uzinduzi wa  uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote mjini Morogoro leo. Tigo imetangaza punguzo la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR pamoja na kuzindua shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo. Tamasha la kwanza la msimu huu wa Tigo Fiesta 2018l inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro siku ya Jumamosi. 

TIGO FIESTA 2018 – VIBE KAMA LOTE KURINDIMA MOROGORO
Punguzo kabambe la bei ya tiketi kwa watakaonunua kupitia Tigo Pesa Masterpass QR 

Morogoro, Septemba 28, 2018 – Huku nchi nzima ikisubiri kwa hamu kuanza kwa msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote, mdhamini mkuu Tigo Tanzania pamoja na waandaaji Clouds Media Group wameanza maandalizi rasmi ya tamasha hilo litakalorindima Jumamosi hii tarehe 29 Septemba katika viwanja vya Jamhuri, mjini Morogoro..

Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 – Viba Kama Lote, Gardner G. Habash aliwahakikishia wote watakaohudhuria tamasha hilo usalama na mapokezi mazuri. ‘Tunawakaribisha nyote kwenye shamrashamra za mwanzo wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote,’ Gardner alisema. 

‘Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Morogoro, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim,’ Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema. Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika Kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

‘Katika miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Bali na kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika, pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama nitilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,’ Gardner aliongeza.

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu litashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.

GAIRO YAENDESHA KAMPENI YA UKAGUZI WA VYOO YENYE KAULIMBIU YA “USICHUKULIE POWA NYUMBA NI CHOO”

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe na Mkurugenzi Mtendaji Bi . Agnes Mkadya wanaendelea kukagua nyumba hasa za Serikali yaani nyumba za waalimu, Ofisi za Kata na Vijiji, Shule za Msingi na Sekondary, minadani na magulioni bila kusahau nyumba binafsi hasa kuanzia za biashara, ili kujiridhisha na utekelezaji wa agizo la kujenga vyoo bora.

Mara baada ya kampeni ya ” Usichukulie powa nyumba ni choo” iliyosimamiwa na Clouds Media chini ya mwanadada makini kwa jina la Farida.
Mhe. Mchembe alitoa miezi mitatu kwa nyumba zenye uhusiano na Serikali kuanza kuwa na vyoo bora kabla ya kwenda kwa wananchi. Hata hivyo haikuwa na maana wananchi waachwe la hasha. Wao awamu yao inaendelea kwa elimu zaidi na kuanzia Novemba faini zitaanza kuchukuliwa.

Wale wasio na uwezo kabisa Halmashauri itaangalia namna ya kuwasaidia. Aidha tunatafuta ufadhili wa kujenga choo cha watu wote kwenye maeneo ya vijiji ambavyo nyumba zipo karibu na umasikini ni mkubwa huwezi kuwalipisha faini.
Mhe. Mchembe alisema haiwezekani kuna maeneo unakuta mtu ana ng’ombe wengi na mifugo mingine na mali kadhaa lakini hana choo kabisa au hana choo bora. Maji ya Gairo ni ya mseleleko hivyo tunakunya maji yanayoporomoka na vinyesi.

Picha inayoonekana hapo juu ni choo kilichojengwa kwenye nyumba ya Mwalimu Mkuu Njungwa Shule ya Msingi. Choo cha awali kinaonekana na choo cha kisasa pia. Kampeni hii ni muhimu na inafatiliwa Wilaya nzima Kata 18, Vijiji 50 na Vitongoji 302 muda ni 24/7. Mpaka sasa wenye vyoo bora ni asilimia 33 na ambao hawana vyoo kabisa ni asilimia 11.

Afya yako ni jukumu lako na langu ni letu sote.

PRINCE WILLIAM ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, kushoto, akimkaribisha Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William bandarini mara baada ya kufanya ziara ya kujionea utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam jana. Price William yupo nchini kwa ziara maalumu ya siku tatu. Pembeni ya Mhandisi Kakoko ni Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, katikati, akitazama sanamu ya Twiga aliyomzawadia Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William, kushoto, mara baada ya kufanya ziara ya kujionea utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Price William yupo nchini kwa ziara maalumu ya siku tatu.
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, katikati, akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Twiga Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William, kulia, mara baada ya kufanya ziara ya kujionea utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Price William yupo nchini kwa ziara maalumu ya siku tatu. Kushoto ni Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi. 
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, katikati, akitambulisha watendaji wake kwa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William, kushoto, mara baada ya kufanya ziara ya kujionea utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Price William yupo nchini kwa ziara maalumu ya siku tatu. Nyuma ya Mhandisi Kakoko ni Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

KAMISHNA JENERALI MSTAAFU WA MAGEREZA, DKT. JUMA MALEWA AAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0


 Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Alli Malewa akiwasili katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam leo Septemba 28, 2018 kwenye Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wake Jeshi tangu julai 1, 2018.
PIX 2 (5)
. Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake katika Sherehe za kumuaga zilizoandaliwa kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam leo Septemba 28, 2018.
PIX 3 (5)
Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kumuaga.
PIX 4 (2)
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, CGP – Phaustine Kasike akiwa na baadhi ya  Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wageni mbalimbali waliofika katika Sherehe hizo. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na katikati ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala.
PIX 5 (1)
Gadi ya wanaume iliyoundwa na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya jukwaa kwa mwendo wa pole kama inavyoonekana katika picha.
PIX 6
Gadi ya wanawake iliyoundwa na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya jukwaa kwa mwendo wa haraka kama inavyoonekana katika picha.
PIX 7
Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Alli Malewa akiwa kwenye gari maalum akipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wake Jeshini tangu Julai 1, 2018. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam leo Septemba 28, 2018.
PIX 8
Askari wa vyeo mbalimbali wakipunga mikono ikiwa ni ishara ya kumuaga na kumtakia kheri Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Alli Malewa(hayupo pichani) katika hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Septemba 28, 2018.
PIX 9
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike (kulia) akimpongeza Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Malewa mara baada ya gwaride rasmi la kumuaga lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.
PIX 10
Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wakuu wa Magereza Mikoa nchini (wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KIKOSI KAZI CHA KUTATUA CHANGAMOTO ZA VIUMBE WAGENI/VWAMIZI NCHINI

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ni vema kama nchi tukajipanga mapema kuhakikisha kwamba viumbe vamizi hawaendelei kushamiri ili kuepusha Taifa kuingia kwenye gharama kubwa za kukabiliana na janga hilo hapo baadaye.

Makamu wa Rais ameyasema haya wakati wa uzinduzi wa Kikosi Kazi cha Kutatua Changamoto za Viumbe Wageni/ Vamizi nchini uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Pamoja na kwamba viumbe hawa ni janga la kiuchumi, kimazingira na kiafya  lakini bado halijashughulikiwa kikamilifu hususani katika elimu ya kuzuia viumbe hawa na kuwa na mipango madhubuti ya kukabiliana nalo” alisema Makamu wa Rais.Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Janga hili si la sekta moja. Kama tulifanya makosa huko nyuma kushughulikia jambo hili kila sekta kivyake tangu sasa TUACHE.  

Amezitaka Sekta zote na Taasisi zifanye kazi kwa pamoja kwa kupeana taarifa na mikakati ya kukabiliana na changamoto hii. Na kutaka ushirikishwaji wa wadau wote wakiwemo, Halmashauri za wilaya ,Wizara za kisekta, Serikali za Mitaa, Asasi za Serikali na zisizo za Serikali, Sekta binafsi pamoja na wananchi pamoja na vyombo vya habari.

Akitoa rai kwa waliochaguliwa kuunda Kikosi Kazi cha Kitaifa, Makamu wa Rais alisema “Tambueni kuwa mmepewa jukumu kubwa la kulisimamia suala hili kikamilifu. Kafanyeni kazi kulingana na Hadidu za Rejea tutakazo wakabidhi ili mwisho wa yote kuwe na matokeo chanya ya kazi mliyopewa na Taifa”.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano wa Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuwa aligundua tatizo hili mara baada ya kufanya ziara yake ambapo amekuta athari za mimea na viumbe vamizi zimekuwa kubwa na tishio kwa wananchi hivyo kuona kuna kila sababu ya kuanza kulishughulikia.Kikosi kazi hicho chenye wajumbe 18 kilichozinduliwa leo kitaongozwa nchi ya Mwenyekiti Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Awesu, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega pamoja na wadau mbali mbali wa mazingira.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kikosi kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa  Uzinduzi wa Kikosi cha kutatua changamoto za Viumbe Wageni/ Vamizi nchini uliofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi john Malongo akiwatambulisha Wajumbe 18 wa Kikosi Kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi hicho kilichozinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kikosi kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini mara baada ya uzinduzi wa Kikosi kazi hicho uliofanyika kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wengine Pichani ni Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Awesu, Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah  Ulega (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MTENDAJI MKUU TIC,BALOZI WA DENMARK NCHINI TANZANIA WAFANYA MAZUNGUMZO KUHUSU UWEKEZAJI

0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO

MTENDAJI Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geophrey Mwambe amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen.

Miongoni mwa mambo ambayo wamezungumza ni pamoja na wawekezaji wa nchini Denmark kuja kuwekeza kwa kudai Tanzania kuna mazingira mazuri ya uwekezaji. Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa TIC amesema Balozi Jensen amekuwa mdau mkubwa katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na pande hizo mbili kufanyabiashara.

“Balozi Jensen ni rafiki mkubwa wa biashara na amekuwa akishiriki kikamilifu katika kuandaa mazingira mazuri ya kiabiashara.Tumekuwa tukishirikiana na Balozi Jensen kuratibu za kuwezesha wafanyabiashara,” amesema Mwambe.

Pia amesema Balozi Jensen katika kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo kwa kuhakikisha wakulima wanakuwa na soko la uhakika huku akieleza kwamba Balozi amekuwa akihamasisha wawekezaji wa Denmark kuwekeza nchini Tanzania. Mwambe amesema siku za karibuni amefanya mazungumzo na Balozi huyo na moja ya mambo waliyoyazungumza ni namna ya kusaidia katika mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea kufanywa na TIC.

“Balozi amekubali kuisaidia TIC katika mabadiliko ya kimfumo kiutendaji kama nchi, tumedhamiria kushindana kidunia, tunakuza uwezo wa kuongeza ajira kwa Watanzania,” amesema .Pia wamekubaliana na Balozi Jensen katika kuandaa maeneo ya yaliyopimwa kwa ajili ya uwekezaji.”Nchini kwetu hatuna tatizo la ardhi kwani ipo ya kutosha ila changamoto ipo kupata eneo ambalo limepimwa.

“Hivyo moja ya mipango yetu ni kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanapimwa na mwekezaji anapohitaji eneo inakuwa rahisi kupata.Bolozi amekubali kusaidia katika upimaji wa maeneo,” amefafanua. Mwambe amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Denmark kuna kampuni kubwa za nchi hiyo ambazo zimejenga viwanda.

Pia amesema kupitia Balozi huyo Denmark kwa sasa kuna mchakato wa mradi wa umeme wa upepo unaoendelea mkoani Dodoma. Kwa upande wake Balozi Jensen amesema nchi hizo mbili zimekuwa kwenye ushirikiano mkubwa kwa miaka 50 na kwamba nchi ya Denmark imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji.

SPIKA NDUGAI AFUNGA RASMI MKUTANO MKUU WA ALAT JIJINI DODOMA

0
0


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) pamoja na wadhamini wa Mkutano huo (hawapo kwenye picha) wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 34 wenye kauli mbiu inayosema “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
V25A8994
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) pamoja na wadhamini wa Mkutano huo (hawapo kwenye picha) wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 34 wenye kauli mbiu inayosema “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
V25A8972
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) pamoja na wadhamini wa Mkutano huo, wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 34 wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
1. Spika
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb), akifunga Mkutano wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT), katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma (Picha na Atley Kuni- OR TAMISEMI)
V25A8949
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa Tanzania pamoja na wadhamini wa Mkutano huo (hawapo kwenye picha) wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 34 wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
2. Jafo
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo, akito salam za Wizara mda mfupi kabla yakufungwa kwa mkutano wa 34 wa ALAT na Spika wa Bunge Job Ndugai jijini Dodoma (Picha na OR TAMISEMI).
7. TFDA
Mwakilishi wa TFDA, akipokea cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi Job Ndugai kufuatia ushiriki wa mamlaka hiyo kuwezesha kutano wa 34 ALAT jijini Dodoma.
V25A9048
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimpatia cheti mwakilishi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa, Ndg. Tuntufye Mwambusi  mmoja wa wadhamani waliofanikisha Mkutano Mkuu wa 34 wa Tawala za Mitaa Tanzania, wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” kabla ya kufunga Mkutano huo katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
V25A8925
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Tawala za Mitaa Tanzania, wadhamini wakiwa kwenye Mkutano wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma. 
V25A8964
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Tawala za Mitaa Tanzania, wadhamini wakiwa kwenye Mkutano wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live




Latest Images