Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1680 | 1681 | (Page 1682) | 1683 | 1684 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Muwakilishi wa wadau wa BancABC  Mr. Michael Wilkerson, akizungumza na wateja pamoja na wadau wa BancABC wakati wa mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena Dar es Salaam. Mkutano huo ulikuwa mahususi kwa ajili ya kusisitiza juu ya ahadi ya BancABC kuendelea kutoa na kutengeneza bidhaa bora kwa ajili ya wateja wake.
  IMG_2226
  Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mara Group Mr. John Staley akiongea na wateja, wadau na wafanyakazi wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam hivi karibuni, kwa lengo la kusisitiza ahadi ya kuendelea kutoa bidhaa za kipekee haswa kwa “retail banking” ambayo anajivunia uzoefu wake. Stejini ni muwakilishi wa wanahisa Mr. Michael Wilkerson, Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa BancABC Mr. Imani John.
  IMG_2457
  Wateja wa BancABC walipowasili kwa ajili ya hafla. Hafla hii iliwaleta pamoja wadau, wateja, uongozi pamoja na wafanyakazi wa benki.
  IMG_2129
  Katika picha ya pamoja, toka kulia Mkurugenzi mtendaji wa Atlas Mara Group Mr John Staley, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Mr. Imani John pamoja na muwakilishi wa wanahisa wa BancABC Mr. Michael Wilkerson
  IMG_2120
  Wafanyakazi wa BancABC katika picha ya pamoja baada ya hafla yenye mafanikio iliyoandaliwa na BancABC

  0 0

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

  Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepongeza maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge inayoendelea kujengwa kwa awamu ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.

  Mwaka 2015, CCM iliweka ahadi kwa Wananchi wake kuimarisha, kuboresha na kuiunda upya Miundombinu ya Usafirishaji nchini ikijumuisha Usafiri wa Ardhini na Ndege.

  Akizungumza wakati wakutembelea maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo eneo la Soga mkoani Pwani, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kukamilika kwa kipande hicho (Dar hadi Morogoro) itasukuma malengo ya dira ya maendeleo ya Taifa mwaka 2020/2025 kufikia Uchumi wa Kati.

  Polepole amesema Reli ni kiungo muhimu kuchochea Taifa la Tanzania kufika katika Uchumi wa Kati wenye sifa ya wingi wa Viwanda vitakavyoongeza ajira kwa vijana.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Ramadhan Maneno amesema Chama hicho kimefika katika eneo hilo la Pwani kuthibitisha ujenzi wa Reli hiyo iliyoahidiwa mwaka 2015, amesema Mkoa wa Pwani umetoa ushirikiano kwa Kampuni ya Yapi Merkezi kutoka Uturuki ambayo imechukua tenda ya ujenzi wa Reli hiyo.

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema wamepata faraja kwa ujumbe wa CCM kufika katika eneo la Pwani kutembelea ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa. "Tuna Wataalamu 57 Wanajeshi maeneo mbalimbali ya Ujenzi wa Reli hii, tunafarijika sana", amsema Kadogosa.

  Pia Kadogosa ametoa wito, Wataalamu wanaoendelea na ujenzi wa Reli hiyo kutoka hapa nchini watapata mafunzo ya vitendo kusomea nje ya nchi, amesema mapaka sasa Reli hiyo imetandikwa zaidi ya Urefu wa Kilometa 5 akisisitiza kuwa Reli zilizofika ni Kilometa 60.

  Akizungumza kwa niaba ya Bodi ya Shirika la Reli nchini, Prof. John Kondoro amesema kuna watu wanafaidika na uwepo wa Kampuni zinazotengeneza Reli ya Kisasa, pamoja na maendeleo ya ujenzi wake.

  Prof Kondoro amesema hadi kufika mwisho wa mwaka lengo ni kuondoa miinuko na mabonde ili kufanikisha utandikaji wa Reli hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kadogosa (kushoto) akimuelezea Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole (kulia) maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa wakati wa ziara kuona maendeleo ya ujenzi wa SGR nje kidogo ya kambi ya Soga Kibaha mkoani Pwani Septemba 26, 2018.
  Meneja Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Mhandisi Maizo Mgedzi akiwaelezea, Katibu wa Itikadi na Uendezi wa CCM Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Prof. John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu wa TRC ndugu Masanja Kadogosa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la treni ya Umeme linalojengwa kuanzia Stesheni ya ¬Dar es Salaam hadi Ilala Septemba 26, 2018.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa ziara kuona maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR nje kidogo ya kambi ya Soga Kibaha Septemba 26, 2018.
  Mhandisi kutoka kampuni ya Yapi Merkezi akiwaelezea Katibu wa Itikadi na Uendezi wa CCM Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Prof. John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu wa TRC ndugu Masanja Kadogosa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba kuhusu hatua za ujenzi wa daraja la treni ya umeme linalojengwa kuanzia Dar es Salaam Stesheni hadi Ilala Septemba 26, 2018.


  0 0

  Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani kufanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23.
  Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani kufanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23.
   Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani kufanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23.
  Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani kufanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kibondo, Mkoani Kigoma (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo jana kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi pamoja na Taasisi zilizopo ndani Wizara yake. Lugola ametoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi mkoani humo, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri katika Wilaya hiyo pamoja na sehemu zingine mkoani humo. Kulia ni Mwanasheria wa Sekretaireti ya Mkoa wa Kigoma, Said Kamugisha ambaye pia ni Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Louis Bura. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Louis Bura, wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa Community Centre mjini Kibondo, kwa ajili ya kuzungumza na watumishi waliopo chini ya Wizara yake. Lugola katika mkutano huo alitoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi mkoani humo, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri katika Wilaya hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Meja Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza katika Kikao cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya mkoa wake, baada ya Waziri Lugola kufanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kibondo mkoani humo, jana. Lugola katika mkutano wa hadhara na wanannchi mjini humo, alitoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi mkoani humo, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri mkoani humo. Kulia ni Mwanasheria wa Sekretaireti ya Mkoa huo, Said Kamugisha. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Louis Bura. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kibondo, katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wilaya hiyo. Waziri Lugola akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kibondo, alitoa wiki mbili kwa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  Na Felix Mwagara, MOHA-Kibondo

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi Mkoa wa Kigoma, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri katika Wilaya ya Kibondo pamoja na sehemu zingine mkoani humo.

  Lugola aliongeza kua, katika kupambana na majambazi hao ambao wanasumbua wananchi wilaya hiyo ya Kibondo na kukosa amani katika maeneo yao, polisi ifanye operesheni maalumu kuwatia mbaroni watuhumiwa hao. Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Community Centre mjini Kibondo, leo, Lugola alisema katika operesheni hiyo pia itambatana na utoaji onyo kwa watu wasio waaminifu wanaowahifadhi raia wa kigeni ambao wengi wao ni wahalifu. 

  ‘’Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, natoa wiki mbili tu, kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya fanyeni operesheni ya kuwasaka majambazi hawa usiku na mchana mpaka jambazi wa mwisho awe amekamatwa,’’ alisema Lugola.

  Lugola alisema haiwezekani tukasalimu amri kwa majambazi, haiwezekani kunyoosha mikono kwa jambazi waliopo katika maeneo mbalimbali wa wilaya hiyo pamoja na mkoa kwa ujumla.Waziri Lugola pia aliwataka wananchi wilayani humo kutoa taarifa polisi za wahalifu hao ili kuwezesha operesheni hiyo ifanikiwe zaidi na wananchi waweze kuishi kwa amani na kufanya shughuli zao za kuijenga nchi. 

  Waziri huyo pia licha ya kusema anajua changamoto mbalimbali zinazowakibili polisi ikwemo ukosefu wa magari lakini aliwataka aliwataka wawahi katika matukio ya uhalifu yanapotokea, wanaweza kutumia pikipiki ili kuwahi kwa wakati katika matukio hayo. 

  Waziri Lugola yupo katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kigoma ambapo anatembelea Wilaya zote mkoani humo kwa kufanya kikao na watumishi walio chini ya wizara yake pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero zao pamoja na kuzitatua.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia uwekezaji uliopo katika shamba la Farm Africa Agro Focus (T) Ltd kwa kutumia ndege ya anga (Drones) wakati akikagua mashamba yaliyopo katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Anayechukua picha ni Afisa Habari wa Wizara ya Ardhi Hassan Mabuye.

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akikagua eneo la shamba la Magore wakati akikagua mashamba yaliyopo katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.


  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akioneshwa eneo la shamba la Farm Africa Agro Focus (T) Ltd na Meneja wa Shamba hilo Venkat Chelikani wakati akikagua uwekezaji wa mashamba katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.


  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akisalimiana na Ofisa Uhamiaji mara baada ya kuwasili katika wilaya ya Kilosa kukagua uwekezaji wa mashamba katika wilaya hiyo jana.
   
   
  Na Munir Shemweta, Morogoro


  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amebaini ujanja wa baadhi wa wawekezaji katika mashamba makubwa wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro kumilikishwa mashamba huku wengi wao wakiwa hawajaendeleza jambo alilolieleza kuwa ni kinyume na taratibu za uwekezaji.

  Aidha, Mabula alijionea jinsi baadhi ya mashamba yakionekana kwa nje kama yameendelezwa lakini kwa ndani hakuna kitu kilichofanyika na badala yake umiliki unaendeshwa kinyume kabisa na taratibu za umiliki mashamba hayo.

  Akiwa katika ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro jana, Mabula alisema lengo la kutembelea mashamba ya uwekezaji katika wilaya hiyo ni kubaini wawekezaji wasiofuata taratibu za uwekezaji mashamba na kutoa rai kuwa wale wote wasiozingatia sheria za uwekezaji basi mashamba yao yatafutwa.

  Alisema yeye na timu yake wamebaini ujanja unaofanywa na baadhi ya wawekezaji wa mashamba kwa kuhodhi maeneo makubwa huku wakiwa hawayaendelezi na kubainisha kuwa kazi ya kutoa mapendekezo ya kunyang’anywa mashamba kwa wale wasiyoyaendeleza ishaanza kufanywa na halmashauri husika huku baadhi ya mashamba yakiwa tayari yamefutwa na kusisistiza kinachoangaliwa ni kama wamiliki wamefuata sheria.

  Hata hivyo, alizitaka halmashauri wakati wa kupendekeza kufuta baadhi ya mashamba ni lazima zihakikishe zinatoa wito wa kushindwa kuendeleza shamba kwa muwekezaji ndipo taratibu za kufuta umiliki zifanyike hasa baada ya kujiridhisha kuwa mmiliki ameshindwa kabisa kufuata taratbu za uwekezaji ndipo anyang’anywe.

  Alisema, lengo la kuyachukua mashamba kwa walioshindwa siyo kwa ajili ya kuyagawa tu kwa wananchi bali ni kuyagawa kwa wawekezaji wengine wenye nia njema ya uwekezaji katika sekta husika, kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, kuwapatia ardhi wale wananchi wasiokuwa na ardhi kabisa pamoja na kuwa na ardhi ya akiba itakayosaidia katika shughuli za uchumi.

  Huku akitumia ndege ya anga (Drones) kuangalia uwekezaji wa mashamba Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alikagua mashamba ya wawekezaji ya Farm Africa Agro Focus (T) Ltd, Sadrudin Rajabah Meghs la Chanzuru, MS Sino Dev Co lililopo Kimamba, Sumagro Limited Co la Madoto, Noble Agricultural Enter lililopo eneo la Mvuni, New Msowelo Farm pamoja na mashamba ya Magore.

  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi alisema wilaya hiyo ina mashamba mengi na yenye rutuba lakini tatizo ni kuwa asilimia tisini ya mashamba katika wilaya yake ni mapori na mpango wa serikali ya kuchukua mashamba yasiyoendelezwa na kupatiwa watu wengine wenye nia ya kuwekeza.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akizungumza na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018 kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akiwa ameongozana na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani kuelekea baharini kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini. 

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani wakisaini makubaliano baada ya kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia katika Viwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akizungumza akipokea mkataba kutoka Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, baada ya kusaini makubaliano ya kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia katika Viwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah HamisUlega amekabidhi boti mbili za doria kwa BMU za Kilwa Kivinje na Mafia. Zoezi hili limefanyika katika Wilaya ya Kilwa eneo is Kivinje. Boti hizo zina thamani ya fedha za Kitanzania milioni 144 ambazo zimefadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia miradi ya WWF.

  Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya Bibi Jenny amesema wanafadhili miradi ya WWF hapa Tanzania yenye jumla ya bilioni 7 za Kitanzania. Aidha, amefurahi kusikia kwa uvuvi wa mabomu umepungua sana na hii ni sababu ya juhudi za serikali na wananchi wa maeneo haya. Pia alisema wao wamenunua boti ila jukumu za kuzilinda ni la Serikali ya Wilaya husika. Naye Mkurugenzi wa WWF nchini amesema wamepata taarifa kutoka kwa wavuvi kwamba sasa samaki wanaongezeka na kupatikana kwa samaki ambao walishapotea na haya yote ni kwa sababu ya kupungua kwa asilimia kubwa uvuvi wa mabomu. 

  Mhe Ulega Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema Umoja wa Ulaya umenunua hizi boti kuunga mkono kati kubwa inayofanywa na Mhe Rais John Pombe Magufuli ya Serikali yake ya awamu ya tano. Alisema amezunguka wilaya za Mkinga, Tanga Mjini, Muheza, Pangani na Lindi kote huko wavuvi wanakiri samaki wameongezeka kwa sasa. 

  Ukanda huu wa Pwani hauna viwanda vya samaki na kumuomba Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kutafuta wawekezaji kuja kuwekeza viwanda vya samaki katika mwambao wa bahari ya Hindi, pia alimuomba kufadhili ujenzi wa soko la samaki Kilwa Kivinje. Mhe. Ulega aliwaasa umoja wa vikundi vya BMU kutunza boti hizo na kuwaagiza Wilaya kusimamia ulinzi wa boti hizo. Mwisho aliwaomba WWF kuwaangalia BMU na wavuvi wa maeneo mengine kama Mkinga, Pangani, Lindi Vijijini na Mkuranga kwani nao wana mahitaji ya boti kama hizi katika ulinzi wa rasilimali zetu za bahari.

  0 0

  Hii ni kufuatia huduma za ndege kupitia Jumia kukua kwa 400% ndani ya Julai 2017 na Julai 2018.

  Katika kuadhimisha siku ya Utalii Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Septemba 27 ya kila mwaka, Jumia imejitanua tena katika huduma za ndege, safari hii ni kupitia ushirikiano baina yake na Amadeus, kampuni inayoongoza kwa teknolojia za usafiri duniani. Ushirikiano huu ni msingi wa soko jipya la huduma za ndege kwenye mtandao wa Jumia, ikiwa ni hatua nyingine mbele katika kufanya huduma za usafiri barani Afrika kuwa rahisi na nafuu.

  Jukwaa hili linalenga kuwawezesha mawakala wa usafiri, ndege, na tovuti za usafiri kuleta masuala yote yahusuyo huduma za ndege mtandaoni, kwa kuwapatia wateja bei nzuri za huduma za ndege zinazopatikana. Takwimu za sasa zinaonyesha kwamba 90% ya soko la huduma za ndege bado liko nje ya mtandaoni wakati ni 10% tu ndiyo lipo mtandaoni. Hii inakuja kufuatia kuongezeka kwa wateja wa huduma za ndege kupitia Jumia, ikiwa imeongezeka kwa kasi mpaka kufikia 400% ndani ya kipindi cha Julai 2017 na Julai 2018.

  “Jumia inaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika bidhaa zenye ubunifu kwa wasafiri na watoa huduma za ndege ambazo zitawasaidia kufanya mapinduzi kwenye uendeshaji wa shughuli zao na kuongeza mapato,” anasema Kijanga Geofrey, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia. “Tunalielewa soko na tunayashughulikia mahitaji yake. Jukwaa lenye ushindani litawaunganisha kwa pamoja watoa maudhui wote kutoa viwango vya chini na tozo ndogo ili kukidhi kuongezeka kwa mahitaji ya wasafiri kupata huduma bora zaidi kwa gharama nafuu,” anaongezea.

  Soko pia litatoa uchambuzi wa taarifa ambazo watoaji huduma wa tiketi za ndege wanaweza kuzitumia kutambua fursa mpya, njia na kuwasaidia kutengeneza vifurushi vya wateja wa ndege wanaowalenga.

  “Tunayo furaha kufanya kazi na Jumia katika kuwapatia machaguo wanayoyapenda wasafiri mtandaoni na kulifahamu vizuri soko. Usafiri wa anga unakua kwa kasi duniani, ambapo ongezeko la abiria barani Afrika linatarajiwa kukua kwa kasi na kuyazidi maeneo mengine kufikia mwaka 2035,” amesema Francesca Benati, Makamu Mkuu wa Rais wa Njia za Usafiri Mtandaoni katika Ulaya Magharibi, Mashariki ya Kati na Afrika, kutoka Amadeus.

  Bi. Benati ameongezea, “Ili kukidhi ongezeko hili la mahitaji, Jumia imeichagua ePower kutoka Amadeus ambayo inapatikana kupitia huduma za kwenye tovuti, ambazo zina matumizi rafiki ya kufanya huduma za mtandaoni kwa kutumia simu na tabiti (tablet). Imetengenezwa kuwasaidia watumiaji kutafuta ofa nzuri kwa haraka, ikiwa ni kwa msaada mkubwa wa bidhaa zetu za kiteknolojia za kufanya manunuzi na huduma za mtandaoni. Ninayo furaha kutokana na ushirikiano huu ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa wasafiri barani kote Afrika.”

  Jumia imejikita kwa kutoa bei nzuri ambazo huwatofautisha na washindani wengine kila kukicha. Kati ya mwezi Agosti na nusu ya kwanza ya Septemba, imefanya vizuri ukilinganisha na washindani wake wa mtandaoni katika njia 341. Aidha, 48% ya viwango vya utofauti huo, Jumia ina viwango bora vya nauli kwa ajili ya mapendekezo ya huduma za ndege nafuu na za moja kwa moja. Jumia inauchukulia utofauti katika njia hizo kama viwango bora vya nauli, ambapo bei ya nauli yake ni nafuu zaidi ukilinganisha na washindani wake kwa zaidi ya 60% katika viwango vilivyowekwa.

  Soko la huduma za ndege la Jumia tayari ni njia ya mauzo inayopendekezwa zaidi na watoa huduma na hupendelewa kama sehemu ya kukata tiketi na wasafiri wengi kwa njia kuu. Sasa hivi, sekta ya usafiri wa anga Afrika imechangia katika shughuli za utoaji wa ajira takribani milioni 6.8 na mapato ya dola za Kimarekani bilioni 72.5.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  RAIS Dk.John Magufuli ameagiza flyover ya Mfugale iliyopo makutano ya Tazara ifungwe kamera haraka ili watakaosababisha ajali wawe wanajulikana huku akisisitiza umuhimu wa daraja hilo kutunzwa na isiwe chanzo cha ajali.

  Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi flyover ya Mfugale ambapo pamoja na mambo mengine amesema ni lazima kamera zifungwe tena haraka.

  Rais Magufuli amefafanua "Nataka hapa katika flyover ya Mfugale pafungwe kamera.Tangazenu zabuni haraka kama mtaamua kumpa aliyejenga daraja sawa kama kumpa zawadi." Daraja hili ni la Mfugale na bahati nzuri Mhandisi Mfugale yupo ,hivyo naamini mtalifanyia kazi haraka,"amesema Rais Magufuli.

  Amefafanua kwamba kukiwa na kamera itakuwa rahisi hata ambaye amelewa na akasababisha ajali na kukimbia iwe rahisi kumfahamu na ajulikane.Pia amesema madaraja mengine makubwa na flyover ambazo zitajengwa lazima kufungwe kamera na hiyo itasaidia kulinda miundombinu mbalimbali ya madaraja na flyover.

  Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa watanzania kulinda miuondombinu hiyo na kubwa zaidi kuhakikisha haiwi sehemu ya kusababisha ajali na kupoteza maisha ya Watanzania.Wakati huo huo Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Dar es Salaam kwamba kuna mikakati mingi inaendelea ya kuhakikisha adha ya msongamano wa magar inapungua.

  Amezungumzia ujenzi wa flyover mataa ya Chang'ombe pamoja na eneo la Magereza ambapo amesema mazungumzo yalikwishaanza.Pia amesema kuna ujenzi unaendelea eneo la mataa ya Ubungo jumla ya sh.Bilioni 247 zitatumika kwa ajili ya eneo hilo ambapo  katika eneo hilo kutakuwa na daraja la ghorofa tatu,hivyo magari yatakuwa yanapishana juu kwa juu.

  Pia amesema tayari ujenzi wa barabara ya mwendo kasi kutoka Mbagala hadi Grezani mchakato wake unakwenda vizuri na itaanza kujengwa.Amesema anataka kuipendeza Jiji la Dar es Salaam na kwamba mipango na mikakati inakwenda vizuri huku akiwahakikishia wananchi wa Jiji hilo kwamba atafanya ziara.


  0 0


  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita na kuwasisiitiza umuhimu wa kuitumia kada ya habari katika kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita na kuwasisiitiza umuhimu wa kuitumia kada ya habari katika kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita na kuwasisiitiza umuhimu wa kuitumia kada ya habari katika kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel Robert akiongea katika kikao Kilichowahusisha Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa Halmashari, Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Maafisa Habari katika Mkoa wa Geita na Kumhakikishia Msemaji Mkuu wa Serikali na Viongozi wa TAGCO kuwa Mkoa utafanya mageuzi katika sekta ya habari ikiwamo kuwanunulia vifaa muhimu maafisa Habari katika mkoa wa Geita.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel Robert akiongea katika kikao Kilichowahusisha Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa Halmashari, Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Maafisa Habari katika Mkoa wa Geita na Kumhakikishia Msemaji Mkuu wa Serikali na Viongozi wa TAGCO kuwa Mkoa utafanya mageuzi katika sekta ya habari ikiwamo kuwanunulia vifaa muhimu maafisa Habari katika mkoa wa Geita.
  Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari na kuwahakikishia viongozi hao kuwa Maafisa Mawasiliano Serikalini watatumia Taaluma yao kuwafikia wananchi na kuwaeleza yale yanayotekelezwa na Serikali.

  Na Mwandishi wetu-MAELEZO GEITA

  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel ameahidi kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya habari katika Mkoa wake ili kuhakikisha taarifa za mkoa huo zinawafikia watanzania.

  Akiongea wakati wa kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel amesema kuwa Mkoa unatekeleza miradi mingi ya maendeleo hivyo ili kuweza kuwafikia wananchi ataviwezesha vitengo vya mawasiliano ili viweze kutekeleza jukumu hilo

  “Nawaahidi Viongozi wa TAGCO na Msemaji Mkuu wa Serikali nitawanunulia vifaa vyote muhimu Maafisa Habari katika Mkoa wa Geita, wanipe mahitaji yao najua nitakapopata fedha tutavinunua hivyo vifaa vyote ili kuweka mazingira mazuri ya kuwahabarisha watanzania, Serikali inatekeleza hivyo lazima watanzania wajue”-Alisema Mhandisi Robert

  Akiongea wakati wa Semina elekezi kwa Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewaeleza viongozi hao umuhimu wa kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwataka kuwashirikisha Maafisa Habari kwenye vikao vya kawaida vya maamuzi ili wawe Maafisa Habari wenye Habari

  Aidha Dkt. Abbasi alisisitiza Kuwa ni muhimu kwa viongozi wa Serikali kuwekeza katika Mitandao ya kijamii kwani huko ndio dunia ilipo kwa sasa. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete watahakikisha Maafisa Mawasiliano Serikalini Wanatumia Taaluma yao kuwafikia wananchi na kuwaeleza yale yanayotekelezwa na Serikali.

  “Makandarasi wako kazini wanatengeneza madaraja, wengine wanatengeneza reli ya kisasa hivyo kama ilivyo wao na sisi tutaingia kazini na kuhakikisha tunatumia taaluma yetu vizuri lengo ni kuieleza jamii mambo makubwa mazuri yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano .Katibu Tawala Mkoa wa Geita aliwataka Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari kufanya vikao vya kila mara ili kupeana mrejesho wa kile kinachofanyika katika mkoa ikiwemo utekelezaji wa Miradi

  0 0


  JOSEPH MPANGALA

  Waziri wa Nishati Dr.Medard Kaleman amezindua Mradi wa matumizi ya Nishati ya Gasi awam ya kwanza katika kiwanda cha Saruji cha Dangote kwa lengo la kuzalisha umeme wa megawatts 45 unaozalishwa na mashine tatu zenye uwezo wa Kuzalisha Megawats 15 kila moja.

  Uunganishwaji wa Nishati ya gas katika kiwanda Utaongeza uzalishaji wa Saruji katika Kiwanda cha dangote pamoja na Kupunguza matumizi ya gaharama za uendeshaji kwa asilimia 40 ambapo kwa sasa Dangote anazalisha Saruji kwa kutumia mafuta ya dizeli ambayo yanagharimu shilingi Milion315 kwa siku Gharama ambazo ni kubwa ukilinganisha na gharama za Umeme wa Nishati ya Gas.

  Akiongea mara baada ya Kuzindua matumizi ya Gas kutumika katika kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara Waziri wa Nishati Dr Medard kaleman amesema dhamira ya serikali kuweka mazingira Rafiki kwa wawekezaji wote ili waweze kuvutika kuwekeza hapa Nchini ili kuongeza Ajira kwa wananchii.

  “Punguzo la asilimia 40 katika Gaharama za Uzalishaji katika Kiwanda cha Dangote ni Tija kwa kampuni lakini ni Tija kwa serikali,kwa sasa Kiwanda Kinaweza Kuajiri wafanyakazi watu elf moja hadi elfmoja na miatano lakini wanafanya hivyo kwa sababu gharama za uendeshaji zilikuwa ni kubwa lakin kwa Kutumia Gas ambayo inawapunguzia gharama kubwa za uendeshaji wameniambia wanaweza kuongeza ajira kwa Watanzania”Amesema Dr.Medard.

  Akiongea kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Avod Mmanda amesema uzalishaji wa Saruji utakapoongezeka utaleta maendeleo ya Mtu Mmoja mmoja pamoja na ajira kwa wingi zaidi.

  “Kiwanda Hichi kitakapo zailisha Simenti kwa wingi maana yake ni kwamba usambazaji utakuwa Mkubwa,Hapa katikati Kiwanda Kiliposimama Mji Ulitikisika kwenye swala zima la Ujenzi kwa hiyo Siment Inapokuwa nyingi na kwa bei nafuu Ujenzi utaongezeka na ajira zitakuwepo kwa wingi”Amesema Mmanda. Mradi huu ni wa Awamu ya Kwanza wa Megawats 45 na awamu ya pili itakuwa na Megawats 75 kuingia katika kiwanda cha dangote na unatarajia kukamilia mwezi October 2019.
   Waziri wa Nishati DR.Medard Kaleman akikata Utepe Kuashiria Uzinduzi wa Matumizi ya Nishati ya Gas tayari kwa uzalishaji wa Umeme wa Megawats 45 katika kiwanda cha Saruji kilichopo Mkoani Mtwara.
   .Mtendaji Mkuu wa Kiwanda Cha Sarauji Cha Dangote kilivhopo Mkoani Mtwata akimuonesha Wazirir wa Nishati dr.Medard Kaleman Mitambo ya Umeme ya Umeme ya Megawats 45 ambayo imeanza kutumika katika Kuzalisha Saruji ya Dangote.
   .Waziri wa Nishati Dr.Medard Kaleman akitazama baadhi ya Mitambo ya Umeme ya Megawats 45 inayomilikiwa na Kiwanda cha Dangote ambacho tayari kimeanza kupokea Nishati ya Gas tayari kwa Uzalishaji wa Saruji.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa wa Japan Masaharu Yoshida anayetarajia kumaliza muda wake wa kuiwakilisha Nchi ya Japan hapa Nchini mwisho wa mwezi Septemba 2018.Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa wa Japan Masaharu Yoshida anayetarajia kumaliza muda wake wa kuiwakilisha Nchi ya Japan hapa Nchini mwisho wa mwezi Septemba 2018.Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU 


  0 0

  Na. VERO IGNATUS, ARUSHA. 

  Ubalozi wa Indonesia umeridhika na kazi zinazofanywa na Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini katika kudhibiti matumizi ya nyuklia sanjari na kushirikiana katika kuhakikisha matumizi sahihi ya nyuklia yanakwenda katika sekta ya viwanda.

  Akizungumza Balozi wa Indonesia Ratlan Pardede nchini Tanzania amesema upande kwa upande Indoneshia nyuklia wanaitumia katika viwanda na kilimo hivyo wanataka kuutumia uzoefu huo kwa kushirikiana na Tanzania ili kuinua uchumi kupitia teknolojia hiyo. 

  Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchini Profesa Lazaro Busagala amesema ujio wa Balozi wa Indonesia nchini a utaleta mafanikio katika sekta mbalimbali zinazotumia nguvu za nyuklia.Profesa Busagala amesema mbali na kutembelea katika Kituo hicho cha Nyulkia kilichopo Jijini Arusha pia aliweza kutembembelea mahabara ya kuzalishia nguvu za nyuklia na amesema kituo hicho kipo katika hatua nzuri kwani kazi za ndani zimeshamalizika kwa sasa wanamalizia za nje.

  Sambamba na hayo Balozi huyo amesema Mhe Rais Magufuli alimweleza Kwamba atafute maeneo mbalimbali nchini ambayo ataleta viwanda Tanzania kwa kupitia wafanyabiashara mbalimbali na ndicho anachochokifanya kwa sasa.Uwezekano wa Indonesia kuleta viwanda vinavyotumia teknlojia ya nyuklia na madawa, uchumi wa Tanzania utaongezeka kwani unaendana na sera sahihi ya serikali wa kujenga Tanzania ya viwanda.

  '' Tunapoongelea teknolojia ya nyuklia tunaongelea uwezekano wa kiwa na viwanda vingi zaidi uchumi wa nchi utaongezeka. "alisema Busagala. Licha ya nchi ya Indonesia kufanya vizuri katika viwanda, huku Tanzania nayo ikiweka mkazo na msisitizo katika uongezaji wa viwanja ameeleza ushirikiano huo wa Teknolojia mpya utasaidia nchi ya Tanzania kuondokana na upotevu wa asilimia 40 ya mazao ya kilimo na kuongeza mapato ya nchi kwa kiasi kikubwa
  Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Profesa Rtlan Pardede akizungumza na menejimenti ya Nguvu ya Atomiki iliyopo Njiro Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
  Mkurugenzi mkuu wa Nguvu za Atomiki nchini Profesa Lazaro Busagala akizungumza mara baada ya kuwasili ugeni kutoka Ubalozi wa Indonesia katika Makao makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Njiro Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
  Kaimu Mkurugenzi - Kurugenzi ya matumizi ya Teknolojia ya Mionzi Yesaya Sungita akimuonyesha Balozi wa Indonesia mahali pa kufanya vipimo na kuangalia usalama wa vyakula, Mahali pa kufanyia utafiti wa vitu vinavyotoa mionzi.
  Mkuu wa Idara ya Mionzi DennisMwalongo (watatu kulia) akitoa maelekezo kwa Balozi wa Indonesia Profesa Ratlan Pardede namna ambavyo mashine za kuhakiki, vifaavya mionzi, mashine za Kupima mionzi katika mwili wa Binadamu kama kuna dharura au ajali, wa pili kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Nchini Profesa Lazaro Busagala. Picha na Vero Ignatus. 
  Mgeni rasmi Balozi Indonesia Nchini Profesa Ratlan Pardede, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Nchini Profesa Lazaro Busagala, aliyepo kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Aquline Kessy, Mkurugenzi wa kinga ya mionzi John Ben Ngatunga na Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya matumizi ya Teknolojia ya Mionzi Yesaye Sungita. Picha na Vero Ignatus
  Picha ya pamoja na Mgeni rasmi Menejimenti ya Tume ya Nguvu ya Atomoki na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Picha na Vero Ignatus.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
   . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William aliyeambatana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William picha ya wanyama wanaopatikana katika mbuga mbalimbali nchini mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William Kamusi ya Kiswahili mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Picha kutoka kwa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha hiyo inamuonesha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa anazungumza na Malkia wa Uingereza Elizabeth II.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

  0 0

   Uchimbaji wa barabara hiyo inayotoka Kinondoni Mkwajuni nyuma ya Muslim ukiwa unaendelea
   Moja ya Greda likiendelea na kazi ya uchimbaji wa barabara wa eneo la Mkwajuni
   Greda jengine likiwa limepumzika kwa muda wakati wa kuendelea kusawazisha barabara hiyo
   Hili ni eneo ambalo Usawazishaji wa Barabara unaendelea, ambapo kifusi hicho mbele kinakaribia kuondolewa.
  Baadhi ya wahusika wa ujenzi wa barabara hiyo wakiwa wanashauriana jambo wakati kazi inaendelea
   Huu ni uzio uliowekwa ili wananchi wapite huko na wasiharibu utaratibu wa ujenzi wa barabara hiyo.Picha zote na Fredy Njeje.

  0 0

  Atuma salamu kwa watalaam wa mazingira..awaambia ole wao.

  Na Said Mwishehe,Globu ya kijamii

  RAIS Dk.John Magufuli amewataka watalaam nchini kuwa wazalendo kwa nchi yao huku akieleza kuwa baadhi ya watalaam ndio chanzo cha kukwamisha miradi na hasa ya maendeleo.

  Pia ametoa onyo kwa wataalam wa mazingira ambao wametoa mapendekezo ambayo ameyaita ua hovyo na yenye lengo la kukwamisha mradi wa umeme wa maji wa Stiglers georg na amewataka kuyafuta mapendekezo yao mara moja na ole wao wakishindwa kuyabadilisha.

  Rais Magufuli amesema hayo leo wakati anazindua rasmi flyover ya Mfugale katika makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi kueleza namna ambavyo baadhi ya watalaam nchini wamekuwa chanzo cha kukwamisha miradi."Ngoja nitoe mfano mmoja tu wa namna ambavyo baadhi ya watalaam wetu wanakwamisha miradi yenye tija kwa watanzania."Tena ni wataalam ambao wamezaliwa Tanzania na wamesomeshwa na Serikali,wengine ni weusi kuliko hata mimi lakini wanafanya maamuzi ya hovyo kabisa.

  " Tunafahamu umeme wa maji ndio wenye bei nafuu kabisa kuliko umeme wowote .Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tunapata umeme wa maji kupitia mradi wa Stiegler's Gorge,"amesema.Ameongeza wakati Serikali inataka kuanza ujenzi huo na fedha zipo tayari lakini watalaam wa mazingira wametoa mapendekezo yao.

  "Ukiisoma ile ripoti yao utakutana na mapendekezo mengi na baadhi ya mapendekezo yanasema watakaokuwa wanajenga eneo hilo wasijisaidie eneo hilo,waende umbali wa kilometa 10." Pendekezo lingine chochote ambacho kitapelekwa hapo kipimwe kwanza,yaani kama unataka kupeleka mchicha kwa ajili ya watu waliopo eneo la mradi basi lazima upimwe.Chochote ambacho utakipeleka eti wanataka kipimwe.

  *Pia kuna pendekezo la kwamba ikitokea gari ambayo ipo kwenye eneo la mradi ikiharibika haitakiwi kutengenezwa hapo ,yaani hata kubadilisja mafuta,kisa hawataki yamwagikie eneo hilo.Haya ni mapendekezo ya kijinga,"amesema Rais Magufuli.

  Ameongeza kuwa ukiangalia mapendekezo hayo unapata picha kwamba hawataki mredi huo utekelezwe na wanaoshiriki kuweka mazingira hayo ni baadhi ya watalaam ambao wanaendekeza maslahi binafsi.*Sasa niwahakikishie mradi huo utajengwa ili kupunguza bei ya umeme ambayo ni kubwa.Hatuwezo kushindana katika viwanda wakati umeme weti bei iko juu.

  "Hivyo nimewaagiza hao watalaam wa mazingira kubadilisha mapendekezo hayo na ole wale huyo mtaalam asipoyabadili," amesema Rais Magufuli.Akifafanua muhusu bei ya umeme amesema uniti moja ya umeme nchini Marekani ni Senti 0.12,Uingereza uniti moja ni senti 0.15 lakini hapa nchini Unit moja ya umeme ni Senti 10.7.Amefafanua mkakati wa Serikali ni kuwapunguzia gharama ya bei ya umeme na hilo halitabadilika,hivyo amewataka watalaam kuwa wazalendo badala kusikiliza watu kutoka nje.

  Amesema kumewepo na changamoto kubwa hasa unapotaka kukopa fedha kwa ajili ya kufanya maendeleo na unaweza kuomba na usipate fedha lakini ukitaka mkopo kwa ajili ya mambo ambayo hayana tija kwa wananchi unaupata haraka."Sasa tunazo fedha za kufanikisha mradi huo lakini watu wanakwamisha.Watalaam wetu igeni utumishi wa kizalendo na wa kutukuka kama Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale," amesema Rais Magufuli.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  wakati akizindua rasmi wa Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018.   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida akipena mikono na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa  baada ya kuzindua rasmi  Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018.   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa akimpongeza   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale  baada ya kuzindua rasmi  Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018. 
  Mke wa Rais Dkt. Magufuli, Mama Janeth Magufuli, akiongozana na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na mwakilishi wa BAKWATA Sheikh Alhad Mussa Salum wakielekea kushuhudia uzinduzi rasmi wa Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018.   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakisalimia mamia ya wananchi waliofurika kushuhudia uzinduzi rasmi wa Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018.   
   Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  ukipita katika Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam baada ya uzinduzi rasmi leo Septemba 27, 2018.  

  0 0


  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mwananjiolojia, Batwenge Chakutema kuhusu vifaa mbaIimbali vinavyotumika katika utafiti na upimaji madini wakati alipofungua Warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 .
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia zawadi ya kinyago cha njiwa wawili kilichotokana na jiwe wakati alifungua Warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . Kushoto ni Waziri wa Nishati, Angela Kairuki na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi
  Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakihesabu misokoto ya Bhangi iliyopatikana katika moja ya nyumba ya wakazi wa kijiji hicho katika operesheni iliyofanyika katika kijiji cha Kisimiri Juu kilichopo tarafa ya King’ori wilayani Arumeru.
  Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Elias Mwita akiwaonyesha waandishi wa habari misokoto ya bhangi iliyopatikana katika operesheni hiyo

  ………………………….

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Wananchi wa kijiji cha Kisimiri Juu Kilichopo tarafa ya King’ori wilayani Arumeru walikiacha kijiji chao kwa muda huku viongozi wao wakifunga ofisi zao na kukimbia kisa operesheni ya bhangi iliyofanywa na vikosi vya Jeshi la Polisi Alfajiri leo hii.

  Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi alisema kwamba walitapata taarifa kwamba kuna kiasi kikubwa cha bhangi kinatarajia kusafirishwa siku ya leo ndipo walipoandaa askari hao ambao walifanikiwa kufika eneo la tukio na kupata jumla ya magunia 27 yenye uzito wa Kilogramu 25 kila gunia shambani kwa mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa pamoja na Misokoto 583 ya Bhangi.

  Kamanda Ng’anzi alisema kwamba kwa sasa Jeshi la Polisi mkoani hapa linawatafuta viongozi wa kijiji cha Kisimiri Juu kwa kukiuka agizo la Serikali linalomtaka kila kiongozi katika eneo lake ahakikishe kwamba halilimwi bhangi.

  “Tunaendelea kuwatafuta viongozi wa kijiji pamoja na kamati zake za ulinzi na usalama na mkondo wa sheria utachukua nafasi kwani wao kama viongozi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha katika eneo lao hakuna biashara yoyote ya Madawa ya kulevya inayofanyika”. Alifafanua Kamanda Ng’anzi.

  Kamanda Ng’anzi alisema kwamba Jeshi hilo mkoani hapa lipo makini na litaendelea na mapambano dhidi ya Madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali na kubainisha kwamba katika eneo la mpaka wa Namanga matukio ya uingizaji wa madawa umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni wa Jeshi hilo mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Elias Mwita alisema kwamba operesheni hiyo sio ya kwanza kufanyika katika eneo hilo na itakuwa endelevu kuhakikisha kwamba zao hilo haliendelei kulimwa.

  Si mara ya kwanza kwa viongozi pamoja na wananchi hao kutotoa ushirikiano kwa Jeshi hilo pamoja na vyombo vingine vya usalama pindi wanapofanya operesheni ya bhangi katika eneo hilo ambapo huwa wanaacha makazi yao na kukimbilia milimani.

  0 0


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua moja ya machine mpya ya X-ray ya kisasa ambayo iko tayari kutumika. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akipata maelezo ya hatua iliyofikiwa katika usimikaji wa mashine ya CT Scan, wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt Respicious Boniface pamoja na viongozi waandamizi wa taasisi hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile Dkt Ndugulile akimjulia hali mtoto anayepata Huduma katika Taasisi ya MOI
  Mtaalamu wa viungo bandia wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Deus David akitoa ufafanuzi kwa Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile kuhusu namna viungo bandia vinavyotengenezwa na kufanya kazi.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na moja ya mgonjwa ambaye anatengenezewa kiungo bandia MOI ili kubainisha changamoto zilizopo zinazomkabili mgonjwa huyo.(Picha zote na MOI).  Serikali yatumia Bilioni 5.6 Kuiwezesha Taasisi ya MOI Kuwa na MRI,CT SCAN, X- ray na Ultra Sound

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile leo ametembelea na kukagua hali ya utoaji wa huduma katika baadhi ya vitengo katika Taasisi ya MOI na kukagua usimikaji wa mitambo ya kisasa katika kitengo cha radiolojia yenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 5.6 .

  "Lengo la ziara yangu ni kukagua maendeleo ya usimikaji wa mitambo hii ya kisasa ya MRI, CT SCAN, X-ray, Ultra sound, nimeona na kujiridhisha imekamilika kwa asilimia 99% . Naomba niwaelekeze mkamilishe mambo machache yaliyobaki ndani ya wiki hii ili wiki ijayo wagonjwa waanze kupata huduma hapa". Alisema Dkt Ndugulile.

  Pia, Dkt Ndugulule ametembelea vitengo vya mazoezi tiba pamoja na utengenezaji wa viungo bandia ambapo amekagua na kujiaonea hali ya utoaji huduma na kujiridhisha kwamba huduma zimeboreka katika kipindi cha miaka 3 ya Serikali ya awamu ya tano na kwa sasa watanzania wanapata huduma kwa wakati ijapokuwa kuna changamoto chache ambazo Serikali inazishughulikia.

  Aidha, Dkt Ndugulile ameupongeza uongozi wa MOI kwa kuhakikisha usimikaji wa Mitambao unafanyika kwa wakati na hali ya utoaji huduma ni nzuri na ya kuridhisha kwani wagonjwa wamekuwa wakipata changamoto ya kwenda nje ya MOI kufuata vipimo hivyo.

  Akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma na usimikaji wa mitambo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amemueleza Dkt Ndugulile kwamba hali ya utoaji wa huduma ni nzuri, wagonjwa wanapata huduma stahiki kwa wakati na idadi ya wagonjwa wanaopata huduma imeongezeka maradufu baada ya eneo la kutolea huduma kuboreshwa.

  "Mhe. Naibu Waziri, hali ya utoaji huduma katika taasisi yetu ni nzuri, idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji imeongezeka na kufikia 700-900 kwa mwezi kutoka 500 kutokana ongezeko la vyumba 2 vya upasuaji katika jengo hili, awali tulikua na vyumba 6 sasa vimekuwa 8, hii nikutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali hii ya awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli" alisema Dkt Boniface

  Akihitimisha yake Dkt Ndugulile amesema ni adhma ya Serikali kuhakikisha huduma zote zinapatikana hapa nchini hivyo ni vyema kama kuna kifaa chochote kinachohitajika taarifa itolewe Wizarani ili kifaa hicho kiwekwe kwenye mpango na bajeti na kununuliwa kwani utaalamu na weledi upo wakutosha.


  0 0

  KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Airtel, inaendelea na mpango wake wa kuboresha huduma zake, ambapo kwa sasa imekuja na mipango ya kufungua maduka yanayotoa huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni hatua ya kusogeza huduma hizo kwa wananchi.

  Katika kutekeleza mpango huo, tayari Airtel imefungua maduka zaidi ya 400 katika maeneo mbalimbali Nchini na hivyo kusogezakaribu na wateja wake huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuma na kupokea pesa, kurudisha namba iliyopote, kuswap Sim Card na kununua vifurushi mbalimbali vya Airtel.

  Akizungumzia mpango huo wa kufungua maduka na kutoa huduma kwa Mkoa wa dare s Salaam, Meneja wa Biashara Airtel Mkoa wa Dar es Salaam, Brighton Majwala amesema, miongoni mwa maduka yoa ya mkoa wa Dar es Salaam yamewezesha wateja wao kupata huduma za kampuni hiyo kwa urahisi zaidi.

  “Sisi Airtel, tumeamua kuanzisha maduka haya ili kusogeza karibu huduma zetu kwa lengo la kuwawezesha wananchi na wateja wetu kupata huduma hizo kwa urahisi na pia karibu na maeneo yao,”.amesema Majwala.

  “Hata hivyo hii ni fursa ya kipekee kwa mawakala wetu kuweza kupata huduma za Airtel Money na huduma nyingine bila kutembea umbali mrefu kuzifuata kama ilivyokuwa hapo awali”. ameongeza.Kwa upande wao baadhi ya wateja na mawakala wa wa Kampuni hiyo, wameeleza namna ambavyo wananufaika na huduma zinazotolewa na maduka hayo ya Airtel katika maeneo yao.

  “sisi wateja, tunafurahia huduma hizi kusogezwa karibu na maeneo yetu kwani inaturahisishia kupata huduma na kuokoa muda ambao tungeutumia kufuata huduma hizo maeneo mengine ya mbali na hapa” walieleza wateja hao.“Mawakala wengi wa hapa maeneo ya Tangi Bovu tunanufaika sana na uwepo wa Duka hili la Airtel katika maeneo yetu kwani kwa sasa tuweza kumuhudumia mteja kiasi chochote cha Airtel Money bila kuhangaika kufuata floti maneo ya mbali” aliongeza wakala Elizabeth Madeje

  Kufunguliwa kwa maduka hayo katika maeneo ya karibu na wananchi, kumeelezwa kuwasaidia wananchi na wateja wa Airtel kupata huduma za kampuni hiyo kwa urahisi na hivyo kuokoa fedha na muda wa kufuata huduma hizo maeneo ya mbali.

  Mkuu Wa mauzo wa Airtel Dar es salaam, Bryton Majwala akiongea na baadhi ya wateja wakati wa kuzindua moja kati ya maduka madogo madogo ya Airtel maarufu kama Airtel Money Branch mkoani Dar es salaam Mbezi Tangi bovu ambapo zaidi ya maduka 400 yameshafunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini. Anaehudumia wateja ni Afisa huduma kwa wateja wa duka hilo la Airtel Money Branch Tangi Bovu Bw, Thobias Bango. Duka hilo la Airtel limezindualia rasmi jana na Airtel ambapo litatoa huduma zote za Airtel kama vile kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea na kuharibika, pamoja na kusajili laini mpya kwa wateja wapya
  Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Branch ya Mbezi Tangi Bovu bw, Thobiasi Bango akitoa huduma ya kusajili laini mpya kwa wateja wa kwanza kwenye duka hilo mara baada ya uzinduzi wa duka hilo, Duka hilo la Airtel Money Branch Mbezi Tangibovu ni moja kati ya maduka 400 yaliyofunguliwa nchini na Airtel ikiwa ni mkakati wake wa kufikisha huduma zao kila mahali, huduma zinazotolewa ni pamoja na le kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea na kuharibika, pamoja na kusajili laini mpya kwa wateja wapya 

  Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando ( wakwanza kulia) pamoja  na msimamizi wa duka la huduma kwa wateja la Airtel Money Branch la Mbezi Tangi Bovu Thobias Bango wakisajili laini ya mteja wa kwanza Bi Elizabeth Gundula mara baada ya uzinduzi wa duka hilo jana. Duka la Airtel Money Branch Mbezi Tangibovu ni moja kati ni ya mikakati wa Airtel wa kufikisha huduma kila mahali, katika maduka hayo mteja ataweza kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea au kuharibika au kusajili laini mpya kwa wateja wapya.

older | 1 | .... | 1680 | 1681 | (Page 1682) | 1683 | 1684 | .... | 1898 | newer