Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1679 | 1680 | (Page 1681) | 1682 | 1683 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Karama Kenyunko,  blogu ya jamii.

  MWALIMU Mkuu wa  Shule  ya  Msingi ya Kimataifa  ya Hazina iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam na walimu  wake wanne wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya  Hakimu  Mkazi  Kisutu.

  Sababu za kupandishwa kizimbani inatokana na kutakiwa  kujibu  tuhuma za kupata  mitihani ya Taifa ya darasa la saba na kufanya mawasiliano ya maudhui yake na watahiniwa wa shule hiyo isivyo halali.

  Mwalimu Mkuu huyo Patrick Cheche (43) Wa shule hiyo ambayo mara kwa mara imekuwa ikitangazwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya darasa la nne na la saba na walimu wenzake wamesomewa mashtaka yao leo mbele  ya  Hakimu  Mkazi  Mfawidhi Huruma  Shahidi.

  Mbali na Cheche (43), anayeishi Mpinga Bagamoyo, washtakiwa wengine ni Laurence Ochien (30), Justus James (32), Nasri Mohamed (32) na Mambo Idd (32), ambao wote wakazi wa Dar es Salaam.

  Akisoma hati  ya  mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi  Mutalemwa Kishenyi  akisaidiana na Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amedai washitakiwa hao Septemba 4, mwaka huu, katika Jiji na Mkoa wa  Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama  ya kutenda kosa la kuingilia mitihani ya Taifa ya darasa la saba isivyo halali.

  Washtakiwa katika Shtaka hilo la  kula njama wanashtakiwa chini ya Sheria ya Kanuni za adhabu.

  Katika shtaka la pili ambao washtakiwa hao wanashitakiwa chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani la Taifa, wanadaiwa Septemba 5 mwaka huu katika shule hiyo ya Hazina, iliyoko Magomeni, kujibu, kinyume cha sheria walipata uwezo wa kupata mitihani wa taifa wa darasa la saba na kuonesha maudhui yake kwa watahiniwa waliosajiliwa Katina shule hiyo.

  Pia imedaiwa Katika shtaka la tatu, Septemba 5 mwaka huu katika shule hiyo washtakiwa hao kwa makusudi walitoa mitihani kwa watahiniwa waliosajiliwa katika shule hiyo wakati hawakustahili kufanya hivyo.Hata hivyo washtakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo  na wako  nje kwa dhamana.

   Kwa Mujibu wa  upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.Akisoma masharti ya dhamana,  Hakimu Shaidi amesema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana, kila mmoja anatakiwa awe na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho, vitambulisho na mmoja kati ya wadhamini hao awe anatambulika katika taasisi yoyote.

  Pia kila mdhamini anatakiwa kusaini bondi ya Sh.milioni sita na mshtakiwa wa kwanza na wa pili watatakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria kwani wao ni raia wa Kenya.Hata hivyo washtakiwa hao walifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana kasoro mshtakiwa wa pili  ambaye alipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana.

  Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama laa.

   Mwalimu Mkuu wa  Shule  ya  Msingi ya Kimataifa  ya Hazina iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam na walimu  wake wanne wakipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya  Hakimu  Mkazi  Kisutu mapema leo.

  0 0

  *Fly Over ya kwanza kujengwa nchini ,wananchi Dar watoa ya moyoni kwa Rais


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  FLY Over ya kwanza kujengwa nchini Tanzania inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho  na Rais  Dk.John Magufuli.

  Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo ni wazi Tanzania imeingia kwenye historia ya aina yake katika kuhakikisha inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza adha ya msongamano wa magari.

  Kwa sasa wananchi wa Dar es Salaam ambao wanapita katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere tayari wameanza kuonya raha ya uwepo wa Fly over hiyo iliyopo Tazara na kesho ndio siku ya uzinduzi rasmi.

   Taarifa ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari jana na leo inaelezwa kuwa uzinduzi huo wa Fly Over ya Tazara utafanyika kesho asubuhi.Fly Over hiyo tayari imepewa jina la Mfugale.

  Wakati uzinduzi huo ukisubiriwa kwa hamu na Watanzania na hasa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusu kukamilika kwa Fly over hiyo.

  Wakizungumza zaidi na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam wananchi wamesema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Rais Dk.John Magufuli kwa kuhakikisha ujenzi wa Fly Over hiyo unakamilika kwa wakati.

  Wamesema wameanza kuona namna ambavyo kero ya msongamano wa magari iliyokuwepo eneo la Tazara ambayo kwa sasa haipo tena.

  "Tunamshukuru Rais Magufuli kwa namna ambavyo Serikali yake ilivyodhamiria kuboresha maisha ya wananchi na hasa katika hili la ujenzi wa miundombinu.Imesaidia kutuondolea adha ya kutumia muda mwingi katika foleni ya Tazara ambayo kwetu ilikuwa kero kubwa.

  " Nchi yetu imeingia kwenye historia ambapo sasa nasi Watanzania tunayo nafasi ya kujivunia kukamilika kwa Fly Over hii ya Tazara,"amesema Shaban Chuma mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam.

  Jamila Jonathan amesema hakuwa akifikiria kama ipo siku katika Jiji la Dar es Salaam kutakuwa na Fly over lakini anamshukuru Rais kwani ameweza kufanikisha hilo.

  "Nimesikia kesho ndio inazinduliwa rasmi.Nashukuru binafsi nimeonja raha ya kupita katika Fly over ya Tazara.Hongera Rais wetu kwa kutuondolea  foleni iliyokuwa Tazara," amesema Jonathan ambaye ni Mkazi wa Pugu Stesheni.

   Ameongeza anatamani kuona katika makutano yote ambayo yanachangamoto kubwa ya msongamano basi yanakuwa na Fly over huku akieleza anafahamu kuwa kuna ujenzi unaendelea Ubungo ambao lengo ni kupu guza msongamano, hivyo anatoa pongezi kwa Serikali ya Rais Magufuli ambayo ikisema inatekeleza.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo katika kuzungumzia mambo mballi mbali ya kiutendaji wa Kazi
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo katika kuzungumzia mambo mballi mbali ya kiutendaji wa Kazi
  Viongozi wa Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji wakiwa katika kikao cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya Viongozi katika Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
  Mfanyakazi wa Kiwanda cha Wakala wa Uchapaji wa Serikali Jamal Khamis Juma alipokuwa akichangia katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Kiwanda hicho kilichofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),katika mkutano ulijumuisha Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati pichani) akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uchapaji wa Serikali Nd,Perera Ame Silima wakati wa kikao cha Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Uchapaji ulipokutana na Rais, leo katika Ukumbi wa Ikulu MJini Zanzibar,
  Picha na Ikulu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake nchini Mhe. Masaharu Yoshida aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Rais leo Ikulu jijini Dar es Salaam kuaga.
  1
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha leo Ikulu, jijini Dar es Salaam.
  4
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha leo Ikulu, jijini Dar es Salaam.
  13
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha ya Mwanamke shujaa katika Historia ya Kenya aliyefahamika kwa jina la Mekatilili Wa Menza kutoka kwa Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kujitambulisha.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
  ……………………………….
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Dkt. Alex Mubiru ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.

  Makamu wa Rais amesema kuwa AfDB imeahidi kuendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania kutokana na hatua kubwa ya kimaendeleo ambayo nchi yetu imeonyesha.Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika alisema kuwa wapo hapa kusaidia Serikali ya Tanzania pamoja na Watu wake.

  Wakati huo huo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alikutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Kenya nchi Mhe. Dan Kazungu ambaye alifika Ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.Mwisho Makamu wa Rais alikutana na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida ambaye amemaliza muda wake hapa nchi.

  Makamu wa Rais alimshukuru Balozi Yoshida kwa ushirikiano wote alioutoa kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.Nae Balozi Yoshida aliishukuru Serikali ya Tanzania pamoja na watu wake kwa Ushirikiano mzuri waliompa  kwa kipindi chake alichohudumu kama Balozi wa Japan hapa nchini


  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanya upasuaji mkubwa wa watoto pacha walioungana sehemu ya tumboni na kufanikiwa kuwatenganisha watoto hao wenye jinsia ya kiume.

  Upasuaji huo ambao ulitumia saa tano ulifanywa na wataalamu wa upasuaji wa Muhimbili kwa kushirikiana na watalaamu kutoka Ireland. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema hospitali imefanikiwa kufanya upasuaji kwa mafanikio na kwamba upasuaji huo umewezekana baada ya kuboreshwa kwa miundombinu ya utoaji huduma katika vyumba vya upasuaji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wataalamu.

  Prof. Museru amesema kuongezwa kwa vyumba hivyo kumesaidia kupunguza msongamano wa huduma ya upasuaji na hivyo kurahisisha utoaji huduma kwa watoto kutoka mara 4 hadi mara 10 kwa wiki.Amesema awali baada ya watoto hao kufikishwa Muhimbili walilazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha.

  Naye Daktari Bingwa Upasuaji wa Watoto, Dkt. Petronila Ngiloi amesema walishirikiana vyema na wataalamu wa upasuaji kutoka Ireland katika kuhakikisha watoto hao wanatenganishwa na kwamba lengo kubwa lilikuwa ni kupunguza hatari yoyote inayoweza kutokea kwa watoto hao wakati wa upasuaji.

  Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Dkt. Zaituni Bokhary amesema upasuaji huo ulihusisha timu ya wataalamu 10 wa upasuaji wa watoto, wauguzi na wataalamu wa tiba ya usingizi.

  “Nashauri watoto pacha walioungana au wenye matatizo ya kiafya waletwe Muhimbili ili wafanyiwe uchunguzi wa kina na baada ya kujiridhisha tutawapatia huduma stahiki,” amesema Dkt. Bokhary.
   Watoto pacha wakiwa wamelazwa wodini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kabla ya kufanyiwa upasuaji na wataalamu wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Ireland.
   Mama wa watoto pacha waliokuwa wameungana, Ester Simon akiwa amembeba mmoja wa watoto pacha baada ya kufanyiwa upasuaji na kutenganishwa na mwenzake ambaye amebebwa na Meneja wa Jengo la Wazazi namba mbili, Bi. Stella Medadi Rushagara
   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha waliokuwa wameungana sehemu ya tumboni. Watoto hao hivi sasa wanaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji.
  Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutoka kulia, Dkt. Zaitun Bokhary,  Dkt. Petronila Ngiloi na Dkt. Victor Ngotta wakiwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha waliokuwa wameungana kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto kutoka Ireland, Prof. Martin Carbally.

   

  0 0

           Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limeshiriki maonyesho ya kwanza ya madini yanayoendelea mkoani Geita kwa lengo la kuwafikia kwa ukaribu zaidi watanzania wote watakaoshiriki maonyesho hayo kwaajili ya kutoa elimu na kuandikisha.

  Maonyesho hayo ambayo yameshirikisha wadau wote wa sekta ya madini yameanza Septemba 24 hadi Agosti 30 2018 katika viwanja vya kalangalala mkoani Geita.

  Kufuatia mabadiliko ya sheria, NSSF sasa inalenga kuandikisha wale wote waliopo sekta binafsi ya ajira na sekta isiyo rasmi, ili wanufaike na mafao yatolewayo na shirika hilo ikiwemo fao la matibabu bure kwa mwanachama na familia yake.

  Akizungumza leo kutoka viwanja vya kalangalala Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita Bwana Shaban Mpendu ametoa wito kwa watanzania wote kutembelea maonyesho hayo ya migodi na kufika katika banda la NSSF ili kuweza kupata elimu ya mafao yanayotolewa na NSSF pamoja na elimu ya hifadhi ya jamii kwa ujumla. 

  Vilevile meneja amewataka wananchi hasa wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi kujiandikisha na NSSF. Uandikishaji unaofanyika katika banda la NSSF ni pamoja na uandikishaji wa waajiri, wanachama na usaijili wa matibabu bure.
   Meneja wa NSSF  mkoa wa Geita akimkaribisha mgeni rasmi Mh Stanslaus Nyongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini katika banda la NSSF kwenye maonyesho ya kwanza ya madini mkoani Geita
   Meneja wa NSSF mkoa wa Geita Shaban Mpendu akitoa elimu kwa wadau wa sekta ya madini juu ya huduma zitolewazo na nssf katika maeonyesho ya kwanza ya madini yanayoendelea mkoani geita
  Afisa mafao wa NSSF mkoa wa Geita bi Annastazia Ngallaba akimjazisha fomu ya uandikishaji mdau aliyetembelea banda la nssf kupata elimu na kuelewa somo hatimaye akaamua kujisajili.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stanslaus Nyongo akipewa maelezo kwa ufupi katoka kwa Meneja wa NSSF Geita Ndugu Shaban Mpendu juu ya huduma zitolewazo na NSSF alipotembelea banda la NSSF muda mchache kabla ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 


  WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeziasa halmashauri kuhakikisha zinapima maeneo ya wananchi na kuyaingiza kwenye mfumo ili kutambua idadi ya viwanja na mashamba wanayopaswa kulipa na kupatiwa hati miliki. 

  Imetoa rai kwa halmashauri hizo kutotumia kigezo cha kutopewa fedha na wizara hiyo kwa ajili ya bando la kuweka katika mfumo kama kikwazo cha kushindwa kukusanya mapato yatokanayo na ardhi. 

  Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Angeline Mabula.Alisema , suala hilo ni aibu kwa halmashauri kudai wanakosa kiasi cha sh. 20,000 ama 30,000 ya vocha . Angeline alieleza, halmashauri wasigeuze jambo hilo kama ni changamoto ya kushindwa kukusanya mapato yatokanayo na ardhi na kusubiri kupewa na wizara wakati hilo liko ndani ya uwezo wao. 

  “Mnakusanya mabilioni ya fedha kupitia viwanja mnashindwaje kukusanya mkiwa mnasubiri vocha ya shilingi 20,000 au 30,000 hili halikubaliki " 
  Angeline alifafanua,, halmashauri zihakikishe zinawezesha idara ya ardhi iweze kukusanya mapato badala ya kuiacha kama mtoto yatima . 

  “Tumerejesha maeneo mengi lakini nia njema ya kufanya hivyo baadhi halmashuri zimekiuka mnaweza kuwa na kasi ya kutaka maendeleo lakini unapaswa kufuata taratibu hatuwezi kutoa maeneo bila kufuata taratibu,” alisema Angeline. 

  Ofisa ardhi mteule wilaya ya Kibaha ,Majaliwa Jafari alieleza viwanja 1,700 vimepimwa lakini havijauzwa ambapo Kisabi 800 Disunyala 700 . Awali akisoma taarifa ya wilaya katibu tawala wa wilaya hiyo Sozi Ngate alisema , halmashauri ya wilaya ilikusanya milioni 504 na kutoa hatimiliki za kimila na imepima vijiji 22. 

  Anasema, mpango shirikishi wa matumizi bora ya ardhi umegusa maeneo tisa kati 25 vilivyopo ikiwemo Lukenge, Gumba, Magindu, Mpiji Station, Kwala, Dutumi, Minazimikinda, Mperamumbi.
   Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama akizungumza wakati Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha.
   Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akieleza jambo, wakati Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha.
  Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula ( wa katikati) akimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama (wa kwanza kulia )wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha, (wa kwanza kushoto) ni mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.(Picha na Mwamvua Mwinyi)

  0 0

  JOSEPH MPANGALA, MTWARA      
  Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetoa mafunzio kwa Wafanyabiashara wa Mkaoni Mtwara kuhusiana na Msamaha wa Riba na adhabu ya malimbikizo ya Madeni ya kodi kwa lengo la kuwawezesha wafanyabishara hao kuweza kutambua masuala yanayohusu Kodi pamoja na kuwahi Kuomba Msamaha wa Riba na Adhabu zake.
  Akifungua mafunzo hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda,Katibu Tawala Msaidizi  wa Mkoa wa Mtwara  Renatus Mongogwela amesema katika kipindi kirefu walipakodi wengi walikuwa wanashindwa kulipa Kodi zao kikamilifu kutokana na kuelemewa na malimbikizo makubwa ya Madeni yaliyotokana na Riba na Adhabu.
  “Nipende Kuwafahamisha Kuwa Serikali imesikia kilio cha Walipa kodi na kuweka taratibu maalim wa kuyaondoa hayo malimbikizo ya madeni ya riba,hivyo niwasihi ndugu zangu tutumie fursa hii adhim kuweka sawa masuala yenu ya kikodi na kupitia Msamaha huu Serikali inaaamini walipa kodi wataanza upya kuzifuata na kuzitii Sheria hizi”amesema Mongogwela.
  Mafunzo hayo ya Siku moja yamejumuisha mabadiliko ya Sheria ya kodi ya  mwaka 2018 pamoja na mfumo wa maadili wa watumishi wa mamlaka ya Mapato Tanzania {TRA} kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara  kuweza kutoa maoni na kapata huduma Bora.
   Katibu Tawala Msaidi wa Mkoa wa Mtwara Renatus Mongogwela akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na mamlaka ya mapato Tanzania {TRA} juu ya elimu ya Msamaha wa riba na adhabu kwa wanyabishara wa Mkoa wa Mtwara.
   Afisa maadili mwandamizi Mika Kiremera  kutoka mamlaka ya mapato Tanzania {TRA}makao makuu akiwasilisha mada kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi pamoja na maadili kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mtwaa.
   Msimamizi wa Shule ya Sekondari Aquinas Sister Paula Ngagani akiongea na Afisa Mkuu wa elimkwa Mlipa Kodu Makao Mkauu  Julius Ceasar  pamoja na Meneja wa Mamlaka ya mapato mkoa wa Mtwara  Naomi Mwaipola mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya TRA kwa Wafanyabiashara Mkoa wa Mtwara.
   Baadhi ya wafanyabishara waliohudhuria Mafunzo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania {TRA}Mkoani Mtwara kwa lengo la kutoa elim ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya Kodi,mabadiliko ya sheria ya kodi ya mwaka2018 pamoja na Maadili.
   Wafanyabishara Mkoa wa Mtwara wakiwa pamoja na maafisa wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mara baada ya Kumalizika kwa mafunzo ya siku moja kuhusina na elimu ya Msamaha wa Riba na adhabu pamoja na maadili kwa watumishi wa TRA>

  0 0

  Ikiwa imepita miezi miwili tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kuagiza pikipiki zote zinazotumika kusafirisha abiria zifungwe tela katika kile kinachoaminika kudhibiti wimbi la ajali za bodaboda,Taasisi mbalimbali za Serikali zimekutana jijini Dodoma ikiwa ni mazungumzo ya awali kuelekea mkakati huo wa kupunguza ajali.

  Akizungumza jijini Dodoma baada ya mkutano na ukaguzi wa pikipiki ya mfano iliyofungwa tela iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga,lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amesema Serikali imedhamiria kuondoa na kukomesha ajali za bodaboda pamoja na kulinda usalama wa watumiaji wa usafiri huo.

  Akielzezea juu ya mazungumzo hayo yaliyokutanisha taasisi hizo, Katibu Mkuu Meja Jenerali Jacob Kingu, amesema Wizara yake kwa kushirikiana na wadau wengine kutoka taasisi za serikali; Shirika la Mzinga, Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Kiwanda cha Kutengeneza Magari (NYUMBU) na Jeshi la Polisi watahakikisha wanakuwa na mpango wa pamoja wa kuratibu na kuhakikisha mkakati huo utakaosaidia kupunguza ajali unakamilika.

  “Leo tumekutana hapa kujadili jinsi ya kuliendea jambo hili la kufunga tela na kamati ya wataalamu hawa ndio itakutana na kuratibu andiko ambalo litapelekwa kwa viongozi wa wizara mbalimbali zinazohusika na suala la kudhibiti ajali za barabarani na kumlinda mtumiaji wa huduma ya usafiri huo,” alisema Meja Jenerali Kingu.Aliwaomba wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ambacho kamati hiyo ya wataalamu inaenda kuandaa mpango huo, na mapema mwishoni mwa mwaka huu mpango huo utatangazwa .

  Akizungumzia pikipiki hiyo ya mfano yenye tela, Mtaalamu kutoka Shirika la Mzinga, Mhandisi Salum Kipande alisema pikipiki hiyo wameitengeneza vizuri na itakua na uwezo wa kubeba abiria wanne na dereva mmoja huku akiahidi kuunga mkono adhma hiyo ya serikali kupunguza ajali za bodaboda nchini kwa kutengeneza pikipiki hizo kwa ustadi.

  Naye Kaimu Mkurugenzi Elimu na Mafunzo wa Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Stella Ndimubenya alisema wao kama VETA watahakikisha wanatumia teknolojia waliyonayo kuweka kifaa maalumu ambacho kitadhibiti upakiaji wa abiria kupita kiwango kilichopitishwa na mamlaka husika huku akiahidi kutoa mafunzo kwa madereva pindi pikipiki hizo zitakapopitishwa na kuanza kutumika.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akiwa amepanda Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akiwa amepanda Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akiwa amepanda Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu(aliyepanda pikipiki), akisikiliza maelezo ya kiufundi kutoka kwa mmoja wa wataalamu kutoka Shirika la Mzinga, Whemy Lyimo(kulia) waliotengeneza pikipiki hiyo yenye tela ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri, Kushoto ni dereva wa pikipiki hiyo,Stanley MsuyaTukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akipanda Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na timu ya wataalamu kutoka Taasisi za Serikali baada ya kukagua Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (ambaye alikuwa mgeni rasmi) akizungumza  katika Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na kufanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG.
  Wageni waalikwa na  Wanafunzi wa MUHAS waliohudhulia kongamano hilo.
   Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha MUHAS Prof. Andrew Pembe akitoa maneno ya kutambulisha Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
   Meza Kuu.
   Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS anayeshughulikia Taaluma, Tafiti na Ushauri Prof. Appolinary Kamuhabwa akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Dkt. Ndugulile.

  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

  Serikali imewataka watafiti kote nchini kufanya tafiti katika maeneo ya vipaumbele vya serikali, badala ya kufuata matakwa ya wafadhili. Amesema kufanya hivyo kutasaidia kuboresha sera na mipango ya maendeleo itakayowezesha kufikia malengo katika sekta mbali mbali ikiwemo afya na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025 Akizungumza katika Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amewataka watafiti kufanya tafiti zitakazozingatia takwimu sahihi ambazo zinachangia katika kuboresha sera na programu za afya. 

  "Natoa rai msifanye utafiti kwa sababu tu kuwa wafadhili wanatupatia fedha na msifanye tafiti na mkaridhika kwa vile tafiti zenu zimechapishwa kwenye majarida, bali mje na zile zitakazofanya mabadiliko ya sera mbali mbali hususani kuboresha upande wa afya," amesema. 

  Nae Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha MUHAS Prof. Andrew Pembe amesema matokeo ya utafiti yanaonyesha tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya bado ni kubwa na waathirika wa madawa ya kulevya hawawezi kushiriki katika shughuli za kuzalisha. 

  Ameongeza kuwa watumiaji wengi wa madawa ya kulevya wanajishughulisha katika vitendo vya uharifu, na wanauwezo mkubwa wa kupata magonjwa mbali mbali likiwemo UKIMWI. Upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS anayeshughulikia Taaluma, Tafiti na Ushauri Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema kuwa chuo kimejipanga kutoa taarifa inayotokana na matokeo ya tafiti ambayo itakuwa imeandikwa kwa lugha nyepesi na kuwapelekea wizara ya afya ambao badae wanaweza kuangalia ni mambo gani yanaweza kuwasaidia katika kuborsha sekta ya afya.

  0 0

  0 0

  Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala amesema TAWLA inatekeleza mradi wenye kuongeza ushiriki wa wawakilishi wanawake na vijana katika shughuli za kisiasa na Uongozi katika serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikiwa ni pamoja na ngazi za serikali za mitaa na vijiji.

  Ngw'anakilala ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kuimarisha uwezo wa majukwaa ya wanawake na vijana katika kujadili Changamoto zinazowakabili wanawake katika kushiriki kwenye shughuli za kisiasa uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

  Amesema lengo la mkutano huo ilikuwa kujengeana na kuimarisha majukumu na kujadili Changamoto zinazowafanya wanawake washindwe kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kiuongozi na siasa.

  "Nataka wanawake tuliomo katika mkutano huu tukishajadiliana tutoe mapendekezo namna ya kuainisha na kutatua changamoto ili kumwezesha mwanamke kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa na kupata fursa ya kuwa kiongozi katika serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

  Mkutano huo ulijumuisha majukwaa ya wanawake katika ngazi mbalimbali wakiwemo wabunge, Madiwani na wale waliowahi kugombea ubunge na udiwani kutoka vyama vya siasa vya CCM, CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo.
  Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala akizungumza wakati akifungua mkutano wa kuimarisha uwezo wa majukwaa ya wanawake na vijana katika kujadili Changamoto zinazowakabili wanawake kushiriki kwenye shughuli za kisiasa uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam jana.
  3
  Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala akisisitiza jambo wakati akizungumza alipofungua mkutano.
  04
  Sara Kinyaka Mwanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) akitoa mada katika mjadala wa mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
  4
  Isabela Nchimbi Mwanasheria wa Chama cha Wananasheria wanawake (TAWLA) akifafanua jambo wakati akichangia hoja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
  IMG_0593
  Josephine Arnold Afisa Mradi TAWLA akifafanua jambo wakati akitoa ratiba ya mkutano huo
  5
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika majadiliano hayo.
  6 7 8 9
  Sara Kinyaka Mwanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) akifurahia jambo wakati akitoa mada katika mjadala huo uliofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
  11

  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akiwa na Balozi Getrude Mongella kabla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata zao la muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe.


  NA DANIEL MBEGA, KISARAWE

  SPIKA wa zamani wa Bunge la Afrika, Balozi Getrude Ibengwe Mongella, amemtabiria mambo makubwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akisema kwamba anaamini atafika mbali katika uongozi wa nchi hii.

  Balozi Mongella, ambaye alipata umaarufu kimataifa alipoongoza Mkutano wa Wanawake uliofanyika Beijing, China mwaka 1995 akiwa mwenyekiti, alisema mkuu huyo wa wilaya atafika mbali katika uongozi na kinachotakiwa ni kuendelea kuchapa kazi bila kusikiliza kelele za pembeni, kwani hata yeye alikumbana na vikwazo vingi.

  “Nilifurahi sana ulipoteuliwa, nami nilianza harakati za siasa nikiwa binti mdogo kama wewe, nikakumbana na vikwazo vingi sana, lakini sikugeuka nyuma, kushoto wala kulia, ndiyo maana niliweza kufika mbali.

  “Hata wewe unayo nafasi kubwa ya kufika mbali, unaweza kuwa rais wetu katika siku za mbele kwa sababu naamini wanawake tunaweza,” alisema Balozi Mongella wakati wa uzinduzi wa kiwanda kidogo cha kuchakata muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe hivi karibuni, ambapo DC Mwegelo alikuwa mgeni rasmi.

  Mama Mongella alipongeza jitihada zilizoanzishwa na DC Mwegelo wilayani Kisarawe za kuhakikisha kwamba hakuna ‘sufuri’ katika elimu, huku akisema kwamba elimu ndio msingi mkubwa unaoweza kulikomboa taifa.

  “Unafanya kazi nzuri sana, nimekuona mwenyewe siku moja unakimbia huku umevaa kombati, nilifarijika sana kwa sababu hata mimi nilianza nikiwa binti kama wewe, nakuombea uendelee na kasi hiyo hiyo ya kuwaletea watu maendeleo na ndiyo itakayoonyesha ufanisi wa utendaji kazi wako,” alisema Mama Mongella.

  Kwa upande wake, DC Mwegelo alisema anashukuru kupata nasaha kutoka kwa Balozi Mongella, ambaye kwake amekuwa mwanamke wa mfano katika uongozi kutokana na utendaji wake katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

  “Nimefarijika mno kukutana na Mama Mongella ambaye kwangu amekuwa ‘role model’, binafsi ninatamani sana walau kufikia hata nusu ya mafanikio uliyofikia, ingawa ni kazi ngumu,” alisema.

  Mkuu huyo wa wilaya alitumia nafasi hiyo kujitambulisha katika Kijiji cha Kitanga, ambapo aliwataka wananchi kubuni na kushiriki shughuli za maendeleo kwa kuzingatia kwamba Serikali, chini ya Rais Dkt. John Magufuli, imedhamiria kwa dhati kuwaletea wananchi wake maendeleo.

  Alisema kwamba, wilaya hiyo ina ardhi kubwa yenye rutuba na kuwahamasisha wananchi kushiriki kilimo ili kuzalisha malighafi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya viwanda ili kwenda na falsafa ya Serikali ya kuifanya Tanzania ya Viwanda.

  “Nawaombeni tushirikiane katika maendeleo, tushiriki kilimo hasa cha mihogo na korosho na Serikali inaendelea kuandaa mazingira bora zaidi kuboresha kilimo pamoja na kuwatafutia masoko,” alisema.

  Siku hiyo mkuu huyo wa wilaya, akimwakilisha Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo, ambaye ni Mbunge wa Kisarawe, aliweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo kinachomilikiwa na akinamama wakiongozwa na Abia Magembe, ofisa kilimo mstaafu ambaye amejikita katika kilimo cha muhogo pamoja na kuchakata na kutengeneza bidhaa mbalimbali.

  Kiwanda hicho, ambacho ni sehemu ya Mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya Women for Africa Foundation inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, Maria Thereza de la Vega, kinachakata muhogo ili kupata unga ambao unatumika kuzalisha bidhaa mbalimbali.DC Mwegelo aliwapongeza akinamama hao na kuahidi kwamba, Serikali itakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha wanasonga mbele katika kujiletea maendeleo.

  “Nawapongeza sana akinamama, pamoja na kiongozi wenu Mama Magembe, hakika hizi ni jitihada zinazotakiwa kuungwa mkono na serikali yangu itafanya kila njia kuona kwamba mnasimama,” alisema.

  Aidha, aliwapongeza wafadhili wa Mradi wa Green Voices waliotoa mafunzo kwa akinamama 15 huko Hispania, ambapo akinamama 10 kati yao, akiwemo Mama Magembe, walianzisha miradi ya aina hiyo baada ya kurejea nchini huku wakiwafundisha akinamama wengine.

  Miradi mingine ni utengenezaji wa majiko banifu, ufugaji wa nyuki, kilimo cha uyoga, kilimo nyumba (green house) cha mboga mboga, ukaushaji wa matunda na mbogamboga kwa kutumia umeme-jua, kilimo cha matunda, kilimo cha viazi lishe pamoja na utengenezaji wa majiko ya umeme-jua.

  Miradi hiyo iko katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro, Morogoro, Kigoma na Mwanza.Balozi Getrude Mongella ni Mjumbe wa Bosi ya taasisi ya Women for Africa Foundation.

  0 0


  Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma jana kwenye Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) unaoendelea Jijini hapo. Mkutano huo unaoshirikisha zaidi ya washiriki 500 kutoka Halmashauri, Wizara na Idara mbalimbali za Serikali umedhaminiwa na benki hiyo.
  Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya NMB, Nsolo Mlozi akizungumza na Waandishi Habari Jijini Dodoma jana kwenye mkutano mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) unaoendelea Jijini hapo, Mkutano huo unawashirikisha washiriki zaidi ya 500 kutoka Halmashauri, Wizara na Idara mbalimbali za Serikali umedhaminiwa na benki hiyo.
  Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakipata maelezo walipotembelea banda la Maonesho la Benki ya NMB Ukumbi wa Dr. Jakaya Kikwete Jijini Dodoma jana- mkutano huo umedhaminiwa na benki ya NMB.

  BENKI ya NMB Plc imesema itaendelea kusaidia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kukuza uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

  Akizungumza na vyombo vya habari jana katika mkutano mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaoendelea jijini Dodoma, Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, amesema benki yake imetengeneza program mbalimbali za kusaidia kuchochea kasi ya uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

  Hata hivyo, amesema, benki ya NMB ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 31, ni miongoni mwa taasisi chache za fedha hapa nchini zinazofanya kazi kwa ukaribu sana na Serikali.“Kwa mfano, NMB imekuwa mdhamini mkuu wa mikutano mikuu ya ALAT miaka sita sasa, na kwa mwaka huu, benki imetoa udhamini wa shilingi milioni 100. Hii inaonyesha utayari wetu katika kufanya kazi pamoja na Serikali,” alisema.

  Aidha, amesema NMB inafanya kazi pamoja na wilaya na halmashauri zote nchini, ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo rafiki kwa wafanyakazi wa Serikali.“Lengo ni kuhakikisha huduma za kifedha za NMB zinawafikia Watanzania wote nchini hususani wale wanaoishi katika jamii za vijijini ambapo kunachangamoto nyingi za kimaisha na kiuchumi,” alieleza.

  Amesema kwa sasa benki imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kutoa mikopo rafiki kwa wajasiliamali wa kati na wadogo nchini, lengo kuu likiwa ni kuchochea uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo na mifugo.“Uchumi wa viwanda unategemea sana sekta ya kilimo na mifugo na hivyo, NMB itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo kupata mikopo nafuu na rafiki ili waweze kujikita katika miradi husika,” aliongeza.

  Pamoja na hayo, amesema ili kuhakikisha wajasiliamali wanufaika wa mikopo ya NMB wanafikia malengo yao, benki imefungua vilabu vya biashara nchi nzima, ili kutoa mafunzo maalumu ya mipango biashara.
  “Kutokana na usimamizi na utendaji mzuri wa benki ya NMB, tumefanikiwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 98 kama gawio kwa Serikali katika kipindi cha miaka saba iliyopita (2010 -2017),” aliongeza.Mponzi aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, benki imetumia zaidi ya shilingi bilioni 280 kutoa mikopo mbalimbali kwa wakulima na wachakataji wa mazao mbalimbali hapa nchini.

  Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Msolo Mlozi, amesema benki imejipanga vyema kusaidia maendeleo ya sekta mbalimbali katika kanda ya kati, hususani kipindi hiki ambacho Serikali imehamishia makao yake makuu rasmi jijini Dodoma.

  “Baada ya Serikali kuhamia jijini Dodoma kumekuwa na ongezeko kubwa la watu, hali ambayo imepelekea pia ongezeko kubwa la mahitaji mengi ambayo yanahitaji huduma bora na karibu za kifedha. NMB itaendelea kuboresha huduma zake katika kanda ya kati ili kuchochea kasi ya maendeleo pamoja na kutoa huduma nzuri zaidi kwa wateja wake,” alieleza.

  Mlozi ameitaja baadhi ya mikakati ya benki hiyo katika kanda ya kati kuwa ni pamoja na kusaidia wakulima wa alizeti, zabibu na mahindi, pamoja na kutoa mikopo mingine rafiki kwa wajasiliamali.Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakipata maelezo walipotembelea banda la Maonesho la Benki ya NMB Ukumbi wa Dr. Jakaya Kikwete Jijini Dodoma jana- mkutano huo umedhaminiwa na benki ya NMB.
  Wajumbe wa Mkutano Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakishiriki mkutano huo ndani ya ukumbi wa mikutano wa Dr. Jakaya Kikwete Jijini Dodoma- mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya NMB.

  0 0

  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwaonyesha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mpanda Mjini ushahidi wa ripoti ya TBS juu ya mabomba mabovu yaliyotumika kwenye mradi wa Manga, mkoani Katavi.
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Mradi, Mhandisi Edward Mulumba (kushoto) na mbele yao ni Mkurugenzi wa Mamalaka ya Maji mjini Tabora (TUWASA), Mhandisi Mkama Bwire.
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na wakandarasi eneo la mradi Nzega.

  ……………………….

  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ameagiza mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Manga uliopo Wilaya ya Mpanda Mjini, mkoani Katavi achunguzwe na TAKUKURU kutokana na kutumia mabomba yasiyokidhi viwango.

  Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha majumuisho na uongozi wa mkoa mara baada ya kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Katavi.

  Mradi huo wa Manga wenye thamani ya Shilingi milioni 575 unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingia mjini Mpanda (MUWASA) na kutekelezwa na mkandarasi anayejulikana kama Nyalinga Investment Co. Ltd, uligundulika kuwa una kasoro ya mabomba mara baada ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji mji wa Mpanda (MUWASA), Mhandisi Zacharia Nyanda kubaini ubovu wa mabomba hayo na kuyapeleka Shirika la Ubora wa Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya vipimo na kuonekana hayakidhi viwango.

  Amesema kuwa ripoti hiyo ya TBS imeonyesha kuwa kuna tofauti kubwa ya vipimo vya mabomba yaliyotumika na vipimo vinavyoonekana kwenye mkataba, hivyo kuthibitisha udanganyifu wa mkandarasi huyo na kumpongeza Mhandisi Nyanda kwa kugundua mapungufu hayo.

  ‘‘Nampa pongezi Mkurugenzi wa MUWASA kwa kugundua jambo hili; mabomba haya hayaonyeshi hata yametengenezwa wapi, achilia mbali kutofautiana kwa vipimo na vile vilivyo kwenye mkataba. Huu ni udanganyifu wa hali ya juu, ambao nimekuwa nikiusema kuhusu wakandarasi wababaishaji na sitafumbia macho wakandarasi wa aina hii’’, amesema Profesa Mbarawa.

  ‘‘Nataka TAKUKURU wafanye uchunguzi mkandarasi huyu alipataje kazi wakati hana uwezo, na kama kuna mtu kutoka wizarani anahusika kwa namna yoyote katika jambo hili siku zake zinahesabika maana nitamchukulia hatua’’, alionya Profesa Mbarawa.

  Profesa Mbarawa ametamka kuwa atamripoti mkandarasi huyo kwenye Bodi ya Wakandarasi nchini (CRB)ili wamchukulie hatua na kutaka asipewe tena kazi zozote za miradi ya maji, kwa kuwa wizara yake haitaruhusu wakandarasi wasio na uwezo kuendelea kula kodi za wananchi hali wakiendelea kukosa huduma ya majisafi na salama.

  Aidha, Profesa Makame Mbarawa ametembelea Mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tabora, Igunga na Nzega kwa lengo la kufuatilia utekelezaji; kufahamu na kutatua changamoto za kiutekelezaji ili ukamilike haraka iwezekanavyo.

  Ametembelea mradi huo katika mji wa Tabora na Nzega na kuridhishwa na kazi inayoendelea na kumtaka mkandarasi Larsen & Tourbo Ltd akishirikiana na Kampuni ya Shriram EPC zote kutoka India wanaojenga sehemu ya pili inayoanzia Nzega Mjini hadi Manispaa ya Tabora kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Uyui waongeze bidii.

  Profesa Mbarawa amesema atahakikisha changamoto zote zinazokabili ujenzi wa mradi huo zinapatiwa ufumbuzi haraka ili mradi huo unaogharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 268.35 zilizotokana na mkopo nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim Bank unakamilika ifikapo Novemba, 2019 baadala mwaka 2020 kulingana na mkataba.

  0 0   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika mkakati wake wa kuwapa tumaini jipya watu wenye ulemavu leo ameahidiwa Kiasi cha Shilingi Billion 5 na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi kwaajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachowaajiri watu wenye ulemavu ambao wana ujuzi wa aina mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi.
  4
  Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kueleza mpango wa kuwasiliana na wizara ya ardhi ombi la kupatiwa eneo la kujenga kiwanda cha kuajiri watu wenye ulemavu jambo lililomgusa Dr. Mengi na kuahidi kutoa shilingi billion 5 kuunga mkono mpango huo.
  1
  Hayo yote yamejiri leo wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya kusaidia walemavu ya Dr. Reginald Mengi persons with disabilities Foundation iliyozinduliwa na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambae pia amemsifu RC Makonda kwa agizo alilotoa kwa wenye viwanda kuwapa ajira walemavu kwa mujibu wa sheria na pia kampeni ya miguu bandia inayoendelea kuwasaidia walemavu.
  2
  Aidha RC Makonda pia ameeleza Mkakati wa kukutana na wamiliki wa shule binafsi kwaajili ya kuwaomba kusomesha watoto wawili wenye ulemavu bure kwa kila shule kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari ili kuwawezesha walemavu kupata elimu bora.
  3
  Kwa upande wake Naibu waziri Wizara ya Ajira, Wazee, watoto na watu wenye ulemavu Mhe. Anton Mavunde, Mbunge wa viti maalumu Mhe. Amina Molel na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu wamemshukuru RC Makonda kwa namna anavyopambana kuwakwamua watu wenye ulemavu.
  HUU SIO WAKATI KWA WALEMAVU KULIA WALA KUJUTA, NI WAKATI WA KUINUKA.

  0 0


  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike akiwasili katika viwanja vya Kikosi Maalum Cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) kabla ya kuelekea katika Baraza la maafisa na askari wa vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es salaam leo Septemba 26, 2018.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza katika Baraza la maafisa na askari wa vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es salaam leo Septemba 26, 2018 lililofanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga.

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike (katikati) akiwa meza kuu pamoja na Makamishna pamoja na Manaibu Kamishna wa Magereza katika Baraza la maafisa na askari wa vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es salaam leo Septemba 26, 2018 lililofanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga.
  Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia maelekezo mbalimbali ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike (hayupo pichani) katika Baraza la maafisa na askari wa vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es salaam leo Septemba 26, 2018 lililofanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga.

  Baadhi ya askari wa vyeo vya kati wa wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Phaustine Kasike (hayupo pichani) katika Baraza la maafisa na askari wa vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es salaam leo Septemba 26, 2018.
  Askari wa vyeo mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Phaustine Kasike(hayupo pichani) kama Inavyoonekana katika picha Picha na Jeshi la Magereza

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Taasisi ya watu wenye ulemavu ya Dk Reginald Mengi (DRMP), Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dk Reginald Mengi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi, Shimimana Ntuyabaliwe.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya kuzindua Taasisi ya watu wenye ulemavu ya Dk Reginald Mengi (DRMP), Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dk Reginald Mengi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi, Shimimana Ntuyabaliwe.  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuzindua Taasisi ya watu wenye ulemavu ya Dk Reginald Mengi (DRMP), Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dk Reginald Mengi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi, Shimimana Ntuyabaliwe na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, vijana na Ajira, Anthony Mavunde.  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mlemavu wa viungo aliyepooza viungo baada ya kupata ajali akiwa shuleni, kabla ya kuahidi kumsomesha mpaka hapo atakapomaliza elimu yake, baada ya kuzindua Taasisi ya walemavu ya Dk Reginald Mengi, Dar es Salaam jana.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu  SERIKALIi imeipatia Taasisi ya Dr Reginald Mengi Foundation ( DRMF) kiasi cha Tsh Milioni 10 ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za taasisi hiyo mpya itayojihusisha katika kulinda na kutetea haki za watu wenye ulemavu nchini.

  Akikabidhi Msaada huo leo (Jumatano Septemba 26, 2018) kwa niaba ya Serikali wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema jamii ya walemavu ni kundi mtambuka hivyo ni jukumu la wadau wa maendeleo kujitokeza katika kusaidia juhudi za Serikali katika ulinzi na haki yao.

  Waziri Mkuu Majaliwa alisema Serikali imendelea kutekeleza sera, sharia, miongoni na mikataba mbalimbali inayohusu haki za walemavu nchini ili kuliwezesha kundi hilo kupata huduma zote za msingi ikiwemo afya, elimu, kazi, ajira n.k

  Alisema Serikali tayari imetoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya kukusanya taarifa rasmi za watu wenye ulemavu waliopo katika vijiji, kata na vitongoji mbalimbali na kutambua umri, jinsia na shughuli wanazofanya.

  Aidha Majaliwa alisema Serikali pia imetoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini kutenga asilimia 2 ya mapato ya makusanyo ya ndani kwa ajili ya kusaidia ili kuliwezesha kundi hilo kuondokana na utegemezi wa kiuchumi pamoja na kupata mitaji ya biashara.

  “Serikali itachukua hatua kali kwa Mkurugenzi wa Halmashauri yoyote nchini ambaye atakikua matakwa haya ya kisheria na sasa tumeagiza pesa hizi zikusanywe na mapato yake yatangazwe hadharani kwa njia mbalimbali za matangazo ili kila mmoja ajitokeza na kupata” alisema Majaliwa.

  Akifafanua zaidi Waziri Mkuu Majaliwa alisema katika kutekeleza haki za kisheria na mikataba mbalimbali ya kimataifa kwa watu wenye ulemavu, Serikali imefanya mageuzi makubwa katika sekta za ajira na kazi, ambapo idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wameweza kuajiriwa nchini kupitia Sekretarieti ya Ajira na kupangiwa kazi katika taasisi mbalimbali za umma.

  Kwa mujibu wa Majaliwa alisema Serikali pia imetoa miongozo kwa mamlaka mbalimbali za udhibiti wa masuala ya majengo ikiwemo Bodi ya Wabunifu Majengo na Bodi ya Usajili wa Makandarasi kujenga miundombinu rafiki kwa kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kuwa vipando, viti, maliwato, lifti.

  Aliongeza kuwa Serikali pia imekuwa ikitenga kiasi cha Milioni 6.5 na kuzipeleka katika Halmashauri mbalimbali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ikiwemo mafuta pamoja na vyombo vya usikivu.Nitoe wito kwa mashirika, makampuni, taasisi pamoja na wadau wa ndani na nje ya nchi kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za Taasisi ya Reginald Mengi Foundation, kwa kuwa suala hili linagusa kila mtu katika jamii yetu” alisema Majaliwa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dkt. Reginald Mengi alisema Ofisi yake imepanga kutenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kitachojengwa Jijini Dar es Salaam na kitakachotoa ajira kwa watu wenye ulemavu nchini.Aidha Dkt. Mengi aliitaka jamii ya watu wenye ulemavu nchini kutokata tama kwa kuwa ulemavu haimfanyi mtu kupoteza uwezo wa kufanya kazi, na badala yake aliwataka kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo waliyofikia.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania Mussa Kabimba alisema kuanzishwa kwa Taasisi hiyo kutatoa fursa kwa watu wenye ulemavu kuwa na umoja wao utaowawezesha kuwa na sauti moja ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kiuchumi na kujiletea maendeleo yao.

  0 0   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo  Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongeza na viongozi wa  Wizara ya Afya Zanzibar wakati viongozi hao walipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano katika matibabu ya moyo. Ushirikiano huo utaimarishwa katika matibabu ya wagonjwa badala ya kuwapa rufaa kwenda kutibiwa nchini India wataanza kutibiwa JKCI na   madaktari kufanya matibabu ya pamoja ili wabadilishane  ujuzi wa kazi.
  Zanzibar 2
  Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dkt. Jamala Adam Taib akiongea jambo kwenye kikao kilichofanyika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baina ya viongozi wa  Wizara ya Afya Zanzibar na JKCI. Viongozi hao  walitembelea JKCI kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano katika matibabu ya moyo ikiwa ni pamoja na kuwapeleka wagonjwa katika Taasisi hiyo badala ya kuwapa rufaa ya kwenda kutibiwa nchini India na madaktari kufanya matibabu ya pamoja ili wabadilishane  ujuzi wa kazi.
  Zanzibar 3
  Kikao baina ya viongozi wa  Taasisi ya Moyo  Jakaya Kikwete (JKCI) na  viongozi wa  Wizara ya Afya Zanzibar kikiendelea.
  Picha na JKCI

  0 0

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi – Mh Abdallah Hamisi Ulega amefanya ziara ya siku 1 Pangani na kukagua miradi mbalimbali. Ametembelea soko la samaki Pangani Mashariki na kuahidi jokofu la kusindika samaki lenye thamani ya Mil 20. Aidha ameitaka halmashauri kumaliza migogoro na BMU mara moja.

  Aidha Mh Ulega ametembelea Chama cha Wafugaji wa ng’ombe wa Maziwa (WAWAPA) ambao kwa siku wanazalisha zaidi ya litre 10,000. Mh Ulega ameahidi kuleta josho la kuogeshea mifugo; ameahidi kuzungumza na Benki ya Kilimo ili wafugaji hawa wapatiwe mkopo nafuu; pia amewaunganisha wafugaji wetu na Taasisi ya uzalishaji na utafiti wa mifugo (TALIRI) ili waweze kupatiwa ufumbuzi wa magonjwa ya mifugo yao.

  Aidha, Mh Ulega ametembelea Chuo cha Uvuvi (KIM) na amewataka kabla ya 10 Oktoba wawe wamefika Wizarani na mikakati ya kukifanya chuo hiko kiwe na manufaa kwa wavuvi wa Pangani.

  Mwisho; Mh Ulega ametembelea BMU ya Kipumbwi na kuwataka wataalam wake kuja kutoa mafunzo na vitendea kazi kwa wavuvi hawa. Serikali ya Wilaya ya Pangani inampongeza sana Mh Ulega; inamshkuru sana Waziri – Mh Mpina kwa kufanikisha maombi yetu. Hakika Mh Rais amewatendea haki watanzania kwa kuletea majembe haya ya kazi. Pamoja tunaijenga Tanzania Mpya.

older | 1 | .... | 1679 | 1680 | (Page 1681) | 1682 | 1683 | .... | 1897 | newer