Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 166 | 167 | (Page 168) | 169 | 170 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea kombe kubwa kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa atakalokabidhiwa mshindi wa kwanza wa mashindano maalum kwa shule za sekondari Mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa na Wizara.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Yasoda. Vodacom ilikabidhi pia jezi za soka seti 12 na mipira.
   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akishirikiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa kukagua vifaa vya michezo muda mfupi kabla ya Waziri kukabidhiwa rasmi vifaa hivyo vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa. Vifaa hivyo vitatumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom ilikabidhi jezi za soka seti 12, mipira 40 na kombe kubwa la Mshindi
  ---------------------------

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala leo amepokea vifaa vya michezo kutoka Vodacom kwa ajili ya kutumika kwenye mashindano maalum ya sekondari yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar es salaam.  Akipokea vifaa hivyo ambavyo ni jezi seti 12 na mipira 40 pamoja na kombe kwa ajili ya bingwa wa michuano hiyo Waziri Dk Mukangala ameelezea kufurahishwa kwake jinsi ambavyo Vodacom walivyopokea ombi la Wizara la kusaidia mashindano hayo.  Amesema lengo la mashindano hayo ni kuendeleza azima ya serikali ya kutengeneza fursa ya ukuzaji na uendelezaji michezo kwa ngazi za chini kupitia falsafa ya michezo jamii.  “Michezo ni gharama inahitaji fedha nyingi kugharamia vifaa, mafunzo kwa walimu, viwanja na gharama nyengine za uendeshaji ndio maana naipongeza sana Vodacom kwa kukubali ombi letu la kusaidia mashindano haya maalum yatakoyoshirikisha shule 12 za sekondari za Mkoa wa Dar es salaam.”Alisema

  “Mashindano haya ni ya majaribio tukiangalia namna ambavyo tunaweza kuwekeza vya kutosha kwenye michezo ngazi ya mashuleni kwa nchi nzima, tutaanza na mchezo wa soka ila mipango ni kupanua wigo kwa kuongeza mpira wa pete na riadha kwa hapo mwakani ikihusiha mikoa mingi zaidi.”Alisema Dk. Mukangala.  Waziri Dk. Mukangala amesema Wizara yake inaimani kubwa juu ya mpango huo huku akizitaka jamii kuyapokea na kuyaona kuwa ni sehemu yao ili pamoja na kuyapapa mafanikio bali pia kuwatia moyo watoto wakati wote watakapokuwa waskishiriki.  Amesema kuwa anatambua kuwa mahitaji ni makubwa na kwamba kila shule hapa nchini ingependa kushiriki lakini kwa kuanzia watachagua shule 12 za sekondari kama majaribio huku mipango ikiendelea kuwekwa sawa ili mashindano hayo yawe mapana zaidi kwa hapo mwakani.  “Tuna shule nyingi hapa tu Dar es salaam tumepata wakati mgumu sana kuchagua wawakilishi wa kila Wilaya lakini kwa sasa tunaanza na hizo chache tukiwa na Vodacom na baada ya kumalizika tutafanya tathmini kuona namna ya kuyaongezea wigo wa ushiriki na wa kijiografia.”Alisema Dk. Mukangala Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa amesema Vodacom inatambua umuhimu wa kuwaandaa wachezaji katika ngazi za chini ili kuwa na uhakika wa maendeleo ya michezo nchini.

  “Kukubali kwetu kuwa wadhamini kumesukumwa na imani yetu juu ya maendeleo ya michezo nchini tukiamini katika kuwekeza kwa wanafunzi mashuleni, leo tunafuraha kuwa sehemu ya miapngo ya serikali kukamilisha kile ambacho kila mtu anapenda kukiona kikifanyika katika michezo.”Alisema Twissa.  “Tumekuwa wadhamini wa Ligi Kuu Vodacom ambayo imekuwa ikipiga hatua kubwa kimaendeleo hasa kwenye eneo la ushindani hivyo ili mafanikio hayo yawe endelevu ni lazima tuwe na misngi mzuri wa kuzalisha wachezaji wenye ubora na viwango na kwamba njia moja ya msingi ni kuwa na mashindano ya ngazi za chini hasa mashuleni”Alisema Twissa.  Amesema vifaa walivyovitoa ni sehemu ya Vodacom kuunga mkono juhudi za serikali za kutekeleza mikakati ya uzalishaji, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na kwamba Vodacom inafurahia mpango huo.


  Mashindno hayo maalum yataratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa – BMT na kwamba utaratibu umewekwa wa kuapat sekondari 12 kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es salaam ambapo kila Wilaya itatoa sekondari  4.
  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets the CEO of the Millenium Challenge Corporation (MCC) Mr.Daniel Yohannes in New York
    Zanzibar's Minister for Labour, Economic Empowerment and Cooperation Mr.Haroun Ali Suleiman meets MCC CEO Mr.Daniel Yohannes in New York
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with the Foreign Minister of the Sultanate of Oman Mr.Yousef Bin Alawi Bin Abdullah in New York

  Rais Kikwete: Tunaifanyia mageuzi makubwa TANESCO


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali yake inalifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa nia ya kuharakisha jitihada za Serikali kusambaza umeme kwa wananchi wengi zaidi.


  Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali imechukua hatua nyingi na kali za kupambana na rushwa kwa nia ya kukomesha vitendo hivyo katika Tanzania na kuinua kiwango cha utawala bora.


  Rais Kikwete ameyasema hayo Jumatano, Septemba 25, 2013 wakati alipokutana na kuzungumza na ujumbe wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani la Millennium Challenge Corporation (MCC) ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Bwana Daniel W Yohannes.


  Ujumbe huo umekutana na Rais Kikwete katika Hoteli ya JW Marriott mjini New York ambako Rais Kikwete amefikia kwa ziara yake ya kikazi katika Marekani ambako miongoni mwa mambo mengine atahutubia Mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) ulioanza jana, Jumanne, Septemba 24, 2013.


  Katika mazungumzo hayo, Bwana Yohannes amemwelezea Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya ombi la Tanzania kuingizwa katika awamu ya pili ya misaada ya Serikali ya Marekani kupitia MCC chini ya Akaunti ya Milenia Tanzania (MCA(T)). Nchi nyingine za Afrika ambazo maombi yao yanafikiriwa katika awamu hiyo ya pili ni Morocco, Mozambique na Lesotho.

             

  Tanzania ndiyo nchi iliyopokea sehemu kubwa zaidi ya msaada wa MCC duniani katika awamu ya kwanza ambako ilipewa kiasi cha dola za Marekani milioni 698 ambazo zimeingizwa katika miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, usambazaji wa umeme vijijini, miradi ya maji na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mafia.


  Serikali ya Tanzania imeamua kuwa fedha za awamu ya pili ya MCC zitaingizwa kupanua zaidi huduma za umeme na ujenzi wa barabara za vijiji kwa nia ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata huduma za umeme na kwa nia ya kuboresha barabara za vijijini katika maeneo yanayozalisha mazao kwa wingi zaidi.


  Serikali ya Rais Kikwete imeliweka suala la usambazaji umeme kwa Watanzania mijini na vijijini miongoni mwa maeneo yake ya kipaumbele. Wakati anaingia madarakani mwaka 2005, ni asilimia 10 tu ya Watanzania waliokuwa wanapata umeme. Katika miaka saba iliyopita, asilimia hiyo imepata hadi kufikia 21 ikiwa ni asilimia 11 zaidi kuliko katika miaka yote 50 ya Uhuru. Lengo la sasa ni kuifikisha asilimia 30 ama zaidi mwaka 2015.


  Katika mazungumzo hayo na Rais Kikwete, Bwana Yohannes ametaka kujua ni hatua zipi Serikali inazichukua kurekebisha changamoto zinazoikabili TANESCO na hatua gazi zinachukuliwa kuzidi kukabiliana na matatizo ya rushwa.


  Rais Kikwete amemweleza Bwana Yohannes: “Kama unavyojua, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepitia safari ngumu na kukabiliwa na changamoto nyingi lakini sasa tumeamua katika Serikali kulifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa kwa maana ya muundo wake na pia kuangalia viwango vya malipo ambayo Shirika hilo linawatoza wateja wake. Mageuzi haya katika TANESCO ni muhimu sana na yameanza kufanyika na kwa hakika Serikali imedhamiria kukayamilisha mageuzi hayo katika muda mfupi iwezekanavyo.”


  Kuhusu rushwa, Rais Kikwete amemwambia Bwana Yohannes, “Jitihada zetu katika kupambana na rushwa zinaendelea. Tumeimarisha taasisi inayohusika na kuzuia na kupambana na rushwa.Tumeimarisha mtandao wa kukabiliana na balaa hili na Serikali yangu imewafikisha mahakamani waliopata kuwa viongozi na maofisa waandimizi wa umma katika Serikali kujibu mashitaka ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.”

  Imetolewa na:

                                                     Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,


  DAR ES SALAAM.


  0 0

   
   Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi,akipata maelezo kwenye banda la Wakala wa Barabara (TANROADS) kutoka kwa Mkuu wa Kitendo cha Usalama na Mazingira,Zafarani A Madai.Dkt Nchimbi alikuwa akikagua mabanda mbalimbali kabla ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani yanayofanyika Jijini Mwanza Kitaifa.
    Mhandisi Rwehura wa TANROADS ,akimwonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani,Dkt Emmanuel Nchimbi,jinsi barabara zinavyojengwa chini ya usimamizi wa Wakala huyo wa barabara.  
    Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira wa TANROADS,Zafarani A Madai akimwonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi,jinsi madereva wanavyopaswa kutumia barabara ili kuepusha ajali kwa kutumia michoro mbalimbali . 
   Mhandisi wa TANROADS Jonas Matete, akiwapa maelekezo ya matumizi ya barabara vijana wawili ambao walitembelea banda la wakala huyo wa barabara ili kufahamu mambo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani yanayofanyika jijini Mwanza. Picha na Aisha Malima

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula akimkabidhi Sadock shilingi laki moja.
   Mlemavu Sadock akishukuru kwa kupewa fedha hiyo.
  ======
  Na Edwin Moshi, Makete
  Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimetekeleza ahadi yake kiliyoitoa mwezi uliopita kwa mlemavu Sadock Mahenge ya kumpatia shilingi laki moja kwa ajili ya kukarabati baiskeli yake

  Akimkabidhi fedha hizo taslimu nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula amesema kwa kuwa walimuahidi kumsaidia kurekebisha baiskeli yake na yeye kuaninisha gharama, ndipo wamempatia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya marekebisho hayo ili kumsaidia kutembea

  "nakumbuka wakati wa ziara yangu mwezi uliopita nilikuahidi mimi kwa niaba ya chama, hivyo ahadi hiyo tumeitekeleza naomba nikukabidhi fedha hizi shilingi laki moja zilizotolewa na CCM" alisema Chaula

  Kwa upande wake Sadock Sanga amekishukuru chama hicho kwa kutekeleza ahadi hiyo, na kuahidi kuzitumia fedha hizo kama zinavyotakiwa kwa kurekebisha baiskeli yake ili imsaidia kuzunguka maeneo mbalimbali kutekeleza wajibu wake

  Makabidhiano hayo ya fedha yameshuhudiwa na diwani wa kata hiyo Ashel Mwalyoyo, pamoja na viongozi mbalimbali wa chama

  0 0


  Wana kikundi cha Cash Money wakiwa tayari kwa kutoa msaada katika hospitali ya Temeke
  Mlezi wa Kikundi cha Cash Money ,Ratifa Masasi kulia akimkabidhi muuguzi wa wodi ya watoto bi, Nuswe Ambokile zawadi mbalimbali walizoleta kwa ajili ya watoto waliolaza katika hospital ya Temeke
  Baadhi ya wana kikundi cha Cash Money wakiwa katika picha ya pamoja na wauguzi wa wodi ya watoto Hospitali ya temeke baada ya kukabidhi msaada


  000000000  000000  00000.
  MSANII nguli wa muziki wa dansi aliyestaafu, Muhidini Gurumo, atapanda
  jukwaani leo kutumbuiza na mkewe, sambamba na kupewa zawadi za
  heshima.

  Gurumo atatoa  burudani hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaaga mashabiki,
  ambapo shughuli hiyo itaambatana na uzinduzi wa kundi la Cash Money,
  la Tandika mjini Dar es Salaam.

  "Tumeandaa zawadi kwa mzee Gurumo kutokana na heshima kubwa aliyonayo   katika tasnia ya muziki na kujenga maadili kwa taifa kutokana na   nyimbo zake.  Hivyo zawadi zetu zitaenda sambamba na uzinduzi, ambapo tumepanga   hivyo, ili lee mwenye chochote ampe mzee wetu,"Aliongeza Latifa Masasi    mlezi wa kundi hilo.  Uzinduzi huo unafanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Aziz
  Ali, Dar es Salaam na utapambwa na bendi mbalimbali za taarabu
  zikiwemo Coast na G Five.

  Kundi la Cash Money ambalo lilianzishwa mwaka 2011, pia limetoa vitu
  mbalimbali kwa wodi ya watoto, na vituo vya watoto yatima jana, ikiwa
  ni sehemu ya uzinduzi huo

  Mlezi wa kikundi cha Cash Money akimfariji mama Samir Nassoro, Naomi Ramadhani walipokutana wakati kundi hilo likitoa msaada kwa wagojwa katika wodi ya watoto
  Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Cash Money wakimfariji Bi Naomi Ramadhani
  Msanii wa bendi ya Msondo ngoma Saddy Ally katikati akisalimiana na wanakikundi cha cash money walipokutana katika hospitali ya Temeke wakitokea kutoa msaada
  Wana kikundi wa chass money kushoto Amina Uredi 'Mmanyema ' na Zulfa Kasongo
  Mlezi wa kikundi cha cash money bi, Ratifa Masasa akimfariji mtoto Salimu Ally wakati walipokwenda kutoa msaada katika hospitali ya temeke dar es salaam mwingine ni mama mtoto Tabu Salumu mkadhi wa Tandika

  0 0

   Mojawapo ya chemba ya vyoo hivyo.
   Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula akizungumzia hali hiyo.
   Mwenyekiti wa shule Hussen Mwalyoyo akizungumzia hali ya ujenzi huo.
   Choo hicho kikiwa hakina sakafu kwenye korido.
  ======
  Na Edwin Moshi, Makete
  Inawezekana ikawa ni mara ya kwanza kwa wilaya ya Makete kushuhudia kituko cha mwaka ambapo vyoo vya shule ya msingi Iwale wilayani hapo kujengwa bila ramani na BOQ, hali iliyopelekea mdari huo kutekelezwa chini ya kiwango

  Wakizungumza na mtandao huu kwa masikitiko makubwa wananchi wa kijiji hicho wamesema mradi huo ulianzwa kutekelezwa tangu mwaka 2009 ambapo hadi leo hii mradi huo haujakamilika kiasi cha kuanza kutumika

  Kutokana na maagizo yaliyotolewa na Bwana afya wa wilaya Bw Boniphace Sanga kuwa vyoo hivyo vianze kutumika kuanzia leo Septemba 26, hali hiyo imepelekea kamati ya ujenzi pamoja na mwenyekiti wa shule kugoma kuupokea mradi huo kwa madai kuwa umetekelezwa chini ya kiwango na hawako tayari kuruhusu uanze kufanya kazi licha ya maagizo ya maafisa wa wilaya ya kutaka uanze kutumika

  Hali hiyo imewalazimu mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula na viongozi wengine wa chama chake, pamoja na kaimu afisa elimu msingi Bw Fredrick Mkadange kufika shuleni hapo kujionea hali halisi ya vyoo hivyo pamoja na sababu za mradi huo kukataa kupokelewa

  Akizungumza kwa masikitiko makubwa mwenyekiti wa shule hiyo Bw. Hussen Mwalyoyo amesema sababu za mradi huo kutekelezwa chini ya kiwango ni pamoja na kukosekana kwa ramani pamoja na mchanganuo wa mradi huo (BOQ) hivyo kudai kuwa walishindwa kuhoji wakati wa ujenzi huo kwa kuwa hawafahamu namna vyoo hivyo vilitakiwa viwe

  'kila tukidai BOQ tunaambiwa mara ipo kijijini, mara wilayani yaani ni longolongo tu na kazi inaendelea hivyo hatukuweza kuhoji chochote kwa kuwa hatuna hiyo BOQ wala ramani ya vyoo hivi" alisema Mwalyoyo

  Afisa afya wa tarafa hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Chengula ambaye alikuwa mshauri wa ujenzi huo amesema hakukabidhiwa vifaa wala hakuna aliposaini yeye kupokea vifaa vya ujenzi huo badala yake aliambiwa awe mshauri wa ujenzi huo ambapo alikiri kufika eneo la ujenzi na kuwaelekeza mafundi hao.Mtaalamu huyo alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hata mkandarasi aaliyekuwa akijenga vyoo hivyo yeye hamfahamu

  Hali hiyo iliwalazimu wajumbe wote kufika kujionea vyoo hivyo, ambapo walishuhudia mapungufu mengi ikiwemo milango kutofunga, bati kuwa za geji 30 badala ya 20, vyoo havina madirisha, sehemu ya kujisaidia haja ndogo kwa wavulana kukosa sakafu laini, korido kutowekwa sakafu pamoja na chemba ndogondogo za kupitishia uchafu kutotengenezwa kwa kiwango

  Kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa CCM Francis Chaula alitamka kutoafiki vyoo hivyo vianze kutumika kama vilivyo na kusema vitaanza kutumika pale tu vitakapofanyiwa marekebisho waliyoyagundua ili kutosababisha madhara zaidi, jambo lililoungwa mkono na wajumbe wote wa kikao hicho ambapo pia wameagiza mchanganuo wa vifaa vyote vilivyoletwa kwa ajili ya ujenzi huo itolewe pamoja na BOQ

  Mwenyekiti aliahidi kufika ofisini kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Makete kwa ajili ya kupewa orodha hiyo na taarifa ataitoa kwa wananchi hao

  0 0


  Meneja wa kiwanda cha Pareto Martin Oweka kilichoko Wilayani Mufundi katika mji wa Mafinga.
  ========  ======  ========
  KIWANDA CHA PARETO(PCT) WAPATA HASARA BILIONI 1.4


  Na Denis Mlowe,Mufindi


  KIWANDA cha Pareto(PCT) cha Wilayani Mufindi, mkoani Iringa kimepata hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.4 baada ya kushindwa kununua pareto kwa wakulima na kuizalisha kwa kipindi cha miezi miwili. Meneja wa kiwanda Martine Oweka alisema mpaka sasa mitambo ya kuzalishia zao hilo ilisimama kwa muda kutokana na kukosekana kwa malighafi hiyo baada ya kuwepo kwa wanunuzi wengi, ambao wamekuwa wakisafirisha nje ya nchi licha ya kuwepo kiwanda.


  Alisema hasara kubwa inatokana na uwekezaji wao katika zao hilo ambapo, kwenye msimu wa kilimo walitumia Sh milioni 500, kuwanunulia wakulima miche ya pareto, elimu juu ya kilimo hicho sambamba na ujenzi wa maeneo ya kukaushia zao hilo, ili kuongeza sumu. " Mwezi Julai ilikuwa tupate tani 100 za pareto kwa wakulima lakini tuliambulia tani 20 wakati mwezi huu wa agosti kati ya tani 200 ambazo ilikuwa tukusanye, tumeambulia tani 30 tu, hii ni hasara kubwa sana kwetu hatukuwa na kibali cha kununua pareto kwa wakulima japo hiki ni kiwanda pekee Tanzania,”alisema Oweka.


  Alisema kibali cha kununua zao hilo kwa wakulima ilikuwa wapatiwe mwezi juni mwishoni, lakini badala yake walipewa August 21, mwaka huu kikiwa kimechelewa kwa miezi miwili.Hata hivyo alisema hasara ya Sh Bilioni 1.4 waliyoipata kwa kushindwa kuzalisha zao hilo, inawaghalimu wakulima ambao, wengi wao wamehifadhi pareto ndani kinyume cha taratibu za zao hilo, ambalo ubora wake hutegemea ukali wa sumu.


  “Mkulima akivuna Pareto halafu akahifadhi ndani kwenye unyevu kwa muda mrefu inapoteza sumu kiasi ambacho hata sisi wanunuzi inakuwa vigumu kuinunua kwani, ubora wa pareto ni kiwango cha sumu iliyopo,”alisema.Aliongeza kuwa kushindwa kununua pareto hiyo kumeisababishia hasara serikali kwa kuwa imekosa fedha za kigeni ambazo hutokana na mauzo ya nje ya zao hilo mara baada kuzalishwa kiwandani hapo. Aliwataka wakulima kutokata tamaa na badala yake waendelee kuzalisha zao hilo na kuiomba serikali kulinda soko la pareto.


  Kwa upande wao wakulima, wameiomba serikali kuhakikisha kuwa zao hilo halifi na kuona namna ya kulinda viwanda vya ndani vyenye uhakika wa soko badala ya kuruhusu soko huria, wakati malighafi hiyo hata ndani ya nchi haitoshelezi mahitaji. Uwezo wa kiwanda cha Pareto cha Mafinga ni kuzalisha tani 6,000 kwa mwaka lakini badala yake, kimekuwa kikiambulia tani 2,5000 pekee.
  0 0

    Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati walipokuwa katika mazoezi yao leo asubuhi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI. Katibu Mkuu alipita kuwajulia hali wachezaji wake na kujua maendeleo ya kambi hiyo. Picha na OMR
   Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akizungumza na wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati alipowatembelea kuwajulia hali katika Kambi yao mjini Dodoma leo wakiwa katika mashindano ya SHIMIWI. 
   Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ofisi yake, wakati alipofika katika Kambi ya timu hiyo kuwajulia hali mjini Dodoma leo asubuhi, wakiwa katika mashindano ya SHIMIWI. Picha na OMR

  0 0

  26th September 2013 - fastjet, Africa’s low cost airline, announces that its first international flight between Dar es Salaam and Johannesburg, previously scheduled to take place on Friday 27 September 2013, has been temporarily postponed.
   
  This postponement is due to unexpected administrative delays caused by the South African Department of Transport this week making a very late request for additional documentation.
   
  Although, fastjet delivered these documents without delay, the South African Department of Transport has said it will take several days to process these documents, thus delaying the start of fastjet flights on this international route. The delayed launch of this route is not expected to have any material effect on the financial performance of fastjet Tanzania.
   
  Commenting on the news, fastjet Chief Executive Ed Winter said: “This postponement is very disappointing. Unfortunately however, administrative delays of this nature are not unusual in the markets in which we operate. Having complied with all the requests made of us and secured all the necessary licenses and permits in an extremely diligent and timely fashion, fastjet was led to believe that we were fully on-track to launch this route on the 27th September.”
   
  fastjet would like to apologise to its customers for the inconvenience. All passengers affected by this delay will receive a full refund and assistance with re-booking a complimentary seat to fly within the next month.
   
  Tanzanian based customers can contact fastjet customer services on +255 685 680 537 and oncustomer.tanzania@fastjet.com for any queries.
   
  “Launching flights on this route remains a key priority for fastjet, and we are confident we will be operating on this service by mid-October, starting a new era of choice for passengers who continue to suffer inflated prices on flights between two of Africa’s largest and fastest growing cities” Winter continued.
   
  Flights between the two cities will initially be operated by fastjet three times a week on Mondays, Wednesdays and Fridays, increasing in frequency as soon as consumer demand dictates.
   
  “fastjet has been on an incredible journey since we started flying domestically in Tanzania with a single A319 plane nearly 12 months ago between Dar es Salaam, Mwanza, and Kilimanjaro,” said Winter.
   
  “Our Johannesburg route, where we will compete head-to-head with South African Airways to provide real value for money flights, represents the next step on that journey. Healthy and fair competition is vital in any economy and in any industry. Competition will bring choice and lower fares – a win-win for consumers,” he concludes.

  0 0
 • 09/26/13--04:12: TAARIFA KWA UMMA • 0 0

   Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi kushoto na dereva wa kampuni ya Tasia Hogistic ya jijini Dar es Salaam, Verry Philiph (39) wakikabidhiwa cheti baada ya kupimwa shinikizo la damu na wateknolojia wa maabara wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Theodol Babwanga kushoto na Daniel Mwita wakati mkuu huyo alipozindua mpango wa upimaji wa afya kwa madereva wa malori makubwa katika mizani ya Mikese kufuatia kampuni ya TBL kuendesha zoezi la upimaji wa afya kwa madereva wa malori ikiwa kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikibeba ujumbe wa "usalama unaanza kwangu kisha kwako na sisi sote" mkoani Morogoro.Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL. Steve Kilindo.
   Mkuu wa Usalama Barabarani Chalinze, Innocent Sule akiwa anazungumzana baadhi ya madereva wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya mikoa ya Dar es Salaam na Arusha zoezi lililofanyika katika mizani ya
  Kiangaiko iliyoko Msata Bagamoyo. Kampuni ya Bia Tanzania TBL, sh. mil. 13 kwa uongozi wa Hospitali Teule ya Tumbi kwa lengo la kufanikisha kupima madereva wanaotarajiwa kufikia 800 ikiwa na lengo la kupunguza kama si kumaliza ajali.
  Mmoja wa madereva akichukuliwa vipimo na daktari
   Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi kushoto na dereva wa kampuni ya Tasia Hogistic ya jijini Dar es Salaam, Verry Philiph (39) kulia wakipimwa shinikizo la damu na wateknolojia wa maabara wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Theodol Babwanga kushoto na Daniel Mwita wakati mkuu huyo alipozindua mpango wa upimaji wa afya kwa madereva wa malori makubwa katika mizani ya Mikese kufuatia kampuni ya TBL kuendesha zoezi la upimaji wa afya kwa madereva wa malori ikiwa kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikibeba ujumbe wa "usalama unaanza kwangu kisha kwako na sisi sote" mkoani Morogoro. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL. Steve Kilindo.
  MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Ahmed Kipozi (kulia) akizungumza na mmoja wa Daktari wakati alipokwenda kushuhudia zoezi la upimaji afya kwa madereva, makondakta na watu mbalimbali kwenye siku ya kwanza ya wiki ya nenda kwa usalama ambayo imefanyika katika mizani ya Kiangaiko iliyoko maeneo ya Msata Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.Katikati ni Meneja Uhusiano wa TBL,Doris Malulu.

  0 0

   Staa wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo,Rehema Chalamilla 'Ray C', akiingiza sauti ndani ya Studio za THT, chini ya maprodyuza Emma The Boy na Tudy Thomas,ambao wamepania kumrejesha katika game kwa kishindo msanii huyo, ambaye alipotea kwenye ulimwengu wa Burudani baada ya kutopea katika utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo kwa sasa ameachana nayo na kumrudia mwenyezi Mungu sambamba na kuendelea kutumia dozi ya kuondoa sumu ya madawa hayo.
   Ray C akiingiza sauti tayari kwa maandalizi ya ujio mpya kwenye game la Bongo Fleva.
   Prodyuza  Tudy Thomas (kulia), akijadiliana jambo lililotokana na majadiliano ya kuboresha ngoma mpya ya Ray C, pichani kati ni  Emma The Boy akipiga mzigo tayari kwa kumkamilishia Ray C ngoma yake mpya ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni.
   Ray C, akijaribu kutoa akapela kwa Maprodyuza hao, wakati wakiendelea kuiboresha ngoma yake mpya.
   Ray C, Emma The Boy &Tudy Thomas ndani ya Studio
  Ray C, akiwa katika pozi ndani ya studio hiyo.

  0 0

  MH. MUNDE TAMBWE (KATIKATI), MBUNGE WA VITI MAALUMU NA MJUMBE WA NEC, MGENI RASMI MAHAFARI YA DARASA LA SABA KATIKA S/M ISIKE MJINI TABORA LEO
  KUSHOTO NI KADUCHA J, ZINDUNA KISAMBA, CHARLES KIDIFU, MUNDE TAMBWE, ALLY KITENGE (M/KITI KAMATI YA SHULE)
  MGENI RASMI AKIKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU
  KATIKA MAJIBU YA RISALA YAKE AMETOA TASILIMU LAKI TATU (300,000/=) KAMA MCHANGO KWA BAADHI YA MAPUNGUFU YALIYOPO SHULENI HAPO.
  MWL. MKUU AKIZIHESABU PESA HIZO TSH 300000/= ZILIZOTOLEWA NA MUNDE TAMBWE MBUNGE WA VITI MAALUM MKOANI TABORA.
  VIGEREGERE VYA WANAFUNZI


  MGENI RASMI AKIKABIDHI NGOMA ZA BENDI YA SHULE
  MGENI RASMI AKIKABIDHI NGOMA KWA MWL MKUU WA SHULE BWANA CHARLES KIDIFU
  MWL WA BENDI AMBAYE PIA NI MLEMAVU WA MACHO AKIMPONGEZA MGENI RASMI AMBAYE NI MWANAFUNZI WAKE PIA
  WAHITIMU WA DARASA LA SABA
  WAZAZI NA WAGENI WAALIKWA
  NIDHAMU KWA WATOTO HAIENDI BILA BAKORA
  PICHA YA PAMOJA KATI YA WALIMU NA MGENI RASMI
  "LAZIMA TUMWONE MGENI RASMI HATA KAMA WAFUPI"
  (PICHA ZOTE NA ALOYSON BLOG)
  *****
  MGENI RASMI MUNDE TAMBWE AMEKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU 140, WASICHANA 78 NA WAVULANA 62 NA KUWASISITIZIA KUWA HAPO NI HATUA KUBWA LAKINI NI NDOGO SANA UKILINGANISHA NA WANAKO ELEKEA. AMEWASISITIZIA WAKAZANE ZAIDI KUSOMA ILI KURUDISHA ASANTE KWA WAZAZI WAO NA KUTIMIZA NDOTO ZAO ITI KULINUSURU TAIFA DHIDI YA JANGA LA UJINGA.

  MGENI RASMI, AKIJIBU RISALA LILILOSOMWA NA WANAFUNZI KATIKA SHULE HIYO AMETOA FEDHA TASLIMU 300,000 NA NGOMA ZA KISASA ZA BENDI YA SHULE HUKU AKIAHIDI KUENDELEA KUWA BEGA KWA BEGA NAO IKITOKEA WAMEPATWA NA MAPUNGUFU YANAYOWEZA KUTEKELEZEKA.

  CHANGAMOTO KUBWA ALIZOZIPOKEA ILIKUWA NI UCHAKAVU WA BAADHI YA VYUMBA VYA MADARASA MATATU NA UPUNGUFU WA MADAWATI.

  0 0

  Promota wa Mpambano wa Ubingwa wa UBO Kaike Siraju katikati akiwanyoosha mikono juu mabondia Ramadhani Shauri kushoto na Cosmasi Cheka watakaopigana tarehe 27 Mwezi wa kumi  jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


  MPAMBANO WA mwingine wa masumbwi unatarajia kufanyika Oktoba 27 katika ukumbi wa Friends Coner  Manzese Dar es salaam litakalo wakutanisha mabondia Ramadhani Shauri na Cosmas Cheka mpambano huo ulidhaminiwa na Hotel ya Tanamera ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani
   
  Akizungumza mratibu wa mpambano huo Kaike Siraju amesema amepata sapoto katika hotel hiyo ili aweze kuendereza vipaji vya vijana unakumbuka mimi ndie ninae andaaga mapambano makubwa nchini kama utakumbuka ila nilisimama kidogo kwa ajili ya kutafakali na kulekebisha mambo yangu binafsi lakini kwa sasa nimekuja kuinua mchezo huu kwa vijana chipkizi kwanza ndio msingi wa ngumi duniani kote
   
  aliongeza kwa kutaja mapambano ya utangulizi kuwa ni Mohamed Matumla anamenyana na Sadiki Momba huku Amosi Mwamakula akizichapa na Hamisi Ajali na Juma Fundi atazipiga na Shabani Kilumbelumbe
   
  Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama.Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
   
  DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
   
  Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (katikati) akionyesha kwa waandishi wa habari fomu ya usajili ya mbio za Rock City Marathon 2013 iliyodhaminiwa na kampuni yake jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bw. Geoffrey Nangai na Meneja Matukio wa CPI, Bw. Mathew Kasonta (kulia).
   Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam jana kutangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon 2013 zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI). Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bw. Geoffrey Nangai na Meneja Matukio wa CPI, Bw. Mathew Kasonta (kulia). 
   Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam jana kutangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon 2013 zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI). Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bw. Geoffrey Nangai na Meneja Matukio wa CPI, Bw. Mathew Kasonta (kulia) 
  Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Mathew Kasonta (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon 2013 jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mbando na Meneja Uhusiano wa CPI Bw. Geoffrey Nangai.

  ============   =========  ==========
  Airtel yapiga jeki mbio za Rock City Marathon 2013

  KAMPUNI ya Airtel ya Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money kwa mara ya tano mfululizo imetangaza kudhamini mbio za Rock City Marathon za mwaka huu zilizopangwa kufanyika mkoani Mwanza tarehe 27, Oktoba 2013 ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya mchezo wa riadha nchini.

  Airtel imekuwa mdhamini mkuu kwa upande wa mawasiliano katika mbiyo hizo, wakishirikiana na wadhaminiwa wengine kama NSSF, Africa Barrick Gold (ABG), Precision Air, Bank M, PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza Hotel, Sahara Communications pamoja na Umoja Switch, ili kutoa fursa ya kuinua mchezo wa riadha inchini.
  Akizungumza wakati wa tukio fupi lililofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando alisema kampuni yake imejidhatiti kusaidia  shughuli mbali mbali za maendeleo ya jamii na mbio za Rock City Marathon pia ni fursa pekee ya kukuza vipaji katika michezo huo kwa ujumla.

  “Kampuni ya Airtel Tanzania kwa mwaka wa tano mfululizo, leo hii tunatangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu ikiwa ni sehemu ya jitihada zetu za kusaidia maendeleo ya michezo nchi nzima. “Tunaamini kuwa mchango wetu utasaidia katika kuvumbua vipaji vipya vitakavyoshiriki si tu kwa mashindano ya kitaifa lakini pia na ya kimataifa,” alisema. 

  Mmbando aliongeza kuwa washiriki kwa mwaka huu wataweza kusajili moja kwa moja kupitia huduma ya kampuni yake ya Airtel Money kwa kutuma malipo yao kwa neno MARATHON na kuhifadhi ujumbe kwa ajili ya kuuonyesha wakati wa kuchukua fomu katika vituo mbali mbali.

  Kwa upande wake mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta wakati wa tukio alisema kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa na bora zaidi kwa kuleta pamoja washiriki kutoka ndani ya nje ya nchi.

   “Kwa mwaka huu tumeungana na kampuni ya Airtel lakini kupitia Airtel Money ili kutanua wigo wa ushiriki zaidi. Katika miaka iliyopita, watu wengi wamekuwa wakikosa nafasi ya kushiriki au wakilazimika kusafiri umbali mkubwa kwenda kwenye vituo vichache tulivyoviandaa ili waweze kununua fomu za usajili, kwa kupitia Airtel Money zoezi hili litakuwa limerahisishwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Kasonta.

  Kasonta aliongeza, “ukishamaliza zoezi hilo, utapokea ujumbe utakaouonyesha pale utakapokwenda kuchukua fomu za usajili katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mbeya, Arusha na Mwanza.”

  Alisema kuwa washiriki wenye vigezo pia wataweza kusajili kwa kupata fomu zipatikanazo katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza, na katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu, upande wa kulia katika jengo la ATC, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.

  Kasonta alibainisha kuwa fomu za usajili zitapatikana katika viwango vya bei vifuatavyo; shilingi 5,000 kwa mbio za km 21 (kwa watu wote), shilingi 3,000 kwa mbio za km 5 (mbio kwa makampuni na taasisi). Alisema kuwa fomu kwa mbio za kilometa 3 (kwa wazee kuanzia miaka 55 na watu wenye ulemavu wa ngozi) na mbio za kilometa 2 kwa watoto (wenye umri wa miaka 7 mpaka 10) zitapatikana bure.

  0 0

  Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Mswaga, anaondoka nchini siku ya Jumanne Tarehe 1-10-2013 kuelekea Equatorial Guinea kuwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Dunia ya Miss Tourism World 2013. Atasafiri kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airline.

  Katika mshindano hayo yanayo shirikisha nchi 126 duniani kote, na kuonyeshwa LIVE katika Televisheni Duniani kote, Miss Utalii Tanzania 2013, anabeba ujumbe wa kutangaza Hifadhi ya Ngorongoro Crater kama moja ya maajabu ya Dunia Afrika. 

  Akitoa sababu za kuibiba Hifadhi ya ngorongoro katika mashindano hayo, Hadija Mswaga, alisema kuwa mbali ya hifadhi hiyo kuwa ni ya kipekee duniani, lakini ndiyo hifadhi ambayo chimbuko la binadamu wa kwanza kuishi duniani, pia hifadhi hiyo ndio kitovu cha hifadhi ya faru nchini, mbali ya kuwa ndiyo hifadhi pekee duniani ambako binadamu na wanyama wanaishi na kushirikiana maisha ya kila siku bila ya kudhuriana.

  Wakati sasa umefika tena wakati sahihi kwa hifadhi ya ngorongoro kuwa hifadhi kiongozi kwa umaarufu ,pato la utalii na kutembelewa na watalii wengi zaidi duniani alisema hadija.

  0 0

  DSC_0019Mkurugenzi wa Mambo ya Kale toka Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Donatius Kamamba(kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mikakati ya serikali katika kulinda na kuhifadhi kumbukumbu na urithi wa Taifa, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi.Fatma Salum.DSC_0025Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Doreen Makaya(kushoto) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) akiwataka kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuzuia ujangili.Kulia ni Mkurugenzi wa Mambo ya Kale toka Wizara Hiyo Bw. Donatius Kamamba.  
  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
  IDARA YA MAMBO YA KALE 
  KUMBUKUMBU NA URITHI WA TAIFA
  Wizara, kupitia Idara ya Mambo ya Kale, inao wajibu wa kutambua, kulinda, kutunza na kuhifadhi Kumbukumbu na Urithi wa Taifa na Urithi wa Dunia kwa mujibu wa Sera ya Malikale ya 2008, Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 (R.E 2002) na Mkataba wa Kimataifa wa 1972 wa UNESCO.  Kumbukumbu na Urithi huu unatokana na rasilimali za Utamaduni zinazoshikika na zisizoshika; zinazohamishika na zisizohamishika kama zinavyoainishwa katika Sera ya malikale (2008), Sheria ya Mambo ya Kale, Sura 333.
  Wizara, kwa maana ya Idara ya Mambo ya Kale, ili kutekeleza azma hii inao wajibu, kwa kuwashirikisha wamiliki wa Urithi huu, kufanya na kuratibu Utafiti; kutambua umuhimu wa malikale husika kihistoria, kiimani, kisayansi, kisiasa na kiuchumi. Wizara, kupitia Idara ya Mambo ya Kale inalo jukumu la kutambua, kulinda, kutunza, kuhifadhi Kumbukumbu na Urithi wa Taifa na ule wa Dunia kwa mujibu wa Katiba ya nchi (1977); Sera ya Utamaduni 1999; Sera ya Malikale (2008) na Sheria ya Mambo ya Kale, (Sura 333).  Aidha, Serikali ya Tanzania imeridhia mikataba ya Kimataifa ya UNESCO ya mwaka 1954, 1970 na 1972.
  Malengo mahususi ya Sera ya Malikale 2008 ni pamoja na kufafanua dhima na majukumu ya  Serikali za mitaa, jamii, watu binafsi, mashirika na asasi mbalimbali katika kuhifadhi na kusimamia malikale; kuweka ufafanuzi sahihi wa kulinda, kusimamia, kutunza, kuhifadhi, kuendesha na kuendeleza malikale; kuweka Kumbukumbu  za Urithi wa Taifa kwa ujumla, na kuainisha namna bora ya kusimamia utafiti na uhifadhi wa malikale.
  Sera imeweka bayana kuwa suala la urekebu kuhusu utafiti na uhifadhi wa Urithi wa Taifa utafanywa na Serikali.  Aidha, suala la uhifadhi na uendelezaji malikale linahusisha sekta mbalimbali katika jamii na jamii kwa ujumla.  Wizara kwa kuwashirikisha wadau inakamilisha utaratibu wa kutunga sheria mpya kuhusu malikale ili Sera iweze kutekelezeka.
  Kimsingi, Urithi tegemewa (Potential heritage) wa Utamaduni unatengenezwa kila siku kutokana na kazi za binadamu wakati wa kupambana na mazingira ili kukidhi mahitaji yake.  Aidha, kwa msingi huo huo, Urithi tegemewa hutoweka kila siku.  Kwa mujibu wa misingi ya uhifadhi, umri wa miaka 100 na zaidi huonekana kuwa ni kigezo  na ni msingi muhimu.  Hata hivyo,  umri pekee yake hautoshi ni lazima umuhimu wake nao uainishwe na uwekwe bayana.
  Wizara hutenda yote hayo kwa ajenda ya kuhakikisha kuwa vielelezo halisi vya chimbuko na maendeleo ya binadamu vinarithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kijazi kingine.

  0 0

   Mwenyekiti wa soko kuu Makete mjini akizungumza kwenye ofisi za CCM.
   Mfanyabiashara Mia Sanga akizungumza ya moyoni mwake.
   Mfanyabiashara Andrea Sanga akiweka wazi aliyonayo
   Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula akizungumza na wafanyabiashara hao.
  ======
  Na Edwin Moshi,Globu ya jamii Makete
  Wafanyabiashara eneo la sokoni Makete mjini ambao wanatakiwa kubomoa mabanda yao ya biashara kupisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, wamebisha hodi kwenye ofisi za chama cha mapinduzi wilaya hiyo kupeleka malalamiko yao kufuatia kuandikiwa barua na halmashauri ambayo wamedai inawaumiza

  Wakiwa katika ofisi hizo, Mwenyekiti wa soko hilo Hosea Mpandila alitoa sababu za wao kuongozana kwa pamoja hadi kwenye ofisi hizo kuwa wanasikitishwa na kitendo cha wao kuzuiwa na halmashauri kuendelea na ujenzi wa vibanda vyao kwenye eneo ambalo walipangiwa awali na halmashauri licha ya baadhi yao kupeleka vifaa vya ujenzi kwenye eneo hilo

  Amesema jana waliandikiwa barua na mkurugenzi wa halmashauri ya Makete (mtandao huu unayo barua hiyo) ambayo amedai ina masharti ambayo hawawezi kuyatekeleza kwa kuwa yanawaumiza, ikiwemo la kutakiwa kuomba upya kupatiwa viwanja vya kujenga mabanda, na mabanda wakishayajenga wanatakiwa kuainisha gharama za ujenzi kwa halmashauri ambapo watakuwa wakilipa kiwango nafuu cha ushuru na kiasi kingine cha fedha kinachukuliwa na wafanyabiashara hao na wakisharudisha gharama za ujenzi, vibanda hivyo vitakuwa mali ya halmashauri na watakuwa na mamlaka ya kumpangisha yeyote wanayemuona anafaa

  "Kwa kweli inatusikitisha sana, hivi inawezekanaje sisi tujenge vibanda kwa gharama zetu wenyewe halafu tuje kurejeshewa gharama kidogokidogo na zikishakamilika mabanda yawe ya halmashauri, hii ina maana gani? kama ndivyo basi halmashauri ijenge vibanda itupangishe sisi" alisema Andrea Sanga

  Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mia Sanga amepinga uamuzi wa wao kuomba upya kupewa viwanja hivyo wakati wote walishapimiwa na serikali na kuruhusiwa kuendelea na ujenzi, na kuitaka serikali kuwarejeshea kama walivyowapa awali ili waendelee kujenga kwa kuwa muda waliopewa wa kubomoa mabanda yao kwa hiari unakaribia kuisha
   
  Akizungumza na wafanyabiashara hao kwenya ofisi za CCM wilaya hiyo, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula, amewapa pole wafanyabiashara hao na kushangazwa na barua hiyo waliyopewa na kuwataka kuwa na subira kwani wamefikisha malalamiko yao kwenye eneo sahihi na kuahidi kulishughulikia
   
  Chaula amesema haimuingii akilini wafanyabiashara hao kusimamishiwa ujenzi na kutakiwa kuomba upya huku akisisitiza wao kama chama watafika kwenye ofisi ya mkurugenzi kupata muafaka wa suala hilo mara moja
   
  Mtandao huu ulipofika kwenye ofisi ya mkurugenzi mtendaji kuzungumzia suala hilo, haukumkuta na badala yake mwandishi wetu alijibiwa kuwa mkurugenzi amesafiri kwenda Matamba kwa ajili ya kuangalai maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru

  0 0

  TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) leo (Ijumaa) itacheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya timu ya kombaini ya Shirikisho la Kandanda la Tanzania (TFF) na Chama cha soka cha mkoa wa Dar es salaam (DRFA).

  Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na TFF itaongozwa na Katibu wake mkuu, Angetile Osiah, Boniface Wambura (Msemaji), Saad Kawemba, Sabri na kipa, mzee Mshangama.

  Mbali ya wachezaji timu hiyo itakuwa na viongozi wengine wa DRFA akiwemo, Msanifu Kondo, Almasi Kasongo, Mohamed Mharizo. Pia kocha mkuu wa timu ya Taifa, Kim Poulsen, kocha wa timu za vijana, Jacob Michelsen na wasaidizi wao kama Jamhuri Kihwelu, Peter Manyika na wengineo watakuwepo uwanjani.

  Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa mbali ya yeye kuongoza jahazi la timu yake, pia watakuwepo wachezaji wengine kama Ali Mkogwe, Juma Pinto, Wilbert Molandi, Sultan Sikilo, Salum Jaba, Deogratius “Super Deo” Maganga, Kelvin Kiwia, Julius Kihampa, Sweetbert Lukonge, Elius Kambili, Zahoro Mlanzi, Frank Balile, Mwarami Seif, Saidi Seif na wengine wengi.
  “Huu ni mchezo wa kudumisha ushirikiano wetu kwani sisi ni waandishi wa habari za michezo na wao ni miongoni mwa wadau wetu, hivyo nawaomba wachezaji wote wafike kwa wingi ili kuona mechi hiyo ya aina yake,” alisema Majuto.

older | 1 | .... | 166 | 167 | (Page 168) | 169 | 170 | .... | 1897 | newer