Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

SERIKALI INATAMBUA NA KUHESHIMU MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA-WAZIRI UMMY MWALIMU

$
0
0





Mkurugenzi wa Watoto toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii kwaniaba ya waziri wa wizara hiyo. Mkutano huo uliandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation kwa kushirikiana na asasi ya An Nahl Trust.

Mkurugenzi wa Watoto toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai (kulia) akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii kwaniaba ya waziri wa wizara hiyo. Mkutano huo uliandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation kwa kushirikiana na asasi ya An Nahl Trust.
Mwenyekiti wa Asasi ya An Nahl Trust, Mhandisi Alliy Kilima akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na asasi yake kwa kushirikiana na NAMA Foundation leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa asasi ya An-Nahl Trust, akizungumza katika mkutano huo

Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.



SERIKALI inatambua na kuthamini juhudi za wadau mbali mbali zinazofanywa zenye lengo la kuhakikisha maendeleo ya Watanzania yanawezeshwa kikamilifu, hasa zinazochochewa na asasi za kiraia.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Watoto wa wizara hiyo, Margaret Mussai alipokuwa akifungua Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii ulioandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation.

Akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha asasi mbalimbali za kiraia, alisema Serikali inafarijika kuona wadau wakiungana na kupanga mikakati ya kufikia malengo ya mafanikio ya utendaji kwa pamoja kuihudumia jamii.“...Asasi za kiraia mmekuwa muhimili muhimu kwenye kuhimiza maendeleo ya jamii, mmekuwa mnabuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha vijana na wanawake kiuchumi na kutoa huduma za maendeleo ya Jamii kwa kutumia gharama nafuu na hata muda mwingine kwa kutumia rasilimali za wanaojitolea,”

“...Tunatambua mchango wa asasi nyingi za kiraia zinazotoa elimu juu ya mapambano ya magonjwa yanayoambukizwa, mila na desturi zenye madhara kwa vijana wakiwemo watoto wa kike na wanawake. Lakini pia kuna asasi zinazowezesha vijana kuwekeza kiuchumi katika miradi midogomidogo ya uzalishaji mali,” alisema Ummy katika hotuba hiyo.

Aidha alisema licha ya Serikali kutambua mchango mkubwa wa asasi za kijamii, alizitaka kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu na ushirikishwaji wa rika zote, huku zikizingatia sheria na katiba ya nchi ili kufikia malengo yao.Alizipongeza asasi za An Nahl Trust pamoja na NAMA Foundation kwa kufanikisha mkutano huo uliowakutanisha kwa pamoja wadau mbalimbali toka asasi za kiraia kuwajengea uwezo ukiwa na lengo la kuwajengea uwezo katika shughuli wao.

Kwa pande wake Mwenyekiti wa An Nahl Trust, Mhandisi Alliy Kilima alisema mkutano wa mwaka huu umekuja na maudhui mapana zaidi kuliko ule wa mwaka jana na umedhamiria kutoa taarifa kuhusu Maeneo yanayo lengwa na NAMA na Washirika wake ambayo ni 'Kuwezesha sekta ya Elimu, Kuwezesha sekta ya asasi za kiraia na Kuwawezesha vijana,' Na uwezeshaji wenyewe ni ule ule katika kukuza vipaji, maarifa, stadi na jinsi ya kuyaangalia mambo kwaupana wake.

Alisema mkutano huo utakuwa na watoa mada wataalam wa masuala mbalimbali watakao wajengea uwezo washiriki hususan katika mafunzo na idili za kujiendesha kwa kufuata taratibu na misingi mwafaka katika asasi zao.
Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ng’arika Kata ya Sapiwi Septemba 14, 2018 wilayani humo, katika Uzinduzi wa zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo ambayo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Simiyu kitakapojengwa .
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Igegu Kata ya Sapiwi Septemba 14, 2018 wilayani humo, kuhusu uzinduzi wa Zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo ambayo Uwanja wa Ndege wa mkoa wa Simiyu utakapojengwa.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Bi.Beaster Dotto Madale akifafanua jambo katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa eneo la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mkoa wa Simiyu, uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14, 2018.
Afisa Ardhi Mkuu kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bi. Cecilia Mwing’uri akifafanua jambo katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa eneo la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mkoa wa Simiyu, uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Igegu katika Kata ya Sapiwi Wilaya ya Bariadi, wakinyoosha mikono yao juu kumhakikishia Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Festo Kiswaga kuonesha utayari wao wa kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha mkoa huo, wakati wa Mkutano wa kuzindua Zoezi la tathmini na upimaji wa maeneo hayo, Septemba 14, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ng’arita katika Kata ya Sapiwi Wilaya ya Bariadi, wakinyoosha mikono yao juu kumhakikishia Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Festo Kiswaga kuonesha utayari wao wa kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha mkoa huo, wakati wa Mkutano wa kufungua Zoezi la tathmini na upimaji wa maeneo hayo, Septemba 14, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Wananchi wa Vijiji vya Igegu na Nga’arita Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi wameridhia kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mkoani Simiyu ambacho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Igegu wilayani .

Wananchi hao wameyasema hayo Septemba 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uthamini na upimaji wa maeneo hayo, ambalo linatarajiwa kumalizika baada ya mwezi mmoja na wiki mbili kuanzia sasa.

Wamesema kuwa wamefurahishwa na hatua ya Serikali kujenga Kiwanja cha Ndege wilayani Bariadi na kwa kuwa ujenzi huo ni suala la maendeleo hawawezi kupinga, huku wakiiomba Serikali kuhakikisha wanalipa fedha za fidia kwa wakati mara tu baada ya kukamilisha zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo hayo.

“Kwa kuwa ujenzi wa kiwanja cha ndege ni maendeleo hatuwezi kukataa kutoa maeneo yetu, tumekubali kutoa maeneo ila ombi letu kwa Serikali tunaomba tulipwe fidia ya maeneo yetu kwa wakati na tulipwe kwa haki” alisema Ndaturu Malemi mkazi wa Kijiji cha Igegu.

“Tumekubali kutoa maeneo yetu Uwanja wa Ndege ujengwe, ushauri wangu tu ni kwamba kwa kuwa tunaelekea msimu wa kuandaa mashamba baada ya tathmini tunaomba tuliokuwa na maeneo hapa tuambiwe mapema kama ujenzi utaanza au tunaweza kuendelea na shughuli za kilimo”alisema Mahembe Mayumba mkazi wa Kijiji cha Igegu

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amewataka Wataalam wa Ardhi watakaohusika na zoezi la uthamini na upimaji wa eneo litakojengwa Kiwanja hicho cha Ndege kufanya zoezi hilo kwa kufuata haki na sheria za nchi.

“Nimewaagiza wataalam watakaohusika kufanya zoezi la tathmini na kulipa fidia kwa kumuogopa Mungu, watende haki, kila ambacho mwananchi anapaswa kufidiwa wahakikishe kinafidiwa kwa mujibu wa sheria; tumekubaliana wataalam watavaa vitambulisho ili watambuliwe na ikitokea mtu akihujumu zoezi hili iwe rahisi kumfahamu na kuchukua hatua” alisema Kiswaga.

Akizungumzia suala la taarifa ya uthamini kutolewa mapema kwa wananchi, Kiswaga amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa muda wa mwezi mmoja na wiki mbili na baada ya hapo wenye maeneo watapewa taarifa.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Bi.Beaster Dotto Madale amesema Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa utawasaidia wananchi kupata usafiri wa anga ambao ni wa haraka, uhakika na salama, huku akisisitiza kuwa kiwanja hicho kitakapoanza kujengwa wananchi hususani vijana watapata ajira kwenye kazi za ujenzi na wanawake watajiajiri katika kazi za kupika na kuuza vyakula

Naye Afisa Ardhi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bi. Bi. Cecilia Mwing’uri amesema Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini (TAA) imeshatoa fedha kwa ajili ya tathmini, uthamini na upimaji wa maeneo Kiwanja kitakapojengwa na mara baada ya zoezi hilo kukamilika wananchi wanaohusika watalipwa fidia.

Bi.Cecilia amewahakikishia wananchi wa Vijiji vya Igegu na Ng’arita kuwa watalipwa fedha zao zote mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki , kwa kuwa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini (TAA) imetenga fedha hizo kwa ajili ya fidia ya Kiwanja cha Ndege cha Simiyu.

Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Bi.Beaster Dotto Madale Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mkoani Simiyu kitakapokamilika kitakuwa ni miongoni mwa Viwanja vikubwa hapa nchini ambavyo vina uwezo wa kupokea ndege kubwa.

TAA yawasilisha tozo ya huduma za usalama viwanja vya ndege

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati) jana akijadili jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara, Bw. Pius Wankali (kulia) na Kaimu Meneja Mipango na Takwimu, Nasib Elias (mwenye fulana ya bluu bahari) kabla ya mkutano na Wendeshaji wa Mashirika ya ndege kuanza kwenye ukumbi wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Myerere (JNIA-TB2). Kushoto ni Kaimu Mwanasheria wa TAA, Bw. Elius Mwashiuya.
DG AIRLINES2Meneja Uwajibikaji wa Shirika la ndege la Safari Plus LTD, Bw. Lauriano Balilemwa jana akitoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho ya tozo ya usalama wa abiria wakati wa mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Waendeshaji wa mashirika ya ndege zinazofanya safari kuanzia kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
DG AIRLINES3Waendeshaji wa Mashirika ya Ndege zinazofanya safari zake kwa kuanzia kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati mbele) jana alipozungumza nao kuhusiana na tozo ya usalama wa abiria ambayo itaanza rasmi kutumika Oktoba 1, 2018.
DG AIRLINES4Sammy Ndiramgu (kushoto) jana akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela baada ya kumalizika kwa mkutano na Waendeshaji wa Mashirika ya ndege uliofanyika kwenye ukumbi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
DG AIRLINES5Mwenyekiti wa Waendeshaji wa mashirika ya ndege ndogo za abiria, Chief Uyeka Rumbyambya akitoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho wakati wa kikao kati ya uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na waendeshaji hao uliofanyika jana kwenye Jengo la Pili la abiria la Julius Nyerere (JNIA-TB II).


MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), jana imewataarifu Waendeshaji wa Mashirika ya ndege za abiria zinazofanya safari zake kuanzia kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) juu ya tozo mpya ya usalama wa abiria.

Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amewaeleza kuwa utekelezaji wa tozo hiyo ambayo ni dola tano (5) kwa abiria wan je ya nchi na abiria wa ndani ni sh. 5,000 utaanza rasmi tarehe 1 Oktoba, 2018.

Bw. Mayongela amesema lengo la tozo hiyo ni uboreshwaji wa huduma na miundombinu ya Usalama katika Viwanja vya Ndege nchini ili kuhakikisha vinafikia viwango vya ubora vya Kimataifa na pia kutoa huduma bora za kiusalama kwa wadau wake.

Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na ada hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa TAA, Bw. Pius Wankali ameeleza kwamba agizo la ukusanywaji wa tozo  hiyo ulitangazwa rasmi na Mamlaka ya Usafiri wa  Anga (TCAA) mwezi Juni mwaka huu.

“Tangazo la kuanzishwa kwa tozo hii lilichapishwa na TCAA kutoka kwenye nyaraka AIC Doc No. TCAA/FRM/ANS/AIS-30, tarehe 29 Juni, 2018 na utekelezaji wake utakuwa ni kuanzia Oktoba Mosi, 2018,” amesema Bw. Wankali.

Kwa upande wa wawakilishi wa mashirika ya ndege kubwa kutoka Shirika la ndege Tanzania (ATCL), Bw. Ismail Ismail alitaka kuwepo kwa maelezo ya kina juu ya tozo hiyo, ambayo alitaka ijumuishwe ndani ya tiketi ili abiria awe ameilipia moja kwa moja.

Kwa upande wake mwakilishi mwingine wa ndege kubwa ya KLM, Bw. Alexander Van de Wint ameomba tozo hii ianze baadaye mwakani kutokana na wao tayari wameshauza tiketi za msimu hadi Desemba 2018 ili wasiwaumize abiria wao.

Mwenyekiti wa Waendeshaji wa Ndege ndogo za abiria, Chief Uyeka Rumbyambya amesema kuwe na taratibu za kumuhusisha Mkurugenzi Mkuu katika mikutano mbalimbali ya Waendeshaji wa Mashirika ya ndege, ili waweze kuwasilisha.

Naye Kaimu Meneja Mipango na Takwimu wa TAA, ambaye ni mratibu wa mkutano huo, Bw. Nasib Elias alitoa ufafanuzi juu ya ukusanywaji wa tozo hii, ambayo inatarajiwa pia kuwa ni moja ya chanzo cha mapato cha Mamlaka.

VIJANA 3,440 WANUFAIKA NA PROGRAMU YA UKUZAJI UJUZI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiwasisitizia wahitimu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana ili waweze kujiajiri kupitia programu ya ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifurahia jambo na Mkuu wa Shirika la DonBosco Kanda ya Afrika Mashariki Padre Saimon Asiri wakati wa mahafali kwa vijana walipata mafunzo ya kujengewa uwezo kupitia programu ya ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akishiriki kuimba na kucheza wimbo wa kuipongeza Serikali kwa kuanzisha programu ya ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania leo Jijini Dodoma pamoja na Wanafunzi wa chuo cha Don Bosco kutoka Mkoani Iringa.

Padre Celestine Kharkongor akieleza jambo kwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) kabla ya kuanza kwa mahafali ya vijana waliopata mafunzo ya ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania leo Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Msaki akieleza faida za mafunzo ya ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania leo Jijini Dodoma wakati wa mahafali ya vijana walioshiriki katika mafunzo hayo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiwa na sehemu ya vijana walinufaika na programu ya ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akimkabidhi cheti mmoja wa vijana waliohitimu mafunzo ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania leo Jijini Dodoma.
Watumishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) hii leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) hii leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifurahi na kucheza pamoja na vijana walipokuwa wakiimba nyimbo ya kuishukuru Serikali kwa kuanzisha programu ya ukuzaji ujuzi nchini kupitia vituo vya Don Bosco Net Tanzania.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu

………………………..

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mbunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amewaasa vijana 3,440 waliomaliza mafunzo ya ufundi kupitia programu ya ukuzaji ujuzi nchini inayotekelezwa na Serikali kutumia mafunzo hayo kujiajiri.

Akizungumza leo wakati wa mahafali ya vijana waliohitimu mafuzo hayo katika vituo vya Don Bosco Net Tanzania Mhe. Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuendelea kukuza ujuzi kwa vijana ili kuchochea maendeleo na ujenzi wa uchumi wa viwanda.

“Kazi ya kuwaandaa vijana kielimu na kiujuzi inayotekelezwa na Serikali ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka ya 2015 kupitia ibara ya 59 na 60 zinazoelekeza Serikali kuwaandaa vijana kielimu kiujuzi ili waweze kushiriki katika kujiletea maendeleo” Alisisitiza Mhe. Mhagama

Mafunzo ya ufundi kupitia programu ya kukuza ujuzi yalijikita katika fani za magari, ushonaji nguo, ujenzi wa nyumba, uchongaji vipuri,TEHAMA, Useremala ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na Serikali ya Tanzania.

Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa programu ya kuwajengea uwezo vijana kwa kukuza ujuzi wao ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa tuwapatie vijana ujuzi utakaowawezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Takribani wanagenzi zaidi ya 3000 wamehitimu mafunzo ya kukuza ujuzi kwa vijana yalifonyika ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwawezesha vijana kujiajiri.Katika kutekeleza azma hii Serikali imeelekeza juhudi za kuwawezesha vijana kupitia sekta mbalimbali ikiwemo Mpango wa Maendeleo ya Kilimo kupitia mpango wa Maendeleo ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II) kwa kuwa sekta ya kilimo inaajiri asilimia 66.3 ya ajira zote nchini.

Pia alizikumbusha Halmashuri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya Vijana ikiwa ni pamoja na kilimo, Pia aliwahimiza wanawake kushiriki kwa wingi kwenye mafunzo haya yatakapo anzishwa tena ili wakapate taaluma itakayowasaidia kuwawezesha kimaisha.Alizitaka Halmashauri pia kutenga asilimia 4 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha vijana na akina mama ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi na ustawi wao.

Naye Mkuu wa Shirika la Don Bosco Kanda ya Afrika Mashariki Padre. Saimon Asira amesema kuwa anawapongeza wakufunzi walioshiriki katika kuwaandaa vijana hao kwa kuwa wametekeleza jukumu hilo kwa ufanisi mkubwa.“Ninawaomba vijana waliopata mafunzo haya kutumia ujuzi waliopata kupitia programu hii na wakawe chachu kwa vijana wengine kwa kufanya kazi kwa biddii na maarifa” Alisisitiza Padre Asira

Kwa upande wake mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ally Msaki amesema dhamira ya Serikali ni kuondoa tatizo la ajira kwa vijana kwa kuwajengea uwezo wa kujiajiri ili waondokane na changamoto ya umasikini.

“Mafunzo haya yameweza kuwajengea uwezo Vijana ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuwakwamua vijana kiuchumi ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali.” Alisema Msaki.

Nae mmoja wa wahitimu Bi. Selestina Katwazo aliweza kuishukuru Serikali kwa kuwafanikishia kuweza kupata mafunzo haya ambayo yamewabadilisha kimaisha na kuwajengea uwezo wa kujiamini katika kufanya shughuli za kimaendeleo.

TIGO YAZINDUA MTANDAO WA 4G+ TANZANIA

$
0
0

Tigo 4G+ inawapa wateja huduma bora na za uhakika kwa gharama ile ile.

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali Tigo Tanzania, leo imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za mtandao wenye kasi ya juu zaidi nchini baada ya kuzindua teknolojia ya 4G+.

Uzinduzi wa mtandao wa 4G+ unathibitisha kuwa Tigo ni kampuni pekee ya mawasiliano inayofanya ubunifu unaoboresha huduma zake kuendana na mahitaji halisi ya wateja nchini kote.

‘Uzinduzi wa  4G+ ni sehemu ya safari ya mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo hapa nchini. Lengo letu ni kuwawezesha wateja kufurahia huduma bora zaidi za kidigitali. Daima tuko mbele katika kuleta teknologia za kisasa za mawasiliano nchini,’ Afisa Mkuu wa Tigo – Teknologia na Mawasiliano Jerome Albou aliwaambia waandishi wa habari katika uzinduzi wa mtandao wa Tigo 4G+ jijini  Dar es Salaam. 

Sasa wateja wa Tigo wanaweza kufurahia huduma bora, za uhakika na zenye kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui kutoka kwenye mtandao kwa gharama zile zile. Ili kufurahia mtandao wa 4G+, mteja anahitaji kuwa na simu yenye uwezo wa 4G+.

Teknologia ya kisasa ya Tigo 4G+ inaongeza wigo wa matumizi ya huduma za kidigitali nchini. Teknologia hii inapanua utoaji wa huduma za intaneti yenye kasi ya juu zaidi, pamoja na kutoa huduma za sauti zinazoendana na mabadiliko ya maisha.

‘Kampuni yetu inajivunia kuzindua teknolojia ya 4G+ inayoiweka Tanzania katika ramani ya teknolojia ya mawasiliano duniani. Sasa tunashindana na nchi zilizoendelea ambazo tayari zinawekeza katika teknolojia ya 5G. Kupatikana kwa teknolojia ya kisasa ya mawasiliano nchini Tanzania kunaibua fursa mpya za matumizi ya mtandao kwa wateja wetu,’  Afisa Mkuu wa Biashara - Tigo, Tarik Boudiaf alibainisha.  

Mbali na kujivunia mtandao wa 4G ulionea katika miji 22 nchini, mtandao wa Tigo 4G+ tayari unapatikana katika miji ya; Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Moshi na Dodoma, hata hivyo mipango ya kuendelea kuupanua mtandao huo kufikia miji mingine zaidi nchini inaendeliea.  Wateja wanaotumia simu zenye uwezo wa 4G+ sasa wanaweza kufurahia kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui mbali mbali kwa gharama zile zile za intaneti.

Mtandao wenye kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+ una kasi mara mbili ya ule wa Tigo 4G, kwani Tigo  4G ina kasi ya 60Mbps ilihali mtandao mpya wa Tigo 4G+ unaweza kufikia kasi ya hadi 120Mbps. Kwa ujumla, wateja wanaotumia Tigo 4G+ katika eneo husika hugawana kasi hii ya juu zaidi miongoni mwao.
 
Katika juhudi za kuboresha na kupanua huduma za kidigitali nchini, Tigo ilikuwa mojawapo ya kampuni za mawasiliano za kwanza kabisa kuwekeza katika teknolojia ya 3G na  4G ambapo Tigo ndio kampuni pekee yenye mtandao mpana zaidi wa 4G nchini. Tigo pia ilikuwa ya kwanza kuzindua simu janja yenye lugha ya Kiswahili pamoja na huduma ya Facebook kwa lugha ya Kiswahili iliyoongeza matumizi ya huduma za kidigitali kwa idadi kubwa ya Watanzania wanaotumia lugha ya Kiswahili kwa mawasiliano yao ya kila siku.

MHADHIRI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM DK.MISANYA BINGI AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MUHIMBILI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

NI pigo!Ndivyo unavyoweza kuelezea taarifa za kufariki dunia kwa Mhadhiri wa  Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM),Dk.Misanya Dismas Bingi.

Dk.Misanya ambaye pia amewahi kuwa mtangazaji maarufu nchini  wa Radio One na ITV amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuz Blog Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbii Aminiel Aligaeshi amesema Dk.Misanya amefia MOI ila mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti Muhimbili.

 Dk.Misanya Bingi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.Alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili  baada ya kupata ugonjwa wa kupooza(stroke) na kupelekwa katika chumba cha Uangalizi maalum (ICU).

Kwa sasa msiba upo eneo la Makongo Juu jijini Dar es Salaam wakati taratibu nyingine zikiendelea.Michuzi Blog itaendelea kukujuza kila kinachoendelea kuhusu msiba huo.

Pia Michuzi Blog inaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki kutokana na msiba huo mzito wa kuondokewa na mendwa wao Dk.Misanya Bingi.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN.

WAZAZI WATAKIWA KUONDOKANA NA DHANA POTOFU.

$
0
0

Na Frankius Cleophace Tarime.

Wazazi na walezi Wilayani Serengeti mkoani Mara wametakiwa kuondokana na dhama potofu kwa kupotosha jamii pale seriklai inapopeleka huduma ya afya huku wakitakiwa kukujenga tabia za kupima afya zao mara kwa mara bila kusahua watoto wa kike ili kuondona na vifo vya ghafla ambavyo vimekuwa vikijitokeza.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara Mchungaji Abel Obura kipindi akifunga tamasha la kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia ukiwemo Ukeketaji lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY nakufanyika katika Shule ya Msingi Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara.

Mchungaji amesema kuwa jamii imekuwa ikipotoshwa pale serikali inapopeleka madawa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya za watoto nakusababisha baadhi ya watoto wengine kokosa huduma hiyo.“Serikali inaleta dawa za minyoo lakini jamii inapotoshwa kuwa wakimeza dawa hizo hawatazaa jambo ambalo siyo kweli na serikali inaleta dawa ambazo tayari zimethibitishwa hivyo sasa jamii iondokane na dhana potofu” alisema Mchungaji.

Pia Mchungjai amewataka wazazi na walezi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwapima watoto wao kwani ni haki zao za msingi ikiwemo kupatiwa pia elimu ya msingi mpaka sekondari.

Kwa upande wake Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirika la RIGH TO PLAY ambao wanatoa elimu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia kupitia matamasha ambayo yanahusisha michezo mbalimbali yakiwemo maigizo, Nyimbo, Ngoma, Mpira wa miguu kwa wasichana, kuvuta kamba na Mashariri, michezo hiyo imebeba ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia.

“Michezo inakusanya watu wengi hivyo sisi kama shirika tumeamua kutumia michezo kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa katika jamii ya Mkoa wa Mara ili kulinda na kutetea haki za watoto ikiwemo kupata elimu” alisema Leah.

Aidha wananchi na wakazi wa kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti mkoni Mara wanazidi kupongeza uwepo wa matamasha hayo ya kutoa elimu katika jamii huku wasema kuwa suala la ukeketaji linazidi kupungua kila kukicha bali elimu ienndelee kutolewa katika jamii ili kuondoa usiri uliopo kwa sasa.

“Baada ya serikali kutilia mkazo suala la kupinga ukeketaji kuna usiri mkubwa unafanyia sasa elimi izidi kutolewa katika maeneo ya vijijini” walisema Wananachi hao.
Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkiani Mara Mchungaji Abel Obura akifunga tamasha hilo la kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji lililoandaliwa na shirika la RIGTH TO PLAY.
anaume wakivutana kwa kamba katika tamasha hilo.

Wanawake wakivutana kwa kamba katika tamasha hilo lengo ni kufikisha ujumbe ulikusudiwa.

Vijana wa kijiji cha Maburi wakitoa igizo lenye fundisho jinsi wazee wanavyooa watoto wadogo na kushindwa kutimiza ndoto zao za kielimu.

Watoto wakikimbia katika magunia kwenye tamasha hilo.
Leah Kimaroambaye ni mwezeshaji kutika Shirika la RIGHT TO PLAY akitoa Elimu ya kupinga Ukatili katika jamii kwenye tamamsha liloandaliwa na shirika hilo na kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Maburi kata ya Nyambureti wilayani Serengeti Mkoani Mara.
mgeni rasmi ambaye ni Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara, Mchungaji Abel Obura akisalimiana na wachezaji baina ya timu ya Nyambureti Sekondari FC na Kerukerege FC.

MABONDIA 18 LEO KUONESHA UMWAMBA KATIKA ULINGO WA CCM MWINJUMA DAR

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


MABONDIA 18 leo wanatarajia kupanda ulingoni katika ukumbi wa ulingo wa CCM Mwinjuma uliopo Mwananyamala kuwania mataji mbalimbali katika mchezo wa ngumi likiongozwa na pambano la raundi 10 kati ya Bushiri Kulwa na Seba.

Mapambano hyao yaliyoandaliwa na Kampuni ya ‘Golden Boy Africa’ yanawakutaniosha mabondia hao wanaowania mkanda wa Dunia katika uzito wa kilo 84 ‘Cruiser weights’ linatajwa kuwa la kipekee na hasa kutokanana na viwango walivyonavyo mabondia wote wawili katika medani ya ‘masumbwi’

Mbali na pambano hilo ,.michezo mingine inatarajiwa kuwakutanisha mabondia Simba na Allen, Chidi Mbishi dhidi ya Moro Best,Mkalekwa Junior dhidi ya Abdala Luwanje, Hamisi Maya dhidi ya Karage Suba itakayochezwa kwa raundi nane kila mmoja.

Mapambano mengine ambayo ni pamoja na bondia Mbunju Laga dhidi ya Iman Tavez, Nurdin Mohammed dhidi ya Issa Mbwana , Mlekwa dhidi ya Rama, pamoja na pambano kati ya Modest John dhidi ya Kassim Juma, yote yakichezwa kwa raundi 6.

Mratibu wa mapambano hayo Shomari Kimbau, alisema tayari maandalizi yote yamekwisha fanyika ikiwemo mabondia kupima afya zao kabla ya mchezo na kwamba kinachosubiriwa na kutimia kwa muda husika.

Alisema ‘mpambano’ huo unaotarajiwa kuanza saa 10 za jioni, unatarajiwa kuwa wa kuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mabondia wote, hasa kutokana na namna ambavyo kila kambi ya mabondia hao iolivyojipanga ili kupata ushindi.

Awataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia vipaji kutoka kwa mabondia mbalimbali wa hapa nchinim huku akisisitiza uwepo wa suala la ulinzi na usalama kwa mashabiki watakaojitokeza kutazama pambano hilo.

DAWASA WAANZA KUDHIBITI UVUJAJI WA MAJI TABATA

$
0
0
* Yazindua siku tatu za kumaliza tatizo la uvujaji maji katika kata 11.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamezindua uzibaji wa mivujo ya mabomba inayomwaga maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wakianzia katika maeneo ya Tabata zoezi litakalodumu kwa muda wa siku tatu ikiwa ni katika kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya siku 100. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhaandisi Aron Joseph alipozindua mkakati huo wa kuhakikisha maeneo yote yanayotiririsha maji kutoka kwenye miundo mbinu ya Dawasa yanafanyiwa kazi kwa asilimia 90 na kisha kukabidhi kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata. 

Akielezea zoezi hilo lilioanza leo, Aron amesema kuwa watatembelea maeneo yote ya Tabata yenye kata 11 zinazopata huduma za maji na kupambana na mivujo na tayari wataalamu wameshaingia kazini kwa ajili ya kuyafanyia kazi. 

"Kuna timu zaidi ya watu 70 katika maeneo 20 tofauti ndani ya Tabata ambapo kuna kata 11 yenye maji na watalaamu hao wote wapo kuhakikisha mivujo yote inayojulikana na ile mipya wanafanyia marekebisho maeneo hayo yamefanyiwa kazi ndani ya siku tatu na iwe imeondoka,"amesema Aron. 

Amesema nia na madhumuni ya kufanya zoezi hili ni kuhakikisha eneo lote la Tabata lenye maeneo sugu na mapya yanayovuja kupatiwa ufumbuzi na iwe imeondoka kabisa na katika hilo na wamemtaka Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata kuhakikisha inapotokea mivujo anatakiwa kuidhibiti na kuziba ndani ya masaa 6. 

Aron amesema kuwa anatambua kuna baadhi ya maeneo ya Tabata na sehemu zingine miundo mbinu yake ni chakavu na hilo suala linajulikana, kama Dawasa mpya wameweka mikakati ya kuhakikisha ndani ya miaka mitatu miundo mbinu hiyo inabadilishwa na ili wananchi wasikose maji idara ya uzalishaji na usambazaji maji utahakikisha katika kipindi chote hicho watakuwa wanasimamia miundo mbinu hiyo ili kuondokana na uvujaji wa maji. 

Akiongezea, Aron amewasihi wananchi kutoa taarifa kwa Mamlaka husika pindi wanapoona maji yanavuja kupitia namba yao ambayo haina malipo pia hata watakapowaona mafundi wa Dawasa wawape taarifa ili wakarekebishe eneo hilo. 

Meneja wa Usambazaji maji Mhandisi Paschael Fumbuka amesema zoezi hili ni kwa ajili ya kuhakikisha wanaboresha miundo mbinu ya maji kwa kuzuia upotevu wa maji kitu ambacho kinaathiri biashara ya maji maana kila tone la maji linahesabiwa. Fumbuka ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Dawasa kuwabaini watu wanaochafua miundo mbinu yao ikiwamo kutiririsha maji taka na hatua za kisheria zitachukuliwa juu yao. 

Dawasa wameanza kutekeleza moja ya mikakati yao siku 100 ya kumaliza miradi mbalimbali na changamoto ikiwemo uvujaji wa maji kutoka katika miundo mbinu yao. 
Baadhi ya mafundi waliokatika maeneo mbalimbali ya Tabata wakiziba uvujaji wa maji baada ya kuzinduliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) utakaofanyika kwa muda wa siku tatu.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Aron Joseph akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika baadhi ya maeneo yanayofanyiwa ukarabati wa uzibaji wa mabomba uliozinduliwa na utachukua siku tatu kukamilisha eneo la Tabata.

MAADHIMISHO YA SABA YA SIKU YA MARA (MARA DAY) YAFANYIKA NCHINI KENYA

$
0
0


Maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mara (Mara Day)

Bonde la mto Mara linalounganisha Tanzania na Kenya linashikilia uhai sio wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pekee, bali uhai wa nchi za Sudan, Ethiopia na Misri nazo kwa kiasi kikubwa unategemea bonde hilo.

Kauli hiyo ilitolewa na viongozi mbalimbali walioshiriki sherehe za maadhimisho ya saba ya Siku ya Mara (Mara Day) zilizofanyika katika Kaunti ya Narok, Kenya siku ya Jumamosi tarehe 15 Septemba 2018. Maadhimisho ya Siku ya Mara ambayo kwa mwaka huu yalikuwa na kaulimbiu "Mto Mara unatuunganisha wote" hufanyika kwa kupokezana kati ya Tanzania na Kenya kila mwaka tarehe 15 Septemba kwa madhumuni ya kuhamasisha matumizi endelevu ya bonde la mto Mara.

“Siku ya Mara hailengi chochote, isipokuwa kutukumbusha jukumu letu la kutunza mazingira”, Gavana wa kaunti ya Narok, Mhe Samuel Oletunai alisema katika maadhimisho hayo.Mhe. Samuel Oletunai aliwaasa Wakenya kutunza msitu wa Mau ambao ndio chanzo kikuu cha maji yanayotiririka mto Mara na kuiomba Serikali ya Kenya kuhakikisha kuwa mgogoro katika msitu huo unapatiwa ufumbuzi haraka. 

Mwakilishi wa Serikali ya Tanzania katika maadhimisho hayo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso (Mb) alieleza kuwa maji hayana mbadala kama chakula ambapo ukikosa wali utakula ugali, hivyo aliwahakikishia wadau waliohudhuria sherehe hizo kuwa Serikali ya Tanzania haitakuwa kikwazo cha harakati za kuhifadhi ikolojia ya mto Mara.

Utunzaji wa ikolojia ya mto huo ilielezwa kuwa ni muhimu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo utalii na shughuli nyingine za kiuchumi ambapo Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) katika sherehe hizo alisema kuwa Tanzania na Kenya zinapata zaidi ya Dola milioni 300 kwa mwaka kutokana na shughuli za kiuchumi katika mto Mara.Tukio kubwa linalovutia watalii wengi duniani ni uhamaji wa wanyamapori aina ya nyumbu zaidi ya milioni 1.2 baina ya mbuga ya Serengeti nchini Tanzania na Masai Mara nchini Kenya katika kipindi cha Julai hadi Oktoba ambapo mara zote wanyama hao hukatiza mto Mara.

Mwakilishi huyo wa USAID alitaja sababu zinazoharibu ikolojia ya mto huo kuwa ni pamoja na uharibifu wa misitu, matumizi makubwa ya maji, ujenzi wa miundombinu mbalimbali na mmomonyoko wa udongo. Hivyo, aliahidi kuwa USAID itaendelea kushirikiana na wadau kukabiliana na changamoto hizo kwa kusaidia miradi ya maji na utunzaji wa mazingira. Alisema mto huo lazima uhifadhiwe kwa sababu ni mali ya watu waliopita, wasasa na wajao.

Waziri wa Maji na Usafi wa Kenya ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizo, Mhe. Simon Chelugui aliwahakikishia waliohudhuria maadhimisho hayo kuwa Serikali ya Kenya imejizatiti kulinda na kuhifadhi ikolokia ya mto Mara kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo. Hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Kenya, alizitaja kuwa ni pamoja na kuanzisha miradi ya maji na usafi katika mashule na aliutaja mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika kwenye mpaka wa Isebania ambao utawanufaisha pia Watanzania wanaoishi maeneo ya Sirari.

Sherehe hizo zilipambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo maonesho ya bidhaa na huduma ambao uzalishaji wake unazingatia uhifadhi wa mazingira.Aidha, kulikuwa na burudani za ngoma, michezo ya mpira wa miguu mashairi, tunzo na ngojera ambazo zote zililenga kutoa ujumbe wa kuhimiza utunzaji wa mazingira. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Narok, kenya
16 Septemba 2018 
Waziri wa Maji na Usafi wa Kenya, Mhe. Simon Chelugui ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya saba ya Siku ya Mara akitoa hotuba ya ufunguzi ambayo ilielezea mikakati mbalimbali inayochukuliwa ili kukabiliana na vihatarishi vya kutokomeza ikolojia ya Mto Mara. 
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Mara yaliyofanyika kaunti ya Narok nchini Kenya
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Pindi Chana akitoa salamu katika maadhimisho ya Siku ya Mara. 
Gavana wa akaunti ya Narok, Mhe. Samuel Oletunai akihutubia watu mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Mara ambayo yalifanyika katika kaunti yake ya Narok. 
Watu mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Mara wakifuatilia hotuba za viongozi. 
Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) akivalishwa vazi la kimasai kabla hajatoa hotuba yake katika maadhimisho hayo. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Bibi Caroline Mthapula ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akitoa neno la mkoa katika maadhimisho hayo. 
Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana; Katibu Tawala wa mkoa wa Mara, Bibi Caroline Mthapula; Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso; Waziri wa Maji na Usafi wa Kenya, Mhe. Simon Chelugui wakipata maelezo kutoka moja ya banda la maonesho ya Siku ya Mara kuhusu utunzaji wa mazingira. 
Mstari wa kulia kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana; Katibu Tawala wa mkoa wa Mara, Bibi Caroline Mthapula; Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso; Waziri wa Maji na Usafi wa Kenya, Mhe. Simon Chelugui wakipata maelezo kutoka mmoja wa washiriki wa maonesho ya siku ya Mara namna anavyoshiriki katika shughuli za kutunza mazingira. 
Kaimu Murugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii, Bw. Eliabi Chodota akiteta jambo na Katibu Tawala wa mkoa wa Mara, Bibi Caroline Mthapula. 
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria maadhimisho ya saba ya Siku ya Mara wakisikiliza hotuba za viongozi. 
Burudani kutoka kwa wanafunzi wakihimiza umuhimu wa kutunza mazingira. 
Mmoja wa wanaharakati wa kutunza Mazingira akipokea cheti cha kutambua mchango wake kutoka kwa Gavana wa kaunti ya Narok, Mhe. Samuel Oletunai. katikati ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Dkt. Ally Said Matano.

WAZIRI LUKUVI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI YA MIKOA NANE KWA WIKI MBILI

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akicheza na Wakazi wa kijiji cha Lolkisale Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipotembelea na kutatua mgogoro mkubwa wa wakazi wa maeneo hayo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisoma mabango ya Wakazi wa kijiji cha Nafco Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipotembelea na kutatua migogoro mikubwa ya wakazi wa maeneo hayo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akivishwa mavazi ya heshima ya kimasai na Wakazi wa kijiji cha Eng’arooji Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipofika kuwatatulia mgogoro wa ardhi uliokuwa umewagawa wananchi hao katika makundi mawili ambapo Waziri Lukuvi aliweza kutatua mgogoro huo.


 Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anataraji kufanya ziara ya kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi katika mikoa nane ya Tanzania bara katika wiki mbili kuanzia tarehe 17 hadi 30 Septemba 2018.

Ziara hii ni katika utekelezaji wa kampeni yake ya “Funguka kwa Waziri wa Ardhi” ambayo aliizindua rasmi mwezi Januari mwaka 2018 yenye lengo la kuzunguka nchi nzima kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi papo hapo.

Katika wiki mbili hizi za kutatua migogoro ya ardhi katika mikoa nane waziri Lukuvi ameeleza kuwa kuanzia tarehe 17 hadi 19 atakuwa katika mkoa wa Mara katika wilaya ya Bunda, Musoma na Tarime na baadae tarehe 20 hadi 30 atakuwa katika mikoa ya Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Njombe, Iringa na Morogoro.

“Nipo njiani kuelekea mkoa wa Mara ambapo siku ya jumatatu tarehe 17 Septemba ntaanzia wilayani Bunda ili kutatua mgogoro wa Bibi Nyasasi Masike na kukagua kiwanja chake kama nilivyomuahidi Mheshimiwa Rais wakati alipofanya ziara yake wilayani Bunda na kunipigia simu moja kwa moja” Amesema Waziri Lukuvi.

Akaongeza Waziri Lukuvi, “nimeagizwa na Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano hii hadi kufikia 2020 migogoro ya ardhi iwe imepungua kwa kiasi kikubwa kama sio kuisha na kazi hii ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, na ninawaagiza viongozi wajitokeze kuwasikiliza na kutafutia ufumbuzi kero za wananchi wanyonge ambazo zimekuwa zikiwatesa kwa muda mrefu”

Aidha, ameongeza kuwa siku hiyo hiyo atasikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu sekta ya ardhi na kuzitafutia ufumbuzi katika mkutano wa hadhara uliyopo ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Ameongeza kuwa baadae ataelekea wilaya ya Musoma na Tarime ambapo atasikiliza na kutatua kero za wananchi zinazohusu migogoro ya ardhi papo hapo pamoja na kusikiliza na kutatua kero ya ardhi ya Bibi Ghati Mwita Bukura na kuona eneo lake.Baada ya ziara ya mkoa huo Waziri Lukuvi ataelekea mkoani Tabora na mkoani Katavi kutatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa mikoa hiyo na kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi kwa kufanya mikutano ya hadhara na wananchi kwa kutumia Kauli Mbiu ya Funguka kwa Waziri wa Ardhi na baadae kuelekea mkoani Rukwa.

Waziri Lukuvi katika Mkoa wa Rukwa anataraji kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa ardhi wa Shamba la Malonje lililo na mgogoro wa muda mrefu pamoja na kusikiliza migogoro ya ardhi na baadae kuwasili mkoani Songwe wilayani Tunduma ambapo atakagua na kusikilisa changamoto za mpaka wa Tanzania na Zambia.

Ziara hiyo itaendelea katika mikoa ya Njombe na Iringa kutatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa mikoa hiyo na kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi kwa kufanya mikutano ya hadhara na wananchi kwa kutumia Kauli Mbiu ya Funguka kwa Waziri wa Ardhi na baadae kumalizikia katika mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mgogoro wa eneo la Mabwegere

Waziri Lukuvi katika mwezi huu wa Septemba ameweza kutatua migogoro mikubwa katika mikoa ya Dar es salaam na Arusha katika nyakati tofauti, miongoni mwa migogoro hiyo ni ule wa mwekezaji wa kiwanda cha Minjingu na wananchi wa Pugu Stesheni jijini Dar es salaam ambao ameupatia ufumbuzi na wananchi wamefurahi kwa uamuzi wake.

Mgogoro mwingine alioupatia ufumbuzi ni ule wa eneo la msitu wa Kazimzumbwi ambao ulivamiwa na wananchi ambao walishindwa katika kesi na Waziri Lukuvi akatoa siku 30 ili kuwasaidia wananchi hao. Aidha mgogoro mwingine uliopatiwa ufumbuzi na Waziri Lukuvi akishirikiana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi ni ule wa eneo la Pugu Mnadani ambalo pia wananchi wamevamia na limepatiwa ufumbuzi tayari.

Katika Mkoa wa Arusha Waziri Lukuvi ametembelea na kutatua migogoro mikubwa ya wakazi wa Wilaya ya Monduli katika vijiji vya Lolkisale, kijiji cha Lemooti, kijiji cha Eng’arooji, na Kijiji cha Nafco nyingine ni kata ya Sepeko, kata ya Mfereji iliyo na mgogoro kati ya Wilaya za Monduli na Arumeru ambapo ametatua kwa ufanisi mkubwa jambo ambalo limewafanya wakazi wa maeneo hayo kummwagia sifa na kumuombea kwa Mungu ampe umri mrefu wenye mafanikio.

Wizara inaendelea na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi kwa kufanya mikutano na wananchi kwa kutumia Kauli Mbiu ya Funguka kwa Waziri wa Ardhi. Katika mikutano hiyo hadi sasa jumla ya malalamiko 4,168 yameshapokelewa na Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri mbalimbali na imepatiwa ufumbuzi na mingine inaendelea kuchambuliwa ili kupatiwa ufumbuzi.

Ratiba ya RC Hapi katika tarafa mbalimbali wilaya ya Iringa mjini

TIMU YA MAANGAIKO YATWAA UBINGWA WA KOMBO LA MABODI CUP

$
0
0

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi (kushoto) akimkabidhi Kombe la ushindi nahodha wa Timu ya Maangaiko ndugu Mkongea Mohamed Hamada (kulia) mara baada ya timu hiyo kushinda wa penalti 4-2 dhidi ya timu ya Ubina katika Fainali ya Ligi ya Mabodi CUP iliyochezwa Kajengwa Makunduchi Unguja.


TIMU za Ubina na Maangaiko zikichuana katika Uwanja wa Uhuru uliopo Kajengwa Makunduchi katika mechi ya fainali ya ligi ya Mabodi CUF.



WANANCHI wa vijiji mbali mbali vya Jimbo la Makunduchi walioudhuria katika mechi ya Fainali za kombe la Mabodi CUP wakishuhudia utoaji wa zawadi mbali mbali kwa timu zilizoshiriki mashindano hayo.




NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla (Mabodi) amewataka vijana kuchangamkia fursa za ajira zilizopo katika sekta ya michezo nchini.

Rai hiyo ameitoa wakati akifunga fainali ya Mechi za ligi ya Mabodi Cup iliyochezwa katika uwanja wa Uhuru uliopo Kajengwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.Dk.Mabodi amesema CCM inaendelea kusimamia ipasavyo Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika kuimarisha sekta ya michezo kwa kujenga Viwanja vya kisasa na Vifaa vya kisasa vya michezo.

Akizungumzia historia fupi ya ligi hiyo kuwa imeasisiwa na Marehemu Juma Abdulla Saadalla Mabodi kwa lengo la kudumisha mshikamano kwa wananchi wote wa Vijiji vya Makunduchi.Amesema ni muhimu kwa wananchi hao hasa vijana kuthamini na kuendeleza tunu za maendeleo zilizoasisiwa na Wazee wa vijiji vya Jimbo la Makunduchi kwa sababu jitihada zao haziwezi kulipwa ila zithaminiwezi kuwarithisha vijana.

“Endelezeni ligi hii iwe miongoni mwa chachu za kuleta Umoja na Mshikamano na isiwe chanzo cha mifarakano kwani aliyeasisi ligi hii hakuwa na nia mbaya bali alitaka kuimarisha Muungamo wa wanavijiji wanaoshi ndani na nje ya makunduchi.Pia Sekta ya Michezo inaimarika kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020, chini ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya saba inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.”, alisema Dk.Mabodi.

Alisema Jimbo la Makunduchi limekuwa ni kitovu cha kuenzi utamaduni wa asili ulioasisiwa na wazee wa vijiji vilivyomo katika Jimbo hilo hatua inayotakiwa kuendelezwa kwa vitendo na vijana wa sasa.“Wazee wetu wametuachia vitu muhimu vya asili tunavyotakiwa kuvienzi kwa mfano ligi hii ya Mabodi Cup, Hasnuu Makame CUP, Sherehe za Mwaka kogwa pamoja na tamasha la vyakula vya asili linalowaunganisha wananchi wa Makunduchi na vijiji jirani.” alisema.

Aidha aliwasihi wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuunga mkono juhudi za maendeo yanayoletwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya usimamizi mzuri wa CCM.Dk.Mabodi alisikishwa na kukemea vikali kuibuka kwa utashi binafsi wa kuigawa ligi hiyo katika makundi mawili na kuagiza ligi hiyo iwe na jina moja la Mabodi CUP lenye uongozi mmoja na ligi nyingine yoyote itakayoibuka itafutiwe jina jingine mbadala kwa ajili ya kuimarisha ushindani wa kimichezo.

Dk. Dk.Mabodi aliahidi kushiriki kikamilifu katika kuendeleza ligi hiyo iweze kutoa wachezaji wenye vipaji vya kucheza katika timu kubwa za kitaifa na kimataifa.Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini Unguja anayekaimu Wilaya Kusini Unguja Rajab Ali Rajab alisema michezo ni sekta muhimu inayodumisha urafiki na afya za vijana.Akizungumza Mgeni mwalikwa ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Mkoa wa Kilimanjaro Haji Miraj Abdallah alisema michezo ni sehemu muhimu ya kuwaunganisha vijana wa vikundi mbali mbali kuwa wamoja katika kulinda maslahi ya nchi.

SSP Haji aliwashauri vijana hao kujiepusha na vikundi viovu badala yake watumie vizuri vipaji vyao kupitia michezo kwa kujiajiri wenyewe.Awali mechi hiyo ya fainali katika ligi ya Mabodi CUP 2017-2018 ilizikutanisha timu mbili za Ubina na Maangaiko ambazo zote zilionyesha ujuzi wa soka na kumaliza mechi wakiwa wametoka sare ya 1-1.

Baada ya matokeo hayo mechi hiyo ilienda katika hatua ya penalti ambapo timu ya Maangaiko ilishinda kwa goli 4-2 dhidi ya timu ya Ubina.Kupitia michuano hiyo Timu ya Maangaiko ambayo ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo walipata zawadi ya Shilingi milioni moja na kikombe cha mshindi wa kwanza na timu ya Ubina imepata shilingi 500,000 pamoja na kikombe cha mshindi wa pili.Pia mshindi wa tatu alipata shilingi 300,000 mshindi wa nne amepata shilingi 200,000 ambapo timu nne zilizoshiriki mashindano hayo kila timu imepewa kiasi cha shilingi 75,000.

Katika fainali hiyo pia ilipambwa na michezi mingine ikiwemo ya kuvuta kamba pamoja na mbio za magunia ambapo kila mshindi wa kwanza katika timu za michezo hiyo amezawadiwa kiasi cha shilingi 50,000.

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WAKABIDHIWA KUKU MKURANGA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

MWENYEKITI  wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga mkoani Pwani Mariam Ulega amekabidhi msaada wa kuku 4000 ambao watatolewa kwa wanawake wajasiriamali 400 ambao wamehudhuria mafunzo ya ujasiriamali.

 Akizungumza wakati akikabidhi kuku hao kwa wajasirimali ,amesema kuwa kwa hicho kidogo wakitumie katika kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla na amewataka wawe na ushirikiano ili wafiikie malengo yao.

Kwa upande wa baadhi ya akina mama hao wameshukuru kwa  kupewa msaada huo na kuahidi kuwatunza kuku hao na kueleza kuwa kuku hao watakuwa chanzo cha miradi mikubwa zaidi
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza na wanajasiriamali kuhusu kuwatunza kuku waliopewa ili kujiongezea kipato.
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga,Mariam  Ulega  akiwakangua kuku kabla ya kuwakabidh wananchi walilaya hiyo kwajili ya kufunga iliwaweze kujikwamua kiuchumi.
 Mwenyekiti wa jukwaa la la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam  Ulega akiwakabidhi wananchi kuku 3000 kwajili ya kufunga iliwaweze kujikwamua kiuchumi nakuongeza pato la Taifa. ambapo kila mwananchi alipewa kuku10 (picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Wananchi wa wilaya ya Mkuranga wakiwa katika foleni ya kupokea kuku ambapo kila mwananchi alipewa kuku 10 kwajili ya kwenda kufunga.


 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akisalimiana na wanawake wajasiriamali
Wajasiriamali wakiwa na makasha waliyo bebea kuku.

CEO MHANDISI LUHEMEJA NA SIKU 100 NDANI YA DAWASA MPYA

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa utambulisho wake kwa Menejimenti mpya iliyozinduliwa Septemba 09 Mwaka huu.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
HII KAZI ITAFANYIKA: Hiyo ni kauli ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa utambulisho wake baada ya kuteuliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka hiyo.

DAWASA mpya, iliundwa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutoa kauli na kutaka DAWASCO na DAWASA ziwe kitu kimoja, agizo ambalo Wizara ya Maji na Umwagiliaji kama wasimamizi wa mamlaka hiyo kuunda DAWASA mpya itakayokuwa na bodi ya wakurugenzi moja.

Uteuzi wa kwanza wa Rais Dkt Magufuli ni wa Mwenyekiti wa Bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na baadae kuteuliwa kwa bodi ya wakurugenzi iliyoundwa na wataalamu mbalimbali wa maji.

“Nimshukuru sana Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kwa uteuzi wake, ameniamini sana kwa kunipa majukumu haya makubwa kuongoza mkoa wa Dar es Saalaam na Pwani,” alianza kwa kusema.

Alisema, Mabadiliko haya ni mabadiliko ya kihistoria, kwa kuona hatua nyingine inapigwa kwa kutatua tatizo la umaskini, malazi na ujinga. Stadi mbalimbali zinaonesha huduma za maji zikiboreshwa kwa asilimia moja uchumi wa nchi huongezeka kwa asilimia nne na huduma zikizorota kwa asilimia moja uchumi hupungua kwa asilimia nne.

Ni kwelil; Kuna changamoto zinazowakabili DAWASA katika suala la upatikanaji wa maji pembezoni mwa mji, Kwa Mkoa wa Dar es Salaam ifikapo mwaka 2030 utakuwa ni moja ya majiji makubwa barani Afrika na ongezeko la watu litakuwa ni Milioni 11 na makadirio ya maji kwa siku yatakuwa ni n Lita Milioni Moja na Laki Moja (110,000).

Mhandisi Luhemeja ameweka mikakati mbalimbali ya DAWASA  baada ya kukabidhiwa dhamana ya kuiongoza Mamlaka hiyo na hatua ya kwanza ni kuhakikisha miradi iliyokuwa inasuasua inamalizika kwa wakati tena ndani ya siku 100.

Siku 100 za Mhandisi  Luhemeja ndani ya DAWASA, mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo ameweza kumuahidi ndani ya siku 100 miradi ya maji iliyokuwa inasuasua na mingine kutokumalizika kwa wakati imepata dawa nayo ni uongozi mpya wa DAWASA.

Mhandisi Luhemeja ameweka wazi , Mradi wa Chalinze tayari wakandarasi wa mradi huo wameshaitwa kujieleza kwenye bodi ,waeleze kwanini mradi huo umekuwa unasuasua kwa kipindi chote na kama tayari wameshatekeleza yale waliyoaizwa na Profesa Mbarawa.

Mradi wa pili ni wa usambazaji maji katika maeneo ya Goba, Salasala, Bunju, Bagamoyo na Kiluvya na mardi huu unatakiwa kukamilika mwisho wa mwezi Oktoba, huku mradi mwingine ukiwa ni Ruvu Juu na Rais Dkt Magufuli aliahidi mradi huo utapeleka maji maeneo ya Kisarawe na tayari serikali imeshalipia malipo ya awali na wapo katika mikakati ya kukamilisha Milioni  700 ili usambazaji huo uanze mara moja.

Mita za malipo ya awali (Prepaid Meter) zilizozinduliwa na Waziri Mbarawa, Mhandisi Luhemeja amesema Kuna changamoto kubwa sana ya madeni  na ndani ya siku 100 za DAWASA mpya atahakikisha mita hizo ambazo tayari zimeshaanza kufungwa kufanyika kwa zoezi hilo kwa taasisi zote kubwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam. Mita hizi zitaweza kusaidia wizi wa maji unaofanyika na kusababisha hasara kubwa kwa Mamlaka.

Wakati wa uzinduzi wa mita hizi, Profesa Mbarawa aliweka wazi mkakati wa kukomesha wadaiwa sugu ambapo mtumiaji wa maji atatakiwa kulipia maji kabla ya matumizi na hela yake ikimalizika maji nayo yatakatika na pia itasaidia katika kupunguza madeni kwani pindi anapokuja kununua maji atalazimika kulipa kiasi Fulani cha deni.

Mita hizo tayari zimeshafungwa kwenye baadhu ya maeneo ikiwemo viwanda na wateja wa kubwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam na Profesa Mbarawa aliagiza hilo zoezi liende kwa kasi sana, na baada ya uteuzi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA mpya ameahidi ndani ya siku 100 wateja wote wakubwa watakuwa wameshafumgiwa mita hizo za malipo ya kabla.

Muelekeo wa DAWASA mpya,Mhandisi Luhemeja amesema kwa sasa wana mikakati ya kupeleka maji Dar es Salaam ya Kusini na ameshakabidhi maradi wa maji wa Kiwalani  utaaokuwa na dizaini ya kusambaza maji katika maeneo ya Kitunda, Yombo, Mwanagati, Gongo la Mboto.

Kumekuwepo na malalamiko kuhusu mardi wa Kimbiji na Mpera, utakaozalisha maji Lita Milioni 260 kwa siku ulio chini ya Kampuni ya Serengeti ksuhindwa kukamilika kwa wakati Visima vya maji vikiwa tayari vimeshachimbwa kwa asilimia kubwa,  Mhandisi Luhemeja ameahidi kupitia upya usanifu wa Matanki yatakayotumika kuweka maji yanayotoka kwenye visima hivyo  na matanki hayo ni ya Gongo la Mboto, Chanika, Luanda na Pugu. Luhemeja amesema kuna wahandisi 12 wenye leseni na mihuri na kwa pamoja  Kamati ya wahandisi kwa pamoja wataanza kujenga matanki hayo kwa uwezo wa ndani.

Kukamilika kwa matanki hayo kutasaidia  upatikanaji wa maji katika maeneo ya Chamazi, Kitunda, Pugu, Ukonga, Kinyerezi na Uwanja wa Ndege. Mradi wa Kimbiji Mpera umekamilika ila umekuwa hauendelezwi ila mpaka kufikia Desemba 9 mwaka huu utakuwa umefikia hatua za mwisho.

Desemba 9 2018 DAWASA mpya inaazimia kutangaza Uhuru wa Maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam , Mhandisi Luhemeja amesema kuwa siku ya uhuru maji miradi mingi itakuwa imekamilika na itakabidhiwa kwa Katibu Mkuu Profes Mkumbo ikiwemo na kukabidhi ripoti ya  mradi wa Benki ya Dunia wa Km 1426 ambao unatarajiwa ifikapo Septemba 15 mkandarasi atakuwa eneo la ujenzi.
Maji Taka, Mhandisi Luhemeja amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya huduma za maji taka toka kwa Mamlaka kutoka na uwekezzaji wake kuwa mkubwa ila tayari wameshapana bajeti kwa kutumia uwezo wa ndani kuwa ifikapo Desemba 9  wawe wanamiliki malori 20 ya kutoa huduma za maji taka nkwa wananchi, ila ameainisha changamoto nyingine katika mradi huo ni wamiliki binafsi kujipangia bei na zimekuwa kubwa sana na kuja kwa malori hayo kutasaidia kutoa huduma kwa watanzania kupata huduma kwa bei nafuu.

Ukarabati wa mabwawa, Mhandisi Luhemeja ameweka wazi mkakati wa DAWASA mpya kukarabati mabwawa yote ya maji taka yaliyoharibika na kutengenezwa yaliyopo maeneo ya Mikocheni, Mabibo, Airwing na Buguruni kwa ajili ya kuanza kupokea makazi malori kutoka makazi ya watu.

Akielezea changamoto ya upotevu wa maji, Mhandisi Luhemeja amesema DAWASA mpya imeacha yale yote yaliyofanywa na DAWASCO, upotevu wa maji umebaki historia, na kwa sasa watahakikisha wanapunguza upotevu mkubwa wa maji  na wametenga asilimia 35 ya mapato ya ndani ya kila mwezi kwa ajili ya upanuzi wa mtandao wa usafirishaji maji.

“Mtandao mdogo wa maji umekuwa unaleta changamoto kubwa katika upotevu wa maji, maji ni mengi yanapokuja kwa wingi yanasababisha kupasuka kwa mabomba na yanapelekea kupotea kwa maji na mapato yatakayotengwa yatasaidia kulaza mabomba na kutatengwa akaunti maalumu kwa ajili ya kuingiza makusanyo hayo ,” amesema Mhandisi Luhemeja.

Tatizo lingine la upotevu wa maji unatokana na mita za maji, kuna  mita elfu sitini na nane (68,000) kwa ajili ya kuwafungia wananchi  na ili kuhakikisha upotevu wa maji unaondoka, Pia Mhandisi Luhemeja amewaonya wezi wote wa maji kuwa tayari DAWASA mpya imeshasharikiana na kitengo cha Polisi  na kuwataka wananchi kushirikiana na Polisi kuwabaini wezi wa maji ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.

Ongezeko la Mapato ndani ya DAWASA mpya, Mikakati iliyopo ni pamoja na kuhakikisha mapato ya ndani yanaongezeka kutoka Bilioni 9.3 mwezi Agosti na kufikia Bilioni 12 na hili litafanikiwa kwa kudhiditi upotevu wa maji kwa asilimia 35 kufikia Desemba ikiwa ni ndani ya siku 100.

Hali ya watumishi ndani ya DAWASA mpya, Mhandisi Luhemeja ameweka wazi kuwa kunzia mwezi ujao mishahara ya wafanyakazi itakuwa na maslahi mazuri yatakayomuwezesha mtumishi maslahi mazuri

Mhandisi Luhemeja ameweka wazi kuwa DAWASA mpya  kushindwa sio sehemu yao bali watashirikiana kwa pamoja kuijenga ili ilete manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Malengo hayo ni mikakati madhubuti waliyojiwekea ya kuwa na DAWASA mpya yenye tija na itakayoiinua Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

DAWASA mpya rasmi imeanza kazi yake Septemba 9, baada ya kutambuklishwa kwa menejimenti mpya iliyo chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa sambamba na Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na amewahidi watanzania wote kuwa hususani wa Mkoa wa Dar es Saalaam na Pwani maji yatawafikia sehemu zote chini ya uongozi wake.

Hitimisho, kuundwa kwa DAWASA mpya kunakuja kujena taswira ya mapinduzi ya sekta ya maji iliyokuwa inasuasua kwa kipindi kirefu katik jiji la Dar es Salaam, ili nchi iweze kuinuka kiuchumi haina budi kuwa na maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu na hata katika viwanda mbalimbali vikiwemo vya Vinywaji ambao takribani lita laki moja (100,000) zinatumika kwa siku kwenye kiwanda kimoja, ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali nayo imekuwa inatumia maji kwa wingi ili kufanikisha shughuli zao za ujenzi wa maendeleo ya nchi.Napenda kuipongeza Serikali kwa kuunganisha DAWASCO na DAWASA kwa manufaa ya nchi

NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama

$
0
0
Na Seif Mangwangi, Arusha

MFUKO wa bima ya afya (NHIF), mkoa wa Arusha umewataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kusajili watoto wao kwenye mpango wa bima ya afya ya Toto kadi ili kuwaondolea usumbufu wa kupata matibabu na kuwapunguzia gharama.

Akizungumza katika mji wa Loliondo Ngorongoro Mkoani Arusha, jana katika zoezi la Uhamasishaji Wananchi na Jamii kwa ujumla juu ya Usajili wa Watoto kupitia Toto Afya Kadi na Usajili wa Wajasiliamali wadogo kupitia mpango wa KIKOA, afisa masoko wa mfuko huo Miradji Kisile alisema toto kadi ni mkombozi mkubwa kwa watanzania maskini.

Alisema gharama za Toto kadi ni ndogo kiasi ambacho kila mtanzania mwenye nia ataweza kuimudu na kumwezesha mtoto mdogo kupata huduma ya afya popote nchini.

Kisile alisema watendaji wa NHIF mkoa wa Arusha umeendelea kuhamasisha wakazi w mji huo kujiunga na mfuko huo na sasa wameanzisha zoezi la kuhamasisha wakazi wa Loliondo wilayani Ngorongoro kupitia Minada na Magulio yaliyopo Loliondo.

" Katika zoezi hili la hamasa tumeshapita kwenye minada ya Digodigo, Malambo, Piyaya na Wasso ambapo wananchi wamehamasika vizuri na kuahidi kujiunga," Alisema.

Kisile alisema katika zoezi hilo lililofanyika kwa siku nne kuanzia septemba 10 hadi 14 wananchi wamepata fursa ya Kuelimishwa Juu ya huduma za NHIF na jinsi ya kujisajili na mfuko wa Watoto na Wajasiliamali Wadogo Wadogo

Alisema zoezi hilo la kuhamisha litaendelea katika wilaya zingine za mkoa wa Arusha na kuhakikisha watu wengi wanajiunga na mfuko huo kwa lengo la kupata huduma bora za afya.

Afisa Masoko wa mfuko wa bima ya Afya NHIF mkoa wa Arusha Miradji Kisile akiwa katika mnada wa digodigo wilayani Ngorongoro akihamasisha wananchi wa wilaya hiyo kujiunga na huduma za bima ya afya kupitia mpango wa Kikoa na toto afya kadi

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 17, 2018

JAFFO APONGEZA UJENZI WA BARABARA YA OLJORO - MURRIET JIJI LA ARUSHA.

$
0
0
Na Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) amepongeza ujenzi wa barabara ya oljoro murriet inayojengwa kupitia mradi wa TSCP awamu ya tatu wenye gharama ya Shilingi Bilioni 22. 3 inayojengwa na mkandasi kutoka kampuni ya Sinohydro Co-Operation Ltd ya nchini China.

Mhe. Jaffo ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Jijini Arusha mapema leo hii alipotembela mradi huo wa ujenzi wa barabara unaosimamiwa na mhandisi wa barabara wa Jiji Eng. Agust Mbuya na kujionea hatua nzuri iliyofikia ujenzi huo ambapo kwa sasa upo kwenye hatua za awali na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 11 mwaka 2019 na kuanza kutumiwa na wananchi.

“Nichukue fursa hii kukupongeza mhandisi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huu, pia nitoe rai kwa mshauri elekezi wa ujenzi wa mradi huu kufanya kazi kwa niaba ya halmashauri , kushauri kwa weledi na kuwa mtetezi mkuu kwa upande wa Serikali kwani atakapokuwa upande wa mkandarasi basi Halmashauri itashindwa kufikia malengo kwani itakosa mshauri mwenye kusimamia haki ” Alisema Mhe. Jaffo.

Sambamba na ziara yake hiyo kwenye mradi wa ujenzi wa barabara Mhe. Jaffo pia alitembelea kituo cha afya cha Kaloleni kilichopo Jijini hapa ili kujionea matumizi ya kiasi cha Fedha shilingi milioni 400 zilizotolewa na Serikali tagu tarehe 26 June, 2018 kwa ajili ya kukarabati majengo katika Kituo hicho pamoja na ujenzi wa wadi mbalimbali.

"Nimepokea barua nyingi kutoka hapa kutaka mbadilishe matumizi ya ujenzi wa majengo ya hospitali pamoja huduma za meno ,sitaki mbadilishe chochote hapa na jumatano kazi ianze na nitakuja kukagua mwenyewe ukamlishwaji wa jengo hili novemba 30 mwaka huu " alisema Mhe. Jafo.

Pia Waziri Jafo alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqqaro kufuatilia na kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unaanza Jumatano wiki ijayo. 

Naye Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dk. Simon Chacha alimhakikishia Waziri Jaffo kuwa wataanza ujenzi wa majengo ya upasuaji na wodi ya wazazi, jengo la X Ray, sehemu ya Kusubiria wagonjwa (waiting bay),Jengo la kufulia na ukarabati wa chumba cha meno, dawa, Maabara na mfumo wa maji taka katika kituo hicho cha Kaloleni ili kuboresha huduma za afya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) (Kulia) akitoa maelekezo wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) ( kushoto) akiwa katika moja ya chumba cha kutolea huduma za afya katika Kituo cha Afya Kaloleni

Vijana kufaidika na programu ya kitalu nyumba (green houses) katika mikoa yote nchini

MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO.

$
0
0
Khadija Khamis –Maelezo 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe, Riziki Pembe Juma aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano na Serikali kuhakikisha vitendo vya uzalilishaji vinaondoka nchini .

Hayo alisema leo huko katika kiwanja cha kufurahishia watoto kariakoo wakati wa mdahalo wa wazi wa kupokea maoni ya wananchi dhidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wanawake na watoto ulioandaliwa na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto..

Alisema serikali imetunga sheria kwa wale wote wanaofanya vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto lakini kila siku vitendo vinaendelea hivyo iko haja ya mashirikiano ya pamoja kati ya walezi wazazi na serikali ili kuvidhibiti vitendo hivyo .

Aidha alisema tupange mikakati madhubuti kwa pamoja jinsi ya kuondoa wimbi sugu la udhalilishaji wanawake na watoto na hata watu wazima na kuhakikisha kila mmoja anahusika katika mapambano ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia ..

Nae mshiriki wa mdahalo huu Shadida Machano alisema wazazi wawe karibu na watoto wao na kuwalea malezi ya kirafiki ambayo yanazingatia maadili ili kumjengea mtoto uwezo wa kusema kwa kila ambalo linamtokezea .Alisema skuli ziandaliwe masomo maalumu ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari ili kuweza kujielewa na kujihami.

Hata hivyo alisema ingawa jamii imeharibika kwa kiasi kikubwa kutokana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hivyo iko haja walimu wa skuli pamoja na madrasa kupewa mafunzo maalumu.Nae mshiriki wa mdahalo huo kheir Miraji othmani wa Chukwani alitoa rai ya nini kifanyike ili kudhibiti vitendo hivi alisema itolewe adhabu ya mara moja uliyo madhubuti kwa haraka .

“Amekutwa pale pale avuliwe nguo apigwe mikwaju katikati ya umati wa watu, kwani yeye si kadhalilisha basi adhalilishe,afungwe kifungo ch maisha. “ alisema kheir Miraji mmoja wa wazazi.

Bi Raya Mohamed Sleiman wa Mchangani alieleza hali halisi ya kukosa mashirikiano kwa polisi na mahakama jambo ambalo linavunja moyo na kurejesha nyuma juhudi za kupiga vita vitendo hivyo.

“Tatizo hatuna nia ya dhati kuliondoa hili jambo kwa sababu kwa nini tunalindana? udhalilishaji imekuwa kama biashara ya kujiingizi fedha kwa njia ya ruchwa hivi kweli muhalifu anatoroka kituoni “alisema bi Raya.

Alisema sheria zinaachwa katika makaratasi hazitekelezwa hii inaonyesha wazi huu ni mtandao maalum ambao kama serikali ipo tayari kuuvunja unaweza kwani ushahidi umeonyesha imepiga vita mifuko ya plastic imeweza helment imeweza na hili haishindwi .

Nae Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Mhe,Maudline Castico alitoa wito kwa wazazi na walezi kuvuata maadili katika malezi na makuzi ya watoto ili kujenga maandalizi mema kwa ajili ya taifa la kesho.

Nae Jaji Mshebe Ali Bakari alieleza suala la kuporomoka kwa maadili kwa vijana na watoto kunachangia kuimarisha vitendo vya udhalilishaji hivyo iko haja ya wazazi na walezi kurekebisha maadili ilI kuzuia udhalilishaji kwa pamoja Baina ya wazazi na serikali.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Riziki Pembe Juma akizungumza na Washiriki katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni ya Wananchi zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar uliofanyika Viwanja vya Kariakoo kwa kuwataka Wazazi kuzidi kutoa mashirikiano juu ya vitendo vya udhalilishaji vinavyotokea ( kulia) Naibu waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na WatotoShadia Mohamed na Mshauri wa Rais wa Zanzibar masuala ya Wanawake Zainab Omar.
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe,Maudline Castico Akielezea juu ya wazazi kuwalea watoto katika maadili mazuri wa Kwanza( kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Fatma Gharib.Bilali na Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe 
Mmoja wa wachangiaji katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar Shadida Machano akichangia kwa kusema kuna vyuo mbali mbali vya madrasa vilivojitokeza bila ya kusajiliwa.
Baadhi ya Washiriki kutoka Taasisi mbali mbali waliohudhuria katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar wakifuatilia kwa umakini mdahalo huo uliofanyika Viwanja vya Kariakoo Mjini Unguja.
Picha na Maryama Kidiko – Idara ya Habari Maelezo Zan
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images