Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI MHANDISI NDITIYE AZINDUA WIKI YA SHIRIKA LA RELI NCHINI

0
0



Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiy amefungua wiki ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na kuzindua nembo na kuzindua nembo mpya ya shirika hilo.

Akizungumza na waaandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mhandisi Nditiye amesema juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kupitia ilani ya CCM katika sekta ya usafirishaji zitapelekea kuondoa kero mbalimbali na kukuza vipato vya wananchi 

Mhandisi Nditiye amesema hayo ili huhakikisha kauli mbiu ya uchumi wa viwanda inatekelezwa kwa ufanisi kwa kutumia miundombinu ya reli ya kisasa na uboreshaji wa reli ya kati kuelekea Dar -Isaka.Mhandisi amesema juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa wananchi wa Tanzania tushirikiane kwa pamoja kuunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Mh.Rais Dkt.John Joseph Pombe Magufuli.

"Nawahakikishia kuwa serikali ya awamu ya tano itaendelea kuboresha huduma kwa wananchi na kuimarisha miundombinu ya reli na yenye lengo la kuleta manufaa na maendeleo ya Taifa la leo na kesho,"alisema Mhandisi Nditiye
Mwenyekiti wa bodi ta Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania (TRC),Profesa John Wajanga akizungumza waandishi wa habari katika ufunguzi wa wiki ya Shulilika la reli Tanzania leo hadi September 15 mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza leo na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa wiki ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuwapongeza kwa nzuri na kusimamia vema shunguli za miradi mbalimbali inayoendelea ikiwemo wa ujenzi wa reli.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa bodi ta Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania (TRC),Profesa John Wajanga (picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa wiki ya Shirika la reli Tanzania.
Meneja Uhusiano shirika la Reli Tanzania-TRC,Jamila Mbarouk akifafanua jambo katika ufunguzi wa shirika la Reli Tanzania.
Wafanyakazi wa shirika la Reli Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 13, 2018

0
0
















JAFO AWATAKA WATENDAJI WA MANISPAA ZA DAR ES SALAAM KUONGEZA KASI YA UTENDAJI

0
0
1.       Viongozi wakikagua ujenzi wa jengo la Ofisi za Manispaa ya Kigamboni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda na Mkuu wa wilaya Kigamboni Sara Msafiri  kwenye ukaguzi wa miradi ya maendeleo Kigamboni.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa maelekezo baada ya kukagua miradi ya maendeleo Kigamboni.
Viongozi wakikagua kituo cha Afya Kimbiji.

                            ...........................................................................................

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka watendaji wote wa Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam kuongeza kasi ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao. 

 Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo inayo tekelezwa na serikali katika Manispaa hiyo.  Katika ziara yake leo ametembelea Manispaa ya Kigamboni na kukagua ujenzi wa Ofisi za Manispaa hiyo pamoja na ujenzi wa Kituo cha afya Kimbiji. 

 Katika miradi hiyo, Waziri Jafo hakufurahishwa na kasi ya ujenzi wa Miradi hiyo ya maendeleo huku akiagiza ujenzi wa Ofisi za Manispaa ukamilike kabla mwezi Januari mwaka 2019 ili waondokane na tatizo la kupanga kwenye nyumba ya mtu binafsi.  Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda amemuahidi Waziri Jafo kwamba wao kama mkoa wamejipanga kutekeleza maagizo yote na kuwataka watumishi wote wa mkoa huo kubadili utendaji kazi wao ili kutekeleza kwa wakati miradi.

CHUO KIKUU ARDHI CHAANZA KUTUMIA NDEGE TIARA KATIKA UKUSANYAJI TAARIFA NA USOMAJI RAMANI NCHINI

0
0


Mtaalam wa ndege tiara kutoka kampuni ya China TOPRS Tech Limited, Yu Jing Run akiiandaa ndege tiara tayari kwa kuirusha katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Septemba 12 2018, wakati wa uzinduzi wa ndege hiyo itakayokusanya taarifa na upimaji ramani. Wanaoshuhudia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa (wa tatu kushoto), Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (Taaluma), Profesa Gabriel Kassenga na wana taaluma mbalimbali.  
Mhandisi upimaji ramani wa kampuni ya China TOPRS Tech Limited, Ren Ya Feng akitoa muhtasari wa jinsi ndege tiara inavyofanya kazi muda mfupi kabla ya kuirusha kwa upigaji picha jijini cha Dar es Salaam Septemba 12 2018. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa, Naibu Mkuu wa chuo Kikuu Ardhi (Taaluma), Profesa Gabriel Kassenga (Kushoto Makamu Mkuu) na wana taaluma mbalimbali.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akifafanua jambo kwa wageni mbalimbali walioshiriki uzinduzi huo. 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wageni na wataalam walioshiriki uzinduzi huo.  
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa  (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wageni na wataalam walioshiriki uzinduzi huo.

NCHI ZA AFRIKA ZAENDELEA KUWA NA UHABA WA MBEGU ZA MSINGI

0
0
Meneja  Biashara Wycliffe Ingoi  kutoka kampuni QualiBasic seed Company Ltd yenye makao yake  nchini Kenya Na. Vero Ignatus, Arusha. 

Kutoka kushoto ni Msemaji wa Mradi  kutoka kampuni ya African Agriculture Technology Foundation (AATF) ya nchini Kenya Kenya Everlyn Situma, akiwa na Meneja  Biashara Wycliffe Ingoi  kutoka kampuni QualiBasic seed Company Ltd yenye makao yake  nchini Kenya wakizungumza na waandishi wa habari leo. Picha na Vero Ignatus

Na. Vero Ignatus, Arusha. 
Imeelezwa kuwa uhaba wa mbegu za misingi utaendelea kuwa tatizo katika nchi za Afrika kutokana na uzalishaji mdogo wa mbegu hizo

Hayo yameelezwa leo na meneja  biashara Wycliffe Ingoi  kutoka kampuni QualiBasic seed Company Ltd yenye makao yake  nchini Kenya  wakati akitoa taarifa hiyo ya hali halisi ya upatikanaji wa mbegu hizo kwa vyombo vya bahari Jijini Arusha. 

Ameongeza kuwa kutokana na uzalishaji wa mbegu hizo za msingi ambapo kampuni nyingi za uzalishaji wa mbegu kutokumudu gharama za uongezaji ubora katika mbegu hizo 

Aidha amesema kuwa hivi sasa kuna kampuni moja tu inayoongeza ubora wa mbegu hali ambayo hailingani na mahitaji ya mbegu za msingi kwa wakulima. 

Kwa upande wake Msemaji wa Mradi  kutoka kampuni ya African Agriculture Technology Foundation (AATF) ya nchini Kenya Everlyn Situma ameiomba serikali nchini Tanzania kupitia watafiti wa mbegu kuweza kuangalia namna ambayo wanaweza kuruhusu mbegu za mahindi zanye kinga kutumiwa kwa wakulima

Ameitaka jamii kubadili mtazamo hasi ambao wengi wao  wamekuwa wakidhania mbegu hizo   zenye kinga zina mbalimbali ikiwemo   kansa na utasa kwa wanaume na wanawake. 

Amesema utafiti umefanyika kwa nchi 12 barani Afrika ambao unaonyesha mbegu hizo ni salama kwa matumizi ya kilimo na kuzuia mazao kushambulia na wadudu.

MAGEUZI SEKTA YA UVUVI PANGANI,DC NA VIONGOZI WAKUTANA NA WAZIRI MPINA JIJINI DODOMA

0
0

 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa kulia akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani wakimsubiri Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina kufanya nae kikao ikiwa ni mpango mkakati wa kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina kulia akimlaka Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani wa pili kutoka kushoto na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani kulia akiwa na Afisa tawala wa wilaya hiyo Gipson mara baada ya kufanya mazungumzo nao leo Jijini Dodoma

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani ikiongozwa na Mh. Zainab Abdallah kwa ushirikiano na Ofisi ya Mbunge imefanya ziara ya kikazi makao makuu ya nchi mkoani Dodoma ikiwemo kukutana na kuwa na kikao na Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina na kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani.

Akizungumza baada ya kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alisema kikao hicho kilihusisha agenda nne kubwa muhimu kwa ukombozi wa sekta ya Uvuvi wilayani Pangani ikiwemo Upatikanaji wa mashine ya Storage (Compressor) na Jokofu kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya baharini kwa ajili ya soko kubwa la Samaki Pangani Mashariki ambalo ujenzi wake umefanikishwa na mapato ya ndani ya halmashauri.

Hatua hiyo imepelekea Waziri Mpina kuwapongeza kwa jitihada za awali na kuahidi kuwa Wizara yake itatoa fedha ili jokofu na compressor vipatikane mara moja na soko lianze kufanya kazi.

Alisema kuelekea utekelezaji wa kampeni ya “VIJANA NI WAKATI WETU” iliofanyika Wilaya ya Pangani; sekta ya uvuvi ndio iliongoza kwa uandikishaji wa Vijana wengi.

Hivyo pia Mkuu huyo wa wilaya aliwasilisha  ombi la kupata Engine za Boti za uvuvi kwa ajili ya vikundi vya vijana walio tayari kujiajiri na kujipatia kipato kupitia sekta hii. Wizara kupitia ruzuku yake itagharamia 40% na 60% igharamie halmashauri husika.

Ambapo kufuatilia ombo hilo Wizara hiyo  imeridhia kutoa Engine za kutosha kwa vijana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Halmashauri itatumia mfuko wa vijana na mfuko wa Jimbo kufanikisha upatikanaji wa Engine hizi ili vijana wapate vifaa hivi vya kisasa na utaratibu utawekwa kupitia Idara ya Vijana ya wilaya juu ya usimamizi na mafunzo. Hii ni ishara ya ukombozi kwa vijana wa Pangani.

Mkuu huyo wa wilaya alisema pia walizungumzia suala la kuanzishwe kwa  Chuo cha mafunzo na utaalamu kwa Sekta ya Uvuvi Pangani ikiwa ni kuelekea kupata muarobaini wa sintofahamu ya Chuo cha KIM kurudi mikononi mwa wananchi na kuwanufaisha zaidi ya ilivyo sasa.

Hatua hiyo ilimlazimu Waziri huyo kuamua kuunda timu ya wataalamu ambayo itakwenda Pangani mara moja kuchunguza suala hili ili ripoti itakayo wasilishwa aweze kuitolea maamuzi kwa maslahi mapana ya wana Pangani.
.
Sambamba na hilo liligusiwa suala la ujenzi wa  Soko la Samaki na Dagaa Kipumbwi ambapo Waziri Mpina ameweka wazi kuwa suala hili lipo sasa kwenye mipango ya Wizara na kilichobaki ni Utekelezaji wa haraka. na ikumbukwe mipango ilishawekwa sawa juu ya urasimishaji wa Bandari ya Kipumbwi.

" Sekta ya Mifugo nayo  haikuachwa nyuma kwa Waziri kuhahidi upatikanaji wa Rambo la malisho ya mifugo Pangani ikiwa ni faraja iliopotea muda mrefu kwa wafugaji wa Pangani "Alisema.

DC GODFREY CHONGOLO ASEMA KIPAUMBELE CHAKE NAMBA MOJA WILAYANI KINONDONI NI MAPATO

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Godfrey Chongolo amesema kipaumbele chake namba moja,mbili na tatu ni mapato.

Amesema ili halmashauri ifanye mambo yake vizuri ni lazima iwe na mapato ambayo yatasaidia katika kufanikisha mambo mbalimbali yakiwamo ya kutatua changamoto zilizopo wilayani Kinondoni.

Chongolo amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Dk.John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.Awali Wilaya hiyo alikuwa Ali Hapi ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.Chongolo kabla ya kuhamishiwa Kinondoni alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido.

"Kwangu mimi kipaumbele changu namba moja ni mapato,kipaumbele changu namba mbili ni mapato na kipaumbele changu namba tatu ni mapato." Kwanini? Ni kwasababu ukiwa na mapato unaweza kufanya mambo mengi yakiwamo ya kutatua changamoto zilizopo.

"Kwa mfano kuna malalamiko ya kuwepo kwa makelele mengi kutoka kwenye mabaa lakini ukiwa na fedha itakuwa rahisi wanaohusika na mazingira wakaenda kukagua na kuchukua hatua," amesema Chongolo.Ametoa maelezo hayo leo wakati anajibu swali aliloulizwa na mtangazaji Baby Kabaye wa Clouds Tv ambaye alitaka kujua mikakati ya Chongolo katika eneo la mapato.

Hivyo amesema unahitaji msuli wa kimapato ili kutatua changamoto,ukiwa na kipato ni rahisi kuwajengea uwezo watumishi kufika kwenye maeneo yenye changoto na kuzitatua kwa wakati.Amesema inafahamika Wilaya ya Kinondoni huko nyuma ilikuwa inasifika kimapato na anao uhakika mapato yataongezeka kutokana na mikakati ambayo wameiweka.

Amefafanua wao wanaangalia mapato kama sehemu ya kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi na kusisitiza miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na kuimarisha ulinzi wa wananchi na mali zao.Akifafanua kuhusu ulinzia anasema amepata nafasi ya kuzungumza na Kamanda wa Polisi Kinondoni na moja ya mipango iliyopo ni kuhakikisha inatengenezwa mifumo ya kuimarisha ulinzi.

Amesema kuwa anatambua changamoto ya uhalifu katika Wilaya hiyo ambapo alielezea huko nyuma namna ambavyo kulikuwa na uhalifu ukiwamo wa wizi wa vifaa vya magari."Katika eneo la ulinzi hatutakuwa na msamaha kwa atakayebainika kujihusisha na uhalifu."Atachukuliwa hatua na kwa mamlaka niliyonayo mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

"Hivyo tumejipanga kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha kwa wananchi," amesema Chongolo.Kwa kukumbusha tu Rais Magufuli katika moja eneo ambalo alipata nafasi ya kuzungumzia ni kuhusu mapato na hiyo ni baada ya Wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika mapato.

LUSINDE NA JAFO WATIKISA KAMPENI ZA UKONGA

0
0
Umati wa wananchi uliofurika eneo la Bombambili wakati wa kampeni za CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Livingstone Lusinde(Kibajaji) akizungumza na wananchi wa Bombambili.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiteta na Mgombea wa Jimbo la Ukonga kupitia CCM Mwita Waitara na viongozi wa CCM.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akimwaga sera katika kampeni za Ubunge Ukonga.
.................................................................................

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Livingstone Lusinde(Kibajaji) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo wametikisa kwenye kampeni za kumnadi Mgombea wa Jimbo la Ukonga kupitia CCM Mwita Waitara kwa kutoa hoja mbalimbali ambazo zimesababisha wanachama kadhaa wa vyama vya Chadema na CUF kuhamia CCM.

 Wapambanaji hao wa walilindima katika maeneo ya Magole na Mbombambili ndani ya Jimbo la Ukonga wakiwahutubia mamia ya watu waliohudhuria mikutano hiyo. Ajenda kuu zilizotawala mikutano hiyo ni kushughulikia matatizo ya wananchi hususan suala la mipaka, barabara, ujenzi wa hospitali ya Kivule pamoja na Umeme.

 Kwa upande wake, Mgombea ubunge wa Jimbo hilo Waitara amewataka wananchi hao kumpigia kura siku ya Jumapili ya tarehe 16/09/2018 kwa kuwa kwasasa yupo katika chama sahihi cha kushughulikia matatizo yao yanayowakabili.

 Amesema awali alipokuwa Chadema alizuiwa hata kuongea na Mawaziri pamoja na kulazimishwa kuikataa bajeti wakati wa vipindi vya Bunge kitendo kilichosababisha kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa Jimbo hilo.

TIGO YAZINDUA MTANDAO WA 4G+ TANZANIA

0
0

Tigo 4G+ inawapa wateja huduma bora na za uhakika kwa gharama ile ile.

Dar es Salaam, Septemba 12, 2018; Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali Tigo Tanzania, leo imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za mtandao wenye kasi ya juu zaidi nchini baada ya kuzindua teknolojia ya 4G+.

Uzinduzi wa mtandao wa 4G+ unathibitisha kuwa Tigo ni kampuni pekee ya mawasiliano inayofanya ubunifu unaoboresha huduma zake kuendana na mahitaji halisi ya wateja nchini kote.

‘Uzinduzi wa  4G+ ni sehemu ya safari ya mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo hapa nchini. Lengo letu ni kuwawezesha wateja kufurahia huduma bora zaidi za kidigitali. Daima tuko mbele katika kuleta teknologia za kisasa za mawasiliano nchini,’ Afisa Mkuu wa Tigo – Teknologia na Mawasiliano Jerome Albou aliwaambia waandishi wa habari katika uzinduzi wa mtandao wa Tigo 4G+ jijini  Dar es Salaam. 

Sasa wateja wa Tigo wanaweza kufurahia huduma bora, za uhakika na zenye kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui kutoka kwenye mtandao kwa gharama zile zile. Ili kufurahia mtandao wa 4G+, mteja anahitaji kuwa na simu yenye uwezo wa 4G+.

Teknologia ya kisasa ya Tigo 4G+ inaongeza wigo wa matumizi ya huduma za kidigitali nchini. Teknologia hii inapanua utoaji wa huduma za intaneti yenye kasi ya juu zaidi, pamoja na kutoa huduma za sauti zinazoendana na mabadiliko ya maisha.

‘Kampuni yetu inajivunia kuzindua teknolojia ya 4G+ inayoiweka Tanzania katika ramani ya teknolojia ya mawasiliano duniani. Sasa tunashindana na nchi zilizoendelea ambazo tayari zinawekeza katika teknolojia ya 5G. Kupatikana kwa teknolojia ya kisasa ya mawasiliano nchini Tanzania kunaibua fursa mpya za matumizi ya mtandao kwa wateja wetu,’  Afisa Mkuu wa Biashara - Tigo, Tarik Boudiaf alibainisha.  

Mbali na kujivunia mtandao wa 4G ulionea katika miji 22 nchini, mtandao wa Tigo 4G+ tayari unapatikana katika miji ya; Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Moshi na Dodoma, hata hivyo mipango ya kuendelea kuupanua mtandao huo kufikia miji mingine zaidi nchini inaendeliea.  Wateja wanaotumia simu zenye uwezo wa 4G+ sasa wanaweza kufurahia kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui mbali mbali kwa gharama zile zile za intaneti.

Mtandao wenye kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+ una kasi mara mbili ya ule wa Tigo 4G, kwani Tigo  4G ina kasi ya 60Mbps ilihali mtandao mpya wa Tigo 4G+ unaweza kufikia kasi ya hadi 120Mbps. Kwa ujumla, wateja wanaotumia Tigo 4G+ katika eneo husika hugawana kasi hii ya juu zaidi miongoni mwao.


Katika juhudi za kuboresha na kupanua huduma za kidigitali nchini, Tigo ilikuwa mojawapo ya kampuni za mawasiliano za kwanza kabisa kuwekeza katika teknolojia ya 3G na  4G ambapo Tigo ndio kampuni pekee yenye mtandao mpana zaidi wa 4G nchini. 

Tigo pia ilikuwa ya kwanza kuzindua simu janja yenye lugha ya Kiswahili pamoja na huduma ya Facebook kwa lugha ya Kiswahili iliyoongeza matumizi ya huduma za kidigitali kwa idadi kubwa ya Watanzania wanaotumia lugha ya Kiswahili kwa mawasiliano yao ya kila siku.


SHUGHULI MBALIMBALI ZA WIKI YA TRC BADO ZINAENDELEA

0
0

TANESCO KUOKOA ZAIDI YA SH. MILIONI 450 KILA MWEZI BAADA YA MITAMBO YA UMEME WA DIZELI SONGEA KUZIMWA

0
0
 Moja ya mitambo ya kufua umeme wa mafuta ya dizeli uliokuwa kwenye kituo cha Songea ikiwa imezimwa.

 NA K-VIS BLOG, SONGEA

KUTOKANA na kuzimwa kwa mitambo ya dizeli iliyokuwa ikitumika kufua umeme kwa matumizi ya mji wa Songea na vitongoji vyake Septemba 13, 2018 baada ya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, Shirika la umeme Tanzania TANESCO sasa litaokoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 450,108,508 zilizokuwa zikitumika kununua dizeli kila mwezi.


Septemba 13, 2018 TANESCO iliwasha rasmi kituo kipya na cha kisasa cha kupoza na kusambaza umeme cha Madaba, ambacho kimeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kuondoa matumizi ya umeme wa mafuta kwenye Halmashauri ya Manispaa ya mji wa Songea na vitongoji vyake.

Kuwashwa kwa mtambo huo ni baada ya kukamilika kwa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea ambao ulihusisha ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Makambako na Songea sambamba na upanuzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Makambako, lakini pia  Ujenzi wa njia kuu ya usafirishaji Umeme wa kilovoti 220 yenye urefu wa kilometa 245 kutoka Makambako hadi Songea kupitia Madaba. Usambazaji Umeme wa msongo wa 33kV zenye urefu wa kilomita 900 na kuunganisha wateja 22,700 katika Wilaya za Njombe , Ludewa na mji wa Makambako katika Mkoa wa Njombe, Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo na Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma.

Tayari wakazi wa mji wa Songea wamepokea taarifa za mji wao kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kuondoa ile adha ya kukatika umeme iliyokuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu. 

Songea kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kuna maanisha mji huo sasa umeanza kupata umeme ulio bora na wa uhakika na hivyo wananchi sasa wanapaswa kuchangamkia fursa ya uwepo wa nishati hiyo kwa kufungua viwanda vidogo na miradi mbalimbali ya kiuchumi inayotegemea nishati ya umeme.
 Kituo cha Umeme TANESCO Songea ambacho kilikuwa kikitumia mashine zinazoendeshwa kwa mafuta ya dizeli. Kituo hicho sasa kimezimwa.
 Tenki la kuhifadhia mafuta ya dizeli, ambalo sasa litabaki kama kumbukumbu, baada ya matumizi yake kukoma rasmi Septemba 13, 2018.

Vituo vya Huduma ya Pamoja Vyaleta Neema kwa Wawekezaji -TIC

0
0
Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeendelea kufanya jitahada mbalimbali za kuhakikisha wawekezaji wanahudumiwa kwa urahisi na haraka kwa kutumia mfumo wa huduma mahala pamoja.

 Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji  Uwekezaji  wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Ayubu Sizya, anasema lengo la kuanzishwa utaratibu huu ni kuondoa ule wa awali uliomlazimu mwekezaji kufuatilia usajili, leseni na vibali mbalimbali katika ofisi za idara zinazowahudumia wawekezaji.
Utaratibu wa awali  ulikuwa unapunguza ari na juhudi za kuvutia uwekezaji sambamba na kumwongezea mwekezaji gharama zisizo za lazima, wakati wa kufuatilia taratibu mbalimbali .

Sizya  anasema kuwa  jukumu la kwanza la TIC baada ya mwekezaji kuanza mchakato wa kutaka kuwekeza ni kuhakikisha anapata usajili kwa kupewa cheti cha uwekezaji kabla ya kupata vibali na leseni mbalimbali.

“Tunaendelea na juhudi za kufanya azma ya uwekezaji ifanikiwe. Hivyo wawekezaji wote wanaohitaji huduma hizi wasiende katika ofisi hizo kwa sababu zitapatikana hapa TIC,” anasema Sizya.
Aidha, katika kudhihirisha hilo, wataalamu wa sekta mbalimbali wamekuwepo TIC katika kuhakikisha wanaandaa mazingira mazuri kwa  wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi  yatakayowezesha kutolewa kwa  vibali na huduma mbalimbali muhimu kwa ajili ya kufanikisha shughuli ya uwekezaji nchini.

Aidha, Mwakilishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Joseph Klerruu anasema kuwa kuwepo kwa  mazingira mazuri kwa wawekezaji  wa viwanda na kilimo, imechangia katika kuanzishwa kwa benki ya ardhi inayolenga kusaidia upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji kutoka kwa wananchi, halmashauri na idara mbalimbali za Serikali.

 Utaratibu uliowezesha upatikanaji wa hekta 63,000 huko Ngerengere mkoani Morogoro kwa ajili ya kilimo cha miwa kinachoendesha na mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF.

Klerruu anasema, “Katika utaratibu tuliouanzisha tunalenga kupata mashamba matano ya hekta 5,000, na viwanja 50 vya viwanda vyenye ukubwa wa mita za mraba 5,000 licha ya kuwa changamoto hapa ni fedha kwa sababu kwa viwanja hivyo vinahitaji karibu Shilingi bilioni 800”.

Halikadhalika, Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) lina jukumu la kuhakikisha linawaongoza wawekezaji kufahamu sheria, kanuni na taratibu mbalimbali sambamba na kutoa mwongozo wa mchakato wa tathmini ya mazingira kwa miradi mipya na  inayoendelea, huku wakijiandaa kuanza kufanya tathmini baada ya kukamilika kwa kanuni mpya za mazingira baadae mwaka huu, kabla ya kuanza kutoa huduma zote kituoni hapo.

Aidha, kuwepo kwa mfumo huo,wa  vituo vya huduma za pamoja kumerahisisha uombaji wa usajili wa kampuni kushughulikiwa haraka na kwa wepesi zaidi kutokana na kutokuwapo kwa mrundikano wa maombi ya usajili katika Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA).

BRELA imeweka mfumo wa uombaji usajili na leseni ya biashara kwa njia ya mtandao, pamoja na kutumia maofisa biashara wa halmashauri kutoa elimu kwa wananchi ili kuwawezesha kutuma maombi popote walipo. 

Aidha, TIC imeendelea kushirikiana na Taasisi na Mamlaka mbalimbali ili kufanikisha azma yake ya kuweka mazingira rafiki na rahisi kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ndani ya TIC imeendelea  kumrahisishia mwekezaji aliyeanza uzalishaji kusajili bidhaa na kupata alama ya ubora kwa kumpa leseni ya ubora ya ukaguzi.

Vilevile inamsadia mwekezaji kupata msamaha wa ukaguzi kwa mashine, mitambo na malighafi zisizopatikana nchini kwa lengo la kumpunguzia gharama za uwekezaji nchini. 

Kupitia huduma hizo za mahala pamoja Mamlaka ya Mapato (TRA)  nayo ina  jukumu la kutoa elimu ya mlipakodi na kupokea na kuwasilisha maombi ya  misamaha ya kodi kwa wawekezaji kwa Kamishna wa Ushuru wa Forodha mwenye mamlaka ya kuchakata na kutoa msamaha wa kodi.

Aidha, uwepo wa mwakilishi wa TRA kituoni hapo unatoa nafasi ya kupata elimu ya ziada kuhusu kodi mbalimbali kama vile kodi ya ongezeko la thamani (VAT), forodha na kodi ya mapato na kurahisisha utoaji huduma kwa wawekezaji.

Kuhusu maombi ya vibali vya kazi kwa wawekezaji wa kigeni pamoja na wafanyakazi wa kigeni walioajiriwa na miradi ya uwekezaji , Wizara ya Kazi imeendelea  kuchakata maombi hayo.

Licha ya changamoto ya uelewa mdogo wa Sheria Namba Moja ya Mwaka 2015 ya kuratibu ajira za wageni ya kuruhusu mwekezaji kuleta wafanyakazi watano sheria inaelelekeza kuwa ni lazima wawe na uwezo wa kurithisha ujuzi kwa wazawa, tofauti na baadhi ya wawekezaji wachache ambao hutaka kuingiza wafanyakazi bila kuangalia sifa hizo.

Sambamba na hilo uwepo wa Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) umesaidia kusajili na kuwafahamisha wawekezaji taratibu za kufuata, ambapo kutokana na kuwa chini ya TIC imewawezesha kufanya usajili ndani ya siku tatu tofauti na kutoa huduma hiyo katika ofisi ya mamlaka ambapo usajili hupatikana ndani ya siku 28 tangu siku ya kuwasilishwa maombi.

Aidha, Taasisi nyingine zinazowahudumia wawekezaji zilizopo kituoni hapo ni pamoja na  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) huku mchakato wa kuhakikisha mwakilishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) anapelekwa katika Kituo hicho unaendelea ili kuwarahisishia wawekezaji taratibu za kuwekeza nchini.

Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza dhamira yake ya dhati ya kuvutia uwekezaji nchini ili kuongeza ajira na pato la Taifa kupitia uwekezaji huo. TIC kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazohusika na uwekezaji imeondoa ukiritimba katika suala hilo.

JAFO AAGIZA USAFI NA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

0
0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu ya barabara.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu ya barabara.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu mbalimbali.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa jiji la Arusha alipotembelea kituo cha Afya Kaloleni kukagua ujenzi wa miundombinu.

.................................................


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo amewaagiza Viongozi wa Jiji la Arusha kudumisha usafi ili kulinda miundombinu ya barabara ambazo zimejengwa jijini humo kwa gharama kubwa. Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayo tekelezwa chini ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Katika ziara hiyo,Waziri Jafo hakupendezwa hata kidogo na uchafu uliooneka kutapakaa ndani ya mifereji hiyo ambayo imejengwa hivi karibuni chini ya mradi wa uendelezaji Miji mkakati (TSCP).

 Kufuatia hali hiyo, Jafo ameugiza uongozi wa jiji hilo kuunda makundi ya wamama na wajane ambao wapo tayari kufanya usafi ili kila kikundi kikabidhiwe barabara yao kwa ajili ya kuitunza huku wakipata kipato ambacho kinaweza kikawasaidia kulea watoto na familia zao. 

 "Barabara za lami nzuri pamoja na mifereji iliyojengwa na zinazoendelea kujengwa zimeonekana kujaa uchafu kitendo ambacho kinahatarisha miundombinu hiyo kuharibika haraka,"amesema Pamoja na ukaguzi wa miundombinu ya barabara inayojengwa Jijini Arusha Jafo alitembelea kituo cha afya Kaloleni kilichopokea shilingi milioni 400 kutoka serikali huu lakini alikuta ujenzi haujaanza. Kutaokana na hali hiyo Jafo ameuagiza uongozi wa Jiji la Arusha kuanza ujenzi huo kabla ya kumalizika kwa wiki ijayo na ametaka ujenzi huo uwe umekamilika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.

Makamu wa Rais azindua Tamasha la Urithi festival

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi Tamasha la Urithi (Urithi Festival) katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi Tamasha la Urithi (Urithi Festival) katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo ya Nguli wa Sanaa za Ngoma ya Urithi Festival mwaka 2018 Mjukuu wa Mzee Morris Nyunyusa kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kutunza na kudumisha utamaduni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa kwa mikono na kikundi cha Eddie Collection wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi (Urithi Festival) kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa kwa mikono na kikundi cha Eddie Collection wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi (Urithi Festival) kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii kwa uchumi wa nchi yetu, na kwamba ili kuweza kupata watalii wengi zaidi lazima kuwa na usafiri wa anga ulio na uhakika; ndiyo maana Serikali imeamua kufufua shirika letu la ndege (ATCL) na tayari Serikali imenunua ndege mpya saba.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Mwezi wa Urithi wa Utamaduni wa Mtanzania linalojulikana kama Urithi Festival liliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.

“Ni wazi pia kwamba utalii unahitaji usafiri bora na wa uhakika wa nchi kavu, hususan reli na barabara. Kwa kujua hili, Serikali imeamua kujenga reli mpya ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, katika awamu hii ya kwanza.
 
 Vilevile, Serikali inakarabati reli yetu ya zamani kutoka Tanga hadi Arusha. Ukarabati wa reli hii utawezesha pia kuanzisha utalii wa reli (railway tourism) utakaohusisha vivutio mbalimbali, hususan Milima ya Usambara (Lushoto), Hifadhi ya Taifa Mkomazi, na Mlima Kilimanjaro. Kwa upande wa barabara, barabara nyingi kuu na za mijini zinajengwa kwa kiwango cha lami.” Alisema Makamu wa Rais

Makamu wa Rais amebainisha kuwa Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na rasilimali nyingi za asili ikiwemo milima, misitu, mito, maziwa, bahari, wanyama wa aina mbalimbali na urithi wa utamaduni wa aina mbalimbali.

Makamu wa Rais amesisitiza ni vyema kwa umoja wetu tuweke nguvu kufanya Urithi wa utamaduni wetu kuwa ni zao la uhakika kwenye sekta ya utalii na ukarimu. Vilevile, thamani ya utamaduni inaonekana kwenye sekta nyingine kama elimu, afya, michezo, kilimo, viwanda na maendeleo ya jamii.

Katika Tamasha hilo ambalo lilitanguliwa na burudani mbali mbali za ngoma na nyimbo za asili pia Viongozi wa Serikali na Taasisi mbali mbali walihudhuria.

Aidha Wasanii Nguli katika lugha ya kiswahili, sanaa na utamaduni walitunukiwa Tuzo, wasanii hao ni Shaaban Robert ambaye alitunukiwa Tuzo ya Nguli wa Lugha ya Kiswahili katika Uandishi ya Urithi Festival mwaka 2018 na kupokelewa na Mtoto wake Ikbali Robert, na Mzee Morris Nyunyusa ambaye alitunukiwa Tuzo ya Nguli wa Sanaa za Ngoma ya Urithi Festival kwa mwaka 2018 ambayo ilipokelewa na mjukuu wake.

NEC YAVITAKA VYAMA NA WAGOMBEA KUZINGATIA NA KUHESHIMU SHERIA SIKU YA KUPIGA KURA

0
0

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya siasa, wagombea, wananchi na watendaji wa uchaguzi kuzingatia na kuheshimu matakwa na masharti ya Sheria za Uchaguzi, Sheria za Nchi na Maadili ya Uchaguzi wakati wa upigaji kura, kuhesabu, kujumlisha kura, na kutangaza matokeo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika kesho Jumapili kwenye majimbo ya Ukonga na Monduli na kata 9 za Tanzania Bara.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage katika risala yake kuelekea uchaguzi huo mdogo unaofanyika kufuatia sababu mbalimbali ikiwamo wabunge na madiwani kujizulu, kufariki, kutohudhuria vikao na kufutwa uanachama.

Jaji Kaijage aliwataka wadau hao wa uchaguzi kushirikiana na Tume kuhakikisha kuwa viashiria vya kuvunjika kwa amani na utulivu vinaepukwa ili uchaguzi utakaofanyika uwe huru, wazi na wa haki.
Mbali na wito huo, Mwenyekiti huyo aliwasihi wapiga kura wote waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na wanaoishi kwenye maeneo yanayofanya uchaguzi mdogo, kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi cha takribani miaka miwili ijayo. 

“Wananchi wafanye na kutekeleza zoezi la kuwachagua wawakilishi wao bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi kwani chini ya Kanuni ya 3.1 (b) ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Serikali imepewa wajibu wa kuhakikisha kuwa kuna hali ya usalama, amani na utulivu katika kipindi chote cha Uchaguzi.”, aliongeza Jaji Kaijage na kusisitiza kuwa:

“Ni matumaini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa, hali ya amani na utulivu kwenye maeneo ya Uchaguzi ambayo imekuwepo hadi hivi sasa, itaendelea kudumishwa ili kuhakikisha uchaguzi huu mdogo unafanyika na kumalizika salama kwa ustawi wa Taifa letu.”

Alivikumbusha vyama vya siasa na wagombea kuwa mwisho wa mikutano ya kampeni ni leo saa kumi na mbili kamili (12:00) jioni na baada ya muda huo, vyama, wagombea na mashabiki wasifanye kampeni za aina yoyote, kama vile kutumia alama za vyama zinazoashiria kampeni, vipeperushi, bendera, mavazi na vingine kwa kuwa kesho ni siku ya uchaguzi. 

“Pale panapokuwa na malalamiko yoyote ya ukiukwaji wa Sheria na Taratibu za Uchaguzi, malalamiko hayo yafikishwe kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria. Vivyo hivyo, viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao na wananchi kwa ujumla wajiepushe na vitendo vinavyoweza kusababisha fujo au vurugu katika vituo vya kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura”, alisema.

Jaji Kaijage aliwataka wapiga kura kuondoka kituoni na kwenye maeneo ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura yake kwa kuzingatia tafsiri sahihi ya Kifungu cha 104 (1) kikisomwa pamoja na Kifungu cha 72(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye Shauri la Madai Anuai (Misc. Civil Cause No. 37 la mwaka 2015) mpiga kura.

Aliongeza kuwa mbali ya wale ambao Sheria za Uchaguzi zinawaruhusu kuingia na kuwepo kwenye vituo vya kupigia kura, wananchi wanatakiwa kujiepusha na mikusanyiko au mikutano katika maeneo ya vituo vya kupigia kura na vyama vya siasa vimeweka mawakala vituoni ambao watalinda maslahi ya vyama husika na wagombea wao.

Alikumbusha kuwa wanaoruhusiwa kuingia kwenye Vituo vya kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura ni wale tu walioainishwa kwenye kifungu cha 72(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na kifungu cha 63(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Alivitaka vyama siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo kuweka mawakala katika vituo vyote vya kupigia na kujumlishia kura kwa utaratibu ambao vilikubaliana na Tume tarehe 10/07/2018 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Alivikumbusha kuwa mawakala hao wanaruhusiwa kuwepo katika vituo vya kupigia kura na wanatakiwa kufuata na kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zinazoongoza Uchaguzi katika kipindi chote cha kupiga, kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo.

Jumapili ya tarehe 16 Septemba, 2018, ni Siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Majimbo ya Ukonga katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, Monduli katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha na uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata Tisa (9) zilizopo katika Halmashauri 5, za mikoa 4 ya Tanzania Bara.

“Uchaguzi huu Mdogo wa Ubunge na Udiwani Tanzania Bara, utahusisha jumla ya wapiga kura 470,936 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kutakuwa na Vituo vya Kupigia Kura 1,143.

Jaji Kaijage aliwakumbusha wapiga kura wa Majimbo ya Ukonga, Monduli na kata zote kuzingatia kuwa upigaji kura utafanyika katika vituo vile vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambavyo vitafunguliwa saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni.

Alisema iwapo, wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao wamefika kabla ya saa kumi jioni na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura.  Mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya saa kumi kamili (10:00) jioni.

Alisisitiza kuwa watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu ambao wamo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Jimbo au Kata husika na wana kadi ya mpiga kura na wale walio wamepoteza kadi zao za kupigia kura au zimeharibika au zimechakaa watumie Pasi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Hata hivyo, alisema mpigakura ataruhusiwa kutumia vitambulisho hivyo mbadala, iwapo tu; atakuwa aliandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015, jina lake liwe katika orodha ya wapiga Kura katika kituo anachokwenda kupiga Kura na majina yake yaliyopo katika Daftari la Mpiga Kura yafanane kwa herufi, maneno na tarakimu na majina yaliyopo katika kitambulisho mbadala.

CCM YAFUNGA KAMPENI MONDULI KWA KISHINDO

0
0

Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Rodrick Mpogoro akiwa na viongozi wengine katika ufungaji wa kampeni za ubunge jimbo la Monduli. 

Mbunge wa Kisarawe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akizungumza katika ufungaji wa kampeni za ubunge jimbo la Monduli. 

Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli
Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli

Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli



Chama cha Mapinduzi(CCM) leo kimehitimisha kampeni zake za ubunge jimbo la Monduli kwa aina yake kutokana na wapambanaji wake kujipanga vyema katika kubwaga sera wakimnadi mgombea wa chama hicho Julius Kalanga. 

Kampeni hizo zimefurika mamia ya wakazi wa jimbo hilo katika eneo la Mto wa Mbu na zimefungwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Rodrick Mpogoro na mgeni mashuhuri Selemani Jafo ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI). 

Timu ya wapambanaji wengine iliyokuwa kwenye kampeni hizo kwa siku zote iliongozwa na William Ole Nasha, pamoja na timu ya wabunge mahiri Joseph Msukuma, Sixtus Mapunda, Catherine Magige, Ester Mahawe, Venanse Mwamoto, Dk. Kiluswa, Mariam Ditopile, Matha Mlata, Dk. Godwin Mollel, Anna Lupembe, Edwin Sanda, Godluck Mlinga, Jitu Son, Fratei Massey, na viongozi wengine wa Jumuiya zote za CCM Taifa. 
Wapambanaji hao wamewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua mgombea huyo kuwa Mbunge wao ili aweze kutatua vyema kero zinazowakabili kwa kushirikiana vyema na wabunge wengine huku wakiahidi kumsaidia kuwasilisha bungeni kero za watu wa Monduli ili zitatuliwe na serikali.

UFARANSA YAAHIDI KUZIDISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

0
0
Rais wa Jumuiya ya Utamaduni ya Ufaransa na Zanzibar Khamis Abdalla Said akiwakaribisha Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter na maseneta watatu kutoka Ufaransa na wageni waliohudhuria hafla maalumu iliyofanywa na viongozi hao katika kituo cha Jumiya hiyo Migombani Mjini Zanzibar.
Balozi wa Ufansa nchini Tanzania Frederic Clavieter akizungumza wageni waalikwa waliohudhuria hafla maalumu katika Ofisi ya Jumuiya ya Ufaransa na Zanzibar iliopo Migombani Mjini Zanzibar
Seneta Ronan Dantec kutoka jimbo la Loire-Atlantique akizungumza na wageni waliohudhuria hafla maalumu iliyoandaliwa na Jumuiya ya Ufarans na Zanzibar katia ofisi zao ziliopo Migombani Mjini Zanzibar
wageni waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter wakati balozi huyo akifutana na maseneta RonaDantec, Cyril Pellevat na Bernard Jomier walipotembelea Ofisi ya Jumuiya Ufaransa na Zanzibar.

Wageni waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter wakati balozi huyo akifutana na maseneta RonaDantec, Cyril Pellevat na Bernard Jomier walipotembelea Ofisi ya Jumuiya Ufaransa na Zanzibar.

Na Khadija Khamis – Maelezo

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter amesema nchi yake itaendelea kuongeza ushirikiana wake na Tanzania katika masula ya Uchumi, Kijamii na Utamaduni. Balozi Frederic Clavieter alieleza hayo katika Ofisi ya Jumuiya ya Ufaransa na Zanzibar Migombani alipofanya ziara ya kutembelea ofisi hiyo akiambatana na Maseneta watatu kutoka Ufaransa.

Maseneta waaliofutana na Balozi Clavieter ni Ronan Dantec kutoka Jimbo la Loire-Atlantique, Cyril Pellevat wa Jimbo la Haute-Savoie na Seneta Bernard kutoka Jimbo la Paris .Alisema katika kuimarisha ushirikiano huo, Ufaransa imeamua kuongeza msaada wake kwa Tanzania kutoka Euro milioni 50 kwa mwaka kufikia Euro milioni 100 ili kuharakisha maendeleo yake.

Alisema mahusiano kati ya Ufaransa na Tanzania ulianza muda mrefu uliopita na wananchi wa mataifa hayo mawili wamekuwa na ushirikiaano mkubwa katika masula ya Utamaduni kwa kushiriki katika Matamasha mbali mbali yanayoandaliwa na nchi hizo. Alisema ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo hivi sasa yameleta maafa makubwa katika baadhi ya nchi hasa nchi changa.

Balozi Frederec amefurahishwa na kuona vijana wa Zanzibar wanajifunza lugha ya Kifaransa na ameshauri vituo zaidi vya kufundishia lugha hiyo viongezwe ili kuimarisha zaidi Utamaduni wa nchi hizi mbili. Aidha alisema kujitokeza vijana wengi kujifunza Kifaransa kutawasaidia vijana hao kupata ajira kwani zaidi ya Watalii 20 elfu kutoka Ufaransa wamekuwa wakitembelea Zanzibar kutokana na vivutio vingi vya Utalii viliopo.

“Vijana wengi watakapoweza kuzungumza kifaransa itakuwa moja ya njia ya kuimarisha utamaduni wa nchi hizi mbili na kupata ajira, “alisema Balozi wa ufaransa . Nae Seneta kutoka Jimbo la Loire-Atlantique Ronan Dantec alisema Zanzibar inanafasi kubwa ya kushirikiana na Ufaransa katika kukuza na kulinda utamduni wa nchi hizo na kuimarisha utalii.

Rais wa Jumuiya ya Ufaransa na Zanzibar Khamis Abdalla Said alisema lengo la kuwepo Jumuyiya hiyo ni kuwapa nafasi Wazanzibari kujifunza lugha ya Kifaransa katika ngazi mbali mbali na kuwawezesha kufanya mitihani ya kimataifa ya lugha hiyo .

Aliongeza kuwa kituo chao kimekuwa kikiandaa matamasha ya Utamaduni wa Zanzibar na Ufaransa katika juhudi za kuimarisha tamaduni zao na kulinda Mila Silka za mataifa hayo mawili. Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Sensa na Filamu na Utamaduni Dkt Omar Abdalla Adam ameeleza kufurahishwa na ujio wa wawakilishi hao kwani utatoa fursa zaidi kwa vijana wa Zanzibar kutembelea Ufaransa kwa lengo la kudumisha ushirikiano uliopo

MAGARI YAANZA KUPITA KATIKA BARABARA YA JUU (FLYOVER) ENEO LA TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

 Magari yakipita kwa ajili majaribio leo (Jumamosi Septemba  15, 2018) katika barabara za juu (flyover) ya Mhandisi Patrick Mfugale lililopo eneo la Tazara Jijini Dar es Saalam ambalo hivi karibuni linatarajiwa kufunguliwa rasmi na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
3. (1)
Magari yakipita kwa ajili majaribio leo (Jumamosi Septemba  15, 2018) katika barabara za juu (flyover) ya Mhandisi Patrick Mfugale lililopo eneo la Tazara Jijini Dar es Saalam ambalo hivi karibuni linatarajiwa kufunguliwa rasmi na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
2.Magari yakipita kwa ajili majaribio leo (Jumamosi Septemba  15, 2018) katika barabara za juu (flyover) ya Mhandisi Patrick Mfugale lililopo eneo la Tazara Jijini Dar es Saalam ambalo hivi karibuni linatarajiwa kufunguliwa rasmi na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
4 (11)
Magari yakipita kwa ajili majaribio leo (Jumamosi Septemba  15, 2018) katika barabara za juu (flyover) ya Mhandisi Patrick Mfugale lililopo eneo la Tazara Jijini Dar es Saalam ambalo hivi karibuni linatarajiwa kufunguliwa rasmi na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

DKT TIZEBA AWASILISHA TAARIFA YA ZAO LA KAHAWA KWA KATIBU MKUU CCM, USHIRIKA WAUNGWA MKONO KWA KAULI MOJA

0
0

Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo akitoa ufafanuzi kuhusu zao la kahawa wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini kwa Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Washiriki wa mkutano wa uwasilishaji wa mwenendo wa zao la kahawa wakifatilia kwa makini taarifa iliyowasilishwa na Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo mbele ya Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. 
Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi akizungumza mara baada ya Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo kutoa ufafanuzi kuhusu zao la kahawa wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. 
Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Wa pili kushoto) akiendesha kikao mara baada ya uwasilishwaji taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. Wengine ni Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo (Kushoto), Naibu waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba (wa kwanza kulia) na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (wa tatu kulia)
Wataalamu kutoka wizara ya kilimo wakifatilia mkutano wa uwasilishaji wa mwenendo wa zao la kahawa taarifa iliyowasilishwa na Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo mbele ya Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma.

Na Mathias Canal-WK, Dodoma


Katika vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania masoko ya Kahawa yamekuwa yakiendeshwa kwa mfumo wa ushirika na soko huria, Mfumo wa soko huria uliruhusu makampuni na watu binafsi kununua mazao moja kwa moja kutoka kwa wakulima pasipo udhibiti hali iliyopelekea kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo bei isiyokuwa na tija kwa mkulima, ubora hafifu wa mazao, ukwepaji wa kodi kwa wanunuzi na ukosefu wa takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo.


Kutokana na changamoto za mfumo wa soko huria, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli iliamua kurejesha ununuzi wa mazao matano ya kimkakati (Korosho, Tumbaku, Pamba, Kahawa, na Chai) kupitia vyama vya ushirika tangu mwaka 2016 ili kunufaisha wakulima, wanunuzi/wafanyabiashara na serikali.


Hayo yamebainishwa jana tarehe 14 Septemba 2018 na Mhandisi Mhe Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini kwa Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao makuu maarufu kama White House, Mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Makongoro Nyerere, Naibu waziri wa Kilimo, Mhe Omary Mgumba, wataalamu kutoka wizara ya kilimo akiwemo Naibu katibu mkuu Prof Sizya Tumbo, Mrajis wa vyama vya ushirika,vyama vya ushirika na wawakilishi wa wakulima kutoka maeneo yanayolima kahawa.


Katika taarifa hiyo Dkt Tizeba alieleza kuwa kamwe hawezi kuruhusu mtu mmoja mmoja au kundi la watu kuvunja ushirika ambao hivi karibuni umeanza kuimarika mahususi kwa ajili ya kumkomboa mkulima uamuzi ambao umebainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 katika sura ya pili ibara ya 22 ikisisitiza kuviimarisha na kuviwezesha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji wa thamani na biashara.


Alieleza kuwa zipo faida nyingi kwa mkulima anapouza kupitia ushirika na hasa vyama vya msingi ambazo ni pamoja na wakulima kuwa na nguvu ya pamoja ya kushauriana ili kupata bei nzuri na kunufaika na kilimo, wakulima kupata nguvu ya kuanzisha na kuendesha maghala na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yao, kuwawezesha wakulima kutunza ubora wa mazao kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya mazao husika.


Faida zingine ni kuwawezesha wakulima kupunguza gharama za uzalishaji kwa kuagiza pembejeo kwa pamoja, kuwezesha upatikanaji mazao ya uhakika na yenye ubora kwa wanunuzi, kuwezesha serikali za mitaa na serikali kuu kupata mapato yake stahiki kulingana na uzalishaji halisi, kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi za idara ya wakulima na uzalishaji; na kuwawezesha wanunuzi kufanya malipo ya mazao kwa kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa katika minada.


Aidha, Dkt Tizeba alisema kuwa mwenendo wa mauzo ya kahawa kwa msimu wa mwaka 2016/2019 ni mzuri ukilinganisha na misimu miwili iliyopita ya mwaka 2016 na 2017. Mauzo ya kahawa kwa mwezi Agosti 2018 ni mara mbili ya mauzo ya msimu wa mwaka 2017 ni mara nne ya msimu wa mwaka 2016. “Mauzo ya kahawa mwezi Septemba 2018 kwa mnada mmoja uliofanyika ni zaidi ya mauzo yote ya mwezi Septemba 2017 na ni sawa na mauzo yote ya kahawa kwa mwezi Septemba msimu wa mwaka 2016” Alisisitiza Dkt Tizeba


Kwa upande wake Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi akizungumza mara baada ya mjadala huo kutuama kwa masaa 8 kujadili namna ya kupata masoko ya mazao ya kilimo, urahisi wa upatikanaji wa mitaji, siasa ya kilimo kupitia ushirika na maandalizi ya miundombinu rafiki katika kilimo, alisema kuwa nchi ya Tanzania ipo katika mageuzi makubwa ya kimfumo na kimuundo hivyo mgogoro wa kiuchumi ni lazima ujitokeze kutokana na watu kulazimisha mazoea na haramu kuwa halali.


Alisema kuwa viongozi wote wa chama na serikali wanapaswa kuunga mkono jitihada za serikali kumkomboa mkulima kupitia ushirika, kujenga uchumi kupitia mshikamano lakini ushirika unaotakiwa ni ule wa Demokrasia wenye mizizi imara ili kuimarisha usalama wa nchi katika kilimo ambao unategemea wakulima wadogo.


Dkt Bashiru aliongeza kuwa ni lazima CCM kiwe chama kinachoingoza na kuisimamia serikali kwa kujenga utamaduni wa kujadiliana mambo muhimu ya kitaifa ili kukifanya chama hicho kuongeza imani maradufu kwa wananchi waliokiamini chama hicho na kukipa dhamana ya kuongoza Dola kupitia ilani ya ushindi ya mwaka 2015-2020.


Katika hatua nyingine ameitaka Wizara ya kilimo na Wizara zingine zote sambamba na taasisi za umma kutoa taarifa za mara kwa mara kwenye vyombo vya habari kuhusu yale yanayofanywa na serikali, kueleza mikakati ya serikali katika kuimarisha uchumi, sambamba na kutaja mafanikio yanayofanywa na serikali ili kuongeza uelewa kwa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipotoshwa.

POLEPOLE AHITIMISHA KAMPENI ZA UDIWANI VINGUNGUTI

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

 Kampeni za  udiwani kata ya Vingunguti Zimefungwa leo katika uwanja wa Msikate tamaa, ambapo pole pole alikuwa mgeni rasmi na kuwaeleza Waliofika kwenye mkutano huo kuwa chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti wake Dkt John Pombe Magufuli kimefanikiwa  mambo mengi ya maendeleo  ambapo hata wapinzani wamekosa hoja za msingi.

 "Watu wenye akili zao vijana na kama Kumbilamoto na akinamama mtatiro wameona Mazuri ya CCM na kuamua kumuunga mkono Rais, nami na waaomba  kesho siku ya jumapili tarehe16/2018 wakazi wa Vingunguti mpigieni kura Omary Said Kumbilamoto mapematu tuwetumeshinda Jina lake kwenye karatasi litakuwa nambambili"amesema

 Viongozi wengine waliomwombea kura Kumbilamoto ni pamoja na mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu , Bonna Kaluwa, wa Segerea, Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Dar es salaam Frank Kamugisha na Julius Mtatiro aliyejiunga na CCM akitokea CUF  na Wenyeviti saba wa Mitaa ya kata hiyo.

Katika hatua nyingine Diwani wa kata ya Buguruni kwa mnyamani Shukuru Dege leo amejivua uanchama wa Chama cha wananchi CUF na kujiunga na CCM, ambapo amesema ameamua kujiunga na CCM kwa kuwa CUF imepoteza mwelekeo na pia ameamua kuunga mkono serikali ya awamu ya tano.

Pamoja na hayo Mgombea wa kata hiyo Omary Said Kumbilamoto amesema amefurahishwa na wananchi wa kata hiyo kwa kumuunga mkono na kuwaomba tena kesho kumpigia kura kwa wingi iliaendeleekuwatumikia  akiwa CCM na kuwaletea maendeleo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwisho wa Kampeni za Mwisho Udiwani kata ya Vingunguti
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa , Humphrey Polepole akimnadi mgombea wa Udiwani wa kata ya Vingunguti Kupitia CCM , Omary Kumbilamoto
 Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Vingunuti Omary Kumbilamoto akiomba Kura kwa mara ya mwisho wakati w akuhitimisha kampeni
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kombo kupitia  Chama Cha Wananchi CUF ,Sharifu Mbulu akizungumza mara baada ya kurejea CCM katika mkutano wa kufunga kampeni Vingunguti
 Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akizungumza Jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika Mkutano wa kuhitimisha Kampeni Vingunguti
 Aliyekuwa Diwani wa Mtoni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam , Benard Mwakyembe akizungumza wakati wa Mkutano wa kuhitimisha Kampeni kat aya Vingunguti


Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images