Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI AZINDUA MAFUNZO YA VYUO VIKUU 12 VYA AFRIKA KUHUSU MBINU NA NAMNA YA KUTATHMINI ATHARI ZITOKANAZO NA MAAFA

$
0
0







Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa akiongea machache wakati wa ufunguzi wa semina ya wiki mbili ya washiriki wa kozi ya kimataifa kuhusu maafa inayondeshwa na Chuo Kikuu Ardhi ikiwalenga wanafunzi wa shahada za juu na watendaji wa taasisi za kiserikali, binafsi na mashirika ya kimataifa jijini Dar es Salaam. Washiriki wanatoka nchi 12 za Afrika na Taasisi ya World Food Programme (WFP) Wakufunzi wanatoka Vyuo Vikuu vya Afrika vinavyounda mwamvuli wa Periperi U, UNDP na WHO Kozi hiyo imefadhiliwa na UNDP, USAID, WHO na WFP. Kushoto ni Kaimu Naibu Mkuu Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
Sehemu ya washiriki wa semina ya kozi ya mafunzo ya mbinu za namna ya kutathmini athari zitokanazo na maafa wakifuatilia matukio wakati wa ufunguzi wa semina hiyo Dar es Salaam leo Septemba 10 2018.


Mkurugenzi wa Utafiti wa Majanga na Mratibu Mratibu wa Mradi wa Periperi kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch Dk Ailsa Holloway akiongea wakati wa ufunguzi wa semina ya kozi hiyo.
Sehemu ya washiriki wa semina ya kozi ya mafunzo ya mbinu za namna ya kutathmini athari zitokanazo na maafa wakifuatilia matukio wakati wa ufunguzi wa semina hiyo Dar es Salaam leo Septemba 10 2018.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (Taaluma), Profesa Gabriel Kassenga (katikati) akibadilishana mawazo na Makamu Mkuu wa ARU, Profesa Evaristo Liwa (kulia) baada ya ufunguzi wa semina hiyo Dar es Salaam leo Septemba 10 2018. Kushoto ni Kaimu Naibu Mkuu Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi.

Mgeni rasmi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina ya kozi ya mafunzo ya mbinu za namna ya kutathmini athari zitokanazo na maafa Dar es Salaam leo Septemba 10 2018.

Sehemu ya wanahabari wakifanya mahojiano na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (Taaluma), Profesa Gabriel Kassenga.

JAFO AISHUKIA MANISPAA YA ILALA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

$
0
0
1   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema katika eneo la Machinjio ya Vingunguti.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu katika kituo cha afya Mnyamani.
1.       Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akipata maelezo ya ujenzi wa Hospitali ya Kivule inayo jengwa katika Manispaa ya Ilala.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akipata maelezo ya ujenzi wa Hospitali ya Kivule inayo jengwa katika Manispaa ya Ilala.
Wadau wa Machinjio ya Vingunguti wakitoa maoni yao wakati wa ujio wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo.
 .....................................................................................

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amechukizwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Ilala.

 Jafo ameonyeshwa kukerwa wakati alipokuwa katika ziara ya Kikazi Mkoani Dar es salaam katika Manispaa ya Ilala. Katika Ziara hiyo,

Waziri Jafo ametembelea Machinjio ya Vingunguti ambayo hivi kalibuni ilitengewa fedha shilingi bilioni 8 kwa ajili ya kujenga machinjio ya Kisiasa pia ametembelea Kituo cha afya cha Mnyamani ambacho kimepewa fedha shilingi milion 500 pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Kivule.

 Jafo ameonyeshwa kutofurahishwa na kusuasua kwa miradi hiyo kwani ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti haujaanza hadi sasa licha ya kupokea fedha za awali zaidi ya shilingi bilion tatu zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

 Pia amebaini kasi ndogo ya ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha afya Mnyamani licha ya kupokea fedha tangu mwanzoni mwa mwezi Juni 2018. Kutokana na hali hiyo,

Waziri Jafo amemtaka Mkurugenzi Mpya wa Manispaa hiyo Jumanne Shauri kubadilisha kasi ya utendaji katika Manispaa hiyo ili fedha za Serikali ziweze kuleta mabadiliko yanayokusudiwa katika Manispaa hiyo.

 Aidha, Waziri Jafo amewashangaa viongozi na watendaji wa Manispaa hiyo kwa kutotoa fedha zozote kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Kuvule kitendo kilichosababisha ujenzi huo kusimama kwa zaidi ya miaka miwili wakati manispaa hiyo imekusanya zaidi ya shilingi bilion 44 katika mwaka wa fedha 2017/2018 kutoka vyanzo vyake vya ndani.

 Jafo ameelezea kwamba Serikali kuu imetenga fedha shilingi bilioni 1.5 katika bajeti ya mwaka huu 2018/2019 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Kivule lakini ameitaka manispaa hiyo kuacha kubweteka kwa kutegemea fedha za Serikali kuu pekee wakati manispaa hiyo ina uwezo mkubwa wa mapato.

Wananchi Mkuranga wanufaika na Kilimo

$
0
0
Na Emmanuel Massaka,Global ya jamii.

Wilaya ya Mkuranga ni moja ya wilaya saba zilizopo mkoani Pwani,ambapo  wakazi wake  hujishughulisha sana na shughuli za kilimo ili kujipatia kipato.

Wilaya ya Mkuranga inalima mazao  mbalimbali ya biashara na ya chakula ikiwemo Mihogo,Mbaazi, ,Korosho Machungwa Ufuta Mananasi pamoja na Nazi.

Pia wananchi wa Mkuranga wanategemea sana kilimo katika uchumi wao ambapo moja ya zao lililoshika kasi ni korosho,wanasomesha watoto kupitia korosho pamoja na kukuza pato la mtu mmoja mmoja.

Akizungumza wilayani Mkuranga mkoani Pwani Umri  Manage  mkulima wa mihogo na bamia alisema kuwa  kilimo kimemsaidia kwani ndio kinachoendesha Maisha yake"mimi nalima bamia linaniongezea kipato changu cha kila siku pia namsaidia mume wangu baadhi ya majukumu"alisema.

Manage  alitoa wito kwa wanawake wote nchini kuacha kujibweteka na kuacha utegemezi masala yake wajishughulishe katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
 Mfanyabiashara na Mkulima wa Bamia,Umri Manage akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana Kilimo.Wananchi wakivuna Mihogo   kama walivyokutwa na kamera yetu
Wananchi  wa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani wakivuna Mihogo   kama walivyokutwa na kamera yetu.Picha na Emmaniel Massaka wa Global ya jamii)

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA KIGOMA

$
0
0
Mradi wa Kuwawezesha vijana wa kike na wanawake kiuchumi kupitia Tasnia ya Urembo na Vipodozi ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wamemaliza mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Kigoma Yaliofanyika kwa wiki mbili kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Kigoma. Mafunzo hayo yaliyotolewa bure yamewanufainsa wanawake 20 kutoka Mkoani Kigoma na vitongoji vya jirani. 
 Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. Awamu ya pili walipata ujuzi jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi salama vya LuvTouch Manjano.
 Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba ili waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara zao wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea. Taasisi ya Manjano imefanikiwa kuwawezesha zaidi ya wanawake 500 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Kigoma na Unguja - Zanzibar
. Wengi wa wahitimu wa mradi wa Manjano Dream-Makers wamefanikiwa kuanzisha biashara zao na kuwa mawakala wa bidhaa za LuvTouch Manjano. Kwa mwaka huu taasisi ya Manjano wanajipanga pIa kumalizia kwa kuwawezesha kiuchumi na kutengeneza ajira kwa vijana wa kike na wanawake wa Mkoa wa Tabora..

MAHAFALI YA SEKONDARI YA JOHN BAPTIST YAFANA

$
0
0
Shule ya Sekondari ya wasichana ya John Baptist imefanya mahafali ya kidato cha nne na kushuhudia jumla ya wanafunzi 32 wakihitimu kidato cha nne.
Shule hiyo pia ilitumia mahafali hayo kuzindua rasmi masomo ya kidato cha tano na sita kwa wasichana.
Akizungumza kwenye mahafali hayo mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Chemba ya Biashara Tanzania Octa Mshiu alisema " wasichana ni nguzo kuu ya maendeleo ya Taifa letu, tunawaomba muende kutumia maarifa mliyoyapata hapa na muhimu zaidi ni kuendelea kukumbuka kuwa hakuna litakalowezekana bila ya kutilia maanani nidhamu na kufanya kazi kwa bidii".
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Jalia Mayanja alisema shule ya John Baptist imenuia kusaidia wasichana kufikia malengo yao kutumia elimu na kutilia mkazo nidhamu. Aliwakaribisha wazazi kutumia shule hiyo kwa ajili ya masomo ya watoto wao kwa kidato cha tano na sita yaliyoanzishwa. Shule hiyo inayotoa michepuo ya ECA, HKL na HGE na iko Boko Jijini Dar es salaam.

Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet

$
0
0
 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, Ibrahim Pius Mbwilo (28) ameshinda Sh 239,417,800 kupitia mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na kampuni ya M-Bet.

Mbwilo ambaye anasoma shahada ya Utawala wa Biashara (Business Administration) akiwa mwaka wa pili, alibashiri kiusahihi mechi 12 za ligi mbalimbali za ulaya. Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi alisema kuwa Mbwilo ambaye ni shabiki wa timu ya Simba na Chelsea ya Uingereza, amekuwa mshindi wa pili kupata fedha nyingi zaidi tokea kuanzishwa kwa droo ya Perfect 12. Mshindi wa kwanza alipata Sh 280 millioni.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwasaidia watanzania kubadili maisha yao kwa kutumia Sh1,000 tu. “Nawaomba Watanzania kuendelea kubashiri kwa kutumia michezo yetu,kuna nafasi kubwa ya kushinda na mpaka sasa tumepata jumla ya washindi 10 ambao wamefaidika na droo yao,” alisema Mushi.

Alisema kuwa Serikali imepata Sh 47 millioni kutokana na kodi kutokana na ushindi huo wa Mbwilo. Akizungumza baada ya kupokea hundi yake, Mbwilo alisema kuwa amefarijika sana kupata fedha hizo ambazo atazitumia kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo, kuwasomesha ndugu zake na kusaidia familia.

Mbwilo alisema kuwa pia atatumia fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza biashara yake ya kuuza matofali na kuanzisha biashara nyingine. Alisema kuwa yeye ni mtoto yatima na aliishi maisha ya mitaani huku akiokota taka na kuziuza kama mbolea (samadi) kwa akina mama ambao walikuwa wateja wake kwa lengo la kumsaidia.

“Niliishi mitaani, nilikwenda jalalani kutafuta matunda, taka, kutafuta taka na kuziuka kama mbolea, nilifanya hivyo baada ya kuachwa na mlezi wangu nikiwa kidato cha pili, naguswa na aina hiyo ya watoto yatima hiyo. “Tarehe 6 mwezi huu, nilitumia sh 1,000 kubashiri na kupata kiasi kikubwa cha fedha, namshukuru Mungu kwani wanaobashiri wengi, nitasaidia kituo cha watoto yatima kwa kunua magodoro, kuna kituo cha watoto yatima ambao hawana vitanda hata magodoro, nitafanya hivyo kwa sababu mimi mwenyewe nimetokea huko,” alisema Mbwilo.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa mchezo wa Perfect 12, Ibrahim Mbwilo (28) ambaye ameshindia Sh milioni 239.4. Mbwilo ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Chuo Kikuu Cha Iringa. Picha: Mpigapicha wetu 

MAKAMU WA RAIS AMALIZIA ZIARA YAKE WILAYA YA BUHIGWE MKOANI KIGOMA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiuandaa mti kabla ya kuupanda kwenye shamba la miti la Buhigwe, kushoto anayemsaidia Makamu wa Rais ni Meneja Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Kanda ya Magharibi Bw. Valentine Msusa
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye mti wa kumbukumbu alioupanda kwenye shamba la miti la Buhigwe katika kijiji cha Munzenze wilaya Buhigwe mkoani Kigoma.
  Sehemu ya miche laki mbili na nusu iliyopandwa kwenye shamba la miti Buhigwe mkoani Kigoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wanaoishi jirani na  shamba la miti la Buhigwe katika kijiji cha Munzenze wilaya Buhigwe mkoani Kigoma.
 : Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Mbunge wa Jimbo la Buhigwe Mhe. Albert Obama wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Munzenze, Buhigwe mkoani Kigoma.
  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubiwa wananchi katika kijiji cha Munzenze, Buhigwe mkoani Kigoma.
Sehemu ya Wakazi wa kijiji cha Munzenze waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KAMATI YA MAADILI YA TAIFA YAITAKA CHADEMA KUTEKELEZA MAAMUZI YALIYOTOLEWA NA KAMATI YA MAADILI JIMBO LA UKONGA.

$
0
0

Kamati ya Maadili ya Uchaguzi Ngazi ya Taifa, imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiendelee kutekeleza maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo la Ukonga yaliyokitaka chama hicho kusahihisha makosa yaliyotendeka na kuomba msamaha hadharani kwa kosa la kimaadili walilotenda.

Uamuzi huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jaji Mst. Mary Longway baada ya kikao cha kamati hiyo kupitia na kujadili rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Maadili Jimbo la Uchaguzi Ukonga, iliyowasilisha na Chadema Septemba 5, 2018 ikiitaka kamati hiyo itengue uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Jimbo.

Alisema kwa mujibu wa vielelezo vilivyoambatishwa katika Rufaa hiyo, Kamati ya rufaa imefikia maamuzi ya kuwa rufaa hiyo imewasilishwa nje ya muda wa saa 48 kinyume na maelekezo ya  kipengele cha 5.7 (b) cha Maadili tajwa.

“Rufaa iliyowasilishwa yenye Kumb. Na. CDM/ILALA/MAADILI/2018/28 ya tarehe 5 Septemba, 2018 iliyopokelewa Tume tarehe 7 Septemba..Imewasilishwa nje ya muda wa saa 48 kinyume na maelekezo ya  kipengele cha 5.7 (b) cha Maadili tajwa. Hivyo, Kamati inaelekeza kuwa mrufani aendelee kutekeleza maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo.”, alisema Jaji Mst. Longway.

Kwa mujibu wa uamuzi wa Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo la Ukonga, Chadema kimeonywa kuhakikisha kuwa kinafuata Kanuni na Taratibu za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 na kutekeleza maamuzi hayo ndani ya saa 48 tangu kutolewa na adhabu hiyo.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ukonga Jumanne Shauri mnamo Agosti 27, 2018 alipokea malalamiko na kupitia utetezi wa Chadema na kujiridhisha kuwa Chadema kilitumia kiongozi wa dini kumpigia kampeni mgombea wa chama hicho kinyume na kifungu cha 2.2 (k) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.

Msimamizi huyo wa Uchaguzi aliongeza kuwa “Dr. Makongora Mahanga akiwa kiongozi wa Chadema, siku ya kampeni tarehe 25/8/2018 alitumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji dhidi ya mgombea wa CCM, ikiwa pia ni kinyume na kifungu cha 2.2 (k) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015” aliongeza taarifa ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ukonga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Jimbo hilo” 

Mbali na uamuzi juu ya rufaa hiyo, Kamati hiyo pia imepitia barua ya tarehe 5 Septemba, 2018 iliyowasilishwa Tume tarehe 7 Septemba, 2018 kupinga maelekezo ya Kamati ya Maadili Jimbo la Ukonga yaliyokiagiza Chadema kuwasilisha ndani ya Saa 48 kuanzia tarehe 4 Septemba, 2018 vielelezo vilivyothibitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano na wataalamu wa lugha ya Kikurya ili kutoa maamuzi ya shauri husika.

Akizungumzia barua hiyo, Jaji Mst. Longway alisema baada ya kupitia vielelezo na kujadili barua husika, imeamuliwa kuwa rufaa hiyo imekosa sifa kwa kuwa hakuna maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Maadili Jimbo la Ukonga. 

Kutokana na jambo hilo, Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Taifa imekielekeza Chadema kuwasilisha vielelezo Kamati ya Maadili ya Jimbo la Ukonga kwa uamuzi kama ilivyoelekezwa na Kamati husika.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TAKWIMU ZA DENI LA SERIKALI KWA BENKI KUU YA TANZANIA

$
0
0

Benki kuu ya Tanzania (BoT) inakanusha taarifa potofu zinazozosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikidai kuwa Benki Kuu imechapisha noti zenye thamani ya shilingi trilioni 1.5 kwa ajili ya matumizi ya serikali.

Benki Kuu inauarifu Umma kuwa, taarifa hiyo sio sahihi na inalenga kuathiri imani ya Wananchi na wadau wa kimataifa kuhusu uthabiti wa fedha ya Tanzania. Aidha, Benki Kuu inawaasa Wananchi kuwa utoaji wa taarifa potofu kuhusu sekta ya fedha unaweza kuleta athari kubwa kwa mwenendo wa uchumi. Hivyo ni vyema Wananchi wajue yafuatayo kuhusu utoaji wa fedha kwa matumizi ya Serikali:

  • Mapato ya serikali hayawiani moja kwa moja na matumizi yake mwezi-hadi-mwezi. Kuna wakati mapato yanakuwa makubwa mfano miezi ya mwisho wa robo mwaka na wakati mwingine yanakuwa madogo. Kwa sababu ya kupishana kwa mapato na matumizi ya serikali, sheria imeruhusu serikali kuchukua mkopo wa muda mfupi kutoka Benki Kuu ili kuziba pengo pale linapotokea na kurejesha baadaye. Utaratibu huu unatumika duniani pote na hapa Tanzania sheria inairuhusu Serikali kukopa kutoka Benki Kuu kwa vipindi vifupi hadi ukomo wa asilimia 12.5 ya mapato ya ndani ya serikali ya mwaka uliotangulia.

  • Ili kupata picha halisi ya utekelezaji wa bajeti ya serikali na hali ya deni la Taifa, ni vyema kuangalia mwenendo mzima katika kipindi cha miezi kumi na mbili ya mwaka wa fedha husika, badala ya kuangalia mwezi mmoja mmoja, ambapo kuna mabadiliko ya kimsimu. Mtazamo wa mwaka mzima hutoa uhalisia wa mapato na matumizi, na ongezeko la deni lililohitajika kuwezesha utekelezaji wa bajeti ya serikali katika kipindi hicho. Taarifa ya kila mwezi ya uchumi ya Benki Kuu toleo la mwezi Julai inaonesha kwamba mkopo wa muda mfupi (overdraft) wa Benki Kuu kwa serikali uliongezeka kutoka shilingi bilioni 610.0 mwezi Mei 2018 hadi shilingi bilioni 1,937.4 mwezi Juni 2018, sawa na ongezeko la shilingi bilioni 1,327.4. Ongezeko hili halipaswi kuangaliwa kama tukio la mwezi Juni 2018 pekee kwani taarifa hiyohiyo inaonesha kuwa kati ya mwezi Juni 2017 na mwezi Mei 2018 overdraft ya Benki Kuu ya Tanzania kwa serikali ilipungua kwa shilingi bilioni 936.6, kutoka shilingi bilioni 1,546.6 hadi shilingi bilioni 610.0.  Kupungua huku kulichangiwa na mapato ya kawaida ya serikali pamoja na mikopo kutoka nje ya nchi.

  • Aidha, Benki Kuu haijachapisha noti mpya katika kipindi hiki, hata hivyo noti mpya, hazichapishwi kiholela ili kutoa pesa kwa serikali, bali huchapishwa kulingana na taratibu za kisheria. Kwa kawaida utengenezaji wa noti na sarafu huanza baada ya kukamilika kwa mchakato wa usanifu wa michoro, aina ya karatasi itakayotumika, alama za utambulisho wa nchi pamoja na alama za usalama. Na mara baada ya kukamilika kwa mchakato huo, Benki Kuu huandaa kiasi gani kitakachoweza kutosheleza mahitaji ya nchi kwa kipindi maalum kwa kuzingatia ukuaji wa pato la Taifa, Mfumuko wa bei na pia kufidia fedha zilizochakaa ambazo hazipaswi kurudi katika mzunguko na kiasi kilichobaki (buffer stock) ili kutosheleza kipindi chote cha mchakato wa uchapishaji.
Benki kuu inawaasa Wananchi kutotoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuupotosha Umma na kusababisha hofu na kupoteza imani juu ya uthabiti wa fedha ya Tanzania na badala yake wawe wanaomba kupewa taarifa kutoka Taasisi husika.

BENKI KUU YA TANZANIA

Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki

11 Septemba, 2018

WAZIRI DKT KIGWANGALLA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI

$
0
0
Jopo la Madaktari Bingwa wa MOI linalomhudumia Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla limemruhusu kutoka wodini baada ya kujiridhisha kwamba afya yake imetengamaa na anaweza kurejea nyumbani na atakuwa anakwenda hospitalini hapo  kama mgonjwa wa nje kwa ajili ya muendelezo wa matibabu yaliyosalia.

Jopo hilo la madaktari bingwa watano  wa kada za Mifupa, Usingizi na magonjwa ya ndani limefikia maamuzi hayo baada ya kumhudumia Dkt. Kigwangalla toka tarehe 12/08/2018 alipohamishiwa katika taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya kibingwa ya mkono wake wa kushoto baada ya kupata matibabu mengine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt.Respicious Boniface amemtakia kila kheri Dkt Kigwangalla katika kutekeleza majukumu yake ya kitaifa kwani ni muda muafaka wa kwenda kuwatumikia wananchi.

“Kwa niaba ya jumuiya ya Taasisi ya Mifupa MOI, tunakutakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu yako ya ujenzi wa Taifa. Ilikuwa ni  heshima kubwa kuwa nawe hapa kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja... Tunaamini umeridhishwa na huduma zetu na kama kuna mahali umeona mapungufu ni vyema ukatujulisha ili turekebishe” alisema Dkt Boniface. 

Dkt. Boniface amemueleza Dkt. Kigwangalla kwamba kwa kuwa yeye ni daktari itakua rahisi kubaini mabadiliko yoyote ambayo sio ya kawaida na hivyo kushauriana na madaktari wa MOI ili kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake Dkt. Kigwangalla ameushukuru uongozi wa Taasisi ya MOI, madaktari na wauguzi ambao wamekuwa wakimhudumia katika kipindi chote alipokuwa wodini.
“Nichukue fursa hii ya kipekee kuwashukuru watoa huduma wote kuanzia pale nilipopata tatizo na hadi kufika MOI, watanzania wote ambao mmekua mkiniombea na kunitembelea hapa hospitali baada ya kupata ajali, namshukuru Mungu afya yangu inaendelea vizuri sasa na nimeruhusiwa kwenda nyumbani” alisema Dkt Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla alipata ajali ya gari tarehe  4/08/2018 na kupata matibabu ya awali mkoni Manyara kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na baadae katika Taasisi ya Mifupa MOI.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt.Respicious Boniface (kushoto) akizungumza jambo na  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt.Respicious Boniface (kushoto) wakifurahia jambo na  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mara alipokuwa amekwenda kumuaga. Kulia ni Mkuu wa Wod hiyo, Happyness Mligo 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiondoka hospitalini kwa furaha kubwa baada ya kuruhusiwa na madaktari.
 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) 


Waziri Mkuu Majaliwa Afungua Mkutano wa Tano wa Wadau wa Lishe, atahadharisha ULAJI USIOFAA

$
0
0
WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesemalishe duni pamoja na ulaji usiofaa na mitindo ya maisha vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususan kwa vijana na watu wazima, ambao ndiyo nguvu kazi kwa Taifa.

“Ni jambo lisilopingika kuwa hatua za kukabiliana na magonjwa ya kusendeka (mfano matatizo ya moyo, saratani, kisukari na shinikizo kubwa la damu) zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kasi ya maendeleo yetu kwani gharama za matibabu yake ni kubwa mno; si kwa kaya zinazoathirika tu bali kwa Taifa zima.” Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 11, 2018), wakati akifungua mkutano wa tano wa wadau wa masuala ya lishe, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema lishe iliyozidi inadhihirishwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa yanayotokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha na ulaji usiofaa kama vile uzito uliozidi, viriba tumbo, shinikizo la damu pamoja na kisukari.

Amesema kasi ya ongezeko la magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza inapaswa kudhibitiwa kwa kuzingatia ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha. “Huu ni wakati wa kuangalia kwa pamoja kama jitihada zetu zinaleta matunda tunayotarajia.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya Taifa letu hivyo, uwepo wao katika mkutano huo unaonesha umuhimu wa kuimarisha ushiriki wa kila sekta, kila mdau ikiwemo sekta binafsi kwa nafasi yake katika kupambana na aina zote za utapiamlo.

Amesema ushiriki wa kila sekta ni wa muhimu kwa sababu hakuna sekta moja pekee inayoweza kuondoa tatizo la utapiamlo, pia ni vema kwa wadau hao wakajitathmini mmoja mmoja katika sekta zao kuona kama wanaelekea katika muelekeo sawa na mipango ya Serikali.

“Kwa kuzingatia hilo, ofisi yangu imeweka utaratibu maalum wa kuratibu utekelezaji wa kazi za lishe nchini, ambapo kamati ya Kitaifa ya Usimamizi na Ushauri kuhusu masula ya lishe nchini yaani High Level Steering Committee on Nutrition imeundwa ili kusimamia utekelezaji wa azma hiyo.”

Waziri Mkuu amesema kwamba watu wote wanatambua jitihada kubwa zilizowekwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau katika kupambana na matatizo ya lishe nchini, ambapo taarifa za wataalamu zinasema kuwa kwa sasa nchi inakabiliwa na aina mbili za utapiamlo yaani lishe duni na lishe iliyozidi au iliyokithiri.

Amesema walengwa wakubwa wa lishe duni ni pamoja na watoto chini ya miaka mitano, wanawake walio katika umri wa kuzaa hususani wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na vijana balehe (hususan wa kike). “Hii ni kwa sababu mahitaji ya virutubishi kwa ajili ya miili yao ni makubwa, ukilinganisha na ule unaohitajika na makundi mengine.”
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Benilith Mahenge akizungumza wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Dkt. Vicent Asey akizungumza wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".
Mwakilishi wa kundi la vijana Rika Balehe ambaye pia ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Notre Dame ya jijini Arusha, Bi. Najma Mohamed akiwasilisha maoni yao kuhusu masuala ya lishe mbele wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".


Mtaalamu wa Lishe kutoka UNICEF, Mauro Brero akichangia mada wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".

FARU WA SERENGETI KULINDWA KWA VIFAA MAALUMU

$
0
0

Na Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha.

Vita dhidi ya ujangili wa Faru, imeendelea kushika kasi na sasa Faru wa serengeti,wataanza kulindwa na vifaa maalum vya kielekroniki katika mradi ambao utagharimu zaidi ya 2.5 bilioni

Mradi huo,unafadiliwa na shirika la uhifadhi za Friedkin conservation Fund(FCF) kwa kushirikiana na shirika la Frunkfurt zoological society na kusimamiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini(TANAPA) na taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI).Mratibu wa Mradi wa uhifadhi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Philbert Ngoti alisema, vifaa hivyo ambavyo vitawezesha Faru wa Serengeti kuwa salama zaidi.

Alisema Faru wa Serengeti wanafungwa vifaa vya aina mbili,vya kielekroniki VHF transmitter ambacho kinawezesha kuwafatilia walipo kila siku na pia wanafungwa katika mguu wa kulia kifaa cha kisasa cha LoRa collar ambacho pia kinafatilia na kuonesha mienendo yao kila siku.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga, alisema zoezi la ufungwaji wa vifaa ya utambuzi na usalama kwa Faru ni muhimu sa katika kuimarisha vita dhidi ya ujangili.

Alisema zoezi hilo pia litasaidia kuongeza ufatiliaji wa faru,wanyama ambao wapo hatarini kutoweka duniani na sasa kila siku watajulikana wapo wapi, wanakula nini, wanaumwa ama wanamatatizo na hivyo kuchukuliwa hatua.
Meneja miradi wa shirika la Frunkfurt Tanzania, Rian Habuschagne, alisema katika mradi huo ambao ni mara ya kwanza kufanyika nchini, pia kumejengwa minara ya mawiliano katika maeneo yote ya mapito ya Faru.

Alisema zoezi la kufungwa vifaa hivyo linasimamiwa na watafiti na wahifadhi maarufu wa Faru barani Afrika, wakiongozwa na Pete Morkel na wanatarajia Faru wote wa serengeti kufungwa vifaa hivyo."hili zoezi linagharama kubwa tunawashukuru Friedkin Conservation Fund kwa msaada mkubwa wa fedha na helkopta, pia Frunkfurt ,TANAPA na taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI)"alisema.HIfadhi ya Taifa ya Serengeti ni moja ya maeneo yenye Faru wengi kwa sasa hapa nchini kutokana na kuimarishwa ulinzi

Picha naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Japhet Hasunga akiwa anashikiri zoezi la kuwafunga Faru wa serengeti vifaa vya ulinzi na mawasikiano
 
  Faru wa serengeti wakianza kulindwa na vifaa maalum vya kielekroniki katika mradi ambao utagharimu zaidi ya 2.5 bilioni

WAMBURA AWAONYA WAAMUZI, LIGI KUENDELEA WIKIENDI HII

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

LIGI kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena mapema wikiendi hii kwa timu zote 20 kuanza kukamilisha  mzunguko wa nne  wa ligi huku timu za Simba, Yanga na Azam ratiba zao za zikitafutiwa ratiba nyingine.

Akizungumzia ratiba ya ligi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi  Boniface Wambura amesema mzunguko wa nne wa ligi utaanza wikiendi hii baada ya kumalizika kwa ratiba ya michezo ya kimataifa ya kirafiki ya FIFA iliyochezwa tarehe 3 hadi 11 Septembe.

Amesema kutokana na kalenda ya FIFA, kuna baadhi ya mechi za Simba, Yanga na Azam zuki zilizoondolewa kwa ajili ya kupisha ratiba hiyo na wao kuwa na mechi pungufu baada ya  wachezaji wao kwenda katika timu za taifa na kupelekea kuhairisha mechi zao.

Wambura amesema kuwa, kwa timu zilizokuwa hazijakilimisha mzunguko wa pili na wa tatu watapangiwa tarehe ya kucheza mechi zao kwani kwa sasa kutakuwa na ligi ndefu ,mechi nyingi 380 na hiyo ni  kutokana na timu kuwa nyingi."timu ambazo hazijafanikiwa kufikisha idadi ya mzunguko wa mechi zao na watapangiwa ratiba ili kucheza mechi hizo, ila kwa sasa ligi itakuwa ndefu na itahitaji umakini mkubwa kutokana na timu kuwa nyigi,"amesema Wambura.

Akizungumzia kuhusu waamuzi wa ligi kuu kutokuwa makini katika maamuzi yao uwanjani, Wambura amesema kuwa waamuzi waliofanya makosa katia mzunguko wa kwanz ana wa pili tayari wameshawachukulia hatua na kuwataka waamuzi wengine kuchezesha mpira wa kutumia kanuni 17 za mpira.Wambura amesema, waamuzi wanatakiwa waangalie mechi zao zilizopita pamoja na kufanya mazoezi kwa sana na hii inatokana na idadi ya mechi na msimu huu watakuwa wamepata mechi nyingi za kuchezesha.

Amesisitiza kwa sasa wana waamuzi makini wakiwa wanasimamiwa vizuri na kamati ya waamuzi na hawatasita kwuachukulia hatua wale ambao watashindwa kuchezesha kwa sheria 17 za soka.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi  Boniface

QUEEN MLOZI AWAOMBA WAPIGA KURA KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOWALETEA MAENDELEO

$
0
0
Pichani kulia Katibu Mkuu UWT ,Queen Mlozi akimuombea  kura Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya ccm katika kata ya kizota mkoani Dodoma ndugu Jamal Paul. Katika Kampeni hizo Ndugu Mlozi amewaomba wakazi wa kata hiyo kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura na kumchagua kiongozi  atakae wafaa na kuwaletea maendeleo ya kweli na si maneno matupu.
katibu Mkuu Uwt Queen Mlozi akiagana na Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Antony Mavunde mara baada ya Mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani kwa tiketi ya  chama cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya kizota,uliofanyika jana.

SOMA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 12,2018


EMIRATES WAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA

$
0
0
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer (wa sita kutoka kushoto) akiwa na wanahabari waliohudhuria mkutano wake.Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam kuelezea mafanikio na jinsi wanavyoliendesha shirika hilo. Pembeni ni mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo, Tununu Kasambala. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwandishi wa TBC1 Stanley Ganzel akiuliza swali. Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania (hayupo pichani).

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer amesisitiza kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wanaosafiri na ndege zao katika mataifa mbalimbali duniani.

Pia amezungumzia fursa zilizopo kutokana na uwepo wa safari za ndege zinazofanywa na Emirates kati ya Tanzania na nchi nyingine ikiwemo ya usafirishaji mizigo ya kibiashara kutoka Dar es Salaam ambako kumekuwa kituo kikubwa cha kibiashara kwa Afrika Mashariki.

Alfajeer amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari katika mazungumzo yaliyolenga kujenga uhusiano kati yake na vyombo vya habari kuhusu masuala ya kibashara na maisha.

“Emirates nia yetu ni kuendelea kuhakikisha wateja wetu wanakuwa wenye thamani bora kadri inavyowezekana,” amesema.

Hivyo wanaendelea kuwa wabunifu katika kutoa huduma bora zaidi. “Kila siku tumekuwa tukiangalia njia za ubunifu ili kuboresha huduma zetu kwa wateja ikiwa pamoja na kurahisi safari zao kati ya eneo moja ya jingine.”

Kuhusu mizigo amesema mingi kupitia Emirates kuna mizigo mingi ambayo inasafirishwa kutoka Dar es Salaam.

“Wapo wanaosafirisha nyama ya mbuzi, kondoo na dagaa kutoka Tanzania. Hivyo uwepo wetu umetoa fursa za kiabishara,” amesisitiza.

Pia Alfajeer amesisitiza wanayo mikakati ya kuhakikisha wanaendelea kujiimarisha kibiashara.” Mkakati wa biashara wa Emirates daima tunazingatia fursa za biashara,” amefafanua.

Amezungumzia huduma za kipekee wanazozitoa kwa wateja wao. “Wakati wa safari wateja wetu wanapata vyakula vilivyo bora huku wakipata burudani za aina mbalimbali .

“Kwa watoto wanasafiri na Emirates nao tumezingatiwa mahitahi yao yakiwamo ya kuangalia game wakati wa safari.

“Pia mahitaji ya chakula kwa watoto wenye umri kati ya umri wa miaka 2 na 12 yanapatikana ndege za Emirates,” amesema.

Ameongeza kuwa “Menyu ya chakula inahusisha mapendekezo ya watoto ikiwa ni pamoja na chaguzi za mboga”.



Pamoja na mikakati yao ya kibiashara ameahidi wataendelea kushirikiana na Tanzania ili kuongeza uzoefu wa kibiashara.

TAWA yawakamata,pokonya baiskeli 60, Nyaya 100 za majangiri

$
0
0
 Afisa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA),Twaha Twaibu kushoto akiwa na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Magharibi-Msolwa Pori la Akiba Selous Augustine Ngimilanga wakiangalia baiskeli zilizotumiwa na majangiri kubebea wanyamapori.
  Ofisa Kampuni ya uwindaji wa Kitalii ya Mkwawa Hunting Safari Benson Kibonde akisisitiza jambo mbele ya Afisa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA),Twaha Twaibu kushoto na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Magharibi-Msolwa Pori la Akiba Selous Augustine Ngimilanga.
 Mofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi -Msolwa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Kijiji cha Msolwa Station Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea Shule ya Msingi Ukombozi kujionea mchango wa uhifadhi kutoka kampuni za uwindaji wa kitalii. 
 Mofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi -Msolwa wakiwa katika picha ya  na viongozi na Kijiji cha Msolwa Station Kilombero mkoani Morogoro baada ya kutembelea jengo la Ofisi ya Kijiji cha Msolwa Station linalojengwa kwa fedha kutoka kampuni za uwindaji wa kitalii. 
Afisa habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Twaha Twahibu akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa Kijiji cha Msolwa Station kinachopakana na Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi-Msolwa mkoani Morogoro.

NA RIPOTA WETU,KILOMBERO
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), katika kipindi cha mwaka 2017/18 imekamata baiskeli 60 za watuhumiwa wa ujangiri zikiwamo Nyaya zaidi ya 100 ndani ya Pori la Akiba Selous Kanda ya Kaskazini Magharibi- Msolwa.

Mkuu wa Kanda hiyo, Augustine Ngimilanga alisema pamoja na kukamata nyenzo hizo askari wa doria pia walikamata watuhumiwa wa ujangiri waliofunguliwa kesi 92 zinazoendelea Mahakama ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

“Watuhumiwa 18 wameshasomewa kesi zao na kuhukumiwa baadhi wamefungwa miaka mitatu na wengine miaka tisa jela,” alisema Ngimilanga na kuongeza:

“Tumeweka mkakati wa kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na ulinzi wa doria muda wote, hii ni pamoja na kukabiliana nao kabla hawajaingia na kufanya uharibifu,” alisema.

Ngimilanga alizitaja changamoto katika kukabiliana na ujangiri zinachangiwa na hali ya umasikini ya wananchi katika vijiji vinavyopakana na pori hilo.

“Baadhi ya wananchi wameona njia pekee ya kujipatia kipato ni kufanya ujangiri wa kuwinda wanyama na kuvua samaki kwenye mito ndani ya Pori la Akiba.

“Mbali ya kukamata tunaowakuta, tumeendelea pia kutoa elimu maeneo mbalimbali ya vijiji ikiwamo mikutano ya vijiji kwa kuwaelimisha na kuwapa mifano ya umuhimu wa kutunza haya maeneo,”alisema.

Alisema ili kuwasaidia kutoshiriki vitendo vya kijangiri wamekuwa wakiwapa elimu ya ujasiriamali wa ufugaji nyuki kwa ajili ya kuvuna asali na kuuza kwa lengo la kujiongezea kipato.


“Tumewasaidia kupata ufadhili wa mizinga kutoka kwa wawekezaji ili waendeshe shughuli za ufugaji kwenye msitu wa Magombela,” alisema Ngimilanga.

DC KAWAWA APIGA MARUFUKU WANAOSHIRI KUKARIBISHA MIFUGO KIHOLELA

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa akizungumza na watendaji na madiwani. 
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya watendaji na madiwani wa Bagamoyo wakifuatilia yaliyojiri kwenye kikao cha baraza.

NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa ametoa onyo kwa baadhi ya viongozi wa vijiji na watendaji wanaoshiriki kukaribisha wafugaji bila utaratibu na waache mara moja ,kwani ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani na migogoro baina yao na wakulima.

Aidha, amepiga marufuku wafugaji kuingiza mifugo yao kiholela wilayani humo pamoja na maeneo ya wawekezaji ili kuondoa migogoro inayojitokeza mara kwa mara.

Rai hiyo aliitoa ,wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na madiwani na watendaji wa halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo. 

Zainab alieleza ,wapo viongozi wanaokula na wafugaji suala linalosababisha ongezeko la mifugo kwenye maeneo yasiyo rasmi. 

Alisema kuwa, kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji kutokana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima ama wawekezaji hali inayosababisha mapigano.

“Nasema inatosha, wilaya kwasasa ina mifugo hiyo 300,000 yaani halmashauri ya Chalinze ina ng'ombe 240,000 na Bagamoyo ng'ombe 60, 000,"

Zainab alielezea, baaadhi ya viongozi wamekuwa wakijihusisha na uingizaji mifugo kwa kutumia njia ambazo ni kinyume cha sheria hali ambayo inasababisha madhara makubwa ndani ya jamii .

Hata hivyo alisema, NARCO inaanzisha maeneo ya wafugaji na inatenga heka 100,010 ambapo watakodishwa ndani ya miezi mitatu ng'ombe mmoja sh. 10,000 na ukiisha muda huo unaanza mkataba upya. 

Zainab alifafanua, njia hiyo itapunguza ongezeko la mifugo hiyo, hivyo madiwani na watendaji wampe ushirikiano kuwasiliana na wafugaji kuwashirikisha kwenye mpango huo. 

Mkuu huyo wa wilaya ya Bagamoyo, aliahidi kukutana na wafugaji kuzungumza nao kuhusu kuheshimu mipaka isiyowahusu na juu ya kupeleka mifugo yao NARCO.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu alisema wamepokea maelekezo hayo kwani anaamini ni semina elekezi kwa wataalamu ,madiwani, watendaji na wananchi ili kuhakikisha wanaleta maendeleo .

Nae diwani wa kata ya Yombo, Mohammed Usinga alisema changamoto ya kuingizwa makundi ya mifugo ni kero kubwa .

Aliwataka wakulima na wafugaji waheshimiane ili kuishi kwa amani. 


Usinga aliahidi kwa niaba ya madiwani wengine kumpa ushirikiano mkuu huyo wa wilaya ili kudhibiti kero hiyo.

SERIKALI KUKUZA UCHUMI KWA KUDHIBITI FEDHA ZA ZIADA KATIKA MZUNGUKO

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
FEDHA za ziada kuwepo katika mzunguko wa uchumi sio kigezo cha kukua kwa uchumi wa Taifa bali ni ishara ya Taifa hilo kushindwa kudhibiti ukuaji wa uchumi wake.
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Konde Mhe. Khatib Said Haji, aliyehoji kuhusu dhana ya kukua kwa uchumi nchini ilihali kuna upungufu wa uuzaji bidhaa nje na wananchi kukosa fedha.
Dkt. Kijaji alieleza kuwa matatizo ya kuwepo kwa fedha za ziada katika uchumi ni makubwa, hivyo inapongezwa hatua ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kudhibiti hali hiyo kwa manufaa ya ukuaji wa uchumi wa Taifa.
“Uchumi wa Tanzania unakua kutokana na hali halisi na takwimu zilizopo, ambapo katika Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) uliofanyika hivi karibuni ulieleza kuwa nchi nyingi mwanachama wa Jumuiya hiyo hazijafanikiwa katika ukuaji wa viashiria vya uchumi mkubwa isipokuwa nchi ya Botswana, Lesotho na Tanzania”. Alieleza Dkt. Kijaji.
Akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo kuhusu vigezo vinavyoainisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania, Dkt. Kijaji alisema kuwa vigezo kwa mujibu wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa ni ongezeko la pato la Taifa, ongezeko la pato la wastani la mwananchi kwa mwaka na ongezeko la uuzaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi.
Vigezo vingine ni kupungua kwa uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, utulivu wa bei za bidhaa na huduma, utulivu wa viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni,  kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni na kuongezeka kwa makusanyo ya Serikali kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo na huduma za kijamii.
Vilevile alieleza kuwa, uwekezaji unaofanyika katika nchi ni kigezo cha msingi cha ukuaji wa uchumi kwa kuwa huongeza kasi ya uzalishaji wa bidhaa na huduma, ajira, kipato cha mwananchi mmoja mmoja na pato la Taifa hivyo kupunguza umaskini katika jamii.
Naibu Waziri Dkt. Kijaji alibainisha kuwa, mchango wa Serikali katika ukuaji wa uchumi ni pamoja na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuwekeza zaidi kwenye shughuli zinazochochea ukuaji wa uchumi, kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji wa bidhaa na huduma nchini.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU, KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA PAMOJA NA BALOZI MMOJA IKULU YA CHAMWINO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. John Kiang’u Jingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Azizi  Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Kiang’u Jingu wa kwanza kulia, akifatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Azizi Ponary Mlima pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya wakila Kiapo cha Uadilifu mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Kiang’u Jingu wa kwanza kulia, akifatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Azizi Ponary Mlima pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya waki tia saini kwenye hati ya Uadilifu katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya akizungumza mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya tukio la Uapisho lililofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya pamoja na Balozi mteule Valentino Mlowola mara baada ya tukio la Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Septemba, 2018 amewaapisha viongozi watatu aliowateua hivi karibuni.
Viongozi walioapishwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) Dkt. John Kiang’u Jingu, Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Aziz Ponary Mlima na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) CP Diwani Athumani Msuya.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mawaziri, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Satano Mahenge.

Akizungumza baada ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Jingu kwa kushirikiana na viongozi wengine wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufuatilia usajili na utendaji kazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), na kuhakikisha yanafanya kazi kwa kuzingatia sheria ambazo pamoja na mambo mengine zinayataka kuendesha shughuli zao kwa uwazi hususani masuala ya mapato na matumizi ya fedha za ufadhili wa shughuli zake.

Mhe. Rais Magufuli amemtaka Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Mlima kusimamia vizuri ushirikiano wa Tanzania na Uganda hasa biashara na uwekezaji unaoendelea kati ya nchi hizi mbili na kuhakikisha Tanzania inanufaika na ushirikiano huo.

Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Diwani Athumani Msuya kuongeza kasi ya kushughulikia tatizo la rushwa nchini kwa kuhakikisha wote wanaokabiliwa na tuhuma za kujihusisha na rushwa wanafikishwa mahakamani na sheria inachukua mkondo wake.

Mhe. Rais Magufuli pia amemtaka CP Diwani kuungalia upya muundo wa TAKUKURU ili uweke bayana majukumu ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, na kuhakikisha watendaji wa taasisi hiyo wanaoonekana kutofanya kazi kwa tija na kujihusisha na vitendo vya rushwa wanachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuondolewa kazini na kufikishwa mahakamani.

“Nataka ukaisafishe TAKUKURU, kuna baadhi ya wafanyakazi wa TAKUKURU wanajihusisha na rushwa, kawaondoe, nataka kuona TAKUKURU inashughulikia rushwa kwelikweli hasa rushwa kubwakubwa, ukipita huko vijijini wananchi wanateseka sana, wananyanyaswa na kuna dhuluma nyingi sana, na tatizo kubwa ni rushwa”amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Viongozi walioapishwa na Mhe. Rais Magufuli pia wamekula kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela na baada ya viapo vyao wamemshukuru Mhe. Rais kwa kuwateua na wamemuahidi kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
12 Septemba, 2018
 

Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images