Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

KUTEMBELEA JUMLA YA MIRADI 55 YENYE THAMANI YA SH. 78,138,549,216 KATIKA ZIARA YA TARAFA KWA TARAFA

0
0

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya tarafa kwa tarafa ambayo anatarajia kuianza siku ya kesho katika wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuijenga Iringa mpya yenye maendeleo



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi anatarajia kuanza ziara ya kikazi kwa kuzitembelea tarafa zote 15 za wilaya zote 3 za mkoa wa Iringa lengo likiwa ni kufanya jumla ya mikutano 37 na kutembelea jumla ya miradi 55 yenye thamani ya shilingi 78,138,549,216 ambayo itausisha ukaguzi,uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mh: Hapi alisema kuwa anatarajia kutembea jumla ya kilometa 2,611 wakati wa ziara hiyo ya kikazi kwenye mkoa wote wa Iringa.

“Nitatembea tarafa tano za wilaya ya Mufindi ambazo ni Ifwagi,Malangali,Kibengu,Sadani na Kasanga,wilaya ya kilolo nitatembelea tarafa tatu ambazo ni Mazombe,Kilolo na Mahenge na kumalizia wilaya ya Iringa yenye tarafa saba ambazo ni Kalenga,Ismani,Pawaga,Idodi,Mlolo,Kiponzelo na Iringa mjini hapo ndio nitakuwa nimemaliza ziara yangu ya tarafa kwa tarafa” alisema Hapi

Hapi alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuijenga Iringa mpya katika dhana ya kuboresha utendaji wa serikali,kuimarisha sekta za kilimo,ujenzi wa viwanda,utalii,miundombinu,biashara,huduma za afya,maji,elimu,utatuziwa kero za wananchi na kutengeneza fursa zilizopo katika mkoa wa Iringa.

Aidha Hapi alisema kuwa atafanya mikutano mikubwa kumi na saba na midogo 20 ambapo mikutano kumi na tano itafanyika katika tarafa kumi na tano kwa kuambatana na wataalam mbalimbali kutoka idara zote za serikali na taasisi za UMMA.

“ Katika ziara yangu zitatoa sana fursa kwa wananchi kuuliza maswali na kutoa kero zao kwa lengo la kutatua matatizo ambayo yanawakumba wananchi na nitawaeleza muelekeo wa kujenga Iringa mpya” alisema Hapi

Hapi aliwataka viongozi wote wa mkoa kuanzia wakuu wa wilaya haviongozi wa chini kuiga mfano wake wa kwenda kutatua kero za wananchi na wasipofanya hivyo hatakuwa na msamaa kwa viongozi wote wazembe na ambao hawatatui kero za wananchi.

Naomba kumalizia kwa kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yangu na kuhumiza viongozi wanatakiwa kuwepo kwenye ziara yangu bila kukosa.

TANZANIA YAIKABIDHI SEYCHELLES UONGOZI WA MAPAMBANO DHIDI YA UTAKASISHAJI FEDHA HARAMU NA UFADHILI WA UGAIDI MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

0
0

Mwenyekiti wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), aliyemaliza muda wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia), akiwa Meza Kuu na Mwenyekiti mpya wa umoja huo, Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles, Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, wakati wa mkutano wa 18 wa Umoja huo uliofanyika, Mahe-Seychelles.
Mwenyekiti wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), aliyemaliza muda wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia), akipongezana na Mwenyekiti mpya wa umoja huo, Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles, Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, wakati wa Mkutano wa 18 wa Umoja huo uliofanyika, Mahe-Seychelles. Kulia ni Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Maafisa Waandamizi wa ESAAMLG aliyemaliza pia muda wake kutoka Tanzania, Bw. Onesmo Makombe. 
Wajumbe wa Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano huo ambao umeshuhudia Tanzania, ikikabidhi kijiti cha uenyekiti wa Umoja Seychelles, Mjini Mahe, nchini Seychelles. Wa nne kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Seychelles, Mhe. Danny Faure na wa sita kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa (kushoto) na Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, Bi. Mwanahija Almas Ali, wakifuatilia kwa makini Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) uliofanyika Mahe, Nchini Seychelles.
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi zaidi ya 19 za Afrika, wakifuatilia kwa makini Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) uliofanyika Mahe, Nchini Seychelles, ambapo Tanzania imeikabidhi Seychelles uongozi wa Umoja huo kwa kipindi cha mwaka mmoja ukiwa ni utaratibu wa nchi wanachama kupokezana uongozi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), aliyemaliza muda wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia), akizunguza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhi kijiti cha uongozi wa umoja huo, kwa Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles, Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, wakati wa Mkutano wa 18 wa Umoja huo uliofanyika, Mahe-Seychelles.

Rais wa Seychelles Mhe. Danny Faure (katikati), akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), aliyemaliza muda wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), wakati akitoa hotuba ya kukabidhi uongozi wa Umoja huo kwa nchi ya Seychelles.
Katibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Edwin Makamba, na Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu ya Tanzania -BOT, Zalia Mbeo, akifuatiwa na Bi. Tausi Abdallah, Mwanasheria BOT, wakifuatilia matukio mbalimbali ya Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) uliofanyika Mahe, Nchini Seychelles
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) akiwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BOT, Dkt. Bernard Kibesse (kushoto), na Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome (kulia), wakati wa Mkutano wa 18 Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG).

Makamu wa Rais wa Seychelles, Mhe. Vincent Meriton, akifungua Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), mjini Mahe, Seychelles ambapo nchi hiyo imekabidhiwa kijiti cha kuongoza Umoja huo kwa mwaka mmoja (2018/2019) ukiwa ni utaratibu wa nchi wanachama kukabidhiana uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja mmoja.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango, Seychelles



Na Benny Mwaipaja, WFM, Mahe, Seychelles

TANZANIA imekabidhi uongozi wa mwaka mmoja wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) kwa nchi ya Seychelles, huku ikijivunia mafanikio makubwa ya kuhakikisha kuwa nchi wanachama wa umoja huo zinakuwa na sera, sheria, taasisi na mifumo imara inayowezesha mapambano dhidi ya vitendo vya utakasishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekabidhi uongozi huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwa Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, wakati wa Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja huo, uliofanyika Mjini Mahe, nchini Seychelles na kushuhudiwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Danny Faure.

Miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi hicho cha mwaka mmoja, ni kufanyika kwa tathimini ya mifumo ya kudhibiti utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi wa nchi tatu wanachama wa umoja huo za Mauritius, Madagascar na Seychelles, na kwamba zoezi la kuzitathmini nchi nyingine mbili za Zambia na Malawi, linaendelea.

“Rasilimali za nchi zetu zinahitaji kutumika vizuri, kwa sababu zinapotumika vibaya zinapunguza uwezo wa nchi zetu kuchochea maendeleo haraka, pale zinapo hatarisha sekta yetu ya fedha, matumizi adili ya rasilimali hizi na usalama wa nchi zetu” alisema Dkt. Mpango

Aidha, Dkt. Mpango amesema kuwa utakasishaji wa fedha haramu unazuiwa kwa sababu unamadhara makubwa kiuchumi, kijamii na kiusalama kwa nchi wanachama.“Fedha ambazo zinakuja kuja tu hivi! Hujui kama zinakwenda kugharamia ugaidi, au ni fedha za wananchi wetu lakini wanazitorosha ambapo badala ya kuzitumia ipasavyo wanazitumia kufanya mambo haramu” aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika ESAAMLG, Dkt. Elliawony Kisanga amesema kuwa tangu umoja huo uanzishwe miaka 19 iliyopita, yamekuwepo mafanikio makubwa na kazi iliyopo mbele ya uongozi mpya ni kuanza na kuendelea kufanyika kwa tathmini ya mifumo ya udhibiti ya nchi za Zambia, Malawi na Tanzania.

Mwenyekiti Mpya wa ESAAMLG, Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, ameipongeza Tanzania chini ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kwa uongozi wake mahili na kuuwezesha umoja huo kutekeleza majukumu yake ipasavyo na msukumo wake utakuwa kuwezesha nchi wanachama kuendelea kusimamia utekelezaji wa sheria.

Aidha Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa ESAAMLG ulitanguliwa na Mkutano wa 36 wa Kikosi Kazi cha Maafisa waandamizi wa ESAAMLG, ambapo Bw. Onesmo Makombe alikabidhi kwa niaba ya Tanzania Uenyekiti wa Kikosi Kazi hicho kwa Bw. Philip Moustache wa Jamhuri ya Seychelles.

Tanzania ilipokea uongozi wa Umoja huo Septemba 7 mwaka jana wakati wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika uliofanyika Zanzibar, ikipokea majukumu ya uongozi huo kutoka nchi ya Zimbabwe ambapo Umoja huo unaundwa na nchi 18 ambazo ni Angola, Botswana, Eswatini, Ethiopia, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Rwanda, Seychelles, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

POLEPOLE AMNADI MWITA WAITARA ULONGANI ''A''

0
0
Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndg Hamphley Polepole (kulia) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga Ndg.Mwita Waitara katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Ulongoni A Jijini Dar Es Saalam
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam Bi Cathy Kamba akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndg Hamphley Polepole kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga Ndg.Mwita Waitara katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Ulongoni A Jijini Dar Es Saalam.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam Bi Cathy Kamba akimkaribisha Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndg Hamphley Polepole kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga Ndg.Mwita Waitara katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Ulongoni A Jijini Dar Es Saalam.
Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndg Hamphley Polepole (WAPILI TOKA KUSHOTO) akicheza nyimbo pamoja na wanamuziki wa Bendi ya TOT  katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Ulongoni A Jijini Dar Es Saalam.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (Kulia)akizungumza na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam Bi Cathy Kamba atika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Ulongoni A Jijini Dar Es Saalam.
Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndg Hamphley Polepole akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga Ndg.Mwita Waitara katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Ulongoni A Jijini Dar Es Saalam.
Wananchi wa Kata ya Ulongoni A Jimbo la Ukonga wakishangilia katika Mkutano wa Kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga Ndg.Mwita Waitara katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya Ulongoni A Jijini Dar Es Saalam. (Picha na Fahadi Siraji wa UVCCM)

RAIS DKT. MAGUFULI AWAHUTUBIA WANANCHI WA TARIME MKOANI MARA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tarime mjini mara baada ya kuwasili akitokea katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
 Kwaya ya Chuo cha Ualimu Tarime ikitoa burudani mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili Tarime mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanakwaya ya Chuo cha Ualimu Tarime mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano Tarime mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tarime vijijini wakati akitokea katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Tarime mjini mara bada ya kuwahutubia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondary Ingwe iliyopo Nyamongo Wilayani  Tarime Monica Benard kiasi cha Shilingi milioni tano kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya shule hiyo kutokana na vipaumbele vyao.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ingwe ya Nyamongo Tarime mkoani Mara Monica Benard akionesha kiasi cha Shilingi milioni tano alizokabidhiwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya maendeleo ya shule yao. Pia Rais Dkt. Magufuli aliendesha Harambee ya papo kwa hapo ambapo zilipatikana jumla ya Shilingi milioni 26 kwa ajili ya maendeleo ya Shule hiyo. PICHA NA IKULU

KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA

0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akifuatilia kwa makina taarifa ya mkoa wa Tanga kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmanuel Lwinga alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7,2018.
PIX 2
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya maafisa wa ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga, Gereza Kuu Maweni na gereza la Mahabusu Tanga  mara alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Maweni jijini Tanga akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.
PIX 3
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (mwenye “microphone” ) akizungumza na maafisa na askari wa vituo vya ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Gereza Kuu Maweni na Gereza la Mahabusu Tanga (hawapo pichani) kwa pamoja katika bwalo la Gereza Kuu Maweni Tanga alipofanya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmauel Lwinga, wa tatu kulia ni Mkuu wa Gereza Kuu Maweni Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Felichism Masawe na wa kwanza kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Marakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Hamis Mbwana.
PIX 4
Baadhi ya maafisa na askari  wa vituo vya ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga,  waliokusanyika kwa pamoja katika bwalo la gereza Kuu Maweni  wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani)  alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo leo Septemba 7, 2018. Katika hotuba yake CGP ametilia mkazo suala la kubadili mtazamo wa kiutendaji, kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kufanikisha majukumu yetu kama serikali na jamii nzima inavyotarajia kutoka kwetu.
PIX 5
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi askari wa magereza wa kike mkoani Tanga alipofanya ziara ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.
PIX 6
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) walioko mkoani Tanga alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.Picha zote na Jeshi la Magereza.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 11 katika ajali Jijini Mbeya

0
0

KESI YA AKINA AVEVA NA KABURU BADO NGOMA MBICHI

0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, upande wa utetezi umeomba iwafutie mashtaka aliyekuwa rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa kuiendesha kesi hiyo.

Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko ameyasema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba baada ya Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai kueleza mahakamani hapo kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba bado wanasubiri kwa muda wa wiki tatu, Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwani yupo katika harakati ya kuanzisha ofisi mpya jijini Dodoma hivyo hajapata muda wa kupitia jalada hilo.

Hakimu Simba alikubaliana na maombi ya Jamuhuri na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 14, mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utajibu hoja za upande wa utetezi.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka upo katika mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa washtakiwa zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo ili kesi iweze kuendelea kwa Evans Aveva na Godfrey Nyange.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.

MGODI WA BULYANHULU WATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA HALMASHAURI YA NYANG’HWALE KUCHANGIA VIFAA VYA UJENZI VYA MIL 500

0
0
Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, umetiliana saini Makubaliano na Halmashauri Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita kuchangia vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kusaidia umaliziaji wa ujenzi wa zahanati 32 za vijiji wilayani humo.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nyang’hwale na kushuhudiwa na Uongozi wa Mkoa wa Geita ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama na waandishi wa habari.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Luhumbi amepongeza Mgodi wa Bulyanhulu kwa kuchangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya zahanati hizo huku akimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri Nyang’hwale ahakikishe majengo hayo yanakamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.


“Hii inamaanisha katika kipindi cha miezi minne tunaweza tukajikuta tunatimiza malengo yetu ya kuwa na zahanati katika kila kijiji katika wilaya ya Nyangh’wale, kwa hiyo nipongeze Mgodi wa Acacia, nawashukuru sana huo ni uzalendo wameweza kuonyesha kwamba haya yanaweza kufanyika, wito wangu kwa uongozi wa wilaya, vifaa vitakuja kuwe na utaratibu mzuri wa ufuatiliaji, inawezekana tukienda vizuri wilaya ya kwanza kumaliza zahanati kila kijiji ikawa ni Nyang’hwale.” 

Mkuu huyo wa Mkoa wa Geita amepongeza pia kazi nzuri iliyofanywa na viongozi wa vijiji na wananchi kujenga maboma ya zahanati hizo za vijiji na kuonya viongozi wa vijiji vichache ambavyo bado havikamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati.


“Napenda niwapongeze pia viongozi wa vijiji ambao wameweza kuwahamasisha wananchi kuchangia nguvu zao kuchangia mawe, mchanga, kuchimba msingi na kuweka jitihada za kusimamia miradi hii, kwa hiyo wito wangu kwa mkurugenzi kama kuna vijiji watendaji hawafanyi kazi wang’oe mara moja tunataka viongozi wanaoleta matokeo.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyang’hwale Mariam Chaurembo ameahidi kufuatilia kwa karibu mradi wa ujenzi wa zahanati hizo ili zikamilike kwa wakati na kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya hasa za mama na mtoto na kutimiza lengo la serikali kusogezea wananchi huduma muhimu za afya kwenye vijiji vyao.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Japhet Simeo amebainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale ina vijiji 62, na katika vijiji hivyo kuna zahanati 14 na vituo viwili vya afya vya umma.


“Kwa idadi hiyo tunasema ni asilimia 25 ya wananchi wenye uhakika wa kupatiwa huduma za msingi za afya ndani ya vijiji vyao, na wengine asilimia 75 hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hali ambayo inahatarisha maisha hasa ya mama na mtoto kwa maradhi ambayo ni rahisi kuzuiliwa na kutibika huduma inapotolewa mapema.”


Naye Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi Benedict Busunzu amesema, “Leo tunafurahi kutiliana saini ya kuchangia vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 500 itakayochangia ukamilishaji majengo ya zahanati kwenye vijiji 32 vya Wilaya ya Nyang’hwale.


Kama wadau wa Maendeleo mchango wetu unaenda sambamba na malengo ya serikali katika sekta ya afya na kampeni ya kijiji kimoja zahanati moja jitihada zinazolenga kupunguza umbali mrefu wa kufuata huduma muhimu za afya.
Busunzu aliongeza kwamba mapema mwaka huu uongozi wa Wilaya ya Nyang’hwale uliutaarifu mgodi kuhusu jitihada inayozifanya ili kuboresha huduma za afya wilayani humo,


“Uongozi wa wilaya ulisema katika jitihada hizo rasilimali za ziada zinahitajika kutoka kwa wadau ili kukamilisha kampeni ya jitihada hizo za “kijiji kimoja, zahanati moja” ambazo inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wote wilayani humo wanafikishiwa huduma za afya kwa urahisi.”


Katika mpango wa serikali wa miaka mitano wa Maendeleo juhudi zinaendelea kuongezwa kuboresha upatikanaji huduma za kuzuia na kutoa matibabu kwa wakati. mkakati wa uwajibikaji wa kampuni ya Acacia kwenye jamii unalenga kuchangia katika maendeleo ya jamii endelevu ambazo zina miundombinu muhimu ya kijamii kama huduma za afya, maji, na usafi wa mazingira.


“Mchango huu ambao Mgodi wa Bulyanhulu unatoa kwa ajili ya kampeni “kijiji kimoja zahanati moja” katika Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita, unatanguliwa na michango mingine ambayo tumeshaitoa kama vile fedha kwa ajili ya miradi ya miundombinu ya afya Mkoani Shinyanga ambako mgodi umetoa dola milioni Moja za Marekani sawa na shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Bugarama na zahanati katika kijiji cha Kakola, katika wilaya ya Msalala.


Tunatumaini kwamba baada ya kukamilisha, kituo cha Bugarama ambacho ujenzi wake unaendelea kitakuwa na hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya na kutoa huduma muhimu ya matibabu ya akina mama na watoto kwenye jamii ya watu zaidi ya 150,000.” Alifafanua Busunzu.

Waliokaa kutoka Kushoto: Meneja Mahusiano Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi Zumbi Musiba, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale Bi Mariam Chaurembo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyanghwale Aloyce Mussa Lumambi, Waliosimama kutoka kulia Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale Tiberus George Rweyemamu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Fabian Yinza, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi, Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Hamim Gwiyama, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Japhet Simeo, wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale wakati wa zoezi la kusaini hati za makubaliano ya mchango mgodi wa Bulyanhulu wa kumalizia ujenzi wa zahanati za vijiji 32 vya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale.

Kutoka Kushoto: Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale Bi Mariam Chaurembo katika ukumbi wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Mkoani Geita baada ya kusaini na kubadilishana hati za makubaliano ya mchango wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati za vijiji 32 vya Halmashauri ya Nyanghwale, Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyanghwale Aloyce Mussa Lumambi, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi, Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Hamim Gwiyama, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Japhet Simeo.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu na Buzwagi Benedict Busunzu akizungumza wakati wa zoezi la utiaji saini makubaliano

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Mariam Chaurembo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale Bi Mariam Chaurembo akizungumza

Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Hamim Gwiyama, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi Bwana Benedict Busunzu.

Kutoka kulia Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale Tiberus George Rweyemamu, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Japhet Simeo na Msaidizi wa Katibu Tawala Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Geita Herman Matemu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi akiwa Nyanghwale kwenye hafla ya utiaji wa saini

Picha ya Pamoja kutoka kushoto: Katibu Tawala wa Halmashauri ya Nyang’hwale Fabian Yinza, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale Bi Mariam Chaurembo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyang’hwale Aloyce Mussa Lumambi, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria Mkoa wa Geita Sarah Mwangole, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu, Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita Sania Mwangakala, Katibu Tawala Mkoa wa Geita Dennis Bandisa, Msaidizi wa Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Geita Herman Matemu, Meneja Mahusiano Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi Zumbi Musiba, na Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu William Bundala nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kusaini hati za makubaliano ya mchango wa kumalizia ujenzi wa zahanati za vijiji 32 vya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale

Kushoto: Mganga Mkuu Mkoa wa Geita Japhet Simeo akisalimiana na Meneja Mahusiano Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi Zumbi Musiba

BODI YA PAMBA TANZANIA YATEMBELEA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA

0
0
Na Shani Amanzi,

Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi Bodi ya Pamba Tanzania Ndg.James Shimbe amesema wakulima wakiweka kipaumbele kulima zao la pamba litaleta kipato kikubwa kwa Taifa kwani zao la Pamba nje ya nchi linauzwa kwa 80% na 20% ndani ya nchi ambapo mahitaji makubwa yanaenda Viwandani. 
 
Shimbe aliyazungumza hayo alipokuwa kwenye Kikao kazi cha Baraza la Madiwani tarehe 31/9/2018 kama mgeni mualikwa kuelezea zao la Pamba linavyoweza kulimwa katika wilaya ya Chemba kwa kuwa ardhi iliyopo inafaa kwa kilimo hicho.

Aidha Shimbe amesema “nchi yetu inapata mapato makubwa kwa kuuza pamba nje ya nchi katika nchi za China, India, Pakistan na Indonesia na tunapaswa kuuza kwa wingi katika Viwanda vyetu ili vitengeneze nguo na kuepuka nchi kuagiza nguo za mitumba nje ya nchi kama ilivyo sasa ”.
Shimbe amesema, uzalishaji wa pamba kwa ekari moja ni kilo 560-912 katika mikoa ya Iringa, Manyara,Tanga,Singida ,Katavi,Geita ,Mwanza, Shinyanga na tunapaswa kuzidi kuwahimiza wakulima wetu walime pamba kwa wingi kwani Pamba ni dhahabu nyeupe inayohitajika kwa wingi zaidi katika soko la dunia.

“Katika utafiti tulioufanya katika wilaya ya Chemba kilimo cha pamba tutaanza kuwawezesha wakulima wa kata ya kidoka, gwandi,Lahoda, na mrijo kwa kuwapatia pembejeo za kilimo cha pamba na msimo wa kilimo unaanza mwezi wa novemba 2018 na mvuno ni mwezi wa aprili, 2018”. Alisema Ndg. Shimbe.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amewapongeza wageni kutoka bodi ya Pamba kwa kuja wilayani Chemba na ameahidi watashirikiana na Wataalam wa kilimo, Wahe. Madiwani na Wananchi ili kuweza kurahisisha kuwaelimisha wakulima umuhimu wa zao la pamba ili kuwainua .

“Tunaelewa katika kilimo kunachangamoto ikiwemo uwezo mdogo wa vyama vya ushirika,mabadiliko ya tabia nchi,kuwepo Maafisa ugani wachache ,wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo na mtazamo hasi wa zao la pamba lakini nawaahidi tutajitahidi kukabiliana nazo ili uzalishaji wa zao la pamba uwe tegemeo kubwa kama ilivyo zao la alizeti”aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Mashimba.

JKCI yaibuka mshindi wa kwanza katika utoaji wa huduma ya upimaji na kutoa elimu ya magonjwa ya moyo katika mkutano wa wahandisi

0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeombwa kuwafikia wananchi wengi zaidi wakiwemo wafanyakazi ili waweze kufanyiwa vipimo vya moyo pamoja na kupata elimu ya jinsi ya kuepukana na ugonjwa huo. Ombi hilo limetolewa leo na washiriki wa mkutano wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee uliopo jijini Dar es Salaam.

Wahandishi hao pia wamewashauri wafanyakazi kutenga muda wa kupima afya zao na kufanya mazoezi ambayo yatawasaidia kiafya. Mhandisi Alex Kalanje alisema kama Taasisi hiyo itawafikia watu wengi zaidi kwa kwenda katika mikusanyiko mbalimbali kutawasaidia watanzania wakiwemo wafanyakazi ambao kutokana na majukumu yao ya kazi wanakosa muda wa kwenda kupima afya zao kupata huduma ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo.

“Wafanyakazi wengi wanakosa muda wa kwenda Hospitali kupima afya zao, lakini kama kutakuwa na utaratibu wa kuwepo kwa wataalam wa afya katika mikutano mbalimbali kutawasaidia kupata muda wa kupima kirahisi zaidi kuliko wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi”, alisema Mhandisi Kalanje..

Kwa upande wake Mhandisi Dkt. Gemma Modu aliwashauri watanzania kutenga muda wa kupima afya zao kwa kufanya hivyo kutawasaidia kujuwa kama wanamatatizo au la na kama wanayo wataweza kupata matibabu mapema.

Aidha Dkt. Gema pia aliwasihi kinamama kubadilika na kuhamasisha familia zao kwenda kupima na ikifika muda wa kupima waende wao na waume zao pamoja na watoto.

Akizungumza wakati wa kufungwa kwa mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim James Yonazi aliipongeza Taasisi ya Moyo kwa huduma ya kijamii iliyoitoa ya upimaji na kutoa elimu ya lishe pamoja na mazoezi na kusema kuwa kazi waliyoifanya ni kubwa.

Taasisi hiyo ilishika nafasi ya kwanza ya mtoa huduma za kitaalam kwa kutoa huduma za upimaji wa vihatarishi vya magonjwa ya Moyo, ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, elimu ya lishe bora na mazoezi, kueleza kwa kina huduma zinazotolewa na Taasisi, kutoa dawa bure kwa watu waliokutwa na matatizo ya moyo na kutoa rufaa ya moja kwa moja kwa wagonjwa waliokutwa na matatizo ya moyo yaliyohitajika kupewa rufaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea cheti cha nafasi ya kwanza ya mtoa huduma za kitaalam kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa kutokana na Taasisi hiyo kushiriki katika kutoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwenye mkutano wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dorica Burengelo akimpima ugonjwa wa kisukari mhandisi aliyetembelea banda la hiyo kwa ajili ya kupima afya na kupata elimu ya lishe na mazoezi wakati wa mkutano wa 16 wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophylly Mushi akimpima msukumo wa damu (PB) mhandisi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima afya na kupata elimu ya lishe na mazoezi wakati wa mkutano wa 16 wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hussein Mube akimpa ushauri wa kiafya mhandisi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima afya na kupata elimu ya lishe bora na mazoezi wakati wa mkutano wa 16 wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa upimaji afya, utoaji wa elimu ya lishe bora na mazoezi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kupokea cheti cha kushika nafasi ya kwanza ya mtoa huduma za kitaalam kwenye mkutano wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakiwasaidia kuvuka kwenye kivuko wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Trafiki akisikmamisha magari ili kurughusu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakiwasaidia kuvuka kwenye kivuko wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakikabidhi mfano wa cheki yenye tahamani ya shilingi milioni tano kwa mwalimu Mkuu wa wa shule ya msingi Upanga Ailika Yahya mara baada ya shule hiyo kuibuka mshindi katika shindano hilo lililoshirikisha wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba katika shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde akimkabidhi zawadi za mshindi wa kwanza Mwanafunzi wa shule za msingi ya Maktaba Francisco Salvatory kwa mwakilishi wake Elisha Msafiri katika hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya Upanga Ailika Yahya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti pamoja na majaji wengine wakichambua picha za wanafunzi walioshinda katika shindano hilo.Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde akizungumza katika hafla hiyo kushoto aliyekaa ni Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Upanga wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Mavunde. Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Maktaba wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Mavunde.




NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kujali usalama wa wanafunzi kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya uchoraji kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa huo.Amesema tangu mwaka 2013, kampuni hiyo ilipoanzisha kampeni ya usalama barabarani ambayo imekuwa na lengo la kupunguza ajali za usalama barabani na sasa mafanikio yanaonekana.

“Tangu ilipozinduliwa kampeni hii tunaona kuna mafanikio na katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya wanafunzi 9,152, wamepewa mafunzo usalama barabarani ikiwamo kushiriki katika michoro hongereni sana Puma.
“….na la kufurahisha zaidi ni hatua ya kuzishirikisha na shule za wanafunzi wenye ulemavu ikiwamo ya shule mojawapo ya Mkoani Ruvuma,” amesema Mavunde.

Awali Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwaelimisha wanafunzi kuhusu usalama barabarani tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kampeni hiyo.“Tangu ilipoanza kampeni hii tumetoa mafunzo kwa wanafunzi wapatao 68,000 katika shule 63 za mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Geita, Kilimanjaro na Ruvuma,” amesema .

Alisema madhumuni ya kuwahusisha wanafunzi wa shule za msingi imetokana na kuamini kwamba mafunzo ya salama barabarani yanatakiwa kutolewa kwa watto wadogo ili waweze kukua wakiwa na uelewa kuhusu usalama barabarani.
“Tumeamua kuweka mkazo katika mafunzo haya kwa wanafunzi tukielewa kuwa wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani. Na kuyafanya mafunzo haya kuwa kipaumbele chetu cha kwanza,” amesema Philippe.

Meneja huyo alisema kuwa kwa mwaka huu wamefundisha wanafunzi 9,152 wa shule za msingi 16 za Mkoa wa Dar es Salaam na Ruvuma pamoja na kuendesha mafunzo hayo kwa shule za walemavu na kuwa kampuni ya kwanza ya mafuta kuendesha mafunzo hayo.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka mwanafunzi Francisco Salvatory wa Shule ya Msingi Upanga ambaye alinyakua kitita cha Sh 500,000 wa pili ni Magreth Andrew wa Shule ya Msingi Maktaba, ambaye alivyakua kitita cha Sh 300,000 na wa tatu ni pia alikuwa mwanafunzi wa shule ya Msingi Upanga ambaye alizwadiwa Sh 150,000 .

BENKI KUU YATOA MAFUNZO KWA WABUNGE

0
0
 Kushoto ni Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia kwa makini maelezo ya mwezeshaji katika Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza katika Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa Wabunge wote yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wabunge wakifuatilia Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa Wabunge wote yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.

NITAENDELEA KULINDA NIDHAMU KWENYE VIKAO VYA BARAZA LA MADIWANI-MEYA TANGA SELEBOSI

0
0
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Selebosi Mustapha akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo Mustapha Selebosi MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza katika kikao hicho Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi kulia akisistiza jambo kwenye kikao hicho kushoto ni Naibu Meya Mohamed Haniu NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Mohamed Haniu akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi Sehemu ya baadhi ya madiwani wakifuatilia kikao hicho Sehemu ya Madiwani wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho Madiwani wakifuatilia hoja mbalimbaliMSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mustafa Seleboss amesema atahakikisha anaendelea kulinda nidhamu ndani ya vikao vya baraza la madiwani ili kutoa mwanya kwa madiwani kujadili kwa kina maslahi ya wananchi badala ya kuingiza itikadi za kisiasa.

Hayo ameyazungumza mbele ya waandishi wa habari baada ya kumalizika kikao hicho cha kufunga mwaka baada ya madiwani wanne toka chama cha wananchi [CUF] kuruhusiwa kuingia katika baraza hilo kutokana na kusimamishwa kutokushiriki vikao hivyo kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Aidha alisema mbali ya kuweka mbele maazimio ya kikao hicho cha kufunga mwaka 2017/2018 na kuelekea kuanza mwaka wa 2018/2019 bado alisisitiza swala la nidhamu ndani ya mijadala ya vikao hivyo iliilete tija kama azma ya madiwani wote ya kupeleka maendeleo katika kata zao.

Seleboss alisema madiwani hao walisimamishwa kwa mujibu wa kanuni hivyo kutokuwepo ndani ya vikao kadhaa iwe fundisho kwao na wengine kutokana na kutokushiriki vema katika jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wao.

“Hatufanyi kazi kwa kumuonea mtu bali tunaangalia kanuni ndizo zinazotuongoza hivyo madiwani wenzangu tuunganeni kwa pamoja katika harakati za kusukuma maendeleo katika kata zetu ……na niweke wazi humu ndani tulumbane kwa hoja na sio siasa”Aalisema Seleboss.

Katika hatua nyingine Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tanga Ruth Mkisi aliwaapisha madiwani wawili Omari Mzee kata ya Makorora na Jumaa Ramadhani kata ya Mabokweni ambao walishinda katika uchaguzi mdogo uliomalizika Agosti 12.Kwa uapande wake Diwani wa kata ya Duga Khalid Rashid alisema ni wakati wa kwenda kuwawakilisha wananchi wake katika baraza hilo kiukamilifu ili kuweza kufikisha kero zao na kuwaletea maendeleo.

Rashid alisema walizuiliwa kwa kutokuhudhuria vikao vitatu kwa mujibu wa Meya jambo ambalo liliwalazimu kukaa nje ya baraza hilo takriban mwaka mmoja huku wakishindwa kufikisha kero za wananchi wao.“Tuliambiwa tumepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vitatu lakini tulikaa nje ya baraza hili mwaka mmoja sasa tangu Agosti 31 mwaka jana lakini nashukuru tumerudi wakati umewadia wa kuwatetea wananchi wa kata yangu na kupigania maendeleo yetu”Alisema Rashid.

Nae Diwani wa kata ya Msambweni Abdurahman Hassan alisema wamerejea kwenye kikao hicho na si muda wa kumtafuta mchawi huku jambo la msingi kuangalia maendeleo ya kata hiyo na kuwawakilisha wananchi wake vizuri katika baraza hilo.

Madiwani ambao walisimamishwa ni pamoja na Abdurahman Hassan kata ya Msambweni,Khalid Rashid kata ya Duga,Seleman Mbaruku kata Majengo,mwasaju Juma kata ya Mabawa na Rashid Jumbe ambae hakuwezakufika kutokana na kuwa na kesi mahakamani ya kuvuliwa uwanachama.

WALIOFARIKI MBEYA KWA AJALI WAFIKIA 15

0
0
Na Emanuel Madafa,Michuzi Blog , Mbeya

WATU 15 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matano ikiwemo gari dogo la abiria aina Hiace katika eneo la mteremko wa mlima Igawilo Kasoko Nje kidogo mwa Jiji la Mbeya.

Akizungumza Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Mbeya, Petro Siame, alisema hospitali hiyo jana ilipokea miili ya marehemu 13 na majeruhi 15 ambao kati yao wanne walitibiwa na kuruhusiwa.

Siame amesema kuwa alisema, kuwa majeruhi wawili walipoteza maisha wakati wakipatiwa matibabu hivyo idadi ya vifo kuongezeka na kufikia 15 ambapo miili ya watu 12 imetambulika.

‘Jana tulipokea miili ya watu 13 na majeuri 15 lakini kati ya hao wanne wamepatiwa matibabu lakini wawili wamefariki wakati wakiendelea na matibabu hivyo kufanya vifo kuwa 15 na mmoja yupo chumba cha wagonjwa mahututi ICU” alisema Siame .Amesema, majeruhi ambao wanaendelea kupata matibabu wengi wao wamepata majeraha makubwa vichwani na kuvunjika kwa mifupa ya viungo mbalimbali vya mwili ikiwemo mikono na miguu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, akizungumza mara baada ya kuwatembea majehurui waliolazwa katika Hospital ya Rufaa alisema watu 15 kupoteza maisha ni tukio kubwa sana tena kwa ajali ya aina ile ile licha ya serikali kuendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo.

Mashuhuda wa ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne katika eneo la Mteremko wa Igawilo wakitazama moja ya Roli lililopata ajali katika eneo hilo la tukio.

Muuguzi Mkuu Hospital ya Rufaa Kanda ya Mbeya Petro Seme akizungumzia taarifa ya Majeruhi wa ajali.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) akimpa pole mmoja wa madereva wa malori kampuni ya (Asasi) Sabu Mohamed ambaye amelazwa katika hospital ya rufaa Mbeya anako patiwa matibabu.
Mashuhuda wa ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne katika eneo la Mteremko wa Igawilo wakitazama moja ya basi dogo la abiria lililopata ajali katika eneo hilo la tukio.

MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI KIGOMA TAYARI KWA ZIARA YA SIKU 4

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 4. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na vijana wa Skauti mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku 4.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi vya ngoma vikitoa burudani wakati wa mapokezi mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku 4. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SIMIYU.SEPTEMBA 8,2018

0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.wengine ni Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia na watoto Ummy Mwalimu,Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthon Mtaka,Mbunge wa Jimbo la Bariadi Andrew Chenge,Mbunge wa Chemba Juma Nkamia.hafla hiyo imefanyika Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.wengine ni Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia na watoto Ummy Mwalimu,Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthon Mtaka,Mbunge wa Jimbo la Bariadi Andrew Chenge,Mbunge wa Chemba Juma Nkamia.hafla hiyo imefanyika Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mojawapo ya wgonjwa aliyepumzishwa katika chumba cha mapumziko katika hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kuifungua rasmi hospitali hiyo,Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi mara baada ya kuifungua rasmi hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018. 

   Sehemu ya jengo la wagonjwa wa nje (OPD)la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu lililofunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.
. PICHA NA IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,jinsia na watoto Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthon Mtaka kabla ya kufuangua jengo la wagonjwa wa nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.hafla hiyo imefanyika Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi kabla ya kufungua rasmi jengo la wagonjwa wa nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.hafla hiyo imefanyika Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.

 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,jinsia na watoto Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.hafla hiyo imefanyika Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Septemba, 2018 ameendelea na ziara yake katika Kanda ya Ziwa ambapo ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Lamadi na kufungua barabara za Mji wa Lamadi katika Wilaya ya Busega, amefungua jengo la wagonjwa wa nje (OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, na ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Maswa – Bariadi. 

Mradi wa maji wa Lamadi utakaozalisha lita Milioni 3.3 za maji kwa siku ambayo ni mara mbili ya mahitaji ya lita Milioni 1.8 ya wakazi wa mji huo kwa sasa, utatatua kero ya miaka mingi ya uhaba wa maji kwa wakazi hao ambao kwa sasa wanapata maji kwa asilimia 23 tu ya mahitaji yao. 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa mradi huo ambao umepangwa kukamilika mwezi Mei 2019 utagharimu shilingi Bilioni 12.83 na ni sehemu ya mpango wa uboreshaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira wa ziwa Victoria (LV WATSAN) unaotekelezwa katika miji ya Mwanza, Musoma, Bukoba, Magu, Misungwi na Lamadi kwa gharama ya shilingi Bilioni 276, fedha ambazo zimetolewa kwa mkopo nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Serikali ya Tanzania. 

Ujenzi wa barabara za Mji wa Lamadi zenye jumla ya kilometa 6.26 umegharimu shilingi Bilioni 9.192 ambapo barabara hizo zimewekewa taa, mifereji, njia za waenda kwa miguu na eneo la kuegesha magari lenye ukubwa wa meta 900. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa pamoja na barabara hizo Serikali itajenga kituo cha mabasi na kilometa nyingine 1.5 ya barabara, kununua gari la taka na kuandaa ramani ya mpango mji katika Mji wa Lamadi kwa gharama ya shilingi Bilioni 6.47, na kwamba mradi kama huo unatekelezwa katika miji mingine 17 hapa nchini kwa gharama ya shilingi Bilioni 561 ikiwa ni fedha za mkopo nafuu ktoka Benki ya Dunia. 

Jengo la wagonjwa wa nje la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu limejengwa katika eneo la Nyaumata kwa ghamara ya shilingi Bilioni 1.8, na ni sehemu ya mradi mzima wa ujenzi wa miundombinu ya hospitali hiyo uliopangwa kugharimu shilingi Bilioni 11. Gharama za ujenzi huo zimepungua kutoka makadirio ya awali ya shilingi Bilioni 46 baada ya Mhe. Rais Magufuli kutembelea mradi huo mwaka juzi na kutoa maelekezo ya kutaka zipunguzwe ili ziendane na gharama halisi za ujenzi. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali imetenga shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya kujenga miundombinu mingine ya hospitali hiyo katika kipindi cha miezi 6, na kwa kuunga mkono ukamilishaji wa haraka wa hospitali hiyo Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuongeza fedha nyingine shilingi Bilioni 4. 

Ujenzi wa barabara ya Maswa – Bariadi yenye urefu wa kilometa 49.7 utagharimu shilingi Bilioni 88.877, na barabara hii ni sehemu ya barabara ya Mwigumbi – Maswa – Bariadi – Lamadi yenye urefu wa kilometa 171.8. 

Akizungumza katika miradi hiyo Mhe. Rais Magufuli amezishukuru taasisi zote za kimataifa zilizotoa mikopo nafuu kwa Tanzania kwa lengo la kufanikisha miradi hiyo, na ameahidi kuwa Serikali itahakikisha miradi hiyo inatekelezwa vizuri na inaleta manufaa yanayotarajiwa kwa wananchi. 

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Simiyu kwa kupata miradi hiyo na ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuwaletea maendeleo, ikiwa ni pamoja na kulipa kodi kwa kuwa fedha za kugharamia miradi hiyo zinatokana na kodi zao. 

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka, viongozi na wakulima wa mkoa wa Simiyu kwa juhudi kubwa walizofanya katika kuongeza uzalishaji wa zao la pamba, ambapo katika msimu uliopita kati ya kilo Milioni 226 zilizozalishwa hapa nchini, kilo Milioni 120 zimezalishwa katika Mkoa wa Simiyu. 

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameitaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha haraka ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu. 

Mhe. Rais Magufuli pia ameagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kuhakikisha fedha za vijana na wanawake (asilimia 10) zinatengwa kama inavyopaswa ili kuwawezesha vijana kupata fedha za kufanya shughuli za ujasiriamali. 

Mhe. Rais Magufuli kesho anaendelea na ziara yake hapa Mkoani Simiyu kwa kutembelea Wilaya ya Meatu. 


Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Bariadi 
08 Septemba, 2018

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI ATIMIZA AHADI ALIYOITOA JWTZ KWA AJILI YA UFUGAJI WA SAMAKI MKOANI MARA

0
0
  Katibu wa Rais Ngusa Samike akikabidhi fedha kiasi cha shilingi Milioni 40 kwa Mkuu wa kikosi cha 27KJ Luteni Kanali Js Mshashi kilichopo Makoko mkoani Mara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kutoa fedha hizo Septemba 6,2018 alipokuwa ziara Mkoani humo kwaajili ya kuongeza Vizimba 10 vya kufugia Samaki.Makabidhiano hayo yamefanyika Jijini Dodoma mbele ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.Septemba 11,2018. 
Katibu wa Rais Ngusa Samike akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kukabidhi fedha kiasi cha shilingi Milioni 40 kwa Mkuu wa kikosi cha 27KJ Luteni Kanali Js Mshashi kilichopo Makoko mkoani Mara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kutoa fedha hizo Septemba 6,2018 alipokuwa ziara Mkoani humo kwaajili ya kuongeza Vizimba 10 vya kufugia Samaki.Makabidhiano hayo yamefanyika Jijini Dodoma mbele ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.Septemba 11,2018.
PICHA NA IKULU

SPIKA NDUGAI AZINDUA FILAMU ILIYOANDALIWA NA TAKUKURU KUELIMISHA JAMII JUU YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (katikati) akizungumza na Waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wa pili  kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza  kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akikata utepe  kuzinduzi Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wakwanza kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza  kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) wakionesha kwa  Waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) CD za  Filamu ya ‘Bahasha’ mara baada ya kuizindua. Filamu hiyo imeandaliwa  na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wa pili  kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza  kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia uzinduzi Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan awataka Wakazi mkoa wa Kigoma kupima afya zao

0
0
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakazi wa mkoa wa Kigoma kupima afya zao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kujitambua na pia kutaisaidia Serikali kuwa na takwimu kamili za afya na kurahisisha utoaji huduma kwa waathirika.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano wa Kazuramimba, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.

Pia alihimiza wakina mama kuzingatia lishe bora kwa watoto kuepuka athari za udumavu “Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa uzalishaji chakula ni mkoa ambao hautuumizi kichwa katika kutafuta chakula cha Watanzania, unajitosheleza kabisa lakini kuna tatizo la lishe duni hasa kwa watoto”alisema Makamu wa Rais.

Takwimu zinaonyesha mpaka mwaka 2015 kiwango cha udumavu katika mkoa wa Kigoma ni asilimia 37.9

Makamu wa Rais amewaambia wakazi wa Kigoma kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa hasa kwa wageni wanaotoka nchi jirani ya Congo ili Taasisi za Serikali zifanye kazi yake haswa katika kuzuia waathirika wa ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

“Mgeni anapokuja semeni amekuja mgeni ili taasisi ya serikali zifanye kazi yake,kazi ya kuhakikisha mgeni aliyeiingia yupo msafi anakaa wapi, ataishi na nani, hatukatai wageni lakini toeni taarifa tuwajue na hii ni kwa faida yetu kama Taifa lakini yenu kama wana Kigoma, wana Uvinza ni kwa faida yenu wenyewe tunawalinda na maradhi, tunawalinda na uharamia,tunawalinda na mambo chungu mzima ya kiusalama wenu kwa hiyo ndugu zangu msifiche wageni wanapokuja tuambieni ili tuweze kuchukua zinazostahili”. Alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema Serikali ya awamu ya tano imeamua kutumia pesa zake za ndani kwenye vipaumbele vikubwa vya Kitaifa katika ununuzi wa ndege, umeme wa kudumu na uhakika, kupeleka maji kwa wananchi, elimu bure pamoja na kuboresha huduma za afya na kuhakikisha madawa yanapatikana kwa urahisi.

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Kigoma aliwaambia wananchi wa mkoa huo kuwa Kodi zinazokusanywa na Serikali ndizo zinajenga miundo mbinu.Maelezo ya Picha:

10: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipungia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa mikutano tayari kuhutubia mkutano wa hadhara jana jioni katika kata ya Kazuramimba,wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WATAALAM WA AFYA KUTOKA MAREKANI WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (kushoto) akizungumza na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani Dkt Deborah Stith. Wataalam kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani pamoja na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini katika mkutano huo. Baadhi ya wakurugenzi wa (MNH) wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo Mkuu wa Idara ya Macho Dkt. Mtemi Baruani (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt Praxeda Ogweyo (kulia).
 
. Wataalam wa Afya kutoka Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na uongozi wa hospitali hiyo lengo likiwa ni kushirikiana katika utoaji wa huduma za afya.  
 
Ujio huo wa wataalam 9 umeongozwa na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani, Dkt. Deborah Stith akiwa na wataalamu hao wakiwemo madaktari wa macho, mfumo wa mkojo na meno. Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema lengo la ugeni huo ni kuangalia jinsi ambavyo pande hizi mbili zinavyoweza kunufaika kwa kujenga mahusiano katika ufundishaji ,kuboresha huduma pamoja na utafiti. 
 
“Ushirikiano ambao tunautafuta hasa ni katika nyanja ya ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuwaongezea ujuzi madaktari wetu katika sehemu tulizokuwa tunafikiri kutoa huduma ambazo tulikuwa hatutoi awali” Amesema Prof. Museru. Aidha Dkt. Deborah Stith amesema wako tayari kushirikiana kwa karibu na Muhimbili kwa kubadilishana wataalam kwa manufaa ya jamii.
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images