Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Tamasha la Utamaduni Handeni Kwetu kufanyika Desemba 14, 2013

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Handeni.
TAMASHA la Utamaduni lililopewa jina la ‘Handeni Kwetu 2013’ linatarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga, likiwa na lengo la kutangaza sekta ya utalii na utamaduni wilayani humo.
 Mratibu wa Tamasha la Handeni Kwetu 2013, Kambi Mbwana, ambaye pia ni Mmiliki wa mtandao huu wa Handeni Kwetu Blog, pichani.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya Handeni, Dr Khalfany Haule, akizungumza na Handeni Kwetu, ofisini kwake muda mchache baada ya kuruhusu Tamasha la Handeni Kwetu kufanyika wilayani humo, Desemba 14 mwaka huu.
 Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akizungumza na Handeni Kwetu Blog, jana ofisini kwake wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Handeni Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa wilaya hiyo inayoongozwa kwa sasa na Mkuu wa wilaya Muhingo Rweyemamu.

Akizungumza jana wilayani Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema wameamua kuandaa tamasha hilo ili kushirikiana na wadau wote kutangza utamaduni nchini Tanzania.

Alisema kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, jamii nyingi zimekuwa zikiiga tamaduni za watu hasa kutoka nje ya nchi, jambo linaloleta mkanganyiko wa kiasi kikubwa.

“Tumeamua kuandaa tamasha hili kwa kupitia kampuni ya Raha Company and Entertainment, ambapo lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa linafanyika kwa mafanikio makubwa.

“Mipango kabambe inawekwa kulifanya tamasha letu liwe na mguso wa aina yake, ukizingatia kuwa linafanyika mwishoni mwa mwaka, hivyo tunaamini watu wengi watashiriki na sisi, hasa wale waliokuwa kwenye kipindi cha mapumziko ya mwisho wa mwaka,” alisema Mbwana.

Mbali na kufanya tamasha la Utamaduni wilayani humo, pia kutafanyika mchezo wa riadha kwa ajili ya kuzindua hamasa katika mchezo huo wilayani Handeni, mkoani Tanga.

"WALIOJENGA KATIKA MAENEO YASIYORUHUSIWA KISHERIA WABOMOE MARA MOJA" KAULI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizingumza katika kikao na wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wa hoteli katika Manispaa ya Sumbawanga tarehe 23 Septemba 2013 katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Pamoja na mambo mengine alipiga marufuku uchafuzi wa mazingira na kwamba watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupigwa faini. Kwa wale waliojenga katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria kama karibu na vyanzo vya maji amewataka kubomoa mara moja kwa mujibu wa sheria kabla hawajabomolewa kwa nguvu. Katikati ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta. 
Sehemu ya Wafanyabiashara wakifuatilia moja ya mada katika kikao hicho. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisisitiza jambo katika kikao hicho. Aliwataka wafanyabiashara katika Manispaa ya Sumbawanga kuzingatia usafi katika maeneo yao ya biashara pamoja na kuacha tabia ya kutiririsha maji machafu katika mitaro ya maji taka na sehemu nyingine za mji ili kuweka Manispaa hiyo katika hali nzuri ya usafi. 
Sehemu ya wafanyabiashara waliohudhuria katika kikao hicho. 
Ndugu Dattoo ambaye ni Mfanyabiashara  wa Hoteli Mkoani Rukwa akitoa maoni yake katika kikao hicho ambapo alishauri ubora wa maji katika Mji wa Sumbawanga uboreshwe na vilevile wafanyakazi katika nyumba za kulala wageni waelimishwe juu hatari ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi pamoja na umuhimu wa kupima kujua afya zao. Hata hivyo kuna miradi mikubwa ya maji inaendelea kujegwa Mkoani Rukwa na Serikali na wadau wa maendeleo ambayo ikikamilika tatizo la maji litakuwa limekwisha katika Manispaa ya Sumbawanga. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

TWIGA CEMENT YAKABIDHI MSAADA WA SARUJI KWA REDDS MISS TANZANIA 2013 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE YA WENYE ULEMAVU WA NGOZI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne  (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa  mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule na zahanati zitakazojengwa mkoani Shinyanga. Katikati ni Meneja Mahusiano  ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. Hafla
ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne (kulia) akimkabidhi Redds  Miss Tanzania Happiness Watimanywa mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa  mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino)  itakayojengwa mkoani Shinyanga. wa pili kushoto ni Mkuu wa Nidhamu wa Miss Tanzania, Albert Makoye na Meneja Mahusiano  ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam 
 Mshindi wa tatu wa Redds Miss Tanzania 2013, Clara Bayo akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Pascal Lesoinne wakati wa hafla hiyo. Katikati ni mshindi wa pili, Latifa Mohamed na kulia  ni Redds Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa. Msaada wote wa mifuko 900 ya saruji unagharimu shs milioni 30.

MOTO WATEKETEZA MISITU MAKETE

$
0
0




Picha zikionesha moto ulivyoacha madhara makubwa kwa wenye misitu hii baada ya kuteketeza miti na mimea mingine iliyokuwa katika eneo hilo. Haijafahamika mara moja nini chanzo cha moto huo(PICHA ZOTE NA EDWIN MOSHI)

CCM YAFANYA MKUTANO MKUBWA SHIRATU

$
0
0
  • KINANA AWEKA HISTORIA KATIKA VIWANJA VYA SHIRATI OBWERE
  • MAELFU YA WATU WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU
  • VIONGOZI 43 KUTOKA UPINZANI WARUDISHA KADI
  • WANACHAMA 126 WAJIUNGA HAPO HAPO
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye viwanja vya Shiratu Obwere na kuwaambia wakazi wa Shiratu kuwa CCM inatekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wakazi wa wilaya ya Rorya ,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao mipango iliyofanyika na itakayofanyika kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo,hasa katika suala zima la mradi wa umeme vijijini,maji,shule na huduma za afya.
 Sehemu ya Umati wa watu walifurika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Shiratu Obwere tarehe 24 Septemba 2013.


 Mbunge wa Rorya Ndugu Lameck Okambo Airo akihutubia wakazi wa Shiratu waliofurika kwenye uwanja wa Shiratu Obwere,Mbunge huyo alieleza jinsi gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa Shiratu ,na kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Rorya kwa umoja na mshikamano walio nao.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchini Ndugu Amina Makilagi akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni Rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu wilaya ya Rorya na kuwataka wananchi hao kuwapuuza wanaotaka kuharibu mchakato wa kupata Katiba Mpya kwani Mchakato wa Katiba hiyo imefuata taratibu zote za kisheria.

mpiganaji athumani hamisi atangazwa kuwa balozi wa baraza la taifa la usalama barabarani

$
0
0

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisalimiana na Mhariri wa Picha wa zamani wa magazeti ya Daily News na Habari Leo, Athumani Hamisi na kumtangaza kuwa Balozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani wakati wa ufunguzi wa wiki ya Usalama Barabarani jijini Mwanza.
Mpiganaji Athumani Hamisi akiwa na waratibu wa shughuli zake
za ubalozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.
-------------------------------------
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, amemtangaza Mhariri wa Picha wa zamani wa magazeti ya Daily News na Habari Leo, Athumani Hamisi , kuwa Balozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.



Hamisi, ambaye aliwahi pia kuwa mfanyakazi wa Kampuni ya The Guardian Limited kama Mpigapicha, alipata ajali mbaya mwaka 2008 na kupooza sehemuya mwili.

Katika uteuzi huo uliotangazwa na Waziri Nchimbi jana, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani litamtumia Hamisi kutoa elimu na hamasa kwa Watanzania kuepuka ajali kwa kuwa zina madhara makubwa kwa maisha ya binadamu.


Aidha, Waziri Nchimbi alisema ajali za barabarani zimeendelea kuwa janga linalogharimu maisha ya watu wengi, hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuzidhibiti.

Alisema hayo jijini jana alipokuwa akizindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa Waziri Nchimbi, hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2,012, jumla ya watu 17,820 wamekufa katika ajali za barabarani.


Miongoni mwao ni abiria 5,237, watembea kwa miguu 5,771 na madereva 1,292. Vifo vilivyotokana na ajali 98,693 za barabarani, kuna waendesha pikipiki 2,887, waendesha baiskeli 2,385 na wasukuma mikokoteni 245.


Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti, mwaka huu, ajali 15,682 zimetokea na kusababisha vifo 2,541 na majeruhi 13,752. Kati ya ajali hizo, pikipiki ni 5,433, ambazo zilisababisha vifo 704 na majeruhi 4,312.

“Hali hii ya matukio ya ajali za barabarani inatisha. Lazima tuchukue hatua madhubuti kukabiliana nazo kwani zinapoteza maisha ya watu wengi na kusababisha ulemavu wa kudumu na hivyo kupunguza nguvu kazi ya taifa,” alisema Waziri Nchimbi.
Chanzo: NIPASHE
Kupata mkasa mzima wa yaliyomsibu 
mpiganaji Athumani Hamisi

Vitz kutolewa kwa mashabiki wa Fiesta Mwanza jumamosi hii.

$
0
0
Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya push Push Media Mobile Rugambo Rodney.

Kampuni ya Push Mobile Media itatoa zawadi ya gari aina ya vits kwa mshindi wa promosheni ya tamasha la Fiesta litakalofanyika mkoani Mwanza jumamosi hii.

Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa watatoa gari aina ya Vitz kwa mpenzi wa Fiesta atakayeshiriki katika tamasha hilo kwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 na kuingia katika bahati nasibu hiyo.

Rodney alisema kuwa mbali ya kushinda gari, mshiriki pia anaweza kushinda fedha taslimu kiasi cha shs 100,000 kwa siku. Pia mpenzi wa Fiesta anaweza kushinda pikipiki.

Mshindi wa mkoa wa Mwanza atakuwa wa pili kupata gari ambapo mshindi wa kwanza wa gari alikuwa Abdallah Ally Ngagari (51) aliyeshinda kupitia tamasha la fiesta la Kigoma.

 “Tumepania kutoa zawadi katika mikoa yote ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga zaidi ya sh milioni 80 ili kufanikisha zoezi hili ambapo magari aina ya vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki, tunawaomba mashabiki kushiriki kwa nguvu zote,” alisema Rodney.

Wakati huo huo; mkazi wa Shinyanga Rose Mahenda amefanikiwa kushinda pikipiki baada ya kushiriki katika bahati nasibu hiyo.

WARSHA YA VYOMBO VYA HABARI NA ASASI ZA KIRAIA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YA CAG

$
0
0
WARSHA YA VYOMBO VYA HABARI NA ASASI ZA KIRAIA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YA CAG NA KUELEWA RIPOTI ZA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI-LANDMARK HOTEL-MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM.


Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam.


SERIKALI inayoendesha mambo yake kwa uwazi inatimiza sharti la msingi la utawala bora kwa kuwajibika ipasavyo kwa wananchi wake.


Hayo yamesemwa  na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa vyombo vya habari na asasi za kiraia kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya CAG na kuelewa ripoti za Mdhibiti Mkuu wa hesabu za serikali.


Bw. Utouh amesema kuwa kutokana na ongezeko la matumizi ya ripoti zake kwa vyombo vya habari na wadau wengine kumekuwa na upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwa namna zinavyotumiwa na wadau mbalimbali, hivyo warsha hiyo inatoa fursa ya pekee ili kupunguza upotoshwaji huo kwa kuelimishana, kurekebishana na kusaidiana ili kuzielewa vizuri ripoti hizo na kuzilipoti kwa usahihi.


“Warsha hii inalenga kutoa fursa ya kipekee kwa wadau wetu kushiriki na kutoa mawazo yao ya namna ya kuboresha mahusiano ambayo yataleta ufumbuzi na wa madai mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na asasi mbalimbali”. Alisema Bw. Utouh.


Bw. Utouh ameongeza kuwa ni vema kufahamu madhara juu ya utoaji taarifa za upotoshwaji ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kujitokeza baina ya pande mbili na pia amesema kuwa ana imani kubwa kuwa kila mwanahabari anatambua umuhimu wa habari na pia kutambua umuhimu wa uwajibikaji na utawala bora. “Msiweke madoido, msipambe taarifa ili kwamba zionekane zina mvuto”. Alisisitiza Bw. Utouh.

Aidha, Bw. Utouh amevitaka vyombo vya habari kwa kushirikiana na asasi za kiraia kwa pamoja kuhakikisha kuwa kuna mfumo mzuri wa upatakinaji wa taarifa na utaoji wa taarifa za serikali kwa usahihi.



Warsha hiyo imefunguliwa leo Landmark Hotel iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na inalenga kuwajengea uwezo maafisa habari nchini juu ya kazi za Mdhibiti wa Hesabu za Serikali na juu ya ubora wa upatikanaji wa habari zilizosahihi na kuziripoti kwa usahihi.


JUMUIYA INAYO SHUGHULIKIA SKULI ZA MAANDALIZI ZA KIJAMII (ZMRC) YA FANYA SHEREHE SIKU YA AFYA YA MTOMTO KUSINI UNGUJA.

$
0
0
 Mmoja kati ya wazee wa kijiji cha Muungoni jina halikufahamika kwa mara moja  akishirikiana na kinamama wa watoto wa wanafunzi   katika mafunzo ya upikaji uji wa lishe huko Skuli ya Maandalizi ya Istimraa iliyopo Kijiji cha  Muungoni.
 Daktari Salma Rashid akimchunguuza Masikio mwanafunzi wa Skuli ya Maandalizi ya Istimraa iliyopo Kijiji cha Muungoni.
 Diwani wa Viti Maalum Salama Ali akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wanafunzi wa skuli ya Pete kwa niyaba ya wanafunzi wenzake.
Diwani wa Viti Maalum Salama Ali akitowa maelezo kwa walimu pammoja na wazazi wa wanafunzi jinsi ya kuyatumia mafunzo waliyopatiwa katika upikaji wa Uji.

Rais Kikwete na mama salma wakutana na Michelle na Barack Obama na melinda gates

$
0
0
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mwenyeji wao Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya viongozi wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa 68 wa Umoja wa Mataifa jijini New York. Picha kwa Hisani ya Rae Lynn Wargo wa  Umoja wa Mataifa.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mama Melinda Gates wa Bill and Melinda Gates Foundation walipokutana katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York leo. Picha na Freddy Maro

OMMY DIMPOZ AKIWA SHOPPING NDANI YA JIJI LA NEW YORK KUJIANDAA NA SHOW YA HOUSTON JUMAMOSI HII TAREHE 28

$
0
0
Kama ilivyo kawaida yetu Kampuni ya DMK Global Promotions na J&P Ent sikuzote ni kuhakikisha kuwa Msanii anapofika Marekani mbali kufanya Show mbali mbali pia huwa tunahakikisha msanii ana have fan nakuutumia muda wake kutembelea sehemu mbali mbali za marekani kama mtalii na Entertainer.Tou Hii ya Nai Nai pia imewashirikisha Swahili Tv/Swahili Radio online ambao wanafanikisha kutuletea habari na matukio ya Dimpoz akiwa USA.
Kushoto ni Promoter/USA Tour Manager Mr "DMK" pamoja na Dimpoz wakipiga picha na Fan. 
Ommy Dimpoz akiwa na Promoter "DMK" Time Square NYC baada ya Shopping.KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Serikali yaipongeza timu ya wasichana Airtel Rising Stars

$
0
0
Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza timu akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt.
katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt. 
Kocha wa timu ya wasichana ya Airtel Rising stars Rogatician Kaijage akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt. 
Wachezaji waliozawadia kwa kungara katika michuano ya Airtel Rising stars pamoja na captain wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo (mwisho kushoto) katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.

BLOG MPYA MAALUM KWA VIDEO A BONGO TU - ONLY FOR BONGO VIDEO'S

$
0
0

MAMBO,
POLE NA KAZI ,NAOMBA MSAADA WAKO WA KUITANGAZA AU KUISHARE KATIKA SOURCE YOYOTE YA SOCIAL NETWORK ULIOKUWA NAYO 

KUTOKA KAPITALI ONLINE MARKETING & ADVERTISING COMPANY INAWALETEA BLOG HII MAALUM KWA AJILI YA MUSIC WA BONGO TU ,LIVE SHOW ZA WASANII WA BONGO NA INTERVIEW ZAO.

UKITEMBELEA BLOG HII UTAWEZA KUPATA VIDEO ZOTE KALI ZA BONGO
NA MATUKIO YANAYOHUSU WASANII KWA VIDEO
...KWA WASANII WANAOHITAJI VIDEO ZAO ZIWEKWE KWENYE HII BLOG WANAWEZA WASILIANA NASI KWA 
PIA TUNAFANYA VIDEO PROMOTION

KUTOKA:
FOUNDER ,ERICK KISAI
KAPITALI ONLINE MARKETING & PROMOTION COMPANY
DAR ES SALAAM.

WAZIRI WA HABARI AKUTANA NA WANAKIJIJI CHA PAJE NA WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE KUJADILIANA JUU YA UPIGWAJI NGOMA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akizungumza na wananchi na wamiliki wa kumbi za starehe wa kijiji cha Paje Wizarani kwake Kikwajuni leo.
Wananchi wa Kijiji cha Paje wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na michezo Saidi Ali Mbaouk walipokuwa na mazungumzo ofisini kwake Kikwajuni leo.
======  =====  ======
Khadija Khamis na Patima Mtumwa – Maelezo Zanzibar. 

Wananchi wa Kijiji cha Paje Mkoa wa Kusini Unguja wamewalalamikia wamiliki wa baa na kumbi za starehe zilizomo katika kijiji hicho  kutokana  na vitendo viovu vinavyo kwenda kinyume na  heshima na maadili ya kijiji hicho.  Wananchi hao wametoa malalamiko yao katika mkutano wa pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na wamiliki wa baa zilizomo kijiji hapo uliofanyika Ofisini kwa Waziri Kikwajuni.

Walisema wamiliki wa baa na kumbi za starehe wamekua wakiwasumbua  kwa kupiga disco usiku kucha na kusababisha kushindwa kulala majumbani mwao. Waliongeza kuwa  tabia hiyo inapelekea vishawishi kwa watoto wao  na kujiingiza katika   mambo maovu  yanayokwenda kinyume na mila silka na utamaduni wa kijiji chao.

“Disco linatuletea usumbufu mkubwa kwa watoto wa kijiji chetu wapo baadhi  hawalali makwao usiku mzima,” alisema Mbaraka Salum askari Jamii wa kijiji hicho.

Mbaraka alisesema  vitendo vya ngono  na kubakwa kwa watoto wa kiume vimekuwa vikifanywa bila woga  na vijana 30 wa kijiji hicho tayari wameshaambukizwa virusi vya ukimwi.  Wananchi hao wa Paje wameishauri Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuzuia vibali vya kupiga Disco kumbi zote za starehe ndani ya kijiji hicho kwa kuhofia kutokea madhara makubwa zaidi.

Wamiliki wa Baa na kumbi za starehe kwa upande wao  wameitaka serikali iwaangalie kwa jicho la huruma kwa sababu burudani  ya ngoma ndiyo inayopelekea  kupata wateja na  kuongeza kipato chao kinyume chake ni hasara katika biashara yao.

‘’Tunaiomba Serikali  ituruhusu  japo siku moja kwa wiki tupige ngoma ili  tuweze kuingiza  mapato,”alisema  Mariyam Simba Mkwasi mmiliki wa baa la Vuvuzela.

Waziri  wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe, Said Ali Mbarouk  alisema kuwa vibali vya  musiki  vitaendelea kuzuiliwa ikiwa  wamiliki wa sehemu hizo  watashidwa kufuata taratibu ziliziowekwa .

‘’Ni bora tukose mapato  Serikalini  kuliko kuendelea kuwanyima uhuru wananchi wetu tutaendelea  kuzuiya vibali vya disco mpaka mujenge kumbi zisizotoa sauti,‘’alisema Waziri wa Habari.

Alisema iwapo kuimarika kwa sekta ya  utalii  Zanzibar kutasababisha Utamaduni wake  kumongonyoka hilo halitawezekana na hatuwezi kupanda mbegu ya ufuska katika visiwa vyetu.

Alisema  Zanzibar ina ustaarabu  na utamaduni wake, hivyo ametaka kila mmoja ahakikishe kuwa utamaduni huo unalindwa, unadumishwa na  kurithishwa kwa vizazi vijavyo.
Kumbi za starehe na burudani zilizolalamikiwa zaidi na wananchi wa kijiji cha Paje ni pamoja na Vuvuzela, Jambo, Gereje na Deman Loge.

MKURUGENZI IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR AKUTANA NA UJUMBE WA UNICEF LEO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Rafii Haji Makame (kulia) akitoa ufafanuzi wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa UNICEF yaliyofanyika Ofisi ya Tume ya Utangazaji Kikwajuni.
 Ujumbe wa UNICEF ulipokuwa na mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo katika Ofisi ya Tume ya Utangazaji Kikwajuni leo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

====  ====== =========
Khadija Khamis na Patima Mtumwa – Maelezo Zanzibar

Shirika  la  Umoja wa Mataifa  linaloshughulikia  Watoto UNICEF limeonyesha azma  ya  kuendelea kusaidia kutoa taaluma katika nyanja za Afya, Elimu na Jamii nchini.

Shirika  hilo kupitia Taasisi za Habari na Mawasiliano  limeahidi kusaidia katika  kuaandaa  vipindi  vya Radio na TV kwa lengo la kuelimisha jamii   mjini na vijijini. Maafisa wa Shirika hilo wakiongozwa na Mkurugenzi wake Elephase Kamugushi  wameeleza hayo walipokutana  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Rafii Haji  katika ukumbi wa Tume ya Utangazaji  Kikwajuni  mjini Zanzibar .

Kamugisha ametaka  vipindi hivyo vielekezwe katika kuelimisha matatizo yanayowakabili watoto ikiwemo ajira za watoto, watoto  wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na  maradhi yanayowasumbua watoto ikiwemo cholera, malaria  na  utapia mlo.

Amesema UNICEF litasaidia upatikanaji wa nyenzo za kufanyia kazi na utaalamu ili kuviwezesha vipindi hivyo kuwa na mvuto kwa wasikilizaji. 
 Kamugisha ameahidi kukutana na Wizara na Taasisi  zinazoshughulikia watoto Zanzibar ili kuhakikisha azma hiyo ya UNICEF inafanikiwa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Rafii Haji  Makame alieleza  kufarijika na uamuzi huo wa UNICEF  ambao  umeleta  faraja hasa wakati huu ambapo Zanzibar inaandaa vipindi mbali mbali kwa ajili ya Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi.

Alisema  Idara ya Habari Maelezo imeanzisha utaratibu wa kuonyesha vipindi vijijini kwa njia ya senema na kumekuwa na upungufu mkubwa wa vipindi, hivyo msaada wa UNICEF utasaidia kupatikana kwa vipindi vya uhakika.
 Mkurugenzi Rafii amelishukuru Shirika hilo kwa msaada wake huo na ameahidi kusimamia kikamilifu kuhakikisha vipindi vinavyowahusu watoto vinaandaliwa kwa wingi.

MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA KINANA WILAYA YA RORYA

$
0
0
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu Obwere wilaya ya Rorya mkoa wa Mara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu Obwere katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa wakati wa uzinduzi wa mradi wa bwawa la maji ya safi ya matumizi ya binadamu na kunyweshea mifugo kata ya Rocha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda nyasi katika (lambo) bwawa la maji linalojengwa katika kata ya Rocha,wilaya ya Rorya.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akiwa ameketi pamoja na wajumbe wa shina namba 12 kata ya Utegi tayari kwa kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Tawi la Nyanduga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya Daraja la Asili la Lorbimbe kutoka kwa mbunge wa Rorya Ndugu Lameck Airo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bukura baada ya kukagua ujenzi wa Maabara,Madarasa na Nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Bukura.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Tai kijiji cha Masonga baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba ya Kikundi cha akina Mama  cha Upendo Women Group Masonga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimbeba mmoja ya watoto yatima wanaolelewa na kituo cha  akina mama cha Upendo Women Group.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Hostel ya chuo cha waganga wasaidizi cha RAO HEALTH TRAINING CENTER.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha RAO HEALTH TRAINING CENTER
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa RAO HEALTH TRAINING CENTER ,mwenye kofia ni Mkuu wa chuo hicho Dk. Ziki Makoyo.

Mshindi wa BSS 2011 Haji Ramadhani. aibuka na singo yake mpya.

$
0
0

Baada ya Ney wa mitego kumdisi Haji Ramadhani kwenye wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la Salam zao,Haji sasa anasema hajafuria na anaishukuru BSS na huu ni wimbo wake mpya aliofanya chini ya stodio za Jaraman Record iliyopo kinondoni na video chini ya Apex Video by Pablo. Haji anapenda kuwafahamisha mashabiki wake kua wakae mkao wa kula kwa sasa anaandaa Movi yake ya kwanza ambapo nimoja ya kuonesha uwezo wake kwenye upande wa kuigiza. Nashukuru mungu Video yangu ina wiki moja mpaka sasa na inafanya vizuri kwenye Tv stesheni za Tanzania na nnje pia.

Bagamoyo intercollege night (BIN), kuwashika wasomi tasuba

$
0
0
Sunday Mangu“ Linex” akiwapagawisha mashabiki wasomi(hawapo pichani) kwenye usiku wa BIN uliyofanyika kwenye ukumbi wa TaSuBa Bagamoyo Oktoba 12,2012.
Waliopendeza BIN 2012
Edna Richard kutoka TaSuBa Lady of the night akiwa kwenye Pozi la pamoja na Man of the night Regan Wilnelvin kutoka chuo cha Slads mara baada ya kutangazwa kwenye ukumbi wa TaSuBa Bagamoyo  Oktoba 12, 2012.

=======  ======  =======
BIN   KUWASHIKA WASOMI OKTOBA


Bagamoyo intercollege night (BIN), tukio taaluma na burudani linaloendelea kujipatia umaarufu kwa kasi, ambalo hufanyika kila mwaka katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo linatarajia kufanyika tarehe 19Oktoba 2013. Kwa mujibu habari zilizopatikana mchana wa  leo mjini Bagamaoyo kutoka kwa msemaji wa Bodi ya Wakurugenzi wa tukio hilo Bw. Kim Kimenya, BIN kwa mara ya kwanza itashirikisha vyuo vya Bagamoyo na Dar es salaam.

Aidha zaidi ya kushirikisha vyuo vya Dar es saalam BIN itakuwa na shughuli za kijamii za kujitolea na kutembelea watu wenye mahitaji maalumu na,  utoaji wa tuzo kwa wanavyuo bora kitaaluma ikiwa ni tofauti na miaka miwili iliyopita ambapo tuzo zilitolewa kwa waliopendeza yaani Lady of the night na Man of the night,walioweza kujibu maswali ya bahati pamoja na, waliong’ara kwenye michezo ya ufukweni.


Pia Kimenya amefafanua kwa upande wa shughuli za kijamii kutakuwa na usafi wa mazingira na kwa upande wa michezo kuta kuwa na mechi kamambe ya maveterani wa mji wa Bagamoyo watakaocheza dhidi ya timu ya mchanganyiko wawanavyuo.


Michezo mingine kama kuvuta kamba,riadha  itakuwepo kama ilivyokuwa mwaka jana,na kwa upande wa taaluma wanafunzi bora kitaaluma kutoka kwenye vyuo shiriki ndiyo watashika dhamana za vyuo katika uwasilishaji wa mada.


Kwa upande wa burudani kama ilivyo kwa miaka iliyopita itaongozwa na msanii maarufu akisindikizwa na wasanii wengine binafsi na wasanii wa makundi  ambapo  msanii maarufu na wasanii wengine  watajulikana mwanzoni mwa mwezi Oktoba.


Kuhusu udhamini hoteli ya Mikocheni Resort Centre (MRC) ya jijini Dar es salaan ndiyo ambayo imethibitisha kudhamini na mazungumzo yanaendelea na makampuni menginei ili yaweze kudhamini.“Ninayaomba makampuni mengine yajitokeze kudhamini BIN 2013.” alisisitiza Kimenya.


BIN inayofanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo,inaandaliwa kwa pamoja na kampuni za Kimkev entertainment,Mrimi classic wear ,na Free voice investment ltd

TAMASHA LA KIMATAIFA LA 32 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO 2013.

$
0
0
 wanachuo wa chuo cha sanaa bagamoyo wakicheza ngoma kwenye tamasha la sanaa la kimataifa linalofanyika katika viwanja vya chuo cha sanaa bagamoyo wakionyesha umahili wao wa kuisakata ngoma .mbele ya mgeni rasimi jana katika ukumbi wa chuo bagamoyo mkoani pwani.  
  msanii maarufu hapa nchi wa muziki wa kisasa Misoji  Nkwambi   wa katika  wa kushoto ni mwanachuo  Safina Amani na wakulia ni Clement Chares akicheza ngoma na hivi sasa misoji ni mwanachuo wa chuo cha sanaa bagamoyo .(Picha kwa Hisani ya Simon Makala, Mwanamakala blogspot.com).
Picha no 1409, watoto wadogoGozibet Bwere miaka minne na mwingine  Nyambuli Aginess Muganga wa kikundi cha ngoma cha Utandawazi  Theater Group Matwigachallo, kutoka kijijij cha Nansore Wilaya ya ukerewe mkoa wa mwanza wakiwa wanacheza ngoma jana katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamo kwenye Tamasha  la kimataifa la  32la sanaa na Utamaduni Bagamoyo, kauli mbiu ni sanaa na utamaduni katika kukuza Utalii linalo endelea katika chuo cha sanaa bagamoyo mkoani Pwani.

======  ====== =======
TAMASHA LA KIMATAIFA  LA 32 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO 2013.
 
NAIBU WAZIRI AMOSI MAKALA; “ Sanaa na utamaduni kuleta ajira”
 
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
 
NAIBU  Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala  amesma Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta ajira vijana pindi watakapokuwa tayari kuienzi kwa vitendo na kuisomea.
 
Makala alisema hayo mjini hapa alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa tamasha la 32,  la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lenye kauli mbiu ‘Sanaa na Utamaduni katika kukuza utalii’ linaloshirikisha vikundi zaidi ya 70, kutoka ndani na nje ya Tanzania.
 
Akihutubia, umati wa wananchi,wanafunzi wa chuo hicho cha sanaa na vikundi mbalimbali vinavyoshiriki, Waaziri Makala alisema akiwa waziri mwenye dhamana atahakikisha utamaduni na sanaa nchini inakua huku ikiwanufaisha watu wote kwa vizazi vya sasa  na vya baadae.
 
“Katika kuenzi  Sanaa na Utamaduni, Wizara ina mipangilio mingi ikiwemo nay a kuakikisha tunakuza utamaduni wa Taifa letu na hata ajira kwa vijana ambao watajiunga na sanaa hivyo tutaendelea kushirikiana na chuo cha TasuBa  na wadau wengine katika kufikia malengo” alisema Makala.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Michael Kadinde  alisema  watahakikisha tamasha hilo kongwe nchini  wanafikia vikundi na wasanii  mbalimbali ilikupata kushiriki na kuonesha kazi zao.
 
“Lengo kufikia wasanii wote na hilo tunafanya kila mwaka na zaidi milango ipo wazi kwa mashirika binafsi ya ndani na nje kuja kuwekeza na kukuza sanaa zetu” alisema Kadinde.Na kuongeza kuwa kwa sasa TaSUBa ina enzi na kulithisha sanaa na utamaduni kwa vitendo ikiwemo kutoa mafunzo kwa watoto wadogo na wale wa elimu ya msingi.
 
Kwa upande wa Vikundi   vinavyoshiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja na ;
Alisema, vikundi 40 kati ya 60, ni kutoka Tanzania na vingine ni kutoka nje ya nchi vikiwemo vilivyowahi kushiriki tamasha hilo na vipya ambavyo itakuwa ni mara ya kwanza kuja.  Alivitaja vikundi vya Tanzania kuwa ni Ngome International Magic Show – JWTZ,  Splendid Theatre, Kigamboni Community Centre, Malezi Youth Theatre na Jivunie Tanzania Sanaa.
 
Vingine ni Mapoloni Culture Centre, Albino Revolutionary, Cocodo African Music, Imani Theatre, Safi Theatre, Imara Boma, Bagamoyo House of Talents, Bwagamoyo Africulture, Godykaozya & Tongwa Band na Mtoto Mchoraji. Vimo pia Shada Acrobatics, Bagamoyo Players, Bayoice, Jikhoman & Afrika Sana Band, Vitalis Maembe & The Spirit Band na Bagamoyo Dance Company.
 
Aidha, kuna vikundi vya Makini Organization (Arusha), Tumaini Group (Manyara), Kimanzichana Vijana Group (Mkuranga), Utandawazi Theatre Group (Matwi Gha Chalo), kutoka visiwa vya Ukerewe, Hiari ya Moyo (Dodoma), Moshi Police Academy (Moshi), CBM Acrobatic Group, Man Kifimbo Band na Midundo ya Sanaa. Pia kuna vikundi kutoka Ethiopia , Kenya , Norway , Uganda , Rwanda na Ujerumani.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MARA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya sanamu ya mfano wake kutoka kwa Ndugu Elia Bugurilo Kamoga.
Josephat Amon Muruga akiwa na wenzake sita baada ya kujiunga na CCM wakitokea Chadema.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa anavuka na kivuko cha MV Musoma kutoka Kinesi kuelekea Musoma mjini,Kivuko hicho ambacho kimekuwa  mkombozi  wa usafiri kinauwezo wa kubeba abiria 330.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu vazi la kujiokoa wakati wa hatari wakati wa kuvuka  na kivuko cha MV Musoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Balozi wa shina namba 6 Tabitha Edgar wa kata ya Kitagi.
Balozi wa nyumba kumi Tabitha Edgar wa shina namba 6 kata ya Kitagi akitoa shurani zake za kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abbulrahman Kinana.
Katibu Mkuu akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria uliopo eneo la Bukanga(Makoko) mradi huo utakamilika katikati ya mwaka ujao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akikagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji huku akipatiwa maelezo na mhandisi Jairos Chilema ,mradi huo utakuwa na bomba kubwa la kilomita tisini na ukikamilika utaondoa kabisa tatizo la maji Musoma Mjini.

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images