Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1667 | 1668 | (Page 1669) | 1670 | 1671 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Salome Majaliwa - JKCI.

  ULAJI wa vyakula visivyokuwa na afya ni moja ya sababu zinazosababisha watu kupata magonjwa  yasiyo ya kuambukiza ukiwemo ugonjwa wa moyo.
  Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akitoa mada kuhusu afya na mazoezi   kwenye  mkutano wa wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Katika mada hiyo ya afya na mazoezi Prof. Janabi alifundisha kuhusu ugonjwa wa shambulio la moyo na kiharusi, tezi dume, saratani, kukoma kwa hedhi na huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
  Prof. Janabi ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema hivi sasa  watu wanapenda kula vyakula ambavyo ni hatari kwa afya zao zikiwemo chips na bagger badala ya kula kwa wingi matunda na mboga za majani.

  “Dhibitini vyakula mnavyokula hii ikiwa ni pamoja na kutokula vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo vinapelekea mishipa ya moyo kuziba kutokana na mafuta na kusababisha tatizo la kiharusi pia  fanyeni mazoezi ya mara kwa mara”, alisisitiza Prof. Janabi.

  Alisema ugonjwa wa moyo ni moja ya magonjwa yanayoua watu wengi wakiwemo watoto ambao wasipopata chanjo za muhimu zinazotolewa chini ya umri wa miaka mitano pia mama mjamzito asipopata chanjo   kuna uwezekano mkubwa kwa watoto kuzaliwa na kupata magonjwa ya moyo.

  Kwa upande wa  ugonjwa wa shambilio la moyo  alizitaja dalili zake kuwa ni maumivu kwenye kifua ambayo yanakwenda kwenye mgongo upande wa kulia na kushoto na kuwasihi wanapoona dalili kama hiyo wawahi  mapema kwa daktari.
   Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  wakitoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo  kwa wahandisi wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
   Pix 3 & 4: Baadhi ya Wahandisi wakiwa katika foleni ya kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo katika  banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi ulifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo ilishiriki kutoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya  moyo kwa wahandisi hao.
  Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adela Martine akitoa ushauri kwa mhandisi aliyepata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi hiyo wakati wa mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari za Jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada ya Afya na mazoezi kwa wahandisi wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.Picha na JKCI


  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla amempongeza msanii nyota wa kizazi kipya nchini Bongo flava, Elias Barnaba maarufu kama Barnaba Classic kwa hatua yake ya kutoa albam ya Gold ambayo itasaidia kukumtangaza zaidi kwenye medani za muziki ndani na nje ya nchi.

  Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo mapema leo Septemba 6,2018 wakati alipotembelewa na msanii huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4, na kumkabidhi rasmi CD ya album yake ya GOLD ambayo imeingia sokoni 31 August mwaka huu. Katika hatua hiyo Waziri alimshukuru kwa kumtembelea ambapo pia alimpatia ushauri namna bora ya kuiuza albam hiyo ya GOLD ikiwemo soko la kimataifa.

  "Nilipata mwaliko wako wa uzinduzi wa albam ya Gold. Bahati mbaya sikuweza kufika kutokana na ajari. Lakini naendelea vizuri na nashukuru kwa kufika kuja kuniona na kunikabidhi rasmi..natambua wasanii pia ni nguzo katika kukuza Utalii wetu ikiwemo kuutangaza kupitia ala na mashahiri yenu na ndio maana mwezi huu wa Septemba tunakuja na tamasha la Urithi ambalo Wasanii wamepewa nafasi ya kipekee" alieleza Waziri Dkt.Kigwangalla.

  Kwa upande wake Barnaba alimshukuru Waziri Dkt Kigwangalla kwa kuipokea Album hiyo ambayo imezingatia vigezo vyote na ubora wa hali ya juu. "Kwanza nikupe pole kwa ajari. Naamini wasanii na wadau wote tunakuombea upone haraka na urejee kwenye majukumu yako ya kila siku ya kukuza Maliasili zetu na Utalii kwa ujumla na upokee albam hii ya Gold ikuburudishe unapoendelea kuuguza majeraha, Asante Sana" alisema Msanii huyo wakati wa kumkabidhi Albam hiyo.

  Kwa upande wake Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa Mxcater amesema albam hiyo iliyosheheni nyimbo Bora na kali zikiwemo Chausiku, Lover Boy na nyingine nyingi inapatikana katika maduka ya mtandao yaani (Online) kupitia Boomplay Music."Kwa watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia App ya BoomplayMusic_tz na wataipata moja kwa moja" alisema Mxcater.
   Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akipokea CD ya albma ya Gold kutoka kwa msanii nyota wa Bongo flava Elias Barnaba 'Barnaba Classic' mapema leo Septemba 6, 2018, wakati alipotembelewa  na msanii  huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4 mwaka huu. Kulia kwa Waziri ni Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa 'Mxcater'.NA  ANDREW CHALE,DAR.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akipokea CD ya albma ya Gold kutoka kwa msanii nyota wa Bongo flava Elias Barnaba 'Barnaba Classic' mapema leo Septemba 6, 2018, wakati alipotembelewa  na msanii  huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4 mwaka huu.


  0 0

  Mwenyekiti wa mdahalo katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Mhandisi Lucas Chogo (katikati) akizungumza na Wahandisi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho hayo, kulia ni mtoa mada ya usafirishaji, Prof. David Mfinanga na kushoto ni mtoa mada ya maendeleo katika sekta ya maji, Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo. (06/09/2018)
  Pix 01 (1)
  Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akijibu maswali ya wahandisi kuhusu maendeleo katika sekta ya maji wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa mdahalo huo  Mhandisi Lucas Chogo na kulia ni mtoa mada ya usafirishaji, Prof. David Mfinanga. (06/09/2018)
  Pix 01b
  Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akijibu maswali ya wahandisi kuhusu maendeleo katika sekta ya maji wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa mdahalo huo  Mhandisi Lucas Chogo na kulia ni mtoa mada ya usafirishaji, Prof. David Mfinanga. (06/09/2018)
  Pix 02 (1)
  David Mfinanga (kulia) akijibu maswali ya wahandisi kuhusu maendeleo katika sekta ya usafirishaji,  wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa mdahalo huo  Mhandisi Lucas Chogo na kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo mtoa mada ya maendeleo katika sekta ya maji. (06/09/2018)
  Pix 03 (1)
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akitoa mada kwa wahandisi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (06/09/2018)
  Pix 03b
  Mhandisi Zacharia Katambala akitoa mada ya usafirishaji kwa wahandisi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (06/09/2018)
  Pix 05
  Wahandisi wakitembelea na kupata maelekezo katika mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (06/09/2018)
  Pix 04
  Baadhi ya wahandisi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (06/09/2018)
  Pix 06
  Wahandisi wakitembelea na kupata maelekezo katika mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (06/09/2018)
  Pix 07
  Wahandisi wakipata huduma ya afya katika banda maalumu la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (06/09/2018)

  0 0


  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) pamoja na wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walipowalisi katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya Makao Makuu UVCCM Upanga Dar Es Salaam

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl.Raymond Mwangwala (MNEC) akizungumza na watumishi wa Makao makuu wakati akiwatambulisha wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walioteuliwa na Kuthibitishwa na baraza kuu la UVCCM Taifa lililoketi jijini Dodoma wiki iliyopita
  Wakuu wa Idara za Makao makuu UVCCM wakifuatilia mazungumzo ya Katibu Mkuu UVCCM Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) alipokuwa akiwatambulisha kwa watumishi wa UVCCM makao makuu.


  watumishi wa UVCCM makao makuu wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) alipokuwa akiwatambulisha wakuu wa idara za UVCCM makao makuu kwao  Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Siasa Ndg Peter Kasela akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM


  Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg.Hassan Bomboko akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
  Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Kamana Juma Simba akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
  Katibu wa Idara ya Uchumi na Uwezeshaji Ndg.Nelson Lusekelo akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM


  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) akiwakabidhi Mpangokazi wa Utekelezaji wa UVCCM Mwaka 2018/2019
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) akiwaongoza wakuu wa Idara za Makao makuu ya Umoja wa Vijana wakati akiwatembeza maeneo mbali mbali ya Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam(Picha na FahadiSiraji wa UVCCM)

  0 0
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Geogre Mkuchika akieleza umuhimu wa muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018) wakati wa kupitishwa kwa muswaada huo leo Bungeni Jijini Dodoma.
  2 (8)
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa  Sima akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha inatunza mazingira ya ziwa manyara ili kuondoa athari za mabadiliko ya tabia nchi.
  3 (8)
  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati akijibu hoja za wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kupitisha muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018)
  4 (6)
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso akisisitiza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama kote nchini.
  5 (4)
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi waliokuwa na akaunti katika iliyokuwa  Benki ya FBME  wanalipwa haki zao kwa mujibu wa sheria na Kanuni za utumishi baada ya Benki hiyo kufungwa.
  7 (3)
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akisisitiza kuhusu umuhimu wa wananchi kupata huduma bora za maji safi na salama wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
  8 (5)
  Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Zungu akisisitiza jambo wakati wa kupitishwa kwa muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018.(The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018) leo Bungeni Jijini Dodoma.
  9 (1)
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima, leo Bungeni Jijini Dodoma.
  10 (4)
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kuondoa mgogoro kati ya wananchi na Manispaa ya Mtwara Mikindani unaotokana na eneo la Mjimwema na Tangira lililopimwa kwa ubia kati ya Manispaa na Taasisi ya UTT-PID mwaka 2003.
  6 (5)
  Sehemu ya wageni waliofika Bungeni  kama wanavyoonekana katika picha.
  (Picha zote na Frank Mvungi)

  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka ,Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.2 (9)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka , Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.
  3 (9)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka ,Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.
  4 (7)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima mara baada ya kukata kuzindua rasmi mradi wa ufugaji wa Samaki wa kwenye mabwawa katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.
  5 (5)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mradi wa ufugaji wa Samaki wa kwenye mabwawa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mradi huo katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.
  6 (6)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mradi wa ufugaji wa Samaki wa kwenye mabwawa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mradi huo katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.
  7 (4)
  Askari wa Jeshi la kujenga Taifa wakiwawekea samaki chakula katika Mabwawa ya kufugia samaki hao wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.
  8 (6)
  Askari wa Jeshi la kujenga Taifa wakiwawekea samaki chakula katika Mabwawa ya kufugia samaki hao wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.
  9 (2)
  Askari wa Jeshi la kujenga Taifa wakiwvua samaki katika Mabwawa ya kufugia samaki hao wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi akitangaza utabiri wa hali ya hewa ya msimu wa mvua za vuli kwa miezi mitatu katika makao makuu ya taasisi hiyo jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam leo kushoto ni Meneja uendeshaji wa vituoHellen Msemo
  KIJ2
  Mkurugenzi Mkuu wa Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi akisoma taarifa hiyo wakati akitangaza utabiri wa hali ya hewa ya msimu wa mvua za vuli kwa miezi mitatu katika makao makuu ya taasisi hiyo jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam leo kushoto ni Meneja uendeshaji wa vituo Hellen Msemo na kulia ni Mkurugenzi wa Utabiri Dkt. Hamza Kaberwa
  ………………………………………………………………………………………
  index
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
  MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
  MWELEKEO WA MVUA TANZANIA
  KIPINDI CHA MSIMU WA MVUA ZA ‘VULI’ OKTOBA –DISEMBA, 2018

  DONDOO MUHIMU ZA MSIMU WA VULI OKTOBA HADI DISEMBA, 2018 Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2018, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbali mbali wanaohitaji taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Wanyamapori, Maliasili na Utalii, Uchukuzi na Mawasiliano, Nishati na Maji, Mamlaka za Miji, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa.Muhtasari wa mwelekeo wa mvua hizona athari zake ni kama ifuatavyo:
  a)         Katika msimu wa mvua za Vuli 2018
  ·         Kunatarajiwa kuwa na mvua za wastani katikamaeneo mengipamoja na uwezekano mkubwa wa kupata mvua za juu ya wastani hususan katika maeneo yaMikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani,Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja and Pemba.
  ·         Ongezeko la mvua linatarajiwa hususan katika mwezi Novemba, 2018 kutokana na uwezekano wa kutokea vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa bahari ya Hindi.
  b)         Athari 
  ·         Hali ya unyevunyevu wa udongo katika maeneo mengi yanayotarajiwa kuwa na mvua za wastani na juu ya wastani itatosheleza shughuli za kawaida za kilimo katika maeneo mengi yamikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dar es Salaam, Tanga, Pwani ; Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro.
  ·         Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza na hivyo kuongeza uwezekano wa mafuriko hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
  1. MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA KIPINDI CHA OKTOBA – DISEMBA 2018.
  Mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa (Tazama kipengele II cha taarifa hii), inaonesha uwezekano mkubwa wa mvua za vuli kuwa za wastani katika maeneo mengi ya nchi. Aidha, mvua za juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya pwani ya kaskazini katika kipindi cha msimu wa mvua wa Oktoba hadiDisemba, 2018. Maelezo ya kina juu ya mwelekeo wa mvua hizo ni kama ifuatavyo:
  • Mvua za msimu wa Vuli
  Mvua za kipindi cha mweziOktoba hadi Disemba (Vuli) ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Ukanda wa Ziwa Viktoria, nyanda za juu kaskazini mashariki, Ukanda wa Pwani ya kaskazini nawilaya ya Kibondo). Mvua za Vuli 2018 zinatarajiwa kuanza mapema katikati ya mwezi Septemba na mwanzoni mwa Oktoba, 2018 katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua.Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo ya mkoa wa Kagera, Geita na wilaya ya Kibondo; mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na maeneo ya mashariki na kusini mwa Ziwa Viktoria. Mvua za juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya pwani ya kaskazini.
  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,S.L.P. 3056 Dar es Salaam, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Simu: 255 (0) 22 – 2460706- 8; Nukushi: 255 – (0) 22 – 2460735; Barua pepe :Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,S.L.P. 3056 Dar es Salaam, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Simu: 255 (0) 22 – 2460706- 8; Nukushi: 255 – (0) 22 – 2460735; Barua pepe :
  Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga):
  Mvua zinatarajiwa kuanza mapema, kati ya wiki ya pili  naya tatu ya mwezi Septemba,2018 katika maeneo ya mkoa wa Mara na kusambaa katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita na Kagera ifikapo wiki ya tatu ya mwezi Oktoba,2018. Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Simiyu. Mvua za wastani na vipindi vya mvua za chini ya wastani zinatarajiwa katika mikoa ya Kagera, Geita na wilaya ya Kibondo. Mvua za msimu wa Vuli zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba,2018 katika maeneo ya mikoa ya Mara na Simiyu, na kwa maeneo mengine ya ukanda wa Ziwa Viktoria mvua zinatarajiwa kuisha kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Januari, 2019.
  Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani, Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro):
  Mvua zinatarajiwa kuanza mapema wiki ya nneya mwezi Septemba, 2018. Mvua za juuya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi.Vipindi vya ongezeko la mvua vinatarajiwa hususan katika ya miezi ya Oktoba na Novemba, 2018. Mvuaza Vuli zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu ya mwezi Disemba, 2018.
  Nyanda za juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):
  Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya pili ya mwezi Oktoba, 2018 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.Mvua hizi zinatarajiwa kuisha wiki ya pili ya mwezi Disemba,2018.
  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,S.L.P. 3056 Dar es Salaam, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Simu: 255 (0) 22 – 2460706- 8; Nukushi: 255 – (0) 22 – 2460735; Barua pepe : met@meteo.go.tzMamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,S.L.P. 3056 Dar es Salaam, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Simu: 255 (0) 22 – 2460706- 8; Nukushi: 255 – (0) 22 – 2460735; Barua pepe : met@meteo.go.tz

   
  Picha 1 – Ramani – Kushoto: Mwelekeo wa mvua katika msimu huu wa Oktoba hadi Disemba 2018. Ramani- Kulia: Kiwango cha Wastani wa muda mrefu wa mvua za mwezi Oktoba hadi Disemba katika kipimo cha milimita za mvua.
  Matukio mengi ya mvua kubwa yanatarajiwa kujitokeza hususankatika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani. Hata hivyo, izingatiwe kuwa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanatarajiwa hata katika maeneo yanayopata mvua za wastani na chini ya wastani.

  II.      MIFUMO YA HALI YA HEWA

  Hali ya joto la juu ya wastani katika eneo la kati la Kiikweta katika Bahari ya Pasifiki inatarajiwa kuendelea katika kipindi cha Oktoba-Disemba, 2018.  Eneo la magharibi mwa bahari ya Hindi linatarajiwakuwa na joto la juu ya wastani.Hali hiyo sambamba na joto la wastani linalotarajiwakujitokeza mashariki mwa bahari ya hindi katika miezi ya Oktoba na Novemba itachangia katika uwepo wa upepo wenye unyevunyevu kutoka mashariki kuelekea katika Pwani ya nchi.Aidha, matukio ya Vimbunga yanayotarajiwa kujitokezakatika eneo la kusini magharibi mwa bahari ya Hindi sambamba na hali ya joto la chini ya wastani katika eneo la pwani ya Angola, vinatarajiwa kuchochea msukumo wa upepo wenye unyevunyevu kutoka misitu ya Congo katika maeneo mengi.Hali hivyo inatarajiwa kuchangia vipindi vya kuongezakakwa mvua hapa nchini.Hata hivyo, hali ya joto la wastani katika eneo la mashariki mwa bahari ya Hindi inatarajiwa kujitokeza mwishoni mwa msimuna kupunguza msukumo chanya kutoka eneo la Kiikweta la bahari ya Pasifiki kwa mwenendo wa mvua katika pwani ya Afrika mashariki.
  • ATHARI NA USHAURI.
  Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Wanyamapori.
  Katika kipindi cha msimu wa mvua za vuli (Oktoba hadi Disemba) 2018 hali ya unyevunyevu wa udongo na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi ya ukanda wa nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na pwani yakaskazini. Hata hivyo, mazao yasiyohitaji maji mengi yanaweza kuathiriwa na hali ya unyevunyevu wa kupitiliza na maji kutuama. Magonjwa ya wanyama na upotevu wa samaki kutokana na uharibifu wa miundombinu ya kufugia samaki vinaweza kujitokeza kutokana na mvua za juu ya wastani zinazotarajiwa katika maeneo hayo.
  Upungufu wa unyevunyevu unaweza kujitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani. Hivyo, wakulima katika maeneo hayo wanashauriwa kupanda mazao yanayotumia muda mfupi kukomaa na yanayostahimili ukame.
  Malisho na upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo na wanyama pori vinatarajiwa kuwa vya kuridhisha katika maeneo mengi yanayotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani na wastani. Hata hivyo upungufu wa maji kwa ajili ya mifugo na wanyamapori, ufugaji samaki, kupungua kwa samaki katika maji ya asili kutokana na kupungua kwa chakula cha samaki unaweza kujitokeza katika maeneo machache ya magharibi mwa Ziwa Viktoria. Teknolojia ya uvunaji maji ya mvua iimarishwe ili kukidhi mahitaji ya maji katika kipindi cha ukavu.Pamoja na ushauri huu watumiaji wa taarifa za hali ya hewa wanashauriwa kupata ushauri zaidi kutoka kwa wataalam wa sekta husika ikiwemo maafisa ugani.
  Nishati, Madini na Maji
  Maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani, yanatarajiwa kuwa na ongezeko la maji katika mabwawa. Wachimbaji madini katika migodi midogomidogo wanashauriwa kuwa makini kwani ongezeko la maji katika udongo linaweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi.Wadau katika sekta husika wanashauriwa kuchukua hatua stahiki zikiwemo za kupunguza hasara kwa kuimarisha migodi. Hata hivyo, maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani kina cha maji katika maziwa na mabwawa kinatarajiwa kupungua, hivyo matumizi sahihiya maji yanapaswa kuzingatiwa.
  Mamlaka za miji
  Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika msimu wa mvua, hivyo Mamlaka za Miji pamoja na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuchukua hatua za kuhakikisha mifumo na njia za kupitisha maji zinafanyakazi ili kuepusha maji kutuama na kupelekea mafuriko na uharibifu wa miundombinu pamoja na upotevu wa maisha na mali.
  Hatua hizo zinashauriwa kuchukuliwa pia katika maeneo yanayotegemewa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani kutokana na kuwa na uwezekano wa vipindi vifupi vya mvua kubwa.
  Afya
  Kutokana na uhaba wa maji salama unaotarajiwa kwa shughuli za binadamu ikiwemo usafi hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za chini ya wastani, milipuko ya magonjwa inaweza kujitokeza. Aidha, maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani pia yana uwezekano wa kukumbwa na milipuko ya magonjwa, hivyo sekta ya Afya inashauriwa kuchukua hatua stahiki kama kugawa dawa za kutibu maji ya kunywa, kuzuia na kuharibu mazalia ya mbu, kudumisha usafiwa mazingira pamoja na hatua nyingine stahiki ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
  Menejimenti ya Maafa:
  Menejimenti za maafa zinashauriwa kuandaa mkakati wa kupunguza athari zinazoweza kujitokeza katika msimu wa mvua za Vuli, 2018. Kuandaa mbinu za kukabiliana na mafuriko na majanga yatokanayo na mafuriko kama vilekuimarisha na kuweka rasilimali tayari kwaajili ya kukabiliana na maafa, kuandaa vikosi kazi na kamati za maafa na kuandaa maeneo ya kuhudumia waathirika wa mafuriko.
  Aidha, inashauriwa kuimarisha njia za mawasiliano katika ngazi mbalimbaliili kuhakikisha taarifa za tahadhari zinaifikia jamii kwa wakati ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
  Vyombo vya habari:
  Vyombo vya habari vinashauriwa kufuatilia, kupata na kusambaza taarifa sahihi za mienendo ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kutumia wataalam wa sekta husika katika kuandaa na kufikisha taarifa za masuala mtambuka ya hali ya hewa kwa jamii.Vile vilevyombo vya habari vinashauriwa kutafuta na kutumia ushauri wa kisekta kutoka kwa watoa taarifa wa sekta mbalimbali zinazotumia taarifa za hali ya hewa ili kuujulisha umma athari za kisekta.
  Zingatio: Mwelekeo wa mvua uliotolewa hapa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi. Watumiaji wa taarifa za utabiri huu wanashauriwa pia kufuatilia tabiri za saa 24, siku 10 pamoja na za mwezi kama zinavyotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania.
  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini ipasavyo.
  Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania:
  Dkt. Agnes L. Kijazi
  MKURUGENZI MKUU

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna wa Kazi, Bw. Gabriel Malata (wa kwanza kulia). (Kushoto ni) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakimsikiliza Kamishna wa Kazi Bw. Gabriel Malata (hayupo pichani).
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza jambo walipomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Ofisini kwake Jijini Dodoma, (kulia ni) Kamishna wa Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Gabriel Malata. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amekutana na Kamishna mpya wa Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu hii leo Septemba 6, 2018 Jijini Dodoma.

  Aidha, Waziri Mhagama amemkaribisha Kamishna wa Kazi Bw. Gabriel Malata na kumtaka akasimamie utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kwa ufasaha.

  0 0

  Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.

  MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sofia Mfaume amesema kuna kila sababu ya sekta binafsi na sekta za umma kushirikiana kuhakikisha Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla inapiga hatua kimaendeleo.

  Amesema sekta hizo zikishirikiana katika kutatua changamoto zilizopo katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Namtumbo wananchi watapiga hatua kubwa kimaendeleo huku akiomba sekta binafsi kuwekeza ndani ya wilaya hiyo.

  Mfaume amesema hayo leo wakati wa mkutano kati ya sekta binafsi na sekta za umma wilayani Namtumbo.Amesema lengo la mkutano huo ni wadau wa maendeleo kupitia sekta hizo kujadili na kuweka mikakati ya kutatua changamoto na kisha kufanya maendeleo.

  Amewaambia wadau wa maendeleo ni vema wakatambua Wilaya ya Namtumbo kuna fursa nyingi ambazo zikitumika vizuri kutakuwa na maendeleo.“Wilaya yetu ya Namtumbo tunayo ardhi ya kutosha na yenye rutuba inayokubali mazao ya kila aina.Wananchi wanaitumia vema ardhi iliyopo katika kujiletea maendeleo.

  “Ombi langu kwa wadau wa sekta zote hizi tushirikiane katika kuleta maendeleo na kwetu tutafurahi tukiona viwanda vinajengwa zaidi na hasa vya kuongeza thamani ya mazao ya wakulima,”amesema Mfaume.

  Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Namtumbo ambao wamepata nafasi ya kuuzungumzia mkutano huo wamesema unaonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa maendeleo ndani ya wilaya yao na zaidi wanampongeza Mkuu wao wa Wilaya kwani amekuwa chachu ya maendeleo ya wananchi. 
  Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume akizungumza wakati wa mkutano kati ya sekta binafsi na sekta za umma uliofanyika wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma leo
   MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sofia Mfaume akiwa sambamba na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Homera wakifautilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

  0 0
  0 0

  Baadhi ya maduka ya wafanyabiashara katika soko la Mnarani, Loliondo halmashauri ya Mji wa Kibaha Pwani yakiwa yamefungwa kutokana na kushindwa kulipa kodi. Picha na Mwamvua Mwinyi


  NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

  MADUKA ya baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mnarani ,Loliondo ,halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Pwani ,yamefungwa kwa siku tatu baada ya kushindwa kulipia kodi kwa zaidi ya mwaka sasa.

  Kufuatia kufungwa kwa maduka hayo ,wameiomba ofisi ya mkuu wa mkoa huo iingilie kati suala hilo kwani wanatakiwa kulipa sh.8,000 kwa mita za mraba kiasi ambacho ni kikubwa kwao.

  Mfanyabiashara aliyefungiwa duka lake ,Henry Makundi alisema wamehamishiwa kutoka Maili Moja stendi na kupewa maeneo Loliondo ili wajenge maduka na fedha zao watafidia kwenye kodi.

  Alieleza, walikuwa wanataka kuwe na mafungu matatu ya malipo moja ya tatu mkurugenzi na moja ya tatu mfanyabiashara na moja ya tatu iwe ya mfanyabiashara kama wawekezaji moja ya tatu iwe kama faida.

  Makundi alielezea ,halmashauri inataka asilimia 50 na mfanyabiashara 50 ili kurudisha gharama jambo ambalo hawakubaliani nalo. Nae mwenyekiti wa soko hilo ,Ramadhan Maulid alishangaa kuona maduka yanafungwa .

  Alisema kwamba,kulikuwa na makubaliano walipe mita za mraba 4,000 huku akiwepo mkurugenzi na mbunge wa mji huo hivyo wanashangaa kuambiwa walipie sh 8,000. Maulid alifafanua, kutokana na hali hiyo wanaendelea na mazungumzo na katibu tawala wa mkoa ili kuangalia namna ya kulishughulikia suala hilo .

  Akijibu hoja za wafanyabiashara hao mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Jeniffer Omolo alisema ,walikubaliana kuwa wafanyabiashara wajenge maduka kwa gharama ya sh .milioni tano na halmashauri walitoa ardhi lakini hawajalipa kodi zaidi ya mwaka sasa. Kwa mujibu wake ,wamegundua wengi wanaofanya biashara ni wapangaji na sio waliojenga maduka ambayo wanapangisha kuanzia sh.300,000 hadi sh.400,000 kwa mwezi.

  Jennifer alibainisha ,kwa mwaka wanapata kati ya sh.milioni 3.6 – milioni 4.8 kwa miaka miwili anakuwa amerejesha gharama zake za ujenzi . Mkurugenzi huyo aliwataka ,wale ambao gharama zimezidi ya waliyokubaliana waende ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo.

  Jennifer alielekeza ,wafanyabiashara ambao hawajalipa kodi kulipa kwani kutolipa kodi ni kinyume cha sheria , ili waepukane na usumbufu.

  0 0  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) na Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma (kulia) wakiangalia moja ya mawe ili kubaini madini yaliyomo kwenye machimbo ya Suguta yaliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
  Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (hayupo pichani) kwenye machimbo ya Suguta yaliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (mbele) pamoja na msafara wake wakiendelea na ziara kwenye kwenye machimbo ya Suguta yaliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
  Mmoja wa watendaji wa migodi ya shaba ya Rays Metal Corporation na Tambi Minerals Resources iliyopo katika kijiji cha Tambi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati). Kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega.
  Sehemu ya mgodi wa shaba wa Rays Metal Corporation uliopo katika kijiji cha Tambi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembie. Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega.
  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Deogratius Ndejembie (kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
  Kutoka kushoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya, Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Deogratius Ndejembie na Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho.
  .

  Na Greyson Mwase, Dodoma

  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amemwagiza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya kuhakikisha wanakipatia kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini kijulikanacho kwa jina la “Hapa Kazi Tu” kinachoendesha shughuli za uchimbaji wa madini aina ya sunstone katika kijiji cha Suguta wilayani Kongwa mkoani Dodoma leseni ya uchimbaji madini ndani ya mwezi mmoja kwa kufuata kanuni na sheria za madini.

  Profesa Kikula alitoa agizo hilo tarehe 05 Septemba, 2018 katika machimbo ya madini hayo yaliyopo katika kijiji hicho kwenye ziara yake ya siku mbili katika wilaya za Kongwa na Mpwapwa yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo, kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.

  Katika ziara hiyo, Profesa Kikula aliambatana na Makamishna wa Tume, Profesa Abdulkarim Mruma na Haroun Kinega, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya pamoja na waandishi wa habari.

  Mara baada ya kusikiliza kero za wachimbaji wadogo hao Profesa Kikula mbali na kutoa agizo hilo alimwelekeza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto, kuhakikisha anasaidia kikundi cha wachimbaji wadogo hao katika taratibu zote za usajili wa kikundi kabla ya kuanza kushirikiana na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma katika upatikanaji wa leseni ndani ya mwezi mmoja.

  Aidha, Profesa Kikula alimtaka Mwenyekiti huyo kuwasaidia wachimbaji hao katika usajili kwenye vyama vya wachimbaji madini Tanzania pamoja na utafutaji wa masoko na bei elekezi kwenye masoko ya kimataifa.

  “Kutokana na kuwa na mtandao mkubwa na uelewa kwenye masoko na bei elekezi za madini kwenye masoko ya kimataifa, nakuelekeza kama Mwenyekiti wa wachimbaji kuhakikisha unawasaidia wachimbaji hawa hususan kwenye maeneo ya masoko na bei elekezi ili uchimbaji wao uwanufaishe wao na Serikali kupata mapato stahiki,” alisema Profesa Kikula.

  Profesa Kikula alisema Serikali kupitia Tume ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia uboreshaji wa sheria na kanuni za madini pamoja na utoaji wa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu sheria na kanuni hizo.

  Katika hatua nyingine, Profesa Kikula aliwataka wachimbaji wadogo nchini kuhakikisha kupitia viongozi wao kwenye vyama vya wachimbaji madini wanashirikiana kwa karibu na viongozi wa vijiji, wilaya na ofisi za madini ili uchimbaji wao ulete tija zaidi kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Awali, wakiwasilisha kero mbalimbali wachimbaji hao walisema kuwa wamekuwa wakikutana na vikwazo mbalimbali kwenye usajili wa kikundi chao hali iliyopelekea ucheleweshwaji wa maombi ya leseni.

  Akizungumza kwa niaba ya kikundi hicho, Job Pandila alisema awali waliwasilisha maombi yao kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya taratibu za usajili lakini kumekuwa na ugumu katika usajili wa kikundi chao kutokana na kutokuwa na uelewa wa namna bora ya kuwasilisha viambatisho kwenye maombi ya usajili wa kikundi.

  Pandila aliendelea kusema kuwa uchelewaji wa usajili wa kikundi umepelekea kushindwa kuomba leseni ya madini na kuomba msaada katika usajili wa kikundi pamoja na maombi ya leseni ili waendelee na uchimbaji wa madini na kujipatika kipato.

  Awali kabla ya kufika katika kijiji cha Suguta, Profesa Kikula alikutana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembie na kuelezwa changamoto mbalimbali kwenye shughuli za uchimbaji madini zilizopo katika wilaya ya Kongwa.

  Katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembie alisema kumekuwepo na mgogoro kwenye eneo la Suguta lililopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma kutokana na wachimbaji wengi kutokuwa na leseni za uchimbaji madini pamoja na uelewa mdogo wa sheria na kanuni za uchimbaji madini.

  Aidha, Ndejembie alimpongeza Profesa Kikula na timu yake kwa kutembelea wilaya ya Kongwa na kusisitiza kuwa ziara hiyo mbali na kutoa elimu kwa wachimbaji madini, itapunguza migororo isiyo na lazima iliyokuwa ikijitokeza.

  Wakati huo huo katika kikao chake na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Profesa Kikula aliwataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Nchini kuandaa utaratibu wa utoaji wa mafunzo kwa wachimbaji madini kuhusu sheria na kanuni za uchimbaji madini.

  Katika ziara hiyo Profesa Kikula pamoja na ujumbe wake, walitembelea pia machimbo ya Rays Metal Corporation na Tambi Minerals Resources yaliyopo katika kijiji cha Tambi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

  0 0

  Diwani wa kata ya Pangani Kibaha mkoani Pwani, akielezea kero ya kivuko kwa wakazi wa eneo la Lumumba na Kidimu. Picha na Mwamvua Mwinyi


   
  NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

  BAADHI ya wakazi wa mitaa ya Lumumba ,Muheza na Kidimu (LUMUKI) wilayani Kibaha ,mkoani Pwani ,wanahitaji serikali iwasaidie kuwajengea daraja ama kivuko kwenye mto Mpiji ili kunusuru maisha yao. Wakazi hao kwasasa wanapata shida ya kuvuka kwenda mtaa wa Kibwegere kata ya Kibamba ,wilaya ya Ubungo ambako ndipo wanategemea kupata huduma za kijamii. 

  Walifikisha kero hiyo ,walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi la ujenzi wa nguzo kwa ajili ya kuvusha watu . Mwenyekiti wa ujenzi wa daraja hilo la LUMUKI, Iddi Chamale alisema ,changamoto kwenye eneo hilo ni kubwa .

  Aidha , wamekuwa wakiweka vivuko vya muda ambapo huweka mabanzi kwa ajili ya kuvuka ambapo wakati wa mvua kubwa yanasombwa na maji hayo. “Kivuko kikisombwa shida ndipo zinapoanza kwani hubidi watu wavushwe kwa kubebwa ambako kuna mamba wengi na ni hatari kwani maji yakiwazidia ni hatari watu wanapoteza maisha,” alifafanua Chamale. 

  “Makao makuu ya wilaya ya Kibaha ni mbali lakini kwa kuvuka mto ni karibu hivyo inatubidi twende Kibwegere, tumetenganishwa na mto Mpiji lakini kinachotusumbua ni sehemu ya kuvuka ” alisema Chamale.

  Nae Neema Zawadi alisema , kipindi cha mvua ni taabu kwani mawasiliano hukatika na watu hupoteza maisha wanapojaribu kuvuka huku wajawazito hujifungulia njiani kabla ya kuvuka mto. “Wanafunzi hushindwa kwenda shule wazazi huogopa wasivushwe,wafanyakazi huwabidi wakae ngambo hivyo kutorudi nyumbani hivyo hata ndoa zetu zinayumba”alisema Neema. 
   
  Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Pangani iliko mitaa hiyo Agustino Mdachi ,alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema jitihada wanazofanya ni kujenga vivuko lakini havidumu . Alielezea, amekuwa akiwasilisha changamoto hiyo halmashauri lakini tatizo ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kujenga daraja. Mdachi alisema atawasiliana na wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili walishughulikie suala hilo.

  0 0
 • 09/06/18--21:58: Article 2

 • 0 0

  Meli ya Kwanza iliyobeba Tani 7,250 za Reli za SGR kutoka Japan imetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na kazi ya kupakua reli na kupeleka eneo la ujenzi imeanza jana Septemba 06, 2018 tayari kwa ajili ya kutandika reli. Meli nyingine ya Reli za SGR inatarajiwa kufika mwezi Oktoba 2018.

  Meli iliyobeba Tani 7,250 za Shehena ya Reli za SGR ikiwa katika Bandari ya Dar es Salaam Septemba 06, 2018.

  Kazi ya kupakia Shehena ya Reli za SGR ikiendelea katika Bandari ya Dar es Salaam Septemba 06, 2018.


  Tani 7,250 za Shehena ya Reli za SGR zikipakuliwa kutoka kwenye Meli katika Bandari ya Dar es Salaam Septemba 06, 2018.
  Kazi ya kupakia Reli kwenye mabehewa ikiendelea katika Bandari ya Dar es Salaam Septemba 06, 2018.

  0 0


  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Nyamongo mkoani Mara wakati akitokea Mugumu Serengeti.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua daraja hilo la mto mara lenye urefu wa mita 94 linalounganisha katika ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyansura Serengeti mara baada ya kukagua mradi wa daraja la mto mara lenye urefu wa mita 94 linalounganisha katika ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Nyambura Nyamarasa ambaye alikuwa na kero ya kulishiwa na shamba lake na mfugaji mmoja huko Mugumu Serengeti mkoani Mara.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa shilingi milioni moja Nyambura Nyamarasa ambaye alikuwa na kero ya kulishiwa na shamba lake na mfugaji mmoja huko Mugumu Serengeti mkoani Mara.

  Sehemu ya Daraja la mto mara mita 94 ambalo ujenzi wake unaendelea na litaunganisha kati ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara. PICHA NA IKULU

  0 0

  Bw. Jacob Steven akishusha Juisi yake mara baada ya kupata Mbuzi Choma kwenye mgahawa wa Food Point uliopo Namanga jijini Dar es salaam.


  Mwigizaji wa filamu Nguli nchini Bw. Jacob Steven maarufu kama JB ameusifia mgahawa wa Food Point na kusema amekula mbuzi ya kuchoma katika mgahawa huo imemvutia sana na haina harufu testi yake ameifananisha na mbuzi ya kuchoma ambayo aliwahi kula katika moja ya migahawa aliposafiri kwenda nchini Uturiki kwa ajili ya shughulizake za kibashara.

  JB amesema Food Point nitapafanya mahali pangu pa kupata chakula cha mchana na wakati mwingine hata jioni kwa sababu pia hawauzi pombe kama sehemu zingine ambako mara nyingi kunakuwa na vurugu kutokana na wanywaji wa pombe, Hivyo kwangu mimi naona hapa ni mahali salama sana na unaweza kupumzika na marafiki zako pia.

  JB Anaongeza kuwa "Mahali hapa ni pasafi sana na kuna hali ya hewa nzuri yaani wanajitahidi sana lakini pia mtu yeyote mwenye kujielewa anapenda usafi na hata ukiwa na wageni wako unaweza kuwakaribisha hapa kwa sababu usafi wao.

  Ameongeza kuwa nitajaribu kuonja vyakula mbalimbali na vinywaji vinavotengenezwa na kupikwa hapa nadhani vyakula vingi vitakuwa vitamu sana na mimi ni mtu ninayependa sana kula vyakula vizuri hivyo nitapenda kuonja vyakula mbalimbali nione ladha yake.

  Amemaliza na kusema "Kitu cha ziada kinachomvutia katika mgahawa wa Food Point ni ukaribu na barabara kuu jambo ambalo linakufanya mtu kutopata tabu kuhusu usafiri, unatoka hapo unaita gari wakati wowote na kama una usafiri wako pia muda mfupi unaingia barabara kuu jambo ambalo linanifanya kupenda zaidi Food Point.

  0 0

   Waheshimiwa Mashakimu Wakzi wa Mikoa na Wilaya kutoka Mikoa mitano ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara, wakiwa kwenye mahakama ya mfano ili kujipima kuona uelewa wao kuhusu Sheria ya Bunge ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu namba 5  [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] naada ya kushiriki mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na kuratibiwa kwa pamoja na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kufanyika mkoani Morogoro kuanzia Septemba 5-6, 2018.  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro

  MAHAKIMU wakazi wafawidhi wa Mahakama za Mikoa na Wilaya kutoka mikoa mitano ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara, wamefurahishwa na mafunzo ya kuwajengea uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] ambapo jukumu lake kubwa ni kutoa fidia kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya.
  Kutokana na jukumu hilo la Mfuko, Chuo cha Uongozi wa Mahama Lushoto ambacho ndicho chenye dhamana ya kutoa mafunzo kwa watumishi waandamizi wa mahakama, kiliandaa mafunzo hayo ili kuwawezesha viongozi hao wa mahakama wa ngazi za mikoa na wilaya kuelewa vema Sheria hiyo ili iwe rahisi kwa wao kutoa maamuzi sahihi endapo mashauri yahusuyo fidia kwa wafanyakazi na shughhuli za Mfuko yatafika mbele yao. Amesema Mkuu wa Huduma za Sheria wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Abraham Siyovelwa.
  Wakizungumza katika mahojiano baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Elizabeth Nyembele, alisema
  “Nimefurahia sana kupata mafunzo haya, mimi nina nafasi mbili, kwanza kabisa kama mfanyakazi,  lakini pia kama mdau mkubwa wa Sheria ya Mfuko huu kama hakimu, nimefaidika sana na elimu hii kwani nimeelewa vitu vingi ambavyo hapo awali sikuwa nikivijua.”
  Alisema, elimu aliyoipata kama mtumishi wa mahakama, ameelewa haki zake za msingi kuhusiana na Mfuko huo wa Fidia ameridhika na kufurahia kuwa anafanya kazi katika mazingira ya uhakika na akiamini pia hata wategemezi wake lolote likimtokea kutegemea na Mungu amepanga nini, basi wategemezi wake wanaweza kunufaika licha ya yeye mwenyewe.
  “Uelewa nilioupata baada ya mafunzo haya ni mkubwa sana hususan kwenye makosa ya jinai yameelezwa bayana, na nimeelewa jinsi nitakavyosimamia sheria hii endapo nitakutana na kesi yoyote itakayoletwa mbele yangu, kwa sababu ninailewe sheria hii kwa kina.” Alisema
  Alishauri pia Mfuko uendelee kutoa elimu hususan kwa wafanyakazi, kwani wengi hawajui manufaa ya huu Mfuko.
  Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi, Mhe. James Mutakyahwa Karayemaha amesema, mafunzo aliyoyapata yamemfanya apate uelewa mpana kuhusu sio tu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na namna gani anapaswa kuisimamia wakati atakapokutana na mashauri yahusuyo Fidia kwa wafanyakazi, lakini pia amepata uelewa wa faida anazoweza kupata yeye binafsi kama mtumishi wa umma.
  “Nimejua kuwa mwajiri kwa mujibu wa Sheria hii, anao wajibu wa kujisajili na kuwasilisha michango ya kila mwezi kwa Mfuko na asipofanya hivyo anatenda kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo,  faini au vyote viwili.” Alisema
  Alisema pia amejua kuwa kama mfanyakazi hapaswi kushwishiwa kwa namna yoyote ile na mwajiri wake, kutoa taarifa mbili tofauti za viwango vya mishahara, ambapo taarifa za malipo ya mtumishi zikionyesha kiwango cha juu cha mshahara na taarifa zinazopelekwa WCF zikionyesha kiwango cha chini cha mshahara.
  “Taarifa hizi zisizosahihi kama hizi ni janga kwa mfanyakazi kwani endapo atapatwa na tatizo lolote la kuumia akiwa, kuugua au hata kifo akiwa kazini, inapofika wakati wa kufidiwa, malipo hayo yatazingatia taarifa za malipo ya mshahara zilizokuwa zikiwasilishwa  kwenye Mfuko.” Alisema.
  Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara, Mhe.Godfrey Mwambapa, alisema kimsingi yeye ameongeza weledi kuhusu sheria inayoendesha na musimamia shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
  “Mfuko huu nunatuhusu watu wote tulio kwenye ajira na kwakweli unatusaidia hasa kuwa salama sehemu ya kazi endapo utapatwa na matatizo sehemu ya kazi Mfuko huu utakuja na kunifanya niishi kama vile nikiwa kazini na kuniondolea magumu yote ya kimaisha.” Alsiema.
  Alisema, yeye kama hakimu ameweza kuelewa sheria inayosimamia Mfuko na hata kama shauri lihusulo masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi litamfikia mbele yake yuko katika nafasi nzuri ya kusimamia sheria hii kwani ameielewa vilivyo.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, mafunzo hayo ni muendelezo wa mipango ya Mfuko kutoa elimu kwa wadau wote ambapo tayari Mfuko umetoa elimu kw amadaktari kote nchini, Waajiri kote nchini, lakini pia elimu kwa wafanyakazi kwenye maeneo yao ya kazi kupitia ziara za maafisa wa WCF kwenye taasisi mbalimbali hapa nchini.
   Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Chuom cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, (IJA), Mhe. jaji Dkt.Paul Kihwelo, akitoa nasaha zake kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya JIA na WCF. Aliyesimama kushoto ni mratibu wa mafunzo, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo hicho, Mhe. Lameck Samson.
   Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Temeke jijini Dar es Salaam, Mhe. Susan P. Kihawe (kuli) akifurahia jambo wakati akizungumza na mwenzake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Ilala, Mhe. Martha Mpaze.
   Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Elizabeth Nyembele, akizungumza.

   Waheshimiwa mahakimu wakiwa kwenye majadiliano ya vikundi.
   Mhe.S.Mwalusamba (kushoto) na Mhe.Godfrey Mwambapa wakifuatilia kwa makini.
   Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Mhe. Gofrey Isaya, akizungumza
   Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Pwani, Mhe.Joyce J. Mkhoi, akitoa maoni yake kwenye semina hiyo.
   Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Mhe. Batista Kashushe, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
   Mhadhiri Msaidizi Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Lameck Samson akifafanua jambo.
   Hakimu Mkazi wa Mfawidhi Mahakama ya Kilombero/Ifakara Mkoani Morogoro, Mhe. L.Khamsini akisikiklzia kwa makini wakati Mkuu wa Huduma za Sheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada.
   Majadiliano ya vikundi
   Majadiliano ya vikundi
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba, (wapili kushoto), akimkabidhi cheti cha ushiriki, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka, mwishoni mwa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo mahakimu wakazi wa mikoa na wilaya yaliyofikia kilele mkoani Morogoro Septemba 6, 2018. Wengine pichani ni Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa. na kulia ni Mhadhiri Msaidizi, Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Lameck Samson.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba, (kulia) na Mkuu wa Huduma za Sheria, wa Mfuko huo, Bw. Abraham Siyovelwa, wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kuwapongeza mahakimu hao baada ya kumaliza mafunzo.
   Majadiliano ya vikundi.
  Afisa Uhusiano na Mawasiliano mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, (kushoto), na Afisa Sheria wa Mfuko huo, Bw. Deo Victor wakijadiliana jambo mwishoni mwa mafunzo hayo.

  Afisa Sheria WCF, Bw. Deo Victor (aliyesimama kulia) akisimamia majadiliano ya vikundi kuhusu kile kilichofundihswa. 

  0 0  Wahitimu wa programu ya kampuni ya Vodacom Tanzania wakikata keki kusherehekea kumaliza programu ya miaka miwili iitwayo 'Discover Graduate'. Programu hii iliyoanzishwa July mwaka 2017 inalenga kufunza na kusaidia wanafunzi bora kutoka vyuo mbalimbali nchini kuja kuwa viongozi bora wa kesho.
  Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Perece Kirigiti akimkabidhi Gervas Mfubusa, moja kati ya watahitimu waliochaguliwa kuingia kwenye programu ya 'Discover Graduate'. Discover Graduates ni programu ya miaka miwili iliyodhamiriwa kufunza na kusaidia wahitimu bora kutoka vyou mbalimbali nchini kuja kuwa viongozi bora wa kesho.


  Programu nyingi za mafunzo kwa wahitimu wa vyuo vikuu wasio na uzoefu wa kazi duniani kote, zimekuwa zinalenga kuwawezesha wasomi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuwa na dhamira ya kuajiriwa kwenye makampuni mbalimbali yanayohitaji wataalamu. Huwawezesha wahitimu hao kupata msingi na ujuzi kuhusiana na taaluma zao, sambamba na kuwaanda kuwa viongozi wa siku za mbele.

  Tofauti na programu nyingine za kuwafundisha wahitimu wa vyuo vikuu kazi,Programu ya Vodacom Tanzania (ambayo imeasisiwa na Vodafone Group) inajulikana kama ‘Gundua Vipaji vya Wahitimu wa Vyuo Vikuu). Humuwezesha mhitimu kufanya kazi kwenye vitengo muhimu vya kampuni.Programu hii ya miaka 2 inalenga kuwapata viongozi wa baadaye wa kuendesha biashara za kampuni kutoka kwa wahitimu wa vyuo vikuu waliobobea katika fani mbalimbali.Kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya hapa nchini,lengo ni kukuza vipaji na kuwapata wataalamu ambao watafanikisha kuiwezesha Vodacom kwenda sambamba na mabadiliko katika sekta ya mawasiliano.

  Programu hii ya ‘Gundua vipaji vya wahitimu wa Vyuo vikuu’ nchini Tanzania, ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi Julai,mwaka 2015 na ilianza kwa kupokea maombi ya wahitimu 10 kutoka vyuo mbalimbali ambao walichukuliwa katika awamu ya kwanza ilipoanzishwa.

  Ili kujiunga nayo,mhitimu anapitia mchakato mkali uliowekwa, kuhakikisha wanapatikana washiriki wenye sifa zinazostahili. Wahitimu wanafanyiwa tathmini kwa njia ya mtandao,kupitia uelewa wa majukumu watakayotekeleza,tathmini kwa njia ya makundi,uwezo wa kuwasilisha mada na kujieleza na mahojiano ya uso kwa uso.
   
  Vilevile,moja ya vigezo vya kuchaguliwa ni kufanyiwa tathmini kuhusiana na ujuzi unaofaa kwa shughuli za kampuni na jinsi anavyoelewa kanuni za kazi za kampuni ya Vodacom (kuhudumia wateja kwa ufasaha,kuwa mbunifu,uwezo wa kutatua changamotoharaka,kuwa tayari kubadilika),mchakato huu una lengo la kuwapata wahitimu walengwa kwenye programu ambao wanafaa na wanaweza kwenda sambamba na utekelezaji wa kanuni za kampuni. Wahitimu wanaofanikiwa kujiunga hupatiwa mafunzo na msaada wanaohitaji ili kuhakikisha kila mmoja anapata ujuzi na uzoefu wa kazi.

  Mkurugenzi Rasilimali Watu, Bi.Perece Kirigiti, anakiri kuwa programu imepata mafanikio makubwa tangia kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2015 , anazidi kufafanua zaidi mafanikio hayo “Jambo la kipekee na la kufurahisha kuhusiana na programu hii ni mchakato wa kuwapata washiriki wake,wahitimu wanaofanikiwa kushinda na kupata nafasi wanakuwa sawa na wafanyakazi wengine walioajiriwa moja kwa moja na kampuni.
  Wanaaminiwa kufanya kazi za kila siku za kampuni ,wakiwa wanapata maelekezo na mafunzo kutoka kwa viongozi wa vitengo vyao vya kazi,”alisema na kuongeza kuwa wahitimu hao wanapokuwa kwenye mafunzo hayo wanaweza kufanyiwa tathmini kutokana na jinsi wanavyotekeleza kazi zao na kuzungushwa kwenye vitengo mbalimbali ili kuelewa biashara za Vodacom,ili kuwawezesha kupata ujuzi wa kuwawezesha kufanya kazi wanazopangiwa kwa ufanisi na kuwa wabunifu wa kukabili changamoto mbalimbali.

  Sifa nyingine muhimu katika hii programu ni jinsi inavyowezesha wahitimu wanaojiunga nayo kujifunza utendaji kazi kwa haraka kupitia mtandao wa programu unaotekelezwa katika nchi mbalimbali duniani. Baada ya kipindi cha miaka miwili,mhitimu aliyepo kwenye mpango huu anakuwa na sifa ya kuomba kujiunga na programu nyingine ya mafunzo kwa wahitimu ya Vodafone Group, inayojulikana kama Columbus.Wanaofanikiwa kujiunga na programu hii hupata fursa ya kufanya kazi nje ya Tanzania na kuzidi kupata ujuzi na uzoefu kwa ngazi ya kimataifa na kuishia kuwa wafanyakazi wa ngazi za juu ndani ya kampuni.

  “Wahitimu wanaojiunga na mpango huu na kufanya vizuri katika kazi za kampuni,wanakuwa na nafasi ya kushindania kupata fursa ya kujiunga na programu ya mafunzo ngazi ya kimataifa ya Columbus,ambayo huwezesha kupata uzoefu wa kufanya kazi mwaka mmoja nje ya nchi, katika kipindi cha muda mfupi tangu kuanza kazi.Tunahakikisha wahitimu hawa wanaendelezwa kwenye fani zao kwa kupatiwa uzoefu wa kazi kwa kuaminiwa na kukabidhiwa majukumu ya kazi siku hadi siku.Ushirikishwa wao huu huwawezesha kuelewa uendeshaji wa biashara za Vodacom vizuri na kuwa na uwezo wa kuonyesha uwezo na vipaji vyao”Alifafanua.

  Vodacom Tanzania imebaini kuwa programu ya kufundisha wahitimu wasio na uzoefu wa kazi kutoka vyuo vikuu ni njia mojawapo ya kuwapata wafanyakazi wa kuendeleza kazi za kampuni wakiwa wanaelewa misingi ya kazi ya kampuni na ni moja ya njia ya kuwaendeleza wafanyakazi wake kukuza taaluma zao na kuleta mabadiliko katika kipindi kifupi tangia wanapoanza kazi baada ya masomo “Tunao utamaduni tunaojivunia nao wa kuendeleza wafanyakazi wetu,Ni jambo la fahari kwetu kama kampuni kuona vipaji vya vijana wetu vinaendelezwa.”Alisema Perece.

  Gervas Mfubusa, Keisha Mushi na Amandus Madyane, ni wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao walibahatika kujiunga katika awamu ya kwanza ya Programu ya ‘Gundua vipaji vya wahitimu wa Vyuo Vikuu’ ya Vodacom Tanzania.Walichaguliwa kutokana na uwezo wao na utayari wao wa kufanya kazi na kujifunza kazi kwa vitendo kwa ajili ya kufungua njia za kukuza taaluma zao.Wameweza kutoa ushuhuda wao,wameeleza uzoefu na mafunzo waliyofanikiwa kuyapata kupitia programu hii.

  Gervas, ambaye kwa sasa anafanyia kazi katika kitengo cha Raslimali Watu, anasema kuwa Programu hii imemsaidia kwa kiasi kikubwa kupata uzoefu wa kazi “Nilikuwa mwepesi wa kujifunza ili kufanya vizuri katika muda wote nilipokuwa kwenye mafunzo .Nilipata uzoefu mkubwa na kuwa na nafasi ya kuwajibika kufanya maamuzi ambayo yaliweza kuchangia kuongeza mapato ya kampuni,”alisema Gervas.

  Kwa upande wa Keisha, anaeleza kuwa mbali na kujifunza kazi alipata bahati ya kufundishwa na wafanyakazi wataalamu na wenye uzoefu mkubwa wa kazi. Alipata fursa ya kufundishwa kazi na Mkurugenzi wa Kitengo alichopangiwa kufanya kazi , alifanikiwa kupati ujuzi mkubwa wa kazi kutoka kwake.”Tunafundishwa mbinu za kupata ujuzi mpya wa kazi kupitia kupewa majukumu ya kutekeleza kwa kufanya kazi kwa karibu na viongozi waandamizi katika kampuni,”aliongeza kusema Keisha.

  Naye Amandus, kwa upande wake aliipongeza programu hii inayowalenga wahitimu kutoka vyuo vikuu wasio na uzoefu wa kazi na kuwekeza kwao kwa kuwapatia ujuzi na kuwabadilisha kuwa wataalamu katika kipindi cha muda mfupi.”Kitu mojawapo kikubwa kuhusu Vodacom ni jinsi inavyojikita kuhakikisha mchango wa mshiriki wa programu katika kufanya kazi bila kujali mwonekano wake wa nje-Ingawa ni jambo la muhimu kuwa maridadi kimavazi na kujiamini,lakini mambo hayo sio ya msingi sana wakati wa mchakato wa kuchagua washiriki wa kujiunga na programu hii,”Amandus alifafanua.

  Uongozi mzuri na usimamizi ni mambo ya msingi yanayowezesha kupata mafanikio ya Programu ya Kugundua na kukuza vipaji vya wahitimu wa vyuo vikuu wasio na uzoefu wa kazi ,wanathibitisha washiriki wake.Wafanyakazi wenye ujuzi na uzoefu wamekuwa wakifanya kazi na kujenga uhusiano wa kikazi wa karibu na wahitimu wa vyuo vikuu wanaokuwa kwenye mafunzo ,na kuhakikisha wanawasiliana kwa kila jambo kuhusiana na mambo wanayohitaji kuyafahamu sambamba na kutoa taarifa kuhusiana na majukumu ya kazi wanazokuwa wamepangiwa kufanya.

  Gervase ,safari yake katika kampuni ya Vodacom imekuwa ni kujifunza kazi na kupata uzoefu “Kufikia matarajio ya mafanikio kunaenda sambamba na kukumbana na changamoto,lakini inafurahisha unapopata mafanikio mazuri kutokana na kutumia vizuri fursa za kukuwezesha kuyafikia”.

  “Ukiwa katika programu hii unapata msaada na kutiwa moyo na wafanyakazi wa Vodacom wakati wote,na hii inakufanya ujiamini katika kutimiza majukumu kutumia ujuzi wa taaluma yako”aliongeza Keisha.

  Kwa mujibu wa Amandus,Vodacom imekuwa ikitafuta vijana wenye vipaji kwa ajili ya kufanya ubunifu wa kurahisisha huduma wa wateja wake “Maoni na mapendekezo yetu yamekuwa yakisikizwa na kufanyiwa kazi,na hii ili ilitutia moyo kushiriki kuchangia mawazo yetu katika kuboresha kazi na kufanya ubunifu zaidi wa kukabili matatizo mbalimbali yaliyopo katika kuboresha kazi.”

  Alipoulizwa anatoa ushauri gani kwa wahitimu watakaojiunga na programu hii katika siku zijazo,Gervas alisema “Wanatakiwa kufanya kazi kwa bidi,wasikilize vizuri wasimamizi wako wanaokufundisha ,kutoogopa kuwauliza maswali unapokumbana na suala ambalo huelewi namna ya kulitatua.Kuwa tayari kukubali kushindwa kwa baadhi ya mambo ila uwe mwepesi wa kujipanga na kuanza tena kujifunza,Hakikisha unazingatia kila unalofundishwa. Kuwa Msikivu na nia ya kujifunza mambo mengi zaidi!”

  Keisha, kwa upande wake aliongeza kusema “Siku zote kuwa mstari wa mbele kujifunza,tumia vizuri fursa hii uliyoipata ambayo wapo wenzako wengi hawakufanikiwa kuipata,huwezi amini kwa jinsi utakavyofanya kazi kwa bidii ndio matarajio yako yatakavyotimia.”

  Amandus, alisisitiza suala la kuwa myenyekevu unapokuwa katika mchakato wa mafunzo haya,alifafanua zaidi “Programu hii ya kuendeleza wahitimu katika kampuni ya Vodacom ni fursa bora na pekee kuipata ,itumie vizuri, kuwa msikivu na kumheshimu kila mmoja.Huwezi kujua nani anaweza kukupendekeza kupata fursa mbalimbali nzuri katika maisha yako.

  “Ubora wetu unaletwa na ubora wako”ni kauli mbiu inayotumika Vodacom kuelezea umuhimu wa kuwa na timu nzuri ya wafanyakazi wanaoleta tija na ufanisi katika kampuni inayowafanya waonekane tofauti na wafanyakazi wa taasisi nyinginezo.

  Ukifanya kazi Vodacom,unajisikia upo sehemu nzuri kutokana na jinsi kampuni inavyokujali.Afya yako na Usalama mahali pa kazi ni mambo yanayopewa kipaumbele kuliko kitu chochote.Mazingira mazuri ya kazi na taratibu nzuri za kazi ndio yanaifanya Vodacom kuwa Mwajiri Bora nchini Tanzania”Alimalizia kusema Keisha Mushi.

  Kampuni imefanikiwa kushinda tuzo ya Mwajiri Bora barani Afrika kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo,hii inadhihirisha Vodacom ina mazingira mazuri ya kazi yanayoleta furaha kwa wafanyakazi wake.Ikiwa ni mshindi wa Tuzo za Mwajiri Bora,wenye vipaji wengi wamekuwa wakivutiwa kuajiriwa na Vodacom kutokana na kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi ambayo pia yanayavutia vijana wengi wenye taaluma tofauti wanaohitaji kufanya mafunzo ya vitendo.

  Wakati kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, ikitambua kuwa kuna mambo mbalimbali katika uendeshaji wa shughuli zake yaliyowezesha kufanikiwa kupata tuzo hii,Programu ya kuendeleza wahitimu imechangia kwa kiasi kikubwa kufikia vigezo vya ushindi huo.

older | 1 | .... | 1667 | 1668 | (Page 1669) | 1670 | 1671 | .... | 1898 | newer