Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1666 | 1667 | (Page 1668) | 1669 | 1670 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile alipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa Nduli kwa kufahamu maendeleo ya ukarabati mdogo wa uwanja huo na kubaini baadahi ya changamoto zinaukabili uwanja huo hasa katika swala la majengo kuto kidhi mahitaji ya wasafiri 
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile wakiwa kwenye eneo ambalo linafanyiwa ukarabati mdogo 
   Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakipata maelezo kutoka kwa meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile juu ya ukarabati wa uwanja unaoendelea

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kamanda wa police mkoa wa Iringa Juma Bwire wakiangalia jengo la wasafiri katika uwanja wa nduli mkoani Iringa
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile wakiwa ndani katika sehemu ya abiri ambao wanasubiri kusafiri.  
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari wakati wa ziara katika uwanja wa nduli na kubaini mapungufu mengi ikiwapo gari hilo ambalo linaonekana la zimamoto ambalo toka lifike hapo halijawi kufanya kazi kutokana na kuwa bovu na spea zake kutopatikana.


  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
  MKUU wa mkoa wa Iringa Ally
  Hapi hajaridhishwa na hali halisi ya uwanja wa ndege wa nduli uliopo kata ya
  nduli kuelekea kuijenga Iringa mpya kwa maendeleo ya wanairinga.

  Akizungumza wakati wa ziara
  ya kukagua ukarabati mdogo unaoendelea katika uwanja huo,hapi alisema kuwa
  uwanja huo wa ndege unahitaji ukarabati wa maana ili kukidhi mahitaji ya
  watumiaji na kukuza maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa.

  “Nimetembea kwenye maeneo
  mengi ya uwanja huu hayaridhi wala hayavutii kwa wawekezaji kuja mkoani hapa
  kwa kuwa saizi wawekezaji wengi wanapenda kutumia usafiri wa anga hivyo ni
  lazima kuwa na kiwanja cha ndege ambacho kitakidhi na kuvutia watalii na
  wawekezaji wanapokuja mkoani hapa” alisema Hapi

  Hapi alisema kuwa jengo la
  wageni la uwanja huo ni dogo,halina ubora unaotakiwa na halikidhi kuwa katika uwanja
  huo ambao hivi karibuni utaanza kupokea wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali
  ya ndani ya nje ya nchi.

  “Sehemu hii ya kupumzikia
  wageni hakuna,sehemu ya wasafiri wanapoongokea bado ni ndogo na haina vigezo
  vya kuwa eneo la kupuzikia wasafiri,vyoo havifai eneo lenyewe bado halina
  miundombinu ya kisasa ambayo itawavutia watu wengi kuja mkoani Iringa hivyo tunahitaji
  kujenga jengo jipya na la kisasa kabisa” alisema Hapi

  Haiwezekani uwanja wa ndegehuu
   ukawa unamajengo na vifaa vingi ambavyo
  vimechoka na havikizi mahitaji ya kuijenga Iringa mpya hivyo ni lazima kuwekeza
  kwenye uwanja ili kuvutia wawekezaji na watalii ambao watakuja mkoani hapa.

  Hapi aliongeza kuwa uwanja
  wa ndege wa Nduli hauna hapa gari la fire ambalo litasaidia kuongoa majanga
  yoyote yatakayotokea kwenye uwanja huu,hivyo ni lazima tserikali ijue kuwa
  tunahitaji kuwa na gari la fire hapa kwa kuwa Iringa ni kitovu cha utali nyanda
  za juu kusini.

  “Nimejionea hapa mwenyewe
  kuwa hakuna gari la fire linalofanya kazi kwa kuwa lililopo ni bovu na haliwezi
  kutengenezeka kwa kuwa liltengenezwa kwenye viwanda vya miaka mingi iliyopita
  na spea zake hazipatika hata nje ya nchi kwa mjibu wa wataalamu ambao
  wamenieleza hapa” alisema Hapi

  Hapi alisema kuwa gari ambalo
  lipo katika uwanja wa ndege wa Nduli halijawahi kufanya kazi toka liletwe na
  inasadikiaka kuwa litengenezwa miaka ya themanini huko hivyo hakuna gari la
  zimamoto katika eneo hili  hivyo ni
  hatari kwa watumiaji wa uwanja huu.

  Aidha hapa alisema kuwa
  uwanja wa ndege wa Nduli unaumuhimu mkubwa wa kukuza uchumi wa mkoa wa Iringa
  kwa kuwa watalii na wawekezaji wengi watautumia uwanja huu wa ndege kufanya
  kazi kwa muda muafaka na kurudi walikotoka kwa kutumia usafiri wa anga.

  “Ukiwa na uwanja wa ndege
  ambao unakidhi vigezo vinavyotakiwa utasaidia kuongeza utalii wa kusini kama
  ambavyo unajua kuwa Iringa ndio kitovu cha utalii na kuvutia wawekezaji wengi
  ambao mara nyingi wamekuwa wakitumia usafiri wa anga tofautia wachache ambao
  wamekuwa wakitumia usafiri wa barabara za chini” alisema Hapi

  Naye meneja wa uwanja wa
  ndege wa Nduli Anna Kibopile alisema kuwa jengo la abiria halikidhi mahitaji
  kupokea abiri wengi ambao pia watakuwa wakitumia ndege ya serikali aina ya Bombardie
  ambayo itaanza safari mkoani Iringa hapo baadae.

  “Unajua kuwa ndege yetu ya Bombardie
  ataanza safari ya kuja hapa mkoani hiyo itakuwa inachukua abiria wengi sana
  hivyo jengo letu la abiria halitoshi kuwahudumia wasafiri ambao watakuwa
  wakiutumia unjwa huo kufanya safari zao” alisema Kibopile

  Kibopile  alisema kuwa ndege ya Bombardie inabeba abira
  zaidi ya sabini hivyo ni lazima kuhakikisha tunataua au tunajenga jengo kubwa
  la abira ambalo mkuu wa mkoa wa iringa ameshauri kuwa jengo hilo halikidhi
  mahitaji ya abiria ambao watakaokuwa wanakuja mkoani Iringa.

  0 0  0 0
 • 09/05/18--22:02: NZEGA WAISHUKURU SERIKALI

 • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua maeneo ambapo majengo mapya yatajengwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega.
   Viongozi wa Nzega wakimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
  Wananchi wa Nzega wakisubiri huduma katika hospitali ya wilaya ya Nzega.
  1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akitembelea kukagua miundombinu ya hospitali ya wilaya ya Nzega


  Wananchi na viongozi wa wilaya ya Nzega wameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuifanyia ukarabati mkubwa wa hospitali ya wilaya ya Nzega.

  Shukrani hizo zimetolewa wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea wilayani hapo kuangalia maandalizi ya ukarabati wa hospitali hiyo ya wilaya.

  Hospitali hiyo imepokea sh. milioni 800 ili kujenga majengo kwa ajili ya huduma zote za uzazi pamoja na ukarabati na ujenzi wa wodi ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

  Katika Ziara hiyo Waziri Jafo amezielekeza Halmashauri ya wilaya ya Nzega na ya Mji Nzega kuunda timu ya pamoja ya usimamizi wa ujenzi huo ili mradi huo ukamilike ndani ya miezi mitano.

  0 0

  Awaahidi kuwa serikali itaendelea kuwa mtetezi wao siku zote
  Wampa tuzo ya Rais Magufuli kwa utekelezaji wa ilani, kuwatetea

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amekutana na kuzungumza na wamachinga wa Mkoa wa Iringa ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya makundi mbalimbali ya jamii mkoani humo.

  Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara hao maarufu Machinga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameeleza mikakati ya serikali ya mkoa ya kuwatetea na kusimamia maslahi ya wamachinga ili watambuliwe na kusaidiwa kufanya shughuli zao vizuri.

  Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watendaji wote wa Mkoa wa Iringa kutowahangaisha machinga na badala yake kuwatengea maeneo mazuri ya biashara, kuanzisha magulio, kuwapanga vema machinga na kuwawekea utaratibu mzuri wa kuchangia maendeleo ya nchi yao jambo ambalo machinga wameeleza kuwa tayari kulifanya.

  Aidha Hapi ameeleza kutoridhishwa na manispaa ya Iringa kushindwa kukusanya mapato kikamilifu kutoka kwa machinga wote ambao wamekuwa na utayari wa kuchangia mapato.Kati ya machinga zaidi ya 2000 waliopo, taarifa za manispaa ya Iringa zinaonesha ushuru unakusanywa kwa machinga 353 pekee.Mkuu wa Mkoa ameagiza jambo hilo kurekebishwa haraka.

  Katika hatua nyingine, uongozi wa Machinga umemkabidhi RC Hapi hati maalum ya shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kwa jinsi serikali yake ilivyokuwa mtetezi wa wamachinga wakati wote.

  Mikutano hii ni utangulizi wa ziara kubwa ya Mkuu wa Mkoa ijulikanayo kama IRINGA MPYA tarafa kwa tarafa inayotarajiwa kuanza tarehe 8 septemba wilayani Mufindi na kisha wilaya za Kilolo na Iringa.
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi aakifafanua jambo awakati akizungumza na Wamachinga wa Mkoa wa Iringa, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya makundi mbalimbali ya jamii mkoani humo.Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara hao maarufu Machinga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameeleza mikakati ya serikali ya mkoa ya kuwatetea na kusimamia maslahi ya wamachinga ili watambuliwe na kusaidiwa kufanya shughuli zao vizuri.
  Baadhii ya Wafanyabiashara hao a.k.a Wamachinga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Ally Hapi alipokutana nao na kuzungumza nao mambo mbalimbali

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  Huduma ya kiroho ya Grow in Christ Children Ministry imeandaa kambi ya mafunzo ya siku tatu kwa ajili ya kuwanoa wanafunzi waliohitimu darasa la saba wa jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Mratibu wa kambi hiyo Pastor Mercy Sang'enoi (pichani) alisema kambi hiyo itaanza Septemba 10,2018 hadi Septemba 13 na kuwa itafanyika katika Hosteli za Magufuli Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo mada mbalimbali zitatolewa.

  Sang'enoi alisema mbali ya mada za kiroho pia watatoa mada zingine mbalimbali zitakazohusu namna ya kumuandaa mwanafunzi huyo kabla ya kuanza masomo yake ya sekondari ikiwa ni njia ya kumjengea uwezo wa kujitambua.

  "Watoto wengi wanao hitimu elimu ya msingi bado umri wao ni mdogo hivyo wanahitaji kuelekezwa mambo muhimu kabla ya kuanza kidato cha kwanza ndio maana tumeona tuweke kambi ya siku tatu ili kuwanoa " alisema Sang'enoi.Alisema katika kambi hiyo watoa mada watakuwa ni yeye, Mwalimu Asanterabi Sang'enoi, Msaikolojia Bupe Mwabenga, Mwalimu Apaisaria Minja na Shadrack Mgonja.

  Alisema wanafunzi wataohudhuria kambi hiyo kila mmoja atalazimika kuchangia huduma za chakula na mambo mengine ambapo atachangia sh.50,000.Pastor Sang'enoi aliongeza kuwa huduma hiyo ya Grow in Christ hushirikiana na madhehebu mbalimbali ya kikristo kama Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania

  (KKKT), Anglikana, Moravian, Pentekosti na Kanisa la CCT Chuo Kikuu.Alisema kuwa wapo tayari kushirikiana mtu na taasisi yoyote yenye kuwiwa kuhudumia watoto.


  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiongea na Viongozi na wananchi wa Nyang'wale.
  Madiwani wa Nyang'wale wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea Halmashauri  hiyo.
                    ..................................................................................

   Watumishi sita pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Geita baada kubainika kuchezea fedha za miradi ya maendeleo zilizoelekezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale. 

   Watu hao ni Aliyekuwa mkurugenzi wa Nyang'wale Calous, wahasibu Robert na Godson, Mweka Hazina Ronatus, Afisa habari Zahoro, Katibu wa Afya Alfred Joseph, na Afisa utumishi Muhando B.Mhando.

   Wizi uliofanyika katika fedha za miradi ya Afya, Elimu, Jengo la Utawala, na Maji ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuna ubadhirifu wa Sh.Bilioni 2.2. 

   Kushikiliwa kwa watumishi hao kumetokana na agizo alilolitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ambapo ameelekeza vyombo vya dola kufanya kazi yake na tayari wanashikiliwa na jeshi hilo. 

   Jafo akiwa katika mkutano wa kikazi wilayani humo amevitaka vyombo vya Dola kusimamia vyema jambo hilo ili waliohusika mali zao zishikiliwe ili kufidia fedha zilizopotea sambamba na hatua zingine za kisheria. 

   Hata hivyo Waziri Jafo amemtaka mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pamoja na Makamu wake kujitafakari kama wanafaa kusimamia fedha za wananchi wa Nyang'wale. 

   Aidha Waziri Jafo amepongeza Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo Mariam Chaurembo kwa kubaini kwa haraka ubadhirifu huo wakati wa makabidhiano na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wa awali. 

   Amewataka wakurugenzi nchini kuwa makini katika kusimamia majukumu yao.

  0 0

    MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa mahakimu wakazi wa wilaya na mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro kuhusu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura  263 marejeo ya mwaka 2015 iliyoanza Septemba 5, 2018 mkoani Morogoro. Semina hiyo imeratibiwa kwa ushirikiano wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wengine pichani ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Paul F. Kihwelo (kulia) na Mkurugezni Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba.

    Na K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
  MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, amesema hategemei kesi zinazohusiana na masuala ya fidia kwa wafanyakazi zikichelewa pindi mashauri yake yanapofika mahakamani.
  Dkt. Feleshi ameyasema hayo Mjini Morogoro Septemba 5, 2018 wakati akifungua mafunzo kwa mahakimu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Morogoro yanayoratibiwa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na kuendeshwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia leo.
  “Sitegemei kesi za namna hii ziingie kwenye kundi la njoo kesho… njoo kesho, mashahidi wake  ni wangapi? Kesi za namna hii zikiingia zisikilizwe mfululizo, kumbukeni inamuhusu mtu aliyeumia, inagusu uhai, inahusu ulemavu wa kudumu kwa hiyo nyuma kuna wategemezi na yeye mwenyewe kwa hiyo inahusu maisha ya mtu, pia ushahidi wake uko wazi na adhabu zake ziko bayana” Alifafanua Dkt. Feleshi.
  Aidha Mhe. Jaji Kiongozi alisema, kila mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi anayo haki ya kupata fidia stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria na kwa yule atakayefariki katika mazingira hayo basi wategemezi wake nao wanapatiwa haki zao zilizoanishwa kisheria.
  Alisema huduma ya Hifadhi ya Jamii ni haki inayotambulika na kulindwa na Katiba, ibara ya 11 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mambo mengine inatamka kwenye ibara ndogo kwamba Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi, au hali ya ulemavu na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi, na bila kuathiri haki hizo Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.
  “Hayo ni maneno ambayo yamewekwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo ni haki ambayo imetamkwa na inalidwa na Sheria na kwa kuzingatia matakwa hayo ya kikatiba ndio maana ilitungwa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi iliyoanzisha Mfuko huu wa WCF.” Alifafanua Dkt. Feleshi.
  Alisema Mafunzo hayo kwa Mahakimu kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo, yana manufaa makubwa na ndio maana yameratibiwa na Chuo cha Uongozi   wa Mahakama ambacho ndio chenye jukumu la kutoa elimu kwa watumishi wa mahakama.
  “Katika sheria ya sasa kwa mujibu wa vifungu vya 22 (1) 46 na 48 na majedwali ya 2,3 na 4 ulipaji wa fidia unazingatia zaidi uhalisia wa tukio, kiwango cha hasara na madhara ambavyo vinafanya fidia inayolipwa ikokotolewe kwa kufuata asilimia ya vigezo hivyo na malipo ya ujira wa mwezi au malipo ya mwisho ya mhusika.” Alibainisha Dkt. Feleshi.
  “Takwimu zinaonyesha kuwa Mfuko umekwishalipa Fidia kiasi cha Shilingi bilioni 4.4 tangu ulipoanza kulipa fidia hadi Julai 31, 2018, na hii inaonyesha umuhimu wa Mfuko huu kwa jamii, taifa lakini hata sisi wenyewe kama watumishi.” Alisema.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Masha Mshomba alisema kwa sasa Mfuko umeweka kipaumbele kwenye utoaji elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mahakimu ili na wao waelewe vizuri shughuli za Mfuko na jinsi ya kutekeleza sheria iliyoanzisha Mfuko.
  Kwa sasa Mfuko umekwisha wafikia wadau wengi na kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika uelewa wa kutekeleza sheria hii na ni wachache sana ambao bado wanakuwa wazito kutekelza sheria, alisema Bw. Mshomba.
  Washiriki wa mafunzo hayo wanatarajiwa kujifunza sheria inayosimamia shughuli za Mfuko, lakini pia muundo na shighuli za Mfuko na taratibu za utoaji Fidia.

   Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akizungumza kwenye semina hiyo.
   Baadhi ya Wahwshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
  Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka.
   Mhe. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Bi.Elizabeth S. Missana, akipitia kipperushi chenye maelezo kuhusu shughuli za Mfuko.
    Baadhi ya Waheshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
   Hakimu Mfawidhi wa Mahaka ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mheshimiwa Elizabeth Nyembele, akizungumza kwenye semina hiyo.
  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kibaha, Mhe.Joyce J. Mkhoi, akitoa maoni yake kwenye semina hiyo.
   Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akishauriana jambo na Mkuu wa Huudma za Sheria wa Mfuko huo, Bw.Abraham Siyovelwa
   Bw. Mshomba (katikati), akimtambulisha Dkt. Feleshi kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, wakati akiwasili ukumbini.
   Dkt. Feleshi akisalimiana na Bw. Siyovelwa.
    MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba, wakiwa na furaha baada ya Dkt. Felishi kufungua mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa wa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Kifungu namba 5 [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] kwa mahakimu Wakuu Wakazi wa Mikoa na Wilaya kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara. Semina hiyo iiyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Cha Uongozxi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) imeanza Septemba 5, 2015 mjini Morogoro. 
   Kutoka kushoto ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe. Godfrey Isaya, Mhe. Dkt. Feleshi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa  Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Jaji Paul Kihwelo, Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa.
  Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu sharia zinazosimamia Mfuko huo.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada
  Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, akiongoza semina hiyo.
  MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, akisalimiana na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor.
  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Dkt. Paul F. Kihwelo, (kulia), akisindikizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe.Elizabeth Nyembele, (kushoto) na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor.
  Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe.Lamek Samson akiwa na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence.

  0 0
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Clubs, Sharmila Bhatt akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kumkaribisha kwa Rotary Club ya Dar es Salaam jijini Septemba 5 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
  Sehemu ya wana Rotary Club wakishiriki katika hafla ya kumkaribisha District Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda, Sharmila Bhati jijini Dar es Salaam Septemba 5 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
  Washiriki wakijihudumia kifungua kinywa.
  Wana Rotary Club wakitost ishara ya kufunguliwa rasmi kwa hafla hiyo.
  Sehemu ya wana Rotary Club wakishiriki katika hafla ya kumkaribisha District Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda, Sharmila Bhatt jijini Dar es Salaam Septemba 5 2018.
  Sehemu ya wana Rotary Club wakishiriki katika hafla ya kumkaribisha Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Clubs, Sharmila Bhatt jijini Dar es Salaam Septemba 5 2018.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Clubs, Sharmila Bhatt akitoa nasaha zake kwa wana Rotary Club katika hafla ya kumkaribisha iliyofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 5 2018.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Clubs, Sharmila Bhati (kushoto) akipongezwa na washiriki wa hafla hiyo.
  Mmoja wa washiriki akijitambulisha.
  Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Rotary Club, Nikki Aggarwal akiwasilisha mchanganuo wa matukio na shughuli zilizofanywa na club kwa washiriki wa hafla hiyo.
  Mmoja wa wana Rotary Club, Agnes Batengas akijitambulisha kwenye hafla hiyo. Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Clubs, Shamila Bhatt (wa tatu kulia) akimkabidhi miwani mwakilishi wa Hospitali ya CCBRT, Lydia Kiwelu wakati wa hafla kumkaribisha Gavana huyo kwa Rotary Club ya Dar es Salaam jijini leo, sanjari na msaada huo uliotolewa na Club kwa hospitali hiyo. Kutokea (kushoto) ni Msaidizi wa Gavana, Mohamed Versi, Mwenyekiti wa Tanzania wa Rotary Clubs, Adeline Rutabanzibwa, Rais wa Rotary Club ya Dar e Salaam, Mili Rughani na Mkurugenzi wa Miradi wa club hiyo, Abdulqadir Ahameed.
  Mwana Rotary Club Mkongwe, Hamza Kassongo (katikati) akiwatambulisha wageni aliowahalika kwa Club wakati wa hafla hiyo.
  Mwenyekiti wa Rotary Clubs Kanda ya Tanzania, Adeline Rutabanzibwa akijitambulisha kwa washiriki wakati wa hafla hiyo.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda, Sharmila Bhatt (wa pili kulia) akiwa na sehemu ya viongozi wa Rotary Club. Kushoto ni Rais wa Dar es Salaam Rotary Club ya Dar es Salaam, Mili Rughani, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rotary Club, Nikki Aggarwal na Rotarian Anagha Bhattbhatt.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda, Sharmila Bhatt (mwenye gauni jekundu) akiwa katika picha ya pamoja na wana Rotary Clubs wakati wa kuhitimisha hafla hiyo.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda, Sharmila Bhatt (wa nnea kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Rotaractors wakati wa kuhitimisha hafla hiyo.
  Mkurugenzi wa Miradi wa club hiyo, Abdulqadir Ahameed, Rotarian Abdulqadir Ahameed akifafanua shughuli na huduma zilizofanywa na Rotary Club ya Dar es Salaam kwa washiriki wa hafla hiyo.
  Sehemu ya Rotaractor walioshiriki hafla hiyo wakifuatialia jambo.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Clubs, Sharmila Bhatt akipongezwa na Msaidizi wake Mohamed Versi pia Mwenyekiti wa Tanznia wa Rotary Clubs Adeline Rutabanzibwa kwa mambo makubwa aliyofanya na kufikia wadhifa alionao sasa.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Club, Sharmila Bhatt (kushoto) akipokea nembo maalum kutoka kwa Rais wa Dar es Salaam Rotary Club, Mill Rughani wakati wa hafla hiyo.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Clubs, Sharmila Bhatt akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mweka Hazina wa Rotary Club, Anver Rajpar wakati wa hafla hiyo.
  Gavana wa Kanda ya Tanzania na Uganda wa Rotary Clubs, Sharmila Bhatt (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Rotary Club na Rotaractors wakati wa hafla hiyo.

  0 0


  *Ni kutokana na mikakati ya kuendeleza Afrika aliyoitangaza

  WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amempongeza Rais wa China Xi Jinping kwa mikakati mbalimbali kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika aliyotangaza kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Serptemba 05, 2018) alipokutana na Meya wa Manispaa ya Shenzhen na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China wa Jimbo hilo Wang Wanzhong katika hoteli ya Wu Zehou iliyoko Shenzhen.
  Amesema anampongeza Rais Xi kwa kutangaza mkakati wa kuimarisha ushirkiano na nchi za Afrika kwa sababu Tanzania nayo itaendelea kunufaika zaidi kupitia mipango na mikakati hiyo.

  Waziri Mkuu amesema licha ya asilimia 70 ya Watanzania kutegemea kilimo katika kuendeshaji wa maisha yao, Serikali imeamua kuboresha uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda hususani vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Hivyo, inahitaji washirika wengi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

  “Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kuboresha uchumi kupitia viwanda. Mkakati wa kuwekeza katika viwanda unatoa fursa kwa Watanzania na watu kutoka nje ya nchi ikiwemo China kuja kuwekeza.”


  Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wakezaji kutoka Manispaa ya Shenzhen waje wawekeze kwenye maeneo mbalimbali nchini kama uchimbaji na uchakataji wa madini hususani ya Tanzaniteili kuiwezesha nchi kunufaika na madini hayo yanayopatikana Tanzania tu.

  Waziri Mkuu amesema anaamini kuwa miji mbalimbali Tanzania inaweza kufikia maendeleo ya viwanda yaliyofikiwa na mji wa Shenzhen katika kipindi cha miaka 38 tangu kuanzishwa kwa mji huo kama eneo la kwanza la kiuchumi.

  “Nawakaribisha wawekeze kwenye sekta ya teknolijia ya habari na mawasiliano nao waje nchini kama ilivyofanya kampuni ya HUAWEI ya Shenzhen ambayo inafanya kazi nzuri na kutoa mchango mkubwa kwa sekta hiyo nchini kwetu.”

  Kwa upande wake, Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Wang amemshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kutembelea Shezhen na kwamba Shenzhen itaitikia wito wa Rais Xi wa kushirikiana na Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya uchakataji mazao ya kilimo.

  Kuhusu uwekezaji wa viwanda, kiongozi huyo aliahidi kuwasiliana na EPZA kuona namna bora ya kushirikiana na Tanzania . Aidha aliahidi kutuma ujumbe nchini kutoka Shirikisho la Wasanifu na Watengenezaji Vito vya Madini waje waangalie namna ya kushirikiana na Tanzania hususani katika madini ya Tanzanite.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea Kampuni ya Huawei Technologies, Kituo cha Sanaa na Makumbusho cha Sea World na Kampuni ya China Merchant ambayo ina mpango wa kuwekeza kwenye mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda.

  0 0


  0 0
  MWANANFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Rau iliyopo katika manispaa ya Moshi,mkoani Kilimanjaro Emmanuel Tarimo (18), amejinyonga hadi kufa baada ya kudaiwa kuhojiwa na walimu wake kwa zaidi ya saa tano, akituhumiwa kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi mwenzake wa kidato cha kwanza.
   
  Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kati ya majira ya saa nne za usiku nyumbani kwao mtaa wa Sababa, Rau Madukani, manispaa ya Moshi.

  Sababu inayotajwa kusababisha kifo cha mwanafunzi huyo ambaye anajiandaa kufanya mitihani ya kuhitimu kidato cha nne mwaka huu ni kuhusishwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwenzake katika moja ya ofisi ya walimu iliyokuwa wazi shuleni hapo.

  Mkuu wa shule ya sekondari Rau Bw.Nyoni Njinjinji amekiri mwanafunzi huyo kuhojiwa na walimu kuhusiana na tuhuma za kujihusisha kimapenzi na mwenzake ambapo baada ya kukataa, alielekezwa kujieleza kwa barua na alipomaliza aliondoka na kuelekea nyumbani badala ya kuingia darasani.

  Kwa upande wake mama mdogo wa marehemu Bi. Teddy Maro na baadhi ya wanafunzi kwa nyakati tofauti ,wameeleza kusikitishwa kwao na kifo cha mwanafunzi huyo,huku wakiwasihi walimu kutojenga tabia ya kuwasukuma wanafunzi kukiri kosa ambalo huenda linaweza kuwa si kweli na likawaathiri kisaikolojia.

  CHANZO: ITV

  0 0

  WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa kutokana na kushiriki kwake katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

  Amesema kikao hicho kimekuwa na tija kwa Tanzania kutokana na maeneo ya vipaumbele yaliyojadiliwa katika mkutano huo hususani masuala ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Septemba 05, 2018) alipokutana na waandishi wa habari katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi China ambako alikwenda kumuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano wa FOCAC. 

  Alisema maeneo yaliyopewa kipaumbele katika mkutano huo ni masuala ya usalama wa nchi, maendeleo ya kiuchumi hususani uboreshaji wa sekta ya viwanda, elimu, kilimo, afya, elimu na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

  “Kikao hiki kimekuwa na tija kwa Tanzania kwa sababu maeneo yote yaliyojadiliwa ni muhimu kwetu. Tumeanza kuona idadi nzuri ya wawekezaji kutoka China na ni matokeo ya mpango uliowekwa katika kikao cha kwanza cha FOCAC kilichofanyika Afrika Kusini.”

  Waziri Mkuu alisema maeneo mengine yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya madini, mifugo na uvuvi, ambazo nazo zimewekewa mikakati ya namna ya kuziboresha ili ili ziweze kuchangia ukuzaji wa uchumi katika mataifa hayo.

  Kadhalika, Waziri Mkuu alisema kikao hiko pia kilijadili namna ya kuboresha sekta ya utalii kwa kuvutia watalii kutoka za Afrika na nje ya bara hilo ikiwemo na China, hivyo Tanzania inatakiwa kutumia fursa fursa zilizopo kuvutia watalii kutoka nchi mbalimbali.

  Alisema ushirikiano huo unaanza mara moja na China imetenga dola bilini 60 za Marekani kwa ajili ya kusaidia Afrika ili ziweze kuboresha maeneo hayo yaliyoainishwa. Tanzania inatakiwa kutumia vizuri fursa hiyo.

  Pia Waziri Mkuu alisema atakaporejea nchini ataitisha kikao cha kazi cha Mawaziri na kutoa maelekezo kwa mawaziri wote ambao sekta zao zimeguswa kwenye mpango wa FOCAC ili waweze kuandaa utaratibu mzuri wa namna tukavyonufaika na fedha hizo.

  “Watanzania tushirikiane kwa pamoja na watendaji katika wizara zote ili tuweze kujipanga vizuri. Wataalamu katika kila sekta waweke mpango kazi utakaokwenda kuhitaji fedha hizo kwa ajili ya kuimarisha sekta husika ili maeneo yote yapate tija.”

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amempongeza Rais wa China, Xi Jinpingkwa kuitambua Tanzania kama moja kati ya nchi rafiki wa muda mrefu wa China na kuipa kipaumbele kwenye mkakati wa kuwekeza kwenye viwanda.

  Alisema wawekezaji wengi kutoka China wamedhamiria kuja Tanzania kujenga viwanda na kuviendesha kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi ili viweze kuzalisha kwa uhakika na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. 

  Waziri Mkuu alisema tayari Tanzania ilishafanikiwa katika mkakati wa kuboresha mazao makuu matano ya biashara ambayo ni korosho, chai, kahawa, pamba na tumbaku na sasa imejipanga kuboresha mazao ya mbegu za kuzalisha mafuta na ameitaka mikoa husika ifuatilie mazao hao ambayo ni michikichi, alizeti na ufuta.

  Mkutano huo wa FOCAC wa siku mbili ulifunguliwa Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini Beijing China na Rais wa China, Xi Jinping. Ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi 53 kutoka Afrika.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, SEPTEMBA 06, 2018.

  0 0


   MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kuwaingiza watoto wao kwenye Mpango wa Toto Afya Kadi ili waweze kupaa huduma za matibabu wanapougua kwenye kijiji cha Gitu wilayani Kilindi mkoani Tanga
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu kwa muuza nguo kwenye soko la Gitu wilayani Kilindi mkoani Tanga juu ya umuhimu wa kuwaingiza watoto wao kwenye mpango wa Toto Afya kadi wakati wa uhamasishaji wa mpango huo
  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga{NHIF) Ally Mwakababu akitoa elimu kwa wakazi wa Kijiji cha Gitu wilayani kilindi kuhusu umuhimu wa Toto Afya kadi kwa ajili ya watoto wao ili waweze kunufaika na matibabu wanapougua
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga{NHIF) Ally Mwakababu katikati akitoa elimu kwa wakazi wa Kijiji cha Gitu
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga{NHIF) Ally Mwakababu akitoa elimu juu ya umuhimu wa Mpango wa Toto Afya Kadi kwa mkazi wa Kijiji cha Gitu wilayani kilindi juu umuhimu wa watoto wao wakati wanapougua wakati wa uhamasishaji huo
   Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Macrina Clemens kushoto akihamasisha mpango wa Toto Afya Kadi kwa wananchi wa Kijiji cha Gitu
   Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Macrina Clemens akigawa vipeperusi kwa watoto vinavyoelezea mpango wa Toto Afya Kadi wakati wa uhamasishaji wa mpango huo
   MUUGUZI wa Afya akimpima mkazi wa Kijiji cha Gitu wilayani Kilindi
  Mratibu wa NHIF wilaya ya Kilindi katika akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Gitu kushoto ni Mhasibu wa NHIF mkoani Tanga Hellena Manyanda
  Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Macrina Clemens kulia akichukua maelezo ya mkazi wa Kijiji cha Gitu ambao walijitoikeza kwa ajili ya upimaji wakati wa uhamasishaji wa mpango wa Toto Afya Kadi wilayani Kilindi
   Mmmoja wa wahudumu wa Afya akimpima mmoja wa wakazi wa kijiji cha Gitu wilayani kKilindi
  Sehemu ya wananchi wakisubiri huduma ya Upimaji wakati wa uhamasishaji wa Mpango wa Toto Afya Kadi katika Kijiji cha Gitu wilayani Kilindi Mkoani Tanga uliofanywa na NHIF mkoani Tanga

  NA MWANDISHI WETU,KILINDI.

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga(NHIF) umepiga kambi Kijiji cha Gitu wilayani Kilindi mkoani humo kuhamasisha umuhimu wa mpango wa Toto Afya kadi kwa wananchi ili kuwawezesha watoto wao kupata matibabu wanapougua.

  Uhamasishaji huo ulifanywa na Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga Ally Mwakababu akiwa ameambatana na watumishi wengine wa mfuko huo ambao walitembelea maeneo mbalimbali wilayani humo.

  Akizungumza wakati akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wakiwemo watoto wao ambao utawasaidia kuweza kupata huduma za matibabu wakati wanapougua 

  Meneja Mwakababu alisema suala hilo ni muhimu kwa watoto wao hususani wakati wa ukuaji wao kutokana na kukabiliwa na magonjwa mbalimbali hivyo mpango huo utawasaidia wazazi kuondokana na gharama za matibabu

  “Kama unavyojua huu mpango wa Toto Afya Kadi ni mzuri na unampa uhakika mtoto wako kuweza kupata huduma za matibabu pindi wanapougua kwani sio nyakati zote wanaweza kumudu gharama za matibabu kutokana na kupanda kila wakati”Alisema.

  Hata hivyo aliwataka pia wananchi wa Kijiji hicho kuona namna bora ya kujiunga kwenye mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapokumbana na magonjwa mbalimbali.


  Uhamasishaji huo unafanyika umefanywa na mfuko huo kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ili kuwawezesha wananchi kuchangamkia fursa hiyo wa kujiunga na mpango wa Bima ya Afya wao na Watoto wao

  0 0

   Baada ua kukabidhi barua zao kwa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohane Sintoo,waliamua kupiga picha ya pamoja
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohane Sintoo akipokea barua za baadhi ya Wenyeviti wa vijiji kati ya 20 walioamua kujivua vyeo vyao vyote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi mapema leo.  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mama Maria Nyerere mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Maria Nyerere mke wa Hayati Mwalimu Julius  Kambarage Nyerere mara bada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiimba na kucheza pamoja na vijana wa Kambi ya  JKT Rwamkoma iliyopo mkoani Mara mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Butiama(hawaonekani pichani) kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
  Mzee Joseph Butiku akiwa amekaa na Mwanasiasa mklongwe Stephen Wassira pamoja na viogozi wengine wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Magufuli katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi Butiama mkoani Mara. 
   Kikundi cha ngoma za asili cha Engubha cha kabila la wakabwa wenyeji wa Butiama mkoani Mara kikitumbuzia katika sherehe hizo. PICHA NA IKULU

  0 0

   Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akibadilishana mawazo na Balozi wa India nchini Mh. Sandeep Arya mara baada ya kuwasili kwenye mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo – TCCIA Bw.Octavian Mshiu (aliyeipa kisogo kamera) wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ONGC Petro additions Limited ya nchini India, Avinash Joshi.
  Katibu Mkuu (idara ya usambazaji maji) na Mwenyekiti wa GWSSB wa Serikali ya Gujarat nchini India, J.P. Gupta akieleza fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali jimbo la Gujarat nchini India wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara wa jimbo la Gujarat na Tanzania wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Bw. Shubhash Patel akizungumza na wageni waalikwa wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ONGC Petro additions Limited ya nchini India, Avinash Joshi, Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi, Balozi wa India nchini Mh. Sandeep Arya pamoja na Katibu Mkuu (idara ya usambazaji maji) na Mwenyekiti wa GWSSB wa Serikali ya Gujarat nchini India, J.P. Gupta wakifurahi jambo wakati wa risala ya Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Bw. Shubhash Patel (hayupo pichani) katika mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Bw.Octavian Mshiu akihitimisha wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara wa Tanzania walipokutana na wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat iliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Pichani juu na chini ni sehemu ya Wafanyabishara kutoka Tanzania walioshiriki mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akisalamiana Mtalaam Mshauri wa Mambo ya Biashara, Bw. Victor Tesha (kulia) wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa India nchini, Bw. Gagan Gupta.
  Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akibadilishana ‘contact’ na wafanyabiashara wa jimbo la Gujarat mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa India nchini, Bw. Gagan Gupta.
  Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akipiga picha za ukumbusho na baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania katika sekta mbalimbali waliohudhuria mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Sektretarieti iliyoandaa mkutano huo kutoka jimbo la Gujarat katika picha ya pamoja na meza kuu mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat 2019 uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  Meza kuu katika picha Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ONGC Petro additions Limited ya nchini India, Avinash Joshi, Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi, Balozi wa India nchini Mh. Sandeep Arya pamoja na Katibu Mkuu (idara ya usambazaji maji) na Mwenyekiti wa GWSSB wa Serikali ya Gujarat nchini India, J.P. Gupta, Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Bw. Shubhash Patel, Kaimu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Bw.Octavian Mshiu pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa India nchini, Bw. Gagan Gupta.


  Wafanyabiashara wa Tanzania wamehamasishwa kushiriki maonyesho ya Kimataifa ya Biashara katika Jimbo la Gujarat nchini India ili kupata fursa ya kufanya biashara na uwekezaji.Hayo yamezungumzwa katika mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka jimbo hilo waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat 2019.Jimbo la Gujarat lina pato la ndani la dola za Marekani bilioni 15 na linachangia asilimia 17 ya pato la viwanda nchini India na ni jimbo lenye viwanda vikubwa duniani.Jimbo hilo pia linatoa mchango wa mauzo ya nje kwa asilimia 22 na asilimia 40 ya mizigo inayosafirishwa nchini india.


  Akielezea Fursa za Uwekezaji zilizopo Gujarat katika semina maalum kwa wafanyabiashara wa Tanzania jijini Dar es salaam, Balozi wa India nchini Bw. Sandeep Arya amesema Watanzania wana fursa kubwa ya kushiriki uchumi wa Gujarat kwa kuona maeneo ya kushrikiana kiuchumi katika pande hizo mbili.Akizungumza katika  mkutano huo Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi, ambaye ni   Mwenyekiti mstaafu wa TPSF, aliwataka wawekezaji wa India kuja nchini kuwekeza kwa ubia na Watanzania, hususan katika maeneo ya utafiti,  ubunifu na  uongezaji thamani kwa mazao ya kilimo.


  Aidha Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Bw. Shubhash Patel, Kaimu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo – TCCIA Bw.Octovian Mshiu walisema mkutano huo ni muhimu katika kuendeleza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na India wenye historia ndefu.Naye Katibu Mtendaji wa Chama cha watengeneza vitambaa vya nguo na  mavazi (TEGAMAT), Adam Zuku amesema kuwa semina hiyo  ina maana kubwa kwa watanzania  hasa viwanda vya nguo.


  Alisema Tanzania inahitaji kufufua viwanda vyake vya nguo ili viweze kutoa ajira na pia kuwa na matumizi ya pamba yetu.Alisema kuna changamoto kubwa katika viwanda vya nguo nchini, tatizo la soko linalotokana na nguo zinazotoka nje zinazosababisha tatizo kwenye ushindani sokoni.Alisema nguo zinazozalishwa nchini zinakuwa ghali kulingana na zinazotoka nje na hivyo kuyumbuisha viwanda vya nguo nchini.Alisema teknolojia si tatizo, tatizo ni wananchi kuwa wazalendo na kununua bidhaa zao ili kuwezesha viwanda kuendelea kuwapo.


  Katika mkutano huo alisema wakati umefika kwa Wafanyabiashara na wadau mbalimbali nchini kushiriki katika fursa za uwekezaji kwenye nguo.

  0 0  Katika mkutano wa hadhara Kata ya Ukonga Wilaya ya Ilala wa kumnadi Ndg. Mwita Mwikwabe Waitara mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Ukonga, Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitalivalia njuga suala la utatuzi wa kero za wananchi kwa umahiri zaidi katika Jimbo la Ukonga pindi wananchi watakapo mchagua Ndg. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga.

  Akifananua namna ambavyo CCM itasimamia, itaratibu na kufanikisha utatuzi wa kero za wananchi na kuleta maendeleo ya Jimbo la Ukonga mbele ya mamia ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano huo Ndg. Polepole amesema CCM kupitia Serikali yake itafanikisha upatikanaji wa maji safi na salama, ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ukonga, ukarabati na uimarishaji wa miundombinu ya barabara za mitaa na kukomesha kero za tozo kubwa zenye maudhi za ukusanyaji wa taka zinazowakumba wananchi wa Jimbo la Ukonga.
  2
  “Kampuni inayokusanya taka hapa Ukonga imeonyesha haina uwezo wa kukusanya taka wala haina dhamira njema nina muelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri afanye utaratibu kampuni hii itafute kazi nyingine… CCM imeelekeza kutengwa na kutolewa zaidi ya Bilioni 4 kwa ajili ya Mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na hii ni mikopo isiyo na riba… wiki moja toka leo watu wa DAWASCO wataanza kuchimba mitaro na kutandika mabomba ya kusambaza maji hapa ili mpate maji safi na salama… Tunaomba mtupatie Ndg. Mwita mtu tunayemuamini vizuri ili tushiriki naye kuwaletea maendeleo kwa haraka” amesisitiza Ndg. Polepole
  3
  Huu ni muendelezo wa Mikutano ya hadhara ya kuwanadi wagombea Ubunge na Udiwani katika maeneo ambayo yana uchaguzi mdogo wa marudio ambapo CCM imejipambanua kwa siasa safi, hoja na sera nzuri zinazogusa maslahi ya wananchi.

  0 0

  Jumla ya waendesha bodaboda 117 kutoka wilaya ya Temeke wamejiandikisha katika mfumo wa hiari wa kuchangia mafao kwenye Shirika la Tiafa la hifadhi ya Jamii NSSF. 

  Hatua hii ni alama njema kwa wananchi kuendelea kutambua na kuona muhimu wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini jambo ambalo litasaidia wananchi kuweza kujiwekea akiba yao ya maisha ya baadae. 

  Afisa mwandamizi uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)Abbas Cothema akizungumza na waendesha bodaboda wa wilaya ya Temke ambapo amesema wameitikia wito kwa wingi wa kujiandikisha na kujichangia wenyewe kwa hiari kwamba hivyo hii ni hatua kubwa wananchi kuelewa elimu kuhusiana na suala la hifadhi zao za baade. 

  Cothema amesema kuwa wanachama hao wapya wataweza kufaidika na mafao mbalimbali yakiwemo mafao ya matibabu ambapo mwananchama anapata matibabu ya bure kutokana na michango yake anayoichangia kwa kila mwezi ambapo atachangia kiwango cha kuanzia kiasi cha shilingi elfu ishirini. 

  ‘Hii ni fursa pekee kwa wananchi ambao wapo kwenye sekta isiyorasmi kuweza kujiandikisha na kujiwekea akiba ambayo itawasaidia hivyo ni wakati wao sasa nao kufaidika na matunda ya jasho lao kwa kujichangia wenyewe” alisema Cothema. 

  Cothema amesema mpaka sasa wameshatoa elimu kwa mikoa zaidi ya kumi ambapo wananchi wameweza kuelimishwa umuhimu wa mifuko ya hifadhi ya jamii na umuhimu wake. 

  NSSF imepewa jukumu la kuandikisha wanachama wapya watakaojichangia kwa hiari wenyewe. 

  Afisa matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Abbas Cothema akitoa maelekezo kwa waendesha bodaboda wa wilaya ya Temeke wakati walipokuwa wakijiandikishai ili kujiunga kwenye mfumo wa Hiari wa NSSF katika kampeni ya Zamu yako maalumu kwa wananchi ambao wako kwenye sekta isiyorasmi.
  Baadhi ya waendesha bodaboda wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha kwenye mfumo wa hiari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF jana wilayani TemekeJijini Dar es salaam.
  Afisa matekelezo Kassim Mfundo akiwaandikisha wanachama wapya kwenye mfumo wa Hiari hapo jana wilayani Temeke ambapo waendesha bodaboda 117 walijiandikisha.

  0 0


  Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Fatma Toufiq (kulia) akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu (katikati) kwa lengo la kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi, kikao kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mwandishi Mwandamizi wa Taarifa Rasmi za Bunge, Ndg. Patson Sobha
  Wajumbe wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Fatma Toufiq (watatu kushoto) wakimsikiliza Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu (wa pili kushoto) wakati wa kikao baina yao kilicholenga kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi, kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.
  Wajumbe wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Fatma Toufiq (katikati) wakiwa katika mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu (wa pili kushoto) wakati wa kikao baina yao kilicholenga kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi, kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.
  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu (kulia) akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki walioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Fatma Toufiq (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kililenga kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi
  Mjumbe wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki na Mbunge wa Chilonwa, Mhe. Joel Mwaka akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu na Wanachama wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki (hayupo kwenye picha) katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi

  0 0


  Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeahidi kuipanua zaidi kampeni yake ya ‘Happy Hour’ inayoendelea katika vituo vyake vya mafuta vilivyopo mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ili kuwafikia wateja wa kampuni hiyo kote nchini kufuatia muitikio mkubwa ulionyeshwa na wateja katika kuipokea kampeni hiyo.

  Kampeni hiyo ambayo kwa sasa inahusisha vituo vya mafuta vya Puma vilivyopo vilivyopo mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, inamuhakikishia mteja rejesho la asilimia 5 ambalo ni sawa na Tsh 100 kwa kila Tsh 2,000 atakayotumia kununua mafuta kwa njia ya simu za mikononi au akaunti ya benki kupitia huduma Masterpass QR katika siku zote saba za wiki kuanzia saa 10:00 hadi 12:00 jioni.

  Akizungumza kupitia taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw. Philippe Corsaletti amesema kwa sasa wateja wa kampuni hiyo wanaweza kufanya malipo kwa urahisi, haraka na kwa usalama zaidi kwa kutumia pesa zilizopo kwenye akaunti zao za simu au akaunti za benk.

  “Kupitia kampeni hii tunashuhudia wateja wetu wakihamia kwenye ulimwengu wa kidigitali zaidi na kuungana na wenzao wengi ulimwenguni ambao tayari wapo huko. Aidha, ili kufanikisha hili tumewajengea uwezo wahudumu wetu waliopo kwenye vituo vyetu na sasa wapo tayari kuwasaidia wateja watakaopatwa na changamoto ya aina yoyote katika kufanikisha miamala yao,’’ alifafanua.

  Kwa mujibu wa Bw. Corsaletti, kampuni ya Puma Energy imekuwa ya kwanza katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara kutumia mfumo wa Masterpass QR kufanya miamala ya manunuzi ya nishati ya mafuta kwenye vituo vyake, hicho kikiwa ni kielelezo tosha kwamba kampuni hiyo inabaki kuwa ya kipekee katika ubunifu ndani ya bara la Afrika.

  Alizitaja benki ambazo tayari zinahusishwa na matumizi ya Masterpass QR katika kufanikisha huduma hiyo kuwa ni pamoja na Access Bank, Akiba Commercial Bank, Amana Bank, BancABC, Canara Bank, Exim Bank, I&M Bank, Standard Chartered Bank pamoja na Benki ya Posta Tanzania (TPB), huku akiwashukuru wadau wenza katika kufanikisha huduma hiyo ambao ni kampuni za Mastercard na Selcom.

  Akizungumzia huduma hiyo Makamu wa Rais na Mkuu wa kitengo cha Biashara ukanda wa Afrika Mashariki wa kampuni ya Mastercard, Bw. Chris Bwakira alisema inalenga kuwaondolea wateja wa kampuni ya Puma Energy adha ya kubeba fedha taslimu au kuwa na kadi ya benki muda wowote wanapohitaji kununua nishati ya mafuta.

older | 1 | .... | 1666 | 1667 | (Page 1668) | 1669 | 1670 | .... | 1898 | newer