Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

BFT KUTOTAMBUA UONGOZI ULIOJIINGIZA MADARAKANI KINYUME NA TARATIBU WA DABA


VIGEZO UTOAJI MIKOPO ELIMU YA JUU VYABAINISHWA

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya mikopo Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utoaji mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2013⁄2014,  kulia ni Afisa Habari Idar ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi.

kumekucha miss universe Tanzania 2013

uwanja wa Kambarage palikuwa hapatoshi serengeti fiesta 2013 mjini shinyanga

Ratibu ya Dar es salam festival

UCHUMI WA TANZANIA WAENDELEA KUIMARIKA

$
0
0
Waziri wa Fedha William Mgimwa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Vincent Tiganya.

PICHA NA ELIPHACE MARWA-MAELEZO

Dr Slaa awahutubia waTanzania wa DMV katika Mkutano wa CHADEMA Washington DC

$
0
0

t
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbrod Slaa,  katika Mkutano wa CHADEMA DMV alipozungumza na waTanzania waishio DMV mustakabali mzima wa Taifa letu, Siku ya Jumapili Sept 22, katika ukumbi wa Mirage uliopo Nirvesty Blvd. Langley Park. Maryland Nchini Marekani. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbrod Slaa, akiwahutubia waTanzania wa DMV katika Mkutano wa Chadema DMV Washington DC
Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bwana Iddy Sandaly (kushoto) pamoja na waTanzania waishio DMV wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbrod Slaa, katika Mkutano wa CHADEMA DMV.
Katibu wa wanawake Tawi la Chdema DMV, (wapili kushoto) Dada Maryam akiwa na mkereketwa wa Chadema Boston Ma, Dada Rehema, wakiwa na baadhi ya wageni walikwa  katika Mkutano wa CHADEMA DMV alipozungumza na waTanzania waishio DMV mustakabali mzima wa Taifa letu, Siku ya Jumapili Sept 22, katika ukumbi wa Mirage uliopo Nirvesty Blvd. Langley Park. Maryland Nchini Marekani.
Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere CHADEMA, Mke wa Dr Slaa Mama Josephine Mushumbuzi, wamoja na Viongozi wa Tawi la Chadema DMV
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbrod Slaa,  katika Mkutano wa CHADEMA DMV alipozungumza na waTanzania waishio DMV mustakabali mzima wa Taifa letu, Siku ya Jumapili Sept 22, katika ukumbi wa Mirage uliopo Nirvesty Blvd. Langley Park. Maryland Nchini Marekani. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com) Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbrod Slaa, akiwahutubia waTanzania wa DMV Jijini Washingtton DC. Sikiliza kwa makini Video ya hotuba, Sehemu ya kwanza na yapili ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbrod Slaa, katika Mkutano wa CHADEMA DMV Jijini Washington DC Video ya Maswali na Majibu kutoka kwa waTanzania washio DMV Itawajia punde.

OMMY DIMPOZ ALIVYO ITIKISA WASHINGTON DC

$
0
0
OMMY DIMPOZ akifanya vitu vyake
     Poz kwa Poz akifanya vitu vyake
Maana ya TUPOGO = TUPO NA TUNA GO maisha yanakwenda mbele
Mwanamuziki Mtanzania aishiye Marekani AJ Ubao Katika Picha na Dimpoz
Super Promoter DMK Akipata Interview ya Swahili TV na Ommy Dimpoz back stage kabla ya kupanda jukwaani.Mbali na Kuwa Mkurugenzi wa DMK Global Promotions huyu Ndugu pia ni Mkurugenzi wa MMK Media Group,Kampuni ambayo inamiliki Swahili Radio Online,Swahili TV online,na Blog hii ya Swahilitv Blog.
MR "DMK"  akipata Ukodaki na Warembo ..Pia DMK alisherekea Bday Yake siku hiyo hiyo KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA SWAHILITV.BLOGSPOT.COM



NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI

$
0
0

RafikiElimu  Foundation  ni  Taasisi  Isiyokuwa ya  kiserikali  ( NGO )  inayo  jihusisha  na Maendeleo  Ya  Sekta  ya  Elimu  Tanzania. Taasisi   inatangaza  nafasi  za  MAFUNZO   YA UPISHI  WA  VYAKULA  MAALUMU  KWA WATU  WENYE  MATATIZO  MAALUMU KAMA  VILE  WAZEE, WATU  WANENE, WAGONJWA  WA  PRESHA  & KISUKARI, V.V.U  nakadhalika. Wahitimu wote  watapata nafasi  ya  kufanya  kazi ya UPISHI  WA VYAKULA  MAALUMU  KWA  WATU MAALUMU  kwenye   migahawa  &  mahoteli mbalimbali, kwenye  vituo mbali   vya  afya  pamoja  na  kwa  watu  binafsi.

SIFA  ZA  KUJIUNGA  NA  MAFUNZO:
1.            Awe  na  elimu  ya  kuanzia  kidato cha  nne, sita  na  kuendelea.

2.            Awe  mkaazi  wa  Dar  Es salaam.

3.            Awe  na  uwezo  wa  kuwasiliana  kwa lugha  za  Kiswahili  na  kiingereza.

MUDA  WA  MAFUNZO : Mafunzo  haya yatafanyika  kwa  muda  wa  wiki  tatu  kuanzia tarehe  07 OKTOBA 2013   hadi  tarehe  25 OKTOBA  2013.
Kazi  kuanza  tarehe  04  NOVEMBA  2013.

ADA  YA  MAFUNZO: Ada  ya  mafunzo  haya ni  SHILINGI  LAKI  MOJA  NA  NUSU  TU  ( Tshs.150,000/-)  ambayo  italipwa  kwa  awamu mbili.
FOMU  ZA  KUJIUNGA  NA  MAFUNZO: Fomu  za  kujiunga  na  mafunzo   haya zinapatikana  kwa  SHILINGI  ELFU  KUMI NA  MBILI  TU ( Tshs.12,000/-)

katika  ofisi zetu  zilizopo  katika  eneo  la CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA DAR  ES  SALAAM.

Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe  05 oktoba  2013.

 Kufika   katika  ofisi  zetu  panda  daladala  za UBUNGO- CHANGANYIKENI  kisha  shuka kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako wa  kulia  utaona  ofisi  imeandikwa RAFIKIELIMU  FOUNDATION.
Kwa  maelezo  zaidi  wasiliana  nasi  kwa SIMU  :  0782405936  AU  0756606085.

Au   Tembelea


TIMU ZA WIZARA YA HABARI ZAANZA KWA KUTOA VIPIGO SHIMIWI

$
0
0
1Wachezaji wa Waizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa wamembeba Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Ole Sante Gabriel kusherehekea ushindi walioupata timu za kuvuta kamba za wizara hiyo2Mshambuliaji wa timu ya mpira wa pete Hadija Jaha akijiandaa kutoa pasi kwa mwenzake wakati walipokutana na timu ya Wizara ya Maji. Wizara ya Habari ilishinda kwa alama 19 kwa 15.3Kiungo wa timu ya mpira wa pete ya Wazara ya Habari Flora Mwakasala akijiandaa kutoa pasi kwa mshambuliaji wa timu hiyo Grace Kingalame, wakati timu hizo zilipokutana katika mashinfdano ya SHIMIWI.4Kiungo wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari Mbozi Katala akimtoka beki wa timu ya Wizara ya Maji wakati timu hizo zilipokutana katika mshindano ya SHIMIWI.Habari ilishindwa kwa 1-05Wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya Wanawake ya Wizara ya Habari wakiivuta timu ya Afrika Mashariki (haipo pichani) katika mchezo wa mashindano ya SHIMIWI Septemba 22.
Hussein Makame, MAELEZO-Dodoma
TIMU za mpira wa miguu, pete na kuvuta kamba za  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo zimeanza vyema mashindano ya Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) baada ya kushinda michezo yao ya kwanza kwenye  mashindano hayo iliyochezwa Septemba 22 mwaka huu.
Timu ya mchezo wa kuvuta kamba ndiyo iliyoanza kufungua mlango wa ushindi kwa Wizara hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mivuti 2-0 kwa kuishinda Wizara ya Afrika Mashariki huku ikishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Ole Sante Gabriel.
Baadaye timu ya mpira wa miguu ilifungua pazia la michezo yake kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa bao la ushindi lililofungwa na James Mapepele aliyemchambua kipa wa timu ya Ardhi na kuiandikia timu yake goli pekee la mchezo huo.
Mchezo huo ulikuwa wa kuvutia kufuatia timu ya Wizara ya Ardhi kuonesha upinzani mkubwa lakini uimara wa kikosi cha Wizara ya Habari uliiwezesha kudhibiti upinzani huo na hatimaye kujihakikishia ushindi huo ambao pia ulichagizwa na Naibu Katibu Mkuu Gabriel aliyeitembelea timu hiyo majira ya asubuhi.
Kwa upande wa timu ya  mpira wa pete ya Wizara hiyo, iliibuka na ushindi katika mchezo wake wa ufunguzi baada ya kuitandika timu ya Wizara ya Maji kwa alama 19 kwa 15 baada ya safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Grace Kingalame kufanya kazi nzuri.
Naibu Katibu Mkuu Gabriel ambaye alihudhuria siku ya ufunguzi ya mashindano hayo Septemba 21 mwaka hu,  alitembelea kambi ya timu za Wizara hiyo jambo lililowapa wachezaji hamasa ya ushindi katika mashindano hayo.
Akizungumza na wachezaji hao katika kambi hiyo Naibu Katibu Mkuu  Gabriel aliwakumbusha mambo muhimu ya kuzingatia katika mashindano hayo hasa katika baadhi ya  masuala ya kiufundi kutokana na uzoefu alionao katika michezo kadhaa inachezwa katika mashindano hayo.
Pamoja na mambo mengine, Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara aliwataka wachezaji kuzingatia sheria za michezo husika bila ya kusahau nidhamu katika mashindano hayo ili kuhakikisha wanarejea na ushindi kwani Wizara hiyo ndiyo yenye dhamana na michezo nchini.
Mashindano hayo ya SHIMIWI yanaendelea katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma na Chuo Kikuu cha Dodoma na kushirikisha Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Makamtibu Tawala mkoa ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 5 mwaka huu.
Katika mchezo mwingine uliochezwa jana asubuhi timu za kuvuta kamba za Wizara ya Habari za wanaume na wanawake zimeshinda baada ya kuzifunga timu kamba kutoka                   wakati za mpira wa miguu na pete zilitarajiwa kucheza mchana na jioni.

CCM YAWA LULU NYAMONGO TARIME

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ,leo amefanya ziara katika wilaya ya Tarime Mkoani Mara .  Katibu Mkuu akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilazimika kupangua ratiba ya ziara ya baada ya kuona kuna jambo la muhimu zaidi angependa kupata muda na wakazi wa Nyamongo ambao wamekuwa na kero za muda mrefu bila kupata majibu.

Baada ya mapokezi katika kijiji cha Mrito, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya kamati ya siasa kisha kuelekea katika shughuli ya kufungua Tawi la Nyabichune,mara tu shughuli za ufunguaji Tawi ilipokamilika alipokea taarifa mbali mbali na ndipo akagundua kuna haja ya kupangua ratiba na kwenda kusikiliza ya wananchi.
  • Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye awaambia mkutano huu ni wa kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwani CCM peke yake ndio inaweza kutatua hilo tatizo

  • Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele asitisha huduma ya kulipiwa ada mpaka taratibu na makubaliano yapangwe upya,asikitishwa na watendaji wazembe,azungumzia mpango wa kugawa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo,awataka waunde vikundi watafute leseni,ahimiza kuna Dirisha la Mikopo TIB Bank,pamoja na serikali kuwasaidia vifaa.

  • Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana atoa wawakilishi wa wananchi kutoka kwenye mkutano, akaa nao kikao cha ndani pamoja na viongozi wa Serikali ,chama na wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi leo tarehe 23 Septemba 2013..
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyamongo na kuwaeleza namna ambavyo wamejipanga kutatua tatizo la muda mrefu baina ya wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mgodi wa North Mara .
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Nyamongo Chacha Magayo Butora ambaye alifafanua kwa kina matatizo yanayowakabili wakazi wa eneo hilo,Katibu Mkuu alitumia Demokrasia ya hali ya juu baada ya kuwapa nafasi watu watatu mbali mbali ambao wananchi waliwachagua waje kuelezea matatizo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani mara ambapo aliamua kufuta kila kitu kwenye ratiba yake na kutaka wananchi wateue wawakilishi wao ili wakakae kikao na watu wa serikali ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele akifafanua mambo kadhaa ambayo Wizara yake inataka wananchi wafaidike na migodi ikiwa pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo ambao wanatakiwa wajiunge kutengeneza vikundi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakiongea na wananchi wa Nyamongo ,Wananchi wa Nyamongo wameshukuru sana kwa kusikilizwa kwa ukaribu haijawahi tokea na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Viongozi hao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma moja ya taarifa inayofafanua matatizo ya wakazi wa Nyamongo.
Sehemu ya wakazi wa Nyamongo wakiwa kwenye kikao cha ndani pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele na Viongozi wengine wa Serikali ambapo walikaa na kujadili matatizo yao namna ya kuyatatua.

MZEE MWINYI AWAONYA WANAOTUMIA ELIMU NA UJUZI WAO KUANGAMIZA USTAWI WA JAMII.

$
0
0
DSC_1196
Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akihutubia wageni waalikwa (Hawapo pichani) wakati wa sherehe za Siku ya Kimataifa ya Amani leo asubuhi jijini Dar. Kulia ni balozi wa Rwanda nchini Ben Rugangazi na kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) Jama Gulaid.
DSC_1126
Meza kuu.
DSC_1114
Elizabeth Mwase Programu Manager wa Mtandao wa Watoto na Vijana kutoka Imani Mbalimbali (GNRC) akimpokea Mzee Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa awamu ya pili ambaye alikuwa mgeni rasmi ya Siku ya Kimataifa ya Amani iliyoadhimishwa mwishoni mwa Juma jijini Dar es Salaam ukumbi wa Don Bosco.
DSC_1121
Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa jumuiya za maendeleo za nchi wa hisani wakati wa maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam.
DSC_1120
Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akipokea mfano wa ndege wa Amani kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani duniani jijini Dar.
DSC_1130
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari mbalimbali za jijini wakitumbuiza kwa nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wa kudumisha Amani na upendo duniani.
DSC_1216
Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa ofisi za mabalozi waliohudhuria sherehe hizo kwenye ukumbi wa Don Bosco.
DSC_1143
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo.
.awaasa vijana kutotumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao
.ashangaa wajuzi walivyompachika jina la Ruksa enzi za miaka 1990s


Na.Mo Blog Team
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema kuna baadhi ya watu katika jamii hutumia elimu, ujuzi na maarifa yao kuangamiza, kubomoa na kudumaza Ustawi wa Jamii kwa maslahi binafsi na si ya Umma. Mo blog inaripoti.
Mzee mwinyi amesema hayo wakati wa kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Amani Duniani inayoadhimishwa 21th Septemba kila mwaka ambayo imefanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam, amesema kuna baadhi ya watu wanatumia elimu yao vibaya kwa kupanga kuua watu wengine kwa maslahi yao aidha ya kisiasa au ya kiuchumi.
“Elimu kwa kawaida kuleta matokeo mazuri kwa jamii husika endapo itatumika sawia kwa malengo yaliyokusudiwa na kwa maendeleo endelevu ya taifa kwa ujumla, ila kuna baadhi ya wanajamii kutumia ujuzi huu vibaya na kuangamiza ustawi wa jamii husika,” amesema.
Mzee Mwinyi aliendelea kusema kwamba katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani duniani yenye kauli mbiu “Education for Peace” ni lazima elimu kwa ajili ya amani iwe endelevu hapa duniani ili iweze kuleta suluhu na utengamano katika jamii na mataifa yote duniani.
Amesema kwamba vijana nchini lazima waepuke kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao ya kisiasa na wajifunze kutatua matatizo yao kwa njia ya amani bila ya kuwa na mihemko, jazba, misongo na hasira ili kuendelea kudumisha amani na upendo katika nchi yetu ambayo ni kisiwa cha amani.
“nawaasa vijana wakitanzania wa leo hata kama mmenyimwa haki zenu ni bora kutumia njia ya kistaarabu na kutumia elimu mnayopata mashuleni bila kusahau macho, masikio na vipawa vyenu mlivyopewa na mwenyezi mungu katika kutafuta haki yenu kwa njia ya amani bila misukosuko,” aliongeza.
Mzee Mwinyi alitumia nafasi hiyo kuwashangaa baadhi ya watu kwa kutumia ujuzi na elimu yao kwa kumpachika jina la Ruksa bila yeye kujua wametumia muktha gani kumpa jina hilo, lakini Mzee Mwinyi alitumia jukwaa hilo pia kuwapa ruksa vijana kutumia elimu yao kuleta hali ya amani na utulivu ndani ya nchi.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Jama Gulaid amesema kwamba Umoja wa Mataifa uliweka maazimio siku ya kimataifa ya amani duniani ili watu wanaogombana na kupigana kwa shida mbalimbali kupata nafasi ya kuweka silaha zao chini katika siku hii adhimu.
Amesema kupitia azimio hilo ambalo lilizinduliwa mwaka 1982 kwa mara kwanza linatambua uwepo wa watu wanaoathirika na vita katika sehemu mbalimbali duniani na waliokwishapoteza maisha kutokana na matatizo vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Naye Mratibu na Mtathimini wa Mtandao wa watoto na vijana kutoka Imani Mbalimbali (GNRC) Bi, Joyce Mdachi amesema swala la amani na utulivu linaanzia kwenye kaya hadi ngazi ya taifa kwahiyo ni muhimu kwa jamii na vijana kuelewa amani inaanzia nyumbani.
“jamii iliyolelewa katika mazingira mazuri ina nafasi kubwa ya kuleta matokeo chanya kwenye mustakabali wa taifa kwa ujumla lakini jamii iliyolelewa vibaya haiwezi kubadilisha taifa kwa sababu ni zao la tunda baya,” alisema.
Mdachi alisisitiza kwamba kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii ya leo swala hilo pia lilianzia kwenye kaya ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya taifa ambapo leo hii taifa linashuhudia mambo ya kifisadi, rushwa na ubadhilifu wa mali za umma kunakofanywa na viongozi waandamizi.

Tanzania mabingwa wasichana mashindano ya kimataifa Airtel Rising Stars

$
0
0
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania
 Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars wakishangilia ushindi
 

 Mwakilishi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi na Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika
Kikosi cha timu mabigwa ya Airtel Rising stars Afrika cha wasichana cha Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja pichani waliosimama  (wa mwisho kushoto) ni kocha wa timu ya wavulana Abel Mtweve na wa mwisho kulia ni kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage

 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania na kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika.
----------------------------------------
Timu ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yaliyokuwa yanafanyika mwaka huu  nchi Nigeria.

Tanzania ilipata ubigwa huo baada ya kuchuana vikali na timu ya Kenya katika mechi ya Fainali  na kuifunga Kenya goli moja bila na kuibuka mabingwa . Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania.
Tanzania ilikua kundi moja na Sierra-Leone , Malawi , na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1 , wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na Malawi 1-1

Wakashinda 4-2 katika mikwaju ya penati dhidi ya DRC katika robo fainali mechi zilizopigwa katika uwanja wa NIS Sports. Na wakawatoa Uganda kwa mvua ya magoli 8-1

Mbali na ushindi huo wa wasichana watanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana Shelda Boniface.

Kwa upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa  baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6  katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.
Niger wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi  baada ya kushinda michezo yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita . Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo

Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na  Main bowl .

Kulianza na “ gala night” jumapili usiku ikafatia  sherehe za ufunguzi , na mechi za ufunguzi za makudi katika uwanja wa AgegeTownship .
Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili , mashindano haya yamekua bora kwa vijana wadogo na kwakuzingatia jinsia.


UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI UNABAGUA VYOMBO VYA HABARI AU AFISA HABARI WAKE NDIYE ANAYEBAGUA?

$
0
0
Na Alex Kassuwi wa Swahili TV na Swahili Radio Online.

Wiki iliyopita baada ya kulemewa  na maswali kutoka kwa wasomaji,wasikilizaji, watazamaji na wafuatiliaji wa vyombo vyetu vya habari vya MMK MEDIA GROUP watu wengi sana walituuliza  "kwa nini Swahili TV na Radio hawakuwepo katika tukio kubwa la kihistoria lililofanyika jumatano ya sept 18, 2013 katika ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani, ambapo Mabalozi wa Heshima (Honorary Consuls) walisaini mikataba mbele ya Rais wetu Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete. 

UKWELI NI KWAMBA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI UNABAGUA VYOMBO VYA HABARI AU AFISA  HABARI WAKE MINDI KASIGA
Baada ya tukio hafla hiyo kubwa kupita bila kusita  niliandika masikitiko yangu kwa niaba ya MMK MEDIA GROUP wamiliki wa Swahili TV online, Swahili Radio Online na Blog hii ya Swahilitv.blogspot.com kuhusiana na yaliyojitokeza ubalozini.

Leo hii katika tahariri hii nitaelezea na kufafanua makosa yaliyofanywa na  Ubalozi ama Mindi Kasiga na kwa nini hakupaswa ama hawakupaswa kubagua vyombo vya habari katika tukio lile. PIA NIMEAMBATANISHA BARUA YA MAMALIKO TOKA KATIKA CHOMBO KINGINE CHA HABARI KWA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI.

HIVI NDIVYO WAANDISHI TULIVYOTENDWA
Mosi; Mindi alionyesha dharau kwa kuwasiliana na vyombo vya habari kwa ujumbe mfupi wa email kutokea kwenye iPad yake katika akaunti yake binafsi ya gmail na badala ya kuandika barua ya kiofisi yenye nembo husika na yenye kumbukumbu na sahihi husika kama ilivyo kawaida. Kuthibitisha kwamba ni dharau, Mindi Kasiga alionyesha heshima pekee kwa shirika la  habari la kimarekani  VOA (Voice of America) kwa kuwapelekea barua ya kiofisi ya kuwaalika rasmi iliyozingatia taratibu zote za na sheria za kiofisi.

Pili; Mindi alisingizia ufinyu wa nafasi kuwa mdogo kwa vyombo vingine vya habari na huku mwaliko wa VOA ukiwa wazi kwa idadi ya watu wowote wale watakaopenda na watakaotaka kuhudhuria hafla ile wote walikaribishwa bila masharti.

Tatu; Mindi hakupaswa kujiamulia kwa kusema namnukuu "upande wa electronic media wote mtawakilishwa na jamii production". Swali 1. kwa Mindi hivi unaelewa nini kuhusu electronic media? au bado umebaki na mtazamo wa zamani ambapo kulikuwa na print na electronic iliyomaanisha Radio na TV ambavyo vilikuwa analojia, na tena terrestrial zikirusha matangazo kwa minara na mikonga ya mawasiliano. Swali 2. je, vipi kuhusu digital media? blogs, Online TV, Online Radio na Websites? hujui kwamba ndio vyombo vya habari vya leo vyenye wasomaji na wafuatiliaji wengi? Swali 3. Ni Criteria gani Ubalozi ama Mindi Kasiga waliyotumia kuiteua Jamii Production kuwakilisha vyombo vingine vya habari katika tukio la Kitaifa?

Nne; Mindi hukupaswa kuagiza vyombo vya habari vingine vipeleke maswali kwa Jamii production. Nakunukuu "kama kuna maswali yaelekezwe kwao" Mindi huwezi kuagiza chombo cha habari kupeleka maswali yake kwa chombo kingine, kisha kile kingine kwenda kuuliza na kuleta majibu, hii haipo katika dunia ya sasa labda karne zilizopita. Jiulize ni kama vile Ikulu wana hafla halafu unaagiza TBC Taifa wapeleke maswali yao ITV halafu ITV wakaulize na kisha kuwaletea jibu TBC Taifa! uliona wapi hiyo?

BARUA YA MALALAMIKO TOKA KWA MWANDISHI MWINGINE AMBAYO ILITUMWA APRIL 2013 KWENDA UBALOZINI
Na Mubelwa Bandio

Shikamoo Mama Munanka.




Natumai kuwa u-mwema na unaendelea vema na kazi za kila siku hapo ofisini.
Binafsi ni mwema na naendelea na pilika za maisha hapa.
Napenda kutumia nafasi hii kueleza masikitiko yangu kidogo kuhusu hali ninayoona ikitokea kati ya ubalozi na jamii kwa ujumla.



Ntajaribu kufupisha jambo hili linalonisumbua sana
Nimekuwa mmoja wa wanaoletewa maswali ya “kwanini hamjazungumza na viongozi waliokuja hapo ubalozini” na kwangu nimepata wakati mgumu hata kufikiria jibu.  
NI KWA KUWA HATA MIMI HUJIULIZA SWALI HILO
Nilishawahi kuleta maelezo na hata maoni ya namna ya kusaidiana na ubalozi kuunganisha jamii yetu hapa.




Binafsi naamini kuwa HAITATOKEA HATA SIKU MOJA, KUKAWA NA UJIO WA WAZIRI AMA RAIS AMA KIONGOZI YEYOTE WA NCHI KWA DHUMUNI MOJA TU LA KUKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI.




Ina maana, pale wanapopata ziara za kikazi, ndio wakati muafaka wa kukutana na / ama kuwasiliana nasi waTanzania tuishio huku (kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.)
SOTE TUNAJUA HILI SI KAWAIDA




Nilipata kuleta WAZO hapo ubalozini kuwa inapotokea ikajulikana kuna Mheshimiwa anayekuja, waTanzania katika DIASPORA waelezwe na waweze kutuma maoni kwa mhusika wa habari hapo ubalozini (kwa njia ya barua pepe), na mheshimiwa akija, tujumuishe maswali ya wanaDIASPORA na yale yatakayoandaliwa na wadau wa habari na kufanya mazungumzo nao.




Hii ingekuwa NJIA RAHISI NA MUAFAKA ya kuwasilisha mawazo, maswali na hata dukuduku la mTanzania wa Marekani popote alipo. Lakini badala yake, tumekuwa tukisikia kuwa “walikuwepo” na / ama kuwaona katika MATUKIO na kisha wanaondoka.
Katika hili, NAONA KAMA UBALOZI UMETUANGUSHA KATIKA KUTUUNGANISHA NA WALE WANAOTUONGOZA.




Naamini mjadala na kiongozi toka Tanzania (iwe ni Townhall meeting ama mahojiano yanayoratibiwa na ubalozi) ni muhimu kwa jamii yetu Nina hakika kuwa mikutano ya viongozi wanaokuja wanapokutana na viongozi wa Jumuiya na / ama vyama haikidhi mahitaji ya waTanzania wote nchini kwa kuwa wanakutana na viongozi wa Metropolitan waliyopo nao hawakutani na wanachama wote (hata wenye nia).




Nimeona niwasilishe wazo langu hili kwa mara ya mwisho nikiamini kuwa utawekwa utaratibu muafaka wa kuTUMIA VEMA ZIARA HIZI kuweza “kuua ndege wawili kwa jiwe moja” Yaani, ndani ya ziara zao za kikazi, waunganishwe nasi watanzania tulio huku.
Natanguliza shukrani NB: Nimewaambatanisha wanahabari wenzangu wa hapa DMV.
Chanzo:www.changamotoyetu.blogspot.com
mwisho wa barua ya Bandio



NAMALIZIA KWA HILI MUHIMU

Pamoja na mamaliko ya Mwandishi mwenzetu Mubelwa Bandio bado Ubalozi au Afisa habari wake hawajajirekebisha na bado kero ziko palepale na vyombo vya habari. Swali, kwa nini viongozi wa kiserikali wanapokuja katika ziara za kikazi hapa nchini Marekani Ubalozi hautoi taarifa kwa vyombo vya habari? na badala yake Ubalozi unatumia chanzo kimoja cha habari, ambapo mwanahabari mmoja huyo anatumika ku-brake news za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati sisi wanahabari wengine tunastukizwa na habari za ujio wa viongozi walifika lini, wamefanya nini nk toka katika chombo hiki kimoja na tunabaki tukijiuliza hiki ni chombo binafsi ama kitengo cha Ubalozi? Tungependa kuwe na Freedom of Speech, na Ushirikishwaji kwa vyombo vya habari vyote bila kubagua. Vyombo vya habari vipo na vinajulikana na Ubalozi unavitambua kwani vilishajitambulisha.

PRESIDENT KIKWETE ATTENDS HIGH-LEVEL meeting on Scaling up Nutrition in New York

$
0
0
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a High-level meeting on Scaling up Nutrition  in New york this morning. To his left is Dr. Ngozi Okonjo-Iweala, Nigeria's Minister of Finance, and SUN Lead Group Member

Each year since 2010 there has been a High-Level Meeting and a series of other gatherings held in New York during the United Nations General Assembly, to increase political attention to the issue of nutrition and encourage greater support for the efforts of SUN countries and the Movement.
As a result of the dramatic increase in political attention to nutrition throughout 2013, SUN countries and stakeholder groups have sought to create space for more in-depth, structured interaction. The SUN Movement Global Gathering offers an opportunity for this form of interaction. Representatives from SUN countries and across the Movement will participate in the workshop-style event to solve practical bottlenecks and achieve concrete results.
The purpose of the 2013 SUN Movement Global Gathering is to enhance the Movement’s impact through:
  1. *Demonstrating results in SUN countries – contributing to the learning agenda by focusing on how results can best be achieved;
  2. *Enabling countries to seek solutions to help them scale up nutrition from other countries and networks;
  3. *Bolstering mutual accountability within the Movement – with all constituents – countries, networks, Secretariat and members of the Lead Group giving accounts of their contributions; and
  4. *Envisioning the Movement beyond 2015.
  5. For more CLICK HERE
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a meeting on Scaling up Nutrition held in New york this morning. To his left is Dr. Ngozi Okonjo-Iweala, Nigeria's Minister of Finance, and SUN Lead Group Member, behing hi with red tie is Tanzania's Minister for Health Dr Hussein Mwinyi, left is personal assistant to the President on Nutrition  Dr Wilbrad Lorri

Timesofmoney yadhamiria Kuingi katika Soko la Tanzania

$
0
0
KAMPUNI kubwa duniani yenye utaalamu wa kuwezesha uhamisho wa fedha kwa njia ya mtandao (online) ya Timesof Money, imedhamiria kuingia katika soko la Tanzania, kama sehemu ya mpango wake wa upanuzi barani Afrika.

Katika mpango wake huo, kampuni hii yenye makao yake makuu jijini Mumbai nchini India, inatajaria kuzindua mpango/mfumo wa kutuma fedha nchini toka kwa Watanzania walioko nje ya nchi (remittance) kwa njia ya mtandao (Online).  Mfumo huo ambao unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa nchini, utawawezesha Watanzania kupata/kutuma fedha kutoka mahali popote duniani moja kwa moja katika akaunti zao za benki, kadi za malipo ya kabla (pre-paid cards) pamoja na simu zao za mkononi.


“Katika mkakati huo huo wa kijitanua barani Africa, hivi karibuni tumeingia mkataba na Benki ya Diamond Trust nchini Kenya kutoa huduma kwa wateja wake wa mfumo wa ‘NationHela’,” alisema Afisa Mtendaji mkuu wa TimesofMoney, Avijit Nanda.


Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, idadi ya Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchi mbalimbali duniani/ughaibuni (diaspora) inakadiriwa kuwa zaidi ya million mbili. Na kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia, inakadiriwa kuwa Watanzania hao waliingiza nchini kiasi cha shillingi billion 120 (US$ 75million)mwaka jana. Kwa kutumia huduma hii, Watanzania wanaoishi nje ya nchi wataweza kutuma pesa kwa jamaa na marafiki zao nyumbani, hivyo kuondoa usumbufu wa kusimama katika foleni kwa mawakala wa kuhamisha fedha.


"Idadi ya raia wa nchi za Afrika Mashariki na hasa Tanzania wanaoishi nje ya nchi zao inaendelea kuongezeka na hii ina maanisha uhitaji wa kutuma fedha nyumbani (remittance) pia unaongezeka. Ni kwa sababu hii tumeona kuna umuhumi wa kuingia katika soko hili. Tukiwa na teknolojia ya kisasa, tunatoa ahadi ya huduma bora kwa kutumia wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika nyanja hii,” alisema Bw Nanda.


Bara la Afrika linakadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya million 30 wanaoishi nje ya nchi zao za asili. Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo-- International Fund for Agricultural Development (IFAD), unakadiria kwamba mwaka jana (2012) wahamiaji hao kwa pamoja wamechangia/ wametuma kiasi cha dola za marekani millioni 38.6 katika fedha kutoka nje, kwa familia na jamii zao nyumbani.


Hata hivyo, moja ya kikwazo kikubwa kwa ukuaji wa mtiririko kutuma fedha nyumbani (remittance) katika nchi za Afrika hasa zile zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara, ni gharama kubwa ya kutuma fedha. Wastani wa gharama ya kutuma fedha kwa Afrika ni karibu 12 % ya juu kuliko wastani wa kimataifa wa 8.96 % na karibu mara mbili ya gharama ya kutuma fedha kwa Asia ya Kusini.


"Gharama kubwa za ada zinazotozwa na makampuni na mawakala wa kuhamisha fedha barani Africa, imekuwa ni kikwazo na imeathiri mtiririko wa kuingiza fedha toka nje ya nchi. Mtumiaji wa mwisho ndiye anayeathirika na kubeba mzigo wa gharama/ada kwa kiasi kikubwa. Kwa kupitai mfumo wa mtandao (online-transactions) tunatarajia  inaweza kusaidia kupunguza gharama hizi kwa kiasi kikubwa, jambo ambalo litatao ahueni kubwa kwa mtumiaji wa mwisho,” bosi huyo wa TimesofMoney alisema.



 Kuhusu TimesofMoney :

TimesofMoney ni  kampuni inayoongoza duniani kwa kufanya biashara  ya uhamisho wa fedha  kitaalamu. Kampuni hii inisifika kwa kufanya biashara  na wateja mbalimbali wakiwemo wa rejareja na kitaasisi duniani kote. Ikiwa imeanzishwa mwaka 2000, TimesofMoney, inatoa ufumbuzi  wa mifumo ya malipo kwa wafanyabiashara.

Huduma zinatolewa duniani kote - kuwezesha uhamisho wa fedha watu kwenda kwenye nchi zao za nyumbani na kutoa huduma ya urahisi wa kutumia internet au simu. Ikiwa na zaidi ya miaka 12 ya uzoefu, TimesofMoney inajivunia mahusiano mazuri na ya nguvu na wateja wake wakiwemo wale wa rejareja, kitaasisi na pia inaheshima na mafanikio makubwa katika sekta ya fedha kwa miaka kadhaa sasa.
Kampuni hii pia inajuvunia kuwa mbia mkubwa (kuwa na hisa kubwa) katika Mtandao wa Kimataifa, na ni kiongozi wa soko katika mfumo wa malipo. Inasimamiwa na timu ya wataalamu wenye uzoefu kutoka benki na historia nzuri ya fedha.


Maelezo zaidi zinapatikana kwenye tovuti ya kampuni www.timesofmoney.com .



Simply Madini makes a generous donation (sponsorship) to Hassan Maajar Foundation

$
0
0
Simply Madini is a locally owned company, specializing in importing Fine Jewelry, Fashion Jewelry, Kids Jewelry and Watches from the US top jewelers and vend to Top Ladies here in Tanzania.

On Monday  September, 23rd Simply Madini’s PR Manager Loni Stephen presented an Emerald 4 piece sterling silver set, which includes earrings, ring, bracelet and necklace to HMF Managing Director Zena Tenga as part of the sponsorship of the upcoming HMF 2nd annual dinner gala.


‘We are thrilled to be able to make this generous donation which is a result of proceeds from our Vision and Mission Statement (VMS) to continue to have the high quality of corporate and CSR behavior and values’ stated Loni Stephen.


The Annual Dinner Gala is taking place this Friday, 27th September 2013 at Diamond VIP Jubilee Hall. More than 900 of Dar’s top corporate executives, political and social leaders will be in attendance.


Prepared by: Kikoi Innovative Media Ltd.

TAMKO LANGU kuhusu malalamiko ya MMK MEDIA kuhusu Afisa Ubalozi

$
0
0
Kwa wasomaji wa blog / tovuti hii

SALAAM
Binafsi napenda kugusia mambo mawili kuhusiana na lalamiko lao KWA NAMNA AMBAVYO NIMEHUSISHWA / TUMEHUSISHWA (kama Jamii Production).

Katika malalamiko hayo, MMK MEDIA imeambatanisha BARUA YANGU ambayo ilikuwa ni BARUA BINAFSI KWA KAIMU BALOZI (kwa wakati huo) Mama Lilly Munanka.

Barua hiyo (kama nilivyosema hapo awali) ilikuwa ni BARUA BINAFSI na haikupaswa kuchapishwa kwenye blogu kama ilivyotokea. Niliiandika kwa Mama Munanka kama barua ya awali ya malalamiko kwake na haikuwa barua ya kuchapisha kwenye blogu kama ilivyotokea (kwa bahati mbaya) kwa wale niliowaambatanisha.

KAMA INGEKUWA NI YA KUCHAPISHWA KWENYE BLOGU, BASI INGEKUWA KWENYE BLOGU YANGU KABLA YA KWINGINE KOKOTE
Hata hivyo, punde baada ya kuchapishwa niliwasiliana na wanahabari wenzangu (ambao niliwaambatanisha katika barua hiyo) na kuwaeleza kuwa ile ilikuwa NAKALA KWAO NA SIO CHAPISHO LA BLOG.

Nilifanya hivyo kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuwasiliana na Mama Munanka na hivyo halikuwa jambo sahihi kuchapisha barua hiyo bloguni. Lakini pia, katika lalamiko la sasa, MMK MEDIA wameandika kuwa "Baada ya tukio hafla hiyo kubwa kupita bila kusita niliandika masikitiko yangu kwa niaba ya MMK MEDIA GROUP wamiliki wa Swahili TV online, Swahili Radio Online na Blog ya Swahilitv.blogspot.com kuhusiana na yaliyojitokeza ubalozini."

Ni kweli kuwa nami niliyaona malalamiko hayo ambayo pia kwa kiasi fulani yalinisikitisha
Katika malalamiko hayo, MMK MEDIA iliandika kuwa "afisa huyu alikimbia vyombo vya habari rasmi na kualika video production company inayofanya shughuli za harusi kuwa mwakilishi wa Swahili Tv, Swahili Radio, Swahilitv Blog, na vyombo vingine vinavyoheshimika hapa DMV" (tazama screenshot hapa chini)
Licha ya kwamba post hii iliondolewa muda mfupi baadae, lakini bado UKWELI unabaki kuwa MMK MEDIA wameamini, na bado wanaamini (kwa kuwa mpaka sasa hawajakanusha) kuwa JAMII PRODUCTION SI CHOMBO CHA HABARI bali ni kampuni ya kurekodi harusi.

Hilo lilinisikitisha kwa kuwa NI DHAHIRI KUWA TUMEKUWA TUKIFANYA HABARI KABLA NA ZAIDI YA MMK MEDIA.

Tumekuwa tukishirikiana HABARI (sio matukio na taswira tuu) na vyombo vingi vya habari nchini Tanzania KABLA YA KUZALIWA KWA MMK MEDIA.
Na katika hili, ushahidi upo wazi kwani sote tunaweka kazi zetu online, hivyo ni rahisi kwa wewe msomaji kuLINGANISHA UBORA WA HABARI katika KAZI ZETU ZA SAUTI (hapa) NA KAZI ZAO (hizi hapa) ama KAZI ZETU ZA VIDEO (hapa) na KAZI ZAO (hapa)

Kwa kumalizia tu, niseme kuwa SIPINGI HAKI YA MMK MEDIA KULALAMIKA, ila nasikitika kuwa WAMETUMIA BARUA YANGU BINAFSI KUJAZIA MALALAMIKO YAO HADHARANI, na pia wameshindwa kuwa wawazi kuhusu malalamiko yao ya awali ambayo kwa namna moja ama nyingine YALIPOTOSHA KUHUSU JAMII PRODUCTION NA KAZI ZAKE.
Lakini bado (BILA IDHINI) wametumia nakala ya barua yangu kutimiza lengo lao.

Katika hili nimesikitishwa na ningependa NILIWEKE HILO WAZI.

Mubelwa T Bandio
MTAYARISHAJI / MTANGAZAJI
JAMII PRODUCTION
http://www.changamotoyetu.blogspot.com http://www.youtube.com/user/mutwiba

All Hail For The King "He's Back" - Huu ndio ujio Mpya wa CPwaa

$
0
0

All Hail For The King "He's Back" - Huu ndio ujio Mpya wa CPwaa

Mashabiki wake hupendelea kumuita "King of BongoCrunk"....jina halisi ni Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa! Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambaye baada ya ukimya mrefu sasa kuachia kazi zake mpya.

C.P a.k.a CPwaa mwenye tuzo 3 za Tanzania Kilimanjaro Music Awards na Multiple Channel O Africa Music Video Awards nominations anakuja kivingine kabisa mwaka huu. Tarehe 1 mwezi wa October 2013, CPwaa ataachia single yake mpya na ya kwanza kabisa kwa mwaka huu.Single hiyo iitwayo "Chereko Chereko" yenye mahadhi ya AfroDance imefanywa chini ya studio za 'De Fatality Music" na producer "Mesen Selekta" ambaye mwaka huu alichukua tuzo ya mtayarishaji  bora Tanzania anayechipukia.Nyimbo hii itapatikana kwenye mitandao yote na media zote kuanzia tarehe moja October.

CPwaa ambaye amesaini mkataba mnono na Universal Music group vile vile anategemea kuachia single nyingine mwanzoni mwa mwaka 2014 ambapo amewashirikisha mafahari wengine wawili kutoka Afrika. Single hiyo ya kimataifa iitwayo "Cross-Borders Therapy" imekutanisha wakali kutoka mashariki,magharibi na kusini mwa Afrika. CPwaa amemshirikisha "DBlack" kutoka Ghana, DBlack ni moja ya wasanii wakubwa wa Hip Hop Afrika ambaye ana tuzo nyingi ikiwemo zile za Channel O.Kwa upande wa Afrika ya kusini CPwaa amemshirikisha "Hip Hop Pantsula" a.k.a HHP kwenye nyimbo hiyo hiyo ya Cross Borders Therapy.

HHP ni mmoja ya MaMC wakali kutoka bondeni mwenye tuzo nyingi ikiwemo ya MTV Base. Nyimbo hii itakuwa ya kwanza Afrika ambayo imekutanisha wakali kutoka mashariki ,magharibi na kusini ( The first East,West and South African Hip Hop Collaboration in History).Nyimbo hii pia imefanyika chini ya producer Mesen Selekta pale  "De Fatality Music" Studio.

Kifuatacho baada ya nyimbo hizi kutoka ni video zake ambapo Chereko Chereko itafanyiwa Tanzania na Cross Border Therapy kufanyika nchini Afrika ya kusini. Kwa wale mashabiki ambao watakuwa na kiu ya wimbo wa Cross Border Therapy ambao utatoka mwakani wataweza kuupata wimbo huo kupitia iTunes,Amazon, Spotify na digital store zingine bila kusahau mtandao wa "The Kleek" kwa wale watumiaji wa smartphones za Samsung na Androids.

Asanteni sana na tuendelee kutoa support kwa wasanii wetu na muziki wetu.

MBUNIFU WA MITINDO YA MAVAZI NA BALOZI WA OXFAM TANZANIA KHADIJA MWANAMBOKA AZINDUA PROJECT

$
0
0
MBUNIFU WA MITINDO YA MAVAZI NA BALOZI WA OXFAM TANZANIA -KHADIJA MWANAMBOKA AMEZINDUA PROJECT-VVK-GROW CAMPAIGN PROJECT.  HII NI KAMPENI ILIYOBUNIWA NA KUENDESHWA NA BALOZI WA OXFAM KHADIJA MWANAMBOKA NA IKIWA NA LENGO LA KUAINISHA CHANGAMOTO ZA SOKO KWA WAKULIMA WA CHAKULA HASA WANAWAKE,KUANIKA DHULUMA WANAYOFANYIWA WAKULIMA WA CHAKULA WANAWAKE NA KUHAMASISHA WATUMIAJI WA BIDHAA ZA CHAKULA MIJINI,KUTAMBUA THAMANI YA CHAKULA NA KUWA SOKO LENYE TIJA KWA WAKULIMA WA CHAKULA HASA WANAWAKE KAMPENI HII INAHUSISHA WASICHANA"GROW GIRLS" AMBAO NI WANAMITINDO -MODELS WATAKUWA WANAPITA KWENYE MIKUSANYIKO MBALI MBALI, MAOFISINI NA KWENYE TAASISI MBALI MBALI KUHAMASISHA NA KUUZA BIDHAA ZA WAKULIMA WADOGO WANAWAKE.





Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images