Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

MBUNGE JIMBO LA CHUMBUNI AZUNGUMZIA TAMASHA LA YATIMA LITAKALOFANYIKA OKTOBA, 2018

$
0
0

Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Fondeshen ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la Mayatima ambalo hufanyika kila ifikapo Mwezi kumi(10)Mfunguo Tatu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villas mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Fondeshen ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la Mayatima ambalo hufanyika kila ifikapo Mwezi kumi(10)Mfunguo Tatu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villas mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Fondeshen ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza kuhusiana na Tamasha la Mayatima ambalo hufanyika kila ifikapo Mwezi kumi(10)Mfunguo Tatu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villas mjini Zanziba

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO

$
0
0
Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aitwaye Monica Joseph Magufuli aliyefariki dunia Jumapili tarehe 19 Agosti, 1955 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza amezikwa leo katika makaburi ya familia yaliyopo katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita. 

Misa Takatifu ya Mazishi ya Monica Joseph Magufuli ameongozwa na Askofu Jimbo Katoliki la Rulenge Mhashamu Severine Niwemugizi aliyeambatana na Maaskofu wengine saba, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. 

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mhe. Raila Amolo Odinga, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mawaziri, Wabunge, Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wengine mbalimbali wa Mikoa, Wilaya, Taasisi, Idara na Kampuni. 

Akisoma Wasifu wa Marehemu kwa niaba ya Familia, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Bw. Gerson Msigwa amesema marehemu Monica Joseph Magufuli alizaliwa tarehe 25 Novemba, 2018 na ni mtoto wa kwanza wa Mzee Joseph Marco Magufuli (ambaye ametangulia mbele za haki) na Mama Suzana Ngolo Magufuli ambaye yupo hai. 

Msigwa amesema Monica ameacha Mme, watoto 9 na Wajukuu 25. 

Katika salamu zake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi na wananchi wote walijitokeza kuungana na familia katika kumsindikiza Dada yake katika safari yake ya mwisho na amesema familia inatambua upendo, heshima na mshikamano mkubwa ambao wameuonesha kwao. 

“Mmetuonesha upendo mkubwa sana na kweli ujio wenu na kuungana nasi katika tukio hili mmetufariji sana, asante sana kwa upendo huu na Mungu awabariki sana” amesema Mhe. Rais Magufuli. 

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuelezea Dada yake Marehemu Monica Joseph Magufuli kuwa alikuwa mtu mwenye upendo kwa familia nzima na alikuwa tegemeo kubwa la kumtunza Mama yake mzazi Bibi. Suzana Ngolo Magufuli na kwamba alikubali kuondoka nyumbani kwa mmewe kwa zaidi ya miaka miwili na kurudi nyumbani kumlea mama yao mzazi. 

Mhe. Rais Magufuli amesema Marehemu Monica ameacha somo kwa watoto wote na wanandoa kuwa tayari kujitolea kuwalea wazazi wao wanapokabiliana na changamoto za uzee badala ya kuwaacha wakitaabika.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa  Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
3 (1)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsaidia  Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakuweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
6 (2)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kanisani katika Misa takatifu ya kumuombea Marehemu Dada yake Monica Magufuli. Wengine katika picha ni Mama yake Suzana Magufuli, Stanslaus Lori Madulu(Mme wa marehemu) , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.
7
Baba Askofu mkuu Mwandamizi  Yuda Thaddeus Ruwaichi akiongoza Misa ya kumuombea Marehemu Monica Magufuli Chato mkoani Geita
8 (1)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkewe Mama Marry Majaliwa wakitoa heshma zao za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
9
Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
10
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la Dada yake Monica Magufuli mara baada ya mazishi.
12
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo ndani ya kaburi la Monica Joseph Magufuli wakati wa mazishi yaliyofanyika katika kijijini cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai( katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo, kuhusu maendeleo ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kushoto ni Daktari bingwa upasuaji wa mfumo wa mkojo Njiku Kim , kulia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya figo Onesmo Kisanga.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Njiku Kim akiandaa figo kabla ya kupandikizwa kwa mgonjwa. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo wa Muhimbili, Victor Sensa akishirikiana na Dkt. Kim kuaandaa figo kwa ajili ya kupandikizwa kwa mgonjwa mwingine.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt . Isaack Mlatie akitoa figo kwa ajili ya kupandikiza kwa mgonjwa mwenye tatizo la figo. Katikati ni daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo, Muhimbili, Dkt. Gabriel Mtaturu akishiriki katika upasuaji huo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Sakra nchini India, Dkt. Girish Nelivigi akishirikiana na madaktari wa Muhimbili kufanya upasuaji huo.
Wataalamu wakiendelea na upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa mkojo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa mkojo kutoka nchini India.

Dar es salaam 21-08-2018

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma ya kupandikiza figo ambapo hadi hivi sasa tayari wagonjwa 19 wamenufaika na huduma hiyo tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini Novemba mwaka 2017.

Utoaji wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambayo ili elekeza kuweka mipango thabiti ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambayo yalikuwa hayatolewi hapa nchini ama kutokana na wataalam wa kutoa huduma hizo au vifaa vya uchunguzi.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai alipokua akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Prof. Lawrence Museru kuhusu upandikizaji figo.

“Tunapenda kuwafahamisha kuwa wagonjwa wote tuliowapandikiza figo pamoja na ndugu zao waliojitolea figo wanaendelea vizuri na shughuli zao kama kawaida. Hii inaonesha ni kwa kiwango gani huduma hii imefanikiwa tangu ilipoanzishwa Novemba mwaka jana ”. amesema Dkt Swai.

Akifafanua amesem zoezi hilo la upandikizaji figo limeshirikisha wataalamu wazalendo toka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya BLK, Taasisi ya Saifee iliyopo Mumbai India pamoja na Hospitali ya kimataifa ya Sakra ya nchini India.

“Tunapenda kuwataarifu kuwa katika kutoa huduma hii, tayari wataalamu wetu wa ndani hususani Madaktari bingwa wa upasuaji wamepata ujuzi wa kufanya upandikizaji wenyewe kwa kiwango cha asilimia 75 huku asilimia 25 wakielekezwa na wataalamu kutoka nje. Hii ni hatua kubwa sana katika kuongeza ujuzi wa kutoa huduma hiyo. Maeneo mengine tayari wamefikia asilimia 100 hususani wauguzi wa vyumba vya upasuaji, Madaktari bingwa wa tiba ya magonjwa ya figo (Nephrologists), wataalam wa vipimo vya maabara na Radiolojia.

Kwa mujibu wa Dkt. Swai MNH itaendelea kufanya upasuaji kwa wagonjwa watano kila mwezi ikiwa ni mpango wa muda mfupi katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia sasa ambapo mpango wa muda mrefu ni kufanya upasuaji kwa mgonjwa mmoja kila siku sawa na wagonjwa 20 kwa mwezi ambapo watakuwa wagonjwa 200 hadi 240 kwa mwaka.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya figo Hospitali ya Taifa Muhimbili Onesmo Kisanga amesema utafiti uliofanyika Kaskazini mwa Tanzania unaonesha kwamba asilimia 6.8 wana matatizo ya ugonjwa wa figo.

Hivyo amewashauri Watanzania kupima afya zao angalau mara moja kwa mwaka na kuepuka matumizi mabaya ya dawa bila ushauri wa Daktari ili kuepuka magonjwa hayo.

Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda wafunguliwa jijini Kampala

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Balozi Patrick Mugoya akisoma hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda unaofanyika jijini Kampala kuanzia tarehe 21 hadi 23 Agosti 2018. Balozi Mugoya katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa Tanzania na Uganda kuboresha miundombinu na kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kupunguza gharama za kufanya biashara kati ya Tanzania na Uganda

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi ambaye pia ni kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya maafisa waandamizi akisoma hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa JPC. Bw. Mbilinyi alisema kuwa Mkutano huo pamoja na mambo mengine utathimni utekelezaji wa masuala yaliyokubalika wakati wa mkutano wa kwanza wa JPC uliofanyika Arusha mwezi Aprili 2017 na kuweka mikakati ya utekelezaji kwa masuala ambayo hayajakamilika.
Balozi Mugoya na Bw. Mbilinyi wakiwa katika meza kuu kabla hawajasoma hotuba za ufunguzi.

Kutoka kushoto ni Bw. Mbilinyi, Bw. Innocent Luoga, Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Bi. Tuma Abdallah Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) wakiwa katika meza kuu.

Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia hotuba za ufunguzi wa Mkutano wa JPC. Kutoka kushoto ni Bi. Mwadawa Ali kutoka kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Bw. Paul Makelele kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Karim Msemo wa Wizara ya Mifugo.

Sehemu ya ujumbe wa Uganda ukifuatilia ufunguzi wa mkutano wa JPC.

Mhandisi Robert Marealle kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akiongea jambo katika mkutano wa JPC.

Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Erick Ngilangwa na Bi. Elizabeth Rwitunga ambao ni sehemu ya sekretarieti ya mkutano huo wakinukuu masuala muhimu yanayozungumzwa.

Ujumbe wa Tanzania

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Balozi Patrick Mugoya na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi wakibadilishana mawazo baada ya ufunguzi wa mkutano wa JPC kukamilika.

WAJUMBE KAMATI ZA BUNGE WAJENGEWA UELEWA KUHUSU DHANA YA MISWADA ITAKAYOJADILIWA BUNGENI KATIKA MKUTANO WA BUNGE LA KUMI NA MBILI.

$
0
0








Katibu kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Ndg. Chacha Nyakega akizungumza na Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba (Kushoto) akimsikiliza Katibu kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Ndg. Chacha Nyakega (kulia) ambae ni mtoa maada akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo (hawapo kwenye picha) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi wa kamati za Bunge Ndg. Athuman Hussein (wa pili kulia) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambae pia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian kapufi (katikati)akisisitiza jambo wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe na Mbunge wa Mgogoni Mhe. Dkt. Ally Suleiman na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Silafu Maufi
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Ndogo, Mhe. Taska Mbogo (Kushoto)akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo ambao pia Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa majadiliano katika semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Ndogo ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika majadiliano baada ya semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma

WAKAZI WA KILAMBO MKOANI MTWARA WAOMBA KIWANDA CHA KUSINDIKA MAZAO YA KILIMO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Mtwara

WAKAZI wa Kijiji cha Kilambo, Wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara, wameiomba Serikali iwasaidie kuwatafutia mwekezaji atakayejenga kiwanda cha kusindika matunda na mazao ya kilimo katika kijiji chao kutokana na kijiji hicho kuwa na matunda na mazao mbalimbali yanayokosa soko na kuwasababishia umasikini.

Wakazi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo Bw. Mohamed Mkama, wametoa ombi hilo mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, aliyefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Forodha cha Kilambo, kilichoko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mkoani Mtwara, kwamba kijiji chao kina fursa nyingi za kilimo zinazohitaji viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yao na kutoa ajira kwa vijana.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo Bw. Mohamed Mkama, alisema kuwa Kijiji chao kinapakana na nchi ya Msumbiji ambako kuna mwingiliano mkubwa wa watu katika masuala ya biashara na uhusiano wa kijamii ikiwemo pande

mbili za nchi kuoleana hivyo kuwafanya wananchi wa Msumbiji waishio mpakani kutegemea bidhaa kwa wingi kutoka katika kijiji chao.

"Watu kutoka Msumbiji wananunua sana chakula na bidhaa nyingine kutoka kwetu lakini tunawauzia bidhaa bila kuongeza thamani hivyo uwepo wa kiwanda utakuza uchumi wa kijiji chetu na tunakuomba Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, utusaidie kupata kiwanda ili nasi tuweze kunufaika" alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Kijiji

Mkazi mwingine wa Kijiji hicho Bw. Selemani Kumamba, alimweleza Waziri wa Fedha na Mipango kwamba Kijiji chao ni maarufu kwa kilimo cha matunda hivyo wanapendekeza kujengwa kwa kiwanda cha kusindika matunda ili juisi itakayozalishwa katika kijiji chao iwe na soko.

"Mhe. Waziri sisi ni wakulima wazuri wa matunda lakini matunda yetu wakati wa msimu yanakosa soka, yanaoza na tunayatupa jambo linalotulazimu tukuombe utusaidie kuhamasisha wawezezaji waje wajenge kiwanda cha kusindika juisi katika kijiji chetu ili nasi tuondokane na umasikini" alisema mzee Selemani Kumamba

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, aliwaambia wakazi hao kwamba inabidi ufanyike utafiti wa kutosha ili kubaini wingi wa mazao yanayozalishwa na wakulima katika kijiji hicho na vijiji jirani ili kupata takwimu sahihi za uzalishaji wa mazao hayo yakiwemo matunda ili kuiwezesha Serikali kuwashawishi wawekezaji kujenga kiwanda katika eneo hilo na kuwapongeza wakulima hao kwa kufanya kazi kwa bidii na mawazo yao ya kujiletea maendeleo.

"Tukiwa na uhakika huo hata mwekezaji anayekuja tutamwambia kwa mwaka mmoja, kwa wastani, kijiji hiki na vijiji jirani vinazalisha maenbe kiasi fulani, kwa hiyo wazo la kutaka kuwa ni kiwanda ni zuri lakini linahitaji kufanyiwa kazi zaidi" alisema Dkt. Mpango aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bw. Evod Mmanda

Aliwasahauri wanakijiji hao kuanzisha mashamba mapya ya matunda na kupanda mbegu za kisasa zinazozaa kwa wingi na kuushauri uongozi wa wilaya kuwasaidia wananchi hao kupata miche ya kisasa inayozaa kwa muda mfupi ili waweze kushawishi zaidi kupatikana kwa kiwanda kijijini hapo.

Dokta Philip Mpango, yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine amekutana na wafanyabiashara wa mkoa wa Kigoma pamoja na Kutembelea taasisi zilizochini ya Wizara hiyo. 
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), akitoka kukagua Kituo cha Forodha na Ushuru cha Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji (Kilambo), alipofanya ziara na kuzungumza na wafanyakazi wa Kituo hicho, mkoani Mtwara.
 Meneja wa Kituo cha Forodha na Ushuru cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara Bw. Emmanuel William (wa tatu kulia), akitoa maelezo ya eneo jipya la ujenzi wa Ofisi za Kituo hicho katika Kijiji cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. 
 Meneja wa Kituo cha Forodha na Ushuru cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara Bw. Emmanuel William (kulia), akitoa maelezo ya eneo jipya la ujenzi wa Ofisi za Kituo hicho katika Kijiji cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb),  akitembelea maeneo mbalimbali ya  Kituo cha Forodha katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji- Kilambo Mkoani Mtwara. 
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu uhitaji wa Ofisi za Kituo cha Forodha katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji- Kilambo, Mkoani Mtwara ili kurahisisha utendaji katika kudhibiti magendo na ukusanyaji wa mapato wakati wa ziara ya Waziri huyo alipokwenda kujionea hali halisi ya mpaka huo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo Bw. Mohammed Mkama, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara kukagua pamoja na mambo mengine, Kituo cha Forodha na Ushuru cha Kilambo, kilichoko katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
 Diwani wa Kata ya Tangazo Bw.(kushoto), akijadili jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipokutana na wakazi wa Kijiji cha Kilambo, akiwa katika ziara yake ya kukagua Kituo cha Forodha na Ushuru-Kilambo, kilichoko mpakani kwa Tanzania na Msumbiji.
 Wazee wa Kijiji cha Kilambo wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa utendaji wake mzuri wa kazi, alipofanya ziara ya kutembelea Kituo cha Forodha katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji- Kilambo Mkoani Mtwara.
 Mzee Seleman Kumamba (kushoto) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ambapo alimuomba Waziri huyo kuangalia uwezekano wa kuweka kiwanda katika eneo hilo  kikiwemo cha kusindika matunda kwa kuwa watanufaika kutokana na soko la mazao yao lililopo nchi jirani ya Msumbiji.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza na vyombo vya habari (havipo pichani) baada ya kujionea hali halisi ya Mpaka wa Tanzania na Msumbiji eneo la Kilambo Mkoani Mtwara na kueleza kuwa atatatua changamoto mbalimbali za eneo hilo ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti magendo. kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda.(Picha na Kitengo cha Mwasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango).

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), akitoka kukagua Kituo cha Forodha na Ushuru cha Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji (Kilambo), alipofanya ziara na kuzungumza na wafanyakazi wa Kituo hicho, mkoani Mtwara.
 Meneja wa Kituo cha Forodha na Ushuru cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara Bw. Emmanuel William (wa tatu kulia), akitoa maelezo ya eneo jipya la ujenzi wa Ofisi za Kituo hicho katika Kijiji cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. 
 Meneja wa Kituo cha Forodha na Ushuru cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara Bw. Emmanuel William (kulia), akitoa maelezo ya eneo jipya la ujenzi wa Ofisi za Kituo hicho katika Kijiji cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb),  akitembelea maeneo mbalimbali ya  Kituo cha Forodha katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji- Kilambo Mkoani Mtwara. 
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu uhitaji wa Ofisi za Kituo cha Forodha katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji- Kilambo, Mkoani Mtwara ili kurahisisha utendaji katika kudhibiti magendo na ukusanyaji wa mapato wakati wa ziara ya Waziri huyo alipokwenda kujionea hali halisi ya mpaka huo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo Bw. Mohammed Mkama, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara kukagua pamoja na mambo mengine, Kituo cha Forodha na Ushuru cha Kilambo, kilichoko katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
 Diwani wa Kata ya Tangazo Bw.(kushoto), akijadili jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipokutana na wakazi wa Kijiji cha Kilambo, akiwa katika ziara yake ya kukagua Kituo cha Forodha na Ushuru-Kilambo, kilichoko mpakani kwa Tanzania na Msumbiji.
 Wazee wa Kijiji cha Kilambo wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa utendaji wake mzuri wa kazi, alipofanya ziara ya kutembelea Kituo cha Forodha katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji- Kilambo Mkoani Mtwara.
 Mzee Seleman Kumamba (kushoto) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ambapo alimuomba Waziri huyo kuangalia uwezekano wa kuweka kiwanda katika eneo hilo  kikiwemo cha kusindika matunda kwa kuwa watanufaika kutokana na soko la mazao yao lililopo nchi jirani ya Msumbiji.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza na vyombo vya habari (havipo pichani) baada ya kujionea hali halisi ya Mpaka wa Tanzania na Msumbiji eneo la Kilambo Mkoani Mtwara na kueleza kuwa atatatua changamoto mbalimbali za eneo hilo ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti magendo. kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda.(Picha na Kitengo cha Mwasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango).

Tanzania yatia fora Tamasha la michezo Afrika Mashariki jijini Bujumbura

$
0
0
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania (waliovalia jezi nyeupe) ikichuana na timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Burundi katika uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi. Katika pambano hili timu ya Taifa ya Tanzania iliibuka na ushindi mnono wa magoli 8-1 dhidi ya timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Burundi. 

Kufuatia ushindi huu timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania inatarajia kukutana na Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Kenya katika mchezo utakaofanyika siku ya Alhamis terehe 23 Agosti 2018 kwenye uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi.

Aidha, timu ya mpira wa pete ya Taifa ya Tanzania pia iliibuka na ushindi mnono wa magoli 79-14 dhidi ya timu ya mpira wa pete ya Burundi. Kufuatia shindi huo timu ya Taifa ya mpira wa pete inatarajia kukutana na timu ya mpira wa pete ya Uganda hapo kesho tarehe 22 Agosti, 2018 katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha ENS jijini Bujumbura

Vilevile timu ya mchezo wa Karate ya Taifa nayo imeanza kushiriki mchezo huo katika hatua mbalimbali, ambapo hadi sasa mwenyeji wa tamasha hilo Burundi ndiye anayeongoza kushida kwenye vipengele vingi vya mchezo huo.

Tanzania katika Tamasha hili inashiriki katika michezo minne tofauti ambayo ni Riadha (mashindano bado hayajaanza), mpira wa miguu (kwa timu ya wanawake pekee), karate na mpira wa pete.Tamasha la kwanza la Michezo la Afrika Mashariki lilianza kufanyika tarehe 15 Agosti na litafikia tamati Agosti 30, 2018 nchini Burundi. 
Moja wa msambuliaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania akiwachambua mabeki wa timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Burundi. Katika mchezo huo Tanzania iliibuka na ushindi wa magoli 8 - 1 
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania ikicheza dhidi ya timu ya mpira wa miguu ya wanawake ya Burundi katika uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi. 
Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania ikishangilia ushindi pamoja mashabiki waliojitokeza kushuhudia shindano hilo 
Mmoja wa washiriki wa mchezo wa karate akionesha umahiri wake katika mchezo huo kwenye Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea jijini Bujumbura, Burundi 
Washiriki wa mchezo wa Karate kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa pambano 
Sehemu ya watazamaji wa mchezo karate wakifuatilia mchezo huo 
Timu ya mpira wa pete ya Tanzania ikiishambulia timu ya timu ya Burundi kwenye moja ya mchezo katika Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki. Katika pambano hilo Tanzania iliibuka na ushindi wa magoli 79 -14 dhidi ya Burundi 
Timu ya mpira wa pete ya Tanzania pamoja na mashabiki wa wakishangilia ushindi walioupata wamagoli 79-14 dhidi ya Burundi

SOMA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 22,2018


PUMA TANZANIA INAWATAKIA EID MUBARAK

LIVE: SWALA YA EID EL HAJI NA BARAZA LA EID KITAIFA VINGUNGUTI JIJINI DAR

WANANCHI WILAYA YA NYASA WASIFU UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI

$
0
0
*Wasema wanamatumaini makubwa dhidi yake,DC azungumzia ujenzi barabara Mbiga hadi Nyasa


Na David John,Nyasa

WANANCHI wa Wilaya mpya ya Nyasa wamesema hawaamini kama barabara kutoka Mbinga hadi Nyasa inajengwa tena kwa kiwango cha lami.

Wamedai kwamba barabara hiyo ilipimwa tangu mwaka ya 1974 lakini hadi sasa hakuna kilichokuwa kimefanyika.Wakizungumza jana wilayani hapa wamesema wanapongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli na kwamba mara zote imekuwa serikali ya vitendo ikisema inatenda.

Hivyo wanaona kama ndoto barabara hiyo inajengwa tena kwa kiwango cha lami.Wananchi hao wameeleza hayo baada ya mwandishi wa habari hizi kufika katika wilaya hiyo kwa lengo la kuona namna viongozi wamejipanga kwa ajili ya maendeleo, ambapo walisema hawaamini kwani wanaona kama ndoto.

Mwananchi Stephano Nchimbi alisema marais wengi wamepita lakini leo Rais John Magufuli anafanya kazi na wanamuomba Mungu aendelee kumbariki."Eti nasisi leo tunakwenda kuiona lami baada ya miaka lukuki,ndugu mwandishi mimi nakumbuka barabara ilipimwa tangu miaka ya 1974 tena mimi nikiwa bado kijana mdogo lakini Magufuli anafanya kwa vitendo leo Mungu ambariki,"alisema Nchimbi huku wezake wakimshangilia.

Pia Nchimbi ameomba Serikali ya wilaya hiyo kuwapa maelekezo Wakandarasi wanaojenga barabara hiyo kutoa kipaumbele kwa vijana wa kinyasa kupata ajira tofauti na ilivyo sasa ambapo walidai vijana wengi wanaofanya kazi wanatoka mbali."Kumekuwepo na ubaguzi kidogo katika kupata kazi hususani sisi vijana wakinyasa hivyo tunaomba wakandalasi kama anavyosisitiza Rais wetu Magufuli kutoa kipaumbele kwa wenyeji,"amesema Pius Mbawala

Naye Saulo Komba amesema kukamilika kwa barabara kutawezesha kuwepo mwingiliano mkubwa wa kibiashara ukizingatia bandari ipo hivyo wanapongeza juhudi za serikali.Mbali na hilo pia wamepongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya hiyo chini ya mkuu wa wilaya Esabela Chilumba kwamba anafanya kazi nzuri na wanashirikiana naye kwa karibu hususani kwajitihada zake katika upande wa elimu.

" Mheshimiwa Esabela tofauti na wakuu wa wilaya wengine tena huku kwetu kulivyokuwa mbali na haya mazingira yetu kila siku ingekuwa Dar es Salaam lakini yeye tupo naye, "amesema kilian Mbele.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Esabela Chilumba akizungumzia mradi huo wa barabara alisema umetengewa Sh.bilioni 129 na kampuni ya kichina ndio inajenga na kwamba vijana kutoka maeneo mbalimbali wanachangamkia fursa hiyo ya ajira.

Esabela amesema wao kama wilaya wanapambana kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa wananchi ukizingatia wilaya hiyo ni mpya na hakuna vyazo vya uhakika huku akipongeza Serikali kwa kuwa karibu nao."Kwanza nichukuwe fursa hii kwaniaba ya wananchi wa nyasa kumpa pole Rais kwa kuondokewa na dada yake na pia wananchi wa Nyasa wanampenda na hata siku akija nyasa atarajie mapokezi makubwa mno,"amesema Esbela

Amesema wananchi wanyasa hawaamini kama barabara yao kutoka Mbinga hadi Nyasa leo Serikali wanaijenga tena kwa kiwango cha lami ,wanaona kama ndoto .
DC Nyasa  Mh.Esabela Chilumba

WATANZANIA WASHAURIWA KUTHAMINI, KUHESHIMU TAARIFA ZA HALI YA HEWA

$
0
0
*Serikali yazindua rasmi Mfumo wa Taifa wa huduma za hali ya hewa

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SERIKALI imesema ipo haja kwa Watanzania wote nchini kuhakikisha wanajenga tabia ya kuheshimu na kuthamini taarifa za kitaaluma ambazo zinazotolewa nchini zikiwamo zinazohusu taarifa ya hali ya hewa.

Pia imesema taifa lolote linapanga mipango ya maendeleo ni lazima kuwepo na mfumo madhubuti wa kupata taarifa za hali ya hewa hasa kwa kuzingatia uwepo wa changamoto ya mbadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliyekuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa nchini wenye lengo la kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinafika kwa wakati na kufanyiwa kazi kikamilifu.

Uzinduzi huo umeshuhudiwa na wageni waalikwa kutoka taasisi na Wizara mbalimbali za Serikali ambapo pia Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani naye ameshuhudia tukio hilo baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Rwanda.

Akizungumzia mfumo huoMavunde amesema umekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwenye mchakato wa maendeleo ya watu na uchumi wa viwanda.Na hivyo kupata taarifa sahihi za hali ya hewa ni muhimu kwani hata unapopanga mipango ya maendeleo ni vema kujua na taarifa za hali ya hewa.

"Nchi yetu kwa sasa imejikita katika maendeleo ya watu na uchumi wa viwanda ,hivyo ni lazima kufuata taarifa ya hali ya hewa.Tuanze kujenga utamaduni wa kuheshimu na kuthamini taarifa za kitaaluma.

" Tunapoheshimu taarifa za hali ya hewa itatusaidia kuwa na tahadhari ya madhara ambayo yanaweza kusababishwa na mabadiliko ya tabia nchini.Tunafahamu mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kusababisha mafuriko, ukame na kuongezeka kwa kina cha bahari,"amesema Mavunde.

Amesema kupitia mfumo huo ambao umezinduliwa rasmi utasaidia kuwawezesha watu wote wakiwamo wadau wa hali ya hewa katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchini katika kuchukua hatua kwa kuzingatia taarifa ya hali ya hewa.

Ameelezea Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini inaendelea kutekeleza majukumu yake huku akisisitiza umuhimu wa mfumo huo ambao umezinduliwa.Pia Mavunde ameishukuru Serikali ya Norway kwa kuwa mfadhili katika kuhakikisha mfumo huo unaandaliwa na kukamilika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi amezungumzia umuhimu wa Mfumo huo huku akielezea ujio wa Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani.

Ambapo amesema ujio wake ni fursa kubwa kwani akiwa nchini atapata nafasi ya kutembelea na kushuhudia namna mamlaka ya hali ya hewa inavyofanya kazi zake.

"Pamoja na kushuhudia Mfumo huo ambao umezinduliwa pia atapa nafasi ya kutembelea ofisi zetu za Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini.Ratiba yake ilikuwa no nchini Rwanda lakini akataka kuja na nchini Tanzania," amesema.
Katibu Mkuu Shirika la Hali ya Hewa Duniani Prof.Petteri Taalas ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agnes Kijazi na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari.

SUA WAKABIDHIWA MAJENGO KWA AJILI YA KUANZA KAMPASI MPYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA MSIMU MPYA WA MASOMO 2018/2019

$
0
0
WANANCHI wa Kijiji cha Daraja mbili katika kata ya Namwinyu wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameahidi kutoa ardhi bure kwa ajili ya
matumizi ya Chuo cha kilimo (SUA) ikiwa ni kivutio kwa chuo hicho kuharakisha ukamilishaji wa shughuli zake.

Ahadi hiyo ilitolewa na wananchi hao katika hafla fupi ya makabidhiano ya majengo yaliyo kuwa kambi ya wakandarasi wa shauri wa kampuni iliyojenga barabara kwa Kiwango cha lami Kilimesera-Matemanga.

Wananchi hao wamefikia uamuzi huo kwa tamko hilo kwa pamoja katika mkutano huo wakiwa wanajibu kauli mbali mbali za viongozi.Ambapo walisema kuwa mbali na mkutano mkuu wa kijiji hicho wapo tayari kutoa zaidi ya hekari 500 kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho na kwamba wapo tayari kuongeza endapo kutakuwa na mahitaji zaidi.

Kauli hiyo ambayo pia ilisisitizwa na Diwani wa Kata hiyo Thabiti Said walisema kuwa ujio wa chuo hicho katika eneo la kijiji chao kutasaidia kupanua kujengeka kwa Kijiji, kuharakisha maendeleo pamoja na kuwasaidia kuelimisha ndugu, jamaa na watoto wao hali itakayo wafanya kuanza kulima kilimo cha kisasa.

Awali Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Raphael Chibunda amewaeleza wananchi hao kuwa katika utekelezaji huo, Chuo hicho ambacho endapo watakipokea kwa kupeleka wanafunzi wengi kila mwaka kitakua haraka na kuwa chuo kinacho jitegemea katika kipindi kifupi kijacho.

Prof. Chibunda amebainisha kuwa katika utelekezaji huo chuo kimejipanga kuanza Oktoba mwaka huu kwa kutoa mafunzo katika nyanja za utalii, teknolojia na kutunza kumbukumbu."Ila baadae kitajitanua na kuongeza kilimo utaalamu wa vipando, Ugani, lishe,Tiba za wanyama, uzalishaji

wa Lishe ya Wanyama, Ufugaji wa samaki, sayansi ya utunzaji wa mazingira, misitu na wanyama pori, kilimo biashara pamoja na mafunzo ya maendeleo ya vijiji," amesema.

Amesema katika kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinaanza haraka na kuleta tija kwa wananchi wa maeneo hayo Chuo hicho kimepanga kupeleka trekta moja kati ya marekta 10 waliyokabidhiwa na Rais Dk.John Magufuli hivi karibuni na kuanzisha mashamba darasa ambayo yatasaidia wananchi wengi kwenda kujifunza kwa vitendo.

Kwa upande was Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkwanda Sudi amesema kuwa katika utekelezaji huo kwa kuanzia wananchi hao wamekubaliana kutoa hekta tisa na majengo 11 ambayo yalitumika na wakandarasi washauri wakati wa ujenzi wa barabara ya lami.

Mbunge wa jimbo la Tunduru kusini Daimu Mpakate amesema kuwa ujio wa Chuo hicho ni ukombozi wa wananchi waishio mikoa ya pembezoni ikiwemo Wilaya ya Tunduru pamoja na wilaya zilizopo katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amewataka wananchi kujipanga kwa kupeleka watoto wao Shule na kuhakikisha wanafaulu vizuri ili chuo hicho kiweza kuwanufaisha wakazi wa Tunduru, Namtumbo na watanzania wote kwa ujumla.

Amesema kwa vile Chuo kipo Tunduru itapendeza endapo kutakuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaotoka ndani ya wilaya ya Tunduru na wengine maeneo ya jirani kama Namtumbo, Nanyumbu, Masasi na Tanzania kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera pichani kulia akipiga makofi kuashiria furaha ya makabidhiano ya majengo hayo ya chuo ndani ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera  (kushoto) akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA ,Profesa Raphael Chibunda .
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera pichani kati akisoma moja ya taarifa kabla ya makabidhiano ya majengo hayo ya chuo cha SUA ndani ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma

NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA

$
0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Josephat Kandege amefanya ziara  wilayani  Tunduru mkoani Ruvuma.

Katika ziara hiyo, aliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera ambae aliambatana na kamati yake ya Ulinzi na Usalama. Akiwa katika ziara hiyo Kadege alikagua vituo viwili vya Afya cha Matemanga na Mkasale.

Amesema  lengo la ziara hiyo ilikuwa kuona utekelezaji wa mradi unavyoendelea, upanuzi wa majengo ya upasuaji, nyumba ya mganga, maabara, wodi ya mama na mtoto, nyumba ya kuhifadhia maiti, jengo la mionzi na kichomea taka.

Akikagua ukarabati huo Kandege ametoa maagizo yakiwamo ya Serikali izungumze na wananchi wanaoishi jirani na  kituo cha Afya Matemanga ili kupisha upanuzi wa eneo la kituo cha Afya hadi kufikia ekari 8 kwa sasa ni ekari 4.

Pili, usimamizi uendelee kwa miradi ya afya inayoendelea hadi sasa Serikali imetoa Sh.milioni 500 katika kituo cha Afya Matemanga na Sh.milioni 400 katika kituo cha Afya Mkasale.Pia ameagiza wananchi wajitokeze kwa wingi kujiunga na huduma ya Afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa sasa waliojiunga Tunduru ni asilimia 43.5 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.

Amefafanua  huduma hiyi inapatikana kwa Sh.30,000 kwa mwaka  na inajumuisha Mama Baba na watoto wa nne.Pia kujenga majengo ya mionzi kwa kila kituo cha afya ili kurahisha upatikanaji wa huduma ya Mama mjamzito na matatizo mengine yanayofanana na hayo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkasale Mkuu wa wilaya ya Tunduru Homera awewahakikishia wananchi Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John  Magufuli itaendelea kuleta fedha za maendeleo kwa wakati.

"Na kwa sasa fedha za ujenzi wa vitanda kwa ajili ya bweni la wasichana wa shule ya sekondari namasakata imetengwa zaidi ya Sh. milioni sita na umeme wa jua utafungwa hivi karibuni na sh. million 19 zitapelekwa shule ya sekondari Muhuwesi kujenga madarasa mawili inayotarajia kuanza kidato cha kwanza mapema 2019 Januari.Hapa kazi tu," amesema.
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akimkaribisha Naibu Waziri Ofis ya Rais Tamisemi,Mh. Josephati kandenge kazungumza na Wananchi wa kijiji cha Kasale kata ya Namasakata wilayani Tunduru,baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya Mkasale kinachojengwa na serikali ya awamu ya tano ya CCM kwa shilingini Millioni 400.
Naibu waziri Tamisemi Mh  Josephat Kandege (wa tatu kulia) akiwa ameambatana Mkuu wa Wiaya ya Tunduru Mh.Juma Homera na viongozi wengine mbalimbali wakati wa ukaguzi wa kituo cha afya Mkasale ,Matemanga wilayani Tunduru na 
Taarifa ya Ukaguzi wa nyumba ya mganga,maabara,mochwari,jengo la upasuaji la akina mama,wodi ya akina mama,kichoma taka, nk
Naibu Waziri Tamisemi Mhe Josephat kandege akitoa maelekezo kwa DC Homera

Ubalozi wa Uholanzi, NEEC wazindua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana

$
0
0

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi, Beng’i Issa wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul wapili kulia wakati wa uzinduzi wa program ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini na wengine ni wakurugenzi na maofisa kutoka taasisi hizo. (Picha na Mpiga picha Wetu, Dar es Salaam).
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi, Beng’i Issa wa pili kulia akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini, wa pili kushoto ni Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul,kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Baraza hilo, Suleiman Malela na kushoto ni Ofisa wa Ubalozi huo, Bw. Ulrich Juhudi. 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
BARAZA la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi nchini wamezindua program ya mafunzo ya ujasiriamali na malezi ya biashara kwa vijana waliohitimu elimu ya juu katika juhudi za serikali kupambana na tatizo la ajira na kuchochea uchumi wa viwanda.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi, Beng’I Issa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yanawalenga  vijana 50 wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini kuanzia sasa hadi miaka mitano iliyopita ambao wana nia ya kuanzisha, kupanua na kuboresha biashara zao.

“Ni mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanaotaka kujiunga wanahitajika kuandaa michanganuo ya mawazo ya biashara katika maeneo ya utalii, kilimo, nishati mbadala na mazingira,”,  fomu za kujiunga zinapatikana katika tovuti ya baraza ya www.uwezeshaji.go.tz au zinapatikana katika ofisi za baraza hilo aliongeza kusema, Bi. Issa.

Alisema kwamba mafunzo hayo ni ya wiki moja ambapo vijana hao watapata fursa ya kujifunza mambo ya ujasiriamali na kuingia kwenye biashara pamoja na mambo mengine watapata nafasi ya kuandika michanganuo yao itakayo shindanishwa ambapo washindi watatu watapatiwa zawadi.

“Vijana watakao chaguliwa katika program hiyo watapewa mafunzo ya siku nne juu ya mipango ya biashara kabla ya kuendelea na mchujo wa kutafuta washindi watatu ambao watapewa mbegu mtaji,” mshindi wa kwanza atapata milioni 10, wa pili milioni saba na mshindi wa tatu atapata milioni tano na washiriki wengine watanufaika na ushauri wa kitaalamu, alisema, Bi. Issa.

Bi Issa alifafanua kwamba mafunzo hayo yanalenga maeneo manne ambayo ni utalii, Kilimo, Nishati mbadala na mazingira ambayo ni maeneo yenye kuleta matokeo chanya kwa haraka katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na kupambana na tatizo la ajira nchini.

Alisisitiza kwamba mafunzo hayo yanawalenga wahitimu hao wa fani mbalimbali ambao wakiingia kwenye biashara watafanya vizuri na kuanzisha makampuni yatakayopata maendeleo makubwa na kuweza kujiajiri na kuajiri wenzao.

Bi Issa alisema kwamba hii ni programu ya majaribio kwa kushirikiana na Serikali ya ya Uholanzi kupitia program hiyo na na baada ya mafanikio itapanuliwa zaidi. 

“Pamoja na program hii kuwa ya majaribio, sisi kama baraza tumekuwa tukiendesha mafunzo kama haya tangu 2013 kwa kushirikiana na taasisi zingine” kwa sasa ni mwendelezo wa program hiyo.

Kwa upande wake, Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul alisema kwamba mafunzo hayo ni muhimu kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu kama moja ya njia madhubuti ya kuhamasisha ujasiriamali katika kupambana na tatizo la ajira hapa Tanzania.

“ Serikali ya Uholanzi inayo furaha kushirikiana na baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kuhamasisha ujasiriamali kwa sababu kuna wigo mpana na fursa za biashara na kujiajiri,” alisema

Balozi huyo aliongeza kwamba kila mwaka kuna idadi kubwa ya vijana ambao wanaingia kwenye soko la ajira lakini hawana ujuzi na uzoefu wa kutosha kuweza kumudu changamoto hizo za mahitaji ya soko hilo, kwahiyo mafunzo hayo ni muhimu kwao kuweza kuajiri kupitia ujasiriamali.

Alieleza kwamba hapa nchini kuna wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali ambayo yanahitaji vijana wenye ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira na biashara za uwekezaji.

Balozi Verheul alisema kwamba serikali ya Uholanzi inaona program hiyo inamaana kubwa na matarajio yake ni kwamba makampuni mengi kutoka Uholanzi wataweza kusaidia programu hiyo.


WAZIRI MKUU ATUMIA USAFIRI WA BOENG 787-8 DREAM LINER YA. ATCL KUTOKA MWANZA HADI DAR

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisafiri kwa Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner wakitoka Mwanza kwenda Dar es salaam kupitia KIA, Agosti 22, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Phillip Mangula (watatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla kuondoka kuelekea Dar es salaam kwa ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner Agosti 22, 2018.
Ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ikiwa Juu Ziwa Viktoria Mwanza ikijiandaa kutua katika uwanja wa Mwanza leo 22/Agosti /2018 .Picha na Chriss Mfinanga wa Ofisi ya Waziri Mkuu

JESHI LA POLISI PWANI LIMEKAMATA PULI NA MBEGU ZA BANGI HUKO KISARAWE-RPC SHANNA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KISARAWE .

JESHI la polisi mkoani Pwani, linamsaka dereva aliyefahamika kwa jina la Moshi Ramadhan Malinganya mkazi wa Kisarawe kwa tuhuma za kusafirisha bangi puli 193,katika gari alilokuwa akiliendesha .

Pamoja na hilo ,kwenye buti ya gari hilo kumekutwa na ndoo ndogo mbili za lita kumi zenye bangi na kiroba kidogo chenye mbegu za bangi kilo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kisarawe, kamanda wa polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna ambae anasubiri makabidhiano kuhamia Mwanza kikazi,alisema mtuhumiwa ametoroka baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka wakati akiwakimbia polisi.

Alieleza , tukio hilo lilitokea agosti 21 majira ya usiku eneo la shule ya sekondari Minaki akiwa anaendesha gari namba T 801 AAF aina ya Toyota Mark II.
kamanda wa polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna akionesha namba za Gari kwa Wanahabari (hawapo pichani)

“Tulipata taarifa toka kwa wasamaria wema juu ya gari hilo kusafirisha bangi kutoka kijiji cha Gwata kwenda Mombasa Jijini Dar es Salaam tuliweka mtego eneo la mnara wa TBC lakini tulipomsimamisha hakusimama”, alisema Shanna.Shanna alisema ,polisi walimkimbiza lakini walikuta gari hilo limepinduka huku dereva huyo akiwa amelitelekeza .” Vitu vingine vilivyokutwa katika gari hilo ni namba za magari mbili ikiwemo namba T 321 AJH na TZH 7255 jambo linaloashiria kuwa mtuhumiwa alikuwa akibadilisha namba hizo wakati wa matukio ya biashara haramu ya dawa za kulevya,”alisema Shanna.

Hata hivyo, alielezea wanamshikilia mmiliki wa gari hiyo (Majaliwa Salehe) kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusu gari lake kukutwa na madawa hayo.Kwa mujibu wa kamanda huyo ,wataiomba mahakama kutaifisha gari hilo kwa mujibu wa sheria ili kuwakomesha watu wanaojihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya

MRADI WA UMWAGILIAJI MWASUBUYA KUWA MRADI WA MFANO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mratibu wa Matawi ya Kampuni ya Agricom Africa inayohusika na uuzaji wa zana bora za kisasa za kilimo, Bw. Zuberi Lujina akiztoa maelezo ya namna kampuni yake inavyofanya kazi, katika Kikao cha Tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi.



Na Stella Kalinga, Simiyu


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuutumia Mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya kubadilisha maisha ya wananchi wilayani Bariadi, kupitia kilimo cha kisasa kinachotumia zana za kisasa na kuufanya kuwa mradi wa mfano ambao watu wataenda kujifunza.

Mtaka ameyasema hayo katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 yaliyofanyika Kitaifa mkoani Simiyu na kuwashukuru viongozi wa Chama na Serikali, Watendaji, Watumishi, wafanyabiashara na wadau wengine waliofanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.

Amesema mradi huo wenye ekari 514 zitakazolimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia maji ya Bwawa la Mwasubuya lililoigharimu Serikali shilingi bilioni 1.24, utahusisha kilimo cha kisasa chenye kutumia zana za kisasa katika hatua zote kuanzia kuandaa shamba, kupanda, palizi na kuvuna badala ya kuhusisha zana za kilimo za mikono.

“ Nimewaambia watu wa Bariadi tunahitaji Kijiji kimoja ambacho tutabadilisha maisha ya wananchi na watu wataenda kujifunza na kuangalia transformation(mabadiliko) ya kile kijiji, lakini pia tunahitaji lile shamba lote la ekari 514 lilimwe pasipo kutumia mikono ya wanadamu kuanzia hatua za kuandaa shamba, kupanda, palizi hadi kuvuna” alisema

Ameongeza kuwa dhamira ya Mkoa ni kuona wananchi wanalima kisasa kwa kutumia zana bora za kilimo ambazo baada ya mazungumzo na Kampuni ya Agricom Africa imekubali kuikopesha Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi zana zote muhimu ili kuwawezesha wakulima katika mradi wa Mwasubuya kuongeza tija katika uzalishaji.

Aidha, Mtaka amesema Bwawa la Mwasubuya lililopo katika Mradi huu wa Umwagiliaji wa Mwasubuya wilayani Bariadi litawekewa vifaranga vya samaki vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi.

“Huu ni mradi ambao tungehitaji watu wote ndani ya mkoa waende wakaangalie transformation(mabadiliko) ya kile kijiji, lile bwawa tutaliwekea vifaranga vya samaki vya zaidi ya shilingi milioni kumi na tutalifunga mpaka mwezi Agosti 2019, uongozi utakaokuja mwakani kwenye Nanenane moja ya eneo watakalotembelea ni bwawa la Mwasubuya na tutafanya shughuli ya uvuaji wa hao samaki” alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Watumishi na wananchi wa Bariadi watahamasishwa kwenda kutengeneza vizimba katika Bwawa hilo, lengo likiwa ni kutafsiri namna maji yanavyoweza kuinufaisha jamii kwa namna nyingine zaidi ya kilimo cha Umwagiliaji.

Kwa upande wake Mratibu wa Matawi ya Agricom Africa hapa nchini Bw. Zuberi Lujina amesema kampuni hiyo iko tayari kufanya kazi na mkoa wa Simiyu katika kuhakikisha wakulima wanaondokana na kilimo cha mazoea kwenda kwenye kilimo chenye tija na kilimo biashara wakitumia zana bora za kilimo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi amesema wameshazungumza na Viongozi wa Kampuni ya Agricom Africa ambapo wameahidi kufikisha vifaa na zana hizo katika Halamshauri ya Wilaya ya Bariadi katika juma la tarehe 20 hadi 27 mwezi huu

TANZANIA NA UGANDA ZA AZIMIA KUKUZA BIASHARA KATI YAO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Ushirika wa Uganda, Balozi Julius Onen akisoma hotuba ya ufunguzi katika Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kampala siku ya Jumatano tarehe 22 Agosti 2018. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akichangia mada katika mkutano huo ambapo alisema kuwa Mamlaka ya Bandari imeboresha kwa kiasi kikubwa huduma zake 
Mkurugenzi wa Shirika la kukuza Biashara katika nchi za Afrika Mashariki kwa upande wa Uganda (Trademark East Africa), Bibi Dawali Ssali akieleza mikakati ya inayofanywa na shirika hilo katika kuboresha mazingira ya biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. mikakati hiyo ni pamoja na kushirikiana na nchi za EAC kujenga vituo vya kutoa huduma kwa pamoja mipakani. 
Wajumbe wa Uganda na Tanzania wakijadili mikakati ya kukuza na kuimarisha biashara kati ya nchi zao.



Tanzania na Uganda za azimia kukuza biashara kati yao

Tanzania na Uganda zimeazimia kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kukuza kiwango cha biashara kati yao ambacho kwa takwimu zilizopo sasa zinaonesha kipo chini mno.

Hayo yalibainishwa katika mkutano wa Jukwaa la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika leo kando ya Mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) unaofanyika kwa silku tatu jijini Kampala tokea tarehe 21 Agosti 2018.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Ushirikia ya Uganda, Balozi Julius Onen alieleza kuwa Tanzania na Uganda zina nafasi kubwa ya kukuza biashara endapo njia za usafiri zitaboreshwa, vikwazo visivyo vya kibiashara vitaondolewa pamoja na kuwa na mikakati ya pamoja ya kuweka viwango vya ubora vinavyotambulika katika nchi zote na kanda nzima kwa ujumla.

Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wawakilishi mbalimbali wa Tanzania akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko alisema kuwa Mamlaka ya Bandari imeboresha kwa kiasi kikubwa huduma zake ikiwemo kuanza upya kwa njia ya Dar Es Salaam- Mwanza hadi bandari ya Bell nchini Uganda. Alisema kufunguliwa kwa njia hiyo kumepunguza idadi ya siku za kusafirisha mizigo kutoka Dar Es Salaam hadi Uganda ambapo kwa sasa mizigo inasafirshwa kwa siku nne  na kwa kiwango kikubwa na gharama nafuu.

Jambo hilo liliungwa mkono na wafanyabiashara wa Uganda walioshiriki mkutano huo ambapo waliipongeza TPA kutokana na hatua inazozichukua kuboresha huduma katika Bandari ya Dar Es Salaam na walikiri kuwa kufunguliwa kwa njia ya Dar Es Salaam-Mwanza hadi Bandari ya Bell kumepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kufanya biashara pamoja na muda wa kusafirisha bidhaa zao.

Balozi Onen aliendelea kueleza kuwa licha ya changamoto zilizopo za kufanya biashara kati ya Uganda na Tanzania lakini vihatarishi vya kufanya biashara na Tanzania ni vichache ukilinganisha na nchi nyingine.  Hivyo, aliwsihi wafanyabiashara wa Uganda na Serikali kwa ujumla kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na nchi hiyo.

Alibainisha kuwa Tanzania na Uganda zinaweza kufaidika zaidi kibiashara kutokana na nchi zote kuwa kwenye eneo la Maziwa Makuu ambalo lina soko kubwa kutokana na idadi kubwa ya watu katika eneo hilo. Hivyo alizihimiza Serikali zaTanzania na Uganda kufanya uwekezaji mkubwa katika ushoroba wa kati (central corridor) ili kukuza biashara.

Mkutano wa JPC unatarajiwa kufungwa rasmi Alhamisi kwa kikao cha ngazi ya Mawaziri ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (Mb), Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi. Isack Kamwele (Mb) na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (Mb) watashiriki mkutano huo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kampala
22 Agosti 2018

Wananchi Waridhia Bwawa La Urughu kutangazwa kama Eneo Lindwa-kimazingira

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula mara baada ya kuwasili Wilayani hapo kwa ziara ya kikazi. Waziri Makamba ametembelea bwawa la Urughu na Ziwa Kitangiri ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa kuwa maeneo lindwa kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi waishio pembezoni mwa ziwa Kitangiri Wilayani Igunga. Waziri Makamba amewaasa wakazi hao kuwa chachu katika kuhifadhi mazingira ya ziwa hilo kwa manufaa ya sasa na baadae.
Wakazi wa mwalo wa Shauri-Tanga katika Ziwa Kitangiri Wilayani Iramba, wakizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba juu ya namna wanavyotumia ziwa hilo kwa shughuli za uvuvi.

Bwawa la Urughu lilipo Wilayani Singida liko hatarini kutoweka kutokana na matumizi yasiyoendelevu ya shughuli za kibinadamu yanayopelekea kujaa mchanga na kupungua kwa kina cha maji. Waziri Makamba ameazimia kutangaza bwawa hilo kama eneo lindwa kimazingira ili kuweka ulinzi na matumizi endelevu.


…………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameendelea na ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Iramba kwa kutembelea bwawa la Urughu na kuwataka wakazi wa eneo hilo kusimamia rasilimali hiyo kwa mustakabali wa maisha yao ili kuendeleza fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na masuala ya uvuvi na kilimo.

Mhe. Makamba amesema ili bwawa hilo liweze kutangazwa kama eneo lindwa ki-mazingira ni lazima wananchi wawe na utashi, utayari na uwezo wa kutunza bwawa hilo kwa kufuata masharti yatakayotolewa katika tangazo la Serikali ikiwa ni miongoni mwa maeneo 77 yaliyopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.

Waziri Makamba amesema uhifadhi wa bwawa hilo utaendana na makatazo kwa baadhi ya shughuli za kibinadamu ili kulinusuru ikiwa ni pamoja na kuzuia shughuli za uvuvi na kilimo kisicho endelevu katika Vyanzo vya maji. Aidha, Waziri Makamba ameutaka Uongozi wa Wilaya ya Singida kupitisha azimio lao la kuhifadhi bwawa la Urughu na Msitu wa Ushora katika Baraza la Madiwani.

Waziri Makamba ameahidi bila kuchelewa kutangazwa Bwawa la Urughu kuwa eneo nyeti kimazingira na kusaidia kuondoa kadhia ya kujaa kwa mchanga katika bwawa hilo. “Ili sisi tuendelee na mchakato huo tuleteeni sifa za maeneo husika kama vile, milima, mabwawa na mashamba yenye umuhimu mkubwa na historia inayojenga hoja ya umuhimu wa ulinzi katika eneo hilo, pia lipatikane azimio la Baraza la Madiwani kuwa ni eneo nyeti na kuwasilisha ombi ili Waziri aweze kuchukua nafasi yake kisheria” Makamba alibainisha.

Pia, Mhe. Makamba ametembelea Ziwa Kitangiri lililopo katika Kijiji cha Doromoni, Kata ya Tulya, Tarafa ya Kisiriri na kufanya mkutano wa hadhara na wakazi wa eneo hilo ambao wamepaza sauti juu ya changamoto inayowakabili ya kuhifadhi ziwa Kitangiri.

Diwani wa Kata ya Tulya Bw. Wilfred Kizanga amebainisha kuwa ziwa hilo linapakana na Wilaya za Meatu, Igunga na Kishapu ambazo amezituhumu kufanya shughuli zisizo endelevu katika ziwa hilo na kusabisha kina cha maji kupungua na kuendeleza uvuvi haramu. “Sisi wana – Doromoni kwa upande wetu tunahifadhi hili ziwa, tatizo ni wenzetu wa Wilaya tunazopakana nazo, shughuli zao za kibinadamu si endelevu” alifafanua Mhe. Diwani.

Akijumuisha ziara yake katika Wilaya ya Iramba Mhe. Makamba ameagiza Uongozi wa Wilaya kuuanda Kamati za Mazingira na kuahidi kutoa mafunzo kwa kamati zitakazoundwa ili kurahisisha shughuli za uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira wilayani hapo “Natarajia hadi mwezi Desemba kamati ziwe zimeundwa katika ngazi zote na ziwe mfano, Waziri Makamba alisisitiza”

Katika hatua nyingine Waziri Makamba ameahidi kutafuta mradi kwa ajili ya kuhifadhi Ziwa Kitangiri na kidakio cha maji ili kurejesha ziwa hilo katika hali yake ya awali. Mradi huo pia utasaidia kutoa mbadala wa shughuli zisizo endelevu pembezoni mwa ziwa na vyanzo vya maji vinavyopeleka maji katika ziwa hilo ili kurahisisha mchakato wa hifadhi ya ikolojia ya Mto Kitangiri.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images