Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua vifungu vya Sheria ya Mazingira mbele ya Watendaji na Viongozi wa Mkoa wa Singida juu ya maeneo lindwa. Wengine katika picha ni viongozi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijionea uharibifu wa mazingira katika Ziwa Singidani ambao unatokana na shughuli za kibinadamu. Waziri Makamba ameazimia kunusuru Ziwa hilo pamoja na vyanzo vyake. Wengine katika picha ni viongozi kutoka Manispaa ya Singida.
Ziwa Singidani ambalo liko hatarini kutoweka kutokana na shughuli zisizo endelevu za kibinadamu. Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi ya kukagua na kuona namna bora ya kunusuru Ziwa hilo pamoja na mengine kwa mustakabali wa nchi yetu.


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
January Makamba amesema Ofisi yake inaangalia uwezekano wa kutangaza
Ziwa Singidani na Ziwa Kindai katika Halmashauri ya Singida kama maeneo
lindwa kimazingira kwa kuwa yako hatarini kutoweka.

Waziri Makamba ameyasema hayo hii leo Mkoani Singida ikiwa ni siku ya
kwanza ya ziara yake katika Mikoa 9 hapa nchini yenye lengo kukagua,
kutathmini na kuzungumza na viongozi, wataalam, watendaji na wananchi
kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya
Mazingira kifungu namba 51.

Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa mara baada ya kutoa tangazo hilo
katika gazeti la Serikali matumizi sahihi ya maziwa hayo yataainishwa ikiwa nipamoja na kupanda miti rafiki kuzunguka maeneo yote na kuzingatia makatazo yatakayotolewa.

“Ziwa Singidani liko hatarini kutoweka kutona na shughuli za kibinadamu,
hivyo kwa kutumia Sheria ya Mazingira nitashauriana na wataalamu wangu
kuona namna bora ya kunusuru maziwa haya ikiwa ni pamoja na
kuyatangaza kwenye gazeti la Serikali kama maeneo lindwa kimazingira.”
Makamba alisisitiza.

Imebainika kuwa, lengo la kuainisha na kutangaza maeneo hayo ni kulinda
mifumo muhimu ya kiikolojia (ikiwemo vyanzo vya maji, mito, maziwa,
mabwawa, milima na vilima, chemichemi, ardhi oevu, mazalia ya samaki na
misitu) ambayo hayana ulinzi wa Sheria nyingine.

Waziri Makamba pia ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida kwa utayari na uwezo wao katika kusimamia uhifadhi mara maeneo hayo
yatakapotangazwa na kuwataka kuwasiliana na Ofisi yake ili waweze
kupatiwa rasimu ya Sheria ndogo ndogo watakazozitumia katika Halmashauri zao ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira katika ngazi zote.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema Mkoa wake
uko tayari kuingia makubaliano na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yenye lengo la kuhuisha Sheria ndogo ndogo
zitakazosaidia hifadhi ya Mazingira mkoani kwake pamoja na kuundwa kwa
Kamati za Mazingira katika ngazi zote.

Jumla ya maeneo 77 yamependekezwa kutoka Mikoa mbalimbali kwa
kuzingatia vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria na katika awamu ya
kwanza, maeneo takriban 20 yanatarajiwa kuhifadhiwa kwa kutumia Sheria ya Mazingira.

CASTLE LITE YANOGESHA TAMASHA LA MUZIKI LA STR8UP JIJINI DAR

$
0
0
Wakazi wa vitongoji mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki wakipata burudani moto moto ya muziki katika tamasha la muziki lililoandaliwa na kampuni ya masuala ya burudani ya STR8UP na kufanyika katika ukumbi wa Velisas-Kawe, chini ya udhamini wa bia ya Castle Lite.
Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, (katikati) akiwa na Mtalaamu wa Ubunifu nchini Ally Remtulla (kulia) wakati wa tamasha la la Muziki la STR8UP, lililofanyika katika ukumbi wa Velisas Kawe, wakipata burudani kwa udhamini wa bia ya Castle Lite .
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, waliohudhuria katika tamashala la Muziki la STR8UP, lililofanyika katika ukumbi wa Velisas Kawe wakipata burudani kwa sambamba na kinywaji cha Castle Lite.
DJ akionyesha umahiri wake wakati wa tamasha la Muziki la STR8UP, lililofanyika katika ukumbi wa Velisas Kawe jijini Dar es Salaam, kwa udhamini wa bia ya Castle Lite.
Mtaalamu wa kupiga drum, Haidery Vagu, akionyesha umahiri wake katika tamasha hilo.

POLISI KILIMANJARO YANASA KILOGRAMU 520 ZA MIRUNGI

$
0
0
Mtuhumiwa wa usafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi akiwa kwenye gari la Polisi ba Viroba vilivyojaa Dawa hizo zilizokamatwa katika moja Bonde mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Asakari Polisi wakishusha viroba vyenye Dawa za Kulevya aina ya Mirungi.
Mtuhumiwa wa usafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi,Samwel Muro mkazi wa Kitobo nchini Kenya akiwa chini yaulinzi na pemebeni ake ni Vifurushi vya Mirungu alivyokutwa navyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akitoa maelekezo kwa askari wake mara baada ya kukamatwa kwa Dawa za kulevya aina ya Mirungi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akiumuuliza jambo raia wa Kenya ,Samwel Muro aliyekutwa akiwa amebeba moja ya vifurushi kwa ajili ya kusafirihwa kutoka mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akionesha moja ya kifurushi cha Dawa za kulevya aina ya Mirungi kilichopewa jina la mji wa Kibaha.

Na Dixon Busagaga  wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limefanikiwa kukamata viroba saba vya Dawa za kulevya aina ya Mirungi sawa na kilogramu 520 zikiwa zimebebwa na watembea kwa miguu ambao walikuwa wakivusa kutoka nchi jirani ya Kenya kuingia Tanzania.

Mbali na viroba hivyo ,Polisi pia inamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la ,Samwel Muro(21) raia wa Kenya mkazi wa Kitobo baada ya kukutwa akiwa amebeba kichwani moja ya Viroba hivyo huku wakifanikiwa kuwakimbia askari baada ya kutupa mizigo ya dawa hizo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna  Msaidizi wa Polisi,Hamis Issah alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo  jana majira ya 8:30 mchana pamoja na pikipiki moja iana ya Haojue yenye namaba za usajili MC 909 BUZ  ambayo inatajwa kuhusika katika usafirishaji wa mizigo hiyo.

“Hii mirungi ilikamatwa kijiji kinaitwa Mnoa ,kiko kata ya Kileo wilayani Mwanga ,askari Polisi wakiwa Doria walikamata viroba saba vya mirungi ,asakri walienda kwenye bonde moja na kukuta watu wametoka Kenya ,wamejiza hii mirungi kwenye magunia wanaficha kwenye hilo bonde ,kumbe wana utaratibu wao bonde likijaa wanachukua pikipiki zaidi ya 30 kwa ajili ya kusafirisha na wanasafiri kwa makundi makubwa ya pikipiki”alisema Issah.

Kamanda Issah alisema baadhi ya Vifurushi hivyo vya Mirungi vimekutwa vikiwa vimeandikwa majina ya vijiji kuanzia njia Panda ya Himo kuelekea Dar es Salama yakiwemo maeneo ya Segera ,Chalinze hadi Kibaha.

NAIBU WAZIRI ULEGA AKUTANA NA WATENDAJI WA MRADI SWIOFISH.

$
0
0
Mh. Abdalla Ulega (Mb), Naibu Waziri  wa Mifugo na Uvuvi amefuatana na Dkt. Rashid Tamatama Katibu Mkuu Uvuvi kuongea na watumishi kuhusu upande wa Mradi wa SWIOFish katika ukumbi wa Mvuvi House - DSM. 

Mh Naibu Waziri baada ya kupata maelezo kuhusu Mradi huo,  alitoa changamoto kwa watendaji kwa kuwaeleza kuwa elimu inayotolewa kwa jamii za wavuvi iweze kuleta matokeo chanya hata pale mradi utakapo maliza muda wake na kuwepo na matokeo ambayo yataweza kupimika hata kwa macho. Hii itasaidia sana kuweza kuzisaidia jamii zetu ambazo Mara nyingi miradi ikiishà na wao hali zao zinaendelea kuwa duni badala ya kuwa zimeboreshwa.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo leo jijini Dar as Salaam.

KATIBU MKUU WA CCM AKIAGANA NA VIONGOZI WA CCM BAADA YA KUKAMILISHA ZIARA YAKE PEMBA

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk. Bashiru Ally akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kujitambulisha kwa Wana-CCM Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk. Bashiru Ally akiagana na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Bakari Hamad Khamis mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kujitambulisha kwa Wana-CCM Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk. Bashiru Ally akiagana na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Uchumi na Fedha Zanzibar Ndugu Afadhali Taib Afadhali (kushoto) mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kujitambulisha kwa Wana-CCM Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk. Bashiru Ally akiwa katika ndege ya Kampuni ya Assalam Air akiwapungia mkono wana CCM na viongozi wa CCM walioshiriki kumuaga katika uwanja wa ndege Pemba.

Mwakyembe amaliza mgogoro wa ardhi Mwenge Vinyago uliodumu kwa miaka 33

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge jijini Dar es salaam. Katikati ni  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza na kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale.
 Baadhi ya wasanii wa sanaa za uchongaji wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza. Picha na MAELEZO

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI MEJA JENERALI JACOB KINGU ATEMBELEA NIDA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu amefanya ziara kwenye kituo Kikuu cha Uchakataji, Uzalishaji na Utunzaji wa Taarifa (Data Centre) kilichoko Kibaha mkoani Pwani na kukagua shughuli za uchakataji wa taarifa na uzalishaji wa Vitambulisho.

Pia amefanya mazungumzo na Menejimenti ya NIDA na kusisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya Uzalishaji kwa kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa mitambo ya kisasa haraka ili kuongeza nguvu ya Uzalishaji kufuatia asilimia kubwa ya wananchi kukamilisha hatua ya awali ya Usajili na uchukuaji alama za kibaiolojia.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Mkurugenzi wa Uzalishaji Ndg. Alphonce Malibiche ameeleza mpaka sasa Mamlaka imefikia hatua nzuri katika Usajili na uzalishaji wa Namba za Utambulisho na kazi kubwa iliyopo sasa ni ya uzalishaji ambao umekuwa ukienda taratibu kutokana na uwezo mdogo wa  mashine zilizopo kushindwa kuzalisha kadi nyingi kwa mara moja.

Hata hivyo amesema tayari Mamlaka ilishachukua hatua za kuagiza mashine mpya na za kisasa kusaidia kuongeza kasi ya Uzalishaji na tayari mchakato wa kumpata mzabuni umefikia hatua nzuri na pindi taratibu zitakapokamilika mashine hizo zitafungwa mara moja.

Meja Jenerali Kingu amepongeza jitihada kubwa na nzuri zinazofanywa na Mamlaka na kusisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa uzalendo na uadilifu mkubwa huku akiielekeza Menejimenti kuangalia namna bora ya kulinda na kuongeza maslahi ya watumishi wake; ili kuongeza morali na ufanisi katika utendaji.

Mamlaka inaendelea na zoezi la kuwasajili wananchi nchi nzima na mpaka sasa imeshasajili zaidi ya wananchi mil 19.2 nchi nzima; na hadi kufikia mwezi Desemba 2018 imelenga kuwa imesajiliwa zaidi ya watanzania mil 22.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu  (kushoto mwenye Kaunda suti nyeupe) akisikiliza maelezo ya jinsi uchakataji wa taarifa unavyofanywa na maafisa wa NIDA alipotembelea kituo cha Uchakataji wa taarifa. Kulia ni Ndg. Alphonce Malibiche (mwenye tai nyekundu) Mkurugenzi wa Uzalishaji akitoa maelezo; na waliomzunguka ni baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya NIDA.

 Watumishi katika kitengo cha Uchakataji wa taarifa wakiendelea na hatua za uhakiki wa taarifa wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu akikagua kazi inayofanywa na watumishi katika kituo cha Uchakataji wa Taarifa
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu akibadilishana mawazo na Mkandarasi wa Ujenzi wa kituo cha Uchakataji wa Taarifa Kibaha Mr. Kim(Mwenye tai ya bluu), akiwa amezungukwa na wakurugenzi na wakuu wa Vitengo wa Mamlaka.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu katika picha ya pamoja na viongozi wa Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inayoundwa na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Meneja.

NHIF YAPATA CHETI CHA UBORA WA VIWANGO VYA KIMATAIFA "ISO 9001:2015"

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akipokea Cheti cha Mfumo wa Uhakiki bora wa kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) kutoka kwa Muwakilishi wa  Taasisi ya BSI (British Standards Institute), Mini Sharma (kushoto) iliyotolewa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Wanaoshuhudia ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko huo, Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akikabidhi Cheti cha Mfumo wa Uhakiki bora wa kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda kilichotolewa na Taasisi ya BSI (British Standards Institute) kwa Mfuko huo leo Agosti 20, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda (katikati) naye alikabidhi cheti hicho kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akionyesha cheti hicho kwa wageni mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya kupokea Cheti cha Mfumo wa Uhakiki bora wa kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) kilichotolewa na Taasisi ya BSI (British Standards Institute)  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), leo Agosti 20, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda akifurahi jambo wakati akizungumza katika hafla hiyo.


MIGOGORO ya wazazi katika familia, imetajwa kuwa ni moja ya sababu kubwa inayoathiri elimu

$
0
0
Na Emauel Madafa , Michuzi Blog , MBEYA.

MIGOGORO ya wazazi katika familia, imetajwa kuwa ni moja ya sababu kubwa inayoathiri elimu na malezi bora ya watoto.

Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Afisa Utawala Shule za St.Mary's Mkoa wa Mbeya, Anuciata Ngonyani kwenye mahafali ya wanafunzi 63 wa darasa la saba.

Amefafanua kuwa uongozi wa shule hiyo umekuwa ukipokea kesi nyingi za namna hiyo, hivyo kuwaomba wazazi wakiume kutambua wajibu wao kwa watoto ikiwa na kuwatendea haki kwa kutimiza haki zao za msingi ikiwemo elimu.Aidha, amewataka wazazi kujenga mshikamano, umoja, amani na upendo kwenye familia ili watoto waweze kuiga mambo yaliyomema na kukua katika maadili.

Amesema kuna watoto wengi wameacha masomo na wengine kuhamishwa shule kutokana na jukumu la kusomesha mtoto kuachiwa mama pekee jambo hali ambayo imekuwa ikimnyima haki mtoto. Kwa upande wake Meneja wa bima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Consolatha Gabone amesema moja ya changamoto zinazo poteza ndoto za watoto ni mifarakano ndani ya familia hasa pale wazazi wanapo tengana au kufariki.

Amesema kutokana hali hiyo wameamua kuanzisha huduma ya bima ya maisha ambayo inatoa fursa kwa wategemezi kutimiza ndoto zao bila kuathiri mfumo wa maisha licha ya kuondokewa na wazazi.Gabone amesema kuwa imekuwa ni jambo la kawaida kwa wazazi kuwa na bima za magari na mali nyingine na kusahau bima za maisha ikiwemo elimu ambayo ni njia ya kumwezesha mwanafunzi kufikia ndoto zake kabla ya kuanza kujitegemea.

Amesema ili kuweza kuonyesha upendo kwa watoto ni vema wakafungua bima ya elimu ili kuweza kutimiza malengo ya watoto. Wengi wamesau kwa habari ya maisha yao wenyewe unajua mzazi anapo kuwa amekata bima ya maisha ni kuonyesha upendo kwa familia lakini kuna wakati unaweza kupata madhara hivyo ukashindwa kusomesha lakini ukakata bima hasa ya elimu watoto wataendelea na masomo hivyo niwashuri wazazi kukata bima ili kuwezesha kutimza malengo ya watoto wao’alisema Gabone.
Afisa Utawala Shule za St.Mary's Mkoa wa Mbeya, Anuciata Ngonyani akizungumza kwenye mahafali ya wanafunzi 63 wa darasa la saba.
Wahitimu wa elimu ya msingi darasa la Saba katika shule ya St.Merys Mbeya wakiwa makini kumsikiliza Afisa Utawala Shule za St.Mary's Mkoa wa Mbeya, Anuciata Ngonyani katika shehere za mahafali ya 63 ya shule hiyo.
Rose Lwakatare (Mtoto wa Mchungaji Mama Lwakatare ) akizungumza katika sherehe hizo zilizofanyika shuleni hapo .
Meneja wa bima (TIRA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Consolatha Gabone akizungumza katika mahafali hayo 
Wanafunzi wakitoa burudani katika sherehe hizo.
Wazazi na Walezi ambao walipata fursa ya kuhudhuria sherehe hizo 

POLISI KILIMANJARO YANASA RAIA WA ETHIOPIA 25 WALIONGIA NCHINI BILA KUFUATA SHERIA.

$
0
0


Raia 25 wa Ethiopia waliokamatwa wakati wakijaribu kupita nchini bila ya kufuata Sheria wakishuka kwenye gari walipofikishwa kituo kikuu cha Polisi mjini Moshi.
Baadhi ya raia hao wa Ethiopia wakiwemo watoto tisa wenye umri chini ya miaka 18 wakiwa kituo kikuu cha Polisi mjini Moshi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akitoa taarifa juu y akukamatwa kwa raia 25 wa Ethiopia waliongia nchini bila ya kufuata Sheria.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

Jeshi la Polisi linawashikilia raia 25 wa Ethiopia miongoni mwao tisa ni watoto wenye umri chini ya miaka 18 wakiwa katika kichaka eneo la Himo wakisubiri gari kwa ajili ya kuwavusha kuendelea na safari yao ya Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Maidizi wa Polisi,Hamis Issah amesema raia hao wa Ethiopia walikamatwa na askari Polisi wakati wa doria wakiwa na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Baraka itema (25) aliyejitambulisha kama fundi ujenzi .

Raia hao 25 wa Ethiopia wanaendelea kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kwa kusaidiana na jshi la Polisi na kwamba mara baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili za kuingia nchini bila ya kibali.

BALOZI SEIF AKAGUWA MAJENGO MAPYA YA SKULI ZA SEKONDARI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inazidi  kuimarisha miundombinu ndani ya Sekta ya Elimu, Wanafunzi Nchini wanalazimika kujikita zaidi katika kutafuta Elimu itakayowajengea njia ya Maisha ya furaha wao na Familia zao.
Alisema wanafunzi hao wakiamua kusoma kwa juhudi na maarifa na kufikia kiwango cha Elimu ya juu ya Vyuo Vikuu watakuwa na nafasi pana ya kujihakikishia fursa za ajira zilizozoweya kufanywa na Wataalamu wa Kigeni.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akisalimiana na Wananchi wa Mwambe akiendelea na ziara yake ya kukaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari zinazojengwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mshirika wa Maendeleo Mfuko wa Kimataifa wa Opec.
Alisema Taifa linahitaji kuwa na Wataalamu wake wenyewe  watakaotokana na Wanafunzi wake ambao watapaswa kuweka malengo ya kusoma kwa bidii kwa lengo la kuwahudumia Wananchi kwa kiwango cha uzalendo zaidi.
Balozi Seif alimuhimiza zaidi Mtoto wa Kike Nchini kusoma kwa ziada ili zile kazi za Kitaalamu zinazofanywa na Wanaume akatolea mfano za huduma za Afya wazifanye wenyewe katika azma ya kulinda na kuheshima mila, sila, Tamaduni na hata imani za Kidini.
Katika kutilia mkazo nafasi ya mtoto wa kike kusoma kwa malengo Balozi Seif  ameagiza Wazazi wowote watakaohusika na kitendo cha kuwaozesha  Watoto wao wa Kike wakati wanasoma Uongozi wa Serikali ya Mkoa usimamie katika kuona Vyombo vya Dola vinawachukulia hatua za Kisheria mara moja Wazazi hao ikiwa ni pamoja na kuwaweka ndani.
“ Jamii inahitaji kuwa na Ewataalamu wa Kike ambao watahusika kushughulikia huduma zinazofanywa na Wanaume Kitaalamu ambazo hazistahiki kutokana na Tamaduni na Imani wa Kidini”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alionya kwamba tabia hii inayoonekana kuendelea kwa baadhi ya Mitaa Nchini inarejesha nyuma maendeleo ya Mtoto wa kike aliyekandamizwa kwa muda mrefu kutokana na mfume Dume uliozoeleka kwa kipindi kirefu kilichopita.
 Balozi Seif akimchum Mtoto Sulhia Ali wa Kijiji cha Mwambe huku Mama yake Mzazi akitabasamu mara baada ya kusalimiana na Wananchi wa Kijiji hicho alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya Sekondari.
 Mhandisi wa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wara Ali Khamis Shaibu akimpatia maelezo Balozi Seif kuhusu ujenzi wa majengo ya Skuli hiyo unaokwenda kwa wakati uliopangwa.
Naibu Katibu Mkuu Wikzara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Maalim Abdulla Mzee Abdulla akiteta na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  kwenye majengo ya Skuli Mpoya ya Sekondari inayojengwa katika Kijiji cha Wara Chake Chake Pemba.
Balozi Seif akikagua baadhi ya Majengo ya Nyumba za Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar zinazojengwa katika eneo la Pagali Wilaya ya Chake chake Pemba.
Umma wa Wananchi wa Kijiji cha Mwambe waliokuwa wakisikiliza nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani alipofika kukagua Mradi wa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari kwenye eneo hilo.

Kamati ya Bajeti Yaipongeza NBS kwa Ufanisi wa Kazi Zake

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika semina iliyoandaliwa na NBS jana Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Mhe. Hawa Ghasia akisisitiza jambo wakati wa semina ya ya wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS),jijijini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa.
Meneja wa Takwimu za Mazingira, Bibi. Ruth Minja akiwasilisha mada mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika semina iliyoandaliwa na NBS jana Jijini Dodoma.Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Steven Maganda akiwasilisha mada kuhusu utafiti wa kaya mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika semina iliyoandaliwa na NBS jana Jijini Dodoma.Mbunge wa Jimbo la Mvomero, mkoani Morogoro Jeetson Patel akichangia mada wakati wa semina ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jana Jijini Dodoma.[Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania na watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia mada wakati wa semina kwa wajumbe hao iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jana Jijini Dodoma.(Picha na Idara ya Habari - MAELEZO)

TPDC KUKIONGEZEA UZALISHAJI KIWANDA CHA DANGOTE-TANZANIA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (kutoka kulia waliokaa) akisani mkataba wa makubaliano na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha Saruji cha Dangote-Tanzania (wa kwanza) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (kutoka kulia) akibadilishana mkataba wa makubaliano na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha Saruji cha Dangote-Tanzania, Jagat Rathee (wa kwanza) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (katikati) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kusaini makubaliano na Kampuni ya Saruji ya Dangote-Tanzania ya kuwasambazia nishati ya gesi katika uzalishaji na kuachana na matumizi ya Dizeli katika uzalishaji wa umeme. Pembeni kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha Saruji cha Dangote-Tanzania na kushoni ni mmoja ya wafanyakazi wa TPDC.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha Saruji cha Dangote-Tanzania akizungumza na wanahabari katika hafla fupi ya kusaini makubaliano na Kampuni ya Saruji ya Dangote-Tanzania ya kuwasambazia nishati ya gesi katika uzalishaji na kuachana na matumizi ya Dizeli katika uzalishaji wa umeme. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kampeni ya Tanzania ya Viwanda, Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesaini mkataba na Kampuni ya Saruji ya Dangote-Tanzania, utakaosaidia kiwanda hicho kuachana na matumizi ya mafuta ya dizeli katika uzalishaji wa umeme. 

Akizungumza jijini Dar es Salaaam wakati wa hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba amesema mkataba huo na Dangote utadumu kwa miaka 20 tofauti na mikataba mingine ambao huingia na makampuni.

 "Tunajua Serikali iko kwenye hatua za kujenga uchumi wa viwanda, kwa hiyo sisi (TPDC) kwa nafasi yetu tutahakikisha viwanda vinazalisha bidhaa kwa gharama nafuu kupitia matumizi ya gesi, wataanza kutumia futi za ujazo milioni nane na baada ya miaka miwili ijayo wataanza kutumia futi za ujazo milioni 20,” amesema Mhandisi Musomba. Amesema kuwa tokea Septemba mwaka jana wao walikuwa tayari wameshafikisha huduma hiyo mlangoni mwa kiwanda cha Dangote, walichokuwa wanasubiri ni ukamilishwaji wa mitambo ili kuingiza gesi waanze matumizi. 

 Kwa mujibu wa TPDC, kiwanda hicho ni sehemu ya viwanda saba vilivyopo kwenye mpango wa shirika katika mwaka wa fedha 2018/19, hivyo bado kuna vingine sita vitaunganishwa hapo baadaye. Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho cha Saruji, Jagat Rathee ameishukuru serikali kwa kuweza kuwawekeza nishati ya gesi ambao pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji lakini wataweza kutunza mazingira.

 "Kiwanda kilikuwa kinatumia wastani wa lita 106,000 za Dizeli ambazo zilizalisha wastani wa megawatt 20 (18MW -22MW) za gesi asilia kwa siku katika uzalishaji wa tani 2000 tu hivyo kutumia nishati ya gesi tutafikia wastani wa tani 6000 kwa siku huku gharama za uendeshaji zikishuka kwa asilimia 60. Kiwanda hicho kinaongeza idadi ya viwanda vinavyotumia gesi asilia kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kufikia 42 nchini, ambavyo vinatumia futi za ujazo milioni 15 tu kutoka akiba ya futi za ujazo trilioni 57, zinazoweza kutumika miaka 40 ijayo nchini.

GHARAMA UKARABATI WA BARABARA NDANI YA JIMBO KUONGEZEKA ZAIDI-TAASISI YA MAENDELEO JIMBO LA VUNJO (VDF)

$
0
0


Katibu wa Taasisi ya Maeneleo ya Jimbo la Vunjo,James Mbatia akitoa salamu kwa baadhi ya wananchi walioshiriki katika ukarabati wa miundo mbinu ya barabara unaoendelea katika jimbo hilo kwa kuchangia nguvu kazi.
Mmoja wa wananchi waliojitokeza katika ukataji wa miti kupisha upanuzi wa barabara akiandaa mbao kwa ajili ya shughuli nyingine za uakarabati wa barabara hizo. 
Greda likiendelea na kazi ya uondoshaji wa baadhi ya miti iliyokuwa kando ya barabara zinazopanuliwa katika jimbo la Vunjo.
Mafundi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiondosha Nyaya ili kupisha upanuzi wa barabara hizo.
Shughuli ya upanuzi wa barabara ikiendelea.
Baadhi ya wananchi wakichangia nguvu kazi katika ukarabati wa barabara hizo.
Upanuzi wa barabara mbalimbali ukiendelea katika jimbo la Vunjo. 
Moja ya eneo ambalo kazi ya upasuaji wamiamba ililazimika kufanyika ili kupanua barabara .
Muonekano wa barabara katika maeneo mbalimbali wakati ukaraba huo ukiendelea .


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

TAASISI ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo(VDF) imesema gharama zilizotengwa awali kwa ajili ya ukarabati wa Km 272.8 za barabara katika vijiji vyote vya jimbo hilo huenda zikaongezeka kutokana na kuwepo kwa miamba katika maeneo ambayo yanahitaji upanuzi.

Katibu wa taasisi hiyo,James Mbatia amesema ikiwa imengia wiki ya tatu tangu kuanza kwa ukarabati kwa baadhi ya maeneo katika barabara hizo tayari wamekutana na changamoto ya uwepo wa miamba ambayo imelazimika kuvunjwa kwanza .

“Tulipanga hii kazi kutumia miezi sita kuimaliza lakini sasa inaweza kuchukua hadi mwaka mmoja kutokana na changamoto ambazo zimeanza kujitokeza hizi za kukutana na miamba na wakati mwingine hali ya hewa”alisema Mbatia.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo alisema awali walipanga kutumia kiasi cha Sh Bil 7.29 kukamilisha kazi hizo lakini kwa namna shughuli inavyoendelea huenda gharama ikazidi huku akiendelea kutoa wito kwa wadau kuendelea kuchangia

“Hadi sasa tunashukuru kazi inaendelea vizuri tukishirikiana nawenzetu wa TARURA,TANESCO na tasisi nyingine ,lakini kipekee niombe serikali ione umuhimu wa kusaidia katika kutatua changamoto hii ya barabara kwa wakazi hawa wa jimbo la Vunjo”alisema Mbatia.

Kutokana na kuendelea kwa shughuli ya ukarabati wa barabara hizo tayari wananchi katika vijiji vya Shira na Mshiri vilivyopo katika jimbo la Vunjo wameanza kunufaika na mradi huo unaotekelezwa na Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo (VDF).

Shughuli ya upanuzi wa barabara katika kijiji cha Mshiri,Marangu ikiendelea kwa uondoaji wa miti iliyo kando ya barabara ya awali sambamba na uondohaji wa Miundo mbinu ya umeme ili kupisha shughuli za upanuzi.

Michuzi Blog imefika katika maeneo mbalimbali ya vijiji vilivyoko katika jimbo la Vunjo na kujionea mitambo ikiendelea na shughuli za upanuzi wa barabara pamoja na uondoaji wa miti na mawe makubwa yaliyokuwa katika maeneo ya barabara hizo.

Happy Makyao na Neema Temu ni wakazi wa Marangu ambao wanajishughulisha na biashara ya matunda katika eneo la Marangu Mtoni wakazungumzia adha walizokumbana nazo kabla ya kuanza kwa ukarabati huo na matumaini yao mara baada ya kukamilika kwa mrad huo.

“Kabla ya matengenezo ya hizi barabara tulikuwa tikipata shida sana kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na vichaka vikubwa na wakati mwingie ilikuwa ni hatari kwa wanafunzi na wakati mwingine walibakwa kwa sasa tumeanza kuona unafuu mkubwa”alisema Happy Makyao.

Kwa upande wake Neema Tema aliipongeza taasisi ya VDF kwa kazi kubwa waliyoianza katika jimbo la Vunjo na kwamba kwa sasa maeneo ambay yalikuwa hayafikiki kwa urahisi na kwa gharama ya juu sasa yanafikika.

“Kwa mfano bidhaa zetu tukizisafirisha kutoka maeneo ya juu kuja hapa Marangu Mtoni ,tulikuwa tunatumia kiasi cha Sh 2000 hadi 3000 kwa kutumia pikipiki lakini kwa sasa baada ya kufanyika ukarabati tunalipa sh 1000.”alisema Temu.

Exaud Mamuya Diwani wa kata ya Mshiri,Marangu akaeleza juu ya fursa kwa wananch hao zinaoztokana na ukarabati wa miundo mbinu ya barabara katika maeneo yao kwa kukusanya mawe yaliyochimbuliwa na kisha kuyauza.

“Matengenezo haya ya barabara yametoa Fursa pia kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hizo,mfano kupata kibali cha kukata mti wako ilikuwa lazima uingie gharama ,lakini kwa sasa wananchi wanaweza kukata miti yao kwenye maeneo ambayo barabara zinapanuliwa”alisema Mamuya.

“Eneo jingine ambalo wananchi wananufaika nalo ni wakati wa upanuzi wabarabara kuna Mawe ambayo yamekuwa yakiondolewa barabarni ,wananchi wamekuwa wakiyakusanya na kuyauza ambapo wamekuwa wakipata hadi sh 80000 kwa lori moja”aliongeza Mamuya.

Kuanzishwa kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Vunjo (VDF) kutasaidia utatuzi wa kero katika Sekta ya Miundombinu ya barabara ,Elimu ,Afya na Maji ambapo kwa upande wa miundo mbinu ya barabara,Km 272.8 za vijiji vyote katika jimbo hilo zinataraji kupitiwa.

Marais Wastaafu na viongozi mbalimbali wa serikali wawasili Chato kushiriki mazishi ya dada yake Rais Dkt Magufuli

$
0
0
 Marais Wastaafu Mzee Al-Hassan Mwinyi,Mh William Mkapa na Mh Jakaya Mrisho Kikwetee wakiwa na wake zao pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh John Mongella (pichani kushoto) wakiwa wamewasili uwanja wa ndege jijini Mwanza tayari kuelekea Chato mkoani Geita kushiriki mazishi ya Dada yake Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyefariki hivi karibuni hospitali ya Bugando alikokuwa akipatiwa matibabu
 Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh.William Benjamin Mkapa akiwasili uwanja wa ndege jijini Mwanza mapema leo tayari kuelekea kwenye msiba wa dada yake Rais Dkt John Magufuli,wilayani Chato mkoani Geita.
  Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameambatana na mkewe Salma Kikwete sambamba na viongozi wengine wakiwasili uwanja wa ndege jijini Mwanza mapema leo tayari kuelekea kwenye mazishi ya dada yake Rais Dkt John Magufuli,wilayani Chato mkoani Geita.

Mambo 5 ya kuyafahamu kuhusu Eid Al-Adha au ‘Sikukuu ya Kuchinja’

$
0
0
Na Jumia Tanzania

Katika ya dini ya Kiislamu, Eid Al-Adha au ‘Sikukuu ya kuchinja’ ni sikukuu kubwa inayofanyika baada ya kuisha kwa Hija. Sikukuu hii huashiria kuisha kwa ibada ya Hija eneo la Mina, nchini Saudi Arabia, lakini huadhimishwa na Waislamu duniani kote kama ishara ya kumbukumbu ya imani aliyoionyesha Ibrahimu.
Eid Al-Adha huanza siku ya kumi ya Dhu’l-Hijja, mwezi wa mwisho kwenye kalenda ya Kiislamu, na hudumu kwa muda wa siku nne. Huanza baada ya siku ambayo Waislamu kumali Hija wakishuka kutoka Mlima Arafat.

Sikukuu hii husherehekewa na Waislamu duniani kote, kama zilivyo tamaduni za imani ya dini nyingine. Lakini Eid Al-Adha ni nini? Yafuatayo ni mambo matano ambayo Jumia ingependa uyafahamu kuhusiana na sikukuu hii.

Historia ya Eid. Eid Al-Adha, ni sikukuu ya Kiislamu inayoadhimishwa kukumbuka tukio la Nabii Ibrahimu kuwa tayari kumtoa sadaka mwanaye wa pekee kwa kuchinja kama alivyoagizwa na Mungu. Ingawa alikuwa ni mtu mwema na aliyempenda mwanawe; imani yake na kujitoa kwa Mungu vilikuwa na nguvu zaidi kiasi ambacho angeweza kufanya chochote alichoagizwa. Kitendo cha utayari wa Ibrahimu kumtoa sadaka mwanaye wa pekee kwa Mungu kilipelekea Mungu kutoruhusu kuchinjwa kwa mtoto yule na badala yake akampatia mwanakondoo kuwa mbadala.

Kitendo cha kuchinja mnyama. Kwa wengi walio nje ya imani ya Kiislamu wamekuwa wakilitafsiri hili tukio tofauti. Kinyume chake, Waislamu huwachinja wanyama wao kwa kutanguliza sala kwanza na kuwachinja kwa jina la Mungu, ambaye amewapa mamlaka juu ya wanyama hao na haki ya kuwala. Hata hivyo, Wailsamu wanapolitaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja, ni kutukumbusha kwamba uhai ni kitu kitakatifu. Kwa hiyo kiuhalisia, hukifanya kitendo hiko kwa kumbariki mnyama na kumshukuru Mungu, pamoja na kutambua utakatifu wa maisha ya mnyama.

Nyama hugawiwa kwa familia, jamaa na maskini. Eid Al-Adha pia hujulikana kama ‘Sikukuu ya Kuchinja.’ Kondoo, ng’ombe, mbuzi, au ngamia ni sadaka kwa jina la Mwenyezi Mungu. Nyama itokanayo na sadaka hugawanywa katika mafungu matatu: theluthi moja kwa ajili ya familia, theluthi nyingine kwa marafiki na majirani, na theluthi inayobakia hugawiwa kwa maskini. Sehemu ya nyama ya mnyama aliyetolewa sadaka siyo kwa ajili ya matumizi binafsi pekee, bali kuwasaidia watu maskini pia. Kitendo hiki ni ishara ya utayari wetu kutoa vitu ambavyo tunavithamini, ili kufuata maagizo ya Mungu. Pia huashiria utayari wa kutoa fadhila ili kuimarisha urafiki na kuwasaidia wale wanaohitaji msaada.

Huashiria kuisha kwa Hija. Hija ni ibada katika dini ya Kiislamu na ni nguzo ya tano ya imani. Eid Al-Adha ni sikukuu ambayo huashiria kuisha kwa Hija kila mwaka, ambapo Waislamu wenye uwezo wa kiafya na kifedha wanatakiwa kufanya angalau mara moja katika maisha yao ikiwa ni sehemu ya imani. Kila mwaka, takribani Waislamu milioni mbili huenda Maka (Mecca) kwa ajili ya Hija.

Inavyosherehekewa. Asubuhi ya kwanza ya Eid Al-Adha, Waislamu duniani kote huhudhuria ibada kwenye misikiti iliyo karibu nao. Inasemekana kuwa baada ya kumaliza ibada ni vema kubadili njia uliyoenda nayo msikitini saa ya kurudi nyumbani. Kubadili njia saa ya kurudi itakupatia fursa ya kusambaza salamu za Eid kwa watu wengi zaidi.

Ni desturi kwa Waislamu katika kipindi hiki cha sikukuu kusherehekea kwa kutoa zawadi, kuvaa nguo mpya, pamoja na kuwatembelea marafiki na jamaa. Kwa kawaida, watu wazima huwapatia watoto pesa kwa ajili ya kutumia kipindi cha Eid Al-Adha. Eid Mubarak! Kwa wote

DC MJEMA AELEZA ALICHOBAINI KWENYE ZIARA YAKE

WAZIRI LUGOLA AKUTANA NA BAADHI YA WANANCHI NA KUSIKILIZA KERO ZAO

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam, jana kuwasilisha malalamiko mbalimbali ili wapate ufumbuzi wa kero zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam, jana kuwasilisha malalamiko mbalimbali ili wapate ufumbuzi wa kero zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza mmoja wa wananchi, Sheikh Issa, aliyefika ofisini kwa waziri, jijini Dar es Salaam, kuelezea malalamiko yake juu ya ndugu yake kuuawa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza mmoja wa wananchi, Martha Mtungi (wakwanza kulia), aliyefika ofisini kwa waziri, jijini Dar es Salaam, kuelezea malalamiko yake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

UONGOZI WA MAHAKAMA DODOMA WAFANYA JITIHADA ZA KUPATA MAHAKAMA ZA WILAYA KATIKA WILAYA ZISIZO NA MAHAKAMA KATIKA MKOA HUO

$
0
0


 Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Bi. Maria Francis Itala ( wa pili kushoto) akiwa katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba kufuatilia upatikanaji wa majengo kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya ya Chemba.
2 (33)
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma na Hakimu Mkazi Mfawidhi (M) wakitoka katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa ajili ya kwenda kuona eneo lililopendekezwa kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya pamoja na kuoneshwa kiwanja cha Mahakama katika Wilaya hiyo.
4 (18)
Muonekano wa nje wa jengo lililopendekezwa kwa ajili ya Mahakama ya Wilaya ya Chemba.
6 (7)
Muonekano wa jengo linalotumika kwa sasa na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa ambayo inatoa huduma za kimahakama kwa Wilaya ya Kondoa na Chemba.
9 (1)
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma akitoa maelekezo kwa Afisa Tawala wa Mahakama ya Wilaya Kondoa Bi. Edna Edward Dushi juu ya kuanza zoezi la upandaji wa miti katika eneo hilo ambapo Mahakama ya Wilaya ya Kondoa inajengwa.

Na Stanslaus Makendi, Mahakama Kuu Dodoma.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imeanza mpango wa uanzishaji wa huduma za Kimahakama katika Wilaya zisizo na huduma hizo kwa sasa.
Viongozi wa Mahakama katika Kanda hii wameanza kufuatilia na kukutana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na Chamwino ili kupata maeneo ambayo yatatumika na Mahakama za Wilaya katika kipindi ambacho mpango wa kujenga Mahakama za Wilaya katika maeneo hayo unafanyiwa kazi.

Utekelezaji huu unafuatia agizo la Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania juu ya kufanya jitihada ya kuwa na Mahakama hizo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.Katika mazungumzo waliyofanya katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ilibainika kuwa huduma ya Kimahakama inahitajika sana kwa sasa katika eneo hilo kutokana na umbali mrefu uliopo kufikia eneo ambalo huduma za Mahakama ya Wilaya inapatikana kwa sasa (Kondoa).

Baada ya mazungumzo hayo viongozi wote wa pande mbili walitembelea na kuona eneo ambalo Ofisi ya Mkurugenzi imetenga kwa ajili ya matumizi ya Mahakama na Taasisi nyingine muhimu ambazo hazipo kwa sasa katika Wilaya hiyo.
Sambamba na hilo, viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino nao walionesha uhitaji mkubwa wa uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya katika eneo hilo na wameahidi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha huduma hiyo inaanzishwa mapema katika Wilaya hiyo.

 Aidha kwa sasa wanafanya jitihada za kuhakikisha jengo linapatikana ili kuanzisha huduma hiyo muhimu kwa wananchi wa Wilaya ya Chamwino.
Katika zoezi la ufuatiliaji wa suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Wilaya ya Chemba ambayo inahudumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa kwa sasa, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Bibi. Maria Francis Itala waliambatana na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mheshimiwa Arnold John Kirekiano walitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kondoa ambayo kwa sasa umefikia hatua ya uezekaji wa paa na shughuli za kukamilishwa kwake zikiwa zinaendelea vizuri.

Mahakama ya Tanzania kupitia mpango Mkakati wake wa miaka mitano 2015/2016 – 2019/2020 hususani nguzo ya pili ya mpango mkakati huo inalenga kusogeza huduma za Mahakama kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma hizo zinafikika kwa urahisi kwa maeneo yote nchini.

WATUHUMIWA 11 WAPANDISHWA KIZIMBANI KISUTU KWA KESI TATU IKIWEMO YA UHUJUM UCHUMI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Watu 11 wakiwamo raia wawili wa Guinea wamepandishwa katika Kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na vipande 660 vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi bilioni 4.5.

Mapema leo asubuhi washtakiwa hao waliachiwa na kufunguliwa mashtaka mapya baada ya masaa matatu yale yale.

Awali walikuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo hayo ya uhujumu uchumi ambapo waliachiwa huru na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde lakini baada ya kuachiwa walikamatwa na ndani ya Masaa matatu walipandishwa tena kizimbani na kusomewa mashtaka mapya.

Wakiwasomewa mashtaka mapya mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizire, Wakili wa Serikali, Salim Msemo amewataja washtakiwa hao kuwa ni Ally Shariff na Fatoumata Saumaolo raia wa Guinea, Victor Mawalla, Calist Mawalla, Solomoni Kuhembe, Haruna Abdallah’ Kasa’, Abas Hassan ‘Jabu’,Ismail Kasa, Khalfan Kahengela, Musa Ligagabile na Kassim Said@ Bedui

Imedaiwa kuwa washtakiwa kwa pamoja kati ya Aprili 6 na Juni 23, 2016 jijini Dar es Salaam, waliratibu na kusafirisha vipande 660 vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 2,105, 181 ambazo sawa na biklioni 4.5 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na sheria ya wanyama pori.

Imedaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao walijihusisha na nyara za Serikali kinyume na sheria ya wanyamapori ambapo wanadaiwa walisafirisha vipande hivyo.Pia washtakiwa watano kati ya hao, Ally, Victor, Calist,Haruna na Abbaswanadaiwa kuwa walikutwa na vipande vya meno ya tembo kinyume na sheria za wanyamapori.

Hata hivyo, Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea.

Hata hivyo washtakiwa hao walilalamika mahakamani hapo kuwa hiyo siyo kesi mpya ilifutwa Masaa matatu kabla hawajafunguliwa kesi hiyo mpya hivyo waliomba kutendewa haki kwa sababu wanaumia gerezani na upande wa mashtaka unaumiza familia zao.Hivyo waliomba hiyo kesi iende mahakama Kuu kwa sababu hapo hawawezi kupata haki.

Wapo ndani tangu mwaka 2016 wakitaka kuomba dhamana mahakama Kuu Upande wa Mashtaka unawaeleza kesi imeiva, wahisi wanataka kuwauwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 3,2018.
  Watuhumiwa 11 wa kesi ya Uhujumu Uchumi
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images