Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1652 | 1653 | (Page 1654) | 1655 | 1656 | .... | 1897 | newer

  0 0

  NA IS-HAKA, ZANZIBAR.

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Dk.Bashiru Ally amesema CCM inaendelea kuimarika na hakuna Chama chochote cha kisiasa nchini kinachoweza kushindana nacho katika uringo wa siasa za ushindani wa sera za maendeleo kwa wananchi wa makundi yote.

  Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha ambapo amezungumza na wanachama mbalimbali katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Fidel Castro Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  Alisema kutokana na uimara huo hakuna chama kingine mbadala wa Chama Cha Mapinduzi kinachoweza kushuka kwa wananchi nyumba kwa nyumba na kuratibu kero zao kisha kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

  Dk.Bashiru aliwahakikishia wanachama na viuongozi hao kuwa CCM bado ipo imara na itapata ushindi wa kihistoria mwaka 2020 kwa nchini nzima kuliko ushindi unaopatikana kwa sasa katika uchaguzi mdogo unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

  Aliongeza kwamba sababu za kushinda na kusambaratisha upinzani zipo kwani vyama vya upinzani nchini vimekosa muelekeo na ndio maana wanachama wake wanahamia CCM kwa wingi.

  Alisema Tanzania inahitaji vyama vya siasa imara vitakavyolinda na kuhubiri misingi ya utaifa na umoja na msikamano wa Tanzania, bila ya kujali tofauti za kisiasa.

  Kupitia mkutano huo aliwambia wanachama wa vyama vya upinzania kisiwani Pemba kwamba huu ndio wakati wao wa kujitawala kifikra kwa kujiunga na CCM kwani Chama Cha CUF hakina tena mvuto kwa jamii kutokana na tabia ya unafiki na uongo inayofanywa na viongozi wakuu wa Chama cha CUF.

  “Wanachama wa vyama vya upinzani njoo CCM huku tupo shwari na tumekamilika kila idara wala msihofu chochote hakuna mtu yeyote wa kuwagusa, na wale wote waliojiunga na chama chetu leo nahakikishieni kuwa mtafaidika na siasa safi na demokrasia iliyotukuka.

  Pia Wana-CCM wenzangu awa wenzetu wanaojiunga na CCM wapokeeni na kuwathamini kwani wamefanya maamuzi sahihi ambayo hawatoweza kuyajutia.”, alisema Dk.Bashiru.

  Dk.Bashiru kupitia mkutano huo alitangaza rasmi kuwa Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuvunja ngome zote za upinzani kabla ya mwaka 2020, kutokana na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2015/2020.

  Alisema dhamira ya tasisi hiyo kwa sasa ni kuendeleza kwa vitendo mambo mema yaliyoasisiwa na vyama vya ukombozi vya ASP na TANU vilivyoungana na kuzaliwa kwa CCM.

  Pamoja na hayo aliweka wazi kuwa kila kila mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi anatakiwa kulinda Muungano, Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwani tunu hizo ndio chimbuko la mafanikio yaliyopo hivi sasa.

  Kupitia mkutano huo pia Dk.Bashiru aliwapokea wanachama wapya 62 waliotoka chama cha CUF na kujiunga na CCM kisiwani Pemba.

  Aliwapongeza wanachama wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumuamini kasha kupendekeza ateuliwe kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM Tanzania, na akaahidi kuwa atatumia nafasi yake kuleta mageuzi makubwa ya kimaendeleo ndani nan je ya CCM.

  Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla (Mabodi), alisema kazi kubwa ya Chama cha mapinduzi kwa zama za sasa ni kutekeleza kwa vitendo dhana ya CCM mpya na Tanzania mpya kwa maendeleo ya jamii.

  Alisema miradi mbali mbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwa ufanisi kisiwani Pemba ikiwemo mfuko wa maendeleo wa TASAF na kuongeza bei ya zao la karafuu ni kutokana na utekelezaji mzuri wa sera za CCM.

  Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Ndugu Yussuf Ali Juma alisema ndani ya Mkoa huo wanaendelea na mikakati ya kuhakikisha CCM inashinda kwa ngazi zote katika uchaguzi Mkuu ujao.

  Katika ziara hiyo Dk. Bashiru alifuatana na viongozi mbali wa Chama na Jumuiya wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Makamu Wenyeviti wa Jumuiya pamoja na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali Zanzibar.
   KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally Akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM wa Mikoa miwili ya Pemba katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro.
   Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndugu Mberwa Hamad Mberwa akimpa tia Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru zawadi ya ndizi ya mkono wa Tembo.
    KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akitembea kuelekea ofisi ndogo ya CCM Chake chake mjini Pemba.
  Katibu Mkuu wa CCM Tanzania akisalimiana na mwanachama mpya kutoka chama cha CUF aliyejiunga na CCM Amina Juma Nassoro

  0 0

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekabidhi Fedha za fidia kwa Wananchi waliopisha Ujenzi wa Karantini ya Mifugo katika eneo la Nziwengi katika Jimbo la Gando liliomo ndani ya Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  Fedha hizo zilizotolewa na Serikali na Kukabidhiwa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi zimelengwa kwa Wakulima 40 waliokuwa wakiendesha shughuli zao za Kilimo na Mifugo katika eneohilo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa Hekta 60.9.

  Akikabidhi fedha hizo kwa Wakulima hao, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema subra iliyofanywa na Wakulima hao wa Jimbo la Gando hatimae imeleta neema itakayowaenea Wananchi wa jimbo hilo hasa wakati huu wa kuelekea kwenye Siku Kuu ya Iddi El – Hajj.

  Balozi Seif aliwaasa na kuwakumbusha Wakulima na Wananchi hao wa Gando wawe makini katika matumizi ya fedha walizokabidhiwa kuzilenga kwenye uanzishaji wa shughuli za Kilimo walizokuwa wakizifanya katika maeneo mengine.

  “ Nimefarajika kushuhudia kitendo hichi cha ulipaji wa fidia kwa wakulima wa Gando nikiwa kama Mwakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Kazi hii”. Alisema Balozi Seif.

  Alieleza kwamba Serikali Kuu katika kushajiisha Kilimo Nchini imeanza kutoa Miche ya Minazi bure kuwapa Wakulima katika maeneo mbali mbali kama inavyofanywa kwa Miche ya Mikarafuu.

  Akitoa Taarifa fupi ya ujenzi wa Karantini ya Mifugo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Nd. Ahmad Kassim Haji alisema eneo la Gando lilikuwa likikumbwa na miripuko ya Maradhi mengi yanayotokana na uingizwaji wa Mifugo kiholela.

  Nd. Ahmad aliwashukuru Wananchi wa Gando kwa ustahamilivu wao wa muda mrefu na kuridhia maamuzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kulichukuwa eneo hilo kwa kazi ya kuratibu mifugo inayoingia Nchini.

  Akimkaribisha Balozi Seif kulipa Fidia Wananchi hao Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Rashid Ali Juma alisema Serikali imekamilisha azma yake licha ya kuchukuwa muda mrefu tokea Mwaka 2013.

  Waziri Rashid aliwaeleza Wananchi hao kwamba kila mwenye Haki yake sheria, Taratibu na hata Kanuni zinaenekeza wahusika wa madai yaliyoidhinishwa wana haki ya kulipwa fidia kama walivyofanywa wao.

  Waziri wa Kilimo alifahamisha kwamba mikakati inayowekwa na Serikali kupitia Wizara inayohusika na Mifugo ina lengo la kuratibu ukaguzi wa mifugo yote inayoingiz nchini ili kuzuia miripuko ya maradhi inayoweza kuathiri Mifugo iliyopo Nchini.

  Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikagua eneo linalotaka kujengwa Nyumba 33 za Wahanga wa Maafa ya Mvua za Masika zilizotokea Mwaka uliopita hapo katika Kijiji cha Tumbe Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Makame Haji Makame alimueleza Balozi Seif kwamba ujenzi huo unaotarajiwa kuanza kwa haraka umepata ufadhili ya Jumuiya ya Mwezi Mwekundu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE}.

  Ndugu Makame alisema Mradi huo utakaogharimu jumla ya Dola za Kimarekani Laki 850,000 utazingatia mahitaji muhimu ya kibinaadamu kwa uwepo wa Skuli, Msikiti, Kituo cha Afya, Soko, Maduka pamoja na sehemu za Michezo.

  Alisema lipo eneo jengine katika sehemu hiyo lililopimwa kama hakiba endapo kutahitajika uwepo wa huduma nyengine muhimu ikizingatiwa kwamba Kijiji hicho kitakuwa miongoni mwa Miji midogo inayoanzishwa na Serikali katika sehemu mbali mbali za Visiwa vya Unguja na Pemba.

  Naye kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Nd.Juma Bakari Alawi alisema utaratibu wa matumizi bora ya Ardhi utaendelea kuzingatiwa na Taasisi hiyo iliyopewa jukumu la kuratibu Sekta hiyo muhimu kwa Taifa.

  Alisema Taasisi zote zinazohusika na harakati za ujenzi wa Nyumba hizo zimeshakutana na kujadili mpango huo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kama maji na Umeme zitakazohitajika katika eneo hilo.

  Nd. Bakari alieleza kuwa Timu ya Watalaamu imeshafanya utafiti wa Maeneo Sita ndani ya Kisiwa cha Pemba kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Wahanga hao na kuridhika na eneo la Tumbe ambalo ni kubwa na linamilikiwa na Serikali Kuu.


  Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Makame Haji Kushoto akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ramani ya Ujenzi wa Nyumba za Wahanga wa Mvua za Masika zilizopita zinazotaka kujengwa katika Kijiji cha Tumbe Mkoa wa Kaskazini Pemba,
  Balozi Seif akimkabidhi Mkulima Bibi Safia Hamad Khamis wa Kijiji cha Gando Hundi ya Fedha kwa ajili ya Fidia ya mazao yao ili kupisha Ujenzi wa Karantini ya Midugo kwenye eneo la Nziwengi.Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman na kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Kilimo Mh. Rashid Ali Juma na Naibu Wake Dr. Makame Ali Ussi.
  Balozi Seif akimkabidhi Hundi Bwana Ali Khamis Ali kwa ajili ya ulipwaji wa  fidia ya mazao yao ili kupisha Ujenzi wa Karantini ya Midugo kwenye eneo la Nziwengi.Picha na – OMPR – ZNZ.


  0 0


  Bondia Mada Maugo (kulia) akirusha konde kwa Charles Misanjo wa Malawi katika pambano la kimataifa la uzito wa Super Middle lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA juzi. Maugo alishinda kwa pointi.
  Ngumi ni mchezo, lakini ni hatari sana! Bondia Baina Mazola akiuguliwa baada ya kuchanwa na Ibrahim Class katika pambano la uzito wa Super Feather. Class hakutumia kisu wala kiwembe, ila ni nguvu ya mikono yake ndani ya glovu.
  Bondia Ibrahim Class (kushoto) akimchapa ngumi mpinzani wake, Baina Mazola katika pambano la uzito wa Super Feather kwenye ukumbi wa PTA juzi.Class alishinda kwa technical knockout (TKO) raundi ya tano.


  Na Mwandishi wetu

  Dar es Salaam. Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo wa Tanzania amemchapa kwa pointi, mpinzani wake, Charles Misanjo wa Malawi katika pambano la kimataifa la uzito wa Super Middleweight kwenye ukumbi wa PTA jijini.

  Wakati Maugo anashinda kwa pointi, bondia nyota nchini,Ibrahim Class alidhihirisha ubora wake baada ya kushinda kwa Technical knockout (TKO) raundi ya tano katika uzito wa Super Feather. Pambano hayo yaliandaliwa kwa lengo la kutafuta mataulo ya kike kwa wanafunzi wa mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa kushirikiana na taasisi ya She Can Foundation.

  Katika pambano hilo lililoandaliwa na promota wa kwanza wa kike nchini, Sophia Mwakagenda wa kampuni ya Lady In Red Promotion, Maugo alipata pointi 77-75 kutoka kwa jaji, Mwinyi Milla, 78-74 (Modesti Rashid) na 76-76 kutoka kwa jaji, Chaurembo Palasa. Pamoja na ushindi huo ulilalamikiwa na Misanjo na baadhi ya mashabiki wa ngumi za kulipwa, Maugo alisema kuwa Mmalawi alikuwa anapiga makofi baadala ya ngumi ndiyo maana ameonekana kushambulia sana.

  “Mimi nimekuwa nikipigana kwa kutafuta pointi kwa kupiga ngumi, yeye alikuwa anapiga makofi muda wote na kusukuma, hao mashabiki na bondia inaonekana hawajui ngumi, sijapendelewa kwa sababu ya Utanzania, hapana,” alisema Maugo. Misanjo alisema kuwa haikuwa ngumi za kawaidi bali ni vita. “Matokeo sikubaliani nayo, yanaua mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, itatufanya tusiwe tunakuja kupigana kutokana na maamuzi kama haya,” alisema Misanjo.

  Pambano kati ya Ibrahim Class na Baina Mazola ndilo lilikuwa na msisimko mkubwa ambapo mabondia hao walionyesha uwezo mkubwa. Class alianza pambano kwa kasi na kutawala raundi mbili za mwanzoni huku Mazola alikitawala raundi ya tatu. Mabondia hao walipigana kwa visasi na kuleta burudani ya aina yake. Class alionekana kutumia uzoefu zaidi na kufanikiwa kumchana jicho Mazola katika dakika ya 1.47 ya raundi ya tano na kuibuka mshindi.

  “Nimepoteza kwa kuumia, hata hivyo nitamtafuta tena Class ili kuonyesha kuwa mimi ni bora zaidi yake,” alisema Mazola. Class alisema kuwa mpinzani wake ni mzuri na ushindi ni jambo la kawaida sana kwake. “Mimi ni bondia bora, hilo halina ubishi,Mazola bado sana kwangu, afanyekazi ya zaida kunifikia na kunishinda,” alitamba Class.

  Bondia Flora Machela alifanikiwa kushinda kwa TKO raundi ya tano dhidi ya Sarafina Julius katika pambano la uzito wa bantam wakati Asha Ngedere na Happy Daudi wakitoka sare kwa katika pambano la uzito wa Super Light. Akizungumza baada ya pambano hilo, promota Mwakagenda aliwapongeza wadau na makampuni yaliyochangia kufanikisha tukio hilo japo lengo la kukusanya mataulo 40,000 halijafanikiwa.

  “Huu ni mwanzo na jambo hili ni geni kwangu, ndiyo kwanza nimeandaa ngumi za kulipwa na nimeona changamoto zake, nimejifunza na nitaendelea kuandaa kwa malengo maalum,” alisema Mwakagenda.

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MKUU wa Wilaya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro amemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa vitendea kazi kwa lengo la kuboresha sekta hiyo huku akiahidi kusimamia ubora wa elimu.

  Muro amesema hayo wakati anakabidhi Pikipiki mpya 18 kwa waratibu wa elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambazo zimetolewa na Rais kupitia Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, ikiwa sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya kufuatilia Ubora wa Elimu Nchini.

  "Tunashukuru kwa vitendea kazi hivi ambavyo tumepewa na Rais kupitia Waziri wa Elimu.Tunaamini vitendea kazi hivi vitatumika kwa lengo ambalo limekusudiwa.

  " Tutahakikisha tunainua kiwango cha ufaulu katika Halmashauri yetu ya Arumeru pamoja na kuinua kiwango cha elimu.Lengo ni kuhakikisha mtoto wa maskini anapata elimu iliyo bora,"amesema.

  Amefafanua kuwa kupatikana kwa pikipiki hizo na kisha kuzigawa kwa waratibu wa elimu wilayani huo kunatoa nafasi ya wao kutimizamajukumu yao ya kufuatilia ubora wa elimu katika shule za Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru.
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro akiwa na baadhi ya piki piki alizowakabidhi Waratibu wa elimu katika halmashauri ya wilaya ya Meru


  0 0


  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Lusius Mwenda (kushoto) akiwa ameongoza na Watumishi zaidi ya 50 wa Wizara hiyo wakipanda kilima kwenda kuangalia michoro ya miambani katika kituo cha Utalii cha Kolo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma jana ikiwa lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali. Wa pili ni Mkuu wa Kituo cha Kolo, Zuberi Mabie.
  Mkuu wa Kituo cha Utalii, Kolo chenye michoro ya miambani, Zuberi Mabie akiwa na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwaonesha michoro ya miambani katika kituo cha Utalii cha Kolo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma jana ikiwa lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali.
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Lusius Mwenda (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo walipotembelea katika kituo cha Utalii, Kolo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma jana ikiwa lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali.

  Mkuu wa Kituo cha Utalii, Kolo chenye michoro ya miambani, Zuberi Mabie akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipotembelea kituo cha michoro ya miambani, Kolo kilichopo wilayani Kondoa wakati walipotembelea katika kituo hicho ikiwa la lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali.

  Afisa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Nina Kisando akiwa anatelemka kutoka kwenye kilele cha mlima baada ya kuona michoro ya miambani Kolo ambacho ni kivuto cha Utalii cha aina yake.

  Baadhi ya Maafisa wakiwa wameongozana na Mtalii wa ndani wakiwa wanatelemka kutoka kwenye kilele cha mlima baada ya kuona michoro ya miambani Kolo ambacho ni kivuto cha Utalii cha aina yake

  Baadhi ya watumishi wakifurahia mara baada ya kuteremka kwenye kilele cha mlima baada ya kuona michoro ya miambani Kolo ambacho ni kivuto cha Utalii cha aina yake
   
  …………………..
   
  NA LUSUNGU HELELA-DODOMA .

  Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Lusius Mwenda ametoa wito kwa watumishi wa Serikali kuwa mstari wa mbele kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mapya ikiwa pamoja na kupumzisha akili. 

  Pia amewataka watumishi hao kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio hivyo ili waweze kuona na kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo wanaweza kuanza kuzifanya kwa ajili ya kujiingizia kipato ikiwa ni njia mojawapo ya kuanza kujiandaa kwa ajili ya kustaafu. 

  Amefafanua kuwa kila mtumishi wa Serikali anatakiwa kuanza kujiandaa kwa ajili ya kustaafu kuanzia ile siku ya kwanza aliyoajiriwa. Amesema watumishi walio wengi mara baada ya kustaafu hali zao za kiuchumi huteteleka kwa vile katika kipindi cha utumishi wao walikuwa hawatembelei maeneo tofauti na yale waliyoyazoea kwa ajili ya kujifunza na kukutana na watu tofauti. 

  Ametoa Rai hiyo jana katika kituo cha utalii Kolo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma alipokuwa ameongozana na Watumishi zaidi ya 50 kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii , Ikiwa ni moja ya jitihada za Wizara hiyo kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali kwa kuanza na Watumishi wa Wizara yenye dhamana. Kivutio cha Utalii, Kolo kipo ni kivutio mashuhuri sana kwa michoro yake ya miambani kwa vile inafanana na michoro ya Afrika Kusini na kimebeba tamaduni za waafrika. 

  ” Tunataka Watumishi muwe mabalozi wazuri kuanzia kwenye ngazi ya familia hadi ngazi ya taifa kwa kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo maeneo ya kihistoria ambavyo yamesheheni chimbuko la tamaduni zetu pamoja na harakati za binadamu katika kupambana na mazingira yake.” alisema .Akizungumzia kuhusu lengo la ziara hiyo, Bw.Mwenda amesema ziara hiyo ya siku moja imejikita kuhamasisha Utalii wa ndani kwa kauli mbiu ” Utalii wa ndani unaanza kwako na kwangu” 

  Aidha, Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii inaandaa utaratibu maalum wa kuwawezesha watumishi wengine wa Wizara nyingine pamoja na taasisi za serikali waanze kutembelea vivutio vya utalii ili kujenga utamaduni kwa watumishi wa Umma kutembelea vivutio vya utalii nchini kwa ajili ya kujifunza na kufurahia maisha. 

  Awali, Mkuu wa Kituo cha Kolo, Zuberi Mabie alieleza kuwa Kolo ni kivutio cha Utalii cha aina yake chenye michoro ya miambani iliyochorwa na jamii ya Wasandawe miaka 10,000 hadi miaka 6,000 iliyopita. Amesema eneo hilo ni miongoni mwa maeneo manne ya Idara ya Mambokale yaliyopo katika orodha ya Urithi wa dunia  Alisema inaonesha kuwa kabla ya ugunduzi huo watu walikuwa wanaweka kumbukumbu ya kuchora vitu na matukio waliyokuwa wanayaona katika mazingira yao. 

  Akizungumzia kuhusu idadi ya watalii wanaotembelea, alisema kila mwezi hupata watalii zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya nchi. Kwa upande wake, Afisa Utalii, Heda Chale mara baada ya kutembelea kituo hicho alisema ameifurahia safari hiyo na amejifunza vitu mbalimbali ikiwa pamoja na kujionea madhari ya aina yake katika kivutio hicho. 

  Naye, Mhifadhi Mkuu wa Mambo Kale, Wiliam Mwita alitoa wito kwa jamii kutembelea vituo vya maeneo ya kihistoria yaliyotapakaa nchi nzima ili jamii iweze kujifunza historia ya binadamu pamoja na mapambano yake katika kuyamudu mazingira. 

  Pia, Alitoa wito kwa Wawekezaji kuchangamkia fursa ya kuwekeza kwenye vivutio vya Mambokale kwa vile nafasi zipo wazi lengo likiwa ni kuviendeleza kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho. Amesema maeneo hayo yanahitaji uwekezaji wa nguvu ili kuyafanya yawe na mvuto ili kuwavutia wageni kutika nje na pia Watanzania  Kivutio cha Utalii Koli kipo kilomita 150 kutoka jiji la Dodoma na ni michoro ya kwanza kwa bara la Afrika kutokana na uwingi wake na kutapakaa kwake katika eneo kubwa.

  0 0
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael. Dunford

  SHIRIKA la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema kwamba kutoka mwaka 2010 imeingiza katika uchumi wa Tanzania zaidi ya dola za Marekani milioni 278 kutokana na huduma mbalimbali inazotoa kusaidia wakimbizi ambao wapo nchini.

  Aidha fedha hizo zimeingia katika mfumo wakati Tanzania inatumika kama kituo cha lojistiki kusaidia maeneo mengine ya ukanda wa Afrika Mashariki wenye matatizo.

  Hayo yamesemwa katika maadhimisho ya Siku za msaada duniani, inayokumbukwa kuadhimisha mauaji ya watoa misaada wakati wa mashambulio ya anga ya Baghdad, Irak miaka kadhaa iliyopita.

  Aidha siku hiyo inaadhimishwa Agosti 19 kila mwaka kutoa neno kwa jamii ya dunia kuwakumbuka watoa misaada ambao wapo katika hatari ya maisha kutokana na vurugu zinasumbua duniani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwakilishi Mkazi wa WFP  nchini Tanzania, Michael Dunford alisema kwamba kumekuwepo na uingizaji mkubwa wa fedha katika uchumi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa na kusaidia chakula kwa wakinbizi waliopo nchini Tanzania kwa kusaidiana na mashirika mengine.

  Kwa Tanzania kwa sasa inahifadhi wakimbizi 297,000 kutoka Burundi na Kongio (DRC) katika maeneo ya Nyarugusu, Nduta na Mtendeli mkoani Kigoma .

  Katika kambi hizo WFP hutoa chakula ikiwamo lishe na kusaidia kuwapa virutubisho zaidi kwa wanawake wajawazito, wanawake wanaonyonyesha na watoto na wale wenye kuishi na Virusi vya Ukimwi.

  Mwakilishi huyo alisema kwamba Tanzania pia imefaidika na  matumizi ya miundombinu yake kusafirisha bidhaa mbalimbali kupeleka Burundi ambapo karibuni walitumia reli ya kati kupeleka chakula  Uganda kwa ajili ya wakimbizi wa Sudan ya Kusini.

  Akizungumzia umuhimu wa Tanzania kwa shirika lake, Mwakilishi huyo alisema kwamba Tanzania pamoja na kuwa mhimili wa kuhifadhi wakimbizi kwa miaka mingi na pia kushiriki katika ulinzi wa amani inatumika kwa ajili ya lojistiki kusaidia mamilioni ya wananchi wanaohitaji msaada nchini Kongo (DRC) Burundi, Rwanda, Uganda na Sudan kusini.

  Pamoja na kukubaliana na ombi la Rais John Magufuli kwa MkurugenziMtendaji wa WFP wakati alipofanya ziara yake nchini hivi karibuni ya kununua bidhaa zaidi kutoka Tanzania, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita walinunua  metriki tani 200,000 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 68.

  Akizungumzia suala la wakimbizi wa Burundi kulazimishwa kurejea nyumbani, mwakilishi huyo alisema kwamba anachojua ni kwamba wapo wakimbizi wanaotaka kurejea nyumbani jumuiya ya kimataifa husaidia kuwarejesha.

  Aidha alisema kwamba hajui lini wakimbizi wote watamalizika kurejea nyumbani kwa kuwa sababu za kukimbia kwao zinatofautiana kati ya mtu mmoja hadi mwingine japo hali ya kisiasa nchini Burundi inaimarika.

  Alisema kwake yeye anaona jambo bora kabisa ni kutolazimisha wakimbizi kurejea nyumbani lakini juhudi kubwa kufanywa kwa wale wanaoataka kurejea nyumbani kusaidiwa kufanya hivyo.

  Alisema shirika hilio ambalo lipo katika nchi 83 duniani ikisaidia maeneo yenye dhiki ya mahitaji ya binadamu kutokana na migogoro  ya kivita na kisiasa na ukandamizaji.

  Alisema idadi ya wananchi waliokumbwa na migogoro ikiwamo ya kivita ni milioni 489 huku watu milioni 815 duniani wanakabiliwa na tatizo la njaa.

  Alisema watu zaidi ya milioni 91 wanahitaji msaada wa haraka wa chakula na kusema kwamba shirika hilo linalotegemea hisani za watu linahitaji fedha zaidi kusaidia walioathirika na majanga mbalimbali.

  Alisema mathalani kwa sasa wanahitaji dola milioni sita kila mwezi kuweza kulisha wenye mahitaji.

  Alisema kuna haja kubwa kwa dunia kutambua kwamba haiwezekani kulisha jamii hiyo kama migogoro haitamalizwa.

  Aidha ni vyema wakati wa migogoro mashambulio yasielekezwe kwa raia wasiokuwa na hatia.

  Hata hivyo ameshukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kusaidia wakimbizi waliopo nchini na pia mataifa makubwa yanayotoa sehemu kubwa ya mahitaji yanayotakiwa na WFP.

  Alizitaja nchi hizo kuwa ni Marekani, Uingereza, Jumuiya ya Ulaya, Denmark, Sweden, Canada na Ujerumani.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Mabingwa watetezi wa michuano ya Kikapu ya Sprite Bball Kings, Mchenga Bball Stars wamefanikiwa kuondoka na ushindi wa kwanza katika hatua ya fainali, baada ya kushinda game 1 kwenye 'Best of five' dhidi ya wapinzani wao Flying Dribblers.

  Mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa wiki huu kwenye uwanja wa taifa wa ndani uliweza kuwa wa ushindani mkubwa sana huku mabingwa watetezi wakitawala zaidi katika quarter zote nne na kufanikiwa kushindwa kwa pointi 103 dhidi ya 73 vya Flying Dribblers.

  Mchenga walianza mchezo huo kwa kasi wakishinda quarter ya kwanza kwa pointi 27 dhidi ya 10 za Flying Dribblers kabla ya kuendelea kuongoza kwa pointi 62 kwa 25 hivyo kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa tofauti ya pointi 37. Katika quarter hizo mbili mchezaji Baraka Sadick alifunga pointi 32. 

  Baada ya mapumziko Mchenga walirejea kwa kasi tena na kuongoza kwa pointi 62 dhidi ya 44 za Flying Dribblers. Mabingwa hao watetezi waliendelea na moto wao katika quarter ya 4 na kufanikiwa kufikisha pointi 100 ambapo hadi mwisho wa mchezo wakaongoza kwa pointi 103 kwa 73.

  Katika mchezo huo mchezaji Baraka Sadick wa Mchenga Bball Stars ameibuka kinara wa jumla kwa kufunga pointi 48, Assist 6 na kuchukua rebound 4. Amefuatiwa na mchezaji Baraka Mopele wa Flying Dribblers ambaye amefunga pointi 29 na rebound 4.

  Game 2 ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Sprite, itachezwa Jumatano Agosti 22, 2018 kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay. Mechi hizi zinaweza kwenda hadi game 5 endapo Flying Dribblers watarejea na kusawazisha katika game 2 na zinazofuata.

  Mshindi wa mashindano hayo atanyakua kitita cha Shilingi Milioni 10 pamoja na Kikombe, Mshindi wa pili Milioni 3 na mchezaji bora MVP kupata milioni 2.
  Mchezaji wa timu ya Flying Dribblers, Steve Mtemihonda (kushoto), akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa timu ya Mchenga Stars, Mohamed Yusuph, wakati wa mchezo wa kwanza wa fainali ya mpira wa Kikapu Sprite Bball Kings, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa ndani. Mchenga alishinda pointi 103 dhidi ya 73 za Flying Dribblers.
  Mchezai wa timu ya Mchenga Stars, Baraka Sadick (kulia) akimiliki mpira huku akizongwa na wachezaji wa timu ya Flying Dribbers wakati wa mchezo wao wa kwanza wa fainali ya mpira wa kikapu Sprite Bball Kings uliofanyika Uwanja wa ndani wa Taifa Dar es Salaam. Mchenga alishinda pointi 103 dhidi ya 73 za Flying Dribblers.

  0 0


  Tukio maarufu la riadha la Rotary Dar Marathon ambalo hufanyika siku ya 14 Oktoba – siku ya Nyerere kila mwaka tangu 2009 litaadhimisha mwaka wa kumi tangu kuanza kwa tukio hilo.

  Dhima ya Rotary Dar Marathon inaendelea kuwa "ponya maisha, badilisha jamii” na ni katika mwaka wa tatu tangu RDM imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za hospitali ya (CCBRT) kuwa na mradi wa hsopitali binafsi ili waweze kupunguza gharama ya hudua za ulemavu zinazotolewa na hospitali hiyo kwa wana jamii. Fedha zote zitakazokusanywa mwaka huu kutokana na tukio la RDM zitakabidhiwa kwa CCBRT ili kukamilisha ujenzi wa kliniki hiyo binafsi na manunuzi ya vifaa husika.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Rotarian Catherinerose Barreto, alisema kwamba kamati inayojumuisha wajumbe kutoka klabu nane za Rotary za jijini Dar es Salaam imeshaanza maandalizi kuhakikisha mwaka huu RDM inakuwa tukio ambalo ni la ubora wa hali ya juu. Aliongeza pia mlezi wa RDM Mheshimiwa Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi atakuwepo na kushiriki matembezi ya siku hiyo.

  Tukio la Rotary Dar Marathon (RDM) licha ya kulenga lengo msingi la kuchangisha fedha kusaidia shughuli mbalimbali ili kuboresha ubora wa maisha kwa jamii zetu pia linahakikisha kutoa tukio lenye ubora wa kimataifa na la kufurahiwa na wanaoshiriki katika mbio au matembezi. Kila mwaka RDM inachukua hatua za ziada kuhakikisha tukio linafanyika katika kiwango cha juu ili washiriki wote ambao ni wanariadha wataalamu na wengineo wanafurahia siku hiyo na pia kuweza kutumia shindano kama njia ya kuongeza uzoefu wao na kukua katika michezo wa riadha.

  Mkuu wa njia za RDM Rotarian Diamond Carvallo, naye alisema kwamba anatarajia tukio la mwaka kuvutia washiriki ya zaidi 16,000, na baadhi pia inatarajiwa kuwa baadhi ya washiriki watakuja kutoka nje ya nchi. Katika tukio la RDM mwaka huu kutakuwa na mashinda ya riadha na baiskeli kwa kilomita 21.1km na 42.2 vilevile matembezi ya kujifurahisha ya kilomita 5 na 9. Riadha na matembezi yote yataanzia na kumalizika katika viwanja vya Green vilivyopo Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

  Gavana wa Rotary na mwenyekiti wa RDM, Sharmila Bhatt aliongeza, "ni sera yetu kufanya kazi kwa pamoja na mashirika mbalimbali katika juhudi zetu za kuleta mabadiliko katika katika jamii zetu. Tunaamini kwamba kufanya kazi pamoja kutaleta mafanikio makubwa katika jamii kwa ujumla. Tunapenda kuwashukuru Bank M kwa kushirikiana nasi kwa miaka tisa iliyopita na SBC - Pepsi kwa kuendelea na udhamini wao Tshirts,-vinywaji na mwaka huu kwa kuongeza msaada zaidi katika kufanikisha RDM. Mwaka huu tutakuwa washirika wapya na tunafurahi sana kuweza kuleta tukio la Rotary Dar Marathon mwaka huu hii ikiwa ni tukio letu la 10 ."

  Kwa miaka 9 iliyopita, Rotary Dar Marathon imeendeleza miradi kadhaa kama vile kupanda miti 27,000, kutoa vifaa vya maji na usafi wa mazingira kwa shule 27, kujenga wodi ya watoto ya saratani katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia kukarabati na kuweka vifaa katika kituo cha ujasiriamali cha Rotary katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Catherinerose Barretto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.
  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Catherinerose Barretto (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.
  Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Hawa Mkwela akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.
  Mwenyekiti wa bodi ya Rotary Dar Marathon, Sharmila Bhatt akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu. Rotary Dar Marathon inatarajia kuwavutia washiriki 16,000 kwa mwaka huu.
  Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon wakifurahia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wikiendi hii jijini Dar es Salaam ambapo walitangaza rasmi maandalizi ya matembezi hayo kwa mwaka huu yanayotarajiwa kufanyika tarehe Oktoba 14, mwaka huu. Mbio za Rotary Dar zitaanza na kuishia katika viwanja vya ‘The Green’, Oysterbay.
   

  0 0


  Na Gordon Kalulunga, Mbeya

  Baada ya siku chache jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kukamata wananchi 68 wanaodhaniwa kushirki kuhujumu miundombinu ya Maji Kata ya Ilungu Mbeya Vijijini, Shirikisho la vyama vya siasa mkoani hapa limemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila kutoa amri ya kuwakamata wote waliowahi kushiriki kuchoma Barabara Jijini Mbeya.

  Rai hiyo imetolewa jana jijini hapa na Mshauri wa shirikisho hilo Prince Mwaihojo katika ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Peack, wakati wakitoa tamko la kumpongeza Rais Dkt.John Magufuli kwa utendaji wake ikiwemo kuteua wapinzani na kuwapa kazi serikalini.

  Mwaihojo alisema amri ya Mkuu wa Mkoa kuamuru kukamatwa wanakijiji wahujumu wa miundombinu ni amri nzuri inayopaswa kupongezwa kwasababu italeta nidhamu ya kulinda miundombinu ya mkoa wa Mbeya.

  "Rais kumteua huyu RC Chalamila uwepo wake unaonekana na nimuombe atoe amri ya kuwasaka wanaochoma Barabara za Lami kwa kisingizio cha Maandamano" alisema Mwaihojo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho hilo lenye kauli mbiu ya Mbeya kwanza vyama baadae Godfrey Davis Mwandulusya, alisema shirikisho hilo kwa kauli moja baada ya kikao chao wanampongeza Rais Dkt. Magufuli kwa utaifa wake huku akiweka pembeni itikadi za vyama vya siasa.

  "Rais Magufuli anafanya kazi nzuri ikiwemo uteuzi wake wa kizalendo uliotukuka kwa kuwachagua wapinzani na kuwaweka katika serikali yake, kuanzisha miradi ya maedeleo ikiwemo Flyover,  Standard Gauge, kufufua shirika la ndege na miradi mingi ya Afya nk" alisema Mwandulusya.

  Aidha shirikisho hilo liliwapongeza wadau wote wa Maendeleo mkoani Mbeya huku likiwataja Naibu spika Dr. Tulia Ackson na Mdau Ndele Mwaselela kwa kujali jamii ya wana Mbeya.

  "Tunawapongengeza na kuwashukuru Dr. Tulia na Ackson, Ndele kwa kusomesha watoto wetu wa Mbeya Mwaselela na katika kuwezesha madawati, ujenzi wa vyoo, vituo vya Afya nk" alisema Mwenyekiti huyo.

  Mbali na pongezi hizo, wamemuomba Rais Magufuli kuutupia jicho uwanja wa ndege wa Songwe, Ujenzi wa Bandari kavu Inyala kukamilika haraka, Chuo cha Kilimo Uyole ili kiweze kutoa shahada kwa madai kuwa ni mtaji wa uchumi wa viwada na Bypass Road ipewe kipaumbele ili kupunguza ajali.
   

  0 0
 • 08/20/18--02:37: TAARIFA KWA UMMA
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  OFISI YA MAKAMU WA RAIS
   

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ndugu January Makamba (Mb), leo anaanza ziara ya mikoa 19 nchini, ambayo itafanyika kwa awamu tatu. Ziara hiyo inamadhumuni yafuatayo:-

  1. Kukagua, kutathmini na kuzungumza na viongozi, wataalam, watendaji na wananchi wa mikoa husika kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.

  Kama inavyofahamika, Sheria ya Mazingira, hasa vifungu vya 47, 51, 54, 56, na 58 (3), inatoa mamlaka kwa Waziri mwenye dhamana ya mazingira kutangaza, kutamka au kuamuru, kupita kwenye Gazeti la Serikali, baadhi ya maeneo nchini kuwa ni Maeneo Lindwa Kimazingira (Environmental Protected Area) au Maeneo Nyeti Kimazingira (Environmental Sensitive Area). 

  Nyenzo hizi zimewekwa ili kuyalinda maeneo muhimu kwa mifumo ya kiikolojia (ikiwemo vyanzo vya maji, mito, maziwa, mabwawa, milima na vilima, chemichemi, ardhi oevu, mazalia ya samaki, misitu, nk.) ambayo hayana ulinzi wa Sheria nyingine. Sheria imeweka vigezo kwa maeneo hayo.

   Ofisi ya Makamu wa Rais, kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), iliomba na kupokea kutoka katika Halmashauri mbalimbali nchini mapendekezo ya maeneo hayo. Jumla ya maeneo 77 yalipendekezwa, ikiwemo vyanzo muhimu vya maji, mazalia ya samaki na wanyama adimu, maeneo ya ardhi oevu, mabwawa, mito na chemichemi nyeti. Mikoa iliorodhesha maeneo hayo kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na Sheria. Katika awamu ya kwanza, maeneo takriban 20 yanatarajiwa kuhifadhiwa kwa kutumia Sheria ya Mazingira.

  Katika ziara yake, Ndugu Makamba anatarajia kuyaona maeneo hayo, kutathmini hoja na haja ya kuyahifadhi na kuzungumza na viongozi wa mikoa, halmashauri na wananchi katika maeneo hayo ilikubaini utayari na uwezo wao katika kusimamia uhifadhi mara maeneo hayo yatakapotangazwa. Vilevile, katika ziara hiyo, Ndugu Makamba atapokea mapendekezo ya maeneo mapya hasa pale ambapo mapendekezo yaliyotolewa awali hayakutokana na ushirikishwaji mpana. Orodha ya maeneo yanayopendekezwa itatolewa kadri ziara inavyoendelea katika kila mkoa.

  Awamu ya kwanza ya ziara hii, ambayo inaanza leo tarehe 20 Agosti hadi tarehe 6 Septemba 2018, inajumuisha mikoa ya Singida, Tabora, Simiyu, Geita, Mwanza, Mara, Arusha, na Manyara.

  2. Kufuatilia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi Mazingira ya 2004 katika ngazi za Serikali za Mitaa.

  Kama inavyofahamika, Sheria ya Mazingira pia imeweka taratibu na mifumo, ikiwemo ya kitaasisi, ya kusimamia hifadhi ya mazingira nchini na kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira. Sheria pia imeweka wajibu kwa mamlaka mbalimbali, ikiwemo Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Vifungu kuanzia 34 hadi 42 vya Sheria ya Mazingira vinahusu wajibu wa Sektretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

   Katika ziara yake, Ndugu Makamba pia atajionea na kuzungumza na viongozi wa mikoa na halmashauri mbalimbali katika mikoa hiyo ili kusaidiana nao na kuhakikisha kwamba matakwa ya Sheria kwa upande wa wajibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, ikiwemo uundwaji wa Kamati za Mazingira katika ngazi za vitongoji, vijiji na mitaa,yanatimizwa.

  Katika ziara hii, Waziri Makamba ataongozana pia na watendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuangalia namna ya kuwezesha makubaliano kati ya NEMC na halmashauri mbalimbali katika mikoa yote kuhusu masuala kadhaa ya ukaguzi na ufuatiliaji wa hifadhi ya mazingira.


  Imetolea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  20 Agosti 2018

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw.Gervais Abayeho alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo.Picha na Ikulu.

  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege Njombe Bi. Hana Kibopile (wa pili kulia), wakati akikagua Kiwanja hicho, mkoani Njombe. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka.
  A

  Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka, akimuonesha maeneo yaliyovamiwa na wananchi katika Kiwanja cha Ndege cha Njombe Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati alipokuwa akikagua kiwanja hicho.3

  Muonekano wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Njombe. Kiwanja hicho ni miongoni mwa viwanja 11 vilivyopo katika mpango wa kujengwa na Serikali ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika.

  ????????????????????????????????????

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoani humo.

  ????????????????????????????????????

  Muonekano wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania.

  ………………..

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Njombe na Halmashauri yake pamoja na uongozi wa kiwanja cha ndege cha mkoa huo kuona namna  ya kuziondoa nyumba zote zilizopo mita 500 kutoka katika kiwanja hicho ili kupisha ujenzi unaotarajiwa kufanyika katika kiwanja hicho hivi karibuni.

  Waziri Mhandisi Kamwelwe ametoa wito agizo hilo mkoani humo mara baada ya kutembelea kiwanja hicho na kujionea nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya kiwanja hicho.

  Amesema kuwa ujenzi wa makazi hayo umesababishwa na Halmashauri kupima viwanja mpaka kwenye maeneo ya kiwanja hicho hivyo ni lazima waangalie namna sahihi ya kuwahamisha wakazi hao kwa kuwalipa fidia kwa wale wnaaostahili.

  “Kiwanja hiki kipo eneo zuri la tambarare, lakini tumeona wenyewe wananchi wamejenga hadi magorofa katika maeneo karibu ya kiwanja hivyo ni lazima waondolewe ili kupisha ukarabati na watakaoonekana wanahaki ya kufidiwa wafidiwe,” amesema Waziri Mhandisi Kamwelwe.

  Aidha, Mhandisi Kamwelwe amefafanua kuwa eneo hilo ambalo limejengwa ndio linalotumiwa na ndege kupaa, hivyo kama itashindwa kupaa au kutua inaweza kutua juu ya paa la nyumba ya wakazi hao na kusababisha maafa.

  Ameongeza kuwa Serikali ina mpango wa kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa mkoani humo hivyo ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili
  kuhakikisha ujenzi huo unaanza.

  Waziri Kamwelwe ameeleza kuwa ukamilikaji wa ujenzi wa kiwanja hicho utawezesha usafirishaji wa maua yanayolimwa mkoani humo kwani limekuwa ni tatizo katika usafirishaji kwa kuwa hayawezi kukaa muda mrefu kwenye magari.

  Kwa upande wake Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa na Njombe, Bi. Hana Kibopile, amemshukuru Waziri huyo kwa kutoa agizo hilo kwani limekuja wakati muafaka kwa kuwa wananchi wanauhitaji sana na kiwanja hicho kwani mbali na eneo zuri pia kiwanja hicho kina historia kubwa sana.

  Katika hatua nyingine Waziri Kamwelwe amekagua  nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe na nyumba ya Katibu Tawala na ujenzi wa ofisi ambayo itakuwa ya Mkoa na kuwataka Wakala wa Majengo (TBA) kuhakikisha majengo ya Serikali yanazingatia ubora na viwango ili kupata thamani ya fedha katika miradi hiyo.


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (kushoto) akimuonyesha Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi aliyemwakilisha Katibu Mkuu Viwanda wa Wizara hiyo Bw. Joseph Simbakalia Sera ya viwanda endelevu: Mchango wa mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara mara baada ya kuwasili ofisi za ESRF kufungua mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene.

   Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba Katibu Mkuu Viwanda wa Wizara hiyo Bw. Joseph Simbakalia wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki na mgeni rasmi wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

   Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (katikati) aliyemwakilisha Katibu Mkuu Viwanda wa Wizara hiyo Bw. Joseph Simbakalia akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Sera ya viwanda endelevu: Mchango wa mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (wa pili kushoto), pamoja na waandishi wa Sera ya viwanda endelevu: Mchango wa mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara,  Kutoka kushoto ni Dr. Deusdeit Rwehumbiza (kushoto), Profesa Samuel Wangwe (wa pili kulia) na John Shilinde (kulia).

   Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (katikati) aliyemwakilisha Katibu Mkuu Viwanda wa Wizara hiyo Bw. Joseph Simbakalia, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (wa pili kushoto), pamoja na waandishi wa Sera ya viwanda endelevu: Mchango wa mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara Dr. Deusdeit Rwehumbiza (kushoto), Profesa Samuel Wangwe (wa pili kulia) na John Shilinde (kulia) kwa pamoja wakionyesha nakala ya sera hiyo iliyochapishwa CUTS International kwa ufadhili wa serikali ya Sweden.

   Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe akiwasilisha mada kuhusu mambo yanayostahili kuwepo katika sera mpya ya viwanda endelevu – SIDP- kwenye mkutano wa sita wa kitaifa wa mashauriano  wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam

   Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka serikalini, taasisi za kitaifa, wafanyabiashara , taasisi zisizo za kiserikali, waandishi wa habari, wanazuoni wawakilishi wa wakulima, makundi ya wanawake na wawakilishi kutoka UNFCCC wakishiriki katika mkutano  wa sera mpya ya viwanda endelevu. wakichangia mada wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi akichangia mada wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

  Sehemu ya washiriki kutoka washiriki kutoka serikalini, taasisi za kitaifa, wafanyabiashara , taasisi zisizo za kiserikali, waandishi wa habari, wanazuoni wawakilishi wa wakulima, makundi ya wanawake na wawakilishi kutoka UNFCCC wakishiriki katika mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.  SERIKALI ya Tanzania imesema kwamba itaendelea kuhimiza uwapo wa viwanda kila mkoa kama sehemu ya kuleta mabadiliko makubwa ya uchumi nchini kote.
  Aidha imesema itaendelea kuhakikisha kwamba maendeleo hayo yanasaidiwa na sera ya viwanda endelevu kwa lengo la kuliwezesha taifa kuwa na kipato cha kati kwa kutegemea uchumi wa viwanda.
  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Joseph Simbakalia katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Aristide Mbwasi wakati wa kongamano la sita kitaifa kwa ajili ya mradi wa PACT-EAC lililofanyika kwenye ukumbi ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
  Mkutano huo  wa wataalamu kutoka kada mbalimbali  nchini uliangalia uhusiano uliopo kati ya usindikaji wa bidhaa za kilimo, mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula pia  sera iliyopo.
  Washiriki wa kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) walitoka katika taasisi za serikali, wafanyabiashara vyama visivyo vya kiserikali, wanahabari, wanazuoni wakulima na wajasiriamali wa bidhaa zinazotokana na kilimo.Kwa mujibu wa Bw. Simbakalia kongamano hilo lilikuwa limelenga kuangalia hatua zilizofikiwa katika mchakato wa upitiaji Upya wa Sera ya Viwanda Endelevu (SIDP).
  Mwezi Machi mwaka 2018 huu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji ilijihusisha na kuangalia matokeo ya utafiti uliofanywa na ESRF kuhusu SIDP.
  Kwa niaba ya serikali aliipongeza ESRF na CUTS international yenye makao makuu yake Geneva Uswiss kwa kuisaidia Wizara ya Viwanda kuiangalia upya SIDP ili kuwa na sera ambayo inazingatia mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula kwa kuangalia uchakataji wa mazao ya kilimo.
  Sera Endelevu ya Maendeleo ya Viwanda (SIDP) (1996-2020) imeshatekelezwa katika hatua tatu ambapo ya kwanza ilianza 1996-2000 ikijikita zaidi katika ukarabati na uimarishaji wa uwezo wa viwanda vilivyokuwepo. Hatua ya pili (2000-2010) ilikuwa ni uzalishaji mpya wa uwezo kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia na kujifunza; wakati awamu ya tatu (2010-2020) imelenga kufikia matokeo makubwa kwenye uwekezaji katika viwanda bidhaa mbalimbali na kuimarisha viwanda vilivyokuwapo na vilivyoundwa katika awamu zilizopita.
  Bw. Simbakalia alisema kwamba kwa miaka mingi Sera Endelevu ya Maendeleo ya Viwanda (SIDP) imekuwa ikisaidiwa na sera kadhaa, mikakati na mipango mbalimbali ikiwamo mkakati wa maendeleo unaohusisha sekta mbalimbali ya mwaka 2025 na mpango wa maendeleo wa muda mrefu unaotekelezwa kwa hatua za miaka mitano mitano.
  Mipango mingine ni kuimarisha kilimo, biashara na utumiaji wa taasisi za fedha kuendeleza ujasiriamali na kilimo.“ Hakuna shaka kwamba harakati za kuwa na viwanda zimechanganywa vilivyo katika mipango ya maendeleo ya kitaifa. Hata hivyo athari za mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara ya bidhaa za kilimo zilizochakatwa, zimekuwa hazihusishwi sana katika mipango hiyo ya maendeleo na utekelezaji wake” alisema Simbakalia.
  Katibu huyo alisema anafahamu kwamba mkutano huo ni muhimu katika kuongeza vionjo vitakavyosaidia kuangalia upya sera ya sasa iliyopo ili kuifanya iendane na wakati huu ambapo kuna changamoto  kubwa katika mabadiliko ya tabia nchi.
  Naye Mkurugenzi Mtedaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida alisema wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuhutubia alisema kwamba mkutano huo kuwa taasisi yake imepitia kwa ukamilifu SIDP kwa lengo la kuwawezesha watunga sera namna nzuri ya kuboresha sera iliyopo sasa ya viwanda endelevu.Aliongeza  kwamba mkutano huo wa kitaifa wa sita wa mradi wenye lengo la kuboresha kilimo kwa kuangalia mabadiliko ya tabia nchi na biashara Afrika Mashariki (PACT EAC2), umeitishwa ili kuwapa wajumbe taarifa ya hali halisi ilivyo kwa sasa katika SIDP.
  Alisema washiriki pia watapata nafasi ya kutaarifiwa hali halisi ilivyo sasa na majadiliano yanayoendelea huko WTO na UNFCC.Alisema ni kweli kuwa kunahitajika mabadiliko katika SIDP ambayo tangu awali ilikuwa haielezei uhusiano uliopo kati ya kilimo, uchakataji mazao ya kilimo, usalama wa chakula na mabadiliko ya tabia nchi.
  Mkurugenzi alisema pia mkutano huo ambao utawasaidia washiriki kutambua hatua iliyofikiwa na SIDP ili kuiwezesha kuwa na uhuishaji wa sera hizo na hali halisi ya sasa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.Dkt. Kida alisema pamoja na upitiaji huo sekta binafsi imeonekana kuwa muhimu katika utekelezaji wa SIDP na kwamba mafanikio katika mchakato wake wa sasa unaweza kuambukizwa pia kwa Afrika Mashariki kupitia EAC Private Sector Development Strategy (PSDS) (2018 – 2022).

  0 0


  0 0


  Kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa na Klabu ya mpira wa miguu ya Uingereza ya Everton zimezawadiwa zawadi kutokana na ushirikiano wao kwenye tuzo za Sports Industry Awards kwenye vipengele vya Best African Sponsorship na Pan-African Campaign of the year.

  Kwenye udhamini huo ambao ulianza kwa klabu ya Everton kusafiri kwenda Dar es Salaam Julai 2017 kucheza na Mabingwa wa SportPesa Super Cup ambao walikuwa klabu ya Gor Mahia kutoka Kenya, umetambuliwa na kusherekewa kwa kuwaleta Everton wanaoshiriki ligi kuu ya Uingereza kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza.

  Kutokana na mafanikio ya safari hiyo ambayo ilijulikana kama 'Everton in Tanzania' , ambayo pia ilileta hamasa kwenye michezo na kuipa ushindi wa tuzo hizo ambazo zilitangazwa Sandton Convention Centre jijini Johannesburg Ijumaa ya tarehe 17 Agosti 2018.

  Mkuu wa Ushirikiano na Utawala wa klabu ya Everton Mark Rollings alisema "Tunayo furaha kuwa ushirikiano wetu na SportPesa umetambulika kwenye ngazi
  muhimu ya Sports Industry Awards. Tuzo za Sports Industry Awards ndio tuzo zenye heshima kubwa Afrika Kusini kwa upande wa michezo na kwa hivyo kushinda tuzo zote mbili za Best African Sponsorship na Pan-African Campaign of
  the Year ni udhibitisho wa kuendeleza ushirikiano wetu na SportPesa pamoja na
  wadau wake.

  Mafanikio ya miezi kumi na mbili iliyopita na ishara nzuri ya ushirikiano wetu. Hata hivyo tunaangalia kwa mbeleni jinsi ya kudumisha ushirikiano huu na kuzidi kuwa na nguvu zaidi.

  SportPesa ni kampuni ya kubashiri michezo ambayo anafanya kazi zake Kenya,
  Tanzania, Afrika Kusini, Italia na UK. Ndio kampuni ya kubashiri michezo
  inayoongoza Afrika ambao inatoa bashiri zaidi ya 500 kila siku kwa wateja wake na wapenzi wa mpira kujishindia zawadi kem kem na pia inadhamini klabu za ligi kuu

  Mkurugenzi wa Utawalan na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema
  ‘Ni furaha kubwa kwa SportPesa na mimi binafsi kushuhudia heshima kubwa hii
  ambayo kampuni imepata kwa kushinda tuzo hizi. Tuzo hizi zitazidi kutupa hamasa ya kuendeleza michezo Barani Afrika na duniani kwa ujumla.

  Akizungumzia kuhusu kuandaa michezo hapa nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya
  Habari, Sanaa na Michezo Tanzania, Susan Mlawi alisema tuzo hizo ni muhimu sana kwa Afrika Mashariki.Amesema kuorodhesha na hatimaye kushinda tuzo za Sports Industry Awards kunaonyesha ni jinsi ngani Serikali inatumbua na kuungana mkono michezo nchini Tanzania.

  Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo inatoa pongezi kwa waandaji wa tuzo hizi kwa kufanya kazi ya uandaaji wa mafanikio. Hii ni ishara njema ya jinsi kumejitolea kuendeleza michezo nchini na kupeleka mpira wa miguu kwenye ngazi ya juu, na kufanya kazi
  kwa pamoja ili mchezo huo upate mafanikio kwa Tanzania na Afrika nzima.

  Klabu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia kwenye michuano ya kwanza ya
  SportPesa Super Cup kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam mbele ya mashabiki
  zaidi ya 35,000. Mchezo huo ulikuwa na historia kwa Afrika Mashariki kuweza kuwa na timu kutoka Ligi Kuu ya Uingereza kucheza jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza. Mabingwa wa SportPesa Super Cup, timu ya Gor Mahia kutoka Kenya itasafiri kwenda Uingereza kucheza na klabu ya Everton Novemba 2018 baada ya kutetea ubingwa wake kwa mwaka huu na kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika Mashariki kucheza na timu kutoka Ligi Kuu ya Uingereza mara mbili.
   Meneja masoko SportPesa South Afrika Gail Rodgers, Mkuu wa kitengo cha masoko SportPesa Kelvin Twissa, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Susan Mlawi, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas na Mkuu wa kitengo ca Ushirikiano Everton Mark Rollings mara baada ya kukabidhiwa tuzo za Sport Industry Awards.
   Wawakilishi kutoka SportPesa Tanzania, Kenya, South Africa,Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Tanzania, Timu ya Everton wakipokea tuzo mara baada ya kutangazwa kuwa washindi.
   Katibu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Susan Mlawi akiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas  wakiwa na tuzo mbili za Sport Industry Awards ambazo kampuni ya SportPesa imeshinda kwenye vipengele vyote viwili.


  0 0

  Amana Benki inaendelea kujivunia kuwa benki ya kwanza Tanzania inayoendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kiislamu, yenye malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee, kwa njia iliyowazi na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wateja na wadau wote. Amana Benki kwa takribani miaka saba sasa imekuwa kwa kasi huku ikihudumia watu wote bila kubagua dini zao.

  Katika kurahisisha kutoa huduma za kibenki kwa wateja, Amana Bank imekuwa ikiwafikia wateja kwa njia mbalimbali ikiwemo matawi yake, mawakala, huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi na intaneti na hata ikibidi kuwafata wateja mahali walipo.

  Kwa mujibu wa benki hiyo mnamo mapema mwezi Agosti,imezindua rasmi njia rahisi ya mawasiliano na wateja wake kwa kutumia mfumo mpya wa njia ya simu maarufu kwa jina la Whatsapp.

  Kwa sasa wateja wa benki hiyo na watu wote kwa ujumla wanaweza kutumia programu ya simu ya mkononi maarufu kwa jina la Whatsapp kupata huduma moja kwa moja kutoka kitengo cha huduma kwa wateja kupitia namba 0657 980 000.

  Akizungumza ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Benki Dkt Muhsin Salim Masoud alisema kuwa “tumeshawishika kuanza kutumia mtandao wa WhatsApp katika kitengo chetu cha huduma kwa wateja ili kwenda sambamba na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika kuboresha huduma kwa wateja wetu,  matumizi ya WhatsApp yatawezesha wateja wetu kuwasiliana na kitengo chetu cha huduma kwa wateja hata wakiwa nje ya nchi au mahali popote ambapo hawawezi kupiga simu ya kawaida”. Aliongeza kuwa kwa sasa matumizi ya mawasiliano kwa njia ya WhatsApp na Intaneti kwa ujumla yameshika kasi kubwa hivyo ni busara kutumia njia hii ilikuwapa fursa na urahisi watu na wateja wenye kumudu kutumia njia hii kupata huduma kwa wepesi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dk. Muhsin Salim Masoud akizungumza jambo wakati akizungumzia huduma ya mtandao wa WhatsApp katika kitengo cha huduma kwa wateja ili kwenda sambamba na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika kuboresha huduma kwa wateja.

  Teknolojia inakua kwa kasi sana na wateja sasahivi wanahitaji njia mbadala na rahisi ili waweze kuwasiliana na kupata taarifa za kibenki kwa muda wowote. Hii ndio sababu inayotusukuma kubuni namna ya kurahisisha njia zetu za mawasiliano na wateja popote pale walipo”, alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Biashara Bw. Dassu Mussa.

  Njia hii itawawezesha watu wote wanaotumia simu pendwa (smart phone) zilizomo katika mfumo wa IOS na Android kuweza kupata huduma mara moja bila ulazima wa kufika katika matawi ya Amana Benki.

  Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Benki ametoa rai kwa watu kutumia njia hii ya mawasiliano vizuri ili kupata huduma kwa wakati na ameahidi kuwa Amana Benki itaendelea kutoa huduma bora za kibenki kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wadau wote.


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma bi. Sophia Kizigo alikerwa na uhaba wa maji katika mji wa Namtumbo na kuagiza mamlaka ya maji mjini Namtumbo kuanzisha mkakati wa makusudi kunusuru hali hiyo.

  Akipokea taarifa za idara na vitengo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Mh.Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Drt. John PombeMagufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

  Aidha mkuu wa wilaya huyo alionesha kukerwa na uhaba wa maji katika mji wa Namtumbo na kuitaka mamlaka ya maji mjini Namtumbo kuanzisha mkakati wamaksudi ilikutatua tatizo la uhaba wa maji Mjini hapa.

  Mohamedi Mmbaga kaimu Meneja wa mamlaka ya maji mjini Namtumbo (NAUWASA)alimwambia mkuu wa wilaya hiyo tatizo la uhaba w a maji huo linalotokana na miundombinu ya maji inayotegemewa ni ya kijiji na sio yawilaya.Bwana Mmbaga alidai mradi wa unaotumika mjiniNamtumbo ulijengwa mwaka 1981 ukihudumia vijiji vine ambavyo ni Libango,Suluti,NahoronaLuegu na kiasi cha maji kinachozalishwa ni mita zaujazo 1,211 kwa siku huku mita zaujazo 580 pekee kwa siku ndizo zinazofika na kutumika.

  Mmbaga pia alidai kiasi hicho cha maji ni kidogo ukulinganisha na watu wanaohitaji huduma hiyo ni 40,697 mpaka sasa niwatu 8,932 ambao wanapata huduma hii sawa na asilimia 21 na kuwaachan watu 31,765 kukosa huduma hiyo.

  Pamoja na hayo Mamlaka ya maj iMjin I Namtumbo kwa kushirikiana na Mamlaka ya maj I safi na usafi wa Mazingira manispaa ya Songea inatekeleza mradi wa maji mjini Namtumbo kwa kukarabat I bomba kuu umbali wa km.1.08 na pia ujenzi watenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa M135 ambapo mradi huo ulifikia asilimia 82 na utachangia ongezeko la maji kwa asilimia 14katika mji wa Namtumbo pamoja nautekelezaji wa mradi wa maji wa mto Rwinga ambao na utaongeza kiasi mita zaujazo 1000 kwasiku.

  Wilaya ya Namtumbo ilitangazwa kuwa wilaya mwaka 2002 ambapo miundo mbinu ya maji katika mji wa Namtumbo ilikuwa ya vijiji na sasa ni makao makuu ya wilaya ambapo panaongezeko kubwa la watu wakihitaji huduma hiyo ya maji huku miundombinu ni ya mwaka 1981.

  0 0

   Mabingwa wa Mashindano ya Mpira wa Miguu yanayoandaliwa na CLOUDS MEDIA GROUP,ambayo ni NDONDO CUP. Leo 20August 2018 wamefika Ofisini kwa Mstahiki Meya  Boniface Jacob na kulikabidhi kombe hilo kama ishara ya Shukrani kwa Uongozi wa Manispaa ya Ubungo na Mshikamano na wanamichezo. Mstahiki Meya amehaidi ushirikiano wanamichezo wote wa Ubungo watakao kuwa wanaiwakilisha manispaa kwenye michuano mbalimbali.
  Picha ya pamoja baada ya meya wa ubungo kupokea kombe.

  0 0

  Na Gaudensia Simwanza – Urambo.

  TFDA kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora, wanaendesha mafunzo ya siku tano kwa wajasiriamali wadogo 150 wa usindikaji wa vyakula wilayani humo kuanzia leo tarehe 20/8/2018  ili kuchangia  ukuaji wa Sekta ya viwanda nchini sanjari na kuinua uchumi wa wananchi wa Urambo.

  Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Angelina Kwingwa na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa Wilaya hiyo wakiwemo Mbunge,  Mhe. Margareth Sitta (Mb.), Katibu wa CCM wa wilaya, Bi. Jesca Mbogo na Mkurugenzi wa wilaya, Bi. Margareth Nakainga miongoni mwa viongozi wengine.

  ”TFDA inatambua mchango mlio nao katika kukuza viwanda vidogo vya chakula kwani kutokana na uwingi wake vina mchango mkubwa katika; kuongeza ajira na kipato katika ngazi ya kaya, kukuza kilimo cha mazao ya chakula na kuyasindika na hatimaye kuiwezesha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025”, alisisitiza Mgeni Rasmi huyo.

  Ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini kutatua changamoto zinazowakabili katika usajili wa majengo na bidhaa zao, uongozi wa Wilaya umeamua kuweka mkakati wa makusudi ikiwa ni pamoja na kuwaalika wataalam wa Serikali kuja kutoa mafunzo kama haya ili kuinua maisha ya wananchi wake na Taifa kwa ujumla”, Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza.

  TFDA inaendelea kushirikiana uongozi wa Mikoa na Halmashauri zake ili kuwawezesha Watanzania kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwa kuzingatia vigezo vya usalama na ubora ili kupata soko la ndani na nje ya nchi kwa bidhaa zetu kwa maendeleo ya Taifa
   Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Angelina Kwingwa, (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo yanayoendeshwa na TFDA kwa Wajasiriamali wa Wilaya ya Urambo. Viongozi wengine wa wilaya hiyo kutoka kushoto ni Mbunge wa wilaya Mhe. Margareth Sitta (wa tano), Mkurugenzi wa wilaya, Bi. Margareth Nakainga (wa sita), Meneja wa TFDA Kanda ya Magharibi, Dkt. Edgar Mahundi (wa saba), Katibu wa (CCM) wa wilaya, Bi. Jesca Mbogo (wa tatu), na Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Martha Susu (wa n ne).
   Mbunge wa wilaya ya Urambo Mhe. Margareth Sitta (aliyesimama), akiwasalimia wajasiriamali wanaohudhuria mafunzo wilayani Urambo.
  Sehemu ya Wajasiriamali  wilaya ya Urambo wakifuatilia mafunzo yanayotolewa na (TFDA).

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

  MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)kwa kushirikiana na Taasisi ya mafunzo ya masoko ya Mitaji na uwekezaji (CISI) wamezindua mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).

  Ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati ya kuwajengea uwezo na kuimarisha ufanisi kwa watendaji na wataalamu wanaishiriki katika mitaji ili kufikia viwango vya ubora wa kimataifa,
  (EASRA).

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo jijini Dar es Salaam Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama amesema,    mpango huo unaweka utaratibu na vigezo vya ushiriki kwa washiriki wa masoko ya mitaji kufikia angalau masaa 10 ya ushiriki wa mafunzo ya masoko ya mitaji kwa mwaka.

  Na kuwa hiyo itakuwa kigezo kimojawapo cha utoaji wa lesebi ya ushiriki katika masoko ya mitaji ifikapo Januari mwaka 2020.

  Ameongeza kuwa washiriki wa masoko ya mitaji walio na leseni watatakiwa kufanya mafunzo na kutekeleza mipango inayotambuliwa na CMSA na CISI katika kutekeleza vigezo vya mpango wa mafunzo endelevu na kupewa idhini itakayotolewa kwa taarifa maalumu itayowasilishwa CMSA kwa ajili ya taarifa na kuweka kumbukumbu.

  " Mpango wa mafunzo endelevu utawawezesha watendaji ndani ya masoko ya mitaji kutoa huduma kwa umahiri mkubwa zaidi kwa kuendana na maendeleo yanayotokea katika masoko ya mitaji duniani,"amesema Mkama na kuongeza.

  "Ushirikiano kati ya Mamlaka ya taasisi ya CISI unayaweka masoko ya mitaji ya Tanzania katika ramani ya masoko ya mitaji ya dunia kwa kuwa na wataalamu wanaokidhi viwango vhhya kimataifa," amesema.

  Kwa upande wa Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya CMSA, Emmanuel Kakwezi kwa niaba ya mwenyekiti, ameitaka mamlaka kuhakikisha inakuwa na wataalamu wa kutosha katika masoko ya mitaji wanajiunga na mpango huo ili kulinda uwezo wa kitaaluma na uhalali wao katika ulimwengu wa ushindani.

  Amesema masoko ya mitaji ni sekta inayobadilika kwa kasi na yenye kuhusisha viashiria vya aina mbali mbali,

  Wakati huo huo Mkurugenzi wa DCSI, Kevin Moore ushirikiano huo utawawezesha watanzania kuongeza uwezo wa kuelewa kwa nji ya mitandao na hata ile njia halisi.

  Pia amesema mafunzo hayo endelevu yatasaidia wataalamu na kuifanya Tanzania kuendelea kuongeza ufanisi katika soko la kimataifa.
     Mjumbe wa Bodi  ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Masoko ya mitaji na dhamana, Emmanuel Kakwezi akisoma taarifa yake kuashiria uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).
  Mkurugenzi wa CISI,  Kevin Moore akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).
  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama akielezea umuhimu wa wa mpango wa ushirikiano wa CMSA na CISI kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).

older | 1 | .... | 1652 | 1653 | (Page 1654) | 1655 | 1656 | .... | 1897 | newer