Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1651 | 1652 | (Page 1653) | 1654 | 1655 | .... | 1898 | newer

  0 0

   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Njia panda ya Bugando mjini Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea Chato mkoani Geita. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza kuelekea Chato mkoani Geita.

  0 0


  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa ameambatana na Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai na baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wamemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla kwa lengo la kumjulia hali katika Hospitali ya Taifa ya Muhumbili alikolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari.

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla baada ya kumtembelea kwa lengo la kumjulia katika Hospitali ya Taifa ya Mhumbili alikolazwa kw ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari.

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla baada ya kumtembelea kwa lengo la kumjulia katika Hospitali ya Taifa ya Mhumbili alikolazwa kw ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari.

  0 0


  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kushoto akipokea zawadi ya mtungi wa kiasili kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida mara baada ya kufanya mazungumzo katika ofisi ndogo ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam leo. Picha na Mpiga Picha Wetu. 

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizungumza na watendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kuhusu mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya sekta za mifugo na uvuvi alipowatembelea ofisini kwao Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa TPSF, Godfey Sembeye. Picha na Mpiga Picha Wetu
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (kushoto) na Naibu Gavana wa Benki Kuu anayeshughulikia Uchumi na Fedha, Dk. Yamungu Kayandabila mara baada ya kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa benki hiyo alipowatembelea ofisini kwao Dar es Salaam.

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kulia) akifurahia jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (kushoto) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya BOT Dar es Salaam . 
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kulia) akiagana na Balozi waJapan nchini, Masaharu Yoshida mara baada ya kufanya mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dar es Salaam

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (Gavu) alipowasili katika uzinduzi wa Kongamano la tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukumbi katika kiwanja cha Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.] 18 Aug 2018.

  Baadhi ya Wanadiaspora wakisimama wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Wimbo wa Taifa wa Zanzibar na Tanzania wakati wa Uzinduzi wa Kongamano la la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukuimbi wa Uwanja wa Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), [Picha na Ikulu.] 18 Aug 2018.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakipiga makofi baada ya wimbo wa Taifa wa Zanzibar,Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioimbwa katika Kongamano la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukuimbi wa Uwanja wa Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.] 18 Aug 2018.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Viongozi mbali mbali na wanadiaspora katika Kongamano la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukuimbi wa Uwanja wa Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.] 18 Aug 2018.
  Baadhi ya Wanadiaspora wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzanao pamoja na Viongozi mbali mbali katika Kongamano la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukuimbi wa Uwanja wa Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.] 18 Aug 2018.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Tabora kiichopo kwenye Manispaa hiyo, Agosti 18, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Urvesh Rajani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Tabora kiichopo kwenye Manispaa hiyo, Agosti 18, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha nyuzi cha Tabora, Urvesh Rajani (kulia) kuhusu pamba chafu wakati alipotembelea kiwanda hicho katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia akinamama waliojifungua katika wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete Agosti 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua chumba cha upasuaji kilichojengwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete wakati alipotembela hospitali hiyo katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0
 • 08/18/18--12:16: TANZIA


 • 0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za kisasa wa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B”leo,[Picha na Ikulu]. 18Aug 2018. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maopinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ta Nyumba kwa Bibi Yasmin Din na Mumewem Khalil Din wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za kisasa wa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B”leo,[Picha na Ikulu]. 18Aug 2018. 

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipotembelea Nyumba ya Bw.Khalil Din ikiwa ni miongoni mwa Nyumba Sitini zilizokabidhiwa wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za kisasa wa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B”leo,[Picha na Ikulu]. 18Aug 2018. 

  Miongoni mwa Nyumba za Kisasa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B” ambazo leo jumla ya Nyumba 60 zimekabidhiwa katika sherehe za uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) [Picha na Ikulu]. 18Aug 2018. 
  Wananchi waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za kisasa wa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B”leo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake,[Picha na Ikulu].18/08/2018.

  0 0


  KIJANA wa Chipukizi akimvisha kwa ukakamavu shada la maua maalum aina ya Koja Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza visiwani Zanzibar.

  Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Haji Haidar ambaye ni mmoja kati ya viongozi mbali mbali walioshiriki katika mapokezi hayo.


  KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally, akiwa na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakipokea maandamano ya vijana na Wana-CCM walioshiriki katika mapokezi hayo.  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk.Bashiru Ally amezitadharisha baadhi ya nchi za kigeni kuacha tabia ya kuingilia siasa za ndani ya nchi.

  Amesema lazima nchi hizo hasa zenye balozi Tanzania ziheshimu Katiba na miongozo ya kisheria ya nchi, vinginevyo Tanzania itashindwa kuvumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya balozi nazowakilisha nchi hizo Tanzania.

  Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika viwanja vya Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar makuu, Dk. Bashiru amesisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru linalojitawala lenyewe na hakuna nchi yoyote itakayoweza kuyumbisha demokrasia ya nchi hiyo.

  Amesema kumejitokeza baadhi ya mataifa yanayojifanya viranja wa demokrasia ambayo yamekuwa na tabia ya kutoa matamko ya kuhusu ushindi wa CCM wakati haijasajiliwa kufanya kazi za kisiasa.

  Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa katika siku za hivi karibuni kumetokea taifa moja la kibeberu linatuma matamko kwenye mitandao ya kubeza ushindi wa CCM hivyo wanatakiwa waheshimu utawala na demokrasia ilioko nchini.

  Dk.Bashiru amefafanua kuwa hakuna taifa lenye haki ya kubeza ushindi wa CCM inaoupata katika chaguzi ndogo zinazofanyika nchni, kwani kufanya hivyo ni kuingilia siasa za ndani za taifa hili. Katika maelezo yake amebainisha kwamba kinachotakiwa kitambulike ni kuwa CCM haitishwi na matamko ya aina hiyo ya kuibeza na kwamba hawache kuidharau.

  Amesema Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya demokrasia ya kweli kwa kupitia misingi ya Azimio la Arusha na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 hivyo waache kuingilia shughuli za uendeshaji wa Tanzania. Amesema wanaandika matamko ya uongo ya kudanganya ulimwengu ya kuwa Tanzania hakuna uhuru na CCM ina iba kura kwenye uchaguzi na wanatakiwa kutambua CCM imeshinda kutokana na kuwa wananchi wamekuwa na matumaini na CCM katika kutekeleza ilani zake.

  Dk.Bashiru ameongeza kwa kusema kuwa uhuru wowote wa taifa haupatikani ovyo katika kujitawala, hivyo vijana wanatakiwa kuzingatia historia ya ukombozi wa taifa la Tanzania ili kuendeleza kudumisha amani iliyopo. Aidha alisema, CCM imeamua kulinda rasilimani, mali na utu wake bila ya kuhitaji msaada wa viranja hao wa demokrasia katika utawala wao.

  ” hatutwishi wa vipeperushi vinavyoitwa vipeperushi, na rafiki wa
  kweli ni yule anayebeleza maelewano, ambapo nchi yetu ni ndogo ila
  tunaendeleza na mapambano ila hatutwishi na watu na wala hatuwezi
  kuingiliwa kwani hatupo tayari kuingiliwa katika kuongozwa na
  tutaendelea kujiongoza wenyewe” alisema.

  Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa uhuru huu ambao upo wa kujitawala umepiganiwa na haojapewa kwenye kupitia sahani ama msaada, hivyo aliwataka mataifa hayo makubwa na madogo kupitia balozi zake kuacha kudharau CCM ambayo imekomboa uhuru wa kujitawala. Akizungumzia dhana ya CCM mpya na Tanzania mpya alisema zinatakiwa kutekelezwa kwa vitendo kwa kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi ndani ya chama ili kiweze kuwa na nguvu za kutosha za kuendesha mambo yake chenyewe.

  Amesema pia dhana hiyo imelenga kudhibiti vitendo vyote vya rushwa, ubinafsi na makundi maovu yaliyodhoofisha taasisi hiyo ya kisiasa kwa muda mrefu. Katika hatua nyingine Dk.Bashiru amewaonya baadhi ya Wana-ccm walioanza kusaka nafasi za uongozi hasa Urais kabla ya muda wake na kuwambia kuwa wasipoacha tabia hiyo watashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za kimaadili ndani ya Chama Cha Mapinduzi

  Aliongeza kuwa bado Zanzibar ina Rais wake na hajamaliza muda wake hivyo hakuna haja ya watu kuanza kampeni za kusaka kiti hicho. Kupitia mkutano huo Dk.Bashiru amewapokea vigogo wawili ACT wazalendo visiwani humu ambao ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Ramadhani Suleiman na Katibu Mkuu wake Khamis Ali Lila amabye aliyewai kugombe nafasi ya urais mwaka 2016.

  Pia amewapokea wanachama 35 kutoka Chama cha CUF, ambao wote walikuwa ni wanachama wa CUF katika maskani maarufu ya Mtendeni Mkoa wa Kusini Unguja kijiji cha Makunduchi, na wote wamejiunga na CCM. Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Zanzibar Abdulla Juma Saadalla(Mabodi), amesema chama kimejipanga vizuri na wanachama katika ngazi zote tayari wameshashuka nyumba kwa nyumba kujua changamoto zinazowakabili wananchi ili zifanyiwe kazi kwa vitendo.

  Pamoja na hayo ameongeza kuwa CCM itaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 kwa vitendo ili wananchi waendelee kunufaika na maendeleo yanayoletwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Dk. Mabodi ameahidi kulinda,kuendeleza na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na kulinda kwa vitendo Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwani ndio sehemu ya kudumisha udugu uliopo baina ya nchi hizo mbili zilizoungana zote zikiwa huru.

  Mapema akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib amesema hali ya kisiasa katika mkoa huo ipo shwari na CCM imeendelea kuimarika zaidi kutokana na sera zake nzuri zinazokubalika na makundi yote katika jamii.

  0 0


  Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika mjini Windhoek, Namibia, kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti 2018, umemteua Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha Agosti 2018 mpaka Agosti 2019. 

  Kufuatia uteuzi huo, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapewa rasmi jukumu la Uenyekiti wa SADC katika Mkutano mkuu ujao wa 39 utakaofanyika Tanzania mwezi Agosti 2019. 
  Makamu wa wa Rais Mhe .Samia Suluhu Hasan akitoa hutuba ya kushukuru mara baaada ya Tanzania kukabidhiwa Umakamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika - SADC katika ukumbi wa Mikutano katika hoteli ya SAFARI COURT ,Windhoek Namibia,leo Jumamosi tarehe 18 Agosti 2018.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa kwenye siku ya mwisho ya mkutano wa 38 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo mjini Windhoek Namibia ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha Agosti 2018 hadi Agosti 2019. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini moja kati ya nyaraka nne za kisheria ambazo ni Tamko la Kutokomeza Malaria katika ukanda wa SADC, Itifaki ya Kulinda Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina mpya za Mbegu za mimea katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, itifaki ya ajira na kazi pamoja na Maboresho ya Katiba inayosimamia masuala ya kamati Ndogo ya Wakuu wa Polisi katika Organ. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda, Mhe. Cyril Ramaphosa akikabidhi nafasi ya Uenyekiti kwa mwenyekiti mpya na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Hage Geingob. 
  Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akihutubia mara baada ya kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa SADC mjini Windhoek, Namibia ambapo aliishukuru Serikali ya Afrika kusini kwa uongozi mahiri kwa kipindi chote cha uongozi wake na aliahidi kushirikiana na wanachama wote katika kuiletea kanda maendeleo na kupunguza umasikini.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika mjini Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti 2018.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifuatilia ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali mjini Windhoek, Namibia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afika Kusini, Mhe Lindiwe Sisuli.
  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Adolf Mkenda akifuatilia hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali mjini Windhoek, Namibia.
  Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena L. Tax akitoa hotua ya ufunguzi wa mkutano pamoja na taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa Jumuiya ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi waliomaliza muda na nchi wanachama kwa ushirikiano walioutoa katika utekelezaji wa malengo na mipango mbalimbali ya kanda.
  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda, Mhe. Cyril Ramaphosa akikabidhi nafasi ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Hage Geingob.

  Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akihutubia mara baada ya kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa SADC mjini Windhoek, Namibia ambapo aliishukuru Serikali ya Afrika kusini kwa uongozi mahiri kwa kipindi chote cha uongozi wake na aliahidi kushirikiana na wanachama wote katika kuiletea kanda maendeleo na kupunguza umasikini.

  Wanafunzi walioshinda shindano la insha wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax na Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Cyril Ramaphosa njini Windhoek ,Namibia.

  Sehemu nyingine ya Wanafunzi walioshinda shindano la insha wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena L. Tax na Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Cyril Ramaphosa njini Windhoek ,Namibia.
  Waandishi wa habari walioshinda shindano la mwandishi bora wa SADC katika radio, gazeti na televisheni wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax na Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Cyril Ramaphosa njini Windhoek ,Namibia.
  Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SMZ), Bw. Ali Juma Khamis pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikaiano wa Afrika Mashariki , Balozi Innocent Shiyo wakifuatilia mkutano.
  Kutoka Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu wakifuatilia mkutano.

  Wa pili kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Edwin Mhede pamoja na Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agness kayola (kulia) wakifuatilia mkutano.
  Kutoka kustoto ni Balozi wa Tanzania nchini Namibia mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Mhe. Sylisvester Ambokile na Naibu Mwanasheria Mkuu, Bw. Evaristo Longopa wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mkutano.
  Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania ukifuatilia mkutano.

  Sehemu nyingine ya ujumbe huo ukifuatilia mkutano.

  Waasisi wa SADC wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Tiafa wa Namibia na wimbo wa SADC ukipigwa, kushoto ni Rais mstaafu wa kwanza wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Sam Nujoma na kulia kwake ni Rais wa mstaafu wa kwanza wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Joaquim Chissano.
  Wake za Waheshimiwa marais walifuatilia hafla ufunguzi wa Mkutano

  Picha ya pamoja


  0 0

  Bi.Monica Joseph Magufuli enzi za uhai wake

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Ragati, Jimbo la Mwibara, Wilayani ya Bunda, mkoani Mara, jana. Katika hotuba yake, Lugola aliwaonya Polisi nchini ambao wanatumiwa na mafisadi kuwanyanyasa wananchi maskini kwa kupora ardhi zao na kukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha ardhi hiyo kuwa ni mali yao.

  Na Felix Mwagara, MOHA

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewaonya Polisi nchini ambao wanatumiwa na mafisadi kuwanyanyasa wananchi maskini kwa kupora ardhi zao na kukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha ardhi hiyo iwe mali yao.

  Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Ragati, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Lugola alisema amepata malalamiko mengi kutoka sehemu mbalimbali nchini, kuwa mafisadi uonea wananchi maskini kwa kupora kwa nguvu ardhi wakidai wanamiliki wao na wanatumia badhi ya polisi wasiokua waaminifu ili kuwakandamiza wananchi hao.

  Kutokana na hatua hiyo, Lugola amepiga marufuku kwa mwananchi yeyote ambaye anakurupuka kukimbilia kituo cha polisi kufungua kesi za ardhi ambazo hazina uthibitisho wa jinai yoyote, badala yake kesi au malalamiko yake kwanza ayapeleke katika mabaraza ya ardhi katika eneo husika ili ziweze kutatuliwa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akiliangalia panga alilopewa na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ikiwa ni kiashiria cha kupewa ushujaa katika jamii ya Kabila la Wagita, mara baada ya Waziri huyo kumaliza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibara, Mkoani Mara, jana. Katika hotuba yake, Lugola aliwaonya Polisi nchini ambao wanatumiwa na mafisadi kuwanyanyasa wananchi maskini kwa kupora ardhi zao na kukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha ardhi hiyo kuwa ni mali yao.

  Lugola ameongeza kuwa, mafisadi hao ambao wanafedha baada ya kuona mmiliki halali wa ardhi hiyo anagoma kuondoka katika sehemu husika, basi utumia fedha zake kwa kukimbilia polisi kufungua kesi bila ya kuwa na uthitisho wowote huku baadhi ya polisi wasiokua waaminifu wakitumiwa katika kufanikisha ardhi hiyo ananyang’anywa mwananchi huyo.

  “Kuanzia leo mwananchi yeyote atakaeenda kufungua kesi kituo cha polisi inayohusu masuala ya ardhi na endapo kiwanja hicho kimepimwa lazima awe na hati inayoonyesha yeye ni mmiliki halali, ili iwasaidie polisi wajue wewe ndio mmiliki halali, na kwa upande wa ardhi ambayo haijapimwa lazima mwananchi huyo aende polisi akiwa na uthibitisho kutoka kijijini au katika mtaa unaosema kwamba eneo hilo ni la kwako na polisi wathibitishe hilo,” alisema Lugola.

  Lugola aliongeza kuwa, na endapo kesi ya mlalamikaji yeyote ipo mahakamani anapaswa kuheshimu makahama na si kuendeleza kufanya usumbufu katika jamii pamoja na kwenda polisi na kuanza kutafuta njia ya kumsumbua mwananchi ambaye ni maskini katika eneo hilo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimkabidhi zawadi ya shilingi 250,000, mshindi wa kwanza wa Bonanza la Kangi la mpira wa miguu lililofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ragati, Jimbo la Mwibara, Wilayani ya Bunda, mkoani Mara. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Katika hilo, Lugola alifafanua kuwa, endapo mwananchi ana hukumu ya mahakamani inayoonyesha ameshinda kesi hiyo, mwananchi huyo anapaswa kwenda polisi na nakala ya hukumu yake ili polisi waweze kushuhudia kwamba pande zote mbili ziliwahi kugombana kuhusu ardhi na kufikishana mahakamani lakini mmojawapo alishinda.

  “Rais Magufuli alianzisha Mahakama ya mafisadi hapa nchini, kwa taarifa niliokua nayo, mahakama hii ina uhaba wa mafisadi, sasa mimi nitaitafutia wateja kwa kuhakikisha wale mafisadi ambao uonea wananchi, utesa wananchi, uiba fedha za serikali au taasisi yoyote nitawafikisha katika mahakama hiyo, hatutakubaliana na manyanyaso ya aina yoyote katika Serikali hii ya awamu ya tano” alisema Lugola.

  Lugola aliongeza kua, hataki kusikia mwananchi anaonewa, na pia aliapa hatacheka na mafisadi, atapambana nao sehemu yoyote nchini na pia yupo tayari kwalolote na ameanza kupambana na mafisadi ndani ya wizara yake na tayari wameanza kurudisha fedha za Serikali. Aidha, Lugola katika hotuba yake alipiga marufuku kwa waendesha bodaboda wenye tabia ya kubeba abiria zaidi ya mmoja kuiacha tabia hiyo ili kuepusha ajali, lakini aliwataka polisi kutorudi nyuma, wahakikishe wanawakamata waendesha bodaboda wasiofuata sheria za usalama barabarani.

  Waziri Lugola yupo katika ziara jimboni kwake kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuwaunganisha wananchi kupitia Bonanza lake la michezo ya mpira wa miguu ambalo linashirikisha kila kata wakitoa washindi mbalimbali ambao anawapa zawadi pamoja na kuingia moja kwa moja katika mashindano ya kugombea Kombe la Kangi.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Elimu ya Juu , Mafunzo na Ubunifu wa Namibia Mhe. Dkt. Itah Kandjii-Murangi muda mfupi kabla ya kupanda ndege katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako tayari kwa safari ya kurudi Tanzania mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kupanda ndege katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako tayari kwa safari ya kurudi Tanzania mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiaga Viongozi waliomsindikiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako tayari kwa safari ya kurudi Tanzania mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea zawadi ya tai, kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua kozi fupi ya tano ya Viongozi, iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimtunuku cheti Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James baada ya kuhitimu kozi fupi ya tano ya Viongozi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na washiriki wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira akitoa neno la shukrani baada ya kuhitimu kozi fupi ya tano ya Viongozi katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwasili katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam kufunga kozi ya siku tano ya viongozi.  Viongozi na Watumishi nchini wamekumbushwa kutanguliza mbele moyo wa uzalendo na masilahi mapana ya taifa wanapotekeleza majukumu yao ili kupeleka maendeleo ya taifa mbele na kuimarisha usalama wa taifa.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akifunga kozi fupi ya tano kwa viongozi iliyofanyika Chuo cha cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania (NDC) jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Mkuchika amesema, ni matumaini kuwa washiriki waliohudhuria kozi hiyo, utendaji wao wa kazi utabadilika kwa kuwa na tija kwani sasa mbinu zote zinazohusu namna ya kufikiri kimkakati, kufanya tathmini katika mambo mbalimbali ili kufikia maamuzi wamezipata.

  “Sasa mnatambua dhana ya usalama wa Taifa vema na kwa mapana zaidi, si kulinda mipaka na mali za wanajamii tu, bali pia inahusisha kutunza mazingira, kuwa na chakula cha kutosha, kupiga vita rushwa na madawa ya kulevya na mengine mengi ambayo ninyi mnayafahamu zaidi,” Mhe. Mkuchika amesema na kuongeza kuwa usalama wa watu ni muhimu kuliko jambo jingine lolote, hivyo masuala ya usalama yawe ni sehemu ya kuzingatia katika utendaji wa kila siku na hasa pale maamuzi yanayogusa masilahi ya nchi na jamii yanapotolewa.

  Aidha, Mhe. Mkuchika amesema, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kwa dhati kuipeleka nchi katika Uchumi wa Viwanda, lakini suala la rushwa limekuwa kikwazo kikubwa kufikia lengo hilo, hivyo ni jukumu la viongozi wote kutoa majawabu ya namna gani malengo yatafikiwa.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi -Tanzania, Luteni Jenerali Paul Massao ameishukuru Serikali kwa kuhakikisha viongozi na watumishi wengine wanahudhuria kozi hiyo muhimu kwa masilahi ya taifa.

  Jumla ya wahitimu 24 walikabidhiwa vyeti, baadhi yao wakiwa ni Waheshimiwa Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi Waandamizi wa Taasisi za Serikali.

  Mtaala wa kozi hiyo ulilenga katika masuala yanayohusu masilahi, uzalendo na dhana nzima ya usalama wa taifa.


  IMETOLEWA NA:
  KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
  OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
  TAREHE 18 AGOSTI, 2018

  0 0  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza na wanakijiji wa Rubambagwe plot (Chato) wakati alipokwenda kutoa pole kwenye msiba wa Patricia Tibengana Mazigo (75) aliyefariki juzi tarehe 16-8-2018 Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwafariji wafiwa wakati alipokwenda kutoa pole kwenye msiba wa Patricia Tibengana Mazigo (75) aliyefariki juzi tarehe 16-8-2018 Chato mkoani Geita.


  0 0


  Makamu wa Rais wa Botswana Mhe Slumber Tsogwane akipata picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji na viongozi mashuhuri huko Gaborone Botswana.

  Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akibadilishana mawazo na Mhe Maria Ndilla Kangoye ambae ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Kanda ya Afrika na pia Mbunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.

  Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Mabunge wanachama wa nchi za Jumuiya ya Madola tawi la Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said pamoja na Katibu wa tawi hilo ambae pia ni katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Msellem wakisikiliza mada zinazojadiliwa.

  Mwenyekiti wa kamati tendaji ya nchi wanachama wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola Mhe Simai Mohammed Said akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza kutoka Rodrigues Regional Assembly Mauritius Mhe Marie Pricie Anjela Speville, katikati ni Makamu wake Mhe Ramdally Jean Rex.

  Balozi wa Nigeria nchini Botswana HE Moses I. Adeoye (kati) akifurahia jambo pamoja na Naibu Spika Mhe Mgeni Hassan na Mhe Simai Mohammed Said. Kulia wa pili ni Mhe Kabiru Mjinyawa Spika wa Jimbo la Adamawa huko Nigeria.

  Maspika kutoka (kushoto) Uganda, Mauritius, Kenya na Zanzibar wakizungumza na wanachama wa mabunge yao katika kikao cha ndani za nchi za Afrika Mashariki.

  Wajumbe wanachama wa mabunge ya nchi za jumuiya ya madola kutoka kanda ya Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Seychelles, Mauritius, Rwanda na Zanzibar wakisikiliza mada zinazozungumziwa katika mkutano huo.

  Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi (MB) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Tawi la Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, kushoto Mjumbe wa Kamati Tendaji Afrika, Mbunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Maria Ndilla Kangoye.

  Kikundi cha sanaa kinachoitwa “Cultural Ensemble” wakitoa burudani watika Mkutano huo.

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi atakwenda katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ili kutatua kero kubwa za ardhi. Ameyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Agosti 18 ,2018) wakati akizungumza na wananchi wa Manispaa hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chipukizi.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo baada ya wabunge na wananchi kueleza changamoto kubwa zinazowakabili ikiwe ya migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018.

  “Waziri wa Ardhi atakuja hapa na ramani zake, atakutana na watendaji na kumaliza matatizo yote makubwa ya ardhi na yale madogo madogo yatashughulikiwa na Mkuu wa Wilaya,”.

  Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu alisema wilaya zote zinatakiwa zihakikishe zinakuwa na shule moja ya kidato cha tano na sita kwenye kila tarafa nchini na Serikali itapeleka walimu. Alisema uwepo wa shule hizo utaamsha ari ya wanafunzi kusoma kwa bidii, jambo litakaloongeza idadi ya wanaoendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Nley jumla ya shilingi 1,500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa dawati la Jinsia katika Mji wa Tabora na ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa polisi katika wilaya ya Igunga. Makabidhiano ya fedha hizo zilizotolewa na Mbunge wa Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) yalifanyika baada ya Waziri Mkuu kuhutubiua mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Chipukizi kwenye Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na wapili kushotoi ni Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  Kadhalika Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wote kuanzia ngazi ya halmashauri hadi vijiji wawasimamie wanafunzi wa kike na wahakikishe wanamaliza masomo bila ya kukatishwa.

  “Huu ni mkakati wa Taifa tunataka watoto wa kike wote walindwe ili waweze kumaliza shule na marufuku kukatisha elimu yao, iwe kwa kuwapa ujauzito au kuwaoa, adhabu yake ni kali,”.

  Waziri Mkuu jana jioni alimaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora baada ya kuwa amefanya ziara katika wilaya za Igunga, Nzega na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
  Wananchi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri Mkuuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Chipukizi, Agosti 18, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Tabora, Hassan Kasubi katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kiwanja cha Chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora, Munde Tambwe katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kiwanja cha chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Tabora Mjini, Aden Rage baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Chipukizi kwenye Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza naWakazi wa Dar es Salaam juu ya umuhimu wa kutunza amani tuliyonayo na umoja wetu kama watanzania wakati wa Tamasha kubwa la Komaa Concert lililo andaliwa na kituo cha Radio cha EFM katika Viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe
  Msanii wa Muziki wa Hip Pop Nchini Roma Mkatoliki akiimba na kundi kubwa la Mashabiki wake waliofika katika Tamasha la Komaa Concert kwenye Viwanja vaya Tanganyika Parkers Dar es Salaam
  Msanii wa Bongo Fleva Mr Blue akiimba mbele ya Mashabiki wake waliofika katika tamasha la Komaa Concert katika Viwanja vya Tanganyika Parkers Dar es Salaam
  Msanii wa Hip Pop Nchini Yound D akiimba katika jukwa la Komaa Concert lililofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe Jijini Dar es Salaam
  Msanii wa Bongo Fleva Amber Lulu akiimba mbele ya Mashabiki wa Jiji la Dar es Salaam waliofika katika shoo ya Komaa Concert iliyofanyika jijini Dar es Salaam

  Muimbaji Maharufu wa kike katika Mziki wa Bongo Fleva Nandy akiimba na Mashabiki kwenye Tamasha la Komaa Concert Lililoandaliwa na kituo cha Radio cha Efm katika Viwanja vya Tanganyika Parkers
  Msanii wa Bongo Fleva Madee Ally akiimba wakati wa Tamasha la Komaa Concert liliandaliwa na kituo ch aRdaio cha Efm katika Viwanja vya Tanganyika Parker's kawe.
  Msanii wa Muziki wa Singeli Manfongo akiimba mbele ya Maelfu ya Mashabiki ambao waliofika katika Tamasha la Komaa Concert Kawe
  Umati wa Mashabiki waliofika katika Tamasha la Komaa Concert

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

  Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella ametekeleza agizo la Rais Mhe. Dkt. John Magufuli la kuhakikisha anafuatilia kero za wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga) na kuzitafutia ufumbuzi.


  Katika kutekeleza agizo hilo, Mhe. Mongella amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Sengerema Magesa Mafuru kuhakikisha anakutana na wafanyabiashara wadogo (machinga) ambao walinyang’anywa matunda yao (nanasi) zao kwenye oparesheni ya kuwaondoa barabarani ili walipwe fidia.


  Hatua hiyo ilijiri jana Agosti 18, 2018 baada ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli akiwa njiani Mjini Sengerema akielekea Chato mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko, kutoa agizo kwa watendaji wa halmashauri hiyo kutowasumbua machinga na badala yake wawache wafanye biashara zao huku akiagiza watendaji nchini kujikita kutatua kero za wananchi.


  Ni baada ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli kusimama kwa ajili ya kusalimiana na wananchi ambapo wafanyabiashara ndogo ndogo walimueleza kero zao ikiwemo ukosefu wa maeneo ya kufanyia biashara zao hatua inayosababisha kubugudhiwa na viongozi wa halmashauri.


  Kufuatia malalamiko hayo, Mhe. Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella kufuatilia kero hizo na kuzitatua ambapo muda mfupi baadaye Mhe. Mongella alikutana na viongozi mbalimbali wilayani Sengerema akiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi pamoja na machinga kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. Magufuli.

  Meza za wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) katika soko la Kisima cha Chumvi Mjini Sengerema ambalo limetengwa kwa ajili ya wafanyabishara hao. Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara wanagoma kuhamia katika soko hili kwa kile wanachodai ni kukosa wateja na hivyo kuendelea kufanyia biashara zao katika hifadhi ya barabara Mjini Sengerema.  0 0

   KAMPUNI YA MICHUZI MEDIA GROUP KWA NIABA YA UONGOZI WAKE NA WAFANYAKAZI WOTE KWA UJUMLA, INATOA SALAM ZA POLE KWA FAMILIA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT.JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI ,KUFUATIA KIFO CHA DADA YAKE MPENDWA BI.MONICA JOSEPH MAGUFULI KILICHOTOKEA TAREHE 19/08/2018 WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO MKOANI MWANZA

  MICHUZI MEDIA GROUP INAUNGANA NA FAMILIA YA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA KUONDOKEWA NA DADA YAO MPENDWA.

  BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA.JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.older | 1 | .... | 1651 | 1652 | (Page 1653) | 1654 | 1655 | .... | 1898 | newer