Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

JESHI LA POLISI LATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU WAMATAPELI WANAOTANGAZA AJIRA ZA POLISI


WAMILIKI WA VIWANDA VYA SARUJI WAAHIDI KUONGEZA UZALISHAJI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAMILIKI wa Viwanda vya Kuzalisha Saruji wamesema kuwa wataongeza uzalishaji wa saruji ili kuondoa hali ya upunguaji wa saruji nchini pamoja na kurudisha bei ya zamani ya saruji na sio ya 14000 pamoja na 15000.

Wamiliki wa viwanda vya Saruji waliyasema hayo wakati walipokutana na serikali kupitia Wizara ya Viwanda , Biashashara na Uwekezaji wakiongozwa na Najibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanaya walisema walikuwa na changamoto ya upatikanaji wa makaa yam awe pamoja na baadhi ya viwanda kuharibika Mitambo.

Akizungumza na wadau hao Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa wamiliki hao wazalishe saruji ya kutosheleza nchi kwanza na zaida ya saruji hiyo wauze nje ya nchi.Amesema kuwa kuuza saruji nje ya nchi ni fursa kiuchumi hivyo lazima viwanda vizalishe kwa kukidhi mahitaji ya ndani na ziada iuzwe nje, kuuza saruji nje na ndani kukawa na uhaba sio sawa.

Amesema kuwa wazalishaji wa makaa ya mawe wazalishe kwa wingi makaa hayo katika kuweza kulisha viwanda vya saruji pamoja na Tarula na Tanroad kujenga miundombinu sehemu yanakotoka makaa ya mawe.Shirika la Taifa la Madini (Stamico) limesema kuwa litaongeza kasi katika uzalishaji wa makaa ya mawe katika miradi yake ya Kiwira pamoja na Kaburu ili kuhakikisha viwanda vya saruji vinapata makaa ya mawe ya kutosha.

Akizungumza na waandishi habari Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico , Alex Rutagwelela amesema kuwa kazi yao ni kuhakikisha wanalisha makaa ya mawe ya kutosha kwa wazalishaji wa saruji nchini.

Amesema kuwa changamoto ya viwanda vya saruji ni makaa ya mawe hivyo kasi ya uzalishaji lazima iongezeke katika kutatua tatizo la upungufu wa saruji usiwe kujirudia kwa mara nyingine kutokana na miradi mingi inayotekelezwa inahitaji saruji hiyo.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji wa Saruji katika mkutano wa kujadili upungufu wa Saruji nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Profesa Joseph Bushweishaija akitoa maelezo kuhusioana na mkutano na huo kwa wadau wa uzalishaji wa viwanda vya saruji.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico, Alex Rutagwelela akizungumza na waandishi habari kuhusiana na stamico iliyojipanga katika uzalishaji wa makaa ya mawe .
Baadhi ya wazalishaji wa viwanda vya Saruji nchini

MISA TANZANIA,INTERNEWS ZAWANOA WAANDISHI WA HABARI GEITA,SIMIYU NA SHINYANGA

$
0
0
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Internews Tanzania wameendesha mafunzo kwa waandishi wa Habari Kanda ya Kaskazini/Magharibi (Geita, Shinyanga na Simiyu) kuhusu Changamoto za Sheria mpya za habari.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Agosti 17,2018 hadi Agosti 18,2018 yanafanyika katika ukumbi wa Alpha Hotel Mjini Geita.
Akifungua Mafunzo hayo,Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa alisema kupitia mafunzo hayo waandishi wa habari watajengewa uelewa kiuhusu sheria mbalimbali zinazohusu vyombo vya habari na waandishi wa habari na namna waandishi wa habari wanavyoweza kuishi na sheria hizo.
"Lengo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari na kuangalia changamoto zinazotolewa na sheria hizi sambasamba na kukumbushana miiko ya uandishi wa habari lakini pia kufahamu nafasi ya mwandishi wa habari kama mtetezi wa haki za binadamu",alisema.

Naye Afisa Mradi wa Boresha Habari kupitia Shirika la Internews linalofadhiliwa na USAID Victoria Rowan aliwasihi waandishi wa habari waliopata fursa ya kushiriki mafunzo hayo kutumia vyema elimu wanayopewa. 

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari mikoa ya Geita Shinyanga na Simiyu kuhusu Sheria za vyombo vya habari katika ukumbi wa Alpha Hotel Mjini Geita - Picha zote na Kadama Malunde & Joel Maduka
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akielezea malengo ya semina hiyo
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa
Afisa Mradi wa Boresha Habari kupitia Shirika la Internews  Victoria Rowan akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Afisa Mradi wa Boresha Habari kupitia Shirika la Internews  Victoria Rowan akielezea jambo ukumbini
Mwezeshaji katika Mafunzo hayo,Wakili James Marenga akitoa mada kuhusu Sheria ya  Huduma za Habari
Mwezeshaji katika Mafunzo hayo,Wakili James Marenga akifafanua vifungu mbalimbali vya sheria
Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde1 blog akifuatilia mada ukumbini.Kulia ni Bahati Sonda kutoka mkoani Simiyu
Mwandishi wa habari Salma Mrisho kutoka Geita akichangia mada
Mwandishi wa habari Paschal Michael kutoka mkoa wa Simiyu akichangia hoja ukumbini
Mwandishi wa habari Rehema Matowo kutoka Geita akichangia mada 
Semina inaendelea
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Kushoto ni Mwandishi wa habari Rose Mweko kutoka mkoani Geita akiwa na Derick Milton kutoka Simiyu na Editha  Edward kutoka Geita
Washiriki wakifuatialia mada ukumbini
Semina inaendelea
Washiriki wakifuatilia mada 
Mafunzo yanaendelea
Mwandishi wa habari Joel Maduka (kulia) kutoka Geita na Bahati Sonda kutoka Simiyu wakiwa ukumbini
Mwandishi wa habari Stella Ibengwe kutoka Shinyanga akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo
Mwandishi wa Habari Rehema Evance kutoka Simiyu akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo
Mwandishi wa habari Osman Nyamiti kutoka Divine Fm Shinyanga akichangia mada ukumbini
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Geita, Daniel Limbe akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

NIKIKUTANA NA MTATIRO NITAMUULIZA HUNA AIBU-PROFESA LIPUMBA

$
0
0
 
*Adai kuondoka kwake CUF hakuna madhara,aeleze hata ujio wake ulikuwa wa kumuokota

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi(CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amevunja ukimya na kuamua kuzungumzia kuondoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi wa chama hicho Julius Mtatiro kuondoka kwake hakuna madhara.

Kwa mujibu wa Profesa Lipumba amedai  Mtatiro hakuwa na mvuto ndani ya CUF na hata ujio wake ilitokana na kuamua kumuokota tu ili ajiunge nao na ndio maana nafasi zote alizopewa ndani ya chama zilikuwa na kumteua maana hakuwa anakubalika kwa wanachama wengi.

Profesa Lipumba ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Michuzi Blog iliyotoka kupata maoni yake baada ya Mtatiro kuondoka CUF na kujiunga CCM.

"Ukweli ni kwamba Mtatiro kilichomuondoa CUF kwanza ni uchu wa madaraka na ndio maana alikuwa anashikilia cheo ambacho hakipo kwenye Katiba ya chama chetu.

"Pia sababu nyingine ya kuondoka kwake ni njaa ambayo ilianza kupanda kichwani,hivyo akaona njia ni kuondoka CUF.Kuondoka kwake hakuna madhara kwetu kwani ni sawa na mtu kaamua kukuondolea mzigo," amesema Profesa Lipumba.

Katika mahojiano hayo maalumu Profesa Lipumba ameamua kuelezea namna ambavyo Mtatiro alijiunga CUF ambapo amesema waliamua kumchukua kwa staili ya kumuokota tu na ndio maana hakuwa anakubalika kwa wanachama zaidi ya kukubalika kwa viongozi tu.

"Tulimchukua aje kwenye chama chetu lakini baada ya kufika hapa akaanza kujiona yeye ni bora zaidi na ndio amesoma kuliko wote.Hivyo kuondoka kwake ni nafuu kwetu," amesema Profesa Lipumba.

Alipoulizwa kuhusu sabababu ambazo amezitoa Mtatiro wakati anatangaza kuachana na CUF,Profesa Lipumba amesema hizo sababu hazina ukweli wowote ila njaa ndio imemuondoa.

Amesema Mtatiro amekuwa bingwa wa kuandika habari za kukosoa Serikali hata inapofanya jambo la maendeleo na ghafla tu amesahau yote aliyokuwa anakosoa na kuona CCM ndio sehemu sahihi kwake.

Ameongeza kwa namna ambavyo Mtatiro amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya CCM ni bora angeenda hata chama kingine tofauti na hicho.

"Lakini baada ya kuona mambo yamemzidi amekimbilia huko huko ambako muda wote alikuwa akihangaika kukosoa wanayoyafanya," amesema Profesa Lipumba.

Alipoulizwa iwapo atakutana na Mtatiro leo atamwambia nini? Profesa Lipumba amejibu kuwa atamwambia hivi "Mtatiro kwanini huna aibu yaani umesahau yote  uliyokuwa unayaandika kuikosoa CCM.

" Ama kweli Mtatiro huna aibu kabisa yaani umesahau makala zako za mitandaoni za kuikosoa Serikali,"amesema Profesa Lipumba na kuongeza kuwa kuondoka kwake hakuna madhara yoyote kwa CUF.

Kwa kukumbusha tu wakati Mtatiro anaondoka CUF waliamua kueleza kwa kina sababu ambazo zimemfanya aondoke na mojawapo ameeleza wazi kuvutiwa na kasi ya utendaji kazi unaofanywa na Rais katika kuleta maendeleo nchini.

Mtatiro alitaja sababu nyingine ni kutoridhishwa na hali ya ushiriki na mchango wake kwenye siasa za CUF.

Pia akataja mgogoro wa kiuongozi unaoendelea kukikumba chama hicho na sababu ya mwisho kwa Mtatiro ilikuwa ni  mustakabali wake kuhusu masuala ya siasa.

TAARIFA YA HABARI YA ITV LEO TAR 17 AGOST 2018 SAA MBILI USIKU

WAZIRI MKUU AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJI MDOGO WA NZEGA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega Agosti 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara, Agosti 17, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe wakati alipowasili kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara, Agosti 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DC MUHEZA AWAONYA WALANGUZI WA KOROSHO

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo amewaonya walanguzi wa korosho kutoka kwa wakulima wilayani humo kuacha tabia hiyo mara moja kabla hawajakumbana na mkono wa sheria.

Badala ametaka ufuatwe utaratibu ambao umewekwa wilayani humo wa korosho hiyo kukusanywa kwenye maghala na kuuzwa kwa utaratibu uliopagwa ili mkulima aweze kunufaika na kilimo chake.

Hayo yalisemwa wakati akizungumza na mtandao huu ambapo pia aliwahimiza wananchi wilayani humo kujikita kwenye kilimo cha zao la korosho ili kunufaika nacho kutokana na uwepo wa soko la uhakika.Alisema ili kuhakikisha wanafanikisha kwenye jitihada hizo tayari wamegawa miche ya mikorosho bure 62050 ambako wananchi wamehamasika kupitia hekta 152.

Alisema pia kupitia amcos zao zamani zilikuwa zimelala lakini hivi sasa zimefufuka kutokana na kuwepo uhamasishwaji huo ambao umewawezesha kutambua umuhimu wa kilimo hicho .“Ndugu zangu wananchi limeni korosho kwani ni moja kati ya zao linalopewa kipambele na serikali ya awamu ya tano na tayari soko lake ni la uhakika hivyo walitilie mkazo kwa lengo la kunufaikanalo”Alisema DC Muheza.

Aidha alisema wilaya hiyo tayari dawa zipo kwa ajili ya wakulima hivyo watumie dawa zilizosambazwa ili kuwawezesha kulima kilimo chenye tija na cha kisasa ambacho kitawainua kimaisha.Hata hivyo aliwataka maafisa ugani watoke ofisini waende kwa wakulima kuhamasisha wananchi kutumia dawa hizo kadiri ya vipimo vinavyohitaji ili waweze kulima kilimo chenye tija na manufaa kwao ili kuwaezesha wakulima kunufaika.

“Huko kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara kumekuwa na ulanguzi kwenye manunuzi ya korosho hizo lakini kwetu hilo halipo ila nitoe wito kwa wale ambao wanafikiria kufanya biashara hivyo kinyume na utaratibu wao kama viongozi,serikali hawatakuwa tayari yoyote ambaye atataka kununua korosho kwa wakulima kwa bei za ulanguzi hivyo tutahakikisha anachukuliwa hatua “Alisema DC Muheza.

HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI BARABARA YA CHUNYA-MAKONGOLOSI: NAIBU WAZIRI KWANDIKWA

$
0
0
Serikali imesema haitamwongezea mkataba mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation anayejenga barabara ya Chunya –Makongolosi kwa kiwango cha lami muda wake utakapomalizika.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa amesema muda wa miezi 27 aliyopewa kujenga barabara hiyo yenye urefu wa KM 39 unatosha na hivyo ni jukumu lake kuhakikisha kuwa anakuwa na vifaa na wafanyakazi wa kutosha wakati wote.

“Mkishindwa kukamilisha barabara hii kwa wakati hamtapata tena kazi hapa nchini kwani mtakuwa mmeshindwa kazi kwa kukiuka mkataba na kuiongezea Serikali gharama”, amesema Mhe. Kwandikwa.

Naye Kaimu meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Mbeya Mhandisi Selemani Lawena amesema barabara ya Chunya –Makongolosi ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa yenye urefu wa KM 293 ambayo inaunganisha kwa njia fupi mkoa wa Mbeya na mikoa ya Singida na Tabora.

“Barabara hii ikikamilika itafungua uchumi wa mikoa ya Mbeya na Songwe na kuhuisha shughuli za kilimo,mifugo, uchimbaji madini na ufugaji nyuki na hivyo kuongeza fursa za maendeleo kwa jamii na serikali kwa ujumla”, amesema mhandisi Lawena.

Mhandisi lawena amesema sehemu ya Mbeya- Chunya KM 72 imekamilika na ujenzi wa Chunya –Makongolosi KM 39 unatarajiwa kukamilika Januari 2020.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Iwambi-Mbalizi KM 6.5 jijini Mbeya ambayo itatumiwa na magari madogo ili kupunguza msongamano na ajali katika mlima Mbalizi na kusisitiza umuhimu wa wadau wote wa usafiri kushirikiana ili kupunguza ajali na hivyo kulinda maisha na mali.
Ujenzi wa daraja la Kikamba wilayani Songwe linalounganisha Mkoa wa Songwe na Katavi ukiendelea daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Songwe Mhe. Philipo Mulugo alipokagua ujenzi wa daraja la Kikamba wilayani Songwe, daraja hilo linaunganisha Mkoa wa Songwe na Katavi.
Muonekano wa barabara ya Chunya –Makongolosi KM 39 ambayo ujenzi wake unaendelea, barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Mbeya- Rungwa yenye urefu wa KM 293 inayounganisha kwa njia fupi mkoa wa Mbeya na mikoa ya Singida na Tabora.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mbeya mhandisi Selemani Lawena wa kwanza (kulia), akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Chunya –Makongolosi KM 39, kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (wa tatu kulia), alipokagua ujenzi huo, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mary-Prisca Mahundi.

LUGOLA AWAPA WIKI MOJA POLISI KUWAKAMATA WANAFUNZI WATORO, WANAOWARUBUNI WATOTO WA KIKE

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewapa wiki moja Jeshi la Polisi Wilaya Bunda, kuwakamata wanafunzi watoro, wazazi wa wanafunzi watoro pamoja na watu waliowarubuni wanafunzi wa kike ambao wameacha shule wilayani humo.

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, alisema inamsikitisha sana idadi kubwa ya wanafunzi wilayani humo wameacha masomo yao na kurubuniwa wanaume ili waweze kuolewa huku Serikali ikitangaza elimu bure kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha nne.

Akizungumza na mamia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa mpira wa miguu wa Busambara, Kijiji cha Busambara, Kata ya Kitengule, wilayani humo, Lugola alisema kiwango cha wanafunzi kuacha masomo inatisha, hivyo serikali haiwezi kukaa kimya, lazima kuhakikisha wanafunzi hao wanasoma ili waje kuwa viongozi wa nchi.

“Mkuu wa Polisi wa hapa Bunda, nawapa wiki moja, mtumie elimu zenu za upelelezi mliofundishwa, wakamateni, wachunguzeni, wahojini ndugu, jamaa, majirani mtawawapata wote wanaowarubuni watoto hawa, halafu mushughulike nao,” alisema Lugola.

Pia Lugola aliongeza kua, kuna sheria zinazoshughulika na wanafunzi watoro na pia zipo sheria zinazoshughulika na wazazi wa wanafunzi watoro, pia zipo sheria zinazowashughulikia wanaume wanaowarubuni wanafunzi, hivyo haiwezekani wanafunzi wa kidato cha tano wakatae masomo, na wengi wao wanaokataa masomo ni wasichana.

Aidha, Lugola alisema ujenzi wa sekondari mbili za kidato cha tano na sita unaendelea ambapo katika kata za Nansimo na Muramba katika Jimbo lake la Mwibara zitanaanza kuchukua wanafunzi mwaka ujao watakao fanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu. “Tunaendelea kuweka miundombinu katika shule hizo ili ziweze kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano katika maeneo haya na hatutarajii wanafunzi kukosa shule wamalizapo kidato cha nne,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Lugola pia aliwataka polisi nchini kuwakamata waendesha magari na bodaboda ambao hawafuati sheria za barabarani ikiwemo baadhi ya bodaboda uvunja sheria kwa makusudi kwa kupakia abiria wanne na kuendelea ambapo ni hatari kwa usalama wa dereva na abiria hao. “Idadi kubwa ya polisi wanafanyakazi kwa umakini na uaminifu mkubwa, ila wachache sana ndio wenye tabia hizo mbaya, nawataka askari hao wafuate sheria na pia kuendelea kuzikamata kama ni magari au bodaboda au wananchi wowote ambao wanavunja sheria za nchi,” alisema Lugola.

Waziri Lugola yupo katika ziara jimboni kwake kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuwaunganisha wananchi kupitia Bonanza lake la michezo ya mpira wa miguu ambalo linashirikisha kila kata wakitoa washindi mbalimbali ambao anawapa zawadi pamoja na kuingia moja kwa moja katika mashindano ya kugombea Kombe la Kangi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Busambara, Kata ya Kitengule katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Busambara jimboni humo, Wilaha ya Bunda, mkoani Mara. Lugola aliwaagiza Polisi wilayani humo kuwakamata wanafunzi watoro pamoja na wanao warubuni watoto wa kike katika shule mbalimbali wilayani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza mwananchi wa Kijiji cha Busambara, Kata ya Kitengule, Kaitila Jumbula, alipokua anauliza swali kuhusu maendeleo ya Kata hiyo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Busambara, jimboni humo, Wilaha ya Bunda, mkoani Mara. Lugola aliwaagiza Polisi wilyani humo kuwakamata wanafunzi watoro pamoja na wanao warubuni watoto wa kike katika shule mbalimbali wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

RAIS DKT. MAGUFULI ASAFILI KWA NDEGE YA BOEING 787-8 DREAM LINER AKIELEKEA JIJINI MWANZA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwasalimia abiria ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwa amemshika mtoto Ikrama Mahadi(Miezi-3) alipokuwa akiwasalimia abiria ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwasalimia abiria ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwa ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018. PICHA NA IKULU

FAINALI YA BBALL KINGS KUANZA WIKIENDI HII

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MICHUANO ya Sprite Bball Kings 2018 imefikia hatua ya fainali baada ya timu za Flying Dribblers na Mchenga Bball Stars kushinda mechi zao za nusu fainali.

Msimu wa pili wa mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 ulizinduliwa Juni 11 mwaka huu katika Viwanja vya Mlimani City Mall na jumla ya timu 51 na zikiwa na jumla ya washiriki zaidi ya 510 kutoka pande mbalimbali Tanzania walijisajili na kushiriki michuano hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Vipindi wa EA Radio, Nasa Kingu amesema kuwa michuano hiyo ilianza rasmi Juni 30 kwa timu 51 kucheza hatua ya mtoano na kupatiakana kwa timu 16 zilizoingia hatua iliyofuata.

Kingu amesema kwa sasa mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 yamefikia hatua ya fainali na timu ya Flying Dribblers pamoja na timu ya Mchenga Bball stars zitachuana vikali kuwania ubingwa mechi hizo zikiwa katika Game 5.

Ameeleza kuwa, timu ya Mchenga Bball stars ndiye bingwa mtetezi akiwa na kumbukumbu ya kumtoa mpinzani wake Flying Dribblers hatua ya nusu fainali msimu uliopita na sasa hivi wanakutana katika hatua ya fainali.

Fainali za mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 yanatarajiwa kuanza rasmi  Jumamosi Agosti 18 - Game 1 utakaochezwa katika Uwanja wa ndani wa Taifa , jumatano Agost 22 - Game 2 katika Viwanja vya Don Bosco, Jumamosi Agost 25- Game 3 Uwanja wa Ndani wa Taifa na kama italazimika kuendelea na game 4 na 5, mechi hizo zitachezwa Jumamosi  Agosti 29 Game 4 na Jumatano Septemba  01- Game 5 na mechi hizo zitachezwa katika Viwanja vya  Don Bosco Oysterbay.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Manase Zablon amesema kuwa michuano hii imeweza kuonyesha njia kwa wachezaji ambapo katika msimi uliopita wapo wachezaji waliofanikiwa kupata timu na wengine wakipata nafasi za kusoma kupitia mchezo huo.

Kwa mara ya kwanza mashindano ya Sprite Bball Kings yalifanyika 2017 na timu ya Mchenga Bball Stars iliweza kuwa bingwa na kufanikiwa kupata fedha taslimu shilingi million 10 pamoja na Kikombe, Mshindi wa pili wa mashindano alipata shilingi milioni 3 na Mchezaji bora (MVP) Rwehabura Munyangi aka Barongo ambaye alipata kikombe na fedha taslimu shilingi milioni 2.
Mkuu wa Vipindi wa EA Redio Nasa Kingu akizungumza na wawakilishi wa timu za Flying Dribllers na Mchenga BBall Stars pamoja na waandishi wa habari kuelekea fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 mchezo utakaoanza kutimi vumbi Agosti 18 mwaka huu katika Viwanja vya Ndani wa Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) Manase Zablon.

ALIYETAFUNA FEDHA ZA KIJIJI CHA KURUYA SASA AREJESHA MILIONI 1.7/-

$
0
0


Kaimu Mtendaji wa kijiji cha Kuruya kata ya Komuge Athumani Juma akifafanua jinsi fedha hizo zilivyolipwa zaidi ya Mill1.7 kutoka kwa aliyekuwa Afiasa mtendaji wa kijiji hicho Mwita Mangondi ambaye alisimamishwa kazi baada ya upotevu wa fedha za serikali na kupewa Mwezi Mmoja aweze kulipa fedha hizo.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya kata ya Komuge wilayani Rorya wakiwa katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kupewa mrejesho kuhusu fedha hizo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kuruya Bernard Wambura akifafanua jambo katika mkutan huo ambapo amesema mwitikio wa vikao na Mikutano ya kijiji ni kidogo hivyo kuna haja kubwa ya kuanza kutekeleza sheria ndogo ya vijiji walizojiwekea ili wananchi washiriki Mikutano hiyo.

Mwalimu Mkuu shule ya Msingi KuruyaRobert John akifafanua changamoto ya ukosefu wa Matundu ya vyoo vya walimu jambo ambalo limesababisha walimu hao kutumia baadhi ya Matundu ya vyoo vya wanafunzi na wakati mwingine kutumia vyoo vya nyumb za walimu ambao wanaishi shuleni hapo.


Na Frankius Cleophace Rorya

ALIYEKUWA Mtendaji wa Kijiji cha Kuruya Kata ya Komuge wilayani Rorya mkoani Mara Mwita Mangondi amerejesha fedha kiasi cha Sh.milioni 1.7 alizokuwa akidaiwa baada ya kuzitumia kinyume cha utaratibu.

Ambapo kutokana na tuhuma hizo alisimamishwa kazi na kupewa mwezi mmoja ili kurejesha fedha hizo za Serikali ya kijiji hichop.Akisoma mrejesho wa fedha hizo Kaimu Mtendaji wa kijiji cha Kuruya Athumani Juma amesema kuwa mtendaji huyo alisimamishwa kazi na kupewa muda ili kurejesha fedha hizo.Amesema tayari amerejesha kiasi cha Sh.1,700,000 na kubakizakiasi cha Sh.298,387 ambapo jumla alikuwa anadaiwa Sh.1,998,387.

Athumani ameongeza baada ya fedha hizo kurejeshwa tayari wametenga kiasi cha Sh. 1,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Msingi kuruya.Huku kiasi kingine wakilipa wananchi ambao wanadaia serikali ya kijiji hicho.Aidha wananchi wa kijiji hicho wamedai kuwa kuna haja kubwa ya kuwekeza nguvu katika shule ya msingi mbatamo ili walimu waweze kupata vyumba vya kuishi.

“Walimu zaidi ya kumi na tano wanaishi nje ya shule kwanini hizo fedha zinazodaiwa zisipelekwe kwenye ujenzi wa nyumba za walimu shule ya msingi mbatamo , wanafunzi hawana Madawati wala vyumba vya adarasa vya kutosha,” wamesema wananchi hao.Mwenyekiti wa Kijiji cha Kuruya Bernad Wambura amezidi kusisitiza wananchi kuhudhuria mikutano huku akimwomba Kaimu mtendaji wa kijiji hicho kuendelea kusimamisha sheria ndogo za kijiji walizojiwekea ili wananchi wazidi kuudhuria Mikutano hiyo.

“Leo mkutano wananchi wamekuwa wachache sasa kuna haja kubwa ya kuanza kutumia sheria zetu zile ndogi ili wananchi washiriki vyema Mikutano,” amesema Wambura.

Aidha Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Kuruya Robert John ameeleza changamoto yua ukosefu wa matundu ya vyoo vya walimu ambapo amesema kuwa walimu hao hawana vyoo jambo ambalo linasababisha walimu hao kutumia baadhi ya matundu ya vyoo vya wanafunzi na wakati mwingine kutumia vyoo vya walimu wanaoishi shuleni hapo.

DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Tarime

KATA ya Nkende iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara katika kipindi cha mwaka 2016 hadi mwaka 2018 imetumia zaidi ya Sh.milioni 458 katika utekelezaji wa miradi mbalimbaliya Maendeleo.

Baadhi ya miradi hiyo ni ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara huku wananchi wakichangiazaidi ya Sh.milioni 22.Wakati Diwani wa kata hiyo Daniel Komote akichangia zaidi ya Sh.milioni 15 kwa lengo la kutekeleza miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuunga juhudi za Serikali.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata hiyo Komote katika kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kata ya Nkende Mjini Tarime.

Komote amesema kuwa amekuwa akishawishi wananchi katika kuchangia maendeleo kupitia sekta zote bila kujali itikadi za vyama ili wananchi waweze kuondokana na adha ambao wamekuwa wakipata kutokana na ukosefu wa huduma za muhimu karibu, likiwemo suala la Afya, Elimu, na Miundombinu ya Barabara na Maji.

Pia diwani huyo amesema katika sekta ya afya ili kutimiza ahadi yake aliyotoa kipindi anaomba ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo amewezakukatia bima ya afya watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo walemavu, wazee na watu wanaoshi katika kaya maskini jumla ya watu 1800.

“Ili suala la kukatia wananchi bima ya afya ili nilitoa ahadai kipindi cha kampeni na sasa tayari nimeisha saidia watu 1800 na nilisema nitakatia kaya 50 lakini mpaka naongeza tayari kaya310 swa na kaya 1,800,” amesema Komote na suala ili limesaidia sasa Serikali imeleta Sh.Milioni nane katika Zahanatiya Magena," amesema Komote.

Kwa upande wa Katibu wa CCM wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao hicho anazidi kusisitiza kata nyingine kuiga mfano wa diwani wa kata ya Nkende .Pia amesisitiza suala la uundaji wa vikundi kwa vijana na akina mama ili kupatiwa ikopo kutoka Halmashauri.

Aidha Wajumbe wa halmashauri kuu ya kata ya Nkende CCM wamempongeza diwani huyo kufanya kazi kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuleta maendeleo ndani ya kata bila ubaguzi wowote.
Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote akifafanua mambo yaliyofanyika kipindi cha Januari mpaka Juni 2018 katika kata yake kupitia sekta ya Afya,Maji,Elimu, Miundombinu ya Barabara na Masuala ya kijamii.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka Kura akisisitiza jambo katika kikao hicho baada ya diwani wa kata hiyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho kata ya Nkende Mjini Tarime.
Wajumbe wa kamati ya Siasa kata ya Nkende wakiwa katika kikao hicho cha kuwasilisha taarifa ya ilani ya chama hicho ngazi ya kata.
Baadhi yawageni wakiwemo Madiwani kutoka kata mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.

MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA

$
0
0
*Ni ishara ya kumuombea dua kwa Mungu,pia kumshukuru kwa kusaidia kutatua kilio chao

MKAZI wa Kijiji cha Kidoka Wilaya ya Chemba, Roza Mkali ameamua kumshika  kichwa mdau wa  maendeleo wa wilaya hiyo, Khamis Mkotya, ikiwa ni ishara ya kumwombea dua.

Pia ikiwa ni  kumshukuru baada ya kufanikisha familia hiyo na nyingine zaidi ya tano kijijini hapo kulipwa fidia ya mashamba yao yaliyokuwa yamechukuliwa na mkandarasi wakati wa ujenzi wa barabara ya Dodoma - Babati.  

Imeelezwa kuwa  wananchi hao walikata tamaa mwishoni mwa mwaka juzi kutokana na kufuatilia malipo yao bila mafanikio. 

Hivyo Mkotya aliguswa na kero hiyo hivyo aliamua kushirikiana nao na kuwapigania hadi walipolipwa stahiki zao. 

Juzi wakati Mkotya akitoka Dodoma kwenda Kondoa aliamua kupita kijijini hapo ndipo familia hiyo ilipomkaribisha nyumbani ili aone matunda ya kazi yake ya kuwapigania.

 Familia hiyo ilimweleza Mkotya kuwa inayofuraha kubwa kwani fedha walizopata wameweza kununua mashamba mengine na kujenga nyumba bora ya bati.
 MKAZI wa Kijiji cha Kidoka Wilaya ya Chemba, Roza Mkali akiwa amemshika kichwa mdau wa  maendeleo wa wilaya hiyo, Khamis Mkotya, ikiwa ni ishara ya kumwombea dua.
 Mdau wa Maendeleo wilaya ya Chemba,Hamis Mkotya akizungumza jambo na Mkazi wa kijiji cha Kidoka Wilayani Chemba,Roza Mkali hivi karibuni mara baada ya tatizo walilokuwa nalo kutatuliwa

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA DHIFA ILIYOANDALIWA NA RAIS WA NAMIBIA MJINI WINDHOEK

$
0
0
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Country Club mjini Windhoek kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wenzake wakisimama wakati nyimbo za taifa zikipigwa katika ukumbi wa Country Club mjini Windhoek kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi wezake katika ukumbi wa Country Club mjini Windhoek kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob (wa tatu kushoto) na wageni wake kwenye dhifa ya kitaifa aliyoandaa kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika ya Kusini, Mama Geingob, Katibu Mtendaji wa Sadc Dkt. Sergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Nambia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah
 
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Edwin Paul Mhede ukumbi wa Country Club mjini Windhoek baada ya dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Elimu ya Juu wa Namibia pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Edwin Paul Mhede (wa pili kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Ali Khamis Wa tatu kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe. Sylvester Ambokile (nyuma ya Makamu wa Rais) na Balozi wa Namibia nchini Tanzania Bi. Theresia Samaria (koti jekundu) ukumbi wa Country Club mjini Windhoek baada ya dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hasna Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Edwin Paul Mhede (wa pili kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Ali Khamis, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe. Sylvester Ambokile na afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika ukumbi wa Country Club mjini Windhoek baada ya dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoka ukumbi wa Country Club mjini Windhoek kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI DADA YAKE ALIYELAZWA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Dada yake Monica Joseph Magufuli ambaye amelazwa katika Chumba cha uangalizi Maalum ICU katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza. Picha na Ikulu

KOFI ANNAN AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 80

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

ALIYEKUWA katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Atta Annan (80) amefariki dunia leo katika hospitali ya Bern nchini Uswizi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kofi alikuwa  Mwafrika wa kwanza kutoka nchini Ghana kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na alihudumu kwa awamu mbili kuanzia Januari 1997 hadi Desemba 2016.

Baadaye alichaguliwa kuwa mmoja wa wajumbe katika kusuluhisha mzozo nchini Syria na alichangia katika kuleta suluhu.

Kofi Atta Annan alikuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa taasisi ya Kofi Annan na mwenyekiti wa wazee katika shirika la kimataifa lililoanzishwa na aliyekuwa Rais wa Afrika ya kusini Nelson Mandela.

Kofi alizaliwa  Aprili 8, 1938 huko Kumasi nchini Ghana na alisoma taaluma mbalimbali ikiwemo Uchumi aliyosoma katika Chuo cha Macalester na Uhusiano wa Kimataifa katika chuo cha Geneva ,Alianza kuitumikia UN mwaka 1962 katika shirika la afya Duniani  (WHO.) Na ameshinda tuzo mbalimbali ikiwemo ya kulinda amani 2001.

Kofi ameacha mke (bi Nane Maria Annan) na watoto (Kojo, Ama na Nina) ambao walikuwa karibu naye  hadi umauti unamfika.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Atta Annan

RC PWANI APIGA MARUFUKU UINGIZWAJI WA MIFUGO KATIKA ENEO LA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA SUKARI CHA BAKHRESA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO 

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amepiga marufuku uingizwaji wa mifugo katika eneo la kampuni ya Said Salim Bakhresa Group Ltd,ambalo amekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda cha sukari Juni 2019 na uzalishaji ifikapo septemba 2020-2021. 

Aidha amewasihi wafugaji kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na kilimo . Ndikilo aliyasema hayo ,wakati kamati ya siasa ya mkoani humo , ilipotembelea shamba hilo kujionea utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa kipindi cha nyuma baada ya kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha kampuni hiyo kilichopo Mkuranga. 

Alisema agizo la Rais lilikusudia kuondoa pengo la uzalishaji wa sukari kwa matumizi ya kawaida nchini . Ndikilo, alisema mradi huo ni mkubwa na ni hazina kwa mkoa na kujivunia kupiga hatua ya kiuchumi na ujenzi wa viwanda. 

Mkuu huyo wa mkoa alishauri sehemu ya mradi kuwe na wakulima wa nje ili kuwaondolea umasikini. Kuhusu fidia walioguswa na mradi huo alisema fidia inalipwa kwa awamu na taratibu za kuwafanyia tathmini hivyo ambao bado wavute subira lakini hawatolipwa wavamizi. Nae msimamizi wa mradi huo, Muharami Mkenge alielezea, kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group LTD imekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda Juni 2019 na uzalishaji wa sukari kiwandani ifikapo septemba 2020-2021. 

Alisema, ujenzi wa kiwanda ,uzalishaji na hatua zote kuanzia shamba utagharimu zaidi ya sh.bilioni 450 hadi kukamilika . Hatua hiyo ni utekelezaji baada ya agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuipatia 
ardhi yenye ukubwa wa hekta 10,000 kwa ajili ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda hicho katika wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani. Alisema, tayari kampuni imetenga sh.milioni 75 kwa ajili ya kuanza uwekezaji katika shamba hilo kwa shughuli za kilimo cha miwa . 

Alifafanua kuwa, hatua ya awali ya upandaji wa miwa kwenye vitalu imeanza. Mkenge alisema, maandalizi ya upandaji wa miwa katika kitalu A chenye hekta 50 umekamilika, upandaji wa miwa katika eneo la jumla ya hekta nane tayari kwa sasa. “Baada ya kukamilika kwa upandaji katika kitalu “A” mwaka huu tunatarajia ifikapo 2019 tutaendelea kupanda miwa kwenye kitalu “B” chenye ukubwa wa hekta 200-300 ambapo mzunguko utaendelea hivyo hivyo. Awali alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kuingiliwa na wimbi la mifugo kiholela hali inayosababisha kuweka walinzi zaidi kwa ajili ya kulinda . 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani Ramadhani Maneno aliomba hatua na zoezi la malipo lifanyike haraka ili kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima . Alisema eneo hilo ni la RAZABA eneo la serikali ,hali inayomfanya apate mashaka na wananchi wanaolalamika na kutaka kuandamana kwa kudai eneo ni la wananchi . Mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo Fatuma Latu alisema ,wameshalipwa awamu ya kwanza ,ya pili na wanaendelea na awamu nyingine hadi hapo watakapohakikisha wanalipwa waliolengwa kupatiwa fidia. 

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Zainab Kawawa aliomba ushirikiano na viongozi,watendaji na wananchi ili kusukuma maendeleo ya wilaya hiyo.
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mbele ya Viongozi wa Serikali na Chama cha CCM,alipokuwa akitoa tamko la kupiga  marufuku uingizwaji wa mifugo katika eneo la kampuni ya Said Salim Bakhresa Group Ltd,ambalo amekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda cha sukari Juni 2019 na uzalishaji ifikapo septemba 2020-2021.

WAZIRI KAMWELWE AAGIZA TANROADS KUICHUNGUZA KAMPUNI YA CHICO

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa pili kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe, Gerson Lwenge (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka (kushoto) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9, mkoani humo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9, mkoani humo.
Mhandisi kutoka kampuni ya Smec International Pty, Adarsh Nayyari, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), ukubwa wa kazi unaoendelea wa kupasua mlima unaofanywa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Moronga-Makete KM 53.5 kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoka kukagua moja ya kalvati katika mto wa Lyamadovela lililopo katika barabara ya Moronga-Makete yenye urefu wa KM 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe.


Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Njombe kumchunguza mkandarasi wa Kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), anayejenga barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9 kwa kiwango cha lami kama ana wataalaamu wa kutosha.

Waziri Mhandisi Kamwelwe ametoa agizo hilo katika wilaya ya Wanging’ombe mara baada ya kukagua hatua zilizofikiwa katika mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambapo mpaka sasa umefikiwa kwa asilimia 14.

Mhandisi Kamwelwe amesema hana uhakika na kampuni hiyo kama ni wenyewe CHICO waliozoeleka katika uendeshaji wa miradi mingi hapa nchini hasa ya barabara.

“Sijaridhishwa na kasi ya huu ujenzi, Meneja wa TANROADS hakikisha unafuatilia kwa makini mradi huu na kubaini sababu zilizopelekea kusuasua kwa mradi na kuondoa wataalamu ambao wataonekana wanaudhaifu na kukwamisha mradi huo”, amesisitiza Mhandisi Kamwelwe.

Amebainisha kuwa hakuna sababu ya mkandarasi huyo kuchelewesha mradi huo kwani vifaa na mitambo yote ipo katika eneo la kazi na tayari Serikali imeshamlipa fedha alizozidai kwa asilimia 95.

Aidha, amemueleza Mkandarasi wa Kampuni ya CHICO kuwa Serikali haitamuongezea muda wa kuikamilisha barabara hiyo na wananchi wanaiongojea kwa hamu kubwa kwani Serikali imewaahidi wananchi hao ambao toka Uhuru hawajawahi kuiona lami.

Katika hatua nyingine, Waziri Kamwelwe amekagua ujenzi wa mradi wa barabara ya Moronga-Makete yenye urefu wa KM 53.5 inayojengwa na mkandarasi kutoka kampuni ya China Railway Seventh Group na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake.

Awali akitoa taarifa Meneja wa TANROADS, mkoa wa Njombe, Mhandisi Yusuph Mazana, amemueleza Waziri Mhandisi Kamwelwe changamoto ya miradi hiyo kubwa ni kazi za ujenzi kuanza katika msimu wa mvua nyingi na hivyo kupunguza kasi ya ujenzi wake.

Pia amemuahidi Waziri huyo kuwasimamia makandarasi hao katika kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na viwango vya ubora.Naye Mbunge wa jimbo la Wanging’ombe, Gerson Lwenge, ameishukuru Serikali kwa hatua ya ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga kwani ni muhimu katika usafirishaji wa mazao ya misitu na viazi.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete yenye jumla ya urefu wa KM 107.4 unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 na unatarajiwa kukamilika Januari 2020.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

WAZIRI MKUU AWAONYA MADIWANI TABORA

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na wa Manispaa ya Tabora na viongozi mbalimbali leo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake Mkoani humo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na wa Manispaa ya Tabora na viongozi mbalimbali leo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maelezo mafupi leo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kwa ajili ya kuzungumza na watumishi na viongozi mbalimbali wa Manispaa na Ofisi yake.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete) leo mara baada ya kukagua majengo Chuo cha Afya. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kutoka kulia) , Mkuu wa Wilaya ya Tabora Erick Komanya (kulia) , Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunin Kamba(wa pili kutoka kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi(kushoto)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akikiongozana na viongozi mbalimbali leo kukagua majengo ya Chuo cha Afya cha Tabora ambacho hakijaanza kutumika.


NA RS TABORA.

MADIWANI wa Manispaa ya Tabora wameonywa kutojihusisha na biashara ya aina yoyote zinazotolewa na Ofisi ya Mkurugezi na wametakiwa kubaki kuwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Onyo hilo limetoelwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na Madiwani,Watumishi wa Manispaa, watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Watendaji wa ngazi mbali mbali wa taasisi za umma zilizopo Manispaa ya Tabora ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake mkoani humo.

Waziri Mkuu amewataka Madiwani ambao wanajihusisha na Kampuni zinazofanya biashara na Halmashauri ya Manispaa hiyo wajiondoe ili waweze kuchukua hatua pale inapotokea tatizo au dosari yoyote.

Alitoa wa mfano wa mradi wa ununuzi wa Magari mawili na kontena za kubebea taka ambao alipewa mmoja wa madiwani wa Manispaa hiyo ambaye hakumtaja jina.

Waziri Mkuu alisema kuwa kampuni hiyo ilinunua magari hayo huku moja likiwa bovu na ili kuwadanganya zaidi alilipaka rangi ili lionokane ni jipya na hadi leo halijafanya kazi na hakuna hatua zilizochukuliwa kutokana na kulindana.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo ambayo ilipewa kazi hiyo pamoja na kupewa msamaha wa kodi lakini cha kushangaza tangu mwaka 2015/16 hadi sasa haijarejesha kwa Manispaa ya Tabora fedha ilizolipwa kama kodi.

Kwa upande Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bosco Ndunguru alisema ni kweli kampuni hiyo ilileta gari moja likiwa ni bovu lakini malipo yake bado hawajamlipa hadi hapo atakapoleta gari jipya.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images