Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MAADHIMISHO YA 15 YA SIKU YA WAZAZI BWAWANI SEKONDARI YAFANA MKOANI PWANI

0
0
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP – Phaustine Kasike akitoa hotuba fupi mbele ya wazazi na wanafunzi wa Bwawani Sekondari katika Maadhimisho ya Kumi na tano ya Siku ya wazazi ya Shule hiyo leo Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.
. Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP – Phaustine Kasike akisalimiana na mmoja wa wazazi alipowasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Bwawani kushiriki Maadhimisho ya Kumi na tano ya Siku ya wazazi ya Shule hiyo leo Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.
Meza Kuu wakiimba wimbo wa Shule ya Sekondari Bwawani kama wanavyoonekana katika picha(katikati) ni Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP – Phaustine Kasike(kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo ambaye ni Kamishna wa Magereza,Gaston Sanga(kushoto).
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP – Phaustine Kasike akikagua gwaride maalum lililoandaliwa na wanafunzi skauti wa Shule ya Sekondari Bwawani leo katika Maadhimisho ya Kumi na tano ya Siku ya wazazi ya Shule hiyo, Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.
Wanafunzi wa Bwawani wakitoa burudani ya Wimbo Maalum wa Shule hiyo kama inavyoonekana katika picha.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP – Phaustine Kasike akisoma ubao mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa nyumba ya walimu wa Shule ya Sekondari Bwawani leo Siku ya wazazi, Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.

Muonekano wa nyumba ya walimu iliyokamilishwa kujengwa kwa kujitolea tayari kwa matumizi katika Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.

Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Bwawani Sekondari wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP – Phaustine Kasike(hayupo pichani) katika Maadhimisho ya Kumi na tano ya Siku ya wazazi ya Shule hiyo leo Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani(Picha na Jeshi la Magereza).

SOMA VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 17,2018

0
0
Magazetini leo Ijumaa August 17 2018 




















KAMISHINA UNHCR AMALIZA ZIARA NCHINI, ATEMBELEA KAMBI NA KUTOA RAI

0
0
ZIARA ya Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk imehitimishwa jijini Dar es salaam huku akihimiza kuwa kila mkimbizi ana haki ya kuamua aidha kurejea nchini kwake au la.

Turk amekuwa nchini kwa siku nne kuanzia Agosti 13 mpaka Agosti 16 Agosti 2018 ,Turk amehitimisha ziara yake kwa kukutana na wanahabari jijini Dar es salaam, katika ziara hiyo aliambatana na Mratibu wa tume Afrika Valentin Tapsob na Mratibu wa wakimbizi (kanda) kutoka Burundi bi. Catherine Wiesner.

Lengo la ziara hiyo ya Kamishina kutoka UNHCR ilikuwa ni kufanya majadiliano yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu changamoto na masuluhisho kwa zaidi ya wakimbizi 34,000 na wale wanaoomba hifadhi (asylum seekers) nchini.Imeelezwa kuwa idadi kubwa ya wakimbizi waliopo nchini wanatoka katika nchi za Burundi na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambapo asilimia 87 wanaishi katika kambi 3 zilizopo Mkoani Kigoma.

Kamishina Turk pia ametembelea kambi ya wakimbizi Nduta ambapo alishuhudia mchakato wa kuwarejesha makwao wakimbizi kutoka Burundi na hadi sasa zaidi ya wakimbizi 42,000 wamerejea nchini Burundi.

" Haki ya wakimbizi lazima iheshimiwe katika kuamua kurejea nchini mwao au la" amesema Turk na kuongeza kuwa maamuzi hayo yaangalie taarifa iliyotolewa bila kulazimishwa aidha arejee au la.Pia wawakilishi kutoka nchini Burundi wamekutana na Kamishina Turk na kueleza kuwa idadi ya wakimbizi imefikia 400,000 hadi kufikia Julai 31 mwaka huu.

Aidha imesemwa kuwa hali ya wakimbizi kutoka Burundi imekua chini zaidi duniani katika kupokea misaada ya kibinadamu, UNHCR na washirika wengine walipokea asilimia 12 ya dola milioni 391 za kimarekani pekee kwa mwaka 2018 na mwaka 2017 asilimia 21 ya misaada ilipokelewa kwa ajili ya wakimbizi kutoka Burundi.

Kutokana na hali hiyo Turk ameiomba jumuiya ya kimataifa kuangalia hali hiyo ya kusahaulika kwa wakimbizi katika kupatiwa misaada ya kibinaadamu.Katika ziara hiyo ambayo Kamishina Turk alikutana na mamlaka za serikali, wakuu wa balozi, wafadhili na wadau mbalimbali nchini ameaidiwa kuwa Tanzania itahakikisha maamuzi ya wakimbizi katika kurejea nchini kwao yataheshimiwa.
Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar kuhusiana na ziara yake ya siku nne,lengo ya ziara hiyo ilikuwa ni kufanya majadiliano yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu changamoto na masuluhisho kwa zaidi ya wakimbizi 34,000 na wale wanaoomba hifadhi (asylum seekers) nchini.
Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jana jijini Dar kuhusiana na ziara yake ya siku nne,lengo ya ziara hiyo ilikuwa ni kufanya majadiliano yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu changamoto na masuluhisho kwa zaidi ya wakimbizi 34,000 na wale wanaoomba hifadhi (asylum seekers) nchini.Pichani kushoto ni Mratibu wa tume ya Afrika Valentin Tapsob,Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi Tanzania (UNHCR), Chansa Kapaya na kulia ni Mratibu wa wakimbizi (kanda) kutoka Burundi,Catherine Wiesner.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk alipokuwa akizungumza nao kuhusu ziara yake ya siku nne aliyoifanya nchini Tanzania

UJAMBAZI WA SILAHA UMEPUNGUA NCHINI-IGP SIRRO

0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli katika mkutano wa hadhara wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoani Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua gwaride baada ya kuwasili Shule ya Polisi Moshi zamani CCP kwa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa waliopo Shule ya Polisi Moshi zamani CCP wakati wa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli wakati alipokwenda kuzungumza nao wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoa wa Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).


Na Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ametoa onyo kali kwa majambazi na wahalifu wengine hususani wanaotumia silaha za moto kuacha mara moja kabla ya kukutana na moto mkali wa Jeshi la Polisi ambapo pia ametoa wito kwa wazazi kuwakanya watoto wao kujihusisha na vitendo hivyo.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na Wakazi wa Mto wa Mbu Tarafa ya Manyara Wilayani Monduli Mkoani Arusha wakati wa Ziara yake mkoani humo yenye lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzitafutia ufumbuzi.Alisema hivi sasa ujambazi wa kutumia silaha umepungua kwa kiasi kikubwa na baadhi ya matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza yanaendelea kudhibitiwa na Jeshi la Polisi.

“Nawasihi wanaofikiria kuendelea kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo vya utumiaji wa silaha na kuua watu waache mara moja kwa kuwa wakikutana na moto wa Jeshi la Polisi wasije wakajilaumu mana kwa sasa moto wetu ni mkali hivyo nawashauri wazazi wakanye watoto wao” Alisema Sirro.

Aidha amewataka Wakazi wa Mto wa mbu Wilayani Monduli kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa usalama umeimarishwa katika kupambana na wahalifu waliokuwa wakifanya vitendo vya kuwaua watu hususani wanawake ambapo katika kipindi cha hivi karibuni kuliripotiwa matukio kadhaa ambayo yalileta wasiwasi katika eneo hilo muhimu kwa utalii.Amewataka Viongozi wa Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa suala zima la ulinzi na usalama linatiliwa mkazo ili kuhakikisha hakuna mhalifu katika maeneo yao na wageni wanapoingia wachukue taarifa zao mapema.

Kwa Upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Bi. Kuluthum Hassan alisema Wahalifu wanaouza bangi, pombe ya gongo na dawa za kulevya wanaendelea kuwafichua ili wafikishwe katika vyombo vya dola na hivi sasa wanaendelea na mipango ya ujenzi wa kituo kikubwa cha Polisi kitakachoendana na hadhi ya eneo hilo.

Nao wananchi mbalilmbali wa Mto wa mbu wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama wakati wote hususani kipindi hiki cha watalii wengi katika maeneo hayo na wameahidi kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi ili kuboresha usalama katika eneo hilo.

ASILIMIA 90 YA MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI KUFIKIWA BAADA YA MIAKA MITATU-MAJALIWA

0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo mipya ya kuchambua pamba inayofungwa katika kiwanda cha Manonga wilayani Igunga akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora Agosti 16, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo inaposimikwa mitambo mipya ya kuchambua pamba katika kiwanda cha Manonga wilayani Igunga wakati alipokitembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora, Agosti 16, 2018. Kiwanda hicho ambacho kilisimamisha uzalishaji miaka 25 iliyopita kimefufuliwa na wamiliki wake , Chama Kikuu cha Ushirika cha mkoa wa Tabora, Igembensabo na Kampuni ya M/S Rajani Metals and Machinery kutokana na hamasa kubwa ya uchumi wa viwanda inayofanywa na serikali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Chomachankola wilayani Igunga akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora, Agosti 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema baada ya mitatu Serikali itakuwa imefikia asilimia 90 ya lengo iliyojiwekea la kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda.

Amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi waTaifa na wa wananchi ili kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuipa ushirikiano.Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Agosti 16, 2018) alipozungumza na wananchi katika kijiji cha Chomachankola wilayani Igunga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Igunga, Tabora.

“Tunaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waipe ushirikiano Serikali yao katika kipindi hiki ambacho inaendelea kutekeleza ahadi yake ya kuinua uchumi,” alisema.Kadhalika, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaendelea na utekelezaji wa ahadi zote zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli pamoja na zile zilizomo kwenye Ilani ya uchaguzi.

Waziri Mkuu alitaja ahadi hizo kuwa ni pamoja na ujenzi na ufufuaji wa viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali nchini, kikiwemo kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga.Alisema kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga ambacho kisimama kuchambua pamba kwa miaka 25 na sasa kimefufuliwa na kinafanya kazi, hivyo aliwaomba wananchi watoe ushirikiano kwa mwekezaji.

Wakati huo huo, wananchi wa wilaya ya Igunga waliishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt Magufuli kwa kuwezesha kukufuka kwa kiwanda chao cha kuchambua pamba cha Manonga.Akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya wananchi, Mbunge wa jimbo la Manonga, Seif Gulamali alisema ufufuaji wa kiwanda hiko umeongeza tija kwa wakulima wa zao la pamba na wananchi kwa ujumla.

Alisema mbali na kufufuliwa kwa kiwanda hicho, pia wanaishukuru Serikali kwa hatua mbalimbali za kuboresha maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kupeleka sh. milioni 500 za ujenzi wa daraja la Mto Manonga.“Umbali wa kutoka Manonga hadi Shinyanga ni kilomita 40, lakini tunalazimika kwenda hadi Nzega ili kufika Shinyanga ambako ni zaidi ya kilomita 130, tunaishukuru Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa litaturahisishia safari,” alisema.

Mbunge huyo aliongeza kuwa miradi mingine mingine inayotekelezwa Serikali inayotekelezwa katika jimbo la Manonga ni pamoja na ujenzi wa mabweni kwenye shule tatu za sekondari na ujenzi wa kituo cha afya cha Simbo ambayo gharama yake inakadiriwa kuwa sh. milioni 880.

Kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano huo wa hadhara, Waziri Mkuu alitembelea na kukagua ufungaji wa mitambo mipya na shughuli ya kuchambua pamba katika kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga, ambapo amisema amefurahishwa na kazi inayoendelea kiwandani hapo.

NDC wazindua Uuzaji wa Trekta za URSUS Mkoa wa Mwanza

0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya NDC Dr Samuel Nyantahe akitoa maelezo juu ya mradi wa kuunganisha matrekta unaotekelezwa hapa nchini chini ya NDC wakati wa uzinduzi wa Uuzaji Trekta hizo mkoa wa Mwanza katika eneo la Viwanda Makuyuni.( 16.08.2018)
Mwakilishi kutoka Bneki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw Steven Kang’ombe akitoa maelezo ya namna ya kupata mikopo ya ununuzi wa Trekta za URSUS wakati wa uzinduzi wa uuzaji Trekta hizo mkoa wa Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg John Mongella akibadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa Serikali wakati wa Uzinduzi wa Uuzaji wa Trekta za URSUS mkoa wa Mwanza katika eneo la Viwanda Makuyuni jana (16.08.2018)

KATIBU MKUU CCM AAMUA KUWAJIBU UBALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA

0
0

*Awataka Marekani kuheshimu uhuru kamili wa Taifa letu
*Asema chaguzi hizo zimefanyika kwa misingi ya kisheria

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Bashiru Ally ameamua kutoa msimamo wa Chama hicho kuhusu taarifa iiliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kuhusu uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu pamoja na kata 71 uliofanyika hivi karibuni.

Baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao CCM imepata ushindi mkubwa , Ubalozi wa Marekani waliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya habari wakionesha kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo.

Hivyo Dk.Bashiru Ally leo amezungumzia taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani ambapo amesema ameisoma na kuilewa na wao kama Chama wanazingatia zaidi uhuru wa kitaifa na wanayo dhama ya kuulinda.

“Kauli ambayo wameitoa inagusa maeneo mengi na matarajio yangu taasisi zote zinazohusika zitazingatia madukuduku yao.

“Ninachojua mimi chaguzi hizi zimefanyika kwa misingi ya kisheria na mataifa mengine likiwamo la Marekani wanapaswa kuheshimu chaguzi zetu,”amesema Dk.Bashiru Ally.Mbali ya kauli hiyo ya Dk.Bashiru pia wachambuzi waliobobea kwenye medani za siasa nchini akiwamo Dk.Benson Banna wameonesha kusikitishwa na taarifa hiyo ya ubalozi wa Marekani nchini.

ELIM MSINGI KUENDELEA KWA MIAKA7

0
0
JOSEPH MPANGALA -MTWARA.

Serikali imesema Imefuta Mpango wa Kufanya Elimu ya Msingi Kuishia darasa la Sita Kutokana na Kuonekana Mfumo wa Kuishia Darasa la Saba Hauna matatizo Yoyote na Umeendelea Kufanya Vizuri kwa Wanaomaliza.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha mara baada ya Kumaliza kutembelea Chuo cha Ualimu Kitangali Kilichopo Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara.Ole Nasha Amesema Mpango wa Elim ya Msingi Kuishia darasa la Sita Ulikuwepo lakini baada ya Kupokea mawazo Wameamua Kuacha kama Ilivyo.

“Kulikuwa na Mpango wa kujaribu kufanya sasa Elimu ya msingi iishie darasa la Sita iwe miaka sita lakini kwa sasa hakuna huo Mpango tumerudi kwenye mfumo wetu wa kawaida kwa sababu moja tu hakuna kitu kilicho haribika, kila mtu aliyesoma Nchi hii amesoma kwa mfumo ule hatujaona kama unamapungufu yoyote kwa hiyo tutaendelea na utaratibu wetu wa Miaka Saba”amesema Ole Nasha

Aidha Naibu waziri amewataka Makandarasi wanaojenga Katika Mradi wa Chuo Cha Kitangali Kuhakikisha wanamalizia Ujenzi Pindi watakapo pata Pesa Kutoka serikalini.

“Mimi ninaloondoka nalo hapa ni kwenda kuhakikisha kwamba Fedha Yaani Certificate hizo ambazo zimetoka karibuni kwamba zinalipwa mapema, Rai yangu kwenu Jamani Mradi huu umechukua muda mrefu,karibia miaka miwili kwa hiyo fedha zikilipwa kila mmoja ajitahidi huu Mradi sasa uishe na ukabidhiwe ili lengoletu lile na chuo kuweza kudahili Wanafunzi wengi zaidi Liweze Kufikia”Amesema Ole Nasha..

Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Ualimu kitangali Unagharimu Shilingi billioni 8 lakini mpaka sasa Wakandarasi wamekwisha Pewa Shilingi Billion 3.2 jambo ambalo limepelekea Mradi huo Kuchukua Miaka 2 Kushindwa Kumalizika.
Kulia Naibu waziri wa Elim Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa na Mkuu wa Chuo Cha mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Mtwara Samweli Kibehele wakati wa ziara ya Kutembelea Chuo hicho kwa lengo la kutazama mazingira yanayotumika kufundishia Wanafunzi wa VETA. 
Naibu waziri wa Elim Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipewa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Chuo Cha Ualim Kitangali na Mshauri wa Ujenzi Nicodemus Mgaya katika ziara yake ya kutazama Maendeleo ya Ujenzi Huo.
Naibu waziri wa Elim Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha Akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchii FDC ambacho kimeanzishwa mwaka 1975 ambacho kinafundisha masomo ya Umeme,Ufundi wa Magari pamoja na Ushonaji.

BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKAGUA MIRADI NA KUWAASA WATUMISHIWILAYANI SONGWE

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Mbuyuni Wilayani Songwe, kituo hicho kilipokea shilingi milioni 400 kutoka serikali kuu na kinatarjiwa kukamilika mwezi ujao.
Wananchi wa Kata ya Mbuyuni Wilayani Songwe wakijitolea shughuli mbalimbali za ujenzi katika Kituo cha Afya Mbuyuni ambapo serikali kuu ilitoa shilingi milioni 400 na kituo hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi ujao.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela akikagua mradi wa maji Mbuyuni ambao ulikamilika mwaka 2014 lakina bado wananchi hawapati maji kutokana na maji katika chanzo hicho kuwa na rangi mbaya, Brigedia Jenerali Mwangela amemuagiza mhandisi wa maji wilayani humo kufaya utafiti wa chanzo kingine haraka.



Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela jana jioni amehitimisha ziara yake ya siku mbili Wilayani Songwe, ambapo amekagua miradi kumi ya maendeleo na kisha kuzungumza na watumishi na watendaji wa taasisi mbalimbali zilizomo wilayani humo.

Brigedia Jenerali Mwangela akiwa ameambatana na baadhi ya maafisa wa Mkoa wa Songwe akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe wametoa maelekezo yaliyohusu kuboresha utendaji kazi kwa watumishi wa Wilaya ya Songwe.

Amesema “nimegundua kila ambacho alinieleza Mkuu wa Mkoa aliyestaafu kuhusu wilaya ya Songwe ni sahihi, upungufu alio uona nami pia nimeuona, napenda kusema mlikuwa mnamuona ni yeye Mkali ila mimi nasema alikuwa Mvumilivu”.

Brigedia Jenerali Mwangela amesema hatosita kumsema na kumchukulia hatua mtendaji anayeenda kinyume na sheria na taratibu za utumishi wa umma hivyo basi watumishi hao wabadilike na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano, watembelee na kukagua miradi inayotekelezwa wilayani humo.

Aidha amempongeza Mkuu wa Shule ya Sekodari ya Kanga wilayani humo ambapo alifanya ziara ya kushtukiza na kuwakuta walimu wote wapo darasani wanafundisha na mwalimu mkuu huyo akiwa anafundisha huku akisimamia ujenzi wa mabweni shuleni hapo, amemshauri mwalimu huyo kutumia wataalamu wa ujenzi wa wilaya ili Kusimamia ubora.

Baada ya kutembelea Daraja la Kikamba linalounganisha kata ya Kapalala na Gua, Brigedia Jenerali Mwangela amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Songwe Kumsimamia mkandarasi ili aweze kukamilisha ujenzi wa daraja hilo kwa muda uliopangwa ambao ni Septemba 7, mwaka huu.

Katika kituo cha Afya Mbuyuni amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo kuhakikisha ujenzi unapokamilika, vifaa tiba, dawa na wataalamu wa Afya wawepo ili kituo hicho kianze kutoa huduma kwa wananchi na meneja wa Tanesco kwa kushirikiana na Mkoa kuhakikisha kituo hicho kitakapoanza kutoa huduma kiwe na umeme.

Brigedia Jenerali Mwangela amemtaka mhandisi wa maji Wilayani humo kufanya utafiti wa haraka wa chanzo kingine cha maji kwa ajili ya mradi wa maji Mbuyuni kwakuwa wananchi wamekataa kuyatumia maji ya chanzo cha awali kutokana na maji hayo kuwa na rangi mbaya.

Ameongeza kuwa wataalamu waliofanya utafiti awali hawakutendea haki taaluma yao na hivyo kusababisha hasara kwa serikali huku wananchi wakiendelea kupata kero ya maji tangu mradi huo ukamilike mwaka 2014.

Brigedia Jenerali Mwangela amemtaka Afisa Afya wa Wilaya ya Songwe kutoa elimu kwa wananchi ili wajenge vyoo bora, elimu ya masuala ya lishe, pia ahamasishe upimaji afya zao hususani kwa magonjwa yasioambukiza kama tezi dume, kisukari, VVU pamoja na kufanya tohara.

Ameongeza kwa kuwataka watunze mazingira na kuendelea kusimamia agizo la katazo la ukataji ovyo miti kwa ajili ya biashara ya mkaa, aidha ameelekeza wananchi wanaruhusiwa kuvuna miti katika maeneo maalumu yaliyotengwa na wakala wa huduma za misitu (TFS).

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Mathias Nyange amewataka watumishi kuacha utoro kwakuwa wengi wao ifikapo siku ya ijumaa hutoroka na kuelekea Mkoa wa jirani walipoweka makazi yao.


RPC Nyange amesema, “nitamshauri Mkuu wa Mkoa vikao viwe vinafanyika siku ya Jumamosi ili kufuta utoro huu, nawashauri watumishi unapopangiwa kituo cha kazi ndio kwenu papende, ufanye kazi kwa bidi”.


Ameongeza kuwa serikali inatukanwa kutokana na uzembe wa baadhi ya watumishi hivyo wajitume wabadilike na wafanye kazi kwa ushirikiano hasa katika kumsaidia mwananchi masikini apate maendeleo.

JAJI MZUNA NA MAJAJI WENZAKE WAKABIDHIWA RASMI OFISI YA MAHAKAMA KANDA YA ARUSHA

0
0
Aliyesimama ni Jaji Mfawidhi Mhe Jaji Mzuna akiwa anazungumza na watumishi
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Mhe Jaji Mosses Mzuna (katikati), kushoto ni aliyekuwa Kaimu Jaji Mfawidhi Mhe Jaji Sekela Moshi na Mhe. Jaji Thadeo Mwenempazi walipokuwa wakizungumza na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Arusha (hawapo pichani).
Mhe Jaji Thadeo Mwenempazi akizungumza jambo na Watumishi.




Na Catherine Francis –Mahakama Kuu Arusha

Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Mhe. Mosses Mzuna amekabidhiwa rasmi Kanda hiyo ya Mahakama na aliyekuwa Kaimu Jaji Mfawidhi, Mhe Jaji Sekela Moshi.

Makabidhiano hayo yamefanyika mapema Agosti 16 katika kikao cha utambulisho wa wahe.Majaji wapya pamoja na Jaji Mfawidhi ambayo pia yalihudhuriwa na baadhi ya Watumishi wa Mahakama.

Katika kikao hicho Mhe Jaji Moshi aliwasisitiza watumishi wa Mahakama Arusha kuendeleza ushirikiano, uwajibikaji na kufanya kazi kwa malengo kwani hiyo ndiyo sababu inayoifanya Arusha kuwa kanda ya mfano kwa mafanikio.Jaji Sekele aliendelea kuwahimiza watumishi waache kufanya kazi kwa mazoea bali wajitume kwa bidii ili kuweza kuondoa kabisa mlundikano wa kesi Mahakamani.

Kwa upande wake, Mhe Jaji Mzuna alimshukuru Mhe Jaji Moshi kwa mapokezi mazuri aliyoyaandaa yeye pamoja na viongozi wake, pia aliwaomba watumishi ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kila siku.Kwa kusisitiza hilo alinukuu usemi wa mwandishi John C Maxwell usemao “VALUE TEAM LEADERSHIP ABOVE INDIVIDUAL LEADERSHIP” akiwa na maana ya kuwa uongozi mzuri ni ule wa ushirikiano na siyo wa mtu binafsi.

Vilevile; Mhe Jaji Mwenempazi ambaye amepangiwa kazi katika Kanda hiyo ya Mahakama naye aliwaomba ushirikiano wa hali ya juu Watumishi kwa kuwa yeye ni mgeni.Mhe. Jaji Mwenempazi alisema kuwa yupo tayari kujifunza kutoka kwa Watumishi mbalimbali pasipo kujali ngazi ya mtumishi husika,hivyo aliwaomba watumishi kuwa tayari kumsaidia pindi atakapohitaji msaada.

Sambamba na Mhe Jaji Mfawidhi, Majaji wengine walioripoti katika Kituo hicho ni pamoja na Mhe Jaji Issa Maige aliyetokea Mwanza na Mhe Jaji Thadeo Mwenempazi ambaye ni Kituo chake cha kwanza tangu ateuliwe kuwa Jaji.

Kabla ya uhamisho huu, Mhe . Jaji Mzuna alikuwa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Dar es Salaam na Mhe. Jaji Sekela alikuwa Kaimu Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, ambaye naye amepata uhamisho wa kwenda Mahakama Kuu kanda ya Songea kuwa Jaji Mfawidhi.

Madaktari Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Afrika wa nchini Marekani washirikiana kutibu wagonjwa 22 kambi maalum magonjwa ya moyo

0
0
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakiangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo wa mgonjwa unavyofanya kazi kabla ya kumwekea kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Implantable cardioverter defibrillator – ICD) katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakiandaa vifaa vitakavyotumika katika upasuaji mdogo wa kumuwekea mgonjwa kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufa nya kazi vizuri (Implantable cardioverter defibrillator – ICD) katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.

Na Genofeva Matemu na Salome Majaliwa

17/08/2018 Jumla ya wagonjwa 22 wenye matatizo ya moyo yatokanayo na mfumo wa umeme wa moyo usiofanya kazi sawasawa wamefanyiwa upasuaji mdogo na kuwekewa vifaa maalum vitakavyousaidia moyo kufanya kazi vizuri.

Matibabu hayo yamefanyika katika kambi maalum ya siku saba iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mgonjwa kufanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Magonjwa ya moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge alisema kambi hiyo inafanywa na madaktari wa Taasisi ya Moyo kwa kushirikiana na wenzao wa nchini Marekani kutoka Shirika la Madaktari Afrika.

Dkt. Kisenge alisema kambi hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo ambao mapigo yao yako chini kwa asilimia hamsini kwa dakika kwa kuwawekea kifaa maalum akinachosaidia mapigo ya moyo kuongezeka (Pacemaker).

“Kazi ya kifaa hiki maalum cha mfumo wa umeme wa moyo ni kuwasaidia wagonjwa wasipoteze maisha ghafla, kwani mara nyingi wagonjwa wenye matatizo ya mapigo ya moyo ambayo yako chini hufa vifo vya ghafla”, alisema Dkt. Kisenge.

Kuhusu matibabu waliyopatiwa wagonjwa katika kambi hiyo Dkt. Kisenge alisema zoezi limeenda vizuri na kwa ufanisi mkubwa kwa wagonjwa kuwekewa vifaa vya pacemaker na ICD (Implantable cardioverter defibrillator – ICD) kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini ya asilimia 30.

Kwa upande wake Prof. Matthew Sackett kutoka Madaktari Afrika alisema kambi hiyo ilienda sambamba na utoaji wa elimu kwa madaktari na wataalam wengine wa afya ambao baada ya mafunzo hayo wataweza kuwawekea wagonjwa kifaa cha ICD ambapo kabla ya hapo hawakuwa wanaweza kufanya hivyo.

“Wiki hii imekuwa ni wiki ya mafanikio kwetu, tumetibu wagonjwa na nimetoa elimu ya namna ya kumuwekea mgonjwa kifaa cha ICD kwa madaktari na wataalam wengine wa afya, kila nitakapopata nafasi nitakuja kutoa huduma kwa wagonjwa na elimu kwa wafanyakazi”, alisema Prof. Sacckett.

WASANII WA FILAMU WAASWA KUJUA THAMANI YA KAZI ZAO

0
0

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akiongoza kikao na viongozi wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association-Kinondoni) walipotembelea ofisi za Bodi ya Filamu kuwatambulisha viongozi wa chama hicho kwa uongozi wa Bodi ya Filamu hivi karibuni katika Ofisi za Bodi ya Filamu Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association-Kinondoni) wakifuatilia taarifa iliyokua ikitolewa wakati wa kikao na Bodi ya Filamu kuwatambulisha viongozi hao hivi karibuni katika Ofisi za Bodi ya Filamu Jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (wanne kulia) katika picha ya pamoja na Wanachama na Wajumbe wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association-Kinondoni) baada ya kikao na wajumbe hao walitembelea ofisi za Bodi ya Filamu kuwatambulisha viongozi wa chama hicho kwa uongozi wa Bodi ya Filamu hivi karibuni katika Ofisi za Bodi ya Filamu Jijini Dar es salaam.

………………………………………………………………………………………

Na Mwandishiwetu

Wanatasnia wa filamu na michezo ya kuigiza nchini wameaswa kujua thamani yao na kazi zao katika kulinda maadili na utamaduni wa kitanzania ili kujijengea heshima mbele ya jamii na wapenzi wa kazi zao.

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association – Kinondoni) walipotembelea na kufanya kikao katika Ofisi za Bodi ya Filamu Mtaa wa Samora Jijini Dar es salaam.

Bibi. Fissoo alisema baadhi ya wanatasnia ya filamu wanaonyesha mwenendo unaokinzana na maisha na maadili ya kitanzania huku miongoni mwao wakifanya vitendo vinavyodhalilisha utu na heshima hivyo kuitia doa tasnia nzima ya filamu na michezo ya kuigiza.

“Nawapongeza Chama cha Waigizaji kwa kushirikiana na serikali katika kukemea wale wanachama wachache wanao chafua taswira ya tasnia. Ni muhimu kuendelea kuongeza nguvu katika nidhamu, matumizi ya lugha zenye staha, mavazi yanayoonyesha taswira chanya ya taifa letu; hivyo endeleeni kuiunga mkono Serikali katika hatua inazozichukua” alisema Fissoo

Kwa upande wake Msemaji wa Chama hicho Bw. Masoud Kaftany alisema lengo la kukutana na Bodi ya Filamu Tanzania ni kuwatambulisha viongozi na kamati ya matukio, maadili na mikataba kutoka kwenye chama cha Waigizaji Kinondoni kwa uongozi wa Bodi ya Filamu kama njia mojawapo ya kuendeleza ushirikiano katika tasnia hiyo.

“Kamati yetu inaundwa na wawakilishi 13 wakiongozwa na Mwenyekiti bwana Ahmad Hussein, Katibu bwana Khalifan Ahmed na Msemaji bwana Masoud Kaftany na leo tumekuja Bodi ya Filamu kujitambulisha na kujifunza Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili zitusaidie katika utendaji wa kila siku wa kazi zetu” alisema Kaftany

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Chama hicho Bi. Vanitha Omari ameiomba Bodi ya Filamu kutochoka kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu ili waweze kupata uelewa stahiki katika tasnia kwa ujumla.

Chama cha waigizaji wa filamu Mkoa wa Kinondoni ni miongoni mwa vyama vinavyounda vyama vya waigizaji wa filamu taifa na ni chama ambacho kimekuwa mfano katika kutetea maslahi na haki za wanachama wake.

WAENDESHA MASHTAKA KUJENGEWA CHUO

0
0


 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Bw. Biswalo Mganga akisalimia na Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  muda mfupi kabla ya  Waziri Mkuu kuzindua Ofisi  ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tukio lilofanyika kati kati ya wiki Jijini Dodoma. Katika taarifa yake DPP Mganga alieleza mpango wa Ofisi yake kujenga Chuo kitakachotoa mafunzo kwa Waendesha Mashtaka nchini. (Picha na  Habari  kwa hisani ya  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali






Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, inakusudia kujenga Chuo cha aina yake kwaajili ya waendesha mashtaka nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo na ujuzi wa uendeshaji wa kesi na mashauri ya jinai.

Mkurugezi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, (DPP) Bw. Biswalo Mganga amesema Chuo hicho kitajengwa eneo la Usagara. Jijini Mwanza ambako tayari hekta 25 zimeshapatika kwaajili ya ujenzi huo.

Kwa Mujibu wa DPP ujenzi wa Chuo hicho unatokana na ukweli kwamba, hakuna chuo chochote kinachotoa mafunzo ya uendeshaji na usimamiaji wa kesi za jinai na kwa sababu hiyo Ofisi yake imeona kuna haja na umuhimu wa kuwapo kwa Chuo hicho.

Alikuwa akizungumza wakati hafla ya uzinduzi wa ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, uliofanywa mwanzoni mwa wiki hii, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jijini Dodoma

“Mhe. Waziri Mkuu, moja ya mikakati na mipango tuliyonayo ni kujenga chuo cha aina yaka katika Afrika ya Mashariki kitakachotoa mafunzo na namna ya kuendesha kesi za jinai. Tumeshapata hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekta 25 eneo la Usagara Mwanza kwaajili ya ujenzi wa chuo hicho”. Amebainisha Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka.

Bw. Mganga ameeleza kwamba ujenzi wa chuo huo utafanywa kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo na wadau mbalimbali, na kuwa sasa hivi ofisi yake ipo katika hatua za mwisho kukamilisha andiko kwa ajili ya kuombea fedha za ujenzi wa chuo hicho.

“Malengo yetu ni kuwa na chuo ambacho baadaye kitatumika kuwafundisha waendesha mashtaka kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika na baadaye Afrika kwa ujumla”.

Akasema baadhi ya walimu watakao toa mafunzo hayo watakuwa ni pamoja na mawakili wa serikali ambao wamekwisha staafu na ambao wamebobea na kuwa na uzoefu mkubwa katika uendesheshaji wa kesi za jinai.

DPP ameiomba Serikali kuunga mkono ujenzi wa chuo hicho na kuhakikisha kwamba ujenzi wake unaanza mara moja.

Akielezea baadhi ya majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kufuatia muundo mpya uliotangazwa kupitia Tangazo la Serikali Namba 49 la mwaka 2018 Ofisi ya Mashtaka ni huru na yenye mamlaka kamili ambayo baadhi ya majukumu yake ni pamoja na;

Kuchukua na kuendesha kesi zote za jinai kwa niaba ya Jamhuri; kuratibu na kusimamia upelelezi wa makosa ya jinai na kusimamia uendeshaji wa keshi hizo katika mahakama zote nchini, kuwasimamia mawakili wa serikali na waendesha mashtaka wote nchini na watumishi wote waliopo katika ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kumtaka mtumishi yeyote wa Serikali kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na uendeshaji wa kesi za jinai.

Majukumu mengine ni kuchukua na kuendeleza mwenendo wa mashauri, rufaa au utekelezaji wa amri inayotokana na shauri lolote ambalo Jamhuri ina maslahi nayo na kutoa mwongozo kwa watumishi wa Umma wanaofanya shughuli zinazohusiana na uendeshaji wa mashauri ya jinai mahakamani.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameunga mkono hoja na mpango wa kujengwa kwa Chuo hicho.

Akasema Waziri Mkuu ” Ofisi ya Mashtaka iendelee na mpango wake wa kupanua wigo wake wa utoaji huduma na kuboresha uelewa wa mwenendo wa mashtaka kwa kutekeleza mpango wa ujenzi wa Chuo mahususi kwa kazi hiyo”.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa ni muhimu na sisi ( Tanzania) tukawahi kukijenga chuo hicho ili tupate faidia ambazo zimeainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Waziri Mkuu amesema kuwa matarajio ya kila mtanzania ni kuwa Ofisi hiyo haitotumia vibaya taratibu za utoaji haki kama vile kuchelewesha usikilizaji wa kesi au kupinga dhamana za watuhumiwa bila ya kuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo.

“Ni matumaini ya watanzania kwambma katika utekelezaji wa majukumi yenu hamtawafungulia kesi watuhumiwa bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuwafungulia watuhumiwa kesi zaidi ya mara mbili au tatu bilaya kuwa na ushahidi wa kutosha hata pale ambapo watuhumiwa hao wameachiwa na mahakama.” Amesisitiza Waziri Mkuu

Na kuongeza ” Sanjari na hayo, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inapswa na inategemewa kuzingatia maslahi ya umma kwa kufungua na kuendesha mashtaka ambayo yana maslahi ya umma tu. Ofisi haipaswi kujishughulisha na masuala ambayo kwa ujumla wake au kwa taathira yake hayazingatii maslahi ya umma na hiyvo, kuisababishia hasara Serikali kwa maana ya upotevu wa muda na matumizi mabaya ya raslimali.


Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Bw. Biswalo Mganga akisalimia na Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa muda mfupi kabla ya Waziri Mkuu kuzindua Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tukio lilofanyika kati kati ya wiki Jijini Dodoma. Katika taarifa yake DPP Mganga alieleza mpango wa Ofisi yake kujenga Chuo kitakachotoa mafunzo kwa Waendesha Mashtaka nchini. (Picha na Habari kwa hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

MAJALIWA APOKEA MIFUKO 50 YA SARUJI KWA AJILI YA JIMBO LA BUKENE

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi mbunge wa Bukene, Selemani Zedi (kushoto) mifuko 50 ya saruji iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora kupitia CCM, Munde Tambwe (wapili kushoto ) baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa wa Bukene wilayani Nzega Agosti 17, 2018 saruji hiyo imetolewa kwa jimbo la Bukene ili isaidie katika ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii jimboni humo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi mbunge wa Bukene, Selemani Zedi (kushoto) mifuko 50 ya saruji iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora kupitia CCM, Munde Tambwe (wapili kushoto ) baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa wa Bukene wilayani Nzega Agosti 17, 2018 saruji hiyo imetolewa kwa jimbo la Bukene ili isaidie katika ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii jimboni humo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Taifa wa Bukene wilayani Nzega, Agosti 17, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waganga Wakuu wa Mikoa/Halmashauri Wapigwa Msasa Kuhusu Sheria ya Takwimu

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya mkutano huo ni; “Uboreshaji wa Mazingira ya Kutolea Huduma za Afya ni Msingi wa Wananchi Kuelelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati”.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akizungumza alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu takwimu za afya katika Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya leo Jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia Sekta ya Afya, Dkt. Zainabu Chaula, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye ndiye mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mkutano huo, Anthony Mtaka na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya. Kauli mbiu ya mkutano huo ni; “Uboreshaji wa Mazingira ya Kutolea Huduma za Afya ni Msingi wa Wananchi Kuelelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati”.


Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akizungumza alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu takwimu za afya katika Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya mkutano huo ni; “Uboreshaji wa Mazingira ya Kutolea Huduma za Afya ni Msingi wa Wananchi Kuelelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati”.
Baadhi ya washiriki wa mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini wakifuatilia mada kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya mkutano huo ni; “Uboreshaji wa Mazingira ya Kutolea Huduma za Afya ni Msingi wa Wananchi Kuelelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati”.

RAIS DKT MAGUFULI AAGA MWILI WA MAREHEMU MEJA JENERALI MSTAAFU JOSEPH ANAEL LESULIE. ADA ESTATE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akitia saini katika kitabu cha Maombelezo cha Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Joseph Anael Lesulile, Ada Estate Kinondoni nyumbani kwa marehemu,aliyefariki dunia agosti 14,2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam,Agosti 17,2018
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwapa pole familiya ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Joseph Anael Lesulile, Ada Estate Kinondoni nyumbani kwa kufiwa na baba yao aliyefariki dunia agosti 14,2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam,Agosti 17,2018
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Joseph Anael Lesulile, Ada Estate Kinondoni nyumbani kwa marehemu,aliyefariki dunia agosti 14,2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam,Agosti 17,2018

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Joseph Anael Lesulile, Ada Estate Kinondoni nyumbani kwa marehemu,aliyefariki dunia agosti 14,2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam,Agosti 17,2018
Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Joseph Anael Lesulile, Ada Estate Kinondoni nyumbani kwa marehemu,aliyefariki dunia agosti 14,2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam,Agosti 17,2018. Picha na Ikulu.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI UFUNGUZI RASMI WA MKUTANO WA KILELE WA 38 WA SADC

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa meza kuu na viongozi wenzake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kilele wa kawaida wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika ukumbi wa hoteli ya Safari mjini Windhoek nchini Namibia leo Ijumaa Agosti 17, 2018 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa meza kuu na viongozi wenzake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kilele wa kawaida wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika ukumbi wa hoteli ya Safari mjini Windhoek nchini Namibia leo Ijumaa Agosti 17, 2018

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga akiwa na ujumbe wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kilele wa kawaida wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika ukumbi wa hoteli ya Safari mjini Windhoek nchini Namibia leo Ijumaa Agosti 17, 2018 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa meza kuu na viongozi wenzake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kilele wa kawaida wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika ukumbi wa hoteli ya Safari mjini Windhoek nchini Namibia leo Ijumaa Agosti 17, 2018

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na viongozi wenzake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kilele wa kawaida wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika ukumbi wa hoteli ya Safari mjini Windhoek nchini Namibia leo Ijumaa Agosti 17, 2018

Waziri Dk. Kigwangalla kuruhusiwa muda wowote MOI, Kikwete amtembelea tena

0
0


Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI anapopatiwa matibabu alipomtembelea kwa mara nyingine jana.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI anapopatiwa matibabu alipomtembelea kwa mara nyingine jana. Picha zote na Andrew Chale,

………………………………………………………………………………….

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtembelea na kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa katika wodi maalum kitengo cha Taasisi ya mifupa MOI, hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa mara nyingine tena.

Hii inakuwa ni mara ya tatu kwa Kikwete kumtembelea Dk Kigwangalla ambapo awali alimtembelea Agosti 8,2018 alipokuwa amelazwa Wodi ya Mwaisela akipatiwa Matibabu ya awali na juzi Agosti 15,2018 katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI.

Akiwa hospitaini hapo mapema jana, Kikwete ameweza kumjulia hali na kubadilishana nae mawazo mbalimbali huku akimtakia unafuu aendelee na majukumu yake ya kila siku na akimpongeza kwa shughuli zake anazozifanya katika kuinua sekta ya Utalii pamoja na kulinda rasilimali za Maliasili.

“Nikutakie kheri. Nashukuru kwa kukuta unaendelea vizuri sasa na nilikuja ukiwa upo unaongea ukiwa umelala kitandani na kwa sasa nimekuja tena umeweza kuimarika na hata kutembea na kukaa kama hivi hongera sana” alieleza Kikwete wakati akimjulia hali Waziri Kigwangalla wodini hapo.

Tayari jopo la Madaktari bingwa wa MOI wamebainisha kuwa Dkt. Kigwangalla kwa sasa anaendelea vizuri na muda wowote anaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani ambapo kwa sasa sehemu zilizobakia ni mkono wake wa kushoto ambao kila siku unaendelea kuimarika.

Hata hivyo, Dkt. Kigwangalla amemweleza Kikwete kuwa kwa sasa hali yake inaendelea kuwa vizuri na muda wowote anaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani huku akiendelea na mazoezi kidogokidogo.

Aidha, jioni ya jana Dkt. Kigwangalla ameweza kufanya mazoezi ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa moja kuanzia kwenye viunga vya Hospitali hiyo na kuzunguka maeneo yanayozunguka Muhimbili na baadae kupanda kwa kutumia ngazi katika jengo anapopatiwa matibabu kwa miguu mpaka gorofa ya sita.

Waziri Dkt. Kigwangalla alipata ajali ya gari mnamo Agosti 4, 2018 huko Manyara akiwa katika ziara ya kikazi ambapo katika ajali hiyo iliyokuwa na watu 6, Afisa Habari wa Wizara hiyo Hamza Temba alifariki dunia huku watano wakijeruhiwa akiwemo yeye anaendelea na matibabu Hospitalini hapo.

MKUCHIKA AWATEMBELEA BAADHI YA VIONGOZI WAKUU WASTAAFU IKIWA NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE

0
0








Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Cleopa D. Msuya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Cleopa D. Msuya alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Cleopa D. Msuya alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Joseph S. Warioba alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Joseph S. Warioba alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mwanza aunga mkono juhudi za mbunge wa Nyamagana

0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kampuni ya Mwanza Huduma imeunga mkono juhudi za maendeleo za mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe.Stanslaus Mabula (CCM), kwa kumkabidhi mifuko 230 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu.


Akikabidhi mifuko hiyo leo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Zulfikar Nanji ametoa rai kwa wafanyabiashara wengine kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo badala ya kuitegemea serikali pekee.


Akipokea mifuko hiyo, Mhe.Mabula ameishukuru kampuni hiyo kwa kuendelea kusaidia miradi ya maendeleo katika jimbo la Nyamagana na kwamba mifuko hiyo itasaidia kukamilisha shughuli za ujenzi katika sekta ya elimu na afya jimboni Nyamagana.


Naye Mwenyekiti wa taasisi ya maendeleo ya First Community, Ahmed Misanga ametoa pongezi kwa mbunge Mabula pamoja na kampuni ya Mwanza Huduma kupitia kwa Mkurugenzi wake Zulfikar Nanji kwa ushirikiano huo ambao unaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano za kufikisha maendeleo kwa wananchi.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Zulfikar Nanji (kushoto) akimkabidhi mifuko 230 ya saruji (simenti) mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe.Stanslaus Mabula (wa tatu kulia) kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo jimbo la Nyamagana
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images