Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1648 | 1649 | (Page 1650) | 1651 | 1652 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Aliyekuwa mhasibu wa Chuo cha ustawi wa Jamii, Gryson Mnyawami, amehukumiwa kwenda jela miaka mitano baada ya kupatikana na hata wizi wa zaidi ya sh. Milioni 9 akiwa mtumishi

  Hukumu hiyo, imesomwa leo Agosti 15,2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega,

  Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mtega amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watano wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa la wizi.Hata hivyo, kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Hakimu Mtega alitaka mwendesha mashtaka kusema kumbukumbu kama mshtakiwa anamakosa mengine au  La

  Mwendesha Mashtaka, wakili wa Serikali Janeth Magoho ameieleza mahakama kuwa, hakuna kumbukumbu za makosa kwa mshtakiwa, hili ni kosa lake la kwanza.Mheshimiwa Hakimu, sina kumbukumbu za zamani za mshtakiwa, ila naomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa kitendo cha wizi alichofanya mshtakiwa haswa akiwa kama mtumishi wa umma ni kibaya, kinaitia hasara kubwa Serikali

  Wakili Janet ameongeza, suala la wizi katika Chuo cha ustawi limekuwa likitokea mara kwa mara Kitendo cha yeye kudhulumu wanafunzi siyo haki kwani ile ni hela ya walipa kodi, adhabu kali itakuwa fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo

  Katika utetezi wake, mshtakiwa Mnyawami, ameiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu, alikubali kulipa fedha hizo taratibu lakini taasisi ndiyo ilimkatalia,Ameongeza kuwa Dada yake ni mgonjwa na mama yake ni mjane na wote wanamtegemea yeye.

  Awali ilidaiwa, May 31, 2014 katika Chuo cha ustawi wa jamii kilichopo Kijitonyama wilayani Kinondoni mtuhumiwa akiwa ameajiriwa kama mhasibu wa Chuo hicho aliiba sh, 9,714,000 Mali ya muajiriwa wake ambayo  ameipata kutokana na nafasi yake kazini hapo,

  0 0


  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza mjini Babati jana kwenye kikao cha uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na Naibu Waziri wa Maliasili na
  Utalii, Japhet Hasunga.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza mjini Babati kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (kulia) akimuongoza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa jana mjini Babati.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akizungumza mjini Babati kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

  …………………………………………………………………………..

  WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi amezindua mpango wa kupimwa jumla ya vijiji 392 vinavyopakana na hifadhi za Taifa nchini kwenye mikoa mitano kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo hayo.

  Waziri Lukuvi akizungumza katika uzinduzi huo, uliofanyika Babati mkoa wa Manyara alisema mpango huo utasaidia kutatua migogoro baina ya vijiji na hifadhi lakini pia vijiji kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.

  Alisema, katika mpango huo, awamu ya kwanza itahusisha vijiji 95 katika mikoa mitatu nchini ila lengo ni kufikia mikoa mitano ya Manyara, Mara, Simiyu, Dodoma na Arusha.

  “Vijiji hivi vikipimwa vitakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ambapo maeneo ya makazi yatajulikana maeneo ya mifugo na maeneo ya kilimo yatatengwa” alisema

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga,alisema Wizara hiyo, imejipanga kushirikiana na Wizara ya ardhi na wadau wengine kutatua migogoro ya ardhi.

  Alisema mpango wa kupima vijiji 392 vinavyopakana na TANAPA utakuwa ni shirikishi na utasaidia sana kutatua migogoro ya uhifadhi lakini utasaidia vijiji.

  “Katika mpango huo,zitatolewa hati 2375 ambazo zitasaidia wananchi kumiliki maeneo yao” alisema

  Mkurugenzi wa uhifadhi wa TANAPA, Martin Loiboki alisema mpango , utasaidia sana kulinda Shoroba na maeneo mtawanyiko wa wanyama kwani mengi yamezibwa kutokana na shughuli za kibinaadamu.

  Alisema kufungwa kuvamiwa na kufungwa maeneo ya mtawanyiko wa wanyama na uvamizi unaoendelea maeneo ya hifadhi kuna athari sana maendeleo ya uhifadhi na utalii nchini.

  Alisema kutokana na hali hiyo,TANAPA imeamua kushirikiana na tume ya matumizi bora ya ardhi kupima vijiji 392 vinavyopakana na hifadhi.

  Awali , Mkuu wa mkoa wa Manyara,Alexander Mnyeti alisema,mkoa wa Manyara unaunga mkono jitihada za kutatua migogoro ya ardhi.

  Hata hivyo alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watendaji wa wizara ya Maliasili na Utalii kwenda vijijini kupima Ardhi na kuweka mipaka bila serikali ya mkoa,wilaya na vijiji kutojua.

  Alisema mpango huo wa sasa wa TANAPA kwa sababu ni shirikishi unaungwa mkono asilimia 100 na mkoa wa Manyara.

  Mkuu wa mkoa Dodoma Dk Beneth Mahenge alisema kumekuwepo migogoro ya ardhi baina ya hifadhi na wananchi na akataka ipatiwe ufumbuzi.

  “Kuna vijiji vimesajiliwa ndani ya hifadhi sasa lazima tuamuwe cha kufanya ama kulinda hifadhi ama kuviacha vijiji hifadhini” alisema.

  0 0


  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Bakari akitoa mada kwenye mafunzo ya uongozi bora yaliowahusisha viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
  Baadhi wakurugenzi, wakuu wa idara, wakuu wa vitengo na mameneja wa majengo wakiwa kwenye mafunzo hayo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akipongezwa na Dkt. Kassim Hussein kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) baada ya Dkt. Bakari kumkabidhi cheti baada ya mafunzo hayo kufungwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa hospitali hiyo, Prof. Charles Majinge.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Muhimbili, Aminiel Aligaesha akipokea cheti kutoka kwa Dkt. Bakari baada ya mafunzo hayo.
  Dkt. Vicent Tarimo akipokea cheti baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo.
  Meneja wa Jengo la Utasishaji, Sister Batusaje naye akipokea cheti baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo.Meneja wa Jengo la Utasishaji, Sister Batusaje naye akipokea cheti baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo.
  Meneja wa Jengo la Wagonjwa wa Nje, Sister June Samwel akipokea cheti.
  Mwenyekiti wa Bodi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akifunga mafunzo hayo.

  ……………………………………………………………………………

  Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umeshauriwa kuongeza kasi na kuboresha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kutekeleza mipango mkakati iliyojiwekea ili kuokoa muda wa kutoa huduma na kufikia malengo yake.

  Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Kuwe Bakari wakati alipokua akiwasilisha mada juu ya matumizi ya TEHAMA, katika mafunzo ya utawala bora yaliyohusisha wajumbe wa bodi , wakurugenzi, wakuu wa idara pamoja na mameneja majengo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Kwa mujibu wa Dkt. Jabiri, mifumo ya TEHAMA inasidia kuwasiliana kwa wakati kutoka upande mmoja na mwingine tofauti na mfumo wa kutumia karatasi katika kutekeleza majukumu mbalimbali.

  Kutokana na umuhimuwa TEHAMA, amewashauri viongozi hao kuboresha mifumo ya TEHAMA kwa kutumia watalaam ambao wanaujuzi wa kutosha ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

  “Kama nyie wenyewe mtaweza kutengeneza mfumo wa TEHAMA itakua rahisi kuboresha ama kurekebisha pale inapotokea hitilafu, tofauti na kwenda kununua mfumo kutoka nje kwani hutojua ametumia utaalam gani kutengeneza mfumo huo,’’ amesema Dkt. Jabiri.

  Kwa upande wake Dkt. Kassim Hussein amewataka viongozi na watendaji wote kwa ujumla kukubali kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika kazi ili kufikia mafanikio na vilevile kutoa huduma yenye viwango vya juu.

  ‘’Changamoto zinapojitokeza katika majukumu yenu lazima mzichangamkie, mzipokee na mzishughulikie ipasavyo ili kufikia malengo ya taasisi, lakini pia muwe tayari kujifunza na kukubali kukosolewa, ‘’ amesema Dkt. Hussein.

  Mafunzo hayo ya siku mbili yamefungwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge ambapo pamoja na mambo mengine amewataka viongozi wa MNH kuzingatia mafunzo hayo ili kutekeleza vema majukumu ya Utumishi wa Umma.

  Washiriki wote wa mafunzo hayo walitunukiwa vyeti vya ushiriki kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT).

  0 0

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akitoa maelezo ya muundo mpya ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  na majukumu ya Ofisi hiyo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Uzinduzi wa Ofisi hizo tatu ulifanywa na Waziri Mkuu siku ya Jumatano jijini  Dodoma ( picha na habari na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali) 
   
   ………………………………………………………………
   
  Na Mwandishi Maalum, Dodoma
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, amezikumbusha  Wizara  na Taasisi  za Serikali ambazo bado hazijawasilisha mikataba ambayo imeombwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwaajili ya  marejejo kufanya hivyo  mapema iwezekanavyo.

  Ametoa wito huo siku ya  jumatano wiki  hii wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka . Uzinduzi huo ulifanywa na Mhe.  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Kassim  Majaliwa  Jijini Dodoma.

  Akielezea  Muundo  mpya wa Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu  wa Serikali  kwa  Mhe. Waziri Mkuu na majukumu ambayo Ofisi hii imepanga kuyatekeleza. Mwanasheria Mkuu ameyataja  baadhi  hayo ni pamoja na   marejeo ( review) ya mikataba muhimu kwa lengo la kuhakikisha mikataba hiyo ina masharti yanayolinda maslahi ya  taifa.

  “Tumepanga kufanya marejeo ya mikataba muhimu kwa lengo la kuhakikisha kuwa mikataba hiyo ina masharti yanayolinda maslahi ya taifa. Zoezi hili litahusisha mikataba yote ya kimataifa,  mikataba ya  uendelezaji  madini ( MDAs) na mikataba ya uzalishaji na mauzo ya gesi asilia”, ameeleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Mikataba mingine itakayofanyiwa marejeo ni  mikataba inayohusu uwekezaji baina ya Tanzania na nchi nyingine pamoja na mikataba mingine ambayo Serikali ina maslahi.

  “Mhe. Waziri Mkuu, ninaomba kutumia fursa hii kuzishukuru Wizara na Taasisi za Serikali kwa kuendelea kutupatia mikataba tunayoihitaji kufanyia marejeo. Kwa  Wizara na Taasisi ambazo  hazijawasilisha mikataba iliyoombwa, zinakumbushwa kufanya hivyo mapema ili shughuli hiyo ianze”.Pamoja na kufanya marejeo ya mikataba muhimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, Ofisi yake inapanga kuweka mfumo utakaokuwa na regista ya mikataba yote ya kimataifa ili iwe rahisi kuifanyia rejea au kupatikana pindi inapohitajika kwa matumizi mbalimbali ya kiserikali na kisheria.

  Vilevile Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Kilangi ameeleza  kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pia imejipanga kuwa na mkakati wa kutumia maendeleo ya  teknolijia ya  mawasiliano katika utekelezaji wa majukumu yake ya utoaji wa huduma za kisheria kwa Serikali na Taasisi za Serikali na Wananchi.Kwa mujibu wa  Mwanasheria Mkuu,  mkakati huo utahusisha kuweka kanzi data ya Mawakili wa Serikali walioajiriwa katika utumishi wa umma ili kuwezesha kuwasimamia na kuratibu  shughuli zao ipasavyo.

  Aidha mkakati huo wa matumizi ya teknolojia za kisasa za mawasiliano pia utahusu uanzishwaji wa kanzi data ya mikataba ya  kitaifa na kimataifa ambayo imeingiwa na Serikali za mitaa na Taasisi za Serikali, kanzi data ya sheria zilizofanyiwa marejeo na kutafsriwa, kanzi data ya huduma za  maktaba na masjala ya sheria na kanzi data ya kesi ambazo Serikali ni  mdaawa.

  Mwezi February mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , kwa mamlaka aliyonayo chini ya Ibara ya  36 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, alitoa “Amri ya Maboresho ya Muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu” kupitia Tangazo la Serikali  Na 48 la mwaka 2018  kwa lengo la kuboresha huduma za kisheria katika sekta ya Umma.

  Amri hiyo ya Maboresho ilitambua kuwepo kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yenye wajibu wa kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali Kuu, Mamlala za Serikali za Mitaa, Idara za Serikali na Mashirika ya Umma, kuandaa Miswaada ya Sheria; kuandaa nyaraka mbalimbali za kisheria na rasimu za maazimio ya Bunge pamoja na majukumu mengine.

  Amri hiyo ya Maboresho pia  ilitambua kuanzishwa kwa Ofisi ya  Taifa ya Mashtaka  yote ya jinai mahakamani; na kutambua kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inayosimamia na kuendesha mashauri yote ya madai.
  Imetolewa na Kitengo cha Habari na  Mawasiliano
  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
  Dodoma

  0 0

  Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bibi. Stella Nguma akifafanua jambo kwa Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo (hawapo katika picha) wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (Government Eletroniki Payment Gateaway-GePG), leo Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.
  Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Goodluck Mbano( aliyesimama),akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kwa njia ya kieletroniki wakati wa mafunzo hayo kwa Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo leo Jijini Dodoma, katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.
  Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo ,wakifuatilia kwa makinimaelekezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (Government Eletroniki Payment Gateaway-GePG) yaliyokuwa yakitolewa na wachambuzi wa mifumo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango (hawapo katika picha), leo Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.(Picha na WHUSM).
  Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo ,wakifuatilia kwa makinimaelekezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (Government Eletroniki Payment Gateaway-GePG) yaliyokuwa yakitolewa na wachambuzi wa mifumo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango (hawapo katika picha), leo Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.(Picha na WHUSM).

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Igunga, John Mwaipopo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya watumishi wa Halmahauri ya wilaya ya Igunga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018.  *Ni baada ya upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Bw. Francis Zuakuu kumkamata aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Bulagamilwa, Bw. Ntemi James kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji hicho.

  Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Agosti 16, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Manonga, Bw. Seif Gulamali kumuomba awasaidie katika kulipatia ufumbuzi suala hilo la upotevu wa fedha za kijiji kwa kuwa ni la muda mrefu na hakuna hatua zilizochukuliwa.

  Kutokana na malalamiko hayo Waziri Mkuu amemtaka kamanda wa TAKUKURU wa wilaya hiyo ahakikishe anawatafuta watu wote waliohusika na upotevu wa fedha hizo za kijiji akiwemo na alitekuwa mtendaji wa kijiji cha Bulagamilwa, ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa kata ya Igurubi.

  Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wilayani Igunga wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwatumikia wananchi kwa weledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

  Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma lazima wabadilike na wafanye kazi kwa bidii, waachemazoea na watumie utalaamu wao vizuri katika kuwahudumia wananchi na Serikali haitowavumilia wafanyakazi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

  “Msimamo wa Serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo haitawavumilia watumishi whv atakao jihusisha navitendo vya rushwawa na matumizi mbaya ya fedha za umma.”

  Pia Waziri Mkuu amewataka wakuu wa idara na watumishi wengine wajiwekee utaratibu wa kuwatembelea wananchi katika maeneo yao hususan ya vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi

  0 0

  Na Veronica Kazimoto,Geita

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaelimisha wafanyabiashara na wadau mbalimbali walioshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara mkoani Geita na kuwafafanulia juu ya masuala mbalimbali yanayohusu kodi ikiwa ni pamoja na msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi.

  Akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu kodi katika jukwaa hilo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo amewataka wafanyabiashara wenye malimbikizo ya madeni ya kodi na wale wote waliokuwa wakifanya biashara bila kusajiliwa kuchangamkia msamaha huo ipasavyo kwani hilo ni zoezi la miezi sita pekee.

  "Nachukua fursa hii kutoa wito kwa wafanyabiashara wote wenye malimbikizo ya madeni ya kodi na wote waliokuwa wakifanya biashara bila kusajiliwa kuwasilisha maombi yao TRA ili waweze kupata msamaha huu wa riba na adhabu wa asilimia 100 ambapo mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Novemba, 2018.

  Aidha, Mkurugenzi Kayombo amewahimiza wafanyabiashara wadogo waliopo kwenye utaratibu wa makadirio kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ambayo hutolewa na TRA bure bila ulazima wa kulipa kodi ya awamu ya kwanza kabla ya kuanza biashara isipokuwa ndani ya siku 90 baada ya kuanza biashara.

  “Awali wafanyabiashara walikuwa wanalipa kodi mara tu baada kusajili biashara zao na kukadiriwa kodi, lakini sasa hivi tumeweka utaratibu wa kulipa kodi ndani ya siku 90 kwa awamu ya kwanza baada ya kusajiliwa na na kuanza biashara, alifafanua Kayombo.

  Pamoja na mambo mengine, Kayombo amewakumbusha wafanyabiashara na washiriki wa jukwaa hilo la fursa za biashara suala zima la kutoa risiti za kielektroniki za EFD kila wanapouza bidhaa na huduma mbalimbali na kudai risti kila wanafanya manunuzi.

  Vilevile, amewasisitiza wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Geita na wilaya zake wenye changamoto mbalimbali wasisite kuonana na Meneja wa TRA mkoani humo kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili ili waweze kufanya biashara zao kwa uhuru.

  Jukwaa la Fursa za Biashara limeandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania imeshiriki jukwaa hilo kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali hususani wa mkoani hapa.

  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akiwasilisha mada kuhusu kodi wakati wa Jukwaa la Fursa za Biashara linalomalizika leo mkoani Geita likiwa na lengo la kuibua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika mkoa huo pamoja na changamoto mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi.

  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akiwasilisha mada kuhusu kodi wakati wa Jukwaa la Fursa za Biashara linalomalizika leo mkoani Geita likiwa na lengo la kuibua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika mkoa huo pamoja na changamoto mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia) akizungumza wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa maonyesho yaliyoambatana na Jukwaa la Fursa za Biashara linalomalizika leo mkoani Geita kwa lengo la kuibua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika mkoa huo pamoja na changamoto mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi.

  0 0  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge yalioyoanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar.

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akifurahi kwa pamoja na Maspika wastaafu Mhe. Anna makinda (wa kwanza kushoto) ,Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Pandu Kificho, Mhe. Pius Msekwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuber A Malulid, wa mwisho ni Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson. Waheshimiwa Maspika wastaafu wamehudhuria mafunzo ya Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge yalioyoanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar.

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akiwa Katika picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ambao ni Kamati ya Uongozi ya Bunge, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya utumishi ya Bunge. waliokaa mbele wa kwanza ni Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuber Ali Maulid, Spika Mstaafu Mhe. Anna Makinda, Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa na Katibu wa Bunge Mhe. Stephen kagaigai. Mafunzo hayo yameanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amepokea ugeni wa viongozi mbalimbali wa Jiji la Kampala nchini Uganda wakiongozwa na Waziri wa Jiji hilo Bennie Namugwanya Bugembe ambao wamekuja kujifunza na kupata uzoefu wa kuendesha na kusimamia shughuli za Jiji.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meya Mwita amesema anaamini viongozi hao kuna mambo mengi watajifunza kwa kipindi ambacho watakuwa katika Jiji hilo huku akiwahakikisha watapata kila wanachokitaka.

  Mwita amesena kuna mambo mengi mazuri ambayo yanefanyika na yanaendelea kufanyika katika Jiji la Dar es Salaam hivyo viongozi hao wa Jiji la Kampala kuna mambo watajifunza kwa ajili ya kuliboresha Jiji lao huku akiwahimiza kibuni vyanzo vipya vya mapato ili fedha zitakazopatikana wazitumie kufanya maendeleo.

  Amesema kuwa ni vema wakatambua Jiji la Dar es Salaam kupitia viongozi wake wa ngazi mbalimbali wamefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwamo ya usafiri kwa kuanzisha huduma ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi pamoja na treni ya Jiji.

  "Nafahamu kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka Jiji la Dar es Salaam,hivyo niwaombe mtakapokuwa hapa kila ambacho mnataka kufahamu basi kuweni huru kuuliza watalaam na viongozi wetu ambao wapo tayari kutoa majibu.

  " Tumeweka mfumo mzuri katika kukusanya kodi ni vema mkajifunza na mtakaporudi Kampala muweke mikakati ambayo itasaidia kuwaongezea mapato na hatimaye mtafanya maendeleo kwa ajili ya wananchi ambao wamewachagua,"amesema Mwita.

  Ametumia nafasi hiyo kuwaeleza kwamba Jiji la Dar es Salaam lipo kwenye mchakato wa kuleta mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi ikiwa ni mkakati wa kuwaondolea adha ya usafiri na hivyo ni vema viongozi wa Kampala wakaanza kuweka mikakati ya kushughulikia changamoto za usafiri ambazo kwa sehemu kubwa zinafafana katika majiji mengi.

  Amewahimiza kuwa wamoja na kumisha mshikamano ili kupata fursa ya kuwatumikia wananchi na kwamba anatambua Uganda na Tanzania ni nchi ambazo wananchi wake ni ndugu na marafiki.Kwa upande wa Waziri wa Jiji la Kampala Bugembe amesema anatambua pamoja na kufanikiwa katika kulisimamia Jiji la Kampala ambalo lina idadi ya watu milioni nne na linaongoza kwa uchumi bado kuna mambo wanatakiwa kujifunza kutoka Jiji la Dar es Salaam.

  Amefafanua mipaka yake ya kiutendaji kama Waziri wa Jiji la Kampala na kwamba katika kuhakikisha wanapiga hatua zaidi wameona haja ya kuja Dar es Salaam ili kupata uzoefu wa kuendesha Jiji na miongoni kwa maeneo ambayo watajifunza ni kushughulikia changamoto ya usafiri.


  Baadhi ya viongozi wa Jiji la Kampala nchini Uganda wakiwa kwenye ofisi za Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambao wamekuja kujifunza namna ya kusimamia shughuli za Jiji 

  Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita(kulia) akiwa na Waziri wa Jiji la Kampala nchini Uganda Bennie Namugwanya Bugembe ambaye yupo katika Jiji hilo kwa lengo la kujifunza na kubadilisha uzoefu wa kusimamia shughuli za Jiji

  0 0
 • 08/16/18--05:51: tangazo


 • 0 0


  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anaetambuliwa na Msajili wa Vyama Pro,Ibrahim Haroun Lipumba akizungumza na wanachama wa chama hicho waliohudhuria katika Mkutano wake wa kwanza uliofanyika katika Ukumbi wa Baitul Yamiyn bwawani mjini Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

  Baadhi ya Wanachama wa chama cha Wananchi CUF waliohudhuria katika Mkutano wa Kwanza wa Mwenyekiti wa CUF anaetambuliwa na Msajili wa Vyama Pro,Ibrahim Haroun Lipumba uliofanyika katika Ukumbi wa Baitul Yamiyn bwawani mjini Zanzibar.

  -Baadhi ya Wanachama wa chama cha Wananchi CUF waliohudhuria katika Mkutano wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anaetambuliwa na Msajili wa Vyama Pro,Ibrahim Haroun Lipumba uliofanyika katika Ukumbi wa Baitul Yamiyn bwawani mjini Zanzibar.

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazin.

  MKUU wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa na kuwekwa rumande kwa saa 48 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudi inayomiliki Shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Jensen Natal pamoja na Manasheria wa kampuni hiyo,Edward Mroso.

  mbali na kukamatwa kwa atu hao,Mkuu huyo wa wilaya ameamuru kushikiliwa kwa muda kwa Pasi ya kusafiria ya anayetajwa kuwa mwekezaji wa Shamba la Kibo and Kikau Estate,Trevor Robert kutokana na tuhuma za kukwepa kulipa kodi ya serikali inayokadiliwa kuwa Zaidi ya Sh Mil 700.
  Askari Polisi wakiwa wamemshikilia ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley Tanzania,Jensen Natal inayotajwa kukwepa kulipa kodi ya serikali kutokana na uwekezaji katika shamba la Kibo and Kikafu Estate,Natal amekamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai.
  Askari akimsindikiza Mwanasheria wa kampuni ya Tudeley Tanzania,Edward Mroso baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya TudeleyTanzania,Jensen Natal na Mwanasheria wa kampuni hiyo,Edward Mroso wakiwa kwenye gari la Polisi muda mfupi baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo baada ya kutembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa na Katibu tawala wa wilaya hiyo,Upendo Wela wakimngoja Muwekezaji wa Shamba la Kibo and Kikafu Estate alipofanya ziara ya ghafla.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley ,Jensen Natal akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya kabla ya kuingia katika eneo hilo.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiangalia pasi ya kusafiria ya anayedaiwa kuwa mwekezaji wa katika shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Trevor Robert raia wa Zimbabwe ambalo anatajwa kutokuwa na uhalali wa kuwa mwekezaji wa shamba hilo.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo walipotembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate linatajwa kuwa na mwekezaji asiye halali. 
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akimsikiliza Meneja wa Shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Trevor Robert wakati akitoa maelezo ya uhalali wa kuwekeza katika shamba hilo.
   

  0 0


  Na Mwandishi wetu
  KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu ameiyomba Serikali kutambua mchango  katika sekta binafsi (TPSF) katika kukuza uchumi wa nchi hususani katika suala la Biashara na masoko.

  Aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi mtendaji wa TPSF, Dk. Geofrey Simbeye kuusu maadhimisho ya kutimiza miaka 30 ya kuazishwa kwa taasi ya TCCIA ambapo TPSF nao wataadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa.

  Mshiu alisema serikali ya amwamu ya tano imekuwa ikitoa fursa za uwekezaji katika kampuni mbalimbali za nje ya nchi katika ujezi wa miundo mbinu hivyo kama wanaomba watambue taasisi hizo katika kukujenga uchumi ndani ya nchi.

  “Watu wote tupo katika kuakikisha uchumi wa nchi yetu ianakuwa hivyo kama tukiwa na ushirikiano katika sekta binafsi na serikali lazima tutapata maendeleo,” alisema.

  Aidha Mshiu alisema wanatarajia kufanya sherehe ya pamoja tangu kuazishwa kwa TCCIA miaka 30 kwa kuungana na TPSF  ambao nao wanatimiza miaka 20, lengo likiwa ni kuangalia namnagani sekta binafsi zimeweza kusaidia maendeleo ndani ya nchi na kwa wafanya biashara.

  Alifafanua kuwa TCCIA ndio waazilishi wa TPSF hivyo katika sherehe hizo zinazo tarajia kufanyika Novemba mwaka huu watalenga namnagani wadau na wafanyabiashara wamefanikiwa .

  Nae Mkurugenzi  wa TPSF, Dk.Simbeye alisema ushirikiano wa taasisi hizo umelenga kuimarisha ukuwaji wa maen deleo kwa wafanyabiashara .
  Alisema kupitia kauli mbalimbali za serikali ya Rais Magufuli alizokwisha kutoa kwa wafanya biashara kuwekeza katika awamu hii ni wazikuwa ndio fursa ya peke ndani  kwa wana chama wa taasisi hizo kuakikisha  wanafungua viwanda  .
  Hata hivyo Dk Simbeye amewataka wafanya biashara kujitokeza kuchangamkia fursa za uwekezaji katika hawamu ya tano ili kukuza uchumi maana ndiyo awamu pekee iliyowapa wawekezaji kipaumbele
   Mkurugenzi wa TPSF Godfrey Siambeye kushoto akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano wa Biashara na kukuza uchumi wa wilaya, mkoa na Taifa, kulioa ni KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu
  Mkurugenzi wa TPSF Godfrey Siambeye kushoto, kulia ni KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu wakipongeza mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano wa Biashara na kukuza uchumi wa wilaya, mkoa na Taifa.


  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WADAU wa Usimamizi wa kemikali taka kutoka sekta ya mafuta na gesi kutoka taasisi za umma na binafsi wamehimizwa kuendelea kusimamia sheria,kanuni na sera kuhakikisha hakuna madhara yatakayotokana na matumizi ya kemikali.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Magdalena Mtenga wakati akifungua warsha ya Usimamizi wa Kemikali taka katika sekta ya gesi na mafuta iliyowashirikisha wadau kutoka taasisi za umma na binafsi.

  Mtenga aliyemuwakilisha Mkurugenzi Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira) Ester Makwahiya ,amesema ipo haja ya kukumbusha wadau umuhimu wa kuwa na matumizi sahihi ya kemikali hasa kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa kati unaokwenda sambamba na ujenzi wa uchumi wa viwanda.Amesema matumizi ya kemikali hayaepukiki na hasa kutokana na maendeleo ya teknolojia na kwamba kemikamil inatumika katika matumizi mbalimbali yakiwamo ya viwandani na majumbani.

  Amesema hivyo ipo haja ya kuwa na matumizi sahihi ya kemikali kwani iwapo hakutakuwa na matumizi sahihi kuna hatari ya kupatikana kwa madhara kwa mtumiaji."Kuna mifano ya athari ambazo zinatokana na matumizi mabaya ya kemikali na miongoni mwa athari hizo ni kupatwa kwa ulemavu wa viungo," amesema.Amesema katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama Serikali imechukia hatua mbalimbali za kuhakikisha kemikali inatumika katika matumizi sahihi na salama kwa kufuata sheria,kanuni,Sera na miongozo iliyopo.

  Pia amesema hata kemikali ambazo zinatumika kwenye mafuta na gesi haina tofauti na aina nyongine za kemikali na kwa mazingira hayo ndio maana wameona haja ya kuwa na warsha hiyo ambayo itasaidia kukumbusha na kuwekwa mikakati sahihi ya kudhibiti athari za kemikali na kemikali taka."Kupitia warsha hii wada watajadiliwa mikataba mbalimbali ikiwemo ya usafirishaji wa kemikali taka kutola nchi mmoja kwenda nyingine," amesema na kusisitiza Serikali imechukia hatua mbalimbali za kuzuia athari za kemikali.

  Kuhusu changamoto ya baadhi ya watu kutofuata sheria amesema ipo haja kwa wadau wa warsha hiyo kujadili nini kifanyike katika kuondoa changamoto zilizopo na kwamba Serikali ipo tayari kusaidiana wadau.Kuhusu.ongezeko la kemikali taka amesema kwa kuwa nchi inaelekea kwenye ujenzi wa viwanda ni wazi kiwango kitaongezeka lakini tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa kuhakikisha kemikali inatumika kwa usahihi.

  Kwa upande wa Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafuniko amesema warsha hiyo ni muhimu kwasababu wanaoshughulikia kemikali na kemikali taka watajadili kwa kina na kuangalia namna ya kuondoa athari za kemikali iwapo kutakuwa na matumizi ambayo si salama.Amefafanua warsha hiyo ya siku mbili inalengo la kuwajengea uwezo wadau na kwamba maoni yao yanahitajika kuhusu namna nzuri ya kutumia kemikali.

  "Mada ambazo zitatolewa kupitia watalaam waliobobeba katika masuala ya kemikali na kemikali taka ziwasaidia kuongeza uelewa,amesema.Alipoulizwa kuhusu kiwango cha athari zitokanazo na matumizi mabaya ya kemikali amesema hill ni suala ambalo linahitaji takwimu ma hivyo si wakati sahihi kulijibu na linahitaji muda huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya kemikali.


  Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Bi. Magdalena Mtenga, akifungua (kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira)) warsha ya wadau wa Usimamizi wa Kemikali na Kemikali Taka za Sekta ya Mafuta na Gesi inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu, Dar es Salaam .

  Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), akiongea na washiriki wa warsha kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa ufunguzi
  Mgeni Rasmi, Bi. Magdalena Mtenga (aliyekaa katikati) na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kushoto, waliokaa) wakiwa pamoja na wadau wa warsha ya Usimamizi wa Kemikali na Kemikali taka inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam .
  Mtaalam wa Jiolojia kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Bw. Simon Nkenyeli (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusiana na masuala ya usimamizi wa petroli kwa washiriki wa warsha ya Usimamizi na Usimamizi wa Kemikali taka za sekta ya Mafuta na Gesi inaeyoendelea jijini, Dar es Salaam.

  Mwanasheria kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Risper Koyi (aliyesimama) akiwasilisha mada kwa wadau kuhusiana na Mikataba ya Kimataifa ya Usimamizi wa Kemikali.
  Wadau wa warsha ya Usimamizi wa Kemikali na Kemikali taka katika Sekta ya Mafuta na Gesi kutoka taasisi za umma na binafsi wakifuatilia mada.

  0 0

  Wangoni ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, hasa upande wa Kusini wa Songea. Pia wako Msumbiji. Lugha yao ni Kingoni. Fuatilia simulizi hii kutoka kwa Chifu wa kabila la wangoni uweze kujua kiundani zaidi.

  0 0

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku nne visiwani humu Agosti 17 hadi 20 mwaka huu.

  Dk.Bashiru anafanya ziara hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo Mei mwaka huu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Abdulrahman Omar Kinana kustaafu.

  Akitoa taarifa ya ziara hiyo ya Katibu Mkuu huyo, Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu Taifa(NEC),Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Zanzibar Catherine Peter Nao, alisema CCM Zanzibar tayari kimekamilisha maandalizi yote ya mapokezi ya kiongozi huyo.

  Catherine alisema katika ziara yake hiyo pamoja na mambo mengine anatarajia kuzungumza na viongozi mbalimbali wa CCM na jumuiya zake na makundi ya kutoka taasisi za vijana visiwani humu.

  Aliongeza kuwa ziara hiyo ya Dk.Bashiru itakuwa ni ya kikazi na kujitambulisha kwa wana-CCM ambapo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Katibu Mkuu huyo ambapo atawahutubia wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla katika uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui saa 9 alasiri.

  “Tunawaomba wanachama wote tujitokeze kwa wingi kushiriki mapokezi hayo ya kiongozi wetu mpendwa ambaye ni mara ya kwanza kuja tukitambulisha na kuzungumzia sera na masuala mbalimbali ya kuimarisha CCM na Jumuiya zake, alisema Catherine.

  Akizungumzia ratiba ya ziara hiyo Katibu huyo wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,Catherine alisema siku ya siku ya kesho Agosti 17 mwaka huu katibu Mkuu huyo atakutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.

  Katibu huyo aliongeza kuwa Dk.Bashiru anatarajia kukutana na na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

  Alisema mchana wa siku hiyo ya ijumaa atazuru Kaburi la Muasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Hayati Mzee Abeid Karume na kuzungumza na watumishi pamoja na Wazee wa CCM Zanzibar ambapo jioni atazungumza na Viongozi na wanachama wa Mikoa minne ya CCM Unguja hapo katika viwanja vya CCM Kisiwandui.

  Catherine aliendelea kueleza kuwa jumamosi ya Agosti 18 mwaka huu Katibu Mkuu huyo atazungumza na Wenyeviti wa CCM wa Mikoa na Wilaya, Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya, Kamati za siasa za Mikoa na Wilaya, Wabunge, Wawakilishi na madiwani katika ukumbi wa Kamati Maalum Kisiwandui pamoja na kuzungumza na makundi ya vijana katika ukumbi wa CCM Mkoa wa mjini.

  Aliongeza kuwa siku ya Jumapili Agosti 19, mwaka huu Katibu Mkuu huyo asubuhi atasafiri kuelekea Pemba kwalengo la kuendelea na ziara yake hiyo ambapo atazungumza na Watumishi wa CCM na wazee wa Pemba katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kitengo.

  Katibu huyo alisema Dk.Bashiru anatarajia kuzungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Mikoa miwili katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Mkoa wa Kusini Pemba na jioni anatazungumza na Wenyeviti wa CCM wa Mikoa na Wilaya, Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya, Kamati za siasa za Mikoa na Wilaya, Wabunge, Wawakilishi,madiwani na maafisa wadhamini katika ukumbi wa Makonyo Pemba.

  Katibu Mkuu huyo atahitimisha ziara yake hiyo siku ya Juma tatu Agosti 20 mwaka huu, kwa kuzuru kaburi la Dk.Omar Ali Juma kisiwani Pemba na kumalizia ziara yake kwa kuzungumza na makundi ya vijana ambapo jioni atasafiri kuelekea Dar es salaam kuendelea na majukumu mengine.

  0 0

  Mhe Jaji Makaramba akisaini kitabu cha wageni.
  Mhe. Dkt. Levira akisoma taarifa ya makabidhiano ya ofisi.
   
  Watumishi wakimsikiliza Mhe. Makaramba (hayupo pichani)
  Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya, (wa tatu kushoto) ni Mhe. Jaji Paul Joel Ngwembe, (wa pili kulia) ni Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira, wa kwanza kulia ni Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. George Herbert, wa pili kushoto ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. William Mutaki na wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Bw. Moses Mwidete.
  Mhe Makaramba akipanda mti wa kumbukumbu
  Mhe Ngwembe akipanda mti wa kumbukumbu  Na Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya

  Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali vyeo na kufanya kazi kama timu moja, kupendana na kufuata C tatu yaani ‘Coordination, Cooperation na Consultation’ ili kuwahudumia wananchi ipasavyo.

  Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba alipokuwa akiongea na Watumishi wa Kanda hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi Agosti, 15 2018, katika ofisi za Mahakama Kuu mkoani Mbeya.

  Mhe. Jaji Makaramba alisisitiza viongozi wa ngazi ya juu ya Kanda hiyo yaani Jaji Mfawidhi, Naibu Msajili na Mtendaji wa Mahakama kufanya kazi kwa kufuata kile alichokiita ‘utatu mtakatifu’. 

  Aidha, pamoja na mambo mengine, Mhe. Makaramba alisisitiza juu ya nidhamu na uadilifu wa watumishi wa Mahakama huku akikemea Watumishi kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kwa pamoja kuweza kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa Mahakama. 

  “Mtumishi akikamatwa kwa tuhuma za rushwa nitamsindikiza mwenyewe hadi TAKUKURU nikifika nawakabidhi wamalizane naye wenyewe” alisema Jaji Mfawidhi huyo.

  Mhe. Makaramba vilevile aliupongeza uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kazi nzuri ya ukarabati wa jengo la Mahakama Kuu Mbeya ambalo pia hutumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi pamoja na Mahakama ya Wilaya Mbeya na kuwataka Watumishi kulitunza vyema jengo hilo pamoja na vitendea kazi vya kisasa vilivyomo.

  Aidha; Mhe. Jaji Makaramba alitoa maagizo ya kuwa na mpango kazi wa Kanda ambao utaenda sambamba na mpango Mkakati wa Mahakama kitaifa ili kutengeneza mazingira mazuri na wezeshi ya kuwahudumia wananchi. 

  Aliongeza kwa kusema kwamba yupo tayari kutoa mchango wake kadri akatavyojaaliwa na Mwenyezi Mungu vile vile ataendelea kujifunza kutoka kwa watumishi wa Kanda ya Mbeya mambo mbalimbali yatakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa wakati.

  Viongozi na Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya wamempokea Mhe Robert Makaramba ambaye amehamishiwa mkoani humo kuwa Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo kujaza nafasi ya Jaji Mfawidhi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwepo kustaafu kwa mujibu wa sheria.

  Pamoja na mapokezi hayo, makabidhiano ya ofisi yalifanyika kati ya Mhe. Makaramba na Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira akimwakilisha Mhe. Kaimu Jaji mfawidhi ambaye alipatwa na udhuru. 

  Katika hafla hiyo Mhe. Dkt. Levira alisoma taarifa ya makabidhiano ya ofisi ikijumuisha mambo muhimu ikiwepo eneo la utawala wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kwa kueleza kuwa Kanda ya Mbeya inajumuisha Mikoa ya Mbeya na Songwe.

  Vilevile katika taarifa hiyo kulikuwa na taarifa ya hali ya mashauri, hali ya watumishi, hali ya miundombinu, hali ya fedha na hali ya vyombo vya usafiri.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Sabra Issa Machano akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Khamis Mussa Omar ambae ni Mgeni Rasmin katika ufunguzi wa Mafunzo ya Kwanza kwa Wastaafu watarajiwa yaliyofanyika Ukumbi wa Mkutano kariakoo Mjini Zanzibar.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipaqngo Khamis Mussa Omar akifunguwa Mafunzo ya kwanza kwa Wastaafu watarajiwa yaliyofanika Ukumbi wa Mkutano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) uliopo Kariyakoo Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya Wastaafu watarajiwa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar hayupo pichani wakati wa Uzinduzi wa mafuzo hayo. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.  Na Maryam Kidiko na Khadija Khamiss – Maelezo Zanzibar.

  KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Khamis Mussa Omar amewataka wastaafu kujitayarisha wakati wa kukaribia kustaafu na kujipanga vizuri kimaisha ili kuepuka baadhi ya matatizo yasiyokuwa ya lazima.

  Hayo aliyasema wakati akifunguwa mafunzo ya mara ya kwanza kwa wastaafu watarajia yaliyotayarishwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) yaliyofanyika Ukumbi wa mkutano wa Kariakoo Mjini Zanzibar.

  Alisema kuwa kustaafu nijambo kubwa ambalo linahitaji mtu kujitayarisha vizuri anapokaribia kustaafu ili kujiimarisha katika mpangilio wake wa kimaisha wakati wa kustaafu.

  Aidha alisema wastaafu wengi huonekanwa kuanguka kimaisha mara baada ya kustaafu kutokana na kutojiandaa vizuri wakati wa utendaji wao kazi jambo ambalo linawafanya kupata mawazo yanayopelekea maradhi.

  “Wastaafu wengi huwa hawajiandai kimaisha kabla ya kustaafu hivyo husababisha kupata maradhi mbali mbali kitu ambacho kinapelekea mfumo mbaya katika maisha yao“alisema Katibu Mkuu huyo.

  Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafahamu matatizo yanayowakabili wastaafu hivyo watahakikisha kuyatatua matatizo hayo katika kuwajengeya maisha yaliyobora.

  Pia alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha wastaafu wanapata haki zao kwa wakati na kuimarisha mazingira mazuri ya kustaafu ili kutimiza malengo waliyojiekea.

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) Sabra Issa Machano alisema kuwa (ZSSF) imeamua kufanya semina kwa wastaafu ili kuwapa ushauri wa kujiandalia mazingira mazuri kabla ya kustaafu.

  Hata hivyo alisema Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) umetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake hivyo watahakikisha wanachama wa mfuko huo wanapata huduma nzuri kupitia mfuko watakaotumia.

  Sambamba na hayo alisema mfuko huo wa ZSSF ni kwa watu wote waliyojiunga hivyo watafanya juhudi mbali mbali katika kazi yao ili kutimiza lengo lilokusudiwa ndani ya mfuko huo.

  “Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) ni kwa watu wote waliojiunga hata kwa wajasiria mali mbali mbali hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanatumia mfuko huo ili kuendelsha maisha yao.”alisema Mkurugenzi Mtendaji Sabara.

  Mkurugenzi Sabra aliongeza kuwa mfuko huo kwasasa imekuwa hivyo watazidisha juhudi katika huduma zao kwa wahusika kwa kuendelea kuwajali kwa kuwaelekeza vitu mbali mbali ili kuepukana na matatizo katika maisha yao.

  Kwa upande wa mtoa mada Bwana Daudi Mattaka aliweza kuwasilisha mada mbali mbali kwa wastaafu hao ili kuwasaidia wakati wa kustaafu miongoni mwa mada hizo ni ikiwemo utangulizi wa maisha,Maandalizi ya nini kifanyike pamoja na umuhimu wa kujiandaa kabla ya kustaafu.

  Pia aliwataka wastaafu hao kuridhika na hali ya kipato walichonacho katika maisha yao ili kuepuka tamaa ambayo itawapelekea kuharibu maisha yao.

  Mafunzo hayo ya siku moja ya kuwandaa wafanya kazi wastafu yameandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na kufadhiliwa na Benki ya NMB na Benki ya TPB.

  0 0

   Pichani kulia Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali wakishirikiMkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018.Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
  Sehemu ya Meza kuu wakati wa  Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018.
   Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stregomena Tax akizongwa na wanahabari  kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018.
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Watu wa Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila  kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018.Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
   Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Joseph Kabila wa DRC, Rais Dkt. Hage Geingob wa Namibia na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini wakibadilishana mawazo  kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018
   Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Joseph Kabila wa DRC, Rais Dkt. Hage Geingob wa Namibia na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini wakibadilishana mawazo  kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018

   Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stregomena Tax akizongwa na wanahabari  kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Watu wa Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila  kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018. Kushoto ni Rais Edgar Lungu wa Zambia
  .
   Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Joseph Kabila wa DRC, Rais Dkt. Hage Geingob wa Namibia na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini wakibadilishana mawazo kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018
   Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Joseph Kabila wa DRC, Rais Dkt. Hage Geingob wa Namibia na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini wakibadilishana mawazo baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018
  Rais Dkt. Hage Geingob wa Namibia akiongoza Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018
  .
   Rais Joseph Kabila wa DRC akiondoka baada ya kuhudhuria  Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018
  1. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais  Edgar Lungu wa Zambia baada ya kumalizika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018

  0 0

  Na James Ndege – Dar es Salaam.

  Mamlaka ya Chakula na Dawa imekutana na wadau wapatao 50 kujadili udhibiti wa gesi tiba (medical gases) katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya TFDA tarehe 16 Agosti, 2018 kwa lengo la kulinda afya ya jamii. 

  Mkutano huo umehusisha wadau bidhaa hiyo wakiwemo wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, hospitali,Wizara na taasisi za udhibiti za Serikali kutoka mikoa mbalimbali nchini. Katika mkutano huo, wadau walijadili na kuelezwa matakwa ya kisheria ya udhibiti wa bidhaa hiyo nyeti kwa afya ya binadamu. 

  Mamlaka imeanza udhibiti wa bidhaa hiyo ambayo ipo katika kundi la bidhaa za Vifaa Tiba kuanzia mwezi Aprili 2018 ambapo katika kipindi cha mpito cha mwaka mmoja, wadau wametakiwa kuwasilisha TFDA orodha na taarifa ya bidhaa walizo nazo kwa utambuzi (notification) na kwamba waanze utaratibu wa usajili kwa kuwa kipindi cha utambuzi kitamalizika mwezi Aprili 2019 na baada ya hapo bidhaa ambazo hazijasajiliwa na TFDA hazitaruhusiwa kuingi katika soko. 

  “TFDA inatarajia wadau wote kukidhi kwa hiyari matakwa ya kisheria ya udhibiti wa gesi tiba kwa muda uliopangwa ili kuepusha usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wale wataokiuka maalekezo haya”, alisema .Meneja wa Majaribio na Usalama wa Dawa, Bi. Kissa Mwamwitwa, aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA katika hotuba yake ya ufunguzi. 

  Wadau hao pamoja na TFDA walikubaliana na kuweka maazimio kadhaa kwa lengo la kuwezesha zoezi husika kufanyika kwa ufanisi, miongoni mwa maazimio hayo ni kuanzisha chama cha wadau wa gesi tiba, kuboresha Mwongozo uliopo wa udhibiti wa gesi husika na watengenezaji wa bidhaa hiyo kuzalisha kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika ikiwa ni pamoja na kuweka maelezo ya kiusalama katika bidhaa zao kwa nia ya kulinda afya ya jamii. 
  Picha ya pamoja baina ya viongozi wa TFDA na wadau wa gesi tiba kutoka Serikalini na sekta binafsi nchini. waliokaa kutoka kulia ni Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA (wa pili), Meneja wa Vifaa Tiba, Vitendanishi na Vipodozi wa TFDA, Bi Grace Shimwela (wa tatu), Mwenyekiti mteule wa kikao hicho, Eng. Daudi Mlwale (wa kwanza) na Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. 2. Msajili wa Dawa Mkuu wa TFDA, Bi. Rose Aaron akisisitiza jambo katika mada aliyowasilisha 3. Eng. Samwel Hayuma wa TFDA akiwasilisha mojawapo ya mada 4. Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akitoa hotuba ya ufunguzi. 
  Msajili wa Dawa Mkuu wa TFDA, Bi. Rose Aaron akisisitiza jambo katika mada aliyowasilisha. 
  Eng. Samwel Hayuma wa TFDA akiwasilisha mojawapo ya mada 
  Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akitoa hotuba ya ufunguzi 


older | 1 | .... | 1648 | 1649 | (Page 1650) | 1651 | 1652 | .... | 1898 | newer