Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, WAKILI MKUU WA SERIKALI NA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA JIJINI DODOMA

0
0




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikiali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Dodoma Agosti 15, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Devis Mwamfupe, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria , Profesa Sifuni Mchome, Mkurugenzi wa Mshtaka, Biswalo Mganga na kulia ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Posi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshirki katika uzinduzi wa Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. Waliokaa wanne kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi na watatu kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi na wanne kulia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi wakati alipowasili kwenye eneo la uzinduzi wa Ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa, Paramagamba Kabudi (kushoto), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde (wapili kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vitabu wakati alipotembelea maktaba ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka aliyoizindua jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa tukio la uzinduzi wa Ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika uzinduzi huo Jijini Dodoma, Agosti15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaaga washiriki wa uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka baada ya kuzindua Ofisi hiyo jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramnagamba Kabudi na kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WATAALAM KUCHUNGUZA UCHIMBAJI MADINI HIFADHI YA AMANI, TANGA

0
0


Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko,( mwenye Tshit nyekundu) na Mbunge wa Mheza Balozi Rajab Adad (mbele) wakielekea eneo lililokuwa likitumiwa na wachimbaji wadogo kuchimba madini pia likidaiwa kuwa chanzo cha maji katika hifadhi ya misitu wa asili wa amani, mheza Tanga.
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko,( katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sakale, Mheza mkoani Tanga, waliokuwa wakiomba kuruhusiwa kufanya shughuli za uchimbaji madini katika eneo linalodaiwa kuwa ni chanzo cha maji yanayotumika Mkoa wa Tanga.

Na Zuena Msuya, Mheza ,Tanga

Serikali imesema itawaleta wataalam kutoka kituo cha Utafiti wa Miamba(GST), Wizara ya Maliasili na Mazingira kwenye eneo walilokuwa wakitumia wachimbaji wadogo kwa shughuli za madini, ambalo pia linadaiwa kuwa liko katika chanzo cha maji, kufanya utafiti na kujiridhisha kama eneo hilo liruhusiwe kuendeleza na shughuli za uchimbaji madini ama laa.

Hayo yalisemwa na Naibu waziri wa Madini Dotto Biteko alipotembelea katika kijiji cha Sakale katika Kata ya Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Mheza mkoani Tanga, wakati akizungumza na wananchi waliomuelezea kero yao ya kuzuiwa na serikali kutokuchimba madini eneo hilo licha ya kuwatokuwepo na viashiria vya uharibifu wa mazingira na misitu kama serikali inavyosema.

Naibu Waziri Biteko, alisema kuwa kiu ya serikali ni kuwapatia maeneo ya uchimbaji wachimbaji wadogowadogo ili waweze kubadilisha maisha yao kupitia uchumi wa madini, hii ni kutokana Rais kubadilisha sheria za nchi kwa upande wa madini kutoka kuwanufaisha wageni na sasa kuwanufaisha watanzania.

“Serikali yenu ni sikivu,Mheshimiwa Rais amebadilisha sheria ya madini ili kuwanufaisha watanzania badala ya wageni ,hapa leo tumekuja kuangalia kwa macho ili tufanye uamuzi sahihi …siwezi kumiambia mchimbe sasa hivi ila tutaleta wataalamu wetu wa GST,maliasili na mazingira kwa pamoja ili waje kuona uwezekano wa kupewa eneo la kuchimba ikiwa hapa au kwengine”alisema.

Aidha aliongeza kuwa wananchi lazima wafundishwe kufuata sheria za madini haswa katika kuhama matumizi ya zebaki katika kuchenjua madini ambayo yana athari kubwa kwenye mazingira na miili ya binadamu kutumia madini ya Sayayi ambayo hayana madhara.

Kwa upande wa wananchi wa eneo hilo, walimueleza naibu waziri huyo kuwa madini katika eneo hilo yaligunduliwa mwaka 2013 na yanapatikana kwenye miamba na siyo kwenye chanzo cha mto kama serikali inavyosema lakini walizuiwa kwa tahadhari ya uharibifu wa mazingira na misitu ya asili.

Walisema kuwa kutoka uliopo mwamba unaosadikiwa kuwa na madini na chanzo cha maji ni zaidi ya mita sitini na ilipo hifadhi ya msitu wa asili wa Amani ni zaidi ya mita 3,000 lakini wamekuwa wavumilivu kusubiri hatima ya serikali.

“Mheshimiwa Naibu Waziri uchumi tunao lakini tunakufa maskini…hapa madini yapo lakini serikali imetuzuia kwa hatari ya uharibifu wa mazingira ..sisi tunakuhakikishia hakuna uharibifu wowote wa mazingira utakaotokea,” alisema Shetwai

Naye diwani wa kata hiyo Anord Mlowe alisema kuwa wataalamu walikuja kupima mwamba na baadae ukaanza kutoa madini lakini baadae kukaanza mabishano kati ya watu wa maliasili,maji na mazingira kuhusu usafishaji wa madini kwa kutumia zebaki lakini mkuu wa wilaya ya Muheza aliyepita Subira Mgalu alijiridhisha kuwa hakuna madhara lakini serikali ikaweka zuio.

Alimuomba waziri kuwaruhusu ili waweze kuchimba kutoka maeneo yalipo mmwamaba wa madini ni mashamba ya wananchi na sio eneo la hifadhi kutokana wameyarithi kutoka kwa mababu zao.

Akizungumzia eneo hilo, mbunge wa jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu alimuomba Naibu Waziri , Biteko kuleta wataalamu wa madini kuja kupima ili kuona kama madini hayo yanatoka milimani au yapo kwenye mto ili kuona namna ya kuwasaidia kupewa eneo la uchimbaji.

“Mheshimiwa naibu waziri pale mwamba uko pembeni kutoka chanzo cha maji na wananchi wa Sakale kata ya Mbomole wametunza msitu wa asili wa Amani….hivyo wakipewa eneo la uchimbaji wataweza kutunza msitu bila ya kuathiri chanzo cha maji” alisema.

Aliongeza “kwa niaba yao tuma wataalamu wako waje ili wakuletee taarifa ili wananchi hawa waweze kuchimba”.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo akisoma taarifa ya zuio la uchimbaji wa madini eneo hilo, alisema lengo ni kulinda mazingira na chanzo cha maji licha ya sheria katika maeneo hayo matatu ya madini, mazingira na maliasili kukinzana jambo ambalo linaleta ugumu kwa watendaji kuwadhibiti wachimbaji hao.

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WAPATIWA KUKU 4000 WILAYANI MKURANGA

0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

WANAWAKE wajasiliamali wapatao 400 Wilayani Mkuranga wamepewa mafunzo na kuku wa kufuga ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuendeleza shughuli za kijasiriamali Wilayani humo.

Akiongea na vyombo vya habari Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga ameeleza kuwa hadi kufikia mwakani akina mama wa Mkuranga watakuwa mbali sana kutokana na ufugaji huo wa kuku hao ambao watainua uchumi wa familia zao.Aidha amewataka akina Mama wa Wilaya ya Mkuranga kutumia mradi huo vizuri ili kuleta maendeleo kwani wamebahatika sana.

Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa kuku hao ni kwa ajili ya ufugaji katika kujikwamua kiuchumi na sio zawadi na amewataka akina mama hao kutumia ujuzi kuendeleza ufugaji na kuwaelimisha wengine kuhusiana na mafunzo hayo.

Pia ameeleza kuwa wajasiriamali hao wamepokea kuku 1058 kati ya kuku 4000 waliohaidiwa na akina Mama 100 wamepata kuku 10 kwa kila mmoja.

Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake jukwaa la Wilayani Mkuranga bi. Mariam Ulega kuku 4000 ambao watagaiwa kwa akina mama 400 watagaiwa kwa wanawake wajasariamali waliohudhuria katika mafunzo hayo.Ameeleza kuwa kwa hicho kidogo wakitumie katika kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla, amewataka wawe na ushirikiano ili waweze kufikia malengo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akizungumza mbee ya Wanahabari (hawapo pichani),mapema leo kuhusu kupokea kuku kwa ajili ya Wajasiliamali Wanawake mkoa wa Pwani(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Baadhi ya kuku waliopewa Wanawake wajasiliamai wilaya ya Mkuranga kwa ajili ya ufugaji
Baadhi ya Wanawae wa Wilaya ya Mkuranga wakiwahifadhi kuku wao katika matenga ya mbao,Wanawake 400 walipata kuku 10 kila mmoja kwa ajili wa mtaji wa kufuga kuku.

CHUO CHA DIPLOMASIA CHAFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI INDIA

0
0
Chuo cha Diplomasia Tanzania (Center for Foreign Relation -CFR) wamefanya ziara ya kikazi nchini India kuanzia tarehe 13-15 Agosti 2018. 

Ziara hiyo imekuja kufuatia mwaliko wa Taasisi ya Mafunzo ya Kidiplomasia ya India (Foreign Service Institute-FSI), na ililenga kujua shughuli za FSI na taasisi zinazoshirikiana nazo, pamoja na kujadiliana juu ya uwezekano wa kuingia katika makubaliano ya ushirikiano. 

Wajumbe wa CFR waliongozwa na Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi (Mst.), ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya CFR. Wajumbe wengine walikuwa ni pamoja na Kaimu Mkuu wa cha Diplomasia (CFR), Dr Bernard Achiula, Dr Lucy Shule wa CFR, Dr Richard Mbunda kutoka UDSM, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia (DAA), Bibi Justa Nyange. Kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India, alikuwepo Balozi Baraka Luvanda na Bibi Natihaika Msuya, Afisa Mambo ya Nje.

Aidha, wajumbe hao walipata fursa ya kutoa mihadhara katika Kituo cha Stadi za Masuala ya Afrika katika Chuo Kikuu cha Nehru, Taasisi ya Stadi za Masuala ya Ulinzi na Usalama (IDSA) pamoja na Taasisi ya Tafiti Mahususi kuhusu ushirikiano baina ya Nchi za Kusini (South Cooperation Research Information System-RIS).

Kwa ujumla, ziara hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa ambapo taasisi wenyeji zimeonesha dhamira ya dhati ya kushirikiana na CFR katika kujenga uwezo wa wanadiplomasia wa Tanzania.
Balozi Ombeni Sefue akimkabidhi Mkuu wa Taasisi ya Stadi za Masuala ya Afrika, Profesa Ajay Dubey zawadi ya Kinyago. 

WAFANYABIASHARA KIGOMA WAIOMBA SERIKALI IONDOE GHARAMA ZA VIZA NA CHANJO MIPAKANI ILI KUKUZA BIASHARA

0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiwaeleza wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji umuhimu wa kutoa lisiti na kulipa kodi, wakati changaoto za biashara na nchi jirani zikitatuliwa, alipofanya Mkutano na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo Mkoani Kigoma, wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Kassim Mchatta na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiwaeleza wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji umuhimu wa kutoa lisiti na kulipa kodi, wakati changaoto za biashara na nchi jirani zikitatuliwa, alipofanya Mkutano na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo Mkoani Kigoma, wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Kassim Mchatta na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko.
Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA) Bw. Baghayo Saqware, akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma kuhusu umuhimu wa Bima wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na wafanyabiashara hao.
Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zito Kabwe, akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya Kodi zinazotozwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo.


Wafanyabiashara Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kuondoa gharama za Cheti cha Matibabu na utaratibu wa Viza kwa nchi ambazo hazipo katika Jumuiya ya Afrika mashariki hasa kwa wafanyabiashara wadogo ili kuchochea biashara kati ya Mkoa huo na nchi jirani zikiwemo Burundi na Congo.

Hayo yamebainishwa Mkoani Kigoma wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, na Wafanyabiashara wa mkoa huo uliowakutanisha pia Madiwani wa Kigoma Ujiji na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na viongozi wengine.

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kigoma, Bw. Raymond Ndabhiyegetse, alisema kuwa Serikali imeweka gharama ya Viza ya Dola 50 na Dola 10 kwa ajili ya cheti cha chanjo kwa nchi ambazo si wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wadogo ambao ndio waliokuwa chachu ya biashara mkoani Kigoma.

“Waliobaki katika biashara ni wafanyabiashara wakubwa ambao hununua bidhaa za jumla kutoka viwandani na kusababisha wafanyabiashara wadogo wa mkoa wa Kigoma kutonufaika na kusababisha mzunguko wa pesa na biashara kuwa mdogo ikilinganishwa na kipindi ambacho hakukuwa na masharti ya kulipia viza na chanjo”, alisema Bw. Ndabhiyegetse.

Aidha Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Mkoani Kigoma, Bw. Prosper Guga, alisema kuwa matatizo mengine yanayodhoofisha biashara na kudidimiza uchumi wa Mkoa wa Kigoma unaopakana na Nchi ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni kutokuwepo kwa Benki za Kimataifa hususani nchini DRC jambo linalowafanya wafanyabiashara kutembea na fedha taslimu hivyo kuwa hatari kwa usalama wa fedha hizo kwa kuzingatia mazingira ya nchi wanzaofanyanazo biashara.

“Wizara ya Fedha na Mipango isaidie kuzishawishi Benki za Biashara kufungua matawi katika nchi za DRC, Burundi na nyingine ili kukuza zaidi biashara katika ukanda huu ambao una fursa kubwa za biashara” aliongeza Bw. Guga.

Kuhusu suala la Gharama za Viza na Cheti cha Matibabu, Bw. Guga aliitaka Serikali kuondoa utaratibu huo na badala yake cheti maalum cha ujirani mwema kitumike kama ilivyo mipaka mingine ya Goma- Rwanda na Uvira-Bunjumbura.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, ameishauri Serikali kuufanya mji wa Kigoma kuwa Bandari Kavu ili mizigo yote inayosafirishwa kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa ajili ya kuivusha kwenda nchi jirani za Congo na Burundi, ianzie katika mji huo wa kibiashara ili kukuza ajira na uchumi wa mkoa huo

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa amefurahishwa na hoja za wafanyabiashara hao hivyo akaahidi kushirikiana na Wizara nyingine ikiweo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na pia Wizara ya Mambo ya Ndani ili kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa haraka.

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Congo mwaka 1991/92 walikubaliana kuwa na soko na mahusiano mema kati ya Mkoa wa Kigoma na mikoa jirani ya Congo, lengo likiwa wafanyabiashara hao kuuza bidhaa Kigoma na kununua bidhaa na mazao kwenda Congo hivyo kurahisisha wafanyabiashara wadogo kufanyabiashara na kuibua matajiri wakubwa katika kipindi cha mwaka 1990 hadi 2000.

Naibu Waziri Dkt. Kijaji, amefanya Ziara ya Kikazi mkoani Kigoma ambapo ametembelea na kukagua miradi iliyopewa fedha na Serikali na pia kuzungumza na wafanyabiashara kuhusu uboreshaji wa mazingira ya biashara na ulipaji wa kodi.

WABADHILIFU MALI ZA MAGEREZA KUKIONA

0
0

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) akikagua moja ya nyumba zinazojengwa kwa mtindo wa kujitolea gerezani Mpwapwa. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Salum Omari na wa kwanza kushoto ni mkuu wa Gereza Mpwapwa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Nobert Ntacho.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (mwenye miwani) akikagua mradi wa ufyatuaji tofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi maafisa na askari kwa njia ya kujitolea.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa kwanza kulia) akikagua shamba la mikorosho la gereza Mpwapwa alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo Agosti 13 mwaka huu. Shamba hilo lina ukubwa wa ekari 58 na kati ya hizo ekari 15 tayari zimeanza kutoa matunda. Kwa msimu wa mwaka 2017/18 zaidi ya kilo 2400 zilipatikana.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akisalimiana na maafisa wa gereza Mpwapwa mkoani Dodoma alipowasili kituoni hapo kwa ziara ya kikazi Agosti 14,2018.
Baadhi ya maafisa wa gereza Kongwa mkoani Dodoma wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo Agosti 14, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) akiongea na baadhi ya maafisa gereza Kongwa (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo Agosti 14, 2018.Wa pili kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Salum Omari. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mnadhimu katika ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoani Dodoma Kamishna Msaidizi wa Magereza Mwaruka Dugange, wa pili kulia ni Mkuu wa gereza Kongwa Mrakibu wa Magereza John Nyonyi na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kambi Mkoka Mrakibu wa Magereza Felix Samson.

WABADHILIFU MALI ZA MAGEREZA KUKIONA

Na Deodatus Kazinja

Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza nchini wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kujinufaisha na mali za Jeshi hilo kinyume na utaratibu.

Hayo yalisemwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Phaustine Kasike wakati akizungumza na maafisa na askari wa gereza Mpwapwa na Kongwa kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya kikazi katika vituo hivyo Agosti 14 mwaka huu.

Kamishna Kasike alisema si jambo la kificho kukuta shamba, mifugo na mali nyinginezo za gereza zinamilikiwa na kuendeshwa na mkuu wa gereza kama mali yake binafsi.

Mkuu huyo wa magereza nchini akionesha kukasirika alisema siyo siri kukuta shamba la mkuu wa gereza au mkuu wa magereza wa mkoa likiwa limestawi huku shamba la serikali limesinyaa kabisa kwa visingizio vya hali ya hewa wakati vyote viko sehemu moja na vinatumia nguvu kazi ya wafungwa na raslimali nyinginezo hizo hizo za serikali.

“Nawataka maafisa na askari ndani ya Jeshi la Magereza kutambua kuwa tabia za namna hii ndizo zimesababisha Jeshi letu kutosonga mbele. Tunatazamwa kama watu tulioshindwa kutimiza wajibu wetu kwa tabia zetu za udokozi, wizi na ubinafsi na tunaoweza kurekebisha hali hii ni sisi wenyewe” alisema Kamishna Kasike.

Akitolea mfano wa mifugo kama ng’ombe na mbuzi Jenerali Kasike alisema ni jambo la kawaida kukuta kituo kiko na idadi hiyo hiyo ya mifugo kwa miaka kadhaa bila kuongezeka mfugo hata mmoja na ikiwa kuna mabadiliko ni ya kupungua tena kwasababu ambazo hazina mashiko.

“ Binafsi nakataa. Mwaka mzima ng’ombe au mbuzi wasiongezeke haiwezekani. Ni ubadhilifu tu. Nataka kila mmoja atambue kuwa zama hizo zimekwisha na niseme ni ama unabadilika au tunashughulikiana ” Alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Na kuongeza “wakati serikali inatutaka tuzalishe chakula cha kujitosheleza kwa wafungwa na ziada tuuze ili tuingize maduhuli serikalini ni lazima kubadilika kabisa kiutendaji ili kufikia lengo hilo.”

Naye mmoja wa askari wa gereza Mpwapwa akichangia katika kikao hicho alisema wao kama watendaji wa ngazi za chini wako tayari kumuunga mkono Kamishna Jenerali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika kuifanya magereza mpya endapo na viongozi wao katika vituo watakuwa wepesi wa kuwa wabunifu na kupokea ushauri kutoka kwao.

Akitolea mfano wa ng’ombe wanaokufa wakati wa kiangazi katika baadhi ya maeneo askari huyo alisema ni jambo la kushangaza kuona ng’ombe wanakufa kwa kukosa maji wakati ng’ombe wasiozidi kumi wakiuzwa wanatosha kugharimia huduma za kuchimba kisima ili kunusuru walio wengi.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali Kasike alikubaliana na askari huyo akisema wakati mwingine tumefika hapa kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kuwa wabunifu na kutotaka kupokea ushauri kutoka kwa walio chini yao.

“ Mimi ni muumini wa uongozi shirikishi. Natoa wito kwa viongozi wote katika Jeshi letu kushirikisha wataalam bila kujali vyeo vyao. Pokeeni mawazo na ushauri. Cheo ni ngazi tu lakini mawazo ya mtu yanaweza kuwa ya msingi sana.Alihitimisha Kamishna Kasike.

Kamishna Jenerali Kasike amehitimisha ziara ya kikazi mkoani Dodoma iliyomfikisha katika ofisi mpya ya Makao Makuu ya Magereza mkoani humo, gereza Isanga, Msalato, Mpwapwa na Kongwa.

Akiwa mkoani humo amezungumza na maafisa na askari ambapo ujumbe wake mkuu kubadilika kabisa kwa namna tunavyofanya kazi. Aidha, ametembelea miradi mbalimbali ikwemo ufyatuaji matofali, ujenzi wa nyumba za kuishi za maafisa na askari kwa njia ya kujitolea, mradi wa upigaji kokoto wa Msalato, shamba la zabibu-Isanga na shamba la korosho la gereza Mpwapwa.

SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA KUACHA MIGOGORO KATIKA UBIA WA UWEKEZAJI

0
0

Naibu waziri wa madini, Dotto Biteko, akikagua uchimbaji sehemu ya hatua inapopitishwa Mbale ya shaba kabla ya kupatikana shaba halisi.
Naibu Waziri wa madini, Dotto Biteko, akizungumza na akina mama wanaofanya kazi katika mgodi wa shaba wa Mega.

Na Zuena Msuya, Kilimanjaro ,

Serikali imewataka Watanzania kuepuka migogoro katika maeno ya migodi hasa inayomilikiwa Kwa ubia na wawekezaji wazawa ili kuondoa taswira mbaya kwa wawekezaji kutoka Matifa mengine yanayokuja nchini kwa lengo la kuwekeza badala yake waungane kuweka mazingira mazuri na rafiki ya kuvutia wawekezaji hao kuwekeza nchini .

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati wa ziara yake mkoani Kilimanjaro alipotembelea mgodi wa Madini wa Mega unaochimba madini ya shaba .( Mega Copper Company) uliopo katika Kijiji cha Chang`ombe wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Kwan lengo la kumaliza mgogoro uliopo katika mgodi huo unachimba na kuchenjua madini ya Shaba.

Mgodi huo wa madini ya Shaba unaomilikiwa na Watanzania umekuwa katika migogoro ya kutoelewana wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka 10 sasa, Licha kumepiga hatau katika uchenjuaji wa shaba na kwamba hausafirishi madini ghafi nje ya nchi kama serikali ilivyoagiza.

Kwa mantiki hiyo, Biteko alisisitiza kuwa migogoro haipaswi kupewa nafasi na inarudisha nyuma maendeleo ya watanzania na kuleta taswira mbaya ya Uwekezaji Tanzania katika Mataifa mengine Duniani Kwani kusengskuwa na mgogoro katika mgodi huo wangekuwa wamepiga hatua zaidi kwa manufaa yao na Taifa kwa jumla.

Biteko alisema “migogoro miongoni ya wabia hasa wazawa haipaswi kufumbiwa macho na mtu yeyote Yule, ambapo alishauri kuwa kama watu, au kikundi wameingia makubaliano ya pamoja katika kuendeleza mgodi au jambo fulani basi, makubaliano hayo yapelekwe Wizara ya madini au katika mamlaka husika yasajiliwe kuepusha migogoro.

Aidha aliweka wazi kuwa kutokana na mgogoro, Serikali imetoa Miezi 3 kwa mgodi huo kumaliza tofauti zao na kuendelea na shughuli za uzalishaji, na endapo watashindwa kufanya hivyo, itawaandikia hati ya makosa na kisha kuwanyang’a mgodi huo na kuwapa watu wengine.

“Ninyi wote ni Watanzania tena ni ndugu kwa nini mnagombana? , Mnakuja kuwa Sheria ya madini inaruhusu kuwafungulia hati ya mashitaka na kuwafutia leseni endapo mgogoro huo hautakwisha na utakuwa na viashiria vya uvunjivu wa amani na Mkishindwa kuumaliza ndani ya muda uliotolewa Serikali unaingia Kati na kufanya maamuzi, nawakumbusha watanzania wote hasa wanaoishi katika maeneo karibu na migodi kuepuka migogoro ili sekta ya mdini iendeleee kuimarika” alisisitiza Naibu waziri Biteko.

Vilevile alitoa wito kwa wanatanzania wenye uwezo wa kuongeza thamani ya madini wafanye hivyo ili kuongeza pato la taifa na mwananchi mmoja mmoja kuliko kusafirisha madini ghafi nje ya nchi kwa kuwa faida kubwa zinapata nchi zinazo nunua madini ghafi hayo na kuyaongeza thamani .

Kwa mujibu wa Naibu waziri Biteko mgogoro ulipo katika mgodi huo kati ya wabia Watanzania wawili ambao kila mmoja alikuwa na mbao wake kutoka nje, ambao waliingia makubaliano ya kuanzisha mradi huo ndani ya miezi sita, baadae Kuliitokea kutoelewana na kUsababisha mmoja kati yao kuanza uzalishaji kabla ya kumshirikisha mwenzie.

Mmoja wa wabia hao ni Ally Nyanza kutoka ambaye alisema kuwa mgodi huo una ukubwa wa heka 25, ambapo kwa sasa wapo kwenye majaribio ya kuchimba na kuchenjua shaba Ambapo wanauwezo wa kuzalisha tani 8-10 za shaba kwa siku.

Alisema Bado wanaendelea na tafiti huku wakiendelea na uzalishaji, soko kubwa la shaba hiyo liko nchini China na kutokana na tafiti hizo wamegundua eneo hilo lina chokaa ambayo hutumika kwenye uzalishaji wa saruji.

Nyanza alismea changamoto kubwa ilikuwa na mgogoro kati yao na uliosabababisha kusimamisha uzalishaji kwa muda mrefu, kwa sasa wanafuata maelekezo ya Naibu waziri kupata muafaka wa kufanya kazi pamoja.

Naye Nassib Mfinanga alisema wamemeridhika na maamuzi ya Naibu Waziri wa Madini na kwamba watakaa kama familia ili tusonge mbele kwani mgogoro huo umekuwa ukituchelewesha na kutupa hofu kuwekeza bila kuwa na usalama, jambo hili lilikuwa ngumu kwetu.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Aaron Mbogho alisema uwepo wa mgodi huo ni chachu ya maendeleo katika wilaya hiyo tunasuburi wameanza uzalishaji pamoja wazingatie sheriana kanuni za wizara serikali bado inatamani kuona watoka kwenye uongezajiwathani ya shaba 90% hadi kufikia 100%.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NAMIBIA KUMWAKILISHA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA 38 WA SADC.

0
0
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christine Hoebes alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli 
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga  alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli 




  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christine Hoebes mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili  Mjini Windhoek Namibia leo Agosti 15, 2018 kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), utakaofanyika tarehe 17 – 18 Agosti 2018.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia, Makamu wa Rais amepokelewa na  Waziri wa Elimu ya Juu , Mafunzo na Ubunifu wa Namibia Mhe. Dkt. Itah Kandjii – Murangi , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christin Hoebes na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Namibia.

Hii ni sehemu ya mikutano ya awali ya maandalizi ya mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia. 

Mikutano mingine ya awali ni pamoja na mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC uliofanyika tarehe 9 na 11 Agosti 2018 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa , Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2018 ambao utapitia na kujadili hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018. 

Mkutano huu utahusisha nchi tatu za SADC Organ TROIKA na wajumbe wake ambao ni Angola Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Zambia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Organ na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Mwenyekiti wa Organ aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi hiyo.

Aidha Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utapokea, kujadili na kutolea maamuzi ya mapendekezo mbalimbali yanayotokana na mikutano ya kisekta na kamati za jumuiya kwa kipindi cha mwaka 2017/18.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huu utafanya uteuzi wa Mwenyekiti wa SADC na inatarajiwa kuwa Jamhuri ya Namibia ambayo ni Makamu Mwenyekiti wa sasa itateuliwa kuwa  Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha 2018/2019, nafasi ya Makamu mwenyekiti itajazwa pia na nchi itakayoteuliwa itajulikana tarehe 17Agosti 2018.

Uteuzi wa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, inatarajiwa kuwa Jamhuri ya Zambia, ambayo ni Makamu Mwenyekiti wa sasa itateuliwa kuwa Mwenyekiti kwa kipindi cha 2018/2019.

Mambo mengine yanayotarajiwa kujitokeza na kujadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na;  masuala ya fedha,Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda wa SADC na Maendeleo ya Viwanda,  Kutia saini itifaki mbalimbali ikiwa ni pamoja na itifaki ya Kulinda Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina Mpya za Mbegu za Mimea ya mwaka 2017. Pia Mkutano huu utatoka na tamko la nchi wanachama wa SADC la kutokomeza malaria katika ukanda wa SADC ifikapo mwaka 2030. 

Windhoek Namibia
15 Agosti 2018.




ELIMU WALIYOYAPATA UFUGAJI KUKU ITAWASAIDIA:ULEGA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri na Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Abdallah Ulega amefunga mafunzo ya siku mbili ya ufugaji wa kuku kwa Baraza la  wakina mama wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na kampuni ya AMK Gliters inayojihusisha na ufugaji wa kuku yalianza jana yakihudhuriwa na jumla ya wakina mama 326 kutoka kata mbalimbali za Mkuranga.Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Ulega amesema kuwa anatarajia kuona wakina mama wa jimbo la Mkuranga wanafuga kuku kwa ajili ya maendeleo pamoja na kukuza kipato chao.

Ulega amesema kuwa, elimu waliyoipata ya ufugaji wa kuku wa kibiashara utawasaidia wananchi hao kujiendeleza zaidi kiuchumi na kuwapa hamasa kuwa majukwaa kama haya yana faida kubwa kwa maendeleo ya Mkuranga.

Amesema, mafunzo ya ujasiriamali  kama haya yanawezekana ila changamoto kubwa imekuwa ni kufika kwa wakina mama hao kutokana na umbali wanapokaa ila amewaomba wasikate tamaa na kumtaka Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Jimbo la Mkuranga Mariam Ulega  kutoa taarifa ili wadau mbalimbali wawezw kujitokeza kuwawezesha pindi zinapojitokeza.

Hata hivyo Ulega, amemtaka Mwenyekiti Wa Baraza kuhakikisha vikundi vilivyojiandikisha tayari kuwa na akaunti za benki ili kuwe na nidhamu ya fedha hususani  usimamizi mzuri.Ameongezea kuwa, tayari ameshapata cherehani 50 na majora kwa ajili ya kuwapatia wakina mama na kila kata watapata cherehani 2 ikiwa ni njia nyingine ya kujiinua kiuchumi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Jimbo la Mkuranga Juma Abeid ameishukuru kampuni ya AMK Gliters kwa kuleta mafunzo hayo kwa wakina mama wa Mkuranga ikiwa ni moja ya maendeleo makubwa sana na elimu hiyo itawasaidia wakina mama hao kuweza kuongeza kipato chao cha kila siku.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Jimbo la Mkuranga Mariam Ulega amewataka wakina mama wa jimbo hilo kutumia fursa za mafunzo hayo kama chachu ya maendeleo na kuongeza kipato chao.

Katika mafunzo hayo makampuni mbalimbali yaliweza kutoa elimu ikiwemo Farm Base inayojihusisha na madawa ya kilimo na mifugo,Benki ya  CRDB ilitoa elimu ya uhifadhi fedha na mitaji ya vikundi pamoja na Taasisi ya  Mwanamke na Uongozi iliyotoa elimu kwa mwanamke ili kuweza kujitambua.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, (Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wajasiria mali katika kongamano la uwezeshaji kiuchumi lililo fanyika mkoni Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisalimiana na Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko.
Sehemu ya wajasiliamali mara wakiendelea na kongamano lililo fanyika mkoa wa Pwani.

PROMOSHENI YA UNLOCK CASTLE LITE YAANZA KUWA GUMZO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Watumiaji wa bia ya Castle wakipiga picha wakati wa promosheni eneo la Boko.
Kata mti panda mti ikiendelea wakati huo huo wadau wakipiga picha kwa pozi mbalimbali.
Maofisa Waandamizi wa Masoko wa TBL ndani ya promosheni hiyo.
Mambo ya Unlock na Castle yakiendelea.
Vijana hawakubaki nyuma katika ku unlock na Castle Lite.
Maofisa Waandamizi wa Masoko wa TBL ndani ya promosheni hiyo.
Ni mambo ya Castle Lite kwenda mbele. Kampuni ya TBL kupitia bia yake ya Castle Lite, imezindua promosheni kubwa ya wiki 13 inayojulikana kama Unlock Castle Lite, kwa lengo la kuleta burudani kwa wateja wake katika mabaa mbalimbali yaliyopo katika wilaya zote za jiji la Dar es Salaam. Lengo kubwa la promosheni hiyo ni Kutangaza chapa na kuwashukuru wateja kwa kuendelea kufurahia EXTRA COLD CASTLE LITE!. 

Tofauti na promosheni zilizozoeleka ,promosheni hii imesheheni kila aina ya burudani ambapo inaweza kuwakutanisha ndugu ,jamaa na marafiki pamoja na kupiga picha mbalimbali huku wakifurahia kinywaji bia ya Castle Lite. Unlock Castle Lite,ambayo inafanyika katika siku za Alhamisi na Ijumaa baada ya saa za kazi pia inawashirikisha wafanyakazi wa kampuni ya TBL ambao wanajumika pamoja na wateja na kuwapatia zawadi mbalimbali za promosheni.Tayari wakazi wa Kawe,Boko na Tegeta wamefikiwa na Unlock Castle Lite.

TANZANIA YANG'ARA KONGAMANO LA WATAALAMU WA MAGONJWA YA DAMU (HAEMATOLOGY) BARA LA AFRIKA

0
0
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Damu (Haematology), MUHAS Prof. Julie Makani (kulia) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuelezea mafanikio ya kongamano la kwanza la wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) linalokutanisha watalaam wa Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla. Pembeni yake ni Msimamizi wa Mafunzo hayo Prof. Lucio Luzzatto. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Msimamizi wa Mafunzo ya Wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) Prof. Lucio Luzzatto akionyesha chembe chembe zinazosababisha upungufu wa tamu mwilini wakati wakizungumza na wanahabari jijini  Dar es Salaam.
  Wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo bara la Afrika wakiwa katika sherehe ya kukaribishwa nchini Tanzania.


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

 Tanzania yang'ara kwa nchi za Afrika kwa kuwa nchi pekee ya kwanza kuandaa kongamano linalowakutanisha wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) kutoka mataifa mbalimbali duniani.

 Hayo yamezungumzwa na jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Damu (Haematology), MUHAS Prof. Julie Makani wakati akielezea mafanikio ya  kongamano la wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) linalokutanisha watalaam wa Tanzania na mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Bara la Afrika. 

 "Nitoe pongezi kwa serikali na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya afya na ndiyo maana kila kukicha kunakuwa na mabadiliko yanayopelekea kutokea matokeo chanya, wagonjwa badala ya kukimbilia nje ya nchi wanapata matibabu ndani" amesema Prof. Makani. 

Kongamano hilo lililoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Mfuko wa Kimataifa kusaidia masuala ya elimu Menarini (Fondazione Internazionale Menarini) la nchini Italia, ambalo limeweza kuwakutanisha madaktari bingwa ikiwemo watoa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology) takribani nchi zipatazo 15 barani Afrika wanaojadili changamoto wanazokumbana wakati wa utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology). 

Aidha Prof. Makani amesema kuwa mpaka sasa Tanzania imeweza kujitahidi kufanya jitihada za kipekee katika utoaji wa huduma japo changamoto inayowakumba ni uhaba wa wataalam zaidi wanaopenda kusomea utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology). 

Nae Msimamizi wa Mafunzo hayo Prof. Lucio Luzzatto amesema kuwa ni vyema Tanzania ikajivunia bahati iliyopata kwa kuweza kuwapa mafunzo watalaam wengi zaidi ili kuweza kuondokana na tatizo la magonjwa ya damu (Haematology) na kumekuwa na muitikio mkubwa wa kupokea mafunzo hayo. 

 Ameongeza kuwa Tanzania ndiyo itakuwa ikiandaa Kongamano hilo kila mwaka huku wakiongeza ushiriki wa nchi toka bara la Afrika ili kuweza kusambaza elimu hiyo zaidi. "Tutawafundisha njia za bora ya kutoa tiba ya kisasa kwa magonjwa ya damu na hata kuanzisha tiba hiyo sehemu zao walizotoka ili kuweza kupunguza idadi ya wagonjwa wengi ambao wanaokimbilia kupata huduma hiyo hospitali kubwa," amesema. 

 Nchi zinazoshiriki Kongamano hilo kutoka bara la Afrika ni Tanzania ambao ndiyo wenyezi, Uganda, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Ivory coast, Swaziland, DRC, Madagascar, Ghana, Ethiopia pamoja na Burkinafaso.

DIWANI WA CHADEMA AJIUZULU MAKETE NA KUHAMIA CCM

0
0
Aliyekuwa Diwani kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Kigala Wilayani Makete Mkoani NJOMBE  Kelvin Nguvila ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na nyadhifa zake zote ndani ya Chadema na kujiunga rasmi CCM jana jioni.

Akitangaza uamuzi huo jana jioni mbele ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Mh.Ona Nkwama,alisema Bw.Nguvila ameamua kuondoka Chadema na kujiunga CCM kwa lengo la kumuunga mkono Rais John Magufuli katika jitihada za kuwaletea Maendeleo Wananchi wake wa Kata ya Kigala

Imeandikwa Vitalis Konga,Makete

SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA

0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wataalam wa mkandarasi China Geo-Engineering Corporation anayejenga barabara ya Mpemba-Isongole kwa kiwango cha lami alipokagua barabara hiyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA mkoani Songwe msanifu majengo Christine Shayo, wakati wa ukaguzi wa shughuli za TBA mkoani Songwe .
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Songwe inayojengwa na Wakala wa Majengo Nchini TBA mkoa wa Songwe.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wataalam wa mkandarasi China Geo-Engineering Corporation anayejenga barabara ya Mpemba-Isongole kwa kiwango cha lami alipokagua barabara hiyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa amemtaka mkandarasi China Geo- Engineering Corporation aneayejenga barabara ya Mpemba-Isongole KM 50.3 kwa kiwango cha lami kuongeza kasi ya ujenzi ili barabara hiyo ikamilike kwa muda uliopangwa.

Amemtaka mkandarasi huyo kuongeza vifaa, wafanyakazi ili ujenzi wake ugawanywe sehemu mbili na hivyo kuwezesha ujenzi huo kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwakani.

“Kutokana na umuhimu wa barabara hii kwa uchumi wa mkoa wa Songwe hakikisheni inakamilika ili kufungua uchumi wa Wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe kwa ujumla”, amesema Mhe, Kwandikwa.

Barabara hiyo ambayo inaunganisha Tanzania na Malawi kupitia mto Songwe itachochea huduma za uchukuzi na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe.

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Songwe mhandisi Yohana Kasaini amesema barabara hiyo inahusisha ujenzi wa madaraja makubwa manne, ya kati 14 na madogo 172, imesanifiwa kubeba magari ya aina zote na itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 107 itakapokamilika.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Songwe na hospitali ya Tunduma zinazojengwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA),mkoani Songwe na kumtaka kaimu meneja wa TBA mkoani humo msanifu majengo Christine Shayo kuhakikisha ujenzi huo licha ya kutoa fursa za ajira kwa wakazi wa maeneo hayo pia ukamilike kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

Zaidi ya kilomita 3,856 za barabara nchini zitasanifiwa ili kujengwa kwa lami katika mwaka wa fedha 2018/2019

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

WANAFUNZI ZANZIBAR UNIVERSITY WAZURU UBALOZI WA OMAN

0
0
BALOZI Mdogo wa Oman anayefanya kazi zake Zanzibar Dk. Ahmad Hamood Al Habsy (Kulia), akizungumza na wanafunzi wanaosomea fani ya Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa, wakati walipofanya ziara kwenye ofisi za ubalozi huo zilizopo Migombani mjini Zanzibar.
DK. Ahmed Hamood Al Habsy, Balozi Mdogo wa Oman visiwani Zanzigar (Kulia) na Mhadhiri wa somo la Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu Zanzibar kilichoko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, Mohammed Yussuf.
WANAFUNZI, wahadhiri na baadhi ya maofisa wa Ubalozi Mdogo wa Oman mjini Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mdogo Dk. Ahmad Hamood Al Habsy nje ya jengo la ubalozi huo Migombani, Zanzibar baada ya ziara ya wanafunzi hao iliyolenga kubadilishana mawazo na kujifunza shughuli za Kidiplomasia na Mahusiano ya Kimataifa. (PICHA ZOTE NA HAROUB HUSSEIN). 

Na Salum Vuai, ZANZIBAR 

JUKUMU la mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika mataifa ya nje, ni kuwaunganisha wananchi na sio kuwa karibu na serikali na viongozi pekee. 

Kauli hiyo imetolewa na Balozi mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Dk. Ahmad Hamood Al Habsy, alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wanaosomea diplomasia na uhusiano wa kimataifa walipomtembelea ofisini kwake Migombani mjini Unguja. 

Balozi huyo alieleza kuwa, kwa kutambua hilo, amefungua milango ya ofisi yake kutoa fursa kwa wananchi mbalimbali wa Zanzibar pamoja na viongozi, kwenda kujifunza masuala muhimu kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi yao na Oman. 

Alisema, baadhi ya watu wanadhani kwamba kufanya kazi katika ofisi za kibalozi kuna mipaka inayowatenganisha mabalozi na wananchi wa kawaida, jambo alilosema sio sahihi. 

Dk. Al Habsy alisema licha ya mabalozi kuwajibika kiserikali katika mataifa wanayopelekwa kufanya kazi, pia wanapaswa kuwa karibu na wananchi wa nchi za nje wanazokuweko, wakitambua kuwa nayo ni sehemu ya majukumu yao. 

“Kwa kuwa balozi huwa anapeperusha bendera ya nchi yake ugenini, anapaswa kujua kwamba wenyeji wake sio serikali na viongozi pekee, bali wananchi wana haki ya kuwa miongoni mwa wahudumiwa wake kwa mambo mbalimbali,” alieleza. 

Balozi huyo alieleza kufurahishwa kwake na ziara ya wanafunzi hao iliyolenga kubadilishana mawazo pamoja na kujifunza juu ya shughuli za kidiplomasia, akiwataka pia kujibidiisha katika kusoma lugha mbalimbali za kimataifa ikiwemo Kiarabu. 

Alisema kutokana na uhusiano wake na Oman uliodumu kwa zaidi ya karne mbili sasa, Wazanzibari hawana sababu ya kutokujua lugha ya Kiarabu ambayo pia ndiyo msingi wa dini ya Kiislamu inayofuatwa na asilimia kubwa ya wananchi. 

Kwa upande mwengine, alisema mahusiano ya Zanzibar na Oman sio ya kirafiki ambao unaweza kufa, bali ni ya udugu wa damu utakaobaki milele hadi mwisho wa dunia. 

“Oman inasaidia nchi nyingi lakini kwa Zanzibar ina msaada wa kipekee kwani watu wa nchi hizi ni ndugu wa damu na hilo haifutiki. Ziara kati ya nchi zetu zimeongezeka sana, hata nafasi za ndege kati ya Muscat na Zanzibar au Tanzania, zinakuwa shida kutokana na wingi wa wasafiri,” alifafanua Dk. Al Habsy. 

Kwa hivyo, alisema ofisi yake itahakikisha inatanua fursa mbalimbali za kuisaidia Zanzibar hasa katika uwanja wa elimu, ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya watu wa pande mbili hizo. 

Mapema, Mhadhiri wa somo la diplomasia na mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mohammed Yussuf, akitoa shukurani kwa ubalozi huo alisema, ziara hiyo imewafunza mengi yenye tija. 

Aidha alisema ziara kama hizo katika ofisi za kibalozi, ni sehemu ya mafunzo yanayoweza kuwaongezea maarifa wanafunzi wa fani hiyo ambao ndio mabalozi wa miaka ijayo. 

“Namna wewe Mhe. Balozi unavyofanya kazi ya kuwaunganisha wananchi wa Oman na Zanzibar, ni darsa tosha kwetu na hasa wanafunzi hawa, kujua nidhamu inayohitajika kwenye kazi hii ya kidiplomasia,” alisema Mhadhiri huyo. 

Kwa upande wao, wanafunzi hao walieleza kufarijika kwa mapokezi waliyopata, na kusema wana matumaini makubwa ziara hiyo itafungua milango zaidi ya ushirikiano kati yao na ubalozi huo. 

Aidha walimuomba balozi huyo mambo mbalimbali, ikiwemo kuangalia uwezekano wa kuwatafutia Chuo Kikuu chochote nchini Oman kitakachokuwa tayari kuanzisha urafiki na chuo chao, na hatimaye kujenga utamaduni wa kutembeleana kwa lengo la kujifunza. 

Halikadhalika, walishauri kusaidiwa njia za kujiendeleza katika lugha ya Kiarabu ambayo pia wanafundishwa katika chuo chao, kuwaandaa kumudu kazi ya kidiplomasia. 

Balozi mdogo Dk. Al Habsy, aliahidi kuangalia namna ya kuyatafutia majibu maombi yao, huku akiutaka uongozi wa chuo hicho kuyawasilisha rasmi kwa barua ili yafanyiwe kazi kadri itakavyowezekana.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHE.HASUNGA ATAKA USHIRIKISHWAJI KWENYE UHIFADHI

0
0
NA LUSUNGU HELELA - MANYARA 

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewaagiza Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zake kuwashirikisha viongozi wa mikoa na wa wilaya wakati wanapokwenda katika maeneo yao kwa ajili ya kushughulikia migogoro ardhi kati ya Hifadhi na wananchi. 

"Nasema ni marufuku kwa Watumishi wa Wizara yangu kwenda kwenye maeneo ya Hifadhi bila kushirikisha uongozi wa eneo husika kwa jambo lolote litalohusisha wananchi  na Hifadhi" amesema Mhe.Hasunga. 

Aliyasema hayo jana kwenye mkutano mkoani Manyara kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.William Lukuvi kwa ajili ya kuzindua utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na Hifadhi utakaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi. 

Mpango huo una lengo la kutatua migogoro ya ardhi kati ya wananchi na Hifadhi utakaoshirikisha mikoa mitano ya Manyara,Dodoma,Mara,Arusha na Simiyu kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi. 

Naibu Waziri, Mhe. Hasunga alitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo kwa awamu ya kwanza kuwa ni Manyara, Arusha na Mara yenye jumla ya vijiji 95 kati ya vijiji 392 vilivyolengwa nchi nzima. 

Alisema kwa sasa Wizara imepiga hatua kubwa baada ya kupokea ushauri wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanza kuutekeleza kwa kuwashirikisha wananchi pamoja na Wizara ya Ardhi yenye dhamana kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi kati ya vijiji na Hifadhi. 

'Tumekuja kutambua kuwa sisi ni wahitaji wa ardhi na wananchi pia ni wahitaji wa ardhi hivyo hatuwezi kuamua wenyewe kwa kutambua hilo tumeanza kufanya kazi kwa ukaribu na Mkurugenzi wa upimaji na ramani kutoka Wizara yako lengo likiwa kumaliza migogoro kati ya Hifadhi na wananchi. 

Aliongeza kuwa Wizara inajikita kusaidia kufanya mipango shirikishi ya matumizi Bora ya Ardhi kati ya vijiji vinavyopakana na hifadhi kwa vile itasaidia kupunguza au kuondoa kabisa migogoro katika maeneo yanayopakana na hifadhi. 

Alisema mpango huo ni muhimu kwa vile idadi ya mifugo pamoja na binadamu wanazidi kuongezeka wakati maeneo hayaongezeki. Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema hatua ya kupanga matumizi bora ya ardhi ni hatua muhimu sana katika kumaliza migogoro kati ya Vijiji na Hifadhi. 

Aliongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya vizuri kuishirikisha Wizara yake kwa vile kipindi cha nyuma ilikuwa na migogoro ya ardhi kati ya vijiji na hifadhi isiyoisha ila kwa sasa itatuliwa kwa kubaini mipaka halisi. 

Katika hatua nyingine alisema hatua hiyo ni muhimu na hivyo viongozi wa mikoa itakayopitiwa na mpango huo watoe ushirikiano wa kutosha .Aidha, Aliwataka maafisa ardhi watakaoufanya kazi hiyo wafanye kazi kwa uaminifu na weledi wa hali ya juu na kwa haraka ili kuleta ufanisi wa Wizara yake. 

Naye, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Martin Leibook alisema sababu ya kufanya uzinduzi huo ni kutokana na ongezeko kubwa la migogoro siku hadi siku ambao unapelekea kutokuwepo na ushirikiano mkubwa kati ya wananchi na Hifadhi.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wajumbe kwenye mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara -liowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na wajumbe wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo.

 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (katikati) mara baada ya kufanyika mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. Wa tatu kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania, Martin Leibook. 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanyika mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) akiagana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge Mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo . 
1. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia) wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexandar Mnyeti.

(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT) 


MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA

0
0


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akitizama mvinyo uitwao (Perfect Wine) iliyoandaliwa kwa matunda ya nanasi iliyotengenzwa na kikundi cha Cris Food Products wa mkoani Geita alipokuwa akitembelea mabanda ya wafanyabiashara waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara leo katika viwanja vya Gadeco,ambapo jukwaa hilo limeandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) (pembeni kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na wenzake mara baada ya kupewa magazeti ya Habari Leo na Dailynews kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipokuwa akitembelea mabanda ya wafanyabiashara waliyoshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara lililoandaliwa na (TSN) leo mkoani Geita katika viwanja vya Gadeco (wakwanza kushoto) ni Msemaji Mkuu wa Serikali Tanzania Dkt.Hassan Abbas na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu kusaidia wadau wa sekta ya filamu mkoa wa Geita kupatiwa Stika za TRA katika ofisi ya TRA mkoani hapo badala ya wasanii hao kulazimika kwenda mpaka ofisi za Dar es Salaam alipowatembea katika banda lao la Maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara katika viwanja vya Gadeco,wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Bw.Richard Kayombo na katikati ni Meneja wa Ofisi ya TRA Mkoa wa Geita James Jilala.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia)akionyeshwa asali iliyopitishwa katika viwango vya kimataifa inayozalishwa katika wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita na mmoja wa wajasiriamali ambaye jina lake halikutambulika kwa harakaalipotembelea mabanda ya Maonesho ya wadau waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).
Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Dkt.Hassan Abbas akitizama bidhaa za wajasiriamali waliyoshiriki Jukwaa la Biashara linalofanyika leo Mkoani Geita lililoandaliwa na (TSN ) katika maonesho yanayofanyika katika viwanja vya Gadeco Halmashauri ya Mkoa wa Geita.

NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU.

0
0
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akitamburishwa baadhi ya viongozi walioshiriki mkutano mkuu wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa J.K Nyerere uliopo Chuo Kikuu cha Ushirika,Moshi (MOCu) kwa ajili ya kufungua mkutano wa Tano wa chama hicho.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.
\Baadhi ya Wajumbe wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) Dkt Paul Loisulie akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa kamati ya Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania(THTU),Salma Fundi akizungumza katika mkutano huo.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akizungumza katika mkutano huo.
Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu ca Ushirika Moshi (MOCU) Dkt Gudluck Mmari akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) Amina Mdidi akizungumza katika mkutano huo.
Mjumbe wa kamati ya wananwake ya THTU,Sophia Nchimbi akitoa neon la shukrani katika mkutano huo.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwa katika picha ya pmaoja na washiriki wa mkutano huo.

NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.




Na Dixon Busagaga,Moshi.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) kimeiomba serikali kutunga sera ya uwepo wa eneo rafiki la kulelea au kunyonyeshea watoto katika sehemu za Kazi  pamoja na kuunda chombo cha kusimamia utekelezwaji wa uwepo wa sera ya unaynyasaji wa kijinsia katika taaasisi za elimu ya juu nchini.

Mbali na ombi hilo THTU pia kimewasilisha ombo kwa serikali la kuundwa Vyombo vya kufuatilia waajiri ambao hawazingatii maagizo ya sera zinazotungwa na serikali ili kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi  sambamba na uwepo wa muundo wa utumishi kwa wafanyakazi waendeshaji katika taasisi za umma za elimu ya juu nchini.

Hayo yalibainishwa wakati wa mkutano mkuu wa tano wa chama hicho unaofanyika kwa siku mbili katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ukishirikisha zaidi ya wanawake 80 kutoka vyuo vikuu 36,vitatu vikiwa ni vya binafsi  na 33 vya serikali .

Katika risala yao kwa mgeni rasmi ,iliyosomwa na katibu wa THTU,Amina Mdidi ,wanawake hao walisema THTU imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kutokuwepo kwa mwongozo wa mishahara au bodi ya kusimamamia na kudhibiti malipo ya watumishi kwa vyuo binafsi.

“Changamoto nyingine zinazootukabili ni baadhi ya taasisi kutolipa nauli za likizo kwa enza wa wafanyakazi wanawake (Mume) na watoto chini ya miaka mitano na ukosefu wa vituo rafiki kwa malezi ya watoto wachanga”alisema Mdidi.

Katika hatua nyingine ,Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania kilitoa ripoti ya utafiti juu ya utekelezaji wa sera ya maendeleo ya mwananmke na jinsia ya mwaka 2000 katika taasisi za elimu ya juu Tanzania ikionyesha aslimia 80 ya taasisi hizo zilionyesha kutokuwepo kwa masuala ya jinsia katika mpango mkakati wa taasisi.

Akisooma utafiti huo ,Mwenyekiti wa kamati ya Wanawake (THTU) taifa Salma Fundi alisema asilimia 80 ya taasisi hazikuonyesha uwepo wa mafunzo kwa wanafunzi au wafanyakazi kuhusiana na masuala ya jinsia.

“Asilimia 70 ya taasisi hazina sera ya unyanyasaji wa kijinsia ambazo ni muhimu katika kupunguza ubaguzi wa kijinsia na ukatili huku asiliamia 60 ya washiriki walikuwa na mtazamo hasi juu ya sera ya jinsia kwa kuamini ni sera inayomhusu mwanamke tu”alisema Fundi.

Katika hotuba yake Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo,Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella  Ikupa alisema THTU kwa muda mfupi kimekuwa chama kinachotoa chachu ya maendeleo na amani ndani ya taasisi za elimu ya juu Tanzania.

“Ni chama ambacho kiko makini katika shughuli zake za utatuzi na hata mfumo na uwasilishaji wa hoja zake umekuwa ni wa aina ya kipekee kwa kufanya tafiti zilizochambuliwa kwa kina wa nini wanawake wanafikilia kifanyike”alisema Ikupa.

Waziri Ikupa aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wan chi ,ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge,KAZI,Vijana ,Ajira na Wenyeulemavu ,Jenista Mhagama aliahidi kuwasilisha mapendekezo yao pamoja na changamoto walizo wasilisha  kwa serikali  kwa ajili ya kuafanyiwa kazi.

MAVUNDE AITAKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI(CMA) KUFANYA KAZI KWA UADILIFU NA KUAMUA MASHAURI KWA UHARAKA

0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Peter Mavunde akizungumza katika mafunzo ya Wafanyakazi wa CMA kutoka nchi nzima ambapo ameongoza mazoezi ya Viungo na mashindano ya mpira wa miguu,kamba na kufukuza kuku yaliyoandaliwa na CMA.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Peter Mavunde akishiriki katika mafunzo ya Wafanyakazi wa CMA kutoka nchi nzima ambapo ameongoza mazoezi ya Viungo na mashindano ya mpira wa miguu,kamba na kufukuza kuku yaliyoandaliwa na CMA.

Baadhi ay washiriki wa mazoezi hayo wakiendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Peter Mavunde akkokota mpira wakati akishiriki mazoezi katika mzoezi ya Wafanyakazi wa CMA kutoka nchi nzima ambapo ameongoza mazoezi ya Viungo na mashindano ya mpira wa miguu,kamba na kufukuza kuku yaliyoandaliwa na CMA.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Peter Mavunde amewataka WASULUHISHI na WAAMUZI wa TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI(CMA) kufanya kazi zao kwa uweledi na kwa kuzingatia maadili katika utoaji wa haki na pia kuhakikisha wanatoa maamuzi kwa wakati pasipo ucheleweshaji ili kusaidia kuchochea maendeleo ya Uchumi wa Viwanda.

Mavunde ameyasema hayo leo asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri-Morogoro wakati akihitimisha ratiba ya awali ya siku 3 ya mafunzo ya Wafanyakazi wa CMA kutoka nchi nzima ambapo ameongoza mazoezi ya Viungo na mashindano ya mpira wa miguu,kamba na kufukuza kuku yaliyoandaliwa na CMA.

Akimkaribisha Naibu Waziri Mavunde,Mkurugenzi Mkuu wa CMA Ndg. Shines Nungu amebainisha kwamba kwa sasa wamejiwekea mpango mkakati kabambe wa kumaliza mashauri yote kwa wakati ambapo hadi hivi sasa migogoro ya usuluhishi 7,017 kati 9,379 na migogoro ya uamuzi 2,895 kati 5,209 imeshafanyiwa uamuzi.

WANANCHI ZAIDI 2000 WANUFAIKA NA MAJI SAFI SALAMA SIMIYU

0
0
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwisha ndoo ya maji Bi. Perusi Makeleja Mkazi wa Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima mara baada ya kufungua mradi wa maji utakaowahudumia zaidi ya wananchi 2000, katika mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo leo Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akifungua bomba la maji kujiridhisha ikiwa linatoa maji kabla ya kuzindua mradi wa maji wa Lagangabilili wilayani Itilima wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akiweka Jiwe la Msingi Maboresho ya Kituo cha Afya Ikindilo wilayani Itilima mkoani Simiyu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho (wa pili kulia) akiangalia baadhi ya vifaa vya maabara ya Somo la Bailojia katika Shule ya Sekondari Budalabujiga kabla ya kufungua vyumba vitatu vya maabara vya shule hiyo wilayani Itilima, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018. 


Na Stella Kalinga, Simiyu


Zaidi ya wananchi 2000 wa Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima Mkoani Simiyu wamenufaika na mradi wa maji safi na salama na kuondokana na adha ya kutumia muda mrefu kutafuta maji kwa kusogezewa huduma ya maji karibu na makazi yao.

Hayo yamesemwa na Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Goodluck Masige wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho, aliyefika katika mradi wa maji wa Lagangabilili wenye thamani ya shilingi milioni 967, kwa ajili ya kufungua.

Masige amesema Mradi wa Maji wa Lagangabilili ulianza kutekelezwa mwaka 2015 na kukamilika mwaka 2018 na kuanza kutumika huku akibainisha uwezo wake kuwa, una kisima chenye uwezo wa kutoa maji lita 15,000/= kwa saa, vituo vya kuchotea maji 23 na mtandao wa maji wenye urefu wa mita 29,431.

“Kukamilika kwa mradi huu wakazi 2228 wanapata huduma ya maji safi na salama kwa ajili ya kunywa na matumizi mengineyo,mradi umepunguza muda waliokuwa wanaoutumia wananchi kutafuta maji kwa kuwasogezea huduma ya maji karibu na makazi kwa saa 24,mpaka sasa kaya 25 na taasisi za Umma 20 zimeunganishiwa maji” alisema Masige .

Awali Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi amesema kuwa tangu Uhuru eneo hilo lilikuwa halina maji kabisa, na baada ya kupatikana kwa huduma hiyo kutapunguza adha ya uhaba wa maji, huku akibainisha kuwa Serikali inategemea mradi mkubwa kutoka Ziwa Victoria kuwa suluhisho la kudumu la changamoto ya maji ka ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama pia.

Perusi Makeleja mkazi wa Kijiji cha Lagangabilili amesema kukamilika kwa mradi huo kumewapunguzia adha wananchi hususani wanawake ya kusafiri umbali mrefu na kuamka alfajiri kufuata maji lakini umesaidia kupunguza magonjwa.“Kabla ya mradi huu tulikuwa tunaamka usiku usiku kwenda kutafuta maji mbali tunapishana na fisi njiani, watoto wetu walikuwa wakiugua magonjwa ya tumbo na kuhara kutokana na kunywa maji ambayo hayakuwa salama, , lakini kwa sasa hizo shida hamna tena, tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kutuletea mradi huu sisi Wanalagangabilili” alisema

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kutatua changamoto za wananchi wake, ambapo katika ujenzi wa mradi huo Serikali ya Tanzania imechangia kiasi cha shilingi milioni 907 huku serikali ya Misri ikichangia kiasi cha shilingi milioni 60 ili kukamilisha ujenzi huo.

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Itilima umefungua vyumba vinne vya madarasa shule ya msingi Lagangabilili pamoja na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa maboresho ya kituo cha afya Ikindilo unaojumuisha jengo la wodi ya wazazi, jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti na nyumba ya mganga na kukagua Shamba darasa la Ufugaji wa Nyuki na Utunzaji wa Mazingira.

Aidha, kiongozi huyo ariridhishwa na ubora wa majengo ya miradi hiyo, huku akiwapongeza viongozi wa wilaya na Halmasharui kwa usimamizi makini ambapo aliwataka kuhakikisha majengo hayo yanakamilika ujenzi wake na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.Katika hatua nyingine akiwa Wilayani Itilima Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuendelea kuchangia chakula cha mchana shuleni ili watoto wapate Muda wakujisomea zaidi hali itakayosaidia kupunguza utoro.

Mwenge wa Uhuru unaendelea na Mbio zake Mkoani Simiyu ambapo Agosti 15 Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Wilaya yaItilima umepita katika miradi sita yenye thamani ya bilioni 1.6

MultiChoice yawawezesha vijana,yamwaga Bajaji 27

0
0
Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeimarisha mkakati wake wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

Katika kutimiza hilo kampuni hiyo imekabidhi ofisi na bajaji tisa kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam na inatarajia kupanua mradi huo kwenda mikoa mingine ikiwemo Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma.

Akizungumza katika makabidhiano ya Bajaji hizo yaliyofanyika leo Alhamisi Agosti 16 katika makao makuu ya MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo Salum Salum, amesema hii ni awamu ya kwanza ya mradi huo ambapo wametoa jumla ya bajaji 27 kwa viunga 9 vya Dar es salaam na kwamba baada ya awamu hii watafanya tathmini na kisha kuupanua hapa Dar es Salaam ni mikoa mingine.

Amesema katika mradi huo, MultiChoice inawafadhili vijana hao ofisi za uwakala wa DStv na pia inawadhamini vitendea kazi muhimu kama vile Kompyuta na Bajaji ili viwawezeshe kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mmoja wa mawakala wapya wa mauzo wa DStv wa kiunga cha Temeke Rose Haule wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

“Tumekuwa tukifanya kazi na vijana wengi ambao ni mawakala wa mauzo wa kujitegemea (direct sales) lakini sasa tumeamua tuwafanye wabia wetu wa kibiashara na kuwawezesha kuendesha biashara rasmi ya uwakala wa DStv” alisema Salum na kuongeza kuwa vijana hao watakuwa wakitoa huduma katika maeneo maalum yajulikanayo kama ‘viunga’. Kila wakala atakuwa na kiunga chake, na atakuwa na jukumu la kuhakikisha wateja wa eneo lake wanahudumiwa kwa haraka

“Vijana hawa watakuwa na mtandao wa vijana wengine wa mauzo na mafundi wa kufunga DStv ambao wamepata mafunzo maalum na kuthibitishwa. Kwa hiyo, kama mteja yuko Mbagala, atahudumiwa na wakala wa kiunga cha Mbagala, hivyo hivyo aliyeko Tabata atahudumiwa na kiunga cha Tabata na hii itakuwa kwa viunga vyote ambavyo ni Mbagala, Tabata, Kigamboni, Ilala, Chang’ombe, Mbezi beach, Mbezi Kimara, Manzese na Ukonga.
Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum (wa pili Kulia) akizungumza na kiongozi wa Kiunga cha DStv Temeke Rose Haule (wa pili Kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj). Kulia ni Khalfani Soni na kushoto ni Omari Ali wote wa Gongo la Mboto.

Amesema kwa kuwarasimisha vijana hawa, sasa watakuwa wanafanya biashara rasmi, wakiwa na leseni na ofisi na hivyo kuweza pia kulipa kodi stahiki kwa serikali na hivyo kuongeza mchango wao kwa uchumi wa nchi.

Wakizungumza bara baada ya kukabidhiwa bajaji hizo sambamba na laptop, wakuu wa viunga hivyo wamesema wamekuwa wakifanya kazi kama mawakala wadogo wa kujitegemea kwa muda sasa lakini walikuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kutokuwa na ofisi rasmi na pia vitendea kazi hususan usafiri.

“Tulikuwa tunafanya mauzo kwa tabu sana kwani kwanza kutokuwa na ofisi ilikuwa ni vigumu kwa wateja kutupata. Pia hata ukipata mteja unalazimika kubeka vifaa kwenye usafiri usio wa uhakika kwenda kwa mteja na hii ilikuwa inapoteza muda na kuongeza gharama” alisema Rose Haule mkuu wa kiunga cha Temeke.
Wakala wa mauzo wa DStv Rose Haule wa Temeke (aliyeko ndani ya Bajaji) akifurahia na wenzake Khalfani Soni wa Gongo la Mboto, Omari Ali wa Gongo la Mboto na Sarah Makasia wa Manzese wakifurahia muda mfupi baada ya hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

Naye Yusuph Migeto wa kiunga cha Mbagala amesema kuwa kuwepo kwa ofisi na usafiri wa uhakika kutawahakikishia wateja wao huduma ya haraka na yenye ufanisi. “wakati mwingine wateja walikuwa wanalalamika kwa kucheleweshewa huduma kwani ukipata mteja inabidi ufuate vifaa DStv kisha uende kumfungia mteja. Hii ilikuwa inachelewesha sana. Lakini kwa sasa tutakuwa na uwezo wa kuwa na vifaa karibu na pia kuwepo kwa usafiri wa uhakika kutatufanya kufanya kazi kwa haraka zaidi”
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images