Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46338 articles
Browse latest View live

BENKI KUU YA TANZANIA YAPONGEZA UBUNIFU WA BENKI YA NMB KATIKA KURAHISHA HUDUMA ZA KIBENKI NCHINI

$
0
0
Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese akizungumza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa huduma ya kibanki ya NMB inayojulikana kwa jina la Klik App ya NMB kwenye hoteli ya Hyyat jijini Dar es salaam leo.
Bi. Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Hyyat jijini Dar es salaam.
Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese akiwa amekaa pamoja na wageni mbalimbali waalikwa na viongozi wa benk ia NMB wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo mbalimbali Benki ya NMB wakiwa katika hafla hiyo.
Bi. Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB akiwa pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Bi. Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB pamoja na Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.



*Yazindua huduma ya Klik App NMB inayowezesha kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeipongeza Benki ya NMB kwa uamuzi wake wa kuzindua huduma ya kufungua akaunti kwa kutumia mtandao wa simu ya mkononi.

Imesema hatua hiyo imethibitisha namna benki hiyo inavyotumia ubunifu na kukua kwa teknelojia ya mawasiliano kwa kurahisisha huduma za kibenki nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese wakati akizindua Klik App ya NMB inayowezesha mteja kufungua akaunti kupitia simu ya kiganjani.

Amesema kuwa ubunifu huo ambao umefanywa na benki ya NMB utarahisha watanzania wengi kufungua akaunti za benki hiyo kupitia simu zao na kwamba hivi sasa watumiaji wa simu za mkononi ni wengi na hivyo huduma hiyo ya NMB imekuja wakati sahihi.

“Tunaipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao wa kuhakikisha wanatumia teknolojia iliyopo kuanzisha huduma za kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi na kizuri zaidi hata wenye simu za tochi bado wanaweza kufungua akaunti kupitia huduma hiyo,”amesema Dk.Kibese.

Amefafanua kuwa kama mnavyofahamu idadi kubwa ya Watanzania wanapotaka kununua bidhaa wanakwenda na fedha mkononi na hiyo imekuwa changamoto kubwa hasa ya usalama wa fedha.Lakini sasa NMB mbali ya kuja na huduma ya kukuwezesha kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi pia wanayo huduma nyingine ambayo inakuwezesha kununua bidhaa kwa kutumia simu.

“Kuna kifaa ambacho unatumia kupitisha kwenye simu yako na kupata huduma ambayo pia hata kwenye simu ya tochi bado atapata huduma.Kwa mazingira ya aina hii lazima tutoe pongezi kwa NMB kwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu kwa kutumia teknolojia iliyopo kurahisha huduma za kibenki nchini,”amesisitiza.

Ameleezea namna ambavyo huko nyuma yametokea mambo mengi ya uporaji wa fedha na wakati mwingine yamesababisha baadhi ya watu kuuawa kwasababu ya fedha ambazo wameshika mkononi lakini sasa NMB wamekuja na huduma ambayo inaweka usalama wa fedha kwani hakuna sababu ya kutembea na fedha mkononi.“Kuna kijana siku za nyuma alivamiwa na kuporwa Sh.milioni 10 na kibaya zaidi aliuawa .Hivyo kama kungekuwa na huduma kama hii ambayo NMB yangeendelea kuwa hai,”amesema.

Dk.Kibese amesema kwa sasa Watanzania wengi wanamiliki simu na kikubwa ni matumizi ya huduma za mtandao yaongezeke na kwamba wanachokifanya NMB ni kutimiza ndoto ya usalama zaidi wa fedha.Pia amesema NMB wanayo huduma ambayo inamuwezesha mtu kufanya miamala mbalimbali na kwamba benki hiyo wamekuja na App inayomuwezesha mtanzania kukopa kupitia simu.

“Bot inao wajibu wa kuangalia usalama wa fedha za mteja na pia kuhakikisha ubunifu katika nchi hii unapewa kipaumbele.Hivyo kwetu sisi tunayo sababu ya kuipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao,”amesema.

Ameongeza kitendo cha kutumia simu kufanya miamala mbalimbali ya kibenki maana yake inatoa nafasi ya fedha kuwa salama na ndicho ambacho BoT wanasimamia kuhakikisha kunakuwa na mifumo imara ya usimamizi wa fedha.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AITAKA CMA KUONGEZA KASI YA UTATUZI WA MIGOGORO YA KIKAZI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba (wapili kushoto), mara baada ya kufungua mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa Tume katika Utatuzi wa Migogoro ya Kikazi na Tathmini ya Utendaji Kazi(CMA), mjini Morogoro leo Agosti 14, 2018. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw. Shanes Nungu, (wakwanza kulia), Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini, Bi. Regina Chonjo, na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw.Noel Kazimoto. Mafunzo hayo yameandaliwa kwa pamoja na WCF na CMA. Ili kuwajengea uwezo watumishi hao katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kuwajengea uwezo watumishi wa Tume katika Utatuzi wa Migogoro ya Kikazi na Tathmini ya Utendaji Kazi. Mafunzo hayo yaliyowezeshwa kwa pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, na CMA, yamewaleta pamoja watumishi kutoka Tanzania Bara na yameanza leo Agosti 14, 2018 Mkoani Morogoro.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ameitaka Tume ya utatuzi wa migogoro ya kikazi na tathmini ya utendaji kazi, (CMA) kuongeza kasi ya kushughulikia migogoro ya kikazi.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo leo Agosti 14, 2018 wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa Tume hiyo mjini Morogoro.

“Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kwa dhati kujenga uchumi wa Kati kupitia Viwanda. Hivyo basi, katika kuunga mkono dhamira hiyo ya Serikali, rai yangu kwa Tume ni kuhakikisha kuwa migogoro yote ya kikazi inayohusiana na masuala ya Viwanda inatatuliwa kwa wakati na bila ya upendeleo.” Alisema.

Akifafanua zaidi Mhe. Waziri alisema suala la kutatua migogoro kwa wakati, kwa haki na kwa kuzingatia sheria lina mchango mkubwa katika kudumisha amani na utulivu mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na viwandani na kuleta tija, lakini pia kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza nchini. 

Aidha Mheshimiwa Waziri Jenista alisema, Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wadau hasa wafanyakazi kwamba baadhi ya Wasuluhishi na Waamuzi wanachelewesha maamuzi na baadhi wanatoa uamuzi kwa upendeleo, hivyo kuleta hisia ya kujihusisha na vitendo vya rushwa. 

Alisema, anayotaarifa kwamba, mwaka 2017/2018 mtumishi mmoja (1) aliachishwa kazi kwa tuhuma za rushwa, mmoja (1) alifikishwa mahakamani, na mmoja (1) amepewa onyo kali sana kwa tuhuma ya kuondoka kazini bila ya ruhusa. 

“Nichukue nafasi hii kuuagiza uongozi wa Tume kuendelea kuchukua hatua kali kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa naitaka TAKUKURU kuimulika Tume hii kwa macho yote ili wote wanaotaka kuichafua Tume waondolewe haraka na kukabidhiwa kwenye mkono wa Sheria.”

Ili kutilia mkazo suala la kuzingatia maadili ya kazi, Mhe. Waziri alisema atamuandindikia barua Waziri mwenye dhamana ya Utawala Bora, ili kumchunguza kila mmoja wenu, na hatimaye kuwabaini wote wanaojificha na kufanya vitendo viovu katika kutekeleza majukumu ya kazi. 

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Waziri, Mkurugrenzi Mkuu wa CMA, Bw.Shanes Nungu alisema, mafunzo hayo yameandaliwa na tume kwa kushriikiana na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), ili kuwajengea uwezo watumishi wa Tume kutoka Tanzania Bara.

Aliishukuru WCF, kwa kuwaunga mkono katika kuandaa mafunzo hayo ambayo yataboresha uwaji bikaji kutokana na kuongezewa ujuzi. 


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema, CMA ni wadau wakubwa wa Mfuko, na kwakuwa wameandaa mafunzo ili kuelimisha watumishi, Mfuko nao umechukua fursa hiyo kuendelea kutoa elimu kuhusu majukumu ya Mfuko, ikiwa ni pamoja na huduma mpya ya usajili wa waajiri kupitia mtandao.

"Wataalamu wetu wako hapa na watatoa elimu kuhusu shughuli mbalimbali za Mfuko, namna ya kufanya tathmini lakini kuhusu masuala ya sheria zinazotuongoza katika kutekeleza majukumu yetu." Alisema Bw. Masha Mshomba. 
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akitoa neon la utangulizi.
Waziri Jenista Mhagama, akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini, Bi Regina Chonjo.
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja na watoa mada 
Baadhi ya washiriki
Kutoka kushoto, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omary, na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa.
Mkurugenazi Mkuu wa CMA, Bw. Shanes Nungu, (kulia), akitoa hotuba yake. Kushoto ni Bw. Masha Mshomba.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, akitoa mada ambapo alizungumzia maswala ya kisheria yanayohusu Mfuko katika utendaji kazi wake.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akizungumzia muundo wa Mfuko, wajibu mbalimbali kuhusu utekelzaji wa majukumu ya Mfuko, Mwajiri na mwajiriwa.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omary, akitoa mada kuhusu hatua mbalimbali ambazo mwajiri na mfanyakazi wanapaswa kuzifuata sambamba na jinsi tathmini inavyofanyika kabla ya zoezi la kulipa fidia halijatekelezwa.
Bw. Ponziano Lukosi, kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kiwasilisha mada, ambapo alielezea shughuli za ofisi ya AG 
Bw.Frank Mwalonga, kutoka Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), akitoa mada kuhusu namna CMA inavyoweza kushughulikia masuala ya migogoro inapofika mahakamani.
Bw. Mshomba na Bw. Peter wakijadiliana jambo.
Picha ya pamoja meza kuu na watendaji wakuu wa CMA.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), na Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko huo Bi. Amina Likungwala, wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw. Shanes Nungu, akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mafunzo.

LUGOLA ATOA ONYO KALI KWA TRAFIKI WAOMBA RUSHWA, WANAONYANYASA WAENDESHA BODABODA WAFUATA SHERIA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Igundu, Jimboni kwake Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. Katika hotuba yake, Lugola alitoa onyo kwa baadhi ya polisi wa usalama barabarani kuacha tabia ya kuomba rushwa pamoja na kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu waendesha bodaboda ambao wanaofuata sheria za usalama barabarani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akipiga ngoma ya asili ya Lukuyamoyo ya Kabila la Wajita wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Kisorya, Mwibara, Wilaya ya Bunda Mkoani Mara. Lugola alitoa ovyo kwa baadhi ya polisi wa usalama barabarani kuacha tabia ya kuomba rushwa pamoja na kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu waendesha bodaboda ambao wanaofuata sheria za usalama barabarani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimkabidhi Nyajoke Masatu, Kapteni wa Timu ya Brendabuke, zawadi ya shilingi 250,000 baada ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuifunga kwa penati timu ya Igundu katika mashindano ya mpira wa miguu la Bonanza la Kangi, linaloendelea katika kata 12 za Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. Katika hotuba yake, Lugola alitoa ovyo kwa baadhi ya polisi wa usalama barabarani kuacha tabia ya kuomba rushwa pamoja na kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu waendesha bodaboda ambao wanaofuata sheria za usalama barabarani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto) akimkabidhi dawati Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwigundu, Masele Kadoke, mara baada ya Waziri huyo kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Igundu, Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. Lugola aliikabidhi Sekondari hiyo madawati 30 katika mkutano huo na alitoa ovyo kwa baadhi ya polisi wa usalama barabarani kuacha tabia ya kuomba rushwa pamoja na kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu waendesha bodaboda ambao wanaofuata sheria za usalama barabarani.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SERIKALI YAKABIDHI BOTI YA DORIA NA KITUO CHA POLISI WILAYANI CHATO

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyeshika koti), akishuka katika boti maalumu aliyowakabidhi Kikosi cha Polisi wilayani Chato ikiwa ni mkakati wa Serikali kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na Bahari nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla akimshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kumkabidhi Kituo cha Polisi kinachohamishika wilayani Chato.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea eneo la mwambao wa Ziwa Victoria baada ya kuikabidhi boti hiyo ya doria kwa Jeshi la Polisi, kutoka kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na Diwani wa Chato, Richard Bagolele . Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Mwandishi Wetu

Serikali imejipanga kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kote nchini ili kuweza kudhibiti uhalifu unaotekelezwa majini ikiwepo uvuvi haramu, usafirishaji wa magendo na uhalifu mwingine unaotokea katika maeneo ya ziwa na bahari.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya boti maalumu ya doria na ufunguzi wa Kituo cha Polisi Wanamaji, wilayani Chato, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inadhibiti uhalifu katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kwa kutumia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya serikali, ili kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kuchumi bila ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao

Alisema moja ya changamoto kubwa aliyoelezwa wakati alivyofanya ziara ya awali wilayani Chato ni kuwepo kwa matukio ya uhalifu ziwani yaliyopelekea baadhi ya wananchi kusitisha shughuli za kiuchumi katika mwambao huo wa Ziwa Victoria.

“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuleta maendeleo katika nyanja zote na kuwawekea mazingira mazuri wananchi wake kujishughulisha na shughuli za kiuchumi, hivyo basi tutahakikisha tunaimarisha ulinzi katika sehemu zote ambazo wananchi wanafanya shughuli zao ikiwepo ukanda wa ziwa na bahari na leo hii tunaanzia hapa wilayani Chato.

“Pia nawasihi askari polisi kufanya kazi kwa maadili na agizo hili nalitoa kwa nchi nzima na serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aitomvumilia askari yoyote atakaebainika kuwabambikia kesi wananchi,hatua kali zitachukuliwa kwa atakaebainika” alisema Masauni ambae pia ni Mbunge wa Kikwajuni

Naye Diwani wa Kata ya Muungano, wilayani Chato,Johnson Kilimokwanza alisema anaishukuru serikali kwa kuleta boti hiyo na ufunguzi wa kituo cha polisi kwani moja ya changamoto iliyokuwa inawasumbua wavuvi katika mwambao huo ni masuala ya uhalifu unaotokea ziwani huku akiweka wazi uwepo wa kituo na boti ya doria vitapunguza masuala ya uhalifu.

Mmoja wa askari polisi ambae hakupenda jina lake litajwe alisema wao wanaishukuru serikali kwa kuwaletea boti na kituo ambavyo vitawarahisishia kupambana na uhalifu

“Muhimu naomba serikali pia waweze kutuletea gari ambalo litasaidia pia katika mapambano hayo ya uhalifu kama unavyoona tayari tuna kituo hapa cha wanamaji naibu waziri amekizindua,muhimu sasa tuletewe usafiri utakaowezesha kupeleka mahabusu mahakamani,” alisema askari polisi huyo.

THE NGOMA AFRICA BAND 'GOLDEN VOICE OF EAST AFRICA" TAKES OVER EUROPEAN FANS BY STORM AGAIN

$
0
0




The Ngoma Africa Band aka FFU also known as Anunnaki alien, the most successfull African live Band based in Germany has been vastly gaining popularity through an extra ordinary rhythm “Bongo Dance” from Tanzania and Neighbouring East African countries which always drives the europeans funs crazy.
Its more than two decades now that Band has a very concrete and stable recognition in the music market. This can be proved due to the invitations and angegements of the band in different international music festivals. It was only recently the Ngoma Africa Band performed in town and the outskirts of Tübingen , during the fastest and largest growing diaspora cultural event worldwide.
The natural dynamic music of the singers of the Ngoma Africa Band as a result of a largely a fusion and research between traditional and modern elements, creating a completely irestitible dancing groove and hypnotic sounds that makes the fans always going wild. The fans are the one who baptised the band into several names like FFU (Field Force Unit), because you are hit by a music by this force, also known as the Anunnaki aliens from special planet who appear on stage with only one job to thrill and make fans crazy!or “watoto wa mbwa ” which means the fierce puppies because when you come across there rhythm you have no choice, one way or the other you will be biten by the beat, its a metaphorical expression which means find yourself unconciously dance!
All the compositions are written by the Ngoma Africa band leader Ebrahim Makunja aka commander Ras Makunja. The Ngoma Africa has two albums and several singles that topped the East African Charts. The domination of the music through international radios and other medias its no doubt an evidence. And all Albums and singles has become favorite. Always returning to the charts. The radios playing in a compilation thread like, because all the tracks you don’t want to forget or ignore , attempt to resist no chance!.
More than 50,000,000 fans are estimated to admire the band, according to the different media sources. The band has gained the reputation the same to the cultural institution or music academy most of the musicians and dancers were once fans or those who adored the band before. For instance the youngest soloist Matondo Benda and even the drummer Jo Sousa aka surgent Major Jo Sousa,Gayle Mayimona , were once fans who always followed the band wherever performed.Ngoma Africa Band led and founded by Kamanda Ras Makunja have talented musicians like Flora William,Jessicha Ouyah,Liga Nionso,Aj Nbongo,Mo Benda,Vially Nbongo, including mult-talented Chris-B Bakotessa.
The fans emotions, feelings, happiness, tears, smiles, laughs, memories, kilometers driven travelling, new friendships, old friendships getting together and stronger. Love, affection, support, planes, airports, train stations, visiting new places are all the results and experience one makes during concerts,”All concerts were and are as special to us” insisted the fans in Tubingen!

The Band is owned by the fans, thats why its hard during concerts for the security to calm down the storm of the fans who are draging to reach to the edges and premisses of the platform or the stage.

The Ngoma Africa is the first and foremost group to built a brigde reinforced with East African danceable concrete rhythm which connects people all over the World. Thats why the Band is eager to make a World Tour. It is possible to listen the music at www.ngoma-africa.com or www.reverbnationa.com/ngomaafricaband

The Ngoma Africa Band aka FFU also known as Anunnaki alien, the most successfull African live Band based in Germany has been vastly gaining popularity through an extra ordinary rhythm “Bongo Dance” from Tanzania and Neighbouring East African countries which always drives the europeans funs crazy.
Its more than two decades now that Band has a very concrete and stable recognition in the music market. This can be proved due to the invitations and angegements of the band in different international music festivals. It was only recently the Ngoma Africa Band performed in town and the outskirts of Tübingen , during the fastest and largest growing diaspora cultural event worldwide.
The natural dynamic music of the singers of the Ngoma Africa Band as a result of a largely a fusion and research between traditional and modern elements, creating a completely irestitible dancing groove and hypnotic sounds that makes the fans always going wild. The fans are the one who baptised the band into several names like FFU (Field Force Unit), because you are hit by a music by this force, also known as the Anunnaki aliens from special planet who appear on stage with only one job to thrill and make fans crazy!or “watoto wa mbwa ” which means the fierce puppies because when you come across there rhythm you have no choice, one way or the other you will be biten by the beat, its a metaphorical expression which means find yourself unconciously dance!
All the compositions are written by the Ngoma Africa band leader Ebrahim Makunja aka commander Ras Makunja. The Ngoma Africa has two albums and several singles that topped the East African Charts. The domination of the music through international radios and other medias its no doubt an evidence. And all Albums and singles has become favorite. Always returning to the charts. The radios playing in a compilation thread like, because all the tracks you don’t want to forget or ignore , attempt to resist no chance!.
More than 50,000,000 fans are estimated to admire the band, according to the different media sources. The band has gained the reputation the same to the cultural institution or music academy most of the musicians and dancers were once fans or those who adored the band before. For instance the youngest soloist Matondo Benda and even the drummer Jo Sousa aka surgent Major Jo Sousa,Gayle Mayimona , were once fans who always followed the band wherever performed.Ngoma Africa Band led and founded by Kamanda Ras Makunja have talented musicians like Flora William,Jessicha Ouyah,Liga Nionso,Aj Nbongo,Mo Benda,Vially Nbongo, including mult-talented Chris-B Bakotessa.
The fans emotions, feelings, happiness, tears, smiles, laughs, memories, kilometers driven travelling, new friendships, old friendships getting together and stronger. Love, affection, support, planes, airports, train stations, visiting new places are all the results and experience one makes during concerts,”All concerts were and are as special to us” insisted the fans in Tubingen!

The Band is owned by the fans, thats why its hard during concerts for the security to calm down the storm of the fans who are draging to reach to the edges and premisses of the platform or the stage.

The Ngoma Africa is the first and foremost group to built a brigde reinforced with East African danceable concrete rhythm which connects people all over the World. Thats why the Band is eager to make a World Tour. It is possible to listen the music at www.ngoma-africa.com or www.reverbnationa.com/ngomaafricaband

PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya Premier Bet imezindua mchezo mpya wa Football Jackpot utakaowapa fursa wateja wa kampuni hiyo kujinyakulia kitita kikubwa cha fedha cha Shillingi Milioni 15.5 za Kitanzania.

Jackpot hiyo iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Premier Bet, Samir Matar utakuwa mchezo wa kwanza wa Jackpot wenye kima kidogo katika michezo ya kubashiri nchini. Akizungumza na waandishi wa habari, Matar amesema kuwa Jackpot hiyo itakayohusisha mechi 12 za ligi mbalimbali droo yake itakuwa inachezwa kila siku ya Jumatano saa 3.55 usiku na Jumamosi saa 10.55 jioni. 

Ameeleza kuwa, wateja watatakiwa kubashiri mechi 12 zitakazokuwa zimeorodheshwa kwa mawakala wote nchini na atafanikiwa kushinda kitita hicho cha Milioni 15.5 na ikitokea mteja akabashiri mechi 10 au 11 atapatiwa fedha kulingana na ubashiri wake. 

Meneja Rasilimali watu na Utawala Amanda Kombe amesema kuwa lengo la kuanzisha Jackpot hii ni kwa ajili ya kukuza burudani ya soka kwa wateja wa Premier Football Betting ili kuwapa fursa ya kushinda kitita kikubwa cha fedha kwa kutoa hela kidogo. Amanda amesema, kama ikitokea katika siku ambayo Jackpot imechezeshwa mshinda wa Milioni 15 hajapatikana hivyo inapelekea kuongezeka kwa kiwango cha fedha.

Kwa sasa Premier Bet ina jumla ya mawakala 2000 nchini kote na ratiba za mechi zitakazokuwa zinashindanishwa zitakuwa zinapatikana kwa mawakala hao na mteja anaweza kucheza kadri ya uwezo wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Premier Bet, Samir Matar (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Football Jackpot   utakaowapa fursa wateja wa kampuni hiyo kujinyakulia kitita kikubwa cha fedha cha Shillingi Milioni 15.5 za Kitanzania.
Meneja Rasilimali watu na Utawala Amanda Kombe akiwaonyesha waandishi wa Habari aina ya tiketi ya michezo ya kubashiri ya Premier Bet wakati wa uzinduzi wa Jackpot ya Premier Bet Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Premier Bet wakionyesha namna ya kutoa risiti katika mashine kwa Mkurugenzi Mtendaji Samir Matar ( picha ya juu)  pia wakitoa tiketi kwa waandishi wa habari waliofika katika uzinduzi huo.

JK amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI

$
0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya tarehe 14, Agosti 2018 amemtembelea na kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa katika wodi maalum kitengo cha Taasisi ya mifupa MOI,  hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Kikwete kumtembelea Dk Kigwangalla ambapo awali alimtembelea Agosti 8,  alipokuwa amelazwa Wodi ya Mwaisela akipatiwa Matibabu ya awali.

Kikwete amemtakia kila lakheri katika kipindi hiki kwa kuuguza majeraha ya mkono na sehemu za mwili ikiwemo mbavu ambazo kwa sasa hali yake inaendelea kuimarika kwa majibu wa Madaktari wa kitengo hicho cha mifupa MOI.

Awali tokea kufanyiwa operesheni ya mkono ameweza kufanya mazoezi taratibu ikiwemo kutembea mwenyewe katika viunga hivyo vya Muhimbili.

Dkt. Kigwangalla alipata ajali ya gari mnamo Agosti 4, 2018 huko Manyara akiwa katika ziara ya kikazi ambapo katika ajali hiyo iliyokuwa na watu 6, watano walijeruhiwa na mmoja alifariki dunia ambaye alikuwa afisa habari mwandamizi wa Wizara hiyo, Hamza Temba.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI anapopatiwa matibabu. Kulia ni Mke wa Waziri Dk Kigwangalla, Dkt. Bayoum Awadhi Kigwangalla.

TCU imefunga dirisha la awamu ya kwanza

$
0
0
Katibu mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Prof Cherles Kihampa akizungumza na waadishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ya kujiunga na masomo katika vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini, alisema Agost 15 mwaka huu itakuwa siku ya mwisho kutuma maombi hayo.
Na Chalila , Kibuda,Globu ya Jamii.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunga dirisha la awamu ya kwanza la maombi ya kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu hapa nchini.

Akizungumza na wanahabari makao makuu ya Tume hiyo jijini Dar es salaam, Prof. Charles Kihampa amesema kwamba dirisha hilo linafungwa leo Agost 15, na kufunguliwa kwa awamu ya pili septemba 3 mwaka huu.

Aidha Prof.Kahampa amewasisitiza waombaji wasome mwongozo wa programu zilizoidhinishwa kudahili pamoja na vigezo vya udahili vinavyotakiwa kwa kila programu ya masomo kabla ya kuanza kutuma maombi yoyote ya udahili.

Ikumbukwe kuwa dirisha la maombi ya elimu ya juu lilifunguliwa rasmi kwa awamu ya kwanza Julai 20, 2018.

CRDB BANK YAWAPIGA MSASA WA MWISHO WAJASIRIAMALI WANAWAKE WAFUGA KUKU

$
0
0

Meneja Mwandamizi Dawati la Akinamama wa CRDBBank, Rehema Shambwe (kulia), akielezea sera za benki hiyo, kwa Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakati wa siku ya ufungaji wa semina yao, ya siku mbili inayokuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa Flex Gardern. Semina hiyo, imefungwa na Mbunge wa jimbo hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega. CRDB Bank imedhamini semina hiyo.
Baadhi ya Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, wakimsikiliza Meneja Mwandamizi Dawati la Akinamama, Rehema Shambwe, alipokuwa akizungumza nao kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo, kwa wateja wake.
Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam, Midlaster Nsanzugwanko, akizungumza na Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga katika siku ya mwisho ya semina hiyo, kuhusu kutoa mikopo mbalimbali ya kuwawezesha kufikia malengo yao, ya kuwa wafugaji wa kutegemewa na taifa.
Mwakilishi wa Taasisi za US CEVA Animal Health na US Grains Ancil Tanzania, Dk. Peter Makang'a, akitoa elimu kuhusu ufugaji bora na vyakula gani na vyenye virutubisho gani vinafaa kwa ufugaji kuku. Pia aina za dawa zinazofaa kutumiwa kwa mifugo katika kuwafanya kutopata maradhi ya kuambukiza.
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya uuzaji wa vyakula na dawa za mifugo ya Farmers Centre, Muhsin Awadhi, akitoa maelezo ya dawa mbalimbali za mifugo kwa wanasemina, Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, waliofika kwenye banda lao katika siku ya ufungaji wa semina yao hiyo. Kampuni hiyo, ni moja wa wadhamini wa semina hiyo.
Baadhi ya Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, wakiwa kwenye banda la CRDB Bank kupata huduma mbalimbali, zikiwemo za kujiunga na benki hiyo.
Wanasemina Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, wakicheza kwa furaha wakati wakitoka kumpokea mgeni rasmi katika ufunguji wa semina yao, Mbunge wa jimbo hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega.
Mgeni rasmi katika ufungaji wa semina hiyo, Mbunge wa Mkuranga, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akipongezwa kwa kupeana mikono na wanasemina hao, Wajasiriamali wanawake wafuga kuku.
Mgeni rasmi, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akizungumza na Wanasemina Wajasiriamali wanawake wafuga kuku, wakati akiifunga semina yao hiyo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega, wa tatu ni Makamu Mwenyekiti wa Jikwaa, Christina Mrema na kushoto ni Mhazini wa Jukwaa, Shufaa Msangi.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wao, Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, jijini Dar es Salaam, Midlaster Nsanzugwanko.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega (katikati), akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Juma Abeid (kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wake Afisa Maendeleo ya Jamii, Mkuranga, Safina Msemo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wao, Mwakilishi wa Benki ya NMB, Mkuranga, Halima Nkya.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akiwaeleza jambo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega (katikati) na Makamu wake, Christina Mrema.

Athari zinazoweza kukukumba kwa kusitisha huduma ya malazi hotelini

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania


Ushawahi kukumbana na kadhia ya kunyimwa huduma ya malazi? Au kulipishwa kwa kutozingatia masharti ya hoteli kuhusu huduma zao?

Wasafiri wengi siku hizi hufanya maandalizi ya mapema pindi wanapotaka kusafiri. Lengo la kufanya hivi linaweza kuwa kupata bei nzuri zaidi au kuepuka usumbufu wa maandalizi ya dakika za mwisho. Lakini kwa baadhi yetu, kufanya maandalizi ya namna hiyo huona kama ni kujisumbua tu kwa sababu kuna uwezekano wa kuahirisha safari yenyewe.

Unaweza kuona kuwa ni jambo la kawaida wewe kama mteja kuamua kuahirisha safari yako na kuwaambia hoteli wasitishe huduma ya malazi uliyoweka. Lakini kuna masuala muhimu ya kuzingatia kuhusu sera zinazowekwa na hoteli hususani katika kusitisha huduma ya chumba ambayo Jumia Travel ingependa kukupatia ufahamu. 

Kuna umuhimu kwa wasafiri kuzifahamu sera za hoteli husika ukizingatia kumekuwa na mitandao mingi iliyoibuka kwa kasi katika utoaji wa huduma za malazi. Ushauri wa kwanza, msafiri anashauriwa pindi anapofikiria kusitisha huduma ya chumba hotelini aliyoifanya ni kujaribu kusoma kwa makini sera za hoteli ili kufahamu kwamba hatohitajika kulipia gharama zaidi pale atakapoamua kusitisha huduma.



Mambo muhimu ya kuzingatia

Endapo utakuwa umefanya huduma ya malazi ya chumba hotelini moja kwa moja utakuwa na faida mbili:

Kwanza, kama umeenda hotelini moja kwa moja na kufanya huduma kwa utaratibu uliozoeleka unaweza kuwa na faida ya kusitisha huduma yako hata masaa 24 kabla ya kuripoti. Utaratibu huu unaweza kukupa faida ya kurudishiwa takribani pesa zako zote kama ulishalipa au hautokatwa chochote kama hautokuwa umelipa. Mara nyingi njia hii ni rahisi na huwa haina matatizo.

Pili, kama utakuwa umefanya huduma ya malazi ya kabla basi ujue suala la kusitisha huduma kwako litakuwa ni changamoto kwako. Hii ni kutokana na sababu ya kwamba kwa mtazamo wa hoteli, utakuwa umepewa ofa ya bei nzuri tofauti na wengine na hawatokuwa tayari kukuachia uende kirahisi. Ukiachana na kufanya huduma ya malazi moja kwa moja hotelini, siku hizi kuna njia za kufanya huduma kupitia mitandao mbalimbali.

Mfumo wa kufanya huduma za malazi kwa njia ya mtandao unakupatia fursa ya kuperuzi na kulinganisha huduma za hoteli mbalimbali kwa urahisi na wakati mmoja. Faida ya kutumia mitandao kama hii ni kwamba mingi miongoni mwao huonyesha sera za hoteli katika kusitisha huduma ya malazi uliyoifanya.

Hata hivyo, unatakiwa makini na mitandao ambayo inakuonyesha kwamba hoteli husika ina sera ya kutodai malipo yoyote kwa kusitisha huduma. Kipengele hiki kinaweza kuwa na maana mbili kama ifuatavyo:

Kwanza, inaweza kuwa hautodaiwa malipo ya kusitisha huduma ya malazi kwa muda fulani kabla ya kwenda hotelini. Inaweza kuonekana kama sera nzuri kwako, lakini unapaswa kutazama sera hiyo inamaanisha kusitisha huduma kabla ya muda gani kwa sababu inaweza kuwa hata mwezi mmoja kabla ya kuripoti hotelini. Ukizingatia kwamba katika hoteli nyingi sera zao huruhusu kusitisha huduma hata kabla ya masaa 24 kabla ya kuripoti.
Pili, sera ya kutodaiwa kulipa gharama yoyote inaweza kumaanisha kuwa mtandao ambao unautumia hautozi gharama yoyote pindi unapositisha huduma ya malazi lakini hoteli hufanya hivyo. Katika mazingira kama haya msafiri unashauriwa kuwasiliana moja kwa moja na mtandao kama wana huduma kwa wateja au hoteli ili kupata ufafanuzi zaidi.

Hivyo basi kama msafiri masuala ya kusitisha huduma ya malazi hotelini yapo na kuna wakati mwingine hayazuiliki kutokana na changamoto mbalimbali. Jumia Travel inakushauri kuwa makini unapokuwa unafanya huduma za malazi ili kuepukana na changamoto kama hii ambayo inaweza kukupoteza muda, gharama na kukuletea usumbufu.

KENYA YAZUIA UINGIZAJI WA VIGAE, HALI INAYOSABABISHA HASARA KWA WAWEKEZAJI KUTOKA TANZANIA

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

KIWANDA cha Goodwill Tanzania Ceramic co.ltd kilichopo Mkiu ,Mkuranga Mkoani Pwani, kinachozalisha vigae kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa soko baada ya nchi ya Kenya kuzuia uingizwaji wa bidhaa hiyo. Hatua hiyo iliyochukua nchi hiyo inasababisha shehena kubwa ya vigae kurundikana kwenye magodauni na kupata hasara.

Meneja uajiri katika kiwanda hicho ,Msafiri Figa aliyasema hayo wakati kamati ya siasa mkoa, ilipokwenda kutembelea kuona shughuli za uzalishaji kiwandani hapo. Alisema ,walikuwa wakitegemea soko la Kenya zaidi kutokana na kupata oda nyingi kutoka kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo . Figa alisema ,kipindi kiwanda kinaanza lengo lao ilikuwa kuzalishaji mita za mraba 80,000 sawa na vigae 800,000 kwa siku lakini kwa sasa tangu waanze kuzalisha wanazalisha vigae 600,000 kwa siku.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (wa nne kulia) akiangalia kigae wakati kamati ya siasa mkoani Pwani ilipokwenda kutembelea kiwanda cha Goodwill ceramic co.ltd Mkuranga na kukuta shehena ya vigae iliyorundikana katika kiwanda katika kiwanda hicho kwa kukosa soko.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akiongea jambo na MNEC Kibaha ,Hajji Jumaa , wakati kamati ya siasa mkoani Pwani ilipokwenda kutembelea kiwanda cha Goodwill ceramic co.ltd ,Mkuranga na kukuta shehena ya vigae iliyorundikana katika kiwanda katika kiwanda hicho kwa kukosa soko.

"Kadri siku zikienda imekuwa tukizalisha mita za mraba 50,000 kutokana na tatizo soko ,tulilenga soko la ndani kwa asilimia 60-70 na soko la nje asilimia 30-40 lakini imebadilika na kuwa soko la ndani 30-40 nje ikawa asilimia 60-40 huku tukizalisha mita za mraba ya vigae 30,000-20,000 kwa siku " .

Figa alielezea, wana wafanyakazi 900 kutoka Tanzania,ajira zisizo za moja kwa moja 2,000-3,000 na wachina 60 ambao ni pamoja na wataalamu mbalimbali.Nae mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema hali iliyopo ni hatari kwani inakwenda kuuwa viwanda na kuweka hofu ya kuzima ndoto yetu.

"Mwaka mmoja na nusu uliopita eneo hili lilikuwa pori ambapo sasa kuna kiwanda kikubwa ambacho kinatengeneza ajira na kuliingizia mapato Taifa"Ndikilo alieleza ,tatizo la ukosefu wa soko sio la kubeza ,sio la masihala,hivyo amekiomba chama kisimamie hilo. Alisema ,wapo wafanyabiashara wanaagiza vigae China suala hili linakandamiza wawekezaji wa ndani .
Mfanyakazi katika kiwanda cha Goodwill ceramic co.ltd ,Mkuranga akipakia mabox ya vigae, wakati kamati ya siasa mkoani Pwani ilipokwenda kutembelea na kukuta shehena ya vigae iliyorundikana katika kiwanda katika kiwanda hicho kwa kukosa soko .

"Wapo watendaji serikalini wanaotoa vibali kwa wanyabiashara kuagiza nondo Uturuki na vigae China,Spain na wengine kuchukua chuma nje hivyo kuna kila sababu kuliangalia tatizo hilo" alisisitiza Ndikilo.Alisema, serikali inafanya kazi lakini baadhi ya watendaji wanasababisha tatizo hili kwa maslahi binafsi.

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ramadhani Maneno alisema ,wataishauri serikali kupitia wizara husika kuanza kutazama muundo wa sera ya masoko . Alisema, wataangalia namna ya kukaa na wizara ya viwanda na biashara ,wizara ya fedha kuweka masharti kwa wafanyabiashara ,"Kuwawekea masharti bila kuwaonea haya kuwa ukiwa Tanzania hakuna budi kutumia bidhaa zinazozalishwa viwanda vya ndani.

"Duniani kote ukizalisha lazima utegemee soko hivyo kama ukizalisha bila kuuza ni kazi bure kwani uzalishaji ukipungua kwa kukosa soko ajira zitapungua na kukatisha tamaa wawekezaji" alibainisha Maneno.
Shehena ya vigae iliyorundikana katika kiwanda cha vigae cha Goodwill Ceramic co.ltd ,Mkiu Mkuranga mkoani Pwani kwa kukosa soko .(picha na Mwamvua Mwinyi).

TUKEMEE MAPEPO YA MCHANA NA USIKU-RC RUVUMA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA Christine Mndeme amemtaka mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mh.Sophia Kizigo kuhakikisha anawashirikisha viongozi wa dini na wazee katika wilaya hiyo ili kuweka mambo sawia katika utendaji wa kazi za serikali.

WANANCHI WATAKIWA KIJITOKEZA KWA WINGI KATIKA UJENZI WA VIBANDA ENEO LAO LA STENDI MPYA MUGUMU MJINI

$
0
0
WANANCHI wilayani Serengeti mkoani Mara wametakiwa kijitokeza kwa wingi katika ujenzi wa  vibanda eneo la ujenzi wa Stendi mpya inayojengwa eneo la Stendi Kuu Mjini Mugumu baada ya stendi iliyokuwaikitumika kuwa finyu na miundombinu kuwa mibovu.

Ambapo hali hiyo  kusababisha mabasi makubwa kupaki nje ya stendi hiyo kinyume cha sheria.Hayo yamesemwa leo  na Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara Juma Porini  katika baraza la madiwani la mwaka.Amesema  kuwa mwitikio wa wananchi katika ujenzi wa vibanda hivyo umekuwa mdogo baada ya kutangaziwa mpaka sasa.

Hivyo Mwenyekiti ametumia fursa hiyo kuwatangazia tena wananchi kujitokeza kwa wingi kwani muda ambao ulitolewa kwa ajili ya kukamiliasha maombi umeisha.Lakini amesema  wameamua kuongeza muda kwa lengo la wananchi kijitokeza kwa wingi.“Mwitikio wa wananchi katika ujenzi wa vibanda hivi umekuwa mdogo licha ya kuwatangazia na bei ni nafuu kuchukua fomu ni Sh.50,000 tu, na akishajenga kibanda hicho atakitumia kwa muda wa miaka mitano.

"Katika kipindi hicho  akatakuwa anakitumia kwa kulipa 20,000 tu na baada ya miaka mitano kibanda kitarudishwa na ataanza kukitumia kwa kupangisha kulingana na mikataba itakavyosema” amesema Mwenyekiti.Aidha Mbunge wa Jimbo la Serengeti mkoani Mara Samson Ryoba(Chadema) anasema kuwa wanaendelea kujenga Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti bila kujali itikadi za vyama kwa lengo la kuletea wananchi Maendeleo.

Huku Katibu wa Madiwani Chadema Samson Wambura akitoa mapendekezo ya Chama hicho likiwemo suala la uboreshaji wa masoko katika Mjini Mugumu.Aidha Mkurugenzi wa Halmashaurti Juma Hamsini amesema kuwa tayari Halmashauri hiyo imeishaagiza taa za kufunga katika baadhi ya masoko ya jioni ili kuongeza ulinzi wa mali za wananchi.Pia ameahidi  kuendelea kutafuta wadau kwa lengo la kufunga taa za barabarani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Juma Porini akisisitiza suala la wananchi kujitokeza kwa lengo la ujenzi wa vinanda eneo la Stendi Kuu ambapo kunajengwa stendi mpya ya Magari.
Madwani WilayaniSerengeti Mkoani Mara wakiwa katika baraza la Mwaka.
Mbunge wa Jimbo la Serengeti CHADEMA Samson Ryoba akisisitiza suala la Ushirikiano baina ya Madiwani wote bila kujali itikadi za vyka kwa lengo la kuletea wananchi Maendeleo.
Katibu wa Madiwani wanaoyokana na CHADEMA Wilaya ya Serengeti Samson Wambura akisoma hoja pendekezi za kamati ya chama hicho likiwemo suala la kuboresha Masoko katika Mji wa Mugumu.
Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya ya Serengeti Juma Hamsini akifafanua jambo kwa madiwani hao na kueleza jitiada za Halamashauri hiyo likiwemo suala la ununuzi wa taa za barabarani pamoja na Masoko ya jioni.

BRANCH YAADHIMISHA MWAKA MMOJA NCHINI, AGUSIA MALENGO YA KUANZISHWA KWAKE

$
0
0

Na Khadija Seif , globu ya jamii.

KAMPUNI ya kidigital ya huduma za kifedha (Branch) imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuanza kwake.

Ambapo imejikita katika sekta ya teknolojia-fedha kwa kutangaza kujiunga na mfumo wa huduma mpya na Airtel jijini Dar es salam.

Mwanzilishi wa Kampuni hiyo Branch, Ofisa Mtendaji Mkuu Matthew Flannery ameeleza dhumuni la kuanzishwa kwa Kampuni hiyo ni kutokana na uhitaji mkubwa wa kifedha ili kuendeshea biashara mbalimbali kwa wateja ambao wanakosa mikopo ya kufanikisha mahitaji yao, hivyo basi huduma hiyo itawapa fursa za kupata fedha haraka zaidi.

Flannery amesema zaidi ya asilimia 75 ya wateja wanatumia mikopo ya Branch kuwasaidia kuanzisha na kukuza biashara zao au kutimiza mahitaji mengine ya kifedha. 

Akizungumzaa na wanahabari Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Afrika Masharki Dan Karuga amefafanua kuwa Branch ni kampuni ya kipekee inayotoa huduma vyenye viwango vya hali ya juu katika huduma za kifedha,kupitia mpango wao wa kutoa mikopo hususani kwa makundi ya watu wasiofikiwa kiurahisi.

Na kufanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wateja mbalimbali nchini kote. Karuga ameeleza lengo la huduma hiyo ni kutoa fursa kwa wananchi kupata mikopo haraka kupitia simu za mikononi ,na watumiaji wanaweza kutumia smartphone zenye uwezo wa Internet kujipatia mkopo kuanzia Sh. 50,000 hadi Sh.100,000.

" Inachukua sekunde chache kutoka kutuma maombi hadi kukubaliwa kwa ombi la mkopo,pia haihitaji kuonana ana kwa ana na mtoa huduma kwa njia ya vikao."Utaratibu mrefu wenye sura simu,dhamana ya kujaza fomu za karatasi. Pia tangu ianze huduma zake Tanzania,Branch imekwishatoa mikopo ya zaidi ya Sh.billioni 12 na mikopo zaidi ya 400,000,"amesema Karuga

Amesema kuwa Branch international, inatarajia kutoa mikopo ya Sh. Billioni 570 na kutoa mikopo mipya zaidi ya laki tano amesema Karuga.

Nae mmoja wa watumiaji wa hudumu ya Branch, Mtangazaji mahiri wa Radio ya EFM Dina Marios alikiri wazi urahisi wa kuitumia huduma hiyo popote na kwa wakati wowote ule kujipatia mkopo ambao unaweza ukatumia kuanzisha biashara yako.

Hivyo amewahimiza Watanzania kujitokeza kutumia huduma hiyo ili kujiongezea kipato kwa namna moja ama nyingine na hatimae kujikwamua kiuchumi.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Branch Afrika Masharki, Dan Karuga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar kuhusu kampuni hiyo kuadhimisha mwaka mmoja na mikakati yake mbalimbali ikiwemo na kujitanua kibiashara zaidi nchini Tanzania
Pichani kushoto ni Mwanzilishi wa Kampuni Branch, Ofisa Mtendaji Mkuu Matthew Flannery akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar kuhusu kampuni hiyo kuadhmisha mwaka mmoja ,dhumuni la kuanzishwa kwa Kampuni hiyo hasa kwa nchini Tanzania pamoja na mikakati mingine ya kujitanua zaidi kibiashara
Mmoja wa watumiaji wa hudumu ya Branch, Mtangazaji mahiri wa Radio ya EFM Dina Marios akitoa ushuhuda mbele ya Waandishi wa Habari,namna kampuni hiyo inavyoweza kuwanufaisha Watanzania,kupitia mikopo inayotelewa iliyo na masharti nafuu kabisa.
Baadhi ya Wanahabari wakifutilia yaliyokuwa yakijir ukumbini humo

MAKAMU WA RAIS KUMUWAKILISHA RAIS KATIKA MKUTANO WA SADC NCHINI NAMIBIA

$
0
0




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kuelekea Windhoek, Namibia kushiriki kwenye Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (38th Ordinary Summit of SADC Heads of State and Government) unaotarajiwa kufanyika tarehe 17 na 18 Agosti, mwaka huu akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 

Mkutano huo utakaofanyika chini ya Uenyekiti wa Namibia, utatanguliwa na Mikutano mingine mitatu ambayo ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Organ Troika, Mkutano wa Baraza la Mawaziri na Mkutano wa Makatibu Wakuu. Aidha, Mkutano huo utapokea na kujadili agenda mbalimbali ikiwemo Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC, Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama, taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ, taarifa ya Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, hali ya kiuchumi katika kanda ya SADC na taarifa kuhusu utekelezaji wa Kaulimbiu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa mwaka 2017.

Vilevile, Mkutano utapokea Kaulimbiu ya Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali na kupokea taarifa ya hali ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa SADC. Katika Mkutano huo, Tanzania inategemea kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha Agosti 2018 hadi Agosti 2019.

Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
15/8/2018

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI WA MWANZA NA PWANI

IGP APONGEZA UTULIVU CHAGUZI NDOGO.

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro

Na Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limewahakikishia wananchi kuendelea kuwepo kwa hali ya usalama na Amani hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa hali ya utulivu na usalama katika chaguzi ndogo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro wakati akiwa katika ziara katika Shule ya Polisi Moshi (CCP) ambapo aliweza kuzungumza na Wakufunzi na Askari waliopo mafunzoni Chuoni hapo ikiwa na lengo la kukagua mwenendo wa mafunzo yanayoendelea katika Vyuo vya Polisi nchini.

IGP Sirro amesema katika maeneo yaliyofanya uchaguzi mdogo hali ilikuwa shwari licha ya kuwepo kwa matukio madogo ambayo yanaendelea kushungulikiwa na upelelezi utakapokamilika majalada yao yatapelekwa kwa Waendesha mashtaka kwa hatua zaidi.

“ Hali iliuwa shwari na ni wazi kuwa wananchi sasa wameelewa umuhimu wa kutii sheria bila ya kushurutishwa na natoa rai waendelee kudumisha hali hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za Wahalifu na uhalifu katika maeneo yao” Alisema Sirro.

Katika hatua nyingine akiwa Shule ya Polisi Moshi zamani CCP IGP Sirro alitoa pongezi zake kwa Walimu na Uongozi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwapika Askari hususani katika mafunzo yao ya awali ambapo ametaka kila Askari kutambua wajibu wake

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Mungi amesema Chuo hicho kinaendelea kutoa mafunzo kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa kila Askari anayetoka anakuwa na ukakamavu wa kutosha na nidhamu ya kuwahudumia Wananchi licha ya kuwepo kwa Changamoto za madeni ya maji na umeme.

Alisema wanaendelea kuboresha miundombinu ya Chuo hicho kwa kutumia miradi iliyopo ili kukiweka katika hali ya usalama zaidi ikiwemo kujenga uzio imara kuzunguka maeneo hayo

Tanzeela Qambrani: Mwanamke mwenye asili ya Tanzania ateuliwa mbunge Pakistan na kuweka historia

$
0
0
Mwanamke mwenye asili ya Tanzania amekuwa wa kwanza wa asili ya Afrika kuteuliwa kuwa mbunge nchini Pakistan, na kutoa matumaini kwa watu wa jamii ndogo na maskini nchini humo yenye asili yake Afrika.

Tanzeela Qambrani, 39, aliteuliwa na chama cha Pakistan People's Party (PPP), cha waziri wa zamani Benazir Bhutto kuhudumu katika kiti kilichotengewa wanawake kwenye bunge la mkoa wa Sindh kusini mwa India.

Ana matumaini kuwa uteuzi wake baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita utasaidia kuondoa unyanyapaa ambao umekuwepo dhidi ya jamii ya Sidi, jina wanaloitwa watu wa asili ya Afrika wanaoishi maeneo ya pwani ya Makran na Sindh nchini Pakistan.

"Kama jamii ndogo iliyopotelea kwenye jamii kubwa za wenyeji, tumekuwa na wakati mgumu kudumisha mizizi yetu ya Afrika na tamaduni, lakini ningependa kuona kuwa jina Sidi linakuwa lenye heshima," Bi Qambrani ambaye mababu zake walitokea Tanzania aliiambia BBC.

Mwanamke huyo aliapishwa Jumatatu wiki hii na amenukiliwa na mtandao wa The News International akisema kwamba alijihisi kama Nelson Mandela.
Alivalia mavazi ya kitamaduni ya Kiafrika wakati wa kuapishwa kwake.

Balozi Dkt. Abdallah Possi atoa wito kwa wawekezaji kuja Tanzania

$
0
0
Ilikuwa katika viwanja vya maonyesho ya International Afrika Festival Tübingen nchini ujerumani ambapo katika maonyesho hayo mwaka huu 2018 nchi lengwa ilikuwa ni Tanzania na mgeni wa heshima rasmi alikuwa balozi wa Tanzania nchini ujerumani mheshimiwa dkt. Abdallah Possi ambaye alihutubia ummati wa kadamnasi ya waudhuriaji wakiwemo wawekezaji kuwa Tanzania kuna fursa kubwa za uwekezaji na pia nchi salama.

onyesho hilo kubwa lilinogeshwa na bendi za muziki kama Ngoma Africa band maarufu FFU-Ughaibuni inayoongozwa na kamanda Ras Makunja,bendi ya Mvula-Mandondo Band inayoongozwa na msanii Saidi Kanda yenye maskani kule Uingereza nayo ilifanya vizuri,wasanii wa kizazi kipya kama Nashi MC kutoka Tanzania naye alitingisha jukwaa msanii wa picha za kuchora Chilonga Haji naye alikuwa moja ya waonyeshaji wa bidhaa toka Tanzania.onyesho lilifana sana sana na kuitanga za Tanzania kimataifa.
Balozi wa Tanzania nchini Ujermani Mhe. Dk. Abdallah Possi akiwa na wawekezaji wakiangalia naadhi ya bidhaa katika maonyesho mjini Tubingen,Ujerumani.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dk. Abbdalaah Possi akiwa katika maonyesho ya Gaiexpo mjini Tubingen,mwaka huu nchi lengwa ilikuwa Tanzania.
Ngoma Africa Band wakiwa jukwaani katika onyesho la Tubingen.

BADO TUNAHITAJI WAWEKEZAJI KWENYE SUKARI-MAJALIWA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Mauritus nchini mwenye makazi yake, Maputo nchini Msumbiji, Jean Pierre Jhumun, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Agiosti 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Mauritius nchini mwenye makazi yake Maputo nchini Msumbiji, Jean Pierre Jhumun (wapili kushoto) Balozi wa Heshima wa Mauritius nchini, Kazim Rizvi (kulia), Mwenyekiti wa Mfuko wa Uwekezaji Sukari nchini Mauritius, Gansam Boodram (wapili kulia) na kushoto ni Mwenyeji wa ujumbe huo katika jiji la Dodoma, Kapteni Mstaafu John Chiligati.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Mauritius nchini mwenye makazi yake Maputo nchini Msumbiji, Jean Pierre Jhumun (wapili kulia) na ujumbe wake, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma Agosti 15, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Heshima wa Mauritius nchini, Kazim Rizvi, Mwenyekiti wa Mfuko wa Uwekezaji Sukari nchini Mauritius, Gansam Boodram na watatu kushoto ni Mwenyeji wa ujumbe huo katika jiji la Dodoma, Kapteni Mstaafu John Chiligati. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania bado inawahitaji wawekezaji zaidi katika sekta ya uzalishaji wa sukari ili iweze kukidhi mahitaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Mauritius nchini Tanzaniamwenye makazi yake Maputo nchini Msumbiji, Mheshimiwa Jean Pierre Jhumun, ofisini kwake jijini Dodoma.

“Mwaka jana nilikiwa nchini Mauritius nilihudhuria Jukwaa la Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Tanzania na Mauritius, ambapo nilipata fursa ya kuwashawishi wawekezaji wa Mauritius waje kuwekeza kwenye viwanda vya sukari nchini,”.

Ameongeza kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya maeneo ya uzalishaji wa sukari ambayo bado hayajaendelezwa, hivyo kama kuna wawekezaji walio tayari na wamekidhi vigezo waendelee na hatua za uzalishaji.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa mbali na kuhitaji wawekezaji kwenye sekta ya sukari, pia amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Mauritius kuja kuwekeza kwenye sekta ya uvuvi. “Mnaweza kuja kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji wa samaki kwani tuna bahari, mito na maziwa yenye samaki wa aina mbalimbali,”

Kwa upande wake, Balozi Jhumun amesema wawekezaji wa Mauritius wapo tayari kuwekeza katika uzalishaji wa sukari pamoja na uvuvi na wameshafanya utafiti katika baadhi ya maeneo. Balozi Jhumun amesema ameambatana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Uwekezaji wa Sukari, Bw. Gansam Boodram kutoka nchini Mauritius kwa ajili ya kufuatilia maeneo ya uwekezaji.

“Tumeitikia wito wa Rais Dkt. John Magufuli wa kututaka kusaidia katika upatikanaji wa wawekezaji watakaokuja Tanzania kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji wa sukari,”.

Naye Bw. Boodram amesema tayari wameshatembelea baadhi ya maeneo wanayohitahi kwa ajili ya uwekezaji na wameshafanya utafiti wa udongo pamoja na masoko. Maeneo waliyoyafanyia utafiti ni Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma pamoja na Rufiji mkoani Pwani.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 15, 2018.
Viewing all 46338 articles
Browse latest View live




Latest Images