Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1645 | 1646 | (Page 1647) | 1648 | 1649 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  SHULE ya sekondari ya Seminari ya Kiislamu Al Muntazir kwa mara nyingine tena wamewakutanisha wanafunzi wa shule za Sekondari nchini na nje ya nchi kwa lengo la kufanya mashindano ya kujadili mada mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

  Mjadala huo umepewa jina la "Mwalimu Nyerere Schools Invitational Debate Championships" ili kuwajenga na kuwaandaa wanafunzi hao kuwa wataalamu na wajuzi kwa miaka ijayo.Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa shule ya Al Muntazir Reuben Kimani ameeleza kuwa mashindano hayo kwa shule za Sekondari na hiyo ni mara ya tatu yamefanyika yakihusisha washiriki zaidi ya 200.

  Na hiyo ni kwa lengo la kuwafanya wawe na fikra pana kwa elimu ya chuo watakayoendelea nayo, ambapo ameeleza kuna shule kutoka Zimbabwe na Kenya na wenyeji Tanzania wakiwakilishwa na shule za Tusiime, Shaaban Robert, shule ya wavulana na wasichana Feza, Aghakan na wenyeji Al Muntazir.

  Aidha ameeleza kuwa mashindano hayo yatachukua siku 3 wale watakaofanya vizuri watatunukiwa vyeti na watashiriki mdahalo mkubwa utakaofanyika Desemba mwaka huu nchini Botswana. Kuhusiana na maandalizi kwa wanafunzi wao Kimani ameeleza kuwa wametoa mafunzo kwa wiki mbili yakihusisha utafiti hivyo hawana shida kwa shindano hilo na amewataka wanafunzi kuja kujishiriki kwa kutazama na kupata uzoefu kutoka kwa wanafunzi kutoka barani Afrika.

  Kwa upande wa washiriki kutoka Al Muntazir Seminari Saloha Aboud wa kidato cha nne ameeleza kuwa wamejipanga kwa ajili ya mashindano licha ya kuonekana kwa magumu ila wamejipanga na watakuwa washindi.

  Wameeleza kuwa waliwakilisha nchi mwaka huu katika mashindano ya kuzungumza yaliyofanyika mwezi June nchini Croatia na licha ya kutokuwa washindi ila walipata kitu cha kujifunza na wameeleza changamoto wanazokumbana nazo ni uwelewekaji wa mada hasa kwa wanafunzi wa sayansi kukutana na mada zilizo nje ya uga wao kama uchumi na sanaa.

  Naye Mlezi na mwalimu wa somo la Kiingereza katika shule ya Al Muntazir bi. Getrude Mtenga amesema kuwa uzoefu walioupata katika mashindano ya kuzungumza nchini Croatia utawasaidia katika kupata ushindi mwaka huu, maandalizi waliyoyafanya kwa muda mrefu utawasaidia sana na amewashauri wanafunzi kushiriki katika midahalo hiyo na walimu kuanzisha vyama vya midahalo shuleni ili kuwajenga wanafunzi na hiyo itawasaidia wanafunzi kujijenga, kujiamini, kupanga hoja na kuchanganua masuala ya kiulimwengu.  Mwalimu na mlezi wa klabu ya Lugha ya kiingereza kutoka Al Muntazir Seminari Bi. Getrude Mtenga akieleza namna shule yao ilivyojipanga katika kukabiliana na mashindano hayo.
  Mkuu wa shule ya Sekondari ya Seminari ya Al Muntazir, Reuben Kimani akitoa neno kwa washiriki kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
  Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mdahalo huo kutoka shule za sekondari nchini.
  Wanafunzi kutoka Zimbabwe (wenye suti za bluu) wakisikiliza mjadala uliokuwa unaendelea.

  0 0

  Na Said Mwishehe

  SITAKI kuamini hiki...yaani hata Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe naye ameamua kuhamia CCM.

  Ni nini kimetokea kwa Mbowe?Hivi kweli ameamua kwa ridhaa yake kujiunga CCM? Amenunuliwa?Ujue unaposikia Mbowe naye ameamua kujiunga CCM lazima kuna maswali ya msingi ambayo utajiuliza tu.

  Au Mbowe ameamua kuondoka Chadema kutokana na kulalamikiwa na baadhi ya wabunge wa chama hicho kuwa anaendesha chama kwa maamuzi yake.Hili sidhani.Haiwezi kuwasababu ya kumfanya Mbowe kujiunga na CCM.

  Au ameamua kuondoka Chadema na kuachana na nafasi zake zote alizonazo kwasababu tu ya kuchoshwa na tuhuma ambazo zinaelekezwa kwake kila kukicha na wale wanaohama kuwa hataki kuachia Uenyekiti kwa wengine.Hata hivyo kwa kuwa Mbowe yupo nitaelewa tu sababu zilizomfanya naye aondoke Chadema na kwenda kujiunga na CCM.

  Hata hivyo wakati hayo yakiendelea nikawa natafakari hivi ni kweli Mbowe hizi habari za kwamba ameondoka Chadema na kujiunga na CCM.Binafsi sawa nilishangaa kusikia Mbowe kaondoka Chadema lakini kwa hali ya kisiasa nchini inavyoendelea nikaona huenda anaweza kuwa na uamuzi huo na ni haki yake kimsingi.

  Wakati bado naendelea kutafakari sababu za Mbowe kuondoka Chadema ...napigiwa simu na marafiki zangu wengine wakiniambia Mbowe ameitisha mkutano anazungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake.Habari za Mbowe kuamua kuitisha mkutano zikaanza kunipa picha na kuanza kuamini huenda ikawa kweli.

  Nikaona isiwe tabu acha niende nikamsikilize angalau niwe na cha kuwaambia watanzania kupitia chombo changu cha habari ninachofanyia kazi.Nikauliza muda wa mkutano nikaambiwa. Sikutaka kupoteza muda nikachukua 'not book' yangu na kalamu na kwa kuhakikisha napata tukio vizuri nikabeba na kamera kwa ajili ya picha.

  Nikaingia kwenye daladala huyo hadi nyumbani kwa Mbowe.Nilipofika nikakutuna na waandishi wengine wengi tena wengi kweli kuliko hata wale waliojitokeza wakati ule anazungumzia matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2015.Muda ulipowadia Mbowe akaingia eneo la mkutano.Wakati anaingia kwenye eneo la mkutano hakuwa na kiongozi yoyote maana aliingia peke yake tu.

  Hata hivyo usoni akawa anaonekana ni mwenye furaha na bashasha kama vile mtu ambaye alikuwa anahitaji jambo fulani kwa muda mrefu na hatimaye amelipata.Nikaona ngoja nikae vizuri kwanza nimsikilize Mbowe .Ni kiongozi mwenye heshima kubwa katika siasa za Tanzania.Kama kawaida yake hakutaka kupoteza muda kwani baada yakuwasalimia waandishi wa habari moja kwa moja akaanza kuzungumza.

  Mbowe hakuwa na papara wakati anazungumza .Akaanza na historia ya Chadema tangu ilipoanzishwa huku akitumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo amekipigania chama hicho.Mbowe akaelezea namna ambavyo Chadema imepita magumu mengi na namna ambavyo walifanikiwa kuyavuka.Hakusita kuzungumzia walivyopambana kuvuna makada wa CCM kwa nyakati tofauti na hasa kuelekea uchaguzi mkuu uliopita ambapo waliamua kubadili gia angani na kumchukua Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa.

  Pia akaeleza walivyomchukua pia aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu Frederick Sumaye pamoja na makada wengine kibao wa CCM akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja.Wakati Mbowe anazungumza binafsi nikawa makini kumsikiliza anataka kutuambia nini leo.Nikawaangalia waandishi wengine nao kila mmoja yupo makini kumsikiliza.

  Baada ya kukizungumzia chama chake Mbowe akaanza kuzungumzia hama hama ya wabunge wa upinzani na madiwani kwenda CCM.Hapa nikashtuka na kuanza kujiuliza anataka kueleza nini? Hata hivyo nikaona acha nijipe muda na kuongeza umakini.Mbowe hakusita kumzungumzia aliyekuwa Mbunge wa Ukonga kupitia Chadema Mwita Waitara.Akaonesha kukasirishwa na tuhuma ambazo Waitara amezitoa dhidi yake.

  Hata hivyo baada ya maelezo mengi Mbowe naye akaanza kueleza namna ambavyo kasi ya Rais inavyomsukuma naye kushirikiana naye katika kuleta maendeleo ya Watanzania.Nikaanza kujiuliza kimoyo moyo ni kweli huyu Mbowe ninayemjua leo hii naye anasifu kazi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli.

  Wakati Mbowe anaendelea kuzungumza na hasa kutokana na maendeleo akawa anatoa mifano pia ya miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa fly over pale Tazara jijini Dar es Salaam.Mbowe akaanza kuzungumzia kazi nzuri ambayo Rais ameifanya katika kukomesha rushwa, kurudisha nidhamu mahala pa kazi, kukomesha ufisadi na kuongeza ukusanyaji wa mapato.

  Waandishi kila mmoja akawa ananong'ona kwa chini chini Mbowe leo amepatwa na nini.Wakati wanajiuliza Mbowe ndipo akaomba waandishi kumsikiliza kwa umakini anachotaka kusema baada ya maelezo yote.Nakumbuka alisema hivi "Kwa ridhaa yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu nami nimeamua kujiunga CCM.Nataka kushirikiana na Serikali ya CCM kuleta maendeleo kwani Rais anafanya kazi nzuri na nijukumu la Watanzania kumuunga mkono kwa kuwa upande wake."

  Hakuishia hapo akasema anajua Waitara tayari amejiunga CCM , hivyo si dhabi naye kwenda huko huko aliko Waitara.Pia akasema anafahamu na Julius Mtatiro naye ameshakwenda CCM kwa ajili ya kushiriki kikamilifu kuleta maendeleo ya Watanzania.

  Maneno hayo ya Mbowe yakaanza kunifanya niwaze ...nikawaaaza weee.nikawaaaaza sana tu.Nikawa nawaza sasa kama Mbowe ameamua kujiunga CCM hivi waliobakia huko wanasubiri nini.Pamoja na Mbowe kutangaza kujiunga CCM bado kwangu niliendelea kuwaza .Hata hivyo wakati naendelea kutafakari siasa za upinzani nikajikuta napiga kelele kwa sauti kubwa.

  Sauti ya mshangao.Si ndio nikakurupuka.Niko wapi?Mbona siko nyumbani kwa Mbowe? Mbona huu ni usiku? Hili la Mbowe kuhama nimelitoa wapi?

  Wakati najiuliza maswali yote haya nikabaini kumbe nilikuwa naota tu.Ilikuwa ndoto, tena ni ndoto ya kipuuzi na hauna sababu ya kuiamini.Siunajua tena mambo ya ndoto.Kumbe koote huko nilikuwa naota?Usingizi baada ya kwisha kabisa na kubaki mwenye akili timamu nikajiridhisha kumbe Mbowe bado yupo Chadema.Kumbe Mbowe bado ni Mwenyekiti wa Chadema na bado mbunge wa Hai.

  Ninachojilaumu hii ndoto imenipotezea muda wangu na kusumbua tu usingizi bila sababu ya msingi.Nikiri katika kipindi hiki ambacho wanasiasa wengi wa upinzani wameamua kurudi CCM kwa ridhaa zao muda mwingi nimekuwa nikitafakari hatma ya upinzani.

  Huenda kutafakari huko kumenifanya niote hiyo ndoto ambayo kimsing ni ya kijinga.Na kwa kuwa ni ndoto achana nayo .Acha tusubiri.Wewe unakasirika kitu gani?Unaikasirikia hata ndoto ...utakuwa wa ajabu sana.

  Acha maisha yaendelee ila leo sitalala kabisa maana naweza kuota na Lowassa naye karudi CCM.

  0 0
  Baadhi ya Wakazi wa Jimbo la Buyungu waliojitokeza Kupiga Kura kumchagua Mbunge wao wakiwa kwenye mistari kuingia ndani ya Kituo cha Kupigia Kura wilayani Kakonko leo. Katika uchaguzi huo vyama 10 vya Siasa vimesimamisha wagombea.
  Karani mwongozaji wa Kituo cha kupigia Kura Na. 1 katika ukumbi wa mikutano wa wilaya ya Kakonko akitoa maelekezo kwa wapiga Kura waliojitokeza kutimiza haki yao ya kikatiba ya kumchagua Mbunge wao katika jimbo la Buyungu leo.
  Mkazi wa wilaya ya Kakonko akipiga kura yake kumchagua Mbunge wa Jimbo la Buyungu leo.
  Mkazi wa wilaya ya Kakonko akipiga kura yake kumchagua Mbunge wa Jimbo la Buyungu leo.
  Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kupigia Kura akihakiki majina ya Mpiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kabla ya kumruhusu mpiga Kura kutimiza haki yake ya kushiriki kupiga Kura katika Uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu leo.
  Mmoja wa wapiga Kura ambaye ni mzee akipata usaidizi wa kutolewa nje ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Buyungu leo.
  Mmoja wa wapiga Kura ambaye ni mzee akipata usaidizi wa kutolewa nje ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Buyungu leo.

  0 0

  *Azungumzia hali ya usalama maeneo yanayofanya uchaguzi


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikiliza mmoja wa wanachama wa Chadema kwa tuhuma za kumjeruhi kada wa CCM aliyefahamika kwa jina moja la Idd baada ya kuibuka kwa vurugu kati ya makundi mawili.

  Akizungumza na Michuzi Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhan Ng'anzi amesema tukio la vurugu hizo zimetokea leo kati ya saa nne na saa tano asubuhi eneo la Mianzini.

  Amefafanua Polisi waliwahi kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima vurugu hizo na kumkamata anayetuhumiwa kujeruhi na anahojiwa, huku aliyejeruhiwa naye amepatiwa matibabu.

  Alipoulizwa jina la anayetuhumiwa kujeruhi Kamanda Ng'anzi amejibu kwa sasa yupo nje ya ofisi yake kwa ajili ya kufuatilia na kuangalia hali ya usalama na hasa kwenye kata zinazofanya uchaguzi unafanyika unaofanyika leo.

  Hata hivyo inaelezwa kada aliyejeruhiwa ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kaloleni mkoani Arusha.

  Kuhusu hali ya usalama amesema Mkoa wa Arusha hali ni tulivu na amani imetawala katika maeneo yote yakiwamo ya kata ambazo yanafanya uchaguzi na kwamba hata vurugu ambazo zilizotokea ni kwenye kata ambayo haina uchaguzi.

  "Arusha hali ni shwari mno.Hakuna vurugu na watu wanaendelea na shughuli zao.Hata katika kata ambazo kunafanyika uchaguzi mdogo kuko shwari na mambo yanakwenda vizuri,"amesema Kamanda Ng'anzi.

  0 0

  Balozi Massuka akimkaribisha nchini Korea Bw.Adonis Bitegeko ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mwakilishi Wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA), moja ya taasisi muhimu za serikali zinazoshiriki katika ziara hiyo ya uhamasishaji viwanda nchini Korea. Anayeshuhudia ni Bw.Francis Mossongo, Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Tanzania.
  Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Dawa na Vifaa Tiba Nchini (Tanzania Association of Phramaceutical Industry, TAPI), Bw.Abbas S.Mohamed, ambaye pia ni Mkurugenzi Wa Kampuni ya Samiro Pharmaceuticals Ltd ya jijini Dar es Salaam, akipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon Seoul na Mhe. Matilda S.Massuka, Balozi Wa Tanzania nchini Korea. TAPI inashirikiana na Serikali katika kufanikisha malengo ya ziara hiyo Nchini Korea na China, wakiiwakilisha Sekta Binafsi ya Tasnia ya Dawa na Vifaa Tiba ya nchini Tanzania.
  Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe.Matilda S. Massuka, akimkaribisha Bw. Asgaral Alimohamed, Mwanachama Wa TAPI na Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni ya Mwafrika Pharmaceutical Ltd ya jijini Tanga, baada ya kutambulishwa kwake na Bw.Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC anayeongoza ujumbe wa Tanzania, nchini humo.
  Balozi wa Tanzania nchini Korea Matilda Massuka akiulaki na kuukaribisha ujumbe wa Tanzania uliowasilini Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seoul Incheon, nchini Korea kwa ajili ya ziara ya uhamasishaji uwekezaji na biashara katika sekta ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania. Katika hatua ya awali, Ujumbe huo unaongozwa na Bw.Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, huku Ummy Mwalimu Waziri wa Afya wa Tanzania akitarajiwa kuungana na ujumbe huo nchini Korea mapema kesho kwa zaira ya kikazi ya siku tano (5) kuanzia Agosti 11 hadi15 mwaka huu

  0 0


  Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), baada ya kupokea mashine kumi za kufyatulia tofali ambapo ni mpango maalumu wa Serikali kuondoa changamoto za makazi ya askari magereza nchini.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Shaibu Ndemanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipima ukubwa wa tofali lililofyatuliwa na moja ya mashine alizokabidhi kwa uongozi wa Gereza la Mkoa wa Lindi ikiwa ni mpango maalumu wa kuondoa changamoto ya makazi kwa askari magereza nchini. Wanaoshuhudia ni viongozi wa gereza hilo wakiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange (kulia). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Magereza mkoani Lindi. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amekabidhi mashine 10 za kufyatulia matofali kwa jeshi la magereza la mkoa wa Lindi na kuwataka kuzitumia ipasavyo ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwemo makazi duni.

  Mashine hizo ni sehemu ya ahadi aliyoitoa mwaka mmoja na nusu uliopita baada ya kufanya ziara katika mkoa wa Lindi. Masauni alikabidhi mashine hizo katika gereza la Lindi mjini mkoani hapa na kuwataka jeshi la magereza kujipanga ipasavyo namna ya kuzitumia ili ziwe na tija na manufaa kwao.

  Alisema mwaka uliopita alifanya ziara ya kukagua shughuli za magereza na kukutana na changamoto mbalimbali ikiwamo makazi duni ya nyumba za udongo hasa katika gereza la Lindi Mjini. “Nawakabidhi mashine hizi leo, natarajia kuona mabadiliko yenye tija kutoka kwenu. Mkifanya vizuri nitawatafuta wadau wengine kwa ajili ya kuongeza mashine hizi,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;

  “Nataka gereza la Lindi Mjini liwe la mfano kwa magereza ya mkoa huu. Tumieni nguvu kazi ya wafungwa mlionao kwa ajili ya kuboresha makazi yenu,” alisema Masauni. Alisema atalishangaa jeshi la magereza endapo hawatumii ipasavyo nguvu kazi ya wafungwa wakati wana changamoto mbalimbali zinazowakabili na njia za kuzitatua zipo wazi.

  Hata hivyo, Masauni alisema ana matumaini makubwa na magereza katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na watazitumia mashine kwa ufanisi ili wapate makazi bora kwa manufaa ya askari na maofisa wao.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza ya Mkoa wa Lindi (RPO), Kamishna Msaidizi Mwandamizi , Rajab Nyange alisema hali ya makazi ya askari wa jeshi hilo siyo nzuri hivyo alimshukuru Masauni kwa msaada wa mashine hizo za ujenzi.

  Mkuu wa gereza la Lindi Mjini (SP), Emanuel Pagali alisema mashine hizo ni nzuri na zitawasaidia kwa utekelezaji wa majukumu yao ikiwamo kuboresha makazi ya maofisa na askari wa jeshi hilo

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  TIMU ya wanawake kutoka jimbo la Manonga Wilayani Igunga, Mkoani Tabora itaingia rasmi kambini kesho Augusti 13, 2018 kujiandaa na michezo ya kirafiki ili kujiweka sawa na michuano ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6 mwaka huu.

  Akizungumza na Blogu ya jamii msimamizi wa kambi hiyo Bi. Pendo Ndaki ambaye pia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Ziba ameeleza kuwa Manonga Queens ipo katika hali nzuri sana na wapo tayari kwa mashindano hayo.Ameeleza kuwa timu hiyo inayojiandaa na ligi daraja la kwanza nchini tayari imeanza kujifua vikali kabla michuano hiyo kuanza kwa kuanza kucheza mechi za kirafiki.

  Aidha mlezi wa timu hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali ameeleza kuwa wamejidhatiti kufuzu kati ya timu mbili zitakazopanda daraja na Ametoa gharama zote za awali kwa ajili ya kambi hiyo ya maandalizi.

  Mh.Gulamali amehimiza wadau wengine kujitoa zaidi kwa timu hiyo ili iweze kung'ara kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali.Timu 18 zimethibitisha kushiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa Wanawake litakaloanza Septemba 6, mwaka huu.

  Ligi hiyo itachezwa katika mfumo wa makundi na timu 2 zitapanda daraja wakati zitakazobaki zitasalia kwenye ligi daraja la Kwanza. 

  Timu zilizothibitisha ushiriki wao ni:

  1.Yanga Princes -Dar es Salaam
  2.TSC - Mwanza 
  3.Mapinduzi Princess -Tanga 
  4.Migoli Queens -Iringa 
  5.Ruangwa Queens -Lindi 
  6.Viva FC -Mtwara 
  7.Singida Warriors -Singida
  8.Katoro Queens -Geita 
  9.Victoria Queens -Kagera 
  10.Tanzanite FC -Arusha 
  11.Mapinduzi Queens -Njombe 
  12.Allans Queens -Dodoma 
  13.Manonga Queens -Tabora
  14.Abeehe Bha Kyela FC -Mbeya
  15.Kisarawe Queens -Pwani 
  16.Testimony -Kilimanjaro 
  17.Mbinga Queens -Ruvuma 
  18.Kizuka Sekondari -Morogoro 

  Timu hizo shiriki ni kwa mujibu wa Afisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Cliford Mario Ndimbo.

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Fadhili Juma, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Fadhili Juma, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Anthon Mandai, akipanda gali la Polisi mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pudencis Protas, kumkamata ili akajibu tuhuma zinazomkabili, Agosti 12.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC

  *Ni baada ya walimu kumtuhumu kwa ulevi, rushwa, kughushi nyaraka

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Bibi. Pudencis Protas kumkamata Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wa wilaya ya Ruangwa Bw. Anthon Mandai kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

  Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa walimu wakimlalamikia kiongozi huyo kuwa na tabia za kudai rushwa, kutowapandisha madaraja, ulevi pamoja na kuwaita walimu hao kwenye vilabu vya pombe kwa ajili ya kuwasikiliza matatizo yao.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Agosti 12, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika siku ya mwisho ya ziara kyake ya kikazi wilayani hapa. Bw. Mandai anakaimu nafasi hiyo tangu Juni, 2012.

  Amesema mbali na kulalamikiwa na walimu kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ulevi na kuwaita walimu katika vilabu vya pombe pindi wanapohitaji kuhudumiwa, pia amekuwa akighushi nyaraka za mirathi, jambo linalosababisha baadhi ya familia za waliokuwa walimu kuchelewa kupata haki zao.

  “Huyu Katibu ameshindwa kuwasaidia walimu katika kutatua changamoto zao na badala yake amekuwa akitumia vibaya majina ya viongozi wakuu, ambapo hata mimi alijaribu kutaka kunichakachua kwa kughushi muhtasari wa kikao cha mirathi ya Mwalimu Suwedi Chikawe akitumia jina langu kuwa nilikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kilichokuwa na agenda ya kumbadilisha msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa na familia jambo ambalo si la kweli,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema mbali na kukamatwa kwa Bw. Mandai, pia amemuagiza Kamanda Pudencis afanye uchunguzi wa kina utakaowezesha kukamatwa kwa mtandao wa watu wote wanashirikiana na kiongozi huyo katika kughushi nyaraka za vikao vya mirathi.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wabadilike na wafanye kazi kwa bidii, waachemazoea na watumie utalaamu wao vizuri katika kuwahudumia wananchi na Serikali haitowavumilia wafanyakazi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

  Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi kuwachukulia hatua watumishi wote wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu wanaitia hasara halmashauri yao na Serikali kwa ujumla.

  “Msimamo wa Serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo watumishi wajiepushe na vitendo vya rushwa na matumizi mbaya ya fedha za umma.”

  Pia Waziri Mkuu amewataka watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi katika maeneo yao hususan ya vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, AGOSTI 12, 2018.

  0 0


  Wanamichezo wa Polisi Tanzania walioshiriki Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufungaji wa michezo hiyo (Picha na Jeshi la Polisi).
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Wanamichezo wa Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi kombe la mshindi wa tatu nahodha wa timu ya mbio ya Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).
  Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Rwanda akimkabidhi Kombe la mshindi wa Pili katika kulenga Shabaha Inspekta wa Polisi Tannzaia wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).
  Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya akimkabidhi kombe la Ubingwa wa mpira wa miguu Inspekta Hashim Abdalah kutoka Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).

  Na. Jeshi la Polisi.

  Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) imemalizika Jijini Dar es Salaam huku Jeshi la Polisi nchini likishika nafasi ya pili katika ushindi wa jumla ambapo nafasi ya kwanza imeenda Kenya na ya tatu Uganda.

  Polisi Tanzania imeshika nafasi hiyo baada ya kuchukua jumla ya Medali 64, 15 za dhahabu, 25 za fedha na 24 za shaba huku Kenya ikiwa na medali 68, 25 dhahabu , fedha 20 na shaba 24.

  Mshindi wa Tatu Uganda alijinyakulia Medali 36, Rwanda 27, Burundi nane, Sudani Kusini sita na Sudani moja ambapo timu za Polisi Tanzania zimetwaa ubingwa katika Soka, Mpira wa pete, Judo, na Kulenga Shabaha kwa upande wa Wanaume.

  Akifunga Michezo hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi amewataka Wanamichezo hao kudumisha umoja na Amani katika mataifa wanayotoka ikiwemo kutumia michezo hiyo kubadilishana mbinu mbalimbali za kuzuia uhalifu.

  Aliwapongeza Wanamichezo wote walioshiriki michezo hiyo kwa kuonyesha nidhamu na ushindani wa hali ya juu jambo ambalo limefanya michezo hiyo kuvutia watazamaji wengi.

  Kwa upande Wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema wanajipanga kimkakati ili kufanya vizuri zaidi katika Michezo ijayo ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Kenya kwa kuwa ushindani ulikuwa mkubwa kutokana na nchi shiriki kujiandaa kwa muda mrefu.

  “ Tumejifunza sana kupitia michezo hii hivyo tuliyojifunza tutayafanyia kazi ili kuhakikisha timu zetu zinafanya vizuri zaidi katika michezo hapa nchini na nje ya nchi ikiwemo kukaa kwa pamoja kwa muda mrefu badala ya kuingia kambini kwa muda mfupi” Alisema Sirro

  Michezo inayoshindaniwa ni pamoja na soka ,mpira wa mikono, mpira wa wavu, mpira wa pete, Ngumi, Taekwondo, Judo na Riadha ambapo nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani, Sudani Kusini na Tanzania.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akifurahia maelezo ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Dkt. Mshana Dastan, kuhusu namna walivyojipanga kuhakikisha kituo hicho kinaanza kutoa huduma kwa wakati kutokana na umuhimu wake kwa wakazi wa Kasulu na maeneo yanayoizunguka Wilaya hiyo.
  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, Dkt. Mshana Dastan (kushoto), akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Chumba cha kuhifadhia maiti ikiwa ni sehemu ya majengo mapya yaliyojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 500, likiwemo jengo la wodi ya akina mama, maabara, nyumba ya mganga na miundombinu mingine, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipofanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho cha afya.

  Benny Mwaipaja, Kasulu, Kigoma

  Serikali imepanga kujenga zaidi ya vituo 120 vya afya nchini kote katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi ikiwemo huduma ya mama na mtoto.

  Hayo yamesemwa Mjini Kasulu, mkoani Kigoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipotembelea na kukagua ujenzi wa majengo mapya ya Kituo cha Afya Kiganamo, yaliyo gharimu shilingi milioni 500.

  Amesema kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani imeongeza bajeti ya Wizara ya Afya kutoka shilingi bilioni 30 hadi kufikia shilingi bilioni 369, hatua iliyolenga kuboresha afya za wananchi kwa kuwa hakuna maendeleo kama wananchi watakuwa na maradhi.

  “Awamu ya Tano ilianza na ujenzi wa vituo 44 vya afya na kufuatiwa na vituo 74 na sasa vituo takribani 120 vinaendelea kujengwa maeneo mbalimbali ili kutimiza lengo la kuwa na Kituo cha Afya kwa kila Kata”, alieleza Dkt. Kijaji.

  Dkt. Kijaji, alisema Serikali imeweka utaratibu wa Kata ambazo zipo jirani kutumia kituo kimoja wakati lengo kuu la kujenga kituo kimoja cha afya kwa kila Kata likiendelea kutekelezwa katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

  Aidha amebainisha kuwa Sekta ya Afya inatazamwa kwa upana wake na ndio sababu Serikali inaboresha pia miundombinu ya Maji ili wananchi waweze kupata maji safi na salama ili kuimarisha Afya zao.

  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Dkt. Mshana Dastan, amemweleza Dkt. Kijaji kwamba kukamilika kwa majengo hayo mapya ya Kituo cha Afya Kiganamo, kutaimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuwa, kinategemewa na idadi kubwa ya watu wanaotoka ndani na nje ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mji wa Kasulu, Bi. Fatina Laay, amesema kuwa wagonjwa katika zahanati hiyo wamekuwa wakilala zaidi ya watatu kwenye kitanda kimoja na kwamba kukamilika kwa ujenzi wa majengo hayo yaliyokamilika kwa zaidi ya asilimia 98 kutaondoa changamoto hiyo.

  “Mbali na Serikali kutupatia kiasi hicho cha shilingi milioni 500, mwisho mwa mwaka wa fedha uliopita, Serikali imetupatia kiasi kingine cha shilingi milioni 400kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Hedu Juu, kitakacho saidia kutoa huduma wa watu walioko pembezoni” Alieleza Bi. Laay.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayopatiwa fedha na Hazina pamoja na kuzungumza na jumuiya ya wafanyabiashara.

  0 0

  Na Dixon Busagaga ,Moshi.

  MGOMBEA udiwani katika kata ya Mawenzi ,manispaa ya Moshi ,Apaikunda Naburi (CCM) amefanikiwa kushinda nafasi hiyo akiwashinda wagombea wengine baada ya kupata kura 400 sawa na asilimia 70.3 kati ya kura 569 zilizopigwa.

  Naburi aliyekuwa diwani wa kata ya Mawenzi katika kipindi cha mwaka 2010-2015 kabla ya kushindwa na aliyekuwa Diwani wa kata hiyo ,Hawa Mushi aliyefariki dunia hivi karibuni baada ya kuugua ghafla.Mgombea huyo amefanikiwa kurejea kwenye nafasi hiyo kwa kuwashinda Afrikana Mlay wa Chadema na na Isaac Kereti wa SAU waliokuwa wakiwania kiti hicho.

  Akitangaza matokeo ya uchaguzi msimamizi wa uchaguzi , Erasmo Silayo alimtangaza Naburi kuwa mshindi halali wa kiti hicho huku akitaja kura za mgombea aliyefuatia kuwa ni Afrikana Mlay (Chadema) aliyepata kura 163 huku mgombea Isack Kireti (SAU) akiambulia kura 2.

  .Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi,Naburi amewashukuru wapiga kura katika kata hio huku akiwaahidi ushirikiano katika kuwatumikia.
  "Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 1821, kati yao idadi halisi ya wapiga kura ni 569 ambapo kura 4 ziliharibika"alisema Silayo.
   Msimamizi wa uchaguzi , Erasmo Silayo akimtangaza Naburi kuwa mshindi halali wa kiti hicho huku akitaja kura za mgombea aliyefuatia kuwa ni Afrikana Mlay (Chadema) aliyepata kura 163 huku mgombea Isack Kireti (SAU) akiambulia kura 2.
   Msimamizi wa uchaguzi , Erasmo Silayo akimkabidhi cheti cha ushindi kwa Naburi mara baada ya kutangazwa mshindi halali wa kiti hicho huku akitaja kura za mgombea aliyefuatia kuwa ni Afrikana Mlay (Chadema) aliyepata kura 163 huku mgombea Isack Kireti (SAU) akiambulia kura 2.
   MGOMBEA udiwani katika kata ya Mawenzi ,manispaa ya Moshi ,Apaikunda Naburi (CCM) akionesha cheti chake mara baada ya kushinda nafasi hiyo akiwashinda wagombea wengine baada ya kupata kura 400 sawa na asilimia 70.3 kati ya kura 569 zilizopigwa.
  Wakisherehekea ushindi wao mara baada ya kutangazwa mshindi

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) pamoja na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani ,Ramadhani Maneno, wakishiriki katika nguvu kazi ya ujenzi wa kituo cha afya Kirongwe wilayani Mafia ,wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano. Kuanza kwa ujenzi huo imetokana serikali kutoa kiasi cha sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huo ambao utakapokamilika kituo kitahudumia takribani wakazi kutoka vijiji vingi vinavyozunguka kata ya Kirongwe .(picha na Mwamvua Mwinyi).
  Sehemu ya ujenzi wa mradi wa maji safi na salama ,(inayoonekana pichani),unaojengwa kijiji cha Jibondo ,wilayani Mafia,mkoani Pwani ,ambao utakapokamilika utakaogharimu karibia bilioni mbili .(picha na Mwamvua Mwinyi).
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akibeba ndoo ya samaki kumimina katika beseni la mama ambae anauza biashara ya samaki kwenye mwalo wa samaki wilayani Mafia.(picha na Mwamvua Mwinyi).

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda amefanya mazungumzo na kampuni ya Burmeister & Partiners (PTY) LTD ya nchini Namibia tarehe 10 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia.

  Akiongea na uongozi wa kampuni hiyo Prof. Mkenda alieleza Tanzania ina eneo kubwa la ardhi yenye rutuba ambayo haitumiki na rasilimali watu ya kutosha hivyo ni fursa kwa mwekezaji mwenye nia thabiti kuwekeza nchini.

  “Lengo la Serikali ni kupata mwekezaji aliye makini kama wewe nimeona una mradi mkubwa wa shamba la mifugo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya machinjio nina imani ukija kuwekeza Tanzania hautajutia kabisa kwakuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa katika miradi itaongeza thamani ya mazao na bidhaa zitakazozalishwa na kuwezesha kupatikana kwa soko la kimataifa” alisema Prof. Mkenda

  Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mhandisi Hendrik Boshoff alieleza kampuni imekuwa ikifanya kazi katika mataifa mbalimbali ambapo kampuni hiyo imefungua kampuni ya maziwa nchini Rwanda ambayo inauza na kusafirisha mataifa mengine pia imewekeza nchini Angola katika miradi ya uvuvi na imekuwa ikifanya vizuri katika biashara zake zote.

  Pia alisema kampuni imebobea katika miradi ya ujenzi, nishati, miradi ya maji, usafiri, usanifu majengo, ujenzi wa majengo, miradi ya machinjio, mashamba ya mifugo na pia ipo katika mpango wa kuanzisha miradi ya viwanda vya dawa za binadamu ambapo utekelezaji wake utaanza mara baada ya kukamilisha mazungumzo na wataalamu kutoka nchini Cuba.


  Prof. Mkenda alieleza miradi yote kutoka katika kampuni hiyo inatija kubwa kwa maendeleo ya taifa la Tanzania hivyo akaikaribisha kampuni hiyo kuja mapema nchini ili kuweza kujionea rasilimali zilizopo na kuainisha miradi watakayoweza kuanza nayo. Vilevile akaeleza kampuni hiyo ina nafasi ya kutumia fursa za mji wa Dodoma katika uwekezaji kufuatia kuhama kwa mji wa Serikali kutoka Dar es Salaam.

  Kampuni ya Burmeisters & Partiners (PTY) LTD ilianza kufanya kazi zake nchini Namibia mwaka 1984 na baadae kuwa miongoni mwa kampuni kubwa zilizowekeza nchini humo. Pia ni kampuni hiyo inatoa huduma za kihandisi na huduma za usimamizi wa miradi katika taaluma mbalimbali.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda(kulia) akizungumza na mwakilishi wa kampuni ya Burmeister and Partners (PTY) LTD alipowatembela katika ofisi za kampuni hiyo iliyopo Windhoek, Namibia tarehe 10 Agosti 2018. Kulia kwa Katibu Mkuu ni ujumbe ulioambatana naye katika ziara hiyo, Mratibu wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa katika Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Tanzania, Bi. Magreth Ndaba, Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Bw. James Lugaganya na Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Sylivester Ambokile. 
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Burmeister & Partners (PYT) LTD, Mhandisi Hendrik Boshoff akielezea usanifu wa miradi mbalimbali unaofanywa na kampuni ya Burmeister & patners (PTY) LTD. 
  Sehemu ya ofisi iliyosanifiwa na kampuni hiyo. 
  Mazungumzo yakiendelea. 
  Mwakilishi kutoka kampuni hiyo akiwasilisha miradi mbalimbali liyosanifiwa na kampuni ya Burmeister & Partners (PTY) LTD 
  Prof. Mkenda akifafanua tunu na rasilimali zilizopo nchini ambazo ni fursa kwa uwekezaji.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi ambae pia alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahengeakizungumza katika kongamano la Usalama. Barrabarani lililoandaliwa na Mabalozi wa usalama barabarani( RSA) na kufanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Dodoma jana. Picha na Vero Ignatus
   Mwalimu wa Elimu ya Usalama barabrani ambae pia ni mmoja wa Baraza la Usalama. Barabarani Nchini. Picha na Vero Ignatus
   Mkuu wa wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akizungumza katika kongamano hilo Jijini Dodoma. Picha na Vero Ignatus
   Baadhi ya Mabalozi wa Usalama barabarani pamoja na wadau wa Usalama barabarani wakiwa katika kongamano la siku moja Bungeni Dodoma katika Ukumbi wa Pius Msekwa. Picha na Vero Ignatus.

  Henry Bantu kutoka Baraza la Usalama barabarani Nchini akizungumza na mabalozi katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Dodoma. Picha na Vero Ignatus.
  Mkurugenzi wa Huduma ya Sheria Nchini Marlin Komba Akiwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Nchini Fortunatus Musilim. Picha na Vero Ignatus. 
   Wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Nchini (RSA) John Seka akifuatiwa na Kamanda wa Polisi Kikosi chq Usalama Barabarani SACP Fortunatus Musilim, Mkuu wa wilaya ya Gairo Siriel Mchembe, Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobas Katambi, Mkuu wa Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Kamotta, na Mkurugenzi wa Huduma ya sheria Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Marlin Komba. Picha na Vero Ignatus. 
  Mkuu wa wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akiwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi 
  Wakiwa wameshikilia bango lenye maandishi yasemayao Tunataka mabadiliko ya sheria ya Usalama barabarani Nje ya Ukumbi wa Bunge Pius Msekwa jana. Picha na Vero Ignatus. 
  Mkurugugenzi wa Huduma ya sheria Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Marlin Komba akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Gairo Siriel Mchembe, Bungeni Dodoma jana. Picha na Vero Ignatus
  Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama barabarani Nchini John Seka, katikati ni Mkuu wa wilaya ya Gairo Siriel Mchembe na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma ya Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Marlin Komba. Picha na Vero Ignatus. 


  Na. Vero Ignatus Dodoma. 

  Taasisi ya mabalozi wa usalama barabarani nchini wamefanya kongamano la siku Mkoani Dodoma dhima kuu ikiwa '' Mabadiliko ya sheria ni muhimu katika kuimarisha usalama nchini''

  Kongamano hilo limefanyika kwasababu ya mkono mabadiliko ya sheria za usalama barabarani kushirikiana /kuwahusisha viongozi wanaohusika na mambo ya kisera na waunge mkono mabadiliko ya sheria hiyo. 

  Mkurugenzi wa habari na mawasiliano RSA, ambae pia ni mjumbe wa Baraza la Taifa usalama barabarani Augustus Fungo amesema kuwa wanahitaji mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani kwani iliyopo haikidhi na imepitwa na wakati kwani ilitungwa mwaka 1983. 

  '' Wakati sheria hii ikitungwa sayansi na teknolojia ilikuwa haijashika kasi kama ilivyo sasa, barabara zetu, vyombo vya moto vilikuwa vichache tofauti na miaka ya leo'' alisemaFungo

  Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania Fortunatus Musilim amewapongeza RSA kwa ushirikiano wao na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa mbalimbali pale ajali inapotokea na hata pale sheria zinapovunjwa hata uhalifu unapotokea. 

  Amesema kuwa ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva, vyombo vya usafiri kuwa vibovu (haswa malori) miundo mbinu ya barabara. 

  '' Tayari tumeanzisha operasheni inayoendelea nchi nzima ya kukagua leseni kwa madereva katika stendi za mabasi na uhakiki wa vyeti ili kutambua kama dereva hiyo amepata mafunzo''Alisema Kamanda. 

  Mkuu wa wilaya ya Gairo Siriel Mchembe amewataka mabalozi hao wa usalama barabarani kutoa elimu chanya kwa wananchi na kuzima elimu hasi inayowashuka askari wa usalama. Barabarani wakati wanatimiza majukumu yao. 

  "ukimuona askari anawavusha watoto au wapitanjia kwa ujumla usiwadharau kwani kazi yake kubwa ni kuhakikisha jamii inakuwa salama

  Amesema kuwa nchi haitoweza kuwa ya viwanda kama watu watakuwa wanapata ulemavu unaotokana na ajali za barabarani. 

  Mkuu wa wilaya ya dodoma. Mjini Patrobas Katambi ambae pia alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa dodoma  Dkt Binilith Mahenge  amesema changamoto Kubwa ya usalama barabarani ufahamu mdogo walionao. Maderwva na haswa wakati wa utoaji wa leseni kwani wanapeqa. Watu wasiokuwa sahihi. 
  Ajali inaepukika.

  Matukuo mbalimbali kama inavyoonekanq pichani katika Kongamano la siku moja lililofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni. Picha na Vero Ignatus. 


  0 0

  Na Felix Mwagara, MOHA

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemtaka Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bunda kuwakamata watu walioshiriki kuwatapeli wananchi katika Sekta ya michezo wilayani humo, Mkoa wa Mara.

  Watu hao ambao walitangaza kuanzisha ligi wilayani humo na kuzitaka timu za mpira wa miguu kata mbalimbali zichangie fedha na baadaye ligi hiyo haikufanyika na watu hao walikimbia na fedha hizo na kufanya wananchi hao waandamane wakitaka fedha zao zirudishwe.

  Waziri Lugola akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Bunda baada ya kulizindua Bonanza la Amani wilayani humo, alisema kitendo walichokifanya watu hao ni ufiadi mkubwa hivyo lazima wakamatwe ili iwe funzo kwa wale wote wenye tabia ya kufanya ufisadi wa aina hiyo katika sekta ya michezo nchini.

  “Nimeambiwa wanamichezo ambao walichangishwa waliandamana mpaka kwa Mkuu wa Wilaya kuelezea jinsi walivyoibiwa na watu hao, hata hivyo Mkuu wa Wilaya alitangaa watu hao warudishe fedha hizo, ila mimi nahitaji hawa watu wakamatwe haraka iwezekanavyo, huu ni ufisadi mkubwa na hakika Serikali hii ya awamu ya nne haitakubaliana na ufisadi huo.

  Aliongeza kua, mahakama ya ufisadi inahitaji wateja hivyo waliofanya wizi huo pia ni mafisadi hivyo lazima wakamatwe haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake. Aidha, Bonanza ambalo alilizindua waziri huyo, linatarajiwa kufanyika nchini nzima limezinduliwa mjini humo na baadaye litafanyika nchi nzima likiwa na lengo kuu kutangaza amani nchini.

  Waziri Lugola alisema, michezo inaleta amani michezo inaleta ushirikinao, michezo inaimarisha undugu, michezo inaimarisha ushikamano na michezo uepusha wananchi wasijiingize katika uhalifu, hivyo Wizara yake inatarajia Bonanza hilo litazidi kudumisha amani zaidi.

  “Michezo ikiimarishwa tunaimarisha amani, tukishiriki michezo kama hivi wanaokuja kutazama na nyie mnaocheza, hivyo muda mwingi tunautumia katika kufurahi pamoja na ndio mana vitendo vya uhalifu vitapungua kwasababu watu tunataka tuwe wamoja kupitia michezo,” alisema Lugola.

  Waziri Lugola aliongeza kua, Bonanza la kuhubiri amani sio kwamba linafanya wilyani Bunda bali litafnyika nchi nzima likiwa na lengo la kuwaweka watanzania pamoja ili amani nizidi kudumu.

  “Hapa tulipo ni uwanja wa CCM na hii ilani ni ya CCM na katika ibara ya 160, 161 na 162 inazungumzia kuimarisha na kudumisha sekta ya michezo, hivyo tupo hapa kutokana na ilani hii ya CCM na lengo kuu ni kudumisha amani,” alisema Lugola.

  Waziri Lugola yupo wilayani Bunda mkoani Mara kwa ajili ya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ndany ya jimbo lake la Mwibara wilayani humo.

  0 0


  Aliyekuwa diwani wa Jibondo wilayani Mafia Hassan Mohammed Hassan ,akimpa mkono Mwenyekit wa Chama Cha Mapinduzi,Mkoani Pwani Ramadhani Maneno baada ya kujihudhuru nyadhifa yake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) (picha na Mwamvua Mwinyi)

  NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA

  MADIWANI wawili kutoka chama cha wananchi (CUF) kata ya Kilindoni na Jibondo ,wilayani Mafia ,Mkoani Pwani, wamejihudhuru nyadhifa zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,kutokana na chama tawala kurudisha heshima na kuwa sikivu nchini.

  Madiwani hao wamerudi CCM katika ziara ya kamati ya siasa mkoani Pwani ,iliyoweka kambi siku mbili wilayani humo,kutembelea miradi na kukagua utekelezaji wa chama hicho . Aliyekuwa diwani wa Jibondo Hassan Mohammed Hassan ,alisema amefanya maamuzi hayo kutokana na chama walichokuwepo kukosa mwelekeo na kukosa sera zinazojiuza. 

  Alisema ,kata ya Jibondo ilikuwa na wafuasi wa CCM ambapo ilipofika 2004 wengi wao walihamia upinzani kutokana na baadhi ya mambo kutokwenda wanavyotaka.“Nampongeza Rais Dk.Magufuli, mkuu wa mkoa wa Pwani, wilaya na CCM Mafia na mkoa kwa juhudi zao katika kuinua uchumi wa nchi na kukuza sekta ya viwanda na uwekezaji” alibainisha Hassan. 

  Nae aliyekuwa diwani wa Kilindoni ,Ahmad Mbonde,alisema hajanunuliwa kwani kata yake ipo mjini, ilikuwa tishio na ilitikisa . “Leo hii nafanya maamuzi haya ,kwa akili zangu ,pasipo kushawishiwa bali ni kutokana na serikali kufikisha fedha nyingi kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo bila ubaguzi “
  “Serikali hii ni sikivu na imesaidia mengi katika kata zetu hasa kwenye utekelezaji wa miradi ya afya ,elimu ,maji na kusikiliza wanyonge” alisisitiza Mbonde.

  Akiwapokea madiwani hao,mwenyekiti wa CCM Pwani,Ramadhani Maneno alisema hawajafanya makosa kurudi CCM. Alielezea inaashiria tosha kuwa CCM ya sasa na mpya kwani inakubalika na wananchi,wasio wana CCM na viongozi wa upinzani ambao wanakimbia vyama vyao kila uchao. Awali mkuu wa wilaya ya Mafia ,Shaibu Nnunduma alisema walikwenda ofisini kwake kuomba kurudi CCM bila kushawishiwa.

  Alisema ushirikiano baina ya mbunge,CCM wilaya ,halmashauri na wilaya pamoja na ngazi za Taifa imewasukuma madiwani hao hivyo aliomba ushirikiano huo uendelee.

  0 0


  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde amebainisha dhamira na mikakati ya serikali katika kuhakikisha inaweka mazingira salama ya kuwawezesha Vijana na Watu wenye ulemavu kiuchumi kwa kuhamasisha makundi mengi ya Vijana kujisajili ili kuunganishwa na fursa za uwezeshwaji kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani na mifuko ya uwezeshwaji wananchi kiuchumi Nchini. 

  Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho wa siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu,Tengeru-Arusha ambapo pia ameeleza juu ya mpango wa ukuzaji Ujuzi kwa Vijana ambapo mwaka huu wa fedha 2018/2019 Serikali imetenga Bilioni 15 kwa ajili ya kuwajengea ujuzi vijana wa Tanzania.

  Aidha akitoa maelezo ya awali,Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Mrisho Mashaka Gambo amewataka Vijana kutumia muda wao vizuri kwa kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda wao kufanya mambo yasiyokuwa na tija. 

  Wawakilishi wa UNFPA na ILO nchini Bi Jaqueline Mahon na Bw Wellingtone Chibebe wameipongeza Serikali ya Tanzania katika programu yake ya Ukuzaji ujuzi na kuahidi kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa mipango hiyo.

  0 0

  Na Benny Mwaipaja, Kasulu, Kigoma

  Naibu Waziri wa Fefha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Wakala wa majengo Tanzania-TBA, kutekeleza kwa wakati mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma ili kuiepusha Serikali kutumia fedha nyingi kutokana na kuongezeka kwa gharama za miradi husika kunakotokana na ucheleweshwaji huo.

  Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendelelo ya ujenzi wa Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu zinazojengwa na Serikali kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 na kutaarifiwa kuwa TBA, wamechelewa kuanza ujenzi huo kwa zaidi ya miezi 12 wakati fedha zilikwisha tolewa na Serikali.

  Aliishauri TBA kujipanga kukamilisha miradi inayopewa na Serikali kwa wakati kwa kuongeza idadi ya wataalam wanaoweza kusimamia miradi mingi inayotekelezwa na wakala huo.

  "Pesa zipo, Serikali haiwezi kuanza kutekeleza mradi wowote kama hakuna pesa, ni jukumu lenu kama TBA kuhakikisha mnawezesha mradi huu ukamilike kwa wakati ili tupate thamani halisi ya fedha za mradi" alisisitiza Dkt. KijajiDkt. Kijaji alitoa wito kwa wakazi wa Mji wa Kasulu na Kigoma kwa ujumla kuchangamkia fursa za ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao kwani lengo la Serikali kujenga miradi hiyo ni kuwawezesha pia wananchi kiuchumi.

  Hatua hiyo inafuatia taarifa iliyotolewa na Mhandisi wa ujenzi wa Jengo hilo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Bw. Abubakari Basuka, kwamba miongoni mwa changamoto inayoukabili mradi huo ni ukosefu wa mafundi mchundo na vibarua ambapo imeelezwa kuwa vijana wengi katika eneo la mradi hawajitumi kufanyakazi.

  "Wakati tunatoa taarifa ya hali ya uchumi mwaka wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Tano madarakani, utafiti ulionesha kuwa mkoa wa Kigoma miongoni mwa mikoa ya mwisho kwa umasikini na tukaamua kuipa kipaumbele kwa kuleta miradi kama hii ili wananchi wake wanyanyuke kiuchumi.

  Alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange, kukutana na wananchi wa wilaya yake ili awaeleze fursa za kiuchumi zinazoletwa na Serikali katika maeneo yao ili waondokane na umasikini kwa kushiriki katika kufanya kazi za kujenga miradi hiyo ukiwemo mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Kisasa za Halmashauri ya Mji wa Kasulu

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Bi. Fatina Laay, amesema kuwa kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi hizo kunasbabisha wafanyakazi wa Halmashauri yake washindwe kutekeleza majukumu yao kikamilifu kutokana na ufinyu wa nafasi kwenye jengo wanalolitumia hivi sasa. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayopatiwa fedha na Hazina pamoja na kuzungumza na jumuiya ya wafanyabiashara.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akiwasili kukagua mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma, katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Bi. Fatina Hussein Laay, na kulia ni Mhandisi wa mradi huo Bw. Abubakari Basuka.
  Mhandisi wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Bw. Abubakari Basuka (aliyevaa kofia) akisoma taarifa fupi ya Mradi kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wa tatu Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Bi. Fatina Hussein Laay (kushoto), akieleza umuhimu wa kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Ofisi za Halmashauri yake ya Mji kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) kwa kuwa ofisi zinazotumika sasa hazikidhi mahitaji, wa pili kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA, Bw. Elijah Mwandumbya.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati), akitoa maagizo kwa Mhandisi wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Bw. Abubakari Basuka (kulia) kutumia nguvu kazi iliyopo Wilayani humo kuharakisha utekelezaji wa mradi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange (kulia) akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani), wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo ya kukagua Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma.
  Muonekano wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mji Mkoani Kigoma litakalo gharimu takribani Sh. Bilioni 2.5.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiagana na Mhandisi wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Bw. Abubakari Basuka (kulia) baada ya ukaguzi wa mradi huo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
   

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

  SERIKALI ya Sierra Leone kupitia wizara Elimu na Ufundi na Elimu ya Juu umetembelea Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) kujifunza na bodi hiyo inavyotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu .

  Ujio huo umekaa kwa wiki moja katika bodi hiyo ikiwa ni kuangalia namna ya kuweza kujifunza na kwenda kuanzihsa chombo hicho nchini Sierra Leone.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) , Abdulzaq Badru amesema kuwa nchi sierra leone kufika hapo ni kutokana na umahiri katika uchakataji wa mikopo kwa wanafunzi kwa elimu ya juu.

  Amesema kuwa ujumbe huo umepita katika nchi ya Ghana na kisha Tanzania kuangalia namna ya uendeshaji wa bodi katika utoaji wa mikopo.

  Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie , Naibu Katibu Mkuu Wizara fedha  Mr. Matthew Dingie , Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Bima Mohammed Gondoe na wajumbe wengine.

  Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie amesema HESLB inafanya vizuri katika uchakataji wa mikopo na kusema kuwa wanatarajia kuanzisha chombo kama hicho nchini kwao.
  Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) , Abdulzaq Badru akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) wakati wa kuwaaga ujumbe wa Sierra Leone waliotembelea bodi hiyo.
  Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie akizungumza na waandishi habari kuhusiana na alichojifunza katika bodi ya mikopo.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kuweka jiwe la Msingi wa ujenzi wa Shule ya awali ya Kizimkazi iliyopo Shehia ya Kizimkazi- Mkunguni katika Wilaya ya Kusini, Jimbo la Makunduchi –Unguja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za siku ya Kizimzikazi. Katika kuchangia ujenzi huo Waziri Makamba atatoa mifuko 50 ya saruji na bati 50.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimiana na watoto katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa Shule yao ya awali Kizimkazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Uratibu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar Bw. Khalid Hamran
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakazi wa Kizimkazi hii leo katika Shehia ya Kizimkazi- Mkunguni katika Wilaya ya Kusini, Jimbo la Makunduchi –Unguja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za siku ya Kizimzikazi, sherehe zilizoenda sambamba na uwekekaji wa jiwe la msingi katika shule ya awali. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman (katikati) akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mhe. January Makamba kulia sherehe za Siku ya Kizimkazi, jimboni Makunduchi.   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amehidi kutoa mifuko hamsini ya saruji na bati hamsini kama mchango wake katika ujenzi wa Shule ya awali ya Kizimkazi iliyopo takiriban kilomita 61 kutoka Mjini Unguja. 

  Ahadi hiyo ameitoa hii leo Shehia ya Kizimkazi- Mkunguni katika Wilaya ya Kusini, Jimbo la Makunduchi katika maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi. “Nawapongeza sana kwa hatua hii mliyofikia na utayari wenu wa kuwekeza katika miradi mikubwa hususan elimu ambayo ndio nguzo kuu” Makamba alisisitiza. 

  Waziri Makamba amewataka wana Kizimkazi kuandaa utaratibu wa kutembeleana na kubadilishana uzoefu baina yao na vijiji vya Tanzania Bara ili kudumisha Muungano na kujenga ushirikiano zaidi. “Mwakani tuweke nguvu zaidi, tuwe na vikundi vya ngoma na sanaa mbalimbali kutoka upande wa pili wa Muungano pia tutaanda ziara ya mafunzo ili kwa pamoja muweze kubadilisha uzoefu” alibainisha Makamba. 

  Aidha, Waziri Makamba amewakumbusha wana Kizimkazi kuuenzi na kuulinda Muungano kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa Muungano haukuanzisha undugu bali Muungano umerasimisha undugu baina yetu, na wakubainisha kuwa changamoto za Muungano zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi. 

  Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa Shule hiyo Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kizimkazi Bi. Rehema Ramadhani amesema kuwa Shule hiyo imeanza kujengwa kwa nguvu za wananchi na baadae kuungwa mkono na wadau mbalimbali. 

  Bi Ramadhani amebainisha kuwa kumalizika kwa ujenzi huo itakuwa ni faraja kubwa kwa wazazi na wanafunzi kutokana na sehemu finyu na hatarishi katika jengo la awali kwa kuzingatia kuwa Shule hiyo ipo mkabala na barabara kuu. 

  Aidha, imebainika kuwa tangu kuanzishwa kwa sherehe hizo za ‘Siku ya Kizimkazi’ wakazi hao wamefanikwa kujenga ukumbi wa shule kwa ajili ya kufanyia mitihani, ukarabati wa nyumba ya daktari, ujenzi wa nyumba ya mwalimu pamoja na ujenzi wa shule ya awali ambayo leo hii jiwe la msingi limewekwa. 

  Sherehe hizi za Siku ya Kizimkazi huadhimishwa kila mwaka mara moja kwa lengo la kuthamini maendeleo pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi wa Mkoa huo na kutafuta mbinu mbadala za utatuzi. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Umoja wetu, Ushirikiano wetu na Mshikamano wetu ndio ngao yetu” 


older | 1 | .... | 1645 | 1646 | (Page 1647) | 1648 | 1649 | .... | 1898 | newer