Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Benki ya TPB Plc yawakaribisha wateja waliokuwa benki ya wanawake Tanzania (TWB).

$
0
0
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi, akiwakaribisha katika benki hiyo, wateja waliokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) Pia amefafanua mambo mbalimbali kuhusu kuwahudumia wateja wao bila ukiritimba wowote watashirikiana pamoja. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

 Baadhi ya wafanyakazi waliokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) wakimsikiliza kwa makini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi,hayupo pichani, wakati wa kuwakaribisha katika Benki ya TPB



 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi,kushoto akisalimiana na wateja waliokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB)na kuwakaribisha rasmi.Hafla hio ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.


WANANCHI WA MONDULI WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa amembeba mtoto aliyeletwa Kliniki katika kituo cha afya Mto wa mbu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akisalimiana na wananchi wa mto wa mbu wilayani Monduli.
Wananchi wa mto wa mbu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
Viongozi wakiwa eneo la Makuyuni wakikagua ujenzi wa miundombinu ya kituo cha Afya Makuyuni.

..............................................

Wananchi wa Mto wa mbu na Makuyuni wilayani Monduli Mkoani Arusha wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kwa uboreshaji wa huduma za afya wilayani humo. Wananchi hao wametoa pongezi hizo katika ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Waziri Jafo anakagua miradi ya maendeleo na kufanya ufuatiliaji wa maagizo yake aliyo yatoa miezi ya nyuma katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo kwasasa ametokea mikoa ya Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, na kigoma. Hatua ya ziara hiyo ilitokana hivi karibuni serikali imepeleka fedha katika kituo cha afya Mtowambu kiasi cha shilingi milioni 400 na baadae imepeleka fedha zingine shilingi milioni 400 katika kituo cha afya Makuyuni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. 

Katika ziara ya Waziri hiyo wilayani Monduli, Wananchi hao wameishukuru serikali na kwamba hatua hiyo itaboresha na kuwezesha huduma bora kutolewa kwenye vituo hivyo. Wamesema ukosefu wa vituo hivyo uliwafanya kukosa huduma za upasuaji. Kwa upande wake, Waziri Jafo amemshukuru aliyekuwa mbunge wa Monduli Julius Kalanga kwa kufikisha kero za wananchi wa Monduli katika Ofisi yake na serikali ikapeleka fedha hizo ili kuwasaidia wananchi hao ambao walikuwa wakitaabika miaka yote bila ya kuwa na vituo vya afya vinavyoweza kufanya huduma ya upasuaji. Jafo amewapongeza sana wananchi hao kwa kuungana na serikali na kufanikisha uboreshaji wa kituo cha afya mtowambu pamoja na juhudi za ujenzi zinazo endelea katika kituo cha afya Makuyuni. 

Aidha Waziri Jafo amewajulisha wananchi hao kwamba serikali itapeleka vifaa tiba vyote katika kituo cha afya Mtowambu ambacho tayari kimekamilika ili wananchi hao wapate kuonja matunda mazuri ya utekelezaji wa Ilani ya CCM. Katika ziara hiyo Jafo amewataka viongozi walio chini ya Ofisi yake kuanzia mikoani hadi wilayani wahakikishe wanajituma muda wote katika maeneo yao kwa lengo la kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

JESHI LA POLISI LALAANI VIKALI TUKIO LA KUPIGWA MWANAHABARI WA KITUO CHA WAPO RADIO, SILAS MBISE

WAZIRI WA MADINI ANGELA KAIRUKI AWAPA ONYO WATOROSHAJI WA MADINI YA RUBY MUNDARARA LONGIDO

$
0
0
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya Vito ya Ruby katika Kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha kujitafakari upya na kuwa wakweli katika biashara hiyo ya madini.

Akiwa katika ziara yake ya kikazi iliyolenga kujionea shughuli za uchimbaji wa madini hayo ya vito pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili Waziri Kairuki alifanya pia mkutano mkubwa wa hadhara kijijini hapo. Akizungumza na wananchi hao wa Mundarara Waziri Kairuki aliwataka wananchi hao kushirikiana na Serikali katika kuwafichua watu wasiowaaminifu kwa rasilimali za taifa.

“Nyinyi wananchi na wafanyabiashara hapa mnawajua wanaotorosha madini kwenda nchi jirani, niwaombe muwafichue kwani madini hayo ni fedha mnazozihamishia nchi nyingine ambazo zingewaletea maendeleo nyinyi. “Tafadhaili sana kwa wafanyabiashara naowamba muache kuanzia sasa kwani mtajikuta mkiwa katika wakati mgumu wa kupteza mitaji yenu na hata kupoata hasara kubwa pindi mtakapokamatwa,” alisema Waziri Angela. “Kiama kikubwa kinakuja kwa watoroshaji wote wa madini sasa nimekuja hapa kuwaambia ole wao wanaowasaidia na wanaoshirikiana nao haoa mpo karibu na mpaka nawaomba mjiepushe na biashara hiyo haramu,” alisema. 

Kupitia ziara hiyo Waziri Kairuki alitumia fursa hiyo kuwataka wawekezaji kumaliza migogoro ya mitobozano inayowakabili ambapo pia alifanya ziara katika Mpaka wa Namanga kwa lengo la kujionea changamoto zinaawakabili wafanyakazi wa wizara hiyo. 
Mkuu wa wilaya ya Londigo Frank Mwaisumbe akiuelekeza msadara wa Waziri wa Madini Angela Kairuki aliyefanya ziara kwenye mgodi wa Mundarara Ruby Miningi unaomilikiwa na mwekezaji Rahim Mollel uliopo Kata ya Mundarara katika ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri wa Madini Angela Kairuki akiangalia kwa makini mgodi wa madini ya Ruby wa Mundarara unaomilikiwa na mwekezaji Rahimu Mollel ambapo alifanya ziara hiyo kujionea shughuli za uchimbaji na kufahamu changamoto zinazowakabili.
Mwekezaji wa mgodi wa Mundarara Ruby Mining uliopo Longodi mkoani Arusha Rahim Mollel akiongoza msafara wa Waziri wa Madini Angela Kairuki aliyefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutembelea mgodi huo.
Mwekezaji wa mgodi wa Mundarara Ruby Mining uliopo Longodi mkoani Arusha Rahim Mollel akimuonyesha Waziri wa Madini kipande cha Ruby mara baada ya kuvunja jiwe gumu.
Waziri wa Madini Angela Kairuki akisoma Leseni ya uchimbaji ya kampuni ya Sendeu inayomilikiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Mbunge wa zamani Longido Michael Laizer
Waziri wa Madini Angela Kairuki akiangalia mazingira ya mgodi wa uchimbaji madini ya vito ya Ruby unaomilikiwa na Kampuni ya Sendeu iliuopo chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Mbunge wa zamani Longido Michael Laizer.
Waziri wa Madini Angela Kairuki akicheza ngoma za kabila la Wamaasai kabla ya kuwahutubia wananchi na wakazi wa Kijiji cha Mundarara yalipo machimbo ya madini ya vito ya Ruby wilayani Longido mkoani Arusha.
Waziri wa Madini Angela Kairuki akihutubia wananchi na wachimbaji wadogo wa madini ya vito ya Ruby katika eneo la Kijiji cha Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha.

 

UCHAFU NI ADUI WA AFYA YAKO,YATUNZE MAZINGIRA YAKO YAKUTUNZE.

$
0
0
 Mfanyabiashara wa Matunda akiendelea na biashara yake huku pembeni kukiwa na mtaro wa maji machafu katika eneo la Mbagala jijini Dar as Salaam,jambo ambalo ni hatari kwa afya ya walaji.Wananchi wanaaswa kutunza mazingira yao na kuwa safi kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababishwa na uchafu.
 Maandalizi ya biashara ndogondogo yakiendelea katika eneo la Mbagala jijini Dar as Salaam.
Maandalizi ya biashara ndogondogo yakiendelea katika eneo la Mbagala jijini Dar as Salaam. (Picha zote  na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

MKURUGENZI MTENDAJI CRDB BANK, DK. KIMEI ATEMBELEA OFISI ZA MKOA ZA SIDO JIJINI DAR ES SALAAM, AZUNGUMZA NA WANASEMINA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (kushoto), akiwa pamoja na mwenyeji wake, Meneja wa Sido Mkoa wa Dar es Salaam, MacDonald Maganga, wakiwasili katika ukumbi wa semina ya wajasiriamali wa Sido, walipofika kwa ajili ya kuzungumza nao, mwishoni mwa wiki Vingunguti jijini Dar es Salaam.   
Wanasemina wajasiriamali wa Sido, wakimpokea Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (hayupo pichani), wakati alipowatembelea na kuzungumza nao katika mafunzo yao ya wiki moja, Sido mkoani wa Dar es Salaam. 
Baadhi ya Maofisa wa CRDB Bank, walioambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na mkurugenzi huyo, kwenye mafunzo ya wajasiriamali wa Sido, Mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Dawati la Akinamama, Rehema Shambwe, Meneja Mwandamizi Wateja Biashara Ndogo na za Kati, Mussa Mwinyidaho (katikati) na kulia ni Meneja Uhusiano wa CRDB, Rachel Senni.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei, akizungumza na wajasiriamali wa Sido, wakati wa semina yao, iliyofanyika Sido Mkoani, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja wa Sido Mkoa wa Dar es Salaam, MacDonald Maganga, Ofisa Mtendaja Mkuu wa Kampuni ya Mlako Purified Ice Cubes, Joseph Mlay (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Jessica Makhuka.
Baadhi ya wanasemina wajasiriamali, wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei, wakati alipowatembelea na kuzungumza nao katika mafunzo yao ya wiki moja, Sido Mkoani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
Baadhi ya wanasemina wajasiriamali, wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei.
Meneja wa Sido Mkoa wa Dar es Salaam, MacDonald Maganga, akizungumza wakati akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (kushoto). 
Mwenyekiti wa semina ya wajasiraimali wa Sido, akitoa shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei. 
Meneja wa Kampuni ya kutengeneza manukato na vipodozi ya efa, Obed Musiba (kulia), akimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (wa pili kulia), kuhusu chupa za vipodozi na manukato zinazotengenezwa na moja ya mashine zao kwenye kiwanda chao. Kushoto ni Meneja wa Sido Mkoa wa Dar es Salaam, MacDonald Maganga.
Meneja wa Sido Mkoa wa Dar es Salaam, MacDonald Maganga (katikati), akimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (kulia), kuhusu mashine ya kutengenezea chupa za vipodozi na manukato (kushoto), alipotembelea sehemu za uzalishaji Ofisi za Sido Mkoa wa Dar es Salaam katika ziara hiyo. 
Fundi mitambo wa Kampuni ya PEC, Hans Mzalia (kulia), akimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (wa pili kulia), kuhusu mashine ya kuzalisha umeme kwa maji zinazotengenezwa na kampuni hiyo. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sido Incubator Programme Star Natural Products, George Buchafwe (kulia), amkimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (katikati), kuhusu vipuri vya mashine za kutengenezea sabuni vinavyotengenezwa na kampuni yake katika Ofisi za Sido Mkoa wa Dar es Salaam, jijini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Jessica Makhuka.   
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sido Incubator Programme Star Natural Products, George Buchafwe (kulia), amkimuonesha Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (katikati), baadhi ya malighafi zinazotumika kutengenezea sabuni kwenye kiwanda chake, ofisini hapo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Jessica Makhuka.  
Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya kuzalisha asali ya Miyombo Golden Resource, Kundaeli Urassa (kulia), akimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Dk. Charles Kimei (kushoto), kuhusu asali inayozalishwa na kampuni hiyo.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAZINDUA USAFI KWA FUKWE ZA BAHARI

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Wizara ya Maliasili na Utalii Nchini imezindua  rasmi kampeni ya kufanya usafi katika maeneo ya fukwe kwa ajili ya kuvutia utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na  Bodi ya Utalii nchini (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo pamoja na kufanya usafi kwenye Fukwe ya Hotel ya Ramada Resort, Mkurugenzi Msaidizi Leseni na Udhibiti Idara ya Utalii Rosada Msoma amesema kuwa utaratibu huu uliowekwa na Bodi ya Utalii Nchini ya kufanya usafi kutasaidia kuboresha na kuvutia watalii wengi zaidi.

Rosada ambaye ameshiriki kusafisha ufukwe wa Ramada Resort, amesema ana imani kampeni hiyo itakuwa endelevu kwani ni miongoni mwa mipango ya Serikali kuvutia utalii wa fukwe.

"Tutakapokuwa tunafanya usafi kwenye fukwe zetu,  zikiwa safi kiukweli zitavutia utalii na watalii wengi watakuja kutoka sehemu mbalimbali kwa wanaopenda matembezi lakini pia kwa wazawa ni fursa ya kufanya biashara,” amesema Rosada.

Rosada amesema kuwa, wao kama Wizara ya Maliasili zoezi la usafi walilizindua Mwezi April mwaka huu wakiwa na lengo la kuboresha maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kuvutia watalii nchini.

Mkurugenzi wa masoko wa TTB, Ernest Mwamaja amesema fukwe nyingi hazipo katika hali ya usafi na uchafu wake kwa asilimia kubwa ni makopo ya plastiki yanayoletwa na maji yanayotiririka kutoka kwa wananchi sehemu mbalimbali wanaotupa kwenye vyanzo vya maji kama vile mito.

Mwamwaja amesema kuwa mkakati huu umewekwa madhubuti kwa ajili ya kusafisha fukwe za bahari ya Hindi zilizopo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na leo ikiwa ni uzinduzi rasmi wamedhamiria kufikisha watalii Milioni 2 kwa mwaka ifikapo 2020 ambapo kwa sasa ni watalii 1.3 ndio wanaofika nchini.

"naweza kusema katika suala la usafi kuna haja ya bodi ya utalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hususani mahoteli kushirikiana kwa pamoja kutoa uelewa kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo yenye vyanzo vya maji ikiwemo na kuwaasa kuacha kutupa taka za plastiki hovyo , madhara yake ni makubwa na lengo letu ni kuongeza utalii kufikia idadi ya watalii milioni mbili kwa mwaka ifikapo 2020,” amesema Mwamaja.

Mwamwaja amesema kuwa wameanza na Hoteli ya Ramada Resort na muitikio ukiwa ni mkubwa na kwa pamoja wameshirikiana na Jeshi la Ulinzi (JWTZ) na Jeshi la Polisi Nchini katika kufanya usafi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa masoko wa Ramada Resort, Bharath Swarup amesema ni jambo jema kuona TTB inawashirikisha wadau katika kampeni kama hiyo ambayo inalenga kutunza mazingira ya fukwe.

“Kupitia fukwe ambazo zimetunzwa vizuri Serikali inaweza kupata mapato ya kodi lakini kama fukwe zimechakaa haziwezi hata kuvutia wageni/watalii,” amesema.

Naye Luteni Kanali JWTZ 43 Kikosi Jeshi Nelson Ponela amesema kuwa tofauti na masuala ya ulinzi wamekuwa wadau wakubwa wa kutunza mazingira wakiwa wanashiriki katika ufanyaji wa usafi wa sehemu mbalimbali na watashirikiana kwa pamoja kulinda mazingira ya fukwe.

Zoezi hili limeweza kushirikiana wakaazi wa Kata ya Mbezi Kutoka serikali ya mtaa ya Kilongawima wakiongozwa na Mwenyekiti wao Paul Richard, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Halmashauri ya Dar es Salaam Gasto Mwakwembe, Kamishna wa Polisi Msaidizi kutoka Makao Makuu Ferdinand Mtui na Afisa utalii Hifadhi za Bahari na Maeneo tengefu Hussein Ngenje.
Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) L, Hoteli ya Ramada Resort, Jeshi la Ulinzi, Wananchi wa Mtaa wa Mlongawima wakiwa katikaPicha ya pamoja baada ya kumalizika kwa usafi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Leseni na Udhibiti Idara ya Utalii Rosada Msoma akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kufanya usafi katika fukwe za Bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.
 Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) Godfrey Meena akiwa sambamba na Kamishna msaidizi wa Polisi Makao Makuu Ferdinand Mtui wakishiriki usafi kafika fukwe za bahari kwa ajili ya kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli ya Ramada Resort Bharath Swarup akiwa anashiriki usafi  katika uzinduzi wa kampeni ya kufanya usafi katika fukwe za bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania ( TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.
Wananchi na wafanyakazi mbalimbali wa Bodi ya Utalii na Hoteli ya Ramada Resort wakiendelea na usafi wakati wa uzinduzi wa kampenk ya kufanya usafi katika fukwe za Bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa  wazawa na wageni.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii (TTB) Ernest Mwamwaja  (katikatk) akiwa anafanya usafi wakati wa kampeni ya uzinduzi ya kufanya usafu katika fukwe za bahari  kwa ajili ya kuvutia utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort. Picha ya chini akiwa anazungumza na wanahabari baada ya kumaliza usafi.

DKT TIZEBA AWAHAKIKISHIA WASINDIKAJI WA PAMBA KUJIAMINI SOKO LIPO LA KUTOSHA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.(Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.
Wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na waendeshaji wa soko la bidhaa nchini Tanzania Merchantile Exchange (TMX) wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.

Na Mathias Canal, WK-Mwanza


Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amewahakikishia wanunuzi na wasindikaji wa zao la Pamba kuendelea kununua na kusindika pamba kwa wingi kutoka kwa wakulima kwani soko la zao hilo kwa sasa limeimarika kwa kiasi kikubwa.


Waziri Tizeba ametoa kauli hiyo juzi tarehe 9 Agosti 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya  wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwanza Hoteli Jijini Mwanza.  


Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwapatia uelewa wanunuzi wa zao la Pamba Mhe Tizeba alisema kuwa kuna njia mbadala zaidi ya waliyonayo sasa ya kuuza Pamba yao katika soko la bidhaa ambapo bidhaa hushindanishwa kutokana na ubora wake kwa wanunuzi walio wengi Duniani.


Alisema kuingia kwenye ushindani wa soko ni miongoni mwa njia muhimu na madhubuti kwao kwani itaongeza thamani ya zao hilo hivyo kuwa na kipato kikubwa kitakachoongeza tija na mafanikio ya kipato.


Tanzania Merchantile Exchange (TMX) inawakutanisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa kwa pamoja na kwa wingi ili washindane katika bei jambo ambalo litawafanya wauzaji kuuza bidhaa zao kwa kiasi kizuri cha fedha na kupelekea kupata bei nzuri.


Katika mkutano huo Mhe Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba aliwataka wanunuzi hao kujifunza namna ambavyo soko la bidhaa Tanzania Merchantile Exchange (TMX) linafanya kazi Kwa kupeleka kiasi cha Pamba kilichozidi kutokana na mkataba walioingia na wanunuzi wao Nje ya nchi ili kujionea manufaa yaliyopo. 


Hata hivyo Mhe Tizeba aliwataka wanunuzi hao kuendelea kununua Pamba kwa wakulima bila wasiwasi wowote, kwani soko la bidhaa litaweza kutumika kwa manufaa makubwa kuuza Pamba yao na kumhakikishia mkulima soko.


Alisema kuwa Katika ngazi ya uzalishaji ni muhimu sana ubora wa pamba ukaimarishwa ili soko la bidhaa liweze kufanya kazi kwa ufanisi.


Aidha, Mhe Tizeba ameilekeza TMX kukutana na kampuni zinazonunua pamba mmoja mmoja ili kubaini kampuni ambazo zitaweza kuanza msimu huu kutumia soko la bidhaa.

TIRA:WANANCHI KATENI BIMA YA KILIMO

$
0
0

Wakwanza kushoto (mwenye miwani) Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akiwa watumishi wengine kutoka Mamlaka hiyo wakitoa elimu kwa wageni waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane Jijini Arusha.
Mmoja wawaliotembelea banda la TIRA akiuliza swali kwa watumishi wa Mamlaka ya Bima nchini katika maonyesho ya nanenane Jijini Arusha.


Na. Vero Ignatus Arusha.


Wito umetolewa kwa wananchi kukata Bima ya kilimo ili iwasaidie wakati wa majanga.

Meneja Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Kanda ya kaskazini Eliezer Rweikiza amesema kuwa mamlaka hiyo inatimiza azma ya serikali ya kuhakikisha kilimo kinasimama, kinachangia pato la Taifa, kunakua pamoja na kuwasaidia wananchi

Amesema Serikali inafanya jitihada nyingi kuhakikisha kilimo kinapata bima, hivyo kupitia ofisi ya Kamishna mkuu wa bima nchini hatua nyingi zimefanyika ikiwemo sera ya bima ya taifa inayozungumzia maswala ya kilimo kwa ujumla, sheria zilizotungwa kuielezea huduma hiyo.

Hivyo mwanachi asiwe na wasiwasi kuhusiana na bima hii kwani uhusika wetu kwenye makampuni yanayotoa Bima iwe ni ya kilimo, Afya, mali au ya maisha lazima tusadajili sisi na kujua utendaji wao, huduma wanazozitoa niyo sababu tupo karibu yao"Alisema Rweikiza.

Amesema Bima hiyo ipo mahususi kwa watu wanaojihusisha na kilimo ambayo inakinga majanga yanayotokana na shughuli za kilimo.'' Majanga haya yanatofautiana kutoka eneo moja kwenda nyingine, majanga ya mvua nyingi, mabadiliko ya hali ya hewa, mafuriko, tetemeko la ardhi, na majanga yanayohusiana na wizi shambani hivi vyote ukiwa na bima hii unaweza ukapata fidia. "alisema.

RISALA YA MWENYEKITI WA NEC KUHUSU UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI MDOGO

ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Glogu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amechagia kiasi cha shilingi milioni 4.7 katika kata ya Nyamato, mifuko 250 ya Saruji kwaajili ya ujenzi wa vituo vya afya, shule na nyumba za Wauguzi hii ni katika kuhakikisha huduma za elimu na afya zinaimarika na kuwa faafu kwa wananchi wote wa Mkuranga.

Wakati huo huo Ulega pia ametoa amechangia shilingi laki sita kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Kimanzichana na ameahidi kutoa kiasi cha milioni 2 kwaajili ya vikundi vya wanawake wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa utoaji wa mchango huo Ulega ameeleza kuwa ushirikiano wa wananchi unampa nguvu ya kufanya makubwa zaidi katika kuleta maendeleo na amewataka watendaji kufuata kasi iliyopo na kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa juhudi anazoonesha katika kuleta maendeleo nchini.

Pia Ulega amesema kuwa yupo pamoja na wananchi wa Mkuranga wakati wote na katika kufanya kila jambo litakaloleta maendeleo bila kujali itikadi wala chama.Katibu wa CCM Wilaya ya Mkuranga, Abihudi Shila ameeleza kuwa wanachama waendelee kufanya kazi na viongozi waliopo na amempongeza Rais kwa juhudi anazozifanya katika kuleta maendeleo hasa katika kukemea rushwa na ufisadi pia katika ujenzi wa miradi ya kimaendeleo nchini kama miradi ya umeme na miundombinu.

Aidha amemshukuru Rais kwa kumteua Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah Ulega katika kumsaidia kuongoza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kama naibu Waziri na wanashukuru kuona mbunge wao anafanya kazi kwa dhati katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Aidha Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamato Idd Kimbapule amempongeza Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega kwa kutoa kipaumbele katika huduma muhimu kama afya, elimu na miundombinu na ameendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha shughuli za ujasiriamali kwa akina mama zinakuwa ili waweze kujipatia kipato.

Kimbapule amewashauri wananchi kuonesha ushirikiano kwa viongozi wa mfano wa Ulega ambaye amejitoa katika kuwahudumia wananchi ili kuweza kujenga maendeleo kwa kasi zaidi. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega akizungumza na wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhi mifuko 250 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya shule pamoja na nyumba za waganga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega  (kulia) akikabidhi Shilingi  laki sita kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kimanzichana ambapo  pia aliahidi kuongeza milioni mbili kwa ajili ya vikundi vya wajasiliamali.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega akiwakabidhi kadi za (CCM) wanachama  waliorudi wakitokea chama cha CUF  Abed Majala, Modesta Antoni katika kijiji cha Kimanzichana Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

MASHABIKI WA SOKA RUANGWA WAFURIKA KUSHUHUDIA MECHI YA SIMBA SC NA NAMUNGO FC

$
0
0








Mashabiki wa soka, wakiwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu ya Simba SC na Namungo FC kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Agosti 11.2018 (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)
Mashabiki wa soka, wakiwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu ya Simba SC na Namungo FC kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Agosti 11.2018 (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)

GESI ASILIA KUTUMIKA MAJUMBANI MKOANI MTWARA – KALEMANI

$
0
0

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa nne kushoto) mara bada ya kuzidua mradi wa ujenzi wa mtambo wa usambazaji wa gesi asilia majumbani mkoani Mtwara. Wengine katika picha ni viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakiwa pamoja na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (wa tatu kulia) na wa kwanza kulia Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia) akifatilia jambo kwenye ramani (haipo pichani) ya jinsi gesi hiyo itakavyo sambazwa majumbani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali serikalini pamoja na wabunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (mwenye kilemba) na wa nne kushoto ni Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota.
Wananchi mbalimbali wakiwa katika mkutano wa uziduzi wa mradi wa ujenzi wa mtambo wa usambazaji wa gesi asilia majumbani mkoani Mtwara wakimzikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalwmani (hayupo pichani).

Na Rhoda James- Mtwara

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani jana tarehe 10 Agosti, 2018 amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa Mtambo wa kusambaza Gesi Asilia majumbani mkoani Mtwara. Waziri Kalemani, amefanya zoezi hilo leo katika shule ya Ufundi ya Mtwara mara baada ya kuzidua MW4 za umeme katika kituo cha Umeme cha Mtwara.

Waziri Kalemani alisema kuwa, ujenzi wa mtambo huu umegharimu jumla ya billioni 1.5 kwa ajili ya kuwapelekea watumiaji wa awali wasiopungua 150 ambao bada ya miezi mitatu wataanza kutumia gesi hiyo majumbani. Aliongeza kuwa matumizi ya gesi asilia ni madogo sana yaani ni kama hayapo, kwa kuwa wananchi wengi wanatumia kuni na mkaa kwa wengi kuliko gesi.

“Sasa mtugi wa gesi ni takriban shilingi 55,000/- lakini ukitumia gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani itakuwa shilingi 25,000/- na utatumia kwa mwezi mzima hivyo ni nafuu kwa mwananchi wa Tanzania,” alisema Wazari Kalemani.

Mwezi mei tulianza matumizi ya gesi manyumbani lakini leo tumeanza matumiz ya gesi asilia katika mkoa wa Mtwara. “hayawi hayawi yamekuwa,” alisema Waziri Kalemani. Aidha, Waziri Kalemani aliendelea kueleza kuwa, Kuna magari zaidi ya 100 wanatumia gesi asilia jijini Dar es Salaam, hivyo kuazia mwezi Machi mwaka kesho (2019) tutaanza usanifu ili magari ya mkoa wa Mtwara nayo yaanze kutumia gesi asilia.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa, anawakaribisha wananchi wa Mtwara na Lindi kuwekeza zaidi kwenye shughuli za uchumi kwa kuwa masuala ya viwanda yanahitaji umeme na matumizi ya kawaida yanahitaji umeme na nimatumaini yake kuwa wananchi watatumia fursa hii vizuri.

Waziri Kalemani pia alitoa wito kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanza kutoa elimu mara moja kwa wiki kwa Chuo cha Ufundi cha Mtwara ili kuhakikisha kuwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo wanapata uelewa mzuri katika matumizi ya gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amempongeza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema kuwa sasa wananchi wa Mtwara wataanza kunufaika na gesi asilia. Mkuu wa Mkoa Byakanwa alieleza kuwa, umeme tunaoutumia kwa sasa, asilimia 60 inatokana na gesi asilia na sasa gesi hii inaweza kutumika kwa matumizi ya majumbani na wananchi watanufaika moja kwa moja na gesi asilia inayozalishwa kutoka Mkoa wa Mtwara.

Akizungumza katika uziduzi huo alisema kuwa, sasa wananchi wa Mtwara watafaida kwa kutumia gesi hii kwa bei nafuu, na faida nyingine ni kuhifadhi mazingira yetu vizuri maana tutaepukana na ukatajiwa miti. Kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Mkoa Byakanwa alitoa wito kwa wananchi kuweka mazingira wezisha ya kupata gesi majumbani kwetu.

“Tuboreshe miundombinu ili tupata gesi kwa urahisi, lakini pia tuwe na nyumba zinazokidhi viegezo ili usambazaji wa gesi asilia ufike kwa urahisi majumbani kwetu,” alisema Byakanwa. Akizungumza katika uziduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Byakanwa aliwaambia wanafunzi wa Shule ya Ufundi ya Mtwara kuwa Serikali imehakikisha kuwa shule hii inakuwa kati ya taasisi ambayo itafaidika na matumizi ya gesi asilia.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia alimpongeza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard kalemani kwa kuwa msikivu na mwepesi wa kutimiza ahadi zake kwa wabunge wezake.

Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia alitoa wito kwa TPDC kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa wananchi wa Mtwara na Lindi ili kuondoa uoga kwa wananchi na kuwaelimisha matumizi bora ya gesi asilia na hivyo kufaidika na gesi hiyo ipasavyo.

UJUMBE WA UAE KUTEMBELEA MIRADI MBALI MBALI PEMBA.

$
0
0


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Abdalla Mzeee ya Mkoani Mkoa wa Kusine Pemba Dk.Haji Mwita (kushoto) akifuatana na Ujumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ulipofika kutembelea Hospitali hiyo leo kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 10/08/2018.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Abdalla Mzeee ya Mkoani Mkoa wa Kusine Pemba Dk.Haji Mwita (katikati) akifuatana na Mkurugenzi Mkuu katika masuala ya taalum wa idara ya mambo ya afya katika kampuni ya afya Abudhabi Dk.Ali Ali Obeid wakati Ujumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ulipofika kutembelea Hospitali hiyo leo kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 10/08/2018.
Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Najla Al- Kaabi akiuliza suala kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd.Shomari Omar Shomari wakati Ujumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ulipofika kutembelea mradi wa Bandari ya Mkoani Pemba leo kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 10/08/2018.
Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za umoja wa Falme za Kiarabu(UAE) ulipotembelea Barbara ya Mkoani- Chakechake leo,wakati ujumbe huo ukiwa nchini kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 10/08/2018.
Mkuu wa Mkoa wa Kusine Pemba Mhe.haemedi Suleiman Abdalla akifuatana na Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Najla Al- Kaabi (kukhoto) pamoja na Ujumbe wake wa Wataalamu kutoka Nchi hizo ulipofika kutembelea mradi wa Barabara ya Mkoani -Chakechake kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 10/08/2018.

NEWZ ALERT: MTATIRO ABADILI GIA ARIDHINI,AONDOKA CUF,ATANGAZA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

JUHUDI za Rais Dk.John Magufuli za kuleta maendeleo zimesababisha Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi(CUF), Julius Mtatiro kuamua kubadili gia aridhini kwa kujivua uanachama wa chama hicho.

Na kwamba amesema kuanzia leo atajikita katika kushiriki katika kufanya siasa za maendeleo na hasa kuunga mkono jitihada za Rais.Wakati anatangaza uamuzi huo ametaja sababu tano zilizomsukuma kufanya uamuzi huo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mtatiro ametaja sababu hizo ambapo ya kwanza ni  kutoridhishwa na hali ya ushiriki na mchango wake kwenye siasa za CUF.

Amesema sababu ya  pili ni mgogoro wa kiuongozi unaoendelea kukikumba chama hicho na sababu ya tatu ni kutoridhidhwa na ushiriki wake kama kijana na kiongozi katika kuchochea maendeleo ya nchi.

 Wakati jambo la nne likiwa ni ajenda ya maendeleo ya nchi, huku jambo la mwisho likiwa ni mustakabali wake kuhusu masuala ya siasa.

“Katika tafakari yangu ya kuhama, nilipitia maeneo kama matano ambayo nimefanyia kazi, niliangalia ushiriki na mchango wangu kwenye siasa za CUF, mgogoro unaoendelea kukikumba CUF, eneo la tatu ambalo nimelitafakari kwa upana sana ushiriki wangu kama kijana na kiongozi katika kuchochea maendeleo ya nchi, jambo la nne ajenda ya maendeleo ya nchi, la mwisho ni ustakabali wangu kuhusu masuala ya siasa,” amesema Mtatiro.

Mtatiro amesema ametumia muda wa mwezi mmoja kutafakari uamuzi huo, na kubaini kwamba huu ni muda wake wa kutumia talanta alizo nazo kumuunga mkono Rais John Magufuli kupitia CCM.Aliekuwa Mwenyeki wa kamati ya uongozi wa chama cha wananchi CUF,Julius Mtatiro chini ya Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar as Salaam kuhusu na tarajio lake la kujiunga na chana cha Mapinduzi (CCM).Waandishi wa habari wakimsikilza aliyekua Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi wa chama cha wananchi CUF Julius Mtatiro (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).

WAZIRI LUGOLA AENDA KUHANI MSIBA NYUMBANI KWA MWANAHABARI MAREHEMU SAGATI, MWIBARA WILAYANI BUNDA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mwanahabari marehemu Shadrack Sagati, katika Kijiji cha Mwiruruma, Kata ya Iramba, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Waziri Lugola alifika msibani ili kutoa pole kwa wafiwa kijijini hapo, leo Jumamosi Agosti 11, 2018. Wapili kutoka kulia ni Mfungo Sagati, baba wa marehemu, na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isaka Mahera. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto) akimpa mkono wa pole Mfungo Sagati, baba wa Mwanahabari marehemu Shadrack Sagati, mara baada ya Waziri huyo kufika cha Kijiji cha Mwiruruma, Kata ya Iramba, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani wa Mara kwa ajili ya kutoa pole kwa familia.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na Dora Mwishangi (kushoto), mama mdogo wa Mwanahabari marehemu Shadrack Sagati, katika Kijiji cha Mwiruruma, Kata ya Iramba, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, leo Jumamosi Agosti 11, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isaka Mahera. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (katikati) akisaini kitabu cha maombolezo, alipofika nyumbani kwa Mwanahabari marehemu Shadrack Sagati, aliyefariki kwa ajali ya gari mkoani Geita Julai 31, 2018. Kushoto ni Mfungo Sagati, baba mzazi wa marehemu, na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isaka Mahera. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WEZI WA MAJI YA DAWASCO WAKAMATWA TEMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) leo limeendesha operesheni ya kuwakamata wale wote waliojiunganishia maji na mkufanya biashara ya maji bila ya kuwa na kibali. Akizungumza Kaimu Meneja wa DAWASCO mkoa wa Kimara, Frank Sulley amesema wameamua kuendelea na operesheni yao maana watu hao wamekuwa wakihujumu shirika hilo kwa kuiba maji huku wakiharibu miundo mbinu. 

"Leo tupo eneo la Kimara Temboni na tumeweza kumkatama mama (jina kapuni) ambaye alikuw akifanya biashara ya maji na kuharibu miundo mbonu, kwa kukata bomba na kujaza tanki lake na kufanya biashara ya kuuza maji ambapo amekuwa akiuza tsh 6,000 kwa tanki la lita 1,000,' amesema Sulley. 

Amesema kuwa kumekuwa na mchezo wa kujiunganishia maji kwa njia ya kinyemela kwa kukata bomba nyuma ya mita na kutumia huku mita ikiwa haisomi jambo linalohujumu uchumi wa shirika hilo. Aliongeza kuwa amewataka wateja kujitokeza kujisalimisha wale wote waliojiunganishia kinyemela kabla ya muda haujaisha.  Wafanyakazi wa DAWASCO wakifukua shimo kuweza kupaini jinsi uunganishani wa maji kinyemela ulivyofanywa na mkazi wa Kimata Temboni jijini Dar es Salaam wakati wa oparesheni ya kuwabaisni wanaofanya biashara ya maji kinyemela iliyofanyika mapema leo. Kaimu Meneja wa DAWASCO mkoa wa Kimara, Frank Sulley akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi stali mpya ya wizi wa maji unavyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Moja ya Tanki la maji lilipo ardhini linalotumika katika wizi wa maji na kuwauzia watu wa magari makubwa (maboza).

Moja ya muunganiko wa maji mabomba ya maji unaopeleka maji kwenye tanki. 
Gari hili lilikutwa eneo la tukio likijiandaa kupandisha maji na kuenda kusambaza kwa wateja, ambapo wao wamekuwa wakinunua maji kwa tsh 6,000 kwa tanki la lita 1,000 na kwenda kuliuza mtaani kwa tsh 12,00-15,000/- 
Bomba la maji lililokuwa likitoa maji kwa winhi ambapo walikuwa wameunganisha kupeleka.

BENKI YA KILIMO NCHINI YAWAHIMIZA WATANZANIA KUJIKITA KWENYE KILIMO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo (TADB) Bw. Japheth Justine akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James wakati wa kukabidhi Matrekta kwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA cha Mkoani Morogoro leo kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha Mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo (TADB) Bw. Japheth Justine mwenye miwani nyuma pamoja na viongozi wengine mara baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika mjini Kibaha.



Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAIMU Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo(TADB) Japheth Justine ameshauri Watanzania kujikita kwenye kilimo kwani kinalipa huku akifafanua wao wapo tayari kutoa fedha asilimia 80 kwa wanaohitaji kukopa matrekta na asilimia 20 iliyobaki itatolewa na mnunuzi.

Akizungumza leo wilayani Kibaha mkoani Pwani mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James , Mkurugenzi wa TADB Justine amefafanua kikubwa ambacho wanataka kuona ni mkulima kufanikiwa kupitia mazao yake na ndilo miongoni mwa jukumu lao.

Akifafanua zaidi Justine amesema wameshatoa mkopo wa Sh.bilioni 41.1 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo na wapo kwenye mikoa mitatu ambayo ni Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma na siku za karibuni watafungua tawi lingine mkoani Mbeya na lengo lao ni kuwafikia wananchi kokote walipo

Pia amesema wameshafanya makubaliano na Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) kwa lengo la kusaidia wale wanaonunua matrekta kwamba benki ya kilimo itaingiza asilimia 80 ya mkopo na mnunuzi atatoa asilimia 20.Ameongeza kwamba wakulima wamefanya vizuri kwenye zao la pamba huku akielezea lengo lao ni kuchoche hamasa kwenye kilimo na kubwa zaidi ni kumuondoa mkulima kwenye jembe la mkono.

“Pale ambapo tutafanikiwa kumtoa mkulima kwenye jembe la mkono na kumpa mashine ambazo zitamsaidia kuongeza tija na kumpa faida hicho ndicho ambacho tunakihitaji.“Kilimo au mkulima ni muwekezaji na hivyo tunataka kuona mkulima anapata faida .Hivyo kwa wakulima waliokuwa kwenye bodi ya pamba watapa mkopo wa asilimia 80,”amesema.

Ameongeza wataanza na matrekta 500 ambayo hiyo itafanyika muda si mrefu kwa kuwapa wakulima waliofanya vema kwenye kilimo cha pamba.Justine amesema mpango wao mkubwa ni kwenda kuziambia benki za biashara kuingiza asilimia 50 na wao wataweka asilimia 50 katika kumkopesha mkulima.

Pia amesema wanaishukuru Serikali kwa kuzindua mpango wa pili kwenye sekta ya kilimo na watahakikisha wanafanikisha malengo ya Serikali.Amesema benki ya kilimo itahakikisha inawakopesha wakulima kwa bei nafuu na kusisitiza kuwa kilimo kinalipa na hivyo Watanzania wajikite kwenye kilimo.

Amesisitiza wameanza na wakulima wa pamba katika kutoa hiyo asilimia 80 na iwapo mpango huo utafanikiwa basi watakwenda kwenye maeneo mengine.Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango , James amempongeza Mkurugenzi huyo wa benki ya kilimo kwani tangu alipoteuliwa na Rais amesimamia mambo mengi aliyoagizwa kuyafanya.

Amesema kwa sasa benki hiyo ina fedha za kutosha kwa ajili ya kuwasaidia wakulima nchini.

TIGO WASHINDA CHETI CHA USHIRIKI KWENYE MAONESHO YA NANENANE DODOMA

$
0
0

Meneja Usambazaji wa Tigo Dodoma na Kondoa, Gidion Morris akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baaada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi kipengele cha mawasiliano kwenye maonesho ya Nanenane juzi mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi cheti cha Kipengele cha Mawasiliano Kanda ya Kati kwa Meneja Usambazaji wa Tigo, Gidion Morris kwenye sherehe ya maadhimisho ya maonesho sikukuu ya wakulima Nanenane viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma juzi.

ASASI ZA KIRAIA ZAOMBWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUTATUA CHANGAMOTO MBALIMBALI

$
0
0
Asasi za kiraia zimeombwa kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa upatikanaji wa huduma ya maji. 

Diwani wa Kata ya Kwembe wilayani Ubungo, Dweza Kolimba amesema asasi za kiraia zina nafasi kubwa ya kuleta maendeleo katika jamii kwa kushirikiana na wananchi na watendaji wa serikali. 

Akizungumza katika semina iliyoandaliwa na asasi ya Pakacha kwa ajili ya kujadili utatuzi wa changamoto ya maji, kuanzia ufuatiliaji wa rasilimali fedha na utekelezaji wake, Kolimba amesema upatikanaji wa maji katika kata yake umekuwa wa shida, hivyo kupitia asasi kama ya Pakacha, wananchi wanaweza kuelimishwa kushirikiana na viongozi ili kutatua kero hizo. 

Amesema upatikanaji wa maji umekuwa wa shida katika kata yake, huku akisema kuwa wananchi wengi watapata maji baada ya mradi mkubwa wa Luguruni kukamilika. “Tayari mabomba yamesambazwa, hivyo tunaomba mradi huu uishe mapema ili watu wapate maji,” amesema Kolimba. Everyline Francis, mjumbe wa kamati ya maji ya Kata ya Kwembe amesema jamii ipewe elimu ya kutunza vyanzo vya maji na kuzuia uharibifu wa mazingira. 

Upatikanaji wa maji umekuwa na changamoto katika kata za Kwembe, Msigani na Kibamba, hivyo asasi ya Pakacha, kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society kulazimika kutoa elimu kwa wananchi juu ya ufuatiliaji na utunzaji wa vyanzo vya maji. 

Akizungumza kwa niaba ya Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Ubungo, Hamad Sendekwa amesema ameomba wananchi washirikiane na watendaji ili kutatua kero za maji na jitihada zinaendelea kuhakikisha huduma hiyo muhimu inapatikana wakati wote. Alisema ushirikiano huo utasaidia kuibua changamoto zinazokwamishwa na rasilimali fedha au kutowajibika kwa baadhi ya watendaji. 

Alisema asasi zinaweza kuleta mabadiliko kwa kufuatilia miradi ya maji, ambayo inakwamishwa kwa sababu mbalimbali na kuwaelimisha wananchi jinsi ya kulinda miundo mbinu ya maji na ufuatiliaji wake. Katibu wa Pakacha, Haroun Jongo amesema lengo la semina hiyo ni kutoa msukumo kwa utelekezaji wa miradi ya maji kwa kuibua hoja kwa wananchi, kwa lengo moja tu, kuleta maendeleo. 

Amesema lengo la semina hiyo ni kuleta jukwaa la majadiliano kati ya viongozi, wananchi na watendaji wa serikali za mitaa ili kutatua kero za maji kwa wananchi kupitia mfumo wa Pets. Pets ni mfumo unaowezesha ufuatiliaji matumizi ya rasilimali za umma zinazotoka Serikali Kuu au halmashauri kwa maendeleo ya wananchi kuanzia ngazi za mitaa hadi kata na kuendelea. 
Mwezeshaji, Enock Daniel Kijo akitoa mafunzo kwa washiriki wa semina ya maji iliyoandaliwa na asasi ya Pakacha Group kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society kwa kata za Kwembe, Msigani na Kibamba za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images