Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live

MGALU AMUAGIZA DC SUMBAWANGA KUTUMIA MAMLAKA YAKE KUWATUPA NDANI SAA 48 WASIMAMIZI WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA REA

0
0
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akihutubia wananchi wa kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, leo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya tatu. (0163 -205, 207)
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akihutubia wananchi wa kijiji cha Kilyamatundu, tarafa ya Kipeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, leo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya tatu. (357,361 na 371)
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwahoji maswali wasimamizi kutoka kampuni ya kampuni ya Nakuroi Investment inayosuasua katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa REA awamu ya tatu katika vijiji vya mkoa wa Rukwa, leo mbele ya wananchi wa kata Mtowisa, Sumbawanga mkoani Rukwa. (0179 - 80)
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akitoa ufafanuzi wa jambo kwa msimamizi wa kampuni ya Nakuroi Investment kuhusu ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa umeme katika kijiji cha Kilyamatundu wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, ambapo yupo katika ziara ya kikazi mkoani humo. (417)
Baadhi ya watumishi wa Shirika la umeme nchini, Tanesco mkoawa Rukwa wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Subira Mgalu wakati aliwahutubia wananchi wa kata ya Mtowisa mkoani Rukwa leo, ambapo yupo katika ziara ya kikazi ya kukaguautekelezaji wa miradi ya REA awamu ya tatu.(0150)




Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Dk. Halfan Haule kutumia mamlaka yake kuwatupa ndani saa 48 wasimamizi wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini (REA) awamu ya tatu wa Kampuni ya Nakuroi Investment iwapo watasuasua katika ujenzi wa miundombinu ya umeme wilayani humo.

Naibu Waziri huyo, ametoa agizo hilo leo akiwa katika kijiji cha Kilyamatundu kilichopo mpakani mwa mikoa ya Mbeya na Songwe tarafa ya Kipeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi inayolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya tatu mkoani humo.

Kabla ya kutoa agizo hilo, Naibu Waziri huyo alionyeshwa miundombinu inayowezesha upatikanaji wa umeme katika kijiji jirani cha Kamsamba iliyopo umbali wa mita 100 na kuonyesha kushangazwa kwanini Kijiji cha Kilyamatundu kinashindwa kunufaika na huduma ya umeme kwa kuwa miundombinu ipo jirani kiasi hicho.

"Mkandarasi nataka nguzo na vifaa vingine vifike hapa Alhamisi ijayo kama ulivyoahadi na ujenzi wa miundombinu ya umeme ianze mara moja,mkuu wa wilaya hakikisha inatumia mamlaka yako kuwatupa ndani saa 48 hawa jamaa kama watasuasua kutekeleza mradi huu, sisi lengo letu umeme upatikane hapa kijijini haraka iwezekanavyo" alisema

Aliongeza kwamba hatua hizi zichukuliwe kwa kuwa kampuni hii imekuwa ikishindwa kutekeleza mradi huu kwa wakati, hivyo kuonyesha dalili ya kushindwa kumaliza kwa muda uliopangwa.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya hiyo Dk. Haule aliahidi kutekeleza agizo hilo kwa kuwa serikali imechoka kuendelea kuchonganishwa na wananchi kwa uzembe wa baadhi ya watu hivyo sheria lazima ichukue mkondo wake. 

Aidha, Mbunge wa jimbo hilo Iginas Malocha alisema kuwa iwapo eneo hilo litapata huduma ya umeme ni wazi kwamba thamani ya mazao yao kama vile mpunga itaongezeka na wakulima kuwa na uhakika wa soko.

MEYA MWITA ATEMBELEA HOSPITAL YA AGA KHAN JIJINI HAPA LEO

0
0


MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amefanya ziara katika hospitali ya Aga Khan ya jijini hapa na kuwaona wagaonjwa sambamba na kupata nafasi ya kuona maendeleo ya mradi wa upanuzi wa hospitali hiyo ulio mbioni kukamilika .

Katika ziara hiyo , Meya Mwita amekutana na uongozi wa juu wa Hospitali hiyo ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utoaji Huduma za Afya Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki, Sulaiman Shahabuddin ambapo walipata nafasi ya kuzungzumza mambo mbalimbali.

Meya Mwita ameipongeza Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan Tanzania kwa kuamua kuwekeza katika Mkoa wa Dar es Salaam hususani sekta ya Afya ambapo bado changamoto ni nyingi jijini hapa pamoja na nchi nzima.

Aidha Meya Mwita amefarijika kuona hosipitali hiyo imewekeza katika vifaa tiba vya kisasa zaidi kuwemo nchini pamoja na uwepo wa Watanzania wengi katika eneo la utoaji huduma za viwango vya juu kabisa Tanzania.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za Huduma za Afya Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki Sulaiman Shahabuddin amemshukuru Meya Mwita kwa kutenga muda wake na kutembelea hospitali hiyo.

Amefafanua kuwa "ni faraja kwetu sana kukuona mahali hapa Mstahiki Meya ,Hospitali hii ni kwa ajili ya Wana Dar es Salaam na Watanzania wote, Ninacho mshukuru Mungu ni kuona hospitali hii sasa ikianza kuhudumia hata mataifa ya jirani kama Comoro, Zambia, Malawi, Msumbiji " amesema.

" Sisi tumedhamiria kuendelea kuwekeza katika eneo la Afya kwa kiasi kikubwa na hadi sasa ukiachilia mbali ujenzi wa hospitali hii ulio gharimu takribani shilingi bilioni 192 za Kitanzania unaokwenda sambamba na uwekaji wa vituo vya Afya 35 nchi nzima ambamo katika mkoa wa Dar es Salaam pekee hadi sasa tuna idadi ya vituo 11 vinavyofanya kazi na kuendeshwa kisasa kupitia mifumo ya kiteknolojia na mawasiliano kuwezesha uwepo wa huduma bora kabisa" ameongeza.

Awali Meya Mwita aliahidi kushughulia chamgamoto mbalimbali za nje ya hosipitali ikiwepo kuwapatia kibali maalum cha Ujenzi wa Daraja la juu ili kuvusha watu kutoka upande wa maegesho ya magari hospitalini hapo kwenda eneo la majengo ya hospitali,.

Aidha aliahidi kufutilia upatikanaji wa kibali kwa hosipitali hiyo kujenga maegesho ya kisasa ya magari kwa aajili ya wagonjwa eneo la ufukwe wa bahari ya Indi, kufuatilia tozo za maegesho eneo lilijengwa na hosipitali na kuzindoa rasmi kama sehemu ya makusanyo ya jiji kwani hilo litawasaidia madaktari na wahudumu katika hosipitali kuongeza morali na ufanisi katika utendaji.

Sambamba na hilo Mstahiki Meya ameahidi kushughulia kwa pamoja maboresho ya eneo la mbele ya hosipitali hiyo kwa kushirikiana na hosipitali kutafuta namna mbadala ya kuwasadia wenye biashara ndogondogo katika eneo kuendesha katika hali ya ubora zaidi.

Katika ziara hiyo Meya Mwita aliambatana na Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia na kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi ya Afya Aga Khan Tanzania ambapo alionekana kufuruhishwa na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa huduma za afya nchini hasa kwa Aga Khan kuweza kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha ili kuboresha mifumo ya utaoji huduma za Afya kwa nchi nzima.

Mwishoo.

Imetolewa leo Agosti 9 na Christina Mwagala , Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji

PASS VINARA KATIKA MAONESHO YA NANE NANE KWA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI

0
0
Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Nane nane na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Benjamini Mkapa akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya Kilimo nchini (PASS) Killo Lusewa baada ya taasisi hiyo kuibuka kinara wa maonesho hayo kwa taasisi zisizo za Kiserikali,maonesho yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
  Mkurugenzi wa Biashara wa taasisi ya kusaidia Sekta Binafsi katika Kilimo (PASS) akionesha cheti cha ushindi baada ya taasisi hiyo kushika nafasi ya kwanza kwa taasisi zisizo za kiserikali na kukabidhiwa na Rais Mstaafu,Benjamini Mkapa.
Wafanyakazi wa Taasisi ya kusaidia sekta Binafsi katika Kilimo(PASS) wakifurahia mara baada ya kutangazwa washindi wa kwanza  kwa taasisi zisizo za Kiserikali katika maonesho ua nane nane ambayo yamefanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Wafanyakazi wa Taasisi ya kusaidia sekta Binafsi katika Kilimo(PASS) wakifurahia kwa pamoja na wanufaika wa msaada wa mikopo kutoka katika taasisi hiyo mara baada ya kutangazwa washindi wa kwanza  kwa taasisi zisizo za Kiserikali katika maonesho ua nane nane ambayo yamefanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Luhaga Mpina akikabidhi cheti kwa Meneja wa Taasisi ya kusaidia sekta Binafsi katika Kilimo(PASS) kanda ya Kaskazini ,Hadija Seif mara baada ya tasisi hiyo kutangazwa washindi wa pili kwa taasisi zisizo za Kiserikali katika maonesho ua nane nane ambayo yamefanyika mkoani Morogorogo . 
Meneja wa Taasisi ya kusaidia sekta Binafsi katika Kilimo(PASS) kanda ya Kaskazini ,Hadija Seif akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa taasisi hiyo mara baada ya kutangazwa washindi wa pili kwa taasisi zisizo za Kiserikali katika maonesho ua nane nane ambayo yamefanyika mkoani Morogorogo . 
Cheti kilichokabidhiwa kwa PASS,Morogoro. 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa mkoani Simiyu.

SPIKA NDUGAI KUTEMBELEA VIJIJI 12 NDANI YA JIMBO LAKE

0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa akilisikiliza kwa makini kikundi cha ngoma ambacho kilitoa buruduni katika Kjiji cha Njoge wilaya ya Kongwa. Spika anatarajia kutembelea vijiji kumi na mbili katika ziara yake wilayani humo.
Wananchi mbalimbali wa Kijiji cha Gomaye wakimsikiliza kwa makini Mheshimiwa Spika Job Ndugai ambaye alifanya ziara katika Kijiji hicho mapema leo.
Wananchi mbalimbali wa Kijiji cha Gomaye wakimsikiliza kwa makini Mheshimiwa Spika Job Ndugai ambaye alifanya ziara katika Kijiji hicho mapema leo.

SIERRA LEONE YAFURAHISWA NA HATUA KUBWA YA MAENDELEO YANAYOFANYWA NA NSSF NCHINI

0
0
Nchi ya SIERRA LEONE imefurahishwa na hatua kubwa ya maendeleo yanayofanywa na mfuko wa Taifa wa Hifadhi wa Jamii NSSF nchini na kwamba italazimika kuiga baadhi ya masuala ikiwemo kuanzisha kitengo kipya cha viatarishi katika mfuko wao ili kuongeza ufanisi na kuzuia kutokea kwa majanga yanayoweza kujitokeza .

Hayo yamesema na  Naibu Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Bima SIERRA LEONE ,Mohammed Gondoe alipotembelea katika makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF, William Erio ambapo amesema kuna mambo mazuri yamefanywa na NSSF hivyo hawana budi kujifunza .

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa NSSF William Erio amesema Tanzania na SIERRA LEONE zitaendelea kushirikiana na kuwa na mahusiano mazuri katika kuhakikisha wanabuni mipango ya kusaidia ukuaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii ya Taifa. 

Mifuko ya Hifadhi ya jamii ya TANZANIA na SIERA LEONE imekuwa ikishirikiana kwa muda mrefu jambo ambalo limesaidia kuongeza ufanisi na weledi katika utendaji kazi wake kwa wafanyakazi wa mifuko hiyo. 

Gondoe na wajumbe wenzake kutoka nchini SIERA LEONE wapo nchini kujifunza masuala mbali mbali ya hapa nchini ikiwemo mfumo wa utoaji mikopo ya elimu ya juu uliopo chini ya wizara ya elimu,sayansi na teknolojia. 

Imetolewa na Idara cha Uhusiano na Masoko.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii-NSSF
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ,William Erio(kulia) akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Naibu MKurugenzi wa mfuko wa Hifadhi  ya Jamii na Bima  wa Sierra Leone,Mohammed Gondoe aliyemtembelea  leo katika makao makuu ya ofisi ya NSSF iliyopo jijini Dar es salaam

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA UINGEREZA (DFID) MHE. PENNY MORDAUNT IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha albamu ya picha Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt inayoonesha Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyobomolewa kabisa na Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera lililotokea Septemba 10, 2016  ambayo imejengwa upya na serikali ya Uingereza kupitia mpango wake wa maendelo  ya elimu kupitia UKAid/DFID. Picha hizo zinaonesha shule hiyo baada ya tetemeko, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi siku ya mwaka mpya wa 2017  na inavyoonekana sasa baada ya kujengwa upya. Mhe. Mordaunt, ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi, alimtembelea  Rais Dkt. Magufuli akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago cha "Umoja"  Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke aliyeongozana na , Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana pia na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy aliyeongozana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke,  walipomtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari kuishukur serikali ya Uingereza  kwa misaada yake  mbalimbali ikiwemo Shilingi Bilioni 307 kwa kuunga mkono juhudi zake za kuopambana na rushwa pamoja na kuboresha sekta za afya na elimubaada ya kukutana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.

Picha na IKULU

UKAGUZI WA CAG KATIKA MASHIRIKA YA TBC NA TANESCO 2016/217

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) halijawahi kupata gawio kutokana na umiliki wa hisa 35 mtaji wa Star Media LTD tangu mwaka 2013 kwa sababu ya star Media kuripoti hasara ya sh.bilioni 61.

Akizungumza katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi na Kukusanya maoni kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2016/2017 iliyofanyika Katika Ukumbi wa PPF Tower Mkaguzi wa Mashirika ya Umma Pascal Mahwago amesema kuwa star media iliripoti uchakavu wa vitu na kufanya TBC kukosa gawio licha ya kuwa na hisa.

Amesema kuwa ushauri wa CAG ulitaka kuhakikisha shughuli zote za kifedha zinafuatiliwa kwa ukaribu katika kuweza kupata gawio kutokana na uwekezaji wa hisa hizo.Kahwago amesema katika ukaguzi mwingine ni Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) lilikabidhi mali zisizohamishika kwa kampuni ya kufua umeme ya Songas mwaka 2004 zilizokuwa ndani ya Ubungo Complex kwa kupewa hisa 10,000 bila ya kukokotoa thamani halisi ya Mali walizokabidhi. 

Amesema Tanesco ilishauriwa kufanya tathimini na kupitia mkataba wa kuhamisha mali uliosainiwa ili kuangalia kama zilizohamishwa zinaendana na thamani ya hisa walizopewa.Aidha amesema kampuni ya Songs iliwekeza Euro 285.7 sawa na asilimia 73 katika mradi wa Songas hata hivyo hauonyeshi sehemu yeyote ya umiliki kwa serikali kwenye mradi huo licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali.

Kahwago amesema mapendekezo ya CAG ni serikali kupitia upya mpangilio wa mradi na kutathimini kama mkataba uliofanyika kwa kuangalia usawa wa pande zote mbili.
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Wendy Massoy akizungumza katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Nje wa Wizara Grace Trofumo akitoa mada kuhusiana na ukaguzi mbambali unaofanywa na CAG katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Mashirika ya Umma Pascal Kahwago akizungumza kuhusiana na mada ya ukaguzi katika mashirika ya umma.
Mkaguzi wa Serikali za Mitaa Ally Said akitoa mada ya ukaguzi wa Serikali za Mitaa katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi na Kukusanya maoni kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2016/2017 iliyofanyika Katika Ukumbi wa PPF Tower.
baadhi ya wadau katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi na Kukusanya maoni kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2016/2017 iliyofanyika Katika Ukumbi wa PPF Tower
Picha ya pamoja ya wadau na mgeni rasmi Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Wendy Massoy

JUMAA AKABIDHI GARI YA WAGONJWA KWALA ILI KUPUNGUZA ADHA YA USAFIRI

0
0
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa akikabidhi funguo ya gari la wagonjwa ambalo limegharimu mil.75 ,kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Mansoor Kisebengo ambae pia ni diwani wa kata ya Kwala.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Mansoor Kisebengo ambae pia ni diwani wa kata ya Kwala, akizungumza na wananchi wa Kwala ,kabla ya mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa kukabidhi gari la wagonjwa ambalo limegharimu mil.75 ,kwenye Kituo cha afya cha Kwala.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa akizungumza na wananchi wa Kwala kabla ya kukabidhi gari la wagonjwa ambalo limegharimu mil.75 ,katika kituo cha afya cha Kwala.

Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha Vijijini

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa amekabidhi gari la wagonjwa (ambulance ),iliyogharimu mil.75 ,katika kituo cha afya cha Kwala .

Gari hiyo itaendelea kusaidia kupunguza adha ya usafiri kwa wagonjwa hasa mahututi na warufaa.Akikabidhi gari hilo ,kwa mganga mfawidhi wa kituo hicho ,diwani wa kata ya Kwala, mbele ya wananchi ,Jumaa alisema ataendelea kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao .

"Serikali yetu inafanya makubwa katika kupunguza changamoto mbalimbali kwenye sekta ya afya na nyingine kama elimu ,miundombinu na nishati ya umeme""Kwa kutambua hayo ,July 2017 nilikabidhi magari mawili ya wagonjwa yaliyotokana na mfuko wangu na jingine moja ni msaada kutoka kwa Rais John Magufuli ikiwa ni kati ya magari ya wagonjwa 67 yaliyogawanywa katika maeneo mbalimbali nchini" alisema Jumaa.

Hata hivyo Jumaa ,alisema ameamua kujikita kutatua kero mbalimbali ili kwenda pamoja na kauli mbiu yake ya SISI KWANZA SERIKALI BAADAE .Mbunge huyo ,aliomba magari hayo yatunzwe na kutumike kwa matumizi lengwa.Nae mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,ambae pia ni diwani wa Kwala , Mansoor Kisebengo ,alisema hairuhusiwi wananchi kugharamia mafuta kwenye magari hayo .

Alielezea, halmashauri hiyo imekuwa inachangia gharama za mahitaji ya mafuta ili kuondoa bugudha kwa wananchi .Kwa upande wake mganga mfawidhi kituo cha afya Kwala ,dk.Mustapha Jaffar alimshukuru mbunge huyo kwa msaada alioutoa .Alisema hajafanya makosa kupeleka gari eneo la Kwala ,kwani litakuwa msaada mkubwa kwa wajawazito na wagonjwa wa rufaa.

Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

0
0
Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (The 38th Ordinary of the SADC Summit of Heads of State and Government) utafanyika tarehe 17-18 Agosti, 2018.

Mkutano huu utatanguliwa na mikutano ifuatayo;

(i) Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2018 ambao utapitia na kujadili hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018. Mkutano huu utahusisha nchi tatu za SADC Organ TROIKA na wajumbe wake ambao ni Angola (Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama), Zambia (Makamu Mwenyekiti wa Organ) na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mwenyekiti wa Organ aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi).

(ii) Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 14 Agosti 2018 pamoja; na 

(iii) Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 11Agosti 2018.

Prof Adolf Mkenda, Katibu Mkuu, Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anaongoza ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Makatibu Wakuu akisaidiana na Eng. Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ( Ujenzi), Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango. Mhe Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ataongoza ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Mawaziri.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utapokea, kujadili na kutolea maamuzi ya mapendekezo mbalimbali yanayotokana na mikutano ya kisekta na kamati za jumuiya kwa kipindi cha mwaka 2017/18. Pamoja na mambo mengine mkutano huu;

1. Utafanya uteuzi wa Mwenyekiti wa SADC na inatarajiwa kuwa Jamhuri ya Namibia ambayo ni Makamu Mwenyekiti wa sasa itateuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha 2018/2019. Nafasi ya Makamu mwenyekiti itajazwa pia na nchi itakayoteuliwa itajulikana tarehe 17Agosti 2018

2. Uteuzi wa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC. Inatarajiwa kuwa Jamhuri ya Zambia, ambayo ni Makamu Mwenyekiti wa sasa itateuliwa kuwa Mwenyekiti kwa kipindi cha 2018/2019. Hivi sasa Tanzania ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake kwenye Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) 

3. Maeneo mengine yanayotarajiwa kujitokeza na kujadiliwa katika mkutano huu ni haya yafuatayo;

(i) Masuala ya fedha;

(ii) Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda wa SADC ( Report on the operaionazaition Maendeleo ya viwanda;

(iii) Kutia saini itifaki mbalimbali ikiwa ni pamoja na tifaki ya Kulinda Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina Mpya za Mbegu za Mimea ya mwaka 2017.

(iv) Pia Mkutano huu utatoka na Tamko la nchi wanachama wa SADC la kutokomeza malaria katika ukanda wa SADC ifikapo mwaka 2030. 
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC), Dkt. Stergomena L. Tax (kushoto) akishuhudia makabidhiano ya uongozi katika nafasi ya Mwenyekiti wa Makatibu Wakuu wa SADC baina ya mwenyekiti anayemaliza muda wake, Bw. K E Mahoai Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti mpya, Balozi Selma Ashipala-Musavya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Namibia.Makabidhiano hayo yamefanyika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC uliofanyika katika Hoteli ya Safari Mjini Windhoek, Namibia tarehe 09 Agosti 2018. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu(kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa Kikanda (kulia), Balozi Innocent Shiyo wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika. 
Mwenyekiti wa Makatibu Wakuu wa SADC,Balozi Selma Ashipala-Musavyi akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano huo ambapo aliwashukuru wajumbe kwa kuwa na imani naye na kumpa jukumu hilo na pia alisisitiza katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha anashirikiana na wanachama kusimamia suala la ulinzi na usalama linapatikana ndani ya jumuiya ili kuruhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Bw. K E Mahoai akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa mkutano mara baada ya kukabidhi nafasi ya uenyekiti ambapo aliwashukuru wajumbe kwa ushirikiano alioupata wakati wa uongozi huo kwa taifa lake. 
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC. 
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ikifuatilia majadiliano katika mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC. 
Picha ya pamoja Katibu Mkuu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena L. Tax (wa nne kutoka kushoto) na Makatibu Wakuu wa Jumuiya hiyo Mjini Windhoek, Namibia. 

3,955 WAENDELEA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI - TASAF SHINYANGA

0
0
Mratibu wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akizungumza na waandishi wa habari.- Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Jumla ya walengwa 3,955 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF wanaendelea kunufaika na mpango huo katika Manispaa ya Shinyanga.

Hayo yamebainishwa jana Agosti 9,2018 na Mratibu wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akizungumza na waandishi wa habari.

Kiwone alisema Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika manispaa ya Shinyanga ulianza kutekelezwa mwaka 2015 ukiwa na walengwa 4,244 ambao hata hivyo walipungua kutokana na wengine kufariki na wengine tuliwaondoa kwa kukosa sifa za kuwa kwenye mpango lakini mpaka sasa tuna walengwa 3,955,

"Tangu mwaka 2015 mpaka sasa tumepokea fedha za serikali jumla ya shilingi bilioni 3,fedha ambazo tumewapa walengwa ni shilingi bilioni 2.7 na tayari zimewafikia walengwa ambapo fedha hizi zinawasaidia kwa sababu wanapewa fedha kisha kufundishwa namna ya kutumia fedha hizo",alifafanua.

Alieleza kuwa vipaumbele ni kuhakikisha mlengwa anapata milo mitatu,huduma bora za afya ambapo tunahamasisha wawe na bima za afya, aweze kuhudumia watoto wake na asikose mahitaji madogo madogo na wawe na miradi ya uzalishaji mali kwa sababu serikali haitatoa fedha milele kwa watu wale wale kwani ina wahitaji wengi sana.

"Tunahitaji walengwa waliopo kwenye mpango huu wazitumie hizi fedha zinazotolewa na serikali kujikwamua kimaisha, tunategemea baada ya miaka mitatu tumkute mlengwa akiwa na kitu ambacho kitamfanya aishi,aweze kutoka kwenye hali aliyokuwa nayo kabla ya mpango hu wa kunusuru kaya maskini",aliongeza Kiwone.

"Kuna walengwa wanafanya vizuri sana,yaani unaona kabisa huyu anachukia kuwa maskini kwa kujitahidi kutumia fedha hizi kujikwamua kimaisha lakini changamoto iliyopo ni baadhi ya watu kutumia vibaya fedha na kushindwa kufikia matarajio yaliyokusudiwa",alisema.

Hata hivyo aliwaondoa hofu walengwa wa mpango huo wanaodai kuwa serikali imesitisha mpango na kubainisha kuwa bado serikali haijatoa maelekezo yoyote mpaka sasa.

"Huu mradi ni wa miaka 10, kuna watu wanasema mtaani kwamba mradi umeisha,naomba niwaambie kuwa sisi hatujapokea maelekezo yoyote ya serikali mpaka sasa kwamba mradi umeisha na ndiyo maana mwaka huu wa fedha 2018/2019 tumeletewa fedha zingine za kuhawilisha,hivyo pindi tutakapopokea maelekezo ya serikali basi tutawaarifu",alieleza Kiwone.

Aidha alisema kwa kutambua kuwa afya ni mtaji wa kufikia malengo ya kujikwamua kimaisha asilimia 90 ya wanufaika wa TASAF katika Manispaa ya Shinyanga wamejiunga na mfuko wa bima ya afya CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya kupata huduma bora za afya na kuongeza kuwa wanaendelea kuhamasisha walengwa kujiunga na bima ya afya.

Alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo katika kutekeleza mpango huo kuwa ni walengwa kutumia vibaya fedha zinazotolewa na wengine wanadhani TASAF ni shirika linalotoa misaada kwamba mtu yeyote anaweza kupata ruzuku msaada muda wowote lakini wanaendelea kuwaelimisha kuwa TASAF ni mfuko na una taratibu zake.

Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni walengwa kuhama mtaa bila kufuata utaratibu matokeo yake inafikia wakati pesa za walengwa zinarudishwa makao makuu kwa sababu mhusika anakuwa hayupo kwenye eneo analopaswa kuwepo.

"Walengwa wa Mjini wanaonekana kutofanya vizuri kutokana na kwamba wengi wamepanga kwenye nyumba za watu na wengine wamekuwa wakihama hama na hawana mashamba na maeneo ya ufugaji hivyo tunaendelea kuwahamasisha kufanya ujasiriamali,kufanya biashara ndogo ndogo zinazoendana maeneo na waliyopo",alisema.

"Walengwa wa Vijijini wanafanya vizuri sana,vitu vinaonekana,mtu atakuonesha kiwanja,mifugo,amesomesha,ameboresha nyumba,Mjini maisha ni gharama kila kitu kinanunuliwa changamoto ni eneo lilivyo maana pesa hiyo hiyo anayopata anailipia pango",aliongeza Kiwone.

Kwa upande wao walengwa wa mpango huo,licha ya kuipongeza serikali kuwainua kimaisha, waliomba serikali kuongeza fedha kutokana na gharama za maisha kupanda na kwamba mpango huo uwe endelevu.


Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Jumia kunogesha sikukuu ya Eid kwa kutoa mbuzi bure kwa wateja

0
0
Dar es Salaam - Agosti 10, 2018. Waumini wa dini ya Kiislamu nchini na duniani kote wanatarajia kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha siku ya Jumanne ya tarehe 21 mwezi wa Agosti. Hata hivyo, hii ni tarehe inayokadiriwa kwa sababu siku rasmi inaweza kubadilika kutegemeana na kuonekana kwa mwezi wa Dhul Hijjah.

Eid Al Adha ni sikukuu ambayo husherehekewa na miongoni mwa Waislamu duniani kote katika kukumbuka sadaka aliyoitoa Nabii Ibrahim (AS) kutokana na imani aliyokuwa nayo kwa mwenyezi Mungu (SWT). Nabii Ibrahim alionyesha utayari wake wa kumtoa sadaka mwanaye wa pekee, Ismail, lakini baadaye Mungu alimtoa mwanakondoo ili awe mbadala wa sadaka. Mwenyezi Mungu alipendezwa sana na usikivu wa Ibrahim kwake na kuwataka Waislamu kukifanya kitendo hiki na imani iliyoonyeshwa kuwa sehemu ya maisha yao.

Hivyo basi, kila mwaka ifikapo siku ya 10 ya mwezi wa Dhul Hijjah, Waislamu wote duniani husherehekea sikukuu ya Eid Al Adha. Katika siku hii, Waislamu huchinja mwanakondoo, mbuzi, kondoo, ng’ombe au ngamia kuheshimu kitendo kilichofanywa na Ibrahim. Sherehe hii hutawaliwa na matendo ya ukarimu na shukrani.
Katika kunogesha shamrashamra za sikukuu hii ya Eid, Jumia Tanzania, kampuni inayojishughulisha na utoaji wa huduma za manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandaoni, imeamua kujumuika na wateja wake kwa kutoa mbuzi bure ili kufanikisha azma zao.

Mbuzi hao watatolewa kwa namna ya kipekee kabisa ambapo wateja watahitajika kutembelea tovuti ya Jumia ili kujishindia. Mbuzi watafichwa kwenye bidhaa tofauti zinazopatikana mtandaoni na mteja atakayefanikiwa kumtafuta mpaka akampata atakuwa ndiye mshindi halali. Washindi wote watapigiwa simu mara baada ya kushinda na kukabidhiwa hadharani.

Zoezi hilo litafanyika kwa kipindi cha wiki yote ijayo kuanzia Agosti 16 mpaka 20 ili kutoa fursa ya kuwakabidhi mbuzi wao na kuendelea na maandalizi ya sherehe za sikukuu ya Eid. Kwa kila siku ya shindano mteja mmoja ataweza kujishindia mbuzi mmoja aliyefichwa kwenye miongoni mwa bidhaa zilizomo kwenye mtandao wa Jumia. Vivyo hivyo kwa siku zitakazofuatia mpaka mwisho wa kampeni.
“Eid Al Adha au Eid ya kuchinja kama inavyofahamika na wengi pia ni sikukuu muhimu kwa ndugu zetu Waislamu. Tunafahamu kuwa sio watu wote wanao uwezo wa kununua mnyama wa kuchinja siku hiyo hivyo tumeona ni vema kutoa fursa kulifanikisha hilo,” alisema na kuhitimisha Afisa Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Hadijah Natalia Tuwano, “nawasihi wateja wetu kujaribu bahati yao kwa kucheza ili kushinda mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid. Fursa hii ni kwa wateja wote bila ya upendeleo wowote. Tunawatakia kila la kheri wote watakaoshiriki katika zoezi hili na ikiwezekana kuwaalika na wenzao, tunaamini litakuwa na manufaa kwao, familia, ndugu na jamaa zao.”

Sikukuu ya Eid Al Adha inalenga kumfanya Muislamu kutenda mema zaidi na kujipima na matendo yake. Haitakiwi kutoa sadaka pekee; bali inamaanisha kujifunza masomo yaliyojificha ndani yake ambayo ni kuwa huru dhidi ya matamanio ya kwa mbinafsi, na kumuinua Muislamu dhidi ya chochote kinachokwamisha uwezo wake wa kutekeleza majukumu yake kama Muislamu.

UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa mashtaka kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo ili kesi dhidi ya washtakiwa Evans Aveva na Godfrey Nyange iweze kuendelea.

Amri hiyo, imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba baada ya Wakili wa Takukuru, Leonard Swai kueleza mahakamani hapo kesi imepangwa kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa Aveva na Nyange wapo mahakamani.

Amedai mara ya mwisho Mahakama ilitoa agizo la kuwaondoa Poppe na Lauwo katika hati ya mashtaka ili kesi iendelee kwa Aveva na Nyange.
Amedai utaratibu umefanyika na jalada limepelekwa kwa DPP na amejitahidi kulifuatilia hadi leo asubuhi na ametoka kwa DPP lakini hajaweza kulishughulikia, yupo nje ya Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo ameomba Mahakama wapewe wiki mbili kwa ajili ya kuhakikisha DPP analifanyia kazi hata kama atakuwa Dodoma watamfuata huko huko.Baada ya Hakimu Swai kueleza hayo, Aveva aliomba wapewe muda wa siku saba kwa sababu siku 14 ni nyingi na kuongeza kuwa upande wa mashtaka wanavyochelewesha jambo hilo wanawaumiza.

Pia Nyange ameongeza kuwa jambo hilo la kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa washtakiwa hao ni la muda wa zaidi ya miezi miwili wakati wanajua wapo mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kuendelea kukaa huko ni tatizo.Amesisitiza kuwa kuendelea kuwapatia upande wa mashtaka wiki mbili ni kama kuendelea kuwaficha Keko bila sababu za msingi.

Baada ya malalamiko hayo ya washtakiwa Hakimu Simba alimuuliza Wakili Swai unaona malalamiko ya washtakiwa hayana msingi. Swai akamjibu Hakimu Simba kuwa malalamiko yao yanamsingi mheshimiwa.Hakimu Simba unasemaje na afya ya mshtakiwa wa kwanza Aveva inaonekana ana kliniki kila wiki hivyo anawapa siku saba wakamilishe taratibu. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 17 mwaka 2018

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.

NZEGA MJI YAHAMISHA STENDI YA ZAMANI KUONDOKA MSONGAMANO KATIKATI YA MJI

0
0
NA TIGANYA VINCENT,TABORA

HALMASHAURI ya Mji Nzega imefanikiwa kuhamisha mabasi yote ya abiria ambayo yalikuwa yakitumia Stendi ya zamani katika upakiaji na ushushaji wa abiria kutoka mjini kwenda katika eneo la Sagara ambalo lina ukubwa wa ekari 10 kwa ajili kuondoa msongamano katikati ya Mji huo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Halmashauri hiyo kufanikiwa kuweka miundo mbinu yenye thamani ya milioni 277.7 ambayo imesaidia katika hatua za awali za ufunguzi wa Stendi hiyo mpya ambayo itatoa huduma kwa magari ya abiria yanayopitia Mkoani Tabora na yake kutoka Mkoani humo.

Kauli hiyo ilitolewa jana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Philemon Magesa wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa Stendi hiyo iliyopo kando kando ya barabara kuu ya kwenda Shinyanga na Singida na maeneo mengine .

Alisema kwa kuwa Nzega iko kwenye ni njia panda eneo la Stendi ya mabasi ya zamani lilikuwa dogo na kulifanya kushinwa kuhimili wingi wa mabasi yaliyokuwa yakitoka nje ya Nchi na yale ya mikoa mbalimbali ambayo yalikuwa yakipitia Nzega na kusababisha msongamano na karaha kwa wasafiri na watumiaji wengine wa barabara.

Magesa alisema baada ya kuona hawawezi kukamilisha kazi zote kwa wakati mmoja waliamua kutumia fedha hizo kidogo kuanza na hatua za awali za kujenga jengo la kupumzikia abiria, Kituo Kiodogo cha Polisi, vibanda sita(6) vya kukatia tiketi, vyoo na ofisi, vibanda vya askari , Mamlaka ya Usafirishaji Tanzania(SUMATRA) na kulipa fidia wananchi waliokuwa katika eneo ilipojengwa Stendi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kazi nyingine ilikuwa ni kujenga uzio wa nyaya kuzunguka eneo la stendi,vibanda vya askari wa usalama barabarani, wakusanyaji mapato ya Halmashauri, kuweka taa za mwanga wa jua katika Ofisi na kwa ajili ya kuimarisha usalama nyakati za usiku .

Alisema gharama halisi ya kujenga hadi Stendi hiyo hadi kukamilika kwa kiwango cha juu kulingana na michoro ya ubunifu zinahitajika bilioni 7.7 ambapo kwa kutumia mapato ya Halmashauri hiyo ya ndani itawachukua miaka 10 ili kukamilisha ujenzi wake.

Magesa alisema kutokana kuhitajika fedha nyingi kukamilisha ujenzi wote walifanya uamuzi wa kuandika andiko maalumu kwa ajili ya mradi huo na kuuwasilisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo limeshawalishwa Wizara ya Fedha na Mipango ili waweze kupatiwa fedha za kukamilisha ujenzi wa mradi huo mapema.

Alisema mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake kutaweza kusaidia Halmashauri hiyo kuongeza uwezo wa kukusanya mapato yake na ndeani na kuiwezesha katika kuelekea katika kujitegemea.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema wako katika hatua ya mwisho ya kupata eneo lenye ukubwa wa ekari 15 kwa ajili ya kuweka maegesho ya magari ya mizigo ambalo nalo litasaidia kuingizia Halmashauri hiyo mapato yake ya ndani.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilitaka Jeshi la Polisi Wilaya ya Nzega kushirikiana na Halmashauri hiyo kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika eneo hilo saa zote kwa kuwa ni jipya na liko mbali na makazi ya watu upo uwezekano watu ambao sio wema wakatumia nafasi hiyo kutenda uovu wa aina mbalimbali ikiwemo kuwapora abiria.

Alisema uhalifu wa aina yoyote ukitokea unaweza kuwakatisha tamaa wasafiri na wawekezaji ambao wangependa kutumia Stendi hiyo jambo ambalo linaweza kusababisha mapato ya Halmashauri kupungua kutokana na wasafiri kuwa na hofu .Aidha Mkuu wa Mkoa alioutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha huduma mbalimbali kama vile vyoo na kuweka taka zinakuwepo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko wakati wa masika.

Naye abiria kutoka Yelayela wilayani Urambo kwenda Dar es salaam Mashaka Maganga aliipongeza Halmashauri hiyo kwa uamuzi wake wa kuihamisha Stendi kutoka mjini kuiweka eneo la Sagara kwani limesaidia kuondoa msongano sio tu magari hata abiria walikuwa wanapata shida kutoka na kuwa wengi katika eneo dogo.
 Baadhi ya Wafanyabiashara ndogondogo wakiendelea na shughuli zao jana  baada ya uzinduzi wa Kituo Kipya cha Mabasi cha Sagara kwenye Halmashauri ya Mji Nzega.
 Magari ya abiria kutoka sehemu mbalimbali yakipita katika Geti la Ukaguzi na malipo ya ushuru katika Kituo Kipya cha Mabasi cha Sagara kwenye Halmashauri ya Mji Nzega baada ya kuzinduliwa jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Philemon Magesa (mbele waliosimama), Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula(wa pili waliosimama) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (wa tatu waliosimama) na abira wengine wakiwa katika gari la abiria ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Kituo Kipya cha Mabasi cha Sagara katika Halmashauri ya Mji Nzega jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mbele) akiwaongoza viongozi mbalimbali kutembelea Kibanda cha Ukaguzi wa Magari na kile cha Malipo ya Ushuru wakati wa uzinduzi wa Kituo Kipya cha Mabasi cha Sagara katika Halmashauri ya Mji Nzega jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Philemon Magesa (katikati walio mbele) akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey (kulia walio mbele)mara baada ya uzinduzi jana wa Kituo Kipya ch Mabasi ya Abiria cha Sagara cha Halmashauri hiyo. Kushoto mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula.

UJUMBE WA SIERRA LEONE WATEMBELEA WIZARA YA FEDHA

0
0
 Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Ufundi toka nchini Sierra Leone Dk. Turad Senesie (kulia) akiuliza swali kwa Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (hayupo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Ofisi za hazina na ujumbe wake ili kujifunza namna Wizara ya Fedha inavyoweza kutoa fedha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Kushoto ni Wajumbe aliombatana nao toka nchini Sierra Leone.
 Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (kulia) akifafanua jambo kwa ujumbe toka nchini Sierra Leone (hawapo pichani) uliokuja nchini kwa lengo la kujifunza namna ya uendeshaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Katikati ni Afisa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Omega Ngole na kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Godfrey Chawe.
 Afisa Msimamizi Mwandamizi wa Fedha toka Wizara ya Fedha,Alexander John akifafanua jambo kwa ujumbe toka nchini Sierra Leone (hawapo pichani) uliokuja nchini kwa lengo la kujifunza namna ya uendeshaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Kulia ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Godfrey Chawe.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha toka nchini Sierra Leone, Mathew Dingie (katikati) akiuliza swali kwa Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (hayupo pichani) wakati walipotembelea Ofisi za hazina ili kujifunza namna Wizara ya Fedha inavyoweza kutoa fedha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Kushoto ni Wajumbe aliombatana nao toka nchini Sierra Leone. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Ufundi toka nchini Sierra Leone Dk. Turad Senesie.
 Afisa Msimamizi Mwandamizi wa Fedha toka Wizara ya Fedha,Alexander John (kushoto) akifafanua jambo kwa ujumbe toka nchini Sierra Leone uliokuja nchini kwa lengo la kujifunza namna Wizara ya Fedha inavyoweza kutoa fedha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
 Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (mwenye kilemba) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe toka nchini Sierra Leone uliokuja nchini kwa ziara ya kikazi ya kujifunza namna ya uendeshaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (kulia) akifafanua jambo kwa ujumbe toka nchini Sierra Leone uliokuja nchini kwa lengo la kujifunza namna Wizara ya Fedha inavyoweza kutoa fedha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Picha na MAELEZO

NAMUNGO FC KUPAMBANA NA SIMBA YA JIJINI DSM

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na wachezaji wa Namungo FC, alipowatembelea kambini kwao Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akionesha jezi ya Namungo FC, baada ya kupokea jezi hizo zilizotolewa na wafadhili wa timu hiyo, Haojue Company Limited Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 Kushoto ni Mkurugenzi wa Haojue Brand Martin Francis. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wachezaji wa Namungo FC, alipowatembelea kambini kwao Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).


*Ni katika uzinduzi wa uwanja wa Halmashauri ya Ruangwa



HALMASHAURI ya Wilaya ya Ruangwa kesho (Jumamosi, Agosti, 11, 2018) inatarajia kuzindua uwanja wake wa michezo, ambapo timu ya wilaya hiyo Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza itapambana na bingwa wa ligi kuu 2018/2019 Simba SC ya jiji Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Namungo FC ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini, imeupa heshima mkoa wa Lindi kwa kuwa ndiyo pekee inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa uwanja huo leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mbali na timu ya Simba pia timu hiyo inatarajia kucheza na timu za Yanga , Azam za jijini Dar es Salaam na Dodoma FC ya jijini Dodoma.

Uwanja wa mpira wa miguu wa wilaya Ruangwa unaoitwa Majaliwa Stadium umejengwa katika kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea na ndio utakaokuwa unatumiwa na timu ya Namungo FC kuchezea mechi za nyumbani.

“Lazima tuisapoti timu yetu ya Namungo FC icheze daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”

Kadhalika Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa timu ya Namungo FC kucheza na timu kama za Simba, Yanga, Azam na Dodoma FC kwa sababu zinasaidia katika kuimarisha viwango vya wachezaji na kuwaondolea uoga wa kupambana na timu nyingine.

Kiingilio katika mechi ya Namungo FC na Simba SC ni sh. 3000. Tayari timu ya Simba imeshawasili wilayani Ruangwa leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018), saa 11.01 jioni kwa ajili ya mechi yake na timu ya Namungo.

MPINA APIGA MARUFUKU UKAMATAJI HOLALA WA MIFUGO

0
0
NA JOHN MAPEPELE, MOROGORO 

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepiga marufuku tabia ya ukamataji mifugo kiholela inayofanywa na baadhi ya watumishi wa umma na kusababisha mifugo mingi kufia mikononi mwa Serikali kwa kukosa huduma muhimu ikiwemo maji, malisho na matibabu na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla. 

Mpina amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali kuendesha operesheni za kukamata mifugo na kuifungia bila kuipatia huduma muhimu ikiwemo maji, malisho na matibabu na matokeo yake mifugo mingi hufa na kusisitiza kuwa operesheni hizo zinapofanyika ni lazima zihusishe pia maofisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuwa na uelewa wa pamoja wa jambo hilo. 

Aidha Mpina alisema utaratibu unaofanyika hivi sasa wa kukamata hovyo mifugo ni ukiukwaji wa sheria namba 17 ya Magonjwa ya Wanyama ya mwaka 2003 na, Sheria ya Ustawi wa Wanyama Namba 19 ya Mwaka 2008 ambazo zinataka mifugo inapokamatwa kuzingatia masuala ya magonjwa na ustawi wa mifugo katika kipindi chote inapokuwa imeshikiliwa. 

Akifunga maonesho ya 25 ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere mjini Morogoro kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Waziri Mpina pia alielezea kutoridhishwa na utoaji wa mikopo wa Benki ya Kilimo (TADB) ambapo kwa taarifa iliyotolewa sekta ya uvuvi hakuna mkopo wowote uliotolewa katika mwaka wa fedha uliopita huku upande wa sekta ya mifugo wakiambulia wajasiamali wanne tu . 

Aidha kiasi cha jumla ya mikopo iliyotolewa ya Sh. Bilioni 39 kwa mwaka mzima ni kidogo sana ikilinganishwa na mahitaji wa mikopo katika sekta za kilimo,mifugo na uvuvi, huku akipongeza kazi nzuri inayofanywa na Taasisi ya PASS na SAGGOT-CTF katika kuwadhamini wakulima , wafugaji na wavuvi katika kupata mikopo. 

Kutokana na changamoto hizo, Waziri Mpina ameitaka benki hiyo kurekebisha kasoro zilizopo na kujipanga vizuri kuhudumia sekta hizo, vile vile amewaagiza makatibu wakuu wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuitambua na kupitia miradi yote ya wajasiriamali katika sekta zao ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo kwa wakati. Sambamba na hilo amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kupitia idara ya maendeleo ya jamii na idara ya ushirika kuwaandaa na kuwaunganisha wananchi katika kukidhi vigezo vya kupata mikopo katika taasisi za fedha. 

Pia aliagiza Halmashauri zote nchini kuwatambua vijana wanaohitimu mafunzo katika vyuo vya ugani vya SUA, FETA, LITA na ATI na kuwatumia katika safari ya kuleta mageuzi ya uvuvi,mifugo na kilimo katika maeneo yao na kwamba hata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa wanawake,vijana na walemavu kundi hili la wagani liangaliwe kwa jicho la pekee. 

Mbali na hilo Waziri Mpina alisema pamoja na Serikali kuwekeza fedha nyingi katika ujenzi wa mialo na masoko ya samaki baadhi ya halmashauri zimetelekeza miundombinu hiyo na kuendelea kutoa huduma katika maeneo yasiyo rasmi, pia baadhi ya mialo na masoko haifanyiwi matengenezo wala ukarabati kiasi cha kukosa huduma muhimu kama maji, vyoo, umeme na majokofu ya kuhifadhia samaki hali inayosababisha usumbufu na hasara kwa wananchi licha ya kutozwa ushuru kila uchao. 

Kufuatia hali hiyo Waziri Mpina ametoa miezi mitano kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakarabati na kuweka huduma muhimu na kwamba wataoshindwa kufanya hivyo mialo na masoko hayo yatarejeshwa chini ya usimamizi wa Wizara na halmashauri hizo hazitaruhusiwa tena kukusanya mapato yatokanayo na sekta hiyo. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alimhakikishia Waziri Mpina kuwa maagizo yote aliyotoa watayafuatilia na kuyasimamia ili kuona utekelezaji wake kwani Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuleta mageuzi ya kweli katika sekta za Kilimo,Mifugo na Uvuvi. 

Pia Ndikilo alisema ni jambo la kusikitisha kuona licha ya fursa kubwa za mifugo na uvuvi zilizoko katika mikoa ya Kanda ya Pwani lakini hadi sasa hakuna kiwanda hata kimoja cha kuchakata samaki wala nyama na kumuomba Waziri Mpina kuandaa kongamano ya mikoa hiyo ili kujadili kwa pamoja namna ya kuwekeza katika viwanda vya kuchakata bidhaa hizo. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stephen Kebwe alisema maonesho hayo ya mwaka huu yamekuwa na mafanikio makubwa kwani wakulima,wafugaji na wavuvi na makundi mengine yamejitokeza kwa wingi na wamepata fursa ya kujifunza teknolojia mpya zitakazoboresha uzalishaji. 

Maonesho hayo yalihudhuriwa na wakuu wa mikoa, wilaya, mameya, wakurugenzi wa halmashauri,madiwani pamoja na sekta binafsi.

KAULI YA MBWANA SAMATA BAADA YA POLISI KUMSHAMBULIA MWANDISHI WA HABARI DAR

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKATI Watanzania mbalimbali wakitoa matamko ya kulaani kitendo cha Mwandishi wa habari wa Wapo Redio Silas Mbise kushambuliwa na Polisi katika mechi kati ya Simba na Asante Kotoko Siku ya Simba Day mchezaji wa kimataifa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’Mbwana Samata amesema kitendo hicho si cha kiungwana.

Samata ametoa kauli hiyo kutokana na kusambaa kwa video inayoonesha namna ambavyo mwandishi huyo akishambuliwa licha ya kujisamilisha.
Hivyo kutokana na video hiyo Samata kupita ukurasa wake wa Tweet ameelezea kusikitishwa na shambulio hilo.

Samata amesema hivi “Sio kitendo cha kiungwana askari kupiga mwandishi katika eneo la michezo , mpira ni mchezo unaoleta amani sio kuvunja amani.”.Wakati Samata akitoa kauli hiyo tayari leo mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linalaani vikali tukio hilo linalosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandishi huyo.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema tukio hilo limetokea Agosti 8 mwaka huu siku ya mechi kati ya Simba na Asante Kotoko ya nchini Ghana.Aidha amesema Polisi Kanda Maalum imeanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha ya video  hiyo inayosambaa na kuonesha askari polisi na mwandishi huyo wa habari ili kubaini ukweli.

Mambosasa amesema hiyo inakwenda sambasamba na kumtaka mtendewa wa kosa hilo la kupigwa kutoa taarifa kituo cha Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe na kwamba mtu yoyote anatakiwa kutoa malalamiko yake pale anapoona ametendewa vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.

NANGANGA-RUANGWA KUJENGWA KWA LAMI-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni tano katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Nanganga-Ruangwa yenye urefu wa kilomita 57 kwa kiwango cha lami.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Agosti 10, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Likunja wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi wilayani hapa.Waziri Mkuu amesemaSerikali imeendelea kuboresha huduma za jamii nchini kwa kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo.

Amesema ujenzi wa barabara hiyo ya Nanganga-Ruangwa-Nachingwea hadi Masasi unatarajiwa kuanza hivi karibu, hivyo amewataka wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao.Akizungumza kuhusu nyumba zilizowekewa alama ya X, Waziri Mkuu aliwataka wahusika wazibomoe wenyewe ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa walivamia eneo na watakaosubiri hadi Serikali iwabomelee watalazimika kuilipia gharama, hivyo ni vema wakatii.

Wakati Huo huo,Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo asilimia 95 ya vijiji vyote vya wilaya ya Ruangwa vinapata huduma hiyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya wananchi wa kata hiyo kueleza changamoto zinazowakabili ikiwemo huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.“Tumeendelea kuboresha huduma za jamii katika vijiji vyote vikiwemo na vya wilaya hii. mkakati wetu ni kuhakikisha wananchi wote mnapata maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yenu na tayari asilimia 95 ya vijiji vinapata maji,” amesema.

Kuhusu changamoto ya zahanati ya kijiji cha Likunja kutokuwa na nyumba ya mganga, Waziri Mkuu amewashauri wananchi hao wafyatue matofali na kisha waanze ujenzi wa boma na Halmashauri itawasidia kuwapa vifaa vya viwandani kama saruji, mabati na misumari.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAAA, AGOSTI 10, 2018.

KAMPENI ZA ‘LALA SALAMA’ WABUNGE WA CCM WATIKISA BUYUNGU

0
0

Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akiteta jambo na Mbunge wa Vitimaalum Matha Mlata
wananchi wakiwa kwenye kampeni za CCM zikiendelea katika Jimbo la Buyungu.
Baadhi ya Wabunge wa CCM pamoja na makada mbalimbali katika moja ya mikutano ya kampeni jioni ya leo.
Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akiwa na baadhi ya makada wa CCM katika kampeni wilayani Kakonko mkoani Kigoma.
Mbunge wa Vitimaalum Mary Chatanda akiwa na viongozi mbalimbali katika harakati za kampeni za Jimbo la Buyungu.

.
Wakati zimebaki siku mbili za kampeni kabla ya uchaguzi wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko Mkoani Kagera kufanyika, Wabunge wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wameonekana kunogesha kampeni hizo kwa hoja mbalimbali wakimdani mgombea Ubunge wa Jimbo hilo wa chama hicho Mhandisi Christopher Chiza.

Katika kampeni za leo wabunge wa CCM waliokuwa wakimwaga Sera kwa wananchi ni pamoja na Peter Serukamba, Selemani Jafo, Matha Mlata, Joseph Msukuma, Josephine Genzabuke, Ashantu Kijaji, na Mary Chatanda. Wabunge wengine ambao wamekuwa katika kampeni hizo kwa nyakati tofauti ni pamoja na Nape Nnauye, Livingstone Lusinde, Hussein Bashe, na aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara ambao wamekuwa wakimwaga Sera za CCM ili kukiletea ushindi chama chao.

Wakizungumza katika kampeni hizo, Wabunge hao wamewahakikishia wananchi wa Kakonko kwamba watampa ushirikiano wa kutosha mgombea huyo watakapokuwa pamoja bungeni katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zikiwemo hospitali ya wilaya, vituo vya afya pamoja na miundombinu ya barabara.


Aidha wamewaasa wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu.

Balozi wa Saudi Arabia akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje

0
0
Mhe. Balozi Dkt.Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), akisalimiana na Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania (kulia) walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam. Mazungumzo baina ya Viongozi wa Wizara na Balozi Mohamed yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Mataifa haya mawili (Tanzania na Saudi Arabia).

Aidha viongozi hao wamekubaliana kukamilisha maandalizi ya kongamano la biashara litakalo husisha wafanyabiashara na wadau wengine kutoka Saudi Arabia na Tanzania. Balozi Mohamed amebainisha kuwa ujumbe kutoka Saudi Arabia utakuwa na wafanyabiashara zaidi ya 40 wakiongozwa na Waziri wa Biashara wa Saudi Arabia.

Aidha Balozi Mohamed ameonesha nia yakuanzisha majadiliano kati ya Tanzania na Saudi Arabia ya kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Saudi Arabia kwa lengo la kukuza biashara baina ya nchi hizi mbili. 
Mhe. Balozi Dkt.Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Bw. Suleiman Saleh Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati (wa kwanza kulia) na Bw. Hangi Mgaka Afisa Mambo ya Nje (wa kwanza kushoto) 
Bw. Suleiman Saleh Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati, akisalimiana na Mhe. Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam 
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam 
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania (wa pili kulia)
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live




Latest Images