Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RAIS MUSEVENI AWASILI DAR ES SALAAM KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA NCHINI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipowasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Agosti 9, 2018
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni (kati kati) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda baada ya kuwasili, kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda

JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUSIMAMIA VYEMA MATUMIZI.

$
0
0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akipata maelezo ya ujenzi wa soko kutoka kwa Mkurugenzi wa mji wa Geita
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Magufuli walipotembelewa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo
Mkuu wa Mkoa na Geita Mhandisi Robert Gabriel akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea katika zahanati ya Buselesele.
Wananchi katika kituo cha afya Bwanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka viongozi wa Halmashauri nchini kusimamia matumizi ya mapato yanayokusanywa katika Halmashauri zao.

Jafo ametoa kauli hiyo alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Geita na Chato katika mkoani wa Geita. Amesema Halmashauri mbalimbali zinatakiwa kusimamia vyema matumizi ya mapato hayo na kwa kiasi kikubwa yaelekezwe katika miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri hizo kwa maslahi mapana ya wananchi.

Waziri Jafo amepongeza viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato.Katika ziara hiyo, Waziri huyo amefanikiwa kukagua ujenzi wa soko la kisasa linalojengwa kwa fedha za ndani za Halmashauri ya mji wa Geita, barabara za lami za mji wa Geita zinazojengwa kwa mradi wa ULGSP, zahanati ya Buselesele, Kituo cha Afya Bwanga kilichopo wilayani Chato, pamoja na kutembelea shule ya sekondari Magufuli.


Akiwa Buselesele, Waziri Jafo amewahakikishia wananchi wa kata ya Buselesele kwamba serikali itajitahidi ili ijenge kituo cha afya cha kisasa katika kata hiyo ya Buselesele kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika eneo hilo.

SIMBA DAY 2018: MBWEMBWE ZATAWALA UTAMBULISHO WA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI LA SIMBA SC...

MTENDAJI MKUU, MAHAKAMA YA TANZANIA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI YA UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI

$
0
0
Hali ya jengo la Mahakama kuu kanda ya Kigoma lilipofikia
Mtendaji Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma Bw. Moses Mashaka akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi mbele ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Bw. Leonard Magacha.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw Hussein Kattanga (wa kwanza kulia) akikagua kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Wilaya Buhigwe ikiwa ni muendelezo wa kusogeza huduma kwa wananchi mkoani Kigoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Kattanga akitoa maelekezo alipotembelea ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kasulu mkoani Kigoma katika ziara yake aliyofanya Wilayani humo Agosti, 08, 2018.
Picha ya pamoja ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama , viongozi wa Mahakama Mkoa wa Kigoma na wakandarasi wa Masasi Construction wakiwa mbele ya jingo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma linaloendelea kujengwa. (Picha na Festo Sanga, Kigoma


Na Festo Sanga, Mahakama ya Mkoa- Kigoma

Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Husssein Kattanga amefanya ziara mkoani Kigoma na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu lililoanza kujengwa rasmi tarehe Oktoba 28, 2017 chini ya mkandarasi Masasi Construction Co Ltd. 

Ujenzi huo wa Jengo la Mahakama Kuu utasogeza huduma za Kimahakama karibu na wananchi wa Mkoa huo kwani wamekuwa wakisafiri kutoka Kigoma kwenda Tabora kufuata huduma za Mahakama Kuu.

Katika ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa Mahakama alipata fursa ya kutembelea mahakama ya Wilaya Kasulu na kukagua ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kasulu inayotegemewa kumalizika mwezi April 2019 chini ya Mkandarasi M/S Molad Tanzania LTD.

Ujenzi wa Mahakama mbalimbali nchini unalenga katika kusogeza huduma ya haki karibu zaidi na wananchi na vilevile ni utekelezaji dhahiri wa nguzo ya pili ya mpango mkakati wa Mahakama (2015/2016-2019/2020) ya upatikanaji wa haki kwa wakati.

Aidha ujenzi wa jingo hilo la Mahakama na unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019 utawezesha uhifadhi wa kumbukumbu na nyaraka mbalimbali na kuimarisha matumizi ya vifaa vya TEHAMA katika huduma ya utoaji haki.

WAZIRI LUGOLA ATOA ONYO KALI KWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI...

TAASISI YA FRIEDKIN CONSERVATION FUND YATOA MILIONI 110 KUSAIDIA ELIMU SIMIYU

$
0
0
Mmoja wa wakurugenzi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund,(FCF) Abdukadir Mohammed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (katikati) Anthony Mtaka akipokea hundi ya shilingi 110 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya vipaji maalum Mkoa wa Simiyu jana katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo na Mifugo, Nyakabindi Mkoa wa Simiyu.
Mmoja wa wakurugenzi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund,(FCF) Abdukadir Mohammed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (katikati) Anthony Mtaka akipokea hundi ya shilingi 110 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya vipaji maalum Mkoa wa Simiyu jana katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo na Mifugo, Nyakabindi Mkoa wa Simiyu.



TAASISI ya uhifadhi na Utalii ya Friedkin Conservation Fund, imetoa msaada ya shilingi milioni 110 ili kusaidia ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Vipaji maalum mkoani Simiyu. Msaada huo, ulikabidhiwa jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka na wakurugenzi wa taasisi hiyo wakiongozwa na Abdukadir Mohamed katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Nyakabindi Wilaya ya Bariadi.

Mohammad alisema taasisi yao ambayo inamiliki kampuni za Uwindaji na upigaji picha za kitalii, Mwiba Holdings Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris, ambazo zimewekeza mkoani humo, zimetoa msaada huo kusaidia watoto kupata elimu.Alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ya kusaidia jamii inayotolewa ili kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Simiyu kiujumla.

"Tunachoomba ni kupewa ushirikiano tufanye kazi zetu za utalii katika pori la akiba la Makao na Maswa na kuondolewa uvamizi," alisema.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alishukuru kwa msaada huo wa shilingi milioni 110 ambazo zitasaidia ujenzi wa shule hiyo.Alisema Taasisi ya Friedkin imekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo katika mkoa huo kwani hivi karibuni ilitoa msaada wa mifuko 3000 ya saruji na bati 1000 kusaidia elimu pia.

Kulikuwepo na migogoro katika eneo la mwekezaji huyo hivyo kabla ya kupokea misaada ya Saruji na bati Mkuu huyo wa mkoa aliongea na Rais Dk. John Mafuguli kuomba idhini ya kupokea."Niliona ningepokea mwenyewe maneno yangeanza ya kuchafuana, hivyo niliomba ridhaa ya Rais na akasema hii ni michango ya maendeleo tupokee. Mh. Rais alisema na shule ikijengwa wanaweza hata kuiita Mwiba," alisema.

Alisema licha ya msaada huo, taasisi hiyo imesaidia kutoa mchango wa ajira na imekuwa ikilipa kodi.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dk. Joseph Chilongani alisema Serikali inatambua mchango wa taasisi hiyo kwa maendeleo ya jamii.Alisema licha ya misaada inayotolewa ngazi ya mkoa, taasisi hiyo kila mwaka inatoa zaidi ya shilingi milioni 610 kama kodi ya pango na sehemu ya mapato ya utalii kwa vijiji 10 vilivyopo eneo la hifadhi ya jamii ya makao.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mkoa wa Simiyu, Gungu Silanga alisema Serikali ya CCM itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo kwani inachangia utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi."Miaka ya nyuma kulikuwa na watu wachache walitaka kutugombanisha lakini sasa chama na Serikali tupo pamoja kufanya kazi na wawekezaji Mkoa wa Simiyu,” alisema.Alisema.

WAZIRI MWAKYEMBE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MZEE MAJUTO ALIYEFARIKI JANA

$
0
0

. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) akizungumza na aliyekuwa nguli wa filamu nchini Bw. Amri Athumani maarufu kama King Majuto Enzi za uhai wake.

WATOA VIBALI SERIKALINI BADO WADAIWA KUWA NI KIKWAZO KWA WAWEKEZAJI NCHINI.

$
0
0
Na John Walter-Babati.

Mwekezaji mkubwa mkoani Manyara wa kiwanda cha Mati Super Brand kinachozalisha vinywaji vikali David Mlokozi amewaangukia baadhi ya watumishi wa idara muhimu zinazotoa vibali kuwa ni tatizo kubwa serikalini.

Aidha Mr.David Mlokozi ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo amesema kuwa mamlaka za serikali ni nyingi sana zipo kisheria lakini baadhi zinadidimiza jitihada za serikali ya Rais Magufuli kuwa na uchumi wa viwanda kukwama kwa sababu za kuchelewesha kutoa vibali.

Mlokozi amesema kuwa ulifika muda alikata tamaa na kutaka kuhamishia kiwanda hicho kwingine lakini kutokana na msaada mkubwa walioupata kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti kuruhusu kuendelea na uzalishaji wameamua kubaki.

“Kiwanda kilipofungwa kwa miezi mitatu nilipata hasara sana kwa sababu nilikuwa nikiwalipa wafanya kazi bila kuingiza chochote’.alisema Mlokozi.

Kwa sasa Mati Super Brand imeanza uzalishaji wa maji ya kunywa ambayo kwa sasa wameshapeleka sampuli mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa na muda wowote wanatazamia kuanza uzalishaji baada ya kupata majibu kutoka TFDA.

Aidha Wamefungua kampuni nyingine inayoitwa Manyara Breweries Limited ambayo itakuwa ikizalisha aina nyingine za vinywaji ikiwemo bia kwa kutumia mtama unaolimwa na wakulima mkoani Manyara.

Kiwanda cha Mati Super Brand kilichopo Babati kimetoa ajira kwa vijana wa kike na wa kiume zaidi ya sitini na kusaidia kupunguza wimbi la vijana wasiokuwa na ajira.

TANTRADE WAIBUKA WASHINDI WA TATU MAONESHO YA KILIMO KITAIFA (NANE NANE) MKOANI SIMIYU

$
0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akimkabidhi Cheti  Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bw. Edwin Rutageruka baada ya Banda la TanTrade "Business Clinic" kuibuka Mshindi wa Tatu kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa (Nane Nane 2018) yaliyofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu. Banda hilo lilizijumuisha Taasisi za Udhibiti za Serikali kwa lengo la kutatua changamoto za Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Wafanyabiashara waliotembelea Maonesho hayo yaliyovutia Wananchi wengi.

Dk.Shein akutana na Ujumbe wa UAE Ikulu Zanzibar.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Reem Ibrahim Alhashimy alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake uliofika nchini kufuatia ziara ya Rais.aliyoifanya mwanzoni  mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Reem Ibrahim Alhashimy (katikati) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake uliofika nchini kufuatia ziara ya Rais.aliyoifanya mwanzoni  mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 09/08/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na  Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Reem Ibrahim Alhashimy baada ya mazungumzo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake waliofika nchini kufuatia ziara ya Rais.aliyoifanya mwanzoni  mwa mwaka katika Nchi hizo,[Picha na Ikulu.] 09/08/2018.

NAIBU WAZIRI WA MADINI ATOA HEKO KWA NFRA KWA ELIMU WANAYOITOA KUHUSU UHIFADHI WA MAHINDI BAADA YA KUVUNA

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo akisikiliza maelezo kuhusu uhifadhi wa nafaka ya mahindi mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-NFRA)
Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo akisikiliza maelezo kuhusu uhifadhi wa nafaka ya mahindi mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.
Baadhi ya wananchi wakipata elimu kuhusu njia bora za kuhifadhi mahindi baada ya kuvuna mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.
Baadhi ya wananchi wakipata elimu kuhusu njia bora za kuhifadhi mahindi baada ya kuvuna mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.



Na Mathias Canal, NFRA-Simiyu

Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo amepongeza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwa elimu wanayoitoa kuhusu njia bora za kuhifadhi nafaka ya mahindi mara baada ya kuvuna.

Nyongo ametoa pongezi hizo jana 8 Agosti 2018 wakati akizungumza na uongozi wa NFRA mara baada ya kutembelea banda la NFRA kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu ambapo Rais mstaafu wa srikali ya awamu ya tatu Mhe Benjamini Willium Mkapa ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho hayo.

Pamoja na mambo mengine Mhe Naibu Waziri Nyongo amepongeza elimu inayotolewa kuhusu utunzaji huo wa mahindi mara baada ya kuvuna kwa kufuata taratibu zote za kuvuna wakati muafaka, ikiwa ni pamoja na Kukausha vizuri mahindi baada ya kuvuna.Mhe Nyongo pia amepongeza elimu inayotolewa na NFRA kuhusu utambuzi wa mahindi kama yamekauka kwa kutumia njia za kienyeji ambazo ni rafiki kwa wakulima wa chini pamoja na njia za kisasa.

Pia alijionea na elimu kuhusu matumizi bora ya mifuko ya kuhifadhia mahindi ikiwa ni pamoja na mifuko ya PICS, Vihenge vya chuma sambamba na maghala ya tofali.Alisema kuwa njia hizo zitaleta ufanisi iwapo mahindi yameandaliwa vizuri kabla ya kuhifadhi huku akiisihi NFRA kuongeza nguvu katika utoaji elimu ili wakulima waweze kunufaika kwani mkulima akielimika ipasavyo ni sehemu ya mafanikio ya mtu mmoja mmoja sambamba na ukuzaji wa uchumi wa Taifa.

TANESCO YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA NANE NANE SIMIYU

$
0
0

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Simiyu Bi. Rehema Mashinje (mwenye fulana ya mistari), akiungana na wafanyakazi wa Shirika hilo kusherehekea ushindi wa kwanza (kipengele cha mashirika ya serikali), kwakuwa banda bora kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane mwaka 2018 yaliyoadhimishwa kitaifa Mkoani Simiyu Agosti 8, 2018.
NA SAMIA CHANDE, SIMIYU
SHIRIKA LA UMEME NCHINI, (TANESCO),  limeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Mashirika ya Serikali kwenye maonesho ya wakulima ( NANE  NANE) katika viwanja  vya Nyakabindi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu ambapo kauli mbiu ya mwaka 2018 ni “Wekeza katika kilimo mifugo na uvuvi  kwa maendeleo ya viwanda”.
Katiaka maonesho hayo TANESCO iliweza kutoa elimu mbalimbali kuhusu umeme pamoja na matumizi bora ya umeme.
Meneja wa TANESCO mkoani Simiyu Bi. Rehema Mashinje alisema katikanmaonyesho haya Nane Nane TANESCO tumejipanga kutoa  huduma bora na kwa welendi mkubwa.
Pia alitoa rai kwa kwa mananchi wote kutumia fulisa hii ya nane nane kutembelea banda la TANESCO ili kupata elimu mbalimbali kuhusu maswala ya umeme hususani  kuhusu miradi ya umeme  vijiji(REA) ili kuhakikisha kila wananchi wote wanaopitiwa na mradi wa Umeme Vijini( REA) wanaonganishwa na huduma hiyo mara moja.
Aliongezea kwa kusema  bila umeme hamna kitu kinaweza kuendelea hivyo wananchi walime kwa bidi ilitupate mazao mengi  tuweze kuendeleza viwanda vyetu na sisi TANESCO tumejipanga kuhakikisha viwanda vyote vinapata umeme wa uhakika.
TANESCO kama mdau muhimu iliweza kuhakikisha mabanda yote katika viwanja vya Nyakabidi vinapata umeme wa uhakika muda wote.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba  alifungua rasmi maonyesho katika hotuba yake alitoa wito kwa wananchi wote wa mikoa inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga Kutumia  fursa  ya kutembelea katika maonyesho hayo ili kujifunza mbinu mbalimbali za kitaalamu katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Katika kufunga maonyesho raisi Mtahafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa alisema kua kiwanja  hiki cha Nyakabindi kitumike kama darasa la wakulima, wavuvi na wafugaji.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Simiyu Bi. Rehema Mashinje pamoja na Mkurugenzi wa REA Bwana Amos Manga  wakisherekea Ushindi katika maonyesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi

 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye banda la TANESCO ili kupatiwa habari mbalimbali zihusuzo huduma zitolewazo na Shirika hilo.
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye banda la TANESCO ili kupatiwa habari mbalimbali zihusuzo huduma zitolewazo na Shirika hilo.

 Wanafunzi wa Simiyu Golden Open School wakiwa wamekabidhiwa madafutari katika banda la TANESCO bada ya kujibu kwa usahihi maswali kuhusu umeme na matumizi yake.(PICHA NA SAMIA CHANDE)




KIJIJI CHA CHIMBILA B KUSAMBAZIWA MAJI-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo katika Kijiji cha Chimbila B, Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne, Agosti 9 2018 .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkuu wa Shule Muhsin Ibrahim, baada ya kukagua darasa la kompyuta katika Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa Agosti 9 2018. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chimbila B, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho, Agosti 9 2018. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. milioni 250 kwa ajili ya usambazaji wa huduma ya maji safi katika kijiji cha Chimbila ‘B’ kichopo kata ya Mnacho.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Agosti 9, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mnacho wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi wilayani hapa.Waziri Mkuu amesemaSerikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji, ambapo itahakikisha wananchi wanapata huduma hiyo katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Amesema mbali ya maji kusambazwa kwa wananchi, pia yatasambazwa kwenye taasisi zote za umma zikiwemo shule za msingi na sekondari pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Mnacho na kuzungumza na wanafunzi, ambapo amesema Serikali inatarajia kujenga mabweni mawili katika shule hiyo ili wanafunzi waweze kuishi shuleni na kupata fursa nzuri ya kujisomea.Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya wanafunzi wa kike shuleni hapo kuiomba Serikali iwajengee mabweni ili waweze kuishi shuleni na kupata muda mwingi wa kujisomea.

Wanafunzi hao wamemueleza Waziri Mkuu kwamba kitendo cha kuishi nyumba kinawakosesha muda wa kujisomea kwa sababu ya hupangiwa kazi nyingi wanapofika nyumbani, hivyo kukosa muda wa kujisomea.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 9, 2018.

WAJAWAZITO CHALINZE WAKEMEWA KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI WAKATI WA KUELEKEA KUJIFUNGUA

$
0
0

Mganga Mfawidhi hospital ya wilaya ya Chalinze Msoga,Patricia Kihula akitoa ufafanuzi wa jambo ,wakati mbunge wa Chalinze Ridhiwani alipokwenda kutembelea hospital hiyo .(picha na Mwamvua Mwinyi)

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE .

HOSPITAL ya wilaya ya Chalinze ,Msoga mkoani Pwani ,inakabiliana na changamoto za uzazi ambapo baadhi ya akinamama wamekuwa wakitumia dawa za mitishamba ili kujifungua haraka hali inayosababisha wakati wa kujifungua kuwa na uchungu mkali ,mtoto kuchoka na kutokwa damu nyingi.
Mganga mfawidhi katika hospital hiyo Patricia Kihula ,alisema wapo akinamama wajamzito wanaoshikwa uchungu kisha kunywa mizizi ama dawa za kienyeji jambo ambalo ni hatari kwa mama na mtoto. Alisema kwasasa wanaendelea kutoa elimu katika klinik . 

Patricia alisema ,hali hiyo inasababisha mama akiwa tayari kanywa mizizi mchungu unakuwa mkali kabla ya njia kufunguka na mtoto kuchoka toka akiwa tumboni . “Tunatoa elimu kwa jamii wasiwe na tabia hiyo ,”na sisi tumeanza kupambana na tabia hiyo kwa kuwapa chai kabla ya kujifungua kwani tumegundua wanapewa dawa hizo ndani ya chai “. 

” Tumetoa maagizo chai inapaswa kutolewa kituoni hapa hapa ,na chai ikitoka nyumbani tunamwelekeza aliyeleta chai aanze kuionja ili kujiridhisha isiwe na dawa za kienyeji”alifafanua Patricia. Patricia alieleza kuwa , hakuna kesi ya kifo cha mtoto ama mama na badala yake zipo kesi mbili kila mwezi, za mama kuwa na uchungu mkali ,kutokwa damu nyingi au mtoto kutokwa kachoka sana . 

“Endapo inatokea mama kutokwa damu nyingi tunawapelekea hospital ya rufaa ya Tumbi kwa ajili ya upasuaji ili kuokoa maisha ya mama na mtoto na akitokwa damu nyingi pia huwa tukimchunguza kujua chanzo na hupatiwa matibabu” Patricia aliiomba akinamama wajawazito waache kutumia vitu,ama madawa ya majani,mitishamba ,dawa za kienyeji kwa kuweka kwenye njia ya uke ama kunywa bali wakisikia uchungu wakimbilie hospital kupata matibabu ya uhakika. 

Nae mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze, Rahim Hangai ,alisema wamepokea kesi za aina hiyo ambapo wameanza kutoa elimu ili kupunguza tatizo hilo . Alielezea ,wakitumia dawa hizo husababisha kupata uchungu wa kasi na kupasua kizazi ama mtoto akafa kabla ya kuzaliwa . Dk.Hangai alisema, dawa za kienyeji haziongezi uchungu ,waepuke madhara ambayo yataleta athari kwao. Mamamjamzito Hamisa Kheri alisema wengi wao wanajidanganya kutumia dawa hizo ili kuzaa haraka bila ya kuwa na uchungu kwa muda mrefu.

Halmashauri Zatakiwa Kutenga Maeneo ya Kilimo kwa Vijana

$
0
0
Na. Georgina Misama - MAELEZO

Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya Vijana kuyatumia katika shughuli za kilimo.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira  Mhe. Antony Mavunde wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhisho ya siku ya Vijana Duniani.

Mavunde alisema hadi hivi sasa Serikali imetenga takribani hekta laki mbili katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwapa vijana fursa ya kuyatumia katika shughuli za kilimo."Nazitaka Halmashauri zote nchini ambazo bado hazijatenga maeneo hayo, kufanya hivyo ili kuendana na kauli mbiu ya mwaka 2018 inayosema 'Mazingira salama kwa Vijana' ambapo serikali ina wajibu wa kuandaa mazingira hayo kwa vijana." alisema Mavunde.

Akiongelea kuhusu mwitikio wa vijana kwenye shughuli za kilimo, Mavunde alisema kuwa vijana wengi wameanza kujishughulisha katika kilimo na ipo mifano mingi hai ya vijana walioamua kujiajiri kwenye kilimo biashara kama SUGEKO na wanafanya vizuri.

Wakati huo huo Mhe. Mavunde amesema kuwa, Agosti 11 litafanyika kongamano kubwa la Vijana na Wadau wa Maendeleo ya Vijana katika Ukumbi Wa Mikutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.

kilele cha Maadhimisho hayo ni Agosti 12 Mwaka huu, ambapo Mhe. Antony Mavunde (Mb) anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika tamasha la vijana ambalo litafanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi kilichopo Tengeru litakalowashirikisha wadau mbalimbali wa Maendeleo ya vijana.

"Natoa wito kwa vijana wote nchini, wazazi na wadau wa Vijana washerehekee siku hii muhimu ili kwa pamoja tuonyeshe na kutambua umuhimu wa vijana kama washiriki wa Maendeleo ya nchi yetu, aidha nawaomba Vijana wote Tanzania wajitokeze na kushiriki katika Maadhimisho haya" alisema Mavunde.

Kauli mbiu ya Maadhimisho haya ni "Mazingira Salama kwa Vijana"

Mwaka 1999 Umoja wa Mataifa (UN) ulipitisha azimio Na. 54/120 la kuifanya tarehe 12 Agosti ya kila mwaka kuwa siku ya Vijana Duniani.Tanzania ilianza kuadhimisha siku hiyo mwaka 2000, ikiwa ni pamoja na nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kupita kwenye Gadi ya Heshma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akiangalia kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya siku moja nchini.

 Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na wanahabari hawapo pichani mara baada ya kikao chake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari hawapo pichani mara baada ya kikao chake na Rais wa Uganda Yoweri Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kutoka kwenye chumba cha mkutano wa Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAZIRI PROFESA NDALICHAKO AAGIZA VYUO VINAVYOTOA ELIMU YA 'UBABASHAJI' VIFUTWE

$
0
0

 Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa maagizo kwa Baraza la Elimu ya Ufundi(Nacte)kutosita kuchukua hatua ikiwamo ya kuvifuta vyuo ambavyo vitabainika kutoa elimu kwa ubabaishaji.

Pia amelishauri Baraza hilo kuhakikisha linasimamia na kutoa muongozo kuhusu program mbalimbali za utoaji elimu ya ufundi ambayo ametaka iwe inaendana na soko la ajira nchini ili kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kuajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi katika miradi mikubwa inayoendelea nchini.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi Baraza la Uongozi la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini ambalo Mwenyekiti wake ni Profesa John Kandoro.

Kuhusu vyuo ambavyo vinashindwa kutoa elimu bora, Profesa Ndalichako amesema baraza hilo lisisite kuchukua hatua ikiwamo ya kuvifutia usajili vyuo ambavyo vitabainika kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa.

Amefafanua haiwezekani vijana wawe wanalipa fedha kwenye vyuo ambavyo elimu wanayotoa ni ya ubabaishaji na kwamba hilo halikubaliki na lazima hatua zichukuliwe.

“Kuna vyuo ambavyo vipo kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kutoa elimu bora lakini pia kuna vyuo ambavyo vimeanzishwa kwa ajili ya biashara na hivyo ndivyo vyenye matatizo.“Kama kuna mtu aliamua kuwekeza kwenye kunzisha chuo kwa ajili ya kufanyabiashara basi atambue ni bora atafute kazi nyingine ya kufanya na sio hiyo tena,”amesema Profesa Ndalichako.

Amesisitiza kuwa anafahamu kuwa kuna vyuo ambavyo tayari vimefutiwa usajili lakini akalitaka baraza hilo kuendelea kuvifuatilia vyuo na vile ambavyo vitabainika kutokidhi vigezo basi navyo vifutiwe usajili.Ameongeza ni jambo la kusitikisha unapoona mtu amehitimu katika chuo fulani lakini uwezo wa kufanya kazi haupo na ukiuliza sababu utaambiwa ni ubabaishaji wa elimu inayotolewa na kwamba lazima hilo lifike mwisho.

Wakati huo huo Profesa Ndalichako ametoa ushauri kwa baraza hilo kuhakikisha elimu ya ufundi ambayo inatolewa kwenye vyuo vilivyopo nchini inakwenda sambamba na mahitaji ya Serikali ya Awamu ya Tano inayozungumzia Serikali ya viwanda nchini.

Amesema ili kufanikisha Serikali ya viwanda maana yake wanahitaji na watalaamu katika fani mbalimbali na hivyo ni jukumu la baraza kuandaa program za mafunzo ambazo zitaleta tija kwa Taifa.“Baraza ni vema mkafanya tafiti ambazo zitawapa picha halisi ya nini ambacho vijana wa Tanzania wanatakiwa kujifunza katika eneo hili la elimu ya ufundi kwa maslahi mapana ya nchi.

“Tunatarajia mafunzo ambayo mwanafunzi atayapata akiwa chuoni na baada ya kumaliza hapati changamoto ya kutafuta ajira.Lazima muandae program ambazo zitawawezesha vijana kuajirika kwa urahisi na hasa kipindi hiki ambacho kuna miradi mikubwa ya kihistoria inatarajia kuanza na mingine inaendelea,”amesema .

Amewakumbusha kuwa pamoja na maelezo ambayo ameyatoa kwa baraza hilo ni vema wataendelea kutekeleza majukumu yao kama ambavyo sheria, miongozo na kanuni inavyoelekeza.Kuhusu baraza hilo Profesa Ndalichako amesema analipongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ikiwemo ya kuhakikisha wanasimamia vyuo vya elimu ya ufundi chini kwa lengo la kuona elimu inayopatikana inakuwa bora.

Kwa upande wake Profesa Kandoro amesema baraza hilo hilo litasimamia vema majukumu yake na kwamba ushauri na maagizo ya Waziri Ndalichako watayafanyia kazi.Pia uongozi wa Baraza hilo nalo limemhakikishia Profesa Ndalichako kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha huku wakitumia nafasi hiyo kuelezea baadhi ya changamoto ikiwamo ya uhaba wa watumishi.
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungunza leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi Baraza la Uongozi la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
 Baadhi ya washiriki kwenye uzinduzi wa Baraza la Uongozi la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako(hayupo pichani).
 Mkurugenzi wa Nacte akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Baraza la Uongozi la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Profesa John Kandoro akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZEE AMRI ATHUMAN ‘KING MAJUTO’ LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Hamza Amri Athuman mtoto wa marehemu Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally akisoma dua kumuombea Marehemu Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Mara baada ya dua hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliongoza mamia ya wananchi kutoa heshima za mwisho katika msiba huo,anaefuta kushoto kwa Rais ni Rais Mstaafu awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete. PICHA NA IKULU

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA UMEPUNGUA KUFIKIA ASILIMIA 3.3

$
0
0

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 3.4 mwezi Juni, 2018.

Hayo yameelezwa leo na Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa sensa na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo alipokuwa akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Julai mwaka huu.Kwesigabo amesema, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.

“Kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula, ambapo bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya Julai, 2017 na Julai 2018 ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 9.5, mtama kwa asilimia 17.8, unga wa mihogo kwa asilimia 14.1, matunda jamii ya machungwa kwa asilimia 22.2, maharagwe kwa asilimia 5.8 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.5,” amefafanua Kwesigabo.

Ameendelea kusema kuwa ni zaidi ya miaka 15 tangu itokee tarakimu kama hiyo ya mfumuko wa bei ambayo iko vizuri kwa uchumi wa nchi.

Aidha ametaja hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kama ifuatavyo; Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 umeongezeka hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018. Kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.35 kutoka asilimia kutoka asilimia 4.28 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.

Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Julai 2018 leo Jijini Dodoma ambapo mfumuko huo umeshuka kwa asilimia 3.3 kwa mwezi Julai 2018 ikilinganishwa na asilimia 3.4 kwa mwezi June 2018.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Said Ameir akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kutoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Julai 2018 Jijini Dodoma.

Meneja wa Takwimu za mazingira na uchambuzi Bibi Ruth Minja akisisitiza kuhusu umuhimu wa takwimu katika kuchochea maendeleo .

Makamu Mwenyekiti NEC atembelea Kata ya Mlowa Bwawani kukagua maandalizi Uchaguzi Mdogo

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (kulia) akimueleza jambo  Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Elizabenth Gumbo (kushoto) wakati alipotembelea kata ya Mlowa Bwawani. Kulia ni Mwanasheria wa NEC, Hamidu Mwanga.
2 (7)
Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera, Elizabenth Gumbo (kushoto) akieleza maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani kata ya Mlowa Bwawani kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (katikati).Kulia ni Mwanasheria wa NEC Hamidu Mwanga.
5 (2)
Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hamidu Mwanga (katikati) akizungumza jambo na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Elizabenth Gumbo nje ya jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Chamwino mkaoni Dodoma.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Jaji Mbarouk Salim Mbarouk.

Hussein Makame, NEC aliyekuwa Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk ametembelea kata ya Mlowa Bwawani katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo.

Akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera Elizabenth Gumbo kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mtera, Jaji Mbarouk ameridhishwa na maandalizi ya Uchaguzi wa kata hiyo.
Jaji Mbarouk amewasisitiza wasimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo kutumia vipaza sauti kufikisha ujumbe kwa wananchi kwani njia hiyo itarahisisha kufikisha ujumbe wa uchaguzi kwa wananchi wengi zaidi wakiwemo wasiojua  kusoma na kuandika badala ya kutegemea zaidi taarifa za mabango.

Akitoa taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi wa kata hiyo kwa niaba ya, Afisa Uchaguzi wa Jimbo hilo Elizabenth Gumbo alisema maandalizi ya Uchaguzi huo yanakwenda vizuri.

Alisema wameshapokea vifaa vya awali vya Uchaguzi ikiwemo mfano wa karatasi ya kupigia, mabango ya Uchaguzi, fomu za Uchaguzi, bahasha za karatasi za kura na fedha za bajeti ya Uchaguzi wa kata hiyo.

Gumbo alisema ameshavitaarifu vyama vya siasa kuwasilisha orodha ya majina ya mawakala wa vyama vyao na kwamba wamewaomba wawsilishe na picha za mawakala hao na ratiba ya kuwaapisha inasubiri muda ambao watakapowasilisha orodha hiyo.

Alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni kuhusu mabadiliko ya ratiba ya kampeni za vyama vya CCM na Chadema ambavyo vimesimamisha wagombea katika uchaguzi wa kata hiyo kwa kuwa chama kimoja kimekataa kubadilisha ratiba yake ambayo tayari ilishakubaliwa na vyama vyote.

Naye Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Mlowa Bwawani Cleopa Leuna alisema kata hiyo ina vituo 19 vya kupigia kura na kuna vitu 12 12 viko kwenye maeneo ya wazi na vinahitaji kujengewa.Kuhusu kamati za maadili, Gumbo alisema tayari imeshaundwa ingawa bado haijafanya kazi yoyote kwa kuwa hakuna malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa utaratibu ambayo yanahitaji kujadiliwa na kamati hiyo.

“Hadi sasa hatujapokea malalamiko yoyote isipokuwa wakati wa uteuzi wa wagombea kulijitokeza malalamiko walituandikia barua, tukawajibu kuwa hamtakiwi kutoa pingamizi kwa njia ya barua tukawataka wajaze Fomu Na. 9 ya malalamiko wakakataa, zaidi ya hayo hatukupata malalamiko yoyote” alisema Gumbo.

“Hakuna uvunjifu wa amani uliojitokeza kwenye kampeni hadi kufikia leo na kampeni zinakwenda vizuri hakuna Mahali ambako tumepata taarifa za vurugu ya aina yoyote, watu wanajitokeza kwenye kampeni ingawa kwenye kampeni za chama kimoja wanakuwa wengi ikilinganisha na chama kingine” alisema.

Jaji Mbarouk baada ya kupokea taarifa hizo alishuhudia uwekaji mabango ya uchaguzi, orodha ya wapiga kura na tangazao la uchaguzi kwenye vituo vya kupigia kura vya Shule ya Msingi Mlowa Bwawani na Kituo cha Shule ya Msingi Nyamalela.

Kata ya Mlowa Bwawani inashiriki katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu ambapo vyama vya CCM na Chadema ndivyo vilivyosimamisha wagombea kwenye uchaguzi wa diwani wa kata hiyo.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images