Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1638 | 1639 | (Page 1640) | 1641 | 1642 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uteuzi wa baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya katika Ukumbi wa mikutano wa Utumishi jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika akisikiliza swali la mwaandishi wa habari (hayupo pichani) katika Ukumbi
  wa Utumishi jijini Dar es Salaam mara baada ya kutangaza majina ya baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya walioteuliwa na Serikali.  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua ramani ya muonekano mpya wa kijiji cha Makumbusho kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018. 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa wakioneshwa ramani ya muonekano mpya wa kijiji cha Makumbusho na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabula, kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania kilichofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam  Agosti 4, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Meja General Mstaafu Said Kalembo
   Wakazi wa Mkoa wa Lindi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania kilichofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.
  PMO_1181
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Lindi kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania kilichofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.
  PMO_1213
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea hundi ya sh. 20,000,000 kutoka kwa mdau wa maendeleo ya Mkoa wa Lindi, Bw. Otieno Igogo, ikiwa ni mchango kwa alibi ya kufanikisha Tamasha la Utamaduni wa Tanzania, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.
  PMO_1333
  Mke wa waziri Mkuu Mary Majaliwa,akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye kikao cha maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.
  PMO_1391 WHATSAPP
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi,kikao cha maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa kuchora ramani ya Tanzania katika Kijiji cha Makumbusho ambayo itatumika kwenye ujenzi wa nyumba za utamaduni wa makabila mbalimbali nchini.Amesema uamuzi huo utarahisisha watu kufika kwa urahisi katika nyumza za tamaduni za mikoa yao kwa kuwa watakuwa wanatumia ramani Tanzania.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumapili, Agosti 4, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa mkoa wa Lindi kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania katika Kijiji cha Makumbusho, jijini Dar es Salaam.“Kwa kutumia ramani hii kila mkoa utaweza kufika kwenye eneo lake kwa kutumia ramani ya Tanzania na mkoa wa Lindi tayari umeshaoneshwa eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba inayozingatia utamaduni wetu,” alisema.

  Alisema kwa tamaduni za makabila ya mkoa wa Lindi nyumba zote hujengwa kwa udongo na kuezekwa kwa makuti upande wa maeneo ya pwani ya upande mwingine huezeka kwa nyasi, ambapo aina zote zitajengwa ili kuwakilisha tamaduni za wakazi wa mkoa huo.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaasa wananchi wa mkoa wa Lindi ambao kwa mwaka huu ndio waandaaji wa tamasha hilo wadumishe mshikamano wao ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea katika kuboresha maendeleo.

  Alisema katika tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuanza Agosti 26 hadi 29 wahakikishe wanapeleka kila kitu ambacho kinahusiana na utamaduni wa mkoa huo ili kuwawezesha Watanzania wengine wajue kama vyakula na mavazi .Pia alishauri wawepo wazee wenye kujua historia ambao watasimulia utamaduni wa wananchi wa Lindi pamoja na kutambulisha ngoma zao za utamaduni. “Halmashauri zote za mkoa wa Lindi zitumie fursa hii kutangaza vivuti vya utalii vilivyopo na Kilwa walete mtu atakayeelezea kuhusu magofu,”.

  Waziri Mkuu alisema tamasha hilo ni muhumu kwa sababu utamaduni ulianza kufifia nchini kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia jambo ambalo lingeweza kuuondoa katika kumbukumbu, hivyo aliwashauri siku ya tamasha hilo wavae nguo za kitamaduni kulingana na kabila husika.Kadhalika, Waziri Mkuu aliwapongeza viongozi wa mkoa wa Lindi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Godfrey Zambi kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri mwenendo wa zao la korosho.

  Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla alisema mwaka huu Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania linawakilishwa na jamii kutoka mkoa wa Lindi na kwamba anatumaini watafanya vizuri kwa kuwa uwezo na nia wanayo.Profesa Mabula alisema mwaka 1994 Bodi ya Makumbusho ya Taifa ilianzisha siku ya utamaduni ili kutoa fursa kwa jamii mbalimbali nchini kuonesha utajiri walionao katika tamaduni zao na ufanisi wa siku hiyo unatokana ushirikishwaji wa wanajamii husika.

  0 0

  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, na mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars  Charles Boniface Mkwasa afanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.

  Mkwasa yuko jijini New Delhi, India ambako amefanyiwa upasuaji huo mkubwa na imeelezwa bado yuko katika chumba cha usimamizi maalum, yaani ICU.

  Mkwasa alisafiri takribani wiki moja iliyopita kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu baada ya kugundulika na tatizo la moyo hapa nchini.

  Mkwasa aliamua kujiuzulu nafasi yake ndani ya Yanga kwa ajili ya kujiuguza.

  0 0  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akiongea na Wahitimu wa mafunzo ya udereva wa magari ya abiria wakati wa Mahafali ya kuhitimisha mafunzo yao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe akiwataka Wahitimu hao wakawe mabalozi wa madereva wengine ambao hawajapata mafunzo kama hayo ili nao wajitokeze siku za usoni.
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe akiwataka Wahitimu hao wakawe mabalozi wa madereva wengine ambao hawajapata mafunzo kama hayo ili nao wajitokeze siku za usoni.(Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)
  Baadhi ya wahitimu waliopata mafunzo ya uendeshaji wa magari ya kubeba abiria ambayo yaliendeshwa na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa muda wa wiki mbili wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo wakati wa Mahafali hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Arusha. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)

  Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha

  Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kanda ya Kaskazini wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa madereva 350 wa magari ya abiria ambao awali walikuwa na Leseni pekee bila vyeti.

  Mafunzo hayo yaliyofungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo katika Chuo Cha Ufundi Arusha, awali yalifunguliwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wiki mbili zilizopita.

  Akizungumza katika siku hiyo ya Mahafali, Mkuu huyo wa mkoa, kwanza kabisa alilipongeza Jeshi la Polisi na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa kuamua kuendesha mafunzo hayo lakini pia kwa wahitimu wenyewe kwani ni jambo zuri na lenye maslahi kwenye maisha yao.

  Alisema jitihada hizo zinalenga kupambana na ajali kwani madhara yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo, ulemavu, kupata hasara kwenye mali lakini pia zinaweza kusababisha kutotoa fursa za ajira kwa madereva wenye matukio ya kusababisha ajali.

  Mkuu huyo wa mkoa alisema pamoja na mafunzo waliyoyapata wahitimu hao lakini watatakiwa waepuke unywaji wa pombe wakati wanaendesha vyombo vya moto kwani ajali nyingi zinasababishwa na ulevi, huku akilitaka Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha usalama Barabarani kuongeza jitihada katika kupima ulevi kwa madereva.

  “Pamoja na Mafunzo mliyoyapata kuwajengea uwezo lakini kama hamtaepuka unywaji wa pombe wakati mnaendesha vyombo vya moto ajali zitaendelea kutokea”. Alionya Bw. Gambo

  Aliwataka Madereva hao kuwa na nyaraka zote na vifaa vyote muhimu kama Vizima Moto pindi wanapokuwa kazini na kusema ukamilifu wa vitu hivyo vitasaidia kuepusha mabishano na askari wa Usalama barabarani.

  Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi alisema anaamini mafunzo hayo yamewajengea uwezo na kuwapa umahiri wa kuendesha magari ya abiria.

  Alisema mafunzo hayo yatasaidia mkoa wa Arusha kuwa ni miongoni mwa mikoa salama kwa kuepuka ajali mbaya na kuahidi kuendeleza na kuzidi kuimarisha ushikiano kati ya Jeshi hilo na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ili mwisho wa siku Madereva wote wapate mafunzo hayo.

  Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe alisema kwamba, wahitimu hao watakuwa Mabalozi wa wenzao na kuonya kwamba wale wote ambao wanatengeneza na wanaonunua vyeti vya VETA bila kupata mafunzo watakamatwa na kufunguliwa Mashtaka.

  Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kaskazini Bw. Anjelus Ngonyani alisema kwamba ajali nyingi zinasababishwa na makosa ya kibinadamu ambayo yanatokana na kukosa mafunzo. Alisema Chuo hicho kinatoa mafunzo bora na yanayokidhi viwango na kuwataka madereva wazidi kujitokeza.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MICHUANO ya Ndondo Cup yamefikia tamati leo baada Timu ya Manzese United kuibuka mabingwa wapya wa Ndondo Cup 2018 baada ya kuifunga timu ya Kivule kwa goli 1-0 mechi iliyofanyika leo Jijino Dar es Salaam.

  Mchezo huo ulioanza majira ya 10 alasiri katika uwanja wa Bandari ulichezeshwa na Mwamuzi mwenye beji ya FIFA Hery Sasii akisaidiwa na Mwamuzi wa pembeni Soud Lila na Hellen Mduma.Mchezo huo ulianza kwa kasi katika dakika ya 9 Manzese United wanapata goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Hamza lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

  Umakini wa safu ya ushambuliaji ya Kiluvya United iliwanyima fursa ya kusawazisha goli hilo ambapo waliweza kukosa nafasi nyingi za wazi.Kipindi cha pili kilianza Kiluvya wakisaka goli la kusawazisha ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika Manzese walifanikiwa kushinda goli 1-0 na kuwa mabingwa wapya wa Ndondo Cup.

  Mgeni rasmi wa mashindano Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shoza aliweza kukabidhi kombe kwa mabingwa wapya wa Ndondo Cup akiwa ameambataba na viongozi mbalimbali Nchini.

  Fainali hiyo ya kipekee ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mbunge wa Iramba Mashariki Mwingulu Nchemba aliyekabidhi hundi ya Milioni 10 kwa mabingwa, Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, Mkuu wa Wilaya Temeke Felox Lyaniva, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu, Rais wa TFF Wallace Karia na Mwenyekiti wa DRFA Almas Kasongo.

  Mbali na hao pia Manzese waliwakilishwa na Meya wa Jimbo la Ubungo Boniface Jacob na wasanii wanaoishi kwenyr jimbo hilo Akiwemo Msanii Madee na Shilole sambamba na viongozi wengine wa kimpira.

   Mbunge wa Iramba Mashariki Mwigulu Nchemba akikabidhi  mfano wa hundi yenye thamani ya Milioni 10 kwa Nahodha wa timu ya Manzese baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Kivule United

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akikabidhi kombe kwa Nahodha wa Manzese United baada ya kuibuka na ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Kivule United katika Mchezo uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 

  Mchezaji wa Manzese United Idd Nado akiwa amemlaza chini mchezaji wa Kivule United katika fainali ya Ndondo Cup iliyofanyika Leo Jijini Dar es Salaam na Manzese United kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0.
   Kikosi cha Kiluvya United wakiwa katika picha ya Pamoja
  Kikosi cha Manzese United wakiwa katika picha ya pamoja

  0 0

  Hiza ni aina ya ya mbegu za viazi lishe zilizopo katika shamba la mfano la SUGECO Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro, ambalo washiriki wa mafunzo ya uongezaji thamani wa viazi lishe walitembelea mwishoni mwa mwezi uliopita, ambapo pia walijinea viazi kutoka kwa mkulima Sparta . Viazi Lishe vina asilimia kubwa ya vitamini A zinazofaa kwa afya za walaji na hasa kwa akina mama mama wanaojiandaa kupata mimba, wajawazito, waliojifungua pamoja na watoto . PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;0689425467,0754264203,0715264202. 
  KABODE
  KABODE
  KABODE 
  KIEGEA
  KIEGEA 
  MAJANI YA MATAYA
  KIAZI CHA MATAYA
  MAJANI YA EJUMULA 
  KIAZI CHA EJUMULA 
  KIAZI LISHE CHA KAKAMEGA 
  KIAZI CHA KAKAMEGA

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kulia) na mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wahitimu wa darasa la saba katika shule hiyo iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kulia) na mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wahitimu wa darasa la saba katika shule hiyo iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi St. Aloysius, Kenneth Sinare (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kulia) mara baada ya hotuba yake.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga na mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam akihutubia wanamahafali na wageni waalikwa.
  VIONGOZI wa shule mbalimbali nchini Tanzania wameshauriwa kuhakikisha wanazifanya shule zao kuwa na mazingira salama, yenye utangamano, ushirikiano, upendo pamoja na furaha kwa wanafunzi ili yaweze kumjenga mtoto vema kielimu na maadili katika jamii.

  Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

  Alisema shuleni, watoto wanapaswa kupewe ushauri nasihi na nasaha kadri inavyoitajika, huku wakiwa huru kutoa dukuduku zao na matatizo yao kwa walimu na kuyatatua kadri ya uwezo wao.

  “Kuna kila sababu watoto kupewa ujuzi wa kutumia uwezo na mikono yao kufanya kazi na ujuzi wa kutumia akili zao za sasa kutatua migogoro yao kwa ngazi yao,” alisema Bi. Sanga katika hotuba yake.Aliwataka walimu mbali na kumjenga mwanafunzi kielimu kuna haja ya kuwaandaa pia kuwa wazalendo wa taifa lao na kikazi kinachojali wasionacho kama tunavyowajali watu walionacho.

  “…Shule inatazamwa kama familia nje ya familia maana watoto wanatumia muda mwingi kuwa shuleni zaidi ya ule wawapo na familia zao nyumbani. Hofu ya Mungu ndio msingi wa mafanikio katika jambo lolote kwani inamjengea mtoto ujasiri, nidhamu na usubutu, naomba haya tuyazingatie pia.

  Aidha aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa elimu, TAMWA katika mpango mkakati wake wa miaka mitano 2016 hadi 202, lengo namba tatu limehimiza kushughulikia masuala ya elimu kwa watoto wa kike, unyanyasaji wa jinsia, ukatili kwa watoto na ndoa za utotoni. Pamoja na hayo, aliwataka wazazi na walezi kutambua kuwa; mtoto umleavyo ndivyo akuavyo., hivyo kumjengea malezi mema mtoto ni kumjengea mazingira bora yenye maadili na usikivu katika jamii.

  “…Wazazi na walezi ambao mmeichagua shule hii kwa vyovyote mlitamani watoto wenu wawe wazalendo, wapenda nchi, na wapate elimu bora ujuzi na maarifa yanayofaa katika kuelekea kutimiza malengo ya mtoto aliyojiwekea (ndoto zake).”

  Aliwataka wazazi kuwasaidia watoto wao kujitathmini na malengo yao hapo baadaye ili waweze kuyatimiza katika maisha yao. Ufuatiliaji wa mwenendo na masomo ya mtoto, kuwapa ushauri, upendo usaidizi pamoja na kuwa karibu zaidi na mtoto ili akiwa na tatizo lolote aweze kuwa huru kujieleza.Alisema TAMWA imekuwa ikishauri siku zote kwamba ni vema mzazi au mlezi akawa rafiki wa mwanaye ili kujenga ukaribu na upendo wa dhati kwao.

  Kwa upande mwingine aliwataka wahitimu hao kuanza kuwa wazalendo na kujitolea kwa jamii ili kuwa mfano kwa wengine na pia kujenga upendo, huku wakitafsiri elimu walioipata katika hali halisi ndani ya jamii.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kulia) na mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wahitimu wa darasa la saba katika shule hiyo iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa darasa la awali wa Shule ya Msingi St. Aloysius wakitoa burudani kwenye sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya shule hiyo iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI,VIGWAZA

  DIWANI wa kata ya Vigwaza ,Bagamoyo , Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),amechangia mabati 242, mifuko ya saruji 100 na matofali 3,000 vyenye thamani takriban sh.milioni 12 katika kijiji cha Chamakweza,Mnindi na kitongoji cha Serengeti.

  Amesema ametoa vifaa hivyo vya ujenzi ,ili kutekeleza ilani ya CCM na kuunga mkono juhudi za wananchi katika miradi wanayoiibua na miradi ya serikali.Bharwani alitoa michango hiyo, katika ziara yake ya kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo katika vijiji vilivyopo kata ya Vigwaza ,ambapo ameanza kwenye vijiji vya Chamakweza,Mnindi na kitongoji cha Serengeti.

  "Shule ya msingi Chamakweza ambayo darasa moja na ofisi havina mabati nimetoa mabati 96 yenye thamani ya sh.milioni 2.8 " #"Katika kitongoji cha Serengeti kilio cha wananchi ni kupata shule ya awali ,na tunashukuru halmashauri imeleta mshauri kutoka idara ya elimu msingi kwenye mkutano huu kwani tumepata nafasi ya kumueleza adhma yetu na kutupa maelekezo" alifafanua .

  Kutokana na hilo ,Bharwani alitoa ,mifuko ya saruji 50 ,matofali 2,000 ,licha ya kuendelea kwa hatua nyingine zitakazozingatia vigezo vinavyotakiwa ili kufikia hatua ya kupata kibali cha kujenga na kuwa na shule si tu ya awali bali shule ya msingi.Akiwa kijiji cha Mnindi ambacho kinaendelea na ujenzi wa zahanati alisema ,"wakati ujenzi ulipoanza alichangia mifuko 50 na kwasasa amechangia mabati 96 yenye thamani ya milioni 2.8.

  "Serikali inafanya mambo makubwa kwa utkeleza miradi mbalimbali ya reli ,barabara,umeme,afya,elimu na maji hivyo lazima viongozi wa chini tuunge mkono juhudi hizo ,na kushirikiana na rais Dk.John Magufuli kutatua kero mbalimbali kuanzia ngazi ya chini ""Rais karudisha imani kwa wananchi na wadau wanaoshiriki kusaidia masuala mbalimbali, katupa jeuri CCM kutokana na kutekeleza ahadi na ilani kwa kugusa kila eneo ili kuinua maendeleo na uchumi ." alisema Bharwani.

  Bharwani aliwataka ,viongozi wa kuchaguliwa na watendaji wengine kuunganisha nguvu na ya wananchi kuisaidia serikali ya CCM ili kipiga hatua zaidi wakati nchi ikielekea kwenye uchumi wa kati .Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ,Erasto Meshack kutoka idara ya elimu msingi alisema ,kwa mujibu wa miongozo kigezo cha kwanza ili shule iitwe shule inapaswa kujengwa katika eneo lisilozidi hekari kumi . .

  Alieleza ,ili shule iweze kufunguliwa isipungue majengo sita,stoo,vyoo vya walimu ,wanafunzi na nyumba za walimu.Nae ,mwenyekiti wa kijiji cha Vigwaza Ramadhani Kirumbi, alimshukuru diwani huyo kwa michango yake anayojitolea ,kwani kutoa ni moyo .Alisema endapo mradi wa ujenzi wa shule ya awali ya Sekibwa kitongoji cha Serengeti ukifanikiwa utawasaidia watoto ambao hutembea zaidi ya km.tano kufuata elimu hiyo nje ya eneo hilo .Mwenyekit wa CCM kata ya Vigwaza ,Shederi Mkole ,alimpongeza Bharwani kwa kujitoa kwake kutekeleza ilani ya CCM.
  DIWANI wa kata ya Vigwaza , Mkoani Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),akizungumza katika kijiji cha Chamakweza wakati alipofanya ziara yake katika kijiji hicho ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti.(picha na Mwamvua Mwinyi)
  DIWANI wa kata ya Vigwaza , Mkoani Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),akizungumza wakati alipotembelea baadhi ya ujenzi  wa madarasa katika kijiji cha Chamakweza wakati alipofanya ziara yake katika kijiji hicho ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti.
  Mkazi wa Chamakweza ,Philemon Molel akimshukuru diwani wa kata ya Vigwaza ,Mohsin Bharwani wakati alipokwenda kutembelea miradi na kijijini hapo ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti. (Picha na Mwamvua Mwinyi).

  0 0

  Na Dotto Mwaibale, Singida

  MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu (pichani), ametoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wote wa kidato cha tano na sita katika Jimbo lake ambao wameenda kusoma katika shule mbalimbali nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kingu alisema wanafunzi hao wamepata ufadhili huo kupitia taasisi yake ya Kingu Scholarship Programe na kuwa tayari wamekwisha walipia ada zao.

  "Nimeona ni vizuri wanafunzi wote waliopo katika jimbo langu ambao wanaenda kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na sita niwalipie ada kwani hilo ni moja ya jukumu langu kama mbunge wao" alisema Kingu.

  Alisema katika suala la kuinua elimu ni jukumu la kila mmoja wetu na si kuiachia serikali pekee ambayo inamaeneo mengi ya kushughulikia ndio maana aliwiwa kuwasaidia wanafunzi hao.

  Alisema watoto wengi wanauwezo wa kimasomo lakini baadhi yao wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali hivyo wakiachwa bila ya kusaidiwa taifa litakosa wataalamu siku za usoni.

  Kingu alisema ameanzisha taasisi hiyo kwa lengo la kuwasaidia watoto wa wakulima ambao watafaulu kidato cha nne na kupata nafasi shule za serikali hapa nchini kuwa watalipa ada zao hadi hapo watakapo maliza masomo yao kwani elimu ndio silaha pekee ya kumkomboa mkulima na mfugaji.

  Alitaja orodha ya baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili huo pamoja na shule wanazokwenda kusoma kuwa ni Magret Emanuel ambaye anakwenda Sekondari ya Monduli, Raymond Yahya (Same Sekondari), Aisha Jumanne (Loleza), Mariam Rashid (Ifakara) na Petro Shija, Tarime.

  Kingu aliwataja wanafunzi wengine kuwa ni Samwel Suku anayekwenda Iyumbu Sekondari, Faudhia Hamisi (Urambo), Yakini Ezekia (Rungwe), Latifa Rashidi (Igowole), Baraka Ibrahim (Aman Abed), Bertha Emmanuel (Bungu), Binzura Shabani (Maweni) na John Lameck (Ilboru)

  Wanafunzi wengine ni Haruna Juma anayekwenda Bihawana Sekondari, Nyamata John (Isimila), Debora Elibariki (Iyumbu), Shamimu Ali (Anaghwai), Lambo Mahona (Loleza) na David Khalfan anayekwenda Sekondari ya Tukuyu TTC. 

  0 0

  Benki ya CRDB imeendelea kung'ara katika maonyesho ya nanenane kitaifa yanayoendelea Mkoani Simiyu kwenye viwanja Vya Nyakabindi Bariadi.

  Ushiriki wa Benk ya CRDB umekonga nyoyo za wananchi kwa kuwa Benki inatoa huduma zake 'live" kwa kutumia Mobile Branch pia kwa kutumia Mawakala wake 'Fahari Huduma Wakala'. Wateja wanaweza kuweka pesa ama kutoa pesa zao ..Pia wananchi wanapata fursa ya kupewa maelezo kwa kina kuhusu huduma zingine zitolewazo na benki ya CRDB .kama salary advance, mikopo y awafanyakazi,simbanking, SimBanking App, QR code/Mvisa, akaunti mbalimbali.

  Akizungumza katika Banda la Benki ya CRDB Meneja wa Benki ya CRDB mkoani Simiyu, Ndugu Richard Karatta ametoa wito na mwaliko kwa wateja na wananchi wote wanaotembelea maonyesho hayo kuembelea Banda la Benki ya CRDB ili kufaidika na uwepo wake thabiti ambapo imedhihirisha kuwa "Ulipo Tupo".

  Kauli Mbiu ya NaneNane-2018 ni WEKEZA KWENYE KILIMO,UVUVI NA MIFUGO KWA MAENDELEO YA VIWANDA BENKI YA CRDB NI MDAU MKUBWA KATIKA HIZI SEKTA AMBAZO NI WEZESHI KATIKA USTAWI WA UCHUMI WA VIWANDA.

  Na udau wa Benki ya CRDB unachagizwa na mtandao mkubwa/mpana wa matawi yake zaidi ya 260 na ATMs zaidi ya 550 na Fahari Huduma wakala zaidi ya 3300 Pia wananchi wanaweza kupata huduma za Benki kupitia Simu zao za mikononi. SimBaking, SimBanking App, Internet Banking. alifafanua Ndugu, Richard Karatta.
  Wateja wakiwa kwenye Banda Benki ya CRDB kupata ufafanuzi kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na na Benki ya CRDB katika kuchochea maendeleo ya viwanda kupitia Sekta za Kilimo, Uvuvi na Mifugo katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
  Ofisa wa Benki ya CRDB Bi. Florence Mboli (kulia), akimueleza mteja kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoa wa Simiyu. 
  Ofisa wa Benki ya CRDB, Florence Mboli (kushoto), akiwaeleza wateja kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, mwishoni mwa wiki.
  Ofisa wa Benki ya CRDB, Florence Mboli (katikati), akiwaeleza wateja kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, mwishoni mwa wiki.
  Wateja wakipata huduma za kuweka na kutoa fedha katika tawi la benki ya CRDB katika viwanja vya Nane Nane.
  Wateja wakipata huduma mbalimbali katika Bande la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.
  Muonekano wa Banda la Benki ya CRDB.
  Ofisa wa Benki ya CRDB, Petronela Beda (kushoto), akiwaeleza wateja kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.
  Ofisa wa Benki ya CRDB, Perpetua Sarwaty, akiwaeleza wateja kuhusu huduma zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB. 
  Ofisa wa Benki ya CRDB, Perpetua Sarwaty, akiwaeleza wateja kuhusu huduma zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB. 
  Wateja ewakiwa katika banda la Benki ya CRDB.

  0 0

  Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua hali ya uhifadhi wa mahindi na kubaini akiba ya chakula mara baada ya kutembelea Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.
  Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akijadili jambo na Mratibu wa mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa Mhandisi Imani Nzobonaliba baada ya kutembelea Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.
  Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akijadili jambo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa katika ofisi ya Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.  Na Mathias Canal, WK-Ruvuma

  Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameupongeza uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa kasi ya utekelezaji Wa ujenzi wa mradi wa maghala na Vihenge vya kisasa.

  Mhandisi Mtigumwe ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi ujenzi wa mradi huo leo Tarehe 4 Agosti 2018 katika kanda ya wakala Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ambapo alitaja maeneo yatakayojengwa mradi huo kuwa ni pamoja na Wilaya ya Dodoma Mkoani Dodoma, Mpanda (Katavi), Songea (Ruvuma), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara).

  Mradi huo ni matokeo ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland kusaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula

  Alisema wizara ya kilimo imeingia katika ujenzi huo wa maghala na vihenge vya kisasa ambao utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

  Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inahitaji watumishi wachapa kazi na kwamba wananchi na jamii kwa ujumla wake inategemea hifadhi ya chakula kilichohifadhiwa na NFRA pindi inapotokea kadhia ya ukosefu au upungufu wa chakula.

  Akikagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa, Mtigumwe alijionea jinsi mkandarasi kutoka kampuni ya Ferum ya nchini Poland anavyoendelea na ujenzi na ujenzi ili kukamilisha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano.Katibu Mkuu huyo alimemsihi mkandarasi kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi hiyo mwezi Desemba mwakani kwa mujibu wa mkataba.

  Pia, alitoa msisitizo kwamba kwa kuwa teknolojia ya ujenzi wa vihenge vya kisasa ni ngeni nchini, atawasiliana na Bodi ya wakandarasi (Engineers Registration Board-ERB) ili kuweza kupatiwa Wahandisi vijana watakaokuwa wakihusika moja kwa moja katika mradi huo kwa ajili ya kujifunza na kubakisha utaalamu huo nyumbani Tanzania.

  Mhandisi Mtigumwe amefanya mazungumzo na watumishi wa NFRA Kanda ya Makambako ambapo aliwasisitiza kufanya kazi kwa weledi mkubwa, nidhamu na utumishi uliotukuka.

  Mikataba ya ujenzi ilianza kufanya kazi tarehe 9 Disemba 2017 ambapo Mradi huo utatekelezwa na kampuni mbili za Kandarasi kutoka Poland ambazo ni (Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o) ambapo msimamizi wa utekelezaji wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na kuhusisha ujenzi wa vihenge vya kisasa, maghala ya kisasa pamoja na ukarabati wa ofisi.

  Mhandisi Mtigumwe amefanya ziara ya siku moja Mkoani Ruvuma akiwa safarini kuelekea Mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki kilele cha maadhimisho ya maonesho ya wakulima MKoani humo.

  0 0

  Ni katika viwanja vya Feste-Platz,wakati onyesho hilo la kimataifa la GaiExpo 2018 na International Afrika Festival Tubingen 2018 mwaka huu,  nchi lengwa ikiwa ni Tanzania.

  Baadhi ya bendi za muziki na wasanii wa Tanzania wameshawasili nchi Ujerumani wakiwa tayari tayari kutumbuiza katika maonyesho hayo makubwa barani ulaya.
  Kundi maarufu ya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni maarufu pia kwa majina kama vile "Viumbe wa ajabu Anunnki aliens" au "Watoto wa Mbwa" na mzimu wao "Bongo Dansi" kutoka special planet Bongo Land Tanzania watatingisha jukwaa siku ya jumamosi 11Agosti 2018.

  Bendi hiyo iliyoanzishwa 1993 na kiongozi wake Ebrahim Makunja alimaarufu kama Kamanda Ras Makunja mkuu huyo wa viumbe wa ajabu wa Ngoma Africa band  muziki wao umewanasa washabiki wa kimataifa kwa takribani zaidi ya miaka 25 na kujizolea sifa za kimataifa majukwaani.

  Miaka miwili hiliyopita waliwadatisha washabiki nchini Israeli kwenye uwanja wa  Yitzhak Rabin Square,mjini Tel Aviv. Hivi sasa wanatamba na CD yao mpya "Awamu ya Tano Uwanjani" ambayo unaweza kuisikiliza hapa www.ngoma-africa.com

  0 0


  0 0


  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya (kulia) mipira itakayotumika kufunza vijana kuhusu SDGs na wajibu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya (katikati) akimkabidhi Necta Mussa (kulia) kijana ambaye aliwakilisha wenzake mipira itakayotumika kufunza vijana hao kuhusu SDGs na wajibu wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto).
  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea mipira hiyo ya kuhamasisha vijana kuhusu SDGs na wajibu kupitia michezo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi wa vijana kutoka YES Necta Mussa na kushoto ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi mipira yenye chapisho la SDGs kwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya (kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa vijana kutoka YES Necta Mussa (kulia) akitoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa mara baada ya kupokea mipira hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

  0 0


  Ofisa Mtenda Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sababa Moshingi,(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Dar es Salaam juzi baada ya Benki kuu kuamua kuziunganisha Beki ya wanawake Tanzania TWB nakuwa benki moja.katikati ni Mkurugenzi wa mpango mkakati Muondakweli Kaniki,na kulia ni Mwanasheria wa Benki ya (TPB)Mystica Mapunda Ngongi.Picha na Prona Mumwi

  0 0

  KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC) ni mojawapo ya taasisi za Serikali zinazoshiriki kwenye Maonesho ya 25 ya Nanenane ambayo yameanza kufanyika nchini kuanzia Agosti 1 mwaka huu na yanatarajiwa kumalizika Agosti 11 huku TIC ikitumia nafasi hiyo kuelezea majukumu yake.

  Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda.Ili kuhakikisha taarifa na huduma kwa wawekezaji zinawafikia wadau wao kwa wigo mpana Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe amefanikisha kituo kushiriki kwenye maonesho katika mikoa mbalimbali nchini kupitia ofisi zao za Kanda.

  Akizungumzia maoesho hayo Mwambe amesema lengo la kushiriki ni kutoa elimu kwa umma kuhusu taasisi yao, kazi wanazozifanya, huduma wanazozitoa kwa wawekezaji na taratibu zinazohitajika ili wadau (wazawa na wageni au ubia) waweze kujisajili na Kituo.

  Hivyo Mwambe, anafafanua kuwa TIC inapatikana kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane nchini ambapo amesema wanashiriki katika Mkoa wa Simiyu(viwanja wa Nyakibindi) na Mbeya(viwanja vya Nanenane).

  Pia mkoani Arusha(viwanja vya Njiro), Lindi (Ngongo),Tabora(Ipuli), Morogoro (Nanenane) na Dodoma(Nzuguni). Hivyo Mwambe ametoa mwito kwa umma na wadau kutoka mikoa ambapo maonesho yanafanyika na kutoka Mikoa jirani kutembelea mabanda ya TIC yanayopatikana katika maonesho hayo.

  "Lengo ni kuwawezesha kupata taarifa na huduma za uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na namna ambavyo wawekezaji wazawa na wageni wanavyonufaika na huduma za Kituo."Kwa ujumla TIC inatumia maonesho ya Nanenane ili kuutarifu umma kuwa TIC inatoa huduma kwa wawekezaji wazawa na wageni kupitia ofisi zetu za Kanda ambazo zinapatikana katika Mikoa ya Mwanza, Moshi, Mtwara, Kigoma, Dodoma, Mbeya na Dar es Salaam,"amesema.

  Ameongeza kuwa wananchi waliopo katika mikoa husika au mikoa ya jirani anawaomba kutembelea ofisi hizo ili kupata huduma kwa karibu na ndani ya muda mfupi badala ya kusafiri masafa marefu mpaka Makoo Makuu Dar es Salaam kufuata huduma ambazo anaweza kuzipata mahali alipo.

  Amesisitiza uamuzi wa kuweka ofisi za kanda ni kumpunguzia mdau gharama za kusafiri ili kufuata huduma Dar es Salaam na pia kupunguza muda wa kupata huduma husika.

  Pia TIC inawakumbusha umma kuwa wadau wa uwekezaji wanapata huduma za vibali vya uwekezaji nchini kupitia mfumo wa mahala pamoja ndani ya jengo moja la TIC ambapo maofisa wa Taasisi za Serikali zipatazo 10 wanatoa kuhudumia hizo. Amezitaja baadhi ya taasisi hizo ni Brela, TRA, NEMC, TFDA, TBS, OSHA, NIDA, Idara ya Uhamiaji , Idara ya kazi na Wizara ya ardhi.

  Pamoja na ufafanuzi huo pia amesema TIC imeshiriki kwenye sherehe za ufunguzi wa maonesho hayo kitaifa uliofanyika mkoani Simiyu kwenye Viwanja vya Nyakibindi Agosti 3 mwaka huu.Ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Kilimo Dk.Charles Tizeba na katika hotuba yake alielezea kwamba maonesho ya 25 ya Wakulima Kitaifa yamefanyika mkaoani Simiyu kwa mara ya kwanza na kufana.

  Na kwamba maonesho ya 26 na 27 vilevile yatafanyika Mkoa wa Simiyu. Kutokana na taarifa hiyo Dk. Tizeba ameutaka Mkoa huo kujipange kwa ujio wa maonesho hayo ikiwa ni pamoja na kuweka majengo ya kudumu na kutumia uwanja wa nyakibinda kwa shughuli mbalimbali. Aidha ameelezea namna ya kuboresha maonesho hayo ili yawe bora zaidi .

  Kuhusu baadhi ya changamoto ambazo zimejitokeza kwa mujibu wa Dk.Tzeba ni uchache wa huduma za jamii mkoani Simiyu hasa hotel kwani washiriki wengi wa maonesho wamelala nje ya Mkoa wa Simiyu wakati wote wa maonesho katika Wilaya za Bariadi na Bunda. Kutokana na changamoto hiyo ametoa maelekezo kuwa Mkoa kuanzia sasa uwekeze zaidi katika ujenzi wa hotel ili kutatua changamoto ya malazi washiriki maoneshona wageni mbalimbali wanaotemnelea Mkoa wa Simiyu.

  Akizunguma katika ufunguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anton Mtaka amewashukuru wadau wote walioshiriki kufanikisha maonesho hayo kutokana na michango ya hali na mali. Hata hivyo Mtaka ameeleza kuwa Mkoa wa Simiyu una fursa nyingi ambazo bado hazijatumika ipasavyo, hivyo anakaribisha wadau wa uwekezaji kuwekeza katika sekta za huduma (hotel, hospitali, shule) kilimo, viwanda, utalii, maji na miundo mbinu kwa ujumla.

  Imeelezwa uwepo wa changamoto mahali ni fursa kwa upande mwingine. Hivyo Kituo kitashirikina na uongozi wa Mkoa wa Simiyu katika juhudi za kuhamasisha na kuvutia uwekezaji katika maeneo husika cha msingi, vigezo na masharti yatazingatiwa.
   Latiffa kigoda Afisa Habari wa TIC akitoa maelekezo kwa wadau waliotembelea banda la TIC  Kanda ya Ziwa
   Bw. Venance Mashiba wa Kanda ya Mashariki akitoa maekezo kwa washiriki wa nane nane yanayofanyika Mkoani Morogoro
   Bw. Sindano Ajelandro Afisa Uhamasishaji Uwekezaji akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea banda la TIC  88 Mkoani Mbeya
   Bw. Fanuel Lukwaro Meneja wa TIC Kanda ya Ziwa akisikiliza kwa makini hoja za mdau alipotembelea banda la TIC 88 Mkoani Simiyu
  Bw.Doto Stanley Meneja Kanda ya Kusini akishiriki 88 Mkoani Lindi

  0 0

  Kutoka kulia ni Mtafiti kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Yesaye Sungita, wa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Tume Peter Ngamilo akiguatiwa na Mtafiti wa Tume hiyo Jerome Mwimanzi wakitoa elimu kwa mmoja wa mgeni aliyetembelea katika banda hilo katika maonyesho ya nane nane Kanda ya Kaskazini katika viwanja vya Themi Njiro Arusha.


  Na.Vero Ignatus -Arusha 

  Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania inaendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji juu ya uthibiti wa viasilia vya mionzi vinavyoweza kupatikana kwenye mazao ya chakula na mifugo ili kuongeza usalama wa mtumiaji dhidi ya madhara hatari yanayosababishwa na mionzi.

  Katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini wanatoa elimu juu ya nyuklia inayoweza kuwa mkombozi kwenye ukuaji wa uchumi wa biashara na viwanda ikilenga matumizi salama teknolojia nchini ili kuboresha ustawi wa kwenye sekta ya afya,maji ,kilimo,nishati na mifugo.

  Mtafiti wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Yesaya Sungita amesema takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 30%ya vyakula duniani vinahribika kila mwaka kwa sababu ya kuharibiwa na na vijidudu au kuoza ,upotevu au kuharibika kwa chakula kuna athari kubwa katika kipato cha wakulima.

  Aidha kila mwaka inakadiriwa hasara inayotokana na kuharibika kwa mazao ya nafaka barani Afrika haswa kusini mwa jingo la sahara inafikia dola za kimarekani bilioni 4 sawa na asilimia 15 ya thamani ya mavuno hayosambamba na matukio ya binadamu kuambukizwa vijidudu vya salmonella yanafikia iddi ya watu 120,000 kila mwaka ambapo maambukizi yamekuwa yakisbabisha vifo vingi.

  "Gharama ya matibabu yanayosababishwa na madhara ya maambukizi haya ya vijidudu vya salmonella na Ecoli yamekuwa yakisababisha hasara ya dola za kimarekani bilioni 6 kila mwaka.alisema Yesaya" 

  Afisa mawasiliano wa Tume Peter Ngamilo amesema Teknlojia ya nyuklia ina mchango mkubwa katika sekta ya kilimo na mazao ya mifugo kwani uhakiki bidhaa zitokananzo na mazao zinakuwa bora na za uhakika ili kuboresha afya ya mlaji .

  Aidha katika hatua za awali tume hiyo imefanya upembuzi yakinifu wa kutumia teknolojia ya nyuklia /mionzi katika kuhifadhi chakula ,mazao na kuboresha bidhaa za viwandani ili kuzipa muda mkubwa wa matumizi na kuzikinga dhidhi ya haribifu unaoweza kusababishwa na bakteria.

  Hivyo wananchi haswa wa Arusha na mikoa jirani wameaswa kulitembelea banda la Tume ya nguvu za Atomiki ili wajipatie elimu juu ya huduma zinazotolewa sambamba na kujionea majukumu kisheria kwenye usimamizi na uthibiti wa mionzi nchini ili kulinda mazingira ,wananchi na wafanyakazi wanaotumia vyanzo vya mionzi katika kutekeleza majukumu ya kila siku.


  "Maonyesho hayo ya 25 ya kilimo na sherehe za nanenane mwaka 2018 kanda ya kaskazini yamebeba kauli mbiu isemayo" Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya Viwanda"

  0 0


  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Ujasiria mali na Ushirika ya Indonesia Bibi Emila Suhaimi alipotembelea Viwanda vidogovidogo vinavyojishuhulisha na ujasiriamali wakati alipokuwa katika ziara Mjini Jakarta ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla,
  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Ujasiria mali na Ushirika ya Indonesia Bibi Emila Suhaimi alipotembelea Viwanda vidogovidogo vinavyojishuhulisha na ujasiriamali wakati alipokuwa katika ziara Mjini Jakarta ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla
  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipokuwa akitembelea Bidha mbali mbali alipotembelea Viwanda vidogo vidogo vinavyojishuhulisha na ujasiriamali wakati alipokuwa katika ziara Mjini Jakarta ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla
  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akimuangalia Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Ujasiria mali na Ushirika ya Indonesia Bibi Emila Suhaimi wakati alipotembelea bidha mbali mbali zilizozalishwa na Viwanda vidogovidogo vya wajasiriamali wakati alipokuwa katika ziara Mjini Jakarta ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla .Picha na Ikulu

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa jana Oktoba 04, 2018 amefungua rasmi maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza.


  “…Maonesho haya ya Nane Nane ambayo ndiyo ya msingi sana, yasiwe tu kama ni maonesho ya nguvu ya soda, tunataka tuone matokeo chanya kwa wakulima wetu. Na kwa maana hiyo ifike mahala basi tuwe na maonesho ya kimataifa…”. Alisisitiza Dkt.Mwanjelwa.


  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Mathao Masele alisema yalianza Oktoba Mosi na yatafikia tamati Agosti 08, 2018 ambapo hadi sasa kuna zaidi ya washiriki 300 kutoka taasisi na makampuni mbalimbali.


  Hii ni mara ya kwanza maonesho ya Kanda ya Ziwa Magharibi yanayoshirikisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera kufanyika baada ya serikali kugawa mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kanda mbili kwa ajili ya kushiriki maonesho ya Nane Nane. Kanda nyingine ni Kanda ya Ziwa Mashariki inayoshirikisha mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.

  Mkuu wa Wilaya Ilemela, Mhe.Dkt. Severine Lalika akizungumza kwenye maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella
  Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi, Mathayo Masele akitoa taarifa ya maonesho hayo
  Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya akitoa salamu zake kwenye maonesho hayo
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa akijionea kikundi cha ngoma cha Bujora wakati kikitumbuiza kwenye maonesho hayo
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa akipokea maelezo kuhusu zao la mpunga kutoka kwa Dkt.Rashid Lussewa (kushoto) ambaye ni mtafiti wa zao hilo Kanda ya Ziwa, Chuo cha Kilimo Ukiriguru
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa alitoa rai kwa wataalam kutoka taasisi ya kilimo Ukiriguru pamoja na Bodi ya Pamba kuhakikisha wanatoa elimu kwa wakulima kuhusu namna bora ya kupambana na wadudu waharibifu wa zao la pamba kwani wakulima wengi wamepata hasara kutokana na wadudu hao

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Mashaka Biteko (CCM) amezindua rasmi wodi ya akina mama na watoto katika Kituo cha Afya cha Charles Kulwa Memorial kilichopo Runzewe jimboni humo.


  Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini amefanya uzinduzi huo jana Agosti 08, 2018 alipofika katika Kata ya Uyovu kuzungumza na wananchi wa Kata hiyo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kabulima.


  Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Biteko aliupongeza uongozi wa kituo hicho cha binafsi kwa kujenga wodi hiyo yenye vifaa vya kisasa na kutoa rai kuwahudumia wananchi wote kwa kuzingatia taratibu zote za afya ikiwemo kutowabagua wanaotumia bima ya afya.


  Mkurugenzi wa kito hicho, Dkt.Baraka Kulwa alisema kilianza kama Zahanati mwaka 1997 kabla ya kupandishwa hadhi mwaka 2015 na kuwa Kituo cha Afya ambapo kinahudumia wagonjwa kati ya 3,000 hadi 4,000 kwa mwezi huku asilimia zaidi ya 70 wakiwa ni akina mama na watoto hivyo ujenzi wa wodi hiyo iliyogarimu takribani shilingi milioni 25 utasaidia kuboresha zaidi huduma za afya kituoni hapo.


  “Kwa kweli nashukuru kwa uzinduzi wa huduma hii, inatusaidia sana. Mimi natoka Kakonko lakini nimekuwa nikisikia kwamba hapa kuna huduma nzuri”. Alisema mama Winfrida John ambaye ni mkazi wa Kakonko aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya kupata huduma.

older | 1 | .... | 1638 | 1639 | (Page 1640) | 1641 | 1642 | .... | 1897 | newer