Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

JUMUIYA YA ZAPHA + YAFANYA WARSHA YA SIKU MOJA KUJADILI WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU ZANZIBAR.

$
0
0
  Mwezeshaji wa warsha Bw. Mwalimu Wilson-olesira alie simama akizungumza na washiriki wa warsha ya kujadili mchango wa jamii katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, katika ukumbi wa zamani wa Radio uliopo Rahaleo Mjini Zanzibar. Warsha hiyo ya siku 1 imeandaliwa na (ZAPHA +). 
 Afisa vituo vya kulelea watoto yatima Idara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar Lahdad Haji Chum akichangia katika mjada wa nini tufanye kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na (ZAPHA +) katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar.
 Maryam Charles Samwel mmoja ya vijana wanaosaidiwa kimasomo na (ZAPHA +) akizihamasisha Jumuiya nyengine kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu magumu katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na (ZAPHA +) katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar uliopo Rahaleo Mjini Unguja.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyo jadili mchango wa jamii katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, huko katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar uliopo Rahaleo Mjini Unguja.
(Picha na makame Mshenga-Maelezo)
=======  =====  =========
Maryam Aboud Ali na Riziki Salum Ali
Mkurugenzi Ofisi wa Elimu Maandalizi Msingi wa Vyuo vya Qur-an Zanzibar amesema suala la kubuni mbinu shirikishi kwa wadau na wanajamii ndilo ambalo litasaidia kutoa huduma endelevu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

 Hayo yalielezwa katika warsha ililoandaliwa na Jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar {ZAPHA PLUS} ililoshirikisha taasisi za serikali na jumuia za binafsi  zinazoshughulikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Redio Zanzibar.
Aidha alisema  lengo kuu ni kuona changamoto zinazowakabili pamoja na kujua ni jinsi gani watoto wataweza  kusaidiwa na kupatia haki zao za msingi ikiwemo kivazi, elimu, malaji pamoja na huduma za kiafya.

Kwa upande wa washiriki katika kongamano hilo walisema kuwa wanahitaji mashirikiano ya pamoja katika jumuiya mbali mbali’ wanakamati, masheha wa shehiya na wanajamii kiujumla ili kufikia lengo la kuwakomboa watoto wanaoishi katika mazing ira magumu. “Watoto wanaoishi katika mazingira magumu tuwakomboe vipi?”walisema washiriki.

 Pia mmoja wa washiriki hao Dadi Ali Chum alifahamisha ipo haja ya kujua takwimu ya watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu ili kuweza kuzisaidia  familia zao.

Jumuia ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi inahusika na kutetea na kuhimiza huduma bora za tiba kushiriki katika mapambano dhidi ya ukimwi kutoa ushauri nasaha na lishe, elimu ya unyanyapaa kwa  wanajamii kuhusu watoto wanaoishi na HIV/AIDS   pamoja na kufanyakazi na watoto hao  kwa lengo la kuwapa elimu ya stadi za maisha
Jumuia imeweza kuwasaidia watoto 749 wakiwa wanawake 386 nawanaume 360  kwa Unguja na Pemba katika kuwasaidia na hali ngumu za maisha.

Nae mratibu wa jumuiya hiyo Mussa Tano Juma alisema kuwa jumuia imeandaa vipindi mbali mbali kwa jamii ili kufanikisha maendeleo ya watoto hao. Jumuia hiyo imeanzishwa mwaka 1994  ikiwa na wanachama 26 ikiwa na klabu moja ya watoto, na hadi sasa imefanikiwa kuwa na klabu  kumi.

WARAKA KUTOKA KWA MDAU MKUBWA WA FILAMU HAPA NCHINI WILLIAM MTITU.

$
0
0
BILA STEPS INAWEZEKANA


Kwa muda mrefu nimekuwa nikiulizwa sababu ya kuamua kusambaza filamu zangu mwenyewe badala ya kuzipeleka kwa wasambazaji ambao nilikuwa nikifanya nao kazi kwa muda mrefu, yaani kampuni ya Steps Entertainment. 


Najua maswali yamekuwa mengi kwa kuwa kuna watayarishaji wengi wa filamu nchini wanaohangaika usiku na mchana ili kupata mkataba wa kufanya kazi chini ya kampuni hiyo kwa kuwa Steps Entertainment ndiyo kampuni ya usambazaji inayolipa vizuri zaidi kuliko makampuni mengine yote kwa sasa. 


Leo nimeamua kuongea walau kidogo …….


“Kwanza nikiri kuwa maneno ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mhesimiwa Dr. Jakaya Kikwete aliyotamka siku aliyoiita Ikulu kamati ya mazishi ya marehemu Steven Kanumba ndiyo yamekuwa yakinisukuma sana hadi kufikia uamuzi huu mzito.


Kati ya waliounda kamati hiyo iliyoitwa Ikulu, mimi nilikuwa katibu, Mwenyekiti alikuwa Gabriel Mtitu au maarufu kama Mtitu Game, pia kulikuwa na wajumbe wengine kama Ruge Mutahaba, Asha Baraka, Jacob Steven ‘JB’ na Mzee Chilo. Baada ya kuongea mengi kuhusiana na msiba wa Kanumba na mazishi yake, mheshimiwa rais aliuliza ‘Hivi marehemu Kanumba kaacha filamu ngapi?”


Kwa aibu tulimjibu mheshimiwa rais kuwa marehemu Kanumba hajaacha hata filamu moja, zote ni za msambazaji wake na hata mbili ambazo zilikuwa hazijatoka yaani ‘Ndoa yangu’ na ‘Love & Power’ tayari zilikuwa ni za msambazaji kutokana na aina ya mkataba tunayoingia na msambazaji.


Mheshimiwa Rais alisikitika sana, akatuambia kuwa yeye hawezi kutumia nguvu kutukataza kuuza mali zetu lakini angependa kuona kuwa tunamiliki wenyewe filamu zetu na tutakapoona tumekwama tumwambie. Aliongeza kuwa kuuza haki zetu ni kama kuuza utu wetu. Maneno ya mheshimiwa Rais yalinichoma sana.


Mimi ni msanii wa kwanza kufanya kazi na kampuni hiyo kama mtayarishaji wa filamu na filamu yao ya kwanza kuisambaza ilikuwa ni ‘Jeraha la Ndoa’ ambayo niliitengeneza mimi. Na kwa kuthibitisha hilo, mwaka huu kampuni hiyo ya Steps ilitoa tuzo ya heshima kwa kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd kwa ajili hiyo.


Nasikitika kukiri kuwa filamu zote ambazo nilizitengeneza kisha zikasambazwa na kampuni ya Steps, siyo zangu tena. Kampuni hiyo imekuwa ikinunua haki zote za filamu wanazopelekewa kwa ajili ya kuzisambaza kwa hiyo baada tu ya kusaini mkataba wao unakuwa huwezi kufaidika tena na chochote kutokana na mauzo au faida nyingine zinazotokana na filamu yako. 



Kwa aina ya mikataba ambayo wasanii na watayarishaji tunaingia na kampuni ya Steps Entertainment, sisi tumekuwa ni wasimamizi tu wafilamu za zao, yaani ni kama manyapara kwenye mashamba ya mkonge wakati kwa ukoloni. Ni waajiriwa tusio na mafao ya uzeeni.


Kwa taarifa tu ni kwamba filamu zote mnazoziona mitaani zikisambazwa na kampuni siyo za hayo makampuni yanayotajwa kutengeneza filamu hizo bali ni filamu za Steps Entertainment. Ndiyo maana hata ukienda kwenye Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) utakuta wasanii wakubwa hawamiliki kabisa filamu lakini kampuni ya Steps inamiliki filamu zaidi ya 400.


Kifupi ni kuwa hadithi ni zetu, sehemu za kuigizia ni zetu, tunaigiza sisi, tunarekodi na kuhariri sisi lakini filamu ni za Steps Entertainment na ndiyo maana hata kampuni ya marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba the Great’ imesambaratika baada ya kifo chake na mama yake akikabiliana na ugumu wa maisha lakini filamu za Kanumba bado zinatesa kwenye soko la filamu ndani na nje ya nchi.


Nawashangaa watu wanaomshutumu mama mzazi wa Kanumba kuwa amemaliza mali za mwanae na sasa anaishi kwa kufadhiliwa na Lulu, wangejua kilicho nyuma ya pazia wangemuonea huruma badala ya kumshutumu. Wakati Steps wanakiri kuwa filamu iliyowahi kuuza sana katika historia ya kampuni yao ni ‘Ndoa yangu’ ya Kanumba, hawasemi kuwa familia yake imenufaika vipi zaidi ya kupewa tuzo.


Pamoja na kununua haki zote za filamu, kampuni ya Steps hawatoi malipo ya filamu wanazozinunua kwa muda muafaka hivyo kutufanya tuendelee kuwa mafukara siku hadi siku. Hii ni sababu ya pili ya mimi kujitoa Steps, sitaki familia yangu ije kudhalilika baada ya kifo changu.


Fikiria unapeleka filamu yako Steps, mnaingia mkataba wa kuuziana, lakini hawakulipi mpaka wakati watakapoamua kuiingiza sokoni hivyo hata wakikaa mwaka bila kuiingiza utakaa mwaka mzima unasuburi pesa. Hivi kweli mwaka huo utakuwa unakula nini kama umeamua kuifanya sanaa kuwa kazi yako?


Cha kuchekesha hata wanapoamua kuiingiza sokoni hawakulipi mpaka baada ya wiki mbili au tatu baada ya filamu yako kuwa imeingia sokoni, utasema hapo wamekulipa au umejilipa mwenyewe baada ya kuwa imenunuliwa?


Mfano mwingine hai ni wa marehemu Said Juma Kilowoko (Sajuki) ambaye ni miongoni mwa wasanii maarufu na watayarishaji wa filamu. Marehemu Sajuki alilazimika kuzunguka na wasanii wenziye mikoani akiwa anamuwa taabani ili tu aweze kupata fedha za matibabu jambo ambalo naamini lilimzidishia matatizo ya kiafya.


Na kutokana na kuuza haki zetu zote ilibidi mkewe Sajuki, Wastara atengeneze ‘Mr & Mrs Sajuki’ ili aweze kupata fedha za kujikimu na kurekebisha mambo mbalimbali yaliyovurugika wakati akimuuguza mumewe. Kama tungekuwa hatulazimiki kuuza haki zetu zote, familia hiyo ingeweza japo kupeleka filamu zake kwenye vituo vya runinga barani Afrika ambako ni chanzo kingine cha mapato kwa msanii.


Baada ya kutafakari kwa kina niliamua kulipia leseni ya usambazaji wa filamu kupitia kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd ili niwe nasambaza filamu zangu nikitegemewa kupata sapoti kubwa kutoka kwa wasanii wenzangu hasa mastaa wakubwa lakini imekuwa kinyume chake. Kwa sasa naonekana adui mbele ya wenzangu.


Kupitia kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd, niliingiza sokoni filamu ya ‘Omega the Confusion’, na ndani ya masaa matano ya kwanza nilifanikiwa kurudisha gharama zangu zote na kupata faida kidogo. Toka hapo hadi sasa inaendelea kukimbia sokoni hivyo natengeneza faida tu na bado filamu ni yangu, naweza kuifanyia chochote kama kuipeleka kwenye runinga za kimataifa n.k


Nimalizie kwa kuweka wazi kuwa sina ugomvi wowote na kampuni ya Steps, mmiliki wake wala mtumishi yeyote wa kampuni hiyo. Pia sina chuki na yeyote kati ya wanaoendelea kufanya kazi chini ya kampuni hiyo. Kikubwa ni kuwa haya ni maisha na kila mmoja ana mtazamo wake katika kuyakabili na kujiletea mafanikio”.


“WOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO”

‘TEAM NYATI’

TCRA YATOA VYETI KWA MABLOGER WAHITIMU WA MAFUNZO YA SIKU MBILI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasilino Tanzania, Prof. John Nkoma, akimkabidhi Cheti cha kuhitimu mafunzo ya siku mbili,mmiliki wa mtandao huu wa Sufianimafoto, Muhidin Sufiani, baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano, yaliyoanza jana Septemba 17 na kumalizika leo jijini Dar es Salaam, huku yakiwashirikisha mabloger mbalimbali kutoka mikoa tofauti ya nchini.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasilino Tanzania, Prof. John Nkoma, akimkabidhi Cheti cha kuhitimu mafunzo ya siku mbili,mmiliki wa mtandao wa Bongo Celeblate, Jeff Msangi, baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano, yaliyoanza jana Septemba 17 na kumalizika leo jijini Dar es Salaam, huku yakiwashirikisha mabloger mbalimbali kutoka mikoa tofauti ya nchini.
 Othman Michuzi, akipokea cheti.
 Shamim Mwasha, akipokea cheti.
 Cathbert Kajuna, akipokea cheti...
 Dj Choka, akipokea cheti.
 Maxence Melo, kipokea cheti.
 Sinta, akipokea cheti.
 Mmiliki wa Mtandao wa Sufianimafoto, Muhidin Sufiani (kulia) akiwa na mmiliki wa Mtandao wa Bongo Celeblate, Jaff Msangi, wakati wa semina maalum kwa wamiliki na waendeshaji wa mitandao pendwa Bloggers, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, iliyoanza jijini Dar es Salaam, jana ambayo imemalizika rasmi leo. 
 Mmiliki wa Mtandao wa Mbeya Yetu, Joseph Mwaisango, akichangia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo.
 Innocent Mungy wa TCRA, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.....
 Jestina george, akichangia mada
 Jeff Msangi, akichangia mada.
 Maxence, akichangia mada.



 Mtoa mada, Liz wachuka, akitoa mada...
 Sehemu ya waliohudhuria semina hiyo...
 Mafunzo yakiendelea 
 Mike Mushi, wa jamii forum, akitoa mada
 Mabloger, wakiwa makini kunasa kila kinachozungumzwa.
 Mtoa mada, Dotto Kuhenga, akitoa mada
 Mtoa mada, Pili, akitoa mada
picha ya pamoja baada ya mafunzo.

VIWANJA VINAUZWA VIKAWE-KIBAHA.

$
0
0
VIWANJA VILIVYOPIMWA VINAUZWA,VINA UKUBWA TOFAUTI TOFAUTI,VIPO VIKAWE KIBAHA,UKITOKEA BAGAMOYO ROAD MAENEO YA BAOBAB SECONDARY.

NI UMBALI WA KILOMETA NANE MPAKA KWENYE VIWANJA.WANAOTAKA KUVIONA NI KILA JUMAPILI SAA NNE  ASUBUHI,SAFARI INAANZIA MWENGE.

KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0756877173

FILAMU YA “HE HURTS ME” YAZINDULIWA KWA KISHINDO.

$
0
0
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

Katibu mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo amezindua filamu mpya ya “He hurts me” (ameniumiza au amenitenda), filamu ambayo imetengenezwa na Bi. Hilda Ngaja hivi karibuni jijini Dar es Salaam.


Bi. Fissoo ametoa pongezi kwa msanii huyo na Kampuni ya Hilderly Straight Film kwa kuthubutu kwao na ameongeza kuwa ana imani kuwa wadau haowataendelea kuzalisha filamu bora, zenye weledi, maadili na zinazoweza kuingia katika soko la ushindani. Pia amewashukuru washiriki wote  kwa kushiriki kwao kikamilifu katika kufanikisha filamu hiyo.


Bi. Fissoo amesema kuwa  filamu ya “He Hurts Me”  (ameniumiza au amenitenda) ni kati ya filamu zinazolenga kutoa elimu katika jamii na ni filamu inayoweza kuonwa na wanajamii kwani imejikita katika kuelimisha, kuburudisha, kuadabisha na ni filamu inayofaa kuingia sokoni.


Maudhui mahususi  ya filamu hii kwetu sote na jamii kwa ujumla ni katika kutukumbusha  umuhimu wa kuwapa malezi mema watoto wetu, jamii zinazotuzunguka zina watu wa aina na tabia mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa zinaathiri nguvu kazi ya taifa”. Alisema Bi. Fissoo.


Aidha, Bi. Fissoo amezungumzia suala kubwa juu ya malezi kwa watoto na vijana pia akaongeza kuwa ujio wa filamu hii utakuwa ni chachu na mchango mkubwa katika malezi na umekuja wakati ambapo taifa linahitaji wazazi na walezi  kushiriki ipasavyo katika kuwezesha  watoto na vijana kukua katika misingi ya malezi bora.


Kwa upande mwingine Katibu Mtendaji huyo amegusia masuala ya ukuaji wa tasnia ya filamu nchini  na amesema kuwa tasnia hii imeendelea kukua kwa kasi sana na hii inadhihirishwa na idadi kubwa ya filamu zinazozalishwa.


Vijana na watu wa makundi mbalimbali wamejikita katika tasnia hii. Ni ukweli usiopingika kuwa tasnia ya filamu inatoa ajira nyingi”. Alisema Bi. Fissoo. Bi. Fissoo amegusia pia masuala ya utamaduni na jinsi gani utamaduni unavyoweza kumuathiri ama kumnufaisha mtu hivyo amesisitiza kuzienzi tamaduni zetu.

Napenda kuwakumbusha waandaaji wa filamu na watengenezaji filamu wote nchini kutengeneza filamu zisizodhalilisha , zisizolenga kuuza tu bali ziwe zinazolinda maadili, zenye kutumia rasilimali , mandhari na lugha yetu ya kiswahili katika kutangaza utaifa na utamaduni wetu ; hata majina ya filamu zetu ni vema yawe kwa lugha ya kiswahili.Tupende na kuenzi utamaduni, maadili na lugha yetu”. Alisisitiza Bi. Fissoo.


Bi. Fissoo alimalizia hotuba yake kwa kuwaasa wadau wote wa filamu wakiwemo watengenezaji na wasambazaji wa filamu kuheshimu Sheria na Kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini ambapo kwa sasa mwitikio wake umeanza kuwa mkubwa pia amewasihi kupeleka sokoni filamu  zilizokamilisha taratibu zote na zilizowekwa stamp za TRA kwani Stamp hizo zina lengo la kuondokana na wizi wa kazi za wasanii pia amewasihi wadau wote kuunga mkono juhudi za serikali za kurasimisha tasnia za filamu na muziki kwani nia ya urasimishaji huu ni kurejesha nidhamu na hadhi katika tasni hizi na kuondokana na kilio cha muda mrefu ambacho kwa kiasi kikubwa kimefanya wasanii wa filamu na muziki kutonufaika na jasho lao.


Filamu ya “He hurts Me” (ameniumiza au amenitenda) imekaguliwa na Bodi na kupewa  daraja 16 yaani inaruhusiwa kuonwa na watu kuanzia miaka 16 nakuendelea.


CUF YAFANYA MKUTANO NA WANDISHI WA HABARI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CUF Hamad Masoud (wakatikati) akizungumza na wandishi wa Habari kuelezea mambo mbilimbali yanayoendea Nchini, kulia Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Omar Ali Shehe na kushoto Mkurugenzi wa Haki za Binaadam Salum Bimani,katika Ofisi ya CUF Vuga Mjini Unguja.
  Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Omar Ali Shehe wa kwanza kulia akielezea kitu kwa wandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu uwandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga Kura, katika Ofisi ya CUF Vuga Mjini Unguja.


 Baadhi ya wandishi waliohudhuria katika Mkuta huo, katika Ofisi ya CUF Vuga Mjini Unguja sep 19.

(Picha zote na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).

WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WATEMBELEA ZBC REDIO RAHALEO MJINI UNGUJA LEO.

$
0
0
 Mkurugenzi wa ZBC Ndugu Hassan Mitawi akiwapatia maelezo baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu matangazo kutoka kwenye analog kwenda kwenye Digitali katika ofisi za ZBC Radio Rahaleo Mjini Zanzibar leo. 
Muhariri Mkuu wa Shirika la Magazeti Bw. Abdalla Moh’d akiwaonyesha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi jinsi utayarishaji wa gazeti kabla ya kuprintiwa, katika ziara ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Rahaleo Mjini Zanziabr leo. Picha na Dula Chaz wa Maelezo Zanzibar.

MHE. LUKUVI ATEMBELEA KIWANDA CHA MAJI CHA DEW DROP KILICHOPO SUMBAWANGA MKOANI RUKWA.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akikagua kiwanda cha maji cha Dew Drop kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndani Ndugu Aziz Tawaqal alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa tarehe 18 Sept 2013. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima.
Kiwanda cha kisasa cha Dew Drop chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 6,000 kwa saa yakiwa na ubora wa hali ya juu. Maji hayo huzalishwa katika hali ya usafi na hayaongezwi  kemikali yeyote ambapo husafishwa kupitia "Sand Filters", "Activated Coal" na teknolojia ya "UV Light". 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji ya Dew Drop Aziz Tawaqal akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi alipofika kiwandani hapo kujionea shughuli mbalimbali za muwekezaji huyo ikiwemo kiwanda cha unga cha Energy Milling.  
Waziri Lukuvi akipokea maelezo ya Maji ya Dew Drop kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji ya Dew Drop Aziz Tawaqal, Waziri huyo aliyasifia maji hayo na kusema kuwa ameyanywa na ni mazuri sana ukilinganisha na maji mengine yanayozalishwa hapa nchini. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa...rukwareview.blogspot.com)

OMMY DIMPOZ ATEMBELEA STUDIO ZA SAUTI YA AMERICA (VOICE OF AMERICA "VOA") ASEMA JUMAMOSI WASHINGTON DC WATEGEMEE MAMBO !

$
0
0
MTANGAZAJI MASHUHULI SUNDAY SHOMARI  AKIMWEKA DIMPOZ KITI MOTO.
      POZ KWA POZI AKIJIBU MASWALI YENYE UTATA KUTOKA KWA SUNDAY SHOMARY
          LARY KING WA VOA NAYE ALIMWEKA DIMPOZ KITI MOTO
                                  BABU ALIKUWA ANAULIZA MASWALI YA KUFURAHISHA TU !

       PROMOTER/MANAGER WA DIMPOZ USA TOUR  BWANA "DMK" MWENYE TSHIRT NYEKUNDU AKIFURAHIA JAMBO PAMOJA NA SUNDAY SHOMARY NA DIMPOZ
POZ KWA POZ NDANI YA MITAA YA WASHINGTON DC AKIWA AMECHILL MBELE YA GARI LA PROMOTER/ USA TOUR MANAGER WAKE BWANA DMK


DIMPOZ NA DMK WAKIWA BUSY KWENYE TEXT WAKIPOKEA REQUEST NYINGI ZA TICKET ZA SHOW  CAMERA YA SWAHILI TV AMBAO NDIO WADHAMINI WA DIMPOZ USA TOUR ITAENDELEA KUKULETEA HABARI EXCLUSIVE ZA DIMPOZ AKIWA MITAANI USA. ENDELEA KUSIKILIZA SWAHILI RADIO ONLINE NA KUSOMA WWW.SWAHILITV.BLOGSPOT.COM KUWEZA KUJISHINDIA FREE TICKETS.

TIMU YA UTUMISHI YAPEWA SOMO KABLA YA SAFARI KUELEKEA MKOANI DODOMA KWENYE MICHEZO YA SHIMIWI.

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu (aliyesimama)akizungumza na  wanamichezo wanaounda timu ya Utumishi leo kabla ya safari ya kuelekea mkoani Dodoma katika michezo ya SHIMIWI.
 Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akiwapa mbinu za kimichezo  wanamichezo watakaiyoiwakilisha  Utumishi katika mashindano ya SHIMIWI mwaka huu wakati wa hafla fupi  ya  kuwaaga mapema leo. 
 Baadhi ya wanamichezo wa Utumishi na viongozi wao wakimsikiliza  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O.  Kombani (Mb) wakati  hafla fupi  ya kuwaaga mapema leo.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.
Celina O. Kombani (Mb)akizungumza katika hafla fupi na wanamichezo
watakaiyoiwakilisha Utumishi katika mashindano ya SHIMIWI mwaka huu mapema 
leo.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.
Celina O. Kombani (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Utumishi
itakayoshiriki  michezo ya SHIMIWI mwaka huu mara baada ya  hafla fupi
kuwaaga mapema leo ofisini kwake.

ECONOMIC JUSTICE:What do women want?

$
0
0
                                   
Leila Sheikh is a Senior Journalist; Producer of documentaries and a Social Justice Defender


In the past, economic institutions and economy analysts relied heavily on income levels as the basis to measure poverty.


However, there is now universal agreement that dimensions of poverty far transcend this traditional definition.


In the current overview, poverty is a deprivation of essential assets and opportunities to which every human is entitled. (Source: Evan Carmichael- Social Discussions on Poverty Reduction, ILO).


Everyone should have access to basic education and primary health services.

Poor households have the right to sustain themselves by their labor and be reasonably rewarded, as well as having some protection from external shocks. (Source: The Beijing Platform of Action for Economic Justice)


 Beyond income and basic services, individuals and societies are also poor—and tend to remain so—if they are not empowered to participate in making the decisions that shape their lives. Poverty is thus better measured in terms of basic education; health care; nutrition; breaking free of Gender Based Violence; water and sanitation; as well as income, employment, and wages.


 Such measures must also serve as a proxy for other important intangibles such as feelings of powerlessness and lack of freedom to participate. In practice, the most broadly used standard for measuring poverty will continue to be the adequate consumption of food and other essentials.  This yardstick (the poverty line) varies from country to country, depending on income and cultural values.


While national measurements are essential for measuring the impact of efforts to reduce poverty, our priority ought to be on ‘Eradication of absolute poverty in the Tanzanian context’ with international comparison also being necessary.


The poor are not a homogenous group. Just as the nature of poverty is diverse, so, too, are its causes and victims.


The poor may not have acquired essential assets because they live in a remote or resource poor area; or because they are vulnerable on account of age, health, living environment, or occupation.


They may be denied access to assets because they belong to an ethnic or a community considered socially inferior, or simply because they are female or disabled.


At a broader level, poverty may stem from situations where gross inequality of assets persists because of vested interests and entrenched power structures. Finally, essential assets may not be available to the poor because of the lack of political will, inadequate governance, and inappropriate public Policies and Programs. (Source: TGNP/2008). 

The primary responsibility for finding solutions to poverty lies with countries themselves, but success will depend on the united efforts of government and civil society, and on strong and sustained support to the community.


 For all stakeholders, the strategies chosen to reduce poverty must be comprehensive enough to address all of its many causes.


There is often conflict while addressing Poverty Eradication. The conflict can be between the body politic and the governance; conflict with multinationals; conflict with oppressive economic structures like Policy and Legislation and often, conflict with patriarchal structures which place women at a disadvantage because of low of access to education; tradition and prejudice which entrench women in a lowly position with little ability to negotiate for access to opportunities.



To overcome this imbalance, women should get training on building group dynamics, advocacy, Human Rights and basic Legal Literacy which would give them the skills to lobby for a Gender Progressive National Loans Policy which would be a Regulatory Mechanism for women to get access to soft loans which would take into account the fact that most women do not have collaterals in order to be “Loan Worthy”.


There is need to introduce special affirmative plans to provide assistance to marginalized women like friendly/supportive CSOs and trade unions during crisis for example when there are threats to the banda of Mama Lishe or when women who do business in the informal sector get harassed by the police or by Municipal Authorities or by big conglomerates which compete with women engaged in the informal sector who sell food or ice cream at a miniscule scale; without funding for advertising or promotion of their wares.


 Such marginalized women need structures so as not to get alienated from the mainstream business sector- their presence and initiatives need to be affirmed and respected.





Women need to get support in their quest for a Gender Progressive National Loans Act, although most of the marginalized women interviewed by this writer do not believe it is possible.



Low income level women engaged in the informal sector need to get assistance and skills in dealing with official matters like obtaining letters from Local Government Authorities to be able to open bank accounts, to be able to get housing without hassle from bigoted landlords, to get their children registered in schools because women who are widowed or are single mothers, tend to undergo discrimination.


Women also need to get access to loans from lending agencies without bias, discrimination or extortion of monies or extortion of sex.


Women in the informal sector should have opportunities to obtain skills in saving their earnings, planning for retirement because small scale business women and farmers do not have pension schemes, as yet!


 Structures should be introduced to get positive images of small scale business women and of women in the agricultural sector portrayed in the media as hardworking, voting citizens who should not be treated as second class citizens, and often, as invisible citizens.


They want to get protection for the lands they own which could be appropriated by municipalities for foreign investors.


They require getting affirmation that they exist, that they have rights like other citizens including the right to respect because there is a prevailing culture in our communities to despise low income or poor peoples, especially poor women.


They want to operate without discrimination or harassment from Village or Local Government Authorities and to be given access to training on business administration; book keeping; marketing; modern agricultural techniques; saving etc.


They want to have a say, and to own the processes that are currently being put in place which have broad based implications for women in the informal sector because their needs are not given priority while planning with foreign investors over equitable resource allocation. 

SWAHILI TV EXCLUSIVE RAIS KIKWETE AKUTANA NA UONGOZI WA CCM DMV JIJINI WASHINGTON D.C. SEPT 19,2013.

$
0
0
   Viongozi CCM DMV wakijadiliana jambo kabla ya kikao cha Faragha na Mhe. Rais Kikwete leo Sept 19,2013 jijini Washington DC, Marekani. Picha na Swahilitv
Picha na Swahilitv
 Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mwenyekiti CCM Taifa akielekeza jambo katika kikao chake na uongozi wa CCM DMV. Kikao hiki kimefanyika leo Sept 19,2013 jijini Washington DC, Marekani. Picha na Swahilitv
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimsalimia Bwana George Sebo mwenyekiti wa  CCM DMV.Picha na Swahilitv
Mhe. Rais Kikwete akiwa na Bwana DMK Mkurugenzi wa MMK MEDIA GROUP: Swahili TV, Swahili Radio na Swahilitv Blog. Picha zote na Swahili TV. KWA PICHA ZAIDI INGIA SWAHILI TV BLOG-

IDARA YA ARDHI NA USAJILI ZANZIBAR YAWAPA MAFUNZO WANDISHI WA HABARI JUU USAJILI WA ARDHI ZANZIBAR.

$
0
0
 Mtalamu wa mambo ya Habari kutoka Smole Bw. Ali Rashid Salim akifahamisha kitu katika mafunzo ya wandishi wa Habari juu usajili wa Ardhi,katika ukumbi wa Wizara ya Habari kikwajuni Mjini Unguja jana.
 Afisa mtambuzi wa Ardhi Unguja Shawana Soud Khamis akitoa elimu ya Utambuzi, kuisajili na kuitumia Ardhi kwa wandishi Habari katika ukumbi wa Wizara ya Habari kikwajuni Mjini Unguja jana.

Baadhi ya wandishi Habari wa vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini mafunzo yanayotolewa na Mtalamu wa mambo ya Habari kutoka Smole Bw. Ali Rashid Salim (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Habari kikwajuni Mjini Unguja jana. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
========  =======  =======
Maryam Fumu na Patima Mtumwa Maelezo- Zanzibar.

Afisa Mkaguzi wa Ardhi Zanzibar Shawana Suod Khamis amewataka wananchi kutoa mashirikiano  katika kufanikisha zoezi zima  la  Utambuzi na usajili wa ardhi nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana  katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo wakati akifunga mafunzo ya siku moja ya utambuzi  na usajili wa ardhi kwa  waandishi wa habari .

Alisema  kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuweza kuwapa mbinu za kisasa  na  uwelewa mpana  kwa  waandishi ili kuweza kuihamasisha jamii kuhusiana na zoezi  hilo.

Alieleza kuwa  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana  na Serikali ya Finland  kupitia mradi wa SMOLE II unaendelea na zoezi la usajili wa Ardhi kupitia maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

 Shawana ameyataja   baadhi ya maeneo  ambayo tayari yameanza zoezi hilo  na kuonyesha mafanikio kuwa  ni   Kijiji cha Nugwi , Jendele, Paje,  Chwaka, Kwaalinatu ,Mji Mkongwe, Mkokotoni ,Mwembetanga , Rahaleo, Muembeladu,  Muembeshauri, Gulion,  Kibondeni, Kisima  Majongoo, Mchangani na Vikokotoni .

Akieleza baadhi ya faida za usajili wa ardhi  kuwa  ni kupunguza migogoro inayotokea mara kwa mara katika jamii na kumsaidia mmiliki wa ardhi katika  kupata mikopo katika benki,  mashirika na taasisi mbali mbali.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Afisa Habari  na Mawasiliano wa SMOLE  Ali Rashid Salim amesema migogoro mingi ya Ardhi husababisha usheleweshaji wa mirathi kwa jimii hasa  kwa wanawake watoto yatima na watu wenye ulemavu na kupelekea kukosekana kwa haki kwa wahusika.

Zoezi  la usajili wa ardhi limeanza rasmi mwaka 2008 inatarajiwa kuwa  ifikapo mwaka 2015 asilimia 50 ya ardhi yote ya Zanzibar iwe tayari  imeshasajiliwa . 

Airtel, Puma, Be Forward, Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, na Baraza la Taifa Usalama Barabarani waungana kuadhimisha wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani 2013

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti wakwanza kushoto akifatiwa na mwakilishi wa Be Forward bw Kohei Shibata na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando kwa pamoja wakimkabithi Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga stika za usalama barabarani kwa mwaka huu. Airtel, Puma pamoja na Be Forward ni wadhamini wa wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akikabithi Tshirt zitakazotumika katika wiki ya nenda kwa usalama kwa mwaka huu kwa Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga ambapo Airtel, Puma pamoja na Be Forward ni wadhamini wa wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu. akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga akionyesha stika za usalama barabarani kwa mwaka huu mara baada ya kukabithiwa na wadhamini wa wiki ya usalama kwa mwaka huu ambao ni Airtel, Puma pamoja na Be Forward wakishuhudia (kutoka kushoto) mwakilishi wa Be Forward bw Kohei Shibata, Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando.

FHI 360 WAISHUKURU OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA KWA MSAADA WA OFISI NA USHIRIKIANO WA KARIBU WALIOUPATA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiongea na Afisa Mwandamizi mradi wa FHI 360 Road II Bi Florence Lema na Mratibu wa Mradi eneo la Sumbawanga Ndugu Nsajigwa Richard walipofika ofisini kwake leo kushukuru kwa msaada wa ofisi waliopewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambayo waliitumia kwa muda wa miaka mitatu.  
Afisa Mwandamizi mradi wa FHI 360 Road II Bi Florence Lema akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima barua ya shukurani kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kuwasaidia Ofisi waliyoitumia kwa mda wa miaka mitatu katika kipindi chote cha mradi ambao ambao hivi sasa umekamilika. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akionyesha barua hiyo mara baada ya kukabidhiwa ofisi iliyokuwa ikitumika na mradi wa FHI 360 Road II Mkoani Rukwa. Afisa Mwandamizi wa mradi huo Bi. Florence Lema ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano Mkubwa ilionao katika kusaidia na kujumuika pamoja na sekta binafsi na mashirika ya kijamii ya kitaifa na kimataifa. 
Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na wawakilishi kutoka FHI 360 Ofisi kwake mapema hii leo.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  Rukwa....rukwareview.blogspot.com)

Operesheni Kimbunga Haikuondoa Wakimbizi Nchini

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI



  



Simu:  +255-22-2112035/40        

          S.L.P.  9223

Nukushi:  +255-2122617/2120486

Barua Pepe:  ps@moha.go.tz

       Dar es Salaam

Septemba 19,2013



Operesheni Kimbunga Haikuondoa Wakimbizi Nchini


Operesheni Kimbunga haikuondoa Wakimbizi nchini kama ilivyoripotiwa na baaadhi ya Vombo vya Habari vya hapa nchini na vya nje. Ifahamike kuwa zoezi hili limehusisha Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) ili kuhakikisha kuwa wakimbizi hawahusishwi katika zoezi la kuondoshwa nchini.

Kwa mujibu wa tafsiri iliyotolewa na Mkataba wa Kimataifa wa mwaka 1951 kuhusu hadhi ya Wakimbizi, Mkimbizi ni mtu anayekimbia nchi yake kwa hofu ya maisha yake kuwa hatarini kwa sababu za  kikabila, dini, utaifa, uanachama wa chama cha kijamii au kisiasa na kufuata hifadhi katika nchi nyingine.


 Mkimbizi anapokimbilia katika nchini nyingine kuomba hifadhi ana haki ya kupewa hifadhi na kuhakikishiwa usalama wake. Pia ana haki ya kupokelewa na kutorudishwa katika nchi ambayo ameikimbia. Hivyo , kutokana na Mkataba huo, Tanzania wakati inatekeleza Operesheni Kimbunga haikumgusa mkimbizi.

Aidha, ieleweke kuwa yapo mazingira ambapo hadhi ya mkimbizi hukoma pale ambapo suluhisho la kudumu la matatizo ambayo yalimfanya mkimbizi kukimbia nchi yake limepatikana na hivyo mkimbizi mwenyewe kutaka kurudi nchini kwake kwa hiari ama pale mkimbizi anapohamishiwa kwenye nchi ya Tatu kwa makubaliano maalum na pale ambapo mkimbizi anapewa uraia  au ukaazi wa nchi  iliyompatia hifadhi.


Hivyo basi, mkimbizi anaweza kuwa mhamiaji haramu pale ambapo hakurudi katika nchi yake kwa hiari baada ya kupatikana suluhisho kwa matatizo yaliyosababisha kukimbia ama hakupata fursa ya kwenda nchi ya Tatu na hakuomba Uraia au ukaazi wan chi iliyokuwa inampa hifadhi.



Ieleweke kuwa Mkimbizi ambaye alirudi nchini kwake kwa hiari yake na baadaye kuamua kurudi katika nchi iliyokuwa inamhifadhi hawezi kuendelea kuwa na hadhi ile ile ya ukimbizi . Mtu huyu anatakiwa kufuata Sheria ya Uhamiaji namba 7 ya 1995. Iwapo ataishi nchini bila kufuata sheria hiyo atahesabika kuwa mhamiaji haramu. Inawezekana kuna watu ambao hadhi yao ya ukimbizi imekoma na wanaishi nchini isivyo halali wakakumbwa na  Operesheni Kimbunga na kudai kuwa wao  ni wakimbizi.

Juhudi za Serikali za kuwataka wahamiaji haramu kuhalalisha ukaazi nchini kwa hiari


Kwa vipindi tofauti, Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji iliendesha zoezi la kuhamasisha watu wanaoishi nchini isivyo halali kurudi nchini kwao kutokana na hali ya usalama katika nchi hizo kuimarika. Aidha, kwa waliotaka kubaki na kuendelea  kuishi nchini walielekezwa kufuata sheria na taratibu za Uhamiaji.


Utafiti uliofanywa na Mradi wa Kimataifa wa kushughulikia masuala ya kiuhamiaji  ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaoongozwa na Prof. Boneventure Rutinwa  2006/2007 katika mkoa wa Kagera  unaonyesha kuwa Wilaya ya Karagwe pekee Inakadiriwa kuwa na wahamiaji haramu 30,850 lakini pamoja na kuhamasishwa kuhalalisha ukaazi wao, watu 2,000 pekee walifuata taratibu walizoelekezwa na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji ili kuhalalisha ukaaji wao nchini.


Pamoja na juhudi zote za Serikali za kuhamasiha wahamiaji haramu kuhalalisha ukaazi wao nchini bado hawakufuata taratibu na badala yake utafiti unaonyesha kuwa waliendelea kuingia na kuhamia katika wilaya nyingine mfano Biharamulo na maeneo mengine.

Taarifa hii imetolewa na Zamaradi Kawawa, Kiongozi wa Timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Septemba 20,2013, Biharamulo, Kagera. Kwa maelezo zaidi Email: zamaradikawawa@yahoo.com.






VYUO VIKUU VYA UMMA VYA NUFAIKA NA MRADI WA STHEP

$
0
0
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,Taalum kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Makenya Maboko(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya utekelezaji ya Mradi wa Sayansi,Teknolojia na Elimu ya Juu(STHEP) wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Utawala Prof. Boniventure Rutinwa.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Rasilimali Prof. Marten Victor(kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi mradi wa Sayansi,Teknolojia na Elimu ya Juu (STHEP) uliotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali na Bank ya Dunia, Utakavyoongeza ufanisi wa chuo hicho,Kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Bank ya Dunia unaotekelezwa katika chuo hicho Bw. Shaaban Mbogo.

 Mratibu wa Mradi wa Sayansi,Teknolojia na Elimu ya Juu (STHEP) kitaifa Dkt. Keneth Hosea (kushoto)  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)jinisi mradi huo utakavyo wanufaisha walimu wa shule za sekondari wenye shahada wanaofundisha masomo ya sekondari.Kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Bank ya Dunia unaotekelezwa katika chuo hicho Bw. Shaaban Mbogo.

 Mhandisi John Kapuku akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Jengo la Sayansi ya Majini na Teknolojia ambayo ni moja ya jengo linalotokana na mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Bank ya Dunia lililogharimu bilioni 4.3. 

 5 Jengo la Urithi wa Utamaduni linalotokana na mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Bank ya Dunia lililogharimu bilioni 2.6

Jengo la Uhandisi Migodi linalotokana na mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Bank ya Dunia lililogharimu bilioni 2.8 .PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

ni serengeti fiesta 2013 ndani ya uwanja wa karume mjini musoma mkoani mara usiku huu.

$
0
0
 Msanii mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa Bongofleva,Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu,mbele ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.
 Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani Mara,ambapo tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea hivi sasa.
 Anajiita tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani wakazi wa mji wa Musoma,wakati tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea hivi sasa ndani ya uwanja wa Karume.
 Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao.
 Kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
 Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man akiwakumusha mashabiki wa muziki wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji wa Musoma usiku huu
Anaitwa Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha mistari yake live mbele ya mashabiki wake waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta usiku huu.
Makamuzi yakiendelea jukwaani usiku huu.
 Sehemu ya umati wa watu.
 Msanii wa muziki wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga hizo,Neylee akiimba jukwaani usiku huu wakati wa tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Karume,Musoma mkoani Mara.
 Kundi la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature wakilishambulia vyema jukwaa usiku huu kwa staili yao mapanga shaa shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.
Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.
 Mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume hivi sasa
 Sehemu ya umati wa watu ndani ya uwanja wa Karume usiku huu.
 Mwanadada Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya watazamaji waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.
 Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani usiku huu
 Watu kibao,kila mmoja akijaichai kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza. 
 Wakali wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.
 Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.


HAPPINESS WATIMANYWA - KUELEKEA REDDS MISS TANZANIA 2013

$
0
0

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa kipindi cha Skonga, utamkumbuka Happiness Watimanywa, msichana pekee kutoka Tanzania aliyeweka historia ya kuongoza nchi zaidi ya 150 za mtandao wa IGCSE katika somo la Uhasibu kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010.
Happy (19) ni mzaliwa wa familia ya kawaida sana ya Mr Louis Roussos ya Morogoro. Wadogo zake Angel na Romeo sasa wanasoma St. Constantine shule iliyomtoa Happy. Pia, Happiness Watimanywa amewahi kusoma Laureatte International School ya Dar-es-salaam, ambapo akiwa hapo, alikutana na mwalimu wa michezo Mr Tchalewa Ndeki ambaye alimfungulia mipaka mingi Happy. Akiwa Laureatte, Happy aliwahi kwenda China na South Korea akiwa na wanafunzi wenzake katika matamasha mbali mbali ya elimu na michezo. Baada ya kumaliza kidato cha nne, Happy alifanikiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Strathclyde cha UK ambapo anasomea digrii ya Biashara.



Kipindi ambacho Happy yupo kwenye likizo ndefu, alipata wakati mgumu wa kutokuwa na kitu cha kufanya, hivyo Happy aliamua kujihusisha na masuala ya urembo na kufanikiwa kutwaa Taji la Miss Dodoma, na Miss Kanda ya Kati na hatimaye kuingia kwenye kambi ya Miss Tanzania.




Akiwa Miss Tanzania, Happy alikuwa ni mshiriki wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano hayo kwa kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2013.



Ndani ya kambi ya Miss Tanzania, Happiness Watimanywa amekuwa mwiba kwa warembo wengine 29 wanaowania taji hilo kwani amekuwa akionesha uwezo wa hali ya juu kuanzia kwenye kipaji hata michezo, ukiachilia mbali upeo mkubwa alio nao.

Leo ndio leo ambapo Happy anatarajia kudhihirisha kuwa pamoja na elimu na uwezo mkubwa alio nao, pia ni mrembo. Tusubiri matokeo ya Redds Miss Tanzania 2013.

KINANA AJILIPUA BUNDA,HAYUKO TAYARI KUONA WATENDAJI WA SERIKALI WANAIANGUSHA (CCM)

$
0
0
1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Busega Ndugu Paul Mzindakaya wakati alipowasili Wilaya ya Serengeti kata ya Nzugu Mkoani Mara akitokea Wilaya Busega Mkoa mpya wa Simiyu na kuanza ziara ya siku 6 katika mkoa wa Mara akianzia Wilaya ya Bunda mkoani humo, Kinana amekagua miradi mbalimbali katika jimbo la Mwibara na Bunda na kufanya mkutano wa hadhara mjini Bunda akikemea watendaji wa serikali ambao hawataki kuwajibika badala yake wamekalia kuvaa suti, kung'ang'ani vikao huku kujilipa posho na kuwa "Mamangimeza" badala ya kuwatumikia wananchi jambo ambalo Chama cha Mapinduzi ambacho ndiyo kimeiweka serikali madarakani hakitakubali badala yake kitawawajibisha watendaji hao kukinusuru chama cha Mapinduzi, Kinana amesema yuko tayari kujilipua ili kutetea wananchi na Chama cha Mapinduzi CCM ili kurudisha heshima ya chama kama Mwalimu alivyokiacha.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BUNDA 5Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wabunge deo Filikunjombe wa jimbo la Ludewa na Kangi Lugora wa jimbo la Mwibara. 6Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi mara baada ya kuwasili Serengeti leo
 
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images