Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

‘RYTHM’ ya QNET kugusa maisha ya jamii za wasiojiweza.

0
0


Walaka wa kampuni ya QNET wkitoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni 9 kwa kituo cha watoto yatima cha Maunga mapema mwaka huu jijini Dar es salaam.
QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inaamini katika maendeleo ya mtu binafsi na jamii kupitia kutengeneza fursa na inasisitizia falsafa hii katika biashara zake na katika shughuli zake za uwajibikaji kwa jamii.

Falsafa hii inatangazwa vyema zaidi kupitia kitengo cha kampuni cha uwajibikaji kwa jamii, RYTHM Foundation. RYTHM inasimama kama kifupisho cha Raise Yourself To Help Mankind, na kinajikita katika kanuni kwamba mtu anahitaji kujiwezesha yeye mwenyewe kwanza ili aweze kusaidia wengine kunyanyuka.

Foundation hii imeandaliwa kwaajili ya kutoa elimu, kuhamasisha na kufanya kazi na wengine kutengeneza maisha mazuri ya baadae ya wale wenye uhitaji. Inagusa dhamiri ya jamii na inatoa ukumbusho wa umuhimu wa kuleta tofauti katika maeneo ya kazi, jamii au umma kwa ujumla.

Tanzania ilikuwa miongini mwa nchi 13 za kiafrika ambako QNET iliungana na IRs kuleta shangwe kwa jamii mbalimbali za watu wasio na uwezo, wakati wa sikukuu za hivi karibuni za mwezi mtukufu wa ramadhani.

MUONEKANO WA JARIDA NA MAELEZO MAFUPI

0
0

JARIDA LA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI – “ARDHI NI MTAJI”

TOLEAO Na. 9 LA JARIDA LA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa Jarida lake la mwaka (2018) – ARDHI NI MTAJI (Toleo Na. 9). Jarida hili haliuzwi. Kuna nakala chache ambazo zitapatikana Wizarani – Dodoma na katika Kanda ya Dar es Salaam (Magogoni, Kivukoni) katika Kitengo cha Huduma kwa mteja.
Aidha Jarida hili litapatikana pia hivi karibuni kwenye Tovuti ya Wizara (www.lands.go.tz)

Mwananchi pata nakala yako upate kuhabarika kuhusu shughuli na Matukio mbalimbali ya Utekelezaji ya Wizara.

Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

NAIBU WAZIRI AWESO AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI WA MAJI KOROGWE MJI

0
0

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akizungumza na Mhandisi wa Maji Korogwe Mji Joseph Mcharo kabla ya kumsimamisha kazi kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akizungumza na watendaji wa Halmshauri ya Korogwe Mji wakati wa ziara yake

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa umakini Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe wakati wa ziara yake

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemsimamisha Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Korogwe Mji Joseph Mcharo kwa kutumia force accout kwenye mradi wa zaidi ya Milioni 700 bila ya kibali toka Wizara hiyo.

Agizo la kusimamishwa kwa Mhandisi huyo alilitoa jana wakati akikagua mradi miwili ya maji ya Mtonga ambao umetumia zaidi ya milioni 700 na msambiazi ambao umetumia zaidi ya milioni 600 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mkoa wa Tanga ambayo ilianza juzi wilayani Handeni.

Alisema mradi huo ulitakiwa kutumia kiasi cha shilingi Milioni 500 na wataalamu hao wakaubadilisha na kuufanya uwe wa milioni 700 ingawa bado unaendelea kusuasua jambo ambalo linaonyesha ubadhirifu wa fedha za Serikali .
 
Akiwa kwenye mradi wa Mtonga baada ya kumalizika kuukagua alitilia mashaka na ndipo alipoamuru mhandisi huyo kumpatia maelezo ya kina kuhusiana na mradi huo lakini pia hakuridhika na maelezo hayo na kuagiza kuwa atapeleka wataalamu kutoka wizara ili kuweza kuhakiki thamani ya fedha na ubora mrai huo.

“Kwa kweli mimi hapa sijaridhika na utekelezaji wa mradi huu unaonekana upo chini ya kiwango na ucheleweshwaji huku wananchi wakiendelea kupata tabu hivyo nitatuma wataalamu kutoka wizarani waje kuhakiki mradi huo”Alisema

Baada ya ukaguzi wa mradi huo Naibu Waziri huyo aliambatana na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Korogwe mji kuelekea kwenye mradi wa Msambiazi ambako kunajengwa tenki kubwa la mradi utakaosambaza maji kwa wananchi.

Akiwa huku ndipo alipomuuliza mhandisi gharama za mradi ambapo alisema zaidi ya milioni 600 zimetumika kwa kutumia mfumo wa mkandarasi na kupelekea mradi huo kufikia kwenye hatua za mwisho jambo ambalo limeibua maswali mengi kwa Naibu Waziri na kuamua kuchukua uamuzi huo.

“Ndugu zangu haiwezekani mradi wa zaidi ya milioni 700 kutumia force account kinyume na taratibu za wizara huku mradi wa milioni 600 ukitekelezwa kupitia mkandarasi ni wazi kwamba kuna ubadhirifu unaendelea hapa na mimi sitakubali”Alisema.

Baada ya maelezo hayo Naibu Waziri aliamua kumsimamisha mkandarasi huyo kwa kigezo miradi inayotumia chini ya milioni 200 ndio inapaswa kutumia force acounti tofauti na alivyofanya mhandisi huyo huku akimdanganya kwamba anakibali kutoka wizarani.

Awali akijib u hoja za Naibu Waziri huyo Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Korogwe Mji Joseph Mcharo alidai anakibali cha wizara kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mtonga kutumia force acounti ndipo Naibu Waziri huyo alipoamua kupiga simu wizara kupata ufafanuzi.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halamshauri ya Korogwe Mji Jumanne Shauri alionekana kushindwa kujibu maswali ya Naibu Waziri jambo ambalo liliibuka mabishoni baina yao kabla ya Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe kumtaka Mkurugenzi akiri mapungufu yaliyojitokeza kwenye mradi huo.

Mradi wa Mtonga ambao Naibu Waziri Aweso aliitulia mashaka ni wa kusambaza tenki,mabomba na sehemu maalumu kwa ajili ya mtambo wa kutibia na kusafisha maji eneo la mradi husika

Sababu 3 zinazoweza kuifanya migahawa kuhimili ushindani

0
0

Na Jumia Food Tanzania

Mabadiliko tofauti ya kijamii na kiuchumi yamechangia kwa kiasi kikubwa kubadilika kwa mifumo ya maisha ya kila siku. Mabadiliko hayo ni pamoja na namna watu wanavyoishi ikiwemo vyakula wanavyokula. Hakuna ubishi kuwa huduma ya chakula ni miongoni mwa sekta kubwa na yenye kuingiza mapato mengi duniani. Hakuna kiumbe yeyote anayeweza kuisha bila ya kula hivyo kupelekea biashara kama migahawa kuzidi kushamiri na kuongezeka. McDonald, Marrybrown, Subway na KFCni mojawapo ya migahawa mikubwa iliyosambaa sehemu mbalimbali duniani ikiwemo hapa Tanzania.   
Zipo sababu kadhaa ambazo zimepelekea mabadiliko kwenye huduma ya chakula. Kwanza, kuongezeka kukua kwa watu wa daraja la kati, wafanyakazi, wenye uwezo wa kutumia. Watu wa daraja hili mara nyingi huwa hawana muda wa kupika hivyo kutegemea kununua chakula kutoka migahawani. Pili, kukua kwa kipato kwenye familia hivyo kumudu gharama ya kupata huduma ya chakula nje ya nyumba. Sababu ya tatu ni pamoja na kukua kwa maboresho katika huduma za utoaji wa chakula kama vile migahawa ambapo inaongezeka kwa kasi huku ikirahisisha namna ya upatikanaji wa huduma zao.

Kwa hiyo, kiwango cha ushindani kwenye sekta ya huduma ya migahawa ni kikubwa kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Jumia Foodinashauri kuwa ili migahawa iweze kufanikiwa kwenye shughuli zao inabidi kuzingatia mambo yafuatayo.       
Utofauti kwenye utoaji huduma. Kwa sasa ambapo soko la huduma ya chakula lina ushindani mkubwa, migahawa inapaswa kuwa na zaidi ya huduma ya chakula au gharama nafuu. Utofauti na upekee katika utoaji huduma unahitajika kwa kiasi kikubwa kwa sasa. Lakini utofauti siyo kitu rahisi. Inahitaji migahawa kuangazia nyanja zote za kuwahudumia wateja kama vile: thamani ya huduma ambayo mteja anaipata, orodha ya vyakula vinavyopatikana, ubora wa huduma, mameneja pamoja na wafanyakazi, lazima vyote hivi viende sambamba.    
Motisha na ushirikishwaji wafanyakazi. Migahawa mingi mikubwa na yenye majina imegundua kuwa na programu za mikakati inayowahusisha wafanyakazi ndiyo misingi ya kuwajua na kuwapatia wateja utofauti wa huduma, kujenga uaminifu, na kukuza soko lao. Wafanyakazi ambao wanapewa motisha na kushirikishwa wana fursa kubwa ya kumpatia mteja huduma bora - kuanzia mteja anapokaribishwa mgahawani, kupeleka huduma kwa wateja wanaoagiza, pamoja na uharaka na namna chakula kinavyoandaliwa na kuhudumiwa. Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa wafanyakazi wanaoshirikishwa na kupewa motisha katika migahawa wanayoifanyia kazi hutoa huduma bora zaidi kwa wateja wao.  

Uwekezaji kwenye huduma ya kuagiza chakula. Teknolojia zinazowawezesha wateja kuagiza chakula na kupelekewa mpaka walipo zimepelekea wateja kujua namna na muda gani chakula kitawafikia. Kwa baadhi ya migahawa, kuamua kushirikiana na mawakala wa nje kuna maanisha kujitangaza zaidi na kuongezeka kwa uhitaji wa huduma. Kwa wengine, ni kupoteza fursa ya kukutana moja kwa moja na wateja wao, kuelewa machaguo yao, na kujenga mahusiano bora zaidi - ukiachilia mbali kupoteza mapato. Wamiliki wa migahawa hawana budi kulitazama suala hili kwa jicho la tatu ili kuleta ustawi kwenye biashara zao.

Kwa kuhitimisha, sekta ya huduma ya chakula inakua kwa kasi nchini Tanzania ambapo tunashuhudia migahawa mashuhuri duniani ikifungua matawi yake. Kutokana na idadi kuongezeka, ushindani nao umekuwa mkubwa. Migahawa inayochipukia imekuwa tishio kwa mikubwa iliyopo na yenye jina kwenye sekta. Hii ni kwa sababu yenyewe inakuja ikiwa imejizatiti zaidi katika ubora wa huduma, teknolojia, aina ya vyakula ilivyonavyo pamoja na namna ya utoaji wa huduma kwa urahisi na haraka. Hivyo basi, kuwekeza nguvu kwenye uvumbuzi na fursa mbalimbali kuna umuhimu mkubwa.      

Tamasha la (Tanzania - China Culture Ferstival) lafanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika Tamasha la Tanzania na China Festival lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho Posta jijini Dar es salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi watanzania pamoja na wananchi wa China waishio nchini Tanzania ili kukuza uhusiano na Urafiki katika kupitia Utamaduni na Sanaa.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza wakati akiakipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei katika Tamasha la Tanzania na China Festival lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho Posta jijini Dar es salaam jana
Katibu wa Chama cha kukuza uhusiano wa Tanzania na china Joseph Kahama akizungumza katika tamasha hilo lililofanyika jana jijini Dar es salaam.
Balozi mpya wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Wang Ke akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema kushoto na Katibu wa Chama cha kukuza uhusiano wa Tanzania na china Joseph Kahama na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Weiwa pili kutoka kulia.
Baadhi ya raia wa China waishio nchini Tanzania wakiwa katika tamasha hilo.
Kikundi cha muziki chenye mchanganyiko wa Wanzania na Wachina kikiimba nyimbo katika tmasha hilo.
Baadhi ya Madaktari kutoka nchini China ambao wametoa huduma za matibabu katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania wakiimba wimbo maalum katika tamasha hilo.
Burudani kutoka China zikiendelea
Waimbaji kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakiimba katika tamasha hilo.
Wageni mbalimbali walioalikwa katika tamasha hilo.

MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema ipo haja ya kuendelea kuudumisha uhusuiano kati ya Tanzania na China kwani una faida nyingi na wenye mambo yanayofanana.

Amesema kuwa Tanzania na china zimekuwa na uhusiano wa kaka na dada na msingi wake mkubwa uliwekwa na waasisi wa nchi hizo mbili ambapo kwa Tanzania ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere na China Mao Se tung.

Mjema aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la burudani lililowahusisha watanzania na wachina waishio nchini Tanzania ambalo lilifanyika ukumi wa Makumbusho ya Taifa

Tamasha hilo limeandaliwa na Chama cha kukuza uhusiano wa Tanzania na China (TANZANIA- CHINA FRIENDSHIP PROMOTION ASSOCIATION) ambapo Mjema amepongeza Chama hicho kwa uamuzi wake wa kuandaa tamasha hilo kwa lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo.

" Wakati tunapata uhuru Tanzania na china kuna mambo mengi yanafanana yakiwemo ya burudani kwa maana utamaduni " alisema.Pia alisema ubalozi wa china nchini Tanzania kupitia Balozi wake Wang ke umedhihirisha namna wanavyotambua na kuenzi utamaduni baina ya nchi hizo mbili kwani ndio waliodhamini tamasha hilo.

Hata hivyo Mjema na balozi Wang Ke pamoja na wageni waalikwa walipata nafasi ya kuangalia burudani huku nyimbo maalumu ya kuzungumzia uhusiano wa china na Tanzania ukiwagusa waliohudhuria Tamasha hilo.Kwa upande wake Katibu wa Chama cha kukuza uhusiano wa Tanzania na china Joseph Kahama alisema tamasha hilo ambaloni kwa mara ya kwaza limefanyika nchini Tanzania lengo haswa nikusaidia uelewa kati ya watu na watu.

Alifafanua kuwa linalenga kufahamiana zaidi na kuendeleza undugu ambao upo kati ya Tanzania na watu wa china na hilo ndio lengo kubwa na ndio maana hata nyimbo wanaimba pamoja kati ya wachina na watanzania.Kahama alisema tamasha hilo ambalo limepewa jina la (Tanzania - China Culture Ferstival) litaendelea kuimarisha na kudumisha uhusiano mzuri na kwa hapa nchini linafanyika kwa mara ya kwaza na litakuwa linafanyika kila mwaka na watakuwa wanafanya maboresho kadri watakavyokuwa wanafanya.

DC Ilala agiza NEMC kuvunja nyumba Tabata

0
0
Na Heri Shaban 

MKUU wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Sophia Mjema ameagiza Baraza la Hafidhi ya Mazingira (NEMC) kivunja nyumba zilizopo mpaka wa Ubungo na Wilaya ya Ilala mto Tenge. 

Tamko hilo lilitolewa Dar es Salaam jana wakati wa ziara yake wilayani Ilala iliyolenga kutatatua kero za wananchi wilayani humo .Akitoa agizo hilo kwa Mratibu wa Mazingira Kanda Mashariki( NEMC) Jaffar Chingaga Mjema alilitaka Baraza hilo kutekeleza agizo la uvunjaji nyumba zote zilizofanya uharibifu eneo la mto Tenge 

"Naagiza ofisini yako ya NEMC ije ivunje nyumba hizi ili upanuzi wa mto uweze kufanyika nyumba zote ziache mita 60 kwa ajili ya hifadhi mto wa bonde la mto Tenge "amesema Mjema. Amesema mara baada kuvunjwa kwa nyumba hizo atawasiliana na Mkuu wa wilaya ya Ubungo waweze kumchukulia hatua watendaji wa Manispaa yake wakiotoa kibali cha eneo la hifadhi ya bonde la mto huo .

Amesema ifikie wakati kila mtu afuate sheria na ajue kwamba Serikali ipo sio kila kitu kuvunja sheria hivyo katika hili sheria itafuatwa. Aidha amesema hivi karibuni katika Wilaya ya Ilala zoezi la urasilimishaji makazi linatarajia kuanza, hivyo washirikiane wote na kutenga maeno ya huduma za jamii ili yawepo. 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Ilala Paulo Mbembelwa amesema mtu yoyote katika eneo lake anayo mamlaka ya kujenga lakini kabla kujenga lazima afute kibali Halmashauri ardhi mali ya Serikali. Mbembelwa amewataka watendaji na wenyeviti wa Serikali ya mtaa kushirikiana wote kulinda mipaka ya wananchi wao kwani ni moja ya jukumu la kazi yao. 

Naye mwananchi Fadhiri Msangi ameomba Serikali kuchukua hatua za haraka ili kupanua mto huo ili wasikumbwe tena na mafuriko na waliohusika wachukuliwe hatua. "Zamani katika Mtaa huu magari yalikuwa yanapita kwa sasa shida iliyopo tunashindwa kupita hata njia ya zarula wajawazito wakiumwa au yakitokea matukio ya uharifu kutokana na mto kuhamia Wilaya ya Ilala, kutoka wilaya ya Ubungo "alisema Msangi.
Mkuu wa wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA akiwa katika ziara yake ya kutatua kero za wananchi wa Kata ya TABATA Dar es Salam Leo kuhusiana na mpaka wa Wilaya ya Ilala na Ubungo,pichani eneo la Mto Tenge Kata ya TABATA (Picha na Heri Shaban)

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SHAMBA LA MITI KATIKA HIFADHI YA MISITU IYONDO MSWIMA,ILEJE MKOANI SONGWE

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo Mswima lililopo Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.

Shamba hilo lililo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni moja kati ya mashamba mapya yakiwemo Biharamulo (Chato Geita), Buhigwe (Kigoma) na Mpepo (Mbinga, Ruvuma).

Akisoma taarifa ya Shamba hilo kwa Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mipango –Wakala wa Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo amesema kuwa mpaka shamba la miti la Iyondo Mswima limeweza kutoa ajira kwa wananchi 400 katika msimu wa kupanda miti, pia shamba limetoa ajira zingine 200 wakati huu wa maandalizi ya bustani ya miti, hekta 201 zimepandwa miti kama sehemu ya upanuzi wa mashamba ya miti ya Serikali ambapo bustani yenye jumla ya miche 430,000 kwa ajili ya upandaji miti wa mwaka 2018/2019.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele ambapo shamba la misitu la Serikali Iyondo Mswima limezinduliwa, Makamu wa Rais amewataka wananchi hao kutunza na kuyalinda mazingira kwa kupanda miti kwa wingi ambapo kila mwaka wananchi watapewa miche 50,000 na Wakala wa Huduma za Misitu wa Serikali.

Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Sange ambapo aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kuwa Mungu amewapa rasilimali nzuri sana hivyo hawana budi kuyatunza.

Makamu wa Rais amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhakikisha Maafisa Ugani wanashuka kwa wananchi na kutoa ushauri namna ya kufanya shughuli za kilimo vizuri.

Makamu wa Rais amesema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1.5 katika bajeti mwaka huu iliyopita kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ileje.

Makamu wa Rais amesema mkoa wa Songwe utapata watumishi 270 katika Sekta ya Afya, na kwenye sekta ya elimu, walimu wengi wameajiriwa mwaka huu ambapo Songwe nayo itapata walimu wapya.

Makamu wa Rais ameandika historia kwa kuwa kiongozi wa ngazi za juu kufika katika vijiji vya Katengele na Sange.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbuge wa Jimbo la Ileje Mhe. Janeth Mbene mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Kikundi cha Ngoma cha Sange kikitumbuiza ngoma ya Ling'oma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 





ZIARA YA DC HAPI KINONDONI YAIBUA MADUDU YALIYOPO SERIKALI ZA MITAA

0
0

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Ally Hapi ameibua madudu yaliyokuwa katika serikali za mtaa na kuzipa ufumbuzi.

Hapi amebaini madudu hayo ikiwa ni siku ya pili toka aanze ziara yake ya kutembelea kata zote za wilaya ya Kinondoni kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Akiwa katika Kata ya Kinondoni Hapi ametembelea mradi wa ujenzi wa mtaro na Barabara ya Best Bite,kuweka jiwe la Msingi wa Ofisi ya Mtaa.

Katika hatua nyingine Dc Hapi alimuagiza mtendaji wa Mtaa wa Kata hiyo nPeter Mayanja kuambatana na askari kwenda katika ofisi za kata kuchukua barua ambayo awali Mtendaji huyo alisema inamfanya ashindwe kuleta gari la kubeba takataka kwenye Mtaa wake ambalo tatizo hilo limekua kero kubwa kwa wananchi.

“Askari mmoja namuagiza mara moja aende na mtendaji huyu kuniletea hiyo barua ambayo anadai imetoka kwa mkurugenzi na kumzuia kuleta gari la kuzoa takataka, na azilete kabla sijaondoka hapa haiwezekani kero ndogo kama hiyo ya takataka mkuu wa wilaya aifanyie kazi wakati kuna watendaji wanaoweza kutatua kwa haraka," amesema Hapi.

Baada ya muda barua umfikia Dc Hapi ilionyesha haimzuii yeye kuleta gari la kubeba takataka hizo na mtendaji huyo kuonekana kama mbabaishaji.Hivyo DC Hapi kuamuru awaombe radhi wananchi wake kwa kutowaletea gari hilo kwa wakati.“Nawaomba radhi wananchi wangu mimi nimekosa na sitarudia tena,” amesema Peter Mayanja.Aidha DC Hapi ameweza kutembelea kikundi cha vijana wanaojihusisha na ufundi wa kutengeneza bidhaa za vyuma maarufu kama “welding” ambacho amewapa shilingi laki tano kama kuwapa nguvu zaidi vijana hao kuboresha kazi zao.

Pia DC Hapi amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni kumkamata na kumuweka ndani saa 48 mmiliki wa kampuni ya Total West Solution kwa kile kinachodaiwa kukaidi agizo la DC Hapi.La kuwalipa kwa awamu tatu wafanyakazi wa kampuni hiyo stahiki zao baada ya kuachishwa kazi kwenye kampuni hiyo.

“OCD nahitaji umtafute na kumuweka ndani saa 48 mmiliki huyo wa kampuni na timu yangu ya wanasheria ifuatilie suala hilo la wananchi hawa kulipwa,” DC Hapi.Kero hiyo imetolewa mbele ya DC na mmoja wa wafanyakazi hao Rasuli Khamis Mkazi wa Kinondoni ambaye pia ni Kiongozi wa wafanyakazi hao waliofukuzwa kazi kwenye kampuni hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akiwahutubia Wananchi wa Kinondoni wakati wa ziara yake hapo jana ya kutembelea kata zote za wilaya hiyo,kusikiliza na kutatua kero za Wananchi, Katika ziara hiyo Mh.Hapi alizisikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzipatai ufumbuzi hapo hapo
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akikagua miundo mbinu ya maji wakati wa ziara yake hapo jana ya kutembelea kata zote za wilaya hiyo,kusikiliza na kutatua kero za Wananchi, Katika ziara hiyo Mh.Hapi alizisikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzipatai ufumbuzi hapo hapo.


KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA, AMANI NA UZALENDO KWA TAIFA LETU

0
0

Na Emmanuel J. Shilatu
Leo ni Julai 25 siku ya Maadhimisho ya Mashujaa waliopambana kwa hali na mali kutetea nchi yetu ya Tanzania katika maeneo mbalimbali.

Hawa walimea uzalendo mkubwa, mwili na nafsi zao walikubali kuviweka rehani kwa ajili ya Tanzania. Bado tunawakumbuka na kuwaombea kheri kutokana na kujali na kudumisha misingi ya amani.

Misingi mizuri iliyojengwa na waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume , imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa amani na utulivu, huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila ya kuingiliwa na mtu yeyote wa ndani ama wa nje.

Tofauti na mataifa mengine, Watanzania wako huru zaidi kwenda kokote wanakotaka na hata kuishi ama kufanya kazi au biashara bila ya bughudha yeyote endapo kanuni, taratibu na sheria za nchi zitafuatwa ama kuzingatiwa vyema. Hali hiyo ni tofauti kabisa na nchi nyingine zikiwamo zile za jirani zetu kama Kenya, Rwanda, Burundi, Kongo na hata Uganda, nchi ambazo kwa kiasi kikubwa ukabila na chokochoko za kisiasa zimetamalaki kuanzia ngazi za kijiji hadi Taifa. Hapa kwetu tumeishi kama Ndugu bila ya u-rangi, udini, ukabila wala harakati za kiitikadi na kisiasa kutugawa.

Jambo la kushangaza ni kuwa misingi hiyo ya amani na utulivu iliyogharamikiwa na Waasisi wetu, hivi sasa ipo shakani na hatarini kutoweka kwani ilishaanza kuchezewa na chokochoko za aina mpya ya siasa (kwa maana ya ukosefu wa uvumilivu na uchu wa madaraka) iliyoanza kurindima katika siku za hivi karibuni.

Tukiwa tunawakumbuka Mashujaa hao inabidi nasi tujitathmini nafasi yetu kwa Taifa letu endapo inaedana na hali ya uzalendo. Hali ilivyo sasa kiwango cha uzalendo kimeshuka sana. Mtu yupo radhi kulalamika na kudai haki pasipo kutimiza wajibu wake kwa Taifa. Wameshajiuliza, wamelifanyia nini Taifa kabla ya kudai haki?

Vijana walio wengi wameweka pembeni uzalendo wa kulipenda Taifa lao kiasi cha kufikia hatua ya kukufuru kwa maneno ya kashfa dhidi ya Taifa lao. Hali hiyo ni tofauti kabisa na mataifa mengine ambayo hatuoni wakiyakashifu mataifa yao hadharani. Hii tabia ya kujivua nguo hadharani ni kwa faida ya nani?

Hapo hapo utakuta kuna baadhi ya Watanzania wanenda nchi za kimataifa na kuanza kuikashfu nchi yao kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kimataifa. Laiti kama Wazee wetu waliotutangulia wangekuwa na akili mbovu kama hizi, leo hii sidhani kama tungelikuta Taifa hili likiwa salama kama lilivyo. Umejiuliza haya ya kulichafua Taifa letu unataka uache urithi gani kwa vizazi vijavyo kwa Taifa letu?

Vijana wengi wa Leo, wananyooshewa vidole kwa kutothamini tunu ya kuwa Mtanzania. Je, U-Miongoni mwao? Kwako uzalendo ni nini? Kwako amani unailindaje?

Ndugu zangu, Wapo wanaosema kuwa amani ni sawa na yai mkononi, ukilivunja hautaweza kuliunganisha kamwe; wengine wanasema kuwa amani haina bei na ikipotea haina soko la kununua. Tuitunze amani yetu na kamwe tusiizoee wala kuichoka, tuige uzalendo waliokuwa nao Mashujaa wetu ambao walihakikisha amani ya nchi wanailinda vilivyo kwa machozi, jasho na damu.

*Shilatu E.J*
0767488622

WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO

0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

SERIKALI ikiwa inaendelea uwekaji wa mifumo ya utoaji huduma kwa njia ya kielekroniki katika taasisi zake kwa upande wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umepiga hatua kubwa katika hilo katika kuhakikisha huduma zitolewazo kwa wananchi zinakidhi haja zao.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Ofisa Habari wa RITA Jafari Malema amesema mifumo hiyo ya kielekroniki ni ya Usajili wa Vizazi na vifo unaojulikana kama Birth Registration Fourth Generation (BRS4), Mfumo wa malipo ya ada ya huduma wa Serikali, Government elecronic Payment Gateway (GePG) na Mfumo wa Uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vifo kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu ya juu na watu wengine.

Malema ameeleza kuwa "Kwa kuwa mwaka jana tulipata changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi kufikika katika ofisi zetu na kusababisha msongamano ndiyo maana mwaka huu tumekuja na suluhisho la kudumu na tumefanikiwa kwa asilimia 98 ya uhakiki na kuwajibu wanafunzi," ameeleza.

Ameeleza hadi sasa wamepokea jumla ya maombi 95,561 kati ya hayo maombi 94,344 sawa na asilimia 99 yamefanyiwa kazi na kujibiwa na maombi 1217 sawa na asilimia 1.3 yanaendelea kufanyiwa kazi na kati ya maombi yote yaliyojibiwa ni maombi 92,304 sawa na asilimia 98 yamehakikiwa na hayana mapugufu yoyote na maombi 2040 sawa na asilimia 2 yameonekana kuwa na mapungufu na yanafanyiwa marekebisho.

Akieleza utofauti wa kiutendaji kwa sasa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo huduma zilitolewa kwa mifumo ya kizamani ya karatasi, Malema ameeleza kuwa mfumo huo umekuwa rahisi zaidi katika utoaji wa huduma ukilinganisha na miaka iliyopita kwani huduma zote hufanyika kwa njia mtandao wanachotakiwa ni kutembelea tovuti ya http://uhakiki.rita.go.tz/uhakiki.

Wanafunzi wengi wameonekana kuvutiwa na huduma hiyo ambapo walipata majibu yao kwa muda wa siku tatu pekee ambapo katika msimu wa sabasaba  wanafunzi wengi walijitokeza kuhakiki vyeti vya kuzaliwa na vifo ili kuweza kuomba mikopo ya elimu ya juu na waliridhishwa na huduma hiyo.

Kuhusiana na ufanisi wa mfumo wa uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vifo imeelezwa kuwa shughuli hiyo itakuwa inafanyika muda wote bila ya kujali wanafunzi au watu wa kawaida kwani kuna mahitaji makubwa kutoka kwa Taasisi nyingine za serikali kama vile Idara ya Uhamiaji, Bima ya Afya na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambao wanawaelekeza wananchi kuhakiki vyeti vyao ndipo waweze kupatiwa huduma husika hivyo wataendelea kutoa huduma hiyo.

Changamoto zilizojitokeza katika mchakato huo hasa kwa upande wa wanafunzi ni kutuma kimakosa nyaraka tofauti na vyeti kwa mfano baadhi yao kutuma picha, vitambulisho vya kupigia kura na fomu za kuombea mikopo.Pia kuna wanafunzi waliokwenda mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa walishakamilisha hatua za maombi lakini tatizo lipo kwa wazazi na walezi ambao wamesahau Nyuwila (password) ya kuangalia majibu ya uhakiki.

Malema amewataka wananchi pamoja na taasisi za umma kutumia huduma zinazotolewa na wakala hiyo na kutoa wito kwa wananchi kuwasilisha nyaraka halisi pindi wanapotaka kupewa huduma.
 Afisa Mawasiliano  wa (RITA) Jafari Malema akizungumza na Michuzi Blog kuhusu Wananchi kuwasilisha nyaraka halisi na kuacha kutumia nyaraka bandia ambazo hazitoki (RITA).Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.
 Afisa Mawasiliano  (RITA) Jafari Malema kushoto na Afisa Masoko RITA, Edwin Mbekenga, wakionesha vyeti feki vya kuzaliwa.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Maofisa wa (RITA) wakiendela na kazi ya uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa 
Makao Makuu jijini Dar as Salaam.

MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE

0
0
*Ni kutaka iendelee na kupanga kusoma usikilizwaji wa awali

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubaliana na ombi la upande wa Jamuhuri la kutaka kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali na uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe iendelee na kupanga kusoma usikilizwaji wa awali (PH)
Julai 31 mwaka 2018.

Pia Mahakama imeruhusu upande wa mashtaka kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo mara moja baada ya PH kusomwa. Hayo yamefikiwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri baada ya kesi hiyo kuja kwa kutajwa kutokana na kusimama kupisha maamuzi ya mahakama kuu. 

Kutokana na maombi ya upande wa mashtaka yaliyokuwa yakiomba mahakama kuu kufanyia marejeo mwenendo wa kesi yao juu ya uamuzi wa mahakama ya Kisutu.Hata hivyo, Julai 20 mwaka 2018 Mahakama Kuu ilitoa uamuzi na kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa yalikuwa ni batili na kwamba yalikosa vigezo kisheria.

Mapema Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba Mahakama kulipangia shauri hilo tarehe ya kuwasomea washtakiwa  PH kwa kuwa uamuzi wa mahakama kuu ulishatoka na ombi la utetezi kutupiliwa mbali. "Mheshimiwa, shauri hili leo limekuja kwa kutajwa kwa sababu tulikuwa tunasubiri maamuzi ya Mahakama Kuu, lakini kwa kuwa maamuzi yameishatolewa.

"Tunaomba tarehe ya kuja kuwasomea washtakiwa PH na kuanza kusikilizwa siku hiyo hiyo mfululizo kwa tarehe zitakazopangwa na mahakama," ameeleza Nchimbi,Hata hivyo, Wakili wa utetezi Nashon Nkungu kwa niaba Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya wanaowatetea washtakiwa amedai kuwa baada ya uamuzi ule wa Mahakama Kuu, washtakiwa wamefaili kusudio la kukata rufaa mahakama ya Rufani ambayo ilipokelewa Julai 20 mwaka 2018

" Kutokana na kusudio hilo la Rufaa tunaomba muda wa kutosha kabla ya kusomwa kwa PH kwa kuzingatia kuwa kuna rufaa," amedai Nkungu.Akijibu hoja hiyo, Wakili Nchimbi amedai mahakama inatakiwa kutoa maamuzi kwa kuzingatia mambo ambayo yako kwenye kumbu kumbu za mahakama, lakini mpaka sasa hakuna chochote kilichopo mbele ya mahakama kuhusu kusudio la kukata rufaa.

Baada ya mabishano ya pande zote mbili mahakama imekubaliana na ombi la Jamuhuri na kupanga  kuhusu shauri kupangwa kwa PH na kuanza kusikilizwa.Pia imeruhusu upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao juu ya maombi yao ni yapi, je ni ya kutaka shauri lao liahirishwe kwa muda mrefu au lisimame kupisha rufaa?Mbali na Mbowe, washitakiwa  wengine ni Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Msigwa, Naibu Katibu Mkuu  Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee,   Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Mbunge wa Tarime mjini, Matiko.Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 12, ambapo wanadaiwa kuwa  walitenda makosa hayo Februari 16, mwaka huu katika maeneo ya Viwanja vya Buibui, Mwananyamala na  barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni.

Wanadaiwa kuwa Februari 16 mwaka huu katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washitakiwa hao wakiwa na wenzao 13 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.
Baadhi ya viongozi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

MAKAMU WA RAIS APOKEWA KWA SHANGWE MKOANI MBEYA

0
0
 Wakazi wa Mbalizi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposimama na kuwasalimia wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za  maendeleo mkoani  humo ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya Wakazi wa mji wa Mbalizi (hawapo pichani) waliojitokeza kumpokea wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za  maendeleo mkoani Mbeya. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa Mbalizi waliojitokeza kumpokea wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za  maendeleo mkoani Mbeya. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

TARURA BAHI WAMWAGIWA SIFA

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akifanya uhakiki wa vipimo vya upana wa Daraja la Chipanga kama vinaendana na BOQ

Daraja la Chipanga lililo katika hatua za mwisho za umaliziaji wilayani Bahi
Viongozi wakikagua maabara iliyoanza kutoa huduma baada ya kumaliza kwa ujenzi katika kituo cha afya Bahi.

Zoezi la ukaguzi wa miradi likiendelea wilayani Bahi
Mbunge wa jimbo la Bahi Omary Baduel akiishukuru serikali kwa kufanikisha miradi ya maendeleo wilayani Bahi



Ujenzi wa daraja la Chipanga lililopo wilayani Bahi Mkoani Dodoma limeleta faraja kwa wananchi na viongozi wa wilaya hiyo huku wakimwagia sifa Wakala wa Barabara wa Mijini na Vijijini (TARURA) kwa usimamizi mzuri.

Hali hiyo imejidhihirisha leo katika ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Bahi.

Akizungumzia kufurahishwa na ujenzi huo, Mbunge wa Jimbo la Bahi Omary Baduel amewapongeza TARURA kwa ujenzi wa daraja hilo kubwa na barabara zake kwa ubora wa hali ya juu ikilinganishwa na siku za nyuma kabla TARURA haijaanza.

Daraja la Chipanga ni daraja kubwa lenye urefu wa mita 45 na limegharimu Sh. bilioni 2.18 na litakuwa mkombozi kwa wananchi wa Chipanga ambao walikuwa wanateseka kwa miaka yote.

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kutembelea ujenzi wa kituo cha Afya Bahi kinacho karabatiwa na serikali kwa Sh.Milioni 500 ambapo hadi sasa kazi ya ujenzi imekamilika na wananchi wameanza kupata huduma katika majengo hayo yaliyojengwa kisasa.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza atembelea Benki Kuu, JWTZ NA TAKUKURU

0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,  Prof. Florens Luoga amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kuendelea kutoa mchango wake katika kudumisha hali ya ulinzi na usalama nchini kupitia majukumu yake ya uhifadhi salama wa wafungwa na utoaji wa huduma za urekebishaji kwani Amani na Usalama ni msingi wa maendeleo katika nchi yoyote duniani.
Prof. Luoga amesema hayo wakati wa mazungumzo katika ziara ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike alipotembelea Benki Kuu ya Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake  za kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa tangu ateulie kuwa Mkuu wa Jeshi hilo Julai13, 2018.
Aidha, Profesa Luoga amelishauri Jeshi la Magereza kuongeza ubunifu katika miradi ya uzalishaji mali kwa kufanya utafiti utakaoongeza ubora  wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ili kuendana na mahitaji ya soko la ndani na hata nje ya nchi kwa kuwa taasisi kama magereza inaaminika.
“Jambo kubwa ni kubadili mtazamo na namna ya kufikiri kwa kusoma alama za nyakati na mabadiliko ya ulimwengu, kila kitu kinawezekana”. Amesisitiza Prof. Luoga.
Prof. Luoga ameahidi kuwa Benki Kuu ya Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Magereza hasa katika ushauri wa kitaalam pale itakapohitajika kufanya hivyo ili kufikia malengo mahususi.
Ameongeza kuwa Taasisi anayoiongoza italipa ushirikiano Jeshi la Magereza kwa kuliunganisha na wadau mbalimbali watakaofanya kazi na Jeshi hilo kufanikisha majukumu yake pale fursa za kufanya hivyo zitakapojitokeza.
Wakati huo huo, Kamishna Jenerali Kasike amekutana na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Valentino Mlowola.
Mkurugenzi Mlowola amemhakikishia Kamishna Kasike ushirikiano wa dhati kwa kuwa vyombo hivyo viwili ni miongoni mwa taasisi  zinazosimamia utekelezaji wa sheria nchini hivyo ukaribu wao katika utendaji hauepukiki.
“Msingi wa amani katika nchi umewekezwa katika vyombo vyetu, kwahiyo ushirikiano ni muhimu sana”. Amesema Mlowola.
Kamishna Jenerali Kasike yuko katika ziara ya kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa ikiwa pia ni sehemu ya kuelezea majukumu ya msingi ya Jeshi la Magereza ambayo ni pamoja na uhifadhi salama wa wahalifu na utoaji wa huduma za urekebishaji kwa wafungwa ili wawe raia wema pindi wamalizapo vifungo vyao.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Flolens Luoga alipotembelea Benki Kuu ya  Tanzania katika ziara yake ya kujitambulisha kwa Viongozi waandamizi Serikalini leo Julai 25, 2018, jijini Dar es Salaam.

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Flolens Luoga(kulia) alipotembelea Benki Kuu ya Tanzania kwa lengo la kujitambulisha leo Julai 25, 2018.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiwa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed alipomtembelea Ofsini kwake leo Julai 25, 2018 jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini, Valentino Mlowola akimkabidhi nembo ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike kama inavyoonekana katika picha alipotembelea Taasisi hiyo leo Julai 25, 2018

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AELEZEA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA

0
0
MSEMAJI Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbasi ameelezea kinachoendelea katika utekelezaji wa ahadi za Serikali huku akitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wanahabari wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa maadili ya kiwango cha juu.

Akizungumza na waandishi mbalimbali Mjini Dodoma Dk.Abbasi ameanza kwa kuwapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano ambao wamekuwa wamekuwa wakiutoa katika kusaidia mwaka wa fedha 2017/2018 katika kusaidia kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Hata hivyo amesema bado wamendelea kushuhudia kuwepo kwa vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya taaluma kwani pale Serikali itakapochokua hatua kusiwe na lawama.Pamoja na hayo akafafanua mambo mbalimbali nchini ambapo katika hali ya uchumi Dk.Abbasi amesema hadi Machi mwaka 2017 pato la Taifa lilikuwa kwa wastani wa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 kwa mwaka 2016.

Amesema ukuaji huo ulitokana na na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuimarika kwa shughuli za kiuchimi."Kilimo kutoka asilimia 2.1 hadi asilimia 3.6, mawasiliano kutoka asilimia 13.0 hadi asilimia 14.7, madini kutoka asilimia 11.5 hadi asilimia 17.7 na ujenzi kutoka asilimia 13.0 hadi asilimia 14.1,"amesema Dk.Abbasi.

Pia amesema maji kutoka asilimia 4.3 hadi asilimia 16.7 , uchukuzi kutoka asilimia 11.8 hadi asilimia 16.6, elimu kutoka asilimia 8.1 hadi asilimia 8.5 na afya kutoka asilimia 5.2 hadi asilimia 5.9.Kwa taarifa zaidi kuhusu ambacho Dk.Abbasi amekielezea kwa watanzania kupitia waandishi wa habari na kufafanua kwa kina kupitia maelezo yake ambayo yamewekwa kama yalivyo

HAPA CHINI



HALI YA USAFI COCO BEACH HAIRIDHISHI - WAZIRI MKUU

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitembea kwa miguu kuelekea kwenye eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam ambako Julai 25, 2018 waliadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy baada ya kuwasili katika eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam  kuadhimisha siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo hilo Julai 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  wakifyeka nyasi kwenye  eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam  wakati waliposhiriki  katika maadhimisho ya   Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo , Julai 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiadhimisha  Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi katika eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipeleka uchafu kwenye gari la takataka wakati waliposhiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  eneo la Coco Beach  baada ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye  eneo hilo Julai 25, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  eneo la Coco Beach baada ya kushirika katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo Julai 25, 2018. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia mti alioupanda baada ya Kuadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi kwenye eneo la Coco Beach jijini Dar es salam Julai 25, 2018. Kushoto ni mkewe Mary na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru mamia ya watu  walioshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakizungumza na Bibi Amina Fadhili (kulia) baada ya kuadhimisha siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira kwenye  eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine ya kukamua juisi ya miwa, mali ya Abdillah Issa (kulia) wakati alipotembelea eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam baada ya kuadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo hilo Julai 25, 2018.

*Ataka Mamlaka za Serikali za Mitaa husika zisimamie fukwe zote nchini 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya usafi Coco Beach hairidhishi na amewataka viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wajipange ili eneo hilo liweze kuvutia.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 25, 2018) wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kushiriki zoezi la usafi wa eneo hilo pamoja na wananchi na watendaji mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambayo hufanyika Julai 25, kila mwaka.

Waziri Mkuu ambaye aliambatana na mke wake, Mary Majaliwa, alishiriki zoezi hilo kwa kufyeka nyasi, kuzoa takataka na kupanda miti kwenye ufukwe huo. Zoezi hilo limefanyika kuanzia kwenye eneo la wafanyabiashara wa mihogo kuelekea Police Officers’ Mess.

“Eneo hili nimelitembelea, bado haliridhishi kwa usafi. Nimeenda kwenye fukwe pale na kukuta takataka nyingi zimelundikwa mahali pamoja. Ni vema Manispaa ya Kinondoni na Mamlaka zote zinazosimamia usafi ziwaratibu wanaotoa huduma na wanaopata huduma ili kuendeleza usafi wa maeneo haya nchini kote,” amesema.

Amesema Manispaa ya Kinondoni haina budi kuratibu eneo hilo kwa kupanga eneo la maegesho, la watu kupumzikia, la huduma za chakula na kuongeza kupanda miti ili wananchi waone ni maeneo mazuri yanayovutia.

“Muandae shughuli za burudani zitakazofanyika kila Jumamosi na Jumapili. Karibisheni watu wa kuleta michezo ya baharini kama vile viboti na vibaiskeli vya majini, wekeni bembea ili fukwe ivutie zaidi. Wazazi wataleta watoto wao kwenye michezo wakati wao wakikaa pembeni na kupumzika,” amesema.

Amesema vibanda vilivyoko kwenye ufukwe huo havipendezi na ikibidi waangalie uwezekano wa kuweka makontena ili kuongeza mvuto. “Vibanda hivi havileti picha nzuri sana, hivyo mnaweza kuweka makontena kutoka Pepsi au Coca-Cola ili kuleta muonekano sawia.”

“Jambo hilo linaweza kuwa ni chanzo cha mapato kwa Manispaa hii. Uongozi wa Manispaa tengenezeni haya wakati mkisubiri andiko lenu lipitishwe na muweze kupata fedha za kuboresha ufukwe huu,” amesema.Alisema eneo jingine linalopaswa kuangaliwa katika ufukwe huo ni kuimarishwa kwa ulinzi ili watu wanaokwenda kupata huduma wasihofie usalama wao.

Waziri Mkuu amesema usafi siyo uishie kufanyika tarehe 25 tu, na akawataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye fukwe zote. “Hii ni changamoto kwenye Mamlaka ya Halmashauri ya Kinondoni, lakini pia Ilala, Temeke, Bagamoyo hadi Tanga, zinapaswa aihakikishe hizi fukwe ziwe safi,” amesema. 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi hao, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Ally Hapi alisema mbali ya wananchi wa kawaida, walikuwepo pia askari polisi 100 na wanajeshi 150 ambao walishiriki zoezi hilo la usafi.

Alisema Manispaa ya Kinondoni wameanza kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu juu ya uboreshaji wa fukwe ya Coco kwa kuandika andiko maalum na kulipeleka Ofisi ya Rais – TAMISEMI. “Manispaa kupitia miradi ya kimkakati, tumeandaa andiko la kuomba sh. bilioni 11 za kutengeneza na kuboresha ufukwe wa Coco, na tumeshalipeleka TAMISEMI na mazungumzo yanaendelea,” alisema. 

Juni 29 mwaka huu, wakati akitoa maelekezo kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha polisi kinachohamishika, Waziri Mkuu alisema: “Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anawataka Watanzania wote waadhimishe siku hiyo ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi katika maeneo yaliyo jirani na makazi yao pamoja na yale ambayo wamezikwa mashujaa ikiwa ni njia ya kuwaenzi. 

Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu alitangaza kwamba Rais Magufuli ameagiza kwamba sh. milioni 308 zilizotengwa kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa, zitumike kuboresha miundombinu ya barabara jijini Dodoma.

Aliitaja miundombinu hiyo ni pamoja na taa za kuongezea magari kwenye makutano ya barabara ya Kisasa na barabara kuu ya Dodoma Dar es Salaam na kuweka taa za barabarani kwenye barabara mpya ya mchepuko kutoka Emmaus hadi African Dream iliyojengwa ili kupunguza msongamano wa magari yanayoingia kutoka barabara kuu ya Dar es Salaam.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, JULAI 25, 2018.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata

0
0
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata bali waendelee kujitoa katika kuokoa maisha ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. 

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima alipokuwa akizungumza na wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam. 

Dkt. Gwajima alisema hivi sasa Taasisi hiyo imekuwa tegemeo kubwa kwa wagonjwa wa moyo kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati hivyo basi ufanyaji kazi kwa ufanisi utasaidia wananchi wengi kuendelea kupata huduma za matibabu ya moyo hapa nchini. 

“Jamii ya Tanzania inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na JKCI, nawasihi wafanyakazi msikubali changamoto yoyote ile inayowakabili ikaitoa Taasisi hii katika mstari wa mafanikio mliyoyapata”. 

“Mtambue kuwa Taasisi hii ni mkombozi wa wagonjwa wenye matatizo ya moyo ambao hivi sasa hawaendi tena kutibiwa nje ya nchi wanatibiwa hapa nchini matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya moyo”, alisema Gwajima. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Prof. Mohamed Janabi alisema Taasisi hiyo itaendelea kutoa huduma bora zaidi, kupunguza wagonjwa wanaoenda nje ya nchi kutibiwa magonjwa ya moyo pamoja na kushirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku. 

“Taasisi imefanikiwa kufanya kazi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa nne usiku, kwa kufanya hivyo tumeweza kuona wagonjwa wote wanaofika kwa ajili ya kupata matibabu kwa wakati na kupunguza msongamano wa wagonjwa”, alisema Prof. Janabi. 

Tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo mwaka 2015 idadi ya wagonjwa wanaotibiwa imekuwa ikiongezeka kutoka elfu kumi na tano kwa mwaka 2015 hadi kufikia wagonjwa 64,093 kwa mwaka 2017. 
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi tuzo ya utendaji kazi bora wa Idara ya Magonjwa ya Moyo ambayo ni moja ya Kurugenzi tano za Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo ambaye pia ni daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpongeza Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Ghati Chacha kwa ajili ya utendaji kazi mzuri wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha walioufanya kwa kipindi cha miezi mitatu wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza washindi iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima.
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo ya utendaji kazi bora wa Kitengo cha manunuzi David Kakoti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika hafla fupi ya kuzipongeza Idara na Vitengo vilivyofanya kazi vizuri kwa kipindi cha miezi mitatu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa mada wakati wa kikao na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pamoja na viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika kivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Tiba Tanzania Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo daktari bingwa wa upasuaji wa Moyo Dkt. Evarist Nyawawa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutokana utendaji kazi bora wa kitengo cha upasuaji wa Moyo wakati wa kikao na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.Picha na Brighton James -JKCI.

GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN)

0
0
Na Luteni Selemani Semunyu.

Klabu ya Gofu ya jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo imetamba kuendeleza wimbi la ushindi katika Mchezo huo kupitia timu yake yenye wachezaji 30 inayotarajia kusafiri kuelekea Mufindi mkoani Iringa kushiriki mashindano ya wazi ya Mufindi yanayotarajiwa kufanyika Julai 27 hadi Julai 29 katika Viwanja vya Klabu hiyo 

Akizungumza na Waandishi wa habari mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu alisema Timu inatarjiwa kuondoka Julai 26 kuelekea Mufindi ambapo mbali na wachezaji wa Ridhaa wapo wachezaji wa kulipwa Sita ambao nao wamejipanga kufanya vyema..

“ Tunawachezaji wengi nyota na chipukizi wengine wapo kwenye majukumu ya kazi lakini wengine wako katika kuwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa kwa kuwa tuna vipaji vya kutosha tutapeleka Timu nzuri na kupata Ushindi” Alisema Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo.

Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo aliwataja Wachezaji wa Kulipwa wa Klabu ya Lugalo watakaowakilisha katika Mashindano hayo kuwa ni David Helela, Abdalah Yusuph, Geofrey Leverian na Brison Nyenza , Iddi Mzaki aliyechukua nafasi ya tatu katika mashindano ya wazi ya Lugalo na Athumani Chiundu.

Aliwataja Wachezaji wengine ambao ni wa Ridhaa kuwa ni pamoja na Mshindi wa Jumla wa mashindano yaliyomalizika hivi karibuni ya Wazi ya Lugalo Geofrey Gwacha, Aliyeshinda Divisheni A kapteni Shaban Kibuna na Mshindi wa Divisheni B Agrey John.

Aliongeza Kuwa Mbali na Wachezaji Nyota Wanawake wa Klabu hiyo pia Mshindi wa Upande wa Wanawake Habiba Likuli naye atakuwemo katika kikosi hicho cha Lugalo ambacho kitaongozwa na mkuu wa Msafara Luteni Kanali David Luoga na Afisa Tawala wa Klabu hiyo Amanzi Mandengule.

Kwa upande wake mkuu wa Msafara Luteni kanali David Luwoga alisema Timu ipo imara na inaendelea na mzoezi huku taratibu mbalimbali zikifanyika kuhakikisha unakuwa mzuri na kuleta ushindi kwa Klabu ambayo ndio lengo kubwa.

Klabu ya Gofu ya Lugalo imekuwa Klabu mahiri ya Mchezo huo hapa nchini na nje ya nchi kutokana na wachezaji wake wakiwemo maofisa na Askari kufanya vyema na kuibuka na ushindo na kuongeza hamasa ya Mchezo huo hapa nchini.
 Mshindi wa kwanza wanawake kutoka klabu ya Gofu ya Lugalo Habiba Likuli akipiga mpira wakati wa mashindano ya wazi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam anayemuangalia ni Amanda Mlula wa klabu hiyo( Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Baadhi ya Wachezaji wa klbu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakiwa katika mazaoezi katika uwanja wa Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam( Picha na Luteni Selemani Semunyu)

MAAFISA BIASHARA WAPEWA SOMO KUHUSU URASIMISHAJI

0
0

WAZIRI JAFO APONGEZA KITUO CHA AFYA BAHI KUKAMILISHA

0
0
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika Kituo cha Afya Bahi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akikagua maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kituo cha Afya Bahi.
 ............................................................................ 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Seleman Jafo leo ameendelea na ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuona maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa.

 Mhe. Jafo amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Kituo cha afya cha Bahi na kuweza kukamilika kwa wakati na tayari kimeanza kutoa huduma kwa wananchi.

 Akiongelea kuhusu watumishi wa huduma ya afya walioajiriwa hivi karibuni amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tayari imepata watumishi 39 ambao watatawanywa katika Halmashauri hiyo. 

 Amesema kutokana na Halmashauri ya Bahi kuwa naupungufu Mkubwa wa vituo vya afyaSerikali imeweza kujenga vituo vya afya vya Mundemu na Bahi ili kutoa huduma bora kwa wananchi, pia tayari Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya.

 Mhe. Jafo amemuagiza wahudumu wa afya wote nchini kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili waweze kuvutiwa kuja kutibiwa kwenye vituo vya afya. "Nawaagiza Wasimamizi wote wa Vituo vya afya na Zahanati kuhakikisha wanatumia lugha nzuri kwa wagonjwa ili kuwavutia kuja kupata huduma za afya" Amesema Jafo

 Aidha amewataka wananchi kuhakikisha wanafuata ushauri unaotolewana na wataalam ili kuboresha afya zao.

Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images