Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MAFUNZO YA MAAFISA UANDIKISHAJI WA CHF ILIYOBORESHWA YAFANYIKA WILAYANI CHEMBA

$
0
0
Na Shani Amanzi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amewataka waandikishaji waliopata Mafunzo ya maboresho ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) wakawatumikie vyema Wananchi kwani lengo kubwa la Serikali ni kuona jamii inapata huduma bora ya Afya. 

Dkt. Semistatus Mashimba aliyazungumza hayo alipokuwa anafungua mafunzo ya siku mbili ya Maafisa uandikishaji wa CHF wa vijiji vyote vya wilaya ya Chemba kwa kushirikiana wadau wa mradi wa HPSS-Tuimarishe afya kuanzia Tarehe 16 mpaka 17 Julai 2018 katika ukumbi wa Godown mjini Chemba. 

“Nawaomba muwe mabolozi wazuri kwa wilaya ya Chemba kwa kupunguza malalamiko na kutoa elimu ya kutosha juu ya mabadiliko ya bei ya uandikishaji wa kitambulisho cha bima ya Afya ya CHF Iliyoboreshwa kutoka tsh 13,000/= kwenda tsh 30,000/=, na lengo kubwa la serikali ni kuwasaidia wananchi hasa walio kwenye hali ya chini kupata huduma za afya katika vituo mbalimbali vya afya vilivyoko nchini” aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Semistatus Mashimba. 

Naye Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) wilaya ya Chemba Ndg. Haruna Haji amesema katika zoezi la uandikishaji Wilaya ya Chemba, atahakikisha kwanza anatoa elimu ya kutosha kwa Maafisa Uandikishaji wa Mfuko wa CHF katika kila kijiji ili kuondokana na vikwazo kwa wanachama wa CHF na pia atahakikisha elimu hii muhimu ya bima ya afya inawafikia wananchi wote wilayani hapo. 

Ndg.Haji amesema “katika uhifadhi wa nyaraka kuna utunzaji mkubwa na kuendelea kuwahamasisha kukusanya fedha kamili kabla ya kutoa kitambulisho pia tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi maboresho yanayoendelea ya CHF ikiwemo bei mpya ya kitambulisho cha CHF. 

Vilevile Afisa wa Mradi wa HPSS- Tuimarishe afya wilaya ya Chemba bi. Salome Chilongani ametoa shukurani zake kwa mkuu wa wilaya pamoja mkurugenzi wa halmashauri ya Chemba kwa kuonesha ushirikiano wao mkubwa kwenye mafunzo hayo. 

Bi. Salome amesema “Kwanza nianze kwa kutoa pongezi na shukurani kwa viongozi wetu wa wilaya ya Chemba, yaani mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wa halmashauri, kwa kuonesha ushirikiano mkubwa sana kwenye mafunzo haya, kwakweli wameshiriki kikamilifu sana na wameweza kuwaelewesha Maafisa Uandikishaji hawa umuhimu wa elimu waliyoipata na kutoa msisitizo kuilinda dhamana waliyoibeba. 

Mimi kama mdau nimefarijika kuona jinsi viongozi hawa walivyotupokea na kujali shughuli zinazotekelezwa na mradi wa HPSS, nina matumaini mwaka mmoja baada ya mafunzo haya tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa na tutakuwa na wanachama wengi sana wa CHF katika wilaya yetu ya Chemba” 
 Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Semistatus Mashimba akizindua Mafunzo ya CHF iliyoboreshwa
Baadhi ya Wadau mbalimbali waliohudhuria mafunzo hayo.

MBEBA MIZIGO ABEID AMRI ANYAKUA KOMBE LA‘SUPA MZUKA CUP’ LA MILIONI 300

$
0
0

Mkurugenzi wa mawasiliano wa TatuMzuka Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),wakati wa akimtambulisha
Mshindi wa kampeini ya ‘SupaMzuka Cup’ aliyeshinda katika fainali tarehe 15 Julai 2018 kitita cha milioni 300 za kitanzania,Abeid Amri mkazi kutoka Mbagala

Abeid Amri, 28 anayeishi Mbagala Wilaya ya Temeke Dar es Salaam ndiye ameibuka mshindi wa Jackpot kubwa kuwahi kutokea nchini Tanzania. Amri hakushinda peke yake bali alichagua timu yake ya watu 10 ili kukamilisha timu yake ya watu 11 ambapo kila mmoja amepata milioni 1. Mwakilishi kutoka kampuni ya michezo ya kubahatisha Abdallah Hemed
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo
Mkurugenzi wa mawasiliano wa TatuMzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa kampeini ya ‘SupaMzuka Cup’ aliyeshinda katika fainali tarehe 15 Julai 2018 kitita cha milioni 300 za kitanzania,Abeid Amri mkazi kutoka Mbagala

TatuMzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini Tanzania leo umemkabidhi Mshindi wa kampeini ya ‘SupaMzuka Cup’ aliyeshinda katika fainali tarehe 15 Julai 2018 kitita cha milioni 300 za kitanzania.

Abeid Amri, 28 anayeishi Mbagala Wilaya ya Temeke Dar es Salaam ndiye ameibuka mshindi wa Jackpot kubwa kuwahi kutokea nchini Tanzania. Amri hakushinda peke yake bali alichagua timu yake ya watu 10 ili kukamilisha timu yake ya watu 11 ambapo kila mmoja amepata milioni 1.

“Tumepata faraja kubwa kushuhudia Mtanzania mwenzetu akipata ushindi mkubwa kiasi hiki. Umetuandikia historia leo kwa sababu haijawahi kutokea nchini Tanzania mtu kushinda million 300. ” Alisema Bwana Sebastian Maganga, Mkurugenzi wa mawasiliano wa TatuMzuka

Kwa Msimu huu wa SupaMzuka Jackpot watu wamecheza na kushinda na marafiki, na Bwana Amri pia alichagua timu yake ambao ni; 1 Mwanaidi Omary, 2.Subira Issa 3. Jasmin Issa 4. Shufwaa Issa 5. Farhat Issa 6. Omary Issa, 7. Amin Issa 8. Mwanaasha Omary, 9. Agness Samwel, 10. Magdalena.

“Mimi sijala vizuri, wala kulala tangu siku hiyo jumapili. Kila saa nawaza kama ni ndoto alafu nitaamka, lakini sasa naamini kabisa kwamba ni kweli nimeshinda” aliezea Amri. “Nina furaha sana na pia kushinda na marafiki, najiskia kama wengi tumeshinda!” alisisitiza Amri.

TatuMzuka imeuutarifu umma kwamba mshindi tiyari ameanza kupatiwa mafunzo kuhusu mikakati na mbinu za kutumia na kutunza fedha zake.“ Tangu alipopata Ushindi wake, tumeanza kumsaidia kutafuta wataalamu wa masuala ya utunzaji na uwekezaji wa fedha ili wawawe kumshauri namna nzuri ya kuwekeza fedha zake ili ziweze kumsaidia zaidi” alifafanua Bwana Maganga

TatuMzuka wanaendelea kuwapa watanzania fursa ya kuwa mamilionea . Kucheza Tatu Mzuka kupitia; MPESA, TIGO PESA na AIRTEL MONEY, unaingiza namba ya kampuni ambayo ni 555111 na baada ya hapo ingiza namba zako 3 za bahati kisha ingiza salio kuanzia shilingi 500 mpaka 30,000. Unaweza kushinda kila baada ya dakika 10, kila siku million 10 na Jumapili hii kuna Milioni 60.

MAHAKAMA MORO YAZUIA WATUHUMIWA WANAOACHIWA KUKAMATWA NDANI YA VIUNGA VYA MAHAKAMA HIYO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Morogoro, imezuia watuhumiwa wanaoachiwa kwa kifungu ambacho kinaruhusu wao kukamata, kukamatiwa ndani ya viunga vya mahakama hiyo.

Hayo yameelezwa leo mkoani hapa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro Elizabethi Nyembele wakati wa ziara ya waandishi wa habari za mahakamani walipofika katika Mahakama hiyo.

Waandishi hao wapo katika mafunzo ya siku tano yambayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.Mafunzo hayo yameahirikisha waandishi 30 wa vyombo mbalimbali nchini.

Amesema, wamezungumza na Polisi wasiwakamate watuhumiwa pindi wanapokuwa wameachiwa ndani ya viwanja vya Mahakama kwani ni fedhea.

" Tumezungumza na Polisi wasifanye hivyo, kwa sababu mara nyingine mshtakiwa anakamamatwa hata mbele ya hakimu bila kujali wapo katika eneo gani,

" Mtuhumiwa anakufuata anakwambia mheshimiwa naomba nilinde wanataka kunikamata kitendo ambacho si kizuri na hakileti picha," amesema Hakimu Nyembele

Ameongeza kuwa, hakimu anapoifuta kesi huku akijua inahitilafu kisheria anamueleza mtuhumiwa kuwa anaweza kufunguliwa kesi nyingine.Wengine ni waelewa unamuachia pale pale anaingia mikono ni mwa polisi bila kukimbia

" Zamani watu wamefariki kwa sababu ya hiyo hiyo ya kukimbia, anaweza kuwa ameachiwa ile furaha akakimbia, mwingine hajui kama ameachiwa na ameona amemtoa Magereza atampiga risasi kwa sababu anajua ametoroka, huwa tunawapa elimu wasifanye hivyo," amesema.

Aidha, ameeleza kesi za unyang'anyi, dawa za kulevya na kesi za ujangili ndizo zinazoongoza katika Mahakama hiyo na hiyo inasababishwa na mkoa kuzungukwa na mbuga na mapori

Pia amesema Mahakama hiyo imepiga hatua katika suala la rushwa, kutokana na elimu wanayowapatia watumishi na pia wamebandika matangazo mengi kuwa huduma zote ni bure kwa lengo la kuepusha rushwa.

Kwa upande wake Mtendaji wa mahakama hiyo, Nestory Mujunangoma amesema wanachangamoto ya vyumba vya mahakama, lakini hivi sasa wapo kwenye ujenzi wa jengo la ghorofa nne ambalo litakuwa na huduma zote,kuanzia Mahakama zote hadi vyumba vya rufaa.

Hakimu Mkazi  Mwandamizi  Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Elizabeth Nyembele akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotembelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwenye moja ya ziara za kimafunzo kwa Waandishi wa habari za mahakama mkoani Morogoro
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  Elizabeth Nyembele akizungumza na wananchi waliokuwa wakisubiri kuanza kwa mashauri yao kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro katika ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari  mkoani Morogoro.  (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MOROGORO)
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  Elizabeth Nyembele akionyesha waandishi wa habari nembo ya iliyopo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza maelezo ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele hayupo kwenye picha.
Mtendaji wa Mahakama mkoa wa Morogoro Nestory Mjunangoma akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Morogoro.
Baadhi ya wanahabari wakiendelea na ziara yao
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akimsikiliza mmoja wa waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo ya kimafunzo kwa waandishi hao.

Kamati ya Bunge yazindua minara ya Tigo wilayani Gairo

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Seleman Kakoso (wa tatu kulia), akishirikiana na Naibu Waziiri wa Miundombinu, Mhe Eng Atashasta Ndikiye (katikati aliyevaa kofia), Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, viongozi wa serikali, pamoja na wakurugenzi wa kampuni ya simu ya Tigo na Mfuko wa Kudumu wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kukata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa mawasiliano uliojengwa na UCSAF na Tigo ili kuwezesha mawasiliano ya simu kwa mara ya kwanza katika kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro juzi.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Dk Joseph Kilongola akitoa risala zake wakati wa hafla ya uzinduzi wa minara ya simu itakayowezesha upatikanaji wa mawasilino kwa mara ya kwanza katika kata za Kumbulu, Balama na Nongwe, WIlaya ya Gairo Mkoani Morogoro. Minara hiyo ilijengwa kwa ushirikiano baina ya Tigo na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuzinduliwa jana na wahemshimiwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Mawasiliano ya Bunge. 
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakicheza kwa furaha pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge - Miundombinu, Mhe mbunge Rashid Mohammed Chwachwa (Masasi- aliyejifunga shuka) wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakicheza kwa furaha pamoja na Naibu Waziri wa Miundombinu - Mhe Eng Atashasta Ndikiye (katikati aliyevaa kofia) wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakiigiza adha walizokuwa wanazipata kupata mawasiliano ya uhakika ya simu wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo. Mnara huo pamoja na mingine katika kata za Balama na Nongwe ilijengwa kwa ushirikiano baina ya Tigo na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuzinduliwa na wahemshimiwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Mawasiliano ya Bunge.


Ikiwa sehemu ya juhudi zake kuhakikisha kuwa kila mtu anashiriki kukuza uchumi wan chi na kupata maendeleo yatokanayo na huduma bora za mawasiliano, kampuni ya Tigo Tanzania imepanua mtandao wake katika maeneo ya pembezoni katika kata za Kumbulu and Balama yaliyopo wilaya ya Gairo, Mkoani Morogoro.

Akizindua minara hiyo mipya inayowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza kabisa katika kata hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu. Mheshimiwa Seleman Kakoso alisema kuwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano huleta mabadiliko makubwa ya ukuaji wa uchumi, ubunifu na maisha ya watu kwa ujumla. Mhe Kakoso alimbatana na Naibu Waziri wa Miundombinu, Mhe Eng. Atashasta Ndikiye, waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu pamoja na viongozi wengine wa serikali.

‘Nawashukuru Tigo kwa kuitikia mwito wa Serikali na kushiriki kikamilifu katika kuunganisha maeneo haya ya pembezoni ambayo hapo zamani hayakuwa na mawasiliano yoyote ya simu kwa sababu hayana mvuto mkubwa wa kibiashara. Ninatoa wito kwa kampuni nyingine za simu kuiga mfano huu ili kuhakikisha kuwa kila mtu anapata fursa ya kuwa sehemu ya mageuzi makubwa yatokanayo na Tehama, huku wakizingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali katika kutimiza miradi ya aina hii,’ alisema.  

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Dk Joseph Kilongola alibainisha kuwa minara hiyo ilikuwa imejengwa kwa ushirikiano baina ya UCSAF na Tigo kama sehemu ya zabuni ya zinazolenga kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha mawasiliano ya uhakika kwa wananchi wote.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa alisema kuwa lengo kuu la Tigo ni kuwaunganisha Watanzania zaidi ya milioni 13 ambao kufikia sasa bado hawana huduma za mawasiliano.

‘Tigo inaamini kuwa upatikanaji wa mawasiliano utaibua fursa mpya za kiuchumi, elimu, afya, biashara na kubadili maisha ya watu,’ alisema. Mutalemwa alisema kuwa kampuni ya Tigo imelenga kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga Tanzania ya viwanda kwa kupanua mtandao wake ili kuwezesha nchi nzima kufurahia faida za utandawazi utakanao na mawasiliano ya uhakika.

“Tunafuhari kuwa Serikali imetambua tofauti kubwa ya upatikanaji wa mawasilaino iliyopo baina ya maeneoa ya mijini na vijijini, na kujitolea kwake kufadhili zabuni mbali mbali zinazowezesha kampuni za simu kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo mbali mbali kama kata hizi za Balama, Kumbulu na Nongwe ambazo hapo awali hazikuwa na huduma yoyote ya mawasiliano ya simu kwa sababu hazina mvuto mkubwa wa biashara,’ alisema.

Tigo imeshiriki katika zabuni za UCSAF tangu mwaka 2012 ambapo kufikia sasa imefanikiwa kushinda zabuni zilizoiwezesha kuunganisha zaidi ya kata 100 na huduma za mawasiliano.

MAAFISA UHAMIAJI WAANZA KUNOLEWA KATIKA MAFUNZO YA WADAU KATIKA MNYORORO WA UTALII

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

CHUO KIKUU cha utalii kinachotoa huduma ya utalii, ukarimu na utafiti kimeandaa kozi fupi kwa wadau muhimu katika mnyororo wa utalii wakianza na maafisa uhamiaji ili kuweza kushirikiana katika kukuza sekta ya utalii ambapo Chuo hicho kilicho chini ya Wizara ya Utalii na Maliasili, sekta ya utalii ni moja kati ya sekta ambayo huiingizia kipato serikali.

Akizungumza na vyombo vya habari Ofisa Mtendaji Mkuu Chuo Kikuu cha Utali Shogo Sedoyeka ameeleza kuwa dhima ya kuandaa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na watalii milioni 2 ifikapo 2020.

Ameeleza kuwa nguvu za ziada zinahitajika ili kuweza kuyafikia malengo kwa kuwa sekta hiyo  mtambuka inashirikiana na sekta nyingi kama afya na miundombinu huduma ambazo watalii huhitaji wakiwa nchini.

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wadau muhimu kama vile maafisa uhamiaji, polisi na usafirishaji na wadau wengine ili kuweza kufikia malengo na wameanza na maafisa uhamiaji.

Kuhusu mafunzo hayo Shogo ameeleza kuwa yatahusu mada mbalimbali kama vile: huduma kwa wateja, mapokezi, mbinu za kushughulikia malalamiko ya wateja, muda katika utoaji wa huduma, mawasiliano na wateja na jinsi ya kuhudumia wateja wenye mahitaji maalumu.

Amewataka maafisa wahamiaji kuzingatia mafunzo hayo ambayo mbali na kuongeza kipato kwa taifa wataitangaza nchi na  kupata watalii wengi zaidi kutokana na huduma bora zitakazotolewa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka(kulia) akifungua mafunzo ya  kuwajengea uwezo kwa maafisa uhamiaji ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na watalii milioni 2 ifikapo 2020 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya maafisa uhamiaji wakisikiliza hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka alipokuwa anafungua mafunzo kwa maafisa hao kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam leo.
Mkufunzi Jesca William akitoa mafunzo kwa maafisa uhamiaji kuhusu umuhimu wa wageni pamoja na sifa za mtoa huduma wakati wa mafuzo yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam.
Mafunzo yakiendelea

WAZIRI MKUU ATETA NA BALOZI MBELWA KAIRUKI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa Tanzania nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki na amempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya tangu aende huko.

Amekutana na Balozi Kairuki leo Alhamisi, Julai 19, 2018 katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, na amemtaka Balozi huyo ahakikishe anaboresha mahusiano kati ya Tanzania na China.

“Ni lazima nikupongeze kwa namna unavyoendelea kufanya kazi na unavyojitahidi kudumisha mahusiano na China. Tunashukuru kwamba wageni wanaokuja hapa nchini kutoka China wanatoa taarifa nzuri na jinsi unavyosaidia kuitangaza nchi yetu huko nje.”

“Umefanya kazi nzuri ya kuwaelekeza wawekezaji wa huko kwamba wakati tunaunda Serikali na kutengeneza mfumo wa utawala, tuliamua kujenga kwanza mifumo imara na kutambua fursa zetu tulizonazo ili baadaye Watanzania waweze kunufaika na hizo fursa.”

Amesema kupitia utaratibu huo, Serikali ilitaka Watanzania wamiliki ardhi ndipo mgeni apate, na kama kuna uzalishaji wowote unafanyika basi Mtanzania awe wa kwanza kunufaika, Serikali inufaike na mwekezaji naye anufaike.

“Tunakushukuru kwamba umesaidia kuwaambia wachina watulie wakati Serikali ikirekebisha mifumo yake. Na wao wameyaona mabadiliko hayo, kwani tumesimamia vita dhidi ya rushwa, na wao walikuwa ni waathirika wakubwa, lakini pia tumeongeza uwajibikaji. Watu wetu sasa wanawajibika kwenye viwanda na makampuni yao na Watanzania kwa ujumla, wametambua umuhimu wa kufanya kazi ili waweze kuishi,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali hivi sasa iko kwenye programu ya kutangaza utalii uliopo nchini hasa kwa kuamua kuagiza ndege kubwa zitakazobeba watalii na kuwaleta moja kwa moja hapa nchini.

“Sasa hivi tumepata wageni maarufu kutoka nje ya nchi akiwemo Rais mstaafu wa Marekani, Mheshimiwa Barack Obama na wachezaji maarufu duniani, kwa hiyo tunaendelea na mikakati yetu ya kutangaza utalii huko nje.”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(kulia) akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam Julai 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam Julai 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MHAGAMA AITAKA NSSF KUIFIKIA SEKTA ISIYO RASMI NCHINI

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu akifafanua jambo wakati wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ( wa kwanza) akifuatilia kikao, wakati wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakifuatilia kikao wakati walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam.

……………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuwa na mkakati utakaoliwezesha Shirika hilo kuifikia sekta isiyo rasmi ili kuwezesha shirika hilo kupanua wigo wa hifadhi ya Jamii na kukusanya michango itakayowezesha shirika kulipa mafao kwa wakati na kufanya shughuli za uwekezaji nchini.

Akizungumza na wajumbe wa Bodi na menejimenti ya NSSF jana tarehe 18 Julai 2018, jijini Dar es Salaam, Mhe. Mhagama alifafanua kuwa sekta isiyo rasmi ni moja ya sekta ambayo haijafikiwa na hifadhi ya jamii kwa kiwango cha kuridhisha, hivyo NSSF haina budi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inafikiwa kwa kiwango kikubwa.

“Mfuko huu pamoja na mambo mengine umepewa jukumu la kusimamia sekta isiyo rasmi na katika sekta ambazo hazijafikiwa na hifadhi ya jamii kwa mujibu wa ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na sekta isiyo rasmi, hakikisheni mnaifikia sekta hiyo, hamuwezi kufanya uwekezaji katika miradi bila kuwa na wanachama wanaochangia mfuko ” Amesema Mhagama.

Katika mkutano huo, Mhe. Mhagama alimtambulisha Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii, Bw. William Erio, na kumtaka Mkurugenzi huyo kusimamia kwa weledi shuhghuli za uwekezaji zinazofanywa na NSSF nakuhakikisha mradi wa Mkulazi unafikia malengo na unazalisha sukari kama ilivyokusudiwa.Mhe. Mhagama amemtaka Mkurugenzi huyo kufikia maamuzi ya mwisho kuhusu mradi wa Dege na kufanya mapitio ya miradi yote na kuona hali halisi ilivyo na kufanya maamuzi stahiki na kuleta tija kwa wanachama na taifa.

‘’Mkurugenzi uendelea kulinda fedha za wanachama na kulipa mafao kwa wakati. lakini Bodi pamoja na menejimenti ya NSSF, mpeni ushirikiano Mkurugenzi huyu na fanyeni kazi kwa uadilifu na uzalendo ili kuweza kuhakikisha kuwa mfuko huu unakuwa na tija kwa wanachama na kujenga uchumi wa nchi” Amesema Mhagama.

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilianzishwa chini ya sheria Na. 28 ya mwaka 1997 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sura Na. 50 na Sheria ya pensheni kwa watumishi wa umma Na. 2 ya mwaka 2018.

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUFUKIA VIFUSI BARABARA YA HALTON

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akishiriki kusambaza kifusi kilichowekwa kwa ajili ya kufukia kifusi kwenye eneo la Halton Makorora ambalo mtaro wake ulikatika na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi hasa nyakati wa mvua.MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akishiriki kusambaza kifusi kilichowekwa kwa ajili ya kufukia kifusi kwenye eneo la Halton ambalo mtaro ulikatika na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi hasa nyakati wa mvua. Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku katika akiwa na Naibu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama CUF Taifa Masoud Omari kushoto wakifukia vifusi kwenye barabara ya Halton ili kuweza kuondoa kero ya wananchi kutokana na kuwepo kwa mtaro uliokatika

BILIONI MBILI KUWEZESHA WAHITIMU WA FANI ZA KILIMO SUA KUANZISHA MIRADI YA KILIMO BIASHARA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay akiongea katika hafla ya makubaliano na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo iliyofanyika chuoni hapo mjini Morogoro. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa makini halfa hiyo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda akitoa shukrani zake za pekee kwa Taasisi binafsi ya kusaidia Sekta ya kilimo nchini (PASS) jinsi walivyojitoa kuwasaidia wajasiliamali kujikwamua katika kilimo kibiashara ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa elimu.
Wageni pamoja na wakuu wa idara mbali mbali katika chuo kikuu cha SUA mjini Morogoro wakimsikiliza kwa makini makamu wa chuo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay (katikati waliokaa) na Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda (kwanza kushoto) wakiasaini mkataba wa makubaliano na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa PASS na Chuo Kikuu cha SUA.
Wakibadilishana mkataba wa makuabaliano.
Wakionyesha mkataba kwa furaha.
Picha ya pamoja baina yao.
Wakiagana kwa furaha mara baada ya tukio la makabidhiano kumalizika. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro. Taasisi binafsi ya kusaidia Sekta ya kilimo nchini (PASS) imetenga kiasi cha shilingi Bilioni mbili kwa ajili ya kuwawezesha Wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kuweza kuanzisha miradi ya Kilimo Biashara . Upatikanaji wa fedha hizo umelenga uanzishwaji wa miradi 100 ya majaribio katika Chuo hicho kupitia mpango wa Maalumu utoaji wa Mazoezi na Majaribio kupitia Vituo Maalum (Incubators) vyenye lengo la kutoa uzoefu kwa Wajasiliamali Vijana .

 Hatua hiyo imebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay baada ya kuingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo. “Baada ya kuona uwepo wa changamoto ya Wahitimu katika masuala ya kilimo pamoja na fani nyinginezo wakishindwa kushiriki katika shughuli za kilimo-biashara baada ya kukosa mitaji PASS kupitia Idara yake ya Agribusiness Innovation Center (AIC) imeona ije na mpango huu” Amesema mpango huo utawawezesha Wajasiliamali vijana kupata mitaji pamoja na nyenzo mbalimbali katika maeneo maalumu kwa lengo la kuwaandaa kuwa Wajasilimali watakao weza kumiliki Miradi ya Kilimo-Biashara. 

 Bwana Bohay amesema kipaumbele kitatolewa kwa Wajasiliamali Vijana watakaojihusisha na uzalishaji wa mbogamboga kwenye mahema (greenhouse), ufugaji wa samaki, Kuku, mbuzi, usindikaji na viwanda vidogo vya kuzalisha bidhaa zinazotokana na kilimo kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi. “Wenzetu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine (SUA) wametoa eneo la kutoshereza wa miradi ya Wajasiliamali Vijana kwa lengo la kuhakikisha vijana wetu wanapata mahali pa kuanzia kabla ya kujitegemea” alisema Bwana Bohay. 

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof, Raphael Chibunda amesema kuwa ushirikiano huo na Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo PASS umekuja wakati muafaka na kuwataka wahitimu pamoja na watafiti chuoni hapo kuchangamkia fursa hiyo. “ Kwetu sisi mradi huu wa kuwalea wahitimu wetu kwa kuwapatia mitaji, nyenzo na ushauri na maeneo maalumu ya kutekeleza kile walichokisoma darasani kwa vitendo ni faraja sana kwani siku zote tumekuwa tukiwaandaa vijana wetu waweze kukabiliana na changamoto za Maisha huko mtaani kwa kutumia elimu waliyoipa hapa chuoni” “Sasa tunawapa fursa hiyo hapahapa chuoni kabla hawajaingia huko mtaani……,wataondoka hapa wakiwa ni wajasiliamali mahili wa kilimo Biashara na mchango wao Kiuchumi kwa taifa na jamii utaongezeka sana. alisema Prof Chibunda . 

Mpango huu unatajwa kuwa suluhu ya changamoto ya ajira kwa Wahitimu hususani wa masuala ya Kilimo ambapo kwa vijana watakao pitia katika vituo maalumu vya uwezeshaji (Incubators) watakuwa na uwezo wa kujiajiri na kujiendeleza kiuchumi.

WAZIRI KIGWANGALLA AWAPA NOTISI YA SIKU 45 WALIOVAMIA PORI LA AKIBA KIJERESHI

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Kijereshi na Meneja wa pori hilo, Dianna Chambi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Alitoa siku 45 kwa wananchi wote waliovamia kingo/bafa za hifadhi hiyo kuondoka kwa hiari yao. Kulia ni Mkuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Serengeti, Johnson Msella.

Na Hamza Temba-Simiyu
.........................................................

*Atoa miezi mitatu kwa Muwekezaji kurudisha Serikalini hati miliki ya kipande cha ardhi kilichopo ndani ya Pori hilo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewapa siku 45 wananchi wanaoishi kinyume cha Sheria ndani ya kinga (bufer zone) za Pori la Akiba Kijereshi kuondoka kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu. 

Ametoa agizo hilo jana alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa ni muendelezo wa ziara zake mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.

Baada ya kushuhudia makazi na shughuli nyingine za kibinadam ndani ya pori hilo, Dk. Kigwangalla aliamua kutoa agizo hilo na kusema kuwa sheria za uhifadhi wa wanyamapori haziruhusu vitendo hivyo ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa kisheria pamoja na kingo zake (buffer zone) ambazo ni mita 500 kutoka kwenye mpaka halisi wa eneo la hifadhi.

"Mpaka itakapofika tarehe 31 mwezi ujao (Septemba) wananchi wote hawa wawe wameshaondoka eneo hili kwa hiari yao wenyewe, muwatangazie na mpime eneo hili vizuri muweke alama ili wajue ni wapi wanatakiwa kuondoka.

"Na ikifika tarehe 1 Septemba kama kuna watakaokuwa wamekaidi agizo hili, basi mfanye oparesheni maalum muwaondoe na msafishe kila kitu, ni lazima ifike mahali kila mmoja aheshimu sheria za nchi" alisema Dk. Kigwangalla kuuagiza uongozi wa pori hilo.

Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa muwekezaji wa hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp kurudisha kwa Kamishna wa Ardhi hati miliki ya kipande cha ardhi chenye ukubwa wa hecta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwakuwa ni batili.

Aimesema pori hilo lilianzishwa mwaka 1994 wakati muwekezaji huyo anadai kumilikishwa eneo hilo mwaka 1995 jambo ambalo haliwezekani mtu binafsi kupewa hati ya kumiliki eneo lililopo ndani ya eneo jingine tena hifadhi.

Aidha, amemtaka pia muwekezaji huyo kuheshimu sheria na taratibu za uwekezaji katika eneo hilo ikiwemo kulipa ada na tozo mbalimbali.
 
Pori la Akiba Kijereshi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 65.72 linasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na lilipandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba mwaka 1994 kwa Tangazo la Serikali Na. 215 la terehe 10 Juni, 1994 na hiyo ni kutokana na umuhimu wake kiuchumi na kiikolojia hususan katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Dianna Chambi (wa pili) kuhusu wananchi waliovamia hifadhi hiyo alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.  
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya pori ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua koki ya maji katika eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alipowasili mkoani humo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya eneo la kingo/bafa la Pori la Akiba Maswa ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli kilimo alipolitembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia kwake ni Mbunge wa Itilima, Njaru Silanga na Meneja wa Pori hilo, Lusajo Masinde.

WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE.

$
0
0
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amempa mwezi mmoja mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa kilometa mbili inayo unganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada -Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kukamilisha kazi hiyo hadi tarehe 31 Agosti mwaka huu ili kurahisisha mawasilino kwa wananchi wanao tumia daraja hilo.

Waziri Mhagama ameyasema hayo hapo jana tarehe 19 Julai 2018, alipotembelea katika daraja la Nyerere ili kukagua ujenzi wa barabara hiyo na uendeshaji wa shughuli katika daraja la Nyerere ambapo amesema serikali kutokamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kunasababisha kero kwa wananchi wanaovuka  kwa miguu na wanaovuka kwa kutumia vyombo vya usafiri kushindwa kupita kwa urahisi, hali inayochangia kupungua kwa mapato yanayokusanywa darajani hapo.(PAUSE-INSERT)

Kwa upande wao Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio na Mkandarasi wa barabara hiyo, Mhandisi Jamal Mruma wote kwa pamoja wamemuhakikishia Waziri Mhagama kutekeleza maagizo hayo kwa wakati ili kuondoa usumbufu uliopo kwa sasa katika daraja na kuweza kuongeza makusanyo ya mapatokatika daraja hilo.

Mbali na gaizo hilo la kukamilishwa kwa barabara , pia
Waziri Mhagama amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kuhakikisha unawekwa mfumo bora wa utambuzi wa vyombo vya usafiri vinavyovuka darajani hapo ili kujua gharama halisi ya tozo ya vyombo vinavyovuka na kuepuka upotevu wa mapato kutokana na kutokuwa 
na mfumo wenye kutambua tozo halisi kwa vyombo hivyo.

Daraja la kigamboni tangu lianze kufanya kazi mwezi Mei mwaka 2016
hadi mwezi Juni 2018, mpaka sasa limeingiza mapato ya takiribani shilingili bilioni 17.1 mapato hayo yanayotokana na tozo kwa vyombo vya usafiri vinavyopita katika daraja hilo.

Imetolewa na Afisa Uhusiano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF
Angella Msangi.

NEWZ ALERT:MKURUGENZI WA BRELA ATENGULIWA,KUPANGIWA KAZI NYINGINE

PROF MBARAWA AWATAKA MAKAMPUNI YA UCHIMBAJI VISIMA KUOMBA VIBALI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa ameyataka makampuni ya uchimbaji visima kuomba vibali ili waweze kuchimba visima hivyo pamoja na ulipaji wa kodi ya utumiaji wa maji.

Hayo yamesemwa na Waziri leo alipokagua visima vya kampuni ya Winners Traders iliyochimba visima katika Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.

Prof Mbarawa amesema kuwa jukumu la utoaji vibali la uchimbaji wa visima ni kutoka kwa Bonde la Wami Ruvu na ni lazima wakubaliwe kwa ajili ya kuendelea na shuguli zao za kuchimba wakiwa wamekamilika.

Amesema kuwa, makampuni mengi yamekuwa yanachimba visima bila kuwa na vibali na amewataka wamiliki wote kuanza kufuatilia vibali ili waweze kupewa haki ya uchimbaji ikiwemo na kulipa kodi ya kila mwaka kwa serikali.

"Awali katika Wilaya ya Temeke ukiwa unachimba kisima unatumia mita 40 unakuta maji ila sasa hivi unaweza kufika mita 90 ndio unakutana na maji hilo linatokana na uharibifu uliokuwa umefanywa na watu wasio waaminifu kuchimba pasipo kuwa na kibali kutoka kwa wahusika ambao ni Bonde la Wami Ruvu," amesema Prof Mbarawa.

Kwa upande Bonde la Wami Ruvu, Afisa Maji Wami Ruvu Simon Ngonyani amesema kuwa jukumu la utoaji vibali ni la kwao na utakapokuja kuomba lazima ulipie hicho kibali pamoja na ada ya kila mwaka, yapo makampuni waliyopewa na wengine hawajapewa tuliwakatalia ila wamekuwa wanaendelea kuchimba.

Ngonyani ametoa rai kuwa, wanawapa muda ili makampuni hayo yaende wenyewe kushughulikia vibali kwa wakati kabla hawajaanza kuwachukulia hatua kwani wamekuwa wanakwepa kulipa kodi kutokana na kuchimba visima kinyemela.

Prof Mbarawa amekuwa katika ziara maalumu ya kukagua miradi mbalimbali ya maji ikiwemo kwenye viwanda vinavyopata huduma za maji kutoka DAWASCO.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa anafuatilia namna Mtaalamu Usanifu Maabara wa Maji Ramadhan Zahoro wakati alipotembelea kisima kilichochimbwa katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiangalia moja ya Kisima kilichochimbwa katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kukagua kisima kilichopo Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kuzindua huduma mpya ya kliniki ya moyo inayotembea (Cardiac Mobile Clinic) kwa kufuata wagonjwa popote pale walipo na kuwahudumia. Huduma hii maalum inatarajiwa kuzinduliwa mkoani Ruvuma tarehe 23/7/2018.

Kuanzishwa kwa huduma hii kutasaidia wananchi wengi hasa wa mikoani ambako ni mbali na Taasisi yetu ilipo kufikiwa kwa urahisi zaidi na kupata huduma za matibabu ya moyo ya kibingwa.

Baada ya kufanyika kwa uzinduzi huo tutaendelea kutoa huduma kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 23-28/7/2018. Huduma hii ya kliniki inayotembea itakuwa endelevu katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Siku za karibuni tutatoa ratiba kamili kadri ya maombi yatakavyotufikia kutoka Tawala za Mikoa.

Huduma tutakazozitoa ni kutoa matibabu baada ya kufanya vipimo kwa kutumia mitambo mahususi tuliyokuwa nayo. Ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, elimu ya lishe bora, kutoa Rufaa ya moja kwa moja kwa wagonjwa watakaokutwa na matatizo ya Moyo kuja kwenye Taasisi yetu kwa uchunguzi wa tiba zaidi.

Dhumuni la Taasisi ni kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma bora na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo. Wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma pamoja na mikoa ya jirani tunawakaribisha mfike katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (Songea) ili muweze kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Makatibu Wakuu kuonesha uwezo wao wa kusakata kabumbu

$
0
0
Na Lorietha Laurence -WHUSM,Dodoma.

Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali wataonesha uwezo wao wa kusakata kabumbu siku ya Jumamosi ya tarehe 21 Julai 2018 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya Bonanza la michezo liloandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo.

Hayo yamesemwa leo Jijini hapa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Yusuph Singo ambapo ameeleza kuwa lengo la bonanza hilo ni kuhamasisha michezo kwa jaili ya afya pamoja na kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Makao Makuu ya nchi . 

“Katika bonanza hili mtashuhudia mechi kali itakayowahusisha Makatibu Wakuu wa Wizara zote za Serikali pamoja na Watumishi wa Umma wakichuana vikali” amesema Bw. Singo.Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa mbali na fainali hizo kutakuwa na michezo ya ufunguzi ambayo ni mazoezi ya kutembea (jogging) ambayo yataanzia viwanja vya Jamhuri , kupitia Nyerere Square kuelekea mzunguko wa CDA (Round About)na kuhitimishwa katika viwanja vya Jamhuri.

Anazidi kufafanua kuwa baada ya mazoezi ya kutembea yatafuata mazoezi ya viungo (Aerobic) na baadaye mechi za ufunguzi ambazo ni mpira wa pete kati ya Watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Habari, na baadaye kufuatiwa na Makatibu Wakuu dhidi ya Watumishi wote.

Mechi nyingine ni mpira wa miguu kati ya Wizara ya Habari dhidi ya Ofisi ya Rais Utumishi, Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Viwanda na Biashara , Kampuni ya Tigo na Kikundi cha Muungano na mwisho ni kati ya Makatibu Wakuu na Watumishi.Bw Singo ameeleza kuwa mbali na kuhamasisha michezo pia Bonanza hilo linaunga mkono kauli mbiu ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi kwa afya. 

Wananchi wa Dodoma wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia Bonanza hilo lililosheheni michezo mbalimbali itakayochezwa katika Bonanza hilo ikiwa ni kuamsha ari ya michezo kwa watumishi na wakazi wa Jiji la Dodoma.

HOSPITALI YA AMANA DAR YAKABIDHIWA VITANDA 10

$
0
0
HOSPITALI ya Amana jijini Dar es Salaam , imekabidhiwa vitanda 10 vya kujifungulia wanawake vyenye thamani ya Sh. milioni 14 kama msaada uliotolewa na ubalozi wa China.

Vitanda hivyo vilikabidhiwa jana kwa Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk.  Meshack Shimwera na Waziri wa Madini, Angella Kairuki baada ya kuomba msaada katika Ubalozi huo na kukabidhiwa vitanda 36.

Akizungumza wakati akikabidhi viwanda hivyo, Waziri Kairuki amesema vitanda vitano walikabidhi hospitali ya vijibweni, Temeke vitanda sita na Amana vitanda 10.Amesema pia wataendelea kuvigawa katika Kituo cha Afya Sinza na Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala lengo likiwa ni  kupunguza idadi ya wanawake wanaojifungulia chini au kwenye vitanda vya kawaida.

“Msaada huu ni katika kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini. "Leo nakabidhi vitanda 10 na nitajitahidi kuleta vitanda vingine ili kumaliza kabisa tatizo hili katika Mkoa wa Dar es Salaam  na kuhakikisha kila mwanamke anajifungua sehemu salama, " amesema Kairuki.

Naye Mganga Mkuu, Dk. Shimwera amesema vitanda hivyo vitafungwa kwenye wodi mpya ya kujifungulia wanawake na mahitaji yao yalikuwa ni vitanda 17.“Tunamshukuru Waziri Kairuki na ubalozi wa China, vitanda hivi tutavifunga kwenye wodi mpya hivyo vitasaidia akina mama wanaokuja kujifungua katika hospitali hii," amesema.

Pia amesena wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa magari ya kubebea wagonjwa baada ya waliyokuwa nayo saba kuyagawa kwenye vituo vya afya.Amesema kwa kuanzia wanahitaji magari matano ya kubebea wagonjwa pamoja na mashine ya CT-Scan na vifaa tiba kwenye chumba cha upasuaji na cha wagonjwa mahututi.

“Kutokana na kukosekana kwa mashine ya CT-Scan tunalazimika kupeleka wagonjwa 3,000 katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila lakini kama tungekuwa nazo tungeweza kuwatibu wenyewe," amesema Dk. Shimwera.
Waziri wa Madini,Angella Kairuki akimkabidhi Mganga mkuu wa hospital Amana,Dkt Meshack Shimwela vitanda 10 jijini Dar as Salaam. Picha na Emmanuel Massaka wa MMG.
Waziri wa Madini,Angella Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM)

NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO

$
0
0
Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdalla Hamisi Ullega amefanya ziara mkoani Kilimanjiro kwa kutembele jumla ya viwanda vya ngozi vitatu na wadau wengine wa sekta ya mifugo.

Katika ziara hiyo Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Himo Tanners & Planters LTD Waiso amemweleza Naibu Waziri kuwa changamoto iliyopo kwa sasa katika kiwanda hicho ni pamoja na tozo nyingi zisizo na tija ambazo zinatozwa kuanzia Serikali ya kijiji mpaka Serikali Kuu. 

"Tozo zimekuwa nyingi mno katika Viwanda,ambapo inafikia wakati kiwanda kinashindwa kujiendesha kwa Ufanisi kwa sababu ya Muda na gharama za kufuatilia tozo hizo katika mamlaka husika,"amesema Waiso.

Aidha Waiso ametaja baadhi ya tozo hizo kuwa ni pamoja na Service Levy,Export Permit,Business Licence,Water use fee,Water right fee na Chemical Permit fee. 

Pia Ulega alipata fursa ya kutembele kituo cha Utafiti wa Mifugo, West Kilimanjaro (TALIRI), kiwanda cha kusindika ngozi cha Moshi Leather industries limited,Shamba la mifugo Kafoi,Watengenezaji wa chakula cha Mifugo, Marenga Millers Company LTD na kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Shamba la Kuzalisha Kuku wazazi la The Irvines Group katika Halmashauri ya Siha.

Pia Shamba la Irvines hapa Tanzania ambalo lipo katika Halmashauri ya Siha,Pwani na Dar es salaam.Mpaka sasa Irvines hapa Tanzania kwa mwaka inatotolesha vifaranga milioni 13 na kama soko litaruhusu shamba hilo linauwezo wa kutotolesha Vifaranga zaidi milioni 25 kwa mwaka

Naibu Waziri ameelezwa Shamba la Irvines Group linazalisha na kutotolesha vifaranga milioni 77 vya kuku wa nyama na mayai katika nchi za Botswana,Zimbabwe na Msumbiji.

Ulega akifanya majumuisho ya ziara yake katika Halmashauri ya Siha amezungumza na waafugaji ambapo amesema kuwa viwanda karibu vyote vya ngozi vinafanya kazi nzuri isipokuwa kuna changamoto ndogondogo ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi. 

Awali Ulega akizungumza na wafugaji wa Halmashauri ya Siha amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inawajali wafugaji wake kwani tayari kwa kupitia taasisi yake ya NARCO ipo katika mpango wa kuligawa kiasi cha kekta 700 eneo la NARCO ili liwekewe mpango bora wa matumizi.

Ameongeza lengo wakati wa kiangazi wafugaji waweze kupata malisho ya mifugo yao katika eneo hilo na kuchangia kiasi kidogo cha fedha ili kuweza kuimarisha miundombinu ya eneo husika. "Serikali haiwezi kuvumilia kuona Mifugo inakufa kwa kukosa malisho wakati maeneo ya kulishia yapo,ndio maana ikaamua kuja na huu mpango ili kuokoa Rasilimali hii ya Taifa isipotee,"amesemaUlega.

Ulega amesisitiza tena kwa kusema"Wafugaji lazima tukubali sasa kufuga kisasa,kwasababu ardhi haiongezeki,isipokuwa mifugo inaongezeka na watu wanazidi kuongezeka."Hivyo hatuna budi kuwa na Mifugo michache lakini itakayotuletea tija," amesema.

Ulega amesema ili kufikia Tanzania ya viwanda,tunahitaji mifugo iliyonenepeshwa vizuri ili kupata nyama bora na soko la uhakika.

Naibu Waziri Ulega amewaonya wafugaji hao kuwa mpango huo wa NARCO ukikamilika wa kuwakodisha maeneo ya kulishia Mifugo yao wakati wa kiangazi (ukame) Mfugaji yeyote atakayegundulika kuruhusu mifugo kutoka nchi jirani na kuingia nchini na kulisha malisho hayo,Serikali haita sita kusitisha mara Mpango huo.
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (wapili kulia) akiwa ameambatana na Mmiliki wa kiwanda cha ngozi Himo Tanners & Planters LTD , akipewa maelezo namna viatu vinavyotegenezwa kwa ngozi katika kiwanda hicho kilichopo mkoa wa Kilimanjaro.
Wanachi wa kijiji cha Lekirumuni wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifungo Mhe.Abdallah Ulega katika mkutano uliofanyika kata ya Ndinyika wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega (kijani) akitembelea Shamba la mifugo la Serikali (NARCO)
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mmiliki wa kiwanda cha ngozi  Himo Tanners & Planters LTD   akikagua ngozi kiwandani katika kiwanda hicho kilichopo mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na  wananchi katika mkutano uliofanyika cha kijiji cha Lekirumuni kata ya Ndinyika  wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

NAIBU WAZIRI WA AFYA AIPONGEZA AGPAHI KWA KUIMARISHA HUDUMA ZA TIBA NA MATUNZO KWA WATU WANAOISHI NA VVU

$
0
0

Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akikabidhi Televisheni kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile kwa ajili ya klabu ya watoto katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
***
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile ameipongeza asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa kuimarisha huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU mkoani Mara. 
Dkt. Ndugulile alitoa pongezi hizo Julai 19,2018 wakati akiwa katika katika ziara ya kikazi mkoani Mara na kushuhudia kazi zinazofanywa na AGPAHI katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara katika kuhudumia watu wanaoishi na VVU ambapo pia alipokea vifaa vya michezo vilivyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya klabu ya watoto iliyopo katika hospitali hiyo. 
"Nimekuja kupata ushuhuda wa kazi kubwa ambayo wadau wetu wa maendeleo AGPAHI katika kudhibiti maambukizi ya Ukimwi,niwashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa mnayofanya kwa kushirikiana na serikali katika kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI, na tunawashukuru kwa misaada mbalimbali mnayotupatia”,alisema Dkt. Ndugulile. 
"Serikali inafarijika sana kuona wadau wanakuwa na mchango mkubwa katika kudhibiti UKIMWI, kama wadau wa maendeleo tunatarajia wataziba mapengo pale serikali haijafika kinachotakiwa ni kushirikiana, tunataka NGO's zote zinazofanya kazi katika mkoa wa Mara ziendane na vipaumbele vya mkoa”,aliongeza. 
Aidha Dkt. Ndugulile alisema serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 asilimia 90% ya watu wenye maambukizi ya VVU wanafikiwa na kupimwa,ambapo asilimia 90% ya walioathirika wanapewa dawa za kufubaza virusi na asilimia 90% ya watakaotumia dawa hizo hawataweza kuwaambukiza watu wengine kwa sababu virusi vitakuwa vimefubazwa na tiba hiyo. 
“Mpaka sasa tumewafikia Watanzania takribani milioni 1.4 wanaohisiwa kuwa wanaishi na VVU, bado tunapambana kuwafikia laki nne ambao hatujawafikia, lakini sambamba na hayo tunaendelea kupambana kuhakikisha maambukizi mapya tunayadhibiti kwa kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kudhibiti maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto”,alisema. 
Alisema serikali itaendelea kuhakikisha kuwa dawa za kufubaza makali ya VVU zinaendelea kupatikana kwa asilimia 100 huku akiwasisitiza wanaume kujitokeza kupima afya zao ili kubaini kama wana maambukizi ya VVU na wakibainika wameambukizwa basi waanze kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU. 
Akitoa taarifa ya kazi zinazofanywa na AGPAHI, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa alisema katika mkoa wa Mara,wanatoa huduma katika vituo 113 vya kutolea huduma za afya,68 vya huduma ya matunzo na matibabu kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) na vingine 45 vya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). 
“Tunatekeleza mradi wa Boresha kwa ufadhili wa serikali ya Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control (CDC),ambapo mradi huu unatoa huduma za kinga,tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU”,alisema. 
Dkt. Sekela alibainisha kuwa kuanzia mwezi Oktoba 2017 hadi Machi 2018,AGPAHI imefanikiwa kupima watu 162,389 ambapo kati yao 4,482 sawa na asilimia 2.7 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU wakiwemo watoto 265.
“Katika kipindi hicho pia watoto 988 walizaliwa na akina mama wenye VVU lakini kutokana na huduma za kukinga watoto dhidi ya maambukizi kutoka kwa mama, watoto 934 sawa na 98% hawakuwa na maambukizi, na 16 waliopata maambukizi wanaendelea kupata huduma za VVU”,alieleza Dkt. Sekela. 
“AGPAHI ilipoanza kutekeleza mradi wa Boresha hapa Mara Oktoba 2016 kulikuwa na watu 25,821 wanaopata huduma za VVU na UKIMWI,lakini kwa kushirikiana na serikali tumeweza kuwafikia watu 31,729 ‘wanaume 9,202 (29%),wanawake 22,527 na watoto 1,664,tunaendelea na upimaji hasa tukilenga kuwatambua wanaume wenye maambukizi ili waanze kupata huduma hizi muhimu”,alifafanua Dkt. Sekela. 
Aidha aliongeza kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na upungufu wa wafanya kazi kwa kada ya afya,AGPAHI imewezesha ajira kwa watumishi wapatao 201 kati yao 118 ni makarani takwimu na 83 ni maafisa tabibu,wataalam wa maabara na wauguzi. 
Dkt. Sekela alisema mbali na kuwajengea uwezo Washauri wa Watu Wanaoishi na VVU 123 na kuanzisha vikundi vya WAVIU pia AGPAHI inaendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vifaa vya michezo,televisheni na kutengeneza vifaa vya michezo. 
“Kupitia mradi wa Boresha AGPAHI imetoa kompyuta 86 kwa ajili ya kurahisisha mfumo wa takwimu katika halmashauri zote za mkoa wa Mara,tumetoa Cryotherapy mashines kwa ajili ya matibabu ya dalili za mwanzo za saratani ya mlango wa kizazi,solar panels kwenye vituo vya afya,kuboresha vituo vya afya,majokofu ya kutunzia dawa,darubini na vitu mbalimbali”,aliongeza. 
Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) ni asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali iliyoanza kushirikiana na serikali ya Tanzania katika juhudi za kutokomeza VVU na UKIMWI kwa watoto tangu 2011 katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu kisha Mwanza,Geita,Mara na Tanga kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC). 

Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati wakielekea katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya kushuhudia kazi zinazofanywa na AGPAHI katika kuimarisha huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU.Kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mara, Alio Hussein.- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akielekea katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara,Dkt. Joachim Eyembe akitoa taarifa kuhusu huduma za afya katika hospitali hiyo kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara na kuupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuimarisha huduma za afya na kupunguza malalamiko kutoka kwa wagonjwa.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akitoa taarifa ya kazi zinazofanywa na AGPAHI katika kuimarisha huduma za tiba za matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI mkoani Mara. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Manyinyi Mathayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akifafanua kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na AGPAHI mkoani Mara.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akiwasisitiza viongozi wa serikali kuendelea kushirikiana na AGPAHI katika kudhibiti maambukizi ya VVU.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akiishukuru serikali kwa kuwapa fursa ya kuwatumikia Watanzania kuleta mabadiliko chanya kwenye masuala ya afya hasa UKIMWI.
Vifaa vilivyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya klabu ya watoto na vijana wa kituo cha tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.Vifaa hivyo ni televisheni,mipira,mikeka,viti na vitabu.
Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile,Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Manyinyi Mathayo,Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara,Dkt. Joachim Eyembe na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Anney wakiangalia vifaa vilivyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya klabu ya watoto na vijana katika kituo cha tiba na matunzo cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akielezea kuhusu vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na vifaa vya michezo.Alisema mbali na kutoa vifaa vya michezo pia wameboresha viwanja vya michezo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akikabidhi Televisheni kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile kwa ajili ya klabu ya watoto katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akikabidhi Televisheni kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile kwa ajili ya klabu ya watoto katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi televisheni kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara,Dkt. Joachim Eyembe kwa ajili ya klabu ya watoto katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi vitabu kwa mmoja wa vijana kutoka klabu ya vijana katika CTC ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kijana akiishukuru AGPAHI kwa kuwapatia vifaa vya michezo.
Vijana kutoka CTC ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara wakionesha igizo linalotoa elimu kuhusu umuhimu wa kuwa wafuasi wazuri wa dawa za kufubaza makali ya VVU.
Wafanyakazi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara wakifuatilia igizo.
Mshauri wa Watu Wanaoishi na VVU Nehemia Kaswala Mtumi anayeishi na maambukizi ya VVU tangu mwaka 1995 na mke mmoja na watoto watano wote hawana maambukizi ya VVU akielezea namna wanavyoshirikiana na AGPAHI na serikali katika kuhamasisha masuala ya afya kwa watu wanaoishi na VVU,uzazi wa mpango,TB na uchunguzi wa saratani ya shingo ya mlango wa kizazi,upimaji wa VVU nyumba kwa nyumba na uundaji wa vikundi vya WAVIU.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akiandika dondoo muhimu wakati Mshauri wa Watu Wanaoishi na VVU Nehemia Kaswala Mtumi akitoa salamu za WAVIU Washauri kutoka hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Anney akimweleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakifurahia jambo.
Mshauri wa Watu Wanaoishi na VVU Nehemia Kaswala Mtumi akikabidhi taarifa yake kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Kijana akisoma risala kuhusu klabu ya watoto kutoka Kituo cha tiba na Matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.Alisema tangu AGPAHI ianze kufadhili klabu hiyo mwaka 2017 wamefanikiwa kuongeza uelewa kuhusu VVU,UKIMWI, lishe bora,umuhimu wa mazoezi na ufuasi mzuri wa dawa. Aidha aliitaka serikali na wadau kuielimisha jamii kuacha unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU kwani wanahitaji upendo badala ya unyanyapaa.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza kwenye kituo cha tiba na matunzo (CTC) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara. Aliwataka watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kuwa wafuasi wazuri wa dawa na wale ambao ambao hajapima afya hususani wanaume kujitokeza kupima ili wajue hali ya afya zao.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile pia aliitaka jamii kuacha tabia ya kunyanyapaa watu waliopata maambukizi ya VVU na kusisitiza kuwa dawa za kufubaza makali ya VVU zipo za kutosha.
Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Francis Mwanisi akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile. 
Vijana kutoka CTC ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara wakicheza mchezo wa kuchangamsha akili na mwili 'Chicken Dance'. 
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akicheza na watoto mchezo wa kuchangamsha akili na mwili 'Chicken Dance'. 
Mchezo wa kuchangamsha akili na mwili 'Chicken Dance' ukiendelea. 
Wafanyakazi wa AGPAHI wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

VIONGOZI MBALIMBALI WAMIMINIKA MSIBA WA BABA YAKE MZAZI SALMA KIKWETE JIJINI DAR.

$
0
0
Rais Mstaafu awamu ya nne,Mh Dkt Jakaya Kikwete akimpokea Rais Mstaafu awamu ya pili Mh.Alhaji Al-Hassan Mwinyi wakati wakiwasili Msasani kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar. 
Rais Mstaafu awamu ya nne,Mh Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa aliyeambatana na Mkewe Marry Majaliwa wakati wakiwasili Msasani kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar 
Rais Mstaafu awamu ya nne,Mh Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Mh Pinda,kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar 
Mawaziri Wakuu wa zamani Mh Edward Lowassa na Mizengo Pinda wakisalimiana msibani
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mh Bernad Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu kiongozi Mstaafu,Ombeni Sefue kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar
Mama Maria Nyerere akiwa Wasaidizi wake wakiwasili kwenye kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar
Waziri Mkuu wa Zamani,Mh Edward Lowassa akizungumza jambo na Katibu Mkuu kiongozi Mstaafu,Ombeni Sefue kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar.

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AWAPONGEZA WAKALA WA BARABARA-TARURA

$
0
0
Na ShaniAmanzi,

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Saimon Odunga amewapongeza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kwa kufanya kazi nzuri ya kuboresha barabara za Halmashauri ya Wilaya Chemba.

Mhe.Saimon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anakagua barabara ya Chemba –Ombiri –Soya na kukutana na Wakandarasi waliopewa Mradi wa Ujenzi wa Barabara hiyo na Wakala wa Barabara (TARURA) Wilaya ya Chemba ,tarehe 18/7/2018.

Mhe.Saimon Odunga pia amewataka Wakandarasi wa barabara kuweka vibao vya kuonyesha tani pamoja na Vibao vinavyo kataza Mifugo kupita kwenye barabara kwa ajili ya kuzuia uharibifu wa barabara ili iwe rahisi kwa wale ambao wanapitisha kinyume vibao vya barabara walipe faini.

Mhe.Saimon Odunga amesema “ni vyema miradi mbalimbali ya kimaendeleo jamii ishirikishwe ili waweze kuwasaidia katika kutunza miundombinu ya ujenzi na pale wanapokwama inakuwarahisi kwao kuwasaidia ikiwemo kutoa vijana wao katika kusaidia miradi hiyo kwenda kwa haraka pamoja na Wakandarasi wanapaswa kuzingatia Mikataba wanayopewa ikiwemo kumaliza kazi kwa wakati.”

Aidha Mhe.Odunga aliongeza kwa kusema barabara ya Chemba –Donsee Mkandarasi wanapaswa kusambaza kifusi kwa haraka ili kuepuka ajali kwa mabasi makubwa yanayopita na pia kwa matumizi ya kawaida ya barabara na kuipongeza TARURA kwa kufanya kazi nzuri kwa kupanua barabara na kujenga kwa ubora hivyo kusaidia Wilaya ya Chemba kukua kwa kasi.

Naye Meneja wa TARURA Mhandisi.Mathias Makaju ameshukuru Viongozi kuendelea kukemea uharibifu wa mazingira unaoadhiri miundombinu ya barabara na pia kuwa nao sambamba katika miradi mbalimbali ya barabara wanazotekeleza TARURA.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Saimon Odunga pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba Mhe. Rajabu
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images