Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

Mshindi wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 kuchachangia milioni mbili ujenzi wa kituo cha Polisi Mbagala,Temeke.

0
0
 Katibu Tawala wilaya ya Temeke Ndugu Hashimu Komba (kwa niaba ya MKuu wa Wilaya),akimkabidhi Kombe la Tatu Mzuka kwa kijana mkazi wa Mbagala,Abeid Amir aliyejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 300,alipokwenda kutambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.Katika mazungumzo yake na Uongozi wa Wilaya mshindi huyo ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi kinachojengwa Mbagala.
 Mshindi wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 Abeid Amir akipokelewa kwa shangwe,nderemo na vifijo  mara baada ya kuwasili nyumbani kwao Mbagala-Kilungule,ambapo pia alipokelewa vyema na viongozi wa serikali ya Mtaa kwa heshima kubwa.
  Mshindi wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 Abeid Amir akipokelewa kwa shangwe na Diwani wa Kata ya Kilungule Said Fella na akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kata ya Zomboko Ndugu Hemed Said Njiwa,mara alipowasili nyumbani kwao Mbagala-Kilungule
Diwani wa Kata ya Kilungule Said Fella akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kumpokea mshindi huyo wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018.

WAGONJWA 300 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MACHO WILAYANI MUHEZA

0
0

 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo waliofanyiwa uchunguzi wa  matatizo ya macho  wakati wa zoezi la kufunga kambi ya matibabu ya tiba ya macho iliyoendeshwa na Taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Medewell Health Centre kwenye kituo cha Afya cha Ubwari wilayani Muheza
 Mkurugenzi wa wa taasisi ya Medewell Munir Meral akizungumza katika ufungaji wa kambi hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri akizungumza katika ufungaji huo

 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiingia kwenye Kituo cha Afya Ubwari kufunga kambi ya Macho iliyokuwa ikiendelea kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Julius Mgeni
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akifuatilia matukio mbalimbali
MKUU wa wilaya ya Muheza akiteta jambo
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akiagana nao
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimsikiliza mkazi wa wilaya ya Muheza akitoa ushuhuda wa kupona macho yake baada ya kupata matibabu
 Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga waliopatiwa matibabu ya macho


ZAIDI ya wagonjwa 300 wamefanyiwa uchunguzi wa matatizo ya macho wilayani Muheza mkoani Tanga kwenye zoezi lililoendeshwa na wataalamu kutoka Hospitali ya Medewell iliyopo wilayani ya Kibaha mkoani Pwani huku 121 wakibainika kuwa na tatizo la mtoto wa jicho.

Hayo yalibainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Julius Mgeni wakati wa zoezi la kufunga kambi ya matibabu ya tiba ya macho iliyoendeshwa na Taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Medewell Health Centre kwenye kituo cha Afya cha Ubwari wilayani Muheza

Alisema wataalaamu hao wamekuwa wakiendesha zoezi hilo mara kwa mara ambalo limekuwa na mafanikio makubwa kwa wagonjwa kupona na kuweza kuona na hivyo kupunguza idadi ya watu wenye changamoto za namna hiyo.

Alisema licha ya kufanyiwa uchunguzi lakini wagonjwa 121 walibainika kuwa na tatizo la mtoto wa jicho ambao waliweza kufanyiwa upasuaji na kupewa dawa ambazo wanapaswa kuzitumia wakati wa matibabu hayo huku watu 191 wakipatiwa matibabu ya kawaida.

Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema zoezi la uchunguzi na operesheni ambazo zimekuwa zikifanyika vimekuwa na mafanikio makubwa jambo ambalo limeongeza mwamko wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ambao wanajitokeza kila wakati.

“Kwa kweli niwapongeze Medewell kwa kuendesha matibabu haya ya mtoto wa Jicho nay a kawaida kwani yamekuwa faraja kubwa sana na faida yake imeweza kuonekana na kuwasaidia watu kuona kuweza kurudi kwenye hali zao za kawaida”Alisema.

Alisema hatua hiyo imewawezesha watu kuweza kuona jambo ambalo litawasaidia wananchi wengi waliokumbwa na tatizo hilo kuweza kufanya shughuli za uzalishaji mali ikiwemo zile za kujiingizia kipato na hivyo kusaidia kuinua uchumi wao na jamii zinazowazunguka.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa wa taasisi ya Medewell Munir Meral alisema wananchi wamefarijika kwa kiasi kikubwa kutokana na baadhi yao kukata tamaa kutokana na uwepo wa matatizo hayo ambayo kiuhalisia yana gharama kukabiliana nayo.

Alisema mbali ya kutoa msaada wa matatibabu hayo bure lakini pia kwa kushirikiana na Betacharitable Trust toka Uingereza wamekabidhi kifaa cha kupima na kuchunhuza matatizo ya macho(slit lamp)yenye thamani ya zaidi Shilingi Milioni kumi na vifaa vya kupimia miwani (tria set).

Alisema utolewaji wa vifaa hivyo utarahisisha kituo hicho cha afya kuweza kuanza kufanya uchunguzi wa matatizo ya macho kupitia wataalamu waliopo jambo ambalo lilikuwa likishindikana kufanyika kutokana na uhaba wa vifaa hivyo tiba.

FAHAMU KUHUSU HIFADHI YA MSITU WA ASILI,AMANI.

0
0

DKT. NDUGULILE AHIDI KUZIWAJIBISHA MAMLAKA HUSIKA ENDAPO KITUO CHA AFYA KITAFUNGIWA.

0
0
Na WAMJW-Mwanza

NAIBU Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa hatosita kuziwajibisha mamlaka husika endapo kituo chá kutolea Huduma za Afya kitafungwa kutokana na uzembe wa aina yoyote.

Amesema hayo wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na kutoa vyeti na ngao kwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika utoaji wa huduma za afya  jijini Mwanza.

"Na Bahati nzuri tunapopita tunawapa na maelekezo ya nini cha kufanya, tukishakamilisha hili zoezi letu lá kuweka mifumo ya usajili , ithibati, na utoaji wa leseni tutaanza kufungua visivyokidhi vigezo, Sasa tutapofungia kituo chá Afya Mamlaka husika,  iwe ni Ras, Mganga mkuu wa mkoa au wa Wilaya, Mkurugenzi utawajibika, Vingine ni uzembe wa baadhi ya mamlaka kutosimamia vizuri majukumu yake"Alisema Dkt Ndugulile.

Aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuweka mikakati thabiti katika kuboresha hali ya utoaji huduma za Afya nchini ili wananchi wanufaike zaidi na hali hiyo.

"Tunaongeza rasilimali watu, tumeajiri watumishi  wapya 8000 katika sekta ya Áfya,  ambapo na ninyi mtapata,  pia Vituo vyote tutavisajili, kiwe cha umma au chá binafsi, kitu chá pili tutaweka ithibati kama usipofikisha kigezo katika ngazi husika tutakushusha kigezo unaenda kuanza hatua upya" Alisema Dkt Ndugulile

Aidha, Dkt.  Ndugulile alimtaka Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa kuyasimamia vizuri ili kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa Ubora unaostahili kwa wananchi .

Nae Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa alisema kuwa Mkoa unatarajia kuanza uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya hususani eneo lá uzazi na Mtoto kupitia mradi wa kuimarisha huduma ya afya ya uzazi ya mama na mtoto"Improving access to maternal and Newborn health (IMPACT)  unaotekelezwa na Aga Khan Development Network  (AKDN)  chini ya Ufadhili wa Serikali ya Canadá pamoja na Agriteam kupitia mradi wa Mama na Mtoto ambapo zaidi ya Bilioni 2.8 zinatarajiwa kutolewa na kutumika katika vituo 30

Dkt. Thomas Rutachunzibwa aliendelea kusema kuwa mkoa wa Mwanza Unaendelea kuimarishwa ambapo madirisha maalum 35 yameanzishwa katika hospitali zote 7 za Serikali, vituo vya Áfya 11 na Zahanati 17 ili kuhakikisha wazee wanapata huduma kwa haraka na Ubora unaotakiwa, jumla ya wazee 43,046 wamepatiwa vitambulisho na mabaraza ya wazee 172 yameundwa .
 Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile (katikati) akikagua chumba chá Dawa katika hospitali ya kanda ya Bugando pindi alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza.
 Mwakilishi kutoka Zahanati ya Ihayabuyaga iliyo katika Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) baada ya kushinda nafasi ya tatu katika kutoa huduma bora za Afya.
 Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile  akiongea na wagonjwa waliokuwa wakisubili matibabu katika chumba chá kupumzikia wakati alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya kanda ya Bugando.
 Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua incubator katika Zahanati ya Nyamizeze wakati alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza.

TAMUFO YAIONYA REDIO HABARI MAALUMU YA JIJINI ARUSHA

0
0

Kushoto ni Mkurugenzi wa Redio Habari Maalumu, akijitetea mbele ya viongozi wa TAMUFO.
Viongozi wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Kwaya mbalimbali na Uongozi wa Redio Habari Maalumu wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya matumizi ya kazi zao. Kulia ni Rais wa TAMUFO, Dk.Kisanga na nyuma yake ni Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel.
Mwenyekiti wa Kwaya za Ulyankulu aliyeshika faili akieleza jinsi nyimbo zao zinavyotumika mitandaoni pasipo kunufaika nazo.
Picha ya pamoja baada ya mkutano huo. Wa tatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel na wa pili ni Mkurugenzi wa Redio Habari Maalumu.
Viongozi wa TAMUFO, Dk.Donald Kisanga na Katibu wake, Stellah Joel, studio ya Arusha One Redio kuhakikisha wanamuziki wa Kanda ya Kaskazini wanapata elimu ya kunufaika na kazi zao za sanaa kwani TAMUFO ni mkombozi wa wasanii


Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umetoa onyo kali kwa Redio Habari Maalumu

Kuhakikisha haisambazi nyimbo za wasanii bila kufuata utaratibu halali.

Onyo hilo limetolewa na Rais wa TAMUFO Dk. Donald Kisanga katika mkutano uliowakutanisha TAMUFO na vionozi wa redio hiyo pamoja na wadau wengine.

"Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Kwaya kongwe hapa nchini kuhusu kazi zao kutumiwa na redio hilo bila faida tuliamua kufanya ziara ya kikazi jijini Arusha kwa ajili yakuja kuyatafutia ufumbuzi malalamiko hayo na kuongea na wahusika" alisema Kisanga.

Kisanga alizitaja kwaya zilizotoa malalamiko kuwa ni Ulyankulu Mapigano na Ulyankulu Barabara ya 13 zote za Tabora na Kwaya Kuu Habari Njema Kwaya ya Uinjilist za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mjini kati zote za Mkoani Arusha.

Alisema TAMUFO baada ya kupokea malalamiko hayo iliweza kuwakutanisha Vikundi hivyo vya kwaya Pamoja na redio hiyo na kumaliza mgogoro huo ambapo walifikia muafaka kwa makubaliano kwa Kwaya husika iliitaka redio hiyo iwalipe gharama za usumbufu.Baada ya Makubaliano hayo Dk. Kisanga aliwaonya Redio Habari Maalum kuacha mara moja kuendelea kuuza kazi za Wanakwaya pasipo kuwa na mkataba.

Viongozi wa TAMUFO bado wapo katika ziara ya kikazi mikoa ya Kanda ya Kaskazini kukutana na wadau wa muziki wa injili ili kujua changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.

UTEKELEZAJI WA RBF WILAYANI URAMBO WAMVUTIA WAZIRI WA AFYA

0
0
 
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kulia akikata utepe kuashiria kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya wazazi lilitokana na mpango wa malipo kwa ufanisi katika Zahanati ya Itebulanda wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo,wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Bi. Magreth Sitta.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikakati akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kitabu cha mpango wa malipo kwa ufanisi katika Zahanati ya Vumilia Wilayani Urambo Mkoa wa Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo,.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikakati akionesha kitabu cha mpango wa malipo kwa ufanisi pamoja na watumishi wengine wa sekta ya afya  katika vituo vya fya mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika  katika Zahanati ya Vumilia Wilayani Urambo Mkoa wa Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo wa tatu kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi. Angelina Kwinga,.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akifunua pazia kuashiria  kuashiria kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la upasuaji katika Zahanati ya Uyogo wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Bi. Magreth Sitta.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea maeneo ya Zahanati ya Uyogo wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo.PICHA NA WIZARA YA AFYA.


 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi. Angelina Kwinga kushoto kitabu cha muongozo wa mpango wa malipo kwa ufanisi  mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika  katika Zahanati ya Vumilia Wilayani Urambo Mkoa wa Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo.



NA TIGANYA VINCENT,TABORA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameipongeza Wilaya ya Urambo kwa utekelezaji mzuri wa mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) ambao umesaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Alisema baadhi ya Zahanati , Vituo vya Afya  na Hospitali ya Wilaya ya Urambo imetumia fedha kwa ajili ya upanuzi wa baadhi ya majengo na uboreshaji wa miundo mbinu jambo ambalo limewasaidia wananchi kupata huduma nzuri , bora na katika mazingira yanayovutia.

Pongezi hizo zilitolewa jana wakati akiwa katika ziara Wilayani Urambo kutembelea Hospitali ya Wilaya, Kituo cha Afya cha Ussoke , Zahanati ya Itelebulanda,  Vumilia na zahanati ya  Uyogo ili  kujionea utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na matumizi ya fedha hizo zilivyotumika kujenga majengo mbalimbali ikiwemo Wodi za Wakinamama , vyumba vya upasuaji na nyumba za waganga.

Akiwa katika Zahanati ya Itelebulanda , Mhe. Ummy aliwapongeza kwa kuweza kutumia fedha za RBF kujenga Wodi nzuri kwa ajili ya wanawake na kuahidi Wizara kuwapatia shilingi milioni 20 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu zaidi.

Alisema kazi nzuri ilifanyika imeiwezesha Zahanati hiyo kupanda kutoka Nyota moja hadi kufikia nyota tatu kwa utoaji wa huduma bora jambo ambalo ni zuri na kuwataka watumishi wake kuongeza juhudi zaidi.

Kwa upande wa Zahanati ya Uyogo alipongeza jinsi walivyotumia fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa jengo la huduma ya baba, mama  na mtoto, huduma ya chanjo, uzazi wa mpango, ujenzi wa choo cha watumishi na ukarabati wa nyumba za watumishi.

Alisema kuwa kutokana na Zahanati hiyo kuwa mbalimbali kutoka Hospitali ya Wilaya na kwa sababu inahudumia wananchi wengi aliahidi kuwapatia gari jipya la kubeba wagonjwa ifikapo Desemba mwaka huu.

Akiwa katika Zahanati ya Vumilia aliweza kuchangia mifuko 100 ya saruji baada ya kuona kazi nzuri ambayo imewawezesha kupanda kutoka Nyota sifuri hadi tatu kutoka na matumizi mazuri ya fedha za RBF ambazo zimewawezesha kutoa huduma nzuri ya afya kwa wakazi wa eneo hilo.

Alisema kuwa ukarabati katika jengo la wagonjwa wa nje(OPD), ukarabati wa eneo la kutupa taka , ukarabari wa vyoo vya wagonjwa na watumishi na ujenzi wa vibao vya kuelekeza wagonjwa.

Katika kituo cha Afya cha Ussoke wameweza kutumia fedha hizo za RBF kukarabati wigo unaotenganisha OPD na wodi, kukarabati chumba cha dawa na geti, kutengeneza kabati za kuhifadhia majarada na dawa, kununua samani na kukarabati mfumo wa maji safi.

Kufuatia kazi hiyo nzuri Waziri alisema Serikali inatawapa milioni 40 ili waboreshe kituo hicho zaidi ili kiweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi.

Kwa upande wa Hospitali ya Wilaya kupitia RBF wameweza kukarabati jengo la wagonjwa wa nje na hivyo kuweka mazingira kuwa mazuri ya upataji huduma kwa wagonjwa.



MICHUZI TV: WAZIRI MKUU AMESEMA SERIKALI IMEJENGA VITUO VYA AFYA 108

0
0

DED UBUNGO AFANYA UKAGUZI KATIKA UJENZI WA MADARASA MANNE YA KIMARA SEKONDARI

0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akizungumza jambo na kaimu Mwamlimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimara wakati alipofika kukagua ujeni wa Madarasa Manne yanayojengwa katika Sekondari hiyo Mpya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo, akikagua ubora wa Zege linalotumika katika ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Sekondari Kimara
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akisaidiwa kupanda  juu ya Msingi na Afisa Mtendaji wa kata Kimara
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akitoa maelekezo kwa mkandarasi aweze kumaliza ujezni huo kwa wakati
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akiagana na walimu wa shule ya Sekondari Kimara

--

RC Iringa awaomba wadau wa utalii kuwekeza Nyanda za juu Kusini

0
0
MKUU wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza ametoa wito kwa wadau wa utalii na maendeleo nchini kuwekeza zaidi kwenye sekta ya Utalii katika Ukanda wa Nyanda za juu Kusini ili kuunga mkono adhma ya serikali ya kufungua na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.

Bi. Masenza ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayoenda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu.

Alisema kwa sasa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imejipanga kimkakati kuhakikisha kwamba inatangaza na fursa na vivutio vya kiutalii vinavyopatikana katika mikoa hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli alilolitoa hivi karibuni wakati wa kilele cha sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Iringa ambapo aliitaka mikoa hiyo kufunguka kiutalii.

Mikoa inayounda kanda hiyo ni pamoja na Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Ruvuma, Rukwa na Katavi. 

“Mikoa ya nyanda za juu Kusini inasifika kuwa na hifadhi zenye sifa za kipekee ikiwemo Taifa ya Ruaha yenye makundi makubwa ya tembo na wanyama wengine. Hifadhi nyingine ni Kitulo yenye aina mbali mbali za maua ambayo hayapatikani mahali pengine Duniani; na Udzungwa yenye wanyama adimu duniani kama vyura wa Kihansi na mengine mengi,’’ alitaja.

Akizungumzia maonesho hayo Bi Masenza alisema tofauti na miaka miwili iliyopita maonesho ya mwaka huu yataambatana na nyongeza ya matukio kadhaa ya kimichezo, kitaaluma na kiutamaduni ili kuongeza tija zaidi katika kufikia malengo ambayo hasa ni kuongeza mazao ya utalii katika kanda hiyo. “Mbali na maonyesho yenyewe kutakuwa na Kongamano la kujadili masuala ya Utalii na Uchumi litakalofanyika tarehe 27 Septemba, 2018, pia tutakuwa na matukio ya kimichezo ikiwemo Mashindano ya mchezo wa Golf yanayotarajiwa kufanyika Wilayani Mufindi kuanzia Julai 27 hadi 29, 2018,’’ alitaja.

Alitaja matukio mengine kuwa ni pamoja na Mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili, huku kilele cha maonesho hayo kikitarajiwa kupambwa na na Mashindano ya mbio za nyika (marathon). Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela alisema katika kipindi chote cha maonesho hayo umeandaliwa utaratibu wa usafiri kwa washiriki, wageni pamoja na wenyeji wa Mkoa Iringa ili waweze kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika ukanda huo

“Nawaomba sana wananchi wote wajipange kushiriki katika maonesho haya makubwa. Pia niwaombe sana wadau wetu wa maendeleo ikiwemo sekta binafsi wajitokeze kwa wingi kuunga mkono maonesho haya.’’ Alisema

Naye Mkurugenzi Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ernest Mwamwaja alisema kwasasa bodi hiyo imejipanga vyema kuhakikisha kwamba inawekeza nguvu zaidi katika kutangaza utalii wa Nyanda za Juu Kusini ili kuleta uwiano wenye afya kiutalii hapa nchini. “TTB tumekuwa tukishiriki kwenye maonyesho mbalimbali ya kitalii ndani nan je ya nchi hivyo basi kwenye mkakati huu jukumu letu kubwa litakuwa ni kusambaza ujumbe kwa wadau wote ndani na nje ya nchi kuhusiana na fursa pamoja na vivutio vya utalii katika Nyanda za Juu Kusini,’’ alisema.

Mratibu wa maonesho hayo kutoka Kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI) inayoshirikiana na Mkoa wa Iringa kuratibu maonesho hayo, Bw Clement Mshana alisema kwa mwaka huu yana maboresho makubwa ambapo mbali na kuongeza uhusishwaji wa sekta binafsi wao, kama waratibu wamejipanga kuhakikisha yanaandaliwa katika viwango vya kimataifa.
MKUU wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Iringa Bw. Robert Masunya.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela (kushoto) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ernest Mwamwaja (kulia) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 kutoka Kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI) Bw Clement Mshana (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo. Kampuni hiyo inashirikiana na Mkoa wa Iringa kuratibu maonesho hayo. 


 MKUU wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa huo pamoja na wadau kutoka TTB pamoja na Capital Plus Internanational

MABALOZI WANNE WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) aliyesimama katikakti akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi waliomaliza muda wao wa uwakilishi nchiniTanzania. Mabalozi hao, wakwanza kutoka kushoto ni Balozi wa Norway, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, Balozi wa Malawi, Mhe. Hawa Olga Ndilowe, Balozi wa Sweden, Mhe. Katarina Rangnitt na Balozi wa Canada, Mhe. Ian Myles. Mhe. Dkt. Mahiga aliandaa hafla ya kuwaaga Mabalozi hao iliyofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 17 July 2018. Katika hafla hiyo, Dkt. Mahiga aliwashukuru Mababalozi hao kwa niaba ya Serikali zao kwa mchango mkubwa wanaotoa kuboresha sekta mbali mbali hapa nchni zikiwemo za Elimu, Afya, Biashara, Kilimo pamoja na Miundombinu. Aidha, Mabalozi pia walipata nafasi ya kutoa neno la shukrani kwa Wizara pamoja na watumishi wake kwa ujumla kwa kuwapa ushirikiano wa kutosha uliowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hapa nchini.
Dkt. Mahiga akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga Waheshimiwa Mabalozi walio maliza muda wao wa uwawakilishi nchini.

Sehemu ya Mabalozi walio hudhuria hafla hiyo wakisimsikiliza kwa makini Mhe. Dkt. Mahiga (hayupo pichani).
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya naAmerika, Bw. Jestas Nyamanga (kulia) pamoja na Balozi Rangnitt nao wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mahiga.
Sehemu nyingine ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo
Mabalozi walio maliza muda wa uwakilishi nchini wakigonga glasi na Waziri Mahiga ikiwa ni ishara ya kuwatakia Viongozi wa Nchi zao Afya njema na Baraka tele kwenye kufanikisha gurudumu la maendeleo.
Dkt. Mahiga akimkabidhi Balozi wa Sweden picha ya mchoro wa Tembo wa Tatu pamoja na Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuikumbuka Tanzania pamoja na kuendelea kuvitangaza vivutio vinavyopatikana nchini. 
Balozi wa Malawi naye alipewa Picha yenye tembo wa Tatu na mlima Kilimanjaro
Dkt. Mahiga akimkabidhi Balozi wa Norway picha inayofanana na wenzake isipokuwa yake ilikuwa na Michoro ya Wanyama aina ya Twiga, Tembo pamoja na Mlima Kilimanjaro.
Balozi wa Canada naye alipata zawadi ya picha yenye mchoro wa Tembo pamoja na Mlima Kilimanjaro, kwa pamoja Mabalozi hao walionyesha kuzifurahia zawadi hizo.
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi waliomaliza muda wa uwakilishi nchini pamoja na Mabalozi ambao bado wanaendelea kuziwakilisha nchi zao.

MOJASPESHO YATOA MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 204

0
0


Mshindi RoseMary Onesmo Luhamo (katikati) akikabidhiwa zawadi ya ushindi wake wa milioni 204 kutoka kwa Meneja wa Lucky Games Ltd, Patrick Salamouni, ambayo ni kampuni inayochezesha mchezo wa MojaSpesho pamoja. Kushoto ni Meneja wa tawi la benki ya CRDB Azikiwe Premier Fabiola Msula. Kwa kucheza mchezo wa MOJASPESHO kupitia simu yako ya mkononi nenda sehemu ya KULIPIA BILI kwa watumiaji wa AIRTEL MONEY, TIGO PESA, MPESA au HALOPESA, kisha ingiza NAMBA YA KAMPUNI/BIASHARA ya MOJASPESHO ambayo ni 123255 - kisha INGIZA NAMBA ZAKO 3 SPESHO ZA USHINDI’09
Mshindi RoseMary Onesmo Luhamo wa kwanza wa droo ya milioni 204 ya MOJASPESHO, akifurahi baada ya kukabidhiwa pesa za ushindi wake leo jijini Dar es Salaam. Kwa kucheza mchezo wa MOJASPESHO kupitia simu yako ya mkononi nenda sehemu ya KULIPIA BILI kwa watumiaji wa AIRTEL MONEY, TIGO PESA, MPESA au HALOPESA, kisha ingiza NAMBA YA KAMPUNI/BIASHARA ya MOJASPESHO ambayo ni 123255 - kisha INGIZA NAMBA ZAKO 3 SPESHO ZA USHINDI’

Mchezo wa bahati nasibu wa Mojaspesho umetoa kwa mara ya kwanza mshindi wa kiasi kikubwa cha pesa cha shilingi Milioni 204 kwa ROSEMARY ONESMO LUHAMO, mfanyabiashara kutoka MPWAPWA DODOMA mwenye umri wa miaka 26.

Akuzungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi pesa kwa mshindi, Meneja biashara wa kampuni ya Lucy Games Patrick Salamouni ambayo ndio inajechezesha mchezo wa Mojaspesho alisema kuwa ushindi wa Rosemary umekuja baada ya kucheza Mojaspesho zaidi ya mara nyingi sana bila kukata tamaa, na hatimaye kulinganisha namba zake za tatu spesho ambazo zilikuwa 873 siku ya Jackpot ya Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Julai 2018.

Huu ni mchezo wa bahati nasibu. Unaweza ukacheza mara moja ukashinda lakini pia unaweza isishinde. Ninachoweza kuwaambia ni kuwa kila mtu anayecheza anayo nafasi ya kuwa mshindi. Naomba Watanzania kuwa huu ni mchezo halali na kila anayeshinda anapata zawadi yake, alisema Salamouni. Salamouni aliongeza kuwa huu ni ushindi mkubwa kuwahi kutokea tangu Moja Spesho ianze kuchezesha Droo zake na ni uthibitisho kuwa kila mtu anaweza kushinda Mojaspesho.

‘Unaweza kucheza MOJASPESHO kupitia simu yako ya mkononi kwa kuingia sehemu ya KULIPIA BILI kwa watumiaji wa AIRTEL MONEY, TIGO PESA, MPESA au HALOPESA, kisha ingiza NAMBA YA KAMPUNI/BIASHARA ya MOJASPESHO ambayo ni 123255 - kisha INGIZA NAMBA ZAKO 3 SPESHO ZA USHINDI’ aliongeza Salamouni.

Kwa upande wake, mshindi Rosemary Onesmo alisema kuwa anayo furaha kubwa na kujiona wa bahati kuwa mshindi wa kwanza wa milioni 204. ‘Namshukuru Mungu kwa kunisaidia kuwa mshindi wa MOJASPESHO. Pia nawapongeza MOJASPESHO kwa kuwa wa kweli na kuweza kunipa zawadi yangu hapa leo kila mtu akishuhudia. Napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa mchezo wa MOJASPESHO ni wa ukweli na nawaomba wajitokeze kwa wingi kwani hata haujashinda zawadi kubwa kama mimi unaweza kuwa mshindi wa zawadi zingine, alisema Rosemary.

Rosemary aliongeza kuwa atatumia pesa zake kuendeleza biashara yake kwani ameweza kupewa utaalamu wa biashara kabla ya kubabidhiwa zawadi yake. MOJASPESHO wameweza kunipa elimu nzuri jinsi ya kutunza pesa hizi na pia jinsi ya kufanya biashara bila kuteleleka. Ni heshima kubwa mno kwa upande wangu, aliongeza Rosemary.

TOURISTS FLOCK TO TARANGIRE NATIONAL PARK

0
0
The Tarangire National Park is the sixth largest national park in Tanzania, it is located in Manyara Region. The name of the park originates from the Tarangire River that crosses the park, which is the primary source of fresh water for wild animals in the Tarangire Ecosystem during the annual dry season. 

The Tarangire Ecosystem is defined by the long-distance migration of wildebeest and zebras. During the dry season thousands of animals concentrate in Tarangire National Park from the surrounding wet-season dispersal and calving areas. It covers an area of approximately 2,850 square kilometers (1,100 square miles.)

The landscape is composed of granitic ridges, river valley, and swamps. Vegetation is a mix of Acacia woodland, Commiphora-Combretum woodland, seasonally flooded grassland, and Baobab trees. The park is famous for its high density of elephants and baobab trees. Visitors to the park in the June to November dry season can expect to see large herds of thousands of zebra, wildebeest and cape buffalo. Other common resident animals include waterbuck, giraffe, dik dik, impala, eland, Grant's gazelle, vervet monkey, banded mongoose, and olive baboon.

Predators in Tarangire include African lion, leopard, cheetah, caracal, honey badger, and African wild dog. The oldest known elephant to give birth to twins is found in Tarangire. A recent birth of elephant twins in the Tarangire National Park of Tanzania is a great example of how the birth of these two healthy and thriving twins can beat the odds.

Home to more than 550 bird species, the park is a haven for bird enthusiasts. The park is also famous for the termite mounds that dot the landscape. Those that have been abandoned are often home to dwarf mongoose.

In 2015, a giraffe that is white due to leucism was spotted in the park.Current wildlife research projects in the park include the Tarangire Elephant Project, Tarangire Lion Project, and Masai Giraffe Conservation Demography Project.
 A velvet monkey tries to solicit some cookies from some tourists taking a breather at the gates of the Tarangire National Park, however it is strictly forbidden to feed animals in national parks mainly for fear of spreading deceases to the wild animals.
A motorcade of tourists  is surrounded by a large herd of elephants in the Tarangire National Park. The park is famous for the highest concentration of elephants per square kilometer in the world. Photos by Issa Michuzi

VYAMA VYA UKOMBOZI BARANI AFRIKA VYATAKIWA KUINGIA KATIKA AWAMU YA PILI YA UKOMBOZI WA KIUCHUMI

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

VYAMA vilivyoshiriki kupigania ukombozi wa Bara la Afrika sasa vimetakiwa kuingia awamu ya pili ya ukombozi wa kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya Bara la Afrika huku vikitakiwa kukomesha rushwa, ufisadi na ubadhirifu.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd wakati anafunga mkutano wa siku mbili uliohusisha vyama vilivyokuwa mstari wa mbele kupigania ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika.

"Awamu ya kwanza ilikuwa ni kupigania uhuru kwa nchi za Afrika na sasa uhuru tunao, hivyo vyama hivyo vinatakiwa kuingia awamu ya pili ya ukombozi wa kiuchumi.

"Kuna kila sababu ya kujifunza kutoka China ambapo wameendesha mapinduzi ya kiuchumi na  kuwakomboa wananchi wake wapatao bilioni  mbili,"amesema.

Amefafanua kama si China mambo yangekuwa mabaya na kama ingekuwa inatolewa Kombe la Dunia kwa nchi ambayo imefanikiwa kujenga uchumi imara basi kombe lingekwenda China.

Balozi Idd amesema China imekuwa ikitoa msaada kwa nchi mbalimbali za Afrika ikiwamo Tanzania ambayo imekuwa ikinufaika na misaada ya nchi hiyo na miradi mbalimbali ambayo imeacha alama isiyofutika akitolea mfano reli ya TAZARA.

Amesema kwa upande wa Zanzibar kuna miradi mingi ya maendeleo imefanyika ikiwamo pia ujenzi wa kiwanda cha sukari , viwanja vya kisasa vya mpira.

Akifafanua zaidi kuhusu mkutano huo, amesema ni vema yale ambayo wamekubaliana yakatekelezwa kwa vitendo na si maneno matupu.

"Mada zote zilizotolewa katika mkutano huo zilikuwa za wazi na zimejadiliwa kwa kina.Nitoe rai hakikisheni yale ambayo mmekubaliana basi yanatekelezwa kwa vitendo.

"Pia hakikisheni mnaongeza mapambano katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.Ni wakati muafaka sasa wa kuanza ukombozi wa kiuchumi kwa nchi za Afrika,"amesema Balozi Idd.

Amesisitiza CCM tangu kuazishwa kwake kimekuwa mstari wa mbele kupiga vita rushwa na chini ya Mwenyekiti wake Rais Dk.John Magufuli ameongeza pambano dhidi ya rushwa na ufisadi huku akiimarisha nidhamu katika utumishi kupitia kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

"Tunakipongeza Chama cha Kikomunisti cha China(CPC) kwa kuamua mkutano huu kufanyika nchini Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine vyama vya Afrika vimepata nafasi ya kujadili mambo kwa kina na kufikia maazimio,"amesema.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa  kutoka CPC Xu Lyuping amesema mkutano huo umefanyika kwa mafanikio makubwa na pasipo shaka utakuwa na matokeo makubwa.

Amesema anaamini vyama vyote vilivyo shiriki wamepata uelekeo wa namna ya kwenda kupambana na ukombozi wa kiuchumi kwa maendeleo ya Bara la Afrika na watu wake.

"Cha msingi ni kuwekwa jitihada za kufkia malengo.CPC imekuwa madarakani tangu mwaka 1949 na msingi wa kukaa madarakani kwa muda mrefu ni kuwaletea maendeleo wananchi,"amefafanua.

POLEPOLE NA FAIDA ZA MKUTANO

Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema mkutano huo wa kidunia umefanyika kwa mara ya kwanza Afrika na kwa mara ya kwanza Tanzania.

Amesisitiza vyama vyote ambavyo vimeshiriki kuna mambo kadhaa ambayo wamekubaliana kwa ajili ya maendeleo ya Bara la Afrika huku akitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa CPC kwa uamuzi wake wa kutakaka mkutano huo kufanyika nchini.


Amesema ni wakati muafaka kwa vyama vyote vilivyoshiriki kupigania ukombozi wa Bara la Afrika kuendelea kuweka misingi imara ya kuleta maendeleo ya wananchi wake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Chama cha Kikoministi cha China (CPC)  Xu Lyuping akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati wa kufungwa  kwa mkutano wa Vyama vya Kisiasa Barani Afrika na Chama cha Kikoministi cha China leo Jijini Dar es Salaam.. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dr. Bashiru Ali Kapura, na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara NPhilip Mangula.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufunga mkutano wa Vyama vya Kisiasa Barani Afrika na Chama cha Kikoministi cha China ukiofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam .
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Chama cha Kikoministi cha China (CPC)  Xu Lyuping akitoa salamu za Chama cha Kikoministi wakati wa kufungwa  kwa mkutano wa Vyama vya Kisiasa Barani Afrika na Chama cha Kikoministi cha China leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Kinachotawala Nchini Cape Vade Bwana Miguel Petro akitoa salamu za Chama hicho wakati wa kufungwa  kwa mkutano wa Vyama vya Kisiasa Barani Afrika na Chama cha Kikoministi cha China leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na – OMPR – ZNZ.

MRADI WA MAJI WA KIMBIJI NA MPERA UTASAIDIA UPATIKANAJI WA LITA MIL 260 KWA SIKU-PROF MBARAWA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ametembelea mradi wa uchimbaji wa visima virefu vya Kimbijii na Mpera wenye thamani ya Bilioni 19.6  vitakavyosaidia kupatikana kwa lita za maji Milioni 260 kwa siku.

Mradi huo wa visima vya maji uliochini ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) una lengo la kuongeza wingi wa maji katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na kufikia lita Milioni 720 kwa siku kufikia mwaka 2032.

Prof Mbarawa akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA  Dkt Suphian Masasi ameweza kukagua visima hivyo na kuwataka wakandarasi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Akizungumza wakati wa kukagua visina hivyo, Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huo utawasaidia wananchi wa Dar es Salaam kwa kuwa utasaidia upatikanaji wa maji safi na salama na yatakayotosheleza kwa matumizi yao.

" Mradi huu wa Kimbiji na Mpera utakaotoa Lita Milioni 260 kwa siku utasaidia sana wananchi wa Dar es Salaam, ukichukulia Mradi wa Ruvu Juu na Ruvu chini unatoa lita Milioni 502 kwa siku kwa ujumla wake utaleta chachu ksa wananchi kupata maji kwa uhakika,"amesema Prof Mbarawa.

Amesema kuwa, kukamilika kwa visima hivi kutaimarisha upatikanaji wa maji katika maeneo ambayo hayakuwa na huduma nzuri ya majisafi na yale yasiyo na mtandao rasmi.

Prof Mbarawa akitoa maagizo mbele ya Mkurugenzi Wa DAWASA, ameitaka kampuni ya Serengeti ya nchini Tanzania na Mkandarasi kutoka kampuni ya NSPT ya nchini Iran kuhakikisha mradi huu unaenda na muda ulipangwa kwakuwa tayari umesuasua   kwa mrefu haujamalizika.

" Kampuni yenu naipa wiki moja kwanza wawasilishe malipo ya bima kwa wafanyakazi, vifaa pamoja visima vyenyewe ambapo gharama yake haizidi hata Bilioni 4  na mkishafanya hivyo mniletee nione," 

Kwa upande wa DAWASA, Kaimu Mkurugenzi  Dkt Suphian Masasi amesema kuwa wanategemea mradi huu uende kwa haraka zaidi ili wananchi wapate maji ambapo wameona kuna baadhi ya maeneo wataamua kuyafanya wao kama Mamlaka husika kama ununuaji wa vifaa, kuwalipa baadhi ya watendaji moja kwa moja ili kuweza kurahisha umalizikaji wa kazi ili watu wapate maji.

"Sisi tunafuata maagizo ya Waziri kwahiyo kinachofuata ni utendaji tu na kuna maeneo tutawekea tija ikiwemo kuwalipa watendaji yawekezna ipo changamoto ya ulipaji kwa wakati pia hata ununuaji wa vifaa tutafanya hivyo pale inapohitajika na kisha baadae tutawakata katika malipo yao,"amesema Dkt Masasi.

Naye Msimamizi wa miradi ya Maji kutoka kampuni ya Dkt Charles Kaaya amesema kuwa katika utafiti wao wa visima 19 ambavyo tayari vimekamilika wanaimani upatikanaji wa maji utakuwa ni ule ambao umekadiriwa wa lita Milioni 260 kwa siku.

Tayari visima 19 kati ya 20 vya mradi wa Kimbini na Mpera vimekamilika na vina kina kati ya mita 435 hafi 625 huku baadhi vikiwa na uwezo wa kuzalisha lita 100,000 hadi 450,000 kwa saa na mradi huu umetekelezwa na serikali ya Tanzania ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi wake wa Dar es Salaam.

Maeneo yatakayonufaika kwa mradio huo ni Kigamboni, Chanika, Chamazi, Pugu, Kibada, Kisarawe 2, Kongowe, Gongo la Mboto, Segerea, Charambe, Buyuni, Mbagala, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Tazara, Ukonga, eneo la viwanda la Barabara ya Nyerere, Mji wa Mkuranga mkoa wa Pwani pamoja na  vitongoji vyake vikiwemo Kisemvule na Kibamba.
WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa miradi ya maji wa kampuni ya EGIS, Dk. Charles Kaaya, kuhusu kupima urefu wa kisima kirefu katika mradi wa maji wa visima virefu vya Kimbiji, wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasi.
 WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa  akinywa maji katika moja ya Kisima ya miradi ya maji ya Kimbiji na Mpera wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasi.
 WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiwa pamoja Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasikatika mradi wa maji wa visima virefu vya Kimbiji, wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam utakaofanikisha upatikanaji wa lita Milioni 260 kwa siku.


VIONGOZI WA KISIASA TUHAMASISHE WANANCHI KUENZI UTAMADUNI WAO - WAZIRI MKUU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wakiwemo mawaziri na wabunge wawahamishe Watanzania kuendeleza utamaduni wao.

Ametoa wito huo leo (Jumatano, Julai 18, 2018) wakati akizungumza na wazee na wananchi wa Makunduchi mara baada ya kushuhudia maadhimisho ya sikukuu ya Mwaka-Kogwa yaliyofanyika Makunduchi, wilaya ya Kusini, mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

“Mawaziri wote, tuna dhamana ya kuwahamasisha Watanzania waendeleze utamaduni ili uwe ni jambo hai. Wabunge na wawakilishi tukiwa kwenye majukwaa, tusisitize Watanzania waendeleze utamaduni,” amesema.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zinasimamia uwepo wa utamaduni na zenyewe zinaongozwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo imelenga kuihamasisha  jamii kuuenzi,  kuulinda  na  kuudumisha utamaduni wa Mzanzibari na kushiriki katika uandaaji wa matamasha 50 ya utamaduni.

“Lazima utamaduni uendelezwe ndani na nje ya nchi na ni lazima tufanye jitihada tuwarithishe watoto utamaduni wetu. Kwa mfano, hapa Zanzibar mnalo tamasha la ZIFF, lile ni la kimataifa, vyombo vya muziki ni vya kisasa. Ni vema sasa, tukaangalia uwezekano wa kuwa na tamasha la huku chini ambalo litatumia ala za muziki za asili,” alisema.

Akizungumzia sherehe za Mwaka Kogwa, Waziri Mkuu alisema hii ni mara yake ya kwanza tangu azaliwe kuona watu wakichapana viboko si kwa ugomvi wala chuki, bali wakiwa na furaha.

“Mwaka Kogwa ni utamaduni wetu, pande zote za visiwani na zimekuwa zikifanyika kila mwaka lakini hivi sasa ni Makunduchi peke yake ambao mmeweza kuendeleza utamaduni huu, wengine wameacha kuadhimisha sherehe hizi,” amesema.

“Tanzania tuna makabila zaidi ya 120 wenye tamaduni na mila tofauti lakini si wote ambao wanaenzi mila na tamaduni zao. Utamaduni ni jambo muhimu nchini, utamaduni ni fursa ya kiuchumi kwa sababu watalii wanatoka kwao kuja Zanzibar kuangalia tukio kama hili, ni lazima tuuenzi,” alisisitiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewapongeza wakazi wa Makunduchi kwa kutunza na kuhifadhi mazingira na amewataka waendeleze bidii ya kuyatunza.

“Kati ya mambo ambayo nimeyapenda sana, ni tabia yenu ya uhifadhi mazingira. Lazima niwapongeze wana-Makunduchi kwa kutunza na kuhifadhi mazingira. Kama msingekuwa watu wazuri mgeshafyeka misitu yote, na kusingekuwa na mvuto kama nilivyoona. Endeleeni kuhifadhi mazingira yetu ili yaweze kututunza,” alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Bw. Hassan Khatib Hassan alisema wanafanya maadhimisho hayo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni na kuonyesha urithi kutoka kwa wazazi wao. “Tunaendeleza utamaduni huu sababu ni urithi kutoka kwa wazazi wetu. Ni upendo, amani na mshikamano,” alisema.

Mapema, Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Bw. Idrissa Kitwana Mustafa alisema wamewaalika mabalozi wa Uturuki na Iran kwenye maadhimisho hayo kwa sababu utamaduni huo pia unafanyika kwenye nchi zao.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Makunduchi, Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi, Bw. Haroun Ali Suleiman alisema anaipongeza serikali ya awamu y atano kwa mambo ambayo imeyafanya kwa kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

“Hakuna asiyeona, na kama mtu hataki kuona, basi hataona kabisa. TUnaomba utufikishie salamu zetu kwa Mhshimiwa Rais Magufuli,” alisema.

Alisema anaomba kuwe na ushirikiano wa karibu baina ya watendaji wa wilaya ya Kusini na ile ya Ruangwa ambako Waziri Mkuu anatoka ili watumishi wake waweze kubadilishana uzoefu na kuimarisha muungano.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya asili wakati alipowasili  kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za Mwakakogwa zilizofanyika Makunduchi, Julai 18, 2018.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya washiriki wa sherehe za Mwakakogwa wakati alipowasili Makunduchi Zanzibar kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Julai 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuhitimisha  Sherehe za Mwakakogwa, eneo la Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye eneo la Shereza za Mwakakogwa zilizofanyika Makunduchi, Zanzibar Julai 18, 2018.
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria katika Sherehe za Mwakakogwa zilizofanyika  Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika sala ya kumwombea Rais wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Idris Abdul Wakil kwenye kaburi la Rais huyo enero la Makunduchi, Zanzibar Julai 18, 2018.  Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Sira Ubwa  Mwamboya, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja , Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,  Hassan Khatib Hassan.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mohammed Abdulwakil ambaye ni Kaka wa Rais  wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Idris Abdul Wakil  Wakati  alipozulu kaburi la Rais huyo, eneo la Makunduchi, Zanzibar Julai 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa kofia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Mwakakogwa, Mwalimu Makungu Mwita katika sherehe za Mwakakogwa zilizofanyika Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Sherehe za Mwakakongwa  zilizofanyika Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,  Hassan Khatib Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


VIONGOZI WA KISIASA TUHAMASISHE WANANCHI KUENZI UTAMADUNI WAO - WAZIRI MKUU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wakiwemo mawaziri na wabunge wawahamishe Watanzania kuendeleza utamaduni wao.

Ametoa wito huo leo (Jumatano, Julai 18, 2018) wakati akizungumza na wazee na wananchi wa Makunduchi mara baada ya kushuhudia maadhimisho ya sikukuu ya Mwaka-Kogwa yaliyofanyika Makunduchi, wilaya ya Kusini, mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

“Mawaziri wote, tuna dhamana ya kuwahamasisha Watanzania waendeleze utamaduni ili uwe ni jambo hai. Wabunge na wawakilishi tukiwa kwenye majukwaa, tusisitize Watanzania waendeleze utamaduni,” amesema.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zinasimamia uwepo wa utamaduni na zenyewe zinaongozwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo imelenga kuihamasisha  jamii kuuenzi,  kuulinda  na  kuudumisha utamaduni wa Mzanzibari na kushiriki katika uandaaji wa matamasha 50 ya utamaduni.

“Lazima utamaduni uendelezwe ndani na nje ya nchi na ni lazima tufanye jitihada tuwarithishe watoto utamaduni wetu. Kwa mfano, hapa Zanzibar mnalo tamasha la ZIFF, lile ni la kimataifa, vyombo vya muziki ni vya kisasa. Ni vema sasa, tukaangalia uwezekano wa kuwa na tamasha la huku chini ambalo litatumia ala za muziki za asili,” alisema.

Akizungumzia sherehe za Mwaka Kogwa, Waziri Mkuu alisema hii ni mara yake ya kwanza tangu azaliwe kuona watu wakichapana viboko si kwa ugomvi wala chuki, bali wakiwa na furaha.

“Mwaka Kogwa ni utamaduni wetu, pande zote za visiwani na zimekuwa zikifanyika kila mwaka lakini hivi sasa ni Makunduchi peke yake ambao mmeweza kuendeleza utamaduni huu, wengine wameacha kuadhimisha sherehe hizi,” amesema.

“Tanzania tuna makabila zaidi ya 120 wenye tamaduni na mila tofauti lakini si wote ambao wanaenzi mila na tamaduni zao. Utamaduni ni jambo muhimu nchini, utamaduni ni fursa ya kiuchumi kwa sababu watalii wanatoka kwao kuja Zanzibar kuangalia tukio kama hili, ni lazima tuuenzi,” alisisitiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewapongeza wakazi wa Makunduchi kwa kutunza na kuhifadhi mazingira na amewataka waendeleze bidii ya kuyatunza.

“Kati ya mambo ambayo nimeyapenda sana, ni tabia yenu ya uhifadhi mazingira. Lazima niwapongeze wana-Makunduchi kwa kutunza na kuhifadhi mazingira. Kama msingekuwa watu wazuri mgeshafyeka misitu yote, na kusingekuwa na mvuto kama nilivyoona. Endeleeni kuhifadhi mazingira yetu ili yaweze kututunza,” alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Bw. Hassan Khatib Hassan alisema wanafanya maadhimisho hayo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni na kuonyesha urithi kutoka kwa wazazi wao. “Tunaendeleza utamaduni huu sababu ni urithi kutoka kwa wazazi wetu. Ni upendo, amani na mshikamano,” alisema.

Mapema, Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Bw. Idrissa Kitwana Mustafa alisema wamewaalika mabalozi wa Uturuki na Iran kwenye maadhimisho hayo kwa sababu utamaduni huo pia unafanyika kwenye nchi zao.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Makunduchi, Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi, Bw. Haroun Ali Suleiman alisema anaipongeza serikali ya awamu y atano kwa mambo ambayo imeyafanya kwa kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

“Hakuna asiyeona, na kama mtu hataki kuona, basi hataona kabisa. TUnaomba utufikishie salamu zetu kwa Mhshimiwa Rais Magufuli,” alisema.

Alisema anaomba kuwe na ushirikiano wa karibu baina ya watendaji wa wilaya ya Kusini na ile ya Ruangwa ambako Waziri Mkuu anatoka ili watumishi wake waweze kubadilishana uzoefu na kuimarisha muungano.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya asili wakati alipowasili  kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za Mwakakogwa zilizofanyika Makunduchi, Julai 18, 2018.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya washiriki wa sherehe za Mwakakogwa wakati alipowasili Makunduchi Zanzibar kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Julai 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuhitimisha  Sherehe za Mwakakogwa, eneo la Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye eneo la Shereza za Mwakakogwa zilizofanyika Makunduchi, Zanzibar Julai 18, 2018.
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria katika Sherehe za Mwakakogwa zilizofanyika  Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika sala ya kumwombea Rais wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Idris Abdul Wakil kwenye kaburi la Rais huyo enero la Makunduchi, Zanzibar Julai 18, 2018.  Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Sira Ubwa  Mwamboya, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja , Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,  Hassan Khatib Hassan.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mohammed Abdulwakil ambaye ni Kaka wa Rais  wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Idris Abdul Wakil  Wakati  alipozulu kaburi la Rais huyo, eneo la Makunduchi, Zanzibar Julai 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa kofia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Mwakakogwa, Mwalimu Makungu Mwita katika sherehe za Mwakakogwa zilizofanyika Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Sherehe za Mwakakongwa  zilizofanyika Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,  Hassan Khatib Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MWANAFUNZI KUFANYIWA USAJILI PAPO HAPO BANDA LA TAASISI YA USTAWI WA JAMII KATIKA MAONESHO YA 13 YA VYUO VIKUU MNAZI MMOJA

0
0
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii anawakaribisha wahitimu wote wa kidato cha sita na kidato cha Nne pamoja na wazazi wa wahitimu kwenye banda la Taasisi hiyo katika maonyesho ya 13 ya vyuo vikuu kwenye viwanja vya Mnazi mmoja, kukutana na wahadhiri  wa taasisi na kupata maelezo ya kina kuhusu programu za masomo zitolewazo na Taasisi hiyo pia kupata maelezo ya jinsi ya kujiunga na Taasisi kwa mwaka huu wa maosmo 2018/2019 ambapo mwanafunzi atafanyiwa usajili papo hapo katika banda la Taasisi ya Ustawi wa jamii.

Ili kusajiliwa mwanafunzi afike na Vivuli vya vyeti vya kitaaluma na cheti cha kuzaliwa pamoja na ada a Usajili ambayo ni Tsh. elfu 10,000/ tu. 
Mhadhiri msaidizi wa idara ya Rasilimali watu Bi. Christina fille akitoa maelezo na kujibu maswali kwa wanafunzi mbali mbali waliofika kwenye Banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii. 
Wanafunzi na Wananchi mbali mbali wakipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Taasisi ya Ustawi wa jamii kwenye maonyesho ya 13 ya Vyuo vikuu katika viwanja vya Mnazi mmoja  Dar es salaam.

BENKI YA STANBIC YAZINDUA KAMPENI YA ‘ZAIDI YA BENKI’

0
0

Chachu ya ukuaji wa uchumi jumuishi Tanzania.

Benki ya Stanbic Tanzania imezindua kampeni maalumu kwa ajili ya chata yake, yenye kauli mbiu isemayo “Zaidi ya Benki”, ikijitofautisha na taasisi nyinginezo kwa kuwa benki yenye kugusa wateja wake kwa kutoa huduma na bidhaa zenye kuwezesha wateja hao pamoja na watanzania kwa ujumla kufikia malengo yao ya kimaisha.

"Nia na madhumuni ya kampeni hii ya 'Zaidi ya Benki' ni kudhihirisha mchango wetu katika kuboresha maisha ya watu na ya jamii kwa ujumla; mara nyingi watu wanapofikiria benki, huwa wanawaza miamala ya kifedha tu, huku wakisahau kinachojiri baada ya mteja kuondoka na fedha zake," alisema Bi. Desideria Mwegelo, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Stanbic Tanzania.

"Sisi hapa Stanbic, tuna desturi ya kufikiria yanayotokea kabla na baada ya miamala kufanyika. Tunaamini kwamba kila tunachofanya hata kiwe kidogo vipi, kina athari katika maisha ya mteja wetu kwa namna moja au nyingine, na ndio sababu huwa tunamfikira mteja katika kila tunachokifanya na kuhakikisha tunaongeza matokeo chanya,” aliendelea kusema.

Kwa mfano, tunaposhiriki katika miradi ya kuleta umeme katika jamii, kwa namna nyingine tunakuwa tumewezesha ukuaji wa viwanda, elimu na fursa nyinginezo zitokanazo na kuwepo kwa umeme.Hali kadhalika kupitia mikopo ya nyumba, watu wanawezeshwa kumiliki nyumba ambazo familia zao hazitokaa zisahau.

Tanzania imesheheni jamii ya vijana wenye jitihada, akili na nguvu, na wenye kutafuta fursa za kujikwamua na kujiendeleza kimaisha kwa kila hali, benki ya Stanbic inataka kuwa sehemu ya jitihada hizo katika kufanikisha ndoto zao na za familia na jamii kwa ujumla.

'Kama wanachama wa Standard Bank Group yenye historia ndefu ya zaidi ya miaka 155 na kuwepo katika nchi 20 barani Afrika, tunaelewa changamoto, tamaduni na watu wa bara hili. Sisi ni zaidi ya benki,’ alisema Bi. Mwegelo. 'Stanbic inahamasishwa na vijana wa kitanzania wenye shauku ya kutumia fursa lukuki zilizopo nchini kwa kutumia ubunifu na mawazo mbadala. Tunataka kufanikisha ndoto zao za kufikia mafanikio ya kifedha. '

Dira ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania inatazamia kiwango kikubwa cha maendeleo ya rasilimali watu na inategemea nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Malengo ya Stanbic yanaendana na yale ya taifa huku ikijitahidi kutumia fursa zitokanazo na huduma za kifedha kuboresha maisha ya Watanzania. Hivi karibuni, Benki ilipokea tuzo kwenye tuzo za “Banker Africa Awards” kwa kuwa ‘Benki bora kwa biashara ndogo ndogo na za kati’ nchini Tanzania. Huu ni mfano hai mwingine wenye kudhihirisha nia ya Stanbic katika kuleta maendeleo ya kweli kwenye biashara na ukuaji wa uchumi jumuishi nchini Tanzania.

WADAU SAME WAHIMIZWA KUMALIZIA MICHANGO YAO ILI KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA

0
0

WADAU mbalimbali wilayani Same wamekumbushwa kukamilisha ahadi zao ili kufanikisha ujenzi wa madarasa 50 yaliyokusudiwa ili ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu yawe yamekamilika. 

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule wakati akizungumzia michango ya ujenzi wa madarasa hayo ambapo kata 10 ambazo zimekamilisha michango zimekabidhiwa fedha za kukamilisha majengo. 

Uzinduzi umefanyika katika Shule ya Msingi Moipo iliyopo katika Kata ya Mabilioni.Hivyo moja ya mambo ambayo wadau wamekumbushwa ni kukamilisha ahadi ili kazi hiyo ikamilike.Uzinduzi wa ujenzi umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Wikaya ya Same, Mwenyekiti wa Halmashauri, Diwani na wataalamu. 

" Ukamilishaji wa madarasa haya utawezesha watoto 2250 kupata madarasa ya uhakika ya kusoea,"amesema Mkuu wa Wilaya hiyo wakati anawashukuru wananchi waliochangia.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ameahidi kusimamia vizuri michango hiyo na kuagiza kuwe kunatolewa taarifa ya matumizi kwa wananchi. 

Wakati huo huo wananchi wahimizwa kuhakikisha watoto wanaenda shuleni ili kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli na Serikali yake ya kutaka watoto wote wapate elimu bure, wale watoro wazazi wao kushughulikiwa. 

" Elimu bora ni wajibu wa kila mwanajamii".
 Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule akipokea Mbuzi kwa mmoja wa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi  wa madarasa 50 yaliyokusudiwa  kukamilia ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu.
 Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule akipokea vifaa vya ujenzi  ikiwemo mifuko ua Saruji na Mabati kutoka Wananchi ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi  wa madarasa 50 yaliyokusudiwa  kukamilia ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu. 
 Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wamekaa nje ya jengo la shule ambalo linatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

ELIMU YA KODI NI MUHIMU SANA MASHULENI DKT. NDUMBARO ATOA USHAURI

0
0
Wanafunzi katika shule za sekondari wanatakiwa kufahamu masuala na umuhimu wa kodi kutokana na juhudi ambazo Serikali ya Awamu ya Tano imefanya katika kutoa elimu ya msingi na sekondari nchini bure
Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Dk. Damas Ndumbaro wakati akizindua rasmi mashindano ya vilabu vya kodi kwa shule za sekondari katika Tamasha la Majimaji Serebuka linaloendelea Songea katika Mkoa Ruvuma.
Mhe. Ndumbaro amesema kwamba kutokana na kukosa mtaala wa elimu ya kodi katika shule za sekondari, Mkoa wa Ruvuma uliamua kuwa na mdahalo wa masuala ya kodi kwa shule za sekondari ili wanafunzi waweze kufundishana kwani katika kuwasilisha mada za masuala ya kodi wanafunzi wanajifunza na kufundishana.
“Samaki mkunje angali mbichi. Umri wa vijana walio sekondari ni umri mzuri wa kuwaelimisha masuala ya kodi”, alisema Dk. Ndumbaro na kuongeza kwamba wanafunzi wakifundishana wenyewe kwa wenyewe wataelewa zaidi kuliko wanapofundishwa.
Mbunge huyo wa Songea Mjini alisema kwamba wanafunzi wanatakiwa kufahamu kwamba gharama ya elimu ya bure inayotolewa katika shule za msingi na sekondari, ujenzi wa viwanja vya ndege, barabara, ununuzi wa ndege, na upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Ruvuma wa gridi ya taifa kutoka Makambako zinatokana na kodi.
Aidha amewataka wanafunzi kushiriki vizuri katika mdahalo huo bila kujali kwamba watashinda au la kwani kwa kuweza kufikia hatua ya ushiriki tayari wote ni washindi Mdahalo huo unaohusu mashine za risiti za kielektroniki na umeandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na waandaji wa Tamasha la Serebuka.
Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Richard Kayombo amewataka wanafunzi kuelimisha jamii inayowazunguka kuhusu masuala ya kodi kwani kodi ndio pato pekee linaloiwezesha nchi kuhudumia wananchi wake.
“Sisi tutaendelea kutoa elimu kwa kadiri ya uwezo wetu bila kuchagua na nyinyi tunawaandaa ili muweze kutoa elimu kwa familia zenu, majirani zenu, wanafunzi wenzenu na jamii nzima inayowazunguka”, alisema Kayombo.
Amewataka  wanafunzi kudai risiti wanaponunua bidhaa, kulipa kodi wakati wa kulipa kodi ukifika kwani wanafunzi ni wafanya biashara na walipakodi watarajiwa.
Naye Mratibu wa Mashindano ya Vilabu vya kodi katika Tamasha hilo kutoka TRA Njovu Kilian amesema kwamba Mashindano hayo yamekuwa na mwamko mzuri kutokana na kuongezeka kwa washiriki. “Mwaka jana tulikuwa na washiriki 22 lakini mwaka huu tuna shule 32 ambazo zinashiriki”, alisema Njovu.
Pamoja na kushindana kuwasilisha mada pia kutakuwa na shindano la kuchora katuni inayohusu masuala ya kodi
Mashindano ya Vilabu vya Kodi katika shule za Sekondari katika Tamasha la Serebuka yanashirikisha shule za Sekondari 32 za Mkoa wa Ruvuma ambapo baada ya mchujo shule sita bora zitaingia fainali na kushindana kupata shule tatu bora.
Katika mashindano haya washindi watapata zawadi ya pesa taslimu kuanzia shilingi laki mbili hadi elfu hamsini ambazo zinatolewa na TRA na Benki ya NMB kwa uande wao watatoa zawadi ya kuwafungulia akauti washindi wa jumla watano pamoja na zawadi nyingine.
Washindi wapo katika makundi sita ambayo ni wawasilishaji bora wa mada, washindi wa jumla, walimu bora, shule bora, mwanafunzi aliye wasilisha mada vizuri, na mchoraji mzuri wa katuni.
Mashindano haya ambayo yanaandaliwa na TRA kwa kushirikiana na Songea Mississippi (SOMI) ambao ni waandaaji wa Tamasha la Serebuka yanafanyika kwa mara ya pili tangu yaanzishwe Mwaka 2017 mkoani Ruvuma ambapo shule za sekondari hufanya mdahalo kuhusu mada yoyote ya kodi iliyochagauliwa na washindi hupata zawadi. Mada inayojadiliwa katika mashindano ya mwaka huu ni ‘Mashine za Kodi za Kielektroniki’
Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Dk. Damas Ndumbaro akisisitiza jambo wakati akizindua mashindano ya vilabu vya Kodi kwa Shule za Sekondari katika Tamasha la Majimaji Serebuka linaloendelea Songea Mkoani Ruvuma. (Picha zote na Oliver Njunwa)
Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari mkoani Ruvuma wakifuatilia mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa shule za Sekondari katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Songea.
Mratibu wa Mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa Shule za Sekondari Mkoani Ruvuma Njovu Kilian akifafanua jambo kwa wananfunzi. Wengine ni Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Dk. Damas Ndumbaro (katikati) na Mwakilishi wa Benki ya NMB.
Wawakilishi wa mojawapo ya Shule za Sekondari ikiwasilisha mada wakati wa Mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa shule za Sekondari.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo akizungumza na wanafunzi (hawapo ktk picha) walioshiriki mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa Shule za Sekondari katika Tamasha la Majimaji Serebuka Mkoani Ruvuma. Waliokaa kutoka (kushoto) ni Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma, Rosalina Mwenda na Mratibu wa Mashindano ya Vilabu vya Kodi katika Shule za Sekondari TRA Njovu Kilian. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images