Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1612 | 1613 | (Page 1614) | 1615 | 1616 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye akizungumza kuhusu Serikali wanavyopanua wigo wa kutoa huduma kupitia bandari za Tanzania wakati wa ufunguzi wa kongamano la TPA na wafanyabiashara wanaotumia bandari za Tanzania kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Burundi, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Malawi na Comoro uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignatus Rubaratuka akizungumzia jinsi bandari za Tanzania zilivyojipanga imara kutoa huduma kwa wateja wao bila kuleta malalamiko kwa wateja wao ili kukuzu kipato cha nchi kupitia bandari hizo wakati wa kongamano la wafanyabiashara wanaotumia bandari za Tanzania kutoka nchi saba ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA) ili kuongeza ufanisi kwenye utendaji wa wabandari za hapa nchini.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko akizungumza kwenye kongamano la wafanyabiashara wanaotumia bandari za Tanzania kutoka nchi saba ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA) ili kuongeza ufanisi kwenye utendaji wa wabandari za hapa nchini.
  Baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wadau wa mbalimbali wanaotumia bandari ya Tanzania kutoka nchi saba wakiwa kwenye kongamano la wafanyabiashara wanaotumia bandari za Tanzania kutoka nchi saba ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA.
  Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye akiwa kwenye picha na wafanyabiashara kutoka nchini saba pamoja na wadau wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi Mkazi wa Azania Group Rwanda na Burundi, Mpagaze Jerome akizungumza na waandishi wa habari kuhusu faida pamoja na changamoto wanazozipata kwa kutumia bandari za hapa nchini.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiongozana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) baada ya kupokelewa  leo ofisi ndogo ya wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na viongozi wengine wa wizara hiyo akiwepo Naibu Waziri, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto),Katibu Mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima(wakwanza kulia).Wakwanza kushoto ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Balozi Hassan Simba Yahaya.Kikao hicho kimefanyika leo,jijini Dar es Salaam. 
  Naibu Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa kikao cha viongozi wakuu wa wizara hiyo,Waziri Kangi Lugola(watatu kulia), Katibu Mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima(wakwanza kulia) aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Balozi Hassan Simba Yahaya(wapili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili wa Vyama vya Kijamii, Marlin Komba(wakwanza kushoto).Kikao hicho kimefanyika leo,jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro baada ya kufika Ofisi ndogo ya wizara jijini, Dar es Salaam,leo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na Maafisa wa Jeshi baada ya kufika Ofisi Ndogo ya wizara,jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa Mkoa wa Mbeya akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makala wakitembea mwendo wa mchakamchaka alipokuwa akikagua eneo la Hifadhi ya Msitu wa Palamela wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.

  Na Hamza Temba, Mbeya
  .............................................................


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya uchimbaji wa mchanga wa madini ya dhahabu (makinikia) ndani Hifadhi ya Msitu wa Palamela katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

  Amesema sheria za uhifadhi na mazingira hazihusu mtu yeyote kuchimba madini katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria bila ya kuwa na kibali maalum kutoka mamlaka husika.

  Ametoa onyo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mwaoga, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya baada ya kukagua na kuona uharibifu mkubwa uliofanywa na wachimbaji hao kwenye hifadhi hiyo.

  "Yeyote anayehitaji kuchimba madini kwenye maeneo ya hifadhi ni sharti afuate taratibu za kisheria ikiwepo kupewa kibali halali cha kufanya kazi hiyo, la sivyo tutakaowakamata tutawachukulia hatua kali za kisheria" alisema Waziri Kigwangalla.

  Ili kudhibiti vitendo hivyo visiendelee, Waziri huyo ameagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuweka kituo cha kudumu cha ulinzi katika eneo hilo ili kuwazuia wananchi watakaojitokeza kufanya shughuli hizo za uharibifu wa hifadhi hiyo.

  Amesema, amebaini kuwa maeneo mengi makubwa ya uchimbaji wa madini katika wilaya hiyo yamemilikishwa matajiri wachache hali inayosababisha wananchi wa kawaida kukosa maeneo ya uchimbaji na hivyo kulazamika kuingia kwenye maeneo ya hifadhi.

  Kufuatia changamoto hiyo, Dk. Kigwangalla ameuagiza uongozi wa mkoa wa Mbeya na Wilaya ya Chunya kuona uwezekano wa kuwapa maeneo mbadala wachimbaji wadogowado katika maeneo ya wazi ili nao waweze kufaidika na rasilimali hiyo na hatimaye kuepuka uharibifu wa mazingira kwa kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa.

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala alisema kufuatia malalamiko ya wananchi hao juu ya uwepo wa matajiri wachache waliomilikishwa maeneo hayo ya uchimbaji, ndani ya wiki hii atamtuma Kamishna wa Madini wa Kanda na wataalam wengine kuchunguza ukweli wake pamoja na kubaini mahitaji halisi ya wananchi hao ili aweze kumshauri Waziri husika namna kumaliza mgogoro huo.

  Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Zawadi Mbwambo alisema sheria zinarubusu watu kuchimba madini kwenye maeneo ya hifadhi kwa kufuata taratibu maalum.

  Alizitaja taratibu hizo kuwa ni pamoja na kutambua eneo husika, mmiliki wake, kuomba leseni Wizara ya Nishati, kufanya tathmini ya athari za kimazingira na kama itathibitika kutokuwepo kwa athari hizo, muhusika atapewa leseni kutoka kwa Afisa Misitu wa Wilaya husika.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala wakikagua eneo lililoharibiwa kwa kuchimbwa mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wikaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mchanga wa dhahabu (makinikia) ambao umetaifishwa na Serikali baada ya kuchimbwa kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wikaya ya Chunya mkoani Mbeya jana. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Amos Makala.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi kwenye Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma bango lenye ombi la kutoa eneo la uchimbaji wa madini ya dhahabu ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Mwaoga, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi mkoani humo jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi kwenye Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mwaoga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi kwenye Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akiwa anafafanua jambo kwenye mkutano huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akizungumza katika mkutano huo.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Zawadi Mbwambo akifafanua kuhusu sheria na taratibu za uchimbaji madini kwenye maeneo ya hifadhi.

  0 0


  0 0


  0 0  Nd. Innocent Mgeta Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Afisa Udahili Mwandamizi akitoa maelezo juu ya programme mbalimbali za mafunzo zinazotolewa na Chuo kikuu Mzumbe kwa Mzumbe mzazi aliefika kupata huduma hiyo katika Banda la Chuo kikuu Mzumbe kwenye maonesho ya sabasaba
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof Lughano Kusiluka akitoa huduma kwa waombaji waliofika kupata elimu kuhusu Mfumo wa Udahili wa wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka wa fedha 2018/19. Huduma ya udahili inatolewa katika Banda la Chuo katika maonesho ya 42 ya SABASABA
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof Lughano Kusiluka akikagua baadhi ya vitabu vilivyoandikwa na wahadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe , Kushoto ni Nd. Benjamin Jonas Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya 42 ya SABASABA.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof Lugano Kusiluka akitoa maoni kwa Nd. Baasha kutoka Idara ya TEHAMA kuhusu Mfumo wa Usimamizi na menejiment ya hospitali za umma “GOTHOMIS” ulioandaliwa na Chuo hicho kupitia mradi wa VLIR-UOS alipotembelea Banda la Chuo katika maonesho ya 42 ya SABASABA

  0 0


  Picha ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na Masuala ya Afya, ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na masuala ya Afya wakati akiwa katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
  Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage baada ya kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
   
   

  NA WAMJW-DAR ES SALAAM 

  KIWANDA kikubwa cha kutengeneza dawa kinatarajiwa kujengwa nchini ili kupunguza adha na gharama zinazoikumba nchi wakati wa kuagiza dawa nje ya Tanzania. 

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kujadili uwekezaji wa kiwanda cha dawa hapa nchini leo jijini Dar es salaam. 

  "Leo tumekutana kujadili jinsi ya kuwekeza na kiwanda cha kutengeneza dawa cha FOSUN PHARMA kutoka nchini ili kupunguza changamoto za kuagiza dawa nje ya nchi na kutokomeza tatizo la upatikanaji wa dawa nchini", alisema Waziri Ummy .
   
   Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na kujengwa kwa kiwanda hiko kitapunguza asilimia kubwa ya fedha inayokwenda nje kwa ajili ya manunuzi ya dawa kwani mpaka sasa asilimia 94 ya fedha zinakwenda kununua dawa nje na asilimia 6 ndiyo inannua dawa nchini. 

  Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na uwekezaji huo kutapelekea kupunguza muda wa kuagiza dawa kwani muda mwingine kunachukua miezi 9 mpaka miezi 11 kupata dawa kutoka nje ya nchi hivyo kuifanya Serikali kuagiza mzigo mkubwa zaidi ili kukimbizana na mahitaji ya Watanzania. 

  "Tunatumia mda mrefu sana kupata dawa tangu tunapoagiza na wakati mwingine tunaweza kupata dawa zisizo na ubora kutokana na dawa hizo zinakaguliwa na mdhibiti wa nje hivyo zinaweza zikaruhusiwa tu na zikija kukaguliwa na mdhibiti wa ndani unaweza kukuta hazina ubora" alisema Waziri Ummy. 

  Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kampuni hiyo inayotengeza sindano za kutibu Maralia kali ya ATESUNAT itaweza kutengeneza sindano nyingi zaidi na kuweza kuwahudumia nchi jirani ikiwemo Kenya, Uganda na Burundi. 
   
   Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa hakuna kikwazo kwa Kampuni hiyo kuanzisha ujenzi wa kiwanda cha dawa hapa nchini kwani kitasaidia upatikanaji wa dawa kwa urahisi na kukua kwa uchumi kupitia viwanda. 

  "Tumejadili na kuwakubalia bila ya kuweka kikwazo kwani tumeridhishwa na ubora wao katika utengenezaji wa dawa na mafuta nchini kwao hivyo tunawakaribisha kuja kufanya uwekezaji huo" alisema Waziri Mwijage.  
   
  Naye Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Nchini Bw. Geofrey Mwambe amesema kuwa wameupokea uwekezaji huo na wanaufanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuipeleka Tanzania kuelekea uchumi wa Viwanda. 

  "Kutokana na ahadi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda na kutokomeza kabisa tatizo la uhaba wa dawa hatuna budi kushirikiana na wawekezaji hao kutimiza lengo hilo" alisema Bw. Mwambe. 

  Kika hiko cha kujadili uwekezaji wa kiwanda hiko cha kutengeneza dawa kimeudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, Bohari kuu ya Dawa MSD, Kituo cha Uwekezaji nchini TIC na wadau mbalimbali.
   

  0 0  0 0

  P01
  Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Property International Tanzania Leila Maingu akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wakati akizungumza kuhusu uuzaji wa viwanja katika miradi mbalimbali hapa nchini kutoka Kampuni hiyo.
  P1
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi akizungumza jambo na Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu katika banda la kampuni hiyo lililoko kwenye viwanja vya TANTRADE Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam ambapo maonyesho ya biashara ya Sabasaba yanaendelea
  P3
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi akizungumza jambo na Julius Charles ambaye yuko katika banda hilo ili kuwahamasisha watanzania kujipatia viwanja kwa bei rahisi kutoka kampuni hiyo.
  P4
  Wananchi mbalimbali wakimiminika kuingia katika banda hilo.
  P5P6
  Mmoja wa wafanyakazi akiwahudumia wananchi waliotembelea katika banda hilo.
  P7
  Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu paoja na wafanyakazi wenzake wakiwahudumia wananchi mbalimbali waliofika kwenye banda hilo.
  .....................................................................................
  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
  PROPARTY International Limited imewahimiza watumishi wa umma na hasa walimu na wauguzi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya kujipatia viwanja kwa bei nafuu.
  Tayari Proparty International Limted imesema kuanzia Julai mwaka jana wameuza viwanja kwa watumishi wa kada hizo wapatao 2000 lakini imeendelea kuwahimiza kuchangamkia fursa hiyo kupitia mradi maalumu wa viwanja ambao umetengwa kwa ajili yao.
  Hayo yamesemwa na Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu wakati anazungumzia kuhusu miradi mbalimbali ya viwanja ambayo wanayo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kumiliki kiwanja ambacho kimepimwa na kilicho maeneo sahihi kwa makazi.
  Akizungumza akiwa kwenye banda lao katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Maingu amesema kuwa wanayo miradi mingi ya “Tunawashauri walimu na wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya unafuu wa bei ya viwanja vyetu.Watapa viwanja kwa gharama nafuu kwani kuna punguzo la bei kwa ajili yao.
  “Tangu tuanze kuuza viwanja kwa ajili ya watumishi hao kwa mkoa wa Dar es Salaam muamko umekuwa mkubwa kwani wengi wamenunua.
  “Hata hivyo tunaendelea kuwasisitiza walimu na wauguzi ambao bado hawajununua viwanja waje na tutazungumza nao, lengo letu ni kuona watumishi wetu wanakuwa kwenye makazi salama,”amefafanua.
  Akifafanua zaidi kuwa wameingia mikataba na benki ya Amana , Tpb Bank, CRDB , PBZ na DC Bank ambapo wateja wanaonunua kiwanja kwa mkopo watalipa katika moja ya akanti za benki hizo.
  “Kwa wanaonunua kiwanja kwa mkopo kupitia benk ya PBZ mteja atatakiwa kugungua akaunti na kulipa asilimia 20 ya thamani ya kiwanja na kasha benki itampa asilimia 80 na marejesho ni miaka mitano,”amesema.
  Wakati kwa Amana Bank malipo ya awali ni asilimia 20 na baada ya hapo mteja atapewa asilimia 80 na marejesho yake ni mwaka mmoja au mwaka mmoja na nusu.
  Pia Tpb Bank mteja baada ya kufungua akaunti na kulipa malipo ya awali ya asilimia tano ya thamani ya kiwanja na benki ndipo itampa mkopo wa asilimia 95 na marejesho hadi miaka mitatu.
  Amesema kwa benki ya CRDB mteja atalipa malipo ya awali asilimia 20 ya thamani ya kiwanja na baada ya hapo benki itamuwezesha kupata asilimia 80 na marejesho ni hadi miaka mitatu.
  Amewaomba Watanzania kununua viwanja kutoka kwenye moja ya miradi yao kwani gharama yake ni nafuu na kubwa zaidi maeneo yao yamepimwa na wameweka utaratibu maalumu ambao unawafanya kuwa karibu na wateja wao.
  P01
  Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Property International Tanzania Leila Maingu akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wakati akizungumza kuhusu uuzaji wa viwanja katika miradi mbalimbali hapa nchini kutoka Kampuni hiyo.
  P1
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi akizungumza jambo na Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu katika banda la kampuni hiyo lililoko kwenye viwanja vya TANTRADE Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam ambapo maonyesho ya biashara ya Sabasaba yanaendelea
  P3
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi akizungumza jambo na Julius Charles ambaye yuko katika banda hilo ili kuwahamasisha watanzania kujipatia viwanja kwa bei rahisi kutoka kampuni hiyo.
  P4
  Wananchi mbalimbali wakimiminika kuingia katika banda hilo.
  P5P6
  Mmoja wa wafanyakazi akiwahudumia wananchi waliotembelea katika banda hilo.
  P7
  Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu paoja na wafanyakazi wenzake wakiwahudumia wananchi mbalimbali waliofika kwenye banda hilo.


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  PROPARTY International Limited imewahimiza watumishi wa umma na hasa walimu na wauguzi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya kujipatia viwanja kwa bei nafuu.
  Tayari Proparty International Limted imesema kuanzia Julai mwaka jana wameuza viwanja kwa watumishi wa kada hizo wapatao 2000 lakini imeendelea kuwahimiza kuchangamkia fursa hiyo kupitia mradi maalumu wa viwanja ambao umetengwa kwa ajili yao.

  Hayo yamesemwa na Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu wakati anazungumzia kuhusu miradi mbalimbali ya viwanja ambayo wanayo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kumiliki kiwanja ambacho kimepimwa na kilicho maeneo sahihi kwa makazi.

  Akizungumza akiwa kwenye banda lao katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Maingu amesema kuwa wanayo miradi mingi ya “Tunawashauri walimu na wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya unafuu wa bei ya viwanja vyetu.Watapa viwanja kwa gharama nafuu kwani kuna punguzo la bei kwa ajili yao.

  “Tangu tuanze kuuza viwanja kwa ajili ya watumishi hao kwa mkoa wa Dar es Salaam muamko umekuwa mkubwa kwani wengi wamenunua.“Hata hivyo tunaendelea kuwasisitiza walimu na wauguzi ambao bado hawajununua viwanja waje na tutazungumza nao, lengo letu ni kuona watumishi wetu wanakuwa kwenye makazi salama,”amefafanua.Akifafanua zaidi kuwa wameingia mikataba na benki ya Amana , Tpb Bank, CRDB , PBZ na DC Bank ambapo wateja wanaonunua kiwanja kwa mkopo watalipa katika moja ya akanti za benki hizo.

  “Kwa wanaonunua kiwanja kwa mkopo kupitia benk ya PBZ mteja atatakiwa kugungua akaunti na kulipa asilimia 20 ya thamani ya kiwanja na kasha benki itampa asilimia 80 na marejesho ni miaka mitano,”amesema.Wakati kwa Amana Bank malipo ya awali ni asilimia 20 na baada ya hapo mteja atapewa asilimia 80 na marejesho yake ni mwaka mmoja au mwaka mmoja na nusu.Pia Tpb Bank mteja baada ya kufungua akaunti na kulipa malipo ya awali ya asilimia tano ya thamani ya kiwanja na benki ndipo itampa mkopo wa asilimia 95 na marejesho hadi miaka mitatu.Amesema kwa benki ya CRDB mteja atalipa malipo ya awali asilimia 20 ya thamani ya kiwanja na baada ya hapo benki itamuwezesha kupata asilimia 80 na marejesho ni hadi miaka mitatu.

  Amewaomba Watanzania kununua viwanja kutoka kwenye moja ya miradi yao kwani gharama yake ni nafuu na kubwa zaidi maeneo yao yamepimwa na wameweka utaratibu maalumu ambao unawafanya kuwa karibu na wateja wao.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

  MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emanueli Maganga amewaagiza wakuu wa wilaya za Kibondo na Kakonko pamoja na Wahandisi wa Wilaya hizo kuweka kambi katika Kata ya Muhange kuhakikisha wanasimamia mradi wa maji wa Muhange unatoa maji kwa wananchi ndani ya wiki mbili.

  Kauli hiyo aliitoa wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi ya maji ndani ya Wilaya ya Kakonko ambapo amesikitishwa na kitendo cha mradi wa maji Muhange kutokamilika licha ya kwamba ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2012 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na ulitarajiwa kukamilika Desemba mwaka 2013.

  Brigedia Maganga amesema ni jambo la kushangaza kuona wananchi wanaendelea kupata shida ya maji huku mradi ukiwa umefungwa kwa changamoto ndogondogo ambazo zinaweza kufanyiwa marekebisho na ukizingatia mradi huo unasimamiwa na Wilaya mbili na Wahandisi wawili.
  Hivyo amewataka kutenga muda wa siku mbili kufika katika Kijiji cha Muhange kushirikiana na wananchi kukamilisha mapungufu ya mradi huo. 

  "Ukiwa Mhandisi kazi yako ni kukaa sehemu ya mradi hadi mradi utakapo kamilika, kama mngekuja kukaa hapa changamoto hizi zisingejitokeza mme waachia wakandarasi wafanye mradi kwa kiwango cha chini, wananchi wanapampu maji yana ishia chini na haya wafikii na wananchi wanaendelea kuteseka", amesema Brigedia Maganga.

  Ameongeza kuwa " Wakuu wote wa wilaya mbili kaeni na hii kamati ya watumia Maji na wataalamu wenu mje hapa na Jumuiya ya Watumia maji kama tatizo la mabomba mtafute maeneo yanayo vuja yafanyiwe ukarabati kama kuna tatizo la kisiasa litajulikana suala ni kwenye utendaji na utekelezaji mpaka maji yaende kwenye gati zote 24 wananchi wapate maji".

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya kakonko Kanali Hosea Ndagala alipokea maelekezo hayo na kuahidi kwenda kukaa pamoja na viongozi hao na kujadili mbadala wa kufanya haraka ilikuweza kukamirisha lengo la Serikali kufadhili miradi hiyo kwa wananchi .

  Nae Mhandisi wa Wilaya ya Kibondo Michael Nguruwe amesema mradi huo ulikuwa ukisimamiwa na Wilaya hiyo na Mradi uliukaguliwa ,baada ya kukamilika Kwa mradi huo wakati wa kufanya majaribio mradi ulitoa maji kwa magati yote 24 na matatizo hayo yamejitokeza baada ya wananchi kuanza kutumia mradi huo.

  Amesema mradi unapokuwa hautumiki kwa muda mrefu matanki yanakauka na miundombinu inaharibika hali hiyo inaweza kusababisha mabomba kupasuka na tanki kuanza kuvuja na aliomba wakae pamoja na wataalamu wa Wilaya ya kakonko kufanya marekebisho na kupita kila eneo ambalo linavuja.

  Diwani wa Kata ya Muhange Ibrahimu Katunzi amesema ukweli ni kwamba maji wanapo yaruhusu kwenda kwa wananchi bomba zinapasuka, bomba zilizowekwa hazina ubora na wanapata hasara kwa kuwa maji yote yanaishia njiani na hayawafikii wananchi na kufanya jumuia ya watumia maji kushindwa kuendesha mradi huo.

  Amesema kwenye chanzo kinachotakiwa kuruhusu maji kuingia kwenye tanki tanki halina chujio hivyo tope na vyura vinajaa kwenye tanki na hivyo kupelekea maji kusukumwa kwa kasi ndogo hali iliyo pelekea Wananchi wa Kata hiyo kuukataa mradi huo.Nao baadhi ya wananchi wa vijiji vya Muhange ya juu na chini Simoni Matulane na Anitha Ntibagomba wamesema wananchi wanapata shida kufuata maji wengine wanaamka saa 11 alfajiri kufuata maji baadhi mpaka wanaingilia mito iliyoko mipakani kwa ajili ya kufuata maji.

  Wameiomba Serikali kuwasaidia wananchi kukamilisha mradi huo na utakapo kamilika wananchi wataendelea kuchangia na kuendesha miradi hiyo kama inavyo elezewa.

  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma pamoja na Mradi huo alitembelea miradi miwili ya Nyagwijima na Gwanumpu ambapo katika miradi hiyo yote alibaini baadhi ya mapungufu na kuahidi kupeleka mafuta katika mradi wa Nyagwijima kupampu maji na kuhakikisha kama maji yanawafikia Wananchi na Wataalamu wanatakiwa kurejebisha miradi hiyo wananchi waanze kupata huduma. 
  MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emanueli Maganga akizungumza na baadhi ya viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya za Kibondo na Kakonko pamoja na Wahandisi wa Wilaya hizo kuweka kambi katika Kata ya Muhange kuhakikisha wanasimamia mradi wa maji wa Muhange unatoa maji kwa wananchi ndani ya wiki mbili. 
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga katikati akioneshwa moja ya tanki la maji na Muhandisi Michael Nguruwe (kushoto),katika Katika Kata ya Nyagwijima wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Jana,pichani kulia ni Muhandisi Elinatha Elisha

  0 0

  WAZIRI wa viwanda na Biashara Charles ametoa angalizo kwa watu ambao wamepewa shamba la kupanda miwa mkoani kigoma kuhakikisha kuanza kazi hiyo na akikuta shamba hilo bado halijaendelezwa atawanyan'ganya na kutoa fursa kwa wengine.

  Alisema lengo la serikali nikutaka kuona ifikapo mwaka 2022 Tanzania inadhalisha tani laki sita na kuwezesha nchi kuwa na sukari ya kutosha ikilinganishwa na ilivyo sasa.Waziri mwijage aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa wa Kliniki ya Biashara yenye lango la kusaidia ukuaji wa biashara, na kuimarisha mazingira wezeshi ya biashara kwa wafanyabiashara

  Alisema kuwa kuna uwazishwaji wa mashamba matatu mapya kwa ajili ya kuzalisha miwa ambayo wamepewa wafanyabiashara katika maeneo ya Bagamoyo, Morogoro, pamoja na mkoani Kigoma.Akizungumzia uzinduzi wa Kliniki hiyo ya biashara Waziri Mwijage amezitaka mamlaka husika kufanya kazi katika sura ya kibinadamu kwa wafanyabishara na si kuwapelekea polisi jambo ambalo mfanyabiashara anatakiwa apewe elimu.

  Ameongeza kuwa katika kuelekea Tanzania viwanda wamefika pazuri na wanaendelea kuhamasisha kujenga viwanda vya dawa pamoja na mafuta ya kula ambayo hivi sasa yanaagizwa zaidi kutoka nje ya ya nchi.Kwa upande wake Naibu waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Hassan Hafidh akizingumza katika maonesho hayo amesema amefarijika mno kuona asilimia kubwa ya bidhaa zilizopo hapo ni za watanzania.

  Naye Naibu waziri wa viwanda na biashara Stellah Manyanya ameeleza kuwa lengo kubwa ni kukimbia kuelekea mafanikio na amehaidi kuendeleza suala ambalo waziri amelianzisha na ameshauri wananchi kutoa maoni pindi wanapokutana na mambo yasiyo sawa na kupewa msaada.Pia amewaomba wananchi kutambua dhamira ya dhati ya serikali na kuiunga mkono na kuwa wawazi na amewataka kulipa kodi kwa wakati.

  Naye katibu wa wamiliki wa wenye viwanda Tanzania CTI Leodgar Tenga amemshukuru Mwijage kwa kufungua kliniki hiyo na kueleza kuwa wenye viwanda wanachukia sana urasimu na wapo pamoja katika kupeleka nchi kwenye uchumi wa kati.

  Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ua uongozi wa Rais Magufuli na Wizara husika na amehaidi kutoa ushirikiano kwa serikali katika ujenzi wa viwanda na wameomba uendelevu wa kliniki hiyo.
  Waziri wa Viwanda na Biashara,Cherles Mwijage akizindua kliniki ya Biashara katika Maonesho ya kimataifa yanayo fanyika Sabasaba jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
  Waziri wa Viwanda na Biashara,Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa biashara katika hafla ya uzinduzi wa kliniki ya Biashara uliofanyika katika maonesho ya kimataifa yanayo fanyika Sabasaba jijini Dar as Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe amemtembelea Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo  ili kujadiliana  masuala mbali mbali yanayozikabili wilaya zao. Waheshimiwa hawa waliweza kuangalia uzinduzi wa kitabu cha Dr. Reginald Mengi "I CAN, I MUST, I WILL".

   Katika uzinduzi huo ambao Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alimpongeza Dkt. Regnald Mengi kwa maisha yake ya mfano ambapo hakukata tamaa licha ya changamoto nyingi kumkabili kiuchumi na kimaisha. 

   Mhe. Dkt. Magufuli alizungumzia pia namna ambavyo kuna watu ni wataalamu wa kukatisha tamaa wenzao. Hata Serikali inakutana na changamoto hizo za kukatishwa tamaa. Mfano ni Sera ya Elimu Bure, Ujenzi wa Reli ya SG, Mradi mkubwa wa Umeme wa Stiglers Gorge ambapo uliasisiwa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Nyerere n.k 

   Aidha wakuu hao wa Wilaya walijadiliana namna ambavyo kama wanawake viongozi wanahakikisha wanawasaidia wanawake wenzao kujikwamua kutoka kwenye umasikini. Wanawake ni nguzo muhimu sana katika kuwaingiza Watanzania kwenye Uchumi wa Viwanda na Uchumi wa Kati. Nani asiyejua wachapa kazi wakubwa duniani kote ni Wanawake? Tatizo ni kuwa waliachwa nyuma kwa sababu mbalimbali ikiwemo Mfumo Dume, Sheria na Mila Kanzamizi hasa kwenye Umiliki wa Ardhi na njia nyingine za Uzalishaji Mali, Elimu, Afya, Ukosefu wa Mitaji na Mikopo nafuu n.k 

   Baada ya Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Magufuli kutangaza kwa nguvu zote Sera ya Viwanda na Uchumi wa Kati; wanawake wamekuwa na muitikio mkubwa sana. Matokeo ChanyA+ yanaonekana kila mahali. 

   Aidha waliweka mikakati mbalimbali ya kimaendeleo hasa kuangalia namna ambavyo wataweza kushirikiana Wilaya ya Gairo na Morogoro katika shughuli za maendeleo hasa kwa wanawake ili tufikie 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030 SDG's Goal #5. 

   Wanawake ni nguzo muhimu ya kujenga uchumi imara Tanzania. Stay tuned; "The greater things are yet to come!." Ma DC wanawake Morogoro ni wawili tu na wanachapa kazi kwa pamoja kama sisters. Mhe. Regina Chonjo and Mhe. Siriel Mchembe (Iron ladies) katika ubora wao.  Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo (kushoto) akimkaribisha mgeni wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (kulia) wakati alipomtembelea mapema jana ili kujadili maendeleo ya wilaya zao.
  Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo (kushoto) akimkaribisha mgeni wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (kulia) wakati alipomtembelea mapema jana ili kujadili maendeleo ya wilaya zao.

  0 0

  Na Lorietha Laurence-WHUSM, Mbulu

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mjini kuhakikisha wanatengeneza miundo mbinu ya michezo hususani viwanja vya michezo.

  Akizungumza wakati wa fainali za kombe la Issay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay jana mjini hapo , lengo ikiwa ni kutoa hamasa ya michezo kwa wakazi wa eneo hilo. “Ni jukumu la viongozi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa kila mwaka wanatenga fedha katika bajeti zao ambazo zitasaidia katika kuboresha miundo mbinu ya michezo ” amesema Mhe. Juliana Shonza.

  Anazidi kueleza kuwa michezo ni muhimu sana kwa jamii,mbali na kuwaleta watu pamoja imekuwa ni chanzo kizuri cha ajira kwa vijana na hivyo kuwasaidia katika kukuza uchumi wao binafsi. idha Mhe. Juliana Shonza amempongeza Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe.Zacharia Isaay kwa kuhamasisha michezo na juhudi alizozionyesha katika kufanikisha mashindano hayo na kuwaomba wadau na wananchi wengine kuunga mkono juhudi hizo.

  Vilevile aliwataka Maafisa Michezo kuhakikisha wanaweka mikakati mbalimbali ya kuhimiza michezo mashuleni ili kuweka hamasa kwa wanafunzi kupenda na kujihusisha na michezo. wa upande wake Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay alimshukuru mgeni rasmi kwa kuweza kufunga mashindano hayo na kuaahidi kuendelea kutoa hamasa ya michezo kwa wananchi wa Halmashauri ya Mbulu Mji na Vitongoji vyake.

  Mashindano ya Isaay Cup yalianza tarehe 15 mwezi wa tano na kumalizika tarehe 20 ya mwezi wa sita kwa ngazi ya Tarafa, na baadaye kuingia katika ngazi ya Jimbo kuanzia tarehe 21 mwezi wa sita mwaka huu huku yakishirikisha jumla ya michezo 26 ikiwemo riadha, mpira wa miguu, mpira wa nyavu na netball .
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiongea wakati wa kufunga mashindano ya Kombe la Isaay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay lengo ikiwa ni kutoa hamasa ya michezo kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu pamoja na vitongoji vyake.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (mwenye kipaza sauti ) akitoa nasaha kwa timu zizizoingia fainali ambazo ni Home Boys na Bodaboda Fc kabla ya mechi ya kutamfuta mshindi wa kwanza katika mashindano ya kombe la Issay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay jana mjini hapo.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na wachezaji wa kike wa mpira wa miguu kutoka shule ya Sekondari ya Chief Sarwatt ambao waliibuka washindi dhidi ya shule ya Sekondari ya Nowu wakati wa fainali ya Kombe la Isaay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe.Zacharia Isaay hapo jana .
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimkabidhi zawadi mshindi wa mbio za kilomita 10 kwa upande wa wanawake Bibi. Olivia Alfred wakati wa kufunga mashindano ya kombe la Isaay kulia ni Mbunge wa Mbulu mjini aliyeandaa mashindano hayo Mhe. Zacharia Isaay na kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bibi.Sarah Sanga.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akikabidhi kombe kwa timu ya mpira wa miguu ya Bodaboda Fc ambao waliibuka washindi dhidi ya wapinzani wao Home Boys Fc wakati wa fainali za kombe la Isaay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay hapo jana.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,MBULU MJINI).

  0 0


  Na Lorietha Laurence-WHUSM,Mbulu Mjini

  Serikali imeandaa mpango wa kuwaenzi watu mashughuri wakiemo wanamichezo wakongwe ambao wamewahi kuliletea taifa heshima katika mashindano mbalimbali akiwemo mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari.

  Hayo yamesemwa leo Mbulu Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipomtembelea mwanariadha huyo nyumbani kwake ambapo alipata fursa ya kuona medani , tuzo na vikombe alivyowahi kushinda mwanariadha huyo.

  “ Sisi kama Wizara tumeanzisha kampeni ya Uzalendo ambapo mwaka jana tuliwaenzi wasanii wa zamani wa muziki na mwaka huu mnamo Oktoba 14 ni zamu ya wanamichezo wakongwe akiwemo Bw. John Akwhari ” amesema Mhe. Shonza .Alizidi kueleza kuwa amevutiwa na jinsi mwanariadha huyo anavyotunza kumbukumbu zake huku akiwataka wanamichezo na watu wengine kuiga mfano huo bora ili kuviwezesha vizazi vijavyo kupata historia nzuri katika sekta ya michezo.

  Naye Mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari amesema amefurahi kuona Serikali inatambua na kuthamini mchango wake katika sekta ya michezo na kuhaadi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kwa pamoja kuleta maendeleo katika sekkta hiyo muhimu. 
   
   Bw. John Akwhari ni mwanariadha wa zamani wa Tanzania wa kwanza kufungua milango ya kushiriki riadha nje ya nchi ambapo alijizolea umaarufu katika mashindano ya mwaka 1968 ya Olimpiki nchini Mexico ambapo licha ya kuwa wa mwisho aliueleza umati kuwa nchi yake ilimtuma kumaliza mbio na siyo kuanza mbio.
   Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Kushoto)  akiangalia vikombe vya ushindi alivyowahi kushinda Mwanariadha Mkongwe Bw. John Akwhari (Kulia) alipofanya ziara ya kutembelea nyumbani kwake Mjini Mbulu hapo Jana.

   

  0 0


  Mkurungezi mtendaji wa Azania Bank Charles Itembe akitoaa hotuba kwa wageni waalikwa wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akitoa hotuba kwa wageni waalikwa wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akimpongeza Mkurungezi mtendaji wa Azania Bank Charles Itembe mara baada ya uzinduzi wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Naibu waziri wa viwanda na biashara Stellah Manyanya wakifungua kitambaa wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya wafanyabiasharaa na wagon waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Azania Bank wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Viwanda na Biashara,Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa biashara katika hafla ya ukizindua wa kliniki ya Biashara uliofanyika katika maonesho ya kimataifa yanayo fanyika Sabasaba jijini Dar as Salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akipata maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa Azania Bank kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo mara baada ya uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Azania bank mara baada ya uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

  Ni benki ya kwanza ya kiasili inyowezesha huduma zote za kifedha sehemu moja kwenye Kliniki ya Biashara iliyopo kwenye maonyesho ya Sabasaba

  Benki ya Azania (ABL) ambayo ni benki binafsi ya kiasili hapa nchini, imeelezea nia yake ya kuendelea kusaidia sekta mbali mbali za kiuchumi kwa kutoa huduma mahususi za kifedha hususani katika kipindi hiki cha maonyeshao ya kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Charles Itembe alisema lengo la benki hiyo ni kutoa huduma za kifedha kwa wazalishaji bidhaa, viwanda pamoja wakulima kwa ajili ya kusaidia kukuza biashara zao.

  Kliniki hiyo ambayo itatoa huduma zote za ushauri wa masuala ya kibiashara sehemu moja, imeundwa na mamlaka ya Kuendeleza Biashara Tanzania (TANTRADE)

  Ikiwa na kauli mbiu “Kusaidia Maendeleo Endelevu na ukuaji wa Biashara”, Kliniki hiyo itakuwa ni ya kwanza na ya aina yake ambayo itatoa ushauri kwa aina mbali mbali za biashara ikiwa ni pamoja na biashara ndogo, za kati na kubwa ambazo zitakuwa zinashirikim katika maonyesho ya Sabasaba

  Mkurugenzi huyo alisema benki ya Azania inatoa huduma mbali mbali za kifedha ikiwa ni pamoja na mikopo ya biashara, mikopo binafsi, mikopo ya nyumba na mikopo hiyo hutolewa kwa riba ndogo.“Tunawakaribisha watu wote wanaoshiriki maonyesho ya Sabasaba na wanaokuja kutembea kwenye banda letu kwa ajili ya kupata huduma zan kifedha,” alisema

  Alitaja baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ni pamoja na kusaidia bishara za kuuza bidhaa nje ya nchi na kuingiza ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na malighafi zinazotumika viwandani, kusaidia wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa za kilimo, kusaidia kutoa mitaji ya uendeshaji wa viwanda, kutoa dhamana ya kibenki kwa ajili ya kusaidia miradi ya miundombinu, biashara.

  “Tunaamini kupitia mchango wetu wa huduma za kifedha kwenye sekta ya viwanda na kilimo tutakuwa tumeiunga mkono Serikali kufikia lengo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kufikia mwaka 2025,” alisema

  Itembe aliipongeza TANTRADE kwa kufungua Kliniki ya Biashara ambayo itawaleta pamoja wadau mbali mbali wa biashara kutoka sekta binafsi na umma watakao toa majibu kwa changamoto mbali mbali za kibiasaha na kuongeza kuwa benki ya Azania ni moja ya wadau ambao watakuwepo kwenye kliniki hiyo kwa ajili ya kutoa suluhisho na ushauri kuhusiana na mambo mbali mbali ya kibiashara

  Maonyesha ya Sabasaba ya mwaka huu ni ya 42 na yanabeba kauli mbiu “Undelezaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda “

  0 0

  NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA.

  SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imemwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Igunga (OCD)Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika(AMCOS) vinne kwa tuhuma za ununuzi wa pamba chafu na kuvisababishia kila chama kupigwa faini ya 500,000/-.na kufungiwa na Bodi ya Pamba

  Agizo hilo lilitolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa Mkutano maalumu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo mjini Igunga baada ya kupokea taarifa ya ukaguzi wa Bodi ya Pamba ulifanywa kwenye vyama vya Msingi mbalimbali.

  Viongozi ambao wamekatwa ni Makatibu Meneja na Wenyeviti kutoka Vyama vya Msingi Ushirika vya Mwamakona, Mwajojababi Mbutu, Kining’inila na Mwanyagula.Alisema uongozi wa Chama cha Msingi Mwamakona wanatuhumiwa kwa ununzi wa pamba chafu na kutumia vitabu vya kampuni ya Gaki kukusanya madeni kinyume cha maagizo ya Bodi ya Pamba kutaka watumie vitabu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo.

  Mwanri alisema uongozi wa Mwajojababi Mbutu AMCOS ulinunuu pamba chafu na kile cha Kining’inila AMCOS wanatumiwa kwa ununuzi wa pamba chafu , ununuzi wa pamba nje ya ghala , hakitumii kitabu cha stakabadhi ya mazao na kukosa takwimu.Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa uongozi wa chama cha Msingi cha Mwanyagula unatuhumiwa kwa kununua pamba kutoka kwa wakulima wa Kijiji kingine na hivyo kusababu ukwepaji wa madeni ya mbegu.

  Alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Igunga kuhakikisha Viongozi wengine watatu wanaotumiwa ambao hakuwepo kwenye kikao hicho watafutwe na wakamatwe ili waunganishwe na wenzao watano ambao wameshakamatwa.Mwanri alisema viongozi hao watashikiliwa hadi hapo watakapolipa faini hiyo kutoka mfukoni mwao na sio kutoka kwenye fedha za AMCOS.

  Aliwaonya viongozi wa AMCOS ambao wananunua pamba toka vijiji jirani kwa sababu vinasababisha ukwepeshaji madeni.Aidha Mkuu huyo Mkoa aliwapongeza viongozi wa Itunduru AMCOS kwa kukutwa na Bodi ya Pamba wakitumia vitabu sahihi na kununua pamba safi tu.Mwanri aliwaonya viongozi wa Mwamashimba, Ipumbulya na Bukama kwa upokeaji wa pamba ya vijiji vingine.

  Awali Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Igembensabo alimuomba Mkuu wa Mkoa kusaidia kuvibana vyama vya msingi ili viweze kurejesha madeni ya mbegu kwa kuzuia utoroshaji wa pamba nje ya maeneo husika.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri akitoa amri leo ya kukamatwa viongozi wa AMCOS nne zilizonunua pamba chafu na kukusanya madeni kwa vitabu visivyo halali.
  Baadhi ya watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Igunga mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri kutoa amri ya kuwamata kwa tuhuma za kununua pamba chafu. Watuhumiwa hao walikamatwa jana mjini Igunga wakiwa katika Kikao Maalumu cha Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu Rugambwa (kulia), akiwa na viongozi wenzake kutoka Wizara ya ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dar es Salaam leo wakati wakiupokea ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya Afya kutoka kampuni ya Kimataifa ya Fosun kutoka China, ambao wamekuja kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba. 
  Mkutano na wawekezaji hao ukiendelea. 
  Mkutano ukiendelea. Katikati kulia ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Charles Mwijage.
  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (wa nne kutoka kushoto) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo kutoka China. Wa tatu kutoka kushoto ni Rais wa Fosun Pharma,Willium Yifang WU.


  Na Dotto Mwaibale.

  WIZARA ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wamepokea ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya Afya kutoka kampuni ya Kimataifa ya Fosun kutoka China, ambao wamekuja kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba. 

  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (Mb.) ameeleza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha viwanda vinajengwa nchini ili kupunguza mzigo wa kununua dawa nje ya nchi kwa gharama kubwa,kupoteza ajira na pato la serikali.

  Kwa upande wake,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema asilimia 94 ya fedha za bajeti zinazotengwa kwa ajili ya kununua dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara hupelekwa nje ya nchi,na asilimia 6 tu ndio hununua kutoka viwanda vya ndani.Hii ni kwa sababu hakuna viwanda vinavyoweza kuzalisha dawa tunazozihitaji.

  Wataalamu walioshiriki majadiliano na wawekezaji hao ni pamoja na Bohari ya Dawa(MSD),Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC),Mamlaka ya Uwekezaji(EPZ) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

  Rais wa Fosun Pharma,Willium Yifang WU amesema ili wawekeze wanahitaji ardhi ekari 10 kwa ajili ya kuanzisha kiwanda.Kwa mujibu wa Waziri Mwijage wawekezaji hao wakiwa tayari serikali itawapatia eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho cha dawa.

  0 0

  Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga akiongoza mkutano wa kimataifa wa nchi 12 uliofanyika Nairobi Kenya mapema wiki iliyopita. Mkutano huo umekwisha mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga akijadiliana jambo na mshiriki wa mkutano huo kutoka Botswana, Tumelo Keay.
  Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga akijadiliana jambo na mshiriki wa mkutano huo kutoka, Rwanda.
   Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Afrika.
    Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Afrika. Kushoto ni Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel.
  Washiriki wa mkutano huo kutoka nchi 12 za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani maafufu Profesa Maji Marefu.

  Bw. Ngonyani ambaye alifariki dunia Julai 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi ameagwa leo (Jumatano, Julai 4, 2018) katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanafamilia, wabunge, wananchi wa Korogwe pamoja na Watanzania kwa ujumla. Amewataka waendelee kumuombea marehemu.

  “Natoa pole kwa wake wa marehemu, watoto na nawaomba tuendelee kuwa wavumilivu na watulivu katika kipindi hiki. Tulimpenda sana lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,”.Kwa upande wake, Katibu wa Bunge, Bw, Stephen Kagaigai akisoma wasifu wa marehemu amesema Bw. Ngonyani alizaliwa Mei 25, 1956 katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

  Bw. Kagaigai amesema marehemu alianza kuugua Juni 17 mwaka huu na Juni 18 alilazwa katika Hopitali ya Mkoa wa Dodoma na Juni 20 alihamishiwa katika Hopitali ya Muhimbili.Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi. Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Wabunge na wanafamilia.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, JULAI 4, 2018.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji kuuga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijijini Dar es salam, Julai 4, 2018. 
  Wapambe wa Bunge wakiwa wameubeba mwiili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stehen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza waombolezaji katika kuuga mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Hilary Ngonyani kwenye Viwanja via Karimjee jijini Dar es salaam Juli 4, 2018. 
  Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza Katika tukio la kuuaga mwiili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai wakisikiliza salamu mbalimbali za waombolezaji kabla ya kuaga mwiili wa mbunge wa Korogwe Vijijini , Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson , Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi, John Kijazi na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia wakati alipowaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda (kushoto) wakati alipoongoza waombolezaji kuuga mwili wa mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye viwanja vya Karaimjee jijini Dodoma Julai 4, 2018. Wapili kulia ni Spika wa Bunge Job, Ndugai na wapili kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imewaalika watanzania wenye dhamira ya kuanzisha viwanda nchini kutembelea banda lao katika msimu huu wa sabasaba ili kupata msaada na miongozo kutoka katika mamlaka hiyo.

  Akizungumza na Michuzi blog Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza ameeleza kuwa katika msimu huu wa sabasaba wanasherehekea mafanikio ya mamlaka hiyo kwa miaka 15, kuanzia 2003 hadi 2018 na katika kusherekea mafanikio hayo wanatoa elimu mbalimbali katika kuhakikisha uelewa kuhusiana na mamlaka hiyo unakua zaidi.

  Simwanza ameeleza kuwa kama mamlaka wanatoa mwaliko kwa wanaotaka kuanzisha viwanda nchini,katika kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli ya kuimarisha uchumi wa nchi kama mamlaka watatoa miongozo na elimu kwa wananchi wote watakaotaka kuanzisha viwanda nchini na kuwapatia miongozo ya kufikia malengo yao kwa viwanda watakavyoanzisha vikiwemo viwanda vya vyakula, dawa na vifaa tiba.

  Akieleza kuhusiana na mafanikio ya mamlaka hiyo Simwanza ameeleza kuwa, wananchi wamekuwa na uelewa kuhusiana na bidhaa ambazo zimepigwa marufuku na mamlaka hiyo na bado wanajitahidi kuhamasisha katika kutoa elimu zaidi.

  Aidha ameeleza kuwa kama mamlaka wataendelea na shughuli ya kudhibiti bidhaa ambazo si faafu kwa matumizi ya binadamu na elimu kuhusiana na bidhaa wanazozisimamia itaendelea.Simwanza ametoa wito kwa wananchi wote kutumia bidhaa zilizoainishwa na mamlaka hiyo na kutoa taarifa pindi waonapo biashara ambazo zimepigwa marufuku na mamlaka hiyo zikiuzwa na kutangazwa kwa kupiga bure 0800 110 084.
  Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza akifafanua jambo mbele ya mkemia mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko mara baada ya kutembelea banda lao la sabasaba.
  Mkemia mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akizungumza na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza alipotembelea katika maonesho ya kimataifa ya sabasaba jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
   Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza akionesha baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku leo katika banda lao la sabasaba alipokuwa akifanya mahojiano na Michuzi blog.
  Baadhi ya Vipodozi vilivyopigwa marufuku na TFDA.


older | 1 | .... | 1612 | 1613 | (Page 1614) | 1615 | 1616 | .... | 1897 | newer