Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live

RC MAKONDA VIFAA TIBA KUTOKA KOREA KUSINI

0
0
Na Emmaenul Masaka, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amepokea shehena ya vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.milioni 100 kutoka Serikali ya Korea Kusini kupitia Shirika la KOICA.

Makonda amepokea vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam ambavyo ni Digital X-ray tatu, Ultrasound moja, Kabati la usalama wa viumbe (safety cabinet) moja, Mashine tatu za kupima mkojo, mashine ya kuwapa joto watoto njiti (baby warmer) pamoja na mashine ya utakitshaji.

Baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka kwa Balozi wa Korea kusini Bwana Geum Young Song RC Makonda amekabidhi vifaa hivyo kwenye vituo vya Afya vya Sinza, Mnazi Mmoja na Mbagala ambako kuna uhaba wa vifaa. 

Kabla ya kupokea vifaa hivyo RC Makonda alifanya mazungumzo na Balozi huyo wa Korea Kusini na kuwasilisha ombi la kujengwa kwa Chuo cha kisasa cha mafunzo ya udaktari na uuguzi ambapo Balozi Geum Young Song amepokea kwa mikono miwili ombi hilo.

Makonda pia amemueleza Balozi ombi la kujengwa kwa kituo kikubwa cha upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi kwenye eneo moja ambapo pia Balozi amepokea ombi hilo na kumsifu RC Makonda kwa moyo wake wa kujali wananchi. 

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Geum Young Song amesema wametoa vifaa hivyo kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mkoa wa Dar es salaam katika uboreshaji wa sekta ya Afya na wataendelea kusaidiana na Serikali.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa makabidhiano ya shehena ya vifaa Tiba mablimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka serikali ya Korea Kusini kupitia shirika lake la KOICA.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Balozi wa Korea kusini,Geum Young Song (kushoto) akimuonesha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda vifaa hivyo leo jijini Dar as Salaam.
Barozi wa Korea kusini,Geum Young Song (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda vifaa tiba

MCL YAZINDUA JUKWAA LA FIKRA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa “Jukwaa la Fikra” litakalokuwa linakutanisha wadau wa sekta mbalimbali na wananchi ili kujadili Mada mbalimbali za Kitaifa , Kizalendo,kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa pamoja kuhusu baadhi ya matatizo na changamoto tunazokabiliana nazo kama Nchi.Kulia ni Mkurugenzi wa masoko wa Itv na Redio One, Joyce Luhanse na Mkurugenzi Mtendaji wa Itv na Redio One, Bi Joyce Mhavile.
Mkurugenzi Mtendaji wa Itv na Redio One, Bi Joyce Mhavile(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa “Jukwaa la Fikra” litakalokuwa linakutanisha wadau wa sekta mbalimbali na wananchi ili kujadili Mada mbalimbali za Kitaifa , Kizalendo,kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa pamoja kuhusu baadhi ya matatizo na changamoto tunazokabiliana nazo kama Nchi.Kushoto ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa magazeti ya Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai.
Picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa “Jukwaa la Fikra” litakalokuwa linakutanisha wadau wa sekta mbalimbali na wananchi ili kujadili Mada mbalimbali za Kitaifa , Kizalendo,kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa pamoja kuhusu baadhi ya matatizo na changamoto tunazokabiliana nazo kama Nchi.

DKT. KIMEI AFANYA ZIARAKATIKA MATAWI YA BENKI YA CRDB PLC NYANDA ZA JUU KUSINI

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei (wa tatu toka kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa (wa kwanza kushoto) pamoja Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mkwawa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tawi hilo wakati wa ziara ya Mkurugenzi huyo kutembelea matawi ya nyanda za juu kusini katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei (kulia) akielekezwa jambo na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa wakati walipofika katika tawi la Mkwawa -Iringa kujionea utendaji kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei (kulia) akipata maelezo machache kutoka kwa meneja wa Tawi la Mkwawa - Iringa Kissa.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei akiwaafa wafanyakazi wa Tawi la Mkwawa - Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) pamoja Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mkwawa Iringa Kissa wakielekea ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Mufindi wakati walipoanga kuonana na mkuu wa mkoa wa Iriinga mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa (wa pili kulia) huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei (Kulia) wakati walipofika kumtembelea katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William wakati Dkt. Kimei alipokuwa ziara katika matawi ya nyanda za Juu Kusini.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kulia picha ya juu) akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei na ujumbe wake walipofika kumtembelea katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William wakati Dkt. Kimei alipokuwa ziara katika matawi ya nyanda za Juu Kusini.
 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William (wa kwanza kushoto) akiwa na viongozi wengine wa wilaya wakifuatilia mazungumzo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kulia) aakiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei (Kkushoto) wakati walipofika kumtembelea katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William wakati Dkt. Kimei alipokuwa ziara katika matawi ya nyanda za Juu Kusini.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William (kulia) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akisindikiza waheni wake.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akiagana na viongozi wa Benki ya CRDB PLC akiongozwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa tatu kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei na viongozi wa wilaya ya Mufindi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William (wa pili toka kulia) wakiwa katika icha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei akisalimiana na wafanyakazi wa Benki ya CRDB PLC tawi la Makambako.
Akisaini kitabu cha wageni.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa akisaini kitabu cha wageni.
Kila mfanyakazi akiwa na shahuku ya kumsalimia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  Benki ya CRDB PLC Tawi la Makambako, Njombe.

MAJALIWA AZINDUA VITUO 51 VYA KUFUATILIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA WILAYNI BAHI

0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Wanne kushoto ni Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie Boucly. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chombo cha kupima wingi wa mvua baada ya kuzindua vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama,Waziri wa Maji, Mhandisi Isaack Kamwele, Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie Boucly na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoa wa Dodoma, Felista Bura.

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika uzinduzi wa vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe wakati alipozindua vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA

WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa sekta za kilimo, mifugo na maji watumie taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili waongeze ufanisi katika utendaji kazi wao.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, Dodoma.Amesemakuwa kuongezeka kwa vituo vipya vya kisasa vya ufuatiliaji wa mwenendo wa hali ya hewa kumeboresha uhakika wa utabiri kutoka asilimia 81 hadi 87 kama inavyoshuhudiwa kwenye taarifa zinazotolewa katika siku za hivi karibuni. “Hivi sasa tukiambiwa kwamba mvua itanyesha katika maeneo fulani tunakuwa na uhakika kwa asilimia 87 ya utabiri huo,”.

“Vituo hivi ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa nchi wa utoaji wa huduma za hali ya hewa na haidrolojia kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza ufanisi katika utoaji wa tahadhari za awali za majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi,”. Amesema kupitia mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Serikali imeweza kufungua vituo 51 vya kisasa vya hali ya hewa katika maeneo mbalimbali nchini na vituo 15 vya kupima ujazo wa maji kwenye mito iliyopo kwenye mabonde ya Pangani, Ruvuma na Pwani ya Kusini ambavyo vinajiendesha vyenyewe.

“Pia, mradi huu umeiwezesha Serikali kuanzisha kanzidata ya takwimu na taarifa za mafuriko na ukame na taarifa za hali ya hewa na kuondoa ucheleweshwaji wa kupata takwimu au taarifa kutoka Wizara moja kwenda Wizara nyingine,” amesema. Hata hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano zitenge fedha kwenye bajeti zao ili ziweze kufuatilia na kusimamia mradi huo baada ya wafadhili kumaliza muda wao.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa vituo na mifumo iliyowekwa inafanya kazi ipasavyo kwa usimamizi bora ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.

Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola, Wabunge na Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bibi Natalie Boucly.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMATANO, Juni 27, 2018.

Airtel announces AMSHA AMSHA NA AIRTEL MONEY USHINDE winners

0
0
Airtel Tanzania the smartphone network in partnership with SportPesa has today announced the first winners of The “AMSHA AMSHA NA AIRTEL MONEY USHINDE” promotion which was launched on 14th June this year. The winners have won their prizes as a result of betting through Airtel Money.

Speaking in Dar es Salaam today during a draw to announce the winners, Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando said that the draw to select winners under the supervision of the Gaming Board of Tanzania which is authorized to control all gaming games in the country.

As you can see, the draw has been open to everyone and is very fair which means every Airtel customer betting through Airtel Money stands a chance to be a winner. ‘ All what Airtel Money customer will need to do is simply place a bet within the promotion period to enter the draw, said Mmbando adding that customers must make sure that the SportPesa wallet is prefunded with funds for betting.

Mmbando said that the first winners of the draw are ten customers who have won each a brand new latest smartphone; ten others have each won original jerseys for Simba and Yanga Sports Club while ten others have each won a ticket to attend Simba and Yanga matches for the entire season of 2018/2019. I call upon Airtel customers to come up and participate to this AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY promotion as there are other many prizes yet to be won, said Mmbando adding that one customer has also won a brand new 32 inch color televisions.

AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL gives an opportunity for Airtel to reward its loyal Airtel Money users through this consumer promotion. ‘Airtel has been introducing innovative services and products that are exciting and interactive to create a firm bond with our customers. We are aware of the love for sports and betting that has become a lifestyle for most of our customers, said Mmbando.

On his part, SportPesa Public Relations Manager Subrina Msuya said since the launch of AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY promotion launch on 14 June this year, the entry for each day starts at 00.00 HRS and close at 23.59 HRS for the whole duration of the promotion and what Airtel customer will need to do to participate is to bet on the day that there is a draw and automatically their number will enter into the weekly draw. ‘

Ms Msuya named prizes which are being won on daily basis as smartphones, Jerseys for Simba and Yanga clubs, match tickets to watch Simba and Yanga games for the entire season while weekly draws are 32 inch color televisions and Decoders from Star Times.All what a customer will be required to do is to enroll, top up SportPesa wallet using Airtel Money Waller and proceed to place a bet said Msuya adding that winners can collect their prizes from any Airtel Shop branch across the country.
Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando displays some of winning prizes that where won by winners of the first draw of the AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY promotion today in Dar es Salaam. He is flanked by SportPesa Public Relations Manager Sabrina Msuya – left and Tanzania Gaming Board official Ahmed Hemed. To participate, a customer will be supposed to dial *150*60# then transfer money to SportPesa wallet 150888 and press a bet.
SportPesa Public Relations Manager Sabrina Msuya speaks during the first draw of the AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY promotion today in Dar es Salaam. She is flanked by Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando - center and Tanzania Gaming Board official Ahmed Hemed. To participate, a customer will be supposed to dial *150*60# then transfer money to SportPesa wallet 150888 and press a bet.
Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando speaks to one of the winners of the AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY today in Dar es Salaam. To participate, a customer will be supposed to dial *150*60# then transfer money to SportPesa wallet 150888 and press a bet. He is flanked by Tanzania Gaming Board official Abdallah Hemed.

MAKAMU WA PILI WA RAIS SERIKALI YA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDD APONGEZA UTENDAJI KAZI WA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII TASAF.

0
0
Na Estom Sanga- TASAF

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema mchango unaotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF katika shughuli za maendeleo hususani katika jitihada za kupunguza umaskini wa wananchi ni za kupongezwa kwani unatekelezwa kwa kuzingatia sera za serikali za kupambana na umaskini.

Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Maafisa Waandamizi wa Benki ya Dunia waliokuwako kisiwani Zanzibar pamoja na mambo mengine kuona namna Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAFwanavyonufaika , amesisitiza kuwa maisha ya Walengwa wanaonufaika na huduma za Mpango huo yameboreshwa na kuwawekea msingi imara wa kujitegemea.

Amesema TASAF ni kielelezo stahiki cha namna serikali inavyowajali wananchi hususani wanaoishi katika umaskini uliokithiri kwa kuwawekea mazingira ya kufanya kazi za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato huku pia mkazo ukiwekwa katika sekta za Elimu, Afya na Lishe kwa kaya za Walengwa.

Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pia amesema mchango wa kaya za Walengwa katika ukuaji wa uchumi umeanza kuonekana kutokana na shughuli wanazozifanya hasa katika nyanja za kilimo cha Mpunga, bustani ,ususi na ufugaji wa kuku wa kienyeji na mbuzi kwa kutumia ruzuku kutoka TASAF masuala ambayo amesema yanawaongezea kipato .

Akitoa mfano,Balozi Seif amesema miradi mingi iliyoanzishwa na Wananchi katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} na kupata msukumo wa Benki ya Dunia imeleta ukombozi kwa Wananchi walio wengi kisiwani humo.Mapema Mkurugenzi Mtendaji TASAF} Ladislaus Mwamanga amesema kazi kubwa inayofanywa na Wananchi wa Zanzibar kwenye miradi ya Maendeleo kupitia programu zinazosimamiwa na Mfuko huo imeleta mafanikio makubwa.

Mwamanga amesema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mfuko huo itaendelea kuongeza nguvu mara dufu katika kuona kundi kubwa la Wananchi walio na kipato duni hasa Vijijini wanaongezewa nguvu za uwezeshaji ili kuondokana na mazingira magumu yanayowakabili.

Akitoa salamu kwa niaba ya Ujumbe wa Viongozi hao wa Benki ya Dunia Mkurugenzi na Mkuu wa Mtandao wa Masuala ya Kijamii na Ajira wa Benki ya Dunia Bwana Michal Rutkowski alisema Taasisi hiyo ya Kimataifa ya Fedha haina sababu ya kusua sua katika kuongeza nguvu kwenye miradi ya TASAF inayoendelea vizuri katika utekelezaji wake.

Bwana Michal alisema Uongozi wa juu wa Benki ya Dunia {World Bank} umefurahishwa na jitihada kubwa zinazochukuliwa na Wananchi walio wengi Visiwani Zanzibar katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Jamii inayosimamiwa na TASAF .

Akimkaribisha mgeni rasmi katika tafrija hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed alisema ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Benki ya Dunia umesaidia kupunguza umaskini kwa baadhi ya Kaya Nchini Tanzania.

Waziri Aboud alisema ushirikiano huo unaendelea kuwa kigezo tosha kinachotoa majibu ya uwepo wa utulivu wa kimaisha kwa Baadhi ya Familia za Kaya hizo jambo ambalo limeleta faraja zaidi kwa watoto wao katika kushiriki vyema masomo yao.

Hii ni mara ya pili kwa Mkurugenzi ambae pia ni Mkuu wa Mtandao wa Masuala ya Kijamii na Ajira wa Benki ya Dunia Bwana Michal Rutkowski na Maafisa wake kutembelea miradi ya maendeleo ya Kijamii inayosimamiwa na Mfuko wa TASAF Nchini Tanzania.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza na Maafisa wa Benki ya Dunia,TASAF na serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya mchango muhimu wa TASAF katika kukabiliana na umaskini nchini. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akishukuru ushirikiano uliopo kati ya SMT,SMZ na Benki ya Dunia uliosaidia kuzikomboa Kaya Maskini Nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga akipongeza usimamizi mzuri wa serikali katika kufanikisha shughuli za taasisi hiyo kwenye hafla iliyohudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Maafisa wa Benki ya Dunia.
Mkurugenzi na Mkuu wa Mtandao wa Masuala ya Kijamii na Ajira wa Benki ya Dunia Bwana Michal Rutkowski akizungumza kwenye hafla iliyohudhuriwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Balozi Seif Ali Idd (walioketi katikati )akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na Benki ya Dunia baada ya kutoa hotuba kufuatia ziara ya maafisa hao ksiwani Zanzibar kuona shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Benki ya Barclays yazindua huduma za kibenki kwa njia ya mtandao kwa wateja wake wadogo na wa kati

0
0
Mtaalamu wa Huduma za Kidigitali wa Benki ya Barclays Tanzania (BBT), Jesse Jackson (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma za kinbenki kwa njia mtandao wa intaneti kwa wateja wadogo na wa kati jijini Dar esSalaam jana. Kushoto ni Msimamizi wa Hduma za Kidigitali, Emmanuel Wangwe na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakati, Ahmed Khamis.

MEYA TEMEKE ATAKA WANAOPEWA MIKOPO KUITUMIA KWA MALENGO WANAOPEWA MIKOPO TEMEKE WATAKIWA

0
0
MEYA wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Chaurembo amevitaka vikindu vya ujasiriamali vilivyopo ndani ya halmashauri ya hiyo kutumia mikopo wanayopata kwa malengo ya kujikwamua kiuchumi.

Chaurembo amesema hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi vikundi vya ujasiriamali wilayani Temeke na kukabidhi hundi ya mkopo ya Sh.6000,000 ambazo zilitolewa kwenye vikundi vitatu vya Jitihada, Ismail, pamoja na maendeleo ambao umetolewa na taasisi ya muungano wa vikundi vya vicoba Tanzania (VIGUTA)

Chaurembo amevitaka vikundi hivyo kwenda kutumia vizuri fedha hizo ili kufikia malengo yao huku akiwataka kuepuka kutumia fedha hizo kwa anasa na starehe zingine zisizonafaida.

" Tunawapongeza Viguta kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya kwani wamekuwa ni mkombozi kwa wajasiliamali wadogo wadogo hivyo niwaomba ndugu zangu wanavikundu mkatumie fedha hizi kwa malengo ambayo mmejiwekea,"amesema Chaurembo. Pia ameongeza kuwa mikopo hiyo wanayopewa ni ya riba nafuu hivyo kila mmoja akawe mlinzi wa mwingine ili kuhakikisha marejesho yanarejeshwa kwa wakati ili kuwezesha wengine kupata mikopo hiyo.

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa hundi za mikopo hiyo Mwenyekiti wa kikundi cha Ismail cha Kongowe Emaculatha Mbassa ambaye kikundi chake kimekopeshwa shilingi milioni sita alipongeza Taasisi hiyo ya Viguta kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwainua kiuchumi hususani wao akina mama.

Akizungumzia mkopo wao amesema watautumia vema katika kuhakikisha wanapiga hatua zaidi kimaendeleo na watatumia mkopo huo kuhakikisha wanasimama na wanarejesha kwa wakati. Naye Mwenyekiti wa kikundi cha maendeleo kurasini Maria kilumbo ambao wamepata sh milioni 4.5 alisema kuwa wanajivunia kuwa ndani ya viguta kwani huduma wanazotoa hakika zinawapa faraja

Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dauda Salmin amesema wamejipanga kuhakikisha watanzania wanaondokana na umasikini na kukubali kujiunga kwenye vikundi mbalimbali. Amesema kuwa wao kama taasisi wapo mikoa yote ya Tanzania na wanachama zaidi ya milioni saba nakudai kuwa mikopo wanayotoa ni ya riba nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza kukidhi marejesho yake.

Amesema mbali na kutoa mikopo ya fedha tasilimu pia wanatoa mikopo ya viwanja vikiwa na hati yake pamoja na nyumba.


Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Chaurembo, katikati akimkabidhi hundi ya mkopo ya shilingi milioni 6,000,000 Mwenyekiti wa kikundi cha ujasiliamali cha Simle Vikoba, Emaculata Mbassa (kushoto), katika uzinduzi wa vikundi vya ujasiliamali wilayani Temeke Dar es Salaam jana. ambazo zilitolewa kwenye vikundi vitatu vya Jitihada, Ismail, pamoja na maendeleo kutoka kwa taasisi ya muungano wa vikundi vya vicoba Tanzania (VIGUTA)

Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti Taifa VIGUTA Dkt. Dauda Salmin,akifafanua jambo mbele ya wana chama wa vikundi mbalimbali vya (VIGUTA) Wilayani Temeke Dar es Salaam jana,katika uzinduzi wa vikundi vya ujasilia mali.
Baadhi ya wanachama wakimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti Taifa VIGUTA Dkt. Dauda Salmin,hayupo pichani katika uzinduzi vikundi vya ujasiliamali wilayani Temeke Dar es Salaam jana.

KIGWANGALLA APOKEA TAARIFA YA AWALI YA KAMATI YA KOVA KUHUSU TUHUMA ZA MAUAJI YA TEMBO

0
0


VIDEO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma jana. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Japhet Hasunga na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Iddi Mfunda (kulia). Tuhuma hizo ziliwahusisha watumishi wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST waliokuwa wakiufadhili. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Naibu Waziri, Japhet Hasunga (katikati) wakipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Naibu Waziri, Japhet Hasunga (wa pili kulia) wakipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma jana. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Julius Kibebe, Kresensia Swai na Emmanuel Musamba (kushoto). 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Iddi Mfunda taarifa hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wajumbe wa kamati maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma za mauaji ya Tembo ambazo ziliwahusisha watumishi wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST waliokuwa wakiufadhili. (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii).

NEWZ ALERT: NOAH YAUA WATANO WATWARA

0
0
JOSEPH MPANGALA- MTWARA

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujerehiwa Vibaya kutokana na ajali ya gari kuacha barabara Kuanguka na kisha Kuwaka moto katika barabara ya Mangaka/Tunduru kijiji cha chigweje Wilaya ya nanyumbu Mkoani Mtwara.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa10 jioni ikihusisha gari aina ya Toyota Noah yenye numba T.485 DJE iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka mangaka kwenda Tunduru ambapo Gari hiyo iligonga Gema na kupinduka eneo lumesule ambalo lina kona na mteremko mkali.

Kamanda wa polisi mkoa wa mtwara DCP Lucas Mkondya amesema Jumla ya watu watano wameungua mmoja ni dereva wa gari lakini wengine wanne hawajatambulika hivyo kuwaomba wananchii kujitokeza na kwenda kuwatambua Ndugu zao.

“Tunaomba wananchii wanaohisi kupotelewa na ndugu zao ambao walikuwa wanatambua kwamba nduguzao jana walikuwa na safari ya kutoka mangaka kwenda Tunduru na kama hawajafika nyumbani basi waende Hospital ya Mkoamaindo wilaya ya masasi kwa ajili ya kutazama miili yao.Amesema kamanda Mkondya.

Aidha Kondakta wa gari hiyo Khalid Maneno aliruka kutoka kwenye gari hiyo kabla ya kutokea ajali na hivyo anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa lengo la kusaidia kukamilisha Upelelezi

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva na kutokana na mteremko na kona kali na hivyo kushindwa kuimudu na kupelekea ajali hiyo.

.Muonekano wa gari aina ya Noah iliyokuwa ikufanya safari zake kutoka Manganka kwenda Tunduru baada ya kuungua na kuteketea.
 Baadhi ya wananchii wa kijiji cha Chingweje wilaya ya nanyumbu Mkoa wa mtwara wakitazama Gari aina ya NOAH mara baada ya kugonga gema la barabara na Kupinduka kisha kuwaka moto na kusababaisha watu watano kufariki.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI SIMIYU FESTIVAL 2018

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu,

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio kubwa linalojulikana kwa jina la Simiyu Jambo Festival, ambalo linatarajiwa kufanyika Julai 8 mwaka huu katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo kwa mwaka huu 2018 linafanyika kwa mara ya pili

Tukio hilo ambalo linafanyika kwa mara ya pili , limebeba vipengele vikuu vinne vya mashindano ambavyo ni mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili( wagika na wagalu), mbio fupi kilomita 10 kwa wanaume na wnawake, mbio za uwanjani kwa watoto na uandishi wa insha ambapo kauli mbio yake ni Familia Yangu, Afya Yangu, Furaha Yangu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati ya uzinduzi wa tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema kuwa tukio hilo, linalengo la kukuza vipaji kwa vijana wa Mkoa wa Simiyu na kutangaza tamaduni za kabila la Kisukuma na kwamba litahusisha wananchi wote kutoka mikoa mbalimbali.

“Tutakuwa na mashindano ya mbio za baiskeli kilomita 150 wanaume, kilomita 100 wanawake, kilomita 11 watu wenye ulemavu, mbio fupi za kilomita 10 wanaume na wanawake, mbio za watoto za uwanjani, uandishi wa insha kwa wanafunzi na zaidi ya shilingi milioni 22 zitashindaniwa nitoe wito kwa Watanzania wote hususani vijana kuchangamkia fursa hii” alisema Mtaka

“Hii ni fursa pia kwa Wanasimiyu ambao ni wenyeji, sisi tunasema mbio za barabarani na uwanjani ni biashara , mashindano ya baiskeli ni biashara lakini kikubwa zaidi hili ni tukio ambalo litautangaza utamaduni wa Wasukuma wenye mvuto sana ambapo makundi mawili ya Wagika na Wagalu watacheza ngoma za asili na fisi na chatu, nitoe wito kwa watu wote kuja kuona haya” alisisitiza

Mtaka amesema ushiriki katika mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili na uandishi wa insha ni bure isipokuwa mbio za kilomita 10 kwa wanawake na wanaume ambazo washiriki watatakiwa kulipa gharama ya shilingi 5,000/= kwa ajili ya usajili.

Naye Joseph Paulo Mwenyekiti chama cha Baskeli Mkoa wa Simiyu amesema kuwa uongozi mzima wa chama chao tayari wamejipanga ipasavyo kupokea na kusajili washiriki ambao watakuwa tayari kushiriki mashindano hayo ya Baiskeli kwa wanawake na wanaume.

Dkt. Amir Ibrahimu mwakilishi wa shirika la UNFPA, Mkoa wa Simiyu amesema shirika hilo limeamua kuwa ni moja ya wadhamini wa Simiyu Jambo Festival waweze kufikisha elimu wananchi wa Simiyu na jamii yote kwa ujumla itakayowasaidia kuona umuhimu wa uzazi wa mpango, kupinga mimba za utotoni na kuhamasika wakina mama wajawazito kujifungua kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua.

Aidha Akizungumzia zawadi kwa washindi watakao shiriki mashindano mbalimbali katika tukio hili la Simiyu Jambo Festival , Afisa Masoko wa Jambo Food Products Company ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Anthony Paul amesema kwa mwaka huu zawadi zimeongezeka hadi kufikia milioni 22.

Naye Mratibu wa mashindano hayo Zena Mchujuko alisema maandalizi yanaenda vizuri hivyo wananchi wote ndani ya Mkoa wa Simiyu na nje ya Mkoa wajitokeze kwa wingi kushiriki mashindano hayo.

Simiyu Jambo Festival mwaka 2018 inadhaminiwa na Jambo Food Products Company, UNFPA, Maswa Standard Chalks, Meatu Milk, NGS Petroleum Limited, Alliance Ginneries Ltd, NGM Gold Mine Limited, SIBUKA na Busega Mazao Limited.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo kuhusu, Simiyu Jambo Festival inayotarajiwa kufanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Baadhi ya waandishi wahabari mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza nao kuhusu uzinduzi wa Simiyu Jambo Festival ambayo itafanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Vinywaji Bariadi ya Jambo (Jambo Food Products Company), Anthony Paul akisoma zawadi zitakazotolewa kwa washindi watakoashiriki katika matukio tofauti ya Simiyu Jambo Festival,ambalo litafanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Simiyu, Bw. Joseph Paulo akitoa maelezo juu ya masuala mbalimbali yahusuyo mchezo wa mbio za baiskeli ambao utachezwa wakati wa Simiyu Jambo Festival , ambalo litafanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia idadi ya watu (UNFPA) Mkoa wa Simiyu Dkt Amir Ibrahimu akitoa taarifa ya ushiriki wa Shirika hilo katika Simiyu Jambo Festival, ambalo litafanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Mratibu wa Simiyu Jambo Festival, Bi. Zena Mchujuko akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya tukio hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Kutoka kushoto Mwakilishi wa UNFPA Mkoa wa Simiyu Dkt Amir Ibrahimu, Afisa Masoko wa Kampuni ya Jambo, Anthony Paul, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Simiyu wakionesha vinywaji baridi vya Kampuni ya Jambo, mara baada ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu Simiyu Jambo Festival tukio linatarajiwa kufanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Kutoka kushoto Mwakilishi wa UNFPA Mkoa wa Simiyu Dkt Amir Ibrahimu, Afisa Masoko wa Kampuni ya Jambo, Anthony Paul, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Simiyu wakinywa vinywaji baridi vya Kampuni ya Jambo, mara baada ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu Simiyu Jambo Festival tukio linatarajiwa kufanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
 

Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika

0
0
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 6 ya Jumia barani Afrika na uzinduzi wa kampeni ya Sabasaba. Kulia ni wawakilishi kutoka kampuni ya simu ya FERO, ambao ni mojawapo ya washirika wa Jumia katika maonyesho ya Sabasaba mwaka 2018.
  Bw. Hemraj Bhardaraj, Meneja Ufundi wa kampuni ya simu ya FERO, akionesha mojawapo ya simu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) zitakazopatikana kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba katika banda  la Jumia. Wakifuatilia kwa umakini katikati ni muwakilishi mwenza kutoka FERO Javid Bapu huku kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James.
 Bw. Hemraj Bhardaraj, Meneja Ufundi wa kampuni ya simu ya FERO, akionEsha mojawapo ya simu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) zitakazopatikana kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba katika banda  la Jumia. Wakifuatilia kwa umakini kutoka kulia ni  Meneja Mauzo wa kutoka FERO  Javid Bapu huku akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James na Msimamizi wa Atsoko, Bi. Lisa Kameja.



Takribani wateja 500,000 wanatembelea Jumia ndani ya mwezi katika mwaka huu 2018, kutoka wastani wa wateja 250,000 kwa mwezi mwaka 2017.
Makampuni ya Kiafrika zaidi ya 60,000 na wafanyabiashara wamejiunga na Jumia. 

Ikiwa na dhamira ya kutengeneza mustakabali wa mazingira mazuri ya masoko na fursa za kuuza na kununua bidhaa pamoja na huduma za mtandaoni na kifedha, Jumia inaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya huduma za manunuzi ya mtandaoni barani Afrika.

Ikiwa imeanzishwa mwaka 2012, Jumia inajivunia kufanya kazi na makampuni zaidi ya 60,000 ya Afrika pamoja na wafanyabiashara wa kiafrika kwenye mtandao wake.

Akizungumzia juu ya shamrashamra za maadhimisho haya yakatakayodumu kuanzia Julai 2 mpaka Julai 15 mwaka 2018, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott amebainisha kuwa sherehe za mwaka huu zimekuja sambamba na sikukuu za Sabasaba hivyo kutoa fursa zaidi kwa wateja kununua bidhaa mbalimbali kwa gharama nafuu na ofa lukuki.

“Sabasaba ni maonyesho makubwa ya kibiashara siyo tu nchini Tanzania bali kwenye ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ujumla. Ni muhimu kwa wafanyabiashara na wateja ambapo hupata fursa ya kufanya maonyesho ya bidhaa na huduma tofauti, kuuza na kununua bidhaa mbalimbali. Kwa maneno mengine, Jumia ni kama maonyesho ya Sabasaba yanayofanyika kwa njiaya mtandao. 

Siku zote Jumia ina aina tofauti za bidhaa zinazopatikana kwa bei nafuu kabisa. Kwa hiyo sherehe za Jumia kwa mwaka huu itashiriki maonyesho ya Sabasaba, na kuwapatia wateja (watakaokuwepo Sabasaba na maeneo mengine) fursa ya kununua bidhaa kwa punguzo kubwa la bei, kujishindia zawadi, vocha za manunuzi na ofa kemkem kutoka mtandaoni na washirika wetu,” alisema Bw. Prescott.

Katika kunogesha sherehe hizi kwa mwaka 2018, Jumia imeshirikiana na wadau wake kama vile: Infinix, Samsung, Tecno, LG, Star X, TCL, Aborder, Philips, Fero, HP, Dell, Maybelline, Revlon and Nippotech. Washirika hawa watakuwepo kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba kwenye banda la Jumia ili kuwapatia wateja fursa ya kununua bidhaa kwa punguzo la bei, zawadi na elimu zaidi juu ya namna ya kufanya manunuzi mtandaoni. 

“Jumia inajivunia kuwa kinara katika mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandao barani Afrika, ikiwa ni sehemu pekee kabisa ya kuuza na kununua bidhaa halisi na zenye ubora wa hali ya juu. Japokuwa biashara ya mtandaoni haijashika kasi Tanzania, takribani wateja 500,000 hutembelea Jumia kwa mwezi. Idadi hii inaongezeka kila mwezi, mwaka jana idadi ya waliokuwa wanatembelea mtandao wetu walikuwa ni nusu ya idadi ya sasa!” aliongezea Mkuu Mkuu wa Jumia Tanzania.

Ikiwa imejitanua katika nchi takribani 13 barani Afrika, Jumia imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuunga mkono uchumi wa nchi hizo kupitia biashara kwa njia ya kidigitali. Jumia imejizatiti katika kujenga mustakabali katika nchi za Kiafrika kwa kufungua milango ya ajira - ikiwa na wafanyakazi takribani 3,000, kuendeleza na kukuza ujuzi kwa waafrika na katika sekta nzima kwa ujumla. 

“Ningependa kutoa wito kwa Watanzania kujumuika nasi katika maadhimisho ya miaka 6 ya Jumia kwa kufurahia punguzo la bei kwa bidhaa tofauti, zawadi na ofa hususani katika msimu huu wa Sabasaba.

 Tutakuwepo kwenye viwanja vya maonyesho na washirika wetu, wateja wataweza kufanya huduma za manunuzi, kujishindia zawadi na kufahamu chochote kuhusu masuala ya biashara za mtandaoni. Hii ni fursa kwa wafanyabiashara na wateja kututembelea ili kupata elimu zaidi,” alihitimisha Bw. Prescott. 

Naye kwa upande wake mwakilishi kutoka Atsoko, Bi. Lisa Kamecha ameongezea kuwa, “Tunayo furaha kuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 6 ya Jumia. Ni fursa kubwa kufanya kazi na kampuni ambayo imejizatiti kufanya mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandao nchini na Afrika kwa ujumla. Kwa Watanzania wengi bado dhana hii ni ngeni kwao lakini ina faida kubwa kama ikitumika ipasavyo.” 

“Biashara yetu imenufaika kwa kiasi kikubwa kuwa kwenye mtandao huu. Tumeweza kutanua soko letu kwa kuwafikia wateja wengi zaidi, hapo kabla tulikuwa tunategemea wateja kuja moja kwa moja dukani. Hakuna gharama za kujitangaza kupitia Jumia, ni rahisi wateja wetu kuperuzi bidhaa zetu, kuagiza, kufanya na kupelekewa popote walipo. 

Haya yote tusingeweza kama tungeamua kufanya wenyewe. Nawasihi wafanyabiashara wengine nchini kuitumia fursa kwa kujiunga kwani ndipo dunia ilipo sasa na inapoelekea siku za usoni,” alihitimisha Bi. Kamecha







WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT

0
0

JOSEPH MPANGALA,MTWARA

Wawakilishi wa Baraza la usafirishaji Korosho Kutoka Nchini India (CEPCI) wamefanya ziara Mkoani Mtwara na kukutana na wadau wa usimamizi,ununuzi na usafirishaji wa zao la Korosho kwa leno la kujadiliana namna bora ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa Biashara ya zao la Korosho kati ya nchi ya Tanzania na India.

Mkutano huo wa siku moja, umefanyika katika ofisi za Bodi ya Korosho TanzaniaCBT Mkoani Mtwara na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Vyama vya ushirika, wanunuzi wa Korosho, Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA),pamoja na Mjumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini India.

Aidha Mkutano huo umejikita katika kujadili changamoto zinazojitokeza wakati wa kununua na kusafirisha Korosho kutoka Tanzania kwenda Nchini India ambazo ni pamoja na kuzingatia kwa ubora na uaminifu wa wasafirishaji. Mwenyekiti wa CEPCI Ktuoka Nchini India Raghavanpillai Bhoocles ameishukuru Bodi ya Korosho Tanzania kwa juhudi inazozifanya katika kusimamia Sekta ya Korosho Nchini,Na kushauri kufanyika kwa mikutano ya Mara kwa Mara kwa lengo la kuondoa changamoto chache zinazojitokeza.

Kwa upande wake Meneja wa udhibiti Ubora kutoka CBT Bw.Ray Mtangi amewahakikishia wawakilishi hao kutoka Nchni India kwamba tayari Serikali imeshaanza kushughulikia changamoto zilizojitokeza katika msimu wa Korosho uliopita wa 2017/2018 na kuahidi Kuzifanyia kazi

“Changamoto Chache zilizojitokeza katika Msimu Uliopita tayari Serikali imenza kuzifanyia kazi na tayari Tumejipanga ili kuhakikisha Changamoto Hizo Kutojitokeza tena katika Msimu Unaokuja”Amesema Mtangi



Meneja Uthibiti Ubora Kutoka Bodi ya Korosho CBT Ray Mtangi Akifungua Mkutano wa majadiliano kati ya CBT na wajumbe wa Wakala wa Usafirishaji wa korosho kutoka nchini India uliofanyika Mkoani Mtwara.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Cashew Export Promotioncouncil of India {DEPCI} akizungumza katika mkutano wa pamoja na Bodi ya Korosho Jinsi ya Kuondokana na Changamoto katika Ununuzi na Usafirishaji wa Korosho.

Washiriki wa Mkutano wa wakijadili juu ya namna ya kuimarisha Uhusiano na kuboresha usafirishaji wa korosho kutoka Tanzania kwenda nchini India.

Waogeleaji wa Bluefins kushiriki mashindano ya Kenya

0
0
Dar es Salaam . Jumla ya waogeleaji 11 wa klabu inayokuja juu kwa kasi katika mchezo wa kuogelea nchini, Bluefins watashiriki mashindano ya Mombasa yaliyopangwa kuanza leo.

Mashindano hayo ya kimataifa, yanashirikisha waogeleaji mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki na klabu hiyo ndiyo pekee inayoiwakilisha nchi.

Muasisi na kocha mkuu wa timu hiyo, Rahim Alidina aliwataja wachezaji ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano hayo kuwa ni Aminaz Kachra, Lina Goyayi, Muskan Gaikwad na Aliyana Kachra ambao ni wanawake.

Waogeleaji wa kiume ni Delbert Ipilinga, Christian Fernandes, Parth Motichand, Isaac Mukani, Sahal Harunani, Aaron Akwenda na Hassan Harunani.Alisema kuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo pamoja na kushiriki kwa mara ya kwanza katika historia.

“Haya ni mashindano yetu ya kwanza ya nje ya nchi tokea klabu yetu ianzishwe, na tumeamua kufanya hivi baada ya kupata mafanikio makubwa sana katika michezo ya ndani kwa kushika nafasi ya pili na ya tatu, tumeona kuwa ni wakati sasa kwa waogeleaji wetu kuvuka mipaka ya nchi na kupima uwezo wao,” alisema Alidina.

Alifafanua kuwa wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo ili kuiletea sifa Tanzania.“Napenda kuishukuru BMT na Kamati ya Muda ya chama cha kuogelea nchini kwa kutupa msaada mkubwa pamoja na vibali, tumefarijika sana na tunahidi kuleta ushindi katika mashindano hayo,” alisema Alidina.

NHIF YAWAHAMASISHA WANAUSHIRIKA KUJIUNGA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA

0
0
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga(NHIF) umewahamasisha wanaushirika mkoani Tanga kujiunga na mpango wa Ushirika Afya ili waweze kupata kadi za matibabu ambazo wanaweza kunufaika na huduma ya matibabu nchini nzima kwani bila afya imara mipango wanayopanga inaweza kushindwa kufanyika kwa ufanisi mkubwa. 

Uhamaishaji huo ulifanywa na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia Kaku wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa maendeleo ya ushirika mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga na kufunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Zena Saidi. 

Alisema bila wana ushirika hao kuwa na afya imara mipango yao wanayopanga itashindwa kufanikiwa kwa sababu wanapokuwa wakiungua wanaweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha nyingi kuweza kujitibu lakini wanapokuwa kwenye mpango huo wataweza kupata matibabu kwa gharama nafuu. 

“Lakini niwaambie kuwa mkijiunga na mpango wa ushirika mnaweza kunufaika na huduma za matibabu nchi nzima lakini pia utawawezesha kuweza kuwa na uhakika wa matibabu wakato wote bila kujali kama utakuwa na fedha wakati unapougua “Alisema. 

Alisema mpango wa ushirika afya ni mpango maalumu unaomuwezesha wana ushirika kwa umoja wao kuchangia huduma za matibabu kabla ya mwanachama kupata majanga yakiwemo maradhi,kuunguliwa au magonjwa mbalimbali wakati wakiendelea na shughuli zao. 

Hata hivyo aliwataka wanaushirika hao kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye mpango huo ili kuweza kupata huduma za matibabu wakati wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali ambayo yanaweza kuwapelekea kushindwa kutekeleza wajibu wao kama ilivyokuwa awali. 

“Ndugu zangu niwaambieni bima ya afya ndio mambo yote bila kuwa na afya imara mipango tunayopanga haiwezi kukamilika hivyo niwaase tujiunge na mpango huo wa Ushirika Afya ambao ni mpango maalumu unaowawezesha kuchangia huduma za matibabu kabla ya kupata majanga”Alisema.
Afisa Matekelezo wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia Kaku akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa maendeleo ya ushirika mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga na kufunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Zena Saidi.

Makamu wa Rais aelekea Mauritania kumuwakilisha Rais kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaondoka jioni ya leo kuelekea nchini Mauritania ambako atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika .

Mkutano huo wa siku 2, utakaoanza tarehe 1-2 Julai 2018, utafanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Nouakchott ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa AU. 
Kaulimbiu ya waka huu ni Kushinda Vita Dhidi ya Rushwa chini ya Uenyekiti wa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.

Ujumbe wa Makamu wa Rais unajumuisha Mheshimiwa Dkt. Balozi Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais na ujumbe wake wanatarajia kurejea nchini Julai 5, mwaka huu.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
28 Juni, 2018

RAIS WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS MAGUFULI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Zimbabwe zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya Rais huyo wa Zimbabwe kuwasili nchini.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akipunga mkono kwa wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya ziara ya kazi ya siku mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha pamoja na  Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam limetoa mashine za kupima shinikizo la damu 12 zenye thamani ya Sh.5,000,000 kwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa lengo la kuboresha utoaji huduma hospitali hapo.

NSSF imesema vifaa tiba hivyo vitatumika kwa Watanzania wote watakaofika kupata tiba Hospitali ya Wilaya ya Temeke.Pia vitatumika kutoa huduma kwa wanachama wao wapatao 4000 ambao wanatibiwa hapo.Akizungumza leo katika hosptali hiyo baada ya kukabidhi mashine hizo Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke Barnabas Ndunguru amesema wametoa msaada huo kutokana na maombi ya hospitali hiyo.

Pia amesema msaada huo ni moja ya jukumu la NSSF katika kurudisha fadhila kwa jamii ikiwa ni jitihada za kuisaidia Serikali katika juhudi za kuboresha sekta ya afya nchini.Amefafanua NSSF Mkoa wa Temeke idadi ya wanachama wake wanaopatiwa huduma katika hospitali hiyo ni 4000 na kwa mwezi wanatoa fedha Sh.milioni 42 kwa ajili ya kulipia matibabu hayo."Hivyo tunaamini kutoa msaada huu wa BP Mobile Machine utasaidia katika kuwatibu wanachama wetu pamoja na wananchi wote ambao watakwenda kupata tiba,"amesisitiza.

Ameongeza msaada huo si mwisho na kuahidi kuendelea kusaidia kadri watakavyoweza kulingana na nafasi yao na kueleza wamekuwa wakisaidia jamii katika maeneo mbalimbali.Pia Ndunguru amesema NSSF wanalo fao la matibabu na kinachofurahisha zaidi wanachama wao wamekuwa wakipata huduma za afya za magonjwa yote isipokuwa TB na Ukimwi ambayo hayo huduma zake Serikali inatoa bure.

Ameongeza hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wanachama wao kwani wanapohitaji huduma za matibabu ya afya wanayapata kwa wakati na ya kiwango cha kuridhisha.Akizungumzia zaidi msaada huo amesema kuwa sekta ya afya nchini inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo ya uhaba wa vifaa tiba. ufanisi. 

"Suala la uboreshaji sekta ya afya nchini si jukumu la Serikali peke yake bali ni la Watanzania wote kwa ujumla kuhakikisha wanasaidia Serikali kuimarisha sekta ya afya,"amesema.Kwa upande wa Katibu wa Hospitali ya Temeke Lilian Mwanga amesema mashine hizo za kupima shinikizo la damu zimekuja wakati muafaka kwani hivi sasa robo ya wagonjwa wanaowapokea kwa siku wanasumbuliwa na shinikizo la damu.

"Kupatikana kwa mashine hizi 12 inafanya tuwe ne jumla ya mashine 27 kwani tulipata msaada wa mashine 15 siku za karibuni.Katika hospitali yetu tunapokea wagonjwa wengi wenye shinikizo la damu."Wengi wao ni wazee lakini nishauri tubadilishe mwenendo wa maisha yetu, tufanye mazoezi na tusiwe tunakula vyakula vyenye mafuta mengi,"amesema.

Amewapongeza NSSF kwa msaada huo na kwamba wanatoa ombi tena na kwa NSSF kuendelea kuwasaidia vifaa tiba.

Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam Barnabas Ndunguru (wa pili kulia) akimkabidhi Ofisa Muuguzi wa Hosptali ya Temeke,Deodata Msoma vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi  milioni tano
Picha ya pamoja
Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam Barnabas Ndunguru (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi vifaatiba kwenye Hosptal ya Wilaya ya Temeke vyenye thamani ya shilingi Milioni tano .(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

JAFO ATOA WITO KUSAIDIA WANAFUNZI WASIOJIWEZA ILI KUINUA ELIMU

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba fupi kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza kwa shule za msingi na sekondari Kata ya Sejeli wilayani Kongwa mkoani Dodoma leo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akitoa msaada kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kata ya Sejeli kama sehemu ya kampeni ya
Nipe kalamu na daftari na mimi nisome
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akipokea msaada wa daftari na penseli kutoka kwa wawakilishi wa walimu wazalendo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo walichangia daftari 120, kalamu 115 na penseli 70
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akiongea na walimu wazalendo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) waliofika kijijini Mbande wilayani Kongwa Dodoma kuunga mkono kampeni ya nipe daftari na peni na mimi nisome.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akipokea msaada wa daftari kutoka kwa Viongozi wa Chama cha Waganga wa Tiba Asilia Tanzania (UWAWATA (T)) waliochangia madaftari elfu mbili katika kuunga mkono kampeni ya nipe daftari na peni name nisome kijijini Mbande wilayani Kongwa leo.
Rosemary Chimya mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Sejeli kijiji cha Mbande akisalimiana na waziri Jafo baada ya kutoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo kwa msaada wa vifaa vya kusomea, ameiomba Serikali kuwajengea mabweni ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni pia kuwaongezea walimu wa masomo ya sayansi.


Na. Zulfa Mfinanga na Fred Kibano,

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo, leo amekabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza wa shule ya msingi na sekondari za Kata ya Sejeli kijijini Mbande wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Msaada huo utanufaisha zaidi ya wanafunzi mia tisa ni pamoja na madaftari 9,000, kalamu 4,000, penseli 2,800, vifutio 1,200 na vichongeo 1,200 vyote vikiwa ni msaada kutoka kwa watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Makao makuu kwa lengo la kuunga mkono Programu ya  “Nipekalamunadaftarinamiminisome” iliyozinduliwa mwezi Februari mwaka huu na Mhe Jafo ili kuwasaida wanafunzi wanaotoka katika familia duni.

Akikabidhi msaada huo katika shule ya sekondari Sejeli Mhe Jafo amesema licha ya kuwa serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia elimu lakini gharama za vifaa vya shule pamoja na sare za shule zinatakiwa kugharamiwa na wazazi au walezi, hivyo baada ya kuona kuna changamoto ya kipato kwa baadhi ya familia ndio sababu pekee ya kuanzisha Programu hiyo.

“Leo wadau wameamua kurudisha fadhila kwa watoto ambao wazazi ama walezi wao hawana uwezo, hili jambo ni kubwa sana tena ni jambo la Ibada, nina kila sababu ya kuwashukuru na kuwaombea, niwasihi watanzania wote waunge mkono jitihada hizo ili Sera ya Elimu Bila Malipo isaidie kuondoa tofauti kati ya wanaojiweza na wasio jiweza” Alisema Mhe Jafo.

Katika hatua nyingine Mhe. Jafo alipokea msaada wa vifaa kama hivyo kutoka kwa Chama cha Umoja wa Waganga wa Tiba Asilia Tanzania (UWAWATA (T)) waliochangia madaftari elfu mbili, huku walimu wazalendo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakichangia daftari 120, kalamu 115 na penseli 70 pamoja na ahadi ya daftari 4,400 kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kongwa pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo.

Aidha, Waziri Jafo ametoa agizo kwa maafisa wa ofisi yake na halmashauri ya Kongwa katika mwaka ujao wa fedha kujenga walau mabweni mawili ya kuanzia kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kwa baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Sejeli.


Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambaye pia ni Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Kongwa Bwana Nelson Milanzi alisema kuwa wilaya hiyo ina wanafunzi 87,185 wa shule za msingi na sekondari kati ya hao wanafunzi 3,523 sawa na asilimia 4.637 wa shule za msingi wana uhitaji wa vifaa vya shule na kusema kuwa kuanzishwa kwa Programu hiyo kutasaidia kuongeza mahudhurio pamoja ufaulu wa wanafunzi.

Naye, Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya NIPE DAFTARI NA KALAMU NAMI NISOME, Dkt. Ombeni Msuya amesema wanalengo la kufika nchi nzima lakini pia kuwafundisha wanafunzi suala la uzalendo ili hapo baadaye nao wawasaidie watu wengine wenye mahitaji.

“Tuna lengo la kufika nchi nzima sanjari na kuanzisha kambi maalumu ya kuchangia elimu ili kuwafikia wanafunzi wote wenye uhitaji huu, lakini pia tutakuwa tunatoa elimu ya uzalendo ili vijana wetu waje kuwa wazalendo hapo baadaye ili likitokea jambo kama hili wawe mstari wa mbele kama wanavyofanya wadau wengine”

Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Rosemary Chimya mwanafunzi wa kidato  cha pili shule ya sekondari Sejeli iliyopo Mbande, mbali na kumshukuru Waziri Jafo kwa kuanzisha programu hiyo lakini aliiomba serikali iwajengee mabweni kwa ajili ya kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni pamoja na kuwaongezea walimu wa sayansi,vitabu na madawati.

Halotel, StarTimes waleta kombe la dunia kiganjani

0
0
Bando hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye simu zao kwa gharama nafuu sana.

Huku mshike mshike wa kombe la dunia ukiendelea kukolea, Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel kwa kushirikiana na Kampuni ya StarTimes wameleta wamezindua huduma mpya itakayo wawezesha wateja wa mtandao huo kuangalia mechi za kombe la dunia kupitia simu zao za kiganjani kwa gharama nafuu.

Huduma hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye simu zao kwa gharama nafuu sana, huduma hiyo inawapatia wateja intaneti ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda amesema huduma hiyo itawawezesha wateja wa Halotel nchini nzima kufurahia kutazama mechi za kombe la dunia kupitia simu za mikononi (Smartphone) kwa urahisi na kwa gharama nafuu kwa kutumia intaneti ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.

“Kuanzia sasa wateja wa Halotel wanaweza kupakua Application ya Startimes kupitia simu zao za Android na watalipia kuanzia shilingi 2000 na watapata GB 1 ambayo wanaweza kuitumia kuangalia mechi zote za kombe la dunia kwa intaneti yenye kasi. Alisema Semwenda.“Jinsi ya kufanya malipo mteja wa Halotel anapaswa kufungua Application ya Star times na baada ya hapo atafuata maelekezo ya kununua vifurushi kuanzia vya siku, wiki hadi mwezi mzima,” Alihitimisha Semwenda.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa StarTimes Ndg. David Malisa Alisema, “Ukiwa unatumia intaneti ya Halotel ni rahisi zaidi kulipia na kutumia StarTimes App ambayo ina burudani na mechi zote za Kombe la Dunia. Kwa watumiaji wa mitandao mingine wanalipia maudhui pembeni na intaneti au data pembeni, ukilipia huduma hii unakuwa umelipia maudhui na intaneti kwa pamoja. Pia unaweza kutumia Intaneti hii bila kikomo kwa masaa 24 hata bando inapoisha utaendelea kupata Intaneti ya kutumia kwenye StarTimes App”. Alisema Malisa. 

Hii ni huduma ya kwanza kabisa Tanzania ambayo itamruhusu mteja kuendelea kupata intanenti hata baada ya bando lake kuwa limekwisha. Ushirikiano baina ya StarTimes na Halotel ni katika hatua ya kusogeza Burudani ya kandanda la kimataifa katika Simu za Mkononi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel (kulia) akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kushoto ni Meneja Masoko wa Startimes David Malisa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa kwa pamoja wakionesha namna ambavyo mteja wa Halotel anavyoweza kuangalia mpira kwenye simu yake ya mkononi kupitia App ya Star times. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa pamoja katika uzinduzi wa Halotel na Startimes kuonyesha ishara ya ushirikiano.
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live




Latest Images