Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

VYUO MBALIMBALI HAPA NCHINI VYATAKIWA KUHAMASISHA WATOTO WA KIKE KUPENDA MASOMO YA SAYANSI

$
0
0
Na Pamela Mollel,Arusha

Vyuo mbalimbali nchini vimetakiwa kuhamasisha wanafunzi wa kike kupenda kusoma masomo ya sayansi kuanzia ngazi za chini ili kuondoa changamoto ya uhaba wa wanasayansi wa kike uliopo hapa nchini. 

Aidha imeelezwa kuwa, kumekuwepo na uhaba mkubwa wa wanasayansi wanawake katika sekta mbalimbali hali inayochangiwa na kuwepo Kwa idadi ndogo ya wanafunzi wa kike wanaohitimu vyuoni. 

Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi wa ufuatiliaji na udhibiti kutoka baraza la elimu ya ufundi, Dokta Annastella Sigwejo wakati akifungua kongamamno la kiteknolojia lililowashirikisha wanavyuo mbalimbali na makampuni jijini Arusha. Alisema kuwa, ili kuhakikisha tunapata wanasayansi wa kutosha ni lazima tuanze kuhamasisha wanafunzi wakiwa tangu ngazi za chini mashuleni ili wajijengee tabia ya kupenda masomo hayo hadi kufikia ngazi za juu .

Dokta Sigwejo alisema kuwa,kwa sasa hivi ambavyo nchi yetu inahamasisha Tanzania ya viwanda ni lazima kuwepo na wataalamu wanasayansi wa kutosha ambao wataweza kuziba mapengo mbalimbali yaliyopo na hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhamasisha wanavyuo kupenda masomo ya sayansi. 

Kwa upande wa Mkuu wa idara ya Tehama upande wa taalamu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha, Pamela Chogo alisema kuwa, kongamano hilo ni la kwanza kufanyika jijini Arusha ambapo wameweza kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaosoma masomo ya sayansi jijini hapa pamoja na makampuni ili wajadili changamoto mbalimbali zilizopo .

Alisema kuwa, kumekuwepo na changamoto kubwa ya makampuni mengi kutokupenda na kuzidhamini Kazi zinazozalishwa na wazawa, hivyo kupitia kongamano hilo wanavyuo wataweza kuonyesha Kazi zao Kwa makampuni mbalimbali ili waweze kuzitambua na kuanza kuzitumia. 

Aliongeza kuwa, kumekuwepo na vyuo vingi Sana hapa nchini ambavyo vimekuwa vikizalisha wataalamu wanasayansi lakini wamekuwa wakikosa ajira kwenye makampuni ya hapa nchini kutokana na kutodhamini kazi zao wanazofanya. "tumeamua kuwakutanisha wanavyuo mbalimbali na makampuni ili waweze kutambua umuhimu wa kuwatumia wanasayansi wetu na kuweza kuona Kazi wanazofanya ili mwisho wa siku waweze kuwadhamini wazawa na kutumia Kazi zao. "alisema Chogo. 

Kwa upande wa baadhi wanavyuo katika kongamano hilo, Faith Felix alisema kuwa, uwepo wa kongamano hilo unasaidia Sana kuwapa uelewa zaidi kuhusiana na kile wanachofanya sambamba na kuonyesha Kazi zao Kwa makampuni ili waweze kuwatumia. 

Naye mwanachuo mwingine, Hamis Laizer alisema kuwa, swala la kubwa lililopo katika masomo ya sayansi ni kuhakikisha wanafunzi wanahamasishwa kusoma masomo hayo wakiwa tangu wadogo, ambapo alisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya vifaa vya teknolojia ili kufanya ubunifu, kutokana na vifaa vilivyopo hapa nchini kuwa vichache na ghali Sana, hivyo waliomba serikali kuleta vifaa zaidi .
Mkurugenzi wa ufuatiliaji na udhibiti kutoka baraza la elimu ya ufundi, Dokta Annastella Sigwejo wakati akifungua kongamamno la kiteknolojia lililowashirikisha wanavyuo mbalimbali na makampuni jijini Arusha,Chuo cha Uhasibu Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Mkuu wa idara ya Tehama upande wa taalamu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha, Pamela Chogo akizungumza na waandishi wa habari , alisema kongamano hilo ni la kwanza kufanyika jijini Arusha ambapo wameweza kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaosoma masomo ya sayansi jijini hapa pamoja na makampuni ili wajadili changamoto mbalimbali zilizopo .
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu,akizungumza na vyombo vya habari alisema ni vyema watumiaji wa mitandao wakafanya matumizi salama ya kuelimisha na kuhabarisha zaidi
Wadau wa mkutano huo
Faith Felix chipukizi katka teknolojia ,anawataka watoto wa kike kuziingiza katika teknolojia kwakuwa fani hiyo si kwa wanaume tu 
Hamis Badru ambaye pia ni mwanateknolojia anawataka watanzania kupenda maswala ya teknolojia

WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu (Mb), amefanya ziara ya kikazi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili kukagua utoaji wa huduma za Matibabu katika Hospitali hiyo. 

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri alifahamishwa kwamba mashine zote za tiba ya mionzi ya nje inafanya kazi vizuri na huduma zinaendelea kutolewa kwa wagonjwa.Pia wakati wa ziara hiyo, Mhe.Ummy alitumia fursa hiyo kuzungumza na wagonjwa mbalimbali waliokuwa wakipata huduma za tiba ya mionzi hospitalini hapo, huku baadhi ya wagonjwa walitoa malalamiko kwa Waziri kuwa, wamekuwa wakitumia muda mrefu kusubiri kupata huduma hususani huduma za mionzi ya nje. 

Kufuatia hali hiyo, mhe. Ummy alitoa maelekezo kwa uongozi wa Hospitali kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri ambao utapunguza muda kwa wagonjwa kusubiri huduma za mionzi ikiwemo kuwepo na ratiba ambayo kila mgonjwa atajua anafika saa ngapi kupata tiba hiyo.

Vile vile, mhe. Ummy alitembelea kitengo cha utoaji wa huduma za mionzi ya ndani ambapo alijionea changamoto ya kutokufanya kazi kwa mashine hizo za utoaji wa mionzi ya ndani kutokana na kukosekana kwa vifaa vya 'transfer tubes' na 'gyn applicators'.

Kufuatia hali hiyo mhe.Ummy alitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt.Julius Mwaiselage kuhakikisha kuwa mashine hizo zinafanya ndani ya siku 2 kwa kuazima hivyo vifaa hivyo kutoka Hospitali ya Bugando ili kurudisha huduma hizo kwa wagonjwa ambao wengi ni wanawake wenye tatizo la Saratani ya Mlango wa Kizazi.

"Naelekeza kuwa fanyeni utaratibu wa kupata kifaa kilichoharibika mapema iwezekanavyo" alisema mhe.Ummy.Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road , Dkt.Julius Mwaiselage alimhakikishia mhe.Waziri kuwa atajitahidi ili vifaa vilivyoharibika vinapatikana ndani ya siku mbili kutoka Hospitali Bugando na pia wameagiza vifaa hvyo kutoka kiwandani nje ya nchi kwa gharama ya Euro 43,200.00 
 Mashine mpya na yakisasa ya mionzi iliyopo katika taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu juu ya ufanisi wa mashine mpya na yakisasa ya mionzi iliyopo katika taasisi hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza malalamiko ya mama aliekuwa akisubiri matibabu ya ugonjwa wa kansa katika taasisi hiyo ya Ocean Road. Wa katikati ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Julius Mwaiselage.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsililiza ndugu wa moja kati ya wagonjwa waliofika Hospitalini hapo kupata huduma za matibabu ya Saratani.

Uwezo wa Wataalam Kupandikiza Figo Waimarishwa Muhimbili

$
0
0
Katika kipindi cha miezi minane Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 10 kwa mafanikio makubwa ambapo katika kambi ya tatu ya upandikizaji figo, upasuaji umefanywa na watalaam wa MNH kwa zaidi ya silimia 80, huku wakisimamiwa na watalaam kutoka Hospitali ya Saifee ya nchini India.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 26 Juni, 2018 jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema MNH ilianza upandikizaji figo Novemba 2017 kwa kupandikiza mgonjwa mmoja ambapo Aprili 2018 wagonjwa wanne walipandikizwa figo na Juni 24 hadi 25, 2018 wagonjwa watano wamepandikizwa figo.

‘‘Pamoja na upasuaji huo kufanyika, mwaka 2016 hospitali ilipeleka watalaam wake nchini India kujengewa uwezo wa kupandikiza figo hivyo napenda kuwafahamisha kuwa tangu tumeanza upandikizaji wa figo tunaendelea kupata mafanikio makubwa kwa baadhi ya watalaam wetu wa ndani kuwa na uwezo wa kushika hatamu ya kufanya wenyewe katika mchakato mzima wa uchunguzi hadi kupandikiza figo,’’amesema Prof. Museru.

‘‘Tunaamini katika kambi mbili zinazokuja za upasuaji wa kupandikiza figo, madaktari wa upasuaji wazalendo watafikia kiwango cha asilimia 100. Hii ni hatua kubwa sana katika kipindi cha miezi minane kwani mara ya kwanza walikuja watalaam wote wanaohitajika wapatao 15, tulipofanya mara ya pili walipungua wakaja watalaam saba na safari hii mara ya tatu wamepungua wamekuja watano tu, tunaamini wataendelea kupungua katika kambi tatu zijazo na hatimaye kusimama wenyewe na kufanya kwa viwango na ubora uleule,” amesisitiza Prof. Museru.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya figo kutoka hospitali ya Saifee ya nchini India Dkt. Mustafa Khokhawala amesema Madaktari wa Muhimbili wameshiriki upasuaji huo kwa asilimia kubwa ambapo kati ya wagonjwa watano waliopandikizwa figo, mgonjwa mmoja amepandikizwa na wataalam wa ndani na kwamba hatua hiyo ni nzuri na inaonesha kuwa watalaam wa MNH wanauwezo mkubwa wa kuendelea na upandikizaji.

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Onesmo Kisanga amesema wagonjwa wote waliopandikizwa figo pamoja na wale waliochangia figo wanaendelea vizuri na wanafuatiliwa na wataalam kwa ukaribu zaidi.

Pia amesema mahitaji ya wagonjwa wanaohitaji kupandikizwa figo ni makubwa kwani kuna wagonjwa karibu 1000 nchi nzima ambao wanahitaji huduma ya kupandikizwa figo.Upasuaji wa kupandikiza figo kwa wagonjwa 10 hadi hivi sasa umegharimu kiasi cha shilingi milioni 210 sawa na milioni 21 kwa mgonjwa mmoja ambapo kama wangeenda nje ya nchi ingegharimu kiasi cha shilingi Bilioni moja sawa na shilingi milioni 100 kwa kila mgonjwa.

Kabla ya kuanza upandikizaji wa figo hapa nchini Serikali ilipeleka wagonjwa takribani 230 katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, hivyo kuanza kwa huduma hii nchini kutaongeza idadi zaidi ya hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 26 Juni, 2018 kuhusu wagonjwa watano kupandikizwa figo katika hospitali hii. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Mustafa Khokhawala, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya Damu, Dkt. Aliasgar Behranwala na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Raval Ashiq Ali Ahmad, wote kutoka Hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai nchini India. 
Kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Njiku Kim, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Victor Sensa naDkt. Isaack Mlatie ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo- wote wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Isaack Mlatie akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu hospitali hii kufanikiwa kupandikiza figo kwa wagonjwa watano.
Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo leo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya Damu, Dkt. Aliasgar Behranwala kutoka Hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai nchini India na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Njiku Kim wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakipandikiza figo mmoja wa wagonjwa watano walipatiwa huduma hiyo.





Katika kipindi cha miezi minane Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 10 kwa mafanikio makubwa ambapo katika kambi ya tatu ya upandikizaji figo, upasuaji umefanywa na watalaam wa MNH kwa zaidi ya silimia 80, huku wakisimamiwa na watalaam kutoka Hospitali ya Saifee ya nchini India.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 26 Juni, 2018 jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema MNH ilianza upandikizaji figo Novemba 2017 kwa kupandikiza mgonjwa mmoja ambapo Aprili 2018 wagonjwa wanne walipandikizwa figo na Juni 24 hadi 25, 2018 wagonjwa watano wamepandikizwa figo.

‘‘Pamoja na upasuaji huo kufanyika, mwaka 2016 hospitali ilipeleka watalaam wake nchini India kujengewa uwezo wa kupandikiza figo hivyo napenda kuwafahamisha kuwa tangu tumeanza upandikizaji wa figo tunaendelea kupata mafanikio makubwa kwa baadhi ya watalaam wetu wa ndani kuwa na uwezo wa kushika hatamu ya kufanya wenyewe katika mchakato mzima wa uchunguzi hadi kupandikiza figo,’’amesema Prof. Museru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 26 Juni, 2018 kuhusu wagonjwa watano kupandikizwa figo katika hospitali hii. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Mustafa Khokhawala, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya Damu, Dkt. Aliasgar Behranwala na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Raval Ashiq Ali Ahmad, wote kutoka Hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai nchini India. 
Kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Njiku Kim, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Victor Sensa naDkt. Isaack Mlatie ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo- wote wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Isaack Mlatie akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu hospitali hii kufanikiwa kupandikiza figo kwa wagonjwa watano.
Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo leo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya Damu, Dkt. Aliasgar Behranwala kutoka Hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai nchini India na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Njiku Kim wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakipandikiza figo mmoja wa wagonjwa watano walipatiwa huduma hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

JESHINIMNADHIMU MKUU WA JWTZ KIHANGAIKO BAGAMOYO PWANI

$
0
0
MNADHIMU Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed amewaonya askari wapya wa jeshi hilo kutojiingiza katika masuala ya siasa.

Aidha hakusita kuwapa tahadhari zaidi kwamba atakayebainika atachuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwano kufukuzwa jeshini.

"Jeshini hakuna siasa, hapa mnaenda kutekeleza Katiba ya nchi, jukumu lenu kubwa ni kulinda mipaka ya nchi, Katiba na maelekezo kutoka kwa viongozi wenu," alisema Luteni Jenerali Mohamed.Mafunzo hayo yalihusisha vijana 2,253 yalifanyika kwa miezi 4 katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS), Kihangaiko iliyopo Bagamoyo Pwani.

Kwa upande Kaimu Mkuu wa Shule hiyo Kanali Sijaona Myala alisema kazi ya jeshi ni kuandikisha askari kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi na vita."Kazi ya jeshi ni kuandikisha askari na si ajira, ikitokea vita hata hawa wote wakifa, tutaandikisha wengine," alisema Kanali Myala.

Mbali ya kufungwa kwa mafunzo hayo, askari waliohitimu walionyesha maonyesho ya ukakamavu, sarakasi na vikwazo.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yacoub Mohamed akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunga mafunzo ya awali ya keshi kwa askari wapya 2253 yaliyokuwa yakifanyika katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS), Kihangaiko iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani. 
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Yacoub Mohamed akikagua gwariide la askari wapya wa JWTZ waliomaliza mafunzo yao ya awali katika Shule ya Kijeshi RTS Kihangaiko iliyopo Bagamoyo, Pwani nyuma mwisho ni Kaimu Mkuu wa Shule hiyo Kanali Sijaona Myala.
Maofisa wa JWTZ wakiongoza Gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa askari wapya 2,253 yaliyofanyika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko Bagamoyo mkoani Pwani. 
Kaimu Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko Kanali Sijaona Myala akimuongoza Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed kupanda jukwaani mara baada ya kukagua gwaride la askari wapya 2253 waliomaliza mafunzo yao ya wali chuoni hapo. 
Mwalimu wa moja ya michezo ya ukakamavu akionyesha namna ya kupita chini ya moto wakati wa maonyeshi yaliyofanyika chuoni hapo.
Askari wapya wakipimana nguvu kwa kuzichapa mbele ya mgeni rasmi Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luten Jenerali Yacoub Mohamed aliyefunga mafunzo ya awali ya askari hao 2,253 yalifanyika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijesjhi (RTS) Kihangaiko Bagamoyo Pwani. 
Askari wapya wakimsikiliza mgeni rasmi Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed alipokuwa akizungumza nao kabla ya kufunga mafunzo yao ya kundi la 38A/17 lililokuwa na askri 2253. 
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed katikati akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa jeshi waliopop kazini pamoja na wastaafu wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa askari 2253 yaliyofanyika Shule ya Mafunzo ya Aawali ya Kijeshi RTS Kihangaiko Pwani. 
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed wa kwanza kushoto akijadiliana jambo na maofisa wa JWTZ mara baada ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa wanahitimu 2253 yaliyofanyika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko Bagamoyo mkoani Pwani

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI

$
0
0
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetoa Mafunzo maalum kwa wahandisi watakaosimamia ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye skimu kumi na sita(16) zitakazojengwa mwaka ujao wa fedha, 2018/2019 kutoka kwenye kanda nane (8) za Tume ya Taifa ya umwagiliaji, Halmashauri za wilaya pamoja na wakandarasi, ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo uelewa na uzoefu zaidi wahandisi hao katika usimamizi wa mikataba na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.

Akizungumza katika warsha hiyo ya mafunzo ya siku tatu iliyofanyika Mkoani Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi wa uendelezaji wa miundombinu ya Umwagiliaji kutoka Tume hiyo Mhandisi, Pascal Shayo, alisema kuwa Tume imetoa Mwongozo wa ujenzi wa skimu za umwagiliaji na alisisitiza ya kuwa, wahandisi waliopewa mafunzo hayo wanatakiwa wasimamie ujenzi wa skimu hizo kwa kufuata mafunzo waliyoyapata ili kuhakikisha miundombinu hiyo inajengwa kwa kiwango kinachotakiwa.

“Mhandisi atakayeshindwa kusimamia vizuri atachukuliwa hatua kwani kwa kupitia mafunzo haya wameshapata uelewa wa kutosha.”Alisisitiza

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Sanifu na Uratibu wa Sekta Binafsi kutoka katika Tume hiyo Mhandisi Muyenjwa Maugo alisema warsha hiyo ina lengo la kuhakikisha miradi yote ya umwagiliaji inajengwa katika kiwango elekezi na wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa katika kilimo cha umwagiliaji na kuzalisha mazao bora.

“Lengo kubwa ni kujenga uwezo kwa wahandisi na wataalam wa umwagiliji ili kuweza kusimamia miradi ya umwagiliaji kwa ufanisi, na kupitia miradi hii tunaweza kuwafundisha wahandisi namna ya kutumia mwongozo uliyopo katika kusimamia shughuli za umwagiliaji.” Alibainisha Maugo.

Awali imeelezwa kuwa ,ujenzi wa skimu hizo kumi na sita (16) utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.5 ambazo ni mkopo kutoka serikali ya Japani kupitia shirika lake la maendeleo la kimataifa (JICA).


Katika picha kutoka kushoto, Kaimu Mkurugenzi Muhandisi Willson Karumuna, Kaimu Mkurugenzi Mhandisi Pascal Shayo, Kaimu Mkurunzi Msaidizi Mhandisi Ntonda Kimasa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Mhandisi Muyenjwa Maugo wakifuatila Jambo katika Mafunzo ya wahandisi na wataalam kutoka katika Halmashauri kwenye warsha ya Mafunzo, yalihusu ujenzi wa skimu za umwagiliaji iliyofanyika mkoani Shinyanga.
Katika Picha wahandisi na wataalam wakiwa katika hatua ya mafunzo kwa vitendo katika eneo la Nyida, mara baada ya warsha ya mafunzo iliyohusu ujenzi wa skimu za umwagiliaji iliyofanyika Mkoani Shinyanga.

DOKTA PHILIP MPANGO AHITIMISHA MJADALA WA BAJETI BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
  Baadhi ya wadau wakifuatilia kwa makini mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, kabla ya Waziri mtoa hoja Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) hajahitimisha hoja hiyo ya Bajeti, Bungeni, Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, wakizungumza jambo kabla ya kuhitimishwa kwa hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia hoja za Mawaziri wakati wa kuhitimisha hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma, ambapo alizitaka Halmashauri kuendelea kubuni miradi ya kimkakati ili kujiongezea kipato.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma, ambapo ameahidi kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma kwa ufanisi na kuwatahadharisha wabadhilifu wa fedha za umma kuwa ni sawa na kula sumu. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), na Waziri wa Madini, Mhe. Anjellah Kairuki (Mb), wakijadili jambo muda mfupi baada ya kuhitimishwa kwamjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu (katikati), akipeana mkono na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma baada ya kuhitimishwa kwa hoza za Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19, ambapo mtoa hoja  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) aliwapongeza wabunge wengi kwa kutoa hoja zenye kujenga ili kuboresha Bajeti hiyo, kulia ni Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akipongezwa na Mbunge wa Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza kwa hitimisho zuri la Hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa kusisitiza weledi katika usimamizi wa fedha za umma.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipongezwa na Mbunge wa Kwimba Mhe. Mansoor Sharif, baada ya kuhitimisha ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mipango madhubuti ya kufikia uchumi wa kati. 
NaibuWaziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akipongezwa na Mhe. George Simbachawene (Mb) (kushoto) na Waziri wa Habari,  Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, kwa kujibu hoja za wabunge kwa ufasaha wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango)

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA UGENI KUTOKA LIWALE MKOANI LINDI

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akisalimiana na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) na Ndg. Jivunie Mbunda (aliebebwa) ambae ni mlemavu wa kimo kutoka Liwale Mkoani Lindi walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
  

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) pamoja na wanandoa Ndg. Jivunie Mbunda ambae ni mlemavu wa kimo (kushoto) na Mkewe Ndg. Amina Mbunda wote kutoka Liwale Mkoani Lindi (wa pili kushoto) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) na Wana ndoa Ndg. Amina Mbunda (kushoto) na Mumewe Ndg. Amina Mbunda (aliebebwa) ambae ni mlemavu wa kimo kutoka liwale Mkoani Lindi walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE

DK. KIGWANGALLA AFUNGUA WARSHA YA KITAIFA YA WADAU WANAOPINGA VITENDO VYA UHALIFU DHIDI WANYAMAPORI NA MISITU NCHINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. Warsha hiyo imelenga kujadili na kuainisha mahitaji na vipaombele vya sekta ya mahakama na mashtaka ya kudhibiti uhalifu huo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Iddi Mfunda (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga (wa pili kulia) na Mkuu wa ofisi wa Shirika la Ufuatiliaji wa Wanyamapori (TRAFFIC), Julie Thomson (kulia) wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa warsha ya siku moja ya wadau wanaopinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. 
Baadhi ya wadau wa kitaifa walioshiriki hafla hiyo wakiimba wimbo wa Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. Warsha hiyo imelenga kujadili na kuainisha mahitaji na vipaombele vya sekta ya mahakama na mashtaka ya kudhibiti uhalifu huo. 
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii)

WATU MILIONI 125 WAKO HATARINI KUATHIRIWA NA KEMIKALI AINA YA ‘ASBESTOS”

$
0
0
Na EmanuelMadafa,Mbeya.

Imeelezwa kuwa watu wapatao milioni 270 wanahusika na ajali za kemikali maeneo ya kazi na watu milioni 160 wanasumbuliwa na magonjwa yanayotokana na madhara ya kemikali Duniani .

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Christopher Anyango, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuelimisha wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.

Amesema, kati yao watu milioni 125 duniani, wako katika hatari ya kudhurika na kemikali aina ya ‘asbestos” huku 90,000 wakipoteza maisha kila mwaka na kwamba madini hayo yanatumiwa zaidi kwenye viwanda vya kutengenezea mabati.

Aidha Mkurugenzi huyo amedai kuwa ukiachana na shughuli za kwenye madini, pia kemikali hiyo ya “asbestos” hutumika kutengenezea mabati na watu wanatumia bidhaa hii kwenye ujenzi wa nyumba hivyo ni vema watengenezaji wa vifaa hivyo wakapatiwa elimu jinsi ya njia bora ya kutumia kemikali hii ili isilete madhara kwa binadamu.

Hata hivyo , amesema kwenye madini mbalimbali kemikali zinazotumiwa ni Sodium Cyanide na Sulphuric Acid na nyinginezo ambazo zote ni hatari kwa afya na mazingira na pia ni kemikali bashirifu hivyo matumizi yake na usimamizi unahitaji uelewa unaojitosheleza ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akifungua mafunzo hayo, amewataka wakemia wanahusika na upimaji wa sampuli za madini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi kwa lengo la kuwasaidia wananchi eza kupata dhahabu sanjali na kusaidia kupatikana kwa mrahaba wa serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Christopher Anyango, akisoma hotuba kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuelimisha wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali wakiwa makini katika ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika ukumbi wa mikutano wa Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akifungua mafunzo kwa wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa (katikati ) na viongozi kutoka ofisi ya mkemia walioketi katika picha ya pamoja na wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya katika picha ya pamoja

TaGLA YAENDELEA NA MAFUNZO YA UPANGAJI MIJI, YAJIZATITI KUTUNZA MAZINGIRA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAKALA wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini (TaGLA) wameendelea na mafunzo kwa njia ya mtandao kutoka Korea kusini kuhusiana na masuala ya utunzaji wa upangaji wa miji na utunzaji wa mazingira.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Wakala hiyo Charles Senkondo ameeleza kuwa huo ni mdahalo wa pili kati ya saba inayotarajiwa kufanyika hadi kufikia oktoba mwaka huu, na mdahalo wa kwanza ulifanyika mapema mwezi huu na hii ni katika kujifunza jinsi ya kutunza mazingira na kupanga miji kisasa zaidi.

Senkondo ameeleza kuwa mafunzo hayo yanatolewa na profesa Heungsuk Choi kutoka chuo cha maendeleo cha korea kusini katika kueleza namna ya upangaji wa miji na majiji kisasa na kuzingatia usafi na miundombinu iliyo bora zaidi.Imeelezwa kuwa Korea Kusini ilikuwa sawa na Tanzania ya sasa katika miaka 1960 ila hadi sasa Korea kusini imepiga hatua kubwa sana hivyo kama wakala inajifunza hatua zilizochukuliwa katika uboreshaji wa miundombinu hiyo na usalama kwa ujumla.

Pia Senkondo amewaomba wadau wa serikali na taasisi binafsi kuitumia wakala hiyo ili kuweza kushirikiana na Serikali katika kujenga miji na kutunza mazingira.Naye mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche ameeleza kuwa wao kama taasisi ya serikali inayohusika na masuala ya mazingira semina hiyo inawasaidia sana katika uboreshaji wa mazingira na ulinzi hasa katika masuala ya usafi kwa kuzoa taka ili kuweza kupambana na magonjwa ya mlipuko sambamba na kuwa tayari katika kujipanga na mlipuko wa majanga kama mafuriko.

Aidha Manchare amesema kuwa changamoto kubwa katika suala la upangaji wa miji ni kutopanga mapema maeneo maalumu kama makazi na yale ya viwanda hivyo wamejipanga katika kulitatua hilo hasa katika jiji la Dodoma ambalo limekuwa makao makuu ya nchi.

Pia mdau wa mazingira ambaye pia ni mkurugenzi wa Legendary International Limited Kamugenyi Luteganya,  ameeleza kuwa semina hiyo ni muhimu sana katika jamii katika kuishi mazingira yaliyo bora na safi kama Korea wanavyofanya na kuboresha kwa kila hatua hivyo ni lazima wachukue ujuzi ili kuweza kuboresha makazi  nchini.
 Mwanasheria wa Mwandamizi (NEMC) Manchare Heche akichangia mada katika mkutano  wa mtandao uliofanyika jana jijini Dar,ambao ulihusisha nchi mbalimbali huku Nchi mwenyeji ikiwa ni Korea kusini 
 Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles  Senkondo akizungumza na waandishi wa habari  mbalimbali waliohudhuria mkutano wa mtandao uliohusisha nchi  mbalimbali ,mwenyeji ikiwa Nchi ya Korea kusini  jana  jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
 Mkutano wa mafunzo kwa njia ya mtandao ukiendelea, huku mada kuu ikiwa ni upangaji wa miji na majiji sambamba na utunzaji wa mazingira.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mjadala wa moja kwa moja kutoka Korea kusini.

NAMNA YA KUKATA RUFAA KWA WALIOFUKUZWA KAZI KWENYE UTUMISHI WA UMMA.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.

Wapo watumishi wa umma ambao wameachishwa kazi kwasababu mbalimbali na wanahisi kuwa pengine haki haikutendeka lakini hawajui la kufanya. Basi waelewe la kufanya lipo na ni rufaa. Na wengine wanajua kuwa ni rufaa yumkini wasijue rufaa yenyewe inakatwa kwa utaratibu upi. Nitaeleza hapa, lakini kwanza tujue nani mtumishi wa umma anayeongelewa hapa.

1.NANI MTUMISHI WA UMMA.
Sheria namba 8 ya 2002, Sheria ya Utumishi wa Umma , iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 18 ya 2007 imemueleza mtumishi wa umma. Kifungu cha  3  kinasema kuwa mtumishi wa umma ni yule anayefanya kazi katika ofisi yoyote ya umma. Ili uelewe vizuri mtumishi wa umma anayeongelewa katika sheria hii na katika makala  haya ni yule mfanyakazi/mwajiriwa wa serikali.  Kwahiyo watumishi wa bunge, maafisa wa mahakama, na wafanyakazi wa taasisi/kampuni binafsi  taratibu hizi za rufaa zinazoelezwa humu haziwahusu.

Tunaongelea watumishi wa serikali kuu, za mitaa, mashirika ya umma, idara na taasisi zote zilizopo chini ya serikali tukiondoa wale wa uteuzi japo nao wanaongozwa na sheria hii. 

2.  HAKI YA RUFAA.
Unapokuwa umesimamishwa kazi rufaa ni haki yako ewe mtumishi. Rufaa sio kuonesha ukorofi, sio kuwa mjuaji, sio kupingana na serikali, na sio kukosa utiifu. Rufaa ni haki kama zilivyo haki nyingine za mshahara, likizo, nk. Usiogope kukata rufaa kwani hata huyo aliyekusimamisha kazi naye akisimamishwa anakata rufaa.
Kifungu cha 25( 1 ) (b) cha Sheria ya utumishi wa umma ndicho kinachoeleza haki hii. Kadhalika kwenye barua yako ya kuachishwa kazi  au siku ya kusimamishwa, yafaa na ni haki uelezwe haki hii ya rufaa. 

                   KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

FINCA Microfinance kutoa zaidi ya Milioni 10 kwa Wamiliki wa Biashara ndogo ndogo

$
0
0
· Shindano la miezi mitatu lina lengo la kutoa elimu ya fedha na biashara kwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo. 

· Benki ya FINCA Microfinance inaendelea kuwa benki ambayo inahamasisha  ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi ya uwepo wake nchini Tanzania. 

Tarehe 26 Juni, 2018 Dar es Salaam - Benki inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania, Benki ya FINCA Microfinance leo imetangaza uzinduzi wa programu ya miezi mitatu na shindano ambalo linalengo la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, ufahamu na kisha kuwapatia zaidi ya TZS Millioni 10 kwa wazo bora la biashara litakalokuwa limewasilishwa. 

Shindano linalojulikana kama 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege. 

Akiongea wakati wa uzinduzi jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John alisema kwamba lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa  biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao, Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo. 

"Shindano hili litashirikisha wateja wa FINCA wenye akaunti na wale ambao wanapenda kushiriki watatakiwa kufungua akaunti ya FINCA, ambao pia watatakiwa kuweka kiasi cha TZS 20,000 (Salio jipya katika akaunti zao) Watatakiwa kujaza fomu katika matawi ya FINCA ambapo watabainisha katika fomu hizo kuwa wataenda kufanyia nini zawadi hiyo katika biashara zao iwapo wataibuka kuwa washindi. Baada ya hapo fomu hizo zitawasilishwa katika matawi yetu, mpaka hapo watakuwa wametimiza vigezo vya hatua ya kwanza ya shindano". 

"Hatua ya pili, washindani 8 watachaguliwa na jopo la majaji kushiriki katika kipindi cha TV ambacho kitajulikana kama ‘Kuza Ofisi na FINCA’ kitakachokuwa kinarushwa kupitia TVE. Mwishoni mwa shindano, mshindi mmoja mwenye bahati ataondoka na zawadi nono ya zaidi ya TZS milioni 10", Alisema Nicholous, akiongeza kwamba washiriki wengine wenye vigezo pia watakuwa na nafasi ya kujipatia mikopo kutoka benki hiyo. 

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Biashara wa benki ya FINCA Microfinace Benki, Emmanuel Mongella amesema: "Kampeni ya Kuza Ofisi na FINCA ni sehemu ya FINCA kusherehekea miaka 20 ya uendeshaji wa shughuli zake nchini Tanzania ambapo benki ya FINCA imekuwa maarufu kwa utoaji wa masuluisho bora na aina mbalimbali za akaunti, Mikopo na huduma zingine ambazo zinajumuisha mahitaji ya watu binafsi na taasisi." 

Mongella pia aliongeza kuwa "Ushirikishwaji wa Kifedha na Uvumbuzi wa Kidigitali ni msingi wa biashara yetu, Shindano hili ni ahadi nyingine ambayo Benki ya FINCA Microfinance inatoa kwa watanzania kwamba iko kwaajili ya kuwasaidia katika misaada ya kifedha kupitia elimu na kuwawezesha wateja wetu kuweza kupata maendeleo endelevu ya biashara zao”. 

"Kwa hiyo tunawakaribisha wamiliki wote wa biashara ndogo ndogo walioko Dar es salaam kujiandikisha na kushiriki katika shindano kwa sababu shindano hili ni kwaajili yao. Wateja wote wa Benki ya FINCA Microfinance Banki na wale ambao sio wateja wetu wanapaswa kutembelea matawi yetu ya Dar es salaam kwa maelezo zaidi ambako pia watapatiwa msaada wa mahitaji yote wakati wa kujaza fomu. 

John pia alihitimisha kuwa "Hii ni nafasi kwa wamiliki wa biashara ndogo walioko Dar es salaam kuchangamkia fursa hii adimu na kuja kufungua akaunti na kushiriki katika shindano ili waweze kuwa washindi wa zawadi ambazo zitakuza biashara zao"

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance, Nicholous John (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la Kuza Ofisi na FINCA linalenga kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao. Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo. 

Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. 

Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, mmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. 
Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. 

Shindano la 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. 

Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Benki ya FINCA Microfinance imesema kwamba karibisha wamiliki wote wa biashara ndogo ndogo walioko Dar es salaam kujiandikisha na kushiriki katika shindano kwa sababu shindano hili ni kwaajili yao. Wateja wote wa Benki ya FINCA Microfinance Banki na wale ambao sio wateja wetu wanapaswa kutembelea matawi yetu ya Dar es salaam kwa maelezo zaidi ambako pia watapatiwa msaada wa mahitaji yote wakati wa kujaza fomu.

TRA YAKAGUA MASHINE ZA EFD

$
0
0
JOSEPH MPANGALA, MTWARA 

Mamlaka ya mapato mkoani Mtwara wamefanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya maduka kukagua mashine za kutolea risiti na kujionea kama wafanyabiashara wanatoa risiti lakii pia kama wateja nao wanadai risiti baada ya kufanya manunuzi.

Operesheni hiyo ambayo imeongozwa na kamishna msaidizi wa kodi za ndani operesheni ,Abdul Zuberi wamefanya ukaguzi katika maduka mbalimbali na kutoa elimu kwa baadhi ya wateja waliokuwa wakifanya manunuzi.

Zuberi amesema zipo changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na baadhi ya wafanyabiashara ikiwemo mashine hizo kusumbua katika utoaji wa risiti

Pia amewataka wafanyabiashara ambao mashine zao zinapowasumbua kuwasiliana na wasambazaji wake na pindi wakikosa ushirikiano waende TRA kwa ajili ya ufumbuzi kwani mashine hizo zinakuwa hazina tatizo.

“Mkiona hampati huduma nzuri kutoka kwa wasambazaji mje TRA, kuna bwana mmoja alikuwa analalamikia mashine yake lakini kupata ushirikiano kutoka kwa msambazaji tumefika tumekuta ile mashine haina tatizo,”amesema Zuberi.
Kaim Kamishna wa Kodi za Ndani Operesheni Abdul Zuberi wakiwa na Meneja wa Kodi TRA Lucas Igembe Wakijadiliana Jambo mara baada ya kumaliza Ziara ya Kutembelea Maduka ya wafanyabishara kwa lengo la Kuhakiki Utumiaji wa Mashine za EFD Mkoani Mtwara.
Kaim kamishna waKodi za ndani Operesheni Abdul Zuberi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Duka la uzwaji wa Vipuli la Prashant Mkoani Mtwara Sunil Janaksihn Gandhi wakati akitoa maelezo juu ya Utoaji wa risiti kwa wateja wake Mkoani Mtwara.
Mfanyabishara wa uuzaji wa Duka Kubwa {Supermarket} Dickson Mroso akitoa maelezo jinsi ya Utoani wa risisti kwa Wateja kwa Kutumia Mashine ya EFD kwa Kaim kamishna wa Kodi za Ndani Operesheni Abdul Zuberi mara baada ya Kutembelea katika Duka Hilo kwa Lengo la kutazama Matumizi sahihi ya Risisiti Mkoani Mtwara. 
Lucas Igembe Afisa Kodi TRA akihakiki Utoaji wa Risisti Uliotolewa kuanzia mwezi Juni kwa Kutumia mashine za EFD katika Duka Kubwa,Pembeni yake ni Meneja wa duka Hilo Dickson mroso.

Rais wa Zimbabwe nchini kufanya ziara ya kikazi nchini

$
0
0
Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe atafanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania tarehe 28 hadi 29 Juni, 2018. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Rais Mnangagwa nchini Tanzania tangu aingie madarakani mwezi Novemba, 2017.

Lengo la ziara hii ya Rais wa Zimbabwe ni kujitambulisha kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu aingie madarakani, Mheshimiwa Rais Mnangagwa ameshafanya ziara katika nchi za Namibia, Zambia, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Botswana.

Ziara hii ni muhimu kwa Tanzania kwani itatoa fursa ya kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia, kihistoria, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili. Ziara hii pia itatoa fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili ya kikanda na kimataifa.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Rais Mnangagwa atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Rais Mnangagwa anatarajiwa pia kutembelea Chuo cha Sanaa cha Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika na Mhe. Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho. Mhe. Rais Mnangagwa anatarajiwa kuondoka tarehe 29 Juni 2018 kurejea chini Zimbabwe.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam, 27 Juni, 2018

WAGONJWA 20 WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO WA KUFUNGUA KIFUA KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU YA MOYO

$
0
0
Jumla ya wagonjwa 20 ambao ni watu wazima wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita iliyofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India .

Wagonjwa hao wamefanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) tumefanya kwa wagonjwa nane (8), kubadili valvu mbili za moyo (Valve Replacement) kwa wagonjwa 10, upasuaji wa kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic Aneurysm Repair/Bental Procedure) na mgonjwa mmoja alitolewa damu iliyokuwa imeganda kwenye mshipa wa moyo (Blood Clot).

Wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na wote wameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu pamoja na kufanya mazoezi. Ndani ya siku chache zijazo tutaanza kuwaruhusu baadhi ya wagonjwa ambao hali zao zimeimarika kurudi nyumbani.

Aidha katika kambi hiyo iliyoanza tarehe 18 hadi tarehe 23 mwezi huu wa Juni kwa mara ya kwanza tumefanya upasuaji wa kuvuna mshipa wa damu ndani ya kifua upande wa kulia na kushoto na kuunganisha kwenye misuli ya moyo ili kuuongezea moyo damu.

Kambi hiyo pia ilienda sambamba na utoaji wa elimu pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kati ya wageni na madaktari wetu pamoja na wauguzi.

Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri hivyo basi tunawaomba wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na kama wanamatatizo wataweza kupata tiba kwa wakati.

Kutokana na matibabu ya moyo kuwa ya gharama kubwa tunaendelea kuwasisitiza wananchi wajiunge na mifuko ya bima ya afya ambayo itawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapohitaji kutibiwa. Pia itasaidia Hospitali yetu kuendelea kujiendesha yenyewe kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine.

Tunawaomba wananchi waendeleee kuchangia damu kwani wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanahitaji kuongezewa damu kati ya chupa sita (6) hadi saba (7) wakati wanapatiwa matibabu. Taasisi inamkaribisha mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu ambao wanapenda kuchangia damu waweze kufanya hivyo ili tuokoe maisha ya ndugu zetu wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

RAIS WA ZIMBAMBWE KUWASILI NCHINI KESHO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

RAIS wa awamu ya tatu wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa anataraji kuwasili nchini mapema kesho kwa ziara ya siku mbili kuanzia June 28 hadi 29 mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameeleza kuwa Mnangagwa atapokelewa katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Nyerere na mwenyeji wake Rais John Magufuli majira ya saa tano kamili asubuhi.

Aidha ameeleza kuwa ujio huo wa Rais wa Zimbabwe una lengo kuu ambalo ni kudumumisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya Tanzania na Zimbabwe tangu wakati wa kupigania uhuru wa taifa hili la kusini mwa Afrika.

Makonda amesema kwamba Mnangagwa ataondoka nchini june 29 asubuhi akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Magufuli na ametoa wito kwa wakazi wa Dar es salaam kumkaribisha mgeni na wageni wote waingiao nchini kwa kuwafanya wajisikie wako nyumbani kwa muda wote watakaokuwa jijini.

Ikumbukwe kuwa hii ni ziara ya kwanza ya Rais Mnangagwa wa Zimbabwe kufika nchini Tanzania tangu alipoingia madarakani Novemba 2017.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu ziara ya kikazi  ya Rais wa Zimbabwe Mh. Emerson Mnangagwa.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

MKUU WA MKOA WA IRINGA AWAFUNDA MAKANDARASI WANAWAKE

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, amewataka makandarasi wanawake wote nchini kufanya kazi kwa kujiamini na kutooneana wivu katika maeneo yao ya kazi.

Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuwawezesha makandarasi wanawake kufikia madaraja ya juu ya ukandarasi ili kuwawezesha kuchukua kandarasi kubwa, na hivyo kuinua kipato chao kitakachopelekea kuondokana na umaskini katika familia na jamii zinazowazunguka.

Ametoa wito huo mkoani Iringa, wakati akifungua mafunzo elekezi kwa makandarasi wanawake wa mikoa ya nyanda za juu kusini katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara hapa nchini na kusema kuwa mashindano yao yawe ni ya kutimiza wajibu na siyo kushindana katika kuvaa wala kusuka.

"Nataka mwanamke wa kitanzania ujiamini na kusimama vyema na kusonga mbele kwani sifa yetu kubwa ni kuhakikisha tunatunza familia kwa hali yoyote, wajibikeni ipasavyo katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara bila woga wowote", amesema Mhe. Masanze.

Aidha Mhe. Masenza, amesisitiza umuhimu wa makandarasi hao kujaza nyaraka za zabuni na mikataba wenyewe ili kuepukana na utapeli na baadhi ya watu wanaojidai wanawasaidia shughuli hizo. Amewataka makandarasi wanawake hao kufanya kazi kwa ushirika na sio mmoja mmoja ili kuweza kumiliki kampuni au vikundi vya ujenzi ambavyo vitawasaidia kupata zabuni za miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.

Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake kutoka Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Rehema Myeya, amesema mafunzo hayo yatawasaidia makandarasi wanawake hao kuwajengea uwezo wa namna bora ya kujaza makabrasha ya zabuni pamoja na kusimamia mikataba kwa ufanisi zaidi. Ameongeza kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo katika nyanja za uongozi na namna bora zaidi za kutunza mahesabu na fedha ili waweze kuona faida ya kazi zao.

Naye Bi. Gisela Gongo kutoka mkoa wa Iringa amezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili makandarasi hao ikiwemo uelewa mdogo wa namna ya kujaza mikataba na kulalamikia kuwa lugha zinazotumika kwenye mikataba hiyo kuwa sio rafiki na hivyo kuwasababishia kukosa kazi nyingi za ujenzi na matengenezo ya barabara.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel Kindole, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufungua mafunzo hayo ambayo yanalengo la kuwaongezea uwezo na idadi ya makandarasi wanawake hapa nchini. Jumla ya makandarasi wanawake 35 kutoka katika mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa na Katavi wameshiriki mafunzo hayo yakiwa na lengo kuu la kuwajengea uwezo zaidi ili waweze kushiriki na kushindana katika kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara hapa nchini.


Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano .

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, akihutubia makandarasi wanawake kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo. 
Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake kutoka Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Rehema Myeya, akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kulia), kufungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo makandarasi wanawake katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo.
Baadhi ya makandarasi wanawake kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa na Katavi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani Iringa.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel Kindole, akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, mara baada ya kufungua rasmi mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo kwa makandarasi wanawake katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani Iringa. 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza akiwa katika picha ya pamoja na makandarasi wanawake kutoka mkoa wa Iringa baada ya kufungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

WAHANDISI CHANGAMKIENI UWEKEZAJI WA VIWANDA-MWIJAGE

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amewataka wahandisi nchini kuchangamkia fursa za uwekezaji katika viwanda nchini ili kuiwezesha Serikali kufikia lengo la uchumi wa kati na jumuishi ifikapo 2025.

Akifungua kongamano la siku moja la wahandisi kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo, Mhe Mwijage amesema mchango wa wahandisi ni muhimu sana katika kipindi hiki ili kuwezesha taifa kufikia uchumi wa kati wenye uwiano kati ya pato la nchi na uchumi wa mwananchi.

“Tumejipanga kuanzisha viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na hivyo kugusa uchumi wa wananchi wengi” amesema Mhe. Mwijage.

Amesema uwekezaji katika viwanda vya sukari, mafuta na vifaa vya ujenzi ambavyo vyote malighafi zake zinapatikana nchini, utawezesha idadi kubwa ya wananchi wa Tanzania kupata ajira na hivyo kufikia lengo la Taifa la uchumi wa kipato cha kati. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Nchini (ERB), Eng. Profesa Ninatubu Lema ameiomba Serikali kuthubutu kuwaamini wahandisi wazalendo kusimamia na kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi hapa nchini.

Prof. Lema amesema wahandisi wako tayari hata kupewa sehemu kidogo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya (Standard Gauge), ili nao waweke alama ya uzalendo katika mradi huo mkubwa unaotekelezwa nchini. “Tunapoadhimisha miaka 50 ya ERB tuko wahandisi tuliosajiliwa zaidi ya Elfu 21 tunaweza kufanya kitu kama alama kwa taifa na vizazi vijavyo”, amesema Prof. Lema.

Amewataka wahandisi kutathmini namna gani wanaweza kuendeleza kilimo na viwanda nchini ili kuweza kubadili uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla katika miaka ijayo.

Kaimu Msajili wa ERB, Eng. Patrick Barozi amesema kongamano la wahandisi kuhusu uchumi wa viwanda ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya wahandisi yanayofanyika katika sekta mbalimbali za kihandisi yatakayofikia kilele chake mwezi Septemba mwaka huu yakiwa na lengo la kuwaweka wadau wa uhandisi pamoja kutafakari na kuhamasishana kuhusu namna bora ya kuendeleleza taaluma ya uhandisi kukuza uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja.

Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Nchini (ERB) Eng. Profesa. Ninatubu Lema kabla ya kufungua kongamano la siku moja la wahandisi kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza jambo wakati akifungua kongamano la siku moja la wahandisi (hawapo pichani) lililowakutanisha kujadili kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo. Kulia ni Kaimu Msajili wa Wahandisi, Eng. Patrick Barozi.
Sehemu ya wahandisi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku moja la wahandisi kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia) akifurahia jambo na wahandisi mara baada ya kufungua kongamano la siku moja la wahandisi kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo.

 

RC Wangabo ashauri gereza kutumia ekari elfu 11 kwa kilimo cha alizeti na kahawa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameshauri jeshi la magereza kuhakikisha wanazitumia ekari 11,000 zinazomilikiwa na jeshi hilo kwaajili ya mazao ya alizeti pamoja na kahawa ili jeshi hilo liweze kujipatia fedha za kutatua changamoto mbalimbali walizonazo na kuongeza uzalishaji wa mazao hayo katika taifa.

Amesema kuwa nchi ya Tanzania huagiza asilimia 60 ya mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi wakati jeshi la magereza lina ardhi nzuri na ya kutosha kwaajili ya kuzalisha zao la alizeti kwa wingi na hatimae kupunguza uwingi wa mafuta unaoagizwa kutoka nje na kuokoa mabilioni ya fedha yanayotumiwa na serikali katika kununua mafuta hayo.

“Pamoja na kuinua uchumi lakini pia tunaweza kulisha nchi yetu kwa mafuta, sisi mkoa wa Rukwa tupo katika hali nzuri ya kulima alizeti na kuchangia kupunguza pengo la mafuta yasiendelee kuagizwa kutoka nje, tumejipanga kama Mkoa, karibu kila kaya inayolima iweze kuwa na angalau ekari moja ya alizeti, na kwenye majeshi yetu hapa mna ekari hizi 11,000 mnaweza kuzalisha na kupata ekari za kutosha kutatua changamoto mlizonazo,”Alisema. 

Ameongeza kuwa kwa kuanzia jeshi hilo linaweza kutumia ekari 1000 kuanza kulima na kuona mafanikio yake ndani ya mwaka mmoja kwani kwa mujibu wa Great African Food Company (GAFCO) wanaofanya kilimo cha mkataba hununua kilo moja ya alizeti kwa shilingi 900 huku gunia moja likiwa na kilo 70 na kila ekari moja hupata gunia zisizopungua 15 matokeo yake tunaweza kupata 945,000,000/= na kuwataka magereza kushirikiana na GAFCO ili kufanikisha zozi hilo.

Ameyasema hayo alipofanya ziara fupi katika gereza la Mollo lililopo katika kata ya Mollo, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ili kujionea miradi ya maendeleo ya gereza hilo linalomiliki ekari 11,000 huku wakitumia ekari 400 kwaajili ya kilimo cha mahindi na maharage pamoja na uzalishaji wa mbegu za mahindi.

Kwa upande wake akisoma risala ya gereza Mkuu wa Gereza la Mollo ACP John Mwamgunda amesema kuwa gereza hilo limekuwa na changamoto kadhaa ikiwemo uchakavu wa vifaa vya kilimo, sare za wafungwa na majengo amabyo ni ya siku nyingi lakini alikubali kuwa uzalishaji wa alizeti ni rahisi zaidi ukilinganisha na uzalishaji wa mahindi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji, Tanzania hutumia Shilingi bilioni 189.6 kila mwaka kununua mafuta ya kula nje ya nchi huku ikizalisha tani 91,000 ambayo ni sawa na asilimia 40 za mafuta hayo tofauti na makadirio ya tani 200,000 hadi 300,000 ya uhitaji wa bidhaa hiyo kwa mwaka.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo(mwenye kofia nyekundu) akisalimiana na mmoja wa maafisa wa gereza la Mollo lililopo Manispaa ya Sumbawanga muda mfupi kabla ya kutembelea miradi inayoendeshwa na gereza hilo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo(mwenye kofia nyekundu) akiwashauri Mkuu wa Gereza la Mollo ACP John Mwamgunda pamoja na Kaimu Mkuu wa magereza mkoa wa Rukwa ACP Ihunja juu ya kujikita na kilimo cha alizeti kwa faida ya gereza na faida ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo(mwenye kofia nyekundu) pamoja na maafisa wengine wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfana Haule (kaunda suti ya kijivu) wakiaangalia moja ya majosho ya mifugo ya gereza hilo.

'UMASIKINI NI MOJA YA SABABU INAYOCHANGIA MIMBA, NDOA ZA UTOTONI'

$
0
0
Na Woinde Shizza ,Mwanza

 IMEELEZWA sababu kubwa inayosababisha mabinti wadogo kujiingiza kwenye vitendo vya kujamiana na hatimaye kupata mimba na ndoa za utotoni ni umasikini katika jamii wanazotoka.

Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) ambaye pia ni Balozi wa Kampeni  ya Binti wa kitaa Angello George wakati akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya BINTI  WA KITAA iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mwanza .

Kampeni hiyo inakuja ikiwa ni siku chache toka Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsi ,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndungulile kueleza kuwa tangu Januari hadi Aprili Mkoa wa Shinyanga takribani mimba 18,000 za utotoni zimepatikana.

Hivyo amesema kampeni hiyo itahusisha mikoa yote ya Kanda ya Ziwa naitafanyika kwa muda wa zaidi ya  mwaka mmoja kwa lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba na ndoa za utotoni  nchini.
"Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazosababisha mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,"amesema.

Ameongeza Binti wa kitaa imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 18 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani.
Amesema wanatarajia kwenda kuifanya kampeni katia mikoa zaidi ya 20 nchini huku ikiwa na ajenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa kitanzania.
  
Ameongeza kuwa yeye kama mtanzania ameguswa na tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hasa katika kipindi hiki cha utandawazi, hivyo anaamini kupitia kampeni hiyo jamii itaelimika.
"Inauma kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi tano duniani  zinazotambulika kwa janga la mimba na ndoa za utotoni.

"Hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo,"amesema Angello.Sambamba na uzinduzi huo uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mwanza , Balozi Angelo ametoa mwito kwa watanzania wote kuunga mkono kampeni hiyo  ili kuwasaidia mabinti kuepukana na mimba a ndoa za utotoni.

Nao wanafunzi  kwa nyakati tofauti wamesema ili kufikia malengo yao jamii ya kitanzania iwasaidie kuwalinda na kuwajengea uwezo wa kujitambua .
 Moja ya mabinti waliohudhuria katika uzinduzi huo ni Veneranda Paul ambaye amewaomba wazazi kushiriki kikamilifu kwenye kampeni hiyo.

 Kwa upande wa Mwalimu wa Malezi katika shule hiyo Mwanambesi amesema ili Tanzania iwe salama na yenye maendeleo ni jukumu la kila mtanzania kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF) inayoendesha  kampeni ya BINTI WA KITAA   Angelo David George akiwa anazungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Mwanza,namna ya kuepuka mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni  .
Wanafuzi wa shule ya  Mwanza Sekondari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) ambaye pia ni Balozi wa kampeni ya BINTI WA KITAA  Angelo George  wa pili kushoto (Picha na Woinde Shizza,Mwanza) 
Mmoja wa Wazazi alieyehudhuria katika uzinduzi huo, Bi Carol Nzogere akizugumza na wanafunzi

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images