Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1606 | 1607 | (Page 1608) | 1609 | 1610 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imetangaza kuboresha mfumo wake wa mauzo na usajili wa laini za simu na sasa watakaofanya hivyo ni mawakala waliothibitishwa.

  Uamuzi huo ni mkakati wa kudhibiti usajili na mauzo ya laini za simu za Halotel ikiwa ni hatua ya kukabiliana na udukuzi au udanganyifu wowote unaoenda kinyume na sheria za mawasiliano nchini.

  Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema kampuni hiyo imepunguza idadi ya mauzo ya laini za simu kwa mawakala, lakini pia mawakala watauziwa laini nyingine mpya mara tu watakapokuwa wamemaliza mauzo ya laini za simu za awali pamoja na kuthibitisha kuwa laini walizopewa zimesajiliwa kwa wateja kwa kufuata taratibu zote za usajili zilizowekwa na mamlaka husika”.

  “Tumeweka mfumo thabiti wa kudhibiti uuzaji wa laini za simu na usajili kutoka kwa mawakala wetu, hili pia limeambatana na uhakiki na usajili mpya wa mawakala wote wanauoza laini za simu za Halotel. Alisema Mhina na Kuongeza,

  “Tumewekeza kwenye teknolojia ya kisasa zaidi itakayogundua na kuzuia udukuzi wa aina yoyote ya mifumo ya mawasiliano, Tunafanya haya yote ili kuongeza ufanisi pamoja na kuwadhibiti watu wenye nia ovu ya kutumia miundombinu ya mawasiliano kuvunja sheria” alisema Semwenda.

  Alisisitiza kuwa mara zote, kampuni hiyo inafuata kanuni na sheria zilizopo ndiyo maana imekuwa ikiwekeza fedha nyingi ili kufikisha huduma bora kwa Watanzania hivyo haipo tayari kushuhudia watu wenye niaovu wakiharibu malengo mema yaliyopo.

  “Uwekezaji mkubwa uliofanywa kwa miaka miwili iliyopita nimatokeo ya ushirikiano mwema baina ta Tanzania na Vietnam. Ni uhusiano huo uliochangia kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili hivyo Halotel itaendelea kuzingatia sheria na kanuni za nchi pamoja na kuendelea kuboresha na kutoa huduma zenye gharama nafuu kwa Watanzania,” alisema Semwenda.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu uboreshwaji wa mfumo wa uuzaji na usajili wa laini za simu. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Halotel Stella Pius. 

  0 0

  Fursa ya kwanza ya uandaaji wa mashindano maarufu ya mbio za mbuzi imekua ya mafanikio kwa Klabu ya Rotary ya Oysterbay. Tukio hilo lenye burudani ya aina yake lilikwenda kwa Motto wa ‘Wakanda Goat are You’, na kuvuatia watu zaidi ya 4,500 waliokusanyika katika eneo la The Green, Oysterbay kwa ajili ya kushuhudia mashindano hayo. 

  Matukio muhimu yaliyofuata baada ya mbio hizo ni mchezo wa bahati nasibu ambao uliwezeshwa na wafadhili wa hapa nyumbani pamoja na gwaride la kuonyesha mavazi, ambapo watu mbalimbali walipata fursa ya kuonyesha mavazi yao aina ya Wakanda kwa kurejelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.

  Ni mwaka wa kumi na nane mfululizo wa mashindano hayo lakini kwa mwaka wa kwanza chini ya Rotary Goat Races, tukio hili maarufu la kifamilia lilivutia maelfu ya watu siku ya tarehe 23 Juni. Tukio hilo likifanyika katika eneo la ‘The Green’ chini ya motto wa ‘Wakanda Goat are You”, wahudhuriaji walifurahia aina saba za mbio, vyakula vya aina mbalimbali vya hapa nyumbani, zawadi kubwa mbalimbali za bahati nasibu, michezo ya kuweka dau na gwaride la ushindani la mavazi ya Wakanda.

  Mashindano hayo yalianza kwa mbuzi kusimama kwenye mstari wa mwanzo wa mashindano, huku watazamaji wakivuta pumzi kuona mbuzi wanavyopigania ushindi wa kuwa namba moja.

  KAtika raundi ya kwanza Mbuzi aliyeibuka kidedea ni namba 8 ambapo zawadi yake ilidhaminiwa na Kampuni ya vinywaji ya CocaCola, Raundi ya pili mbuzi namba 7 aliibuka mshindi na zawadi yake kudhaminiwa na East Africa TV/Radio huku raundi ya tatu mbuzi namba tisa akikiibuka mshindi na zawadi yake kudhaminiwa na Kampuni ya Aggreko. 

  Wamiliki wa mbuzi hao walisherehekea ushindi huo kwa staili ya kipekee na watu ambao waliweka dau kwa mbuzi hao kushinda walipokea fedha zao za dau hilo. Katikati ya mbio hizo, michezo ya bahati nasibu kwa washindi wa zawadi kubwa pia ilifanyika na washiriki kadhaa kushinda. Watoto pamoja na watu wazima walipendezesha gwaride la mavazi na kujishindia zawadi kabambe kwa mavazi hayo. Ni wazi watoto walifanya vizuri zaidi kwenye kipengele hiki.

  Viongozi wa mashindano ya mbio za mbuzi, Abdulrahman Hussein na Mathew Hellela walifurahishwa na mwitikio mkubwa wa watu.“Ni mara yetu ya kwanza kuandaa mashindano haya ya mbio za mbuzi na tunafuraha kuwa tukio hili limekuwa la kufana sana kwa kila mhudhuriaji na pia kwa watu kutuamini katika kuwapa kitu kikubwa na cha tofauti kwa mwaka huu”, alisema Abdulrahman Hussein.

  "Pia inaonyesha kuwa timu yetu ya kujitolea, ambayo ilitumia mwezi mzima kuandaa tukio hili, ilikuwa kwenye njia sahihi na nguvu zao leo zimelipa kwa kuwapa wakati mzuri wahudhuriaji wote”, aliongeza Hussein.Kwa upande wake Mathew Hellela aliwashukuru wafadhili wote kwa imani na misaada yao.

  "Tulikuwa wapya katika kuandaa tukio la namna hii na tunashukuru sana kwa imani ambayo wafadhili wametupatia sisi watu wa Klabu ya Rotary katika kufanya jambo lililo sahihi. Mwaka huu ulikuwa mwanzo mzuri na tunatarajia kubeba mafanikio haya kwa miaka ijayo ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary ".

  Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary, Oysterbay alisema kuwa anajivunia sana timu yake na anasubiria kwa hamu kutekeleza miradi ya elimu ambayo Klabu yake itaifanyia kazi hivi karibuni, kwa kutumia mapato ya mbio hizo. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.

  Mashindano ya mbio za mbuzi kwa mwaka huu yamefadhiliwa na Resolution Insurance, SWISS, Toyota, Coca Cola, East Africa TV/Radio, Aggreko, SBL, Mastercard, Le Grand Casino na Red ‘n White. Michango ya ukarimu pia imetoka kwa JC Decaux, PM Group, Almar Containers TZ, SBS, Abstrat, The Slipway Hotel na Pizza Hut pamoja na Advertising Dar, ALAF-Safal Group, Britam Insurance, Selcom Paytech, VClick Professional Photography, WS Insight, Green Waste Pro na CAPS Limited.

  Michezo ya bahati nasibu ilipewa nguvu na SWISS, SBL, The Sea Cliff Hotel, The Slipway Hote, Zen Spa, Engen, Coastal Airlines na 305 Karafuu Restaurant. Michango mingine ilitoka Kwa kampuni za:-Jumia, Advertising Dar, Splendid Cleaners, TAN Management – Insurance broker, Merrywater, Vet Care, Dar Signs, Karafuu Restaurant, Prime Advertising, Reader Rabbits, World Link.

  Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay ilianzishwa mwaka 2009 na hadi sasa ina wanachama 70. Ni klabu kubwa zaidi miongoni mwa Klabu nane za Rotary jijini Dar es Salaam na inasaidia jamii katika miradi mbalimbali ikiwemo: Mpango wa Afya ya Jamii ambao huandaa makambi ya matibabu ya mara mbili kwa mwaka kwa vijijini na mijini, mradi wa Vijana Poa wa kusaidia vijana wa chuo kikuu kupata kazi mbio za Rotary Dar, kusaidia kazi za hospitali ya CCBRT na Rotary Mission Green ambazo ni jitihada za wilaya za kupanda miti. 

  Zaidi ya hayo, Klabu ya Rotary ya Oysterbay kwa sasa inajenga Rotary Community Corps, mradi ambao umejikita katika kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wanufaika katika jamii. Mapato yote ya mbio za Mbuzi za Rotary yatatumika kwenye miradi ya elimu ya Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay, kama mpango wa ufadhili wa elimu ambao unawasaidia wanafunzi wa Chuo Kikuu nchini Tanzania, nipe fagio na Shule ya Msingi Msasani.
  Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwa wamewabeba mbuzi wao tayari kushiriki mbio hizo wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
  Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwakimbiza mbuzi wao wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
  Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
  Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu. 
  Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  WANANCHI wa Vijiji vya Kinyinya na Nyagwijima katika Kata ya Mgunzu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wametakiwa kushirikiana na viongozi wao kujenga nyumba za askari kwa lengo la kupunguza vitendo vya utekaji katika eneo la Kosovo wilayani humo.

  Akizungumza jana kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema katika Wilaya ya Kakonko masuala ya utekaji yamepungua.

  Ameongeza yamebaki katika maeneo machache ambayo hayafikiki kiurahisi huku akiwahimiza wananchi kutoa ushirikiano kujenga nyumba za askari ili wakae maeneo hayo na kukomesha vitendo hivyo."Wananchi wanatakiwa kujitoa kwa michango na kujitoa wenyewe kujenga, kwakuwa wanatekwa na kuporwa mali zao ni wananchi wenyewe.

  "Serikali inatoa msaada mkubwa wa Kuleta maendeleo kwa wananchi, hivyo wanatakiwa kujitoa katika vijiji vyao kutokomeza vitendo hivyo.Niwaombe viongozi wa Kijiji muendelee kuhimiza suala hili la kujenga nyumba,"amesisitiza.Aidha amewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanao wadanganya na kuwashawishi wasijitolee kuleta maendeleo.Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mgunzu Andrea Mashama amesema mkapa sasa wanaendelea kuhimiza wananchi kujitolea.

  "Tumeitisha mkutano na tukakubaliana kila mwananchi kuchanga Sh.1000, hivyo wananchi wanaendelea na michango kufanikisha ujenzi wa nyumba ya Mganga na Kituo cha Afya na kufanya shughuli zingine za maendeleo kwa wananchi wote wa Kinyinya na Nyagwijima,"amesema.

  Kwa upande wao baadhi ya wananchi akiwamo Joachim Jolamu amesema wananchi wanaumia kwani wamekuwa waikiibiwa mazao pamoja na fedha."Tukuahidi mkuu tutahakikisha tunafanikisha ujenzi ili tuwe salama,"amesisitiza.
   Mkuu wa Wilaya hiyo,Kanali Hosea Ndagala akizungumza kwenye mkutano  mbele ya Wananchi wakati wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi .
   WANANCHI wa Vijiji vya Kinyinya na Nyagwijima katika Kata ya Mgunzu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo,Kanali Hosea Ndagala kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi 

  0 0

  Na Estom Sanga-TASAF.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF-bwana Ladislaus Mwamanga amewataka Maafisa Ufuatiliaji wa Mfuko huo –TMOs- kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuzingatia maslahi ya taifa .

  Akifungua mafunzo ya Maafisa Ufuatiliaji kutoka mikoa ya Arusha, ,Kilimanjaro,Singida,Tanga , Mbeya ,Iringa,Katavi,Njombe,Songwe ,Ruvuma na Rukwa katika ofisi za TASAF jijini Dar es salaam ,Mwamanga amesema utendaji kazi wa Watumishi hao unapaswa kuendana na matakwa ya Serikali ya kuhimiza uwajibikaji na kufanya kazi kwa kujituma kwa maslahi ya Wananchi.

  Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema maeneo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kote yameonyesha mafanikio ya kujivunia na hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni kuandaa mazingira wezeshi na kuwapatia mbinu sahihi Walengwa za kuendesha shughuli za uzalishaji mali ili hatimaye waweze kuondokana na umaskini. 

  Bwana Mwamanga pia amewaagiza Maafisa Ufuatiliaji hao kujenga mahusiano mema na Idara nyingine zilizoko kwenye maeneo yao ya kazi ili kuweka mazingira rafiki kwao kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi unaokusudiwa.Ameonya kuwa pale ambapo utendaji kazi wa Maafisa hao utabainika kutoridhisha , Uongozi hautasita kuchukuwa hatua zinazopaswa kulingana na taratibu za utumishi wa Umma , kwani amesema Wananchi hususani Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanahitaji huduma bora na si vinginevyo.

  Mafunzo hayo yanayotolewa kwa Kanda ,yanaendeshwa na Wataalamu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha yanalenga kuwapatia Maafisa Ufuatiliaji hao stadi sahihi za uongozi na kuboresha usimamizi mzuri wa shughuli za Taasisi, mbinu bora ya usimamizi wa shughuli za Mpango na kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wakati na ufanisi .

  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendesha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja nchini kote kwa lengo la kuboresha maisha ya kaya husika huku mkazo maalum ukiwekwa katika sekta za Elimu, Afya,Lishe na Uzalishaji Mali ili kuongeza kipato cha Walenga na jamii inayowazunguka.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye mafunzo ya Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF yanayofanyika kwenye ukumbi wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF –TMOs wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Ladislaus Mwamanga(hayupo pichani)
  Baadhi ya Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF –TMOs wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani)
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi,meneja na Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF baada ya kufungua mafunzo yao kwenye Ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es salaam leo.

  0 0

  Na Grace Semfuko, Maelezo

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga imewekeana saini na Kampuni ya Kanton Investment kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata zao la mihogo, ikiwa ni juhudi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuvutia wawekezaji nchini.

  Ujenzi wa kiwanda hicho utakaogharimu Dola milioni 10 unatarajia kuchakata tani 200 za mihogo pamoja na kusafirisha tani 400,000 za wanga kutoka katika tani milioni 1.6 za mihogo mibichi itayosafirishwa nchini China.

  Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki Wilayani Handeni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kanton Investment, John Rwehumbiza wakati wa hafla ya utiaji saini wa maktaba wa makubaliano hayo iliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali.

  Rwehumbiza amesema kampuni hiyo imeanza majaribio ya kununua na kusafirisha nje ya nchi zao la Muhogo na kuonesha kupendwa raia wa China, na hivyo kuahidi kufanya uwekezaji kwa kujenga kiwanda cha wanga na kununua mihogo ya wakulima na kuisafirisha nchini humo.

  Aidha ameongeza kampuni yake pia imepanga kutoa elimu kwa wakulima wa zao la muhogo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wa zao hilo ambalo litawawezesha kutoa faida kubwa na hasa ukizingatia walaji wengi wa zao hilo wanatoka nje ya nchi ikiwepo China na Japan.

  Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Mafukwe amesema Ofisi yake itahakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hao ili wafanye kazi katika mazingira wezeshi kama ilivyokusudiwa ili kuweza kuwanufaisha wakulima wa Wilaya hiyo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amesema Wilaya yake inayo ardhi ya kutosha ya uwekezaji katika maeneo ya kilimo na viwanda na hivyo makubaliano hayo ya awali yatasaidia kupanua wigo wa biashara ya zao la muhogo.

  “Tunayo ardhi ya kutosha, tunawakaribisha wawekezaji wote na milango ipo wazi na tutatoa ushirikiano wa kutosha na malengo yetu ni kuhakikisha tunakuza uchumi wa wananchi wetu” alisema Gondwe.Ofisa Habari wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Latifa Kigoda amesema lengo la kituo hicho ni kuhakikisha uwekezaji nchini unaleta tija kwa kuzingatia kuwa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania kufikia nchi ya kipato cha uchumi wa kati kupitia viwanda..

  “TIC nia yetu tkuona uwekezaji ukiongezeka siku hadi siku, nia ni kukuza uchumi wa Taifa pamoja na kuunga mkono Dhamira ya Mhe. Rais na Serikali ya Awamu ya Tano viwanda, hivyo ,tunaomba wawekezaji waje kuwekeza nchini,"amesema Latifa. 

  Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ina Kata 21 yenye jumla ya ekari 184,000 za kilimo cha Mihogo, ambapo uwekezaji huo unaelezwa utawezesha wawekezaji wapya kuwekeza katika zao la mihogo, hatua inayolenga kuongeza tija ya kiuchumi kwa Wilaya hiyo ambao asilimia 90 ya wakazi wake ni wakulima.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  WADAU na wataalam wa masuala ya Bima nchini wameshauriwa kufanya kazi kwa weledi,kujiheshimu na kubuni bidhaa mpya na za bei nafuu ili kuwafikia wananchi wote.

  Ushauri huo umetolewa jana na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Bima Nchini (TIRA)Dk. Baghayo Saqware wakati akiwahutubia wanafunzi wanaosoma kozi ya Bima katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mara baada ya matembezi ya utambuzi wa Bima yaliyoanzia katika viunga vya IFM hadi Karimjee.

  "Watoa huduma za bima nchini lazima tuwe na wajihi au taswira njema kwa jamii inayo tuzunguka ,kwani jamii hiyo ndiyo walaji wa bidhaa za bima."Hivyo basi hatunabudi kujiheshimu na hatupaswi kuonekana matapeli,wahuni. Tuoneshe heshima mbele za wananchi wote ili wawe na uthuubutu wa kuwa na bima,” amesema Dk Saqware.

  Amewataka wataalamu wa bima kuwa wabunifu kwa kubuni bidhaa mbalimbali na kuongeza ufahamu wa bima kwa wananchi kwani bima ni kinga na bima ni muhimu kwa kila mwananchi kuwa nayo kwa ajili mali na maisha.Mkuu wa Idara ya wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dk. Mussa Juma amesema IFM kila mwaka hufanya matembezi hayo kwa lengo la kujenga uwelewa kwa wananchi wajuwe umuhimu wa bima katika kuweka kinga ya mali na maisha.

  Amesema matembezi yao ni kuwaelimisha wananchi ikiwa kwa kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kutoa vipeperushi kwa mtu mmoja mmoja pamoja kueleza aina za bima zinazopatikana kwa bei nafuu ili wananchi wa kipato cha chini waweze kumudu.Aidha Dk. Juma amesema kuna changamoto ya wataalamu wa bima na kuongeza pamoja na changamoto za uchache huo bado wanajitahidi kuwafikia wananchi kwa kadri wawezavyo.

  Hata hivyo Sekta hiyo inakumbwa na changamoto ya uwelewa mdogo kwani watu wengi hawajui umuhimu wa bima, hivyo lazima jitihada za msingi zifanyike.
  Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Bima Nchini (TIRA) Dk. Baghayo Saqware akizungumza wanafunzi wa Chuo cha IFM wanaosoma masuala ya bima baada ya kufanya matembezi ya kuhamasisha wananchi kujua umuhimu wa bima.
  Mkuu wa Idara ya wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dk Mussa Juma akizungumza kuhusiana na Chuo kilivyojipanga katika utoaji elimu ya bima kwa vijana na wanaohitaji kutokana na kuwa na soko kubwa la ajira.
  Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anaesomea Bima ,Mkagambage Kyaruzi akizungumza na waandishi kitu ambacho kimemsukuma kusomea bima . 
  Matembezi ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Mawakala wa Bima
  Matembezi ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Mawakala wa Bima
  Matembezi ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Mawakala wa Bima

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akisalimiana na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika Wang Heming alipowasili kwa ajili ya kikao cha maandalizi ya Uwekaji wa jiwe la msingi chuo cha chama Kibaha pamoja na Mkutano wa CPC na Africa , leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
  Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akimpeleka mgeni wake eneo la kufanyia mazungumzo
  Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiongoza kikao cha Wajumbe wa chama cha kikomonisti Cha china (CPC) kwa ajili ya maandalizi ya Uwekaji wa jiwe la msingi chuo cha chama Kibaha pamoja na Mkutano wa CPC na Africa leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma. 
  kikao kikiendelea
  Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akipeana Mkono na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika katika chama cha Kikomonisti China Wang Heming mara baada ya kikao cha maandalizi ya Uwekaji wa jiwe la msingi chuo cha chama Kibaha pamoja na Mkutano wa CPC na Africa leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi akizungumza,leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi akipokea zawadi toka kwa mjumbe wa CPC.
  Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally (kulia) akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika katika chama cha Kikomonisti China Wang Heming pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
  Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally (kulia) akikabidhiwa zawadi ya Picha ya Utamaduni toka kwa Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika katika chama cha Kikomonisti China Wang Heming leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.(Picha na Fahadi Siraji wa UVCCM)
  Picha Mbali mbali za pamoja kati ya Viongozi wa CCM pamoja na Ujumbe wa chama cha Kikomonisti nchini china leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
  Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiagana na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika Wang Heming wa chama cha CPC leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika Wang Heming leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mwl Raymond Mwangwala akiagana na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika Wang Heming leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.(Picha Zote na Fahadi Siraji wa UVCCM)

  0 0


  0 0

  Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam

  Utekelezaji wa mradi wa Farm Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu umeweza kuwafikia wakulima takribani 11,177 ambapo kati yao wanawake ni 5,474 na wanaume ni 5,703 huku kati ya wakulima hao vijana wakiwa ni takribani 5,821 yaani zaidi ya nusu (52%) kutoka wilaya ya Bahi, Manyoni na Babati.

  Hayo yamebainishwa juzi 22 Juni 2018 na Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam.

  Dkt Tizeba alipongeza jitihada hizo kwani zinachangia kukuza kipato cha wakulima na uchumi wa nchi kwa kuingiza fedha za kigeni huku akiwataka watumishi mbalimbali kuwaunganisha wakulima wadogo wadogo katika masoko rasmi na kujenga uelewa wao juu ya vichocheo na fursa za ushiriki endelevu.

  Waziri huyo wa kilimo alilishukuru shirika la Farm Afrika kwa kuona umuhimu na fursa zilizopo katika kilimo cha ufuta katika mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara hivyo kuwanufaisha wakulima kupitia mbinu bora za kilimo cha kisasa katika zao hilo.

  Alisisitiza kuwa zao la ufuta lina fursa kubwa ya soko ambapo kwa sasa mahitaji ya soko ni zaidi ya mara tatu ya kiasi kinachozalishwa kwa mwaka ambapo hali hiyo inatokana na nafasi kubwa kwa wakulima wa ufuta kujipatia kipato na kuboresha maisha yao.

  Alisema kuwa serikali inaweka mkazo mkubwa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta na juhudi hizo zinajidhihirisha katika hatua ambazo serikali inaendelea kuzichukua kwa kuhakikisha uzalishaji wa mbegu za mafuta ndani ya nchi unaongezeka.

  Alisema, kupitia utekelezaji wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili mbegu za mafuta ikiwa ni pamoja na ufuta na alizeti ni miongoni mwa mazao ya kipaumbele ambapo kwa kuanzia msimu wa mavuno ujao zao la ufuta litaingizwa kwenye mfumo wa stakabadhi za ghala na katika kuimarisha upatikanaji wa soko la ziada kwa zao la ufuta na mbegu nyingine za mafuta, Na kuongeza kuwa Bodi ya mazao mchanganyiko kuanza kununua mazao hayo ili kuhakikisha mkulima anapata soko la uhakika zaidi.

  Katika hatua nyingine, Mhe Dkt Tizeba aliwasihi wakulima wa ufuta kote nchini kubadilika kuanza kufanya kilimo biashara na kuachana na kilimo cha mazoea cha kujikimu ikiwa ni pamoja na kujua mahitaji ya soko kwa maana ya ubora wa ufuta na kiasi, kutumia teknolojia hususani zana bora, mbegu bora na mbolea sambamba na kujiunga katika vikundi au ushirika na kuuza kwa pamoja na kuwa na nguvu ya pamoja.
  Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
  Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Farm Afrika Ndg Ryan Whalen akizungumza wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018. 
  Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.
  Baadhi ya wadu waliohudhuria mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.

  0 0


  0 0

  Ulinzi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo ya jirani, unatarajiwa kuimarika zaidi baada ya kuanza mradi maalum wa Faru kufungwa vifaa vya technolojia za kisasa na hivyo kuwalinda na matishio ya ujangili ama kupotea.

  Faru ni miongoni mwa wanyama ambao wapo hatarini, kutoweka duniani, kutokana na kuwindwa na majangili, ambao wamekuwa wakiuza pembe zao na hivyo serikali imekuwa na mikakati kadhaa ya kuimarisha ulinzi wao.

  Akizungumza na wanahabari, Mwakilishi mkazi wa shirika la uhifadhi la kimataifa la Frankfurt zoological Society moja ya mashirika yanayoratibu mradi huo, Gerald Bigulube alisema mradi huo wa aina yake barani Afrika, unatarajiwa kuimalisha ulinzi na ufatiliaji wa faru katika eneo la Seregeti.

  Alisema mradi huo unatarajiwa kutumia zaidi ya sh 253 milioni, zilizotolewa na shirika la uhifadhi la Friedkin Conservation Fund(FCF) na unaratibiwa pia na Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI). 

  Bigulube alisema, tayari utekelezaji wa mradi huo, umeanza, ambapo mwaka jana faru 21 walifungwa vifaa maalum digital VHF na mwaka huu wengine watafungwa vifaa vya kisasa zaidi kutumia mfumo wa LoRa(LoRa System).

  "lengo letu kama wahifadhi ni kuhakikisha Faru waliopo nchini wanaongezeka zaidi sambamba na wanyama wengine ambao maisha yao yamekuwa hatarini wakiwepo Tembo ambao nao tayari kuna miradi ya kuwafunga vifaa vya kisasa ili kuwafatilia "alisema

  Alisema katika kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu wameanza kuwapeleka kwenye mafunzo wahifadhi nchini Uholanzi ambao ndio watakuwa wakiratibu matumizi ya technolojia katika ulinzi na ufatiliaji wa faru."hivi karibuni tutaanza kuwafunga vifaa Faru, zoezi ambalo litatumia techolojia za hali ya juu,helkopta nna vifaa vingine vya kisasa kama ilivyokuwa mwaka jana"alisema.

  Akizungumzia mradi huo, Mhifadhi Mkuu wa hifadhi za Taifa ya Serengeti, William Mwakilema alisema, mpango huo ambao unashirikisha wizara ya maliasili na utalii na wadau wengine utasaidia sana ulinzi wa Faru."Ulinzi wa Faru ni jambo ambalo ni nyeti na serikali na vyombo vyake imekuwa ikifatilia kwa makini hivyo,lengo kuu ni kuhakikisha wanahifadhiwa"alisema

  Mtafiti kiongozi wa taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI),Dk Edward Kohi ,alisema ili kuimarishwa ulinzi wa faru, technolojia mbali mbali zinatakiwa kutumika."hii ni technolojia ya kuwafunga vifaa maalum, itawezesha kujulikana kila siku wapo wapi na hivyo ni rahisi kuwafatilia na kuwapa ulinzi"alisema

  Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani, ambayo bado yana idadi kubwa wa faru ambao wamehifadhiwa katika hifadhi kadhaa za taifa, tofauti za nchini nyingine ambazo zimehifadhi Faru katika mashamba maalum ya wanyama.

  0 0

  Watoto pacha Maryness Benatus Bernado na Anisia Benatus Bernado waliozaliwa wakiwa wameungana ambao kwa sasa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) tangu mwezi Februari mwaka huu, wanatarajiwa kupelekwa nchini Saudia Arabia ndani ya wiki mbili kuanzia sasa kwa ajili ya matibabu zaidi ikiwemo kuangalia uwezekano wa kuwatenganisha.

  Hayo yameelezwa leo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al-Hazzan alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kuangalia watoto hao. Watoto hawa wameungana kuanzia sehemu ya tumboni hadi chini.“Tumekuwa na uzoefu mkubwa sana wa kuwatenganisha watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana kuanzia miaka ya 1990 ambapo hadi hivi sasa watoto zaidi 35 kutoka nchi mbalimbali duniani waliozaliwa wakiwa wameungana tulifanikiwa kuwatenganisha,” alisema Kaimu Balozi Al-Hazzan

  Amesema kwamba kutokana na uzoefu mkubwa walionao, nchi yake kupitia Mfalme wa nchi hiyo ameagiza watoto hao wapelekwe Saudi Arabia kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya ubingwa wa juu.Mbali na hayo Serikali ya Saudi Arabia imesema itagharamia usafiri, malazi pamoja na matibabu hivyo wamemuhakikishia mama wa pacha hao kwamba matibabu yatakwenda vizuri na watarejea nchini wakiwa salama.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amemshukuru Mfalme wa Saudi Arabia na Serikali yake kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa Serikali ya Tanzania hususani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Prof. Museru ameiomba Serikali ya Saudi Arabia kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Afya katika kuangalia maeneo yenye upungufu wa wataalamu pamoja na maeneo mengine zikiwamo huduma za upasuaji.

  Kwa upande wake Mama wa watoto hao, Bi. Jonesia Jovitus amemshukuru Mfalme wa Saudia Arabia kupitia Ubalozi wake hapa nchini Tanzania kwa msaada alioupata kwani anaamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu watoto wake watapata huduma ya matibabu kulingana na uzoefu ulipo nchini humo. Watoto hao kwa pamoja wana uzito wa kilo 7 na gramu 40, walizaliwa Wilayani Misenyi, Mkoani Kagera tarehe 29 Januari, 2018.
   Kaimu Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al-Hazzan akiwa na watoto pacha waliungana, Maryness Benatus Bernado na Anisia Benatus Bernado ambao wamebebwa na mama yao, Jonesia Jovitus. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru.Watoto hao wanatarajiwa kupelekwa nchini Saudia Arabia ndani ya wiki mbili kuanzia sasa kwa ajili ya matibabu zaidi ikiwemo kuangalia uwezekano wa kuwatenganisha.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru akimsikiliza balozi huyo kabla ya kuwatembelea wodini watoto pacha leo tarehe 25 Juni, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa ubalozi huo, Fahad Ali Al Qahtani.
   Kaimu Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al-Hazzan na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru wakielekea wodini kuwaona watoto pacha walioungana leo tarehe 25 Juni, 2018.
  Kaimu Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al-Hazzan na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru wakiwa katika picha ya pamoja leo tarehe 25 Juni, 2018.

  0 0

  *Ni tamasha maalum kwa watoto, lashesheni michezo ya kila aina kwa watoto

  TAMASHA la Mtoto Day Out ambalo limebeba jina la Asas Mtoto Day Out linatarajia kufanyika Juni 30 mwaka huu katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa kiingilio cha Sh.5000 tu.

  Imefahamika kuwa mtoto atacheza michezo ya kila aina huku mzazi akiingia bure huku ikifafanuliwa Mtoto Day Out ni tamasha kwa ajili ya watoto kukutana kwa wingi kucheza na kufurahi pamoja.

  Akizungumzia leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa tamasha hilo Dina Marious amesema tamasha hilo litawapa nafasi watoto kucheza michezo ya kila aina na kuonesha vipaji, huku wakijishinidia zawadi mbalimbali. 

  "Moja ya haki za watoto ni kucheza na katika kucheza hujifunza mambo mbalimbali.Michezo kwa watoto isiwe kero kwa mzazi bali nafasi ya mtoto kujifunza na kuchangamsha akili yake."Katika michezo kuna michezo ya kushindana ambayo ni jambo jema kwa watoto kupanda ndani yao ari ya ushindani hata katika maisha ya baadae."Wazazi kawaida wana Outing zao za kikubwa na watoto huishia mara moja moja kupelekwa kwenye michezo,"amesema,

  Ameongeza kupitia tamasha la Mtoto Day Out wanataka liwe tamasha la watoto kama ambavyo watu wazima wana matamasha yao na kufafanua "unapotoka na mtoto wako kuja Mtoto Day Out unamtoa yeye Out si wewe".Amesema kuwa hiyo ni mara ya tatu kwa tamasha hilo kufanyika na kufafanua tamasha la safari hii litafanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama Sayansi jijini.Muda wa kuanza kwa tamasha hilo ni kuanzia saa nne asubuh mpaka saa 12 jioni na kutakuwa na michezo ya kila aina kwa watoto.

  Baadhi ya michezo hiyo ni jumping castles, face painting, train, magari ya kuendesha,climber,mabembea,swimming pools,water slides,football arena na sarakasi.Marious amesema pia kutakuwa na kona ya michezo ya watoto wadogo wa mwaka hadi miaka 3, kona ya watoto kusoma vitabu na kuchora.Pia atakuwepo Mchekeshaji Mpoki ambaye atasasherehesha watoto huku msanii Msami akiwachezesha watoto. Katika tamasha hilo vyakula uwanjani vitakuwepo na wazazi watawanunulia watoto kwa bei nafuu kabisa.

  "Tamasha hili linafanyika kwa udhamini wa Asas_dairies, Finca microfinance bank,majibora, ara juice, bagtriks, swahilifastfood,saloon ya watoto ya kiddieskingdomtz,dinamarios coconut baby oil, efmtanzania na tvetanzania ."Tunapenda kuwakaribisha wazazi na watoto kutakuwa na timu kubwa ya kuangalia watoto kwa kushirikiana na wazazi.

  Ulinzi na usalama utakuwepo kwa kushirikiana na jeshi la polisi,"amesema Marious.Pamoja na hayo amesisitiza kuwa tamasha hilo limebeba jina la Asas mtoto day out kwasababu Mdhamini Mkuu ni ASAS dairies kupitia maziwa yake ya asas Yogurt. Furaha ya Mtoto wangu ni Furaha yangu.

  Kwa upande wake Meneja Masoko wa Asas Jimmy Kiwelu amesema wanatambua umuhimu wa watoto kushiriki kwenye michezo mbalimbali, hivyo wakaona iko haja ya wao kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa ili kuwapa nafasi watoto kukutana na kucheza kwa pamoja.Amesema Asas siku zote wamekuwa wakiamini katika kuhakikisha mtoto anakuwa na furaha kwani furaha ya mtoto ndio furaha kwa mzazi/mlezi.

  "Tumekuwa tukidhamini mambo mbalimbali ya kimaendeleo lakini hatuko nyuma katika kuhakikisha watoto wetu nao wanapata nafasi ya kushiriki kwenye matamasha hasa ambayo tunaamini mbali ya kucheza lakini kuna vitu watajifunza.

  "Tuwaombe wazazi kuwaleta watoto wao kwenye tamasha hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya watoto wote.Kubwa kwetu tumedhamini tukiamini kuwa Asas imepiga hatua kutokana na kuungwa mkono na Watanzania ambao chaguo lao namba moja ni Asas,"ameongeza.

  Wakati huo huo Balozi wa Asas Mujuni Sylivery maarufu kwa jina la Mpoki amewashauri wazazi kuhakikisha wanapa furaha watoto wao kwa kuwapeleka kwenye tamasha hilo ambapo amewakikishia amejiandaa vema kwa ajili ya kuwafurahisha.Pia ameshauri siku ya tamasha wazazi au walezi wa watoto ni vema wakatoka na wadada wa kazi badala ya kuwaacha nyumbani kwani mdada wa kazi ndio anayeshinda na mtoto muda mwingi na anajua anapenda mchezo gani.
  Mratibu wa tamasha la ASAS Mtoto Day Out Dina Marios akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo,linalotarajia kufanyika Juni 30 mwaka huu katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam,ambapo kiingilio kimetajwa kuwa ni Sh.5000 tu,Pichani kulia ni Mmoja w Waratiu wa tamasha hilo Glory Shayo na kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni ya ASAS Jimmy Kiwelu.
  Mkutano huo ukiendelea na Waandishi mapema leo jijini Dar 
  Balozi wa Asas Mujuni Sylivery maarufu kwa jina la Mpoki akiwaonesha Waandishi wa Habari baadi ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo,huku akiwashauri wazazi kuhakikisha wanawapa furaha watoto wao kwa kuwapeleka kwenye tamasha hilo ambapo amewahakikishia amejiandaa vema kwa ajili ya kuwafurahisha. 
  Meneja Masoko wa Asas Jimmy Kiwelu akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha la Asas Mtoto Day Out,Kiwelu amesema wanatambua umuhimu wa watoto kushiriki kwenye michezo mbalimbali, hivyo wakaona iko haja ya wao kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa ili kuwapa nafasi watoto kukutana na kucheza kwa pamoja.Amesema Asas siku zote wamekuwa wakiamini katika kuhakikisha mtoto anakuwa na furaha kwani furaha ya mtoto ndio furaha kwa mzazi/mlezi.

  0 0

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwanamuziki Mkongwe Mzee Makassy  na wasanii wenzake katika Viwanja vya Bunge , Juni 25/2018 .Kulia ni Mbunge wa Viti maalumu Martha Mlata
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na mwanamuziki, Kikumbi Mwanza Mpango (King Kiki)  na wasanii wenzake  katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma  Juni 25/2018. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, kushoto mwenye kofia nyekundu ni Mzee Makassy na Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Martha Mlata .
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wanamuziki wakongwe kwenye Viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba bungeni jijini Dodoma leo Juni 25/2018
  PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mfumo wa Usajili kwa kutimia Mtandao wa Kompyuta kwa taasisi za Biashara na Amana kwa Mali zinazohamishika,hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar (kushoto) Mkuu wa idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Komptuta katika Wizara ya Biashara na Viwanda Ibrahim Salum Saleh na (kulia) Waziri wa Biashara na Viwanda  Balozi Amina Salum Ali.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika , uzinduzi wa Mfumo wa Usajili kwa kutimia Mtandao wa Kompyuta kwa taasisi za Biashara na Amana kwa Mali zinazohamishika,hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Biashara na Viwanda  Balozi Amina Salum Ali akizungumza mafupi na kumkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ili kutoa hutuba yake katika uzinduzi wa Mfumo wa Usajili kwa kutimia Mtandao wa Kompyuta kwa taasisi za Biashara na Amana kwa Mali zinazohamishika,hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
   Washiriki katika  uzinduzi wa Mfumo wa Usajili kwa kutimia Mtandao wa Kompyuta kwa taasisi za Biashara na Amana kwa Mali zinazohamishika,hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar,mgeni rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. (Picha na Ikulu.)


  0 0


  Na WAMJW - DSM
  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kuingia kwa ugonjwa wa Chikungunya nchini baada ya watu wanne waliotokea  nchini Kenya kubainika kuwa na dalili zinazofanana na ugonjwa  huo.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo jijini katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa Habari.

  “Mnamo tarehe 20, Mwezi Juni, 2018 wasafiri wanne wa familia moja waliotokea tena Mombasa nchini Kenya walishukiwa kuwa na ugonjwa huu baada ya kuwa na dalili zinazofanana na ugonjwa wa homa ya Chikungunya kwenye kutuo cha mpakani cha Holili kilichopo wilayani Rombo mkoani Kiliamanjaro”, alisema Mhe. Ummy

  Waziri Ummy aliwatoa hofu wananchi kuwa Ugonjwa huu si mpya katika nchi yetu kwani hapa nchini  uligundulika katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania, sehemu za Makonde katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji mnamo mwaka 1952 huku  Jina la ugonjwa likiwa na asili ya Kimakonde lenye maana ya “kilichopinda” yaani  hali ya kupinda mwili inayotokana na maumivu makali ya viungo kunakosababishwa na ugonjwa huu.

  Kwa upande mwingine Mhe. Ummy alithibitisha juu ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue nchini hususani katika jiji la Dar es salaam huku idadi ya wagonjwa ambao wamethibishwa kwa kipindi cha Januari hadi Mei ni 226 ambao wanatoka katika mkoa wa Dar es Salaam.

  ‘Dengue ulithibitishwa kuwepo hapa nchini hususani jijini Dar es Salaam kuanzia mwishoni mwa mwezi wa Januari 2018. Hadi kufikia sasa idadi ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huu kwa kipindi cha Januari hadi Mei ni 226 ambao wanatoka katika mkoa wa Dar es Salaam.  Vilevile ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani umewahi kuripotiwa katika miaka ya 2010, 2013 na 2014” alisema Waziri Ummy.

  Aidha, Waziri Ummy ameeleza dalili za ugonjwa wa Dengue zinashabihiana amabazo ni pamoja na homa ya ghafla, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza siku ya 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya magonjwa haya. Wakati mwingine dalili za magonjwa haya yanaweza kufanana sana na dalili za ugonjwa wa malaria. Vilele mara nyingine magonjwa haya yanaambatana na kutokwa na damu sehemu za fizi, mdomoni, puani, kwenye macho na pia kwenye njia ya haja kubwa au ndogo.

  Kwa upande mwingine Waziri Ummy amethibitisha kuwa hadi sasa nchini Tanzania hakuna mgonjwa yoyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya Ebola, huku kwa tathmini ilifanyika na Shirika la Afya Duniani (Regional Risk Assessment) imesema kuwa Tanzania ipo kwenye uwezekano wa kupata ugonjwa wa Ebola na imewekwa katika kundi la pili miongoni mwa nchi 6 zilizo katika hatari ya kupata maambukizi zaidi, kutokana na kupakana na nchi ya DRC pamoja na mwingiliano mkubwa wa watu wake.

  Pia Mhe. Waziri amewatoa hofu Wananchi na kuwataka kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huu hapa nchini, huku akiwaonya wanaosambaza taarifa za uzushi juu ya uwepo wa ugonjwa huu na kuwataka waache haraka.

  Aidha, Wizara itaendelea kushirikiana na Sekta mbalimbali katika kuimarisha ufuatiliaji na kuendelea kutekeleza mikakati ya kudhibiti ili ugonjwa huu usiingie nchini na kuendelea kutoa taarifa pamoja na Elimu kwa Jamii kadri itakavyohitajika.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akieleza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa Chikungunya, Dengue na Ebola katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Katibu mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya na Kulia ni Mkurugenzi Mkazi kutoka shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Adiele  Onyeze.
   Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kuhusu ugonjwa wa Chikungunya, Dengue na Ebola katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mhandisi wa Mifumo ya dot TZ kutoka Tanzania Network Information Centre (TZNIC), Bw. Raymond Linus akiongea na wataalamu wa ICT na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kuwa na kikoa cha .tz (.tz domain name) katika mkutano wa ICT uliofanyika Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA). Dot TZ registry imekua ikidhamini mikutano hii ya ICT kuelimisha wananchi juu ya faida ya kutumia kikoa cha .tz katika mawasiliano ya Intaneti.
  Mkuu wa Idara ya Informatics wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) Bi. Pamela Chogo akiwakaribisha wataalamu na wanafunzi wa ICT kwenye mkutano wa ICT uliofanyika Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA).
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) Dr. Samwel Werema akizungumza na wanafunzi wa ICT kwenye mkutano wa ICT uliofanyika Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA).
  Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha walioshiriki mashindano ya ICT (Arusha ICT Innovative Challenge 2018 – Jiji Hackathon) wakiwa kwenye picha ya pamoja.

  0 0


  0 0

  Na Shushu Joel, Simiyu

  NAIBU waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa Halamshauri zote nchini kubuni miradi ya kimkakati ya itakayoziongezea mapato badala ya kuendelea kutegemea ushuru na tozo mbalimbali kutoka kwa wananchi.

  Dkt. Kijaji alisema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza chaki cha wilaya ya Maswa wakati wa ziara yake ya kujionea utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Vwanda Mkoani Simiyu akiwa na viongozi wa Halmashauri na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa.

  Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Halmashauri zote zinabuni miradi ya kimkakati ambayo itaziongezea mapato na akatoa wito kwa Halmashauri zote nchini kujifunza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo imetengewa shilingi bilioni 8.2 na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ya upanuzi wa Kiwanda cha Chaki na kujenga kiwanda cha vifungashio.

  “Niwapongeze Simiyu mnafanya kazi nzuri, tunataka kuondoka kwenye ule ukawaida wa Halmashauri zetu kulalamika kuwa Serikali Kuu imechukua vyanzo vya mapato, Serikali Kuu haijachukua kinachohitajika ni ubunifu wa miradi kama Halmashauri ya Maswa ilivyofanya, nitoe wito kwa Halmashaui zote kubuni miradi, Serikali ipo tayari kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato ya Halmashauri” alisema

  Naye mbunge wa Maswa Mashariki na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameiomba Serikali kutoa fedha hizo shilingi Bilioni 8.2 zilizotengwa kwa wakati ili Miradi iliyokusudiwa ya upanuzi wa kiwanda cha chaki na ujenzi wa kiwanda cha vifungashio iweze kutekelezwa kwa wakati.

  Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt. Fredrick Sagamiko alisema Halmashauri hiyo imedhamiria kufikisha zaidi ya asilimia 75 ya mapato ya ndani yatakayotokana na viwanda vilivyopo na vinavyoendelea kujengwa wilayani humo ili kuondokana na kutegemea fedha za miradi kutoka serikali kuu.

  Aliongeza kuwa katika kukiongezea kiwanda cha chaki uwezo wa uzalishaji, Halmashauri ya Maswa imenunua eneo kwa ajili ya malighafi ya kutengenezea chaki katika Mkoa wa Singida.

  Awali Dkt. Ashatu alitembelea eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika viwanda la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mahali ambapo patajengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza chak(upanuzi wa hiki kilichopo) na kujenga kiwanda cha vifungashio.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikabidhiwa boksi la chaki za Maswa (Maswa Chalks) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda mkoani humo.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa mkoani Simiyu ambapo aliongozana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda mkoani humo.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiangalia viatu  vya ngozi vinavyotengenezwa katika kiwanda cha Senani wilayani Maswa mkoani Simiyu baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda.(PICHA ZOTE NA SHUSHU JOEL).

  0 0

  Na Frankius Cleophace, Tarime

  WANANCHI wa Kijiji cha Kebweye katika Kata ya Nyakonga wamewatupia lawama wananchi wa Kijiji cha Kyoruba kata ya Pemba kwa madai kuwa wamevamia eneo lililodaiwa kuwa na mgogoro takribani miaka 37 na kufyeka mazao yao.

  Mbali ya kuvamia eneo hilo wamedai kuwa wamekuwa wakijenga nyumba usiku na mchana jambo ambalo limewafanya wananchi wa Kebweye kutoa ombi kwa Serikali kuingilia kati.

  Wakizungumza jana kwenye mkutano wa kufanya maendeleo SAIGA wananchi hao wamedai mgogoro wa eneo hilo linalogombaniwa kati ya Kijiji cha Kebweye na Kyoruba ulianza tangu mwaka 1981 ambapo viongozi wa Serikali wamekuwa wakienda pale lakini uamuzi wanayotoa wananchi hao hawaridhiki.

  Diwani wa Kata ya Nyakonga Riziki Mwita amesema suala la kufyekwa kwa mazao na kuanza ujenzi litasababisha familia nyingi kutaabika kwa kukosa chakula, hivyo Serikali ya wilaya iweze kuingilia mapema na kutatua changamoto hiyo.

  "Mkuu wa Wilaya ya Tarime Luoga alifika eneo hili na kuamua wananchi wote pande mbili walitumie kwa ajili ya kilimo lakini sasa tunashangaa wenzetu wamevamia eneo hilo usiku na kufyeka mazao nakujenga kwa ajili ya Makazi,"amesema Diwani.Mwenyekiti wa Kijiji cha Kebweye Marwa Mniko amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na wametoa taarifa katika mamlaka mbalimbali lakini hata baadhi ya viongozi wanapindisha ukweli na matokeo yake wananchi wanateseka.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Gloriuos Luoga akizungumzia mgogoro huo amefafanua kuwa uanzishwaji wa kijiji linasimamiwa na Rais kwa mujibu wa sheria.Amesema kwa sasa ameagiza Mkurugenzi kufuatilia suala la GN zote katika ofisi za ardhi ili kila sehemu yenye mgogoro wa mipaka wilayani Tarime waweze kusoma GN hizo ili kuondoa migogoro hiyo

  Pia amewatupia lawama viongozi wa kuchaguliwa wakiwemo wenyeviti wa vijiji na madiwani kwa madai ndio chanzo kikubwa cha migogoro hiyo na wamekuwa wakiichochea."Huu mgogoro wa Kyoruba na Kebweye nimeenda zaidi ya mara tatu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kebweye amaeandika barua lakini tatizo hawa viongozi kipindi cha kampeni wanadanganya wananchi,"amesema.

  Pia amesema viongozi hao wa kuchaguliwa wamekuwa wakiuchochea mgogoro huo ili waendelee kuongoza jambo ambalo ni hatari kwani kubadili GN zinazowekwa kipindi kijiji kinaanzishwa haiwezekani.Hivyo amewataka wananchi kutowasikiliza wanasiasa pale wanapokuwa na tatizo wafike mara moja ofisini kwake kwa lengo la kupata ufumbuzi mara moja.

  Wananchi na wakazi wa Kijiji cha Kebweye Kata ya Nyakonga wakiongea na Vyombo vya habari katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji hapo kwa lengo la kuzungumzia kilio chao cha Mgogoro ambao umedumu takribani Miaka 37 kuanzia Mwaka 1981.

  Wananchi na wakazi wa Kijiji cha Kebweye Kata ya Nyakonga wakiongea na Vyombo vya habari katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji hapo kwa lengo la kuzungumzia kilio chao cha Mgogoro ambao umedumu takribani Miaka 37 kuanzia Mwaka 1981.

  Wananchi na wakazi wa Kijiji cha Kebweye Kata ya Nyakonga wakiongea na Vyombo vya habari katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji hapo kwa lengo la kuzungumzia kilio chao cha Mgogoro ambao umedumu takribani Miaka 37 kuanzia Mwaka 1981.

  Viongozi wa Serikali ya Kijiji akiwemo Diwani wa kata ya Nyakonga Riziki Mwita wakiwa katika kikao hicho.

  Wananchi wa kijiji cha Kebweye kata ya Nyakonga Wilayani Tarime Mkoani Mara wakiwa katika Mkutano huo.

  Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akielezea jitihada za Serikali kutatua Mgogoro huo baina ya Wananchi wa kijiji cha Kebweye na Kyoruba ambapo Mkuu wa Wilaya amesema Mgogoro huo unachangiwa kuchochewa na Viongozi wa Kisiasa.

  Ni Maeneo yanayodaiwa kuvamiwa na Wananchi wa Kijiji cha Kyoruba na kufyeka Mashamba kisha kujenga Majengo yao Usiku na kuanzisha Makazi kwa madai ni Maeneo yao.

  Ni Maeneo yanayodaiwa kuvamiwa na Wananchi wa Kijiji cha Kyoruba na kufyeka Mashamba kisha kujenga Majengo yao Usiku na kuanzisha Makazi kwa madai ni Maeneo yao.

  Viongozi wa Serikali za Vijiji na baadhi ya Waananchi wakiangalia baadhi ya Nyaraka zinazozungumzia Mgogoro huo.

  Mwenyekiti wa Kijiji cha Kebweye Marwa Mniko akiongea na wananchi hao katika Mkutano huo kabla ya kutoa Malalamiko yao.

older | 1 | .... | 1606 | 1607 | (Page 1608) | 1609 | 1610 | .... | 1897 | newer