Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1605 | 1606 | (Page 1607) | 1608 | 1609 | .... | 1897 | newer

  0 0

  pika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa hafla Maalum ya Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana

  Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan(kushoto) na Spka wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) wakifurahia maonyesho ya Waheshimiwa Wabunge (hawapo kwenye picha) ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
  Waheshimiwa Wabunge wakiingia kwa kuimba wakati wa Maonyesho yao ikiwa ni njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
  Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia), Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) wakishikilia hundi ya sh. Millioni 100 waliopewa na kampuni ya Uchimbaji Madini ya GEITA GOLD MINING mchango wao kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
  Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Lucy Mayenga akiwapungia mkono wageni waalikwa wakati wa Maonyesho ya mavazi yaliyotolewa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kama njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana 
  Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Vicky Kamata na Waheshimiwa wenzake wakiwaburudisha wageni waalikwa na Wabunge katika onyesho la kuimba lililoandaliwa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kama njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangish a fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  VETERANI wa timu ya soka ya Uingereza ya Liverpool, Sami Hyypia amewataka vijana Watanzania kuongeza bidii katika kuhakikisha kwamba wanafikia hatua za juu za uchezaji soka hivyo kupata nafasi ya kucheza Ulaya.

  Pia amesema ni matumaini yake kuwa mamlaka za utoaji leseni hazitawazuia vijana kwenda Ulaya kujaribu bahati zao.Alisema hayo wakati wa kiliniki ya soka aliyoifanya kwa vijana wa Serengeti boys jana alipokuwa akishiriki nao katika mafunzo na mazoezi.

  Alisema kwamba yeye hakuwa na kipaji kikubwa kuliko alivyoviona kwa vijana hao lakini ameweza kufikia hatua za juu kabisa za uchezaji wa soka kutokana na kujituma kwake.Alisema amewaambia vijana kuangalia zaidi juhudi kwani kipaji pekee hakitoshi kumfanya mtu kuwa gwiji katika soko.Alisema pamoja na mafundisho ya walimu ni kazi ya mchezaji mwenyewe kuona udhaifu wake uliopo na kuufanyia kazi ili aweze kuwa mwanasoka bora wa kutegemewa.

  Akihojiwa mwanasoka huyo ambaye aliwika sana katika enzi zake alisema kwamba amefurahishwa na uchezaji wa timu hiyo hasa kwa pasi ndefu na kusema kwamba vijana wote wameonesha kuwa na vipaji vikubwa.

  Alisema hata hivyo kwamba amewaambia wachezaji awali kuwa na kipaji pekee hakutoshi lakini ni lazima mtu binafsi kufanyakazi ya ziada kuondoa udhaifu wake ambao binadamu wengi wanakuwa nao ili kuwa mahiri katika uchezaji.

  Sami ambaye yupo nchini kuangalia michuano ya kombe la benki ya Standard Charted  inayofanyika leo na kushirikisha timu 32 zinazowania kwenda Anfield kuona mechi za msimu mpya timu ya Liverpool  ndani ya EPL na kuzungumza na magwiji na kupata nafasi ya kunolewa, amesema siri kubwa ya mafanikio ni kujituma kwa mchezaji pamoja na kwamba anakipaji na walimu wazuri.
   Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akimtambulisha Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) kwa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
   Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
   Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kulia) pamoja na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
   Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza kwa makini Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
   Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) na Mshauri Mkuu wa Ufundi katika Programu za Soka la Vijana nchini, Kim Paulsen wakiangalia uzoefu wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya gwiji huyo hapa nchini.


   Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya gwiji huyo hapa nchini.
   Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakijinoa baada ya kupata mafunzo na mbinu mbalimbali wakati wa kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia hapa nchini.


  0 0

  Na Anthony Ishengoma WAMJW.

  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa kati ya asilimia 7 na 16 ya wanawake wote duniani ni Wajane.  

  Jamii imetakiwa kuendeleza mipango na kuongeza juhudi zaidi katika kukabiliana na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kuwainua wajane ili wapate uwezo wa kiuchumi wa kuzihudumia familia na wategemezi wao kwa kuwa ndiyo muhimili pekee wa familia iliyoachwa.

  Akiongea kwa niaba ya Mgeni rasmi wa kongamano la Wajane liliofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa Bi. Honoratha Rwegasira amepongeza juhudi za wadau wa maendeleo na serikali katika kuwasaidia wajane kuleta usawa wa kinjisia na kuinua ushiriki wao katika ngazi za kutoa maamuzi.  

  Aidha Bi.Rwegasira ameitaka jamii kuacha mila potofu kama vile kunyanganya mali mjane, kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo, kurithi wajane na nyingine zote zinazoweza kumdhoofisha mwanamke katika jitihada zake za kujikwamua kifikra, kiutamaduni, kiuchumi,kijamii na kisiasa.

  Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara  ya Afya,Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mwajuma Magwiza amesema kimsingi lengo la maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani ni kutoa nafasi kwa Wadau kushirikiana na Serikali kwa kutoa huduma za msingi kwa wajane na kuondoa aina zote za ukandamizaji ikiwemo haki ya kumiliki mali, umasikini, mira na desturi za kurithiwa baada ya kufiwa.
   Mkurugezi  Msaidizi  Idara ya Jinsia, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza akitoa hutuba yake kwenye  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
   Afisa Mwandamizi  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi .Sirivia Siliwa  akitoa mada kuhusu Chimbuko la  Siku ya  Wajane Duniani wakati wa Kongomano la Wajane lilifanyika leo Mjini Dodoma.
   Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma  Bi. Honoratha Rwegasira  akitoa hutuba ufunguzi  kwa niahaba ya Mgeni rasmi wakati wa  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
  Wajane wa Mkoa  wa Dodoma wakiwa kwenye  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.


  0 0

  Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na watoto wenye sikoseli baada ya matembezi yaliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Sikoseli Tanzania Dkt. Deo Soka akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu baada ya matembezi ya siku ya sikoseli katika viwanja vya Mwembeyanga.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakatikati) akiwa katika matembezi ya siku ya Sikoseli, kushoto kwake ni mwakilishi wa WHO na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva Siku ya sikoseli Duniani huazimishwa Juni 19
  Wadau wa sikoseli wakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kunyoosha viungo baada yakumaliza matembezi ya Km 3 ambayo yalikomea katika viwanja vya Mwembeyanga.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mwembeyanga na Wadau wa Sikoseli wakati wa matembezi ya siku ya Sikoseli ambayo kauli mbiu yake ni *Kuwa mjanja, Ijue Sikoseli*

  0 0


  Naibu Meya wa Jijila Arusha Viola Lazaro akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wajane duniani yaliyoyanyika katika Hotel ya Palace mkoani Arusha ambapo alikuwa mgeni rasmi.Picha na Vero Ignatus
  Mratibu wa chama cha wanawake wajane Jijini Arusha(TAWIA) bi Janet Mgane akisoma risala mbele ya mgeni rasmipamoja na wanawake wajane waliohuduria katika kuadhimisha siku yao mkoani Arusha ambapo zaidi ya wanwake 50 waliwezakuhudhuria huku ikiwa ni mara yao ya kwanza kuadhimishwa mkoani hapo.Picha na Vero Ignatus .
  Wakwanza kulia ni Mratibu wa chama cha wanawake wajane mkoani Arusha bi Janet Mgane,akimkabidhi mgeni rasmi risala Naibu meya wa jiji la Arusha Viola Lazaro,katikati ni diwani wa viti maalum chadema Happy Charles akufuatiwa na Mkurugenzi wa jinsia na mahusiano ya jamii kutoka shirika la Civil and Legal Aid Organization Ranto Muhochi.Picha na Vero Ignatus
  Diwani wa viti maalum chadema Happy Charles akizungumza na wanawake wajane katika ukumbi wa Hotel ya Palace Jijini Arusha.
  Meneja wa Biashara kutoka Benki ya CRDB Rose Wilium akizungumza na wanawake wajane akiwaelekeza namna ya kufungua akaunti na namana ya kujikwamua kiuchumi. Picha na Vero Ignatus
  Pichani ni baadhi ya wanawake wajane (TAWIA)pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha wanawake wajane nchini,wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Meya wa Jiji la Arusha Viola Lazaro.Picha na Vero Ignatus
  Baadhi ya waandishi wa habari Mkoani Arusha walioalikwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa katika Hotel ya Palace.Picha na Vero Ignatus


  Na.Vero Ignatus Arusha.

  Imeelezwa kuwa kuandaa wosia mapema kabla ya kifo inasaidia kuepuka mogogoro ya mirathi ambayo imekuwa ikiwakumba wajane.

  Hayo yamesemwa na Naibu meya wa jiji la Arusha Viola Lazaro katika maadhimisho ya siku ya wajane duniani mkoani iliyofanyika Palace Hotel Mkoani Arusha.Akitoa changamoto wanazo pitia wajane Bi Janet Mgane amesema matatizo ya Mirathi, Wajane kushindwa kufahamu sheria na kesi kuchukua muda Mrefu.

  Akijibu risala iliyosomwa na mratibu wa tawia Kanda ya KaskaziniJuliet Mgani, Naibu meya amesema changamoto kubwa waliyonayo ni wanawake wengi kutokuzifahamu haki zao kisheria na kikariba."Wanawake wengi amabao ni wajane wanashindwa kupambana kushinda kesi kwa kutokufahamu sheria na kikatiba" Alisema naibu meya.Mmoja wa wajane bi Agness Omari (78)ametoa ushauri kwa wajane wajiheshimu na kuwalea watoto walioachiwa na waume zao waliotangulia mbele za haki.

  Kauli mbiu ya siku ya wajane duniani "wajane tusibaki nyuma katika kuelekea uchumi wa viwanda na malengo ya maendeleo endelevu 2030.

  0 0


  Na Emmanuel Masala, Globu ya jamii 

  MKUU  wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Barabara ya Africana Kinzudi yenye urefu wa kilometa 3.3, ambayo ujenzi wake utagharimu zaidi ya Sh.Million 900.

  Ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami inaenda sambamba na uwekaji wa matuta, mitaro ya maji, taa za barabarani, Calvert na alama za watembea kwa miguu ambapo itajengwa na TARURA. 

  Baada ya kuzindua Barabara hiyo jana RC Makonda amefanya mkutano wa hadhara na wakazi wa Kata za Wazo na Mbezi Juu uliolenga kupatia majibu ya changamoto zinazowakabili kwenye sekta ya miundombinu, elimu, afya, maji,ardhi na usafiri.

  Ambapo wakazi wa Kata hizo wamefurahia kuona kero zao za muda mrefu zimepatiwa ufumbuzi wa haraka.Pia wakati wa mkutano huo RC Makonda ameelezea miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa kwaajili ya usafiri wa treni kutoka Wazo kuelekea Mwenge, Airport na Posta ambayo itasaidia usafiri na kupunguza msongamano wa magari.

  Aidha RC Makonda amewataka wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya barabara ya Afrikasana Kinzudi kushirikiana na seri kali kuhakikisha ujenzi unafanikiwa.Makonda amewata wakazi waliojenga ndani ya hifadhi ya bomba la maji kutokea Ruvu kushirikiana kwa kina na DAWASA.

  Pamoja na hayo  ameagiza kila mtaa kuwa na ramani ya mipango miji ili kukabiliana na migogoro ya ardhi na utapeli ambapo pia amewataka wananchi waliocheleweshewa kupatiwa vibali vya ujenzi kufika ofisini kwake Julai 1 mwaka huu.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda sambamba na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi wakiweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Africana Kinzudi jana jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi naMeya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta wakiwasili eneo la Africana kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo jana jijini Dar as Salaam.
  Sehemu ya wanachi wa Africana na Kinzudi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda( hayupo pichani),alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa hadhara

  Muonekano wa barabara hiyo

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Africana Kinzudi jana jijini Dar as Salaam.

  0 0

  Uzinduzi rasmi wa onesho la Adorableweddingtradefair2018  umefanyika  jana jumamosi ndani ya ukumbi wa King Solomon,Namanga jijini  Dar,ambapo Mgeni rasmi alikuwa  ni Naibu waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Juliana Shonza.

  Aidha katika muendelezo wa onesho hilo leo Usisite kupita pale katika ukumbi wa King Solomon, Namanga mkabala na Best Bite leo na kujionea wadau mbalimbali wa sherehe kama wapambaji, Cake,Ma-Mc,Wauzaji wa nguo,Chakula,Picha na wengineo lukuki wakionesha bidhaa zao,bila kusahau Vyakula mbalimbali vitakuwepoo kwa bei nafuu tuu,Ni Onesho la bure kabisa na hakuna kingilio. 
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa onesho hilo la Adorableweddingtradefair2018

  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waandaaji wa onesho hilo la Adorableweddingtradefair2018 sambamba na washiriki wengine mbalimbali waliohakikisha onesho hilo linafana kwa kiasi kikubwa
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza (wa tatu kushoto ) akitazama bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikiuzwa katika onesho hilo laAdorableweddingtradefair2018,lililofanyika ndani ya ukumbi wa King Solom jana,Namanga jijini Dar
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza   akizungumza  mbele ya washiriki na waandaaji wakati wa uzinduzi wa onesho la Adorableweddingtradefair2018,lililofanyika ndani ya ukumbi wa King Solom jana,Namanga jijini Dar

  Muandaaji wa Onesho la 
  Adorableweddingtradefair2018, Anna Lema akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza kabla ya uzinduzi wa onesho la Adorableweddingtradefair2018.

  0 0

  Na Frankius Cleophace Tarime

  MWENYEKITI wa Mtaa wa Mtaa wa Bugosi Kata ya Nyamisangura Mjini Tarime mkoani Mara Zacharia Ghati amevamiwa akiwa njiani na watu wanaodhaniwa kuwa vibaka na kumshambulia kwa kutumia vitu vyenye ncha kali.

  Pia vibaka hao walikuwa na nondo na marungu ambayo waliyatumia kumshambulia nayo,hivyo kumsababishia maumivu makali na kisha wakampora fedha Sh.320,000.

  Akizungumza na Michuzi Blog akiwa amelazwa katika Hospitlai ya Mji wa Tarime Mwenyekiti huyo amedai tukio hilo limetokea Saa Nne ambapo ameporwa pia kitamburisho chake cha kazi na cha mpiga kura pamoja na kumsababisha maumivu.“Nilikuwa nimesindikiza mmoja wa wananchi wangu alienda kwenye harusi kwa ajili ya kuchinjia mama mkwe sasa kipindi tunarudi nilipofika mtaani kwangu nilipigiwa simu na mwenyekiti wa Mtaa.

  "Hivyo wananchi tukaachana na kipindi naenda nilikutana na watu wawili wakanisimamisha wakaanza kunishambulia na panga na kisha wengine kama wanne wakaongezeka ndio wakaanza kunishambulia kwa virungu na nondo,” amesema . Mmoja wa wananchi Chacha Masero aliyekuwa ameambatana na Mwenyekiti huyo kabla ya kutokea kwa tukio hilo amesema saa tatu wakiwa nyumbani baada ya kutoka kwenye harusi Mwenyekiti huyo alipigiwa Simu na Mjumbe wa Mtaa.

  Ameongeza hivyo alimua kuondoka peke yake na baada ya muda alipokea taarifa za Mwenyekiti huyo kuvamiwa na vibaka. “Mie nilipopata taarifa hizo nilikwenda Polisi na kisha tukafanya utaratibu wa kumleta hospitali mpaka sasa anaendelea na matibabu japo ameumizwa sana Mwenyekiti wetu,” amesema Chacha.

  Nao wananchi wa Mtaa wa Bugosi Kata ya Nyamisangura wameiomba Serikali likiwemo Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia ulinzi huku wakichukuliwa hatua kali vibaka wanakamatwa na kufaamika katika mitaa huska.“Kuna vibaka wanafaamika kabisa lakini wanalindwa na baadhi ya viongozi kwa sababu ya undugu, tunaomba washughulikiwe,” amesema mmoja wa Wananchi.

  Aidha Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashir Abdallah amethibitisha kushambuliwa kwa mwenyekiti huyo. Hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi maeoneo yote na kuwahi kwa wakati pindi tukio linapotokea popote. Abdallah amesema kuwa Polisi wamekuwa wakichelewa katika eneo la tukio pale wanapopigiwa simu za haraka hivyo kuna haja kubwa ya jeshi hilo kulifanyia kazi suala hilo.

  “Ndo Maana kukaundwa kanada Maalumu Tarime Rorya siyo kwa sababu ya vita vya koo ni pamoja na kulinda wananchi na mali zao ili wananchi wasiishi kwa hofu,” amesema Diwani.
  Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashir Abdallah akiwa katika Hospitali ya Mji wa Tarime akijulia hali ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugosi Zacharia Chacha Ghati aliyevamiwa na Vibaka na kushambuliwa na Vitu Vyenye Ncha kali zikiwemo Nondo na Vilungu na kumsababishia Maumivu Makali.
  Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugosi kata ya Nyamisangura Zacharia Chacha Ghati akiwa amelazwa katiko Hospitali ya Mji wa Tarime Mkoani Mara kwa ajili ya Matibabu.
  Chacha Masero Mkazi wa Bugosi akisimulia juu ya tukio hilo kwani alikuwa na Mwenyekiti kabla ya kutokea kwa tukio hilo.
  Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashiri Abdallah akidhibitisha uwepo wa Tukio hilo katika kaya yake huku akiomba jeshi la Polisi kujimalisha ulinzi.

  0 0

   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi kombe la Ubingwa wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup nahodha wa timu ya  TOC Bato Diasi  kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama  aliyevaa koti jeupe
   Nahodha wa timu ya  TOC Bato Diasi akiwa amelishikilia kombe lao kulia ni NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto akimvalisha medali mchezaji wa timu ya Ushirika FC ambao walishika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Kombe la Aweso Cup kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
   Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akimkabidhi  sh.50000 Twaha Bungala ambaye ni mfungaji bora kwenye mashindano hayo
   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso katikati akimkabidhi kitita cha sh.milioni 1 nahodha wa timu ya TOC Bato Diasi juzi ambao niMabingwa wa Ligi ya wilaya hiyo maarufu kama Aweso Cup  iliyodhaminiwa na Mbunge huyo
   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)akizungumza wakati akifunga mashindano hayo
   Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa akizungumza
   Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu ya Coastal Union Salimu Bawaziri akizungumza
    NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) katikati na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
    NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) katikati akifurahia jambo na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa  wakati wa mechi ya fainali
    NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakifuatilia mechi ya Fainali ya Ligi ya Aweso Cup kulia ni Abdul Ubinde kutoka Klabu ya Coastal Union
    NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya Pangani (PDFA) wakifuatilia mchezo wa fainali ya Ligi ya Aweso Cup
    NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM akikagua timu shiriki kabla ya kuanza mchezo huo
   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza na timu shiriki kabla ya kuanza mechi ya fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Kumba wilayani Pangani
   Wasanii wa Bongo Movi ambao wamejitokeza kwenye fainali ya Aweso Cup wakitoa burudani
   Mchezaji wa zamani wa Coastal Union Razack Kareka kulia akifuatilia mchezo huo
   Viongozi wa timu ya Coastal Union "Wagosi wa Kaya"wakifuatilia mechi hiyo ya fainali kulia ni Salim Bawaziri ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee  na kushoto ni Abdul Ubinde
  Meneja wa timu ya TOC akiwa amebebwa juu kwa furaha
  KIKOSI cha timu  ya TOC ambao ni Mabingwa wa Kombe la Aweso Cup msimu wa mwaka 2018


  KIKOSI cha timu ya Ushirika FC wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza mechi hiyo.

  TIMU ya TOC FC juzi walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Ushirika FC mabao 4-3 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye viwanja vya Kumba wilayani Pangani.

  TOC ambao ni mabingwa walikabidhiwa kombe la Ubingwa,Medali na kitita cha sh.milioni 1 kutoka kwa mdhamini wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo (CCM).

  Huku mshindi wa pili timu ya Ushirika FC walikabidhiwa kitita cha laki sita na medali wakati mshindi wa tatu akipata laki nne na medali kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.

  Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kushindwa kutambiana ndani ya dakika tisini na hivyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ndipo TOC walipofanikiwa kuibuka videdea.

  Aidha zawadi nyengine zilitolewa ni timu yenye nidhamu ambapo Super Boys ya Sakura ilifanikiwa kuibuka na kukabidhiwa seti jezi moja huku nafasi ya mfungaji bora ikichukuliwea na Twaha Bungala ambaye alikabidhiwa kitita cha sh.50, 000 wakati mwamuzi bora akiibuka Bakari
  Juma “Enye” ambaye alipata Jezi ya waamuzi seti moja.

  Ligi hiyo ilishirikisha timu 20 ambazo zilichuana vilivyo ili kuwezakumpata bingwa ambaye atapata  nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mkoa wa Tanga inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.

  Akizungumza mara kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi Naibu Waziri Aweso alisema ataendelea kusapoti michezo kwenye Jimbo lake ili kuweza kuwasaidia vijana kuweza kuonyesha vipaji vyao sambamba na kunufaika na fursa zinazopatikana kupitia soka ili waweze kujikwamua kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka.

  "Ndugu zangu wana Pangani hususani vijana michezo ni ajira hivyo tucheze mpira kwa malengo ikiwemo kujituma kwani hakuna  mafanikio yanayoweza kuja bila kucheza kwa kuonyesha uwezo wenu kwa lengo la kufika mbali kisoka"Alisema.


  0 0


  Na Hamza Temba-Arusha

  Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) imezua mjadala mzito na mabishano makali katika Mkutano wa Nane wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Arusha juzi.

  Mvutano huo ulisababishwa na hoja iliyowasilishwa na Tanzania ambayo ilitaka kuboreshwa kwa kifungu cha nne cha itifaki hiyo ambacho kinazitaka nchi wanachama kutangaza eneo lote la jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama kituo kimoja cha safari za utalii duniani.

  Tanzania ikiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ilipinga vikali na hatimaye ikagoma kusaini itifaki hiyo ambayo imejadiliwa kwa zaidi ya miaka saba mpaka pale mapendekezo yake yalipoingizwa kwenye kifungu hicho.

  Kifungu hicho kilikuwa kinasema, "Every Partner State shall market and promote the Community as a single tourist destination", (Kila nchi mwanachama itatangaza jumuiya kama kituo kimoja cha safari za utalii (duniani)).

  Tanzania ikapendekeza kwenye kifungu hicho uongezwe mstari unaosema, "while maintaining country identites" (huku kila nchi mwanachama ikibaki na utambulisho wake halisi).

  Mapendekezo hayo ya Tanzania yaliungwa mkono na Burundi na kupingwa vikali na nchi za Kenya, Uganda na Rwanda ambazo zilisema hakuna madhara yeyote ya kutobadilisha kifungo hicho. Nchi ya Sudan Kusini haikuweza kushiriki mkuatano huo.

  Licha ya majadiliano makali yaliyosababisha mkutano huo  kumalizika majira ya saa nne za usiku badala ya saa 12 jioni kwa mujibu wa ratiba ilivyopangwa, wajumbe hao walikubali mapendekezo ya Tanzania na hatimaye itifaki hiyo ikasainiwa.

  Awali itifaki hiyo ilijadiliwa kwenye vikao vya wataalam wa jumuiya hiyo na Makatibu Wakuu, siku tatu kabla ya kuwasilishwa kwenye Baraza hilo la Mawaziri.

  Akizungumza baada ya mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema Tanzania ililazimika kuweka msimamo huo ili kuepuka madhara ya nchi nyingine kutangaza vivutio vyake kuwa viko nchini kwao kama ambavyo nchi ya Kenya imewahi kutangaza mlima Kilimanjaro upo kwao.

  Aidha, alisema msimamo huo pia ulilenga kulinda maslahi ya Tanzania kwakuwa ni nchi pekee yenye vivutio vingi na ambayo imehifadhi ardhi yake kwa zaidi ya asilimia 32 ukilinganisha na nchi nyingine wanachama, mfano Kenya ambayo imehifadhi asilimia 7 tu ya ardhi yake.

  Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Ibara ya 115 (1-3) na Ibara ya 116 unaeleza kuwa jumuiya inaweza kuanzisha sera, mikakati na mbinu mbalimbali za kufanya shughuli za utalii na usimamizi wa wanyamapori kwa pamoja, huku kila nchi ikiruhusiwa kubaki na usimamizi, mikakati na sera zake kadri inavyoona inafaa.


  Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale wa Uganda, Ephraim Kamuntu (katikati) na wawakilishi wa Mawaziri wa Utalii wa Burundi, Kenya na Rwanda wakisaini Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika ukumbi wa EAC Jijini Arusha. 
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasilisha mapendekezo ya Tanzania kwenye kifungu cha nne cha Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika Mkutano wa Nane wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki.
   
   Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale wa Uganda, Ephraim Kamuntu (katikati) na wawakilishi wa Mawaziri wa Utalii wa Burundi, Kenya na Rwanda wakisaini Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika ukumbi wa EAC Jijini Arusha.
  Baadhi ya wajumbe wa Tanzania walioshiriki mkutano huo.

  0 0

  MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa semina ya viongozi na wafanyakazi wa ARU iliyoendeshwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO pia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbass (kushoto) na Mwanadilpomasia Lucas Jackson (hayupo pichani) chuoni hapo mwishoni mwa wiki. Katikati ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi. (Imeandaliwa na Robert Okanda) 
  Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa ARU wakishiriki semina hiyo chuoni hapo mwishoni mwa wiki. 
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO pia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbass akitoa mada ya kuhusu umuhimu wa taasisi za serikali kutoa taarifa kwa umma na kusisitiza kwa mujibu wa sheria zinapaswa kutoa taarifa wana habari ndani ya siku 21 toka zinapokuwa zimehitajika wakati wa semina hiyo iliyofanyika ARU Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa (kushoto) na sehemu ya viongozi wa ARU wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO pia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbass alipokuwa akiwasilisha mada. Kutokea (kushoto) ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Gabriel Kissenga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi na Mwanadilpomasia kutoka Kituo cha Diplomasia Dar es Salaam, Lucas Jackson (kulia). 
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO pia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbass akitoa mada ya kuhusu umuhimu wa taasisi za serikali kutoa taarifa kwa umma na kusisitiza kwa mujibu wa sheria zinapaswa kutoa taarifa wana habari ndani ya siku 21 toka zinapokuwa zimehitajika wakati wa semina hiyo iliyofanyika ARU Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Mmoja wa washiriki wa semina ya viongozi na wafanyakazi wa ARU akichangia jambo katika semina hiyo. 
  Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi na wafanyakazi wa ARU iliyoendeshwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO pia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbass na Mwanadilpomasia kutoka Kituo cha Diplomasia Dar es Salaam, Lucas Jackson wakisikiliza kwa makini mada chuoni hapo mwishoni mwa wiki. 
  Mwanadilpomasia kutoka Kituo cha Diplomasia Dar es Salaam, Lucas Jackson akitoa mada ya kuhusu itifaki na taratibu za kitaalam za utoaji huduma kwa jamii wakati wa semina iliyofanyika ARU Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO pia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbass akichangia pointi kuhusu maswala ya itifaki katika semina iliyofanyika ARU Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi na wafanyakazi wa ARU iliyoendeshwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO pia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbass na Mwanadilpomasia kutoka Kituo cha Diplomasia Dar es Salaam, Lucas Jackson wakisikiliza kwa makini mada chuoni hapo mwishoni mwa wiki. 
  MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO pia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbass (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo. 


  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde akizungumza wakati wa Hafla ya kuwaaga washiriki 70 wa Programu ya Kili Challenge 20018 wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya vita dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi. 
   Baadhi ya washiriki wa Changamoto hiyo pamoja na wageni mbalimbali wakifuatilia hotuba zilizokuwa wakati wa Hafla hiyo iliyofanyika lango la Machame . 
   Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maswala ya UKIMWI,Oscer Mukasa akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
   Mwakilsihi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witnes Shoo (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Hai,Onesmo Buswelu pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook wakiwa katika hafla hiyo. 
   Baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro wakiwa katika Hafla hiyo. 
   Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ,Leonard Maboko akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga washiriki 70 wa changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya UKIMWI ,zoezi hilo linaratibiwa na Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita (GGM). 
   Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Kippi Warioba akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
   Makamu wa Rais wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita (GGM) Simon Shayo akizungumza wakati wa kuwaaga washiriki 70 wa changamoto hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro na kuuzunguka kwa kutumia Baiskeli. 
   Mgeni Rasmi katika tukio hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde akikabidhi Bendera kwa washiriki wa changamoto hiyo kwa njia ya kuzunguka mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavundeakijaribu kuendesha Baiskeli kuashiria uzinduzi wa Changamoto ya kuzunguka Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baikeli.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavundeakishirikia zoezi la Kupanda Mlima Kilimanjaro kuashiria mwanzo wa safari ya wapandaji 40 wanashiriki zoezi hilo. 
   Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah ni miongoni mwa washiriki walioanzisha safari hiyo. 
   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witnes Shoo (kulia) akiwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro Betrita Loibook (Kushoto) pia wameshiriki katika kuanzisha safari ya wapanda Mlima hao.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


  ZAIDI ya Sh Bilioni 20 zimekusanywa kutoka kwa mashirika 40 yasiyo ya kiserikali pamoja na taasisi mbalimbali za serikali kwa ajili ya kusaidia katika kampeni za kupambana dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi ambapo tayari Mamilioni ya watanzania wamekwisha nufaika nazo.

  Fedha hizo zimekusanywa kampuni ya Kuchimba dhahabu ya Geita (GGM) kupitia changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro, ijulikanayo kama “Kili Challenge” tangu mwaka 2001 ilipoanzishwa ,mwaka huu ukiwa mwaka wa 17 ikishirikisha washiriki 70 watakao shiriki kupanda Mlima huku wengine wakizunguka mlima huo kwa kutumia Baiskeli .

  Akizungumza wakati wa Hafla ya kuwaaga washiriki wa Programu ya Kili Challenge 20018 iliyofanyika katika lango la kupanda Mlima Kilimanjaro la Machame ,Makamu wa Rais wa GGM, Simon Shayo amesema Progaramu hiyo imepanua wigo wa kusaidia Taasisi zinazojikita kuhudumia wachimbaji wadogo wadogo pamoja na maeneo ya wavuvi ambako tafiti zinaonyesha wako kwenye mazingira hatarishi ya kuambukizwa VVU.

  “Kila siku na kila mwaka ,tukio hili la hisani linaendelea kuwa na matokeo makubwa kwa jamii inayotuzunguka ,ninayo furaha leo kutagaza kwamba kupitia Kili Challenge tumeweza kuchangisha zaidi ya Bilioni 20 .”alisema Shayo.

  Alisema fedha hizo zimekusanywa kutoka katika Mashirika 40 yasiyo ya kiserikali (N.G.O,S) pamoja na taasisi mbalimbali za serikali kupitia Tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo watanzania zaidi ya Milioni moja wamenufaika nayo.

  Shayo alisema mbali na tukio hilo ,KAmpuni ya GGM imeendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii ikiwemo ya Elimu,Afya,Maji na miundombinu ya barabara katika mkoa wa Geita na kwamba imetenga kiasi cha Sh Bil 9.2 kwa ajili ya huduma za jamii nah ii ni baada ya kuingia makubaliano na Wilaya ya Geita pamoja na Halmashauri yake.

  Mgeni rasmi katika tukio hilo ,Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde amesema Serikali ya Tanzania inajivunia jitihada hizi ambazo zinaonekana kuwa endelevu katika utafutaji wa raslimali za udhibiti wa UKIMWI nchini.

  “Kama nilivyosema TACAIDS imekuwa ikishirikiana kwa karibu na GGM kuhakikisha jambo hili linatekelezwa kwa tafsiri ya kuoanisha Changamoto za mapambano dhidi ya UKIMWI na ugumu wa upandaji wa Mlima Kilimanjaro kupitia njia ngumu ya Machame na uzungukaji wa Mlima Kilimanjaro kwa baiskeli.”alisema Mavunde.

  Hadi sasa zaidi ya Watu 700 kutoka duniani kote wameshiriki katika changamoto hiyo ya kihistoria ya upandaji Mlima kupitia programu ya “Kili Challenge” na kukusanya fedha ambazo zimesaidia maeneo mbalimbali yakiwemo makundi ya Wajane, Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI, Watoto yatima, Vijana, pamoja na Taasisi zinazotoa huduma muhimu za UKIMWI. 

  Aidha, Fedha hizi zimetumika kuboresha huduma za Hospitali mbalimbali nchini zikiwemo za Mkoa wa Geita na Kibong’oto Mkoani hapa na ujenzi wa Vituo vinne (4) vya maarifa kwenye njia kuu za usafirishaji.

  0 0

  BENKI ya Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB) imetanua wigo wake kwa kuzindua huduma ya Mwalimu Bank Wakala itakayowawezesha Watanzania na wateja wa benki hiyo kupata huduma za benki hiyo kuwa karibu katika maeneo yao wanayoishi au kufanyia kazi.

  Akizungumza katika uzinduzi wa Mwalimu Bank Wakala mkoani Tanga juzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu Mwalimu Commercial Bank Plc, Ronald Manongi amesema benki yake imeingia kwenye makubaliano ya kimkakati na Maxcom Africa Plc kupitia mawakala wa Maxmalipo.

  Amefafanua lengo ni kuwawezesha wateja wa benki hiyo kuweza kunufaika na benki yao kwa kupata huduma kwa urahisi, haraka na unafuu."Benki yetu ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa tunasogeza huduma zetu karibu zaidi na wananchi popote pale walipo. "Nia ni kuhakikisha kuwa mtanzania popote alipo aweze kupata huduma za kibenki ili kwa pamoja tuweze kukuza uchumi wa nchi yetu, "alisema.

  Manongi amesema kuwa benki yao imehakikisha kuwa inaendelea kuwa bega kwa bega na wateja wake kupitia zaidi ya mawakala 10,000 wa Maxmalipo walioenea katika maeneo mbalimbali nchini. Ameongeza wateja wa Mwalimu benki watapata huduma mbalimbali kama kuweka fedha kwenye akaunti zao, kutoa fedha ikiwa ni pamoja na mishahara kwenye akaunti zao, kuangalia salio na taarifa fupi, malipo ya luku, maji na muda wa maongezi.

  “Tumejipanga katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu,hivyo kwenye kila huduma tunayoitoa, kwanza tunaangalia mteja wetu anataka nini, ndipo kupitia timu yetu tunabuni njia sahihi yenye ufanisi katika kukidhi mahitaji ya wateja wetu,amesema. Aidha ameongeza wana shauku ya kuona wateja wao wanafanikiwa na wanaamini wateja wakifanikiwa na benki pia itafanikiwa. “Tutaendeleakuja na ubunifu mbalimbali wa kiteknolojia ili kuzidi kurahisisha huduma kwa wateja wetu,"amesisitiza.

  Uzinduzi wa Mwalimu Bank Wakala ulifanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo.
     Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa kampuni ya Maxcom Afrika Plc,  Gasper Mrosso (kulia), akimuelekeza mmoja ya wanahisa wa Benki ya Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Walimu Handeni (CWT), Hamisi Ngomero  jinsi ya kutumia mashine maalum za POS ili kuweza kupata huduma mbalimbali za kibenki kupitia huduma ya MCB Wakala wakati wa uzinduzi wa rasmi wa MCB Wakala uliofanyika pamoja Mkutano Mkuu wa pili wa Wanahisa wa benki hiyo mjini Tanga mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commecial Bank,   Ronald Manongi na Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Afrika Charles Natai.
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Mwalimu Commecial Bank Plc,  Ronald Manongi, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya MCB Wakala uliofanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa pili was Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Tanga mwishoni mwa wiki. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Commecial Benki  Ronald Manongi (kushoto) akishuhudia mteja wa benki hiyo ambae pia ni Katibu wa Chama cha Walimu Handeni (CWT), Hamisi Ngomero (wa pili kushoto), akipata hutuma kupitia MCB Wakala huduma iliyozinduliwa wakati wa Mkutano Mkuu wa pili wa Wanahisa wa benki hiyo mjini Tanga hivi karibuni. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa kampuni ya Maxcom Afrika Gasper Mrosso,  Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Afrika Plc, Charles Natai na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Ubunifu wa Maxcom, Deogratius Lazari.  
    Baadhi ya wanahisa wa benki hiyo wakihudhuria Mkutano wao Mkuu wa pili wa Mwaka mjini Tanga hivi karibuni.

  0 0

  Na EmanuelMadafa,Mbeya

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amewaagiza askari polisi kitengo cha reli kuwakamata watu wanaotuhumiwa kupiga mawe treni pindi zinapopita kwenye maeneo yao na kuhasababisha uharibifu ambao huigharimu serikali pesa nyingi katika matengenezo vingine watawajibishwa wao

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, alipotembelea Karakana ya Tazara iliyopo Jijini Mbeya.Amesema wapo baadhi ya watanzania wamekuwa wakiendelea na vitendo vya kuhujumu treni hivyo lazima wachukuliwe hatua kali ili kukomesha vitendo hivyo kwa kuhakikisha zinatolewa adhabu kali kwa watako bainika kufanya vitendo hivyo.

  Waziri Nditiye amewataka madereva wa treni kusimamisha treni endapo itatokea kuna baadhiya watu wamefanya tukio la kupiga mawe treni mara iwapo safarini ili wahusika wakamatwe na kuhojiwa ili watoe sababu za kufanya kitendo hicho sanjali na kuchukuliwa hatua mara moja.

  Wakati huo Naibu Waziri , amewahakikishia wafanyabiashara na wachuuzi kuwa hatua ya uimarishaji wa usafiri na usafirishaji kupitia Reli nchini,uko pazuri na tayari muda wa kuondoa mizigo mizito inayotumia malori umefika.Amesema katika kuimarisha usafiri huo, zaidi ya shilingi bilioni 10 zimetolewa na serikali kuboresha vichwa vya magari moshi na karakana mbalimbali nchini.

  Amesema serikali haitegemei kuona malori ya kiendelea kusafirisha mizigo mizito ambapo wakati mwingine yamekuwa chanzo cha kuharibu miundombinu ya barabara pamoja na kuua soko la Tazara.“Barabara hizi zimejengwa kwa gharama kubwa sana, tunategemea mizigo hiyo kuanza kusafirishwa kwa kutumia njia ya reli na kwamba ni jukumu la wafanyakazi kuanza kuwashawishi wateja wao wa zamani na wapya ili wafanye kazi na Tazara,”amesema.

  Hata hivyo amesema ,serikali haiwezi kuendelea kuwalipia mishahara lazima itafika pahala ambapo itasitisha na kuiacha Tazara iendelee na majuku yake kwa kujiendesha yenyewe, hivyo wanapaswa kujipanga kwa kuwa wabunifu.

  Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kulia akisikiliza maelezo kutoka kwa Boniface Phiri ambaye ni Mhandisi uzalishaji kiwanda cha kuzalisha mataaluma ya Reli kwa kutumia zege kinachomilika na Tazara kilichopo katika Kijiji cha Mswiswi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya. 
  Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kulia akipokea ufafanuzi kutoka kwa Boniface Phili Mhandisi uzalishaji kiwanda cha kuzalisha mataaluma ya Reli kwa kutumia zege kinachomilikiwa na Reli ya Tazara kilichopo katika Kijiji cha Mswiswi Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya
  Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kulia akisikiliza maelezo namna ya utengenezaji wa mataaluma ya reli kwa kutumia zege kutoka Mhandisi Boniface Phili Mhandisi uzalishaji kiwanda cha kuzalisha mataaluma ya Reli kwa kutumia zege kinachomilikiwa na Tazara kilichopo katika Kijiji cha Mswiswi Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya
  Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye pili kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa mafundi ya karakana ya Reli ya Tazara iliyopo katika kituo cha Iyunga Jijini Mbeya

  0 0

  Rais wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga, akiimba wakati wa ibada iliyofanyika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Anglikana Jijini Dodoma leo.
  Watoto kutoka Kanisa la Anglikana Msalato wakiimba katika ibada hiyo.
  Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Jijini Dar es Salaam, Madamu Ruth Mwamfupe akiimba katika ibada hiyo huku akisindikizwa na waumini wa kanisa hilo. 
  Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
  Waumini wakiwa ibadani.
  Kwaya ya watoto kutoka Msalato ikitoa burudani ya nyimbo za injili. 
  Mwanamuziki Mzee Makasy ambaye hivi sasa ni mwimbaji wa nyimbo za injili baada ya kuokoka akitoa burudani.
  Raia wa kigeni ambao wanasali katika kanisa hilo wakifurahi matukio mbalimbali ya uimbaji.
  Mwimbaji wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha kutoka Dar es Salaam, akiimba.
  Katibu wa TAMUFO ambaye pia ni Muimbaji wa nyimbo za injili Stellah Joel, akiimba.
  Viongozi wa dini wa kanisa hilo wakisalimiana na Emmanuel Mbasha ambaye ni muimbaji wa nyimbo za injili.


  Na Dotto Mwaibale, Dodoma.

  WAIMBAJI wa Nyimbo za injili ambao ni wanachama wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), leo wameshiriki ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Anglikana Jijini Dodoma ambapo pia walipata fursa ya kutoa burudani ya nyimbo mbalimbali ikiwa ni njia ya kuhubiri na kulifanya kanisa hilo kuwaka moto wa furaha kutokana na burudani safi kutoka kwa watumishi hao wa mungu.

  Wanamziki hao ambao wapo jijini Dodoma wamepokelewa na Kanisa hilo na kesho watatembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia umoja wao TAMUFO.Mbali ya kesho kwenda Bungeni leo jioni watashiriki katika tamasha kubwa la nyimbo za injili ambalo litaenda sanjari na uzinduzi wa Albam ya nyimbo ya injili ya Kwaya ya Safina ambayo ipo katika hilo Kuu la Anglikana Dodoma ambapo kwaya mbalimbali zitatoa burudani ya nyimbo za kuabudu.

  Akizungumzia kuhusu wanamuziki hao Rais wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga, alisema wanayofuraha ya kufika Dodoma salama na kuwa leo hii watashiriki katika tamasha hilo na kesho asubuhi watakwenda kutembelea Bunge.Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel, amesema makundi mbalimbali ya wanamuziki wanaounda umoja huo yatakuwepo kama vile, waimbaji wa nyimbo za injili, Dansi, Bongo Fleva, Muziki wa Asili na Taarabu.

  "Wanamuzi wote kutoka katika makundi hayo tayari wamefika Dodoma na kuwa maandalizi yote yamekamilika.Amewataja baadhi ya wanamuziki hao kuwa ni Hamza Kalala, Mzee Makasy, Witness Mweupe, Emanuel Mbasha, Madamu Ruth Mwamfupe , Happyness Sanga kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na wengine.

  0 0


  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii


  NAIBU Waziri wa Mfugo na Uvuvi atembelea shamba la AKM Glitters Company Ltd lililopo Dar es salaam eneo la Mbopo na Mbezi Beach, ambapo lengo la ziara yake ni kuangalia fursa walizonazo Watanzania katika ufugaji.

  Akiwa katika ziara yake katika kampuni hiyo Naibu Waziri ulega ameona kazi mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikiwemo ya shamba la kuku wazazi, sehemu ya kutotoleshea vifaranga na chakula cha kuku wazazi.Ulega amesema ufugaji wa kuku ni fursa kubwa  ambayo ikiitumia vizuri, mhusika anaweza kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja, na taifa zima kwa ujumla wake.

  " Serikali lengo letu ni kuhakikisha nyama ya kuku isiwe kitoweo kwa watu wa juu tu, bali kiwe kwa hali zote kuanzia ngazi ya watu wa kipato cha chini na kati."Tunataka watu wote wajiingize kwenye ufugaji wa kuku, ili tuweze kujitosheleza wenyewe na tutoe ajira nyingi kwa watu ili kuendeleza tasnia hii ya kuku na kuuza kuku kwa bei ya chini kuliko kutegemea kuku kutoka nje,"amesema.

  Amefafanua katika bajeti  ya serikali kwa mwaka huu wamependekeza pendekezo ambalo limeletwa Wizara ya Fedha na Mipango, kwamba riba imeondolewa kwa asilimia 5 kutoka kwa wakina mama na vijana."Sasa haitakuwa ni hiari kwa Halmashauri bali ni sheria kuwa Halmashauri zote kadri ya mapato yao ya ndani yanavyopatikana yatakwenda moja kwa moja kwa vijana na akina mama kwa asilima 5 kila mmoja," ameongeza.Amesema Serikali imeona hivyo, ili kusaidia hasa wakina mama walio wengi na kufuta riba hiyo.

  Kwa upande wake Mkurugezi Mtendaji wa kampuni hiyo Elizabeth Swai alizungumzia suala la usafirishaji vifaranga ikiwa ni changamoto kuwafikia wakazi wa vijijini ambapo Naibu Waziri alisema, Serikali imejiweka katika mazingira mazuri katika hili kuhakikisha usafirishwaji unawafikia pia watu waliopo vijijini.

  "Tunaomba tumuunge mkono Rais wetu Dk. John Magufuli katika kazi hii kubwa wanayoifanya ya kuzindua shirika letu la ndege ATC,ambapo haitakuwa na sababu ya kusafirisha kwa gari, ndio maana tunatakiwa kuleta mafanikio ya kuendeleza miundo mbinu ili liwezekane hili."Pamoja na mifugo iweze kukua inabidi kuimarisha ndege zetu pamoja na reli, ambapo reli yetu ya mwendokasi ikifanikiwa ina maana itawezesha usafiri kwa urahisi zaidi na ksafirisha bidhaa katika maeneo mengi kwa haraka zaidi,"amesema.

  Ulega amesema hiyo ni fursa kubwa  lazima kampuni ya AKM waungwe na kuona jinsi gani watashirikiana  kuendeleza tasnia hiyo na pia kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wafugaji wengine ili waweze kufanikiwa kama walivyofanikiwa kwenye kampuni hiyo. Hata hivyo kampuni ya AKM imetoa nafasi kwa walio na uwezo mdogo wakalipa nusu na robo ya Sh.milion 1.9 kwa ajili ya kupata vifaranga na huduma nyinginezo kama dawa na vyakula vya kuanzia.

  Naibu Waziri ametoa mwito kwa Watanzania kwamba, hawatakiwi kuagiza nyama kutoka nje bali wanatakiwa kuzalisha hapahapa nyumbani na kujitosheleza wenyewe.Ameongeza hiyo inasaidia kuwa na uhakika wa chakula ambacho kina protein ya kutosha ili ukuaji wa watoto wetu na jamii uwe ni mzuri.

  Ulega amesema  " haya mambo yanawezekana tukiungana wote kwa pamoja na sisi kama serikali tupo mstari wa mbele kuhakikisha tunafanikisha hili hasa katika suala la kupunguza zaidi kodi katika vyakula vya mifugo kwa bei ya chini zaidi".
   Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia kuku wa wazazi katika shamba la (AKM) lililopo Mbopo jijini Dar as Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafanyakazi wa shamba la kuku wazazi,kituo cha kutotolea vifaranga mbopo jijini Dar as Salaam.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shamba hilo.

  0 0

  Rock City Marathon yazinduliwa jijini Mwanza 

  Mwanza, 24 Juni, 2018: Msimu wa tisa wa mbio za Rock City Marathon umezinduliwa rasmi jijini Mwanza mwishoni mwa wiki hii huku wito ukitolewa kwa wadau wa utalii na michezo nchini hususani Kanda ya Ziwa kutumia mbio hizo kutangaza fursa na vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo. 

  Uzinduzi wa mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA) ulihusisha pia wawakilishi wa wakuu wa mikoa yote ya kanda ya Ziwa ikiwa ni mikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Kagera. 

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw Mongella katika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall jijini humo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha alisema ipo haja ya wadau wa utalii na michezo katika kanda hiyo kuhakikisha kwamba wanayatumia vizuri mashindano hayo katika kuhakikisha fursa na vivutio vya utalii vilivyopo kwenye ukanda huo vinatangazwa ipasavyo. 

  “Ndio maana serikali tunafarijika sana tunapoona sekta binafsi inajiinua na kubuni mbinu bora kabisa hasa kupitia michezo ili kuiboresha zaidi sekta hii ya utalii hususani kwa kanda yetu ya Ziwa ambayo kwa sasa ipo kwenye mabadiliko makubwa,’’ Alisema. 

  Akizungumzia maendeleo ya mchezo huo Bi Tesha alisema ipo haja kwa wadau kuhakikisha wanatumia vizuri mwamko wa mkubwa mashirika na taasisi mbalimbali hapa nchini ambazo zimeamua kuunga mkono mchezo huo katika kuinua vipaji vipya. 

  “Niombe sana kila kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia mchezo huu katika ngazi tofauti tofauti, idara mbali mbali na vyama mbali mbali, tulirudishe taifa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.’’ Alisema. 

  Mbio hizo zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, PUMA Energy Tanzania, New Mwanza Hotel, Precision Air, KK Security, CF Hospital, Rock City Mall, Dasani, Metro Fm, Global Education Link, Barmedas TV, Gold Crest Hotel, NSSF, EF Outdoor, na SDS huku wengine wakionyesha nia ya kudhamini mbio hizo. 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema uzinduzi wa mbio hizo zinazotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza umefanyika mapema ili kuruhusu wadau wote wapate muda wa kutosha katika kujiandaa kwa ajili ya ushiriki. 

  “Lakini pia katika msimu huu wa mbio hizi tumefungua milango zaidi kwa wadau wa maliasili na utalii ambapo si tu kwamba wataweza kushiriki katika mbio hizo bali pia watapata fursa ya kufanya maonyesho ya utalii pamoja kutoa elimu zaidi kuhusu fursa za kitalii pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.’’ Alisema. 

  Alisema kanda ya Ziwa kwa ujumla ina vivutio vingi vya kihistoria ambavyo vinaweza kutumika kuimarisha sekta ya utalii wa ndani na nje huku akiongeza kuwa ukaribu uliopo baina ya jiji la Mwanza na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni sababu tosha ya mji huo kuvutia watalii wengi zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine iliyo nje ya kanda ya Ziwa.
   Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa msimu wa tisa wa mbio za Rock City Marathon 2018  kwenye hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa mbio hizo, Zenno Ngowi, (Kushoto kwake), Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi (alievaa suti nyeusi) pamoja na Mwakilishi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA), Benjamini Nyagabona (alivaa kofia). 
   Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha akizungumza kwenye uzinduzi huo pamoja na mambo mengine alitoa wito kwa wadau wa utalii na michezo nchini hususani Kanda ya Ziwa kutumia mbio hizo kutangaza fursa na vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.
   Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
   Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye hafla hiyo.
   Mgeni rasmi ambaye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa waliohudhuria uzinduzi huo.
   Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadhamini wa mbio hizo. Miongoni mwao ni pamoja na mwakilishi wa KK Security Bw Meshack Richard (wapili kushoto),  Mwakilishi wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Gloria Munhambo (wa kwanza kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Radio Metro fm, Bw Maganga James (wa pili kulia).
   Wawakilishi wa klabu za wakimbiaji katika mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
   Wawakilishi wa klabu za wakimbiaji katika mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
  Wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini uzinduzi huo.


  0 0

  Na Mwandishi wetu
  TAASISI ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shule ya Uchumi ya Norway (NHH) umekamilisha utafiti uliochukua miaka sita uliopelemba kama uwezeshaji wasichana kiuchumi ndio njia ya kuwezesha uzazi wa mpango.
  Matokeo ya utafiti huo ‘Girls’ Economic Empowerment: The Best Contraceptive?’ umeelezwa kuja kusaidia kuelewa uzazi kwa wasichana na athari ya hali hiyo katika maamuzi yao ya kiuchumi.
  Utafiti huo uliofanywa kuanzia mwaka 2013 hadi 2018, ulifanywa kufuatia programu iliyotengenezwa na Femina Hip, taasisi inayojishughulisha na kubadili tabia za vijana kwa kutumia mawasiliano.
  Katika programu hiyo wasichana wa sekondari walipewa mafunzo ya ziada nje ya utaratibu wao yaliyochanganywa na elimu ya afya ya uzazi, uwezeshaji kiuchumi na elimu ya maisha.
  Ubalozi wa Norway jijini Dar es salaam ulifadhili sehemu ya programu hiyo.
   Maarifa yaliyopatikana kutokana na utafiti huo yanatarajiwa kuwasaidia watengeneza sera, wanazuoni na  watu wa asasi zisizo za kiserikali kutambua athari za kuwezesha au kutowezesha wasichana kiuchumi katika uzazi.
  Lengo kuu la utafiti huo ni kuwa na uelewa mpana utakaowezesha uundaji wa sera stahiki kuhusu uchumi na uzazi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Tausi Kida alisema kwamba amejisikia furaha sana kufanyakazi na  Shule ya Uchumi ya Norway, ubalozi wa Norway na Femina katika kutafuta suluhu kwa matatizo yanayokabili taifa.
  Alisema kwamba tabia, maarifa, ujuzi na maamuzi kwa vijana kuhusu afya yao ya uzazi kuna athari kubwa kwa maendeleo na afya kwa ujumla.
  Imeelezwa kuwa wakati wa kuanza kwa utafiti huo, kundi la utafiti lilionesha kwamba hali ya kimaskini waliyokuwa wanakabiliana nayo iliwafanya wajihusishe na ngono.
  Utafiti ulibaini kwamba kuwasaidia wasichana kabla ya ndoa kunawapa fursa zaidi za kukua kiuchumi.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa wadau na wageni waalikwa wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Wanawake Jinsia Watoto na Wazee (jinsia), Bi. Mboni Mgaza akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad akizungumza jambo wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Vyombo vya habari wa Femina Hip, Amabilis Batamula akielezea jinsi Femina Hip kupitia program hiyo ilivyoweza kufikia wasichana wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
   Profesa kutoka Shule ya Uchumi ya Norway (NHH),  Kjetil Bjorvatn akiwasilisha matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
   Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez,  Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Wanawake Jinsia Watoto na Wazee (jinsia), Bi. Mboni Mgaza wakimsikiliza Mshehereshaji wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
   Shemu ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali wakishiriki kuchangia maoni wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akifurahi jambo katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya wageni waalikwa mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Na Frankius Cleophace Tarime.

  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Tarime Mkoani Mara Marwa Daud Ngicho amechangia Kiasi Cha Shilingi Mill6 na Mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Rogoro Masanga wilayani Tarime Mkoani Mara.

  Ngicho amesema kuwa kama kiongozi ni wajibu wake wa kuchangia Ujuenzi wa Nyumba ya Bwana ili waumini wazidi kuombea Viongozi wanaotawala Nchi ya Tanzania na Ulimwengu akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pome Magufuli.

  “Mimi kama kiongozi nimeambatana na Wafanyakazi wangu wa Mgodini kwa ajili ya kufanikisha zoezi zima naanza kuchangia Millioni Tano na Mifuko Miamoja hapa hapa naomba Waumini wote na Viongozi kuniunga Mkono ili kufanikisha Zoezi ili” alisema Ngicho.

  Mwenyekiti ameongeza kuwa Jamii inayomwamini Mwenyezi Mungu haina budi kuondokana na kuamini Miungu badala ya Mungu huku akipiga vita Waganga wanapiga ramli Chonganishi na kusema kuwa wao kama Viongozi hawatawafumbia Macho kwani wanaweza Kuchocheanakusababisha Upotevu wa Amani.

  Kwa upande wake Baba Paroko Parokia ya Rogoro Baba Paroko Anord Mavumilio amezidi kuwapongeza wote waliofanikisha zoezi hilo la uchanguaji kwa ajili ya Ujenzi wa kanisa hilo huku akisisitiza waumini wa Kanisa hilo kutokata tamaa katika Ujenzi huo ambo umeanza kwa sasa.

  Aidha Mwenyekiti wa kanisa hilo Sebastian Siyange anazidi kusisitiza Waumini kufuata Maandiko yanavyosema huku wakitenda Mema na kuzidi kumtolea na kujitoa kwa ajili ya Bwana Yesu Kristu.

  Hata hivyo Mwenyekiti huyo amesema kuwa Zaidi ya Millioni 10 Zimechangwa katika harambee hiyo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo

  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Tarime Mkoani Mara Marwa Daud Ngicho akionyesha Kiasi ch Shilingi Millioni Sita Waumini wa kanisa la Rogoro katika harambee ya Ujenzi wa kanisa hilo la Romani Katoliki .
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Tarime Mkoani Mara Marwa Daud Ngicho akikabidhi Mwenyekiti wa Parokia ya Rogoro Masanga Sebastian Siyange Kiasi cha Shilingi Millioni Sita kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Tarime Mkoani Mara Marwa Daud Ngicho akiongea na Waumini wa kanaisa la Rogoro kabla ya harambee hiyo.
  Waumini wa kanisa la Rogoro wakiwa katika Misa takatifu kabla ya harambee hiyo.
  Baba paroko Parokia ya Rogoro akiongea na Waumini na kutoa Shukrani kwa harambee hiyo iliyofanyika kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.
  Kanisa Jipya la Parokia ya Rogoro Masanga Wilayani Tarime Mkoani Mara linalojengwa
  Viongozi mbalimbali wakiwemo Waumini wa kanisa hilo wakikagua Ujenzi wa kanisa hilo.

  0 0   Muonekano wa basi dogo mara baada ya kupata ajali hiyo na kupelekea vifo vya watu 14
   Pichani ni sehemu ya tukilo la ajali iliyosaabisha vifo vya watu 14 waliopoteza maisha baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la kubebea mchanga katika eneo la Dundani Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.Ajali hiyo imetokea leo Juni 25i, 2018 Alfajiri wakati basi dogo lililowabeba wanafamilia, ndugu na jamaa waliokuwa wakielekea Msata kuhudhuria sherehe za kumaliza mafunzo ya kijeshi kwa mtoto wao, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Dundani kuchukua mchanga.

older | 1 | .... | 1605 | 1606 | (Page 1607) | 1608 | 1609 | .... | 1897 | newer