Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1604 | 1605 | (Page 1606) | 1607 | 1608 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na. Vero Ignatus , Manyara.

  Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jila la Josephine Peter (51)mkazi wa Mrara kata ya Mamire wilayani Babati ameuawa na watu wasiofahamika huku shingo yake ikikatwa na kitu chenye ncha kali.

  Akizungumza leo Juni  21 Kamanda wa polisi mkoani Manyara Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema mwanamke huyo alifariki dunia juni 19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake na mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kutokana na mauaji hayo.

  Kamanda amesema kuwa hadi sasa chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika kwani mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi nakubainika kuwa hajabakwa kama watu wanavyozusha bali jeshi la polisi unaendelea na upelelezi wa tukio hilo la mauaji amesema kuwa ukikamilika taarifa kamili itatolewa

  Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara)

  Kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara Augustino Senga.
   

  0 0

  Na Mariam Mwayela,Njombe

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kutoa huduma, elimu na kusajili walipakodi wapya katika maeneo ya Ludewa, Matamba, Ilembula, Mlangali, Ikonda na Makete Mkoani Njombe ambapo mpaka sasa jumla ya walipakodi 351 wamesajiliwa.

  Zoezi hili limekuwa na muitikio mkubwa kutoka kwa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kupatiwa elimu ya kodi na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

  Akizungumza wakati wa kampeni hiyo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Bw. Richard Kayombo amewashukuru wakazi wa maeneo hayo kwa kuitikia wito na kuonyesha shauku ya kutaka kujua mambo mbalimbali yanayohusu kodi hususani usajili wa biashara, kuhakiki TIN na kusajili walipakodi wapya.

  “Tunashukuru sana kwa muitikio huu ulioonyeshwa katika zoezi hili hapa mkoani Njombe ambao unaonyesha uzalendo wa kuchangia mapato ya Serikali kwa kujisajili na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi ambayo ni mwanzo wa kutimiza wajibu wa kulipa kodi”, Alisema Kayombo.

  Kayombo amewaambia wafanyabiashara waliofika katika kampeni hiyo, kuwa na ukaribu na maafisa wa TRA ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika kila hatua ya ulipaji wa kodi na kutoa maoni yao ambayo yataboresha huduma zitolewazo na Mamlaka.

  Aidha, Kayombo aliwakumbusha kulipa kodi sahihi na kwa wakati ili kuepuka faini na adhabu zinazoambatana na ucheleweshaji huo. Vilevile, aliwasisitiza umuhimu wa kutunza kumbukumbu sahihi za biashara, kutoa risiti pindi wanapouza bidhaa au huduma na kudai risiti kila wanapofanya manunuzi mbalimbali.

  Naye William Kabupa ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wa duka la Nguo eneo la Ilembula, ameishukuru TRA na kusisitiza kuwa, zoezi hili ni zuri na litasaidia wafanyabiashara kutokuwa na sababu ya kukosa TIN au kukataa kulipa kodi.

  “Nimefurahi sana kupata TIN yangu leo hapa Ilembula kwani ilikuwa inanibidi kusafiri kwenda Njombe mjini kupata TIN. Aidha, nashauri wafanyabiashara wenzangu wa Ilembula wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata elimu na kusajiliwa ili waweze kulipa kodi na kujivunia kuwa mmoja wa wachangiaji wa mapato ya Serikali” alisema Kabupa.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea na kampeni ya kutoa Elimu, Huduma na kusajili walipakodi wapya Mkoani Njombe ambapo hadi sasa Walipakodi wa Wilaya za Makete, Ludewa, Wanging’ombe na Njombe wanaendelea kupata huduma, elimu na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

  0 0


  0 0


  Na Estom Sanga- TASAF.


  Wataalam wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka nchini Sudan Kusini na Nigeria wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa uamuzi wake wa kukuza sekta hiyo inayolenga kuzikwamua kaya za wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na umaskini mkubwa wa kipato.


  Wataalamu hao ambao wako nchini kuona namna sekta hiyo inavyotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF-ambayo inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN-wamesema Mpango huo unawagusa moja kwa moja wananchi hususani wanaoishi katika mazingira ya umaskini uliokithiri.


  Wamesema hamasa waliyoiona baada ya kuwatembelea baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Wilaya za Temeke,Ilala jijini Dar es salaam na Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani katika kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa zilizoko kwenye Mpango huo zimeonyesha kuwa katika kipindi kifupi cha utekelezaji wa Mpango huo maisha yao yameanza kuboreshwa.


  Miongoni mwa mambo yaliyowavutia Wataalam hao ni namna TASAF inavyoshirikisha Sekta nyingine za serikali kuwafikia Walengwa na uwezo  wa Watumishi wa Taasisi hiyo katika kuwatembelea Walengwa na kuwahamasisha kufanya kazi za uzalishaji mali ili kufikia malengo na kuboresha maisha ya Walengwa hao.


  Aidha suala la ujenzi wa makazi ya Walengwa kwa kutumia ruzuku wanayopata kutoka TASAF limewashangaza Wataalamu hao kwani katika maeneo waliyotembelea wamebaini kuwa Sehemu kubwa ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wamekuwa wakidunduliza fedha na kisha kununua vifaa vya ujenzi wa nyumba hususani mabati,na saruji ili kuboresha makazi yao.


  “Hili ni jambo jema ambalo nchi nyingine barani Afrika zinapaswa kuliiga kwani suala la makazi bora kwa wananchi wetu ni changamoto kubwa katika nchi nyingi za kiafrika” amesema mmoja wa Wataalam hao kutoka Sudan Kusini.Kuhusu suala la Elimu, Afya na Lishe, wataalam hao wamesema Serikali ya Tanzania Kupitia TASAF imefanya uamuzi sahihi wa kufanya mambo hayo kuwa miongoni mwa masharti ya kutekelezwa na Walengwa wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya ,mambo ambayo wamesema ni ya msingi katika kujenga rasilimali Watu. 


  Akizungumza na Wataalamu hao Mkuu wa wilaya ya Kibaha Bi. Assumpta Mshama amesema Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF umekuwa chachu muhimu katika kuwahamasisha wananchi kufanya kazi na kujiletea maendeleo na kusema wilaya yake imejipanga kikamilifu kufuatilia utekelezaji wa Mpango huo wa aina yake kupata kutekelezwa nchini.


  Wataalam hao wa Sekta ya Hifadhi ya Jamiii kutoka Sudan Kusini na Nigeria wamekuwapo nchini kwa takriban wiki moja kwa lengo la kujifunza namna Tanzania ilivyofanikiwa kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF ili kwenda kutekeleza katika nchi hizo.

   Baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Disunyala wilaya ya Kibaha wakiwa katika kitalu cha miche ya mboga (nyanya,pilipili hoho) wanazozalisha kwa lengo la kujiongezea kipato.
   Baadhi ya Wataalam wa sekta ya hifadhi ya Jamii kutoka Sudan Kusini wakiangalia matuta yaliyolimwa na Walengwa wa TASAF yanayotarajiwa kupangwa miche ya mboga mboga ikiwa ni mojawapo ya shughuli za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato.
   Mmoja wa Walengwa wa TASAF akiwa amebeba sehemu ya kuku wa kienyeji anaowafuga kwa kutumia sehemu ya ruzuku anayoipata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya maskini.
   Baadhi wageni kutoka Sudan Kusini wakiangalia tanki lililojengwa na TASAF katika kijiji cha Disunyala wilaya ya Kibaha kwa lengo la kuvuna maji ya mvua yanayotumika kumwagilia bustani ya mboga mboga ikiwa ni mojawapo ya miradi ya kuwaongezea kipato Walengwa wake. 
   Pichani ni baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka nchini Sudan Kusini wakiwa katika eneo la Shamba darasa la Muhogo lililoanzishwa na TASAF kwa lengo la kuhamasisha walengwa na wananchi wa eneo hilo kuzalisha muhogo kwa wingi kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha,Bi. Assumpta Mshama(Watatu  kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalam wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka Sudan Kusini walimtembelea ofisini kwake kabla ya kwenda kukutana na Walengwa wa Mpango huo.  0 0

  Na Mathias Canal-WK, Tanga

  Wakulima wa Mkonge Mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kupitia agizo lake alilolitoa kwa Kampuni ya Katani Limited kuhusu kulipa madeni ya wakulima ndani ya siku nne kuanzia 21 Juni 2018 hadi 26 Juni 2018 Kwa madeni ya muda mrefu ya wakulima wa zao hilo jambo lililopelekea kupunguza ufanisi na tija ya Kilimo Kwa wakulima hao.

  Dkt Tizeba ametoa agizo hilo leo 21 Juni 2018 akiwa kwenye mkutano na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) unaotekelezwa kwenye mashamba matano ya Hale, Magunga, Magoma, Mwelya na Ngombezi yaliyo chini ya miliki ya Bodi ya Mkonge Tanzania. 

  Katika Mkutano huu uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Martin Shigela sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe, Msajili wa Hazina, Mtendaji wa BRELA, Muwakilishi wa mwanasheria Mkuu wa serikali, Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge na wataalamu wengine; Waziri wa Kilimo Mhe Tizeba ametoa agizo hilo Kwa Uongozi wa mfumo wa Kilimo cha wakulima wadogo wa kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO), Kampuni ya Katani ltd ambayo ndio mnunuzi pekee wa Mkonge wa mkulima na Bodi ya Mkonge Tanzania.

  Sambamba na agizo hilo pia Mhe Waziri ameiagiza Bodi ya Mkonge Tanzania kupitia upya mikataba yote iliyopo Kwa kushirikisha Bodi yenyewe, Kampuni ya Katani na wadau wa zao hilo haraka iwezekanavyo ili kurekebisha makosa yaliyopo.

  Aidha, ameitaka Bodi hiyo ya Mkonge Tanzania kuitisha kikao na wadau wote wa zao hilo ili kupitia upya utaratibu wa makato ya mgawanyo wa mapato katika kusindika zao la Mkonge.Mhe Dkt Tizeba aliongeza kuwa hati za miliki ya mashamba zitapaswa kutolewa Kwa wahusika Mara baada ya kujiridhisha na mchakato utakapokamilika huku akiwataka wakulima kulipa malimbikizo ya kodi ya ardhi.

  Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemaliza ziara ya siku moja ya kikazi mkoani Tanga huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela Kwa umakini na uwajibikaji katika kusimamia sekta ya Kilimo hususani zao la Mkonge mkoani humo.
  Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akitoa maelekezo ya serikali wakati wa kikao cha pamoja na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) kabla ya mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela akizungumza jambo kabla ya kumaribisha mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kuongoza mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.
  Viongozi mbalimbali Mkoani Tanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela wakiagana na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.
  Wadau wa zao la Mkonge wakichangia mada wakati wa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MWEZESHAJI wa Vijana katika masuala ya maendeleo endelevu nchini Rose Mbaga amesema ikitokea akapata nafasi ya kukutana na Rais Dk.John Magufuli atamuelezea kuhusu changamoto ya ajira kwa vijana nchini.

  Pia amesema katika kutatua changamoto ya ajira ametoa rai kwa Watanzania wote kushirikiana na Serikali katika kuitatua huku akisisitiza ipo haja kwa vijana kuwa na uthubutu wa kufanya mambo yanayohusu maendeleo.

  Mbaga ametoa kauli hiyo jana usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akijiandaa na safari ya kwenda nchini Uingereza baada ya kutambulika kuwa miongoni mwa wanawake 100 wanaosaidia kuwainua wengine kwenye kazi za kijamii .Akiwa huko atakabidhiwa tuzo ya STAR AWARD.

  "Ikitokea siku nikapata nafasi ya kukutana na Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli kikubwa nitakachomwambia ni kuhusu kuwasadia vijana na hasa wanaohitimu elimu ya juu.

  "Kuna idadi kubwa ya vijana ambao wanahitimu elimu ya juu na changamoto yao kubwa ni ajira.Hivyo namatamani kumwambia umuhimu wa kukutana na vijana na kisha kwa pamoja tujadiliane namna ya kutatua changamoto hiyo,"amesma Mbaga.

  Pia Mwanadad huyo ambaye amekuwa akijihusisha na kuhamasisha makundi ya rika mbalimbali yakiwamo ya vijana amesema anaamini kuthubutu ni jambo muhimu na hata yeye amefika hapo kwasababu ya kuthubutu na kutoa mchango wake kwa ajili ya nchi yake na nchi nyingine mbalimbali duniani.

  Ametoa rai kwa vijana wa Tanzania kuhakikisha wanashiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kufafanua baada ya kumaliza chuo mwaka 2010 alikaa nyumbani kwa miaka mitatu na baadae aliamua kuanza kufanya kazi za kujitolea na sasa amekuwa mfano wa kuigwa na vijana wengine

  Alipolizwa amewafikia watu wangapi hadi sasa katika kuhamasisha kushiriki kufanya maendeleo na amesema amekutana na maelfu ya watu wakiwamo vijana wa Tanzania na mataifa mengine duniani.

  Akiwa uwanjani hapo akijiandaa kusafiri kwenda Uingereza Mbaga amesema anakwenda katika nchi hiyo kwa ajili ya kupata tuzo maalumu ya kutambua mchango wake na yumo kwenye kundi la wanawake 100 duniani ambao wameonekana kuwa na mcahngo mkubwa wa kuhamasisha maendeleo.

  Akizungumzia baadhi ya tuzo ambazo amezipata amesema mwaka 2017 alipata tuzo ya "African youth empowerment" chini ya Africa Youth Awards .Amefafanua kwa sasa ni Rais wa World Merit Tanzania chini ya Shirika la World Merit lililopo Uiengereza.

  Amesema shirika hilo limejikita katika kuhamasisha Maendeleo endelevu na kfafanua mwaka 2016 alipata nafasi ya kuhudhuri moja ya program za shirika hilo iliyokuwa inaitwa Merit360."Kupitia programu hiyo niliweze kuhamasisha umuhimu wa mazingira Umoja wa Mataifa na kushinda "Sustainable development goals challenge competition" .

  "Na nilifanikiwa kuwafikia watu zaidi ya 1000 kujua umuhimu wa mazingira nchini Tanzania,"amesema Mbaga.Pia amesema safari yake kwenye masuala ya maendeleo ilianza kwa kujitolea kupitia mashirika mbalimbali kwa miaka mitatu.
  "Baadhi ya tuzo nyingine niliyoipata ni ya "Woman of Influence in events hall of fame chini ya Association for women in event ya Marekani 2017.

  "Na mwaka huu nchini Uingereza nimeweza kutambulika kuwa miongoni mwa wanawake 100 wanaosaidia kuwainua wengine Kwenye Kazi za kijamii Kama STAR AWARD,"amesema Mbaga.

  0 0


  Meneja wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Devis Kisamo katikati pichani akikabidhi mfano wa Hundi kwa washidi shindano la mawakala wa TIGO PESA nyanda za juu kusini kwenye hafla iliyofanyika mjini Iringa mwishoni mwa wiki.

    Heriy Ngesi kutoka kyela Mbeya  Mshindi wa shindano la mawakala la uwekaji miamara kwa wingi ndani ya mwezi mmoja kutoka kampuni ya Tigo Tanzania alkiibuka mshi wa Ml.1  

  Meneja wa Tigo kanda za nyanda za juu kusini, Davis Kisamo (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi kwa Abeid Bathromeo  wa Ilula Iringa Mshindi wa shindano la mawakala la uwekaji miamala kwa wingi ndani ya mwezi mmoja kwenye huduma ya Tigopesa aliyeshinda zawadi ya shilingi milioni 2 mwishoni mwa wiki iliyopita.

  0 0

  MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akitoa nasaha zake kwa viongozi na wafanyakazi wa ARU wakati wa semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuazuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda) 
  Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa ARU wakishiriki semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. 
  Mmoja wa watoa mada kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kinondoni Elly Makalla akiwasilisha hoja kwa viongozi na wafanyakazi wa ARU walioshiriki semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na taasisi hiyo chuoni hapo Juni 21 2018. 
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuwaelezea umuhimu wa mafunzo ya kupambana na kuzuia Rushwa chuoni hapo. 
  Sehemu ya viongozi pia wafanyakazi wa ARU wakifuatilia mada kwenye semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. 
  Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa ARU wakishiriki semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. 
  Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa ARU wakifuatilia mada kwenye semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. 
  Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa ARU wakifuatilia mada kwenye semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. 


  0 0

  Na Abel Daud,KIGOMA,

  MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga amewataka Mahakimu wa Mkoa wa Kigoma kufanya kazi kwa Weredi pamoja na kutoa haki kikamilifu bila upendeleo ili kudumisha uaminifu kwa vyombo vya maamuzi.

  Mkuu huyo wa Mkoa amesema vyombo vya ulinzi na usalama nguvu yake kubwa vinategemea maamuzi kutoka kwa mahakama,nakuongeza kuwa nchi nyingi zilizo katika machafuko sehemu kubwa ni ukosefu was haki,pamoja na kutoa angalizo kuwa haki isipotolewa kikamilifu wananchi wanaweza kuchoka na kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi.

  Hayo ameyasema hii leo alipokuwa akifungua semina ya mafunzo ya siku moja kwa mahakimu wote was mkoa wa kigoma kuanzia ngazi ya mahakama ya mwanzo mpaka mahaka ya hakimu mkazi na waendesha mashtaka pamoja na magereza.

  MKURUGENZI msaidizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze amesema kuanzishwa kwa sheria hii kumepunguza mrundikano wa wafungwa katika magereza na kuongeza pato la Taifa kupitia shughuli zinazofanywa na wafungwa wenye vifungo vya nje katika taasisi za serikali ambazo zingetumia kuajili raia wengine.

  Amesema hadi sasa zaidi ya wafungwa elfu kumi na sita (16) wametumikia na wanaendelea kutumikia kifungo hicho cha nje,ikitajwa kuwa wafungwa wenye vifungo vifupi kuacha kuchangamana na wafungwa wenye makosa sugu,hiyo itasaidia kupunguza uhalifu kwani pindi wawapo pamoja hujifunza tabia za waharifu hao sugu taratibu.

  Naye Afisa Ustawi wa Jamii Manspaa ya Kigoma Ujiji Agnes Punjila amesema kuwa pamoja na sheria hii kuwa nzuri ila bado kuna changamoto kubwa hasa kwa jamii kuona kuwa sheria hiyo ni yakuwabeba baadhi ya watu na kuomba taasisi zote zinazohusika katika sheria hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii hasa kupitia vyombo vya habari.
  MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga  akizungumza mbele ya Washiriki wa mafunzo hayo
  Washiriki wa mafunzo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini.
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wa tatu kulia akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo

  0 0

  Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa shirika la mawasiliano Tanzania TTCL ,Juvenal Utafu amewataka washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2018 ngazi ya mkoa wa Mbeya (Dream Miss Mbeya 2018), kuhakikisha wanatumia urembo wao kama nguzo ya kuzifikia ndoto zao.

  Meneja huyo amebainisha hayo baada ya Walimwende hao waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora ya mashindano hayo, kutembelea afisi za shirika hilo kanda ya nyanda za juu kusini kwa lengo la kutambua mambo mbalimbali yanayo husu TTCL, ikiwa ni pamoja na namna ya uhifadhi wa taarifa za watumiaji wa huduma za mawasiliano. 

  Utafu amesema kwamba Ulimbwende ni moja ya njia za kuonesha mchango katika jamii, lakini hilo litafanikiwa ikiwa walimbwende hao watajitambua na kusimama vema katika nafasi zao. “Ni lazima mtambue ya kwamba mna deni kubwa kwa taifa, la kutoa mchango chanya katika nyanja mbalimbali, hasa katika hali ya sasa ya dunia ya utandawazi na mapinduzi ya sekta ya mawasiliano”, aliongeza Utafu. 

  Kwa upande wake Meneja msaidizi biashara wa TTCL mkoa wa Mbeya Charles Mwita, alisema kuwa amefarijika sana kwa kauli mbiu ya mashindano hayo isemayo “urembo na kazi kwa maendeleo ya jamii”, na kuwapa changamoto walimbwende hao kwamba hawana budi kuitekeleza kauli mbiu hiyo kwa vitendo. 

  Juni 29 mwaka huu ni fainali za mashindano ya Dream Miss Mbeya 2018 yenye lengo la kumpata mlimbwende atakayevikwa taji la Mrembo wa mkoa wa Mbeya (Miss Mbeya 2018). Aidha mshindi huyo wa kwanza ataungana na washindi wengine akiwemo mshindni wa Pili na tatu kuuwakilisha mkoa wa Mbeya katika mashindano ya ngazi ya kanda yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao, kuwatafuta wawakilishi wa kanda ya nyanda za juu kusini katika mashindano ya urembo ngazi ya taifa. 

  Mashindano ya Dream Miss Mbeya 2018 yameandaliwa na redio Dream FM ya jijini Mbeya kwa udhamini wa TTCL Corporation, PII Limited, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Ally Rich Sanaa Arts Limited, Kalulu Safari’s Tours Co. Limited, Pepsi, Paradise Inn Hotel, Michuzi Blog, Michuzi Tv, na Dorcus Beauty Point.
  Afisa huduma kwa wateja wa TTCL Corporation Bi Niva Mkwe akiwaelezea washiriki wa Dream Miss Mbeya 2018 huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo.

  Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa TTCL Corporation Juvenal Utafu akizungumza na washirki wa Dream Miss Mbeya 2018 walipomtembelea ofisini kwake Jijini MbeyaMeneja msaidizi-biashara wa TTCL Corporation Mkoa wa Mbeya Charles Mwita akiwaelezea washiriki wa Dream Miss Mbeya 2018 huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo


  0 0  Video
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga. 

  Na Hamza Temba-WMU-Chemba, Dodoma
  .......................................................................................

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wananchi waliovamia Pori la Akiba Swagaswaga na kuendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, makazi na ufugaji ndani ya pori hilo kinyume cha Sheria waondoke mara moja kwa hiari yao kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

  Ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Handa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua mgogoro wa ardhi kwenye hifadhi hiyo wilayani humo.


  "Tunawapa siku 30 muanze kutoka wenyewe, baada ya siku 30 tunatoa notisi ya siku nyingine 30 za kutumia nguvu, kwahiyo kuanzia sasa hivi anzeni kujipanga wenyewe na kuondoka wakati Halmashauri ikifanya tathmini ya maeneo ya vijiji ambavyo ni halali ya kuwagawia kwa wale watakaopenda kupewa maeneo huko", alisisitiza Dk. Kigwangalla.


  Alisema sheria za uhifadhi haziruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya maeneo ya hifadhi na kuendesha shughuli za kibinadamu na kwamba kufanya hivyo ni kudharau Sheria na Malmlaka zilizopo.


  Alisema kwa upande wa wananchi wa kijiji cha Handa ambacho kilianzishwa kimakosa ndani ya pori hilo wataendelea kubaki mpaka pale wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Tamisemi na Ardhi zitakapoamua hatma yao ikiwemo ama kulipwa fidia kupisha eneo hilo au waendelee kubaki na mipaka ya hifadhi isogezwe.


  Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kujenga miundombinu ya kuvuta maji kutoka katika chemchem iliyopo ndani ya hifadhi hiyo na kuyasogeza kwenye makazi ya wananchi ili kulinda chanzo hicho kwa kuzuia uharibifu unaofanywa na wananchi wanaofuata huduma katika eneo hilo.


  Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga alisema atasimamia ipasavyo maagizo yaliyotolewa na Dk. Kigwangalla na kwamba endapo wanavamizi hao walioingia ndani ya pori hilo kinyume cha sheria watakaidi agizo hilo atatoa notisi ya siku 30 na hatimaye kuwaondoa kwa nguvu ili kupisha eneo hilo liendelee kuhifadhiwa.


  Kwa upande wake mbunge wa Chemba, Juma Nkamia alimshukuru Dk. Kigwangalla kwa kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo na kuwataka wananchi kutii sheria na kuepuka kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa kisheria ili kuepuka usumbufu na mamlaka zinazosimamia eneo hilo.


  Viongozi wengine walioongozana na Dk. Kigwangalla katika utatuzi wa mgogoro huo ni Mbunge wa Hanan'g, Dk. Marry Nagu, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka, na viongozi wengine wa Chama na Serikali wa wilaya za Chemba na Mkalama.


  Kijiji cha Handa kilisajiliwa tarehe 16 Agosti, 2004 kikiwa na ukubwa kilomita za mraba 72.23 na vitongoji vitano, vinne kati yake vikiwa ndani ya Pori la Akiba Swagaswaga. Vitongoji hivyo ambavyo ni Ilala A, Ilala B, Mbugani na Mnang'ana vina ukubwa wa kilomita za mraba 7.85 na kaya 1,169 zenye watu zaidi  ya 5,291.


  Pori la Akiba Swagaswaga lilianzishwa kwa Tangazo la Serikali namba 72 la tarehe 21 Februari, 1997 likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 871. Pori hilo lipo katika wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma na wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.
  Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga akizungumza katika mkutano huo.
  Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia akizungumza katika mkutano huo katika kijiji cha Handa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana.
  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga. 
  Mbunge wa Hanan'g, Dk. Marry Nagu akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Chemba na Mkalama wakikagua mpaka wa Pori la Akiba Swagaswaga ambalo lina mgogoro na kijiji cha Handa alipotembelea eneo hilo jana katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kwa ajili ya kutatua mgogoro huo. 
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia, Mbunge wa Hanang, Dk. Marry Nagu, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka, na viongozi wengine wa wilaya ya Chemba na Mkalama wakiangalia ramani ya mpaka Pori wa Pori la Akiba Swagaswaga alipotembelea eneo hilo jana kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi na vijiji.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Chemba na Mkalama wakikagua mpaka wa Pori la Akiba Swagaswaga ambalo lina mgogoro na kijiji cha Handa alipotembelea eneo hilo jana katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kwa ajili ya kutatua mgogoro huo. 
    Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga. 
   Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.

  0 0

  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

  WAKAZI wa Rufiji mkoani Pwani wametakiwa kulinda miradi inayojengwa ili kupata wataalam wengi watakaoisaidia Serikali.

  Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana baada ya kukagua majengo ya kisasa yaliyojengwa Kijiji cha Dohatul Khayr kupitia Taasisi ya Alat'a Chartable Foundation Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema mradi huo utasaidia kupata wataalamu mbalimbali.

  "Mradi huu ni mkubwa kwa wilaya ya Rufiji utasaidia kupata wataalamu na wengi watakaoisaidia Serikali kwenye kazi mbalimbali za kimaendeleo," amesema Ulega.Ameongeza kuwa Wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti ziko nyuma kimaendeleo hivyo miradi inayoanzishwa itawawezesha kuhimiza maendeleo na kuzalisha wataalamu.

  Mfadhili wa mradi huo kutoka Qata Nusser Al Khal amesema miradi huo ni miradi kwanza kwa Tanzania kujengwa kwa ufadhili ambapo umehusisha nyumba 32,kituo cha afya na msikiti.

  "Miradi huu wa kwanza umegarimu Sh.bilioni 1.3 ambapo umehusisha nyumba ya ibada,hospital na nyumba 32 ambapo miradi utakaofuata utajenga majengo ya taaluma," amesema All Khal.

  Kwa upande wa Shekh wa Wilaya ya Rufiji Othmani Kaporwa amesema kujengwa kwa miradi hiyo itawasaidi wakazi wa maeneo hayo.Wafadhili hao pia wanajenga mradi mkubwa katika jimbo la Mkuranga ambapo itakuwa na nyumba zaidi ya 30, shule ya msingi, sekondari na chuo cha ufundi.
  Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Rufiji kwa niaba ya Waziri Mkuu katika hafla ya ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (alievaa koti) kwa niaba ya Waziri Mkuu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.
  Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega akikagua bweni la kulala watoto yatima na wanaoIshi katika mazingira magumU kwa niaba ya Waziri Mkuu katika ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wa pili kulia alievaa koti akiwa pamoja na waumini wengine katika ibada ya Ijumaa katika msikiti uliopo ndani ya kijiji hicho.
  Muomekano wa wa majengo pamoja yaliyopo katika kijiji cha Dohatl Khayr.
  Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega akiwa ameambatana na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa kukagua majengo yaliyo jengwa katika kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.

  0 0

  Sami Hyypia veterani wa timu ya Liverpool ambaye yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered amesema kuwa mwanasoka wa mafanikio kunahitaji kazi ngumu na kujituma.

  Alisema tangu utoto wake amekuwa akijituma na anaamini katika kujituma katika shughuli zinazokuinua.

  Alisema hayo katika hafla ya kukabidhiana vifaa kwa timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kufanyika jumamosi wiki hii, iliofanyika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.

  Alisema kwamba kuwa juu katika soko kunatokana na mambo mawili makubwa ambayo ni kujituma na kuwa na kipaji.

  Alisema hata ukiwa na kipaji ukibweteka katika mazoezi na kujituma katika kuhakikisha uko fiti katika maisha ya mwanasoka huwezi kufikia ngazi za juu za uchezaji wenye kuheshimika.

  Alisema pamoja na kuja kuangalia michuano hiyo amepata nafasi ya kuzungumza haja ya kukua katika soka kwa kutengeneza nidhamu inayotakiwa ya kujituma, kufanya mazoezi na kutumia kipaji katika kuimarisha usakataji soka.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akizungumza kwenye hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kulia).
   Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na timu (hazipo pichani) zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ gwiji huyo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
   Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kushoto) na Meneja Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered nchini, Mariam Sezinga wakipitia ratiba ya hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani).
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia wakikabidhi vifaa vya michezo kwa Afisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Mubaraka Kibarabara (katikati) ambapo Airtel ni moja kati ya washiriki 32 wa mashindano ya ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya washiriki kutoka kampuni mbalimbali wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (hayupo pichani) wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaa. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.
   Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani).
   Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisaini ‘Autograph’ kwa baadhi ya timu zitakazoshiriki mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
  Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisalimiana na baadhi ya timu kutoka makampuni mbalimbali zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.  0 0

   Askari wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakitoa heshima wakati wa Gwaride lao la kumaliza mafunzo ya wali ya kijeshi yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha
   Askari wakionesha moja ya maonyesho ya ukakamavu wakati wa kufunga mafunzo yao ya awali ya kijeshi yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha
   Askari hao wakionyesha sehemu ya mazoezi ya ukakamavu wakati wa Gwaride la kumaliza mafunzo yao ya awali yaliyokuwa yakifanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha 
   Askari wapya wakionyesha sarakasi wakati wa gwaride la kufunga mafunzo yao yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha 
  Mkuu wa mafunzo na utendaji wa kivita Jeshini Meja Jenerali Alfredy Kapinga akikagua Gwaride la askari 2,081 la askari wapya wa JWTZ waliomaliza mafunzo yao Shule ya Mafunzo ya awali ya Kijeshi Kihangaiko (RTS), iliyoko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo mafunzo hayo yalikuwa yakitolewa Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha.

  Na Ripota Wetu, Arusha 

   MKUU wa Mafunzo na Utendaji wa kivita wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali Alfredy Kapinga amewataka askari wapya 2,081 kuhakikisha wanakuwa na utii, uaminifu na uhodari kwani huo ndio msingi wa jeshi. 

   Hayo aliyasema mjini Arusha wakati wa kufunga mafunzo ya kundi la 38 B la mwaka 2017 lenye askari wapatao 2,081 waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya kijeshi katika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha ambapo mafunzo hayo yalifungwa Juni 22, mwaka huu. 

   Akizungumza kwenye sherehe hizo Meja Jenerali Kapinga amewataka vijana hao kutambua tayari wameiva kuwa askari na hivyo wapo tayari kutumika mahali popote na masuala ya longolongo kwa sasa hayapo tena.  “Jukumu kubwa mbele yenu ni kulinda nchi dhidi ya maadui wan je na ndani, kulinda mipaka na shughuli za kijamii mtakazokuwa mmepangiwa endapo mtahitajika,” amesema Meja Jenerali Kapinga. 

  Katika hotuba yake hiyo amewataka pia wazazi nchini kuwaacha vijana hao wafanye kazi ya jeshi kwani wamekabidhiwa dhamana kubwa kwa taifa hivyo kitendo cha kuendelea kuwachukulia kama watoto si sahihi.  “Hawa tayari ni askari, tumewapokea tutawatunza na kuwafundisha maadili mema kwa taifa, ile mbereko ya kuwabeba sasa mziache hawa ni askari,” amesema Meja Jenerali Kapinga. 

  Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi Kihangaiko (RTS), iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani Kanali Sijaona Myala akizungumza kwenye sherehe hizo aliwataka wazazi kuacha kusikitika pindi watoto wao wanapopangwa kwenda nje ya nchi. 

  Naye Mkuu wa Kikosi cha 883 KJ Oljoro Luteni Kanal i Christopher Kavalambi alisema miongoni mwa wahitmu hao wamo pia wanariadhara 10 na wanamichezo mingine ya mpira wa pete na ngumi. Amewataja baadhi ya wanartiadhara waliomaliza mafunzo hayo ya awali ya kijeshi ni pamoja na Alphonce Simbu na Emmanuel Giniki. 

  Sherehe hizo za kuhitimu mafunzo zilishereheshwa na kwa gwaride la kuhitimu mafunzo na maonyesho ya vikundi mbalimbali yaliyoandaliwa na kuruta waliohitimu mafunzo yao na kuwa askari.


  0 0

  Na Heri Shaaban 
  MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imezifungia maabara bubu na maduka ya dawa yasio na sifa ambayo yanatoa huduma kinyume cha sheria. Oparesheni ya kuzifungia maabara hizo pamoja na maduka ya dawa imeanza Dar es Salaam jana katika Jimbo la Segerea, Ukonga na Ilala.

  Akizungumza jana kuhusu operesheni hiyo Mratibu wa Vituo Binafsi Manispaa ya Ilala Dk.Wille Sangu amesema maduka ya dawa ambayo wanayafungia ni ambayo wahudumu wake hawana sifa za kuendesha huduma hiyo na wengine wanatoa huduma za kuwachoma sindano wateja tofauti na kibali chao.

  "Ofisi ya Mganga Mkuu Ilala imeweka utaratibu wake kila mwaka kufanya ziara ya ukaguzi wa kuzikagua maabara bubu ambazo hazina vibali na duka za dawa mara baaada kuwakamata kuwataka wafuate taratibu za usajili ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Ilala,"amesema Dk.Sangu.Amefafanua katika oparesheni hiyo pia wameyanga maduka ya dawa waliyoyakuta watoa huduma hawana sifa na maduka mengine yakijiusisha na upimaji VVV, utoaji mimba na uchomaji sindano.

  Amewataka watoa huduma wote ambao wamekamatwa kwenda ofisi za Manispaa ya Ilala kwa ajili ya taratibu .Dk.Sangu amewataka wananchi watumie vituo vya tiba kwa ajili ya matibabu ya maabara kwa ajili ya vipimo na maduka ya dawa kwa ajili ya kununua dawa."Ukikuta duka la dawa linatoa tiba au huduma za maabara ni hatari kwa afya yako na toa taarifa kwetu,"amesisitiza.

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dk. Emily Lihawa amewataka wamiliki wa vituo vya kutolea huduma katika wilaya hiyo, wafuate miongozo yote ya hutoaji huduma ya afya. Pia amewataka wamiliki watoe huduma kulingana na vibali vyao wasikiuke kanuni,kikubwa wafuate miongozo ya kukinga na kuthibiti maambukizi wakati wa utoaji huduma za afya. Katika ziara hiyo ilifungia maabara bubu na Zahanati Kiwalani, Tabata, Kivule na Minazi Mirefu.

   Mratibu wa vituo Binafsi MANISPAA ILALA ,DKT Wile Sangu akifungia Mahabara Bubu na vituo  bubu Kijiwe Sam ri Kiwalani kwa kosa la kutoa huduma bila kibali, katika oparesheni endelevu ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam jana (PICHA NA HERI SHAABAN)

  0 0  Viongozi wa kampuni ya Minet wakizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa kufanya mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
  Baadhi ya viongozi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya bima na mafao ya MINET wakisalimiana na baadhi wageni waalikwa waliofika kushuhudia mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
  Baadhi ya viongozi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya bima na mafao ya MINET wakisalimiana na baadhi wageni waalikwa waliofika kushuhudia mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
  Baadhi ya viongozi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya bima na mafao ya MINET wakisalimiana na baadhi wageni waalikwa waliofika kushuhudia mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
  Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET wakifuatilia tukio hilo ambalo limefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
  Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET wakifuatilia tukio hilo ambalo limefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

  Mwanamuziki maarufu barani Afrika Vyone Chaka Chaka akisakata rumba na baadhi ya wageni waalikwa kwenye tukio la uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET.
   
   
  KAMPUNI ya Aon kupitia Minet imezindua rasmi JH Minet Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa safari iliyoanza 1998 ikiwa inatoa huduma za bima pamoja na mafao.

  Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Minet Group Joe Onsando amesema kuwa kampuni hiyo mpya itakuwa chini Aon na hakuna kazi itakayopotezwa baada ya mabadiliko hayo.

  Amesema  kuwa Minet  ni kampuni inayoaminika  kote Afrika na nje ya bara hilo na wafanyakazi wa Aon ambayo sasa itajukulikana Minet katika nchi hizo na viongozi wao ambao wana ujuzi katika masuala ya viwanda wataendelea kuwa nafasi kama watendaji katika utoaji wa huduma.Onsando ameeleza kuwa mwaka 1997  kampuni hiyo ya  JH Minet ilibadilishwa na kuwa Aon Minet na wanaendelea kujenga uchumi imara Afrika na itaendelea kuwa sehemu ya Aon katika utendaji kazi wao.

  Onsando amefafanua kuwa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo hazitabadilika katika sekta zote kama vile kilimo, madini na mawasiliano.Pia amesema wanafurahishwa na namna uwekezaji unavyoendelea na kukua barani Afrika na wataendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao kwa sasa na baadaye.

  Naye Mkurugenzi wa JH Minet Tanzania Raju Dave ameeleza kuwa Tanzania kama sehemu nzuri ya biashara imeendelea kukua kiuchumi Mashariki mwa Afrika ukilinganisha na miaka ya nyuma.Na amehaidi kuendeleza ukuaji wa uchumi kupitia gunduzi mbalimbali katika sekta mbalimbali na amehaidi huduma bora kwa wateja.

  Kwa mujibu wa uongozi wa kampuni hiyo umesema kuwa uzinduzi wa jina hilo la Minet ni awamu ya pili ya muendelezo wa kufanya mabadiliko hayo ambapo tayari nchi nyingine kadhaa barani Afrika wameshabidili jina.Pia uongozi umesema unafurahishwa na namna ambavyo Serikali ya Tanzania inavyojikita katika kuimarisha uchumi.

  Wamesema mwenendo wa hali ya nchini nchini Tanzania inafurahishwa na inavutia kwa kampuni nyingine ikiwemo ya kwao kuwekeza nchini katika masuala yanayohusu shughuli za bima na mafao.Kwa upande wake mwanamuziki maarufu barani Afrika Vyone Chaka Chaka amesema utulivu uliopo katika bara la Afrika unatosha kuwafanya waafrika kupiga hatua zaidi za kimaendeleo.
   

  0 0

  Na Mariam Mwayela,Njombe

  Watendaji wa Halmashauri pamoja na wafanyabiashara wadogo wa Mkoa wa Njombe wameelimishwa juu ya urasimishaji wa wafanyabiashara hao ili waweze kutambulika rasmi na kuchangia pato la taifa ikiwa ni katika muendelezo wa Kampeni ya utoaji wa Huduma, Elimu na usajili wa walipakodi wapya.

  Akizungumza wakati wa semina kwa watendaji na wafanyabiashara hao wilayani Njombe na Makambako, Mkuu wa Wilaya ya hiyo Bi. Ruth Msafiri amewataka wafanyabiashara hao kuchangia mapato ya Serikali kwa kulipa kiasi cha kodi watakachopangiwa ili kuweza kusaidia kuboresha miundombinu pamoja na huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo shule, huduma za afya, maji safi na salama, umeme pamoja na barabara.

  “Tukumbuke kuwa, kila kitu tunachokifanya kinahitaji fedha kwa mfano kuwa na miundombinu na wataalam wa kutoa huduma za afya ni gharama, kuwa na shule pamoja na sehemu safi za kufanyia biashara ni gharama pia. Hivyo basi, kila mmoja achangie kwa kulipa kodi ili kuweza kuendeleza huduma hizi muhimu”. Alisema Ruth.

  Aliongeza kuwa, katika kutafuta maendeleo kitu kikubwa ambacho kila mwananchi anatakiwa kuwa nacho ni uzalendo, utayari na kuelewa kwamba kila mmoja ana mchango wake katika maendeleo husika.

  Aidha alisisitiza kwamba, lengo la semina hiyo ni kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Mkoa wa Njombe wanapokea na kutekeleza maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwarasimisha rasmi ambapo hadi sasa Wilaya ya Njombe imekwisha orodhesha jumla ya wafanyabiashara 589 na wengine wanaendelea kujiorodhesha ili baadaye waweze kupatiwa vitambulisho maalum vya wafanyabishara wadogo.

  Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo, aliwataka wafanyabiashara hao kutoa ushirikiano kwa watendaji wa Halmashauri ili waweze kuwatambua na kurahisisha zoezi zima la usajili pindi litakapofika mkoani Njombe.

  “Tumefanya zoezi la utambuzi wa wafanyabiashara wadogo wadogo katika Mkoa wa Mwanza, Arusha na Morogoro hivyo ni matumaini yangu kuwa wafanyabiashara wa Njombe mtaitikia zoezi hili kwa kiasi kikubwa pindi tutakapofika mkoani hapa”. Alisema Kayombo.

  Kayombo aliongeza kuwa, huduma mbalimbali za kijamii kama shule, hospitali pamoja na miundombinu zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na walipakodi wakubwa na walipakodi wa nchi rafiki wa Tanzania hivyo basi imefika wakati kwa wafanyabiashara wadogo kuchangia kiasi kidogo wanachikipata ili kusaidia maendeleo ya nchi.

  “Wananchi wengi wamekuwa wakiamini barabara zetu zinatengenezwa kwa misaada ya wahisani, jambo hili siyo kweli isipokuwa Serikali imekuwa ikipokea mikopo yenye masharti nafuu ambayo kodi za wananchi ndizo zimekuwa zinalipa madeni hayo” aliongeza Kayombo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao, Sifael Msigalla aliishukuru TRA kwa kuhakikisha inafikisha elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo ambayo itasaidia wafanyabiashara hao kuweza kwenda sawa na malengo ya Taifa katika kukuza Uchumi wa Viwanda.

  “Elimu waliyoipata leo itasaidia sana wafanyabiashara hawa kulipa kodi na hivyo kupelekea kufanya biashara zao huku wakiwa na uelewa wa kutosha kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi,” alisema Msigalla.

  Jumla ya wafanyabiashara wadogo 200 wamehudhuria semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ambapo Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri alikuwa Mgeni Rasmi.

  0 0

   
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick Mpogoro akizungumza  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
   Wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa Wakiimba nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmi kuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
  Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) Bi Theresia Mtewele akiongoza meza kuu kuimba nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmi kuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
  Viongozi na wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa wakiburudika kwa pamoja kwa nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmikuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mwl Raymond Mwangwala akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapindui Mkoa wa Iringa Ndg.Albert Chalamila akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo 
  Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg.Rodrick Mpogolo akimkabidhi cheti cha pongezi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg.Kenani kiongosi katika sherehe ya Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
   Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg.Rodrick Mpogolo akitoa vyeti kwa wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogolo akipokea baadhi ya bendera na jezi za chadema wakati akimkaribisha ndg Godfrey Maiko aliojiunga rasmi na CCM Leo  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogolo akimvisha kofia ya CCM ndg Godfrey Maiko aliojiunga rasmi na CCM Leo  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akipeana Mkono na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogoro akifurahi pamoja na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogoro akizungumza  mara baada ya kumpokea Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo kulia ni Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl Raymond mwangwala.
  PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI CCM BLOG

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza mifumo ya utoaji huduma Serikali kwa njia ya mitandao isitumike kukwamisha shughuli za Serikali au mipango ya utoaji huduma kwa wananchi.

  Amesema watakaobainika kuhujumu mifumo hiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu na amesisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitawavumilia watumishi wasio waadilifu.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 23, 2018) mara baada ya kuzindua mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma.

  Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 iliyotolewa na Umoja wa Afrika (AU) ni “Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Malengo ya Maendeleo Endelevu”.

  Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watumishi wa Umma wote nchini, wananchi, Sekta Binafsi, Sekta ya Umma, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa na Wadau mbalimbali, kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa.

  “Hii ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika (AU) na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ambayo yamehimizwa na Kaulimbiu ya mwaka huu,”.

  Pia Waziri Mkuu amewaagiza Watendaji Wakuu wa Taasisi zinazosimamia mifumo hiyo pamoja na maafisa waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi kupitia mifumo hiyo, wahakikisha wanailinda na kuitumia vema ili iweze kuwa na tija na manufaa yaliyokusudiwa.

  Mifumo hiyo aliyoizundua inahusu utoaji Huduma Serikalini ambayo ni Mfumo wa Usajili wa Vizazi na Vifo, Mfumo wa Taarifa za Kitabibu, Mfumo wa Taarifa za Ununuzi, Mfumo wa Kumbukumbu za Kielektroniki na Mfumo wa Ofisi Mtandao.

  Mingine ni Mfumo wa Ankara Pepe na Ulipaji wa Serikali, Mfumo wa Utoaji Huduma za Serikali Kupitia Simu za Mikononi, Mfumo wa Barua Pepe wa Serikali na Mfumo wa Vibali vya Kusafiri.Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali la kutumia mifumo ya TEHAMA ni kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za Serikali za kila siku.

  “Hivyo basi, mtakubaliana nami kuwa, Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza mifumo ya TEHAMA ili kutekeleza kwa vitendo azma ya kuwapatia wananchi hususani wa vijijini huduma bora na kwa wakati,” amesema.

  Kwa upande wa wananchi,Waziri Mkuu amewataka waendelee kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imejipambanua kwa vitendo pamoja na kuwa na dhamira ya dhati ya kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

  Uzinduzi huo umehudhuliwa na waziri wa nchi, ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Bw. George Mkuchika, waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage, naibu waziri Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, na naibu waziri wa nchi OR-TAMISEMI Josephat Kakunda, wabunge, muwakilishi wa benki ya dunia, makatibu wakuu, watendaji na viongozi wa taasisi za umma.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 - DODOMA.
  JUMAMOSI, Juni 23, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kwenye uzinduzi wa mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
  Katibu Muhtasi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Kholuu Ramadhan, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Johari Swalehe kwa niaba ya mwanae Seif Ramadhan, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Cuthbert Simalenga, wakati akikagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Shukran George kwa niaba ya mwanae Magreth Msomba, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.

  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  WAFANYAKAZI wa ZFDA wakiteremsha Maziwa yalioharibika kwenye gari kwa ajili ya kuyaangamiza katika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
  KAIMU Mkurugenzi ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungumzia zoezi la Uteketazaji wa Maziwa tani 20 yalioharibika katika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
  GARI aina ya Katapila likisaga maziwa yalioharibika na yasiyofaa kwa matumizi ya Binaadamu katika zoezi lililofanyika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Abdalla Omar Maelezo Zanzibar


  Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 23.6.2018

  Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) imewakumbusha Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za Chakula kutoka nje kuhakikisha wanafuata miongozo, sheria na kanuni za usafirishaji ili kuhakikisha bidhaa zao zinafika nchini zikiwa salama kwa matumizi ya wananchi.

  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti wa Chakula na Dawa Dkt. Khamis Ali Omar alisema hayo katika Jaa la Kibele kwenye zoezi la kuteketeza maziwa yaliyoharibika kwa kusafirishwa kwenye kontena moja na mizigo mengine ikiwemo gari kutoka Dubai.

  Alisema baadhi ya maboksi ya maziwa yalipasuka kutokana na msukosuka wa meli baharini na kuharibu maboksi mengine yaliyopelekea maziwa yote yakose sifa ya matumizi ya binadamu.Aliwashauri wafanyabiashara kuheshimu chakula na kukiepusha na viashiria vyote hatari wakati wa kuvisafirisha na kwenye maghala ili kuwaepusha wananchi na athari zinazotokana na chakula kibovu .

  Maziwa hayo yenye uzito wa tani 20 yaliingizwa na mfanyabiashara Essak Suleiman wa Darajani tarehe 6 mwezi huu yakiwa yameshaharibika na kuamua kuyazuia yasiingie sokoni.Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa athari zitokanazo na chakula wa ZFDA Asha Suleiman amewashauri wananchi wanapopewa sadaka ya chakula kuwa waangalifu kwani wamegundua baadhi ya wafanyabiashara hutoa sadaka zilizokwisha haribika baada ya kukosa soko.

  Aidha amewashauri wananchi wanapokuwa na shaka ya chakula na kuhisi kinadalili ya kuharibika kutoa taarifa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodi ili kwenda kukiangalia na kupata uhakika wake kabala ya kuanza kukitumia.Wakati huo Mfanyabiashara Essak Suleiman alieingiza maziwa hayo alisema sababu iliyopelekea mzigo huo kuharibika ni upakiaji mbaya uliofanywa na wenye meli, joto kali na kuchelewa kuondoka meli Dubai kuja Zanzibar.

older | 1 | .... | 1604 | 1605 | (Page 1606) | 1607 | 1608 | .... | 1897 | newer