Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

TATU MZUKA YAZINDUA ‘SUPA MZUKA CUP’ YA MILIONI 300

$
0
0

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka,Sebastian Maganga, akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,wakati wakizindua ushirikiano na VODACOM, ambapo wateja wa MPESA wataweza kushinda dakika za bure, intaneti na bidhaa mbalimbali kwa kipindi chote cha kampeni pichani kulia ni Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana,mbali ya kushirikiana huko
Tatu Mzuka wamezindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka,Sebastian MagangaTatu Mzuka pamoja na Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana wakionesha kombe wakati wa wakizindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka,Sebastian MagangaTatu Mzuka pamoja na Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana wakionesha jezi maridhawa wakati wa wakizindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.

• Pia yazindua ushirikiano na VODACOM ambapo wateja wa MPESA wataweza kushinda dakika za bure, intaneti na bidhaa mbalimbali kwa kipindi chote cha kampeni.

14th June 2018

Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini Tanzania leo umezindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.

Wachezaji wote wa Tatu Mzuka kuanzia leo mpaka fainali, wataweza kuingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda milioni 300 ambapo kwa kila shilingi 500 unayocheza inakupa tiketi ya kushiriki droo siku ya fainali.

‘Mpaka sasa hii ndiyo kampeni inayosisimua zaidi kwa sababu hakuna ushindi mkubwa namna hii wa jackpot ambao ulishawahi kutolewa nchini Tanzania’ alisema Bwana Sebastian Maganga, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka

Kwa kuwa huu ni msimu wa kucheza na kushinda na marafiki, Tatu Mzuka kupitia droo ya Mzuka Deile wanatotoa fursa kwa mshindi kuchagua marafiki wanne ambapo kila mmoja atapewa 500,000 katika ushindi wa milioni 10 zinazotolewa kila siku.

Katika droo ya Jumapili, marafiki 5 kila mmoja atapata milioni 1 kutoka katika ushindi wa jackpot ya kila Jumapili. Siku ya fainali, mshindi wa milioni 300 atatoa milioni 1 kwa marafiki zake kumi ili kukamilisha timu ya ushindi ya watu 11.

Ili kushiriki kwenye Jackpot ya Supa Mzuka Cup, cheza Tatu Mzuka kupitia; MPESA, TIGO PESA na AIRTEL MONEY, unaingiza namba ya kampuni ambayo ni 555111 na baada ya hapo ingiza namba zako 3 za bahati kisha ingiza kiasi kuanzia shilingi 500 mpaka 30,000.

Akiongea katika tukio la uzinduzi huo Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana alisema kwamba kampeni ya SupaMzuka Cup itawanufaisha watumiaji wa Mpesa kipindi chote cha fainali za kombe la dunia, ambapo watashinda sio tu muda wa maongezi na intaneti bali pia zawadi mbalimbali na fedha mpaka siku ya fainali tarehe 15 Julai.

‘Tunayo furaha kutangaza ubia wetu na Tatu Mzuka kwenye kampeni hii. Kwa wale ambao mnatumia MPESA kucheza Tatu Mzuka mbali na kushuhudia timu yako ikishinda nchini Urusi, utaweza kushinda bidhaa mbalimbali, fedha, muda wa bure wa maongezi na intaneti kila unapocheza Tatu Mzuka kila siku’ alisema Bwana Ndekana

Kama nyongeza ya kampeini ya SupaMzuka Cup, Tatu Mzuka pia inadhamini urushaji wa matangazo ya Kombe la dunia kupitia TBC 1 na TV1 ili kuhakikisha kwamba Watanzania wote wanapata fursa ya kutazama michuano hii yenye mvuto.

KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ametoa mwito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha siasa na badala yake kufanyakazi kwa kwaajili ya maendeleo.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya maendeleo katika jimbo lake la Ubungo na kuikabidhi.

Miradi aliyoitembelea Kubenea ni ujenzi wa kibanda cha kupumzikia katika Zahanati ya Mavurunza iliyopo Kimara ambao umegharimu Sh. milioni 7.7, miradi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mabibo ambao umegharimu Sh. milioni 17,mradi wa kisima katika soko la Mabibo uliogharimu sh. milioni 12 pamoja na ujenzi wa ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kawawa.

Akizungumza baada ya kutembelea na kuikabidhi miradi hiyo, Kubenea amesema ni vyema kufanya kazi kwa kushirikiana na sio kuangalia chama."Mimi sifanyi mambo haya kwaajili ya siasa, ninafanya kwaajili ya maendeleo ya wananchi....ninajua hata siku nikiondoka itabaki historia kwamba Kubenea alifanya kitu fulani.

"Kwahiyo niwaombe viongozi wote, tusiangalie siasa eti huyu chama tawala, huyu Chadema...tufanye kazi pamoja katika kuleta maendeleo ya Taifa letu," amesema Kubenea.Amefafanua kuwa maendeleo yana safari ndefu hivyo maeneo ya jospitali na shule yanahitaji kuboreshwa.

Akizungumzia miradi hiyo Kubenea amesema fedha zake zimetoka katika mfuko wa jimbo ambapo ni sehemu ya fedha za bajeti ya mwaka 2017/18.Akitoa shukrani kwa ujenzi wa Kibanda cha mapumziko, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mavurunza amesema walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya msongamano wa wagonjwa ambao ulisababishwa na kutokuwa na sehemu ya kupumzika.

"Kwasasa tunafanya kazi kwa uhuru na usiri kati ya mgonjwa na daktari....tunakushukuru Mbunge wetu alia yemua kujitolea fedha hizi kutoka katika mfuko wako," amesema Dorothy.Aidha Dorothy amesema Zahanati hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo jengo la wazazi kuhitaji ukarabati, kutokuwa na uzio pamoja eneo hilo kuhitaji kusawazishwa ambapo Kubenea aliahidi atalisawazisha kwa kipindi kifupi.

Wakati huo huo Mkuu wa Shule ya Mabibo, Hussein Mabibo amesema fedha zilizotolewa ambazo ni sh. milioni 17 zimesaidia kujenga madarasa matano, kubadilisha vigae vilivyochakaa na kuweka mabati, kupanga rangi shule, kukarabati ofisi ya walimu pamoja na ofisi ya mwalimu Mkuu.

"Tunakuamini wewe Mbunge wetu ukisema hua unatekeleza, hivyo tunaomba utusaidie pia kukamilisha maktaba, ujenzi wa uzio wa shule kwaajili ya usalama wa wanafunzi pamoja na ukarabati wa madarasa tisa ambayo yako katika hali mbaya," amesema Dady.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Soko la Mabibo, Yusuph Kilema amesema kisima kilichojengwa katika soko hilo kimekamilika kwa asilimia 90 ambapo bado vitu vichache ili kianze kutumika rasmi.

Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa kata ya Mavurunza Kimara mara baada ya kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya Mavulunza lililojengwa na fedha za mfuko wa jimbo
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akiwa amembeba mmoja wa watoto waliofika kupata huduma katika Zahanati ya Mavurunza .
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisoma gharama za ujenzi wa Mnara wa kupandisha maji juu katika kisima kilichojengwa katika soko la Mabibo Garment kwa fedha za mfuko wa jimbo
Mhandisi wa maji wa Manispa ya Ubungo akitoa maelezo kwa Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea wakatia alipotembelea miradi iijengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo.
Mwalimu wa shule ya Msingi Mkwawa Mabibo akimueleza Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea kiasi cha fedha zinazohitajika katika umaliziaji wa ofisi za walimu.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akiwa ameongozana na baadhi ya watendaji wa halmashauri na wafanyabishara wa soko la Mabibo
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisalimiana na wananchi na Makada Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi.
Mmoja ya wakazi wa Mavurunza akitoa pongezi kwa Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea mara bada ya kutekeleza ahadi zake kwa wakazi wa eneo hilo 
wakazi wa Ubungo kata ya Mavurunza wakiwa wanasikiliza hotuba ya mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea 
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkwawa Mabibo-

RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiendesha mazungumzo pamoja na mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea katika kikao. Cha siku. Moja cha waandishi wa habari pamoja na wadau wa taasisi za serikali mkoani hapo. Picha na Vero Ignatus. 
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Gabriel Daqarro akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku moja ulioitishwa na mkuu wa mkoa huo. Picha na Vero Ignatus
 Katibu Tawala  wa Mkoa wa Arusha Charles Kwitega akizungumza katika mkutano huo katika Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC Arusha. Picha na Vero Ignatus.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha AICC Arusha Eliashialia Kaaya.
Meneja wa TRA mkoa wa Arusha Faustine Mdesa, akiwasilisha mafanikio, changamoto na mpango mkakati wa mwaka wa serikali unaomalizika tar 30 june 2018.Picha na Vero Ignatus
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa mkoa wa Arusha  Cloud Gwandu akizungumza katika mkutano wa siku moja wa mkuu wa mkoa wa Arusha na waandishi wa Habari. Picha na Vero Ignatus
Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Asangye Bangu akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari. Picha na Vero Ignatus.
Mdau wa utalii kutoka Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) Paschal Shelutete ambae akijibu maswali na kutoa ufafanuzi kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Rc Mrisho Gambo- Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ukiwa na lengo la kuhakikisha kuboresha mahusiano kati ya serikali na waandishi mkoani hapo. Picha na Vero Ignatus.
Kutoka kushoto ni Katubu tawala wa mkoa wa Arusha Charles Kwitega akiteta jamba na mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Gabriel Daqqaro. Picha na Vero Ignatus.
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akiwasilisha kazi na majukumu ya Mamlaka hiyo na umuhimu wa kuwa na Bima haswa kwa vyombo vya moto.Picha na Vero Ignatus.

Na. VERO IGNATUS ARUSHA

Mkuu wa mka wa Arusha Mrisho Ghambo amefanya mkutano wa siku moja na waandishi wa habari ukiwa na lengo la kuimarisha na kuboresha mahusiano kati ya Serikali na wanahabari.

Katika mkutano huo wa siku moja ambao  ni wapili tangia kuingia madarakani  umewajumuisha wadau mbalimbali wa Taasisi za serikali mkoani hapa katika kueleza mafanikio changamoto mbalimbali za maendeleo na namna ya kuzitatua.

Katika ufafanuzi zaidi Gambo amesema kuwa asilimia 80%ya mapato mkoani hapo yanatokana na utalii hivyo amewataka wanahabari kuwa makini  taarifa ambazo wanaandika wazichuje kabla ya kuzipelea katika jamii.

"Mfano habari ya mtalii kutekwa, mwandishi unapoaiandika hiyo habari na kuitoa katika vyombo vya habari, itasomwa na inaweza kuleta madhara, kuwaogopesha wageni kutokuja nchini kwaajili ya utalii, kuweni makini tangulizeni uzalendo kwanza"

Amewataka viongozi mkoani hapa Kuwapa ushirikiano wa kutosha waandishi kwani kuna baadhi ya viongozi wanawakimbia waandishi na kuwalazimisha waandike kadri wanavyoona inafaa,amekemea na kuwataka kutoa ushirikiano. 

RC Gambo amepongeza juu ya jambo la kujiendeleza kielimu kwa waandishi ambapo ameutaka uongozi wa, APC kupeleka data base ili uongozi wa mkoa waone ni namna gani unaweza kuandika andiko kwa wadau mbalimbali kwaajili ya kuwasapoti kielimu. 

Gambo amewataka wanahabari mkoani hapo kutokukubali kurubuniwa au kutumiwa na mtu awae yeyote yule ili kuharibu amani badala yake watangulize Uzalendo kwanza kwaajili ya mkoa na Taifa kwa ujumla.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASALI SALA YA EID MSIKI WA ANWAR- MSASANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika  sala ya Eid kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam Juni 15, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika sala ya Eid kwenye Msikiti  Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Waislamu baada ya kushiriki katika sala ya Eid  kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri   Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kushiriki katika sala ya Eid kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amesema hairuhusiwi katika duka la dawa kuwa na dirisha la ushauri kwani huo si utaratibu huku ikielezea sababu zinazosababisha usugu wa dawa.

Dk.Faustine Ndugulile amesema hayo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Famasi yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Akizungumzia maduka ya dawa kuwa na dirisha kwa ajili ya kutoa ushauri, Dk.Ndugulile amesema kisheria hairuhusiwi kwani kuna mgawawanyo wa majukumu.

"Kuna baadhi ya maduka ya kuuza dawa wameweke na madirisha kwa ajili ya kutoa ushauri.Hairuhusiwi na hivyo baraza la famasi linatakiwa kusimamia hili kwa kuhakikisha hakuna duka la dawa ambalo limeweka dirisha la ushauri,"amesema Dk.Ndugulile.

Akizungumzia usugu wa dawa kwa mtumiaji, Dk.Ndugulile amefafanua zipo sababu nyingi ikiwamo ya matumizi ya dawa yasiyo sahihi na ulaji holela wa dawa.Amefafanua mbali ya kuwapo kwa sababu hizo kuna tafiti ambayo imebaini kuna vimelea ambavyo ni sugu wa hali ya juu kwa dawa zote zilizopo duniani.

Wakati huohuo Dk.Ndugulile ameliezea baraza la Famasi kuwa anao ushahidi wa baadhi ya watalaam wa famasi si waaminifu kwani wamekuwa wakiiba dawa na hivyo hao wachache kuharibu sifa ya famasi.

Ameliomba baraza la famasi kuhakikisha wanachukua hatua dhidi ya wanaokiuka sheria za famasi kwani kukaa kimya kunatoa nafasi ya baadhi yao kukika sheria zilizopo, hivyo wafuatilie.Hivyo amesema wenye tabia hiyo ya kuiba dawa waache mara moja kwani Wizara yao inafuatilia huku akielezea kwa sasa hakuna tatizo la uhaba wa dawa kwani zipo za kutosha.

Kuhusu kilele cha maadhimisho hayo, Dk.Ndugulile amesema anampongeza Msajili wa Baraza la Famasi pamoja na timu yake kwa kuona umuhimu wa kuadaa maadhimisho hayo.

Amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema hivi "Taaluma ya Famasi kuelekea Tanzania yenye uchumi wa viwanda" ambapo amesisitiza kupitia kauli mbiu hiyo wanataaluma wanaunga mkono nia ya dhati na juhudi za Serikali chini ya Rais Dk.John Magufuli katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi ili kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda.

"Sina shaka kuwa wanataaluma kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje mtaweka mikakati thabiti kupitia viwanda vya dawa ambavyo matokeo yake yataboresha uchumi wa nchi na kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi imara,"amesema Dk.Ndugulile.

Kwa upande wa Meya wa Jiji la Dar es Salam Isaya Mwita amesema anapongeza na namna ambavyo baraza hilo limejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za famasi huku akitoa ombi kwa Serikali kuandaa mazingira ambayo yatatoa nafasi kwa kuongezeka kwa viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini.

Wakati huo huo Baraza la Famasi limetumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio na changamoto huku pia wakielezea mikakati waliyonayo katika kuhakikisha wanaboresha huduma za famasi nchini.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Picha ya Pamoja
 Baadhi ya Washiriki 
 Meya wa jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita akizungumza katika madhimisho ya wiki ya wafamasia Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Msajili wa Baraza la Famasia Bi. Elizabeth Shekirego  akitoa maelezo kuhusu maadhmisho ya wiki ya wafamasia yaliyofanyika jana Mnazi Mmoja
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akionesha juu Bango Kitita la famasia baada ya kulizindua wakati  wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Msajili wa Baraza la Famasia Bi. Elizabeth Shekirego Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Bakari

WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA

$
0
0
Na Agness Francis,Globu ya jamii.

WASANII mbalimbali wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya Tamasha la Sport Music Festival ambalo linatarajia kufanyika leo Kanda ya Ziwa.
Lengo la tamasha hilo ni kuhakikisha wananchi wa Kanda ya Ziwa katika Sikuu ya Eid Elfitri wanasheherekea siku hiyo kwa kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.Tamasha hilo la aina yake litafanyika maeneo ya Geita,Mwanza na Kahama.

Kwa mujibu wa waandaaji wa tamasha hilo ni kwamba pia kutakuwa na michezo ya pikipiki pamoja na magari huku wakisindikizwa na wasanii mbalimbali wa Bongo fleva.Mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro Profesa Jay(Chadema)ambaye pia ni msanii wa kizazi kipya amewataka mashabiki zake wafike kumshuhudia akitoa burudani.

"Tangu niwe mbunge sijafanya shoo kubwa, hivyo hii ndio ya kwanza nitafanya maajabu kwenu,"amesema Prof. Jay.Kwa upande wa Snura Mushi a.k.a Snura amesema amejipanga kwa kufanya mazoezi licha ya kukaa mwezi  mzima wa mfungo bila kufanya shoo. "Nimewaandalia vitu vingi na vipya mashabiki zangu,nimejipanga kutengeneza vitu vipya tofauti na mlivyovizoea,"amesema.

Wakati huohuo Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la Weusi G Nako amewasili nchini ambako naye atashiriki katika tamasha hilo kwa kufanya shoo ya kibabe , hivyo amewataka mashabiki kjitokeza kwa wingi. Burudani hizo kwa siku ya leo zitaanzia Geita, kesho Mwanza na kumalizikia Kahama keshokutwa.
 Mbunge wa jimbo la mikumi ambaye ni msanii wa kizazi kipya prifesa jay akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutua katika viwanja vya ndege jijini Mwanza,akizungumzia ujio wake mpya kwa wakazi wa kanda ya ziwa,ambapo amesema bado yupo fiti   licha ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya shoo kubwa.
 Msanii wa kizazi kipya kutoka weusi G Nako akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutua katika viwanja vya ndege jijini Mwanza kuhusu ujio wake tena kwa wakazi wakanda ga ziwa  ambapo amewataka wajitokeze kwa wingi kushudia burudani ya uhakika kutoka kwake na shangwe zakutosha.
Mama wa chura snura mushi akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutua katika  Viwanja vya ndege leo jijini mwanza ambapo amewataka mashabiki wa kanda ya ziwa wajitokeze kumshuhudia akitoa buruda yake ambayo itakua na vitu vingi vipya kwenye tamsha hilo la sport music festival litakalofanyika,Geita,Mwanza,Kahama katika kusheherekea sikukuu ya Iddy.

DK. MNDOLWA AMALIZA ZIARA YAKE MIKOA YA KANDA YA ZIWA NA SINGIDA

$
0
0

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Edmund Mndolwa akipata maelezo kuhusu eneo lenye madini la Jumuiya hiyo lililopo katika Kijiji cha Bigigi, alipokagua eneo hilo akiwa katika ziara ya kikazo mkoani Singida, jana. Anayempa maelezo ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Singida Mjini Ali Balo (Wapili kushoto) na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Sosthenes Masola. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa NEC- CCM Christina Joramu na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Zanzibar Haidar Haji abdallah. Dk. Mndolwa ameagiza uongozi wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Singida kuharakisha kulitafutia leseni na kuliwekea vigingi vya mipaka eneo hilo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, jana. 
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akishiriki kucheza ngoma, iliyokuwa ikitumbuizwa wakati akipokewa kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Singida alipofika kwenye ofisi hiyo kuwanza ziara ya kikazi mkoani humo jana.
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa NEC- CCM Christina Joramu akimtuza msanii wa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Dk. Edmund Mndolwa katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida jana.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa na Makamu Mwenyekiti wake upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah wakisaini vitabu vya wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, jana.
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa NEC- CCM Christina Joramu akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, jana.
 Katibu wa CCM mkoa wa Singida Jimson Mhagama akisoma taarifa ya Chama ya mkoa.
 Kamishna Msaidizi wa Madini kanda ya Kati Sosthenes Masola (wapili kulia), akiwa na baadhi ya viongozi na maofisa wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Singida
 Baadhi ya maafisa kutoka Makao Makuu ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania wakifuatilia wakati Dk. Mndolwa alipongia katika Ofisi ya CCm mkoa wa Singida kusaini vitabu vya wageni.
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Singida Mashigani Kija akisoma taarifa ya jumuiya hiyo mbele ya Dk. Mndolwa
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Edmund Mndolwa akipata maelezo kuhusu eneo lenye madini la Jumuiya hiyo lililopo katika Kijiji cha Bigigi, alipokagua eneo hilo akiwa katika ziara ya kikazo mkoani Singida, jana. Anayempa maelezo ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Singida Mjini Ali Balo.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

TRA YATAIFISHA BOKSI 41 ZA MVINYO NA POMBE KALI DODOMA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dodoma

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata na kutaifisha boksi 41 za mvinyo na pombe kali zilizokutwa katika duka la jumla jijini Dodoma zikiwa hazina Stempu za Kodi.

Boksi hizo zenye thamani ya shilingi milioni tatu ambazo ni mali ya Anthony George, zimekamatwa na kutaifishwa leo wakati Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere akikagua matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) Jijini hapa kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.

Akizungumza mara baada ya kutaifisha boksi hizo, Kichere amesema kuwa, ni wajibu wa muuzaji kuhakikisha kwamba, vinjwaji vinavyostahili kuwekewa Stempu za Kodi vinakuwa na stempu hizo ili kuisaidia Mamlaka kutoza kodi stahiki.

"Inatakiwa Stempu za Kodi ziwekwe kwenye mzigo kabla mzigo huo haujanunuliwa na wauzaji wa rejareja. Hii itaisaidia TRA kukusanya kodi halali na hatimaye kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali," alisema Kichere.Mvinyo na pombe kali zilizokamatwa na kutaifishwa ni pamoja na boksi 27 za Robertson, boksi 7 za Jameson, boksi 5 za Drostdy Hof na boksi 2 za Alko Dompo.

Wakati huo huo, Kamishna Mkuu Kichere amemkamata Dereva wa Bodaboda Issa Athumani na kumtoza faini ya shilingi 30,000 baada ya kununua mafuta ya bodaboda hiyo bila kudai wala kuchukua Risiti ya Kielektroniki ya EFD.Kichere ameeleza kuwa, wananchi ambao hawadai risiti wanatakiwa kutozwa faini ya shilingi 30,000 hadi 1,500,00 au kuhukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015.

"Kuna watu ambao hawadai risiti na kuna mwingine nimemkamata leo ambaye nimemtoza faini ya shilingi 30,000 ili iwe fundisho kwa watu wote wanaonunua bidhaa na huduma mbalimbali bila kudai wala kuchukua risiti", aliongeza Kichere.Aidha, Kamishna Mkuu Kichere ametoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kutoa risiti kila wanapofanya mauzo na wananchi kuhakikisha wanadai risiti kila wanapofanya manunuzi mbalimbali.

"Natoa wito kwa wafanyabiashara wote waendelee kutoa risti lakini pia wanunuaji wadai na kuchukua risiti. Tunataka kujenga utamaduni wa kutoa na kudai risiti ili tuweze kukusanya kodi stahiki," alisema Kichere.

Naye, Mfanyabiashara wa mafuta jijini hapa Faustine Mwakalinga amemshukuru Kamishna Mkuu wa TRA kwa kutembelea kituo chake cha mafuta na kusema kuwa, zoezi hilo analolifanya litaongeza mapato ya Serikali kwasababu linajenga ukaribu na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.

"Namshukuru sana Kamishna Mkuu wa TRA kwa kutembelea kituo changu cha mafuta na nimefurahishwa sana na jinsi anavyofanya kazi yake ukizingatia leo ni sikukuu. Ukaguzi huu anaoufanya Kamishna Mkuu, utasaidia kuongeza mapato ya Serikali na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili sisi wafanyabiashara," alifafanua Mwakalinga.

Kamishna Mkuu Kichere ametembelea jumla ya Vituo vya Mafuta vinane na maduka 15 ikiwa ni moja ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni Dodoma hivi karibuni.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akifungua boksi katika duka la jumla Jijini Dodoma kuangalia kama vinywaji vilivyomo kwenye boksi hilo vina Stepu za Kodi wakati akifanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akiangalia chupa ya pombe kali aina ya Jameson katika duka la jumla Jijini Dodoma kuangalia kama chupa hiyo ina Stepu ya Kodi wakati akifanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza na Dereva wa Bodaboda Issa Athumani ambaye amekamatwa na Kamishna huyo na kumtoza faini ya shilingi 30,000 kwa kosa la kununua mafuta bila kudai wala kuchukua risiti Jijini Dodoma wakati akifanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akiangalia risiti ya kielektroniki ya EFD wakati akifanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta Jijini Dodoma. Mwenye Kanzu nyeupe ni Msimamizi wa Kituo cha Mafuta cha Camel Oil kilichopo maeneno ya Kisasa. (PICHA NA TRA).

WAFANYAKAZI TPA TANGA WATOA MSAADA WA SIKUKUU YA IDDI KWA KAMBI YA WAZEE MWANZANGE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga Ally Senkole kulia akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha kulea wazee wasiojiweza cha Mwanzange Jijini Tanga ambapo walikabidhi vitu vyenye thamani ya sh.milioni 1.5
 Sehemu ya watumishi wa Bandari ya Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wazee hao mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri
 Sehemu ya watumishi wa Bandari ya Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na vitu mbalimbali walivyonunua kabla ya kuwakabidhi wazee hao

 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga Ally Senkole akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vitu hivyo
sehemu ya vitu ambavyo vilikabidhiwa



Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani y ash.milioni 1.5kwa kituo cha wazee wasiojiweza kilichopo eneo la Mwanzange Jijini Tanga 

Msaada wa vitu hivyo ni vyakula mbalimbali ambavyo vitatumika kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitri ambapo halfa ya makabidhiano ilifanyika juzi kwenye kambi hiyo. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Bandari ya Tanga Hassan Senkole alisema waliona ni busara kupunguza sehemu ya mapato yao katika mwezi mtukufu wa ramadhani kuwasaidia wazee hao. 

Alisema waliamua kutoa msaada huo ili kuwa sehemu ya jamii iliyowasaidia wazee hao katika sikukuu ya Eid EL Fitri ili nao waweze kusheherekea sikukuu hiyo bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ile.

TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU

$
0
0
Kutoka kulia Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe na Meneja Mawasiliano wa TFDA Guadencia Simwanza wakimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka taulo za kike zilizotolewa Mamlaka hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa kidato cha nne zaidi ya 3000 walio katika kambi za kitaaluma mkoani humo, kushoto ni baadhi ya wananfunzi hao wakipokea kwa niaba ya wenzao, katika Shue ya Sekondari Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa saba kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kike walio katika Kambi ya kitaaluma Shule ya Sekondari Bariadi baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za Kitaaluma ambao umetolewa na wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) .Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa saba kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kike walio katika Kambi ya kitaaluma Shule ya Sekondari Bariadi baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za Kitaaluma ambao umetolewa na wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) .
Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari Bariadi, Somada, Chenge na Gudui kabla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi.
Meneja Mawasiliano wa TFDA Guadencia Simwanza akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari Bariadi, Somada, Chenge na Gudui kabla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike katoni 210 uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi ambapo shule hizo zimeweka kambi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye suti nyeusi katikati) katika picha ya pamoja wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Bariadi walio katika Kambi ya kitaaluma Shuleni hapo baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za Kitaaluma ambao umetolewa na wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) .

……………………………………………………………………………

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetoa msaada wa taulo za kike katoni 210 zenye thamani ya shilingi milioni tano na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaalum mkoani humo, ambao wanajiandaa na mtihani wa Taifa kwa mwaka 2018.



Akizungumza na viongozi, walimu na wanafunzi wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Bariadi Mjini Bariadi, Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa, Bw. Moses Mbambe amesema msaada huo umetolewa kujibu ombi la Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alilolitoa kwa Mamlaka hiyo kuwasaidia watoto wa kike wa kidato cha nne walio kwenye kambi ya Kitaalum mkoani humo ili wawapo kambini wasome kwa utulivu na kujiamini hususani wakati wa hedhi.



“Tunakabidhi taulo hizi za kike kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo ambazo Mkuu Mkoa wa Simiyu alimuomba ili ziweze kuwasaidia watoto wa kike wa kidato cha nne walioko kwenye kambi za kitaaluma katika maeneo mabalimbali hapa mkoani katika kuwawekea mazingira mazuri ya kusoma kuwa utulivu na kujiamini wakati wa siku zao za hedhi” alisema



Aidha, Mbambe ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa kuanzisha utaratibu wa kambi za kitaaluma na akawataka wanafunzi kuwa na ndoto, kusoma kwa bidii na kuweka mikakati ya kuwawezesha kufikia ndoto zao; huku akiwaasa kufanya vizuri katika mitihani yao ili kutoa nafasi kwa walio nyuma yao kuwekewa utaratibu endelevu wa kambi za kitaaluma katika kuuwezesha mkoa huo kufanya vizuri kielimu.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agnes Sitta Kijo kwa msaada taulo za kike ambao amesema utawasaidia sana watoto wa kike ambao wengi wao wamekuwa wakitumia vipande vya kanga na vitenge kujisitiri wakati wa hedhi.



“Ni wazazi wachache sana wenye uelewa kwamba binti zao wamevunja ungo na wao kama wazazi wanatakiwa kuwapa fedha ya kununulia taulo za kike kwa ajili ya kujisitiri wakati wa siku zao za hedhi, matokeo yake mtoto wa kike katika mazingira fulani anajikuta anashawishika kuingia kwenye mambo yasiyofaa kwa kupewa pedi tu na bodaboda kwa kuwa anaona huyo ndiyo boyfriend(rafiki wa kiume) mzuri” alisema Mtaka.



Kwa upande wa wanafunzi hao wameshukuru kwa msaada wa taulo hizo ambazo wamesema zitawasaidia sana kwani baadhi yao wamekuwa wakitumia vipande vya kanga, vitenge na njia nyingine za kienyeji kujihifadhi wakati wa hedhi , hivyo wamefarijika kwa msaada huo

“Tunawashukuru sana TFDA kutupa hizi taulo za kike maana wengi wetu huwa wanatumia kanga na vitenge kujisitiri, msichana akiwa hedhi halafu akatumia taulo maalum anakuwa anajiamini, anasoma kwa amani na utulivu mkubwa tofauti na atakayetumia njia za kienyeji” alisema Magulu Deogratius kutoka Shule ya Sekondari Bariadi.

Katika hatua nyingine walimu na wanafunzi wa shule za sekondari Bariadi, Chenge, Gudui na Somanda zote za Wilaya ya Bariadi walimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Viongozi wote kwa kuanzisha utaratibu wa kuwa na kambi za kitaaluma, ambao wamekiri umewasaidia wanafunzi kuwa na mtazamo tofauti katika masomo na wakaomba uwe endelevu.

“Utaratibu wa makambi umewasiadia sana wanafunzi wetu, kwanza wameongeza ari ya kusoma yaani hawalali, kila tunapowafundisha wamekuwa wasikivu kwa kuwa wanakiri wanapokea vitu vipya ambavyo hawakousoma shuleni kwao, tunaomba utaratibu huu uendelee maana tuaimani utawasaidia wanafunzi wetu kujiandaa vema na mitihani ya Taifa” alisema Mwalimu Zuhura Yahaya

“Tangu tumeanza kambi hii tarehe 03 Juni imetusaidia sana kuleta mabadiliko ya Kitaaluma, tunapata nafasi ya kubadilisha uzoefu wa kujibu maswali, mada ngumu tunasaidiwa na walimu wetu, tunaelekezwa namna sahihi ya kujibu maswali; naomba tukuhakikishie Mkuu wa Mkoa matokea ya mwaka 2018 yatakuwa ya mfano; yaani binafsi naona siku hazitoshi kama itawezekana mwezi wa tisa turuhusiwe kuja kambi tena” alisema Veronica Kidana kutoka Shule ya Sekondari Chenge.

Jumla ya Kambi za kitaaluma 149 zinaendelea kwa muda wa siku 21 mwezi huu katika maeneo mbalimbali ya mkoani Simiyu, ambapo kambi 35 ni kwa jili ya wanafunzi wa kidato cha nne na kambi 114 ni kwa shule za msingi, kwa ajili ya maandalizi ya Mitihani ya Taifa ikiwa ni moja ya mkakati wa kuondoa daraja sifuri na daraja la nne kwa kidato cha nne na kupandisha ufaulu wa darasa la saba.

WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa akizungumza wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mradi wa “Tumaini la mama kwa viongozi na watendaji mkoani Tanga kilichofanyika mjini Korogwe katikati ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
 MKUU wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akifungua kikao hicho kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa na Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga Ally Mwakababu
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akifuatiwa naKaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa
 KAIMU Mkuu wa wilaya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita
 Meza kuu wakifuatilia hoja mbalimbali za wajumbe kwenye kikao hicho
 Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona,Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa,Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO)Jairy Khanga
 Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia kwa umakini kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Luiza Mlelwa
 Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia kmwa umakini

 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Handeni wakati wa kikao hicho kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi
MKUU wa wilaya ya Mkinga Mark Yona kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mradi wa “Tumaini la mama kwa viongozi na watendaji mkoani Tanga kilichofanyika mjini Korogwe katikati ni Meneja wa Mfuko wa Tafa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu


WAKINA mama 925,342 nchini wamefanikiwa kusajiliwa na mradi wa “Tumaini la Mama tokea ulipoanza mwaka 2012 na kuweza kunufaika huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mradi wa “Tumaini la mama kwa viongozi na watendaji mkoani Tanga kilichofanyika mjini Korogwe.

Alisema idadi hiyo ni kuanzia mpango huo ulipoanza hadi mwezi Mei mwaka huu huku wakina mama wapatao 323,797 wakitokea mkoani Tanga pekee ambao wamesajiliwa.

Aidha alisema pia kaya 323.797 zimenufaika na kulipiwa fedha kwa ajili ya kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambapo sh.milioni 48,077,859,434 zimelipwa kwa watoa tokea mradi huo ulipoanza huku vituo vya mkoa wa Tanga vikilipwa kiasi cha sh.milioni 12,449,902,412.

“Pia vifaa tiba vyenye ya sh. milioni 900 vimenunuliwa na kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma pia mradi umesaidia upatikanaji wa computers katika vituo vyenye mahitaji kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa kumbukumbu”Alisema.

“Kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana mfuko utakaa na mfadhili kuona uwezekano wa kupata fedha zaidi kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi sisi viongozi tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba mradi unatekelezwa kama ilivyokusudiwa ili mfadhili aone umuhimu wa kuongeza muda zaidi”Alisema.

Awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema hatua ya mfuko huo kubuni mpango huo umekuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakazi wa mkoa huo na hasa wakima mama ambao sasa wana uhakika wa kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya bila gharama zozote.

Alisema mkoa huo ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya watu kupitia mpango huo wa Tumaini la Mama ambapo takribani wakina mama 323,797 wamenufaika na mradi huo ambao ni muhimu kwao.

“Lakini kabla ya kuanza kwa mradi huu mwaka 2012 idadi ya wanawake waliokuwa wanajifungulia katika vituo vya matibabu haikuwa kubwa kutokana na sabab u mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa elimu juu ya umuhimu wa uzazi salama pamoja na afya ya uzazi”Alisema

“Pamoja na gharama ya uzazi kuwa juu, kukosekana kwa huduma bora katika vituo vya kutolea huduma hasa upungufu wa dawa, vifaa pamoja na miundombinu isiyokuwa rafiki kwa ajili ya afya ya Mama na Mtoto”Alisema

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa kuwa lengo kuu la mradi ni kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuhakikisha kwamba akina mama wote wanajifungulia katika vituo na wanapata huduma bora.

Aliongeza kuwa hivyo mradi huo unatoa fursa kwa mama mjamzito kupata kadi ya Bima ya Afya kwa ajili ya kupata huduma za afya katika kipindi cha ujauzito na miezi sitaa baada ya kujifungua yeye na mtoto aliyezaliwa ikiwemo familia ya mama mjamzito yenye idadi ya watu wasiozidi sita wanalipiwa fedha kwa ajili ya kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii kwa mwaka mmoja katika halmashauri yake.

WAZIRI JAFO ATANGAZA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO.

$
0
0
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 70,904 wakiwemo wasichana 31,884 na wavulana 39,020 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu kati kwa mwaka 2018.


Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, Mhe. Jafo alisema wanafunzi waliochaguliwa ni kati ya wanafunzi 95, 337 walifaulu kwa kupata daraja la I-III na walikuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya ufundi.

Mhe. Jafo kati ya wanafunzi waliochaguliwa wanafunzi 30,317 watajiunga tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 28,610 watajiunga na taasusi za masomo ya Sanaa na biashara.Alisema kuwa wanafunzi 885 watajiunga na vyuo vya ufundi ambavyo ni vyuo vya ufundi vya Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar-Es-Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kiukuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

Mhe. Jafo alisema jumla ya wanafunzi 11,977 wamechaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za ngazi za Astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada katika vyo vya elimu ya kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)

Aliagiza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2018 wahakikishe wanaripoti katika shule zao kuanzia tarehe 15,Julai,2018 na atakayechelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Mhe. Jafo alisistiza kuwa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya ufundi umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika shule, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yeyoye ya shule kutokana na ukosefu wa nafasi kwenye shule husika.

Alisema wanafunzi waliopangwa kwenye vyuo vya kati wanapaswa kudhibitisha kukubali kujiunga na kozi walizochaguliwa hadi ifikapo 8 Agosti, 2018 ili kuthibitisha kuwa wamekubali kozi na vyuo walivyopangiwa kwa wanafunzi watakaoshindwa kuthibitisha nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine.

Amewapongeza walimu, wazazi na wakezi kwa juhudi walizozifanya katika ufundishaji na kuwezesha wanafunzi kufaulu vizuri na kuwaagiza kuendelea kusimamia na kufuatilia maendeleo ya watoto nchini.Aidha ametoa wito kwa Wakuuwa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji kuhakikisha azima ya Serikali ya kila Tarafa kuwa na shule ya Kidato cha Tano inatekelezwa ili kuwezesha wanafunzi wote wanaofaulu Kidato cha Nne kuapata na fasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha 5 na 6.

“Mikoa ihakikishe inakuwa na tahasusi zote za msingi katika shule zake ili kuwapunguzia wazazi gharama za usafiri kwenda shule za mbali nje ya Mkoa” Alisema Jafo.Aidha amesema kutokana na ongezeko la ufaulu wa masomo ya Sayansi kila shule zinazoanzishwa kuhakikisha zinajengwa maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa tahasusi za Sayansia ambao ufaulu wao umekuwa ukiimarika kila mwaka.

UNICEF Tanzania celebrates Father’s Day with renowned footballer, Ivo Mapunda

$
0
0


Former Taifa Stars goalkeeper calls upon fathers to play an effective role in parenting during their children’s early years.

UNICEF Tanzania celebrated Father’s Day with renowned footballer and former Taifa Stars goalkeeper, Ivo Mapunda, who called on fathers to step up their game in parenting, especially in the early years of their children’s lives.

UNICEF celebrity supporter and father-of-four, Mapunda, shared a video message for all Tanzanian fathers – urging them to be more involved in their children’s lives, especially in the early years.

Evidence suggests that when fathers bond with their babies from the beginning of life, they are more likely to play a more active role in their child’s development. Research also suggests that when children positively interact with their fathers, they have better psychological health, self-esteem and life-satisfaction in the long-term.

Advances in neuroscience have proven that when children spend their earliest years – particularly the first 1,000 days – in a nurturing and stimulating environment, new neural connections form at an optimal speed. These neural connections help determine a child’s cognitive ability, how they learn and think, their ability to deal with stress, and can even influence how much they will earn as adults.

“I read to my two-year-old every day, and encourage her to ask questions. And I play football with my older three on a daily basis. It’s our time to bond, and talk. On Father’s Day, I would like to encourage all dads to make sure they don’t miss out on this precious phase of their children’s lives. I am very happy to collaborate with UNICEF on this day,” said Mapunda. UNICEF is using Father’s Day to renew its call to break down cultural and financial barriers preventing fathers from spending quality time with their young children.

In Tanzania, UNICEF’s partners, including faith leaders, media and celebrities, are promoting messages on positive parenting, in particular the role of fathers and males, as a pivotal aspect of Early Childhood Development (ECD). UNICEF’s online partner, Elimika Wikiendi, will be running an online campaign on positive parenting and raising awareness around ECD issues. The platform will also engage users on the role that they can play to ensure young children are nurtured and cared for, so as to maximize their future well-being.

“I wish I had known before I became a father that stimulating young babies helps in their brain development. But to all the new fathers, I appeal, interact with your baby – it not only promotes their well-being, but jumpstarts brain development and boosts their learning ability,” said Mapunda, who runs a sports centre that identifies and nurtures young talent in football. The centre has 160 children enrolled between 5 and 20 years.

According to a UNICEF analysis released today as part of Father’s Day commemoration, almost two-thirds of the world’s children under 1 year– nearly 90 million – live in countries where their fathers are not entitled by law to a single day of paid paternity leave. Ninety-two countries do not have national policies in place that ensure new fathers get adequate paid time off with their newborn babies, including India and Nigeria – which all have high infant populations.

“Let’s use this day, and every day, to support and encourage fathers to get more involved in their children’s lives, especially in the early years. This is a time of rapid growth, brain development and curiosity in children. By doing simple things like giving children proper nutrition, lots of love, keeping them safe and spending time playing with them, parents can make a huge difference and set children up for a bright future,” said UNICEF Tanzania Representative, Maniza Zaman.

Father’s Day is celebrated in more than 90 countries in the month of June. This year, UNICEF is calling upon fathers to post photos and videos on digital platforms and share their #SuperDad moment with their children and share a parenting tip. In Tanzania, UNICEF is running an online campaign till end of the month, encouraging fathers to share their photos and parenting tips, and engaging them in discussions on their role.

SERIKALI YAPIGA VITA AJIRA KWA WATOTO WILAYANI TARIME, YAWAHIMIZA KUWAPELEKA SHULE

$
0
0
Na Frankius Cleophacee Tarime.

Serikali imepiga vita suala la Ajira kwa watoto wadogo ikiwemo kufanya biashara ndogondogo kwa watoto hao, badala yake wapelekwe shuleni na kuahidi kuwachukulia hatua kali wazazi na walezi watakaokiuka.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashari ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kiwilaya Wilaya ya Tarime Maadhimisho hayo yuamefanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Nyamongo katika Kata ya Matongo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa amepiga vita suala la ajira kwa watoto hususani kufanya biashara ndogo katika Maeneo ya Stendi huku akipiga vita pia suala la Walimu Wa Shule za Sekondari na Msingi kufanya biashara katika Maeneo hayo.

Katika Maadhimisho hayo zimeweza kushiriki Tasisi mbalimbali Likiwemo Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime, ATFGM Masanga, Plan International,Muungano wa Jamii Tanzania MUJATA, Acacia North Mara pamoja na Viongozi wa Dini

Kambibi Kamugisha kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto na Valerian Mgani kutoka Shirika la ATFGM Masanga wanazidi kupaza sauti zao kwa jamii ili kutokomeza Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike Wilayani Tarime huku wakiomba serikali Kuungana na Mashirika hayo kwa lengo la kupiga Vita suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.

Kamugisha amesema kuwa sualala Ukeketaji ndo chanzo kikubwa cha ongezeko la ndoa za Utotoni katika Mkoa wa Mara hivyo Ukeketaji ukitokomezwa Ndoa za Utotoni zitaisha.

Valerian Mgani Kutoka Shirika la ATFGM Masanga ambao ni wadau wa kupiga Ukatili katika Jamii amesema kuwa Mwaka huu Koo nyingi za Kabila la kikurya zinatarajia Kukeketa Mtoto wa kike hivyo ni jukumu la Serikali pamoja na Mashirika hayo kuungana kuendelea kutoa Elimu hiyo.

Vile vile Shirika la Penuary Root Out Alliance Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Maendeleo ya Kilimo Mogabiri nao wameweza kuadhimisha Siku hiyo katika kijiji cha Magoma kata ya Binagi lengo ni kufikisha Ujumbe kwa jamii kwa lengo la kunusuru Mtoto katika suala zima la Ukatili.

Wegesa Mosama kutoka Shirika la Penuary Root Out Alliance Tanzaniai anazidi kuimiza jamii kuendelea kupiga Vita Mila na Destuli zililizopotwana wakati Huku Afisa Maendeleo ya Jamii Kituo cha Maendeleo ya Kilimo Mogabiri Naomi Marwa akisisitiza suala la Mwanamke kupewa Fursa pamoja na Kufanya Maamuzi katika Jamii.

Licha ya hayo wasichana ambao wameunda Vikundi katika Kijiji cha Magoma kwa lengo la kuendelea kutoa Elimu ya kupiga Vita Ukatili nao wanaopaza Sauti zao huku wakibainisha Changamoto wanazokumbana nazo kuwa bado jamii inakuwa ngumu kupokea elimu hiyo kwa kudai wanaingilia Mila zao.

Philomena Tontora ni Diwani wa Viti Maalumu Kupitia CHADEMA Kata ya Matongo anasema kuwa Nyamongo kuna Wimbi kubwa la watoto wanaotangatanga hivyo Serikali ichukue hatua kali kwa Wazazi na walezi ili kunusuru watoto hao.

“Kauli mbiu katika Maadhimisho hayo ni Kuelekea kwenye Uchumi wa Viwanda mtoto asiachwe Nyumbani”
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Apoo Castro Tindwa akizungumza mbele ye Wananchi (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika,ndani ya viwanya vya shule ya sekondari Nyamongo wilayani Tarime .
Muwakilishi Kutoka Shirika la ATFGM Masanga,Valerian Mgani ambao wamekuwa wakipiga vita Ukatili katika jamii akiongea na Wananchi kwenye  Maadhimisho hayo.
Muwakilishi Kutoka Shirika la Plan International , Shaban Shaban akizungumza mbele ya Wananchi katika Maadhimisho hayo.
Wanafunzi kutoka Shule za Msingi zinazozunguka Mgodi wa Uchimbaji wa Mawe ya Dhahabu ACACIA North Mara wakiwa katika Maadhimisho hayo ya Siku ya Mtoto wa Afrika,ndani ya viwanya vya shule ya sekondari Nyamongo wilayani Tarime .
Wanafunzi hao wakiwa na Mabinti kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF wakionesha igizo lenye ujumbe wa kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike
Wanafunzi wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa Siku ya Mtoto wa Afrika.
Baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwa katika Maadhimisho hayo.

TGNP MTANDAO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA NJIA HII

$
0
0
Watoto kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali mapema jana katika kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Elimu bure inatakiwa iende sambamba na huduma muhimu kwa watoto ikiwemo upatikanaji wa maji, vyoo vya kutosha, vyumba vya kujihifadhia watoto wa kike, Mabweni pamoja na chakula kwa wanafunzi wawapo mashuleni.

Hayo yamesemwa mapema jana jijjini Dar es salaam na Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Anna Sangai katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ifikapo tarehe 16 mwezi juni.
Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Anna Sangai akiongea na waandishi wa habari baada ya maandamano ya amani yaliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam.

Afisa huyo alisema kuwa lengo kuu la kukutana pamoja na watoto hao ni kutathmini sera na mipango ya nchi iliyowekwa katika kulinda, kutetea haki na maslahi ya mtoto kulingana na sharia na mikataba ya kimataifa ambayo taifa letu limeingia.

Aliendelea kusisitiza kuwa jambo hili liende sambamba na ulinzi wa watoto wawapo ndani na nje shule, lakini pia kuwalinda dhidi ya mila na desturi zinazowakandamiza watoto hasa wa kike kama vitendo vya ukeketaji, ndoa pamoja na mimba za utotoni.

Lakini pia katika kukuza na kuendeleza uchumi wa viwanda watoto wasiachwe nyuma kwani wao ndio wanaotarajiwa kuja kuviendesha viwanda hivyo tarajiwa katika nchi yetu kwa kuwakuza kwa elimu ya vitendo ikiwemo masomo kilimo.
Mwenyekiti wa vituo vya Taarifa na Maarifa Taifa Janeth Mawinza akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Mwananyamara jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata Makumbusho Dada Janeth Mawinza alisema kuwa wameamua kufanya maadhimisho hayo katika eneno la Mwananyamara Kisiwani kutokana ni eneo ambalo waligundua matukio mengi ya ukatili wa watoto ikiwemo kupigwa kunakopitiliza pamoja na matukio ya watoto kuchomwa moto.

“Eneo la Mwananyamara Kisiwani lina watoto wengi sana waliofanyiwa ukatili na ndio maana tumekuja na ujumbe unaowataka wazazi na walezi kuacha vitendo hivyo mara moja, kwani mtoto ana haki zake na anastahili kulindwa na kuendelezwa ili aweze kufikia malengo yake”. Alisisitiza Dada Mawinza
Watoto kutoka kata mbalimbali wakiwa katika maandamano ya amani Siku ya Mtoto wa Afrika mapema jana jijini Dar es salaam.


BIA YA KILIMANJARO YAFANIKISHA NDOTO ZA WATANZANIA 10 KUONA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA 2018, URUSI

$
0
0
Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo,(kushoto) akiwapa maelekezo baadhi ya washindi wa safari ya Urusi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuangalia mechi za kombe la Dunia iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ili kushiriki kinachotakiwa ni kununua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara 6 kutuma namba iliyopo chini ya kizibo kwenda namba 15451 na droo ifafanyika kila wiki kwa kipindi cha wiki kumi. 
Baadhi ya washindi wakiwa na Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL,David Tarimo (wa pili kutoka kushoto). 
Shamrashamra za hafla ya uzinduzi wa kuangalia mechi za kombe la Dunia jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL katika hafla hiyo *Wengine waendelea kujishindia fedha taslimu shilingi milioni moja Wakati mashindano ya soka ya kombe la dunia 2018 la FIFA, yameanza ,bia rasmi ya kwanza ya Tanzania katika mashindano hayo ya Kilimanjaro Lager, kupitia promosheni yake inayoendelea imefanikisha ndoto za watanzania 10 kwenda nchini Urusi kushuhudia mechi za mashindano hayo makubwa ya soka dumiani mubashara. 

Washindi kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro ya Kombe la Dunia, iliyozinduliwa mapema mwezi uliopita wako katika maandalizi ya safari kwenda Urusi mapema mwanzoni mwa wiki ijayo. Baadhi ya washindi walipohojiwa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na safari hiyo walisema kwa furaha kuwa mwanzoni walikuwa hawaamini baada ya kupewa taarifa za ushindi wa droo za promosheni hiyo lakini hivi sasa baada ya kukabidhiwa tiketi zao wameamini safari ipo. 

Charles John, mmoja wa washindi hao kutoka mkoani Geita,ameeleza kuwa anajisikia furaha kupata fursa kama hii ambayo alikuwa haitegemei,ameishukuru kampuni ya TBL kwa kuandaa promosheni kubwa kama hii ambayo imefanikisha ndoto za wateja wake kuona mechi za kombe la Dunia Live. 

Mshindi mwingine, Leodgard Isaac,alisema kupata nafasi hii ni moja ya jambo ambalo limeleta furaha maishani mwake na kuongeza kuwa mbali na kuona mechi za kombe la Dunia Live pia anafurahi kuona kinywaji kutoka Tanzania cha bia ya Kilimanjaro, kimetumika kuitangaza Tanzania katika mashindano haya makubwa ya mchezo wa soka duniani. 

Naye Kaijage Kironde, mkazi wa Dar es Salaam,alisema ni mpenzi wa mchezo wa soka kwa miaka mingi,na amefurahi kupata nafasi ya kushuhudia mchezo wa kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro. 

Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, alisema,promosheni inaendelea kwa washindi wa fedha taslimu milioni moja kila wiki na muda wa maongezi inaendelea na katika droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki washindi 4 wamejishindia fedha, “Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018”, alisisitiza.

KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO

$
0
0
Kivuko cha MV. Mwanza kikisubiri kutoswa kwa mara ya kwanza kwenye maji kufanyiwa ukaguzi wa mwisho, kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250. Kivuko hicho kitafanya idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vinne
Muonekano wa kivuko kipya cha MV. Mwanza mara baada ya kutoswa kwenye maji kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250 na kitafanya idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vinne.
Muonekano wa Kivuko cha MV MWANZA mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.
Kaimu Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuhudia kutoswa kwenye maji kwa kivuko cha MV.Mwanza ambacho kitakua kikitoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza, kivuko hicho kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuhudia kutoswa kwenye maji kwa kivuko cha MV.Mwanza ambacho kitakua kikitoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza, kivuko hicho kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO



NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)

Wakazi wa jiji la Mwanza mapema leo wameshuhudia tukio la kushushwa kwenye maji kwa Kivuko kipya cha MV. Mwanza baada ya kufikia hatua za mwisho za kukamilika kwa ujenzi wake. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ametoa pongezi kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kusimamia mradi huo kwa mafanikio makubwa. Aidha, ameipongeza Kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Boatyard Ltd ya jijini Mwanza kwa kujenga kivuko hicho kwa ubora wake.

Kaimu Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za vivuko kutoka TEMESA, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alimuwakilisha Mtendaji Mkuu wa TEMESA alisema ni faraja kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza kupata kivuko kipya kwani kitapunguza adha ya foleni ndefu kwa watumiaji wa vivuko vinavyotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi. 

Mhandisi King’ombe aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kuhakikisha kuwa wakazi wa mkoa huo wanapata huduma ya usafiri yenye uhakika na kuwataka wakazi hao kukitunza kivuko hicho kitakapoanza kutoa huduma ya uvushaji wa abiria na magari. Alisema, hatua inayofuata baada ya kivuko hicho kushushwa kwenye maji ni ukamilishaji wa kazi chache zilizobaki na hatimaye kukifanyia majaribio ili kuhakikisha abiria na mali zao wanakuwa salama pindi watumiapo kivuko hicho.

Naye Meneja wa TEMESA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Alex William aliwaomba wakazi wa Mwanza kujivunia kivuko hicho kwa kuwa kimepewa jina la mkoa huo na hii ikiwa ni heshima kubwa kwa wakazi hao.Kivuko hicho cha tani 250 kina uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza hivi karibuni.

CHADEMA YAWAVUA UWANACHAMA VIONGOZI WAKE TARIME,WAPOTEZA SIFA YA KUWA VIONGOZI

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Viongozi watatu Wanaotokan ana Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyamwaga Wilayani Tarime Mkoani Mara wamevuliwa wanachama na kupoteza sifa ya kuwa Viongozi kwa kukiuka Maadili ya uongozi pamoja na Katiba za Chama chao.

Mkutano Mkuu wa CHADEMA Kata ya Nyamwaga umewavua uanachama Viongozi hao akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Nyamwaga Getende Sagirai, Mjumbe wa Serikai ya Kijiji Koroso Sasi na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mchanchara Mniko Chacha

Lukas Ngoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Tarime Mkoani Mara akiongea na Waandishi wa habari amesema kuwa Mkutano Mkuu wa Chama ulioshirikisha Viongozi wa Wilaya umewasimamisha Viongozi hao kwa tuhuma mbalimbali.

Ngoto amesema kuwa Mwenyekiti wa serikalia ya Kijiji cha Nyamwaga natuhumiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake huku baadhi ya Fedha zinazotokana na Mnara pamoja na Maji hazijulikani zimeenda wapi

Pia Ngoto ameongeza kuwa Mwenyekiti huyo amekuwa akikashifu chama hicho katika Vijiwe suala ambalo ni kukiuka kanuni ya Chama hicho.

“Sasa viongozi hawa watatu wamevuliwa uanachama na watapoteza sifa ya kuwa viongozi na tayari tumewateua baadhi ya vuongozi wa Muda wakati huo tukisubiri kufanya uchaguzi wa kuziba pengo na tunaenda kuandika barua kwa ajili ya kutaarifa Maofisa watendaji wa kata ili wasiwatambue” alisema Ngoto.

Jitiada za Kumtafuta Mwenyekiti huyo ili kuongelea juu ya kuvuliwa wanahama zimegonga Mwamba baada ya Simu yake ya Mkononi kuita bila kupokelewa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Lukas Ngoto akiongea na Waandishi wa habari kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Viongozi hao.

WAZIRI JAFO ATOA AGIZO KWA WAKUU WA MIKOA WOTE NCHINI

$
0
0
Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo ametoa muda wa miezi miwili kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini kuanza kusimamia ujenzi wa miundombinu ya shule katika Mikoa yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, Mhe. Jafo amesema miundombunu hiyo itahusisha ujenzi wa vyumba vya Madarasa 478 na mabweni 269 ambapo kila bweni moja litachukua wanafunzi 80.

Mhe. Jafo alisema kuwa ni wajibu wa kila Mkuu wa Mkoa kusimamia kusimamia kwa dhati kazi ya ujenzi wa miundombinu ya Madarasa na Mabweni na kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali zinaendana na majengo yatakayojengwa kama walivyokuwa wakifanya katika miradi ya afya na Elimu.

Aliendelea kusema kuwa Serikali imeweza kuchagua shule 119 ambazo orodha itatolewa wakuu wa Mikoa hiyo wahakikishe wanasimamia kwa haraka zoezi la kubaini maeneo ya yatakapojengwa madarasa na mabweni, pia kusimamia uteuzi wa Kamati za Ujenzi na kuanza mchakato wa kuwatafuta wajenzi wa majengo hayo.Alisema kuwa Serikali itatoa fedha kukamilisha haraka ujenzi wa miundombinu ya mabweni 269 na madarasa 478 kwa ajili ya wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano kwa kipindi hiki na kuagiza fedha hizo zikasimamiwe kwa weledi.

Mhe Jafo alisema ujenzi wa miundombinu hiyo utatumika kwa njia ya “Force Accont” utaratibu unaotumika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na ambao umetuika katika ujenzi wa shule na vituo vya afya Nchini.Aliwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Halmashauri zao kazi ya Ujenzi wa Miundombinu ya Shule inaenda kufanyika kusimamia kwa nguvu mchakato wa kutafuta mafundi wa ujenzi wa majengo na kuhakikisha wanapatikana haraka ili kazi ianze mara moja baada ya kubainisha maeneo.

Aliwataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wamekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni ifikapo tarehe 30/8/2018 ili kuhakikisha wanafunzi walio na sifa ya kujiunga na kidato cha Tano watapata fursa ya kujiunga na kidato cha tano.Wakati huohuo aliwaagiza Wakurugenzi ambao watasuasua katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa na mabwebi pamoja na miradi mingine hatasita kuwachukulia hatua na kuwataka watakapopata fedha wahakikishe kazi hiyo inakamilika mapema.

“Niwatake Wakurugenzi ambao wanatabia ya kusuasua utekelezaji wa mradi mbalimbali kuacha mara moja na katika jambo hili sihitaji masiahara hata kidogo, Mamlaka za Serikali za Mitaa itakapo pokea fedha ihakikishe inakamilisha ujenzi huo haraka.” Alisema Jafo.Aliendelea kusema kuwa Serikali haiwezi kukubali kuona watoto wa maskini wanakosa nafasi ya kujiunga na kidato cha Tano wakati wanasifa, hivyo amewataka nawata Wakuu wa Mikoa kusimamia kazi hiyo haraka kwa lengo la watanzania kuweza kupata fursa ya elimu katika nchi yao.

Aidha alisema Serikali imetenga shilingi bilioni 29 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha vijana wa Tanzania wanapata Elimu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na Waandishi wa Habari wakati akitoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa wote nchini kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa na Mabweni leo ofisini kwake, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo wakati akitoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa wote nchini kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa na Mabweni leo Ofisini kwa Jijini Dodoma

WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi mkoa wa Pwani, limewakamata wahamiaji haramu sita ,raia wa nchi ya Ethiopia na Somalia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Aidha mkoa huo umemaliza kusheherekea sikukuu ya Eid Ul Fitr kwa salama na utulivu kwani hakukuwa na tukio lolote la uvunjifu wa amani.

Kamanda wa polisi mkoani humo (ACP) Jonathan Shanna ,alithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao ambao wamekamatwa maeneo ya Msalabani kata ya Dunda wilayani Bagamoyo .

"Katika misako inayoendelea tumefanikiwa kuwakamata raia hao usiku wa kuamkia leo ambao wameingia nchini kinyume na sheria na taratibu zinazotakiwa " alifafanua kamanda Shanna.

Kamanda Shanna aliwataja wahamiaji haramu waliokamatwa kuwa ni Ahamed Mohamed (26) ,Mahad Ahmad (14) ,Abshir Aboulah wote raia wa Somalia .Wengine ni Beyene Abute (25),Abete Eramo (23), Abraham Adoise (24) wote raia wa Ethiopia.

Kwa mujibu wa kamanda huyo alisema ,watuhumiwa wote watawakabidhi idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.Akizungumzia juu ya kumaliza kwa amani sherehe za Eid Ul Fitr alibainisha mkoa huo hauna tukio lolote la uvunjifu wa amani lililojitokeza .

Kamanda Shanna alisema ,licha ya kumaliza salama sikukuu hiyo ,wanaendelea na misako na doria mbalimbali katika mkoa huo ambayo ni endelevu.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images