Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

WANAFUNZI WATEMBELEA BUNGE KWA LENGO LA KUJIFUNZA SHUGHULI ZA BUNGE

$
0
0
 Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mount Kibo ya Jijini Dar es salaam wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.
 Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Angelico Lipani ya Jijini Arusha wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.
Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Martin Luther ya Jijini Dodoma wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.PICHA NA BUNGE

WAKURUGENZI SITA BODI YA MIKOPO WAACHISHWA KAZI KUTOKANA NA TUHUMA MBALIMBALI DHIDI YAO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BODI ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELB) imewachia kazi wakurugenzi sita kutokana tuhuma mbalimbali dhidi yao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi wa Bodi hiyo Abdulzaq Badru amewataja waliofukuzwa ni Juma Chagonja( Mkurugenzi wa Urejeshaji wa Mikopo)na Onesmus Laizer(Mkurugenzi wa Upangaji na Ugawaji Mikopo).

Amewataja wengine ni John Elias(Mkurugenzi Msaidizi wa Ugawaji Mikopo) Robert Kibona(Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo),Heri Sago(Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Hesabu) na Chikira Jahari (Mkurugenzi Msaidizi wa Upangaji Mikopo).

Amefafanua kati ya hao waliochishwa kazi wakurugenzi ni wawili na wakurugenzi wasaidizi wanne (4). 

Amesema watumishi hao walikuwa wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo; uzembe uliokithiri, kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma 2002 na Kanuni zake, Sheria ya Bodi ya Mikopo Na. 9 ya mwaka 2004, Kanuni za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zinazo ongoza majukumu yao; na kusababisha hasara ya upotevu wa fedha za Serikali;

Badru amesema kuwa sheria na kanuni za utumishi wa Umma zinavyotaka, baada ya taratibu za ndani kukamilika.Amesema Februari mwaka huu bodi ya Wakurugenzi ambayo iliunda Kamati ya Uchunguzi iliyojumuisha wataalamu wa sheria, fedha na utumishi wa umma kwa lengo la kufanya uchunguzi na mahojiano na watuhumiwa hao. 

Amefafanua kamati hiyo imefanya kazi kwa kuwasilisha taarifa yake kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya uamuzi. Baada ya Uchunguzi uliofanywa na Kamati hiyo na utetezi uliotolewa na watumishi hao, Bodi ya Wakurungezi imejiridhisha kuwa watumishi hao walitenda makosa ya kinidhamu na hivyo kustahili adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazosimamia utumishi wa umma.

MAMIA WAMLAKI KATIBU MKUU WA CCM ALIPOWASILI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Mapokezi ya Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM Ofisi ya Makao Makuu ya CCM
 Ndg. Bashiru Ally Kakurwa akihutubia mamia ya wananchi walifika kumlaki katika Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma
Kutoka Kulia Ndg. Rodrick Mpogolo Naibu Katibu Mkuu (Bara), Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Mkanwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Ndg. Lubinga Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Ndg. Pereira Silima Katibu wa NEC Oganaizesheni

MAMIA WAMLAKI NDG. BASHIRU ALLY KAKURWA KATIBU MKUU WA CCM JIJINI DODOMA, MWENYEWE ATANGAZA KUHAMISHIA MAKAZI NA FAMILIA YAKE JIJINI HUMO YALIPO MAKAO MAKUU YA CHAMA NA SERIKALI.

13 Juni 2018

Mamia ya wananchi na wanachama wa CCM asubuhi ya leo wamemlaki Ndg. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipowasili kwa mara ya kwanza jijini humo kama Katibu Mkuu wa CCM na ikiwa ni kituo chake kikuu cha kazi.

Mamia ya wananchi na wana CCM walikusanyika katika uwanja wa ndege wa Dodoma na katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House).

Akizungumza na wananchi wa jiji la Dodoma waliofika kumlaki, wanachama wa CCM, viongozi wa CCM kutoka Mkoa wa Dodoma na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Bashiru amesema amepewa dhamana kubwa na wana CCM, dhamana ya kusimamia Mageuzi Makubwa ambayo yanakirejesha Chama chetu kwa wanachama na katika misingi ambayo kwayo Chama Cha Mapinduzi kiliasisiwa.

Ndg. Bashiru amegusia kwa ufupi kazi kubwa iliyo mbele ya wana CCM kwa ujumla kuwa ni kuhakikisha kazi nzuri ya kuendelea kuhuisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya Mashina, Matawi na Kata inaimarishwa maradufu, na kwamba uhai wa Chama uende sambamba na vikao vya Chama kukaa ili kuimarisha usimamizi wa rasilimali zetu za Chama kote nchini.

Aidha Ndg. Bashiru amezuangumzia hali ya maslahi ya watumishi wa Chama Cha Mapinduzi bado si ya kuridhisha, na akatumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa CCM kwa moyo wao wa kujitolea, utii na nidhamu ya hali ya juu licha ya changamoto walizonazo.
“… nitafanya kazi kwa bidhii kuimarisha misingi ya Chama kujitegemea na tutaboresha maslahi ya watumishi, hiki ni kipaumbele namba moja na ndio Maelekezo na msimamo wa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)” amesema Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM.

Akizungumzia kuhusu Mageuzi yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Ndg. John Pombe John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kubana mirija ya dhuluma na unyonyaji iliyowekwa na wasioitakia mema nchi yetu kutoka nje ya nchi na vibaraka wao hapa nchini, hakutawafurahisha wanufaika wa mfumo wa dhuluma na unyonyaji ndani na nje ya nchi. Ni kazi yetu kama Chama kumlinda na kutetea Ndg. Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania.

Kuna umuhimu wa kuimarisha Chama Cha Mapinduzi, kwasababu mambo haya ya mageuzi yanahitaji chombo cha uongozi, huwezi ukajenga uchumi wa kitaifa bila chombo cha uongozi, huwezi ukapambana na ufisadi, ukaimarisha uwajibikaji na uwazi, ukatoa huduma za kijamii kwa wanyonge bila ya kuwa na chombo imara na chombo imara kinachotegemewa na watanzania ni Chama Cha Mapinduzi na katika Ilani yetu ya Uchaguzi kuna sura mahususi inayohusu uimarishaji wa Chama chetu… Amesema Ndg. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa CCM.

Akitoa salamu za shukrani Mzee Job Lusinde, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Mkoa wa Dodoma amesema ameguswa sana na kauli ya Katibu Mkuu kwamba tunakirejesha Chama chetu katika misingi ya TANU na ASP. Mzee Lusinde amemtakia kwa niaba ya wazee wa Jiji la Dodoma Afya njema, busara, mafanikio makubwa, mfungo mwema wa Mwezi wa Ramadhani na Sikukuu njema ya Eid.

Shughuli ya mapokezi imehudhuriwa na wananchi, wanachama wa CCM, viongozi wa CCM wa ngazi zote Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Ndg. Godwin Azaria Mkanwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma pamoja na Mzee Pancras Ndejembi na Mzee Job Lusinde

Imetolewa na,


IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
OFISI YA MAKAO MAKUU - DODOMA

ETIHAD REDUCES LOSSES IN 2017

$
0
0

·         22%, US$ 432 million, improvement in core operating performance, driven by improved revenues and reduced costs
·         7.3% reduction in unit costs, despite US$ 337 million adverse effect from fuel prices
·         18.6 million passengers and 552,000 tonnes of cargo carried
·         Business transformation programme well underway

Abu Dhabi, UNITED ARAB EMIRATES– Etihad Airways improved its core operating performance by 22% in 2017, despite facing challenges including significant fuel cost increases, the entry into administration of its equity partners Alitalia and airberlin, and initial investment in a comprehensive business transformation programme.

The airline increased revenues from core operations by 1.9% to US$ 6.1 billion (2016: US$ 5.9 billion), while reducing losses in the core operations by US$ 432 million to US$ 1.52 billion (2016: loss of US$ 1.95 billion). Results published for 2017 are for core airline operations and exclude any extraordinary or one-off items; 2016 figures have been restated to show a like-for-like comparison.

Passenger and cargo yields improved as a result of capacity discipline, changes to the network with an increased focus on point-to-point traffic, leveraging of technology, and improving market conditions.

A strong focus on efficiency delivered a 7.3% reduction in unit costs, despite the adverse impact of US$ 337 million from higher fuel prices.

The airline reduced administration and general expenses by 14%, or US$ 162 million, over 2016.

Etihad Airways carried 18.6 million passengers at a 78.5% load factor. Available Seat Kilometres (ASKs) increased by 1% in 2017 reflecting a significant moderation of capacity growth, and contributing to an improvement in the quality of the airline’s revenues.

Etihad Cargo reduced capacity by 6%; however, revenues declined only marginally, down 0.8%, driven by stronger load factors and yields. Etihad Cargo carried 552,000 tonnes of cargo in 2017.

H.E. Mohamed Mubarak Fadhel Al Mazrouei, Chairman of the Board of Etihad Aviation Group, said: “Our airline continues to be a key driver of Abu Dhabi’s vision to develop its tourism sector, grow commerce and strengthen links to key regional and international markets.

“This was a pivotal year in Etihad’s transformation journey. The Board, new executive leadership team and all our employees worked extremely hard to navigate the challenges we faced. We made significant progress in driving improved performance and we are on track in 2018.”

Tony Douglas, Group Chief Executive Officer of Etihad Aviation Group, added: “We made good progress in improving the quality of our revenues, streamlining our cost base, improving our cash-flow and strengthening our balance sheet.

“These are solid first steps in an ongoing journey to transform this business into one that is positioned for financially sustainable growth over the long term. I would like to thank our people for their hard work and dedication in 2017.

“It is crucial that we maintain this momentum, retaining talent and attracting leading professionals from around the world to work alongside our highly-skilled UAE national workforce.”

2017 Operational Highlights

Etihad Airways received twelve new aircraft in 2017, including two Airbus A380s, nine Boeing 787-9 Dreamliners, and an Airbus A330F. These aircraft replaced 16 older Airbus A340, A330, A319 passenger and A330F cargo aircraft, which exited operations, thereby reducing the average fleet age to just six years.

In 2017, the airline announced that it will cease operating to Dallas / Fort Worth, Entebbe, Jaipur, San Francisco, Tehran, and Venice. A new route between Abu Dhabi and Baku was launched in March 2018 and services to Barcelona will start on 21 November 2018.

The global route network was further improved with the introduction of the Airbus A380 on one of Etihad Airways’ two daily services to Paris Charles de Gaulle, and the Boeing 787-9 Dreamliner on services to Amsterdam, Athens, Amman, Madrid, Beijing, Seoul, Shanghai, Nagoya, and Melbourne.

Etihad Airways recorded network punctuality of 82% for flight departures and 86% for arrivals in 2017 – results that place the airline as one of the most reliable airlines in the world for 2017. OTP (on time performance) for departures at the airline’s Abu Dhabi hub was 79%, and 89% for arrivals.

Since its inception, Etihad has placed a strong focus on developing young Emirati talent into world-class aviation professionals, and by the end of 2017 employed 2,729 Emirati staff, representing 11% of the total Etihad Aviation Group workforce.

Peter Baumgartner, Chief Executive Officer of Etihad Airways, said: “Our transformation process has delivered tangible results to date, with a significant improvement in performance for 2017.

“Passenger yields for the last quarter were up a very healthy 9% versus the same period a year before. On-time performance was at record levels and operationally we continue to drive down costs without compromising on safety or quality across all areas of the business.

“The major driver to becoming a more agile and efficient organisation, resilient in a very competitive landscape, is our continued investment in skilled professionals, technology and digital innovation, which is going to allow us to become smarter, faster and even more responsive to the ever-changing needs of our customers, making Etihad the airline of choice. These developments are at the heart of our transformation strategy.”
2017 results
2017
2016
Passenger Revenue (US$ billion)
5.0
4.9
Cargo Revenue (US$ billion)
0.9
0.9
Total revenue (US$ billion)
6.1
5.9
Core airline profit (loss) (US$ billion)
(1.52)
(1.95)
Total passengers (million)
18.6
18.5
Available seat kilometres (billion)
115.0
113.9
Seat factor (%)
78.5
78.6
Number of aircraft
115
119
Cargo tonnage (tonnes ‘000)
552
596

[Note] Results published for 2017 are for core operations only and exclude any extraordinary or one-off items; 2016 figures have been restated to show a like-for-like comparison.

TAMUFO YAMTUNUKU DK.MREMA TUZO YA HESHIMA

$
0
0
 Rais wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga (kushoto),akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kumkabidhi Tuzo ya Amani, Heshima na Utumishi uliotukuka, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema (katikati) iliyotolewa na umoja huo katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa Mrema Sinza jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel .
 Rais wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema (katikati), akimkabidhi sh.milioni 1.5 Katibu wa umoja, Stellah Joel alizizitoa kwa ajili ya kusaidia TAMUFO.
 Katibu wa umoja, Stellah Joel , akizungumza kwenye mkutano huo.
Rais wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga (kushoto), akimkabidhi Tuzo ya Amani, Heshima na Utumishi uliotukuka, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema iliyotolewa na umoja huo katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa Mrema Sinza jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel.



Na Dotto Mwaibale 

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umemtunuku Tuzo ya Amani, Heshima na Utumishi Uliotukuka, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya PAROLE, Dk. Augostine Lyatonga Mrema, kutokana na jitihada zake za kuhimiza umoja, utulivu na mshikamano. 

Dk. Mrema ambaye pia ni Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Naibu Waziri Mkuu katika kipindi cha awamu ya pili chini ya uongozi wa Mzee Alhaj  Ally Hassan Mwinyi, (Mzee Ruksa) alikabidhiwa tuzo hiyo na Rais wa TAMUFO Dk. Donald Kisanga. 

Akizungumza Dar es Salaam jana, mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Dk. Mrema aliwashukuru TAMOFO kwa kutambua mchango wake kwa Taifa katika kipindi ambacho alikuwa akiwajibika serikalini na kwenye jamii. 

Alisema ni muhimu kwa Taifa kutambua watu mbalimbali na hasa wazee waliofanya mambo mengi mema na mazuri kwa Taifa, badala ya kusubiri kutoa pongezi na shukrani wakati wa mazishi. 

Pia Dk. Mrema alitoa pongezi za kipekee kwa TAMUFO kutokana na uamuzi wao wa kuanzisha maombi maalum ya kuliombea Tiafa, akisema kazi hiyo ni muhimu na haipaswi kufanywa kwenye maeneo machache. 

“TAMUFO wameanzisha maombi maalum ya kuliombea Taifa kwa kushirikiana na wanamuziki wa Nyimbo za Injili nchini, lakini walianza kazi hiyo kule Ubungo Anglikana,” alisema Dk. Mrema. 

Aliongeza kusema kwamba, aliwaambia waandaaji wa matamasha hayo ya kuliombea amani Taifa, kutambua kazi kubwa inayofanywa na Dk. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo ni kubwa na muhimu. 

“Hivyo, nimewaomba wao TAMUFO na wadau wengine wakiwamo wafanyabishara, viongozi wa kada mbalimbali nchini, kuona umuhimu wa kuiunga mkono taasisi hiyo ili matamasha kama haya yaweze kufanyika nchini kote,” alisema Dk. Mrema. 

Alisema ikiwa TAMUFO itawezeshwa kuyafikia maeneo mengi nchini, itakuwa imesaidia kutuliza sintofahamu ya sasa ambapo baadhi ya watu bado hawajatambua nia njema ya Rais Dk. Magufuli, katika kuifanya nchi kuwa ya viwanda na yenye amani na utulivu kiuchumi.  

“Nitamfimkishia Mheshimiwa Rais Magufuli tuzo hii ya amani na ujumbe wake kwa Taifa,  ambayo nimepewa mimi binafsi kutambua mchango wangu kwenye nchi hii, lakini pia nashukuru kwa TAMUFO kutambua umuhimu huu,” alsema Mzee Mrema. 

Kwa upande wake Dk. Kisanga, alisema wazo la kumpatia tuzo hiyo Mzee Mrema, ilitokana na tamasha lililofanyika Jumapili katika kanisa la Anglikana Ubungo Jijini Dar es Salaam. 

Dk. Kisanga, alisema TAMUFO iliona kwa hatua za awali na katika kipindi  hiki ambacho Rais Magufuli na serikali yote ya awamu ya tano, amekuwa akisisitiza amani na mshikamano, wao waliamua kuanza mchakato wa kufanya matamasha ya aina hiyo kwa kuwashirikisha waimbaji wa nyimbo za injili. 

“Hivyo, tumempatia tuzo hii mzee Mrema, ambaye alifanyakazi kubwa kuanzisha vituo vingi vya polisi nchini, polisi jamii pamoja na ulinzi shirikishi nchini kote,” alisema Kisanga, na kuongeza kwamba mke wake mzee Mrema alitunikiwa cheti cha Shukran. 

Alisema katika kipindi hicho Mzee Mrema alikuwa tayari kukabiliana na mtu ama kikundi cha aina yeyote kinachohatarisha usalama wa nchi kwa kuwaita wahusika na kuzungumza nao ndani ya siku saba na matukio hayo kusimama mara moja,” alisema Dk. Kisanga. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel, alisema na kumshuikuru Mzee Mrema kwa mchango mkubwa alioutoa kwa Taofa kipindi cha utumishi wake. 

Lakini pia Stella, alisema kwenye tamasha hilo la kuombea amani ya nchi, Mzee Mrema aliahidi kuchangia kiasi cha Sh. Milioni 1.5 kwa TAMUFO kuendelea na matamasha ya kuombea amani nchini pamoja na kumtakia afya njema Rais. 

“Tumekabidhiwa tayari kiasi hicho cha fedha na Mzee Mrema, hivyo tunawaomba na kutoa wito kwa wadau wa maendeleo, haki na amani ya nchi kuungana naye mzee Mrema kufikia malengo ya kuwaunganisha wananchi kwenye matamasha ya aina hii.

Ni lini, Waislamu duniani wanaisherehekeaje na kwanini tarehe hubadilika?

$
0
0
 Na Jumia Travel Tanzania

Ni utamaduni wa kawaida kwa waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr kuashiria kuisha kwa kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa lugha ya Kiarabu neno Eid al-Fitr lina maana ya “sherehe ya ukomo wa mfungo” tukio ambalo hukusanya jamii ya Waislamu wote duniani kujumuika na kusherehekea kuisha kwa tukio hili muhimu la kiimani ndani ya mwaka.

Ingawa tukio hili huwa linafanyika kila mwaka lakini Jumia Travel imekukusanyia yafuatayo ambayo huna budi kuyafahamu kuhusu sherehe hizi.

Eid ni lini?

Tarehe rasmi ya Eid bado haijafahamika kwa kuwa inategemeana na mzunguko wa mwezi lakini tunajua kwamba kuna uwezekano mkubwa ikawa kati ya tarehe mbili tofauti katikati ya mwezi wa Juni.
Mwezi unaweza kuandama kati ya jioni ya Alhamisi ya Juni 14 au jioni ya Ijumaa ya Juni 15, kutegemeana na kuonekana kwa mwezi.

Kwa usahihi, ni kipindi gani waumini wamechagua kuonekana kwa mwezi hutofautiana kwa sababu wengine wamekubaliana mpaka wauone kwa macho huku wengine hata ukionekana kwingineko duniani sherehe hufanyika.

Kwa kuwa kuna siku 354 au 355 katika mwaka wa Kiislamu, siku ambayo Eid huangukia katika kalenda ya kawaida inayotumiwa duniani kote (Gregorian Calender) hubadilika kila mwaka.

Kwanini Waislamu husherehekea?
Waislamu hufunga kula kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanzia alfajiri mpaka kuzama kwa jua.

Ramadhani ni mojawapo ya nguzo tano za Uislamu - pamoja na Shahada ya Imani, Swalah, Kutoa Zakaah (kuwasaidia wenye dhiki) na Kuhiji Makkah - hivyo huwapatia Waislamu wasaa wa kutafakari juu ya maisha yao ya kiimani katika kuifuata Quran takatifu kama ilivyofunuliwa kwa Mtume Muhammad.

Kwahiyo, Eid ni sherehe ambazo huashiria kuisha kwa kipindi muhimu cha kiimani.
Waislamu husherehekeaje Eid?

Kwa kawaida, Eid husherehekewa kwa muda wa takribani siku tatu na ni siku ya mapumziko kwa mataifa ya Kiislamu na baadhi ya nchi nyingine duniani. Kwa Tanzania, husherehekewa kwa siku mbili ambapo wafanyakazi hawaendi kazini na wanafunzi hawaendi shuleni.

Kama zilivyo sherehe nyingine, watu husherehekea kwa namna tofauti, lakini kwa Waislamu huanza kwa kwenda mapema msikitini kuswali. Baada ya swalah kumalizika, waumini hutakiana heri ya Eid kwa kusalimiana, mara nyingi hukumbatiana mara tatu, wakati mwingine watoto hupewa zawadi kutoka kwa wakubwa wao.

Siku nzima iliyobakia hutumiwa kwa kusherehekea pamoja na familia na marafiki, kula na kupeana zawadi pamoja na kwenda kutembea sehemu tofauti. Familia nyingi hununua mavazi mapya kwa ajili ya kusherehea sikukuu hii.

Mara nyingi wakati wa sherehe za Eid huambatana na mapishi ya vyakula maalum ambavyo familia nyingi huwa hawavipiki siku za kawaida. Kwa Waislamu wengi huandaa biryani, pilau au wali, kwa nchini Tanzania, pilau ndiyo chakula maarufu kinachopikwa kwa nyama aidha ya ng’ombe, mbuzi, kuku, ngamia nakadhalika. 

Si jambo la kushangaza kipindi cha sherehe hizi kila mtaa utakaokatiza katika jiji la Dar es Salaam kunukia harufu ya pilau.       

Kuna tofauti gani kati ya Eid al-Fitr na Eid al-Adha?

Huwa kunakuwa na aina mbili za Eid kila mwaka. Ya pili, Eid al-Adha, husherehekewa baada ya miezi miwili na ni sherehe ambayo huja sanjari na Hijja, tukio la kiimani kwenda kuhiji Makka kila mwaka.

Hii inatarajiwa kusherehekewa kati ya Agosti 21 au Agosti 22 mwaka huu, hujulikana pia kama “sherehe ya kuchinja”, ikiwa ni heshima kwa kukumbuka tukio alilolifanya Mtume Ibrahim la kutaka kumtoa sadaka mwanaye wa kiume Ishmael, kitendo cha kutii amri ya Mwenyezi Mungu.

Unawezaje kumtakia mtu Eid njema?

Maneno maarufu ambayo hutumiwa na Waislamu ni “Eid Mubarak”, ambayo kwa Kiarabu yanamaaisha “Heri ya sikukuu ya Eid au Eid njema”

Hivyo basi watu wanaosherehekea sikukuu ya Eid husalimiana kwa mtindo huu kwa

VIJANA WANUFAIKA NA UJASILIAMALI

$
0
0
JOSEPH MPANGALA , MTWARA

Zaidi ya Vijana 200 wa Mkoa wa Mtwara wameunufaika na Ujasiliamali Kupitia Mradi wa KIJANA JIKWAMUE unaotekelezwa na Shirika la Africare na kufadhiliwa na Kampuni ya Uchimbaji na Uzalishaji Nishati ya Gas na Mafuta ya Shell.

Vijana hao waliopo katika Makundi 12 ambapo wanajishulisha na Ufugaji wa nyuki,Ufugaji wa Kukubora,Kilimo,Biashara Ndogondogo pamoja na kuongeza thamani Bidhaa mbalimbali na kuzitafutia masoko kwe lengo la kujipatia Kipato cha kila siku.

Frank Lyimo meneja Mradi anasema Mradi umeanza kuonesha mafanikio kutokana na baadhi ya Vikundi wameanza kuzalisha Bidhaa Bora ambazo zimeonekana kuwa na Ushindani katika Masoko tofauti kutokana na Kupata Vifungashio Bora na vyenye Nembo inayovutia.

“Mradi wa Kijana Jikwamue Unashughulika na kuwajengea uwezo wajasiliamali ambo kwa sasa umeonesha mafanikio kutokana na baadhi ya vikundi wanaweza kuzalisha Bidhaa Bora kwa mfano kuna kikundi kinafuga Kukumiatano mpaka Elfmoja ambao wanapelekwa sokoni wafikapo kuanzia kilo 1.3 na Tumewawezesha mabanda ya kutosha lakini wengine wanaongeza thamani Kilimo cha Mboga mboga pamoja na Asali” amesema Frank.

Naye Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna anasema Kunaonekana kuwa na mafanikio kutoka Mradi wa awam ya kwanza na sasa awam ya Pili ambapo lengo kubwa ni kuwawezesha kupanua Biashara ili kuweza kupata masoko sio tu kwa mkoa wa Mtwa balinchi Nzima.

“Nimefurahi sana kutembelea miradi hii na kuona manufaa ambayo Wananchii wameyapata kutoka kwenye awam ya kwanza na sasa hivi awam ya Pili na Tunaimani kuwa kwenye hii awam ya Pili watu watapata mafunzobora zaidi na waweze kupata masoko kwa sababu lengo la Awam ya Pili ni kuwawezesha waweze kupanua Biasha na kupata masoko Nje ya Mkoa wa Mtwara”

Abdulah Mkumbila ni mmoja wa wajumbe kutoka kikundi cha Jikomboe Kilichopo Mtaa Lwelu Manispaa ya Mtwara Mikindani anasema walianza na Mizinga mitano{5} kwa ajili ya kufuga Nyuki lakini kwa sasa wanamizinga Sitini{60}ambayo inaweza kuzalisha Asali Lita Miambili na Ishiriri{220}

“ Kutokana na Kupata Mizinga hii tayari baadhi ya wajumbe wameweza kujenga Nyumba Bora kwa utaratibu wa kukopa pesa na kurejesha na wengine wamenunua Pikipiki lakini Bado Kikundi kipo kwenye Mchakato wakuongeza Miradi Mingine kama Vile Ulimaji wa Bustani za Mboga Mboga ili kuongeza kipato”
Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna akitoa Ufafanuzi Kuhusiana na Ushiriki wa kampuni yake katika Mkutano kamati ya utendaji ya mradi wa Kijana Jikwamue Unaoendeshwa na Shirika la Africare na Kufadhiliwa na Kampuni ya Shell Mkutano Ulifanyika Mkoani Mtwara
Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna akipokea Taarifa ya Utendaji Kutoka kwa Abdulah Mkumbila ambaye ni Mjumbe wa Kikundi cha Jikomboe Kilichopo Mtaa wa Lwilo ambacho kinajishughulisha na Uzalishaji wa Asali Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Shirika la Africare Alfred Kalaghe.

Kutoka Kushoto Muweka hazina wa Kikundi cha Jikomboe Salum Nampaya akitoa Maelezo Kuhusiana na Uvunaji wa asali kwa Viongozi wa Africare Walipotembelewa Mtaa wa Lwelu Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo tangu walipoanza kikundi kilikuwa na Mizinga Mitano kwa ajili ya ufugaji nyuki lakini kwa sasa wameweza kuwa na Mizinga Sitini {60} ambapo wanaweza kuvuna Asali Lita Miambili na Ishirini 220}


Wajumbe wa kamati ya Utendaji wa Mradi wa Kijana Jikwamue Wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya Kumaliza Kikao cha kupokea Taarifa za Mradi wa Awam ya Kwanza pamoja na Mapendekezo na Mpango kazi wa Mradi kwa awamu ya Pili kwa ajili ya kuwawezesha Vijana wa Mkoa wa Mtwara

MRADI UBORESHAJI RELI YA KATI DAR ES SALAAM - ISAKA (TRC) KUANZA,WANANCHI WAANZA KUPEWA ELIMU YA MABORESHO HAYO

$
0
0
Muonekano wa mradi wa uboreshaji wa reli ya kati Dares Salaam- Isaka ukiendelea.

 
Wanakijiji wa Halmashauri ya kibaha vijijini, wakifuatilia kwa makini maelelezo yanayotolewa katika mkutano unaoendeshwa na wataalamu kutoka shirika la reli Tanzania - TRC Kuhusu uboreshaji wa Reli ya kati Dar es salaam- Isaka
 Afisa maendeleo ya jamii TRC Bi Catherine Mroso, , akitoa maelezo katika kampeni ya uhamasishaji wa uelewa wa uboreshaji wa reli ya kati Dar es Salaam – Isaka katika mkutano na viongozi wa Halimashauri ya kibaha vijijini, Magindu, Mkoani Pwani.

 
Mratibu wa mradi wa uboreshaji wa reli ya kati Dares Salaam- Isaka, kutoka TRC Mhandisi Mlemba Allen Singo ni  akitoa maelezo katika mkutano wa wananchi wa Halmashauri ya Kibaha vijijini, Magindu, Mkoani Pwani




SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

YAH: MRADI WA UBORESHAJI WA RELI YA KATI 

Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Uongozi wa TRC wamedhamiria kukarabati reli ya kati kipande cha kuanzia Dar es Salaam – Isaka (km970). Mradi huu umefadhiliwa na Benki ya dunia na kutekelezwa na Shirika la Reli Tanzania katika kipindi cha muda wa miaka miwili kuanzia juni 2018 hadi juni 2020. 

Lengo la uboreshaji wa reli ya kati ni kutoa usafiri wa kuaminika na kukuza upatikanaji wa huduma bora Nchini. Na maboresho hayo yatasaidia kuinua uwezo wa kubeba mzigo toka chini ya tani 13.5 za uzito wa eskeli hadi tani 18.5 kwa kufanya yafuatayo: 

I. Kutandika upya njia za reli zenye uzani wa paundi 80 kwa urefu wa kilometa 312 

II. Kufanya ukarabati wa njia ya reli iliyosalia kwa urefu wa kilometa 658 

III. Kufanyia ukarabati makaravati na madaraja 442 

IV. Kuboresha mfumo wa mawasiliano 

V. Kuboresha vituo vya kupakia na kupakua mizigo vya bandari ya Dar es Salaam, ilala na Bandari kavu ya Isaka. 

VI. Ununuzi wa vichwa vitatu vya treni (vipya) na mabehewa mapya 44 ya mizigo 

Katika kufikia malengo haya TRC itaingia mikataba 64 kati ya hiyo 32 ni ya kuajiri Washauri mbalimbali, 6 ni ya ujenzi na 24 ununuzi wa vifaa mballimbali na mikataba miwili ni ya huduma. Mpaka sasa zaidi ya 50% ya mikataba hii imeshasainiwa. 

Kupitia Mradi huu TRC pia imetengeneza mpango endelevu wa matengenezo ya miundombinu ili kufanya njia ya usafiri huu kuwa wa uhakika na kuaminika. Kuimarika kwa usafiri wa reli kutapunguza gharama za matengenezo ya barabara na hivyo serikali kuelekeza bajeti iliyookolewa kwenda kwenye huduma nyingine za kijamii. 

Maendeleo ya utekelezaji wa Mradi 

Kabla ya kuanza rasmi ukarabati wa njia za reli mwezi juni, TRC inaendelea kufanya kampeni ya uhamasishaji katika Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, katika Manispaa ya Ilala na Halmashauri ya Kibaha vijijini, ili kujenga uelewa kwa wananchi kuhusiana Mradi huu kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara katika kata na vijiji vinavyopitiwa na mradi huu. 

Kampeni hiyo ya uhamasishaji inaambatana na kuelezea faida za mradi wakati wa ujenzi ambazo ni kuwepo kwa fursa za ajira, kukua kwa kipato cha wananchi maeneo ya mradi na kujengewa ujuzi kwa wote watakaoshiriki kwenye shughuli za ujenzi. 

Pia wananchi wamepata fursa ya uelewa faida za mradi baada ya uboreshaji wa reli ya kati ambazo ni kuboresha na kuongeza kiwango cha ubebaji mizigo kwa miuondo mbinu ya reli na madaraja. Kuongezeka kwa mwendokasi wa treni kutoka kilometa 35 kwa saa hadi kufikia kilometa 70 kwa saa na hivyo kupunguza gharama na muda wa usafirishaji mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi bandari kavu ya Isaka hadi kufikia saa 24 kutoka zaidi ya masaa 36 ya sasa. 

Kampeni ya uhamasisha kwa wananchi imepelekea wapate kutambua hatua za uboreshaji ambapo Mradi huu umegawanyika katika vipande viwili, kipande cha kwanza kitaanzia Dar es Salaam hadi kilosa (kilometa 283), kipande cha pili ni kilosa hadi Isaka (kilometa 687) na vipande hivi vimeshapata wakandarasi na ujenzi unataraji kuanza mapema juni 2018. 

Kampeni ya uhamasishaji ni enedelevu mpaka pale mradi utakapokamilika, Uongozi wa TRC umesisitiza mambo ya kuzingatia kwa wananchi ambao reli ya kati inapita katika maeneo wanayoishi, ambayo ni: Hairuhusiwi shughuli zozote za kibinadamu katika maeneo ya reli ikiwa ni pamoja na biashara,kilimo na ufugaji. 

Wafanyabiashara wote watapaswa kupata kibali maalum cha biashara kutoka katika stesheni.Wakulima na wafugaji hawaruhusiwi kabisa kufanya shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo la reli,vilevele wafugaji wanapaswa kutumia vivuko vya mifugo vinavyotambulika na kuepuka kuvusha mifugo yao maeneo yasiyo na vivuko. 

Tahadhari, Jamii inapaswa kuchukua tahadhari za kiafya na tabia zozote hatarishi ili kuepuka maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kaswende,kisonono na hata maambukizi ya virusi vya UKIMWI. 

Imetolewa na idara ya uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TRC

Hatimiliki za kimila 747 kutolewa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

$
0
0
Evance Kibasa Mwananchi kutoka kijiji cha Usokame akiwa na Hatimiliki yake ya kimila baada ya kukabidhiwa.
Mmoja wa wananchi toka kijiji cha Usokame akikabidhiwa hatimiliki ya kimila na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Simon Mbago
Asafu Mgelekwa na Mkewe Atuganule Lunyungu wakiwa na hati yao yenye umiliki wa pamoja
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ugesa wakiwa na hatimiliki zao za kimila
Simon Mbago Afisa Ardhi Mufindi akimsaidia mwananchi kuweka saini kwenye fomu kama uthibitisho ya kuwa amepokea hati.

Shirika la PELUM Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeanza zoezi la kutoa hatimiliki za kimila zipatazo 747 kwa wananchi wa vijiji vitano ambao wamefanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi kupitia mradi wa ushiriki wa wananchi katika kusimamia sekta ya kilimo ulio chini ya watu wa marekani 

Hatimiliki hizo zinatarajia kunufaisha wanawake 250, wanaume 385, wenza wenye ushiriki wa pamoja 97 pamoja na maeneo ya Taasisis 97 toka vijiji vya Usokame, Ugesa, Magunguli, Isaula na Makungu 

Simon Mbago Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mufindi anayesimamia zoezi hili, mbali na kulishukuru Shirika la PELUM Tanzania kwa kufanya nao kazi kwenye vijiji hivyo amesema kufanyika kwa mpango wa matumzi ya ardhi hadi kufikia utoaji wa hatimiliki imesaidia kutekeleza majukumu ya Halmashauri ambayo yalipaswa kutekelezwa na Halmashauri husika. 

“Ni jukumu la kila Halmshauri kuhakikisha inatenga fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ili kufanyia vijiji vyake mpango wa matumizi ya ardhi lakini uwepo wa mashirika binafsi kutekeleza jukumu hili ikiwemo PELUM Tanzania imesaidia kwa kiwango kikubwa kuchochochea maendeleo katika Halmashauri yetu.” 

Hivyo basi uwepo wa hatimiliki hizi tunazogawa zitasaidia wananchi wa Halmashauri yetu kuzitumia kuomba mikopo kwenye taasisi za fedha kwa kuweka dhamana maeneo yao jambo ambalo wamekuwa wakilisubiri kwa kipindi kirefu ili kuwawezesha kufanya shughuli nyingine za kiuchumi kupita fedha watakazopata. 

Mbali na hilo, Mbago amesema pia zoezi hili si tu limesaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwenye vijiji husika lakini pia limesaidia kwa kiwango kikubwa kubaini kuwa wapo wananchi ambao maeneo yao ya muda mrefu ambayo yamepimwa kupitia mradi huu hayapo kwenye Wilaya ya Mufindi bali yapo kwenye wilaya ya Kilolo na hivyo kupunguza idadi ya hatimiliki walizopaswa kupewa wananchi jambo ambalo pia limesaidia kuzuia uwepo wa migogoro ya ardhi baina ya wananchi walipo mpakani mwa wilaya ya Mufindi na Kilolo. 

Evance Kibasa ni mwananchi wa kijiji cha Usokame ambaye eneo lake lilipimwa anasema hatimiliki ya kimila aliyokabidhiwa sio tu itamsaidia kupata mkopo kwenye taasisi za fedha na kuweza kutanua biashara zake kama njia ya kujiongezea kipato zaidi bali pia imemuhakikishia ulinzi halali na wa kisheria wa eneo lake kijijini hapo. 

Naye Asafu Mgelekwa ambaye amekabidhiwa hatimiliki ya umiliki wa pamoja na mwenza wake Atuganile Lunyungu amesema anashukuru kwa zoezi hili kukamilika na sasa ana uhakika hata akitangulia mbele ya haki amemuacha mke wake kwenye mikono salama kutokana na kuwepo kwa migogoro mingi ya kifamilia baada ya mume kufariki, mke hunyang’anywa mali zote na familia ya mume. 

Kaimu mtendaji wa kijiji cha Ugesa Malianusi Mdalingwa amesema, awali wakati zoezi la upimaji maeneo likiendelea wapo wananchi wengi waliobeza zoezi hilo na kusema maeneo yao yanaporwa ila baada ya kuona wenzao wanahakiki taarifa zao na sasa wamepata hatimiliki za kimila wanarudi ofisini wakiomba wapimiwe maeneo yao. 

“Awali walibeza sana zoezi hili na kutucheka kuwa PELUM Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mufindi wana lengo la kutudhulumu maeneo yetu na walitushawishi tuachane na mafunzo tunayopewa ila baada ya kuona zoezi linakamilika kila mtu anakuja ofisini akilalamika naye anataka apimiwe eneo lake ila baada ya kuwaambia kwa sasa itawapasa watumie gharama zao kidogo tofauti na sisi wa awali bado wanaona kama wanaonewa”. 

Kupitia changamoto hiyo, Mdalingwa ameomba Shirika la PELUM Tanzania kurudi tena kijijini hapo kuwapimia wananchi waliobaki kama watafamikiwa kupata mradi wingine. 

Santina Mdalingwa yeye ni mjane, anasema wakati wa mafunzo na zoezi la upimaji maeneo likiendelea, aliwashauri ndugu wa mume wake wapime eneo la nyumba ambayo alitafuta na mume wake, ila kutokana na ndugu kuona atanufaika walimkatalia kupima eneo hilo na hivyo kuamua kwenda kupima shamba lake la miti leye ukubwa wa hekari moja alilopewa na baba yake. Kwa sasa anasema hatimiliki aiyoipata ni ulinzi tosha wa eneo lake hakuna atakayemdhulumu ikiwemo ndugu aliozaliwa nao. 

Kupitia zoezi hilo endelevu, Simon Mbago amebainisha kuwa kati ya vijiji 121 vilivyo Halmashauri ya wilaya ya Mufindi ni vijiji 50 tu ambavyo wananchi wake wanamiliki ardhi kwa hati hivyo ameliomba Shirika la PELUM Tanzania kurudi tena katika Halmashari hiyo kuendelea kufanya kazi nao kama watapata mradi mwingine lengo ni kuwawezesha wananchi wote wawe na umiliki halali wa kishera wa ardhi zao.

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI MKUU KUTOKA BENKI YA NMB OFISINI KWAKE BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya NMB, Ndg. Ineke Bussemaker alipomtembelea leo tarehe 14 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya NMB, Ndg. Ineke Bussemaker alipomtembelea leo Tarehe 14 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Wageni kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu kutoka NMB, Ndg. Ineke Bussemaker (kushoto kwake) walipomtembelea leo tarehe 14 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wageni kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Ndg. Ineke Bussemaker (wa pili kulia) walipomtembelea leo tarehe 14 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

TMA YATOA MWELEKEO WA HALI YA HEWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MWEZI JUNI – AGOSTI (JJA), 2018

$
0
0

Na. Monica Mutoni 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa mwelekeo wa hali ya hewa nchini kwa kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti mwaka 2018. Taarifa hiyo imetoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa, joto, upepo na mvua, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Mamlaka imeeleza kuwa uwepo kwa hali ya joto la wastani hadi chini ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya baridi inatarajiwa katika maeneo ya miinuko ya nyanda za juu Kaskazini mashariki (Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Nyanda za juu kusini Magharibi (hususani mkoa wa Njombe) pamoja na maeneo ya miinuko ya mkoa wa Tanga (hususan wilaya za Lushoto na Bumbuli). 

Kuhusu hali ya mvua na upepo taarifa hiyo imeeleza kuwa maeneo mengi yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla,pamoja na vipindi vifupi vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo. Aidha, vipindi vya mvua za nje ya msimu vinatarajiwa katika maeneo ya pwani hususan katika wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Juni, 2018 na vipindi kadhaa kwa mwezi Julai, 2018. 

Wananchi wameendelea kushauriwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kama vile hali ya baridi inayotarajiwa katika maeneo mengi ya nchi hususan maeneo ya miinuko nakuweza kusababisha kudumaa kwa mazao kama vile ndizi pamoja na mazao ya nje ya msimu, na kuathiri mifugo. Vile vile, kutokana na hali ya joto katika bahari ya Hindi kuwa juu ya wastani kiasi, ongezeko la siku zenye tija katika shughuli za uvuvi katika kipindi cha msimu wa JJA linatarajiwa. 

Kwa taarifa zaidi temebelea tovuti www.meteo.go.tz

Mafunzo ya Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) kwa wahasibu na waweka hazina Iringa

POLISI YATAJA KILICHOSABABISHA AJALI YA AMBULANCE DAR

Mawakala 12 wajinyakulia mamilioni ya pesa huku wengine lukuki wakipata bonasi kemkem katika promosheni

$
0
0

Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani - George Lugata (kushoto) pamoja na Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni iliyohusisha mawakala 73,000 wa Tigo pesa nchini kote. Tigo imetoa zawadi za mamilioni ya pesa na bonasi kwa mawakala wake nchini kote katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani - George Lugata (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kwa Said Khatib wa Mkunazini, Zanzibar aliyeibuka kama mshindi wa jumla katika promosheni iliyohusisha mawakala 73,000 wa Tigo pesa nchini kote. Tigo imetoa zawadi za mamilioni ya pesa na bonasi kwa mawakala wake nchini kote katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa, Restituta Kedmond. 
Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani - George Lugata (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tatu kwa mwakilishi wa Duka la wakala wa RBB wa Sinza jijini Dar Salaam baada ya kuibuka mshindi wa pili katika promosheni iliyohusisha mawakala 73,000 wa Tigo pesa nchini kote. Tigo imetoa zawadi za mamilioni ya pesa na bonasi kwa mawakala wake nchini kote katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa, Restituta Kedmond.
 

Tigo Tanzania, kampuni inayoongoza kwa huduma za fedha kwa njia ya mtandao kupitia huduma yake ya Tigo Pesa, leo imewazawadia wakala wake 12 kutoka sehemu mbali mbali za nchi mamilioni ya pesa kama shukrani kwa utendaji wao mzuri.

Katika promosheni iliyohusisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa nchini kote, Tigo imetoa zawadi kwa washindi watatu wa kitaifa na washindi wengine watatu kutoka kila moja ya kanda nne za Tigo nchini.

Said Khatib Wakala wa Tigo Pesa wa eneo la Mkunazini, Zanzibar ndiye aliibuka kinara wa kitaifa na kujinyakulia TSH 5 milioni katika promosheni hiyo ‘Nawashukuru Tigo kwa kuwa mtandao unaowajali mawakala wao, kwani Tigo wanajitahidi kusikiliza na kushughulikia changamoto tunazozipata mawakala na kutupa mafunzo ya mara kwa mara yanayotusaidia kuenedana na hali halisi ya biashara hii,’ Said alisema.

Mshindi wa pili kitaifa aliyejinyakulia kitita cha shilingi 3 milioni ni wakala wa Duka la RBB lililopo Sinza, Dar es Salaam, huku Mojelwa Mlinga Mojelwa wa Pugu Dar es Salaam akiondoka na kitita cha shilingi 2 milioni kutoka Tigo Pesa. ‘Kupitia promosheni hii, Tigo wamethibitisha kuwa ni mtandao unaowajali sio wateja wake tu, bali pia mawakala na watoa huduma kwa ujumla. Kwani mitandao mingine huwa inaenedesha promosheni inayolenga wateja pekee yake, ila Tigo wametukumbuka mawakala na kutupa fursa ya kuongeza mitaji yetu,’ Mojelwa alisema.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani – George Lugata alisema kuwa lengo kuu la promosheni hiyo ilikuwa ni kuwarudishia shukrani mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa walioshiriki katika promosheni hiyo kote nchini. “Ningependa kuwapongeza mawakala wetu wote kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kuwa huduma za kifedha zinapatikana kwa urahisi kwa watu wote kote nchini,’ alisema.

Washindi wa kanda katika promosheni hiyo walipata zawadi za shilingi milioni mbili, shilingi milioni moja na shilingi laki tano kila mmoja, huku maelfu ya mawakala wakijishindia bonasi kemkem. Tigo ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya kasi ya juu ya 4G inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia inafahamika kwa promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake. Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini.

TBS NA FCC WATOA ELIM KWA WAFANYABISHARA

$
0
0
JOSEPH MPANGALA,MTWARA

Shirika la Viwango Tanzania TBS kwa kushirikiana na Tume ya ushindani FCC Imetoa mafunzo kwa wafanyabishara mbalimbali mkoani Mtwara yenye lengo la kuwajengea Uwezo wa kutambua Bidhaa Feki ambazo zinaingia sokoni pamoja na Kuwawezesha waweze kuzingatia sheria ya Ubora wa bidhaa Wanazonunua na Kuuza.

Mafunzo HAYO yamepita Duka kwa Duka na kutembelea wajasiliamali na Wauzaji wa Bidhaa mbalimbali na hivyo kubaini kuwa Kwa kiasi kikubwa Bidhaa zinazouzwa zinakidhi Viwango vya Ubora lakni kuna baadhi ya Sehemu kumeonekana kuwa na matatizo.

Frank mndimi ni Afisa mwandamizi mawasiliano na Mahusiano ya Uma kutoka Tume ya Ushindani FCC anasema Elimu hiyo inayopelekwa kwa wananchii na wafanyabiashara inaumuhim kwa sababu inajenga uwezo mkubwa katika kukuza Biashara hasa kwa wajasiliamali.

“Wafanyabiashara wengi wametaka Elim hii Ifanyike mara kwa mara lakini pia tumebaini Bidhaa zinazouzwa kwa kiasi kikubwa kwa sasa zinakidhi Viwango na zinakidhi matarajio na Bidhaa Halisi Kuna sehem Kidogo Bado Bidhaa zinamatatizo matatizo lakini Tumewaelimisha nini cha kufanya kuangalia na kuzingatia kwamba wanaweka bidhaa ambazo ni nzuri,bidhaa zinazo kizi matwakwa ya Sheria ya miliki Bunifu “alisema Frank.

Naye Mkuu wa Maabara ya Uhandisi Ujenzi TBS Stiphen Minja amesema madhara ambayo mfanyabishara yanaweza kumtokea Pindi anapouza Bidhaa isiyokuwa Bora ni pamoja madhara ya kiuchumi pamoja na Uchafuzi wa Afya.

“Mfanyabishara anapoweka Bidhaa sokoni ambayo haikidhi matakwa ya Ubora kwanza atapata madhara ya Kiuchumi,Kiafya na kimazingira,kama Mtu atanunua Bidhaa kwenye eneo lake Supermarket yake au duka la vifaa vya ujenzi popote pale ile bidhaa atakaposhindwa kuitumia hatarudi kwenye Duka lile kwenda kununua Bidhaa kwa sababu ameshakutana na Bidhaa yake ambayo Haina Ubora”.
 Mfanyabishara  wa Bidhaa za Rejareja Hemen Bajaria akimweleza Afisa mwandamizi mawasiliano  na Mahusiano ya Uma  kutoka Tume ya Ushindani FCC Frank Mdim Juu ya Elim aliyoipta katika Kutambua Bidhaa zenye Viwango na Nembo ya TBS
 Stiphen Minja Mkuu wa Maabara ya Uhandisi Ujenzi TBS akitoa elim  kwa  mmoja wa wafanyabiashara wa Spea za Mabari  Mkoani mtwara Mbarak Mabrouk juu ya Uagizwaji wa Bidhaa Kutoka nje ya Nchi na Jinsi ya Kutambua Bidhaa hizo kama zinaubora uanaohitajika kwa Wanunuzi.
Stiphen Minja Mkuu wa Maabara ya Uhandisi Ujenzi TBS akiwa na Afisa mwandamizi mawasiliano  na Mahusiano ya Uma  kutoka Tume ya Ushindani FCC Frank Mndami wakitazama moja ya Kopo la Asali lililofungashwa Vizuri na mmoja wa wajasiliamali kisha kupelekwa katika moja ya Soko kubwa liliko Mkoani Mtwara.

MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA

$
0
0
*Apiga marufuku magari ya vyombo vya ulinzi na usalama kupita barabara ya mwendo kasi


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema magari ya Serikali ndio yanayoongoza kuvunja sheria kwa kupita kwenye barabara ya mabasi ya mwendo kasi na hivyo limesema ni marufuku gari hayo kupita kweye baabara hiyo.

Kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo jeshi hilo limesema litaanza kufanya operesheni maalum kukomesha hali hiyo na kwamba dereva ambaye atakamatwa atachukuliwa hatua.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ambapo amefafanua kumwekuwa na tabia ambayo sasa inaota mizizi ya madereva kuhama kwenye barabara inayohusika na kuingia barabara ya mabasi ya mwendo kasi.

"Vyombo vya ulinzi madereva wake wengi wanapita katika barabra hiyo,magari ya wagonjwa nayo wakati yanapeleka mgonjwa na hata wakati wa kurudi pamoja na dereva kuwa peke yake bado anapita katika barabara hiyo. Matokeo yake inakuwa vurugu kwani ni matumizi ambayo hayakukusudiwa"amefafanua.

Hivyo Kamanda Mambosasa ametoa rai na onyo kwamba ni vema barabara zikatumika kwa mujibu wa sheria na hakuna sababu ya kulazimisha kubadilisha matumizi ya barabara hiyo ya mwendo kasi.

"Juzi Ambulance imesababisha mauaji au vifo vya wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutokana na uzembe ulifanywa na dereva wa Ambulance hiyo kwa kulazimisha kupita katika barabara ambayo hakuwa anaruhusiwa na matokeo yake akawa anapambana na magari yanayokuja mbele yake.

"Katika kulazimisha kupita akaligonga gari iliyokuwa imesimama na matokeo yake akasababisha ajali hiyo ambayo imepoteza maisha ya wanafunzi hao."Hatuwezi kuacha hali hii ikaendelea kuota mizizi, hivyo tutafanya operesheni na dereva ambaye tutamkamata asipige mayoe .Magari ya Serikali yanaoongoza kwa kuvunja sheria na kupita kwenye barabara za mwendo kasi,"amesema Kamanda Mambosasa na kuongeza operesheni hiyo inaanza leo kwa kuwachukulia hatua wote wanaovunja sheria na kwamba matokeo yake yataonekana.

Wakati huohuo Kamanda Mambosasa amepiga marufuku mchezo wa kuvaa viatu vya matairi na kisha kukimbia barabarani huku magari yakipita kwa kasi na kwamba wanaofanya mchezo huo waache mara moja kwani polisi itawakamata na kuwachukulia hatua.

Amesema kila mchezo una maeneo yake ya kuchezea hivyo hakuna sababu ya barabara za Serikali kutumika kwa mchezo huo na ole wao watakaokamatwa.

WANAFUNZI WA CHUO CHA MT.AUGUSTINO MWANZA WATEMBELEA ENEO LA HISTORIA YA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA

$
0
0
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Austine wakiingia  katika chumba cha kuangalia moja ya sinema.

WANAFUNZI wa chuo cha Mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza(SAUT) wa mwaka wa kwanza na wapili wanaosoma kozi ya mawasiliano ya umma watembelea kituo cha kumbukumbu na Makaburi ya halaiki ya wahanga wa mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda.

Kituo hicho ambacho kimebeba historia ya nchi ya Rwanda pamoja na baadhi kumbukumbu ya vitu mbalimbali vya watu wa nchi ya Rwanda kabla na baada ya mauaji ya kimbari.

Baadhi Kumbukumbu zilizopo katika jengo la kumbukumbu ni picha za watu waliofariki dunia pamoja na picha za watoto ambao waliuwawa bila hatia yoyote mauaji na makaburi yalitokea Aprili 7, 1994.

Pia katika ziara hiyo wanafunzi wa chuo cha MT. Augustino walitembelea televisheni ya Taifa ya Rwanda, Rwanda Bordicasting Agency (RBA) na kujifunza vitu mbalimbali katika shirika hilo la utangazaji nchini Rwanda.
Lango la kuingilia katika makumbusho na Makaburi ya mauji ya kimbari Kigari nchini Rwanda. Baadhi ya Wananfunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustino Mwanza wakiingia katika eneo la kumbukumbu.
 Mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha kumbukumbu ya makaburi ya mauaji ya kimbari, Kazinimana Pacifique akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha MT Augustino jijini Mwanza mara baada ya kufika katika kituo cha kumbukumbu na makaburi ya pamoja ya mauaji ya Kimbari ambayo walitokea nchini Rwanda Mwaka 1994 ambapo mpaka kwaka huu 2018 wametimiza miaka 24 ya kumbukumbu ya mauaji hayo.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Chuo cha Mtakatifu Augustino(HOD), Peter Mwidima.

 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Chuo cha Mtakatifu Augustino(HOD), Peter Mwidima akizungumza na wanafunzi wa  huo cha mtakatifu Augustino jijini Mwanza walipowasili katika kituo cha makaburi ya haraiki ya mauaji ya Kimbari Kigari nchini Rwanda.
  Baadhi ya wanafunzi wanafunzi wakipiga picha nje ya Jengo ambalo limebeba historia ya nchi ya Rwanda pamoja na picha za wahanga wa mauaji ya kimbari na vitu mbalimbali ambavyo vimehifadhiwa humo.
 Moja ya kaburi la pamoja la wahanga wa mauaji ya Kimbari Kigari nchini Rwanda.

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika eneo ambapo kunamajina ya watu waliofariki dunia katika mauaji ya kimbali Nchini Rwanda.


Baadhi ya Majina ya watu waliouwakawa wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Augustino jijini wanza wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Kiislam ya nchini Rwanda mara baada ya kukutana katika makumbusho na makaburi ya mauaji kimbari.
 Jengo la ukumbi Mkuu wa Ktituo cha utoaji huduma kwa pamoja Rusumo ambalo lipo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza wakipanda gari maara baada ya kufika mpakani mwa Tanzania na Rwanda. 
Wanafunzi wa chuo cha Mt. Augustino jijini Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri mkuu Mtendaji wa Kituo cha Utangazaji cha Rwanda Broadcasting Agency. na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha chuo cha Mtakatifu Augustino,(HOD), Peter Mwidima. 

 Jengo la Kituo cha Utangazaji cha Rwanda Broadcasting Agency nchini Rwanda ambapo kuna kituo Vituo vya Redio mbalimbali pamoja na Televisheni ya Taifa ya Rwanda(RBA).

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi vifo vya vijana wa JKT 11, Askari JWTZ 1 na Dereva vilivyotokea Mbeya

NEWZ ALERT:NEWZ ALERT:ASKARI VIJANA WA JKT 11, ASKARI JWTZ 1 NA DEREVA WAFARIKI DUNIA MBEYA

$
0
0


Wengine 25 wajeruhiwa...Kamanda Polisi Mbeya aelezea ajali ilivyotokea

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

ASKARI 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.

Akizungumza leo kwa njia ya simu na Michuzi Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.

Amesema kutokana na mwendo mkali aliokuwa anaendesha dereva wa basi gari hiyo yenye namba T 755 BAB aina Scania alishindwa kumudu kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao

Amesema kuwa askari hao walikuwa wakitokea Igunga kwenda Mbeya kwa ajili ya kuendelea na mafunzo mengine ya jeshi baada ya kumaliza mafunzo katika kambi ya Igunga.Amefafanua kuwa dereva wa gari hiyo naye amepoteza maisha na kwamba miili ya merehemu hao ipo chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa Mbeya.

Amesema waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ni askari 25 na wanne hali zao ni mbaya na sasa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya huku majeruhi waliobakia wakipatika matibabu katika hospitali ya JKT Mbeya kwani majeraha yao si makubwa.
Baadhi ya Askari wa JWTZ na JKT wakishriki kutoa msaada kwa Majeruhi  waliopata ajali iliyotokea katika eneo la Kawetele mkoani Mbeya mapema leo mchana.ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.

DK. BILAL AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUSOMA KURANI JIMBONI KIKWAJUNI

$
0
0
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akizungumza wakati wa Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo  katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akimkabidhi zawadi, Salha Mohamed Khamis, baada ya kuibuka  mshindi wa juzuu tano wa  Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni,Saleh Nassoro Jazeera  na  Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia).
 Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Salha Juma Sadalla akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika  leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.
 Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Abdilbaswit Hamis Hassan, akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar. Picha na Mpiga Picha Wetu
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal (watano kulia mstari wapili) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na washindi wa Mashindano ya Kusoma Kurani baada ya kuwakabidhi zawadi.Mashindano hayo yamefanyika katika Kiwanja cha Mapinduzi visiwani Zanzibar. 

Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images