Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI WA VITUO VYA AFYA NCHINI

$
0
0
Majengo ya Upasuaji na wodi ya Wazazi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Mlali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma
Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu      ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo
.................................................
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  John Pombe Magufuli kwa ujenzi wa vituo  vya afya 208 vilivyojengwa na Seriakli kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya nchini.

Wameyasema hayo mbele ya Kamati ya ufuatiliaji wa ukarabati wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iliyofika katika kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichopatiwa shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.

Wananchi hao wamesema Serikali imetambua shida za wananchi wa hali chini na kuona umuhimu wa kujenga vituo vya afya nchini  kwa lengo la kupunguza kero za utoaaji wa huduma bora kwa jamii maskini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha afya Mlali,kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Abbas Mkomwa  ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimeweza kujenga , Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya wazazi, Maabara,  Jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti.

Amesema huduma kama hizi zimekuwa zikifanyika lakini kwa sasa jamii imeweza kushirikishwa katika kila hatua za awali za ujenzi wa vituo vya afya hivyo kuweka uwazi kwa jamii na kuona kuwa nao wanawajibu wa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya nchini.

“Kwa mara ya kwanza Serikali imeweza kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo, hii inaonyesha jinsi serikali ya awamu ya tano inavyojdhamini mchango wa wananchi katika kuleta maendeleo“ AmesemaBw. Mkomwa.

Naye Richard Mgulumu Diwani wa kata ya Mlali ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa vituo vya afya nchini, hasa kituo cha afya cha Mlali ambapo anasema kuwa awali kituo hicho kilikuwa na wodi chache ambazo zilikuwa hazitoshi kuhudumia wananchi lakini kwa sasa zimeongezeka jambo ambalo litasaidia kuondoa kero za utoaji wa Huduma za afya katika Halamashauri hiyo.

Amesema kuwa Kituo hicho cha afya kimekuwa kikipata wagonjwa wengi kutoka Wilaya ya Kiteto, Wialaya ya Mpwapwa na Malali hivyo kwa ujenzi huo kutasaidia kuwahudumia wananchi maskini ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma bora za afya.

Naye Mganga Mkuu Hospitali ya Jiji la Dodoma Dkt. James Kiologwe ameipongeza Kamati ya Ujenzi ya kituo cha afya cha Mlali kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo hicho na kuonyesha uzalendo wa kusaidia jamii.
Aidha timu ya Ufuatiliaji wa ujenzi wa vituo vya afya Jijini Dodoma imekagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Mlali, Chamwino, Hombolo na Makole.
Capt

  1. Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua jambo    kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma.
  2.  
  3. Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo.

Article 6

Rais Magufuli amteua Athuman Selemani Mbuttuka kuwa Msajili wa Hazina

$
0
0
Ndugu Athuman Selemani Mbuttuka alieteuliwa kuwa Msajili wa Hazina

ORXY GAS NI WADAU MUHIMU NA RAFIKI WA KUTUNZA MAZINGIRA

$
0
0

Katika kuadhimisha wiki ya mazingira mwaka huu nchini Tanzania kampuni mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya Oryx ijulikanayo kama Oryx Energies Limited imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali ili kuhakikisha nishati mbadala inatumika badala ya mkaa ambao umeonekana kuwa na gharama kubwa sana.

Oryx Gas kwa nyakati tofauti wamekuwa wadau muhimu sana katika kuunga mkono jitihada za serikali katika  kutunza mazingira, na kwa muda mrefu wamekuwa na  kampeni yao ya Oryx Gas “Rafiki wa Mazingira”. Katika kuhadhimisha wiki ya mazingira  wameamua  kuchukua fursa  kujiunga na wadau wengine kushirikiana katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira kwa ujumla.

Akizungumza katika maonyesho hayo eneo la mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha mauzo  kampuni ya gesi ya Oryx, Jeffrey Nasser  amesema kuwa; Oryx GAS amekuwa rafiki mkubwa sana wa mazingira pale tulipoamua kuwaletea nishati mbadala ya gesi, na haikuishia hapo tuu bali tuliwawezesha wananchi wengi sana nchi nzima kuipata kwa gharama ndogo na hata yale maeneo ya wananchi wa hali ya chini tumewawezesha kupata gesi yetu. Na Tunaamini tumeokoa miti mingi ambayo ingekatwa kwa matumizi ya kupikia.

Ili kuhakikisha kuwa watu wote wanatumia nishati ya gesi, kampuni ya Oryx imewekeza kwa kiwango kikubwa sana kwenye maghara ya uhifadhi na mitambo ya kujaza gesi nchi nzima. Hatutarajii kusikia tena uhaba wa gesi ya kupikia nchini na hatutarajii kabisa watumiaji wa gesi wanarejea kwenye mkaa na kuni kwa kukosa nishati hii ya gesi hapa nchini. Aliongezea Afisa huyo. .

Akielezea kauli mbiu ya mwaka huu ya 'Mkaa ni gharama sana' Bwana Jeffrey amesema kuwa Mkaa ni gharama sana hasa kwa wakazi wa mijini. Sasa hivi gunia la mkaa kwa wakazi wa Dar es Salaam imefikia shilingi 70,000 na wengi wanalalamika kuwa mkaa haumalizi mwezi.Sisi tunawapa mtungi wa gesi wa kilo 15 ambao kwa familia ya watu saba wanaotumia gesi pekee huweza kutumia kati ya siku 30 hadi 40. Mbali na faida za gharama ndogo, gesi yetu pia ni salama kwa afya ya mtumiaji na usafi wa mazingira ambapo tusingeanza usambazaji mkubwa wananchi wangepaswa kuweka bajeti nyingine za matibabu ya madhara ya moshi mwilini na ukarabati wa nyumba ambazo huchafuka sana kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Kampuni ya Oryx imetoa  shukurani sana kwa wananchi kwa muitikio mkubwa sana wa matumizi ya gesi kila siku inayoenda. Muitikio mkubwa umeonekana hasa pale ongezeko la  watumiaji wengi wapya nchi nzima wakinunua mitungi mipya ya gesi ya Oryx kwa matumizi yao. Mbali na hapo wengiwamerudisha mrejesho  kuwa walichelewa kuanza kutumia gesi hiyo na wamehuakikishia uongozi wa kampuni ya Oryx kuwa hawatarudi tena kutumia kuni na Mkaa.

Kampuni ya Oryx inatoa wito kwa jamii yote kwenda na mabadiliko ya matumizi ya nishati ya kupikia, Oryx Gas kama wasambazaji wakubwa sana nchini wameona muitikio mkubwa sana kwa jamii mbalimbali nchi nzima hususani pembezoni mwa nchi.
Kampuni ya Oryx pia  wametoa wito kwa serikali kuzidi kushirikiana nao katika kuhamasisha wananchi katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati mbadala ya gesi. Na pia wameiomba serikali kusimamia Sheria za mazingira kwa ukamilifu ili watu waelewe na waone umuhimu wa kutunza misitu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Afisa Mauzo wa Oryx Gas, Peter Ndoma (kushoto) akimkabidhi jiko na mtungi wake pamoja baada ya kuridhika na kuununua kwa matumizi ya nyumbani  alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya wiki ya mazingira yalifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
Sehemu ya wateja wakihamasika na bidhaa ya gesi ya Oryx walipotembelea maonesho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.  
Afisa Mauzo wa Oryx Gas, Deusdedith Massawe  akiwapatia maelezo jinsi ya kutumia gesi hiyo kwa ufanisi walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya wiki ya mazingira yalifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
Mwakilishi wa Kampuni ya Oryx Gas akiwapatia maelezo jinsi ya kutumia gesi hiyo kwa ufanisi walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya wiki ya mazingira.

MO AANZISHA TUZO SIMBA, KUANZA KUTOLEWA JUNI 11 MWAKA HUU

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii

MWEKEZAJI katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'MO' ameanzisha tuzo zitakazotolewa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki wa klabu ya Simba ambazo amezipa jina la Mo Simba Awards.

Kwa mara ya kwanza tuzo hizo zitatolewa Jumatatu ya Juni 11 mwaka huu katika hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zitakuwa na vipengele 16, ambavyo ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka, Beki Bora wa Mwaka, Kiungo Bora wa Mwaka, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, Shabiki Bora wa Mwaka na Tuzo ya Heshima.

Pia tuzo zingine ni Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka, Tuzo ya Benchi la Ufundi, Kiongozi Bora wa Mwaka, Tuzo ya Wasimamizi wa Mchakato wa Mabadiliko, Mhamasishaji Bora wa Mwaka katika Mitandao ya Kijamii, Mhamasishaji Bora wa Mwaka na Tawi Bora la Mwaka.

Washindi wa tuzo hizo watatokana na kura ambazo zitapigwa na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii na tovuti ya mosimbaawards.co.tz na kamati maalumu ya tuzo ambayo itahusisha wadau mbalimbali wa mchezo wa mpira wa miguu nchini.

Akizungumza kuhusu tuzo hizo, Dewji amesema ameanzisha tuzo hizo kwa lengo la kutambua mchango wa wachezaji, viongozi na mashabiki ambao juhudi zao zimeiwezesha Simba SC kupata mafanikio iliyonayo sasa.

Dewji amesema tuzo hizo ni sehemu ya mikakati yake ya kuifanya klabu ya Simba kuwa timu kubwa barani Afrika, ambayo itakuwa na uwezo wa kifedha ambao utaiwezesha kuwa na wachezaji na benchi la ufundi bora ambalo litaiwezesha kushinda mataji makubwa.

"Simba ni timu kubwa inastahili kuwa na tuzo zake ambazo zitakuwa zinatolewa kwa kutambua mchango wa wenzetu ambao umetuwezesha kupata mafanikio haya ikiwepo kushinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Ni jambo ambalo litawatia moyo kuendelea kujituma lakini hata kwa ambao watakosa itawatia hamasa na hivyo kuongeza juhudi," amesema Dewji.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo itakuwa mbashara kupitia Azam.

Katibu Mkuu mpya UWT akabidhiwa Ofisi rasmi,awataka wanawake kushikamana kujiletea maendeleo.

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Gaudencia Kabaka akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa Katibu Mkuu mpya wa Umoja huo Mwalimu Queen Mlozi pamoja na kukabidhiwa Ofisi rasmi hapo jana jijini Dar.
Katibu Mkuu UWT aliemaliza muda wake Amina Makilagi akimuelekeza jambo Katibu Mkuu mpya UWT Mwalimu Queen Mlozi wakati wa mabdhiano ya Ofisi hapo jana Jijini Dar es salam,Mlozi ,amewataka wanawake kuwa wamoja na kushikamana katika mambo mbalimbali ya kujiletea maendeleo.
Katibu Mkuu UWT aliemaliza muda wake Amina Makilagi pichani kulia akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu Mpya Mwalimu Queen Mlozi hapo Jana katika ofisi za Umoja huo Jijini Dar es salam.
Wakiwa katika picha ya pamoja Uongozi wa sasa na Uliopita wa UWT

DC CHEMBA AWASHAURI WANAWAKE KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KUJENGA UCHUMI, UJASIRIAMALI

$
0
0
Na Shani Amanzi-Chemba.

MKUU wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga amewataka wanawake washiriki  kikamilifu katika shughuli za kiuchumi ukiwamo ujasiriamali  hasa kwa kuzingatia sehemu kubwa ya viwanda vidogovidogo vinaajiri wakina mama hasa Viwanda vya shughuli za mikono.

Odunga ametoa kauli hiyo leo wilayani hapo ambapo amesema shughuli ndogondogo za kiuchimi zinampa faida kubwa mhusika hasa akiwa mbunifu mzuri  na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli unaendelea kuwapa kipaumbele wakina mama na vijana kwa kuwapa mitaji.

"Na kwa hapa Chemba Serikali yetu inaendelea kuangalia ni namna gani wanaweza kuzidi kuwasaidia wakinamama.Ni vema kutumia muda wao kujifunza zaidi kuhusu ujasirimali una faida kubwa ,"amesema.

Kwa upande wa Mratibu wa Taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo Ulingo, Saum Rashidi amesema lengo la kwenda Chemba ni kuwafikia wanawake walioko pembezoni ili kuwawezesha katika mafunzo ya uongozi, jinsia na ujasirimali.

Amesema lengo wanapokuwa viongozi wamudu majukumu yao kama wanawake viongozi na wawe mfano wa kuigwa ndani ya jamii husika.

Amefafanua taasisi hiyo ipo jijini Dar es Salaam na ni jumuiya ya wanawake na kwamba  wanatoa mafunzo kwa wanawake wote bila kujali itikadi za vyama.

"Na kwa hapa Chemba mafunzo hayo ya ujasirimali yamefanyika ndani ya siku mbili kuanzia Juni 5 hadi Juni 6 mwaka huu katika ukumbi wa Godown, Chemba,"amesema.
MKUU wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga akizungumza kwenye semina ya Ujasirimali huku akiwataka wanawake washiriki  kikamilifu katika shughuli za kiuchumi ukiwamo ujasiriamali  hasa kwa kuzingatia sehemu kubwa ya viwanda vidogovidogo vinaajiri wakina mama hasa Viwanda vya shughuli za mikono.
Mratibu wa Taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo Ulingo, Saum Rashidi akizungumza kwenye semina ya ujasiriamali iliyohusu mada mbalimbali ikiwemo kuwafikia wanawake walioko pembezoni ili kuwawezesha katika mafunzo ya uongozi, jinsia na ujasirimali.
Baadhi ya akina Mama wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Semena hiyo ya Ujasiriamali.

WAFANYABIASHARA KATIKA MINADA WILAYANI WATAKIWA KULIPA USHURU

$
0
0
Na Shani Amanzi

WANANCHI wa Wilaya ya Chemba wameshauriwa kutumia fursa ya minada midogo inayozunguka wilayani humo kwa lengo la kufanya shughuli za kimaendeleo ili kukuza uchumi hasa katika shughuli za kibiashara huku wakihamasishwa kulipa kodi.

Hayo yamesemwa na Ofisa Minada wa Wilaya ya Chemba Elisante Sendato wakati alipokuwa katika mnada wa Paranga hivi ambapo amefafanua kwa upande wao watasimamia vema shughuli za mnada ili ziende sawa hasa kwa watendaji na wataalam wanaokusanya mapato kwa kutumia mashine maalum.

Sendato amesema kuwa " pia tunaendelea kutekeleza agizo la Halmashauri kwa kila mnada lazima uwe na choo ambapo agizo hilo lilitoka Januari mwaka huu na kwa upande wa Paranga ujenzi wa vyoo upo kwenye hatua za mwisho,"

Kuhusu mafanikio amesema ni makubwa kwani huduma ya kisoko majumbani, ajira kwa wakazi wa Paranga na kupatia mapato Halmashauri ya Chemba imeongezeka.

Wakati huohuo Diwani wa Kata ya Paranga Hamis Ninga amewataka wafanyabiashara wawe na moyo wa kulipia ushuru wa bidhaa wanazouza na kuhakikisha .Pi wamefanya mkutano na viongozi wa minada ili kuhamisisha wenye biashara kutambua wanao wajibu wa kulipa ushuru.
 Ofisa Minada wa Wilaya ya Chemba Elisante Sendato

PROFESA WA WATOTO MUHAS ATOA UFAFANUZI UGONJWA WA USONJI,MATUNZO KWA WATOTO WENYE USONJI

$
0
0
Prof. Karim Manji, Profesa na Daktari Bingwa wa Watoto akitoa mada ya usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania katika ukumbi wa mihadhara MUHAS.
Kutoka kulia mstari wa kwanza Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Machapisho MUHAS, Dkt. Bruno Sunguya na Mkuu wa Skuli ya Tiba MUHAS, Prof. Sylvia Kaaya wakifuatalia mada ya usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania katika ukumbi wa mihadhara MUHAS.
Kutoka kulia mstari wa mbele, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitafiti, Prof. Appolinary Kamuhabwa, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Andrea Pembe, Mwenyekiti wa mhadhara wa usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania, Prof. Gad Kilonzo na Rais wa Jumuiya ya Alumni wa MUHAS, Prof. Charles Mgone wakifuatilia mhadhara.
Kutoka kushoto mstari w.a kwanza, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Mipango, Fedha na Utawala, HKMU, Prof. Ndosi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Prof. Yunus Mgaya wakimsikiliza Prof. Karim Manji akitoa mada katika ukumbi wa mihadhara MUHAS
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa mhadhara wa usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania, Prof. Gad Kilonzo iliyotolewa na Idara ya Watoto MUHAS.
Prof. Karim Manji akimsaidia Mwenyekiti wa mhadhara wa usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania, Prof. Gad Kilonzo akionyesha zawadi ya saa yenye alama (symbol) ya usonji aliyopewa.
Idara ya Watoto MUHAS wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki (aliyeketi katikati), Mwenyekiti wa mhadhara wa usonji (autism), Prof. Gad Kilonzo (wa tatu kushoto), Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Andrea Pembe (wa pili kushoto), Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitafiti, Prof. Appolinary Kamuhabwa (kushoto), Prof. Karim Manji, Profesa na Daktari Bingwa wa Watoto MUHAS (wa tatu kulia), Rais wa Jumuiya ya Alumni wa MUHAS, Prof. Charles Mgone (wa pili kulia) na Mkuu wa Skuli ya Tiba MUHAS, Prof. Sylvia Kaaya (kulia).

Why you should watch the World Cup on a Smart TV

$
0
0
Smart TVs are the rave of the season and rightly so. Gone are the days when you turn on the television waiting for the channel to start broadcasting. 

Now, the power is in your hands! These devices earned their place by distinguishing themselves from the rest with key features. They have integrated internet and interactive web features. Smart TVs are a combination of flat screen televisions and computers. However, as beautiful and aesthetically appealing as these devices are, they are high-end devices and so come with a hefty price.

For smart TVs, their operating system is preloaded i.e. software apps can be preloaded to the device and updated through an app store similar to smartphones. These devices provide access to content stored on external devices such as an external hard drive and internet applications like YouTube such that one can connect to the internet on the smart TV to watch a YouTube video. Some even enable speech recognition and gestures. The possibilities on these devices are endless!

Features of Smart TVs

Shape: The smart TV is slim. It has no bulge at the back and this makes it easy to fit to the wall. Some have a small stand beneath and can be balanced on a TV stand.

HD Picture Quality: This is perhaps one of the best features of the smart TV. Its high definition picture quality helps the viewer to see a much clearer picture. The picture is brightened than ever before.

Internet access: 
Operating system

Social networking: Some come pre-packaged with room for extension. This addition may provide an interaction between on-screen content and other viewers, something that is not available to most televisions. It also gives room to enjoy a cinematic experience in the comfort of your home, a feature unavailable to computers.

Advertising: Some products support interactive advertising with local advertising insertion. This provides more possibilities in terms of consumer call-to-action and measurement solutions for ad campaigns.

Miracast: This is a standard for wireless connections from other devices such as smartphones to display on smart TV.

With the above features, you might wonder just how much you would need to spend to get one of these high-end devices. Well, the good news is that some of these devices are affordable. 

Five (5) affordable Smart TVs: Sharp LE280X (32 Inches); TCL D2910 (32 Inches); LG 32LJ57M; Hisense & LG.

Want to purchase one of these? Jumia has all of these and more! One will be delivered to your doorstep if you require. Find more categories on the website to make your shopping experience enjoyable.
 

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu baadhi ya watoto walioletwa kwa matibabu katika hospitali ya CCBRT kama wagonjwa wa nje,kulia anayetoa maelezo ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa CCBRT Bw. Erwin Telemans. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Luke Maulid mwenye umri wa miaka 4 kutoka Mtwara ambaye anapata matibabu ya mguu katika hospitali ya CCBRT. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Binti wa miaka 11 anayefahamika kwa jina la Maureen Mbilinyi mkazi wa Mbezi ambaye anapata matibabu ya kuondoa uvimbe jichoni katika hospitali ya CCBRT. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bibi Helena Mjinja mwenye umri wa miaka 64 kutoka Musoma anayepata matibabu ya Fistula katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanawake ambao wamepata matibabu ya Fistula na kupona na kisha kufundishwa kazi za mikono katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw.Erwin Telemans juu ya utengenezaji wa viungo bandia vinavyotengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia watoto Mussa Hussein (kulia) mwenye umri wa miaka 8 mkazi wa Kigamboni na Abdul Hamad (kushoto) mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa Yombo Vituka wakicheza mpira kwa kutumia miguu maalum, Makamu wa Rais leo alifanya ziara kwenye hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya utengenezwaji wa macho bandia kutoka kwa Mtaalamu wa Macho wa Hospitali ya CCBRT Bi. Rehema S. Semindu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi na wagonjwa wa hospitali ya CCBRT mara baada ya kumaliza kutembelea hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

TaGLA YASHIRIKI SEMINA YA UKUAJI WA MIJI NA MAJIJI KUTOKA KOREA KUSINI

$
0
0
Na Leandra, Gabriel, Blogu ya jamii

Tanzania Global Learning Agency (TaGLA) ambayo inajishugha na mafunzo kwa njia ya mtandao nchini leo wameshiriki semina iliyoshirikisha nchi 15 duniani.

Huku Tanzania ikiwa nchi pekee iliyoshiriki barani Afrika kwa kukutana kupitia mtandao na kujadili masuala mbalimbali ya ukuaji wa miji huku Korea kusini wakiwa wenyeji wa semina hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa mafunzo ya mtandao Charles Senkondo ameeleza lengo la semina hiyo iliyoendeshwa na Profesa Heungsuk Choi kutoka Chuo kikuu Korea ni kuangalia mipango mizuri ya ardhi ya jiji na majiji kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye na hata kuleta mvuto kwa wawekezaji.

Ameeleza semina hiyo iliyokuwa inaendeshwa kwa njia ya mtandao wamejifunza kutoka Korea kusini katika kukua kwa miji na majiji hasa wakati huu ambapo taifa limejipanga kukua kiuchumi na upangaji wa miji.

Aidha amesema kuwa wataalamu mbalimbali wameshiriki na wanataraji hapo baadaye washiriki wachache wataenda Korea kujifunza kuhusiana na semina hiyo.Pia semina hizo zitaendelea hadi Agosti mwaka huu, hivyo wadau wajitokeze kujifunza na ametoa rai kwa wananchi kuhusu kubadilika na kujifunza kwani kwa sasa dunia imekuwa kama kijiji.Hivyo kupitia TaGLA wananchi wanaweza kujifunza na kuona ushindani wa kiuchumi kidunia.

Kwa upande wa Ignance Mchallo ambaye ni Mshauri wa mazingira kutoka Legendary International Ltd ameeleza na ameshauri katika kugawana madaraka na utekelezaji wa mipango hasa katika serikali za mitaa kwa kufanya kazi zao katika kukuza maeneo wanayosimamia.

Ameongeza kuwa maendeleo na mazingira ni vitu vinavyoenda sambamba na lazima mazingira yahifadhiwe na kupangwa vizuri ili kuvutia uwekezaji na kuyatunza kwa matumizi ya kizazi cha baadaye.

Naye Mwanasheria mwandamizi wa NEMC Manchare Heche ameeleza kufurahishwa na semina hiyo na kueleza kuwa kama taifa lazima tujifunze katika kupanga miji na majiji na kuhifadhi mazingira hasa katika kipindi hiki ambacho taifa limedhamiria katika kukuza uchumi na mazingira hasa ardhi lazima yatunze kwa kuvutia wawekezaji na kwa manufaa ya vizazi vya baadaye na wananchi wapende kujifunza kwa njia ya mtandao kupitia TaGLA.

Mwanasheria wa Mwandamizi (NEMC)Manchare Heche akichangia mada katika mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15 leo jijini Dar as Salaam.
Wandau wa mazingira wakisikiliza mada mbalimbali katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao uliOhusisha nchi 15 leo jijini Dar as Salaam.
Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles Senkondo (katikati) akifafanua jambo mara baada ya mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15, leo jijini Dar as Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mazingira kutoka Legendary International,Ignace Mchallo na (kulia) Mwanasheria Mwandamizi (NEMC) Machare Heche.
Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles Senkondo akizungumza na mwatendaji mbalimbali waliohudhuria mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15,Mwenyeji ikiwa ni nchi ya Korea kusini leo jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)Mshauri wa Mazingira kutoka Leogendary Intanational, Ignace Mchallo akijibu maswali aliyoulizwa na wadau wa mazingira katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao ambao ulihusisha nchi 15,huku mwenyeji wao ikiwa ni Korea kusini leo jijini Dar as Salaam.

Viongozi wa elimu Geita wapatiwa mafunzo kukabiliana na Malaria

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania APHFTA, imeanza kutoa mafunzo kwa viongozi wa elimu mkoani Geita ili kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani humo. 

 Viongozi wanaopatiwa mafunzo ni pamoja na Waalimu 100 wa Malaria (Afya) kwa shule za msingi, Waalimu Wakuu 100 wa shule za msingi, Waratibu Elimu Kata 66 pamoja na Waratibu Elimu sita kutoka halmashauri zote mkoani GHeita. 

 Akizungumza juzi kwenye kilele cha mafunzo ya siku mbili kwa washiriki kutoka halmashauri za Nyang’hwale, Geita DC, Geita Mji pamoja na Chato, Kaimu Mganga Mkuu mkoani Geita Dr.Moses Simon ambaye pia ni Mratibu Malaria mkoani humo alisema hatua hiyo imelenga kufikisha elimu hadi ya shule ili kusaidia kushusha kiwango cha maambukizi ya Malaria ambapo takwimu za mwaka 2017/18 zinaonyesha mkoa huo ni wa pili kitaifa kwa kiwango cha juu ukiwa na asilimia 17.3 ukitanguliwa na mkoa wa Kigoma wenye asilimia24.3.

 Mratibu wa Afya kutoka taasisi ya APHFTA, Dr.Berezy Makaranga alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ushirikishwaji wa sekta binafi ya afya katika kupambana na ugonjwa Malaria ukilenga kusaidia kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuwashirikisha wanajamii namna bora ya kujikinga. 

 Washiriki wa mafunzo hayo waliahidi kutumia vyema elimu na vitendea kazi ikiwemo bandokitita walivyopewa na kufikisha elimu ya kupambana na Malaria kwa wanafunzi pamoja na wanajamii na hatimaye kushusha kiwango cha maambuzi ya ugonjwa huo mkoani Geita. 

 Mafunzo hayo yaliratibiwa na Chama cha Watoa Huduma za Afya Tanzania APHFTA kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) na yanaendelea katika halmashauri za Bukombe na Mbogwe. 

ZIMAMOTO NCHINI YAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA

$
0
0
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini kutoka katika Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo. Tuzo hiyo imepokelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es salaam.

Akizungumza Kamishna Jenerali baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho. Alisema, anawashukuru Taasisi hiyo kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi nyingi ambazo taasisi hiyo imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo ikiwepo kampeni ya kuitangaza namba ya simu ya dharura 114.

Kamishna Jenerali Andengenye, amezitaka Taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzifufua Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili kuongeza idadi ya vifaa hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga ya moto. ‘‘Jamii ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo (Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya moto yanapotokea’’.

Ni vema sasa mamlaka zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye miji 
na majiji ikazingatia wanapotengeneza miundo mbinu hiyo, wakumbuke kuweka na mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha wamiliki wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya maji.
 Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (wapili kulia) akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye tuzo ya cheti cha heshima, kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. 
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akionesha zawadi ya fulana ya mabalozi wa Taasisi ya Salama Salimini aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (kushoto), kama alama ya kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji, (kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti cha heshima kutoka kwa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (wapili kushoto), (kulia) Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo Billy Mwakatage, (kushoto) Kamishna wa Usalama Dhidi ya moto Jesuald Ikonko na (wapili kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)


KONGAMANO LA KIMATAIFA KUHUSU MAHAKAMA NA JINSIA KUFANYIKA WIKI IJAYO JIJINI ARUSHA

$
0
0

 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi(katikati) akizungumzia jambo wakati  na waandishi wa habari  leo Juni 7 ,mwaka huu  kuhusu Mkutano wa  Kimataifa utakaojadili  masuala ya Kijinsia, utakaoanza Juni 11 hadi 13, mwaka huu  mkoani  Arusha.Kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama  ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati na (kushoto) ni  Katibu wa Jaji Kiongozi, Dustan  Ndunguru.
 Kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama  ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Juni 7, mwaka huu kuhusu  Mkutano wa  Kimataifa utakaojadili  masuala  Kijinsia,( katikati) ni  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi na (Kushoto) ni Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe .Dustan  Ndunguru.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsiliza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye hayupo  pichani, wakati alipofanya mkutano  na waandishi hao.
(Picha na Mary Gwera)

Na Lydia Churi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Kongamano la kimataifa kuhusu Mahakama na Jinsia Barani Afrika litakalofanyika kwa mara ya kwanza nchini na katika Bara la Afrika kuanzia Juni 11 hadi 13 jijini Arusha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amesema kongamano hilo litahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 200 wakiwemo Majaji Wakuu, Majaji, Mahakimu na wadau wengine kutoka nchi 51 barani Afrika.

Jaji Kiongozi amesema pamoja na wajumbe hao, kongamano hilo pia litahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bi. Sandie Okoro ambaye tayari ameshawasili nchini.

Malengo makuu ya Kongamano hilo ni nchi za bara la Afrika kubadilishana uelewa kuhusu changamoto za jinsia na upatikanaji wa haki, kubadilishana uzoefu na mikakati ya kimataifa ya kusukuma mbele ajenda ya jinsia ili kuendeleza sekta ya sheria na kuwapa washiriki nafasi ya kujadili masuala yahusuyo jinsia na upatikanaji wa haki.

Jaji Kiongozi amesema kongamano hilo pia linatarajiwa kujenga ushirikiano baina ya Mataifa katika kuleta usawa wa kijinsia na kuyafanya masuala ya jinsia kuwa sehemu muhimu ya mfumo wa Mahakama. Aidha, kongamano hilo pia litatoa fursa kwa Majaji Wakuu na wadau wengine muhimu kwenye sekta ya sheria kufahamiana na kubadilishana uzoefu.

Akifafanua, Dkt. Feleshi amesema kongamano hilo litajadili masuala muhimu ya jinsia na upatikanaji wa haki na litajikita katika masuala muhimu ya kijinsia ndani ya Mahakama na sekta ya utoaji haki kwa ujumla, ikiwemo umuhimu wa jinsia katika Mahakama, upatikanaji wa haki kwa wanawake na ukatili wa kijinsia.

Amesema kongamano hilo ni alama muhimu katika historia ya Mahakama ya Tanzania kwa kuwa linatarajiwa kutoa mchango utakaoleta mabadiliko makubwa ya kisera kuhusu jinsia na upatikanaji wa haki barani Afrika kwa kuwa ukatili wa kijinsia ni changamoto ya dunia inayohitaji mikakati ya kimataifa na kikanda ili kukabiliana nayo.

Kongamano hilo la siku tatu la kihistoria nchini limeandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia pamoja na wadau wengine ikiwemo Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) na chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).

WAZIRI MWIJAGE AIPONGEZA KAMPUNI YA TOTAL KWA KUZINDUA MAFUTA YA MAGARI RAFIKI KWA MAZINGIRA

$
0
0
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafuta ya Total Excellium ya petrol na Diesel ambayo yana uwezo wa kusafisha injini na kuiwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu, wengine ni Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredric Clavier (watatu kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Total nchini Tarik Moufaddal  (watatu kutoka kulia).
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akitoa huduma ya kujaza mafuta kwenye gari la mmoja wa wateja wa Total wakati wa uzinduzi wa mafuta ya Total Excellium ya petrol na Diesel uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mafuta hayo yana uwezo wa kusafisha injini na kuiwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Total nchini Tarik Moufaddal na ni Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredric Clavier. 


 Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya mafuta ya TOTAL kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kuwa watanzania wanapata mafuta bora ya vyombo vya moto. Mwijage alizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa mafuta ya vyombo vya moto aina ya TOTAL Excellium kutoka kampuni ya mafuta ya TOTAL. 

Mafuta hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya ubora wa juu ya kimataifa ya TOTAL EXCELLIUM, kwa bidhaa zinazotumia mafuta ya Petroli na Diesel katika soko la Tanzania. “Uzinduzi wa mafuta haya umekuja wakati muafaka kwani sasa tuko kwenye wiki ya mazingira na mafuta haya yanapunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na vyombo vya moto, nawapongeza kampuni ya TOTAL kwa kuwaletea watanzania bidhaa bora, na mimi na utaalamu wangu wa mafuta nafahamu hii ni hatua kubwa sana kwenye teknolojia ya kuboresha mafuta,” alisema Mwijage.

 Mafuta haya mapya yana uwezo wa kusafisha injini na kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu, kuwezesha matumizi kidogo ya mafuta na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na moshi wa vyombo vya moto. Mafuta ya TOTAL EXCELLIUM yanapatikana katika vituo vyote vya kuuza mafuta vya kampuni ya TOTAL kwa gharama ya bei ya kawaida ya mafuta kwenye soko. 

 Tarik Moufaddal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya TOTAL nchini anasisitiza, “Kuzinduliwa kwa TOTAL EXCELLIUM, katika soko la Tanzania ni hatua mpya na muhimu kwetu nchini hususani katika kufanikisha dhamira yetu ya kuingiza bidhaa bora za nishati. Tunayo dhamira ya kuwapatia wateja wetu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, sambamba na huduma bora kupitia mtandao wetu ambao umeenea nchini kote, uzinduzi wa TOTAL EXCELLIUM, unadhihirisha kuwa tumejipanga kuleta mapinduzi yenye kuleta manufaa katika sekta ya mafuta nchini.”

 "TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa teknolojia ya juu ya kisasa ambayo inawezesha kusafisha injini, kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu bila kuchoka, matumizi kidogo ya mafuta kuendesha injini, kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na moshi na ni mazuri kwa matumzi ya aina zote za magari kuanzia madogo mpaka makubwa,” aliongeza Tarik. “Uzinduzi huu ni moja ya ubunifu mkubwa wa kampuni uliolenga kuhakikisha wateja wetu wanapata bidhaa bora na kuwawezesha matumizi kidogo ya mafuta yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya Excellium. 

TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa ubunifu wa teknolojia za kisasa zenye kuleta ubora. Timu yetu ya wataalamu wa utafiti wamefanikisha kutengeneza mafuta haya kukidhi mahitaji ya wateja wetu wanaotumia magari ya kisasa ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika matunzo ya injini kwa matumizi yao ya kila siku”  Mkurugenzi wa Mtandao wa TOTAL wa Nikesh Mehta. “Zaidi ya watafiti makini na wataalamu wenye uzoefu mbalimbali wanafanyia kazi suala la kuleta bidhaa za mafuta na vilainishi vya injini na mitambo zenye ubora mkubwa zaidi katika kituo chetu cha utafiti cha Solaize,nchini Ufaransa.

Wataalamu hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili kuboresha mafuta ya TOTAL EXCELLIUM. Zaidi ya kanuni za kisayansi 2,300 zimefanyiwa majaribio katika maabara kwa zaidi ya masaa 6,000 na mafuta haya yamefanyiwa majaribio ya awali barabarani kwa zaidi ya masaa 8,500 sawa na kilometa 300,000. Haya yote yanathibitisha uhakika na ubora wa mafuta ya TOTAL EXCELLIUM na yanasafisha injini za magari na kupunguza uharibifu wa mazingira,” anasema Marsha Msuya, Mkurugenzi wa Masuala ya Ndani ya kampuni ya TOTAL.

WATU WATATU KWENDA URUSI KWENYE KOMBE LA DUNIA 2018 KUPITIA PROMOSHENI YA BIA YA KILIMANJARO LAGER

$
0
0
Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo akitoa ufafanuzi wa promosheni ya Kilimanjaro kwa waandishi wa habari,kulia ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha,Hamidu Semvua na Raj Chandarana aliyeko kwenye mafunzo chini ya mpango wa Global Management Trainee katika kampuni ya TBL.
Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo na Raj Chandarana kutoka TBL wakijadiliana jambo.
Zoezi la droo ya kupata washindi ikifanyika kupitia teknolojia za kisasa.
Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo akiongea kwa simu na mmoja wa washindi wa droo kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro.

Wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam na mmoja wa mkoa wa Geita wameibuka wamejishindia tiketi na kugharamiwa safari ya kwenda, Urusi, kuona michuano ya Kombe la Dunia, mubashara kupitia promosheni inayoendelea ya bia rasmi ya Tanzania, katika msimu huu wa Kombe la Dunia ya Kilimanjaro Lager. 

Droo ya kuwapata washindi hao imefanyika jijini Dar e Salaam, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Taifa na kushuhudiwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Washindi katika droo hiyo wametajwa kuwa ni Charles John (Geita), Kaijage Kironde (Dar es Salaam) na Leodgard Isaac (Dar es Salaam). 

Washindi hao walipokea habari hizo kwa furaha baada ya kupigiwa na Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo,ambapo walieleza kuwa wanaisubiri safari yao kwa shauku kubwa na kuwataka wateja kuendelea kuchangamkia promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa mapema mwezi uliopita. 

Promosheni hiyo inaenda sambamba na kujishindia muda wa maongezi 2,500/= kila wanaponunua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara (sita) 6 kutuma number iliyopo chini ya kizibo kwenda 15451 fedha taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/- Kila wiki kwa wiki kumi. Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, alisema, washindi wapatao 10 watawezeshwa kugharamiwa kuona mashindano ya kombe la Dunia na washindi wengi wataweza kujishindia fedha taslimu, na muda wa maongezi. 

“Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018”, alisisitiza. Ili kujishindia zawadi mteja anapaswa kutuma namba zilizopo kwenye chupa za bia ya Kilimanjaro kwenda namba 15451 ili kujipatia fedha taslimu na muda wa maongezi, zawadi ya tiketi ni kwa wale wataoshiriki kujibu maswali yatakayoendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.Kililager.com na kujipatia pointi za ushindi. Promosheni hii itadumu kwa muda wa miezi miwili na nusu na itaendeshwa nchi nzima na matangazo yake yanaendelea kutangazwa rasmi kupitia televisheni, radio na mitandao ya kijamii.

WAZIRI MKUU AZIONYA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka asasi zisizokuwa za Serikali (NGOs) zitekeleze majukumu yake kama ambavyo zimesajiliwa na ziache kufanya shughuli zilizo nje ya makubaliano.


Amesema Serikali itaendelea kuzichukulia hatua NGOs zote zinazokiuka taratibu kwa kufanya majukumu mengine kinyume na malengo yake.Ametoa onyo hilo leo (Alhamisi, Juni 7, 2018) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Longido, Dkt. Stephen Lemomo Kiruswa kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

“Serikali itaendelea kuzifuatilia NGOs zote zinazokiuka taratibu na kufanya majukumu mengine yanayozua mitafaruku kwenye jamii na Serikali,” amesema.Dkt. Kiruswa alitaka kufahamu ni lini Serikali itazifutia usajili NGOs zote ambazo kwa muda mrefu zimeacha kutekeleza majukumu yake na badala yake zinafanya shughuli za uchochezi.

Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ina utaratibu wa kufuatilia taasisi hizo kubaini endapo zinafanya kazi kama zilivyojieleza kwenye usajili wake.Amesema mara inapobainika kwamba kuna NGOs ambazo zimeacha majukumu yake na zinafanya shughuli zingine nje ya mikataba yao, hatua stahiki huchukuliwa, hivyo alizitaka zijikite katika utoaji wa huduma bora kwa jamii.

“Kwa hiyo nitoe wito kwa NGO’s zote ambazo Serikali imeridhia na tumezisajili ili ziweze kufanya kazi ya kutoa huduma za jamii, zijikite kutoa huduma za jamii kama ambavyo tumekubaliana, ili tuweze kufikia malengo ya pamoja kati ya Serikali na taasisi zisizo za kiserikali katika kutoa huduma kwa Watanzania wote,” amesema.

Akitoa mfano wa hatua ambazo zimeshachukuliwa na Serikali kwa asasi zinazokiuka makubaliano, Waziei Mkuu amesema aliwahi kuzuru wilaya ya Loliondo na kukuta kuna utitiri wa NGOs ambazo zilikuwa zinaenda kinyume na malengo yaliyokusudiwa.

“Niliwahi kutembelea wilaya jirani na yako pale Loliondo; nilikuta kuna NGOs 39 katika wilaya moja tu. Na kulikuwa na migogoro kadhaa ambayo baadhi ya NGO’s, kama ambavyo umesema, zimekuwa zikiacha majukumu yake na kufanya majukumu mengine ambayo ni nje ya utaratibu tuliokubaliana. Kauli niliyotoa, ilikuwa kwanza kuwatahadharisha, lakini pili tulipeleka wakaguzi kujiridhisha kama ni kweli jambo hilo linafanyika; na tatu tulichukua hatua kwa NGO’s ambazo zilibainika kujishughulisha na mambo mengine nje ya kazi zao,” amesema.

Amesema anatambua mchango unaotolewa na NGOs katika kuisadia Serikali kutoa huduma za jamii kwenye maeneo mbalimbali hasa yale ambayo Serikali haitamudu kufanya kila kitu kwa asilimia 100. “Serikali imezipa fursa taasisi hizi zisizokuwa za kiserikali, zenye fursa na utaalamu wa kutoa huduma kwa jamii, na sisi tumetoa ruhusa kisheria kabisa kwa kusajili taasisi hizo ili ziweze kufanya kazi hizo,” amesema.

“Sasa kwa kuwa taasisi hizi zimesajiliwa, na taasisi hizi zina malengo, na malengo yale ndiyo yaliyofanya tuwape kibali ili ziweze kusajili, naamini kila NGO’s inajua wajibu wake. Zitimize wajibu wake ili tuweze kufikia malengo ya pamoja kati ya Serikali na taasisi zisizo za kiserikali,” amesisitiza.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 7, 2018.

JAMII ISHIRIKISHWE MABADILIKO TABIA NCHI KUWA NA KILIMO CHENYE TIJA

$
0
0





Mshehereshaji wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, Mtafiti mshiriki wa ESRF, Abdallah Henku akitoa utambulisho wa wanenaji wa mdahalo huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.




Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.




Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba akizungumzia malengo ya warsha wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.




Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.






Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo Bi. Shakwaanande Natai akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa sera ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa nchi kwenye mikutano ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Richard Muyungi akizungumzia vionjo vinavyotarajiwa kufanywa kuhusu uhifadhi wa mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (wa pili kushoto) akifafanua kanuni za kufauta katika kuhifadhi mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Tafiti zilizoanishwa ESRF, Bi. Vivian Kazi (kulia), Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (wa tatu kulia), Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba (wan ne kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango (kushoto) akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale akifafanua jambo wakati majadiliano kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mshiriki akichangia mada wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya washiriki kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (katikati) akibadilishana mawazo na Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (kushoto) wakati wakielekea kwenye eneo la kupiga picha ya pamoja kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.








JAMII inayojitambua ndiyo inayoweza kutumika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha kushindikana kwa mipango mingi ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira kunatokana na uelewa duni na mipangilio isiyozingatia mahitaji halisi ya wananchi wa maeneo husika.

Kauli hiyo imo katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ofisi za ESRF.Katika mdahalo huo uliowezeshwa na Shirika la Kimataifa la Care kwa kushirikiana na taasisi ya FANRPAN na ESRF imeelezwa kuwa kuna changamoto kubwa kwa maendeleo ya kilimo na ukuaji wake kutokana na n chi nyingi Kusini mwa Afrika kutegemea mvua.

Aidha ilielezwa kuwa changamoto nyingine ni umaskini uliokithiri, upungufu nmkubwa wa raslimali watu, maandalizi hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na miundombinu dhaifu.Mmoja wa watoa mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko alisema kwamba kumekuwa na kulegalega kwa matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira miongoni mwa wananchi na uwezeshaji kwa watendaji kiasi cha kuharibu muitikio unaonekana wakati wa mafunzo.

Chinoko alisema kwamba kutokana na hali hiyo walibuni kanuni ambazo wao wanaziita SUPER kanuni ambazo zikifuatwa vyema zinajibu matatizo yaliyopo sasa. Alisema kwamba Super ni mfumo wa uchakataji wa taarifa na utekelezaji wake unaolenga kuwafikia wananchi wa pembezoni ambao ndio washiriki wakubwa wa utunzaji wa mazingira na uzalishaji wa chakula.

Alisema kwa kutumia kanuni hizo wananchi wanaweza kutambua mwendelezo wa rasilimali ardhi na misitu waliyonayo, wakawezesha kuitumia kwa faida kutokana na uadimu wake.Aidha kanuni hizo zinahitaji mipango kuzingatia usawa wa kijinsia ili kuteketeleza sera katika uchumi.

Alisema mfumo wa masoko unazungumzwa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa sekta binafsi katika kilimo ili kuipaisha na kuifanya kuwa na tija zaidi.Alisema kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la kuwasilisha taarifa huku watengeneza sera wakiwa pekee yao bila kushirikisha wananchi ambao ndio watendaji wenyewe.

Katika mdahalo huo mada zingine ziliwasilishwa na Bi. Shakwaanande Natai, Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo akishughulikia sera katika kilimo cha kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa nchini Tanzania.

Pia kulikuwa na mada iliyowasilishwa na Bw. Richard Muyungi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais ambaye alizungumzia vionjo vilivyokusudiwa katika kuhakikisha wanazungumza kilimo kinachozingatia mabadiliko hali ya tabia nchi (INDCs) Tanzania.

Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network( FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba alisema kwamba matokeo ya ushauri katika mdahalo huo utafikishwa katika kanda na baadae dunia kwa kuwa utekelezaji wa mashauri hayo ni wa lazima kuzingatia mahitaji ya ulinzi wa mazingira kwa kuzingatia kilimo kinachoangalia mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema kwamba watatumia maazimio na ushauri kutoka katika mdahalo huo katika majukwaa mengine muhimu duniani ambayo yanazungumzia makubaliano ya COP 19 na maazimio ya Lome.Alisema mdahalo huo ni muhimu katika kubaini utayari wa Tanzania na changamoto zake katika kuendesha kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi na kuhakikisha usalama wa chakula na lishe.

Alisema pamoja na kuwepo kwa sera nzuri za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kumekuwepo na hasara kubwa katika kilimo kinachofikia dola za Marekani milioni 200 duniani.Alisema hasara hiyo ni tishio kwa maisha na kusema kwamba ni vyema wataalamu naa wananchi wakazungumzia changamoto zilizopo kwa bara la Afrika ambalo linaweza kulisha dunia nzima kama mipango itachambuliwa ipasavyo kwa kushirikisha wananchi na wagani.

Alisema kilimo lazima kifanywe kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya tabia nchi ili kiwe na tija na kukabiliana na mafuriko, ukame, wadudu na magonjwa yanayotokana na mabadiliko hayo.Bi. Shakwaanande Natai alisema kwamba Tanzania ipo tayari kufanya kilimo cha kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na kuwapo kwa sera na sheria zinazohimiza kilimo chenye tija.

Alisema mipango ya kilimo ya sasa inazingatia mabadiliko hayo pamoja na kutengeneza mfumo wa masoko ili kusaidia watu maskini kabisa wakulima kuwa na uwezo unaotakiwa katika kujisaidia kiuchumi.Bw. Danford Sango akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema kwamba mdahalo huo ni muhimu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio kwa ustawi wa wanadamu.

Aidha aliwakaribisha wataalamu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kushiriki katika mdahalo huo wenye tija kwa mataifa ya Kusini mwa Afrika.

TABOA BADO WASUBIRI KUKUTANA NA WAZIRI MKUU,YAWAOMBA WAMILIKI WA MABASI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA ZA USAFIRI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wasafirishaji wa Mabasi Tanzania(TABOA) Enea Mrutu amewaomba wamiliki wote wa mabasi nchini kuendelea kutoa huduma za kusafirisha abiria kwa umakini wa hali ya juu kwa kuhakikisha hawasababishi ajali wakati wakiendelea kusubiri kukuona na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili watoe kilio chao.

TABOA iliomba kuonana na Waziri Mkuu kwa ajili ya kutoa malalamiko yao kutokana kwa madai kuna sheria na kanuni za usalama barabarani ambazo  ni kandamizi kwao na zimekuwa zikiwaweka katika wakati mgumu katika kutoa huduma ya kusafirisha abiria nchii.

Hata hivyo TABOA bado hawajafanikiwa kuonana naye ingawa tayari ameshawapa maelekezo kuwa wakati wowote atakutana nao na kisha kuwasikiliza ili kupata muafaka kwa kushirikiana na wadau wengine wa usafiri wakiwamo Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(Sumatra).

Akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam Mrutu amesema wanatambua majukumu aliyonayo Waziri Mkuu hivyo wana imani akipata muda watakutana naye na kisha kuzungumza kwa kina kuhusu changamoto ambazo wanakabiliana nazo watoa huduma ya usafiri nchini.

"Ombi letu kwa wanachama wa Taboa waendelee kutoa huduma bora ikiwa pamoja na kuwa makini barabarani ili kuepuka ajali.Tunamatumaini makubwa na Waziri Mkuu, hivyo tunajua akipata muda atatuita ,nasi tupo tunasubiri.Hivyo wakati tunaendelea kumsubiri tuendelee kutoa huduma ya usafiri bila kuchoka,"amesema Mrutu.

Taarifa za awali ambazo Michuzi Blog ilizipata ni kwamba Taboa walitaliwa kukutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki iliyopita lakini hawakufanikiwa kukutana naye kutokana na majukumu aliyonayo, hivyo aliwahakikisha atapanga ratiba ya kukutana nao.

Hata hivyo kwa muda mrefu sasa Taboa na Sumatra wamekuwa katika mvutano wa hapa na pale uliosababisha Chama hicho kutishia kutotoa huduma kwa madai ya kutoridhishwa na faini kuanzia Sh 200,000 hadi Sh 500,000 zinazotozwa kwa mabasi hayo pindi yawapo safarini.

Taboa kupitia kwa Mrutu amesema wanasikitishwa na faini hizo ambazo kibaya zaidi hata wakati wa mchakato wa kuziandaa Sumatra hawakuwashirikisha wadau wa usafirishaji wakiwamo wao na hivyo kuibua malalamiko.

"Mbali ya kutoshirikishwa wakati wa mchakato wa uandaaji wa  faini hizo, pia utaratibu wa faini hizo unakiukwa kwa kuwahusisha wamiliki hata katika makossa yanayowahusu madereva.Pamoja na malalamiko yetu tunaendelea kuwahamisha wanachama wetu waendelee kutoa huduma iliyobora kwa manufaa ya nchi yetu,"amesema.

Wakati huo huo TABOA imesema imesikitishwa na ajali ya basi iliyotokea mkoani Kigoma na kusababisha abiria 10 kupoteza maisha na madereva kuwa makini ili kuepuka ajali za barabarani.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images