Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1594 | 1595 | (Page 1596) | 1597 | 1598 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Greyson Mwase, Ruvuma
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa umeme utakaopelekea mikoa ya Njombe na Ruvuma kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa Septemba, 20 mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litaweza kuokoa shilingi bilioni 30 zilizokuwa zikitumika kama gharama ya kuendesha mitambo ya kuzalishia umeme inayotumia mafuta mazito katika mikoa hiyo.
  Waziri Kalemani aliyasema hayo mapema jana tarehe 04 Juni, 2018 kwa nyakati tofauti kupitia mikutano na vijiji vya Suluti kilichopo wilayani Namtumbo na Lukumbule na Mkowela vilivyopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kwenye ziara yake ya kukagua njia ya Makambako – Songea, vijiji vinavyotakiwa kuunganishwa na umeme wa Gridi ya Taifa pamoja na miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
  Katika ziara hiyo Waziri Kalemani aliambatana na wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakandarasi pamoja na wakuu wa wilaya husika.
  Dkt. Kalemani alisema kuwa, shirika la Tanesco limekuwa likitumia gharama kubwa ya shilingi bilioni 30 kwa mwaka kama  gharama ya uendeshaji wa mitambo inayotumia mafuta mazito katika mikoa ya Njombe na Ruvuma na kusababisha hasara badala ya faida.
  Alisema kuwa, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Makambako, Madaba na Songea mapema mwezi Septemba mikoa ya Njombe na Ruvuma itaunganishwa rasmi na Gridi ya Taifa na kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 30 kinachotumika kuendesha mitambo ya mafuta mazito gharama ambazo ni kubwa tofauti na mapato ya shirika hilo ya shilingi bilioni tisa kwa mwaka kwa mikoa husika.
  Aidha, aliongeza kuwa kuingizwa katika Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Njombe na Ruvuma kutapelekea uwepo wa nishati ya uhakika na kuchochea ukuaji wa uchumi.
   Kazi ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Songea kilichopo mkoani Ruvuma ikiendelea.
   Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake katika kituo cha kupoza umeme cha Songea kilichopo mkoani Ruvuma. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema na kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Umeme wa Makambako – Songea, Mhandisi Didas Lyamuya.
   Sehemu ya wananchi wa kijiji cha  Suluti kilichopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipokuwa akiwaelezea mikakati ya serikali katika upelekaji wa huduma ya umeme vijijini.
   Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akielezea matumizi ya kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa kijiji cha  Suluti kilichopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma (hawapo pichani)
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akielezea mikakati ya Wizara ya Nishati kwenye usambazaji wa miundombinu ya umeme katika mikoa ya Njombe na Ruvuma katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Omela.


  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma

  Wataalam mbalimbali kutoka sekta ya madini nchini wameshiriki warsha maalum iliyotolewa na wataalamu kutoka Australia, kwa lengo la kujifunza uzoefu kutoka nchi hiyo ambayo imepiga hatua kubwa katika sekta husika. Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko alifungua rasmi warsha hiyo ya siku mbili, Juni 4 jijini Dodoma na kusema kuwa Tanzania inahitaji kujifunza zaidi kutoka nchi zilizofanikiwa katika sekta ya madini kama Australia, ili iweze kukuza zaidi mchango wake katika katika Pato la Taifa.

  “Wenzetu Australia, sekta yao ya madini ina mchango mkubwa sana; zaidi ya asilimia 40 kwenye Pato lao la Taifa. Kwa hiyo, tunakutana nao kubadilishana uzoefu, ni namna gani wao wamefanya kuwezesha sekta husika kuchangia kwa kiasi hicho kwenye Pato la Taifa.”

  Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa, suala muhimu ambalo Wizara ya Madini inalisimamia ni kuhusu usimamizi wa rasilimali za madini. Alisema kuwa, lengo jingine la warsha hiyo ni kujifunza Australia imefanya nini katika kusimamia na kutatua migogoro kwenye sekta ya madini, ili Tanzania itumie mbinu hizo kutatua migogoro iliyopo kwenye sekta husika.

  Biteko alitumia fursa hiyo kuiomba serikali ya Australia kuangalia uwezekano wa kuendesha warsha husika kwa wachimbaji wadogo nchini ili wapate maarifa ya namna bora ya usimamizi wa rasilimali za madini. Akizungumzia mchango wa sekta ya madini kwenye uchumi wa viwanda, Biteko alieleza kuwa, rasilimali za madini ni tegemeo kubwa katika kukuza uchumi huo.

  “Ndiyo maana mtaona kwamba tunayo miradi mikubwa ya makaa ya mawe, ambayo inazalisha nishati ya umeme utakaotumika kwenye viwanda vyetu. Kwa hiyo lazima tuisimamie vizuri,” alifafanua. Aidha, aliongeza kwamba, Tanzania ina madini mengi ya teknolojia yakiwemo ya Neobium yanayohitajika sana duniani kwa ajili ya viwanda. Alitaja madini mengine muhimu kwa viwanda kuwa ni Graphite pamoja na Marble, ambayo yote yanapatikana kwa wingi Tanzania.

  Kwa upande wake, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi David Mulabwa, alisema kuwa, warsha hiyo ni muhimu sana katika kuwaongezea watumishi ujuzi na maarifa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za kisekta.

  “Kuna mambo ya mazingira, tozo na kodi mbalimbali katika sekta. Kwa hiyo, jinsi watumishi wanavyokuwa na ujuzi na maarifa, tunaamini watakuwa katika nafasi nzuri ya kufanya ya kufanya maamuzi ambayo yatasaidia kuhakikisha kwamba rasilimali za nchi hii zinalinufaisha Taifa ipasavyo.”

  Awali, mmoja wa waratibu wa warsha hiyo, ambaye ni Afisa kutoka Ubalozi wa Australia kutoka Ofisi ya Nairobi, Deanna Simpson, alieleza kuwa; Serikali ya nchi yake imekuwa ikitoa warsha za aina hiyo katika nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Kenya, Madagascar, Ethiopia na Sudan.

  Aidha, aliongeza kuwa, Australia Magharibi ina kampuni zaidi ya 100 zinazoendesha miradi mbalimbali ya madini zaidi ya 350 katika nchi za Afrika takribani 30 ikiwemo Tanzania. Warsha hiyo ya madini imehitimishwa Juni 5, mwaka huu.


  Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya madini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
  Mtaalamu wa Madini kutoka Australia, Rick Rogerson, akiwasilisha mada katika warsha ya wataalam wa madini nchini (hawapo pichani), iliyofanyika Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
  Kutoka kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi David Mulabwa; Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania, Prof Shukrani Manya wakijadiliana jambo, wakati wa ufunguzi rasmi wa warsha ya wataalam wa madini nchini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), akijadiliana jambo na Mtaalamu wa Madini kutoka Australia, Rick Rogerson, muda mfupi baada ya Naibu Waziri kufungua rasmi warsha ya wataalam wa madini nchini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.


  0 0

  *Tayari maandalizi ya jeneza la kipekee na kaburi kubwa yakamilika, kaburi lao kuzungukwa na makaburi ya mapadre, masista

   Na Ripota Wetu,Iringa

  Tayari Maandalizi ya kuipumzisha Miili ya mapachaa hao yamekamilika baada ya jeneza la kipekee na kaburi kubwa lililochimbwa katika makaburi wanayozikwa masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga kukamilika. 

  Maria na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Tosamaganga watakakozikwa. 

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Shule ya Seminari ndogo ya Tosamaganga Padre Benedict Chavala amesema uamuzi wa mapacha hao kuzikwa Tosamaganga, kutawasaidia kuendelee kuwaombea. Awali kulikuwa na msuguano wa eneo watakalozikwa mapacha hao uliohitimishwa na Mkuu wa Masista wa Shirika la Maria Consolata, Jane Nugi kudai walichagua kuzikwa wanakozikwa viongozi wa kanisa hilo. 

  Msuguano huo pia ulitokana na hatua bibi wa marehemu upande mama yake, kudai miili hiyo isafirishwe kwa ajili ya maziko Bukoba jirani na alipozikwa marehemu mama yao. Alipoulizwa endapo kama itatokea wakasema miili hiyo izikwe Bukoba wakati tayari Iringa wameshachimba kaburi Padre Chavala alisema kuwa itategemea watu hawa wana hoja nzito kiasi gani. 

  “Muda mwingi wamechukuliwa ni watoto wetu nahivyo tunapenda watuelewe kwamba tangu mwanzo kama kanisa liliamua kuwachukua kutokana na mazingira waliokuwa nayo na kuwalea tunasikia ni wanetu na kama ni wanetu basi tubaki nao hapa ambapo wapo mama na bibi zao ambao ni masista ili tuweze kuwakumbuka muda wote.”alisema Padre Chavala na kuongeza: 

  “Wanaendelea kuwa karibu nasi kuliko kupelekwa huko hata pengine hawajawahi kufika,kila mmoja atawashangaa inakuwaje hawa watu wanakuja wakiwa wamefariki wakati wakiwa wazima hawajawahi kufika,na kilio ni kilio,msiba ni msiba wakubali tu wazikwe hapa ni pazuri zaidi hata wao wenyewe waje tulie pamoja.”alisema Padre Chavala 

  Alisema masista walio walea kwa muda mrefu tayari ni wazee kuwapeleka hukombali hao masista watajisikia wapweke zaidi kwa sababu wameachana na wapendwa wao halafu kuwapeleka mbali ambapo wao hawawaoni. “Jambo lote hili lina uzito wake,kule nako wakipelekwa kuna uzito wake lakini hapa pia pana uzito zaidi.”alisema Padre Chavala 

  Chavala akizungumzia utofauti wa kaburi la maria na Consolata alisema kuwa wanaweka pana kwasababu wapo watu wawili,lazima ukubwa wake utofautiane na kaburi linalozikwa mtu mmojammoja. “Wapo watu wawili,tumeamua kuwaweka mahali pamoja lakini upekee wa kaburi ni kwamba watu hawa tunaendelea kuwalea katika vituo vyetu,ni wenzetu,tunawaweka hapa ambapo wanalala Masista,Mapadre,Mabrother na hata walei sasa hawa wamepata upekee sana kwa sababu wamebaki wakilelewa na masista.”alisema Chavala 

  Naye sista Calista Ludega ambaye ni mkuu wa shirika la mtakatifu Theresa wa mototo Yesu jimbo katoliki la Iringa alisema kuwa wanawazika Maria na Consolata mahala wanapolala masista wa consolata kwa ajili ya kuwaenzi masista wa mishionari wa consolata kwa kuwa wao wamechukuwa sehemu kubwa ya malezi tangu walipozaliwa watoto hao hadi wanapomaliza maisha yao hapa duniani. 

  Maria na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista ambao walikwisha fariki Maraia Lorenta,Masweta Pagosi na Maria Saglio. Maria na Consolata walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu. 

  Vifo vya mapacha hao vimeleta simanzi na huzuni kubwa kwa Watanzania walio wengi akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk.John Pombe Magufuli ambapo baada ya kupata taarifa za vifo hivyo alisema na hapa namkunukuu “Nimesikitishwa na kifo cha maria na Consolata .Nilipokwenda hospitali waliliombea taifa.Walikuwa na ndoto ya kulitumikia taifa .Poleni familia , masista wa maria Consolata na wote walioguswa , pumzikeni mahali pema wanangu .Bwana alitoa na bwana ametwaaa.Jina la bwana lihimidiwe.
   Baadhi ya Ndugu na Jamaa wakishiriki kuchimba kaburi ambalo Mapacha walioungana Maria na Consolata wanatarajiwa kuzikwa hapo kesho 
   Sehemu ya Makaburi yaliyolizunguka kaburi la Mapacha walioungana ,Marehemu Maria na Consolata,ambapo Masista na Mapadre wamezikwa
   Baadhi ya Ndugu na Jamaa wakiendelea kushiriki kuchimba kaburi ambalo Mapacha walioungana,Marehemu Maria na Consolata wanatarajiwa kuzikwa hapo kesho .
  Zoezi la uchimbaji wa kaburi kwa ajili ya maziko ya mapacha walioungana, marehemu Maria na Consolata linaendelea katika Makaburi ya Masista wa Shirika la Bikira Maria wa Consolata Tosamaganga,  Jimbo Katoliki la Iringa.

  0 0


  Na Hamza Temba-Dodoma

  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza Kikosi Kazi Dhidi ya Ujangili cha Taifa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Serengeti kuwasaka watu waliohusika na mauaji ya simba tisa katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

  Dkt. Kigwangalla ametoa agizo hilo ofisini kwake Jijini Dodoma jana baada ya kupokea taarifa rasmi ya mauaji hayo ya kikatili yaliyoripotiwa hivi karibuni kwa simba hao kulishwa sumu kali katika kijiji hicho huku mmoja akikatwa miguu, mkia, ngozi ya juu ya mgongo na kuchukuliwa baadhi ya viungo vyake ambapo amesema mauaji hayo hayavumiliki kwa kuwa yana athari kubwa kiikolojia, kiutalii na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

  "Bahati mbaya sana ni kuwa anapouawa simba kwa sumu hafi peke yake, inakufa familia nzima ya simba, na mara nyingi wanakufa pia wanyamapori wengine wanaodowea nyama na wanaokula mizoga. Walipouawa simba wa Ruaha hivi karibuni walikufa fisi zaidi ya 70 na ndege mbeshi zaidi ya 100, achilia mbali wadudu," amesema Dkt. Kigwangalla kwa masikitiko makubwa.

  Amesema pamoja na faida kubwa za simba kwa Taifa kiuchumi, Kijiji cha Nyichoka pekee walikouwawa simba hao ni katika sehemu iliyofaidika sana na miradi ya ujirani mwema kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti."Wanyama hawa jamii ya paka wakubwa ni muhimu sana kwa kuweka mizania ya ikolojia sawa, maana wanadhibiti idadi ya wanyama wala nyasi kwa kuwala, bila hivyo hifadhi zote zinaweza kugeuka kuwa jangwa. 

  "Hakuna mtalii atakayekuja hifadhini asitamani kumuangalia simba, mfalme wa pori. Wanapouawa maana yake tunashusha hadhi ya hifadhi zetu kiutalii na hivyo kutishia kupoteza mapato yanayotokana na utalii" amesisitiza Dkt. Kigwangalla. 

  Amesema tukio hilo la kuuwawa kwa Simba wa Ikolojia ya Serengeti sio la kwanza kutokea hapa nchini ambapo mwishoni mwa mwaka jana simba wengine watano waliuawa pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. "Mwaka huo huo mwanzoni simba watatu nao walipigwa risasi kikatili wilayani Serengeti huku mwaka 2015 simba 7 wakauwawa tena kwa sumu, huko huko Serengeti".

  Akizungumzia sababu za ujangili huo amesema mara nyingi ni kwa ajili ya kulipiza kisasi baada ya ng’ombe wa wananchi kuliwa na simba, changamoto ambayo husababishwa na wananchi wenyewe kusogelea na kuweka makazi karibu kabisa na mipaka ya hifadhi za wanyamapori kwa lengo la kulisha mifugo pembezoni na wakati mwingine ndani ya hifadhi hizo kinyemela.

  Simba ambao wanakadiriwa kuwa zaidi kidogo ya 22,000, pamoja na wanyama wengine jamii ya paka wamepungua sana miaka ya hivi karibuni kiasi cha kuwekewa tishio la kutoweka hapa duniani. Duma nao wanakadiriwa kubaki 1,200 pekee.
  Baadhi ya simba kati ya tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara
  Askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikusanya miili ya simba tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara hivi karibuni kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi kubaini chanzo cha vifo vyao.
  Askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikusanya miili ya simba tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara hivi karibuni kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi kubaini chanzo cha vifo vyao.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa ngazi zote kuongeza nguvu katika utekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati na miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

  Makamu wa Rais wa ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.  Ni muhimu, mipango ya maendeleo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu iwe na maendeleo endelevu” alisema Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais amesema kazi ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira unahitaji ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote. Maadhimisho ya Kimataifa yanafanyika India katika mji wa New Delhi yakibeba ujumbe wa kuhimiza kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na matumizi ya bidhaa za plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa nchini Kitaifa ujumbe wa maadhimisho ni “Mkaa Gharama: Tumia Nishati Mbadala”

  Mapema leo, Makamu wa Rais alizindua ukuta wa bahari uliopo kwenye barabara ya Barack Obama wenye urefu wa mita 920, ukuta huo ambao umejengwa kuzuia bahari kuingia nchi kavu unakadiriwa kuwa na maisha kati ya miaka 70 mpaka 100 kutoka sasa. Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda na zipo faida nyingi za hifadhi na usimamizi zitakazotokana na Tanzania kuwa na Viwanda.

  Mwisho, Makamu wa Rais amesema katika kufanikisha suala zima la uhifadhi wa Utunzaji wa mazingira mi lazima tuifanye kila siku iwe siku ya Mazingira.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ukuta wa bahari wenye urefu wa mita 920 uliojengwa pembezomi mwa barabara ya Barack Obama mara baada ya kuizindua, mwingine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Bw. Leonard Kushoka mfano wa hundi yenye thamani ya shiliningi za kitanzania milioni 300 mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa mwaka 2018, wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mwenyekiti Mkazi wa Kampuni ya Shell Bw. Axel Knospe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisisitiza jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January  Makamba, akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikagua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam mara baada ya kuuzindua mapema hii leo, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Sehemu ya kupumzika iliyojengwa katika ukuta wa ufukwe wa bahari ya Hindi uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Msanii Beka Fleva akitoa burudani kwa wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,(hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwapungia wananchi mara baada ya kuzindua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO

  0 0


  -Ni laini zenye gharama nafuu Zaidi, hazihitaji kujiunga kifurushi

  Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua laini mpya za watu mashuhuri zilizopewa jina la VIP zitakazo wawezesha wateja wa mtandao huo kufanya mawasiliano kwa makato ya gharama nafuu zaidi kwa kila dakika na MB za intaneti watakazo tumia.

  Laini hizo za VIP zitawawezesha wateja wa mtandao wa Halotel nchi nzima kuweza kupiga simu au kutumia intanenti kwa gharama nafuu kwa kutumia salio la muda wa kawaida wa maongezi bila kuwa na ulazima wa kujiunga na kifurushi chochote.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, uzinduzi huo wa laini za VIP ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma za mawasiliano kwa wateja wa Halotel kwa kuwaokolea muda na gharama ambapo badala ya mteja kutumia muda na gharama kujiunga na vifurushi vya kupiga simu kwa mtandao wa Halotel na mitandao yote au vifurushi vya intaneti mteja ataweza kutumia salio la muda wa maongezi kupiga simu au kutumia intaneti bila kuhofia matumizi makubwa ya makato kwa gharama nafuu zaidi.

  “Huduma hii inawalenga wateja wa vipato vya aina zote, wale wenye matumizi ya kati, na matumizi makubwa, ambapo katika laini hii ya VIP makundi hayo yamegawanywa kwa kupewa majina ambayo ni Silver kwa wateja wenye matumizi madogo, Gold kwa wateja wa matumizi ya kati na Diamond kwa wateja wa matumizi makubwa. Makundi haya yana lengo la kukidhi mahitaji ya kila mteja kulingana na kundi alilomo.” Alisema Semwenda na kuongeza.

  “Mfano kwa mteja atakayenunua laini ya VIP ya Silver yenye thamani ya shilingi elfu tano (5,000) kwa pesa hiyohiyo anaweza kupiga simu Halotel kwenda Halotel kwa gharama ya makato ya shilingi thelathini (30) tu kwa dakika ambapo kwa makato ya gharama ya kawaida ni shilingi (228) kwa dakika ambapo ni mara punguxo la mara saba(7) ya gharama za kawaida. 

  Vile vile mteja katika kundi hili anaweza kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya makato ya shilingi arobaini na tano (45) tu kwa dakika tofauti na makato ya gharama ya kawaida ambayo ni shilingi (228) kwa dakika ambapo ni punguzo mara tano (5) ya gharama za kawada. Kwa MB 1 mteja atatumia intanenti kwa gharama ya shilingi nne (4) tu akiwa na laini ya Silver ya VIP gharama ambayo ni mara saba(7) pungufu ya makato ya gharama ya kawaida ya shilingi 30.72 kwa MB huku akifurahia kutumia Facebook bure.” Alisema Semwenda.

  Mteja yeyote wa Halotel wa kawaida ana uhuru wa kuweza kubadili laini yake na kuwa laini ya VIP na kuweza kufurahia kupiga simu Halotel na mitandao yote pamoja nakutumia Mb za intanenti kwa kupiga *148*66# kisha anachagua namba tisa (9) na hivyo kuendelea kuchagua kundi atakalohitaji kujiunga, si hivyo tu mteja wa Halotel wa kawaida anaweza kuendelea kujiunga na vifurushi kama kawaida endapo atahitaji.

  Hii ni moja ya maendeleo ya teknolojia katika kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wetu ambao wamekuwa na imani kubwa ya huduma zetu siku zote” alisema Tito.

  “Tunatarajia huduma hii ya VIP itaongeza nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wetu na kwa watanzania wote, na kuokoa kiasi kikubwa cha gharama za mawasiliano zinazokatwa wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana, biashara na kupata taarifa mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia intaneti kwa uhakika. Alihitimisha Semwenda.”
  Meneja wa idara ya ushirika Halotel Emmanuel Tito Malyeta, Halotel akiwaeleza waandishi wa Habari, akitoa ufafanuzi mbele ya waandish wa Habari katika uzinduzi wa huduma ya VIP ambapo Mteja yeyote wa Halotel wa kawaida ana uhuru wa kuweza kubadili laini yake na kuwa laini ya VIP na kuweza kufurahia huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel akiwaeleza waandishi wa Habari, akitoa ufafanuzi mbele ya waandish wa Habari katika uzinduzi wa huduma ya VIP, ambayo ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma za mawasiliano kwa wateja wa Halotel kwa kuwaokolea muda na gharama katika matumizi yao ya kila siku. Kulia ni Meneja wa idara ya ushirika Halotel Emmanuel Tito Malyeta.

  0 0

  Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi Jeshini Brigedia Jenerali, Nicodemus Elias Mwangela pamoja na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye masuala ya Ulinzi katika Wizara ya Ulinzi ya Israel, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Ben-Baruch wakiwekeana saini katika Mkataba wa Makubaliano ya pamoja ya Ulinzi kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania na Wizara ya Ulinzi ya Taifa la Israel, tukio hilo limehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania, Mhe. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Dkt. Florens Turuka, Balozi wa Israel nchini Kenya awakilisha pia Tanzania, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Suleiman Salehe pamoja na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania.Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao Makuu ya Jeshi 
  Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela (kulia) pamoja na Brigedia Jenarali Mstaafu Michael Ben-Baruch wakibadilishana mikataba hiyo mara baada ya kumaliza zoezi la kuwekeana saini. 
  Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela akimkabidhi Brigedia Jenerali Michael Ben- Baruch zawadi ya Nembo ya Jeshi la Kujenga Taifa la JWTZ 
  Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela (wa sita kulia) pamoja na Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Ben- Baruch (wa saba kutoka kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na Israel pamoja na Balozi wa Israel nchini Kenya ambaye anawakilisha Tanzania.

  0 0

  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

  KAMPUNI ya mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya ORYX nchini ijulikanayo kama ORYX ENERGIES LTD imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha nishati mbadala inatumika badala ya mkaa ambao umeonekana kuwa wa gharama sana.

  Akizungumza katika kuadhimisha Wiki ya mazingira leo viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mauzo kampuni ya gesi ya ORYX Jeffrey Nasser amesema kuwa ORYX GAS amekuwa rafiki mkubwa wa mazingira pale walipoamua kuletea nishati mbadala ya ges.

  "Na haikuishia hapo tu bali tuliwawezesha wananchi wengi sana nchi nzima kuipata kwa gharama ndogo na hata yale maeneo ya wananchi wa hali ya chini tumewawezesha kupata gesi yetu. Na Tunaamini tumeokoa miti mingi ambayo ingekatwa kwa matumizi ya kupikia,"amesema.

  Amefafanua kwa ORYX GAS kwa nyakati tofauti wamekuwa wadau muhimu katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutunza mazingira, na kwa muda mrefu wamekuwa na kampeni yao ya ORYX GAS "Rafiki wa Mazingira". 

  Hivyo amesema katika kuadhimisha Wiki ya mazingira wameamua kuchukua fursa kujiunga na wadau wengine kushirikiana katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira kwa ujumla.

  "Lengo letu ni kuhakikisha watu wote wanatumia nishati ya gesi, kampuni ya ORYX imewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye maghara ya uhifadhi na mitambo ya kujaza gesi nchi nzima.Hatutarajii kusikia tena uhaba wa gesi ya kupikia nchini na hatutarajii kabisa watumiaji wa gesi wanarejea kwenye mkaa na kuni kwa kukosa nishati hii ya gesi hapa nchini,"amesema.

  Pia Jeffrey amesema kuwa Mkaa ni gharama hasa kwa wakazi wa mijini na kuongeza hivi sasa gunia la mkaa kwa wakazi wa Dar es salam limefikia Sh.70,000 na wengi wanalalamika kuwa mkaa haumalizi mwezi.

  "Sisi tunawapa mtungi wa gesi wa kilo 15 ambao kwa familia ya watu saba wanaotumia gesi pekee huweza kutumia kati ya siku 30 hadi 40. Mbali na faida za gharama ndogo,gesi yetu pia ni salama kwa afya ya mtumiaji na usafi wa mazingira ambapo tusingeanza usambazaji mkubwa wananchi wangepaswa kuweka bajeti nyingine za matibabu ya madhara ya moshi mwilini na ukarabati wa nyumba ambazo huchafuka sana kutokana na matumizi ya kuni na mkaa,"amesema 

  Amesema kampuni yao ya ORYX imetoa shukurani kwa wananchi kwa muitikio mkubwa wa matumizi ya gesi kila siku inayoenda. "Muitikio mkubwa umeonekana hasa pale ongezeko la watumiaji wengi wapya nchi nzima wakinunua mitungi mipya ya gesi ya ORYX kwa matumizi yao,"amefafanua.
   Mkuu wa Kitengo cha Mauzo  ORYX GAS,Jeffrey Nasser akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu yakuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu  ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kulia) akimzikiliza 
  Menejacha wa Maendeleo ya Biashara Oryx Gas,Mohamed Mohamed ambabo akifafanua juu  ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu  ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira,leo jijini Dar as Salaam katika kilele cha maadhimosho ya wiki ya mazingira Duniani.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico) limesema makaa ya mawe yakianza kutumika kama nishati ya kupikia kutapunguza matumizi ya mkaa kwa asilimia 15.

  Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Madini na huduma za Kiuhandisi, Zena Kongoi wakati akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Dunia yaliyohitimishwa, leo Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam amesema Stamico katika miradi mbalimbali wameweka kipaumbele cha utuzaji wa mazingira katika kulinda vizazi vya leo na vijavyo.

  Amesema kuwa katika ripoti ya Trido inaonyesha hekta 300,000 za miti zinakatwa kwa ajili mkaa hivyo matumizi ya makaa ya mawe kutumika nishati ya kupikia itapunguza ukataji wa miti hiyo.Kongoi amesema makaa ya mawe kuna taasisi ambazo zitakuwa za kwanza kufikiwa na nishati ya makaa ya mawe ni Magereza , Kambi za Wakimbizi pamoja na vyuo vikuu.

  Amesema kuwa nishati hiyo watauza kati ya Sh.350 hadi 500 ambapo kila mtu anaweza kumudu na kuachana na matumizi ya mkaa kutokana na gharama iliyopo katika mkaa.Amesema majaribio ya makaa ya mawe yana gesi hivyo kazi kwa ushirikiano kati ya Stamico na Trido katika kutoa gesi hiyo na kemikali zingine zilizo katika makaa ya mawe.

  Kongoi amesema stamico iko bega kwa bega na wadau mbalimbali katika shughuli za madini katika kuangalia masuala ya mazingira ikiwemo kufanya tathimini ya uhalibifu wa mazingira katika miradi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Madini na huduma za Kiuhandisi, Zena Kongoi akizungumza na waandishi habari katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Mwanasheria wa Baraza la Mazingira (NEMC), Heche Suguta akiwapa vipeperushi pamoja na kuwapa maelezo wananchi waliotembelea maonesho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja

  0 0

  Hili ndilo sanduku litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata likiwa tayari limekamilika kwa maziko hapo kesho katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa

  Maria na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Tosamaganga watakakozikwa.

  Maria na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista waliokwishafariki.Maria na Consolata walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu.
  Baadhi ya Mafundi wakitengeneza  sanduku litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata,kwa maziko hapo kesho katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa.

  Maria na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Tosamaganga watakakozikwa.

  Maria na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista waliokwishafariki.Maria na Consolata walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu.
  Sanduku litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata likiwa tayari kwa maziko hapo kesho katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa
  Baadhi ya Mafundi wakiendelea na maandalizi ya kutengeneza Sanduku litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata,kwa ajili ya maziko hapo kesho katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhandisi Monica Mtege amesema, nchi hiyo imedhamiria kupitisha shehena nyingi za mizigo yao katika bandari ya Dar es Salaam kwa sababu ya vivutio vingi vilivyopo.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kufanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam Mhandisi Mtege amesema bandari hiyo ni njia rahisi kwao ya kupitisha mizigo yao na pia usafiri wa kutumia njia ya maji ni wa bei nafuu.Alisema vivutio vilivyopo katika bandari ya Dar es Salaam hawaoni sababu itakayo wakwamisha kupitisha mizigo yao na kuendeleza uchumi wa nchi yao.

  " Kufika Bandari ya Dar es Salaam ni mara yangu ya kwanza lakini nimeshuhudia mambo mengi ikiwamo maboresho ya miundombinu hivyo napongeza Serikali ya Tanzania ambazo zimechukuliwa hasa za kufungua njia ya ukanda wa kati jambo lililorahisisha kufika kwa mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda Uganda," alisema Monica.

  Amesema tayari wamejiandaa kuhakikisha wanasafirisha shehena kwa wingi kutoka Uganda kuja Dar es Salaam.Amesema tayari wameandaa makampuni makubwa yenye nia ya kuja Dar es Salaam kupitia njia ya ukanda wa kati.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Lydia Malya amesema, tayari bandari wameanzisha kikosi kazi maalum ili kuhakikisha wanapata mizigo mingi zaidi ya Uganda.Amesema watatumia fursa mbalimbali kutangaza njia hiyo kwa faida ya nchi mbili.
  Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhandisi Monica Mtege akizungumza katika mkutano wa menejimenti ya TPA wakati alipotembelea bandari hiyo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho akitoa maelezo wakati  Waziri wa Uganda alipotembelea banadari ya Dar es Salaam
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Banadari , Mhandisi Karim Mataka akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa ujenzi na Uchukuzi wa Uganda alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Profesa Ignatus Rubaratuka akizungumza kuhusiana na mamlaka hiyo kuhakikisha inatoa huduma bora kutokana na ushirikiano kati ya Uganda na Tanzania

  0 0


  0 0

   Habari tulizozipata Globu ya Jamii  hivi punde kutoka mkoani Kigoma mapema leo asubuhi hii ya Jumatano Juni 6,2018, inaelezwa kuwa Basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD lililokuwa likitoka Kigoma kwenda wilaya ya Nzega mkoani Tabora limegonga treni ya mizigo (Garimoshi la mizigo) katika eneo la Gungu Mjini Kigoma.

  Ripota wetu Editha Karlo aliyekuwepo eneo la tukio na kushuhudia mandhari halisi ya jali hiyo,ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri, na mpaka sasa  kwa taarifa za awali inaelezwa kuwa Watu 11 wanahofiwa  kupoteza maisha,huku idadi ya majeruhi ikidaiwa kuwa ni 26.

  Ripota wetu yupo eneo la tukio,hivyo tutaendelea kuwaleta habari kadiri ya zitakavyokuwa zikiingia.
   Baadhi ya majeruhi wa ajali wakiendelea na matibabu katika hospitali  ya mkoa wa kigoma.
   Baadhi ya vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa eneo la tukio la ajali
   Baadhi ya Askari wa JWTZ wakiwa tayari wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa namna moja ama nyingine
   Baadhi ya Wananchi waliofika kushuhudia tukio la ajali hiyo wakishuhudia majeruhi wakipakizwa kwenye gari  ya Wagonjwa ya JWTZ tayari kupewa huduma ya kwanza na baadae kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi
  Mbunge wa Kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe akiwa eneo la tukio la ajali akishuhudia majeruhi wakiokolewa.

  0 0

  JOSEPH MPANGALA -MTWARA
  Shirika la msaada wa  maendeleao ya Michezo SDA Mkoa wa Mtwara Limefanikiwa kutoa Mafunzo pamoja na Vifaa vya michezo kwa Shule Mbili za Msingi Libobe Pamoja na Sekondari zilizopo Kijiji cha Libobe Kilichopo Wilaya na Mkoa wa Mtwara.
  Mafunzo hayo yamelenga Kujenga uwezo kwa wanafunzi hasa wa kike katika maswala ya Afya Kupitia Michezo pamoja na kujua haki zao ili kuweza kujiamini katika kutoa maamuzi mbalimbali ya maisha yao.
  Meneja Mradi wa Mradi wa Kuwezesha wasichana Kupaza sauti  Unaoendeshwa na SDA Thea Swai  amesema Mradi huo unaendeshwa katika kata Tisa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara manispaa kwa lengo la kuelimisha na kujengea Uwezo wa Umuhimu wa Umuhim wa Elim kwa wasichana na Jamii kwa ujumla .
  “Lengo kuu la Mradi huu ni kuelimisha na Kujengea Wasichana na Jamii kuhusu Umuhim wa Elimu kwa ujumla juu ya upatikanaji Ushiriki na ufikiwaji wa elim ya msingi na sekondari hasa kwa watoto wakike ambao wamekuwa wahanga wa matatizo ya ufaulu mdogo wanapomaliza elim ya sekondari na wakati mwingine kwa idadi ndogo ya wasichana wanaomaliza shule za sekondari”
  Lakini naye Afisa maendeleo ya jamii kutoka Halmahauri ya Mtwara Vijijini Maisha Mlaponi amewaomba wazazi kuhakikisha wanawajengea Uwezo wa Kijamini wanafunzi ili waweze kufanya Vizuri wawapo darasani.
  “Wazazi naombeni Muwasaidie watoto wenu wa Kike waweze kujiamini katika Maisha yao na wakiweza kujiamini hata darasani wataweza kufanya vizuri  kwa sababu watakuwa na uwezo wa kuuliza maswali kwa walim na hivyo wataweza kuelewa na kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho’”.

  Mkurugenzi wa Shirika la SDA Adolph Kanda akimkabidhi Mwalim wa Shule ya msingi Libobe Mwanaidi Mtanda Vifaa vya Mchezo wa Mpira wa Pete kwa ajili ya kufanyia mazoezi Shuleni hapo.

  Mkurugenzi wa Shirika na Msaada wa Maendeleo ya mischezo SDA Adolph Kanda akinyanyua Juu kuonesha medali walizokabidhiwa wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Libobe mara baada ya Kumaliza mchezo wa mpira wa Miguu.


  Kutoka Kulia ni Mratibu wa Mradi Anu Nieminen katikati Mratibu wa Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Mtwara Adelina Ndyamukama pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Paralegal Mkoa wa Mtwara Mullowellah A.Mtendah wakiwa wanajadiliana jambo katika mafunzo yaliyofanyika kwa wanafunzi wa Libobe.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mtwara Paralegal Mullowelh A.Mtendah akitoa mafunzo yakisheria kuhusu haki za watoto pamoja na haki za walemavu katika kuhakiksha zinasimamiwa na kutekelezwa na wanakijiji wa Libobe Mkoani Mtwara.

  Meneja wa Mradi wa Kuwawezesha wasichana Kupaza sauti Thea Swai akitoa mafunzo ya kujiamini kwa wanafunzi wa kike pamoja na kuwawezesha waweze kupaza sauti katika Kutetea haki Zao.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma

  IMEELEZWA zaidi ya tani 160 za matumizi ya nishati ya  kuni na mkaa  hutumika katika  kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kwa siku moja, kwa  matumizi ya kupikia.

  Hivyo hali ina sababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo yaliyokaribu na kambi hizo.Hayo yalibainika jana wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ,  yaliyofanyika kimkoa katika Kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani humo.

  Akizungumza  Mratibu wa mradi wa utunzaji wa mazingira  kambini CEMDO Tanzania Frank Kayegameni akitoa taarifa ya mradi huo amesema kutokana na  idadi kubwa ya wakimbizi  kambi ya Nyarugusu ambayo imesababisha uhitaji mkubwa wa matumizi ya mazao ya misitu.Amefafanuana  wakimbizi huenda kutafuta kuni nje ya kambi kwa kukata miti ambapo kwa siku inakadiriwa mtu mmoja anatumia kiasi cha kuni kilo moja na kambi inakadiriwa kuwa na wakimbizi 152,309 hivyo kusababisha  uharibifu mkubwa.

  Amesema katika kupambana na hali hiyo Shirika la uhifadhi wa mazingira  na utunzaji wa mazingira kambini ( CEMDO) Tanzania,  kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameandaa utaratibu wa upandaji wa miti 1,425,223  katika Vijiji 13 vinavyozunguka Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa mwaka 2017/2018 , kugawa majiko banifu kwa kaya 9600 za wakimbizi.

  Pamoja na majaribio ya ugawaji wa gesi  kwa kaya 3180 lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na kuni  yanayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na  kuboresha mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa uoto wa asili  unaotokana na ukataji miti ovyo.

  Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema  kauli mbiu ya maadhimisho ya mazingira ni "Mkaa ni gharama; tumia nishati mbadala",Ambapo amesema kauli hiyo inasaidia utunzaji wa misitu na mazingira, lakini kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakimbizi kupewa majiko banifu na gesi kwenda  kuuza kwa Watanzania ilikujipatia fedha na kuendelea kuharibu mazingira na kuwataka wakimbizi kuacha tabia hiyo na kuendelea kutumia majiko yaliyotolewa na shirika hilo.

  Pia Kanali Ndagala  amesema amefurahishwa na shughuli zilizotajwa na mashirika hayo ya Kutunza mazingira  na kuwaomba kuongeza utaalamu wa kutumia misitu kwa ufugaji wa Nyuki, kwani ufugaji wa nyuki utawaletea kipato na kuongeza uchumi wao kwa ngazi ya kaya na mtu mmoja,Pia, amewashukuru kwa kazi kubwa ya kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira , kwa mkoa huo jamii imekuwa na tabia ya uharibifu wa mazingira hasa kwa kuchoma moto.

  "Kupitia maadhimisho haya  nitoe rai kwa wataalam na Viongozi mbalimbali katika halmashauri kusimamia kwa makini kilimo na shughuli za maendeleo, ili jamii ambazo zimekuwa chanzo  cha uharibifu wa vyanzo vya maji  ziweze kuhifadhi vyanzo vya maji hili halina mjadala sheria zipo wazi  wachukuliwe sheria wale wote wanaolima au kufanya shughuli za kijamii hatarishi katika Vyanzo vya maji", Amesem.

  Pia suala la uchomaji moto misitu suala hilo wahusika wote pamoja na viongozi walio katika eneo lililochomwa watachukuliwa hatua, lazima tutunze mazingira kwa maendeleo ya Nchi yetu hili ni agizo.Naye Rais wa Wakimbizi Kambi ya Nyarugusu  Abilola Angelique amesema wao kama wakimbizi hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na mashirika yanayo wahudumia, kwa kuwa wanapotunza mazingira hata wao wanaendelea kunufaika kwani watatumia ardhi hiyo kulima mazao ya mboga mboga kwa ajili ya kujikimu na watoto wao.

  Amewaomba wakimbizi wenzake kuendelea kusimamia utunzaji wa mazingira.
   Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea  Ndagala akipokea Maelezo ya Mazao ya mboga mboga yanayo limwa na wakimbizi Kambi ya Nyarugusu katika mradi wa utunzaji wa Mazingira
   Mmoja wa Wakimbizi akimuelezea Mkuu wa Wilaya namna wanavyo yatumia Majiko banifu kuhakikisha hawaharibu mazingira
   Mkuu wa Wilaya ya Kakonko kanali Ndagala  akioneshwa na Afisa wa Shirika la CEMDO majiko banifu yanayotumia kuni chache kwa lengo la kutokomeza uharibifu wa mazingira.

  0 0

  Kampuni ya kimataifa ya Regus, ambayo inajihusisha na kupangisha ofisi za kisasa za muda na za kudumu imefungua kituo kipya cha nne cha ofisi za kupangisha jijini Dar es Salaam . Jengo jipya la ofisi za Regus kwa ajili ya matumizi ya kupangisha ofisi zisizo na usumbufu wa masharti liko eneo la Msasani Penisula, na linazo ukubwa wa mita za mraba 590 kwa ajili ya matumizi ya ofisi za kisasa. 

  “Tumefungua jengo la nne la kituo cha biashara lenye maeneo ya ofisi za kupangisha,hii ni fursa pekee kwa Mashirika Yasio ya Kiserikali,na makampuni ya kimataifa kujipatia sehemu za ofisi za kisasa. Eneo hili la biashara limelenga makundi yote ikiwemo wajasiriamali wanaoanza biashara kwa kuwa bei zake za pango ni za kawaida na rahisi kuzimudu” alisema Joanne Bushell,Meneja wa Regus nchini. 

  Regus imepanua huduma zake kutokana na ongezeko la mahitaji ya ofisi kwa matumizi mbalimbali na kwa gharama nafuu bila kuhangaika kununua samani za ofisi, kuingia mikataba ya kipindi cha muda mrefu na kulipia huduma mbalimbali za matumizi ya ofisi kama umeme na maji. Kituo hicho cha biashara cha Regus kinazo ofisi za kupangisha, kumbi za mikutano zenye huduma mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya uhakika kupitia mtandao wa internet na simu za mezani, majiko na sehemu za kupumzikia, huduma za usafi, huduma za mapokezi na utawala. 

  Kampuni inao mpango wa kuendelea vituo vingine vya biashara katika siku za usoni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya ofisi zisizo na masharti na usumbufu,Regus inaendesha vituo vya biashara katika miji ipatayo 900 kwenye nchi zaidi ya 120 duniani,ikiwa inahudumia wajasiariamali wa kawaida, watu binafsi na makampuni makubwa ya kimataifa.

  0 0


  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)umesema ipo haja kwa Watanzania kuhakikisha wanatumia nishati mbadala na hasa mkaa mbadala kwa lengo la kulinda mazingira na hasa misitu iliyopo nchini huku akielezea namna ambavyo kasi ya ubaribifu mazingira ikiendelea kuongezeka.

  Hayo yamesemwa jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa Dos Santos Silayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambapo kwa Tanzania kitaifa yamefanyika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Michuzi Blog, Profesa Silayo amesema takwimu zinaonesha bado kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na hivyo kuiomba jamii kutumia nishati mbadala ili kulinda mazingira na kubwa zaidi ameshauri kutumia mkaa mbadala kwa ajili ya kupikia.

  Akizungumzia Siku ya mazingira duniani ambayo yameambatana na maonesho ya nishati mbadala, Profesa Silayo amesema Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wameshiriki kwasababu msitu inabeba dhamana kubwa katika mazingira na unapozungumza mazingira basi yanaonekana maeneo ya misitu na ekolojia yote.

  Ameongeza maonesho hayo yametoa fursa ya kukutanisha wadau mbalimbali na hasa wanaotengeneza nishati mbadala kwa ajili ya mkaa mbadala."Wadau wote ambao wamefika hapa wanaonekana kutoa mbadala wa mkaa badala ya msitu asili ambayo imekuwa ikikatwa kwa ajili ya matumizi ya mkaa na kuni.

  "Hivyo mkaa mbadala utasaidia kutunzwa kwa mazingira na kuwa salama na hivyo misitu ya asili itabaki ikiendelea kusaidia kutunza vyanzo vya maji na mambo mengine muhimu,"amesisitiza.Akizungumzia umuhimu wa teknolojia ya nishati mbadala amesema kuwa miti iliyokuwa inakatwa kwa ajili ya mbao badala sehemu kubwa ya miti hiyo kupotea sasa itatumika kwa ajili ya kutengeneza mkaa mbadala na hivyo kutapunguza kasi ya ukataji wa miti.

  "Hivyo maonesho haya kwate ni muhimu kwani inatoa nafasi ya kuangalia ushiriki wa wadau katika kuangalia namna ya kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira kwa kuanzisha nishati mbadala ya mkaa na tunafahamu hekta 400,000 zinaharibiwa au kupoteza uwezo wake wa kiasilia,"amesema.Kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa kulinda mazingira, Profesa Silayo amesema kuwa zipo hatua mbalimbali ambazo zinachukuliwa ikiwamo ya kupanda miti na kuhakikisha maeneo ambayo yameharibiwa hayaharibiwi zaidi.

  Ametoa mwito kwa Watazania kutumia teknolojia ya nishati mbadala kwani imekuwa zaidi, hivyo ni vema wakabadilisha fikra na kueleza changamoto iliyopo watu wengi bado hawajaona umuhimu wa kutumia mbadala ya mkaa."Nitoe rai kwa wananchi tutumie nishati mbadala ya mkaa ili kutunza mazingira na hasa ukataji wa misitu kwa ajili ya mkaa,"ameongeza.

  Alipoulizwa kuhusu kasi ya uharibifu wa misitu Profesa Silayo amejibu kuwa kimsingi kasi ya uharibifu wa mazingira ni kubwa na hiyo inatokana na sababu mbalimbali zaidi ya kukata misitu na kufafanua pamoja na hali hiyo bado wanaendelea kuchukua hatua kukabiliana nayo.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos akiteta jambo jana akiwa katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yaliyofanyika kitaifa Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos akiangalia mkaa mbadala ambayo unatengenezwa kwa mabao ambao haujatokana na miti asili baada ya kutembelea banda la Accaso International Ltd jijini Dar as Salaam Jana. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)


  0 0


  0 0
 • 06/06/18--05:01: MATUKIOA KUTOKA BUNGENI LEO
 • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania, Deus Seif kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Juni 6, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe (kushoto ) na Lucy Mayenga kwenye viwanja vya Bunge jijjini Dodoma Juni 6, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 6, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania, Deus Seif kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Juni 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde akijibu maswali bungeni jijini Dodoma, Juni 6, 2018.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI,Joseph Kakunda , Bungeni jijini Dodoma, Juni 6, 2018.

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi wakati alipowasili katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu mkoani Morogoro, kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya wiki nne ya Utayari ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu Wakuu wa Polisi Wilaya (OCDs) na Maafisa Operesheni. Picha na Jeshi la Polisi.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (wa pili kushoto), akiwa ameongozana na Naibu Kamishna wa Polisi Msataafu (DCP) Vennance Tossi (katikati) Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu (DCP) Mpinga Gyumi na baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi hilo wakati alipowasili katika Chuo hicho kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya wiki nne ya Utayari ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu Wakuu wa Polisi Wilaya (OCDs) na Maafisa Operesheni. Picha na Jeshi la Polisi.
   Mmoja kati ya askari Polisi 203 wanaoshiriki mafunzo ya Utayari ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Polisi Wilaya (OCDs) na Maafisa Operesheni katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu mkoani Morogoro akiwa katika onesho la namna ya kukabiliana na uhalifu, mafunzo hayo ya wiki nne yalifungwa jana na  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro. Picha na Jeshi la Polisi.


older | 1 | .... | 1594 | 1595 | (Page 1596) | 1597 | 1598 | .... | 1898 | newer