Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WILAYA YA BUHIGWE YAANZA UGAWAJI HATIMILIKI ZA KIMILA KATIKA VIJIJI

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

HALMASHAURI ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imeanza mchakato wa ugawaji wa Hatimiliki za Kimila katika Vijiji vya Mugera, Kajana na Katundu katika Kata ya Mugera na Kajana katika kaya 1025 zitakazo saidia kupunguza migogoro ya ardhi Katika Wilaya na Mkoa kwa ujumla.

Akikabidhi hatimiliki hizo katika kaya 50 za mfano jana katika kijiji cha Muhegera Kata ya Mugera wilayani humo zinazotolewa na mradi wa usimamizi wa maliasili kwa ajili yq kuongeza kipato kwa mwananchi unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania na Ubelgiji chini ya shirika la ENABEL.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema katika kesi 10 zinazofika ofisini kwake kati ya hizo nane ni za migogoro ya ardhi na mbili ni za urithi.

Brigedia Jenerali Gaguti amesema mradi huo utasaidia usalama wa wananchi na kupunguza migogoro ya ardhi ambayo ilisababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kubaki wakiwa walemavu, kwakuwa wananchi wakiwa na maeneo yaliyopimwa na wakiwa na umiliki wa kisheria itasaidia kesi hizo kupungua.

"Na wananchi wataendelea kufanya shughuli zao za Maendeleo na kuachana na tabia iliyokuwepo kwa wananchi wengi kuzunguka kwenye mahakama za Ardhi, na kupeleka kesi za kuibiana maeneo na kuepuka kutumia gharama nyingi kuendesha Kesi hizo,"amesema.
Ameongeza amefurahishwa kwa mradi huo ambao ameuona maeneo mengi aliyopita kukagua mchakato huo ulivyokwenda aa ameona wananchi wengi wanauelewa na wanajua umuhimu wa hatimiliki.Ametoa mwito kwa ciongozi wa Serikali za Vijiji waendelee kuwahimiza wananchi kuja kufuatilia hatimiliki hizi kwani hati hizo nje na kupunguza migogoro ya ardhi itasaidia wananchi kutumia hati hizo kuombaea mikopo kwaajili ya kuendeleza biashara zao.

alisema Mkuu huyo."Wote wanaouelewa faida ya kwanza ni usalama mtu akimiliki hati yake anauhakika wa kumiliki eneo lake kisheria kesi nyingi zinazo pokelewa wilayani kati ya kesi 10 kesi saba ni za migogoro ya ardhi na kesi nyingine ni za mirathi imepelekea kwa kiasi kikubwa watu wengi kupoteza maisha,"amesema .

Hata hivyo amesema maeneo yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za msitu wa kupanda mti kuanza mchakato wa upandaji miti msimu wa upandaji utakapo anza na kutoa rai kwa viongozi wa vijiji kusimamia ipasavyo maeneo ya huduma za kijamii yaliyopimwa kwaajili ya shughuli za ufugaji na kilimo yatumike kwa lengo lililokusudia na wananchi waelekezwe namna bora ya kuyatumia na Kuepusha migogoro kwa wananchi.

Akitoa taarifa ya mradi Mratibu wa Mradi huo wilayani Buhigwe, William Marandu amesema mpango wa matumizo bora ya ardhi ni tokeo tarajiwa namba mbili la mradi ilipima ukubwa wa ardhi ya Kijiji cha Mugera hekta 9401.856 chenye vitongoji vinne ambavyo ni Ruyange, Mugera, Kishaha na majengo na mradi huo ulianza mwaka 2016 kwa kutenga matumizi ya ardhi ya maeneo ya kilimo kekari (6117.076) Malisho ya mifugo Hekati 1207.1, vyanzo vya maji , maeneo ya maziko , maeneo ya makazi hekari 477.78, misitu ya asili 378 na misitu ya kupandwa hekari 1097.3 kwakuwa aridhi ndio chanzo kikubwa cha Mtaji wa Wananchi.
Amesema hati miliki zilizo gawiwa Kwa kaya 50 za mfano ni kati ya hatimiliki 1025 zilizo andaliwa na mradi wa (NRMLED) Kwa vijiji vitatu vya Wilaya ya Buhigwe na hatimiliki 975 zilizobaki zitaendelea kutolewa baada ya ufunguzi wa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi wengine ambao bado hawajafanya utaratibu wa kupata hatimiliki za kimila kufanya utaratibu waweze kupata hati hizo kwa kupitia Idara ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Thadeo Bitumgwa ni mmoja kati ya wanufaika wa Mradi wa ugawaji wa hatimiliki za kimilqa amesema anashukuru kwa kufahamu mipaka ya kiwanja chake anahakika ya kuwa hata pata mgogoro na mtu yeyote na anauhakika wa Kuwarithisha watoto wake eneo ambalo ni salama na bila kuwa na ugomvi na majirani wenzake.

Nae Sospiter Sabuni mkazi wa Mugera amesema hati hiyo anaweza kunufaika nayo kwa shughuli mbali mbali wananchi wengi wamekuwa wakipoteza uhai kwaajili ya kugombea maeneo, na wengine wamepoteza haki zao za kumiliki kwakuwa hawana hati lakini baada ya Kuwa na hati wanauwezo pia wa kupata fidia pindi wanapokuwa maeneo yao yeamechukuliwa kwa shughuli zingine za maendeleo kwa kutumia hati hizo wanaweza kupata fidia.

Kwa Mujibu wa Sera ya Taifa ya Ardhi na Sheria za Ardhi Namba nne ya mwaka 1999, sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba tano ya mwaka 1999 , sheria ya mpango ya matumizi bora ya Ardhi Namba sita ya mwaka 2007 kila Kijiji hakina budi kuandaa mpango wa amatumizi bora ya ardhi kwa madhumuni ya kuwezesha usimamizi na matumizi endelevu ya ardhi na maliasili na rasilimali zake zote.

Serikali, NSSF wajipanga kumaliza tatizo la uhaba wa maji jiji la Dar es Salaam.

$
0
0
Morogoro, June 4, 2018:SERIKALI kwa kushirikikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF wamejipanga kutekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la Kidunda, hatua inayotajwa kuwa itatatua kabisa tatizo la uhaba wa maji katika jiji la Dar es Salaam katika kipindi chote cha mwaka.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo katika kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi Wilaya ya Morogoro Vijijini, Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwelwe alisema mradi huo unalenga kufanikisha adhma ya Rais John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa Viwanda.
"Tunapozungumzia ustawi wa uchumi wa viwanda hususani kwa jiji la Dar es Salaam ni lazima kuwepo pia na upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika katika kipindi chote cha mwaka. Changamoto iliyopo sasa ni kupungua kwa kiasi cha maji katika Mto Ruvu hususani katika miezi ya Septemba na Oktoba, hivyo mradi huu unakwenda kuhakikisha mto Ruvu unakuwa na uhakika wa maji katika kipindi chote cha mwaka'' alisema.
Kwa mujibu wa Mhandisi Kamwene, mradi huo utakaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu ni wazo la zamani likiwepo tangu serikali ya awamu ya kwanza chini Mwalimu Julius Nyerere na kwamba utekelezaji wake katika kipindi hiki ni mwendelezo wa adhma ya Rais Magufuli ya kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa.
"Kukamilika kwa mradi huu tafsiri yake ni kwamba huduma ya maji katika la Dar es Salaam inakuwa ni ya uhakika katika kipindi cha mwaka mzima'' alisisitiza.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara ambae pia alikuwa ameongozana na wajumbe wa bodi ya mfuko huo alisema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa barabara itakayoanzia eneo la mradi kupitia Ngerengere na kisha kuunganishwa na barabara ya Morogoro -Dar es Salaam katika eneo la Ubena Zomozi ikiwa na urefu wa zaidi ya Km  90.
 "Zaidi pia mradi huu utahusisha ujenzi wa daraja la Kidunda litakalounganisha Wilaya ya Kisarawe na Wilaya ya Morogoro vijijini sambamba na kuzalisha umeme zaidi ya Megawatt 20 tutakazozitumia katika mradi wetu wa sukari unaotekelezwa katika eneo hili,'' alifafanua.
Alisema baada ya kujiridhisha na mradi huo waliamua kuingia ubia na serikali ambapo asilimia 60 ya uwezeshaji wa mradi huo itatolewa na NSSF huku serikali ikiwekeza asilimia 40 na kwamba tayari mfuko huo umeshatenga kiasi hicho cha fedha.
"Pamoja na faida tunayotarajia kuipata kupitia uwekezaji katika sekta ya maji, NSSF dhamira yetu pia ni kuwa sehemu ya historia ya kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa maji katika jiji la Dar es Salaam,'' alisema.
Akizungumzia mradi huo Meneja Mipango na Uwekezaji wa Mfuko huo, Xavier Lukuvi alisema unatarajia kuanza katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha unaoanza Julai mwaka huu na kwamba utekelezwaji wake mbali na faida nyingine pia utaongeza ajira zaidi kwa watanzania ambao pia watakuwa wanachama wa mfuko huo.
"Lakini pia uzoefu na mafanikio tuliyoyapata katika ujenzi wa Daraja la Nyerere lililopo wilaya ya Kigamboni ndio umetusukuma pia kuwekeza katika mradi huu. Katika kipindi hiki cha Uchumi wa Viwanda na Biashara tunaamini kwamba sekta ya maji ni moja uwekezaji mzuri kabisa'' alifafanua.
Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba alisema licha ya mradi huo kuonekana kunufaisha zaidi jiji la Dar es Salaam lakini una faida kubwa kwa wananchi wake kwa kuwa unaambatana na faida nyingi ikiwemo ajira, ujenzi wa barabara, uzalishaji wa nishati ya umeme pamoja na kuongeza pato la taifa kwa ujumla kupitia kodi.
"Tukizungumzia ujenzi wa daraja la Kidunda tu hapo tayari tunamaanisha kwamba wananchi wangu wanaoishi huku Mkulazi hawatalazimika tena kusafiri zaidi ya km 90 kufika Ubena Zomozi kisha zaidi ya km 131 nyingine  kwenda Dar es Salaam na badala yake sasa watavuka tu hili daraja na kutokea Kisarawe kisha kuingia Dar es Salaam'' alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephene Kebwe alisema tayari wananchi wameelimishwa kuhusu mradi huo na tayari wameshaanza kuhama kupisha mradi na kwasasa serikali inaangalia namna ya kuhamisha makaburi ya ndugu wa wakazi hao.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwene (alievaa kofia ngumu) akifuatilia maelezo ya Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Prof Felix Mtalo (wa pili kushoto)kuhusu mradi mkubwa wa Bwawa la Kidunda kutoka utakaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF alipotembelea eneo la mradi huo katika kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi Wilaya ya Morogoro Vijijini mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (katikati). 
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwene (kulia) akibadilishana mawazo na wadau muhimu wa mradi huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephene Kebwe (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (wa pili kushoto) Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Attilio Mwang'ingo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara hiyo.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwene (katikati) akiongozana akiongoza msafara wa wadau kuelekea eneo la mradi wakati wa ziara hiyo. Wengine ni pamoja na Mkoa wa Morogoro, Dk Stephene Kebwe (kushoto) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba (kulia).

 Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka NSSF pamoja na DAWASA wakibadilishana mawazo wakati wa ziara hiyo.
Mchoro wa Mradi wa Bwawa la Kidunda.

UMEME NI NISHATI MBADALA ILIYO NAFUU KWA MATUMIZI YA NYUMBANI: KAMOTE

$
0
0

 Bw. Ally M. Koyya, (kulia), kutoka idara ya Masoko TANESCO, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea kwenye banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya Nishati Mbadala yanayokwenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Juni 4, 2018.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) limesema hakuna sababu yoyote kwa wananchi kuogopa kutumia nishati ya umeme kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani kwani ni nafuu mno ukilinganisha na nishati nyingine.

Afisa Mazingira wa Shirika hilo, Bw.Yusuf Kamote, amesema hayo kwenye maonesho ya Nishati mbadala ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni 4, 2018, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mkaa ni ghali tutumie Nishati mbadala”.

“Siku zote tunasema umeme wa TANESCO ni umeme wa bei nafuu, jambo la msingi ambalo wananchi wanapaswa kuelewa ni matumizi sahihi ya vifaa vya umeme kulingana na mahitaji.” Alisema.
Alisema kwa mfano mtu anatumia kifaa kinachohitaji WATI100 (100watts) kwa saa moja lakini anatumia kifaa cha WATI 200 (200Watts) kwa saa na kwa mahitaji yanayofanana, bila shaka hayo sio matumizi bora ya umeme.
Bw. Kamote pia alishauri, wananchi wanapotaka kununua vifaa vya umeme, wanapaswa kukague kiasi cha umeme kinachohitajika kwenye kifaa husika anachotaka kununua na vifaa hivyo hupimwa kwa kutumia WATI(Watt ).
“Ukitumia pasi ya umeme ya WATI 1000(1000Watts), kwa saa moja ni sawa na kutumia Unit 1 ya umeme kwa hivyo hakuna sababu ya kununua pasi ya umeme ya WATI2000 (2000Watts), kwa matumizi ya kawaida kwani pasi ya aina hiyo kwa matumizi sawa na ile ya WATI1000, matumizi yake yataongezeka, kutoka unit 1 hadi uniti 2.” Alifafannua.
Akieleza zaidi Bw. Kamote hakuna sababu tena ya kutumia mkaa kama nishati ya kupikia kwani hivi sasa yapo majiko ya umeme ambayo yanasaidia kudhibiti matumizi yaumeme yasiyo sahihi kwani.
“Kinachohitajika mpishi unatakiwa kuandaa vyakula unavyotaka kupika kabla ya kuwasha jiko lako la umeme, vyakula vikiwa tayari hapo ndipo unatakiwa kuwasha jiko lako tayari kwa kupika.” Alisema na kuongeza
Maonesho hayoyakliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais,  yalizinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki iliyopita na yanatariwa kufungwa na Rais John Magufuli, Jumanne Juni 5, 2018.

 Wanafunzi wa shule ya sekondari Kanosa ya jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya kitaalamu na wataalamu wa TANESCO (Kushoto).


Afisa Mazingira wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Bw. Yusuf Kamote, (kulia), akimsikiliza Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi. Samia Chande.


Wanafunzi wa shule ya sekondari Kanosa ya jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya kitaalamu kuhusu matumizi bora ya nishati ya umeme walipotembelea banda la Shirika hilo leo Juni 4, 2018.

Bw. Ally M. Koyya, (kulia), kutoka idara ya Masoko TANESCO, akimsikiliza mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la Shirika hilo kupata elimu ya umeme.

RAIS MAGUFULI AZINDUA AWAMU YA PILI YA PROGRAMU YA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO (ASDP ll) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018. Anayemshikia kitabu hicho ya Programu ni Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassa Mwinyi nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kuizindua katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Mahamoud Hassan Mgimwa nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kuizindua katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Tihela Chibunda nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kukabidhiwa  katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Reginald mengi  nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kukabidhiwa  katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  

Picha na IKULU

Wizara yazindua mradi wa VVU na Ukimwi kwa Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Nchini

$
0
0
Na Anthony Ishengoma Singida.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida kwa lengo la kuutambulisha kwa jamii kuhusu wasichana na wanawake vijana walio shuleni na walio nje mfumo wa Elimu.

Mradi huu unatekelezwa na  Wizara pamoja na wadau wa Maendeleo kutoka AMREF, TAYOA, TASAF, TACAIDS na Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund na wakati huu mradi uko katika hatua ya majaribio katika mikoa mitatu ya Tanzania ambayo ni Singida, Dodoma na Morogoro.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mradi huu mapema leo mjini Singida Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel Katemba amesema kimsingi Wizara yake imepewa jukumu la kuandaa mazingira rafiki na wezeshi ya utekelezaji wa Mradi huu na ndiyo maana hatua ya awali ya maandalizi inaanzia kwa kujenga uwezo kwa wataalamu wa maendeleo ya Jamii kutoka mikoa ya majaribio ya mradi.

Aidha Bw. Katemba amesema Serikali ya Tanzania imepata ruzuku kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya mapambano dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya  Ukimwi Nchini  kwa kipindi cha January 2018 mpaka Desemba 2020.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba  akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida.
 Mkurugenzi wa Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai akizungumza na wajumbe wa Mkutano wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akitoa neno la shukrani kwa viongozi wa Wizara hawako pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida.
Uongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida, Taasisi za TASAF na TACAIDS na wadau wa maendeleo kutoka Amref na TAYOA wakiwa katika picha ya pamoja  wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

Waziri Makamba awasihi wananchi kuunda kamati za Mazingira

$
0
0
Tamasha kubwa lililopewa jina la “Tulonge Mazingira na Mimi” limefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo la aina yake lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na lililenga kukuza uelewa wa wananchi juu ya hifadhi ya mazingira msisitizo ukiwa ni kutumia nishati mbadala wa Mkaa kama kauli mbiu ya Siku ya Mazingira kwa mwaka huu inavyosema.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika katika viwanja hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema wananchi wana wajibu mkubwa katika kuhifadhi mazingira na kuwataka kuwa mstari wa mbele kuuliza viongozi wao ni nini wanafanya kuhusu mazingira. “Tuulizeni kuhusu Mazingira na nini tunafanya kuhusu hifadhi ya mazingira” Makamba alisisitiza.

Aidha Mhe. Makamba ameitaka jamii kutoa taarifa juu ya mtu yeyote anaechafua mazingira katika maeneo yao kwani Sheria ya Mazingira inatoa nafasi hiyo ya kumshtaki mtu yoyote. “Sheria ya mazingira  Kifungu cha 5 kimewapa wananchi nguvu ya kushtaki kwa niaba yake kama yanaharibiwa, maana kila mtu ni mdau katika suala la mazingira,  hivyo msilalamike badala yake chukueni hatua stahiki pale mazingira yanapoharibiwa katika maeneo yenu” Makamba alisisitiza. 

Wakati huo huo, Waziri Makamba ameagiza kila mtaa, kijiji na  kitongoji katika nchi yetu kuwa na Kamati ya Mazingira ambayo kisheria ina nguvu kubwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha upelelezi kwenye jambo lolote, kufunga na kufungia kitu chochote kwenye mtaa kinachoharibu mazingira.

Kampeni hiyo ya kuhifadhi mazingira itaendelea nchi nzima na imeambatana na utoaji wa tuzo za hifadhi ya Mazingira ngazi ya Mkoa, tuzo zilizotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Felix Lyaviva. Tamasha hilo pia limehudhuriwa na viongozi wa mbalimbali wa Serikali, Wabunge na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  akihutubia wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ni sehemu ya shamrashamra za wiki ya Mazingira ambayo kilele kitafanyika Juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Kauli mbiu ya Siku ya Mazingira mwaka huu inasema “Mkaa ni gharama, tumia nishati mbadala”
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijumuika katika Tamasha la wananchi  katika Viwanja vya Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha la ‘Tulonge Mazingira na Mimi’ limefanyika mwishoni mwa wiki na kujumuisha wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Sehemu ya wananchi waliojumuika katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam wakifuatilia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

MAKADIRIO YA UJENZI WA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI MURRIET KUPITIWA UPYA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akitoa maelekezo leo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akikagua baadhi ya majengo yaliyojengwa katika Kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
Jengo la Kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha , Jijini Arusha.

1 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akikagua baadhi ya mabati yaliyotumika katika ujenzi wa Kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho

KARIAKOO KWAANZA KUFURIKA MAANDALIZI YA SIKUKUU YA EID EL FITRI.

$
0
0
 Sehemu ya Wakazi wa Dar es Salaam wakichagua nguo za watoto katika Mtaa wa Congo- Kariakoo wakichagua nguo za Sikuu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sikukuu ya Iddi  El Fitri
 Wazazi wawili wakishauriana kuchagua nguo ipi inafaa kwa watoto wao kama walivyonaswa katika Mtaa wa Congo na Agrey Kariakoo,jijini Dar leo.
Umati wa watu uliojazana Mtaa wa Congo Kariakoo kununua nguo za sikuu kwa ajili ya watoto wao katika msimu huu wa siku kuu ya Iddi  El Fitri

WIZARA YA FEDHA YALIOMBA BUNGE SHILINGI TRILIONI 12.058 MWAKA WA FEDHA 2018/19

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake, Bungeni Jijini Dodoma, ambapo ameliomba Bunge, kuiinidhinishia Wizara hiyo kukusanya na kutumia shilingi trilioni 12.058, ambapo shilingi trilioni 10.763 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.295 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, katika mwaka wa fedha 2018/19.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake, Bungeni Jijini Dodoma, ambapo ameliomba Bunge, kuiinidhinishia Wizara hiyo kukusanya na kutumia shilingi trilioni 12.058, ambapo shilingi trilioni 10.763 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.295 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, katika mwaka wa fedha 2018/19.
 Baadhi ya viongozi wa Waziri wa Fedha na Mipango, wakifuatilia Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo, ambapo Bunge limeombwa, kuiidhinishia Wizara hiyo kukusanya na kutumia shilingi trilioni 12.058, ambapo shilingi trilioni 10.763 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.295 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, katika mwaka wa fedha 2018/19.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifutilia kwa makini michango ya waheshimiwa wabunge walioanza kuchangia Bajeti ya Wizara hiyo, ambayo imeomba kudhinishiwa kiasi cha shilingi trilioni 12.058 kwa mwaka wa fedha 2018/19, Bungeni, Jijini Dodoma.
 Mhe. Martha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum wa Jimbo la Singida, akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya kuwasilisha Bungeni Mjini Dodoma, Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo ambapo ameliomba Bunge, kuiinidhinishia Wizara yake kukusanya na kutumia shilingi trilioni 12.058, ambapo shilingi trilioni 10.763 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.295 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, katika mwaka wa fedha 2018/19
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akifurahia jambo na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Francis Mwakapalila (kushoto) na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Mohammed Mtonga, nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma,  ambapo ameliomba Bunge, kuiinidhinishia Wizara yake kukusanya na kutumia shilingi trilioni 12.058, kiasi cha shilingi trilioni 10.763 kikiwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.295 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, katika Mwaka wa Fedha 2018/19
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwa katika Picha ya Pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Mnaibu Katibu Wakuu, Wakuu wa Idara na Vitengo na wafanyanyakazi wengine wa Wizara hiyo, nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma, Baada ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo, ya shilingi trilioni 12.058.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiteta jambo na Kaimu Msajili wa Hazina, Bw. Mafutah Bunini, nje ya viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, baada ya Wizara hiyo kuliomba Bunge, kuiinidhinishia  shilingi trilioni 12.058, ambapo kiasi cha shilingi trilioni 10.763 kikiwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.295 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, katika Mwaka wa Fedha 2018/19
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa, akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa, nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma, baada ya Wizara hiyo kuliomba Bunge, kuiinidhinishia  shilingi trilioni 12.058, ambapo kiasi cha shilingi trilioni 10.763 kikiwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.295 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, katika Mwaka wa Fedha 2018/19.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Dodoma)

SERIKALI KUJADILI KODI ZA MIZIGO KUTOKA ZANZIBAR

$
0
0
NA Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kujadiana kuhusu namna bora ya kupata ufumbuzi wa kudumu wa kero ya ulipaji kodi ya mizigo kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Wingwi, Mhe. Juma Kombo Hamad (CUF)M aliyetaka kujua kama Serikali ipo tayari kuunda Kamati Ndogo ya Bunge kwa ajili ya kushughulikia mfumo wa ulipaji kodi za mizigo kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.

Katika sawli hilo Mhe. Hamad alieleza kuwa mfumo wa ulipaji kodi za kusafirisha bidhaa kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu kwamba unawakwaza na kuvunja harakati za biashara Zanzibar na hivyo kusababisha uchumi wa Zanzibar kushuka.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji, alisema kuwa Serikali hizo mbili zinaendelea kujadiliana ili kuona kuwa suala hilo linapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuongeza kuwa Serikali hizo hazijashindwa kutatua changamoto hiyo na hakuna sababu ya kuunda kamati ya kushughulikia suala hilo.

Alisema chimbuko la malamiko hayo linatokana na kuwepo kwa mifumo tofauti ya kutathmini bidhaa kati ya Zanzibar na Tanzania Bara hali inayosababishwa na viwango tofauti vya ushuru wa forodha vinavyopaswa kulipwa kwa bidhaa ya aina moja kutoka nje ya nchi na kusafirishwa kwenda sehemu ya pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Kijaji alisema kuwa Mfumo wa uthaminishaji bidhaa zote zinazoingia Tanzania Bara unafanyika kwa kutumia mifumo ya TANCIS na Import Export Commodity Database (IECD) inayoratibiwa na kituo cha Huduma za Forodha kilichopo Dar es Salaam, lakini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitumii mifumo hiyo na kusababisha kuwepo na tofauti ya kodi kati ya Bara na Zanzibar.

“Kutokana na utofauti wa mifumo inayotumika, bidhaa zote za nje zinazoingia Tanzania Bara kupitia Zanzibar hufanyiwa uhakiki licha ya kuwa zimethaminiwa Zazibar, iwapo uthamini wa Tanzania Bara utakuwa sawa na ule uliofanywa Zanzibar hakuna kodi itakayotozwa Tanzania Bara na ikiwa kodi iliyolipwa Zanzibar ni ndogo, Mamlaka ya Mapato hukusanya tofauti ya kodi iliyozidi”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisisitiza kuwa utaratibu wa kukusanya tofauti ya kodi kati ya Zanzibar na Bara kwa kutumia mifumo ya TANCIS na IECD haina lengo la kuua biashara Zanzibar, bali hatua hiyo inalenga kuleta usawa wa gharama za kufanya biashara na ushindani hapa nchini.

Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 63 (2) Bunge ni muhimili unaojitegemea na hivyo Serikali haina mamlaka ya kuunda Kamati ndogo ya Bunge kwa ajili ya jambo hilo au jambo lolote

Rukwa kushirikiana na Ireland kuongeza uzalishaji wa alizeti

$
0
0
Balozi wa Jamhuri ya Ireland Paul Sherlock amepokea maombi ya ushirikiano baina ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na nchi yake yaliyolenga kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti mkoani humo jambo litakalopelekea kuinua kipato cha mkulima wa mkoa wa huo.

Maombi hayo yaliyowasilishwa na mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kwa balozi huyo mapema mwezi huu yalionyesha hali ilivyo ya uzalishaji wa zao hilo kwa sasa, ambapo kati ya hekta za shamba la Alizeti 0.5 hadi 2 huzalisha tani 1.1 badala ya tani 2.5.

“Nimefurahishwa sana na jitihada za Mh. Joachim Wangabo kwa kuona umuhimu wa kutafuta zao mbadala la biashara katika Mkoa wa Rukwa ikiwa ni pamoja na kuinua kulimo cha mkoa na kuinua kipato cha wakulima wadogo na hatimae kuwatafutia namna ya kuongeza viwanda vidogo na kuongeza ajira,” Alisema Balozi Sherlock.

Kwa upande wake Mh. Wangabo amesema kuwa zao la mahindi linazalishwa kwa wingi sana katika mkoa wake na wakulima hulichangamkia hilo zaidi ila bei ikitetereka wakulima hao wanakosa pa kujishika hivyo kwakuwa zao la alizeti ni la pili la kibiashara basi ni vyema kulitafutia mikakati liwe sawa na zao la mahindi ili wananchi wachague.

“Kwa mwaka 2016/2017 hekta 47,862 zililimwa alizeti na tukapata tani 53,470 ambayo ni chini ya kiwango tunachotakiwa kuzalisha kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa hekta 47,862 zikilimwa vizuri tunaweza kupata tani 119,655 ambayo ni ongezeko la asilimia 55, tunataka kufika huko, tuzalishe mafuta ya alizeti kwa wingi, kutengeneza ajira na kuongeza viwanda,” Alisema Mh. Wangabo.

Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutalipunguzia taifa mzigo wa kununua mafuta nje ya nchi jambo linalopelekea serikali kutumia pesa nyingi kufanya manunuzi na hatimae pesa hiyo kubaki kwa wakulima wetu. 

Mkoa wa Rukwa unatarajia kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Faida mali ambalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kukuza zao la alizeti katika Mkoa wa Singida ili kuhamishia ujuzi huo katika Mkoa wa Rukwa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji, Tanzania hutumia Shilingi bilioni 189.6 kila mwaka kununua mafuta ya kula nje ya nchi huku ikizalisha tani 91,000 ambayo ni sawa na asilimia 40 za mafuta hayo tofauti na makadirio ya tani 200,000 hadi 300,000 ya uhitaji wa bidhaa hiyo kwa mwaka.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akipeana mkono na Balozi wa Jamhuri ya Ireland nchini Paul Sherlock muda mfupi baada ya maongezi ya mikakati ya kukuza uzalishaji wa zao la Alizeti Mkoani Rukwa.

IMETOLEWA NA 
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi  kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
 Majaji watatu walioapishwa wakila Kiapo cha Maadili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali akifatiwa na Jaji Mwanaisha Athuman pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi .
 Majaji pamoja na watendaji wa Mahakama Kuu pamoja na Mahakama ya Rufani wakifatilia tukio la uapisho wa Majaji watatu Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali akizungumza mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Majaji watatu aliowaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali pamoja na Jaji Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

DIT IMEBUNI MASHINE MAALUM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA, YAWA KIVUTIO MAONESHO WIKI YA MAZINGIRA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


TAASISI ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), imeamua kubuni na kuzindua mashine maalumu ya kutengenezea mkaa mbadala.

Lengo la kubuni mashine hiyo ni jitihada za DIT katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia mikakati yake ya kukabiliana na uharibufu wa misitu na utunzaji wa mazingira.

Akizungumzia kuhusu umuhim wa mashine hiyo leo kwenye Maonyesho ya Wiki ya Mazingira yanayoyendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mkufunzi wa Idara ya Uhandisi wa Mitambo wa taasisi hiyo Asaph Kagina, amefafanua mashine hiyo yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani tatu za mkaa kwa siku ni suluhisho tosha katika kulinda misitu hapa nchini.

Amesema kuwa mashine hiyo inayotumia mabaki ya mazao mashambani, zikiwemo pumba za mpunga, mahindi, vifuu vya nazi, pumba pamoja na makaa ya mawe, imeundwa kutokana na wazo lilitokana na ripoti maalumu ya Banki ya Dunia kuhusu hali ya mazingira, pamoja na ripoti nyingine ya aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Misitu na nyuki Dk. Felician Kilahama.

Amefafanua ripoti ya Dk.Kilahama imeeleza wazi kuwa iwapo kasi ya ukataji miti itaendelea kwa kipndi cha miaka 10 Tanzania hakutakuwa na misitu ya miti na hivyo DIT kupitia watalaamu wake wameona haja ya kutafuta njia mbadala ya kupata mkaa ambayo itakuwa sahihi katika kulinda mazingira

"Ni mashine ambayo tuaamini kama ikitumika ipasavyo itatoa mchango mkubwa kwa Taifa katika kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ambalo kwa kipindi kirefu limekuwa na athari kubwa huku likihatarisha hatari ya kutokea jangwa katika miaka kadhaa ijayo" amesisitiza Kagina.

Amesema mashine hiyo maalumu imetengenezwa na wanafunzi watatu wanaosoma katika taasisi hiyo waliokaa chini na kuja na wazo la kutengeneza mashine hiyo ili kutimiza ndoto zao za ulinzi wa mazingira na misitu kwa ujumla, kitu ambacho wamefanikiwa.

Aidha alisema mashine hiyo inayotumia nishati ya umeme pamoja na dizeli, imeundwa kwa kuzingatia mazingira ya mijini na vijijini huku ikivilenga zaidi vikundi mbalimbali vya ujasiramali ili kuviwezesha kuja na mradi huo utakaovisaidia kujitengenezea faida.

Alisema gharama za ununuzi wa mashine hiyo inatokana na uhitaji wa mteja kwa kuzingatia ukubwa, huku gharama ya juu kabisa ikiwa ni cha Sh Milioni 5, na ikiwa na uwezo wa kutengeneza faida kuanzia kiasi cha Sh 900,000 kwa siku moja.

Ameziomba taasisi za kifedha kuwasadia wajasiriamali kwa kuwapa mikopo ili waweze kununua mashine hiyo na hivyo kujikwamua kiuchumi sambamba na kuunga mkono juhudi za kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini.

Michuzi Blog imeshuhudia idadi kubwa ya wananchi ambao wanafika kwenye viwanja hivyo kufika banda la DIT ambapo pamoja na kuelezwa mambo mbalimbali yanayofanywa na taasisi hiyo wengi wao wamekuwa na shauku ya kutaka kujua zaidi kuhusu mashine hiyo ambapo baadhi yao wameelezea matumaini yao kuwa ikitumika vizuri itakuwa mkombozi katika kulinda mazingira nchini.
 Mkufunzi wa Idara ya Uhandisi wa Mitambo kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT)akifafanua jambo kwa baadhi waandishi waliotaka kufahamu kwa kina machine ya kuzalisha mkaa mbadala ambayo imebuniwa na taasisi hiyo
 Mkufunzi wa Idara ya Uhandisi Mitambo Katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) Akita maelezo ya machine maalum ambayo imebuniwa na taasisi hiyo ambayo inazalisha mkaa mbadala
Mashine ya kutengeneza mkaa mbadala ambayo imebuniwa  na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

DK.KAPOLOGWE ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA VITUO VYA AFYA NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr. Ntuli Kapologwe akikagua moja ya jengo la  upasuaji  leo katika ziara ya ukaguzi wa mendeleo ya ujenzi katika kituo cha afya cha Mudemu kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma.
Jengo la Upasuaji lilojengwa katika kituo cha Afya cha Mundemu katika kituo cha afya cha Mudemu kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma.

 Timu ya Dodoma ikikagua baadhi ya miundombinu ya kituo cha afya cha Mudemu kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr. Ntuli Kapologwe akikagua ramani inayoonyesha jengo la wazazi katika kituo cha afya cha Mudemu kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma.
...............................................
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr. Ntuli Kapologwe amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya nchini  ambavyo vimejengwa  kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wafadhili mbalimbali wa Sekta ya afya nchini.

Ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo cha afya Mundemu kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jiji la Dodoma kuona maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya nchini na kujionea matumizi ya fedha ambazo zimetolewa na Serikali katika awamu ya tatu ambayo ni ya kukarabati vituo 39.

Dr. Kapologwe amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) tayari imeshaagiza vifaa tiba ambavyo vitawekwa katika majengo hayo na imeweza kuajiri watumishi wapatao 6180 ambao watapelekwa katika vituo vyote vya afya viliyoojengwa nchini ili waweze kuanza kutoa huduma kwa jamii.

Amesema vituo hivyo vitaweza kutoa huduma ya upasuaji, pamoja na huduma nyingine za wagonjwa hivyo watumishi wapya watakuwa wakitoa huduma bora kwa wananchi lengo likiwa ni kutoa huduma bora za afya na kupunguza malalamiko kwa wananchi kuhusu huduma za afya nchini.

Anaendelea kufafanua kuwa upangaji wa watumishi hao katika vituo vya afya utakuwa wa kimkakati kwa maana ya kwamba tayari wameshaainisha mahitaji na watapangiwa vituo vya kazi kulingana na mahitaji ya eneo husika ambapo kutaondoa changamoto ya upungufu wa watumishi wa afya nchini.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa Bi. Beatrice Kimoleta ameridhishwa na ujenzi wa vituo vya afya nchini na kuwataka baadhi ya maeneo kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha vituo hivyo kwa wakati.

Amesema kuwa katika Ujenzi wa vituo vya afya nchini umeweza kuzingatia dhamani ya fedha iliyotolewa na Serikali  ukilinganisha na majengo yanayojengwa ambayo ni imara na amewapongeza Kamati ya Ujenzi ya Kituo cha afya cha Mpwayungu kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo hicho.

Aidha Bi. Kimoleta  ameushauri uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa Kituo cha afya cha Mpwayungu kwa  wakati lakini kwa kuzingatia ubora wa majengo ili wananchi waweze kupata huduma za afya katika eneo hilo.

ETIHAD AIRWAYS TO LAUNCH NEW SERVICE TO BARCELONA

$
0
0
  • New flights between Abu Dhabi and Barcelona effective 21 November 2018
  • Starting with five weekly flights, service to increase to daily from 31 March 2019
Abu Dhabi, United Arab Emirates – Etihad Airways has announced the introduction of a new scheduled service linking Abu Dhabi, capital of the UAE, and Barcelona, Spain, effective 21 November 2018. The route will initially be operated five times a week by a two-class Airbus A330-200 before becoming a daily operation from 31 March 2019.

Barcelona will become the second city in Spain served by Etihad Airways, complementing the airline’s existing daily service to the capital Madrid. The new link will provide business and leisure travellers with convenient timings to travel between Abu Dhabi and Barcelona, also providing seamless onward connections through Abu Dhabi to major cities in the Indian Subcontinent, Southeast Asia, China, Japan, Korea and Australia.

Peter Baumgartner, Chief Executive Officer Etihad Airways, said: “As one of the largest unserved markets from our Abu Dhabi base, Barcelona - a hub of culture, commerce, tourism, education, fashion and science, has witnessed a significant increase in travel demand from the emirate, and from across our wider network.

“We are now delighted to announce the first direct link between these two important global hubs. We are confident it will prove very popular with UAE and Barcelona-based customers, allowing us to extend our acclaimed inflight service, hospitality and flair to this vibrant Mediterranean city, and to build on the flourishing cultural and commercial ties between the UAE and Spain.”

The Catalonia region is immensely popular with business and leisure travellers alike. With 7.5 million inhabitants, beautiful mountain scenery and a 214-kilometre Mediterranean coastline, the region is rich in natural parks and protected areas. Barcelona is one of the world’s most visited cities, famed for its unique culture, Gaudi architecture, history and cosmopolitan lifestyle.

Trade between the UAE and the Catalonia region has enjoyed significant growth in recent years, with food, chemicals, motor vehicles, energy and pharmaceuticals being the main industrial sectors.

Barcelona has recently been ranked by the International Congress and Convention Association (ICCA) as the city which hosted the most international association meetings in the world in 2017, overtaking Paris, Berlin and Vienna to claim first place for the first time since 2004. Etihad Airways will increase frequency to the city to meet passenger demand for the Mobile World Congress, which takes place from 25-28 February 2019.

The new service is being launched in time for the start of the 2018 Formula 1 Etihad Airways Abu Dhabi Grand Prix, the Middle East’s largest sporting event, held from 23-25 November at the capital’s 5.55 kilometre Yas Marina Circuit.

Barcelona is one of the busiest cruise ports in the world and an important source market of cruise traffic for Etihad Airways. Abu Dhabi has also emerged as one of the leading cruise destinations in the Arabian Gulf region, with over 329,105 cruise tourists visiting the city during the 2017 season. The new direct service between the two cities will ensure Abu Dhabi remains a leading player in the region’s cruise travel ambitions.

Etihad Airways operates an extensive codeshare partnership with Air Europa (UX), on the Spanish airline’s scheduled services from Madrid to Barcelona and 18 other major European cities.

Flight schedule: Abu Dhabi – Barcelona, effective 21 November 2018:
Flight No.
Origin
Departs
Destination
Arrives
Frequency
Aircraft
EY 49
Abu Dhabi
2:20
Barcelona
06:45
Mon, Wed, Fri, Sat, Sun
Airbus A330-200
EY 50
Barcelona
09:50
Abu Dhabi
20:00
Mon, Wed, Fri, Sat, Sun
Airbus A330-200

Note: All departures and arrivals are listed in local time

CMSA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI KATIKA MASOKO YA MITAJI

$
0
0
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, akizungumza katika mafunzo ya  watendaji  katika masoko ya mitaji ikiwa ni utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kisera, kisheria na kiutendaji unaofanywa na CMSA.
Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Charles Shirima, akizungumza katika mafunzo ya  watendaji katika masoko ya mitaji ikiwa ni utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kisera, kisheria na kiutendaji unaofanywa na CMSA.
Washiriki wa mafunzo hayo.
  Washiriki wa mafunzo.
Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Charles Shirima, akizungumza katika mafunzo ya  watendaji katika masoko ya mitaji ikiwa ni utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kisera, kisheria na kiutendaji unaofanywa na CMSA.
Picha ya pamoja.


MAMLAKA ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) imewaasa watendaji katika masoko ya  Mitaji kuhudhuria mafunzo yanayotambulika katika viwango vya kimaitafa ili kupata ujuzi na kuwa wabobezi katika masoko ya kimaitafa.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama, katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Watendaji katika Masoko ya Mitaji (SICC) iliyoendeshwa kati ya CMSA na Taasisi ya Uwekezaji na Dhamana (CISI) ya nchini Uingereza.

Alisema chini ya kifungu namba 32 cha Sheria ya Masoko ya Mitaji ya 1994 kama ilivyorekebishwa mwaka 2010, mtu yeyote anayetaka kutoa huduma katika masoko ya mitaji kama Dalali wa Soko la Hisa, Mwakilishi wa Dalali wa Soko la Hisa, Mshauri wa Uwekezaji, Mwakilishi wa Mshauri wa Uwekezaji, Mshauri Mteule, Mwakilishi wa Mshauri Mteule au mtendaji yeyote katika masoko ya mitaji ni lazima apitie mafunzo yanayotolewa na CMSA na kufaulu.

Mkama alisema lengo la sharti hilo ni kuhakikisha kuwa watendaji na wataalamu katika masoko ya mitaji wanakuwa na ujuzi stahiki katika utoaji wa huduma za masoko ya mitaji ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri katika uuzwaji wa dhamana kwa umma na uorodheshwaji wake kwenye masoko ya hisa. 

"Tangu kuanzishwa kwake, CMSA imekuwa ikitoa mafunzo hayo na mpaka sasa zaidi ya watalamu 560 wamefuzu," alisema.  

Alisema katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki, (East African Common Market Protocol), Taasisi za Usimamizi wa Masoko ya Mitaji za Afrika (EASRA) zilipitisha na kukubaliana kuwa watendaji wanaotaka kutoa huduma katika masoko ya mitaji ya Afrika Mashariki ni lazima wapitie mafunzo na kufaulu mtihani unaotambulika kimataifa. 

"Hivyo utaona kuwa hii ni moja ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kisera, kisheria na kiutendaji unaofanywa na CMSA ili kuwezesha masoko ya mitaji kuwa na watendaji wengi wenye ujuzi na weledi wa kukuza uwekezaji kupitia masoko ya mitaji na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha, hususani masoko ya mitaji na uchumi hapa nchini," alisema

Alisema ukanda wa wa Afrika Mashariki unaendesha mafunzo hayo kwa kufuata mitaala inayoshabiana ikiwemo kushirikiana na CISI.Mkama alisema lengo la kozi hiyo ni kuandaa watendaji na watalamu wa masoko ya mitaji wenye utaalamu na ujuzi wa viwango vinavyoendana na kasi ya maendeleo na mabadiliko yanayotokea katika huduma za masoko ya mitaji kimataifa, hivyo kuleta weledi na ubobezi katika masoko. 

"Mafunzo haya yanajumuisha washiriki 64 ikiwa ni washiriki 24 zaidi ya lengo la washiriki 40. Mwitikio huu unatokana na ongezeko la uelewa na uhitaji wa wataalamu wa masuala ya masoko ya mitaji hapa nchini," alisema Mkama.

Aidha alisema kwamba wahitimu watapata fursa ya kuomba leseni ya kutoa huduma katika sekta ya masoko ya mitaji kwa ngazi za kimataifa. Hatahivyo alisema kwamba CMSA itaendelea kushirikiana na wadau kujenga mazingira bora, wezeshi na endelevu yenye lengo la kuendeleza na kukuza masoko ya mitaji nchini.

WALINZI WA HIFADHI WATAKIWA KUWA MAKINI NA WADILIFU KUTOKANA NA WANYAMA KUTOKA NJE YA HIFADHI

$
0
0

WALINZI wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wametakiwa kuwa makini na waadilifu kutokana na kuongezeka kwa wanyama adimu wanaofika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA).Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo.

Meja Jenerali Semfuko, alisema kazi ya kupambana na ujangili inahitaji uvumilivu, uadilifu na ujasiri mkubwa kutokana na mazingira hatarishi yaliyopo."La muhimu kuna taatifa maeneo haya wameanza kuja wanyama adimu hivyo ningependa muongeze jitihada hizi mara dufu wanyama hao wasidhurike," alisema.

Katika ziara hiyo wajumbe wa Bodi ya TAWA walipokea taarifa ya timu ya pamoja kati ya TAWA, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Frankfurt Zoological Society ( FZS), TAWIRI na Friedkin Conservation Fund (FCF) katika kuhifadhi na kulinda na kuhifadhi wanyama adimu.Taarifa hiyo iliyowasilishwa na wataalamu Philbert Ngoti wa TANAPA na Gerald Nyaffi wa FZS katika eneo la kitalu kilichopo Maswa Mbono kinachoendeshwa na kampuni ya Tanzania Game Tracker Safaris (TGTS).

Wataalam hao walisema wamefanikiwa katika mradi huo kwa ufadhili wa familia ya Friedkin inayomiliki TGTS ililiyofadhili fedha, vifaa pamoja na helikopta, kazi ijayotarajiwa kuendelea katika maeneo mengine.Katika ziara hiyo TAWA imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na upigaji picha za kitalii, yaliyopo katika maeneo yake kwa kusimamia uhifadhi na ulinzi pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi yenye thamani zaidi ya sh 40 bilioni.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Dk James Wakibara akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchango kwa jamii, uhifadhi na kiuchumi wa makampuni ya uwindaji wa kitalii zilizowekeza katika maeneo yao.Maeneo yaliyotembelewa na TAWA ni pamoja na Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori(WMA) ya Makao wilayani Meatu inayosimamiwa na kampuni ya Mwiba Holdings Limited.

Dk Wakibara alisema, licha mchango wa makampuni kwenye jamii, pia TAWA kupitia malipo ya kampuni hizo, imekuwa ikitoa takriban sh 6.5 bilioni kila mwaka kwa vijiji vyenye wawekezaji hao na halmashauri.Makampuni hayo yamewekeza katika baadhi ya maeneo ya vitalu 159 vilivyopo nchini na maeneo ya hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA) 38 zilizopo nchini.

"Hizi kampuni za kitalii zina mchango mkubwa sana pia katika uhifadhi wa maeneo haya, hasa katika vita dhidi ya ujangili ikizingatiwa asilimia 95 ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini yapo chini ya TAWA"alisema.Alisema kwa sasa mapato ya TAWA kutokana na shughuli za uhifadhi, yamefikia dola 20 lakini kuna mikakati ya kuongeza mapato hayo mara nne zaidi hadi kufikia dola 80.

"kuna dhana potofu kuwa uwindaji wa kitalii ni kumaliza wanyama hili sio kweli, kwani haya makampuni hayajawahi kufikia hata robo kiwango cha kuwinda wanyama ambacho kinatolewa kila mwaka na TAWA na mashirika ya kimataifa"alisema

Mwenyekiti wa bodi ya TAWA, Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko alisema mamlaka hiyo ipo katika mabadiliko makubwa ili kuhakikisha jamii inanufaika zaidi ya uhifadhi wa wanyamapori,katika kusaidia miradi ya kijamii ya maji, afya Elimu na uhifadhi.

Mwenyekiti huyo na bodi yake ambao walitembelea pori la Makao, lilipo mpakani mwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Meatu,alisema wameridhishwa na utendaji wa kampuni ya Mwiba Holding katika eneo hilo
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA) Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko, Akikagua Gwaride la Askari wa Wanyamapori wa pori la akiba Maswa.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA),Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko akiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa Wizara ya Maliasili washirika wake

KANDEGE APONGEZA USIMAMIZI WA UJENZI WA VITUO VYA AFYA ARUSHA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akikagua jengo akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha .
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akipatiwa maelezo wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha
Moja ya jengo lililojengwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Jiji la Arusha.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege amepongeza usimamizi mzuri uliofanyika katika ukarabati na ujenziwa vituo vya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Jijini Arusha.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara hivi karibuni ya kukagua maendeleoya ujenzi wa vituo vya afya vya Nduruma kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Jijila Arusha na Kituo cha afya cha Usa River Kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Meru, Jijini Arusha.

Mhe. Kandege amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya Jijini Arusha, na kuwapongeza kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo ni imara na yanaendana na dhamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

“Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya katika Jiji la Arusha ipo vizuri na kazi inayofanyika inaridhisha ukilinganishwa na fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya nchini.

Mhe. Kandege ametoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili huduma za afya ziweze kutolewa kwa wananchi.Amezitaka Halmashauri kutengeneza mazingira mazuri ya vituo vya afya nchini ikiwa ni pamoja na kuweka uzio, kupanda miti hasa ya matunda ili kutengeneza mandhari inayovutia kwa wagonjwa pindi wanapohitaji kuaptiwa huduma ya afya.

Akiongelea kuhusu vyumba vya kujifungulia wanawake wajawazito Mhe Kandege ameelekeza chumba cha kujifungulia kitenganishwe kila kitanda ili kuwa na usiri wamama mjamzito anapojifungua.

RC MGHWIRA ATOA ONYO KALI KWA WANAOHARIBU MIUNDOMBINU YA TANESCO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza na waandishi wa habari katika kampeni maalumu ya kuzuia uharibifu wa miundombinu ya umeme mkoani humo. 
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi inayoendelea mjini Moshi 
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi ya umeme inayoendelea mjini Moshi pembeni ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Salama
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi ya umeme inayoendelea mjini Moshi pembeni ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Salama.
Mafundi wa Tanesco wakikata miti iliyopita katika njia za umeme Moshi. 

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi Anna Mghwira ametoa onyo kali kwa wakazi wa mkoa huo wanao jihusisha na uhabifu wa miundombinu ya Shirka la Umeme Tanzania (Tanesco) na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema, serikali inatumia gharama kubwa sana kuendesha shirika hilo hivyo kulihujumu kwa kuharibu miundimbinu sio sahihi na halivumiliki. 

Aliyasema hayo jana wakati akiongea na waandisi wa habari, katika kampeni maalumu inayofanywa na Tanesco makao makuu ikiwa na lengo la kuhamasisha juu ya athari za kuhujumu miumbombinu ya shirika hilo. 

“Hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya baadhi ya watu kupoteza maisha baada ya kujaribu kujiunganishia umeme kwa njia ya wizi. naagiza wakazi wa mkoa huu kuacha kabisa tabia hiyo kwani matukio ya aina hiyo ni sawa na matukio ya uhujumu uchumi, ambayo yanarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana na hivyo kufikia uchumi wa kati kupita viwanda,” alisema 

Aliongeza kuwa uhujumu wa miundombinu sio tu inaleta hasara kwa shirika lakini pia inapelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa kupitia maafa mbalimbali ikiwemo vifo na ulemavu kwa watu wanaohusika na matukio hayo. Naye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro Mahawa Mkaka alisema changamoto ya uharibifiu wa miumbombinu unatokana na uelewa mdogo kuhusiana na madhara yatokanayo na umeme. 

Pamoja na hayo shirika katika mkoa linajitahidi kufanya uhamasishaji wenye lengo la kuelemisha watu kujiepusha na uharibifu wa miundombinu. 
“Tunatoa rai kwa wakazi wa mkoa huu kuwa madhalani wanataka kukata miti ambayo ipo karibu ya nyaya za Tanesco watoe taarifa ili wataalamu wetu wasaidie kwenye zoezi kwa kinyume na hapo wanaweza kupata matatizo ikiwemo kifo,” alisema meneja 

Alisema kwa mwaka jana zaidi ya ajali zipatazo 30 ikiwepo ajali za moto na watu kupoteza maisha kutokana na matukio mbalimbali, “Nia ya shirika ni kuona tunamaliza mwaka bila ajali hata moja inayotokana na umeme,” Aidha, maneja alisema kwa mwaka mkoa unapoteza asilimia mbili ya mapato yanayotokana na wizi wa umeme na uharibifu wa miundombinu ambapo fedha hizo zingetumika kuboresha zaidi upatikanaji wa umeme wa uhakika. 

Maneja huyo amewaomba wakazi wa mkoa huo kuendelea kushirikiana na shirika ili kuwabahini wanaoendeleza vitenda vya wizi na uharibifu. Alisema mwaka jana pekee zaidi ya Sh50 milioni zilipatikana kutoka na faini mbalimbali zinazotokana na uharibifu wa miundombinu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

MAKAMU WA RAIS AZINDUA UKUTA WA FUKWE WA BAHARI- BARABARA YA BARACK OBAMA DAR ES SALAAM

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images