Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1592 | 1593 | (Page 1594) | 1595 | 1596 | .... | 1896 | newer

  0 0


  Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akionesha kadi ya uanachama wa mfuko huo alipokuwa akizungumza na wajasirimali kwenye kongamano lililofanyika ukumbi wa vijana mwisho wa wiki Jijini Dodoma
  Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akizungumza na wajasiriamali katika kongamano lililofanyika ukumbi wa vijana mwisho wa wiki Jijini Dodoma
  Wajasiriamali wakiwa kwenye kongamano uliofanyika jana Jijini Dodoma ambalo liliandaliwa na Mfuko wa NSSF.



  MFUKO wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) umewashauri wajasiriamali nchini kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kutambuliwa na kupata mikopo.

  Ushauri huo umetolewa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma wakati alipokuwa akitoa mada yake kwenye Kongamano la Wajasiriamali lilifanyika jijini Dodoma.

  Chuma amesema wajasiriamali hao wakiunda na kuvisajili vikundi vyao watapata mikopo kutoka NSSF ili kukuza biashara zao.Amesema mfuko huo hautaweza kumsaidia mwananchi mmoja mmoja kwani masharti ya mikopo itatolewa kupitia vikundi au Saccos mbalimbali zilizosajiliwa.

  “Lengo la mikopo hii ni kuunga jitihada za serikali katika kuwainua wananchi wa kipato cha chini kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025,”amesema.Pamoja na kupata mikopo wajasiriamali hao, watapata fursa ya kujiunga na pia na kuchangia michango katika mfuko huo jambo ambalo litawawezesha wanachama kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF.

  Alitaja baadhi ya mafao hayo kuwa ni fao la Afya linalomwezesha mwanachama aliyejiunga kupata huduma za afya na mafao mengine kusaidiwa wakati wa majanga ya ajali au msiba.Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira na Vijana Anthony Mavunde amewataka wajasiriamali hao kuwa waaminifu katika kuchukua na kurejesha mikopo hiyo ili na waweze kukopeshwa.

  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amefanya ziara katika mitaa ya Jiji la Dodoma, kukagua upatikanaji wa huduma ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs), ambazo mfumo wake ulipata hitilafu hivi karibuni ambao hivi sasa umetengemaa na kubaini kuwa licha ya hitilafu iliyotokea, wafanyabiashara wengi katika jiji hilo hawazitumii ipasavyo
  mashine hizo.

  Dkt. Kijaji aliyeambatana na Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Elijah Mwandumbya, amewaonya wafanyabiashara kote nchini wanaokiuka masharti ya matumizi ya mashine hizo kuacha vitendo hivyo mara moja na kuiagiza TRA kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara wasiotoa risiti za kieletroniki baada ya kuuza bidhaa zao.

  "Wanauza mauzo yao vizuri lakini hawatoi risiti, tumeongea nao kuwaeleza kuwa wanapaswa kutoa risiti wanapouza bidhaa na huduma zao kwani suala hilo ni la kisheria, ni lazima litekelezwe" alionya Dkt. Kijaji.Alisema kuwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuelewa kuwa maendeleo ya nchi hayawezi kupatikana bila kukusanywa kwa kodi sahihi.

  "Tunadai maji, huduma za afya, barabara nzuri, bila kukusanya na kulipa kodi haiwezekani tukayafikia haya malengo ya kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati" aliongeza Dkt. Kijaji

  Kwa Upande wake, Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA Bw. Elijah Mwandumbya, amesema kuwa wafanyabiashara wasiotumia ipasavyo mashine za EFD watakabiliwa na adhabu kali inayofikia shilingi milioni nne na nusu kwa kutokutoa risiti huku mteja akikabiliwa na faini ya shilingi elfu thelathini kwa kutokudai risiti inayolingana na thamani ya bidhaa alizonunua.

  "Ni kosa kuwa na mauzo ambayo hujayatolea risiti na ndio maana tunawapa fursa hii waweze kuweka kumbukumbu zao sawasawa kwa sababu tumegundua baadhi yao wanayo mauzo lakini hawajatoa risiti" aliongeza Bw. Mwandumbya.Bw. Mwandumbya ameeleza kuwa ukaguzi wao umeonesha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya mashine za kieletroniki zinafanyakazi ipasavyo baada ya kutengemaa kwa mfumo wa kuchakata taarifa za mauzo kwa njia ya kieletroniki uliopata hitilafu tangu Mei 11 mwaka huu na kusababisha baadhi ya mashine hizo za EFD kutofanyakazi.

  Aliwataka wafanyabiashara kuingiza mauzo yote waliyoyafanya katika kipindi chote ambacho kulikuwa na hitilafu ya kimfumo katika mashine ya EFD na kutoa risiti moja ya mauzo hayo ili yaweze kutambulika katika mfumo wa mapato wa TRA kwa ukadiriaji sahihi wa kodi za biashara zao.

  0 0

  Na Agness Francis, Globu ya Jamii

  MCHEZAJI Donald Ngoma aliyesaini na timu ya Azam FC kwa mwaka mmoja akitoke Yanga SC anatarajiwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu yake.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo Jaffary Iddy amesema Ngoma ataambatana na Dk. Mwanandi ambaye ndiye mkuu wa kitengo cha afya Azam FC kuelekea mji wa CaptTown kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya St Parot.

  Amefafanua wataondoka ya saa 9:45 usiku wa leo kwa kutumia usafiri wa Shirika la Ndege la Kenya Airways.“Uongozi wa Azam unampeleka mchezaji huyo katika matibabu kwa kuwa wanaamini ana uwezo na atatoa mchango mkubwa katika klabu yetu,”amesema.

  Mchezaji huyo raia wa Zimbawe alisajiliwa na matajiri hao wa chamazi akiwa majeru wa muda mrefu mpaka kupelekea kutokufanya vizuri msimu mzima uliopita kwa wajiri wake wa zamani Yanga SC.

  Jaffary Iddy amesema Ngoma atafanyiwa matibabu ya vipimo vya afya yake  kwa gharama zozote.

  "Mchezaji huyu akikutwa na ugonjwa atatibiwa kwa gharama zozote ilimradi apone na kucheza na ikionekana hana tatizo lolote atarudi Dar es salaam kwa ajili ya kuongeza mkataba mnono zaidi na kuitumikia Azam FC kwa muda mrefu katika Ligi Kuu Tanzania Bara,"amesema Jaffary.
  Mchezaj Donald Ngoma aikiwa katika Jezi za waajiri wake wa zamani YangasSc.

  0 0


  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mst. Thomas Mihayo (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuhusu Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 kabla ya kuzindua maonesho hayo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (wa tatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kilifair Promotion, Tom Kunkler (kushoto).

  Na Hamza Temba-WMU-Moshi
  ....................................................................... 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa wito kwa taasisi za Serikali, jamii, sekta binafsi na wadau kwa pamoja kushirikiana kuendeleza utalii katika maeneo yao ili sekta hiyo iweze kunufaisha zaidi taifa kwa kiwango kinachostahiki kuliko ilivyo hivi sasa.


  Ametoa wito huo juzi katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi wakati akifungua maonesho ya kimataifa ya utalii ya Karibu/Kili Fair 2018 ambayo yameshirikisha makampuni na wadau wa utalii zaidi ya 350 kutoka nchi zaidi ya 12 duniani huku na kuvutia watu zaidi ya 4,000 kuyatembelea.



  Amesema ushirikiano huo utaiwezesha sekta hiyo kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa ambao kwa sasa ni takriban asilimia 17.2 ya pato la Taifa, zaidi ya asilimia 24 ya mapato yote ya fedha za kigeni sambamba na zaidi ya asilimia 10 ya ajira zote nchini.

  Amesema mchango huo bado ni mdogo ukilinganisha na aina na idadi ya vivutio vilivyopo hapa nchini.

  Dkt. Kigwangalla amesema Serikali ya awamu ya tano imeshaanza kuchukua hatua mbalimbali zitakazosaidia kuboresha sekta hiyo ikiwemo ujenzi unaoendelea wa reli ya kisasa ya Standard Gauge, ujenzi wa Terminal 3 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Saalam na uboreshaji wa Shirika la Ndege la ATCL.

  Pamoja na hayo amesema Serikali kupitia wizara yake inaendelea na mpango wa kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini ili kuongeza idadi ya watalii na mapato ambapo Mapori matano ya Akiba mkoani Kagera na Geita yatapandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa (Burigi, Biharamulo, Kimisi, Ibanda na Rumanyika).

  "Napenda kumshukuru sana Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuridhia mapendekezo yetu ya kupandisha hadhi Mapori matano ya Akiba kuwa Hifadhi ya Taifa ambayo itaitwa Chato National Park, 'Tunatake pia advantage' ya uwepo wa uwanja wa ndege wa Chato ambao unajengwa katika kiwango cha kutua ndege kubwa zitakazowawezesha watalii kufika katika hifadhi hiyo" amesema Dkt. Kigwangalla. 

  Amesema hatua hiyo itafungua utalii wa kanda ya Kaskazini Magharibi tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo ni kanda ya kaskazini pekee inayofanya vizuri zaidi kwenye sekta hiyo. Amesema mpango huo unakwenda sambamba na kufungua utalii wa kanda ya kusini ambapo mradi wa Kusimamia Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (REGROW) upo katika hatua ya utekelezaji.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi amesema Serikali kupitia bodi hiyo itaendelea kushirikiana na wadau kutangaza utalii wa Tanzania katika maonesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi sambamba na kuwashirikisha kunadi kauli mbiu mpya ya utalii wa Tanzania, "Unforgettable, Tanzania".

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kamati hiyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali na wadau hususan katika eneo la mabadiliko na maboresho ya sheria za kusimamia sekta hiyo iweze kuondokana na changamoto zilizopo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akijaribu kuendesha baiskeli maalum ambayo hutumika kwenye utalii wa baiskeli kwenye maeneo mbalimbali ya hifadhi nchini baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 
  Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Devotha Mdachi wakiwa katika meza kwenye hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kabla ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Ltd,Tom Kunkler, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mkurugenzi wa Karibu Fair, Dominick Shoo na viongozi wengine wa Serikali na sekta binafsi wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 
  Mkurugenzi wa Karibu Fair, Dominick Shoo akiratibu ratiba nzima ya ufunguzi wa maonesho hayo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kwenye eneo la mfano wa kilele cha Uhuru cha mlima Kilimanjaro baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na viongozi wengine wa Serikali na sekta binafsi wakiwa kwenye eneo la mfano wa kilele cha Uhuru cha mlima Kilimanjaro baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 
  Waziri Kigwangalla akisalimia baadhi waoneshaji katika banda la utalii wa kiutamaduni kwenye maonesho hayo.
  Waziri Kigwangalla akiangalia moja ya gari la kitalii la wazi katika maonesho hayo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya gari maalum la kusafirisha watalii ambalo limebuniwa hapa nchini na kampuni ya Hanspaul Automechs Ltd ya Jijini Arusha baada ya kufungua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni hiyo, Satbir Singh Hanspaul.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (kulia) kwenye moja gari maalum la kifahari la kusafirisha watalii ambalo limebuniwa hapa nchini na kampuni ya Hanspaul Automechs Ltd ya Jijini Arusha baada ya kufungua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
  Waziri Kigwangalla akipanda gari maalum la kusafirisha watalii katika maonyesho hayo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa wizara hiyo, Deogratious Mdamu wakiwa ndani ya gari hilo maalum la kusafirisha watalii kwenye maonyesho hayo.
  Waziri Kigwangalla akiwa amejilaza kwenye moja ya kitanda maalum katika hema la kitalii katika maonesho hayo. 
  Waziri Kigwangalla akiteta jambo na Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Jorg Herera katika moja ya chumba maalum cha wazi cha kitalii katika maonesho hayo.
  Waziri Kigwangalla, Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Jorg Herera na viongozi wengine wakishuka kutoka kwenye chumba hicho cha wazi cha kitalii katika maonesho hayo.
  Waziri Kigwangalla akiwa kwenye banda la Bodi ya Utalii na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa bodi hiyo, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (kushoto), Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi (wa pili kushoto), wafanyakazi wa bodi hiyo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Promotion Tom Kunkler.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki kupekecha mti maalum uliokuwa ukitumika enzi za mababu kwa ajili ya kufua moto katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 yanayoendelea katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Longido, Dkt. Steven Kiruswa (wa pili kulia) wakishiriki kucheza ngoma za kimasai na kikundi cha ngoma cha kabila hilo baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.

  0 0


  0 0

  Na Agness Francis,Globu ya Jamii.

  KIKUNDI cha  ngoma cha Bujora Dance  kililokwenda Nchini India katika tamasha la michezo ya asili Afrika kimerejea nchini. 

  Kundi hilo lililofanya vizuri zaidi katika mashindano ya Tulia Traditional Dances Festival 2018  ambao waliibuka kuwa ndio washindi limeifanya Tanzania kuwa kivutio huko nchini India.

  Ambapo kundi hilo kutokea mwanza Mei 25 mwaka huu ndio lilianza kufanya kazi hiyo ya michezo  asili ya Mtanzania ambapo waliifanya nchi yetu kuwa kivutio katika tamasha la hilo iliyoshirikisha nchi nane  lenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kitamaduni.

  Kiongozi wa msafara huo Hassan Ngoma amesema kuwa  tamasha hilo lililokonga nyoyo za watu wengi sana  lilifanyika katika miji mitatu  New Delhi, khairagah pamoja na Chandigarh huko nchini India.

  Ambapo Usiku wa May 27 heshima nyingine ya Tanzania ilitengenezwa katika mji wa Chandigarh nchini hapo huku kundi  hilo la ngoma za asili  walionyesha tena uwezo wao katika tamasha hilo.

  Ngoma amesema usiku wa Mei 30 ndio walihitimisha kufanya maonyesho yao  katika tamasha hilo la wiki ya Afrika ambapo walimalizia kwa kutoa burudani ya uhakika katika mji wa Khairagarh wakiwa ndio waalikwa pekee katika mji huo.

  "Imekuwa fursa nzuri kwetu ya kuitangaza tamaduni ya kitanzania kwa nchi mbali mbali lilitoshiriki tamasha la michezo ya asili Afrika" amesema Hassan Ngoma.
   Kiongozi wa msafara Hassan Ngoma(katikati) akiwa pamoja na wanakikundi cha Ngoma cha Bujora cha Mkoani  Mwanza wakiwa wamewasili kutoka Nchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti.
  Kikundi cha Bujora kikiwa kimewasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakitokeaNchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti.

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Moto ambao hadi sasa chanzo chake hakijafahamika umeteketeza maduka nane , stoo pamoja na mali za wafanyabiashara ambazo thamani yake haijafahamika, katika Mji mdogo wa Lamadi wilaya ya Busega Mkoani Simiyu , usiku wa tarehe 02 Juni.

  Akizungumzia jinsi moto huo ulivyoanza mmoja wa wakazi wa Lamadi aliyeshuhudia tukio hilo, Bw. John Balele amesema moto ulianza kuwaka katika moja ya chumba cha duka majira ya saa mbili usiku na baadaye ukaanza kusambaa katika vyumba vingine lakini hawakuweza kufahamu chanzo chake maana vyumba vyote vilikuwa vimefungwa.
  “Huu moto umetokea majira ya saa mbili hivi tulivyouona tukapiga simu polisi, askari polisi wakaja na askari wa zimamoto, Zimamoto wamejitahidi kuwahi kufika na wametusaidia sana kutuelekeza namna ya kukabiliana na moto huu tukafanikiwa kuuzima na kuokoa baadhi ya mali japo mali nyingi zimeteketea lakini hakuna mtu aliyedhurika; binafsi nawashukuru sana wananchi wenzangu wa Lamadi kwa moyo wao wa kujitolea” alisema John Balele.

  Diwani wa kata ya Lamadi, Mhe. Laurent Bija amewashukuru wananchi kwa namna walivyojitoa kushirikiana na jeshi la polisi na kikosi cha Zimamoto na uokoaji katika kuukabili moto huo na kulinda baadhi ya mali zilizookolewa kwa uaminifu .

  Aidha, Diwani huyo ametoa pole kwa wafanyabiashara ambao mali zao zimeteketea na akatoa wito kwa wafanyabiashara wote katika Kata hiyo kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika maeneo yao ya biashara, ili viweze kuwasaidia katika hatua za awali za kukabiliana na moto pindi unapotokea.

  Akizungumza wananchi wa Lamadi waliojitokeza kuzima moto huo wakishirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Polisi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapa pole wafanyabiashara ambao wamepoteza mali zao katika ajali hiyo ya moto na akawashukuru wananchi wa Lamadi kwa ushirikiano na uaminifu waliounesha wakati wa kuzima moto huo.
  Mtaka amesema kwa kuwa chanzo cha moto huo hakijafahamika Serikali kupitia TANESCO na Zimamoto itaendelea kutafuta na kubaini chanzo na tarehe 03 Juni, 2018 Serikali itafanya tathmini kujua madhara yaliyosababishwa na moto huo.

  “ Nawapa pole wananchi wa Lamadi bado hatujajua chanzo hasa, wenzetu wa TANESCO na Zimamoto watatusaidia kujua chanzo, kuhusu madhara kwa kuwa sasa ni usiku kesho Serikali itafanya tathmini ili na sisi tuone namna ya kuzungumza na wenzetu wa benki na kuona busara gani itumike kuwasaidia wafanyabiashara waliokopa namna ya kurejesha, wakati wanajipanga upya” alisema

  Mkuu huyo wa Mkoa pia ametoa wito kwa Taasisi za Bima hapa nchini kupanua wigo na kuwafikia wafanyabiashara na kuona namna sahihi ya kuwa msaada kwao pale wanapokutana na majanga yasiyoepukika yakiwemo ya moto, huku akisisitiza wafanyabiashara kuchukua tahadhari ya moto ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vifaa vyote vya umeme vimezimwa wanapofunga biashara zao. 
  Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Jeshi la Zimamoto kuendelea kutoa elimu ya majanga ya moto hasa kwenye maeneo ya masoko ili waweze kuchukua tahadhari ya moto na akawataka wale wanaojenga majengo ya biashara kupata ushauri wa kitaalam juu ya ujenzi wa majengo yao

  Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Simiyu, Gervas Fungamali amesema Jeshi la polisi litaendelea kutoa elimu kwa wananchi hususani juu ya umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto na kuchukua tahadhari ya moto katika maeneo yao.

  0 0


  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

  NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema sekta ya ufugaji samaki inakua na inasaidia katika kuongeza ajira na kipato kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na hiyo ni kutokana na ubora wa samaki wanaozalishwa nchini.

  Ulega ametoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya kutembelea Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Mbegani, shamba la ufungaji wa samaki la NFCO Ruvu,Ruvu fish farm Mlandizi,Kiwanda cha kuzaliza chakula cha kuku na samaki,Hill feeds Mapiga,wakulima wa Mwani Bagamoyo Milingotini.

  Aidha amesema vijana wengi wanamaliza vyuo na kukosa ajira, hivyo wataboresha sekta hiyo ili kuongeza ajira kwani biashara ya samaki inalipa na kwa kasi iliyopo Taifa na wananchi watapata kipato kikubwa.

  Akizungumzia kuhusu kutopatikana kwa vifaranga Ulega ameeleza wamejipanga katika kutatua tatizo hilo hasa katika kuhakikisha uzalishaji unaongezeka katika vituo vya uzalishaji wa vifaranga vya samaki kama Luhila Songea na Nyegezi mkoani Mwanza.

  Pia amesema changamoto ya chakula cha samaki imetatuliwa na baada ya kutembelea kiwanda cha chakula cha Hill Package kilichopo Mpinga Bagamoyo ameridhika na utendaji na uzalishaji wa chakula cha samaki katika kiwanda hicho. Hivyo amewashauri wafugaji kutumia chakula kutoka katika kiwanda hicho kinachomilikiwa na wazawa na badala ya kuagiza chakula kutoka nje ya nchi.

  Ametoa mwito kwa wananchi kushirikiana na Serikali kutokomeza uvuvi haramu ili kuongeza kipato kwa wavuvi na taifa kwa ujumla. 
   Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia akiangalia sabuni pamoja na mafuta ya kupaka yanayotengenzwa na zao la Mwani katika kijiji cha Bagamoyo mkoa wa Pwani.
   Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (kulia) akimsikiliza Mmiliki wa Shamba la kufugia samaki,Khumbo Kathenga
   Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (katikati) akiangalia vyakula vya kuku na samaki vinanyo zalishwa na kiwanda cha  Hill feeds kilichopo Mapiga mkoa wa Pwani.
  Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (kushoto) akizungumza na wamiliki wa shamba la samaki lilipo Ruvu mkoa wa Pwani.

  0 0

  KIJANA wa miaka 18 kutoka Saudi Arabia, Ibn Rayizah Hatim Abdullah ameibuka na kitita cha dola za Marekani 5,000 kwenye fainali za 26 za tuzo ya Kimataifa ya Quran tukufu.

  Kijana Rayizah ameibuka na kitita hicho baada ya kuwashinda wenzake sita waliofanikiwa kuingia fainali hizo ambao walitoka Yemen, Zanzibar, Malaysia, Mali, Marekani na Tanzania Bara.

  Nafasi ya pili imechukuliwa na kijana Hamza Soukouna (25) kutoka Mali ambaye amejishindia dola za Marekani 4,000 na ya tatu imechukuliwa na Hamza El-Habashiy (18) kutoka Marekani ambaye amejishindia dola za Marekani 3,000. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania, mwaka huu yalishirikisha vijana 16 kutoka nchi 16 duniani.

  Akizungumza na mamia ya waumini wa Kiislamu waliofurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo mchana (Jumapili, Juni 3, 2018), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini hiyo waendelee kuwakamata vema vijana waliohifadhi Quran na kuwaendeleza kitaaluma katika fani nyingine za elimu ya kimazingira.

  “Leo hii nimefarijika sana kusikia kwamba tunao vijana wetu ambao si tu wamehifadhi Quran bali pia wamehitimu fani mbalimbali katika elimu ya juu. Uwepo wa vijana wa namna hii ni muhimu katika kujenga jamii bora na yenye kuzingatia uadilifu katika kutekeleza majukumu yao,” amesema.

  Amesema kazi ya kuhifadhisha Quran haiishii katika kujua kuisoma pekee. “Kuhifadhisha Quran kunapaswa kuwa msingi imara katika kujenga jamii bora kupitia mafunzo sahihi ya tabia njema, utii lakini pia kujua mipaka katika maisha yetu ya kila siku. Kwa kufanya hivyo, tutawasaidia vijana hawa tunaowahifadhisha Quran kuwa raia wema, wazalendo, wanaotambua  wajibu wao, majukumu yao, kwao wenyewe na kwa nchi yao pia,” amesema.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wanaoendesha taasisi za kuhifadhi Quran wakae pamoja na watengeneze ratiba ya mashindano ya kitaifa na kimataifa ili waweze kuwa na mashindano yanayoanzia ngazi za chini hadi za juu.

  “Kaeni pamoja, mtenge ratiba ya kuanzia ngazi ya kimataifa hadi kimataifa, ratiba hizi zipangwe na kutambulika kitaifa. Wekeni ratiba ili washiriki washindane kuanzia mikoani, ushindani uwepo na tuwaone wakipanda kutoka mkoa, Taifa, Afrika Mashariki, Afrika hadi ya Dunia,” amesema.

  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali alisema wameanza kuona matunda ya kazi ya kuhifadhisha Quran kwani vijana wa Kitanzania wamesoma elimu ya mazingira (circular education) na elimu ya dini na wamefaulu vizuri sana.

  “Sasa hivi tunataka watoto wetu wafikie elimu ya juu ya dini na hii ya mazingira. Tunawapongeza hawa vijana wa Kitanzania ambao walienda hadi nje ya nchi kutafuta elimu ya juu na sasa wamerudi nyumbani kuasaidia ndugu zao,” alisema. 

  Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania, Sheikh Othman Ali Kaporo alisema jumuiya ilianza kazi zake kimyakimya mwaka 1984 lakini ilianza kujulikana mwaka 1992 

  Alisema walianzisha jumuiya kwa sababu walibaini kuwa jamii ina kiu ya kupata watu wema watakaochangia maendeleo wa Taifa. “Ukiangalia mwelekeo wa vijana wetu wa Kiislamu si mzuri. Hebu fanya utafiti wa kina wa wale waliokuwemo magerezani. Je tunaumizwa na jambo hili? Na kama tunaumizwa tunafanya nini ili kuwaokoa vijana hawa? Haya ndiyo tunayalenga sisi, na kwa kupitia Quran, tuweze kuwaokoa na majanga yale,” alisema. 

  “Kuna vijana wengi wana vipaji lakini vinakufa kwa sababu hakuna wa kuviendeleza vipaji vyao. Kupitia Quran tukufu, tunahitaji kuwabadilisha wote hawa ili tuwe na jamii imara, inayomjua Mwenyezi Mungu, iliyobora na inayoishi kwa amani,” alisema.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, JUNI 3, 2018.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubary Zubeir (kulia) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh Othman Kaporo (watatu kulia) wakiwa na washindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tanzania baada ya Waziri Mkuu kuwakabidhi washindi hao zawadi zao kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018. Kutoka kushoto ni mshindi wa kwanza Ibn Rayizah Hatim Abdullah wa Saudi Arabia, Mshindi wa pili Hamza Soukouna kutoka Mali na Mshindi wa tatu Hamzah El- Habashiy kutoka Marekani.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi waliofika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambako Mheshimiwa Waziri Mkuu alikabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania, Juni 3,2018. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Mwenyekiti wa Haj Trust Fund, Sheikh, Swaleh Misky, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt, Mohammed Bilal, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh Othman Kaporo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir kabla ya kukabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye ukumbi wa Dimond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye ukumbi wa Dimond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye ukumbi wa Dimond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh Othman Kaporo (kulia) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhadi Mussa Salum (wapili kulia) baada ya kukabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



  0 0

  *Ni baada ya mabasi ya Mashallah, Ngombare kuhamishwa kituo namba 21

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  ABIRIA wanaosafiri kwenda katika mikoa ya Kusini hasa Mkoa wa Lindi na Mtwara, wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa hatua zake za kuhamisha huduma za usafiri wa mabasi ya Kampuni ya Mashalaah kutoka kituo Namba 21 kwenda kituo Namba 48 vilivyopo eneo la Mbagala Jijini Dar es Salaam.

  Hatua hiyo ya kuhamishwa kwa mabasi hayo kumesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wanaotumia mabasi hayo na sasa wanaomba halmashauri hiyo kutafakari upya uamuzi huo.

  Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la kituo namba 21 na baadae katika kituo namba 48 jijini Dar es Salaam, abiria hao walisema kitendo hicho pamoja na mambo mengine, kimekuwa kikiwasababishia baadhi yao kupoteza mizigo na wakati mwingine kulazimika kutumia fedha za ziada kwa ajili ya kukodi piki piki na hata mikokoteni kuyafuata mabasi hayo katika kituo Namba 48, ambacho kipo mbali na neo la Barabara Kuu mahali walipokuwa wakipandia hapo awali.

  Abiria hao akiwemo Mustafa Salehe, alisema kubadilishwa kwa utaratibu wa mabasi hayo kutoka kituo namba 21 kwenda kituo namba 48, kumesababisha changamoto kubwa kwa mamia ya abiria hasa wale wanaotumia kituo hicho cha Mbagala, eneo ambalo ndilo linalotumika kama kituo kikuu cha daladala kutoka maeneo mbalimbali ya mji. “Zamani ulikuwa ukishuka hapa kutoka mahali popote ndani ya mji huu, moja kwa moja unaingia katika basi kuendelea na safari yako, lakini kwa sasa inashangaza kuona huduma hiyo imeondolewa tena kwa baadhi ya mabasi, suala linaloleta wasiwasi kuwa pengine kuna mgogoro unaoendelea baina ya uongozi na wamiliki wa mabasi hayo” alisema Salehe.

  Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mwanakopa Hassan, mbali na kudai kushangazwa na hatua hiyo, alisema hali ya usafiri katika kituo hicho imekuwa ya kutoeleweka kutokana na mkanganyiko unaojitokeza mara kwa mara mahali hapo. “Hapo zamani tulikuwa tunapandia kituo hiki kikubwa cha daladala cha Rangi tatu( kituo namba 21), baadae tukahamishwa tena kwenda huko mitaani(Namba 48),

  “Lakini kabla hatujakaa vizuri huduma zikarudishwa tena eneo la mara ya kwanza, na sasa wamezipeleka tena huko huko mitaani, jambo ambalo sisi kama abiria linatuchanganya ikizingatiwa siyo kila mtu mwenyeji wa mji huu” alisema Mwanakopa .Kwa mujibu wa abiria hao, huduma hizo za usafiri zimehamishwa kituo hicho kwa kampuni mbili za mabasi ambazo ni Ngombale pamoja na Mashallah, huku mabasi mengine yakiachwa jambo lililotoa tafsiri kwa abiria hao kuwa pengine linatokana na mgongano wa kimaslahi baina ya watoa huduma hao, uongozi wa manispaa pamoja na wasimamizi wa huduma za usafiri.

  Walipotafutwa kuthibitisha suala hilo, Uongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA)ulisema hali hiyo inasababisha manyanyaso kwa abiria hao na unatokana na kiongozi Ofisa mmoja wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Temeke pamoja na kiongozi kutoka Manispaa ya Temeke, na suala hilo wanalifuatilia. “Inashangaza kuona kila siku ni kampuni hizi hizi mbili ndiyo zinayumbishwa pale katika eneo la kutoa huduma, kuna tatizo gani, nini kimejificha..kwa taarifa tulizozipata wapo watu wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi, jambo ambalo sisi kama uongozi wa wasafirishaji hatuwezi kulifumbia macho” alisema Katibu Mkuu wa TABOA Enea Mrutu.

  Kwa upande wa uongozi wa mabasi hayo umesema kuwa unasikitishwa na hali inayoendelea dhidi yao na kufafanua kwa sasa wanasubiri haki itendeke baada ya kupeleka malalamiko yao maeneo husika huku wakidai kuna baadhi ya maofisa wa halmashauri na polisi kikosi cha usalama barabarani ambao wanawafanyia hujuma za kibiashara.

  1: Baadhi ya abiria wakipakia mizigo yao kwenye basi la Mashaalah baada ya kuletwa kwenye mikokoteni kutoka kituo namba 21 kuja kituo namba 48 ambacho kinalalamikiwa na abiria kuwa kimewasababishia usumbufu.
  Mmoja wa abiria wa basi la kampuni ya Mashalaah(aliyevaa fulana nyeusi) akitoa malalamiko yake kutokana na adha ambayo wanaipata tangu kuhamishwa kituo namba 21
  Mizigo ya abiria ikitolewa kituo cha mabasi namba 21 kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam ikiwa kwenye mkokoteni kwa ajili ya kupelekwa kituo namba 48.
  Baadhi ya abiria wa basi la Mashalaah wakiwa wamekaa nje ya ofisini ya basi hizo wakisubiri mizigo yao ipakiwe kwenye mikokoteni ili kufuata basi linakoegesha baada ya kuondolewa kituo namba 21 ambacho ndicho kituo kwa ajili ya abiria wanaokwenda mikoa ya Kusini na kupelekwa kituo namba 48.

  0 0


  0 0

  Dar es Salaam. baada ya kusua sua kwa muda mrefu, hatimaye Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA) kimepata katiba mpya itakayo waongoza katika mchezo huo hapa nchini.

  Katiba hiyo imepatikana katika mkutano mkuu uliotishwa na Kamati ya Muda ya TSA iliyoteuliwa na Baraza la Michezo nchini (BMT) hivi karibuni.
  Katika Mkutano huo uliosimamiwa na BMT, wanachama kutoka klabu mbalimbali nchini walipitisha mabadiliko hayo ambayo kwa mujibu wa katiba ya sasa, Zanzibar haitashiriki katika masuala ya uchaguzi kama ilivyokuwa zamani.

  Katiba ya zamani iliruhusu wanachama kutoka Zanzibar kushiriki katika uchaguzi na masuala mengine, jambo ambalo ilikuwa tofauti na michezo mingine kama mpira wa miguu, netiboli na mingineyo.

  Hata hivyo, kutokana na hali ya mchezo wa kuogelea nchini kutokuwa na vyama vya mikoa na wilaya, ushiriki wa Zanzibar katika shughuli za TSA utakuwepo kupitia habibu za rejea (MoU) baina ya Kamati ya Utendaji ya TSA na Kamti ya Utendaji ya Chama Cha kuogelea cha Zanzibar.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Muda wa TSA, Imani Dominick amesema kuwa wamefarijika sana kukamilisha zoezi hilo lililokuwa gumu na vipingamizi vingi kutoka kwa watu ambao hawakuwa wakitaka kukamilisha zoezi hilo.

  Dominick alisema kuwa baadhi ya wadau walipinga waziwazi pamoja na kusambaza ujumbe kuwa Kamati yetu siyo halali kwa lengo la kupotosha pamoja na ukweli kuwa BMT ndiyo iliyowaidhinisha kushika nyadhifa hizo baada ya wanachama kuwapitisha katika mkutano halali uliofanyika shule ya Kimataifa ya Tanganyik Upanga.

  “Naomba niwapongeze kwa kazi kubwa mliyoifanya kuokoa mchezo wa kuogelea, pia nawashukuru wanachama kwa kuitikia wito wa kuijadili na kuipitisha Katiba mpya, huu ni muongozo wa kisasa na tunaamini tutafanikiwa kwa kiwango kikubwa,”alisema Dominick.Pia aliwahasa wanachama walioshindwa kuhudhuria mkutano huo kutofanya hivyo tena kwani maendeleo ya mchezo yanahitaji mchango wao kubwa kwani chama si cha watu wachache zaidi ya vilabu, waogeleaji na wanachama.

  Afisa Michezo wa BMT, Benson Chacha naye aliwashukuru wanachama hao kwa kufanikisha zoezi hilo na kuwaomba kujikita zaidi katika kuuendeleza mchezo huo na kuachana na masuala ambayo yatarudisha nyuma mchezo huo.“Mmefanya kazi vizuri sana kukamilisha zoezi hili ambalo lililkuwa gumu sana, mmefanya kazi kubwa na ya kupongezwa, sasa mnatakiwa kujikita zaidi kwenye maendeleo ya mchezo, BMT itawapa ushirikiano mzuri sana,” alisema Chacha.

  Baadhi wa wajumbe wa Kamati ya Muda na Wanachama wa chama cha kuogelea nchini (TSA) wakiwa katika picha ya pamoja na mjumbe wa Baraza la Mchezo nchini (BMT) mara baada ya kupitisha Katiba mpya.

  0 0

  Raisi wa TCCIA Bwana John Mayanja, akizungumza na wajumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa ambao ni wanachama wa TCCIA.

  Chama cha wenye Biashara, Viwanda na Wakulima ‘TCCIA’ jana kimezindua rasmi safari ya kusherekea mafanikio makubwa waliyoyapata katika miaka 30 tangu kuanzishwa kwake. Wanachama pamoja na viongozi wa TCCIA jana walikutana kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ambao ulifanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mbalimbali yaliyotungumzwa katika mkutano huo, kulifanyika uzinduzi rasmi wa kusherekea mafanikio makubwa ya TCCIA.
  Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group Bw. Imani Kajula ambae ni mshauri wa masuala ya masoko, Alisema ‘Huwezi kuongelea Uchumi wa nchi bila kutaja kazi kubwa iliyofanywa na TCCIA hasa katika kuleta msukumo mkubwa kwenye uboreshwaji wa sera mbalimbali ambazo zimesaidia katika kukuza Uchumi wetu. Miaka 30 hii ni hatua kubwa sana kwa shirika la kizalendo lililowakutanisha watu mbalimbali kutoka katika kada za Biashara, Uchumi pamoja na Kilimo na kuweza kukaa pamoja kwa maslahi mapana ya nchi yetu’

  Pamoja na ufunguzi huo, mkutano huu pia kutoa fursa kwa Rais wa TCCIA Bw. John Mayanja kuweza kutoa taarifa rasmi ya kipindi cha Oktoba 2017 hadi Mei 2018. Akiongea katika mkutano huo aliwasihi wafanya biashara wote kuweza kutumia jukwaa hilo kuongea na serikali ili kuweza kupata majawabu ya pamoja yatakayoibua fursa zaidi za uwekezaji nchini, ‘serikali yetu ni sikivu, ni lazima sisi tuiambie tunataka nini kwa sauti yetu moja’ alisema Rais Mayanja. 
  Wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya Taifa pia walipata nafasi ya kusomewa Taarifa ya Mwaka 2017, taarifa ya fedha kwa kipinndi cha Jauari – Machi 2018 pamoja na kuchagua wajumbe.

  0 0


















  0 0

  Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Dennis David akimpima mkazi wa Jiji la Tanga Octaviani Moshiru kwenye banda lao lililopo kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Dennis David akimpima mkazi wa Jiji la Tanga Octaviani Moshiru kushoto akimsikiliza kwa umakini mkazi wa Jiji la Tanga Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza akimpa ushauri mkazi wa Jiji la Tanga mara baada ya kupima afya.Katibu tawala mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akipima afya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Hillary Ngonyani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lililopo kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Jumanne Shauri kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa Duguza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Jumanne Shauri kushoto akisaini kitabu cha wageni kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa DuguzaMkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Jumanne Shauri kushoto akizungumza na maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata kushoto ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa Duguza
  Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens kulia akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika kwenye banda lao kupata elimu ya mpango wa kujiunga na bima ya Afya Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akiwa na tisheti akijiandaa kuwapa watoto zawadi wakati alipotembelea banda hilo kushoto Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu sehemu ya watoto waliojiunga na mpango wa Toto Afya kadi




  NA MWANDISHI WETU, TANGA.


  WATANZANIA wametakiwa kujiunga na mpango wa bima a Afya ili waweze kunufaika na huduma za matibabu ya uhakika wakati wanapokuwa wakiugua na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuingia gharama kubwa.

  Hayo yalisemwa leo na Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hawa Duguza wakati akizungumza kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya biashara ya kimataifa.

  Licha ya mfuko huo kutoa elimu juu ya umuhimu wa mpango wa bima lakini pia wanaendelea kutoa huduma za upimaji wa afya na kutoa ushauri kwa wananchi ambao wamekuwa wakifika kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesha hayo.

  Alisema mpango wa bima ni mzuri kutokana na kuwapa uhakika wa matibabu wakati wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali na hivyo ni muhimu kujiunga nao ili waweze kuona manufaa makubwa wanayoweza kuyapata.

  Aidha pia aliwahamasisha kujiunga na mpango wa kikoa na toto Afya kadi ambazo ni muhimu kwa ajili ya kuweza kupata huduma nzuri kipindi ambacho wanapatwa na changamoto za kuugua hususani watoto wadogo wakati wa ukuaji wao.

  “Ndugu zangu maradhi huwezi kujua yanakuja lini hasa kwa watoto wadogo wakati wa ukuaji wao hivyo niwasihi muone njia nzuri ya kuwawekea akiba ya matibabu kwa kuwaingiza kwenye mpango huu wa toto afya kadi kwani hii ni kumuhakikisha mtoto wako huduma wakati wote wanapougua”Alisema.

  Alisema pia jamii haiwezi kupata maendeleo ikiwa watakuwa hawana afya bora hivyo ni muhimu kuendelea kuhamasishana kujiunga na mpango huo kwa lengo la kuweza kunufaika na huduma za matibabu (habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0


  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Joyce Fissoo akiongea kuwakaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na wageni mbalimbali kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya Ushauri ya TFB jijini Dar es Salaam Juni 2 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi akiongea na wadau wa filamu wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo. 
  Sehemu ya wageni na wadau wa filamu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo. 
  Sehemu ya wageni na wadau wa filamu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo. 
  Sehemu ya wageni na wadau wa filamu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo. 
  Katibu Mkuu wa Wizari ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi akiongea na wadau wa filamu wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Juni 2 2018. 
  Wasanii Goodhope Zagamba na Christina Pande wakiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi, Mwenyekiti uzinduzi wa bodi ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Profesa Frowin Nyoni (kushoto) na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Mjumbe wa Bodi ya Filamu Nchini, Bishop John Hiluka wakati wa hafla ya kutambua mchango wake na uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB). Wanaaoshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi, na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Mjumbe wa Bodi ya Filamu Nchini, Dk. Visencia Shule wakati wa hafla ya kutambua mchango wake na uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Bodi ya filamu Tanzania. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Frowin Nyoni (kushoto) na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Katibu wa TFB, Joyce Fissoo wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kutambua mchango wake kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB). Wanaaoshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba. 
  Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana tuzo maalum iliyotolewa na Bodi ya Filamu Tanzania kutambua mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya filamu hapa nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi na Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Prof. Frowin Nyoni. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Mjumbe wa TFB Mstaafu, Rose Simon Sayore wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kutambua mchango wake kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB). Wanaaoshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa Frowin Nyoni.  
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Mjumbe wa TFB Mstaafu, Lily Beleko wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kutambua mchango wake sanjari na uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba (kulia).
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Mwakilishi wa Steps Entertainment, wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kutambua mchango wa taasisi hiyo sanjari na uzinduzi wa Bodi mpya
  Msanii Yvonne Cherrie 'Monalisa' akionesha Tuzo aliyopokea kwa niaba ya Kituo cha ITV, kwa kutambuliwa mchango wa kituo hicho kwa TBF wakati wa hafla iliyofanyika sanjari na uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania. Kulia ni Mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba (kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kutambua mchango wake kwenye uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya TFB
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Mwakilishi wa TBC, kutambua mchango wa shirika hilo kwa ukuaji wa Filamu hafla iliyofanyika sanjari na uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB)
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Mwakilishi wa Azam TV, kutambua mchango kituo hicho sanjari na uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB). Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi.
  Mwakilishi kutoka Tasnia ya Sanaa Tanzania, akichukuwa Tuzo kwa Niaba ya Clouds Media, kwa kutambuliwa mchango wakituo hicho pia kwa Tasnia ya Sanaa Nchini. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo mjumbe wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Dk. Vicensia Shule aliyeipokea kwa niaba ya IPP Media 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi tuzo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi kwa kutambua mchango wa Makatibu Wakuu watangulizi wake na yeye binafsi kwa Bodi hiyo. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akionesha tuzo aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi kwa Niaba ya Mawaziri watangulizi wa Wizara hiyo na kwake binafsi kwa kutambuliwa michango yao kwa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB)
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi na Katibu wa TFB, Joyce Fissoo. 
  Mwenyekiti wa TFB, Profesa Frowin Nyoni akiongea na wadau wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) pia Wawakilishi wa Taasisi Mbalimbali waliokabidhiwa tuzo. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TFB pia wafanyakazi wa Bodi wakati kuhitimisha hafla hiyo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) pia wadau wa sanaa wakati kuhitimisha hafla hiyo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye ni mlemavu 
  Naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa akitoa neo kwa wananchi wa kijiji cha Mlanda wakati wa kutoa hati za kimila 
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye alikuwa anawakilisha kundi la wazee
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushirikia zoezi la utoaji wa hati miliki za kimila zilizotolewa na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
  Picha ya pamoja baina ya viongozi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID),viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa pamoja na baadhi ya wananchi walikuwa tayari wamepokea hati za kimila


  NA FREDY MGUNDA.IRINGA.

  JUMLA ya wanakijiji 772 kati ya 1890 wa kijiji cha Mlanda kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamepimiwa maeneo na mashamba yao na kukukabidhiwa hati miliki za kimila zinazotolewa kupitia Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

  Hati hizo zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya wakati wa sherehe fupi za kuwakabidhi hati hizo zilizofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi na wageni mbalimbali walikuwepo katika tukio hilo.

  Akizungumza na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo Masunya alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.

  Masunya aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.“Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Masunya

  Masunya aliupongeza mpango huo akisema utasaidia kupunguza eneo kubwa la ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo haijapimwa.
  Aidha Masunya aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike umalize kupima vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa huku akivikumbusha vijiji vyote vya wilaya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya nchi. 

  “Tunataka katika kipindi ambacho Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na mipango ya matumizi bora na ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,” alisema Masunya.

  Alisema kwa kupitia sera hiyo, kutakuwa na usimamizi zaidi wa ulinzi wa ardhi ya watu masikini ili kupunguza uporaji wa rasilimali hiyo unaofanywa na matajiri.“Marekebisho ya sera hiyo ya ardhi yatawezesha pia kufanyika kwa mrekebisho ya sheria mbalimbali za ardhi ili ziendane na sera na mazingira ya sasa,” alisema Masunya.

  Masunya aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao hawajapimiwa maeneo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya kifamilia kutumia vizuri muda ambao bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na kuhakikisha nao wananufaika na zoezi hilo.

  Wanakijiji ambao hawajapimiwa maeneo yao wanaweza kuendeleoa kuzalisha migogoro ambayo haina tija kwa maendeleo yao na kusababisha waendelee kuwa masikini kwa kuwa hawatakuwa na dhamana ya kwenda kukopa.

  Awali naibu mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa alisema kuwa kijiji cha Mlanda kinajumla ya wananchi 1890 na walio nufaika na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ni wananchi 772 na kufanikiwa kutoa jumla ya hati miliki za kimila 1777 ambapo wanaume walikuwa 409 na wanawake 363. 

  Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Mlanda kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.

  “Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa

  Msigwa alisema kati ya vijiji hivyo 41 vitakavyotayarishiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi kupimiwa na kupewa hati miliki za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na vitano vipo wilayani Mbeya.

  “Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji mashamba na urasimishaji wa kijiji chote cha Mlanda, hivi sasa mradi unaendelea na upimaji mashamba katika vijiji vya mradi ambavyo vipo wilayani Iringa” alisema Msigwa

  Naye diwani wa kata ya Magulilwa Jane Mhangala aliupongeza Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa kuzingatia jinsia wakati walipokuwa wanaendesha zoezi la upimaji ardhi katika kijiji hicho.

  “Hongera sana LTA kwa kuwapa elimu wanawake na wanaume na kuhakikisha kuwa wanapa haki zao sawa bila kuwa na mgogoro wowote tofauti na ilivyokuwa hapo awali,maana miaka ya nyuma mwanamke alikuwa anabaguliwa kwenye kila kitu wala alikuwa haruhusiwi hata kumili ardhi” alisema Mhangala.Mhangala aliongeza kwa kusema kuwa wanakijiji wa kijiji cha Mlanda baada ya kupata elimu ya kumiliki ardhi kumepunguza sana migogoro ambayo ilikuwa inaleta chuki kwenye familia.

  “Kwa sasa ardhi ya kijiji hiki imepanda dhamani kwa kiasi kikubwa na tayari ishapimwa na mmepata hati miliki za kimila ambazo zitawasaidia katika maendeleo yenu ya kiuchumi” alisema Mhangala

  0 0

  Massage ni tiba ya asili na ya kitaalamu yenye uwezo mkubwa wa kuufanya Mwili wako kuwa Imara Kiafya

  Faida za Massage Katika Mwili
  1. Massage inaboresha afya ya ngozi.

  2.Massage hufungua mishipa ya fahamu na kuongeza uwezo wa kufikiri.
  3. Massage husafisha ngozi na kuboresha mfumo wa utoaji takamwili.
  4. Massage Inaondoa kovu la jeraha.
  5. Massage husaidia kupona kwa wenye mivunjiko ya viungo/ mifupa.
  6. Massage huondoa uchovu wa mwili na kukosa usingizi.
  7. Massage huzuia kansa ya ngozi na tishu.
  8. Massage huzuia Saratani ya Matiti.
  9. Massage huondoa maumivu ya wakati wa hedhi.
  10. Massage huboresha mmeng'enyo wa chakula na kuzuia Constipation (choo ngumu).
   11. Massage hupunguza maumivu ya uchungu kwa wamama wajawazito.
  12. Massage huondoa uchovu na kuvimba kwa miguu kwa wamama wajawazito.
  13. Massage huimarisha mifupa kwa kuchochea ufyonzwaji wa Madini ya Kalsiam(Calcium) na Fosforas.
  14. Massage huboresha mzunguko wa damu mwilini.
  15. Massage husaidia kuondoa maumivu ya misuli na majeraha.
  16. Massage huchochea ufanyaji kazi wa homoni mwilini.
  17. Massage huzuia Stroke/ kiharusi.
  18. Massage inasaidia sana kwa wazee kuimarisha misuli na kuwapa nguvu ya kutembea.
  19. Massage huondoa maumivu ya chini ya mgongo.
  20. Massage husaidia kuboresha mfumo wa limfu (lymphatic system)

  🌹 KARIBU UBORESHE AFYA YAKO NA HAPPINESS MASSAGE! 🌹

   Tunapatikana: Lamada Hotel-Manyara 27,
  Ilala Dar Es Salaam.

  Simu / WhatsApp
  📞 0787 343 161
  📞 0756 343 161

  👉🏽Fanya booking mapema ili tukuhudumie kwa wakati

  Happiness Massage Tunaboresha Afya yako na kurejesha Furaha yako

  0 0

  Na Veronica Kazimoto-Dodoma

  Mameneja wote wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nchi nzima wameagizwa kuwa na utaratibu wa kuwatembelea wafanyabiashara mara kwa mara ili kujua changamoto zao na kuzitatua ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara hao.

  Agizo hilo limetolewa leo na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere jijini Dodoma alipohitimisha ziara yake ya kikazi ya kujiridhisha utendaji kazi wa Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutokufanya kazi.

  "Nimepita katika baadhi ya maeneo mengi kuanzia Dar es Salaam, Kibaha, Mlandizi, Morogoro, Gairo na sasa nimemalizia Dodoma. Katika maeneo yote niliyopita nimekuta wafanyabiashara wana changamoto ambazo zinaweza kutatulika kirahisi na Mameneja bila ya kusubiri mpaka Kamishna Mkuu apite, hivyo nawaagiza Mameneja kuwatembelea wafanyabiashara katika maeneo yao, kujua changamoto wanazozipata ili kuzitatua mara moja kinyume na hapo nitachukua hatua," alisema Kichere.

  Aidha, Kamishna Mkuu Kichere alieleza kuwa, tatizo la Mashine za EFD limekwisha na tayari zimeanza kufanya kazi, hivyo Mameneja wote wa mikoa wanatakiwa kupita katika maeneo yao ili kufanya ufuatiliaji wa mashine hizo na kuzitolea taarifa zile zitakazokutwa bado zina matatizo kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi wa haraka. 

  "Ninasema Mameneja wawatembelee wafanyabiashara mara kwa mara kwasababu nimepita katika maduka mbalimbali nimekuta kuna baadhi ya wafanyabiashara tangu Mfumo wa EFD upate hitilafu mpaka leo hawajawasha mashine zao na nilipoziwasha nimekuta zinafanya kazi vizuri, hivyo kinachotakiwa ni Mameneja kupita katika maeneo yao na kufanya ukaguzi wa mashine husika na kuwapa elimu," alifafanua Kichere.

  Kamishna Mkuu Charles Kichere amehitimisha ziara yake iliyoanzia Dar es Salaam mpaka Dodoma akipita katika maduka na vituo mbalimbali vya mafuta kwa ajili ya kujiridhisha kama mashine za EFD zinafanya kazi vizuri baada ya mfumo wake kupata hitilafu ya kiufundi tangu Mei 11, mwaka huu kutengemaa na kuruhusu mashine hizo kuanza kufanya kazi kama inavyotakiwa.

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kushoto) akikagua risiti aliyopewa mfanyabiashara wa Bodaboda Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi kujiridhidha utendaji kazi wa mashine za kielektroniki za Kutolea risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutofanya kazi.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa kofia) akikagua risiti iliyotoka katika Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi kujiridhidha utendaji kazi wa mashine za kielektroniki za Kutolea risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutofanya kazi.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akikagua risiti iliyotoka katika Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti katika kituo cha mafuta kilichopo Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi kujiridhidha utendaji kazi wa mashine za kielektroniki za Kutolea risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutofanya kazi.(PICHA ZOTE NA TRA)


  0 0

   
  Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Philip Mpangango (MB.) akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka 2018/19 mjini Dodoma leo.

older | 1 | .... | 1592 | 1593 | (Page 1594) | 1595 | 1596 | .... | 1896 | newer