Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1591 | 1592 | (Page 1593) | 1594 | 1595 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima (kushoto) akipokea vitendekazi kutoka kwa Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed katika makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika leo jijini Dae es Salama
   Baadhi ya Viongozi wakijiandaa kumlaki Katibu Mkuu huyo mpya
   Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania wakiimba nyimbo za hamasa wakati wakisubiri ujio wa Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya yao leo
   Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania wakiimba nyimbo za hamasa wakati wakisubiri ujio wa Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya yao leo
     Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi, Erasto Sima (kushoto) akilakiwa na Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed jijini Dae es Salama
   Katibu Mkuu wa CCM akikabidhiwa maua kunogesha mapokezi
   Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania akisalimia baadhi ya viongozi waliofika kwenye mapo0kezi yake
    Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima (kushoto) akipewa na Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed vitabu vya kusaini, baada ya kuwasili Ofisi ya Jumuiya hiyo jijini Dar es Salaam
    Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima akipokea akisaini kitabu cha wagerni
    Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi, Erasto Sima (kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed wakati akizungumza katika makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika leo jijini Dae es Salama
    Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima (kushoto) akipokea vitendekazi kutoka kwa Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed katika makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika leo jijini Dae es Salama
    Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima akizungumza na waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya ofisi
   Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Seif Shaaban Mohamed akimkaribisha kuzungumza na  Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima na baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo, mwishoni mwa  makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika leo jijini Dae es Salama. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

   Naibu Waziri Wa Kazi Ajira Na Vijana Mheshimiwa Anthony Mavunde Akigawa Maziwa Ya Asas Kwa Wanafunzi Waliojitokeza Kwenye Viwanja Vya Nyerere Square jijini Dodoma Kwenye Kilele Cha Unywaji Wa Maziwa Duniani Ambapo Kitaifa Imeadhimishwa Mkoani Arusha
   Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Nkuhungu Ya jijini  Dodoma Wakigawiwa Maziwa kutoka ASAS DAIRIES LTD.
   Wanafunzi Wa Shule Ya Nkuhungu Wakifurahia Maziwa kutoka ASAS DAIRIES LTD
   Naibu Waziri Wa Tamisemi Mheshimiwa Josphat Kandege Na Mkuu Wa Mkoa Wa Arusha Mh. Mrisho Gambo Wakipokea Maziwa Kutoka Kwa Mwakilishi Wa Asas Dairies Lipita Mtimila Kwa ajili Ya Shule Za Mkoa wa Arusha Ambapo ASAS DAIRIES LTD Wametoa Maziwa pakiti 15,000 Kwa Wanafunzi wa mkoa huo.
   Naibu Waziri Wa Tamisemi Mheshimiwa Josphat Kandege Akisaini Kitabu Cha Wageni Alipotembelea Banda La ASAS DAIRIES LTD Kwenye Madhimisho Wa Wiki Ya Maziwa Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Arusha.
   Mheshimiwa Richard Kasesela Akuu wa Wilaya ya Iringa Na Mkurugenzi Wa ASAS DAIRIES LTD Ahmed Salim Asas wakiwa  Kwenye Viwanja Vya Ngombe Mjini Iringa Kwenye Kilele Cha Madhimisho Ya Wiki Ya Maziwa Duniani.
   Wanafunzi Wa Shule Ya Kihesa Ngombe Wakifurahia Maziwa Ya ASAS DAIRIES LTD wakati Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesela na Mkurugenzi wa ASAS DAIRIES LTD Bw. Ahmed Salim Asas walipokuwa wakiwagawia.
  Mheshimiwa Kasesela Akimpatia Maziwa Mmoja wa  Mwanafunzi Wa Shule Ya Kihesa Ngome mjini Iringa.
  ....................................................................................................
  ASAS DAIRIES LTD imegawa zaidi ya pakiti 400,000 kwenye shule mbalimbali za mikoa ya IRINGA, ARUSHA, MBEYA na DODOMA. wakati wa  maadhimisho ya  wiki ya Maziwa duniani ambapo kitaifa inafanyika mkoani Arusha.

  ASAS DAIRIES LTD ilianza kampeni hii Tarehe 22 mwezi wa Tano na kufikia zaidi ya shule 108 na Wanafunzi 67,000. Hii inatokana na uhamasishaji wa unywaji wa Maziwa Mashuleni ambao unafanywa na ASAS DAIRIES LTD kila mwaka.

  Katika kufikia lengo la watanzania kunywa maziwa kwa wingi kampuni ya ASAS DAIRIES LTD imejikita katika kampeni hiyo ili kuwafanya watoto ambao watakuwa wazazi wa baadaye kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya zao pamoja na vizazi vyao kwa siku za baadaye.

  Mkurugenzi wa Kiwanda cha ASAS DAIRIES LTD Bw. Amded Salim Asas amesema  huu ni mwendelezo wa kampeni hiyo na lengo la kampuni hiyo kwa mwakani ni kuzifikia shule za msingi nchi nzima, Bw. Ahmed Asas ameishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa ngazi zote  jinsi ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwa kwao na kuifanya ndoto ya Tanzania ya Viwanda kwenda kutimia kwa mafanikio makubwa.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ongezeko la watu katika miji mikubwa kuna changia sana katika uharibifu wa mazingira na matumizi makubwa ya mkaa.
  Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa.
  Makamu wa Rais amesema “Mkaa ni Ghali Tutumie Nishati Mbadala”, kwani kiwango cha miti inayokatwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa ni kikubwa na kinatisha.
  “ Dar es Salaam peke yake inakadiriwa kutumia kati ya magunia kati ya 200,000 mpaka 300,000 yenye uzito wa kilo 50 kila moja ya mkaa kwa mwezi na inategemewa itaongezeka zaidi kutokana na kasi ya ongezeko la watu hasa kwenye miji ” alisema Makamu wa Rais.
  Makamu wa Rais amewata Watanzania, Makampuni pamoja na Taasisi mbalimbali kuungana na Serikali kubadilisha jamii yetu kuanza kutumia nishati ya majani kwa namna ya mkaa na kuni kama vyanzo mbadala vya nishati endelevu.
  Makamu wa Rais amesema kuwa kilele cha Siku ya Mazingira ni tarehe 5 Juni, 2018 ambapo dhima ya Kimataifa ni Kupiga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini Tanzania imelekeza nguvu zake katika kuadhimisha siku hiyo kwa kuwataka Wananchi wake wabadilike badala ya kutumia mkaa ambao unasababisha ukataji mkubwa wa miti ni vyema kuanza kutumia nishati mbadala.
  Mapema; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba alisema kutokana na uhitaji na umuhimu wa kutunza mazingira Serikali, Wadau wa Maendeleo, Taasisi mbali mbali, Sekta Binafsi na Watungaji wa Sera kutafakari kwa pamoja na kuja na majawabu yatakayosaidia katika utunzaji wa mazingira na kuilinda miti.
  Wakati huo huo;  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt amesema tangu mwaka 1972 changamoto za uharibifu wa mazingira hazikuwa za Kikanda tu bali ni kwa dunia nzima hivyo hili jambo linahitaji ushiriki wa Dunia nzima katika kupambana na uharibifu wa mazingira.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshukuru Profesa Mark Mwandosya kwa zawadi ya kitabu mara baada ya ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
   Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Mratibu wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur an Tanzania, Shekh Mohammed Nassor (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya kuhifadhi Qur an Kimataifa yanayotarajia kufayika kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee June 3, 2018. Kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo, Shekh. Mohamed Ali Hassan na Jaji wa mashindano hayo, Dk. Abbas Hamza Mohammad.

  Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Ali Hassan(kulia) akielezea kwa kina kuhusu mashindano hao yanayotarajia kufanyika Juni 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Mmoja wa majaji kutoka nchini Somalia (wa pili kushoto) akizungumzia namna ambavyo wamejiandaa kuchuja washiriki kwenye mashindano hayo.Wa kwanza kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Ali Hassan na anayefuatia ni Mratibu wa mashindano hayo Sheikh Mohamed Nasoro
   
  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi Quran yanayotarajiwa kufanyika Juni 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo mataifa zaidi ya 20 yameshiriki.

  Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania.Mbali ya kuwepo kwa Waziri Mkuu Majaliwa viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo wastaafu nao watakuwa miongoni mwa watakaohudhuria kushuhudia mashindano hayo yenye hadhi ya kimataifa.

  Viongozi wastaafu watakaohudhuria siku hiyo ni Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne mzee Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais mstaafu Dk.Mohammed Ghalib Bilal pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mashindano hayo kutoka Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Nasoro amesema tayari washiriki karibu wote wamewasili chini Tanzania ambapo waliopo sasa ni washiriki kutoka mataifa 18 kati ya mataifa 20 ambayo yamealikwa.

  Pia amesema mbali ya washiriki kuwapo nchini, tayari majaji wa mashindano hayo nao wapo na wamekuwa wakiendelea kuchuja washiriki ili kubaki na wale watakaoingia fainali na hatimaye washindi ukabidhiwa zawadi zao na Waziri Mkuu.

  "Washiriki karibu wote wamewasili nchini na hadi jana tayari washiriki tisa wamesikilizwa na majaji wetu na leo watawasikiliza washiriki wengine tisa ili kuwachuja na kubaki wale watakaoingia hatua ya fainali na hatimaye kupewa zawadi zao ambapo kwa sasa hatuaamua kuweka hadharani mshindi atapata zawadi ya aina gani na tunafanya hivyo kwasababu maalumu.

  "Majaji ambao wapo kwenye mashindano hayo wanatoka katika nchi mbalimbali duniani.Huu ni mwaka wa pili Jumuiya yetu kuandaa mashindano haya na hakika tunakwenda vema,"amesema Sheikh Nasoro.Ametaja baadhi ya nchi zinazoshiriki mashindano hayo ya kimataifa ni Uingereza, Saud Arabia, DRC Congo, Tanzania, Kenye, Uganda, Mali, Sudan, Yemen na Marekani. "Hizo ni baadhi tu ya mataifa ambayo washiriki wake tayari wamefika nchini kwa ajili ya mashindano hayo,"amesisitiza.

  Kuhusu umuhimu wa vijana wa Kiislamu kuhifadhi Quran amesema Quran ndio Katiba pekee isiyobadilika na inatoa maelekezo na miongozo mbalimbali ya namna ya kuishi hapa duniani, hivyo vijana wanapohifadhi Quran faida kubwa wanaishi katika misingi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.

  "Tuishauri jamii ya Kiislamu kuhakikisha watoto wanalelewa katika misingi ya dini na hili la kuhifadhi Quran ni mojawapo.Tunaamini vijana wakiandaliwa katika misingi ya imani ni rahisi kupata viongozi wazuri na wenye hofu ya Mungu,"ameongeza.

  Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Mohamed Ali Hassan amesema wanamshukuru Mungu kwani maandalizi yanakwenda vizuri na mwitikio kwa walioalikwa ni mkubwa na kusisitiza majaji wapo tayari kufanya kazi ya kuchuja washiriki hao ili kubaki na wale watakaoingia hatua ya mwisho ya fainali.   
  0 0  0 0

   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange ofisini kwake alipowasili Makao Makuu ya Magereza leo Juni 1, 2018 katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili.
   Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongoza mazungumzo Ofisini kwake  na Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange(hayupo pichani), leo Juni 1, 2018 alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza.
   Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange akitambulisha ujumbe wake alioongozananao(hawapo piachani) kabla ya utilianaji saini makubaliano ya ushirikiano na Jeshi la Magereza.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akisaini Mkataba  wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Magereza nchini SheliSheli na Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Kushoto ni Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli hiyo Raymond St Ange akisaini mkataba huo.  Hafla fupi ya  utilianaji saini Mkataba huo umefanyika leo Juni, 2018 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) na Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange wakionesha nyaraka za Mkataba wa makubaliano mara baada ya utiliananji wa mkataba huo ambapo Jeshi la Magereza linatarajia kupeleka baadhi ya Maofisa wa Jeshi hilo kwenda nchini SheliSheli kusaidia kuwajengea uwezo wa Uendeshaji wa Magereza nchini humo.
   Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiliananji saini wa mkataba huo (Kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(katikati) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila Kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Charles Novart.
    Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange(kushoto) akiwa pamoja na ujumbe wake  kabla ya kusainiana Mkataba wa makubaliano hayo,(kulia) ni Balozi wa Heshima wa SheliSheli nchini Tanzania, Maryvonne Pool akifuatilia mazungumzo hayo kama inavyoonekana katika picha.
   Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange pamoja na ujumbe wake na Maofisa wa Jeshi la Magereza wakitembezwa ndani ya Kiwanda cha USeremala  Gereza Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.
   Kamishna Jenerali wa Maagereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Magereza nchini SheliSheli, Raymond St Ange(wa tatu kushoto) walioketi, (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga, (wa pili toka kushoto) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila,(wa tatu toka kulia) ni Balozi wa Heshima wa SheliSheli nchini Tanzania, Maryvonne Pool. Wengine waliosimama mstari wa nyuma ni Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Maofisa kutoka nchini SheliSheli(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).  0 0

   Picha no. 1 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika mkutano na  wafanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ofisi za Tanzania ambao walimtembelea ofisini kwake  kwa ajili ya kuingia makubaliano ili  wafanyakazi wa shirika hilo waanze kutibiwa  katika Taasisi hiyo. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na   wafanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)  ofisi za Tanzania walipomtembelea leo  ofisini kwake  kwa ajili ya kuingia makubaliano ili  wafanyakazi wa shirika hilo waanze kutibiwa  katika Taasisi hiyo.Picha na JKCI


  0 0

  *Aagiza Waziri wa Viwanda, RC na Menejimenti wakae na kumpa taarifa leo jioni
  *Asema tofauti ya viwango vya mishahara inatisha, ataka orodha ya watumishi
  *Awataka watumishi walioko kazini, likizo wawe wastahimilivu

  SERIKALI imesema hairidhiki na ubia unaoendeshwa kwenye Kiwanda cha Nguo cha Urafiki. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Juni mosi, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wafanyakazi wa kiwanda hicho mara baada ya kukagua mitambo mbalimbali kwenye kiwanda hicho.
  “Serikali haturidhiki na ubia huu, na huyu mbia aelewe kwamba Serikali haturidhishwi na ubia huu wala kinachoendelea hapa kiwandani,” amesema huku akishangiliwa kwa nguvu na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

  Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aongoze kikao baina ya wabia hao na menejimenti ya kiwanda na apewe taarifa hiyo leo saa 12 jioni baada ya kufuturu.

  “Ubia wenu hauna tija. Kwa hiyo wewe Msajili wa Hazina na huyo mwekezaji, nikitoka hapa, mbaki mfanye kikao na mnipe majibu leo saa 12 jioni. Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Mkuu wa Mkoa muongoze mjadala huo na nikitoka kufuturu mniambie maazimio yenu, na kama haiwezekani, mvunje kabisa ubia huo ili tujue hatuna mbia tutafute mbia,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema wabia wakuu wa kiwanda hicho ni Msajili wa Hazina na kampuni ya Changzhou State owned Textile Assets Operations kutoka China na kwamba Serikali ilipoamua kukaribisha uwekezaji ilitarajia kupata mtaji, teknolojia na ajira za kutosha lakini hali ya sasa ni kinyume kabisa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam baada ya kukagua kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza nao kiwandani hapo, Juni1, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mhandisi Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam, Khamis Mazugo (kushoto)  kuhusu mitambo ya kiwanda hicho iliyokoma kufanya kazi wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita katika eneo zilipong'olewa mashine za kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki, Shadrack Nkelebe kuhusu mashine za kutengeneza  nyuzi za pamba wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa amezindua rasmi kuanza kwa zoezi la Ugawaji Vitambulisho kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya Usajili wa Mkupuo kumalizika kwa asilimia 82%.

  Akitoa taarifa ya mwenendo wa zoezi la Usajili na Utambuzi liloanza mwezi Octoba 2017 kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi hilo; mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bi. Rose Joseph amesema mkoa wa Kilimanjaro umekuwa mkoa wa nne (4) kitaifa kumaliza awamu ya kwanza ya Usajili Wananchi na kuanza kugawa Vitambulisho kwa wananchi waliokidhi sifa na vigezo vya uraia.

  Amesema ugawaji wa awamu ya kwanza ya Vitambulisho vya Taifa utafanyika kwenye ofisi za Watendaji wa Mitaa na Vijiji wananchi walikosajiliwa ambapo zaidi ya vitambulisho 250,000 vitagawanywa huku hatua za mapingamizi, uchakataji na uzalishaji wa Vitambulisho vingine zikiendelea kwa Wilaya zote za mkoa huo.

  Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi; Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba amesema kukamilika Usajili wa Umma hakumaanishi wananchi hawataendelea kusajiliwa; badala yake kuwataka wananchi ambao hawajasajiliwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kwenye ofisi za NIDA zilizoko kila Wilaya kwani manufaa ya Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ni makubwa na mengi, na iwapo mwananchi atakosa kuwa na hati hiyo muhimu atakwama kufanikisha mambo mengi na muhimu ya kimaendeleo ikiwemo kushindwa kushiriki katika masuala muhimu ya kitaifa.

  Mkuu wa Mkoa huo amewataka Wakuu wote wa Wilaya mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha wanahamasisha wananchi na kufuatilia kwa karibu kuhakikisha wananchi wote wenye sifa za kusajiliwa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa kabla wananchi hawajaanza kukwama kufanya shughuli zao au kukumbwa na msako kwa kwa kukosa Hati hii muhimu inayowatambulisha kama Raia.

  Sherehe za uzinduzi wa zoezi la ugawaji Vitambulisho mkoa wa Kilimanjaro zimehudhuriwa na Viongozi wa Dini, Wafanya biashara, Viongozi wa kisiasa, wananchi, watu wenye mahitaji maalumu na vyombo vya habari; ambapo zaidi ya wananchi 20 wawakilishi wa makundi mbalimbali walikabidhiwa Vitambulisho vyao, huku wakuu wa Wilaya za mkoa huo wakikabidhiwa zaidi ya Vitambulisho 250,000 vya awamu ya kwanza.
  Mhe. Anna Mghirwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akihutubia kwenye sherehe za uzinduzi wa kuanza kwa zoezi la ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro. Katikati ni Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour na kushoto ni mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Bi. Rose Joseph.
  Baadhi ya makundi wawakilishi wa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia kwa karibu matukio wakati wa sherehe za Uzunduzi wa zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wanachi wa mkoa wa Kilimanjaro. Sherehe hizo zilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kuanza kwa ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro. Kushoto ni mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Bi. Rose Joseph na Kushoto ni Mhandisi Aisha Amour.
  Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akimkabidhi Ndg. Evance Moshi Kitambulisho chake kwa niaba ya kundi la watu wenye mahitaji maalumu.
  Mwakilishi wa kundi la viongozi wa dini Sista Eliaichi Malisa akikabidhiwa Kitambulisho chake na mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakati wa sherehe za uzinduzi
  Baadhi ya washiriki wa sherehe za uzinduzi wa zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo la ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa akibadilishana mawazo na mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA - Bi. Rose Joseph (kulia)

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake mzazi aliyezikwa leo wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo wameshiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.
   Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake aliyezikwa leo wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na mbunge wa Kigoma Vijijini, Peter Selukamba. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo wameshiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.
   Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa mama yake mzazi mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyezikwa leo wilayani Nzega.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wa tatu kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla (wa sita nyuma kutoka kulia), Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (wa nne kulia), viongozi wengine wa chama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa wilaya ya Nzega wakishiriki kusalia jeneza lenye mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) muda mfupi kabla ya kupelekwa makaburini kwa ajili ya maziko wilayani Nzega leo.
   Jeneza lenye mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) likiondolewa kwenye eneo la makaburi kupisha mwili huo kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milelel (kaburini) wilayani Nzega leo.
  Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbele yake kulia) na viongozi wengine wa vyama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa Jimbo la Nzega wakishiriki kumzika mama yake mzazi, Hussein Bashe katika makaburi wilayani humo leo.

  0 0


  Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza alipokuwa akikabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini
  Vifaa mbalimbali vilivyokabishiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde kwa ajili ya misikiti ya Jimbo hilo.
  Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akimkabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini Shekhe wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab
  Shekhe wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab akizungumza katika Hafla ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya misikiti ya Dodoma.
  Waumini wakiwasikiliza viongozi mbalimbali


  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Peter Mavunde amewaomba waamini wa Dini ya kiislamu kuliombea Taifa,Rais Dk.John Magufuli na Viongozi wote wa Serikali ya awamu ya Tano ili waweze kutimiza majukumu yao kwa Haki na Usawa na kuendelea kuwahudumia Watanzania wanyonge.

  Mavunde ameyasema hayo leo katika Masjid Gaddafi alipokuwa akikabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini ambapo Mbunge huyo amegawa Speaker 20 za misikitini,mikeka,mabusati,Mifuko ya Saruji,matofali,tende,maboksi matano ya Juzuu & Misahafu,Jezi,Mipira vyote vyenye thamani ya Tsh 15,000,000 na fedha taslimu kwa Tsh 1,000,000 kwa kikundi cha Vijana cha UWAZAM na kuwataka wanufaika wa Vifaa hivyo kuvitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

  “Rais wetu pamoja na viongozi wetu wakuu wanafanya kazi nzuri sana ambayo inapaswa kuungwa mkono,tuliombee Taifa na Viongozi wetu ili waendelee kututumikia na kutatua changamoto zetu”Alisema Mavunde.

  Aidha akimkaribisha Mh Mavunde,Sheikh wa Mkoa Wa Dodoma Al-ahi Sheikh Mustafa Rajab amemshukuru sana Mbunge Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na Waislamu na kuwataka waamini wa Dini ya Kislamu kumuombea na kumpa ushirikiano muda wote.

  0 0

  Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Katikati) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP II) katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, jana 1 June 2018. Wengine ni Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wizara ya kilimo Dkt. Thomas kashililah. Picha zote Na Mathias Canal-WK
  Wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Jana 1 June 2018.
  Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kulia), Mratibu wa ASDP II Mhandisi Januari Kayumbe (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa zana za kilimo Mhandisi Joseph Lubilo wakifatilia mkutano wa waziri wa kilimo na waandishi wa habari. Jana 1 June 2018.
  Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakati wa maandalizi ya uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo ASDP II katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Jana 1 June 2018.  Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) tarehe 4 June 2018.

  Katika dhifa hiyo inayotarajiwa kuanzia Saa 2.00 asubuhi katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Rais Magufuli ataambatana na wageni wengine wa kitaifa na kimataifa akiwemo makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dara es salaam Mhe Paul Makonda, Mawaziri wa sekta za kilimo pamoja na wadau wote wa sekta ya hiyo.

  Taarifa ya uzinduzi wa Programu hiyo ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini imetolewa jana 1 June 2018 na waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba wakati akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.

  Dkt Tizeba alisema, Wizara za kisekta zikijumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ndizo zenye jukumu la kuhakikisha ASDP II inakuwa na mafanikio makubwa nchini na kuwa mkombozi wa wananchi katika kilimo.

  Alisema kuwa ASDP II itatekelezwa katika mikoa na wilaya zote kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele kufuatana na ikolojia ya kilimo ya kanda kwa miaka kumi (10) kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ambapo kipindi cha kwanza kitaanza 2018/19 hadi 2023/24. 

  Katika hatua nyingine Dkt Tizeba ametaja lengo la Programu hiyo kuwa ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza pato la wakulima, wafugaji na wavuvi; kuongeza pato la Taifa na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na lishe. 

  Aidha, Programu hii itatekeleza sera mbalimbali kama vile Sera ya Kilimo ya Taifa, Sera ya Mifugo ya Taifa, Sera ya Uvuvi, Sera ya Masoko ya Mazao ya Kilimo, Sera ya Umwagiliaji ya Taifa, Sera ya Usalama wa Chakula na Lishe, Sera ya Ugatuaji Madaraka, Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sera ya Mashirikiano kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi.

  Katika hatua nyingine Mhe Dkt Tizeba ameuarifu umma wa watanzania kuwa endapo mpango huo utatekelezwa kama ilivyopangwa hadi kufikia mwaka 2022 Tanzania itakuwa katika uchumi wa kati.Katika utekelezaji wa ASDP II washiriki ni wadau wa sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Ushirika, Wizara, Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na wananchi wote.

  0 0


   Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Joseph Kandege akikagua moja ya machine inayotumika katika usindikaji wa maziwa kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
   Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akikabidhiwa maziwa kwa ajili ya shule mbalimbali katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
   Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akiwa na baadhi ya viongozi wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye  kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akiongea na wadau wa ufugaji katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
  .............................................................

  Angela Msimbira OR-TAMISEMI

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege  amewaagiza wafugaji nchini kuunda  vyama vya ushirika imara ambavyo vitawezesha  kupata huduma za mifugo na kuboresha ukusanyaji na masoko ya maziwa. 

  Mhe Kandege ameyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maziwa iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nanenane, Themi Mkoani Arusha
  Mhe. Kandege amesema uwepo wa ushirika imara utaboresha ukusanyaji wa  maziwa kwa wingi kwa ufanisi zaidi na hatimaye  kuongeza kiasi cha usindikaji kwa viwanda. 

  “Napenda kutoa pongezi kwa wafugaji wa Mikoa ya Tanga na Njombe kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mafanikio yanayoonekana katika kuendeleza tasnia ya maziwa kupitia ushirika” Amesema Kandege

  Amesisistiza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na idara zake nchini kuhakikisha zinawezesha uundwaji wa vyama vya ushirika imara na pia wanaimarisha vyama vya ushirika vilivyopo.

  “Mtambue kuwa kuwepo kwa ushirika imara kunaweza kutatua changamoto nyingi. uwezo wa viwanda vya kusindika maziwa hapa nchini bado ni mdogo ukilinganisha na uwezo halisi wa viwanda hivyo”. Amesema Kandege

  Mhe. Kandege ametoa rai kwa wadau wa sekta binafsi kujitokeza kwenye maonesho ya wafugaji kwa malengo ya kuongeza tija na kuimarisha viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo kwa kuwa  Serikali itaendelea kutoa msukumo wa pekee katika kuendeleza ufugaji wa kisasa nchini na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya tasnia ya maziwa wanaendelea kukamilisha mchakato wa  kuandaa mpango kabambe wa kuendeleza mifugo ambao unahusisha pia tasnia ya maziwa nchini.

  Amewataka wadau wengine kuwekeza katika kujenga na kuendesha viwanda vya maziwa hapa nchini ili kuongeza uwezo wa kuzalisha zaidi bidhaa ambazo ni bora na zenye viwango vya kimataifa ili kukidhi mahitaji ya soko.

  Kuhusu uhaba wa ng’ombe wa maziwa Mhe Kandege Serikali imeandaa mpango kabambe wa kuhakisha upatikanaji wa ngo’mbe bora wa maziwa kwa kuzalisha ndama milioni moja wa ng’ombe wa maziwa kila mwaka na  TAMISEMI na Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za uhimilishaji na upatikanaji wa gesi ya nitrojeni kwa kukiimarisha kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) na vituo vya Kanda na ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

  Mhe. Kandege amesema Wafugaji wanapaswa kuboresha mbinu zao za uzalishaji kwa kuzingatia kanuni za ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa. Na muhimu zaidi wafugaji waunde vyama vya ushirika ambavyo vitaongeza tija katika upatikanaji wa pembejeo, huduma za ugani na huduma za kifedha. 

  Amesema vyama ya ushirika vitakuwa kitovu cha upatikanaji wa huduma na masoko ya maziwa wanayozalisha. Wasindikaji pia waendelee kukusanya maziwa yanayozalishwa kutoka kwa wafugaji na kuyanunua kwa bei nzuri ili kutoa motisha kwa uzalishaji zaidi wa maziwa na kuyasindika.

  Mhe Kadege  amewaagiza Mameya/ Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wote na wakuu wa Idara za Mifugo na Uvuvi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanahudhuria  bila kukosa katika maonesho yajayo ambayo Kimataifa yatafanyika Jijini Arusha ili waweze kujifunza  na kwenda kutoa elimu kwenye Halmashauri zao. 

  Aidha Katika hatua nyingine Mhe. Kandege alishiriki zoezi la ugawaji  wa maziwa kutoka  kampuni ya Asas ya Iringa katika shule za msingi Terrati, Madosoita,Suye, Losiyo,Nkonoo, Osunyai na Kimandolo zilizoko Mkoani Arusha.

  0 0

  Pichani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alipokwenda kuwajulia hali watoto hao wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao walikuwa wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa 
  Watoto Maria na Consolata ambao ni mapacha walioungana wamefariki Dunia usiku huu katika hospitali ya Rufaa mkoani Iringa.Chanzo cha taarifa ya kufariki kwa watoto hao imetolewa usiku huu na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela kupitia ukurasa wake wa Twitta kama unavyoonekana hapa chini.

  TAARIFA ZAIDI TUTAWAJULISHA KADIRI YA ZIKAVYOKUWA ZIKIENDELEA KUPATIKANA.

  MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Gesi Asilia Mhe. Dustan Kitandula (Mb) akikabidhi taarifa ya Kamati hiyo kwa Mhe. Spika mara baada ya kuiwasilisha mbele ya Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa kitaifa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (kushoto) kwa Mhe. Spika
   Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  kuchunguza na kushauri kuhusu Uvuvi wa Bahari Kuu Mhe. Anastazia Wambura (Mb) akikabidhi taarifa ya Kamati hiyo kwa Mhe. Spika mara baada ya kuiwasilisha mbele ya Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa kitaifa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (kushoto) kwa Mhe. Spika
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akipokea taarifa za Kamati Maalum za Bunge kwa niaba ya Waziri Mkuu zilizoundwa kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia kutoka kwa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Wengine katika picha kutoka kushoto kwa Mhe. Spika ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa Kamati Maalum ya Bunge aliyounda kuchunguza na kushauri kuhusu sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu (waliosimama) katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kutoka kushoto waliokaa ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Anastazia Wambura, Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi.  PICHA NA OFISI YA BUNGE
   Spika wa Bunge (Mb), Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa hafla ya uwasilishwaji na kukabidhi taarifa za Kamati Maalum alizounda  kuchunguza na kushauri kuhusu sekta za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi asilia. Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na mara baada ya kuzipokea taarifa hizo Mhe. Spika alizikabidhi Serikalini ambapo zilipokelewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Waziri Mkuu.


  0 0


   Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Joseph Kandege akikagua moja ya machine inayotumika katika usindikaji wa maziwa kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
   Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akikabidhiwa maziwa kwa ajili ya shule mbalimbali katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
   Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akiwa na baadhi ya viongozi wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye  kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akiongea na wadau wa ufugaji katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
  .............................................................
  Angela Msimbira OR-TAMISEMI

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege  amewaagiza wafugaji nchini kuunda  vyama vya ushirika imara ambavyo vitawezesha  kupata huduma za mifugo na kuboresha ukusanyaji na masoko ya maziwa. 

  Mhe Kandege ameyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maziwa iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nanenane, Themi Mkoani Arusha
  Mhe. Kandege amesema uwepo wa ushirika imara utaboresha ukusanyaji wa  maziwa kwa wingi kwa ufanisi zaidi na hatimaye  kuongeza kiasi cha usindikaji kwa viwanda. 

  “Napenda kutoa pongezi kwa wafugaji wa Mikoa ya Tanga na Njombe kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mafanikio yanayoonekana katika kuendeleza tasnia ya maziwa kupitia ushirika” Amesema Kandege

  Amesisistiza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na idara zake nchini kuhakikisha zinawezesha uundwaji wa vyama vya ushirika imara na pia wanaimarisha vyama vya ushirika vilivyopo.

  “Mtambue kuwa kuwepo kwa ushirika imara kunaweza kutatua changamoto nyingi. uwezo wa viwanda vya kusindika maziwa hapa nchini bado ni mdogo ukilinganisha na uwezo halisi wa viwanda hivyo”. Amesema Kandege

  Mhe. Kandege ametoa rai kwa wadau wa sekta binafsi kujitokeza kwenye maonesho ya wafugaji kwa malengo ya kuongeza tija na kuimarisha viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo kwa kuwa  Serikali itaendelea kutoa msukumo wa pekee katika kuendeleza ufugaji wa kisasa nchini na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya tasnia ya maziwa wanaendelea kukamilisha mchakato wa  kuandaa mpango kabambe wa kuendeleza mifugo ambao unahusisha pia tasnia ya maziwa nchini.

  Amewataka wadau wengine kuwekeza katika kujenga na kuendesha viwanda vya maziwa hapa nchini ili kuongeza uwezo wa kuzalisha zaidi bidhaa ambazo ni bora na zenye viwango vya kimataifa ili kukidhi mahitaji ya soko.

  Kuhusu uhaba wa ng’ombe wa maziwa Mhe Kandege Serikali imeandaa mpango kabambe wa kuhakisha upatikanaji wa ngo’mbe bora wa maziwa kwa kuzalisha ndama milioni moja wa ng’ombe wa maziwa kila mwaka na  TAMISEMI na Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za uhimilishaji na upatikanaji wa gesi ya nitrojeni kwa kukiimarisha kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) na vituo vya Kanda na ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

  Mhe. Kandege amesema Wafugaji wanapaswa kuboresha mbinu zao za uzalishaji kwa kuzingatia kanuni za ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa. Na muhimu zaidi wafugaji waunde vyama vya ushirika ambavyo vitaongeza tija katika upatikanaji wa pembejeo, huduma za ugani na huduma za kifedha. 

  Amesema vyama ya ushirika vitakuwa kitovu cha upatikanaji wa huduma na masoko ya maziwa wanayozalisha. Wasindikaji pia waendelee kukusanya maziwa yanayozalishwa kutoka kwa wafugaji na kuyanunua kwa bei nzuri ili kutoa motisha kwa uzalishaji zaidi wa maziwa na kuyasindika.

  Mhe Kadege  amewaagiza Mameya/ Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wote na wakuu wa Idara za Mifugo na Uvuvi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanahudhuria  bila kukosa katika maonesho yajayo ambayo Kimataifa yatafanyika Jijini Arusha ili waweze kujifunza  na kwenda kutoa elimu kwenye Halmashauri zao. 

  Aidha Katika hatua nyingine Mhe. Kandege alishiriki zoezi la ugawaji  wa maziwa kutoka  kampuni ya Asas ya Iringa katika shule za msingi Terrati, Madosoita,Suye, Losiyo,Nkonoo, Osunyai na Kimandolo zilizoko Mkoani Arusha.


  0 0


  Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo,Proffesa Lettice Rutoshobya akifungua tawi jipya la TPB mkoani Tanga kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi akishuhudia Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo,Proffesa Lettice Rutoshobya akikata utepe kushiria ufunguzi wa tawi la TPB Tanga kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi na kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB Dkt Edmund Mndolwa Wakisalimiana na wateja mara baada ya kufungua Tawi hilo Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Dkt Edmund Mndolwa kushoto akiwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Proffesa Lettice Rutashobya anayesaini kitabu cha wageni mara baada ya kufungua tawi hilo la Tanga leo Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Dkt Edmund Mndolwa akisaini kitabu cha wageni kulia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Proffesa Lettice Rutashobya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi akisaini kitabu cha wageni Meneja wa TPB Tawi la Tanga Mwajabu Mshana kushoto akiwaeleza jambo Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya wakurugenzi wa TPB Dkt Edmundo Mndolwa kushoto aliyekaa na anayemaliza muda wake Proffesa Lettice Rutashobya mara baada ya kufunguliwa kwa tawi hilo leo Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya wakurugenzi wa TPB Dkt Edmundo Mndolwa kulia akitembelea maeneo mbalimbali kwenye benki ya TPB tawi la Tanga mara baada ya kufunguliwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Proffesa Lettice Rutashobya katika kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TPB aliyemaliza muda wake Proffesa Lettice Rutashobya akizungumza katika ufunguzi huo wa tawi kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Sabasaba Moshingi  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TPB Dkt Edmund Mndolwa akizungumza katika hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Sabasaba Moshingi akizungumza katika halfa hiyo Meneja wa TPB tawi la Tanga, Mwajabu Mshana Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses Utoaji wa vyeti ukiaendelea mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi huo Picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi huo Sehemu ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo  MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB Dkt Edmund Mndolwa amesema mtaji wa benki hiyo hivi sasa umekuwa kutoka Bilioni 8 hadi kufikia Bilioni 60 hatua inayoonyesha utendaji mzuri wa wafanyakazi kutokana na kutoa huduma bora zinazowafanya wateja kuvutiwa na kujiunga nao.

  Dkt Mndolwa aliyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa tawi la Tanga la Benki hiyo lililopo eneo la Chumbageni Jijini Tanga ambao ulifanywa na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Proffesa Lettice Rutashobya kwenye halfa iliyofanyika mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa bodi ya wakurugenzi na wafanyakazi.

  Alisema hatua hiyo inatokana na huduma nzuri inayotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo na hivyo kusaidia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wateja jambo ambalo limepelekea kuongezeka matawi nchini kutoka 32 mpaka 74 kwa sasa.

  “Niwapongeze sana TPB kwa kasi kubwa ya utendaji mzuri mliokuwa nayo na kupelekea kuwezesha kupanua wigo wa matawi kwa wateja wenu ambapo awali kulikuwa na matawi 32 lakini hivi sasa yamefikia 74 hii ni hatua nzuri sana hivyo kuwatake muendelee nayo “Alisema.

  “Lakini pia nimpongeze Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi anayemaliza muda wake Proffesa Lettice kwa kazi nzuri aliyoifanya jambo ambalo limewezesha kufikia mafanikio yaliyopo hivi sasa ndani ya benki hii nitaendelea kushirikiana na wafanyakazi “Alisema.

  Awali akizungumza katika halfa hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshingi alisema benki yake imeendelea kukua kwa kasi mwaka hadi mwaka na kupata faida ambayo imewezesha kutoa gawio kwa serikali ya zaidi ya bilioni moja.

  “Mwaka Jana 2017 benki ilipata kiasi cha Bilioni 18.4 kama faida kabla ya kodi lakini pia tumedhamiria kuboresha huduma zetu ili tuweze kufanya vizuri kwani ushindani kwenye sekta hii ya mabenki ni mkubwa “Alisema.

  Kwa upande wake Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo,Proffesa Lettice Rutoshobya alisema wanaamini tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye benki hiyo kwani lengo kubwa ni kuwasogezea huduma karibu wananchi .

  “Ni furaha kubwa sana kwetu sisi TPB kuweza kufikisha huduma zetu hapa Tanga kupitia tawi letu hili Jipya pia tunalo tawi lingine dogo kule wilayani Korogwe ambapo wateja wetu wanapata huduma za kibenki”Alisema.

  Naye Meneja wa TPB tawi la Tanga, Mwajabu Mshana alisema mwitikio wa wakazi wa mkoa huu umekuwa mzuri tangu walipoanza kutoa huduma zake maeneo hayo ya Chumbageni huku akieleza wamejipanga kutoa huduma nzuri kwa wananchi (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamiiya Tanga Raha)

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. 
  Mhe. Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam tarehe 06 Januari, 2018. Pamoja na kuwapa pole Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake. 
  Mhe. Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista wa Consolata Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo. 
  Amewaombea Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi.
  Amina.


  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  CHANGAMOTO ya ukosefu wa soko Katika Kijiji cha Manyovu Kata ya Munanila wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, imekuwa kero ya muda mrefu ambayo imesababisha wafanyabiashara wengi wa eneo hilo kukimbilia Kasulu na mikoa mingine.

  Wanafanya hivyo kwa lengo kuendeleza biashara zao hali inayo sababisha kushuka kwa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.

  Wakizungumza na Michuzi Blog mkoani Kigoma mwananchi na mfanyabiashara wa Manyovu , Jackson Hemana amesema Soko litakapojengwa watapata faida kubwa na kwamba Warundi wamekuwa wakija Tanzania na kwenda kuchukua bidhaa katika Wilaya ya Kasulu kwa kuwa Manyovu hakuna soko.

  Amesema litakapo jengwa wananchi wana muamko wa kufanya biasha na itasaidia pia hata kuongeza pato katika Wilaya na wananchi wote.Azalia Ashery amesema wao kama kafanya biashara wa mazao ya ndizi na nanasi pamoja na vyakula vingine wanapata shida na wanalazimika kuuzia biashara zao juani na mvua kuwanyeshea, hali inayosababisha mazao yao kuharibika na kupata hasara.

  Pia amesema wafanya biashara wengine wanaamua kuuzia mazao yao shambani kutokana na ukosefu wa soko ambapo wanalazimika kuuza kwa bei ya chini kwani hakuna mahali watakapo kwenda kuuzia.

  "Edapo Serikali itajenga jengo la soko itawasaidia sana wakulima kuinuka na kufanya biashara pamoja na kuinua Wilaya ya Buhigwe kwakuwa eneo hilo ni eneo maarufu kwa wakulima wa , Kahawa , Ndizi , Nanasi na Mazao mengine ya chakula na biashara hivyo yatapa soko na kuinua uchumi wa Watanzania," amesema.

  Akizungumza ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia General Marko Gaguti amesema kutokana na changamoto hiyo wao kama viongozi wa Wilaya walishirikiana na kuandaa andiko la kuomba fedha serikalini kwaajili ya ujenzi wa soko la kimataifa litakalo wakutanisha wananchi wa Burundi na Tanzania kufanya biashara Katika soko la kimataifa ambalo litajengwa mpakani.

  Amesema mradi huo umekubaliwa na hatua za awali zimekwisha kamilika ambapo Serikali kuu imetoa fedha Sh.bilioni 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa soko lenye ghorofa moja litakalo kuwa na Ofisi 300 na maeneo ya vibanda vya wazi 500 na ujenzi utaanza mwaka wa fedha 2018/2019 na Julai mwaka huu watatangaza zabuni ya awali na ujenzi utatumia mwaka Mmoja.

  "Sababu Kubwa ya kuuweka mradi huu Manyovu katika Wilaya ya Buhigwe eneo hilo ni eneo maarufu kwa Wilaya hiii na Mkoa kwa ujumla linalo wakutanisha Wafanya biashara Wengi kutoka Nchi za jirani kutokana na mpaka huo kutumiwa na Watu wengi ,soko hilo litakapo kamilika litatoa chagizo kubwa Kwa Wananchi wa Buhigwe na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kupata Fulsa ya Biashara na kuongeza pato katika Halmashauri ya Wilaya hiyo", alisema Brigedia Jenerali Gaguti.

  Aidha aliwaomba Wananchi washiriki kwa pamoja katika ujenzi wa soko hilo pamoja na usimamizi ili malengo ya serikali ya kukamilisha mradi huo unao tarajiwa kuingizia kiasi cha shilingi milioni 230 kwa halmashauri hiyo ukamilike kwa wakati ilikuongeza ukusanyaji wa mapato katika halmashauri.

  Baraka Lupori ni Diwani wa Kata ya Munanila alisema anaishukuru sana Serikali kwa kuweza kuweka mradi mkubwa wa soko katika eneo hilo ambalo lilikuwa kilio kikubwa Kwa Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe na Kata hiyo ,ambapo Wafanya biashara wengi wa eneo hilo walikimbia kutokana na kukosa soko hali iliyopelekea kushuka kwa Mapato kupelekea kata hiyo kukusanya Kiasi cha shilingi milioni tatu tu kwa mwezi.

  Alisema Munanila ni mpaka unaokutanisha Wananchi wa Nchi tatu za Burundi, Rwanda na Congo, na Wananchi wa Burundi wengi wa Burundi wanategemea sana Bidhaa za chakula kutoka Katika Vijiji vya Manyovu na Wilaya ya Buhigwe kwa ujumla soko hilo litakapo kamilika litasaidia sana wafanya biashara wengi walioondoka Manyovu na kuhamia maeneo Mengine kwaajili ya kuendeleza Biashara zao kurejea na kufanya biashara na kipato cha halmashauri na wananchi kitaongezeka.

older | 1 | .... | 1591 | 1592 | (Page 1593) | 1594 | 1595 | .... | 1897 | newer