Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1590 | 1591 | (Page 1592) | 1593 | 1594 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wamachinga wakati  wa kufungua  Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wamachinga wakati  wa kufungua  Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo  akiongea na baadhi ya viongozi wa shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA leo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.

  0 0

  Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

  NAIBU  Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga, Abdalah Ulega ameweka jiwe la msingi  kwa ajili ya  ujenzi wa madaraja matatu wilayani Mkuranga mkoani Pwani

  Akizungumzia ujenzi wa madaraja hayo ,Ulega ameeleza  madaraja hayo matatu yatajengwa katika vijiji vitatu ambavyo ni  Tamabani Mwanabilatu, na Kifaurongo.

  Amesema ujenzi wa madaraja hayo hadi kukamilika kwake Julai mwaka huu utagharimu kiasi cha takribani Sh.bilioni 1.5.Aidha Ulega amemuagiza mkandarasi anayejenga madaraja hayo asichukue vibarua wa kutoka sehemu nyingine bali wachukuliwe katika vijiji ambavyo mradi huo wa ujenzi wa madaraja unafanyika ili wakazi wa maeneo hayo wapate vipato.

  Pia Ulega  amewaomba wananchi wa Wilaya ya Mkuranga kushirikiana na wakandarasi wa ujenzi ili kuweza kurahisisha kazi hiyo na kufanya mradi huo kuisha kwa wakati.Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini(TARULA) Wilaya ya  Mkuranga, Mhandisi Emmanuel Mubofu amesema miradi hiyo ita kamilika ndani ya miezi miwili tu, yaani kuanzia mwezi Mei hadi Julai mwaka huu.

  Mubofu ameeleza  mradi huo umeanza na kufikia Agosti wananchi wataanza kutumia madaraja hayo licha ya kuikamilisha Julai.Kuhusu  fedha za ujenzi Mubofu ameeleza kuwa zimetoka mfuko wa barabara kwa ajili ya kero hizo za kimiundombinu zilizokuwa zinawakabili wakazi hao.

  Aidha ameeleza wakandarasi wawili wameshaanza kazi na kwa asilimia 20 tayari ujenzi umekamilika.
   Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga  Abdallah Ulega (watatu kutoka kulia) akiweka  jiwe la msingi  kwa ajili ya  ujenzi wa madalaja mitatu yatakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5
   Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi, Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wanaichi wa kijiji cha Kifaurongo kabla katika hafla ya kuweka  jiwe la msingi  kwaajili ya  ujenzi wa madalaja mitatu yatakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
   Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega  akimsikiliza Kaimu Mejeneja Tarula Mkuranga Muhandisi Emmanuel  Mubofu alienyosha mkono alipo tembelea mradi wa ujenzi wa madaraja.
   Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa ameambatana na  viongozi wa (CCM) wa Wilaya Mkuranga  wakivuka Mto Mzinga.
  Wananichi wa kijiji cha Kifaurongo wakivuka Mto Mzinga.

  0 0

  Na Emmanuel Masaka ,Globu ya jamii

  MEYA wa  Ubungo Boniface Jacob ametembelewa na Mabingwa ngumi za ridhaa ambao wameshinda mataji mbalimbali ya ubingwa pamoja na Medali sita katika Shindano la Mchezo wa Ngumi kwa Mkoa wa Dar es Salaam
  yaliyofanyika Uwanja wa Taifa .

  Mabondia walioshinda Medali hizo ni Shomari Pendeza kilo 49,Khamisi Maya kilo 69,Mustafa Khalidi kilo 52,Prospa John kilo 60,Frank Lucian kilo 56 na Alex Mshamba kilo 56.

  Hivyo imeelezwa leo na Meya Jacob kuwa mabondia wameiletea Manispaa ya Ubungo medali za Dhahabu 1,Shaba 2 na Fedha 3 na hiyo ni  heshima kubwa  kwa niaba ya vijana wote katika Manispaa ya Ubungo.

  Katika neno la Shukrani Meya Jacob amejitolea kuwa Mlezi wa kambi yao ya Shirikisho la Ngumi kwa Wilaya ya Ubungo zilizopo Kimara.

  Pia ameahidi kuwatafutia udhamini wa mchezo huo wa ngumi ambapo pia  amewaeleza kuwapatia pair za Gloves,boxing pad,Punching Bags,Clip bandage,Head protectors,na Boxing gears zingine.
  Meya wa ubungo Boniface Jacob akiangalia medali za Dhahabu alizoshinda mabondia Mabingwa wa ngumi za ridhaa, ambapo amejitolea kuwa mlezi wa kambi ya Shirikisho la ngumi wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar es Salaam. 
  Meya wa ubungo,Boniface Jacob (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mabondia wa ngumi za ridhaa.

  0 0


  0 0

  Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela amefungua mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga yanayolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kupiga vita ukatili katika jamii.

  Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza leo Jumatano Mei 30,2018 yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga yamekutanisha wadau mbalimbali wanaohusika katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Investing in Children and their Societies (ICS – Africa). 

  Awali akizungumza,Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia alisema lengo la mafunzo hayo ni kupata maoni na mapendekezo mbalimbali katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. “Lengo la mafunzo haya ni kupata uelewa wa pamoja na kutengeneza mkakati namna gani tunafanya katika kutokomeza vitendo vya kikatili katika mkoa”,alisema Mbia. 

  Akifungua mafunzo hayo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo alisema mkoa wa Shinyanga bado una tatizo kubwa la ukatili dhidi ya watoto na wanawake hivyo zinahitajika nguvu za pamoja 

  “Tunamshukuru mwenyezi Mungu mauaji dhidi ya albino yamebaki historia katika mkoa wetu,lakini katika jamii kumekuwa na unyanyasaji hasa wa watoto,kupitia kamati hii naamini kwa pamoja kama tutaamua kwenda pamoja hatua kwa hatua tutaweza kutokomeza vitendo vya ukatili katika mkoa huu”,alieleza Msovela. “Akina mama na watoto wengi wameathirika kisaikolojia,kimwili,wapo watoto wamekosa elimu kutokana na unyanyasaji wanaopitia kwa pamoja naamini sheria ambazo zipo na umoja huu tutaweza kukabiliana na ukatili wanaofanyiwa wanawake na watoto”,alisema. 

  “Kwa namna ya pekee niwashukuru sana wadau wetu wa maendeleo ICS ambao wamejitolea kudhamini mafunzo haya,na hivi sasa kamati imeshaundwa kutoka katika ngazi ya kata,halmashauri na sasa tunaendelea na mafunzo kwa ngazi ya mkoa”,aliongeza Msovela. 

  Kwa upande wake,Afisa Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mathias Haule alisema umaskini umekuwa chanzo cha vitendo ukatili dhidi ya wanawake hivyo ili kutokomeza vitendo hivyo ni vyema wanawake wanapaswa kuwezeshwa kiuchumi huku wadau wote wakiweka nguvu pamoja katika kuwalinda na kuwatetea wanawake na watoto. 

  Naye Meneja wa shirika la ICS nchini,Kudely Sokoine Joram alisema ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,shirika hilo limekuwa likishirikiana na serikali ili kuhakikisha wanawake na watoto wanakuwa salama katika jamii. 

  “Kupitia mradi wetu wa masuala ya ulinzi na usalama wa watoto tunafanya mradi huu katika manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na wilaya ya Kishapu na baada ya serikali kumaliza kutengeneza mwongozo,ilituomba tunapokuwa na rasilimali basi tuweze kusaidia serikali kuhakikisha kamati zinaundwa na zinapata mafunzo ndiyo maana hata haya mafunzo tumeyawezesha sisi”,alieleza. 

  Meneja huyo wa ICS alisema katika ngazi ya halmashauri,kata na vijiji mpaka sasa wamezisaidia kamati 25 wakishirikiana na serikali na wanaendelea kuwezesha uundwaji wa kamati ili kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

  “Sisi kama wadau wa maendeleo tunashughulika na masuala ya malezi na matunzo bora ya watoto,masuala ya ulinzi wa watoto kwa mfano miongozo ya serikali na sheria zilizopo lakini pia kuwezesha familia katika masuala ya kiuchumi,kujenga uwezo wa taasisi ndogo ndogo na maeneo husika yanayoshughulika na maendeleo ya jamii”,alisema Joram. 
  Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifungua mafunzo ya kujengea uwezo kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga leo Mei 30,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifungua mafunzo na kuwataka wajumbe wa kamati hiyo kushirikiana katika kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.
  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
  Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia akielezea malengo ya mafunzo hayo ambapo alisema lengoni kupata maoni na mapendekezo mbalimbali kuhusu namna ya kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
  Meneja wa shirika la ICS nchini Tanzania, Kudely Sokoine Joram akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambapo alisema wameamua kufadhili mafunzo hayo ili kushirikiana na serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
  Meneja wa shirika la ICS nchini Tanzania, Kudely Sokoine Joram akizungumza ukumbini.
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon akielezea namna wanavyoshiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.


  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
  Afisa Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mathias Haule akielezea Muhtasari kuhusu Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
  Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada ukumbini.
  Mafunzo yanaendelea.

  Kushoto ni Afisa Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mathias Haule na Afisa Mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto kutoka shirika la ICS mkoa wa Shinyanga,Shadia Nurdin wakiangalia nyaraka zinahusu masuala ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0


  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina(wa pili kulia) akikata utepe kuzindua Wiki ya Maziwa kitaifa kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro,kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na viongozi wa Baraza la Kilimo nchini na Bodi ya Maziwa.

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina akitoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Wiki ya Maziwa kitaifa kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro jijini Arusha.

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina akiwapa wanafunzi wa Shule ya Msingi Baraa ya jijini Arusha baada ya kuzindua Wiki ya Maziwa kitaifa kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro,kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.
  Meneja wa kampuni ya Milkcom maafuru Dar Fresh,Tunnu Mssika akimpa maelezo Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati akikagua mabanda ya waoneshaji bidhaa mbalimbali zinazotokana na mifugo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina(katikati) akipewa maelezo na Mjasiriamali wa kampuni ya Mpilika Leather kutoka Dodoma,Anna Malongo ,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo .
  Wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Wiki ya Maziwa kitaifa mkoa wa Arusha wakifatilia kwa makini hotuba za viongozi.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina(kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Wakulima nchini(ACT),Dk Sinare Sinare(kulia)kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro,wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa,Lucas Malunde. Imeandaliwa na www.rweyeamuinfo.blogspot.com

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, wakiwemo maofisa tarafa, madiwani, watendaji wa kata, vijiji, walimu na wenyeviti wa vijiji, juu ya kufanya kazi kwa uadilifu na kutumikia jamii, kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo mhandisi Raymond Mushi.
  Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Mhandisi Raymond Mushi akizungumza na wananchi wa Kata ya Madunga juu ya kufanya kazi na kuwahusia kuwa siku mbili ambazo mtu hawezi kufanya chochote ni jana na kesho hivyo waitumie siku ya leo kwa kutimiza wajibu wao, kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Nicodemus Tarmo.
  Mkuu wa Wilaya ya Babati Vijijini Mkoani Manyara, Vrajilal Jituson, akizungumza na wananchi wa Kata ya Madunga ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo yao ikiwemo suala la elimu.
  Mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Manyara, Esta Mahawe akizungumza na wananchi wa Kata ya Madunga ambapo alijitoa mashuka 10 kwa ajili ya wagonjwa watakaotumia kwenye zahanati ya kijiji hicho iliyozinduliwa na Mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti.


  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti ameziagiza Halmashauri za Wilaya za Mkoa huo kuhakikisha zinatekeleza agizo la uanzishwaji wa viwanda 100 na hadi mwezi Septemba mwaka huu viwe vimekamilika. 

  Mnyeti akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, alisema kila halmashauri ya mkoa huo wenye halmashauri saba, inapaswa iwe na viwanda 15. Mnyeti alisema serikali ilitoa agizo la kila mkoa uanzishe viwanda 100 hivyo na mkoa wa Manyara nao unapaswa kuhakikisha unatekeleza agizo hilo kwa kila halmashauri kuwa na viwanda 15. 

  Alisema agizo hilo linatakiwa kutekelezwa kwa kila sekta ikiwemo kilimo na mifugo ambazo ndizo shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wengi wa mkoa huo. “Watumishi wa umma wanapaswa kutambua kila taaluma waliyoisomea wanapaswa kuwekeza kwenye fikra ya viwanda kwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa sekta hiyo,” alisema Mnyeti. 

  Aliwapongeza mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Raymond Mushi na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hamis Malinga kwa kutekeleza agizo hilo la uanzishwaji wa viwanda vipya. “Kwenye miezi mitatu iliyopita Halmashauri ya Babati mlikuwa mmeshafanikisha uanzishwaji wa viwanda nane na hadi kufikia mwezi Septemba mtakuwa mmekamilisha viwanda 15 hongereni sana,” alisema Mnyeti. Mkuu wa wilaya ya Babati, mhandisi Raymond Mushi alisema wananchi wa eneo hilo ni wachapakazi wazuri na hujishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji, uvuvi, ujasiriamali na nyinginezo.

  Mushi alisema kwa kiasi kikubwa wananchi wa wilaya yake ni wachapakazi huku wakishirikiana na serikali katika kufanikisha maendeleo mbalimbali.Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Vrajilal Jitu Son alisema wameshajipanga kutekeleza hilo kupitia viwanda mbalimbali vilivyopo jimboni humo. Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati, Hamis Malinga alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikisha utekelezaji wa vipaumbele mbalimbali ikiwemo elimu, afya na maji.“Kwenye suala la migogoro ya ardhi, kamati ya ulinzi na usalama chini ya Mwenyekiti wake mheshimiwa mkuu wa wilaya kwa kiasi kikubwa imefanikisha kusuluhisha japo kuwa maeneo machache yaliyobaki na yanaendelea kufanyiwa kazi,” alisema.

  Jituson alisema kwenye eneo hilo kuna viwanda mbalimbali vipya vilivyojengwa vikiwemo vya mafuta, sukari, kukoboa mpunga, unga, na kiwanda cha vyakula vya mifugo. Alisema kupitia nafasi ya vijiji vingine 30 kupatiwa umeme wa Rea awamu ya tatu, itasaidia kuanzisha viwanda vidogo na vya kati kwa wajasiriamali mbalimbali waliopo kwenye jimbo hilo. 

  Mkazi wa Kijiji cha Endanachang’ John Lorry alisema serikali na sekta binafsi zinapaswa kujipanga na kuanzisha kiwanda cha biskuti ili zao la mbaazi lipate soko. Lorry alisema changamoto ya soko la mbaazi imekuwa kero kwa jamii ila kupitia viwanda wakulima wengi wa eneo hilo wataweza kunufaika kwa kupata sehemu ya uhakika ya kuuza zao hilo.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa Wabunge, ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwa marehemu kasuku Bilago Wilayani kakonko Mkoani Kigoma.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa heshima za mwisho nyumbani kwa marehemu Kasuku Bilago Wilayani kakonko Mkoani Kigoma.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiwasabai watoto wa marahemu, Kasuku Bilago Wilayani kakonko Mkoani Kigoma.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto)akimfariji Mke wa marehemu Ndg. Pietha Bisangwa Bilago leo Wilayani kakonko Mkoani Kigoma.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe (kulia) katika msiba wa marehemu, Kasuku Bilago Wilayani kakonko Mkoani Kigoma.

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE

  0 0

  Mhe. Mhandisi Stella Manyanya Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji akifuatilia Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea.

  Mkutano huu ulilenga kujadili na kutolea ufumbuzi masuala mbalimbali yakiwemo ya kiforodha, ambayo yamekuwa kikwazo katika ufanyaji wa biashara za kuvuka mipaka katika Jumuiya.Mkutano huu uliofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018 na kuhudhuriwa na nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifikia tamati tarehe 30 Mei, 2018 jijini Arusha.
  Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliofanyika jijini Arusha.
  Kutoka kushoto ni Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji wakifuatilia mkutano 
  Maza Kuu ikiongoza Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliokuwa ukiendelea jijini Arusha 
  Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto) akisaini taarifa ya Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara,Viwanda,Fedha na Uwekezaji. Kushoto Bw. Eliah Chilangazi Afisa Biashara kutoka Wizara ya Biashara, Viwanda, na Biashara 
  Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji (Katikati), na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji (kulia) wakishauriana jambo 
  Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya wakifuatilia mkutano 
  Waheshimiwa Mawaziri, Mabalozi na Watendaji wa Serikali wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano

  0 0

  Mwanablogu kutoka Tanzania Krantz Mwantepele kutoka blog ya Mwanaharakati Mzalendo amechaguliwa na serikali ya Russia kuwa miongoni mwa Blogers na social media influencers 50 dunia nzima kwaajili ya kutembelea nchi hiyo kabla michuano hiyo haijaanza mapema Juni 14.
  Mtanzania huyo pamoja na wenzake atapara fursa ya kutembelea viwanja vyote 5 ambavyo ni Krestovsky Stadim, Fisht Olympic Stadium, Cosco Arena, pamona na Ekaterinburg Arena.z

  Krantz ambaye pia ni Katibu wa Tanzania Bloggers Network (TBN), alisema yeye aliomba nafasi hiyo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kutumiwa link za marafiki zake.
  “Nafurahi kuwa mmoja ya Blogers na social media influencers 50 dunia nzima kualikwa na serikali ya Urusi kufanya Coverage ya kombe la dunia na vivutio mbali mbali vya nchini humo,” alisema Krant.
  Krantz akikabidhiwa bendera na Mkurungezi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi. 
  Aliongeza, “Nitakuwa balozi mzuri pia wa utalii wa hapa nchini kwa udhamini mkubwa wa Wonderfultanzania, Nitawakilisha vizuri huko ughaibuni Endelea kufuatilia na koncept_tv na Mwanaharakati Mzalendo Blog nitakupa exclusive zote kupitia huko,”Mwanabloger huyo pia alipongezwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali pamoja na kukabidhiwa bendera ya Tanzania na Mkurungezi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi.


  0 0

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza Kikao cha 44 cha Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika tarehe 29 hadi 30 Mei, 2018 katika Ukumbi wa Benki Kuu, Zanzibar ambapo TRA ilikuwa mwenyeji. Kushoto ni Mhe. Audace Niyonzima wa Mamlaka ya Mapato Burundi na kulia ni Bi. Doris Akol, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA).

   Mwenyekiti wa Kamati ya Watalaam wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mahariki Bi. Martine Nibasumba kutoka Mamlaka ya Mapato Burundi (OBR) akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo kwa Makamishna Wakuu (hawapo pichani) wakati wa Kikao cha 44 cha Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya hiyo kilichofanyika tarehe 29 hadi 30 Mei, 2018 katika Ukumbi wa Benki Kuu, Zanzibar ambapo TRA ilikuwa mwenyeji.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Wakuu wenzake na baadhi ya wajumbe wa Kikao cha 44 cha Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika tarehe 29 hadi 30 Mei, 2018 katika Ukumbi wa Benki Kuu, Zanzibar ambapo TRA ilikuwa mwenyeji.


  0 0

  Eneo la Kitongoji cha Mferejini lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuanzisha kambi kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko .
  Wahanga wa Mafuriko wakianza ujenzi wa nyumba za Miti kwa ajili ya kujisitiri katika eneo la Ruvu Mferejini.
  Makazi ya wananchi hawa kwa sasa wanalala nje ,wakiteseka na Baridi,Mbu na wanyama wakali kama Nyoka hali ambayo inatishia Afya zao.
  Hata hivyo tayari serikali imeanza kufikisha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo ya Maji kwa ajili ya kunywa pamoja na kupikia.
  Na hizi ndio sehemu za makazi ya wananchi hawa.
  Huduma Muhimu kama Choo zimeanza kujengwa katika eneo hilo.
  Wananchi Jamii ya Massai pia ni miongoni mwa waathirika wa Mafuriko hayo.
  Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akiwa ameongozana  na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour wakitembelea moja ya Kaya ya Jamii ya Wafugaji walioanza maisha mapya katika maeneo yaliyotengwa na Serikali.
  Baadhi ya Nyumba za Jamii ya Kimasai zikianza kujengwa katika eneo hilo.
  Kama ilivyo ada kwa tamaduni za Mila za jamii ya Maasai kina mama ndio watendaji wakubwa wa shughuli za Nyumbani kiwemo ujenzi wa Nyumba kama anavyoonekana Bibi huyu.
  Arikadharika shughuli ya uchotji wa maji vivyo hivyo.
  Na hii ni Familia moja ya Fashet Kimotong wakiwa katika eneo jipya  baada ya kuhama makazi yao ya wali kufuatiwa Nyumba zao kuzingirwa na maji .

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  SERIKALI imetoa siku mbili kwa wananchi waliosalia katika Vijiji vya Ruvu Mferejini na Ruvu Marwa wilayani Same ,Mkoani Kilimanjaro vilivyozingirwa na maji kuondoka mara moja na kwamba watakao kaidi wataondolewa kwa kutumia nguvu na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

  Zaidi ya watu wapatao 2000 wamelazimika kuyahama makazi yao baada ya kufikwa mafuriko kutokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha huku eneo lililoathirika zaidi na mvua hizo ni ukanda wa tambarare wa wilaya ya Same unaopakana na Bwawa la Nyumba ya Mungu.

  Licha ya Idadi hiyo ya watu kuyahama makazi yao lakini bado wapo waliokaidi kuondokana na hapa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Same ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya hiyo ,Rosemerry Senyamule ,ikatoa agizo.

  Serikali imetenga maeneo kando ya milima iliyopo katika kitongoji cha Mferejini kwa ajili ya Kambi za Muda kwa watu waliokosa Makazi ,Clouds Habari imefika katika Kambi hizo na kujionea maisha mapya ya wahanga wa mafuriko huku misaada ya kibinadamu ikihitajika zaidi .

  Licha ya kukosekana kwa baadhi ya huduma katika eneo hili bado wananchi hawa wanahitaji msaada wa hali na mali ili angalau kuweza kunusuru Maisha yao kutokana na Baridi kali ,Mbu na hata wanyama wakali wakiwemo Nyoka.

  Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi ,Aisha Amour ni miongoni mwa baadhi ya viongozi waliowatembelea wahanga wa mafuriko kwa ajili ya kutoa pole . 

  Mafuriko katika vijiji hivi yanatajwa kuwa hutokea kila baada ya Miaka 10 na kwamba mara ya mwisho yalitokea mwaka 2008 huku chanzo kikitajwa kuwa ni kujaa kwa Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo ujazo ulifikia Mita za ujazo 689.88 ambazo kwa sasa zimeanza kupungua hadi kufikia mita za ujazo 689.80 baada ya maji kuanza kuelekea kwenye maeneo ya makazi kwa kupitia mto Pangani.


  0 0

  Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Aisha Amour (aliyenyoosha mkono) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Maafa  ya mkoa wakiwa eneo la Ruvu Darajani ambako magari yanaishia baada ya miuondo mbinu ya barabara kujaa maji .
  Moja ya barabara ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakazi wa maeneo ya Ruvu Muungano na Darajani ikiwa imejaa maji na kusababisha adha kwa wasafiri.
  Baadhi ya wananchi wakijaribu kuyahama makazi yao baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji katika Vijiji vya Ruvu  Marwa na  Ruvu Mferejini.
  Baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia usafiri wa pikipiki kwa maeneo ambayo bado hayajafikwa na maji mengi.
  Kutokana na miundombinu ya barabara kuharibika vibaya baadhi ya wafanyabiashara ya bidhaa ndogondogo wametumia kadhia hiyo kununua bidhaa kama Unga na Mchele na kuwauzia wananchi waliozingirwa na maji kwa bei ya juu.
  Usafiri pekee kwa sasa katika maeneo hayo ni Trekta na Mitumbwi ambayo imekuwa ikitumika kuhamisha mali pamoja na wananchi.
  Na Hii ndio hali Halisi ya wananchi katika maeneo hayo wamelazimka kutumia mitumbwi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine .

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  0 0

   Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akipunga  mikono kuwaaga wafanyakazi na Viongozi wa Ofisi ndogo ya CCM Lumumba mara baada ya kukabidhi ofisi kwa Katibu Mkuu mpya Dkt. Bashiru Aliy ambaye ameanza kazi rasmi leo.
    Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukabidhi ofisi kwa katibu Mkuu mpya wa CCM.
   Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi DK. Bashiru Ali akiwaeleza Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali vipaumble vyake katika uongozi alioupata ndani ya CCM katika awamu hii ya tano .
    Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya Watendaji wa Chama Cha Mapindzui waliofika katika hafla ya kukabidhi Ofisi iliyofanyika  katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba.
    Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana, akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogoro mara baada ya kumaliza kukabidhi ofisi kwa katibu mkuu mpya .
    Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa CCM Lumumba.

  0 0


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuzindua Maadhisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wa nne (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ana Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Evarest Ndikilo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba. (Picha na Robert Okanda Blogs)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Space Engineering Philip Mtui aktika moja ya banda la nishati mbadala alipofanya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ana kaimu Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Evarest Ndikilo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Mei 31, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba (wa pili kushoto).

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Afisa Mtendaji Mkuu, wa Kampuni ya TMBM Powerspot Eco-Energy Limited, Lucas Singili namna wanavyoweza kutumia jiko la nishati mbadala kutengeza mwanga kwa matumizi ya nyumbani wakati Waziri mkuu aliptembelea bando la kampuni hiyo kabla ya kuzindua maadhiisho hayo. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Afisa Masoko wa Kampuni ya Falcon Packaging Anna Mrema jinsi wanavyotengeneza vifaa vya plastic ili kunusuru ukataji wa miti kwa kutengeza bidhaa hizo wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Chilambo General Trade Company, Gideon Chilambo wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea bidhaa mbadala zinazotengenzwa kuzuia uharibifu wa mazingira. Waziri Mkuu alitembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Pamoja naye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, pia Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mkoa wa Dar, Mhandisi Evarest Ndikilo (kushoto kwake).

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya AG Energies, Ibrahim Mussa wakati alipotembelea banda lao kujionea bidhaa mbadala zinazotengenezwa na kampuni hiyo kupunguza uharibifu wa mazingira. Wa tatu (kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi, Evarest Ndikilo (kulia kwake)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Nimwagile Mwaijumba wakati alipotembelea banda lao na kujionea mashine za Kampuni ya Nyumbu ya kutengeneza mkaa bora kwa kutumia takataka iliyobuniwa na kutengenezwa na kampuni hiyo. Waziri Mkuu alitembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Wa tatu (kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Evarest Ndikilo

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya JHS , David Mwendapole wakati alipotoa maelezo kuhusu majiko makubwa yanayotumia gesi kidogo katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Wanne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonesho hayo wakati alipozindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Mei 31, 2018. Kushoto (kwake) ni Waziri wa Mazingira na Muungano January Makamba na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Yesaya Mwita.

  Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018.

  Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018.

  Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018.  Baadhi ya wananchi na viongozi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018.

  Mgeni Rasmi Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiiongoza meza kuu kuimba wimbo wa Taifa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2018.

  Mkuu wa Idara ya Sayansi wa na Usimamizi wa Mazingira katika skuli ya Sayansi na mazingira wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dkt. Chacha Nyangi akimpatia maelezo mmoja wa wageni aliyetembelea banda la ARU, katika maonesho hayo.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakati wa kuagana na viongozi baada ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2018. Kutoka (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Pia Kaimu mkuu wa Mkoa wa Dar, Mhandisi Evarest Ndikilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala, Mwenyekiti wa CC wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva.

  Sehemu ya wasanii wa Kikundi cha Dar Creators wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo.
  Afisa Msaidizi wa Afisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Trend Solar, Iman Ayoub akiwapatia vipeperushi na maelezo ya shughuli zifanywazo na kampuni hiyo walipotembelea banda lao kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Mei 31 2018.
  Msaidizi wa Mradi wa kuhamashisha matumizi ya Bioethanol kama nishati mbadala na safi kwa matumizi ya kupika, Alusaria nkya akifafanua jambo kwa wageni waliotembelea bandao la mradi huo, na maelezo ya jinsi ya kutumia nishati hiyo walipotembelea banda lao kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Mei 31 2018. Kushoto ni Afisa mwingine, Doroth Aminiel.

  Mkuu wa Idara ya Sayansi wa na Usimamizi wa Mazingira katika skuli ya Sayansi na mazingira wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dkt. Chacha Nyangi akimpatia maelezo mmoja wa wageni aliyetembelea banda la ARU, katika maonesho hayo.  Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Gervas Jonas akitoa maelezo kwa sehemu ya wageni aliyetembelea banda la ARU, katika maonesho hayo.  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Evarest Ndikilo (kushoto) akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala baada ya kushiriki uzinduzi huo.


  WIZARA, TAASISI ZA SERIKALI ZITUMIE NISHATI MBADALA – WAZIRI MKUU


  *Aagiza viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wabadilike


  *Ataka wasimamie wananchi waachane na matumizi ya mkaa


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara, mashirika na taasisi zote za Serikali na binafsi zianze kutumia nishati mbadala ili kuondoa kabisa matumizi ya kuni na mkaa.


  “Wizara, taasisi na mashirika yote ya Serikali na binafsi pamoja na vikundi vya uzalishaji wanaotumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia au shughuli za uzalishaji waanze kutumia nishati mbadala ili matumizi ya mkaa yaishe na ikiwezekana yatoweke kabisa,” amesema.


  Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Mei 31, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Mkaa ni Gharama: Tumia Nishati Mbadala.”


  Waziri Mkuu amesema teknolojia bora ya uzalishaji wa mkaa mbadala ambayo ameiona kwenye maonesho hayo, ikuzwe na kusambazwa kote nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi waachane na matumizi ya mkaa wa kawaida na badala yake watumie mkaa-mbadala kwa lengo la kuhifadhi misitu na kupunguza uharibifu wa mazingira.


  Ili kufanikisha matumizi ya teknolojia hiyo, Waziri Mkuu amesema vibali vya ujenzi wa majengo makubwa na taasisi kama shule, vyuo, hospitali navyo pia vianze kuzingatia ufungaji wa mifumo ya nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili kurahisisha upatikanaji na matumizi ya nishati mbadala katika taasisi na majengo makubwa.


  “Wahandisi na wachoraji ramani za majengo waweke njia za kupitisha kwenye michoro yao ili ujenzi wa nyumba na majengo haya ukikamilika, watumiaji waweze kutumia teknolojia hiyo,” amesema.


  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Mkoa wa Dar es Salaam ni lazima ubadilike na uachane na matumizi ya mkaa. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mkoa huo unatumia tani 500,000 za mkaa kwa mwaka.


  “Viongozi wa mkoa na wilaya ondokeni hapa na hili kama ajenda ya mkoa wa Dar es Salaam, mkaifanyie kazi na Wizara pia ifuatilie mmetekeleza kwa kiasi gani. Jitihada zilizofanywa na Jiji la Dar es Salaam kupitia kwa Mstahiki Meya, za kuanza kuwapa mtaji wajasiriamali hawa wanaotengeneza teknolojia mpya ni lazima ziigwe na nyie kwenye Manispaa zenu.”


  “Meya ametoa fursa na amewaanzishia, na ninyi sasa endeleeni. Tengenezeni bajeti kupitia Mabaraza ya Madiwani na muwaunge mkono wajasiriamali wanaotengeneza haya majiko kwa kuwapa teknolojia hii kwenye maeneo yenu. Wanaotengeneza mashine za mkaa mbadala, wawezeshwe watengeneze mashine nyingi zaidi na zije kila Manispaa, ili kila Manispaa ianze kutumia teknonolojia hiyo kupikia,” alisisitiza.


  Amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam wafuatilie kwa karibu usambazaji wa teknolojia hiyo.


  Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Yusuf Makamba amesema hali ya mazingira hapa nchini ni mbaya licha ya kuwa haionekani kwa haraka na watu waishio mijini.


  “Hali ya mazingira nchini mwetu ni mbaya sana na inawezekana watu wanaoishi Dar es Salaam hawaioni kwa haraka kwa sababu mahitaji yao yote wanayapata sokoni na madukani,” alisema.


  “Wenzetu wa mikoani na vijijii wanaotegemea mvua na udongo wenye rutuba wanataabika kwa sababu kipato chao kinaathirika kutokana na uharibifu wa mazingira,” alisema.


  Alisema mazingira yanafungamana na utalii, kilimo, ufugaji, nishati, maji na kwamba maendeleo ya nchi pia yamefungamana moja kwa moja na mazingira. “Asilimia 90 ya Watanzania wanatumia kuni na mkaa kupikia lakini asilimia 70 ya mkaa wote unaozalishwa nchini Tanzania, unatumika jijini Dar es Salaam,” alisema.


  Waziri Makamba alisema taasisi za Serikali kama vyuo, magereza, hospitali na shule zinaongoza kwa matumizi ya kuni na mkaa na hivyo kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira.


  Akitoa mfano, alisema Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kina wanafunzi wapatao 30,000 na kinalazimika kuandaa milo mitatu kila siku.


  “Chuo hiki kina migahawa tisa, kule nyuma kumejaa magogo ya kuni. Kuna mgahawa mmoja mdogo unatumia magunia 17 ya mkaa kwa siku, sasa huo mkubwa unatumia magunia mangapi?” alihoji.


  Maadhimisho hayo yaliyozinduliwa leo, yataendelea hadi Juni 5, mwaka huu ambayo ni siku ya kilele. Pia wiki nzima kutakuwa na makongamano, midahalo na mjadala wa kitaifa.

  IMETOLEWA NA:


  OFISI YA WAZIRI MKUU,


  ALHAMISI, MEI 31, 2018.  0 0  Naibu WAZIRI WA Fedha, Mipango na Uchumi Dr. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurungenzi benki ya BANCABC Imani John (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Binilith Mahenge wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya BANCABC Jijini Dodoma leo.


  Naibu Waziri Fedha, Uchumi na Mipango Dr. Ashatu Kijaji (kushoto) akifungua akaunti katika Tawi jipya la Benki ya BANCABC Jijini Dodoma mara baada ya kulifungua rasmi jana, kulia ni Frida Mmmari wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Binilith Mahenge akiongea wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya BANCABC jjijini Dodoma jana. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi Dr. Ashatu Kijaji na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde (kushoto).
  Naibu WAZIRI WA Fedha, Mipango na Uchumi Dr. Ashatu Kijaji akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya BANCABC jjijini Dodoma jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BANCABC Imani John (kulia).
  Naibu WAZIRI WA Fedha, Mipango na Uchumi Dr. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya BANCABC Jijini Dodoma jana. Wengine ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurungenzi benki ya BANCABC Imani John (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Binilith Mahenge.
  Benki ya BancABC imezindua tawi jipya jijini Dodoma kwa lengo la kukidhi mahitaji ya huduma za kibenki kwa wateja hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi katika kanda ya kati. Hilo ni tawi la saba kwa BancABC nchini Tanzania.

  Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua tawi hilo, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema ufunguzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka kwa kuwa ofisi za serikali zimehamia Dodoma na Dodoma imepandishwa hadhi na kuwa jiji hivyo mahitaji ya huduma za kibenki yameongezeka ili kuwawezesha wananchi kupata mitaji kwa ajili ya biashara na shughuli mbalimbali na pia kuhamasisha watanzania wengi kuendelea kujenga hulka ya kuweka amana.

  “Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza BancABC kwa kuona umuhimu wa kuleta huduma za kibenki kwa kufungua tawi jipya jijini Dodoma. Ninaamini bado kuna watu wengi ambao hawajanufaika na huduma za kibenki na ni imani yangu kwamba mtafanya kazi kwa bidii ili kuwafikia wananchi na wafanyabiashara wengi mjini na vijijini katika ukanda huu”, alisema.

  Dkt. Kijaji ameonyesha kufurahishwa na hatua ya benki hiyo ya kupunguza riba. “Hii itawavutia wafanyabiashara wengi hivyo kukuza biashara zao na kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo ya biashara na nyumba za kuishi. Upatikanaji wa mikopo kwa riba nafuu pia utasaidia kuboresha hali ya maisha ya wakazi wa mkoa wa Dodoma”, alisema

  Ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla kujenga utamaduni wa kukopa katika benki ili kukuza biashara zao na kukamilisha kwa wakati miradi mbalimbali ya maendeleo. Naibu waziri huyo amewakumbusha wananchi kutumia mikopo kwa malengo kusudiwa na kurejesha kwa wakati ili kujiweka katika nafasi ya kuendelea kukopesheka.

  Amezitaka taasisi nyingine za fedha kuangalia uwezekano wa kupunguza riba zao ili kuwafanya Watanzania wengi kuweza kukopa. Ni ukweli usipingika kwamba riba kubwa imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wakopaji.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John amesema uzinduzi wa tawi hilo ni sehemu ya mpango mkakati wa benki hiyo wa kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wakazi wa Dodoma na wananchi kwa ujumla na kuahidi kuendelea kufungua matawi zaidi nchini.

  “Kwetu sisi leo ni siku ya kihistoria na hatua muhimu katika kutufanya kuwa taasisi kubwa siyo tu nchini Tanzania bali katika bara la Afrika na kusini mwa jangwa la Sahara. Vilevile tuna mpango wa kufungua huduma za mawakala katika robo ya nne ya mwaka ambao watawawezesha wateja wetu wengi kutufikia kirahisi na kupata huduma zilezile zinazotolewa na benki yetu”, alisema. 
   
  “Vituo vya mikopo kwa wafanyakazi vitatoa huduma zaidi na tunazidi kuboresha huduma ya kibenki kwa kutumia simu ya kiganjani ili kuwawezesha wateja kupata huduma wakati wowote mahali popote”, alisema.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo ametoa rai kwa wakazi wa jiji la Dodoma kuchangamkia huduma zinazotolewa na benki hiyo ili kufanikisha ndoto zao za miradi mbalimbali ya maendeleo.

  0 0

   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwele akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani wilayani wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo hayo
   MKUU wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika ziara hiyo ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kulia wilayani Muheza
   MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza
   Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Mhandisi Aram Phares akiwapungia mkono wananchi kwenye ziara hiyo
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakitazama namna maji yanavyotoka kwenye Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani wakati alipofanya ziara kutembelea vyanzo vya maji kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi
   Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akimueleza jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe katika akisisitiza jambo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakati alipotembelea eneo la Ngomeni kwenye na kuangalia tanki kubwa la maji  ambalo litakalokuwa la lita milioni saba  linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza kushoto  ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
   Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili wa pili kulia akimuonyesha jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambalo litakalokuwa la lita milioni saba  linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia mchanga unazotumika kwenye ujenzi wa tanki la maji eneo la Ngomeni
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia kikoto  zinazotumika kwenye ujenzi wa tanki la maji eneo la Ngomeni
   Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili kulia akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza  ambalo litakalokuwa la lita milioni saba  linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
  Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili wa pili kulia akimuonyesha jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza  ambalo litakalokuwa la lita milioni saba  linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza

  SERIKALI imeanza kulishughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kwa vitendo baada ya kutoa kiasi cha bilioni 40 kwa ajili ya kutoa maji kwenye chanzo cha mto zigi kupelekwa kwenye vijiji mbalimbali ili kuweza kuondosha kero hizo iliyokuwepo muda mrefu iliyokuwa ikiwafanya wananchi kutumia muda mwingi kusaka huduma hiyo.

  Hayo yalibainishwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwele wakati alipofanya ziara wilayani humo kutembelea vyanzo vya maji Amani na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani.

  Alisema kuwa mpango huo wa serikali unakusudia kuhakikisha changamoto za maji ambazo walikuwa wanakabiliana nazo wananchi hao kwa muda mrefu zinamaliza ili waweze kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa maisha yao na jamii zinazowazunguka.

  Waziri Kamwelwe alisema hatua hiyo ni juhudi kubwa zinazofanywa na Rais John Magufuli kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi zikiwemo za maji ili kuhakikisha tatizo la kutokupatikana kwa huduma hiyo linaondoka kwa watanzania.

  “Ndugu zangu serikali tumetoa bilioni 40 kwa ajili ya kushughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kutoka chanzo cha Mto zigi kupita vijiji vyote hadi Muheza mjini huu ni mpango wa kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji Muheza tunaipatia ufumbuzi wa kina “Alisema.

  Aidha alisema kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli zimeweza kuleta mafanikio ambapo juzi tumesaidia mkataba na serikali ya India wa dola Bilioni 500 kwa ajili ya kutatua changamoto za upatikanaji wa maji ambapo katika fedha hizo dola milioni 100 zitakuja wilaya za Muheza na Korogwe kwa lengo la kuhakikisha wanashughulikia tatizo la maji

  “Ndugu zangu mbunge wenu anafanya kazi kubwa na nzuri sana wakati ofisi ipo pale Jijini Dar es Salaam alinifuata ofisini akaniambia kwenye Jimbo lake kuna tatizo kubwa la maji hasa nyakati za kiangazi kwa wananchi kununua maji ndoo hadi kiasi cha sh.2000 nikachukua maamuzi ya haraka kwa lengo la kulishughulikia “Alisema.

  Alisema kuwa sio muda mrefu serikali itawapeleka wataalamu kwenye maeneo yenu hivyo kuwataka kushirikiana nao wakati wakitekeleza shughuli zao ili kuona namna nzuri ya kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto ambazo za kutokupatikana kwa huduma kwa vijiji visivyo na uhakika wa maji.

  Waziri huyo alisema kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha mpaka ifikapo mwaka 2020 vijiji vyote vinakuwa na uwezo wa kupata maji ili kuweza kufikia asilimia 85 na mijini kufikia asilimia 95 Hata hivyo alisema kuwa eneo la Ngomeni wilayani humo kutajengwa tanki kubwa la maji litakalokuwa la lita milioni saba ambalo litakamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0


  Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (kulia) pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT,Kanali Aristides Rutta (kushoto) wakisaini mkataba wakampuni ya SUMA JKT kulinda Majengo, mali na Miundombinu ya kampuni ya TTCL Corporation. SUMA JKT ambao ni Kampuni Tanzu ya Jeshi la kujenga Taifa itafanya kazi hiyokwa muda wa mwaka mmoja, kuanzia Juni Mosi, 2018. 
  Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (kulia) pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT,Kanali Aristides Rutta (kushoto) wakibadilishana nyaraka zamkataba wa kampuni ya SUMA JKT kulinda Majengo, mali naMiundo mbinu ya kampuni ya TTCL Corporation mara baada ya kusaini. SUMA JKT ambao ni Kampuni Tanzu ya Jeshi la kujenga Taifa itafanya kazi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja,kuanzia Juni Mosi, 2018. Nyuma yao ni wanasheria wa TTCL na Suma JKT wakishuhudia zoezi hilo.
  Picha ya pamoja ya maofisa wa TTCL Corporation na SUMA JKT mara baada ya hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu yaTTCL Corporation jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kutiliana saini na kampuni ya SUMA JKT kuingia makubaliano ya kulinda Majengo, mali na Miundo mbinu ya kampuni ya TTCL Corporation. Kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT, Kanali Aristides Rutta akifuatilia mazungumzo hayo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo SUMA JKT ambao ni Kampuni Tanzu ya Jeshi la kujenga Taifa itafanya kazi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja, kuanzia Juni Mosi, 2018.

  SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania - TTCL Corporation limeikabidhi kandarasi ya Ulinzi wa Majengo, mali na Miundo mbinu yake kwa SUMA JKT, Kampuni Tanzu ya Jeshi la kujenga Taifa kwa mkataba wa mwaka mmoja kuanzia Juni 01 2018.

  Hafla ya utiaji saini Makubaliano hayo imefanyika leo katika Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania- TTCL Corporation na kuhudhuriwa na Viongozi waandamizi wa taasisi hizo mbili na watendaji wa Idara mbali mbali.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba amesema, TTCL ina furaha kubwa kushirikiana na SUMA JKT katika jukumu hili nyeti la Ulinzi na Usalama wa Majengo, Mali na Miundo mbinu yake.

  “Tuliwapa SUMA JKT kazi ya Ulinzi katika Makao Makuu ya Shirika letu na katika Kituo cha Kimataifa cha kutunzia Kumbukumbu(NIDC) kilichopo Kijitionyama Dar Es salaam. SUMA JKT wamefanya kazi yao kwa Weledi, nidhamu na ufanisi mkubwa, ndio maana leo tunayo furaha kuwakabidhi jukumu kubwa zaidi la kutulinda katika Ofisi zetu Nchi nzima.”

  Bw. Kindamba amesema, TTCL Corporation ni Shirika jipya la Mawasiliano Tanzania ambalo limechukua nafasi ya iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL LTD. Miongoni mwa majukumu mahsusi ya TTCL Corporation ni kuchochea kasi ya ukuaji wa Uchumi, kusimamia maendeleo ya Sekta ya Mawasiliano kwa kuwaunganisha Wananchi wote, kusimamia ufanisi wa Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano kwa niaba ya Serikali, kusaidia shughuli za Ulinzi na Usalama wa Nchi, Huduma za Jamii na ukuaji wa Sekta nyingine zote.

  “Hii ni TTCL mpya ambayo imedhamiria kuwahudumia Wananchi kwa Viwango vya hali ya juu. Tutaweza kutimiza vyema wajibu huo tukiwa na uhakika katika ulinzi na usalama wa Watendaji wetu, mali zetu na Miundombinu yetu ambayo ni muhimu sana kwa Ulinzi na Usalama wa Nchi, amesema.”

  Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT, Kanali Aristides Rutta amesema, licha ya Nidhamu na Ujuzi wa Kijeshi walio nao vijana wake, Kampuni hiyo inajivunia mafunzo na vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi, rekodi iliyotukuka katika utekelezaji wa miradi ya Wananchi na nyenzo za Ulinzi na Usalama walizonazo.

  “Tunalishukuru sana Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa Imani kubwa waliyotupa, tunawakikishia utendaji uliotukuka kwa uzalendo wa hali ya juu wakati wote wa kutimiza majukumu yetu katika kandarasi hii. SUMA JKT imepata umaarufu mkubwa Nchini hasa baada ya kutekeleza kwa mafanikio kandarasi mbali mbali katika Sekta za Ulinzi na Ujenzi wa Miundombinu katika maeneo mengi Nchini.

  0 0

  Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga alisema ili kukomesha vitendo hivyo ni lazima kila mmoja ashiriki kwa nafasi yake. 

  “Ni lazima wadau wote waweke nguvu ya pamoja kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,hivyo mafunzo haya mliyopata yawe chachu ya kuleta mabadiliko katika jamii yetu ili wanawake na watoto waishi salama”,alieleza Msovela. 

  Aidha alisema kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga ni kamati ya kwanza nchini kuundwa na kupatiwa mafunzo na tayari uundaji wa kamati katika ngazi ya halmashauri,kata na vijiji unaendelea. 

  Mafunzo hayo yaliyoanza Mei 30,2018 yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wajumbe wa kamati hiyo ambao kwa pamoja watashiriki katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. 

  Kupitia mafunzo hayo,wajumbe wa kamati hiyo wamejifunza kuhusu dhana ya masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini pia wamejifunza maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 
  Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga.
  Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifunga mafunzo hayo.
  Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisisitiza jambo ukumbini.
  Afisa Mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto kutoka shirika la ICS mkoa wa Shinyanga,ambao ndiyo wafadhili wa mafunzo hayo,Shadia Nurdin akiwashukuru wajumbe kuhudhuria mafunzo hayo na kuwaomba kwenda kufanyia kazi mambo waliyojifunza kwa muda wa siku tatu ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
  Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia akiwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuendelea kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
  Picha ya pamoja wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga.
  Picha ya pamoja wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

older | 1 | .... | 1590 | 1591 | (Page 1592) | 1593 | 1594 | .... | 1898 | newer