Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1588 | 1589 | (Page 1590) | 1591 | 1592 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani akizungumza na waandishi wa habari
   Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani(kulia) akipeana mkono na Katibu wa  kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha New Life Orphans Home, Hamadi Kondo mara baada ya kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni Tsh.9/- kwa kituo hicho kilichopo Boko jijini Dar es Salaam jana.
   Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani(wa tatu kutoka kushoto waliosimama nyuma) akiwa na mawakala huru wa kampuni ya QNET Tanzania mara baada ya kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni Tsh.9/- kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha New Life Orphans Home kilichopo Boko jijini Dar es Salaam jana.
  QNET inaleta Faraja kwa jamii zisizojiweza katika nchi 13 za kiafrika


  · Kampuni hii inaleta furaha kubwa katika kituo cha kulelea watoto cha New LifeOrphans Home jijini Dar es salaam

  Dar es Salaam, Mei 26 2018 - QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inayoongoza kwa kushirikiana na mwakilishi wake wa kijitegemea (IRs) kuleta shangwe na faraja kwa jamii mbalimbali zisizojiweza katika kuashiria mwezi mtukufu wa Ramadhan, katika nchi 13 za Kiafrika.

  Kampeni hii ya mwaka ina lengo la kuboresha maisha ya wengi na inaenda sambamba na falsafa ya kampuni hii ya (RYTHM) Jiinue kuwasaidia wanadamu (Raise Yourself to Help Mankind) Mafunzo ya msingi ya (RYTHM) wakati wote yamekuwa yanalenga katika kuongeza juhudi zaidi ya wajibu katika kujali wale ambao hawana uwezo kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kuishi kwaajili yao, hasa watoto ambao ni alama ya kizazi chetu kijacho.

  Kampeni ya mwaka huu ya Ramadhan katika Afrika itashuhudia ushirikiano mkubwa miongoni mwa wafanyakazi wa QNET, wakala na Wawakilishi Binafsi (IR) wakiunganisha jitihada zao katika kuandaa mfululizo wa mwezi mzima wa shughuli za kutoa misaada katika nchi kama Ivory Coast, Togo, Cameroon, Guinea, Burkina Faso, Tanzania, Niger, Uganda, Chad, Mali, Ghana and Senegal.

  Nchini Tanzania, tukio la utoaji wa misaada ya Ramadhan litashuhudia utoaji wa mchele, tambi, sukari na bidhaa zingine za chakula na matumizi kwa kituo cha Kulelea watoto yatima cha New Life Orphans Home jijini Dar es salaam yenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 9/-.

  Kuna watoto 105 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life Orphans Home ambacho kilianzishwa katika mwaka 2002. Makazi haya ya watoto kwa sasa yanasimamiwa na Mwanaisha Ahmed Magambo na wanategemea misaada ya umma na wasamaria wema kuweza kukabiliana na gharama za mahitaji ya watoto ya vyakula na vinywaji.

  Akizungumzia kuhusu tukio hilo mwaka huu, Meneja wa QNET Muqtadir Suwani, amesema "Kampeni za kutoa misaada ya Ramadhan imekua moja kati ya kampeni zetu za msingi za kila mwaka. Kwa kweli ni muhimu sana, inatia moyo na inakamilisha jitihada za QNET. Kampeni kama hizi huhamasisha uwezeshaji wa jamii na pia huwa zinahamasisha sana kwa wafanyakazi wetu na Wawakilishi wetu binafsi (IR's) kwa kushiriki wao binafsi katika kuboresha maisha ya wengine.

  Hii ni kati ya falsafa ya QNET ya kuwezesha wajasiliamali kujiwezesha na kusaidia jamii.

  Katibu wa kituo cha New Life Orphans Home bw. Hamad Kondo alisema “ Tunawashukuru kampuni ya QNET Tanzania kwa msaada huu ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa watoto wetu na naomba wafadhili wengine waige mfano huu.”

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakisalima iana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile wakati walipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kwa ajili yakufungua mkutano wa Chama cha Wanzsheria wanawake Tanzania TAWLA.

  Amesema “Nawapongeza TAWLA kwa namna ya kipekee sana kwa kutimiza miaka 28 ya uhai wake. Ni miaka 28 ya mafanikio makubwa sana. Nawapongeza kwa sababu, katika miaka 28 ya uhai wenu, hamjawahi kuyumba wala kutoka nje ya lengo la kuanzishwa kwenu, ambalo ni kutumia taaluma ya sheria kuwasaidia wanawake wasio na uwezo kupata msaada wa kisheria na haki zao.” alisema Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais amesema anatambua na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) hapa nchini ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia taaluma ya sheria.
  1
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalim iana na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka katikati ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile.
  2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakisalima iana na Bi Tike Mwambipile Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha iwanawake Tanzania TAWLA katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka .
  3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka kuingia kwenye chumba cha mkutano.
  45
  Mweka Hazina wa TAWLA, Asina Omari akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo kuingia kwenye mkutano.
  15
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
  7
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
  9
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa TAWLA Bi. Athanasia Soka wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
  11
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano mkuu wa 28 wa TAWLA .
  6
  Picha mbalimbali zikionyesha wajumbe waliohudhuria katika mkutano huo wa mwaka wa TAWLA.
  789101112
  Baadhi ya maofisa wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA wakiwa katika mkutano huo.
  131415
  Baadhi ya wajumbe wakifurahia jambo.
  16
  Balozi Mwanaidi Maajal na wajumbe wengine wakiwa katika mkutano huo.
  1718192021
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka katikati ni Bi Tike Mwambipile Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA.
  2223
  Baadhi ya maofiza wa TAWLA wakiwapokea wajumbe na kuwasajili kwa ajili ya kuingia kwenye mkutano huo.
  24
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka kulia ni Mkurugenzi wa TAWLA Bi Tike Mwambipile.
  25
  Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akipiga picha ya pamoja na uongozi wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA.
  26
  Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akipiga picha ya pamoja na sekretarieti ya Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA.
  2728
  Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA.
   

  0 0

  Na Ripota Wetu,Mbeya

  Serikali imeendelea kuwasisitiza waajiri wote nchini kuwapeleka watumishi wao Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kupigwa ‘msasa’ namna ya kufanya kazi za utumishi wa umma. 

  Akizungumza jijini hapa mwishoni wa wiki wakati wa Mahafali ya 28 ya TPSC Waziri wa nchi- Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt (Msaafu) George Mkuchika alisema kuwa ni muhimu waajiri hao wakawapeleka watumishi chuoni hapa hasa ikitiliwa maanani kwamba TPSC ndiyo chuo kilichopewa dhamana ya kuendesha mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiri wapya wa serikali.

  Alisema pamoja na makujuku hayo pia Chuo hicho kina wajibu wa kusimamia mitihani ya utumishi wa umma katika program ya kuendeleza watumishi.Pia TPSC inatoa mafunzo ya kozi nyingine za muda mrefu na mfupi katika maeneo ya uongozi, Utawala na ya matumizi ya mifumo ya kisasa ya TEHAMA.

  Waziri Mkuchika aliwaasa wahitimu kwamba mafunzo waliyoyapata chuoni hapo yasiishie kwenye vyeti bali yawe ni mafunzo ya kufanya kazi kwa weledi na kasi mpya yenye ufanisi wa ili kuleta tija kwa lengo kukuza uchumi wa taifa hili.

  “Ninawasihi huu usiwe mwisho wa kujiendeleza kwani mafunzo huongeza ujuzi , weledi na mbinu maridhawa za ufanisi wa kazi hususan katika kujifunza teknolojia mpya,” alisema.
  Waziri wa nchi- Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt (Msaafu) George Mkuchika akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa Mahafali ya 28 ya TPSC chuoni hapo Jijini Mbeya. 
  Mtendaji Mkuu wa TPSC Dkt Henry Mambo akizungumza wakati wa Mahafali hayo ya 28 ya TPSC Jijini Mbeya 
  Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 28 ya TPSC wakiwa kwenye mahafali hayo chuoni hapo Jijini Mbeya 
  Baadhi ya wafanyakazi wa TPSC wakifatilia mahafali hayo

  0 0

  Na Emmanuel J. Shilatu

  Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Abdulrahman Omar Kinana anatajwa kuwa katika orodha ya safu za viongozi mibuyu na migude kwenye misitu minene ya siasa yenye kuhimili tufani za kila aina pia Mwanasiasa anayependa kuheshimu utamaduni, utaratibu na mwenye kuishi kwa misingi ya nidhamu . 

  Kinana anatajwa kama zao miongoni mwa kunga zitokanazo na mazao katika medani za siasa, utawala, uongozi na aliyeshiba ujuzi toshelezi wa masuala ya diplomasia ya siasa pia anayejua mahusiano yatokanayo na historia, harakati za ukombozi na umoja wa Afrika. 

  Sauti yake aghalabu huwa na mvumo wa mawimbi ya busara, fikara njema na hekima zenye wito pele aamuapo kusema, kukosoa, kutetea, kukumbusha, kushauri au kuonya kutokana na tabia yake ya kufanya yote hayo kwa hali ya kujiamini akiwa na nguvu ya hoja.

  Ukimya wa Mwanasiasa huyo siku zote ni kama mfano wa Simba hodari awindae nyikani au mbugani akiwa hana pupa wala kiherehere. Huyafanya yote kwa utulivu na umakini mkubwa ambao baadae haumletei majuto, athari wala taathira.

  Ni Mwanasiasa wa aina yake aliyewahi kuhitajiwa na Marais (Wenyeviti) watatu awe katibu mkuu wa CCM akakataa huku akitoa madai mazito yenye msingi, nguvu ya hoja na maana.Amewahi kutakiwa na Rais Ali Hassan Mwinyi awe Katibu Mkuu wa CCM akakataa huku akitoa hoja. Akasema alikuwa na mchakato wa kazi nyeti na muhimu akishirikiana na wenzake kufanya mabadiliko ya mfumo mpya wa Jeshi utakaokwenda sanjari na mahitaji ya wakati; hivyo asingekuwa tayari kuiacha kabla kazi hiyo kukamilika.

  Akatakiwa tena na Rais Benjamin Mkapa ashike nafasi hiyo akasita kukubali huku akitoa hoja za msingi na zenye mashiko yasio na shaka wala utata.Kinana mara ya kwanza alitakiwa na Mwenyekiti Mstaafu Kikwete akakataa kubeba jukumu hilo kwa sababu kadhaa alizoona ni ngumu kwake kukitumikia chama kwa wakati huo. Hata hivyo mbinu za ushawishi zikafanyika akaafiki kuwa Katibu Mkuu.

  Bila shaka Kinana aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wakati CCM ikiwa katika mgawanyiko mkubwa uliohatarisha uhai na mustakabali wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.Kwa busara zake, pengine na ziada ya maarifa au mbinu za kijeshi, uzoefu wa kisiasa, uongozi na utawala, Chama Cha Mapinduzi na viongozi wake ghafla wakashikamana tena na kuzika yaliopita.

  Amewahi kusema mbele ya Mzee Mkapa kwa wakati ule amejiona mbele yake bado ipo hazina ya Viongozi wajuzi wa muda mrefu ndani ya chama, vingunge wenye weledi na maarifa ya kisiasa kuliko yake hivyo muda wa yeye kushika wadhifa si wakati huo.Akaachwa na kuendelea kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwa Meneja wa kampeni za wagombea urais Mzee Mkapa na Dk. Jakaya Kikwete.

  Katika safu ya Vijana wa TANU Youth League na baadae UVCCM waliolelewa kwenye mikono ya Wanasiasa kama kina Mwalimu Julius Nyerere, Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, Sheikh Thabit Kombo Jecha, Mzee Rashid Kawawa, Mzee Saadan Abdul Kandoro na Mzee Rajab Diwani, Kinana anaweza kusimama kati yao. 

  Ameshiriki pamoja nao katika mbio za siasa, akichuma uzoefu huku mbele yake kukiwa na Wanasiasa kama Mzee Pius Msekwa, Marehemu Kingunge Ngombare Mwiru, Mzee John Malecela, Hayati Daudi Mwakawago, Hayati Moses Nnuye, Balozi Chrispher Liundi, Ali Ameir Mohamed na wengine kadhaa.

  Vijana wanasiasia wa rika lake na wanaopishana kwa umri kiasi kidogo ni kina Dk Kikwete , Dk Mohamed Seif Khatib, Dk Salmin Amour, Yusuf Makamba, Jaka Mwambi, John Chiligati, Marehenu Ukiwaona Ditope Mzuzuri na wengine wengi .Kanali Mstaafu Kinana kama atajigamba amezaliwa na kulelewa ndani ya TANU/ASP na maisha yake yote amekulia CCM na serikali zake, hoja hiyo itajuzu na kuyakinika. 

  Kwa ufupi ni Mwanasiasa asiyebahatisha katika utambuzi wa mizungu ya siasa, mbinu za utendaji, uelewa na upimaji kwenye viwango vya usemaji, ushauri au anapofanya shambulizi la kisiasa dhidi ya hasimu wake.

  Niliposikia tetesi za kujiuzulu kwake kwa siku nzima ya jana nilikuwa nikitafakari bila kupata majibu ya haraka na kuona haikuwa wakati sahihi na muafaka sana kwa kiongozi huyo wa CCM kuachia ngazi na kujiweka kando. 

  Hata hivyo CCM ni chama kikongwe chenye hazina kubwa ya Wanasiasa hodari hivyo lolote linaweza kuwa ila muhimu ni kutega mingo na kusubiri wakati kwa kutega vyema masikio yetu.

  *Shilatu E.J*

  0767488622

  0 0

   Rais wa AIESEC Tanzania, Amani Shayo akizungumza kuhusu AIESEC na kazi zake ambapo alisema jukwaa hilo lengo lake ni kuwasaidia vijana kujitambua katika masuala ya uongozi, anaamini kwamba jukwaa ni sehemu kubwa ya kufanikisha vijana kujitambua na kujiipanga kushiriki maisha yanayotakiwa katika jamii wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
   Mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na vijana wa kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki kwenye jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
   Msimamizi wa mazungumzo ambaye pia ni Mkuu wa Mafunzo na Miradi wa Empower Ltd, Ella Naiman (kushoto) akizungumza na kuwatambulisha wazungumzaji wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd. Kutoka kulia ni Allen Kimambo, Miranda Naiman, Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga pamoja na Petrider Paul.
   Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga (katikati) akizungumza kwenye jukwaa la vijana la AIESEC  ambapo alisema vijana wanatakiwa kutoa mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi inafikia malengo ya maendeleo endelevu ambayo utekelezaji wake unaishia mwaka 2030 wakati wa jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
   Mzungumzaji katika jukwaa la vijana la AIESEC, Mkurugenzi Mtendaji wa Empower Ltd, Miranda Naiman (wa pili kulia) akizungumza wakati wa jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
   Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group, Irene Mutiganzi akiwasilisha mada kuhusu mitandao ya kijamii ambapo alisema matumizi ya mitandao ya kijamii yakitumika sahihi yatasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
   Mshehereshaji wa jukwaa la vijana la AIESEC, Walter Odemba akiendesha shemsha bongo kuhusu uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
   Mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akijibu maswali kwa washiriki wa jukwaa la vijana la AIESEC kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na umuhimu wa vijana kushiriki moja kwa moja ambalo limefanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
  Baadhi ya vijana kutoka vyuo mbalimbali wakichangia maoni wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower.
  Baadhi ya vijana kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
  Sekretarieti ya maandalizi ya jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.


  Na Mwandishi wetu
  MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez amewataka vijana wa Tanzania kuwa washiriki katika mipango ya maendeleo na sio kusubiri kufanyiwa.

  Aidha ameshauri vijana kuacha kuilalamikia serikali na jumuiya ya kimataifa kuhusu ajira na badala yake wajiulize wamelifanyia nini taifa na jumuiya hiyo.

  Alisema katika kipindi ambacho theluthi mbili ya watu nchini ni vijana, wasitarajie kuajiriwa au kupatiwa kazi kirahisi kwa kuwa idadi ni kubwa kuliko hata yeye alipokuwa akisoma.

  Alisema tatizo la ajira kwa sasa haliwezi kusubiri serikali au wahisani ni tatizo linalokuwa kibinafsi zaidi na kuhitaji vijana katika uwingi wao kuamka na kubuni vitu vitakavyoleta maendeleo yao binafsi na pia ya kitaifa.

  Akizungumza katika jukwaa la vijana la AIESEC mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es salaam Mratibu huyo alisema kwamba  vijana  wanatakiwa kushiriki katika kila kitu na kuacha kushutumu serikali au jumuiya ya kimataifa katika kipindi ambacho dunia imebarikiwa na vijana  kama nguvu kazi yake kubwa.

  Aliwataka vijana kujadili kuhusu malengo ya dunia, fursa zake, utekelezaji wake na changamoto zake.

  “Malengo ya Dunia ni ajenga muhimu sana kwa Tanzania, Afrika na ulimwenguni  kote. Ajenda hii imelenga kuleta mabadiliko chanya kwa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika utekelezaji wake” alisema Alvaro na kuongeza kuwa malengo hayo 17 ni lazima yajulikane ili kil kijana ashiriki katika utekelezaji wake.

  Alisema vijana wakiwa ndio viongozi wa baadae ni lazima waelewe malengo hayo ya dunia na namna ya kuyatekeleza kwa kuyafungamanisha na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa taifa.

  Alisema kwa vijana kuangalia na kutambua wataweza pia kuona ni kwa namna gani wao ni watekelezaji wa malengo hayo na wala si wasindikizaji.

  Aidha aliwataka wakiwa kama vijana wanatakiwa kuwa wbaunifu katika eneo  walilipoo na kuhakikisha kwamba linapata mafanikio makubwa.

  “Kwa wale wanaonifuatilia katika twita mtakumbuka  niliposti  habari za kijana wa miaka kumi na minane ambaye alitengeneza mkono wa roboti unaofanyakazi kutoka katika mabaki ya vifaa vya matumizi ya nyumbani. Huu ndio ubunifu tunaoutaka, wa kutambua changamoto na suluhu zake” alisema Alavaro katika jukwaa hilo lililofanyika Makumbusho jijini Dar es salaam.

  Alisema anaamini kuwa Mpango wa dunia wa maendeleo endelevu sio Biblia wala Kurani na kuwataka vijana kuuangalia, kuutafakari kuujadili na kujua namna ya kuendesha utekelezaji wake kwani imebaki miaka 12 kumalizika kwa utekelezaji.

  Alisema ili kufikia adhima ya kuutokomeza umaskini  ifikapo mwaka 2030 ni vyema vijana wakatumia wakati kwa makini kuangalia malengo hayo 17 na kuona namna ya wao kuwa washirika.

  Aidha katika hotuba yake hiyo alihimiza vijana kufanya mambo kwa wakati:” Vijana tufanye ya wakati, wakati tuna wakati, kwani utafikia wakati tunataka kufanya ya wakati, wakati hatuna wakati”

  Akizungumzia nguvu ya mtandao , Alvaro aliwataka vijana kuwa smati katika kuchagua mambo yanayofaa kwa maendeleo yao na sio kuchukua mambo ambayo yatawaangamiza au kuleta vurugu.

  Katika jukwaa hilo ambalo liliongozwa na Mratibu huyo kulikuwa na wasemaji wengine wakiwemo Rais wa AIESEC Tanzania, Amani Shayo; Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Empower, Miranda Naiman wote hao waliwataka vijana kuwa sehemu ya mafanikio.

  Mmoja wa wa shiriki Debora Kaluzi kutoka Chuo cha Diplomasia ambaye pia ni championi wa malengo endelevu ya dunia alisema kama champion amefarijika kuwepo katika jukwaa hilo kujadili mambo mbalimbali yanayosukuma maendeleo ya nchi na vijana.

  Alisema akiwa championi yeye anajikita zaidi katika lengo la nne na la tano ambalo linahakikisha kwamba wasichana wanakuwa na uwezo huku wakijua thamani yao katika jamii.

  Alisema utekelezaji wa malengo hayo yatasaidia wanawake kujitambua na kufikia lengo la wao kushiriki kikamilifu katika masuala yanayohusu mambo mbalimbali ya kidunia yakiwemo ujasirimali na madaraka.

  Alisema wanawake wakipewa fursa na kukawepo na haki sawa ya jinsia wanaweza kubadilisha mambo mbalimbali yanayohusu dunia wanayoishi.

  Naye Amani Shayo katika mahojiano pamoja na kuzungumza na vijana alisema kwamba akiwa Rais wa AIESEC, Shirika la vijana lililoanzishwa mwaka 2000 Chuo Kikuu kwa lengo la kuwasaidia vijana kujitambua katika masuala ya uongozi, anaamini kwamba jukwaa ni sehemu kubwa ya kufanikisha vijana kujitambua na kujiipanga kushiriki maisha yanayotakiwa katika jamii.

  Alisema kupitia kazi za kujitolea vijana wanazungumza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu 17 yaliyopangwa na dunia na kuhakikisha kwamba wanafanikisha adhima ya dunia.

  Alisema utafiti uliofanywa kwa takaribani vijana 2000 umewapa wazo la nini wanatakiwa kufanya na moja ya mambo ambayo yalijadiliwa katika Jukwaa ni namna ambavyo vijana wanaweza kuwezeshwa kujiajiri kuajiriwa na pia kushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ya utoaji huduma na kadhalika.

  Alisema shirika hilo lina mradi wa kuwezesha vijana kushiriki katika kazi za kujitolea ndani na nje ya nchi na pia kutoa elimu ya kuongeza ujuzi.

  Alisema kazi kubwa ya jukwaa ni kuwaleta pamoja watawala na viongozi na wadau wa maendeleo ambao watashirikiana na vijana kudadavua malengo hayo ya dunia na kuyawezesha kufanyakazi katika maeneo ambapo vijana wenyewe wapo.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Bw. Aron Mbogho akikata utepe kuzindua mradi.
  Mmoja wa wakazi wa kata ya Kiruru akitwishwa ndoo ya maji aliyochota kwenye mradi.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wakifuatilia matukio.
  Afisa mwandamizi wa Water Mission Tanzania,Isack Abdiel akiongea wakati wa hafla hiyo --- Wakazi wa kata ya Kiruru iliyopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, wameanza kupata maji safi na salama kwa matumizi mbalimbali ,kutokana na kuzinduliwa kwa mradi wa maji katika eneo lao. 

  Mradi huo ambao una uwezo wa kuhudumia kaya 427 zenye wakazi zaidi ya 2,135 umejengwa na shirika la Water Mission Tanzania, wakishirikiana na shirika la Rotary Club ya Mwanga, Rotary International na Rotary Foundation. Kata ya Kiruru inayojumuisha vijiji vya Heria, Msikitini, Bhughuru na Mighareni, kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na tatizo la maji safi kutokana na kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya maji kutokana na mazingira ya kijiografia ya eneo hilo. Mkuu wa wilaya ya Mwanga,Bw. Aron Mbogho, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo alisema “Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa kata ya Kiruru, kutokana na kuanzishwa kwa mradi huu mpya wa maji safi na salama katika eneo hili,ambao utawahakikishia wananchi kupata maji safi na salama wakati wote. 

  Kwa niaba ya serikali napenda kutoa shukrani kwa shirika la Water Mission Tanzania na Washirika wake kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto ya tatizo la maji safi na salama kwenye jamii mbalimbali” Bw. Mbogho, alisema mradi huu utanufaisha wakazi wote wa kata ya Kiruru, hususani Wanawake ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji safi kwa ajili ya matumizi ya familia zao. Aliwataka wananchi wa Kiruru kutoa ushirikiano kwa wadau waliofanikisha mradi huu sambamba na kutunza miundombinu ya mradi ili uweze kuwa endelevu. 

  “Kuwepo mradi huu katika eneo hili kutapunguza kwa kiasi kikubwa maradhi mbalimbali yatokanayo na matumizi ya maji yasio salama” alisisitiza. Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Mission Tanzania, Isack Abdiel alisema “Tunayo furaha kubwa siku ya leo kutokana na kukamilisha mradi huu mpya hapa wilayani Mwanga ambao unazinduliwa leo. Mradi huu ni mwendelezo wa jitihada za shirika letu kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto ya kumaliza tatizo la maji kwenye jamii. Nina imani wakazi wa eneo hili la mradi mtahakikisha mnatunza miundombinu ya mradi ili uwe endelevu kwa matumizi ya sasa na ya vizazi vijavyo”.

   Isack Abdiel pia alishukuru viongozi wa serikali wa wilaya ya Mwanga na wadau wengine kwa kuunga mkono Shirika la Water Mission Tanzania, na kwa kutoa ushirikiano wakati wote wa ujenzi wa mradi huu hadi kufikia sasa ambapo umefikia hatua ya kuzinduliwa. Shirika la Water Mission Tanzania, lilianza kufanya kazi nchini Tanzania, mnamo mwaka 2013 likiwa linajishughulisha na ujenzi wa miradi ya kukabiliana na changamoto ya maji kwenye jamii. Hadi sasa Shirika lina miradi katika mikoa zaidi ya 6 ikiwemo, Dodoma, Arusha, Geita, Kagera, Kigoma and Tanga na Kilimanjaro. 

   Ofisi za makao makuu ya shirika hili kwa hapa nchini yapo jijini Dar es Salaam ambayo inaratibu miradi yote inayoendeshwa na shirika hapa nchini. Mbali na Tanzania shirika la Water Missions International, linaendesha miradi ya kukabiliana na changamoto ya maji katika nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Haiti, Honduras, Mexico, Peru, Belize na Indonesia.

  0 0

    Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakishangilia baada ya kuwaita  Ndg. Mizengo Pinda na Ndg. Makongoro Nyerere waingie ukumbini baada ya kukubaliwa kuwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
   Wajumbe wakishangilia baada ya  Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli kuwaita  Ndg. Mizengo Pinda na Ndg. Makongoro Nyerere waingie ukumbini baada ya kukubaliwa kuwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
   ais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli   akiongoza  Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein akipendekeza majina ya wanachama wa CCM kutoka visiwani wataopigiwa kura kuwa wajumbe Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukumbi wa Kikwete leo Jumatatu Mei 28, 2018 
  Picha na IKULU

  0 0

   Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuletwa Bungeni kesho Jumanne tarehe 29 Mei, 2018 kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake Kasuga, Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma. Awali mapema leo, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson aliahirisha Bunge kutokana na Msiba huo.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama  akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
  Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt. George akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
  Mbunge wa kuteuliwa na Rais Mhe. Salma Kikwete  akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
   Mbunge wa Tarime Mjini , Mhe. Esther Matiko akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
  Waheshimiwa Wabunge wakijipanga kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago. Aliyeketi kusaini ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mhe. Mahmoud Mgimwa.
   Waheshimiwa Wabunge wakijipanga kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.


  PICHA NA BUNGE

  0 0


    Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimkaribisha, Waziri wa Mambo ya Dini wa Saud Arabia, Dkt. Saleh Alashiek (wapili kushoto) na ujumbe wake wakati alipofuturisha kwenye Makazi ya Waziri Mkuu,  Oysterbay jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofuturisha kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam  Mei 27, 2018. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Dini wa Saud Arabia, Dkt. Saleh Alashiek na kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir.
    Baadhi ya waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika futari aliyoiandaa kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Mei 27, 2018. 
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (kushoto) akiagana na baadhi ya wanawake walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Watoto tisa wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wanaondoka leo tarehe 28/5/2018 kwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto wataambata na wauguzi pamoja na wazazi wao.

  Safari hiyo ya matibabu nchini Israel inahusisha watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka 14 imeratibiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini humo. 

  Taasisi yetu inatibu magonjwa mengi ya moyo (kwa asilimia 90) kwa watoto kupitia wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache ambao ni asilimia 10 wanaohitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi kuliko uliopo hapa nchini kwa sasa.

  Tunaushirikiano mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. Aidha tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita na wauguzi wanne ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu. Daktari wetu mmoja na wauguzi wawili bado wanaendelea na masomo nchini humo hii itasaidia kwa siku za mbeleni zaidi ya asalimia 95 ya watoto watatibiwa hapa nchini.

  Hili ni kundi la sita la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH) wa kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 56 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

  Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

  Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo au la. Kupitia kipimo hiki mtoto akigundulika kuwa na tatizo la moyo ataweza kupatiwa matibabu kwa wakati na hivyo kuwa na afya njema kama watoto wengine.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Uhusiano
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
  28/05/2018

  0 0

   Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akimkabidhi futari Mkurugenzi wa Taasisi ya kulea watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu ya Goodwill Sayyed Muhdhar Idarus ambapo futari hiyo ambapo taasisi 10 zilipewa futari hiyo kwa kila taasisi ni Unga wa ngano kg 50, mchele kg 100,unga wa ngano kg 50,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20na majani ya chai kilo 3,Maharage Kg 100 na Unga wa Dona Kg 25 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
   Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katikati akimkabidhi futari mmoja wa walezi wa vituo vinavyolelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Jijini Tanga vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akigawa futari kwa wawakilishi wa vituo mbalimbali na taasisi za kidini tano zilizopo Jijini Tanga wakiwemo Magereza vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
   Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akizungumza katika halfa hiyo baada ya 

  kuwakabidhi kila taasisi Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
   Sehemu ya wakuu na wawakilishi wa taasisi mbalimbali Jijini Tanga wakimsikiliza Waziri Ummy Kabla ya kupokea futari
   Ustadhi wa Madrasa ya Zaharau Ustadhi Abduswamad Muhammad akipiga dua kumshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia Futari hiyo
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akiwa kwenye Picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali mara baada ya kuwakabidhi Futari
   Sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya Futari kwa Taasisi 10 wakiwemo Magareza na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kupitia Taasisi yake ya Odo Ummy Foundation leo amegawa futari kwa taasisi za kiislamu na magereza zilizopo Jijini Tanga vyakula mbalimbali ili viweze kuwasaidia wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani. 

  Vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi futari hizo mapema leo taasisi zenye wanafunzi waliotika maeneo mbalimbali na wakati mwengine wanakuwa hawana uhakika wa kufutari,watu wengine wajitoleza kulea taasisi hizo pamoja na alisema ameona atoe futari hiyo kwa kila taasisi badala ya kuwaita pamoja kufuturu nao maana wengine wanaweza kushindwa kupata fursa ya kuhudhuria lakini wakikabidhiwa wanaweza kuona namna nzuri ya kuweza kuitumia wakati wa mfungo mtukufu wa ramadhani. 

  “Nimeona ni bora nitoe futari hii badala ya kwenda kufuturu kila mahali kwani tutakapofanya hivyo wanaweza kuja wachache na mimi kutokana na kuwa nimetoka kwenye familia ya watu wa kawaida maskini nimeona angalu hicho kidogo ambacho nimejaliwa nitoa kwa taasisi za dini na watoto kwenye mazingira magumu”Alisema. 

  Alisema ameamua kufanya hivyo kwa taassisi za tano zilizo na wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali ambao wamejifunza dini na vituo vinavyolea watoto kwenye mazingira magumu ili wakati huu wa mwezi mtukufu wa ramadhani waweze kutimiza nguo hiyo muhimu ya funga bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile. 

  Hata hivyo alitoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza kusaidia watoto yatima yanaolelewa kwenye vituo mbalimbali na Taasisi za kidini kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani ili waweze kupata uhakika wa kupata mahitaji yao muhimu wakati wa kufuturu. 

  Akizungumza baada ya kupokea futari hiyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Goodwil inayolea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Sayyed Muhdhar alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwapatia msaada huo wa futari ambao utakuwa chachu kuweza kuondoa changamoto ambazo wanakabiliana nazo hasa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani. 

  Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri Ummy sio jambo dogo ni kubwa kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hasa kwenye kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa ramadhani kutokana na mahitaji kuongezeka. “Namuomba mwenyezi Mungu ampe nguvu na kumjalia maisha marefu na pale alipotoa aweze kuongezewa “Alisema (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) umesema watatumia maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Jijini Tanga kuwahamasisha wafanyabiashara kujiunga nao ili waweze kunifaika na huduma za matibabu pindi wanakuwa wakikumbana na magonjwa mbalimbali. 

  Hayo yalisemwa jana na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kwenye ufunguzi wa maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa yanayofanyika eneo la Mwahako mjini hapa. 

  Alisema watakapojiunga nao wataweza kuwa na uhakika wa matibabu wakati wanapougua lakini pia itawawezesha kuepukana na kutumia fedha nyingi pindi wanapokuwa wakiugua zinazotokana na kupanda kwa gharama. 

  “Ndugu zangu maradhi yanakuja bila taarifa hivyo iwapo tutawekeza kujiunga na mpango wa Mfuko huu unaweza kufaidika na matibabu lakini pia utaepukana na gharama kubwa za matibabu utakazopaswa kulipia wakati unapokumbana na magonjwa mbalimbali “Alisema. 

  Hata hivyo Sophia alisema pia wanatumia nafasi hiyo kuendelea kuhamasisha wazazi na walezi kuwapa watoto wao uhakika wa matibabu wanapokuwa wakiugua kwa kuingiza kwenye mpango wa Toto Afya kadi ambao utamuwezesha kupata huduma. 

  “Ndugu zangu lazima tuona namna bora ya kuwapa zawadi nzuri ya matibabu kwenye msimu huu kwa kuwaingiza kwenye mpango wa Toto Afya Kadi kwani hii itawawezesha kupata uhakika wa matibabu pindi wanapoumwa”Alisema. 

  Maonyesho hayo ambayo yalifunguliwa jana na Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage yamebeba kauli mbiu isemayo Biashara ndio ufunguo wa Tanzania ya Viwanda (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).
   Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa barabara 20 Jijini Tanga aliyetembea Banda lao lililopo kwenye maonyesho ya kimataifa ya Biashara 
  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku kushoto akimmkabidhi vipeperusi Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga,Lupakisyo Kapange mara baada ya kutembelea Banda leo
   Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku akisalimiana na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kuwasAili kwenye viwanja vya Mwahako alipokwenda kufungua maonyesho hayo
  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo watumishi wa NHIF Tanga kushoto ni Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga Sophia Kaku kulia ni Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Macrina Clemens
   Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akisalimiana na Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga 
  Huduma za kupima zikiendelea kwenye banda la NHIF

  Sehemu ya wananchi Jijini Tanga wakiingia kwenye banda la NHIF kupata huduma za upimaji wa afya zao na namna ya kujiunga na mfuko huo
   Afisa Mdhibiti Viwango na Ubora Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dkt Lawi Kupaza kushoto akimpima presha mkazi wa Jiji la Tanga wakati alipotembelea banda lao

  0 0

  Na. Atley Kuni na Mathew Kwembe, OR TAMISEMI

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia zoezi la kuwatambua wazee wote nchini katika mikoa yao na wahakikishe kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2018 Mikoa yao inawasilisha Ofisi ya Rais TAMISEMI orodha ya wazee katika mikoa yao.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo, Mhe. Jafo alisema kuwa tayari amekwishatoa maagizo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha kuwa zoezi hilo linashirikisha ngazi zote za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

  Alisema ifikapo tarehe 15 juni 2018 anatarajia kuona kuwa zoezi hilo liwe limekamilika katika ngazi ya kata ambapo Mtendaji wa Kata atapaswa kuliwasilisha katika ngazi ya halmashauri kabla ya kufika ngazi ya Mkoa.

  Pia alisema kuwa ifikapo tarehe 20 Juni, 2018 anatarajia kuwa zoezi hilo liwe limekamilika katika ngazi ya halmashauri ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri atapaswa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji katika ngazi ya mkoa tarehe 26 juni, 2018.

  Waziri Jafo alieleza kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2018 anatarajia kuwa ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa iwasilishe taarifa hiyo katika Ofisi ya Rais TAMISEMI.

  Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa zoezi hilo Mhe.Jafo alisema kuwa serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ya kuwatambua wazee wote nchini ili wasiendelee kupata manyanyaso kwa kukosa utambuzi rasmi.

  Aliongeza kuwa wazee ni tunu ya taifa na hivyo hawana budi kuenziwa kwa serikali kuhakikisha kuwa wanatambuliwa na kupatiwa vitambulisho vitakavyowawezesha kupata huduma muhimu kama vile afya.

  Kwa mujibu wa Waziri Jafo wazee wanaolengwa ni wale wa kuanzia miaka 60 ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 75 ya wazee wote nchini wapo maeneo ya vijijini.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua majengo ya shule ya Chagongwe wakati wa ziaya yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kushoto) wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kumaliza ufunguzi wa majengo ya shule ya sekondari Chagongwe.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chagongwe waliojitokeza kumpokea wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Gairo na vitongoji vyake.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akimsikiliza mmoja ya wazee waliojitolea eneo la shamba lake kwa ajili ya kujenga sekondari ya Chagongwe ambapo alitoa eneo la heka 25.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipewa zawadi ya mbuzi na Diwani wa Kata ya Chagongwe mara baada ya kuwa amemaliza kuwahutubia wananchi.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakionyeshwa eneo la shule ya Nongwe lililovamiwa na wananchi.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua vyoo vya hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakishiriki ngoma wakati wa mapokezi yao katika shule ya sekondari Nongwe.
  Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) akiwasalimia wananchi wa Kijiji Cha Nongwe waliohudhuria katika mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili kijijini kukagua miradi ya maendeleo.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwahutubia wananchi wa Kijijini Nongwe waliohudhuria katika mkutano wa hadhara.
  Burudani ya ngoma ikiendelea.
  Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya kukagua maendeleo katika wilaya ya Gairo. Hapa alikuwa akielekea Kata ya Kata ya Chagongwe.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe)  akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakikagua ubovu wa barabara ya Chagongwe ambayo kwasasa imeharibika kutokana na mvua inayoendelea kunyesha maeneo mbali mbali.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe wakikagua Daraja la Barabara ya Chagongwe-Kumbulu yenye urefu wa Km 34 lililojengwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kulia) wakiongozwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) kukagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa katikati) wakipewa maelezo machache na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) kukagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kulia) wakipewa maelezo machache na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) wakati wakikagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA. Pembeni ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya (aliyejifunika shuka).
  Msafara ukiondoka Darajani.
  Mmoja ya wazazi akitoa elimu ya jinsia kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Chagongwe. 

  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo. 

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameuagiza uongozi wa wilaya ya Gairo na mkoa wetu kwa ujumla kuhakikisha wanafunzi wa shule msingi mpaka sekondani wanapatiwa chakula mashuleni. Kauli hiyo ameitoa wishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika Ufunguzi wa madarasa ya shule ya sekondari Chagongwe katika ziara yake kwa siku ya tatu Wilayani Gairo kukagua miradi ya maendeleo.

   Ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Gairo kujiwekea mpango kazi ili kuwawezesha watoto wote kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari wanapatiwa chakula cha mchana na kuwawezesha waweze kufanya vizuri katika masomo yao. "Watoto wa shule za Morogoro kutokula chakula mashuleni ni aibu, sitaki kabisa kusikia hili suala watoto kunyimwa chakula, naomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo, upitishe azimio kwenye baraza na shule ambayo hawatatoa chakula shuleni wachukuliwe hatua uongozi wa eneo hilo," amesema Dkt. Kebwe.

   "Mkoa wetu unaongozwa kwa uzalishaji wa chakula cha kutosha sasa inakuwaje watoto wetu tuwanyime chakula, tutakosa matokeo mazuri," amesema.Aidha amesema kuwa mtoto anatakiwa kula chakula mara mbili ya mtu mzima, unapomnyima chakula hata ukuaji wake unakuwa hafifu... "Ubongo unatakiwa kupata chakula gram 6 za grucose" Amesema kuwa kukosekana kwa chakula shuleni kumekuwa kukichangia matokeo mabaya kwa wanafunzi bila kujali ni shule ya msingi au sekondari.

   "Tatizo hili tulilizungumza wakati tunafanya tathimini ya mkoa juu ya kushuka kwa elimu na jambo lililojitokeza ni wakafunzi kutopewa chakula kunachangia matokea mabaya" amesema. Alisisitiza kuwa Halmashauri zote zisimamie suala la chakula shuleni ni lazima na wala siyo hiari naomba uongozi usimamie kwa msisistizo mkubwa, kuanzia walimu wakuu, wakuu wa shule atakula nao sahani moja na akiona ni waheshimiwa madiwani ndiyo hawahamasishi atabanana nao mpaka kieleweke. 

  "Mwaka juzi tulikuwa tunashika mkia nafasi ya 23 katika upande wa matokeo ya elimu, ila tokea tulipoanza kubanana vizuri matokeo yameonekana mpaka sasa tupo nafasi ya 11 kitaifa ni jambo linaloleta faraja sana, Kidato cha sita tunaongoza maana tupo nafasi ya pili kitaifa, sekondari tumesogea mpaka namba 14 kitaifa" amesema. 

  Ameongeza kuwa tamko lake hilo lisije kutafsiriwa vibaya kuwa tunawatoza michango ya hela, michango haipo kwa waraka namba 6 umefafanua elimu bila malipo, tatizo lenu wengine wanasema  elimu bure, hakuna elimu ya bure ni elimu bila malipo kwa mzazi ila serikali ndiyo inagharamia. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe amemshukuru Mkuu hiyo kwa kutenga muda wake na kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo na kumhaidi kufanyia kazi changamoto na maelekezo yote aliyoyatoa.

   "Mkuu wa Mkoa tunakushukuru sana kwa kuweza kufika eneo letu na kuona changamoto tulizo nazo tunahidi kuzifanyia kazi na tunakuomba ufikishe salamu zetu pia kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuikumbuka wilaya yetu kwa kutupa hela za maendeleo," Mhe. Siriel amewaomba vingozi wa wilaya ya Gairo kuendeleza upendo na mshikamano walionao ili kuendelea kuwatumikia wananchi vyema.

  0 0

  Wananchi wa Kijiji cha Mawala, Wilaya ya Kilolo Iringa, wakisaidia kutekeleza baadhi ya shughuli za mpango wa matumzi ya ardhi ya kijiji chao.
  Bahati Mwinyimvua mwananchi toka kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero Morogoro. Akichangia hoja kuhusiana na umiliki wa ardhi kwa wanawake
  Ng’eng’enu Mambega katibu wa kamati ya maamuzi kijiji cha Mela, wilaya ya Mvomero Morogoro akibainisha jinsi elimu ya umiliki wa ardhi kwa wanawake ulivyosaidia kuwabadili kifikra na kuwapa wenza wao maeneo wayamiliki. 
  Angolile Rayson Afisa mradi toka Shirika la PELUM Tanzania akichangia mada kuhusiana na mpango wa matumzi ya ardhi.  Jamii kwa sasa imeanza kutambua na kuthamini haki za mwanamke kwenye masuala ya umiliki wa ardhi na hivyo kumpa nafasi zaidi kisheria kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa wanaume. 

  Kuwepo kwa mabadiliko haya chanya kwa baadhi ya jamii imetokana na kusambaa kwa elimu ambayo imekuwa ikitolewa na Shirika la PELUM Tanzania kupitia mradi wa Ushiriki wa wananchi katika kusimamia sekta ya kilimo unaofadhiliwa na watu wa marekani. 

  Angolile Rayson ambaye ni Afisa Mradi amesema vijiji vyote 30 vya mradi ambavyo 27 kati yake toka wilaya sita za Morogoro, Mvomero, Kilolo, Mufundi, Bahi na Kongwa vimefanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi, wananachi wake walikuwa wakiendeleza mila na tamaduni potofu za kuona kuwa mwanamke si sehemu ya familia hivyo hapaswi kumiliki ardhi kwani ataolewa na kwenda kuendeleza ukoo mwingine. 

  Lakini baada ya kufanya mafunzo kwenye vijiji hivyo juu ya haki za mwanamke kumiliki ardhi, jamii imebadilika na sasa mwanamke si tu amekuwa akimilikishwa ardhi peke yake bali pia ana maamuzi nayo kisheria kuitumia kwa shughuli zozote za kiuchumi, kukodisha na hata akiamua kuiuza. 

  “Tunashukuru baada ya kutoa elimu juu ya haki za mwanamke kumiliki ardhi wakati wa kutekeleza mpango wa matumizi ya ardhi, wanaume wengi wamewapa wenza wao maeneo wamiliki kwa majina yao wenyewe na wengine wamemiliki umiliki wa pamoja yaani mke na mume na zaidi ya yote hata watoto wa kike kwenye baadhi ya familia wamepewa maeneo na wazazi wao wamiliki. Shirika kupitia Hamlashauri za wilaya husika tumewapimia maeneo yao na kwa sasa wanasubiri hatimiliki za kimila ili wawe na umiliki halali jambo ambalo sisi kama Shirika tumeona ni sehemu kubwa ya mafanikio.” Alifafanua Angolile 

  Wakielezea wakati wa kufanyika tathimini ya mradi wananchi wa kijiji cha Ikuka Wilaya ya Kilolo, Iringa walibainisha kuwa katika kijiji chao hapakuwa na mazingira mazuri hasa upande wa wanawake na watoto wa kike wanapoomba kupewa ama kurithishwa ardhi kilichokuwa kinafuata ni muhusika kufariki katika mazingira tatanishi hali iliyowafanya wahusishe suala hilo na imani za kiushirikina 

  Kutokana na hali hiyo, wanawake iliwapasa kutokuzungumzia neno ardhi midomoni mwao. Ila baada ya kupata elimu, kwa sasa wanawake wamepimiwa vipande vya ardhi walivyopewa na wenza wao ikiwemo wengine kuwa na umiliki wa pamoja wa mume na mke. 

  “Tunashukuru Shirika la PELUM Tanzania kwa kutupa mafunzo ya haki za ardhi ambayo yamekuwa msaada na hasa kwa wanawake kwani kupitia elimu hii tumefahamu haki zetu kama wanawake kuwa na sisi tunapaswa kumiliki ardhi na kuwa na maamuzi nayo kisheria. Kwenye kijiji chetu kwa sasa wapo wanawake wamepima ardhi zao mmoja mmoja na wengine wanatarajia kuwa na umiliki wa mume na mke kama mimi na sasa tunasubiri ugawaji wa hatimiliki.”Bahati Mwinyimvua Mwananchi kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero, Morogoro. 

  Ng’eng’enu Mambega yeye ni katibu kamati ya maamuzi kijiji cha Mela, wilaya ya Mvomero Morogoro anasema baada ya kupata elimu ya masuala ya ardhi kwa sasa si tu wamewapa maeneo wenza wao wayamiliki ambao yameshapimwa kupitia mradi ila pia wanawashirikisha mambo mbalimbali wenza wao na kuwaruhusu kufanya maamuzi jambo ambalo halikuwa likifanyika kweye tamaduni za kimasai. 

  “ Zamani tulikuwa tunawathamini na kuwarithisha watoto wa kiume ardhi hata kama mzee kafariki kijana ndio anakuwa mwenye sauti lakini kwa sasa mambo yamebadiliki mama naye ana haki zake kwenye eneo la mume wake na vijana wa kike pia tumewapa maeneo wayamiliki wenyewe.” Alifafanua Mambega 

  Kwa upande wake Zaveria Mdendemi toka kijiji cha Makungu, Wilaya ya Mufindi Iringa anasema, kutokana na mila potofu kuwa mwanaume ama mtoto wa kiume pekee ndio anapaswa kumiliki ardhi, jambo lilimletea mgogoro na mtoto wake wa kwanza wa kiume ambaye alitaka kumpokonywa mali zote ikiwemo ardhi aliyoachiwa na marehemu mume wake lakini kupitia elimu aliyoipata, alimpeleka kwa mwenyekiti wa kijiji akaeleimishwa na hatimaye akamuachia mama yake mali zote akisubiri maamuzi ya mama juu ya mali hizo. 

  “Nashukuru mradi huu kutoa kipamumbe kwa wajane kupimiwa maeneo yao, kwani mila na desturi ambazo tumezikuta mwanamke amekuwa akinyimwa nafasi kumiliki mali yoyote na hasa sisi wajane pindi mume anapofariki tumekuwa tukifukuzwa kwenye nyumba tulizojenga na wenza wetu na kupokonywa mali zote wakati mwingine hadi watoto ama uachiwe watoto bila mali yoyote. Lakini kwa sasa elimu imewezesha jamii kutambua thamani ya mwanamke kumiliki ardhi na hivyo tumefanikiwa kupimiwa maeneo yaliyobaki mikononi mwetu”. Rosemary Ulanga mwananchi kijiji cha Ibugule, wilya ya Bahi Dododma. 

  Kupitia upimaji huo wa ardhi kwenye vijiji 27, Shirika la PELUM Tanzania linatarajia kutoa hatimiliki za kimila zipatazo 4000 kwa makundi ya wazee, wajane, wagane, watu wenye ulemavu na wa kipato cha chini

  0 0

  Wataalamu 16 toka Halmashauri za Wilaya ya Morogoro, Mvomero, Bahi, Kongwa, Kilolo na Mufindi walio chini ya Idara ya Ardhi, maliasili na mazingira wamejengewa uwezo juu ya utumiaji wa mfumo mpya na rahisi wa upimaji ardhi unaofahamika kwa jina la MAST (Mobile Application for secure tenure).

  Akiongea Mkoani Iringa wakati wa ufunguzi wa ziara hiyo ya mafunzo iliyoandaliwa na Shirika la PELUM Tanzania, Donati Senzia Mratibu wa PELUM alisema lengo hasa la ziara hiyo ni kuwapatia elimu wataalamu hao na kuona ni jinsi gani wataweza kuutumia mfumo huo kwenye Halmashauri zao kupitia miradi ya upimaji ardhi ambayo watakuwa nayo. 

  Akifafanua jinsi mfumo huo unavyofanya kazi, Mustapha Issa ambaye ni Mkurugenzi msimamizi wa shughuli za miradi USAID LTA-Iringa, alisema kuwa mfumo huu ulitengenezwa kwa ajili ya uhakiki wa maslahi na upimaji wa vipande vya ardhi ambao hutumia simu za kisasa. 

  Alisema mbali na kuwa mfumo huu kutoa ajira kwa vijana wengi kama wapimaji wasaidizi baada ya kupatiwa mafunzo jinsi ya kuutumia lakini pia mfumo huu ni rahisi na hautumii muda mwingi kuanzia kwenye zoezi la upimaji, uchukuaji taarifa, utunzaji taarifa hadi kufikia hatua ya kutoa hatimiliki. 

  Halikadhalika mchoro unajichora wenyewe moja kwa moja wakati wa upimaji kipande, upigaji wa picha hufanyika na kuhifadhiwa kwenye mfumo mara tu baada ya mpimaji kujiridhisha na taarifa ya mteja wake na wakati huohuo taariza zote za mmiliki wa kipande husika zinachukuliwa na kuhifadhiwa na mfumo kwa ajili ya kukamilisha zoezi la utoaji wa hatimiliki. 

  Akielezea utofauti alioubaini kwenye kipimo hiki cha MAST, Fred Mgeni Afisa Mipango miji na vijiji Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Iringa anasema mbali na mfumo huu wa MAST kuchora mchoro wa kipande kilichopimwa (umbo) moja kwa moja tofauti na kipimo kinachotumika sasa, tofauti nyingine iliyopo ni kuwa kipimo cha sasa kina mapungufu ya uhakiki kuanzia mita 1-10 jambo ambalo halitakiwi na inashauriwa walau mapungufu hayo yasizidi mita 1-3. 

  “Kupitia ziara hii ya mafunzo nimegundua sisi kama PELUM Tanzania tungeweza kupima zaidi ya vijiji 28 na kuvuka lengo la mradi na kugawa hatimiliki mapema zaidi kwa kila kijiji tunachomaliza kupima kwani kwa kupitia mfumo huu, jumla ya hatimiliki 200 hudurufiwa kwa siku kwa kuwa kila taarifa inakuwa ndani ya mfumo hakuna uhamishaji wa taarifa mara mbilimbili na zitatunzwa kwa ufasaha zaidi”. Angolile Rayson Afisa Mradi toka PELUM Tanzania 

  Naye Bernard Kajembe Afisa Mipango Miji na vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Iringa anasema, pamoja na kuwa mfumo wa MAST kuwa rahisi wakati wa utekelezaji wa shughuli za upimaji vipande, uingizaji wa taarifa hadi uandaaji wa hatimiliki lakini pia ananashauri kuwa, 

  “Ni vyema kuhakikisha kila mtaalamu toka Halmashauri husika anayehusika kwenye zoezi la upimaji wa vipande vya ardhi awe anahakiki taarifa zake muhimu kabla ya kutoa hatimiliki ili kusiwepo muingiliano wa taarifa ambazo zinaweza kuchangia kutokea kwa migogoro ya ardhi kati ya wanawanachi wenyewe ama wananchi na serikali kwa kutumia maeneo yaliyetengwa na Serikali kwa matumizi mengine”. 

  Georgina Kallaghe afisa ardhi toka Wilaya ya Bahi anasema, mbali na mfumo huu kurahisisha upachikaji wa picha ya muhusika moja kwa moja kwenye taarifa zake tofauti na mfumo wa sasa ambao unaleta mvurugano kutambua picha sahihi ya muhusika na hasa zikikaa muda mrefu na wakati mwingine kuchangia fomu zilizojazwa taarifa za mteja kupotea ama kuliwa na panya pindi wanaporudishiwa kufanya uhakiki wa taarifa zao muhimu 

  Lakini pia anasema mfumo huu unaweza kutumiwa na mtu yeyote yule na hasa upande wa uchukuaji jira kwani mchoro hujichora wenyewe tofauti na ilivyo sasa hadi umsubiri ama kumtafuta Afisa mipango miji ama mpima ardhi achore mchoro husika 

  Kwa upande wake Andrea Biashara afisa mipango miji na vijiji Halmashauri ya Morogoro amesema, utofauti aliouona ambao nao pia unatumia gharama ndogo ni kudurufu hatimiliki kwa kutoa picha ya muhisika bila rangi jambo ambalo ameshauriana na kamishina wa ardhi wa vijiji pamoja na wataalamu wengine toka Wizarani ili kuendelea kufanya hivyo kama sehemu ya kuwezesha hati nyingi kutolewa kwani gharama ya wino wa rangi kwa mashine kubwa inayotoa hati nyingi inafika hadi milioni sita jambo ambalo halmashauri nyingi haziwezi kulileba. 

  Mbali na kufanikiwa kutengeneza hatimiliki 40,000 kwenye vijiji 28 vya mradi ndani ya miaka miwili, Mustapha Issa ambaye ni Mkurugenzi msimamizi wa shughuli za miradi USAID LTA-Iringa alisema lengo lao kuu ni kuhakikisha mfumo huu unatumika nchi nzima kwani wameshatoa elimu hii kwenye Halmashauri nane nchini, Wizara ya ardhi maendeleo na mkazi, Tume ya Taifa ya usimamizi wa mipango ya matumizi bora ya ardhi, Chuo kikuu cha ardhi pamoja na mashirika binasfi manne. 

  Mustapha Issa  Mkurugenzi msimamizi wa shughuli za miradi USAID LTA-Iringa, akielezea jinsi mfumo wa MAST unaotumia simu za kisasa  unavyofanya kazi wakati wa upimaji wa vipande vya ardhi.
     Sadoth Kyaruzi Afisa Mpango miji na vijiji halmashauri ya Mvomero, Morogoro akichangia jambo wakati wa mafunzo ya MAST.
   Timu ya wataalamu toka Halmashauri za wilaya sita, Morogoro, Mvomero, Kilolo, Mufindi, Bahi na Kongwa. Wawakilishi toka masharika wanachama (INADES na UMADEP) pamoja na maafisa mradi wa PELUM Tanzania wakipewa maelezo na mmoja wa vijana waliopewa mafunzo juu ya utumiaji wa mfumo wa MAST.
   Timu ikichukua alama za shamba la mwananchi (wakiongozwa na mmiliki wa shamba) ili kuweza kupata mchoro kamili na ukubwa wa shamba husika
   Timu ikikagua mchoro wa shamba husika kupitia mipaka/alama walizokuwa wakionyeshwa na mwenye shamba
  Mmoja wa washiriki baada ya kukagua taarifa za wateja akihoji kutaka kufahamu nini hufanyika baada ya kukuta taarifa ya mteja imekosewa na hasa kama mtu alipima eneo lisilo lake ama lina mgogoro wa ardhi.

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili umeagwa leo jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ameongoza mamia ya waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo, Mbowe amesema mwili wa Bilago utapumzishwa kwenye nyumba yeke ya milele Alhamisi wiki hii mkoani Kigoma na kesho wabunge watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho mkoani Dodoma.

  Kuhusu ratiba ya mazishi Mbowe amesema wamekaa kikao na familia na kukubaliana mwili wa marehemu Bilago upumzishwe Almasi ili kutoa nafasi ya wananchi wa jimbo lake kumuaga na kutoa heshima zao za mwisho.Amefafanua wamekubaliana na ombi la Paroko wa Kakonko la kutaka marehemu Bilago ibada ya kumuaga ifanyike Kanisani lakini akaeleza Chadema imeamua Jumatano aagwe katika viwanja vya wazi na kisha siku inayoafuata(Alhamisi) ndio itakuwa kanisani.

  Akizungumzia taarifa za kifo cha mbunge huyo amesema alifariki dunia Jumamosi mchana siku ya Jumamosi wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili na taarifa za kuumwa kwake alizipata akiwa nchini Afrika Kusini.Hivyo aliagiza wabunge na viongozi wengine wa Chadema kufanya jitihada za kuhakikisha anapata matibabu.

  "Akiwa hospitali ya Muhimbili alinitumia ujumbe kupitia simu yangu ya mkononi akinieleza kuwa anaumwa sana na akahitaji nije kumuona.Lakini wakati ananitumia ujumbe huo sikuwepo nchini."Hivyo niliporudi nikaenda kumuona hospitali na tukawa na mpango wa kumpeleka nje kwa matibabu lakini ilipofika Jumamosi akafariki dunia,"amesema Mbowe na kuongeza Chadema imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Mbunge wao makini na ni pigo kwa familia.

  Awali akizungumza mbele ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wa marehemu Bilago, Paroko wa Parokia ya Magomeni jijini Dar es Salaam Christan Nyumayo amesema enzi za uhai wake kiongozi huyo alikuwa ameweka maisha yake kwenye imani ya dini yake na hata Parokia ya Kakonko imethibitisha hilo na ndio maana inataka lazima ibada yake ikafanyike ndani ya Kanisa.

  Pia amesema maisha yake aliyandaa akiwa hai na ndio maana leo hii anaagwa kwa heshima kubwa ,hivyo ametoa rai kwa walio hai kuhakikusha wanatenda mema na kuandaa maisha yao ya baadae."Ukiwa kibaka katika uhai wao kuna uwezekano mkubwa wa kuzikwa na vibaka wenzako na ukiwa mcha Mungu basi utazikwa na wacha Mungu.Hivyo tunachoshuhudia leo hii ndugu yetu 

  amepata heshima ya kuagwa katika mazingira ya utulivu na unyenyekevu kwasababu aliishi maisha ya kumpendeza Mungu.Nilipopata taarifa za kutakiwa kuja hapa sikuwa na shaka ya aina yoyote,"amesema Paroko Nyumayo.
  Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ,ukiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa mapema leo mchana jijini Dar.
  Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema),ukiingizwa ndani ya ukumi wa Karimjee,mapema leo mchana tayari kwa kuagwa na waombolezaji mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa chama cha CHADEMA.
  Baadhi ya viongozi waandamizi wa chama cha CHADEMA,wakiwa ndanni ya ukumbi wa Karimjee tayari kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa bunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .

  Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,tayari kwa kutokewa heshima za mwisho na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho pamoja na waombolezaji wengine.
  Baadhi ya waombolezaji wakishiri sala ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
  Baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA na baadhi ya waombolezaji wakishiriki sala ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
  Baadhi ya waombolezaji wakishiri sala ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
  Baadhi ya Waandishi wa habari wakirekodi tukio la kuwasili mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili

  0 0


   Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akiswalisha viongozi na waalikwa mbalimbali swala ya Magharibi kabla ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ally  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wageni wake wakiingia ukumbinini kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
   Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akipakua futari akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
   Mawaziri Wakuu Wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Sinde Warioba na waalikwa wengine wakichukua futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na wageni mbalimbali kuchukua futari aliyowaandalia 
  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  
   Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akiwa na Jaji Mkuu Profesa Inbrahim Juma na  Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe wakichukua futari

   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) akifuatiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro, Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) na wageni wengine wakichukua futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018   
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Janeth Magufuri, Mama Mary Majaliwa, Mama Anna Mkapa na Mama Khadija Mwinyi wakiongea baada ya kupata  futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  
   Kamishna  Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akiwa na Mama Evelyn Warioba wakiwa katika futari hiyo
   Waalimwa wakibadilishana mawazo baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubery mara baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa masuala ya Dini kutoka Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na  Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula kwenye futari aliyoandaa
  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa amekaa  na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wa pili kutoka kulia, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na viongozi na wageni mbalimbali walioshiriki Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi walioshiriki katika futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
     Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
     Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
     Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
     Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Janeth Magufuri, Mama Mary Majaliwa, Mama Anna Mkapa na Mama Khadija Mwinyi wakati wa  futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  
     Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
     Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
     Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
     Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt, Magufuli baada ya futari
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa pamoja na viongozi na waalikwa wengine wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt, Magufuli baada ya futari
  Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa hotuba  Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek bada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa hotuba  Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek bada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
   Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Ghalib Bilali baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana ujumbe kutoka Saudi Arabia mara baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangwalla baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na IGP Simon Sirro baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na vingozi mbalimbali baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana wakitoka ukumbini baada ya futari.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na  Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinsi Jenerali Venance Mabeyo baada ya futari
   Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangwalla akiongea na wakuu wa wilaya za Kinondoni, Mhe. Ally Hapi, Temeke Mhe. Felix Lyaniva na wa Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa baada ya kufuturu
   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya futari
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim. Nyuma yake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba baada ya kufuturu
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na IGP Simon Sirro  baada ya kufuturu
   Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana akiongea na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa na IGP Simon Sirro
   Mawaziri wakuu wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Sinde Warioba na wake zao Mama Evelyn Warioba na Mama Amne Salim
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameongozana na Mama Janeth Magufuli na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na IGP Simon Sirro
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt.  Mohamed Ghalib Bilali
   Mama Janeth Magufuli akiwa na Mama Mary Majaliwa na Mama Asha Bilali na Mama Zakia Bilali
   Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula
   Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
   Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
   Mama Janeth Magufuli akiongea na Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Shehe Mkuu wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Amne Salim 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulsiha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma  kwa Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.  Zuberi Ali Maulid baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.
  Picha na IKULU


  0 0

  AMREF YAISHUKURU SERIKALI KUAMINI UTENDAJI WAO
   Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu (aliyekaa kushoto), akisaini mkataba wa kufanya kazi pamoja na Tayoa. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tayoa, Peter Masika. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Bodi ya Uratibu ya Miradi ya Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu inayofadhiliwa na mfuko wa dunia Dr. Rachae Makunde.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Services (THPS), Redemputa Mbatia, akipeana mkono na Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu baada ya kusaini mkataba huo.
   Wadau wa masuala ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile, akihutubia kwenye uzinduzi huo.
   Emiliani Busara kutoka MDH, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
   Mchungaji Basilisa Ndonde akizungumza kwenye uzinduzi huo.
   Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu (aliyekaa kushoto), akisaini mkataba wa kufanya kazi pamoja na MDH. Kulia ni Emiliani Busara kutoka MDH.
   Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu, akihutubia kwenye uzinduzi huo.
    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akiwa na viongozi wengine katika uzinduzi huo.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tayoa, Peter Masika (kulia), akipeana mkono na Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu baada ya kusaini mkataba huo.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tayoa,, Peter Masika, akihutubia.
   Mkurugenzi wa Bodi ya Uratibu ya Miradi ya Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu inayofadhiliwa na mfuko wa dunia Dr. Rachae Makunde ,  akizungumza kwenye uzinduzi huo.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mkapa Foundition, Rahel Sheiza (kulia),  akipeana mkono na Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu baada ya kuisaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja.

  Na Dotto Mwaibale

  MKURUGENZI Mkazi wa Amref nchini Tanzania, Florence Temu ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na zilizopita kwa ushirikiano inayotoa kwao.

  Temu alitoa shukurani hizo kwenye uzinduzi wa mradi wa Amref Health Africa wa kupambana na Ukimwi na Kifua Kikuu unaofadhiliwa na Mfuko wa Dunia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Kwenye uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Dr.  Faustine Ndugulile walihudhuria pia Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri  wa Amref Tanzania, Dr. Eric Van Praag, Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Ukimwi (UNAIDS), Dr. Leo Zekeng  na viongozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali  yaliyopewa dhamana ya kusimamia mpango wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ili kufikia asilimia 90 ya  waishiyo na   VVU kupatiwa tiba na asilimia 90 ya walio kwenye tiba za VVU 90 wafanikiwe kufubaza VVU.

  Temu alisema kuwa, baada ya kupitia michakato ya kutambua asasi itakayochukua jukumu la 'Principle Recipient' katika mkondo wa taasisi zisizokuwa za serikali, mwanzoni mwa mwaka jana, Amref Health Africa Tanzania ilihidhinishwa rasmi na hatimaye Februari 21 walisaini kama Principle Recipient wa mkondo wa taasisi zisizo za serikali Mfuko wa Dunia wa Fedha zenye thamani ya Bilioni 55 na milioni 256 na laki 7 (yaani $24,969,174) kwa ajili ya kuibua na kutibia VVU na Kifua Kikuu, wakikabidhiwa jukumu la kusimamia na kuratibu afua za kwenye jamii zihusuzo Ukimwi na Kifua Kikuu kwa kupitia asasi ya kijamii, takriban asilimia 10% ya fedha hizo zitaelekezwa katika afua za kukabiliana na Kifua Kikuu katika jamii.

  Aliongeza kuwa, kwenye mapambano ya maradhi hayo wataifikia mikoa 15 ambayo ni Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Simiyu, Singida,Tanga na Ruvuma.

  "Tunatarajia kupitia mfuko huu jumla ya watu 546,880 watafikiwa na huduma ya kupima VVU na kujua majibu, pia wasichana wa umri rika/ balehe na wanawake 162,064. Lakini pia kuibua na kuwapa rufaa wenye maambukizi ya kifua kikuu wapatao 16,465 watapata uchambuzi zaidi kwenye uwakilishi utakaofuata," alisema Temu.

  Aliongeza kuwa, Amref inathamini kwa dhati jukumu walilopewa la kuratibu na kuongoza mradi huo uliofadhiliwa na Global Fund kwa miaka mitatu ijayo na kuahidi kufuata muongozo stahiki uliopo katika kutekeleza mradi huo, kwa dhana hiyo wanaahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau husika kadiri watakavyoweza.

  "Tutashirikiana moja kwa moja kama Amref lakini pia kwa kuwatumia sub recipients wetu ambao ningependa muwatambue," alisema Temu na kuwataja kuwa ni Tanzania Health Promotion Services (THPS), Management and Development fo Health (MDH), Benjamin Mkapa Foundition (BMF) na Tanzania Youth Alliance (TAYOA).
  Aliongeza kuwa, wanatambua changamoto zilizopo katika kufikia jamii  hasa kwenye malengo ya kuwafikia wanaopaswa kujua hali yao ya maambukizi, ambapo kulingana na takwimu za Tanzania HIV Impact Survey ambao ni asilimia 52.2% ya walio na umri wa miaka 15-64 tu ndiyo wamepima na kujua hali zao za maambukizi; na uhaba wa wanaume kufikia huduma hizo, pia kuwepo kwa makundi yenye mazingira hatarishi zaidi ya kuambukizwa na kuambukiza VVU, pia haja ya kuibua wenye kifua kikuu na kuhudumia wenye TB sugu katika jamii, hizo ni baadhi tu!

  Temu alisema wanatambua juhudi za Serikali ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha anafikia asilimia hizo 90 tatu na nia ya kutokomeza kifua kikuu na kudhibiti maambukizi na kupeleka huduma hizo katika ngazi za jamii kuimarisha mifumo ya usambazi dawa na vifaa tiba, kusomesha wataalam, kuboresha vituo vya afya na hospitali na mifumo ya rufaa ni juhudi za wazi na wanaipongeza wizara ya afya inayoongozwa na Waziri Ummy Mwalimu akishirikiana kwa karibu na naibu wake Dr. Faustine Ndugulile.

  "Mfano nichomekee kidogo hapo jinsi Amref kwa kupitia brand ya Angaza tulivyoweza kuleta huduma rafiki za upimaji wa VVU ulivyoweza kuifikia jamii ya rika zote na jinsi zote na hata kuwa huduma rafiki kwa jinsi za kiume yaani wanaume, tunashauri serikali iendelee kutumia hiyo brand kwani tunaamini neno Angaza ni rafiki na linaondoa hofu na linaleta ujasiri hata kwa wanaokuwa na VVU," alisema Temu.

  Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, wanashukuru uthubutu wa wataalam wa wizara ya afya kuweza kuongeza wapimaji wa VVU kutoka kwa wataalam wa maabara hadi wahudumu wa afya walio wa maabara.

  Alimalizia kwa kusema, wao Amref na wadau  wakiwemo SRs, wataendelea kufanya kazi kwa karibu na kufuata miongozo ya Global Fund, Sera na mitakati ya kitaifa, maelekezo ya vikao mbalimbali vya TNCM na hata kusimamia matumizi ya fedha za ufadhili huo na kutumia vyombo vilivyopo katika kutafuta ushauri ikiwemo wizara ya afya na vitengo vyake ambavyo ni Sekretariet ya TNCM,lfa PR-1 (Wizara ya Fedha) na Programme za NACP na NTLP pamoja na GF Office ya Wizara ya Afya.

  Naye Dr. Ndugulile akizungumza katika uzinduzi huo, aliishukuru Amref na wadau wengine waliopewa jukumu la kupambana na maradhi ya kifua kikuu pamoja na Ukimwi ambao ni THPS, MDH, BMF na TAYOA.

  Naibu waziri huyo aliwataka wote kuwa wabunifu na wenye mikakati ili kufikia malengo ya  kupambana na maradhi hayo kama walivyoyaanisha kwenye mchanganuo wa bajeti waliyoomba.

  Alisema milango ipo wazi kwa wao kufika ofisini kwao kwa lengo la kuhitaji ushauri wowote watakaouhitaji.  0 0


older | 1 | .... | 1588 | 1589 | (Page 1590) | 1591 | 1592 | .... | 1897 | newer