Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WAZIRI JAFO AKERWA NA UJENZI MBOVU WA MADARASA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa maagizo kwa Mkandarasi SUMA JKT baada ya kukagua ujenzi wa madarasa manne LEO yaliyojengwa katika shule ya Sekondari ya Hombolo, Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akikagua ujenzi wa sakafu wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Hombolo, Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Hombolo leo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne katika shule hiyo. 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Hombolo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo alipotembelea shule hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Suma JKT kuhakikisha madarasa yaliyojengwa katika shule ya Sekondari ya Hombolo Jijini Dodoma yanawekewa madawati kwa gharama ya shilingi milioni 20 .

Ameyasema hayo wakati alipokagua shule hiyo leo kuona maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne yaliyojengwa kwa kutumia “FORCE ACCOUNT “ambapo alibaini uduni mkubwa katika ujenzi wa madarasa hayo.

Mhe. Jafo amesema inashangaza kuona maeneo mengine wametumia fedha zilizotolewa na Serikali kujenga madarasa pamoja na kuweka madarasa tofauti na Jiji la Dodoma hivyo ameagiza kuhakikisha wanatumia fedha zilizobaki milioni 20 kwa ajili ya kuweka madawati.“Naagiza, uongozi wa Jiji la Dodoma na SUMA JKT kuhakikisha madarasa yote manne yaliyojengwa kwa fedha za Serikali yamewekwa madawati kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia na kuwa na mazingira mazuri ya kuapata elimu.” Anasema jafo

Mhe. Jafo amefafanua kuwa SUMA JKT wameenda kinyume na matakwa ya Serikali ya kujenga madarasa na kuweka maruru kitendo ambacho kinarudisha nyuma uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kurudisha maendeleo katika jiji la Dodoma.Mhe. Jafo amesema kuwa amekerwa na uhafifu wa zege lililotumika katika ujenzi wa sakafu ya madarasa hayo ambapo mpaka sasa yameanza kuvunjika kabla ya kutumika.Aidha amewataka kurekebisha sakafu hiyo mapema.

“Ninawaagisa kuvunja sakafu ya madarasa na kujenga nyingine, na msinipe mashaka na kuanza kukagua ubora wa majengo yaliyojengwa na kukuta yako chini ya kiwango, nataka madarasa ambayo sakafu yake ni imara na ya kudumu” amesema Jafo.Akifafanua kuhusu matatizo ya maji Mhe. Jafo amesema Serikali imejipanga kutatua kero ya maji nchini na itachimba kisima kitakachotoa maji kwa shule hiyo.

Aidha amewaka wanafuzi hao kunzingatia masomo kwa kusoma kwa bidii na kuwa na kampeni maalum ya kuondoa ziro ili kuondokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne na cha Sita.

RC DKT. KEBWE AAGIZA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI GAIRO WAKAMATWE

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea maelezo ya wizi wa pampu ya maji kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe ili kuweza kuwalejeshea wanachi maji. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema nashangaa kuona pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado wanahujumu miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba Pampu hiyo ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD ufanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane mara moja.
Kisima kilichoibiwa pampu. 
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakielekea kukagua mradi wa maji uliokuwa unasumbua. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakitoa pole kwa wafiwa wilayani katika kijiji cha Tabuhoteli -Gairo wakati wa ziara yake ya siku tatu anayoifanya ili kuchochea maendeleo shughuli za maendeleo wilayani humo. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Tabuhoteli katika kata ya Chigela - Gairo. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa salamu zake kwa wananchi. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Rachel Nyangasi akiwasalimia wananchi wa kata yake. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakiongoza wananchi kuelekea katika mradi wa maji wa Ihenje. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakipokelewa kwa ngoma. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakimsikiliza Mhandisi wa wilaya ya Gairo, Heke Bulugu wakati akitoa maelezo ya 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akitoa neno la shukrani.
 Wananchi waliohudhuria. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Rachel Nyangasi akiwasalimia wananchi wa kata yake. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akizungumza na wananchi. 


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameliagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Gairo kuwatafuta na kuwakamata watu walioharibu miundo mbinu ya maji ikiwemo kuiba pampu ya maji ya Kijiji cha Italagwe katika Wilaya ya Gairo na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.

 Dkt. Kebwe ametoa agizo mapema leo Mei 24 mwaka huu akiwa katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe, wilayani humo wakati wa ziara yake ya siku tatu ya kutembelea na kuhimiza miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro. 

Amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba wananchi wa Wilaya ya Gairo ni pamoja na tatizo la maji, hapati majibu sahihi kuona pamoja na changamoto hiyo bado kuna watu wanaodiliki kufanya hujuma ya kuiba miundo mbinu ya maji na kuwasababishia wengine kukosa maji. "Nashangaa sana kuona pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado wanahujumu miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba Pampu hiyo ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD ufanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane mara moja," amesema.

“OCD Mkong’oto utembee kwenye kijiji hiki. Mkong’oto utembee pampu ipatikane. Kuna wengine watachukulia kisiasa siasa suala hili, hiyo ndiyo kazi ya Mbunge kuangalia kwamba tunachangamoto gani asaidiane na wananchi” alisema Dkt. Kebwe “wezi wapo hapa hapa kijijini. DC banana na Afisa Tarafa, Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji, fanyeni Mkutano wa hadhara pampu ipatikane” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, mradi huo wa maji ulianza mwaka 2014 hadi 2015 ambapo uligharimiwa na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahmed Shabiby na ulihudumia vitongoji viwili vya Dukani na Chang’ombe vyenye watu wasiopungua 2,500 na Oktoba mwaka 2017 mradi uposimama kutoa huduma kwa sababu ya pampu hiyo kuibiwa. 

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchemba amewahakikishia wananchi wa Gairo kuwa changamoto ya Maji wilayani humo inakaribia kuisha kwa kuwa takwimu pamoja na utekelezaji unaonesha upatikanaji wa maji unaongezeka. Upatikanaji wa maji mjini umeongezeka kutoka asilimia 35 hadi asilimia 40.7 na vijijini umefikia asilimia 51.4 kati ya asilimia 85 zinazohitajika hivyo mradi wa maji wa MORUWASA utakapokamilika changamoto ya maji Gairo itakuwa ni ndoto.

 "Nawaomba wananchi wangu wa Gairo waendelee kuwa wapole maana kila kukicha tunajaribu kutatua changamoto zinazotukuta likiwemo hili la maji ambalo halitachukua muda mrefu tutakuwa tumelimaliza kabisa," amesema. 

Mhe. Mchembe ameongeza kuwa wanawake wanaweza hivyo waendeee kuwaamini hawatawaangusha wananchi, "Wilaya yetu inaongozwa asilimia 70 inaongozwa na akinamama hivyo tunajua changamoto zinazokuba ikiwemo zile za majumbani.. vumilieni yatakwisha'.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe bado anaendelea na ziara yake Wilayani Gairo kwa lengo la kutembelea na kuhimiza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kupokea kero za wananchi.

Rais Magufuli na Mwenyekiti wa CCM awateua Ndg. Mizengo Pinda na Ndg. Makongoro Nyerere kuwa wajumbe wa NEC

SIMBA WALAMBA SH.MILIONI 100 KUTOKA SPORTPESA KWA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa, Pavel Slavkov, (kushoto) akiwakabidhi hundi ya Sh. milioni 100, viongozi wa Simba na Nahodha wao John Bocco.Kampuni ya SportPesa Limited leo siku Alhamisi tarehe 24 Mei imekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 100 kwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Simba SC.

Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za SportPesa ambao ni wadhamini wakuu wa Wekundu hao wa msimbazi zilizopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, ilihudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili kutoka SportPesa ni Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Pavel Slavkov, Mkurugenzi wa Utwala na Utekelezaji Tarimba Abbas na Mkuu wa kitengo cha Operesheni Luca Neghesti kutoka Simba ni Kaimu Makamu wa Raisi Ndugu Iddi Kajuna, Katibu Mkuu Hamisi Kissiwa.
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas akizungumza jambo kabla ya makabidhiano ya hundi hiyo kufanyika.Msemaji mkuu wa kampuni Haji Manara pamoja na Mjumbe wa kamati ya Usajili Said Tulliy sambamba na wachezaji wote wa kikosi cha Simba wakiongozwa na nahodha John Bocco.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Ndugu Tarimba Abbas alianza kwa kuwapongeza wachezaji na viongozi wa Simba kwa kutwaa ubingwa.“Awali ya yote nianze kwa kuwapongeza viongozi na wachezaji wa Simba SC kwani mmewapa heshima kubwa wana msimbazi kote nchini na kubwa zaidi ni heshima mliyotupa sisi kama wadhamini wenu wakuu.Ndugu Abbas aliendelea kwa kufafanua kuhusu kiasi hicho cha pesa ambacho SportPesa imekabidhi kwa Simba kwa kusema;
“Simba imeitendea haki nembo yetu ya SportPesa na kampuni inaamini kuwa kwa SportPesa kuwa wadhamini wakuu imekuwa ni moja ya chachu iliyosababisha Simba Sports Club kuchukua ubingwa huu”

Tunachokifanya leo ni kutimiza moja ya ahadi tuliyotoa wakati tunasaini mkataba mwezi Mei mwaka jana kuwa tutatoa bonasi ya Shilingi Milioni 100 endapo mojawapo ya timu tunazozidhamini itachukua ubingwa wa Ligi Kuu, hivyo bila shaka timu ni Simba SC”, alihitimisha.Akiongea kwa niaba ya Simba SC, Makamu wa Rais wa mabingwa hao mara 19 wa Tanzania Bara Ndugu Salim Abdallah alianza kwa kuishukuru kampuni ya SportPesa kwa kuwa nao bega kwa bega


“Moja ya jambo ambalo Simba inajivunia msimu huu ni kuwa na mdhamini kama SportPesa ambaye mbali na udhamini, pia tumekuwa tukishirikiana katika shughuli mbalimbali za kiuongozi.
“Tulifanya maandalizi mazuri msimu huu kuanzia kwenye ngazi ya uongozi hadi benchi la ufundi na ndio maana sio jambo la ajabu Simba kuwa bingwa kwani tulishaandaa mikakati kwa kushirikiana na wadhamini wetu, SportPesa.Niwashukuru SportPesa kwa moyo wao wa kuleta mabadiliko ya soka nchini ambayo sisi kama Simba SC tumeyaona kwa upande wetu na tutaendelea kutoa ushrikiano katika miaka mingine minne iliyosalia kwenye mkataba wetu”, alisisitiza Kajuna.

Simba SC ni miongoni mwa timu nne kutoka Tanzania zitakazoshiriki kwenye michuano ya SportPesa Super Cup itakayofanyika nchini Kenya kuanza Juni 3-10 ikishirikisha timu nane kutoka nchi za Tanzania na Kenya.

Timu nyingine ni pamoja na Yanga, Singinda United na JKU kutoka Tanzania sambamba na Gor Mahia, AFC Leopards, Kakamega Home Boys sambamba na Kariobangi Sharks kutoka Kenya ambapo mbali na kujizolea kitita cha Dola 30,000, bingwa wa michuano hiyo ataenda nchini Uingereza kucheza dhidi ya Everton FC kwenye dimba la Goodison Park.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAGENI MBALIMBALI IKULU AKIWEMO RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Ndg. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Mei, 2018
amekutana na kufanya mazungumzo na Wenyekiti watatu wa Jumuiya
za CCM, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Wenyeviti hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Ndg. Edmund
Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg.
Gaudentia Kabaka na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Ndg. Kheri James.
Baada ya mazungumzo hayo viongozi hao wamesema wamekutana na
Ndg. Magufuli na kumueleza kuhusu maendeleo ya Jumuiya zao na kumpa
salamu kutoka kwa Rais wa Afrika Kusini Ndg. Cyril Ramaphosa na Rais wa
Zimbabwe Ndg. Emmerson Mnangagwa pamoja na viongozi wa vyama
tawala vya ANC cha Afrika Kusini na ZANU-PF cha Zimbabwe ambavyo ni
vyama rafiki vya CCM.
“Tumekuja kumueleza ziara yetu ilikuwaje lakini zaidi ya hapo sisi
kama wenyeviti wake wa Jumuiya tumekuja kuzungumza nae ili
tuweze kuendesha jumuiya zetu kwa ufanisi mzuri zaidi” amesema
Ndg. Mndolwa.
“Tumekuja na salamu kutoka kwa Marais wa Afrika Kusini na Zimbabwe,
wanasema wanatuheshimu sana na wanatutegemea sana, pia wametaka
urafiki wa vyama vyetu uendelee” amesema Ndg. Kabaka.
“Tumefikisha salamu za vijana wa CCM kwa vijana wa vyama rafiki
vya ANC na ZANU-PF na kimsingi vijana wa ANC na ZANU-PF wanatambua
mchango mkubwa wa CCM katika kufikisha mataifa yao kwenye mafanikio
makubwa ya uhuru na maendeleo waliyonayo leo” amesema Ndg. Kheri James.
Katika hatua nyingine Ndg. Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu na Mwenyekiti Mstaafu
wa CCM Ndg. Benjamin William Mkapa na Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Ndg. Philip Mangula, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
25 Mei, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa (kushoto) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Philip Mangula Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa (kulia) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Phillip Mangula (kushoto) mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa   Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

TCRA WATOA LESENI KWA WATOA HUDUMA ZA HABARI MTANDAONI

$
0
0

*Mkurugenzi TCRA asema 45 ndio wamekidhi vigezo kati ya waombaji 262
*Asema mchakato bado unaendelea, atoa sababu kuweke gharama za usajili

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
MAMLAKA ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania(TCRA)imesema leo ni siku muhimu katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na kushuhudiwa wadau wa habari wakiwa wamekamilisha hatua za usajili ili watambulike na kutumia fursa hiyo ya utoaji na upashaji habari kupitia mtandao wa intanenti.
Kutokana na kukamilisha mchakato huo TCRA imetoa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao wa intanenti 45 kati ya watoa huduma 262 walioomba na wengine kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa.

Miongoni mwa waliopewa leseni baada ya kukamilisha taratibu hizo ni pamoja na Michuzi Media Group(MMG) inayoendesha Michuzi Blog na Michuzi TV.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba wakati akikabidhi cheti cha usajili kwa wamiliki 45 wa Blogs, Redio na televisheni za mtandaoni na kusema kuwa zipo faida nyingi za habari na utangazaji kwa njia ya mtandao ambazo zinafahamika kwa wengi.
"Kama tunavyofahamu kwa miongo mingi sasa sekta ya habari na utangazaji imekuwa ikipata habari kwa njia ya redio na televisheni kupitia majukwaa mbalimbali kama mitambo iliyojengwa ardhini,Satellite na Cable.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao , iliyofanyika leo  katika ukumbu wa TCRA jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Krants Mwantepele akizungumza kuhusiana na mwitikio ulionyeshwa kwa wamiliki kujisajili TCRA iliyofanyika , jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group (MMG), Ainde Ndanshau katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mkurugenzi wa Blogu ya Wananchi , William Malecela ‘LE MUTUZ ‘ Vkatika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mwakilishi wa  Mtandao wa Bongo 5, Yassin Ng’itu katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mmiliki wa Habari Mseto , Francis Dande katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa  Mmiliki wa Radio Seven ya Mtandaoni,  Atu Mandoza katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.
 Baadhi ya waandishi na wamiliki wa watoa huduma kwa njia ya mtandao

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAO MAKUU HALMASHAURI YA BUMBULIKUJENGWA KWEHANGALA

$
0
0
PICHANI: Ramani ya jengo la Halmashauri ya Bumbuli litakavyokuwa. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Na Yusuph Mussa, Bumbuli
Immamatukio Blog

HATIMAYE Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Bumbuli katika Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ujenzi wake unatarajiwa kuanza mapema Juni, mwaka huu kwenye Kijiji cha Kwehangala katika kata ya Dule B.

Hafla ya utiaji saini kwa ajili ya ujenzi huo umefanyika leo Mei 25, 2018 Ofisi za Halmashauri mjini Bumbuli na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Ameir Shehiza, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali, baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo, watendaji na wananchi pamoja na mkandarasi.

Nyalali alisema siku hiyo ni ya aina yake, kwani ni Mungu pekee amewezesha kufikia muafaka baada ya vikwazo vingi.

"Ni Mungu pekee aliyewezesha siku ya leo kufikia hapa na kushuhudia utiaji saini kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Bumbuli, Kwehangala. Lakini kama sio yeye (Mungu), wengine sisi tungekuwa gerezani. Mtu wa pili kumshukuru ni Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli. Yeye baada ya kubaini hali halisi, aliamua kuturudishia fedha tuendelee na ujenzi.

"Shukrani pia zimuendee Mwenyekiti wa Halmashauri, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, watendaji na wananchi kwa kusaidia jambo hili kufanikiwa" alisema Nyalali.

Awali, Shehiza alimtaka Mkurugenzi Nyalali awathibitishie maslahi ya mkandarasi anaejenga jengo hilo Kampuni ya Advent Construction Ltd ya jijini Dar es Salaam kuwa yatalindwa na kufanya kazi yake kwa wakati. Lakini pia kujua ataanza lini kazi hiyo.

Mkandasi huyo Ashotosh Jog, mbele ya hafla hiyo, aliwahakikishia wananchi wa Bumbuli kuwa kazi hiyo ataifanya ndani ya mwaka mmoja, jengo la ghorofa tatu linalojengwa kwa gharama ya sh. bilioni 2,227,735,123 litakuwa limekamilika, na ujenzi wake anatarajia kuanza mapema Juni, mwaka huu.

Utiaji saini huo umefanyika ikiwa ni baada ya mvutano mkubwa uliochelewesha ujenzi huo kwa takribani miezi mitano, na Rais Dkt. Magufuli kuamua kuondoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo na kutishia kupeleka halmashauri nyingine.

Mvutano huo ulikuwa kati ya Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba na Madiwani wa Halmashauri ya Bumbuli. Mbunge na baadhi ya madiwani walikuwa wanataka Makao Makuu yabaki mjini Bumbuli, huku baadhi ya madiwani akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ameir Shehiza na watendaji akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Peter Nyalali, wakitaka Makao Makuu yawe Kwehangala.

Wakati Makamba na baadhi ya madiwani wakidai kujenga Makao Makuu Kwehangala ni ufujaji wa fedha kwa vile tayari yapo majengo yanatumika kama Makao Makuu ya Halmashauri ya Bumbuli, na fedha hizo zingetumika kupeleka maji, dawa na barabara nzuri kwa wananchi.

Maamuzi ya Baraza la Madiwani, waliamua ujenzi wa Makao Makuu uwe Kwehangala kwa vile ndiyo kwenye eneo kubwa linalofaa kujengwa ofisi za halmashauri na taasisi zake, tofauti na Bumbuli mjini ambapo eneo lake ni finyu, na haliwezi kuwa endelevu kwa vizazi vijavyo.

Mvutano huo uliingia hadi kwenye Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Lushoto (DCC), huku Makamba akipinga mpaka kwenye kikao hicho Makao Makuu kuwa Kwehangala, hivyo maazimio ya agenda hiyo kushindwa kupelekwa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tanga (RCC) ili yaweze kumfikia Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Ndipo Rais Dkt. Magufuli alipoona mvutano huo, akaamua 'kunyofoa' pesa za awali za ujenzi wa ofisi hizo sh. bilioni 1.5 na kusema ngoja kwanza viongozi wa Bumbuli wamalize malumbano yao.

Lakini wiki moja baada ya kauli ya Rais Dkt. Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela, Makamba, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika, Mwenyekiti wa Halmashauri Shehiza na Mkurugenzi wake Nyalali, walikaa kikao cha 'Demokrasia ya Uchumi' na kukubaliana Makao Makuu yajengwe Kwehangala, ndipo Rais Dkt. Magufuli alipowarudishia fedha hizo.

Madiwani wa Halmashauri ya Bumbuli wakishuhudia utiaji saini wa ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Bumbuli yatakayojengwa Kwehangala. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Ameir Shehiza (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali (kulia) wakitia saini mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Bumbuli na Kampuni ya Advent Construction Ltd ya jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ashotosh Jog na mkewe. (Picha na Yusuph Mussa), Immamatukio Blog.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advent Construction Ltd ya jijini Dar es Salaam akiweka saini mkataba wa ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Bumbuli yanayojengwa Kwehangala. Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika Mei 25, 2018 kwenye Ofisi za Halmashauri ya Bumbuli. Kulia ni mke wake. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).Na Yusuph Mussa, Bumbuli
Immamatukio Blog

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM-ZANZIBAR- RAIS WA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Ofisi ya Taifa ya Takwimu Yatoa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Takwimu

$
0
0

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi.  Zamaradi Kawawa akifungua mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji  la Dodoma leo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
2
Mkurugenzi  Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.  Albina Chuwa akisisitiza kuhusu namna idadi ya watu inavyoongezeka au kupungua wakati  wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
3
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Omary Mdoka akiwasilisha mada kuhusu ongezeko la watu  wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
4
Mwanasheria wa Ofisi ya  Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Oscar Mangula akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya takwimu ya mwaka 2015 wakati  wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
5
Mtakwimu  kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi.  Mariam Kitembe akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi hapa nchini kwa kuzingatia utafiti uliofanyika mwaka 2016/2017 wakati  wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
6
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Bw. Said Ameir akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya siku mbili ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la  Dodoma leo.
7
Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu  Bw. Irenius Ruyobya akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la  Dodoma leo.
8
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi.  Zamaradi Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba  ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la  Dodoma leo.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO

………………
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa mafunzo ya uandishi wa habari za kitakwimu kwa wanachama wa chama cha waandishi wa habari Dodoma ili kuwaongezea uwezo wa uandishi mzuri wa habari za kitakwimu.
Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia tarehe 26 hadi 27 Mei, mwaka huu  yanayofanyika katika ukumbi wa Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Jijini Dodoma yamefunguliwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi.  Zamaradi Kawawa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara hiyo.
Akifungua mafunzo hayo Zamaradi Kawawa amesema kutokana na Wizara zote pamoja na baadhi ya Taasisi kuhamia Dodoma, Dodoma imekuwa ndio kitovu cha shughuli za Serikali kwa maana hiyo imekuwa chanzo kikuu cha habari zinazohusu Serikaki nchini hivyo basi majukumu ya vyombo vya habari vilivyopo mkoani Dodoma yameongezeka na yatazidi kuongezeka kadiri shughuli za Kiserikali  zinavyoongezeka.
“Hapana shaka yeyote kuwa watumishi wote wa vyombo vya habari vilivyopo Dodoma wanahitaji mafunzo kama haya kwa ajili ya kuimarisha weledi wao katika kuripoti matukio mbalimbali yanayotokea mkoani humu,” amesema Zamaradi.
Aidha amesema, maisha ya kila siku ya mwanadamu yanahusishwa na takwimu hivyo takwimu ni sehemu muhimu ya maisha ya ulimwengu wa sasa na ndizo zinazotawala namna ya kufikiri na kufanya maamuzi katika maisha tunayoyaishi.
Ametolea mfano wa ubora wa maisha ya watu kuwa unapimwa kwa kutumia takwimu, hali ya uchumi, hali ya biashara, uwekezaji, huduma za usafiri na usafirishaji na hata michezo. Hivyo basi, uandishi wa habari hauwezi kukwepa matumizi ya takwimu.
Hata hivyo ametoa wito kwa NBS kuendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mikoani ambakk hivi sasa kuna redio nyingi za kijamii ambazo zinasikilizwa na Watanzania wengi. Waandishi wa redio hizo wakipata ujuzi wa uandishi wa habari za kitakwimu itasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Kwa upande wake, Meneja wa Takwimu za Kodi wa NBS Fred Matola amesema matarajio ya NBS baada ya mafunzo hayo ni kuwa na waandishi wa habari mahiri kwa Jiji la Dodoma kwa ajili ya kuhabarisha Umma.
“Mafunzo haya yatakuwa tija kwa waandishi wa Dodoma hivyo kuwanufaisha Watanzania wote kupitia habari watakazoandika,” amesema Matola.
Nae, Mratibu wa Mafunzo hayo Said Ameir amesema mafunzo hayo ni ya kipekee, kutokana  na  Serikali kuhamia Dodoma na shughuli nyingi za Serikali kufanyika mkoani humo. Mafunzo hayo ni ya Siku mbili yanashirikisha waandishi wa habari zaidi ya arobaini kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari.

MAJALIWA AHUTUBIA NA KUKABIDHI ZAWADI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI QU- RAAN TUKUFU JIJINI DAR

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kombo Faki Hamadi kutoka Pemba zawadi ya Shilingi milioni 4 baada ya kuibuka  kuwa mshindi wa kwanza wa Juzuu 30 katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu  yaliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 26, 2018. Katikati ni Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama  Tanzania (Istiqaama Muslim Community of Tanzania), Seif Ali Seif.
PMO_1829
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania, Mei 26, 2018.
PMO_1919
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu  yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 26, 2018.
PMO_1963
PMO_1957
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu  yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,Mei 26, 2018.
PMO_2098
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti  wa  Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama  Tanzania ( Istiqaama Muslim Community of Tanzania), Seif Ali Seif katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu  yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,Mei 26, 2018.
PMO_2114
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu  yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 26, 2018.
PMO_2139 PMO_2140 PMO_2179
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na baadhi ya viongozi wa  Taasisi na Jumuiya za Kiislam waliohudhuria katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu  yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,Mei 26, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka waumini wa dini ya Kiislamu wajiepushe na vitendo vinavyoweza kupandikiza chuki dhidi yao au kwa waumini wa dini nyingine.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Mei 26, 2018) wakati akizungumza na viongozi na mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu walioshiriki mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu kwenye ukumbi wa Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama Tanzania (Istiqaama Muslim Community of Tanzania), yalijumuisha washiriki 29 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.

“Serikali inatambua na inathamini sana, mchango wa dini katika kuwalea waumini kiimani na kutunza amani ya nchi. Hivyo, tujiepushe na kauli au vitendo ambavyo vinaweza kupandikiza chuki na uhasama dhidi yetu au dhidi ya waumini wa imani nyingine,” amesema.

“Nitoe rai kwenu viongozi wangu na waumini wenzangu, tujenge misingi ya kuvumiliana na kustahamiliana. Hilo pekee ndilo linaloisimamisha nchi yetu kuwa ni mfano wa kuigwa na kimbilio la wale waliovurugikiwa na amani katika nchi zao. Kadhalika, amani inajenga na kutoa fursa ya kuweza kutekeleza majukumu yetu ya kiibada, kiuchumi na kijamii bila hofu,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa Surah Al-Imraan Ayah 103, Allah Mtukufu alihimiza umuhimu wa umoja miongoni mwa Waislamu. “Katika umoja huo, Allah amesisitiza Waislamu kuwa wamoja na kutofarakana. Mafundisho na wasia wa Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam ni kuwa tupendane na tushikamane. Wakati wote Mtume wetu aliheshimu na kuwathamini watu wote hata ambao hawakuwa Waislamu,” ameongeza.

“Kwa msingi huo, kama Waislamu nasi ni vema tukajipamba na tabia njema za Mtume wetu Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam. Katika hili, mtakubaliana nami kuwa tabia njema ni miongoni mwa makusudio muhimu sana ya kuletwa Mtume Muhammad kwetu,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuwapa elimu watoto kama ambavyo imesisitizwa kwenye Quran tukufu na kama ambavyo imesisitizwa na mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) kwamba suala la kutafuta elimu ni la lazima kwa muislamu, awe mwanaume au mwanamke.

“Kama mnavyofahamu, Uislamu umeweka mkazo mkubwa sambamba na kusisitiza umuhimu wa elimu. Hili linathibitishwa na aya ya kwanza kabisa ya Quran kuteremshwa kwa Bwana Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam (SAW) ambayo ilimuamrisha kusoma (Surah Al-’Alaq ayah 1).”

“Kwa msingi huo, kama ambavyo mnatoa msukumo kwa vijana wetu kusomeshwa Quran, msukumo huo huo muutoe pia katika kuhakikisha kuwa vijana hawa wanapatiwa mafunzo sahihi kuhusu tabia njema, utii na kuheshimu mamlaka za utawala zilizopo. Kwa kufanya hivyo, tutawasaidia vijana hawa kuwa raia wema na wazalendo kwa nchi yao,” amesema.

Amesema Quran licha ya kuwa ni kitabu cha dini lakini kimebeba masuala yote muhimu katika maisha ya muislamu ya kila siku. “Hivyo, ukitaka kuleta maendeleo ya uchumi ulio imara, ukitaka kujenga jamii inayoheshimu na kufuata misingi ya uadilifu, ukitaka kujenga Taifa lenye amani na utulivu, huna budi kuwekeza zaidi katika elimu. Kwa hiyo, uwekezaji katika elimu haumaanishi tu kuhakikisha watoto wetu wanasoma na kuhifadhi Quran pekee, bali pia wanapaswa kupewa fursa ya kujifunza elimu ya mazingira ili waweze kufikia hatua bora za kimaisha duniani na akhera,” amesema.

Kwa upande wake, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubei alisema mashindano hayo yamefana na imeshangaza kuona mtoto anatajiwa namba tu ya aya na anaweza kuielezea kuwa iko kwenye sura fulani.

Kama ambavyo nabii Yahya aliamriwa kushika kitabu, nasi pia tushike kitabu na tuyashike yaliyo ndani yake, tusije kuishi katika ardhi yenye rutuba na yenye rasilmali madini halafu na sisi tushindwe kuvuna kile kilichomo,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiaya ya Istiqaama Tanzania, Sheikh Seif Ally Seif alisema jumuiya hiyo yenye matawi 20 Tanzania Bara na Visiwani, ilianzishwa mwaka 1993 kwa lengo la kutoa mafunzo ya kiroho na kuwajengea vijana maadili mema ili Taifa liwe na watu wenye kujali amani, wanaoheshimiana na kupendana kidugu.

Alisema jumuiya hiyo imejenga shule 14 za msingi na sekondari kwenye maeneo mbalimbali nchini na inatarajia kujenga shule kubwa ya kimataifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kufungua shule ya ufundi.

Katika mashindano hayo, kijana Kombo Fakhi Hamad (19) kutoka Istiqaama Pemba aliibuka mshindi wa jumla kwa kuweza kuhifadhi juzuu 30 na kupewa zawadi ya sh. milioni nne. Kombo pia aliibuka mshindi wa kwanza kwenye kundi la kuhifadhi juzuu 30 (tahfidh) akifuatiwa na Ally Said Mohamad (18) aliyepata sh. milioni mbili. Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mariam Nassor Said (14) aliyepata sh. milioni 1.5.

Katika kundi la kuhifadhi juzuu 30 (tashdia), Masoud Bakari Ally (18) alikuwa mshindi wa kwanza na alipewa zawadi ya sh. milioni moja akifuatiwa na Mustafa Abdallah Hamad (17) aliyepata sh. 700,000 na wa tatu alikuwa Jumaa Ally Othman (16) aliyepata sh. 500,000.

Katika kundi la kuhifadhi juzuu 20, mshindi wa kwanza alikuwa Hilal Khamis Hamad (14) aliyepata sh. milioni 2.5 akifuatiwa na Ally Suleiman Ally (15) aliyepata sh. milioni 1.3 na mshindi wa tatu alikuwa Salim Khamiis Juma (15) aliyepata sh. milioni moja.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, MEI 26, 2018.

MPINA AMWAGA PIKIPIKI KWENYE MINADA YA MIPAKANI

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(mwenye miwani) akikagua moja kati ya pikipiki kumi kabla ya kuzikabidhi ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha na John Mapepele Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akikata utepe kwenye moja kati ya pikipiki kumi kabla ya kuzikabidhi ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha na John Mapepele Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akienesha moja kati ya pikipiki kumi baada ya kuzikabidhi ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha na John Mapepele




Asema zitasaidia kukomesha utoroshaji wa mifugo nje ya nchi




Na John Mapepele

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameagiza maeneo yote ya minada ya awali na upili yapimwe na kuwekwa alama za mipaka katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kuepuka uvamizi unaofanywa na watumiaji wengine wa ardhi.

Maelekezo hayo ameyatoa leo kwenye hafla ya iliyofanyika kwenye Ofisi ya Dar es Salaam wakati akikabidhi pikipiki kumi ili zitumike kwenye mipaka na minada ya upili kwa lengo la kudhibiti utoroshaji wa mifugo na mazao yake nje ya nchi. Alisema Serikali inakusudia kuifunga minada yote iliyoanzishwa kiholela kwa nia ovu ambapo amesema kuendelea kubaki kwa minada hiyo kunadhoofisha minada ambayo imeanzishwa kwa kufuata taratibu za Serikali.

Aidha, Waziri Mpina alisema kuanzia sasa minada yote itaboreshwa na kuwa katika mfumo wa kielektroniki ili kudhibiti mapato ya Serikali kwa njia za kisasa zaidi.“Kuanzia sasa wizara yangu inaingia kwenye mfumo mpya katika kusimamia minada yote ambapo utaiunganisha kwenye mfumo wa kielektroniki” alisisitiza Mpina

Sambamba na hatua hiyo Mpina amemwagiza Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya mifugo Dkt. Mary Mashingo kuhakikisha miundo mbinu ya minada yote inakarabatiwa mara moja na ili kuboresha usimamizi wa sekta ya mifugo nchini.Alisema Wizara inasimamia minada 12 ya upili na 10 ya mipakani ambapo minada ya upili ipo nchi nzima kwa kuzingatia wingi wa mifugo katika eneo husika.

Mpina alisema hapa nchini kuna minada 465 ya awali ambayo huendeshwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM). Aidha, minada ya mipakani imewekwa kuzingatia njia za kusafirishia mifugo kwenda nje ya nchi.

Alitaja minada ya upili na Wilaya ilipo kuwa ni Pugu (Ilala), Kizota (Dodoma), Sekenke (Iramba), Igunga (Igunga), Ipuli (Tabora) na Mhunze (Kishapu). Mingine ni Nyamatala (Misungwi), Meserani (Monduli), Themi (Arumeru), Weruweru (Hai), Korogwe (Korogwe) na Lumecha (Songea). Aidha, minada ya mipakani ni pamoja na Buhigwe (Kasulu), Kasesya (Kalambo), Kileo (Mwanga), Kirumi (Butiama), Longido (Longido) na Waso (Ngorongoro).

Minada mingine ni Mpemba (Momba), Kakonko (Kakonko), Mtukula (Misenyi) na Rusumo (Ngara). Minada itakayokabidhiwa pikipiki hizi ni Muhunze, Sekenke, Ipuli, Korogwe, Weruweru, Lumecha, Kasesya, Murusagamba, Buhigwe na Kirumi.Aliongeza kuwa lengo la kuwepo kwa minada ya mifugo katika maeneo mbalimbali nchini ni kutoa fursa kwa wafugaji na wafanyabishara ya mifugo kuuza mifugo yao kwa faida zaidi kwa kuzingatia ushindani wa soko.

Naye katibu Mkuu Dkt. Mashingo alimshukuru Waziri kwa kuzindua matumizi ya pikipiki hizo na kuahidi kwamba pikipiki hizo zitaleta ufanisi katika utendaji kazi wa minada hapa nchini.Alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe millioni 30.5, Mbuzi millioni 18.8, na Kondoo millioni 5.7. Aidha, Katika mwaka 2017/18 jumla ya ng’ombe 1,614,321, Mbuzi 1,340,222 na Kondoo 315,636 wenye thamani ya shilingi trillioni 1.1 waliuzwa katika Minada mbalimbali hapa nchini.

Dkt Mashingo alisema kutokana na mifugo hii jumla ya tani 679,962 za nyama zimezalishwa ambapo jumla ya tani 1,248.4 za nyama ya mbuzi, tani 1,030.79 za nyama ya ng’ombe, tani 50 za nyama ya kondoo na tani 280 za nyama punda zenye jumla ya thamani ya dola za kimarekani billioni 5.7 ziliuzwa katika nchi mbalimbali.

Alisema matumizi ya minada yanawezesha ukusanyaji wa ushuru na tozo mbalimbali kutokana na biashara ya mifugo hivyo kuchangia katika pato la Taifa na kuiwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake. Uwepo wa minada, hususani ya mipakani unasaidia katika kudhibiti biashara ya magendo hasa utoroshaji wa mifugo kwenda nje ya nchi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Huduma za uzalishaji wa Mifugo, Asimwe Lovince alisema makusanyo ya ushuru na tozo toka minada ya upili na mipakani kwa mwaka 2016/17 yalikuwa 4,775,682,750 ambapo mwaka 2017/18 ni 10,151,124,000 sawa na asilimia 129 ya lengo la makusanyo ya 7,871,000,000/= lililokuwa limepangwa kukusanywa mwaka 2017/18. Hata hivyo kutokana na uzoefu wa zoezi la doria ya Operesheni Nzagamba linaloendelea, imedhihirika kuwa kuna upotevu mkubwa wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali.

“Tunafahamu kuwa Minada yetu imekuwa na changamoto kadhaa zikiwemo za ukosefu na uchakavu wa miundombinu, wataalamu wachache, ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo vyombo vya usafiri, ukosefu wa fedha za kuendeshea minada na maeneo ya minada kuvamiwa na wananchi mfano Pugu mnada wenye hekta 1900 hivi sasa zimebaki hekta 108 tu.

Wizara ina dhamira ya kuhakikisha kuwa changamoto hizi zinatatuliwa ili kuhakikisha kuwa minada inafanya kazi kwa ufanisi. Katika kulitekeleza hilo Wizara imenunua vyombo hivi vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa kazi katika minada. Vyombo hivi pamoja na mambo mengine vitasaidia kufuatilia watu wanaokwepa ushuru kwa kuuza mifugo nje ya minada hivyo kuongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.” Asisitiza Dkt. Mashingo

Alisema Pikipiki hizi aina ya Honda XL 125 toka Japan zilinunuliwa na Wizara kupitia Wakala wa Serikali wa Manunuzi (GPSA) kwa thamani ya Sh 83,000,000/= sawa na Sh 8,300,000/= kila moja.

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA WCF KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI JIJINI MBEYA

$
0
0

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akipeana mikono na mama mjane, Atulehemu Kiduko, ambaye analipwa fidia ya kila mwezi kufuatia kifo cha mumewe wakati akiwa kazini kwenye kiwanda cha karatasi Mgololo kilichoko Mufindi mjini Iringa. mama huyo alitoa ushuhuda wa huduma anayopata kutoka WCF wakati wa kutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijini Mbeya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijinmi Mneya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya


SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, jijini Mbeya leo Mei 26, 2018 wakati akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Mvunde alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Naibu Waziri.

Aidha Mhe. Mavunde alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.

“Pamoja na uchanga wake, Mfuko huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili kwenye mfuko wetu ni 13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga wakiwa kazini wameshalipwa fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni 2.52 kufikia Februari 2018.” Alibainisha.Alisema Mfuko umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia majukumu haya ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao za uzalishaji. 

“Rais wetu wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati tunapokutana kwenye baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi wasaidizi wake, kama kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri kwamba jambo hili bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi mawaziri kuchukua hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na kushauriana na wadau husika ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja na ndio maana leo tuko hapa.” Alifafanua Mhe. Naibu Waziri Mavunde

Wakitoa ushuhuda mbele ya washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga ya kuumia au kufiwa na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo kwani umekuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi.“Mimi nilikatika vidole vya mkono wangu wa kushoto wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kazi kwenye kiwanda cha Lake Cement kinachozalisha saruji ya nyati (Nyati cement) huko Kimbiji jijini Dar es Salaam na WCF imenilipa fidia ya mkupuo ya kiasi cha shilinhgi milioni 11, alisema Bw. Jimmy Samson Malumbo mbele ya Mkutano huo.

Mwingine aliyetoa ushuhuda wa faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi. Atulehemu Kiduko wa huko Mafinga Mkoani Iringa, alisema mumewe ambaye alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha karatasi Mgololo Mufindi Papers baada ya kuangukiwa na gogo wakati akitekeleza majukumu yake. Hivi sasa mama huyo mjane anapokea malipo ya fidia kila mwezi shilingi 110,000/= na watoto wake wawili kila mmoja analipwa shilingi 55,000/= kila mwezi.

“Kwakweli nimefarijika sana kwa malipo haya, ingawa nimeshampoteza mwenzangu, lakini fidia hii ninayolipwa imekuwa ikinisaidia sana katika kuhudumia familia yangu kijijini ikiwa ni pamoja na kumsomesha motto wangu mmoja aliye darasa la tatu.” Alisema Bi. Atulehemu. Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema Mfuko unaendeshwa kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo ina uwakishi wa serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo Shirika la Kazi Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa wafanyakazi.

Alisema, katika mfumo wa zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa na tatizo njiani sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo inaeleza mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au akielekea kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.“Alisema Mfuko umeweka utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa haraka na rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi kifupi.” Alisema.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akizungumza.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji, wa WCF, Bw. Anselkim Peter, akiwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko.
Mkurugenzi wa huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akitoa mada kuhusu namna tathmini inavyofanyika kwa Mfanyakazi aliyepatwa na madhara wakati akitelekeaza wajibu wake wa kazi.
Mwakilishi kutoka chama cha waajiri Tanzania, (ATE), Bi. Patricia Chao, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mbeya, Dkt. Lwitiko Mwakalukwa, akizungumza kwenye mkutano huo.
Washiriki wakipiatia taarifa mbalimbali za WCF.



Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anselim Peter, (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (aliyeipa mgongo camera), wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge
Emiliana Gwagilo, Afisa Matekelezo wa WCF, akiandaa taarifa kwenye meza kuu

Afisa Matekelezo wa WCF, Bw. George Faustin, akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza kutoka kwa washiriki wa mkutano.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF , akibadilkishana mawazo na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, (kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto) na Afisa Matekelezo, Bi. Emiliana Gwagilo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, (katikati)), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, wakiwajibika mwanzoni mwa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, wakiwajibika kwenye mkutano huo.
Naibu waziri Mavunde, akisindikizwa na Bw. Mshomba wakati akiondoka kwenye eneo la mkutano.

CHUO KIKUU ARDHI (ARU) CHATOA ELIMU KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI DAR

$
0
0
CHUO KIKUU ARDHI (ARU) CHATOA ELIMU KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI DAR Chuo Kikuu Ardhi (ARU) kimetoa mwongozo kwa wanafunzi wa shule za Sekondari za jiji la Dar es Salaam, namna wanavyoweza kujiunga na masomo ya elimu ya juu na ufaulu.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Reginald Chetto akiwapa maelezo wanafunzi wa shule ya Sekondari Zanaki waliposhiriki programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Tambaza jijini humo. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Gervas Jonas akiwapa maelezo wanafunzi wa Sekondari walipotembelea banda mojawapo kujionea na kupata ufafanuzi wa programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Msaidizi wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Mbokani Gama akiwapa maelezo wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania waliposhiriki maonesho yaliyoandaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Gervas Jonas akiwapa maelezo wanafunzi wa Sekondari walipotembelea moja ya banda la ARU kujionea na kupata ufafanuzi wa programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Reginald Chetto akiwapa maelezo sehemu ya wageni waliohudhuria maonesho ya ya programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Hadija Maulid akiwapa maelezo wanafunzi wa Sekondari walipotembelea maonesho hayo kujionea na kupata ufafanuzi wa programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Msaidizi wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Mbokani Gama akimpa maelezo mmoja wa wageni alipotembelea maonesho ya programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Sehemu ya wanafunzi wakipitia vipeperushi vya maelezo ya michepuo ya masomo mbalimbali yatolewayo katika Chuo Kikuu Ardhi (ARU) walipotembelea maonesho yaliyoandaliwa na chuo hicho.

Sehemu ya wanafunzi wakijadiliana jambo walipotembelea maonesho ya programu mbalimbali zinazotolewa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU) jijini Dar es Salaam.

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Reginald Chetto akiwapa maelezo sehemu ya wanafunzi wa shule za Sekondari waliposhiriki maonesho kujionea programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho jijini Dar es Salaam

Msaidizi wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Latifa Rashidi akiwapa maelezo wanafunzi wa Sekondari ya Zanaki walipotembelea moja ya banda katika kujionea na kupata ufafanuzi wa programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa Mwandamizi Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Mary Kagosi akiwapa maelezo wanafunzi wa Sekondari walipotembelea moja ya banda la chuo kujionea na kupata ufafanuzi wa programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Hadija Maulid akiwapa maelezo wanafunzi wa Sekondari walipotembelea moja ya banda kupata ufafanuzi wa programu mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Sehemu ya wanafunzi wakijadiliana jambo.

Sehemu ya wanafunzi wakipitia vipeperushi vya maelezo ya michepuo ya masomo mbalimbali yatolewayo katika Chuo Kikuu Ardhi (ARU) walipotembelea maonesho hayo.

DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma ,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala ameagiza kukamatwa watu wote wanajihusisha na unywaji wa pombe za kienyeji nyakati za kazi huku akifafanua ulevi kupita kiasi ni moja ya mambo yanayochangia kukwamisha maendeleo.

Amesema inasikitisha kuona baadhi ya wananchi kunywa asubuhi badala ya kwenda kwenye shughuli za kimaendeleo.

Hali hiyo ilimlazimu Kanali Ndagala kuagiza Ofisa wa Polisi kuwakamata watu wote waliokuwa wanakunywa pombe katika vilabu vya pombe ya kienyeji nyakati za asubuhi. Pia ametoa maagizo ya Mgambo wawili kunyang'anywa vitambulisho vyao katika Kijiji cha Muhange baada ya kuwashuhudia wakinywa pombe asubuhu.

Ametoa maagizo hayo jana alipokwenda kijijini hapo kwa ajili ya kukagua na kuunga mkono shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo hilo.Amesema anasikitishwa kuona watu wana shindwa kufanya shughuli za maendeleo na kuanza kunywa pombe asubuhi na wengi wao wakiwa ni vijana.

"Wakati wenzao wakijitolea katika ujenzi wa shule ya Sekondari ili kutatua changamoto ya wanafunzi wa kata hiyo kutembea umbali mrefu ili kufuata shule ilipo ambapo wananchi wameanza juhudi zao na serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za wananchi,wao wanakwenda kwenye ulevi na hili hatuwezi kulivumilia," amesema.

Aidha Mkuu huyo amewataka wenyeviti wa vijiji vyote kuhakikisha vilabu vya pombe vyote vinafunguliwa kuanzia saa 10 jioni baada ya watu kumaliza kazi zao na wazingatie hilo na kuendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote wanaokiuka sheria hiyo kwani ndio chanzo cha kuwa vibaka na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi na Serikali kwa ujumla.

" Ni aibu sana kuona vijana wadogo ambao mnanguvu za kufanya kazi kuja kunywa pombe asubuhi mnashindwa kufanya kazi.Ofisa wa Polisi hakikisha unawakamata hawa wote wanaokunywa na waliolewa muda wa kazi, sisi tunakuja kuhimiza maendeleo, wao wanaendelea katurudisha nyuma.

" Niwaombe wazazi mkae na watoto wenu muwafundishe na kuwaonya hatuko tayari kuona Wilaya yetu inaendelea kuwa masikini, lazima tuhakikishe watu wanafanya kazi na muda wa kunywa pombe ni jioni, nikiwakuta tena nitawachukulia hatua kali za kisheria," amesema Kanali Ndagala.

Wakati huo huo Kanali Ndagala ameshiriki katika ujenzi wa shule ya sekondali katika kata ya Muhange pamoja na shughuli mbalimbali za maendeleo, ambapo aliahidi kuongeza mifuko kumi ya saruji na kuwahakikishia kuwa Serikali itawapelekea fedha kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo.Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Muhange Ibrahimu Katunzi amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa namna anavyojitahidi kuhimiza maendeleo katika Wilaya hiyo ambayo ilikuwa nyuma kwa kila kitu.

Ambapo amefafanua kwa sasa inaendelea vizuri na miradi mingi inakamilika ikiwa ni pamoja na wananchi kujitolea kwa uaminifu kwa kuamini Serikali ni sikivu.Amesema atahakikisha anahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kufanya kazi ili huduma muhimu zilizokosekana katika Kata hiyo wanafanya kwa ushirikiano kuhakikisha zinapatikana.

Nao baadhi ya wananchi akiwamo Wistoni Jolamu amesema changamoto waliokuwa nayo ni watoto kutembea umbali mrefu kwa miguu na ukizingatia maeneo mengi kuna mapori hali inayo sababisha usalama wa watoto wao kuwa hatarini na wamelazimika kujenga shule hiyo ilikutatua Changamoto hiyo.

Baadhi ya Wananchi waliokamatwa kufuatia unywaji pome asubuhi badala ya kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akijionea mazingira halisi ya unywaji pombe asubuhi subuhi kwa baadhi ya wananchi kwenye moja ya vilabu vyao vya pombe
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wananchi huku akiagiza kukamatwa kwa watu wote wanaojihusisha na unywaji wa pombe za kienyeji nyakati za kazi huku akifafanua ulevi kupita kiasi ni moja ya mambo yanayochangia kukwamisha maendeleo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akishiriki ujenzi na kuunga mkono shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo hilo.Amesema anasikitishwa kuona watu wana shindwa kufanya shughuli za maendeleo na kuanza kunywa pombe asubuhi na wengi wao wakiwa ni vijana.

WAKULIMA KAKONKO WAHIMIZWA KULIMA KILIMO CHA BIASHARA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

WAKULIMA wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wametakiwa kulima kilimo cha biashara na kuachana na kilimo cha kujikimu wenyewe ili kuweza kuondokana na umasikini.

Mwito huo ulitolewa jana katika Kijiji cha Kiga wilayani hapo na Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Kigoma, Josephu Lubuye wakati wa ugawaji wa mashine ya kuchakata Muhogo kwa kikundi cha Mwendo wa saa, iliyo tolewa na Shirika la BTC kupitia mradi wa kilimo wa ENABEL unaotekelezwa na Serikali ya Ubelgiji na Tanzania.

Lengo ni kuendeleza kilimo cha muhogo na maharage kwa kuwakopesha wakulima mashine na kuwapatia mafunzo ya namna ya kulima kitaalamu.

Hivyo Lubuye amesema wakulima wanatakiwa kubadilika na kuanza kilimo cha biashara na mashine hiyo waliyoipata itumike kuchakata mazao mengi ya mihogo waliyolima kutokana na maombi na aandiko lao la kuomba mashine ya kuchakata mihogo.

Amesema hiyo itaongeza uzalishaji wa zao hilo kwa wingi ili wakulima wengine wajifunze kupitia kikundi hicho kutokana na uzalishaji watakaoufanya kupitia mafunzo ya kilimo cha biashara waliyo yapata kuongeza uzalishaji na ubora.

Akikabidhi mashine hiyo yenye thamani ya Sh.milioni mbili na yenye uwezo wa kuzalisha kilo 700 kwa saa moja na hufanya kazi kwa muda wa saa nane, Mkuu wa wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagala amewataka wakulima kuacha kuuza mazao ambayo hayajaongezwa thamani.

Amefafanu kwa kutumia fursa hiyo ya mashine waliyopatiwa itawasaidia kuinua uchumi wao na kulima kitaalamu ilikuongeza uzalishaji.Aidha Mkuu huyo amesema Serikali ya Awamu ya tano ina lengo la kuongeza viwanda na kikundi cha mwendo wa saa wameonesha nia ya uwanzishwaji wa viwanda kwa kuonesha mfano.

Amewataka wananchi wengine kuja kujifunza kupitia vikundi vilivyo fanikiwa na waache maneno ya kuongea na sasa waanze kuanzisha viwanda kwa vitendo ."Niwapongeze wanakikundi wa Mwendo wa saa kwa juhudi mnazozifanya kuhakikisha mnaondokana na umasikini kwa kilimo cha Muhogo, niwaombe wakulima mjitahidi kulima kwa kufuata maelekezo ya wataalamu ilikilimo mtakacho lima kiwe chenye tija kitakacho wasaidia kutoka mahali fulani na kuinua uchumi wenu.

" Serikali imewapatia mashine hii muitumie kuzalisha zaidi masoko yapo na wafadhiri wa mradi huu wameahidi kuwatafutia masoko,hivyo niwaombe muitumie fursa hii na kuwafundisha wengine waige kwenu", amesema Kanali Ndagala. 

Amewahimiza kuwa ili kuwafikia ambao wamefika mbali ni lazima kuongeza kasi ya uzalishaji, na kwa hatua walioifikia kikundi hicho cha kutoka kwenye vikoba na kuingia kwenye Sacoss na kuwa na hekari 16 za muhogo aliwaomba wabadilike kulima kibiashara.

"Achaneni kulima kilimo cha kujikimu ili kuondokana na umasikini,kilimo cha kisasa na kuacha kulima kilimo kisicho na tija na kutumia mbegu bora, kusikiliza wanayo washauri wataalamu wa kilimo na matokeo wameanza kuyaona," amesisitiza.

Kwa upande wake Katibu wa Kikundi cha Mwendo wa saa Daudi Bukuku amesema kikundi kina wanachama 25 ambapo kati yao wanawake 12 na wanaume 13.Ameongeza kikundi kilianza kwa kununua na kukopeshana hisa huondeshwa kwa kuzingatia sheria na kufafanua wanayo mifuko mitatu ya kujiingizia kipato, mfuko wa hisa ambao una kiasi cha Sh. milioni 13, mfuko wa elimu na afya wenye Sh.milioni mbili na mfuko wa faini na zawadi Sh.300,000.

Amesema kikundi kinaendesha shughuli za kilimo kwaajili ya kukuza kipato ambapo kina hekari tano za migomba ya kisasa, hekari 16 za mihogo na hekari mbili za maharage katika vijiji vya kitangaza na mkombozi.Hata hivyo matarajio ya kikundi ni ifikapo mwaka 2021 kiwe na hekari 30 za mihogo na hekari moja moja kwa kila mwanamundi na kikundi kuhama kutoka vikoba na kuwa Sacoss.

Kuhusu changamoto amesema ni ukosefu wa mashamba ya kutosha na masoko pamoja na mafunzo ya mara kwa mara ya kuwaelimisha namna bora ya kilimo.
 Mkuu wa wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagala akikabidhi  mashine  ya kuchakata muhogo,yenye thamani ya Sh.milioni mbili na yenye uwezo wa kuzalisha kilo 700 kwa saa moja.DC Ndagala amekabidhi hiyo mashine ya kuchakata Muhogo kwa kikundi cha Mwendo wa saa, iliyo tolewa na Shirika la BTC kupitia mradi wa kilimo wa ENABEL unaotekelezwa na Serikali ya Ubelgiji na Tanzania.
 Sehemu ya shamba ka Muhogo. 
 Mkuu wa wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagala akitumbukiza muhogo kwenye mashine ya kuchakata muhogo,ili kujionea ufanyaji wake kazi,mashine hiyo ina uwezo wa kuzalisha kilo 700 kwa saa moja.
Mihogo ilioandaliwa tayari kwa kuchakatwa na mashine

RC KIGOMA AWAPONGEZA VIJANA WALIOHITIMU MAFUNZO YA JKT KATIKA KIKOSI CHA KJ 824 KWA AANDIKO LAO LA KUTENGENEZA SABUNI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Kikosi cha KJ 824 Kanembwa wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Amosi Mollo amewapongeza vijana wa oparesheni Melelani walio hitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa( Jkt ) kwa andiko walilolifanyia kazi la utengenezaji wa sabuni ambalo litapelekea kuanzishwa kiwanda cha utengenezaji wa sabuni kikosini hapo.

Akizungumza jana wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa vijana 732 wanaojitolea yaliyofanyika kwa miezi mitano, Mollo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya tano wameandaa mpango wa kuanzisha kiwanda cha sabuni za kufulia.

Pia sabuni za kuogea na kunawia mikono ilikuhakikisha falsafa waliyowafundisha vijana hao ya kujitegemea katika ujasiriamali kwa kuwa vijana hao wamemaliza mafunzo ya awali wataendelea kujifunza stadi za maisha wakiwa kambini hapo.

Amesema anawapongeza vijana hao kwa kujitolea kuandaa andiko la utengenezaji wa sabuni ambalo wameanza kulifanyia kazi na sasa linaingiza pato kwa Jeshi la Kujenga Taifa ambapo ni matokeo mazuri ya kujifunza na kutumia elimu walioipata ya ujasiriamali, uzalendo, kujituma na kujitegemea inayotolewa kambini hapo kuhakikisha wanaondokana na falsafa ya kwamba hakuna ajira jambo ambalo limekuwa wimbo kwa vijana wengi mitaani.

Amesema nje na utengenezaji wa sabuni kikosi hicho kinajihusisha na ukulima wa alizeti, mahindi, kahawa na ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali, ufugaji wa mifugo mbalimbali na utengenezaji wa mafuta ya kupikia ya Alizeti.Amesema lengo ikiwa ni kuwajenga vijana wanaoingia kambini hapo kwa ajili ya mafunzo kuanza kujifunza namna ya ujasiliamali na kujitegemea hata watakapo rudi uraiani wakawe mfano na fundisho kwa vijana wenzao .

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuja kujifunza namna ya ujasiliamali kikosini hapo, na kuwataka vijana walio hitimu mafunzo hayo kutumia mafunzo hayo kulinda amani ya Nchi na kujishughulisha katika shughuli za maendeleo ili kuondokana na umasikini uliopo katika familia zao.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika sherehe hiyo Mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura aliwapongeza wakufunzi wa kikosi hicho kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwanoa wahitimu hayo na kuwataka vijana kuyaishi yale mema yote waliojifunza pamoja na mafunzo waliyo yapata waendelee kuonesha nidhamu na utii watakapo endelea kuwepo kambini hapo.

Aidha alimuomba mkuu wa kikosi kuhakikisha anatafuta soko la kuuza bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wakurugenzi wa halmashauri kununua sabuni za kusafishia vyoo na kunawia mikono katika kambi hiyo ili kuuunga Mkono jitihada za vijana na jeshi la kujenga taifa.

"Ntoe pongezi zangu za dhati kwa wakufunzi wote najua mnafanya kazi katika mazingira magumu lakini kwa uzalendo mlionao mmehakikisha vijana wetu wAnajifunza namna bora ya maisha ikiwa ni pamoja na ujasili, uzalendo wa kujitoa kwa ajili ya Nchi yetu pamoja na ujasiliamali hii ndiyo falsafa tuliyo achiwa na waasisi wetu", alisema Bura.

Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi mmoja wa Wahitimu hao Deogratiusi Mgaya amesema mafunzo hayo yamewajenga kuwa wazalendo na walipoanza mafunzo hayo walianza vijana 739 baadhi ya hao walishindwa kumaliza mafunzo yao kwa sababu ya Kifo cha mwenzao mmoja na utoro wa baadhi na kupelekea idadi ya walio hitimu kuwa 732 ambao wamepata mafunzo hayo ya awali.

Hata hivyo amewaomba wazazi kuwahimiza watoto wao kuingia jeshi la kujenga taifa ili kuwafanya vijana kuwa wazalendo na kuepukana na vitendo viovu pamoja na kujijenga katika kutegemea kujiajiri wenyewe na bila kusubili mpaka Serikali itoe ajira kwao.

NIDA YAPONGEZWA KWA UTENDAJI KAZI UNAOENDANA NA KASI YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Alexander Mnyeti amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) na kusifu jitihada kubwa za Kaimu mkurugenzi Mkuu NIDA ndugu Andrew W. Massawe ambaye ndani ya kipindi kifupi ameweza kuleta mabadiliko makubwa ikiwemo kuongezeka kwa kasi ya kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa.

Hayo ameyasema wakati alipofanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida ofisi kwake; katika ziara ya Mkurugenzi huyo kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu linaloendelea mkoani Manyara.  

Akitoa majumuisho ya maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu linaloendelea mkoani humo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara amesema mpaka sasa zaidi ya wananchi 650,000 wameshasajiliwa katika wilaya zote tano za mkoa wake.

“ Idadi hii ni zaidi ya  asilimia 84 ya makisio ya idadi halisi ya wananchi wenye umri wa miaka 18 wanaotazamiwa kusajiliwa, idadi iliyobaki tumejipanga kukamilisha usajili mwishoni mwa mwezi Juni, 2018” alisisitiza.

Amesema mwitikio wa watu ni mkubwa kutokana na wananchi wengi kutambua umuhimu wa kuwa na Vitambulisho vya Taifa, ambapo mpaka sasa Wilaya ya Hanang’ na Mbulu zimeshamaliza zoezi la Usajili huku wilaya za Babati, Kiteto na Simanjiro zitakamilisha zoezi hilo mwishoni mwa mwezi Juni,2018. Kwa zile Wilaya ambazo usajili umekamilika wananchi ambao hawakusajiliwa watapashwa kwenda makao makuu ya Wilaya hizo kupata huduma.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA amemshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa jitihada zake za kuhakikisha wananchi wa Manyara wanasajiliwa pamoja na kufanikisha Usajili wa wachimbaji wadogo kwenye machimbo ya Tanzanite - Mererani ambapo jumla ya wachimbaji wadogo 10,495 walisajiliwa na kupatiwa Vitambulisho.

Amesema hatua hii imeleta mafanikio makubwa katika kuhakikisha kupitia Kitambulisho cha Taifa, watakaonufaika na Uchimbaji na biashara katika migodi hiyo wanakuwa watanzania hususani katika kipindi hiki ambacho ukuta katika machimbo hayo umekamilika.

Akifafanua mipango ya Mamlaka kwa sasa; Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA amesema moja ya malengo ya ziara yake Manyara ni kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na kuanza kazi kwa vituo vya Uchakataji taarifa ambavyo vitawezesha taarifa za wananchi zilizokusanywa kuhakikiwa na kutumwa kwenye kituo kikuu cha Uzalishaji makao makuu kwa ajili ya hatua za uzalishaji Vitambulisho. Lengo ni kuhakikisha malengo tuliyojiwekea yanakamilika ndani ya wakati.

“ kiujumla nimeridhishwa sana na utendaji katika mkoa wa Manyara; na jinsi Mkuu wa Mkoa na wakuu wa Wilaya walivyojipanga katika kuhakikisha zoezi la Usajili mkoa wa Manyara linakamilika na wananchi wanapata Vitambulisho. Ndiyo maana umeona hata kituo cha kuchakata taarifa kipo kwenye ukumbi karibu kabisa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuonyesha uwepo wa ufuatiliaji wa karibu wa zoezi hili. Kwa hili nimefarijika sana….” alisisitiza

Katika ziara hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA) aliambatana na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho ndugu Alphonce Malibiche, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Joseph na Meneja Mifumo ndugu Edson Guyai ambaye pia ni msimamizi wa usajili mkoa wa Manyara.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Alexander Mnyeti akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Bw. Andrew W. Massawe ofisini kwake
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Alexander Mnyeti akiongea na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Bw. Andrew W. Massawe ofisini kwake
Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu likiendelea Mkoani Manyara ambapo mpaka sasa zaidi ya wananchi 650,000 wameshasajiliwa katika wilaya zote tano za mkoa huo.
Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu likiendelea Mkoani Manyara ambapo mpaka sasa zaidi ya wananchi 650,000 wameshasajiliwa katika wilaya zote tano za mkoa huo.

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM NDG. KINANA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)) Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 27, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 27, 2018

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHUTUBIA NA KUKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AAN TUKUFU AFRIKA UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM, MTANZANIA ASHINDA

$
0
0

*Waziri Mkuu amtaka Sheikh Kishki akaonane na 
Waziri wa Ardhi atoe maamuzi ya kiwanja
          
KIJANA wa Kitanzania, Shujaa Suleiman Shujaa ameibuka kidedea na kunyakua kitita cha sh. milioni 15 katika mashindano ya 19 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30. 

Shujaa mwenye miaka 23 ambaye ni mkazi wa Morogoro, amejishindia pia laptop, kiwanja chenye hati eneo la Kigamboni kilichotolewa na kampuni ya Property International ya jijini Dar es Salaam pamoja na dola za Marekani 500 kutoka kwa Bw. Ahmed Seif “Magari” aliyetoa dola 500 kwa washindi wote watano. 

Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumapili, Mei 27, 2018), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuilinda amani iliyopo nchini kwani ikipotea hakuna atakayeweza kufanya ibada. 

“Mtakubaliana nami kuwa amani ya nchi yetu, ndiyo inatufanya tutembee vifua mbele dhidi ya wenzetu, ni neema kubwa ambayo kila muumini anapaswa kuilinda kwani ikipotea hata mkusanyiko wetu huu wa leo si rahisi kufanyika mahali kama hapa,” amesema. 

“Leo hii tuko hapa uwanjani kwa sababu tuna amani, kama Serikali isingekuwa inashirikisha Watanzania wote kulinda amani, basi tusingeweza kukutanika hapa. Kuna nchi 18 ziko hapa, na watu wake wamekuja hapa uwanjani kwa kuwa wana uhakika na amani tuliyonayo sisi Watanzania,” alisema. 

Alisema katika nchi ambazo amani imetoweka, watu wanalazimika kufanya shughuli za ibada majumbani au kwa kujificha. “Wenzetu hao, hawapati fursa adhimu kama hii ya kujumuika pamoja na majirani, ndugu, jamaa na marafiki kusikiliza na kufurahia kisomo cha Quran au kufanya shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii,” aliongeza. 

Aliwataka Watanzania waendelee kubeza na kupuuza kauli za walio wachache ambao kwao kuzungumzia amani ni kujipendekeza kwa Serikali. “Watu hao wamesahau kwamba tofauti katika Uislamu hazikuanza leo, lakini tofauti hizo hazikuwa sababu ya wema waliotangulia kuacha kuheshimiana na kushirikiana,” alisisitiza. 

Mshindi wa pili kwenye kundi hilo la juzuu 30 ni Ahmed Noor wa Sudan ambaye ameshinda sh. 12,564,750 pamoja na laptop akifuatiwa na Muzamil Awadh Mohamed wa Sudan alijishindia sh. milion 7.5 pamoja na laptop zilizotolewa na kampuni ya Camara Education.

Mshindi wa nne ni Abdulally A. Mohammed wa Kenya aliyepata zawadi ya sh. 5,711,000 na wa tano ni Ibrahim Maazur kutoka Niger, aliyepata sh. 3,426,000. Washindi hao wote watano walipewa zawadi ya kwenda hijja na Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dk. Saleh Ally Sheikh. 
Washiriki wengine kwenye kundi la juzuu 30 walitoka nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji Djibouti, Kenya, Ethiopia, Congo DRC, Nigeria, Ghana na Afrika Kusini. 

Washiriki wengine waliopewa zawadi ni wale walioweza kuhifadhi Juzuu tatu (washindi watatu), Juzuu tano (washindi watatu); Juzuu 10 (washindi watatu) na Juzuu 20 (washindi watatu). 

Viongozi wengine waliohudhuria mashindano hayo ni Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Mohammed Gharib Billal, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania kutoka Saudi Arabia, Comoro, Oman, Uturuki, Kenya, Msumbiji na Nigeria, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally na Rais wa taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Sharif Abdilkadir Al-Ahdal.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Sheikh Nurdin Mohammed Ahmad (maarufu kama Sheikh Kishki) akaonane na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi ili atoe maamuzi ya kiwanja chao kilichopo eneo la Matumbi ambacho mwaka jana aliagiza kifuatiliwe taratibu zake na kisha wapatiwe.

“Kuhusiana na suala la kiwanja mlichosema, mamlaka ya awali ni Manispaa ya Temeke na ilishakamilisha taratibu zote za kisheria, ikapeleka kwa Afisa Ardhi wa Mkoa kuona kama limepita kwenye vikao vyote ndipo wanaenda wizarani kupata kibali. Hakuna sababu ya wizara kuikatalia manispaa huku eneo lenyewe likiwa kwenye ramani kuu ya manispaa yenyewe, nenda mumuone Waziri mwenye dhamana, awape ardhi,” alisema.

Waziri Mkuu amefikia hatua hiyo baada ya kupewa taarifa akiwa jukwaani kwamba taasisi ya Al-Hikma iliwasiliana na Manispaa ya Temeke, hadi mkoani wakapewa barua zinaonyesha eneo liko sawa lakini walipofika wizarani wamekwamishwa na Afisa mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Mama Mpetula.

Juni 11, mwaka jana katika mashindanio ya 18, taasisi ya Al-Hikma waliomba wapatiwe kiwanja na.118 kwenye kitalu E kilichoshikamana na kiwanja na. 117 chenye shule yao ya Al-Hikma Girls iliyoko Temeke ili waweze kujenga zahanati.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur- aan Tukufu  Afrika yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Al – Hikima, Mei 27, 2018. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Dini wa Saud Arabia, Dkt. Saleh  Alashiek.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dr. Saleh  Alashiek   katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
 Baadhi ya waalikwa waliohudhuria katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
  Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akizungumza katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
 Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dr. Saleh  Alashiek  akizungumza katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018. 
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika  yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimkabidhi Shujaa Suleiman Shujaa zawadi ya shilling milioni 15 baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 17, 2018. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir na watatu kulia ni Rais wa Taasisi ya Al- Hikima, Sheikh Shariff Abdukadir. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MKAZI WA NYAMAGANA ASAIDIWA BAISKELI YA MIGUU MITATU

$
0
0




NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA.

Mkazi wa Mtaa wa Nyerere A katika Kata ya Mabatini wilayani Nyamagana katika Jiji la Mwanza, Fred Kaseko (47) amepata msaada wa baiskeli ya miguu mitatu (wheel chair) itakayomsaidia kwa usafiri.

Kaseko alipata ulemavu wa miguu uliosababishwa na ajali ya gari miaka tisa iliyopita na kusababisha ashindwe kutembea baada ya miguu kukosa mawasiliano kutokana na neva za mgongo kuathiriwa.

Akipokea msaada huo jana uliotolewa na familia ya Mohamed Abass Mahamoud Abbas Mohamud Damji yenye asili ya Kiasia ya jijini Dar es Salaam,Kaseko alisema ameteseka kwa miaka tisa akitembea kwa kujivuta kwa kutumia mikono.

Alisema alipata ajali na taratibu miguu ilianza kupoteza uwezo wa kutembea wala kusimama na alipokwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) na kufanyiwa vipimo iligundulika kuwa disc za mgongo zilikuwa zimekandamiza mishipa ya fahamu baada ya kupata ajali.

“ Wakati nikifanya kazi ya ukaguzi wa tiketi kwenye kampuni ya mabasi ya AM nilipata ajali iliyonisababishia tatizo hili. Nilipokwenda hospitali daktari alinieleza kuwa disc za uti wa mgongo zilipanda kwenye mishipa ya fahamu pamoja na misuli na hivyo kusababisha miguu kupoteza mawasiliano. Tiba pekee niliambiwa ni kufanya mazoezi ambayo hunigharimu sh. 5,000 kwa siku,” alisema Kaseko.

Alisema kwa mujibu wa daktari aliyemuhudumia matatizo hayo husababishwa na madhara yatokanayo na ajali bila kufanyiwa vipimo na kupata tiba ambapo aliwashukuru wafadhili waliotoa msaada huo pamoja na Mwenyekiti The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee.

Mwenyekiti huyo wa The Desk & Chair Foundation alisema familia ya Mohamed Abbas Mohamud Damji iliguswa na tatizo la Kaseko na hivyo ikatoa baiskeli hiyo yenye thamani ya sh. 350,000 kupitia taasisi yake.

“Hii ni baiskeli ya 386 kutolewa na taasisi yetu na imetolewa na familia ya Damji ikiwa ni sadaka ya kumrehemu mtoto wao aliyefia nchini Canada akiwa masomoni iweze kumsaidia Kaseko.Misaada hii ni endelevu, inatolewa kwa watu wenye mahitaji kama haya ya ulemavu wa viungo hasa wa miguu inapotokea,”alisema Meghjee.

Hata hivyo Kaseko licha ya kupata msaada huo wa baiskeli bado anakabiliwa na changamoto ya kukatiwa huduma ya maji na Mamlaka Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) kutokana na malimbikizo ya ankara ya malipo ya maji kiasi cha sh.325,000 pamoja na fedha za kuhudhuria mazoezi ya viungo
 Fred Kaseko , mkazi wa Mtaa wa Nyerere A Mabatini kabla ya kupata msaada wa baiskeli ya miguu mitatu alikuwa akitambea kwa kutumia  mikono.
 Sheikh wa Bilal Muslimu Mission of Tanzania Hashim Ramadhan (kulia) akimkabidhi baiskeli ya miguu itatu Fred Kaseko.Nyuma ni familia ya Kaseko ambaye anasumbuliwa na miguu kupooza baada ya kupata ajali. Baiskeli hiyo imetolewa na familia ya Mohamed Abass Mahamoud Damji . Picha Na Baltazar Mashaka


Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images